Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Kim Kardashian Akanusha Tetesi Kuwa Wameshafunga Ndoa

$
0
0
Siku chache baada ya kusambaa tetesi kuwa Kanye West na Kim Kardashian tayari wamefunga ndoa yao ya kwanza (kiserikali), mrembo huyo ameamua kusema na kuzikanusha tetesi hizo.

Bibi harusi mtarajiwa ambaye ataonekana kwenye TV akiwa na mumewe Kanye West watakapofunga ndoa rasmi May 24, ameekanusha tetesi hizo kupitia akaunti yake ya Twitter.

Tetetesi ya pili aliyoikanusha ni pamoja na ile inayoaminika sana kuwa ndoa yao itaoneshwa kwenye show maarufu ya familia yake, “Keeping Up With The Kardashian”.

Kim K alikanusha pia kuwepo orodha ya wageni 1600 iliyosemekana kuwa na majina mengi ya watu maarufu akiwemo Lupita Nyong’o, Winnie Mandela na wengine.

Na mwisho akawatahadharisha watu kuhusu picha za nguo zake za harusi zinazosambaa kuwa sio za kweli.

“Seeing fake wedding dress pics of me. No one has seen my dress! Those photos are old or photo shopped.”

Bolti Aomba Msaada wa Kupatikana Viatu vyake Vilivyoibwa Uingereza

$
0
0
Bingwa wa Olympic wa mbio fupi Usain Bolti, ametoa taarifa za kupotelewa na viatu vyake vyenye thamani ya paund za kiingereza elfu ishirini.
Usain Bolti, ametoa taarifa hizo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa twitter yenye watu million 3 kwa kumtaka yoyote alieviona viatu hivyo amrejeshee.

Bolti amelazimika kutangaza hadharani taarifa hizo, baada ya kuona hakuna muelekeo wowote wa kupatikana kwa viatu hivyo vyenye rangi ya machungwa sambamba na chapa ya kampuni ya Puma.

Tayari wapelelezi wa Scotland Yard wamethibitisha kwamba viatu hivyo viliibwa juma lililopita katika, mtaa wa Craydon mjini London maeneo ya viwandani ambapo viliwekwa kama maonyesho.

Hata hivyo licha ya viatu hivyo kuchukulia Usain Bolti, ameweka saini katika viatu vingine vitakavyopelekwa katika maonyesho hayo.

Hii Kali:Kuchapiwa Mke ni Faida Kwa Wanaume

$
0
0
Kwa wanaume,
Ukisikia mkeo analambwa nje furahia, na msisitizie awaambie jamaa zake watumie kondomu ili unufaike kwa haya yafuatayo.

1. Unapunguziwa matumizi(Lazima anapewa pesa)
2. Unaletewa staili mpya za mapenzi
3. Mapenzi yanazidi ili husijeshtukia dili.
4. Ukifulia una uhakika wa kukuta msosi mzuri nyumbani.

Je, Kufanya Mapenzi, Ndio Kipimo cha Kuamini Kuwa Mpenzi wako Anakupenda?

$
0
0
Je, kufanya mapenzi, ndio kipimo cha kuamini kuwa mpenzi wako anakupenda?

A: Ndiyo
B: Hapana

Ufuska Bongo Movies Wamkosesha Deal Mwigizaji Nora

$
0
0
MWANADADA wa ‘long time’ kwenye sanaa ya uigizaji amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukosa dili za kazi za maana kutokana na tabia za kifuska kwa baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo Movie.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nora alisema amekuwa akitembelea katika ofi si mbalimbali
na kila anapojitambulisha kwamba ni msanii wa fi lamu watu wanashtuka na sehemu nyingine anakosa dili za maana kutokana na uchafu wa baadhi ya wasanii hasa wasagaji na wanaojiuza.

“Yaani naona aibu sana kujitambulisha kwenye ofi si za watu kwani kila ninakoenda na kujitambulisha watu wanaanza kunong’ona huku wakidai kwamba wasanii wa kike wa fi lamu wana tabia chafu wakati tunachafuliwana watu wachache tu wasiojiheshimu,” alisema Nora.
Stori:GLADNESS MALLYA, GPL

Maimartha Atuhumiwa Kuwauzia Mastaa Dawa za Kukuza Makalio

$
0
0
 
MTANGAZAJI aliyepata kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse, amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini dawa za kuongeza makalio.Habari za moto kutoka kwa sosi wa kuaminika, zinasema kuwa Maimartha ambaye pia huitwa Mai amefikia hatua hiyo baada ya yeye kutumia na kufanikiwa.

“Hamshangai siku hizi kila staa anaonekana kuwa na makalio makubwa? Ni kazi ya Mai hiyo. Anafanya hiyo biashara muda mrefu sana. Ni za kunywa na kupaka.

“Mbona hata yeye ametumia dawa hizo muda mrefu sana? Ukimwangalia utagundua zamani hakuwa na hipsi za kiivyo. Ni kwa sababu ya dawa,”  alisema sosi huyo.

Akaongeza: “Hata Lulu Semagongo (Aunt Lulu)   ndiye aliyemsababishia kuwa na makalio makubwa kwani wakati wako karibu alikuwa akimpa dawa hizo.”

Waandishi wetu walifika dukani kwa Mai bila kujua kama ni waandishi na kuulizia bidhaa hizo ambapo zilitolewa, wakapiga picha bila kugundulika.

Mai akiwa hajui kuwa yupo mikononi mwa mapaparazi waliokuwa na njaa ya habari, aliwaambia: “Ni dawa nzuri, mara moja zinarekebisha umbo na unakuwa wa kuvutia. Kuna za shilingi 250,000 na 260,000 inategemea kama ni vidonge au losheni.”

Mapaparazi wetu walipompigia simu Mai baada ya kutoka dukani hapo na kumweleza kuhusu uuzaji wa dawa hizo dukani kwake, alisema duka lake linauza urembo wa aina zote kwa mastaa na wasio mastaa.

“Kama nimetumia dawa za kuongeza makalio, nyie inawahusu nini? Kifupi duka langu linadili na urembo wa aina zote,” alisema Mai akishindwa kufafanua zaidi.

Lulu alipovutiwa waya na kuulizwa kama makalio yake ni matokeo mazuri ya dawa za Mai alisema: “Sijawahi kutumia dawa za Mai kwa ajili ya kuongeza makalio.

Yangu ya asili lakini watu wakinipigia simu na kuniuliza dawa za kuongeza makalio huwa nawaelekeza kwa Mai.”
Stori: : Hamida Hassan na Gladness Mallya, GPL

Endless Fame Films Watoa kauli Kuhusiana na Ugomvi wa Wema na Kajala

$
0
0
Kampuni ya filamu ya Wema Sepetu, Endless Fame Films, leo imetoa kauli yake kuhusiana na ugomvi wa mmiliki wa kampuni hiyo na aliyekuwa rafiki yake wa karibu Kajala Masanja.

Maneja wa kampuni hiyo, Martin Kadinda ametoa msimamo huo kupitia mtandao wa Instagram.
“Good morning all of You…. I just woke up Like “Hasiraless” kwakuwa hili vugu vugu la kutokuwa na maelewano mazuri kati ya Wema sepetu (myclient) na Kajala limekuzwa katika social networks basi na mimi naomba nitoe taarifa kutoka kwetu endless fame.

Katika urafiki kuna mengi yanajitokeza na endapo kutakuwa na hitilafu sehemu basi ni muhimu kupeana nafasi ili kila mtu aweze kujirekebisha na mwisho wa siku maisha yaendelee hilo ndo lililotokea baina ya hawa wawili. Lakini katika kipindi hicho cha so called mapumziko kuna mambo mengi yamejitokeza, yapo ya kweli na yapo yaliyotengenezwa na baadhi ya watu, kuna media coverage juu ya hawa wawili na wema sikumpa nafasi ya kuzungumza na chombo chochote cha habari kwakuwa nilijua litakuzwa zaidi… ila tulipoona shutuma zinazidi kuja upande wake akafanya interview na gazeti moja na kuelezea upande wake na mwisho alisema hana tatizo na kajala sema tu Kwa sasa anahitaji space…… tukawa tumefunga mjadala huo.

Endless fame(wema sepetu) haijawahi kutamka lolote swala la mahusiano ya kajala na mtu yoyote, EndlessFame haijawahi kudoubt urafiki wa kajala na any of her friends because tunaamini yale ni maisha yake binafsi na hayahusiani na kampuni ya wema au wema mwenyewe, kusaidiana katika matatizo haimaanishi tunammiliki… hapana hapana… Hili linaloendelea sasa sisi pia tumelisikia na kuliona kwenye social networks kama watu wengine wanavyoona.

Tunaumizwa na blogs na magazeti yanapoandika stori kama vile wanaushahidi kutoka endless fame au Kwa mtu wa karibu na wema. Team wema wote waliopo insta sijawahi kuona hata mmoja kati yao hivyo hakuna anayewatuma wala kuwashinikiza ila wao wanafanya kile kinachowapendeza and hatuwezi kuwakataza kwasababu ni maisha yao binafsi na ni mapenzi yao ya dhati Kwa wema.

Poleni Kwa wote mnaoumizwa na haya yanayoendelea ila nadhani tukazane na kazi zetu na maisha yetu maana haya ya instagram tuwaache huku huku ukiyasikiliza utashindwa kumwamini mama yako mzazi.”

Hivi karibuni Kajala alisema kutokana na jinsi ambavyo ugomvi wake na Wema Sepetu ulivyokuwa mkubwa, amefikia hatua anaigopa simu yake zaidi ya kupiga na kupokea.

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV wiki hii, Kajala alisema amekuwa akiumizwa na jinsi anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ugomvi huo. Kajala amesema ugomvi wake na Wema haujatokana na kile kinachodaiwa kuwa alimchukulia ‘bwana yake’ na kwamba umetokana na vitu vidogo ambavyo ni binafsi kwao. Alidai kuwa pamoja na ugomvi wao kusababisha na mambo ya kawaida, umekuzwa mno na watu pamoja na vyombo vya habari kiasi cha kuwafanya wajikute maaudui kweli.

Kuhusiana na tetesi kuwa alianza kumdharau Wema baada ya Miss Tanzania huyo wa zamani kuishiwa fedha, Kajala amesema amekuwa rafiki yake tangia enzi hana chochote. “Alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwahiyo kwamba nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi hana hela mimi sio rafiki yangu tena, sio kweli,” alisema.

Kajala alikiri kuwa kukosana kwake na Wema kumeathiri maisha yake. “Inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea, mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo sometimes nikikaa nammiss,” alisema na kueleza kuwa ameshawahi kumtaka Wema wamalize ugomvi wao lakini ilishindikana japo alisema kwakuwa ugomvi ni wao wenyewe, ipo siku utaisha na watakuwa marafiki tena.

Kafulila Awalipua Mawaziri Akaunti ya Escrow

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilichotwa katika Akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Katika tuhuma hizo, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.

Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.

Kafulila alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.

Mbunge huyo alisema fedha zilizoibwa katika Akaunti ya Escrow ni nyingi kuliko zile zilizoibwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT mwaka 2005.

“Pamoja na hilo, Watanzania wamekuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tanesco wakati ilipokuwa na mgogoro na IPTL walifika mahali wakafungua akaunti ya Escrow,” alisema.

Mbunge huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2004 na hadi jana, akaunti ile ilishafikia Dola za Marekani 122 milioni,” alisema Kafulila.

Alisema fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwapo kati ya IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.

Alitaka jambo hilo liingie kwenye rekodi kwa kuwa linahusu BoT na vigogo akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na pia Waziri wa Fedha.

Alisema wakati Tanesco ikidaiwa madeni zaidi ya Sh400 bilioni, viongozi hao wameidhinisha kugawanywa kwa fedha hizo kihuni jambo alilosema halivumiliki hata kidogo.

Kafulila alisema fedha hizo zilichotwa na Kampuni ya PAP aliyosema ya “Singasinga na ya kitapeli” ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu.

Nakua Chizi Kwa Wivu wa Mke Wangu...

$
0
0
Nina mke mmoja ambae tunapendana sana,tatizo ana WIVU kupindukia.
1.Ninapoingia tu home ananidaka na kuninusa nguo,akisikia pafyum kwa mbali MATATIZO,mim situmii pafyum ila usafir wa kwetu ni shida,mnabana had kupumua shida.Matokeo yake sipend watu waniguse kitu ambacho ni kigumu kwenye usafir wa jumuiya!
2.Kila ninapoenda anataka nitume picha kwa whatsap,hata kama kwenye daladala nimesimama,anataka nipenye dirishan nipige hilo eneo,au nijipige kitu ambacho watu hawakubali maana wanaona unawapiga wao!Hata wakat mwingine ananiambia chukua jiwe,weka sehem flan then piga picha.
Hii inanifanya ntaokota makopo il nipige picha ili aamini,JE NIFANYEJE MAANA TUNAPENDANA SANA.

Master J Ashauriwa na Mama yake Kumtambulisha Rasmi Shaa Kama Mpenzi Wake

$
0
0
Ni miaka mingi sasa imepita toka ifahamike kuwa CEO wa MJ Records Joachim Kimaryo aka Master J na mwimbaji Sarah Kaisi aka Shaa ni wapenzi, kiasi mpaka sasa hata wanapoulizwa kwenye interviews na mitandao ya kijamii hukiri kuwa wao ni couple.

Lakini mama mzazi wa Master J ameona kuna haja ya mwanae kuuweka wazi rasmi uhusiano wao ili jamii iwe na taarifa sahihi, hivyo amemshauri mwanaye kuwaita waandishi wa habari kuzungumzia uhusiano wao na mipango yao ya ‘ndoa’.

“Hili ni jambo ambalo kusema kweli limekuwa kubwa sana sasa hivi,” Alisema MJ kupitia E-News ya EATV. “Nilikuwa nimekaa na mama yangu mzazi amenishauri ameniambia sikiliza uite watu wa media wewe na huyo Sarah muwe open kwa sababu kiukweli mnavyoendelea kukaa kimya kila mtu anakuwa ana assume mambo yake ambayo mwisho wa siku yanaweza kuleta madhara flani”.

Mj ambaye ni baba wa watoto watatu ameahidi kuwaita waandishi wa habari mwaka huu ili kumtambulisha rasmi Shaa kama mpenzi wake na mipango yao ya baadaye.
Bongo5

Alichokisema Master Jay kuhusu uhusiano wake na Shaa pamoja na Mke wake wa Ndoa.

$
0
0
Ingawa kuna fununu ambazo si rasmi kuhusu uhusiano wa kimapenzi kati ya Master Jay na Shaa,hapa kuna stori tofauti ambayo Soudy Brown anai-amplify kuhusu mke wa Master Jay kutoka na msanii wa Bongo fleva,hapa utamsikia Master Jay na msanii anayesemekana kumchukua Mke wa Master Jay. Sikiliza Hapa:

Wimbo Mpya wa Diamond platnumz -Kitorondo Download hapa

$
0
0
Huyu Mtoto ni Noma , Haya Sikiliza ama download Wimbo mpya wa Diamond hapa chini:

Diamond: Wimbo Wangu Mpya Haujatoka Rasmi Kuna Mtu Kauiba na Kuuweka Mtandaoni

$
0
0
"Moja ya nyimbo zangu ambazo ziko store hazija toka nimeikuta mtandaoni na sijui imefikaje, tena ikiwa kwenye mfumo wa Voicenote, yaani haina quality kabisaa... Tafadhari, kwa yoyote atakaeipata Asiitumie kwenye media ama hadhara, kwasababu Haijatoka na haiko Qualified" Diamond

B-Dozen mchokozi eti amuuliza Ommy Dimpoz kuhusu viatu vyake kama ni vya kike au kiume?

$
0
0
Kwenye mtandao wa twitter, mtangazaji wa Clouds FM Hamisi Mandi au wengi tukimfahamu kama B12 "B-Dozen" amemuuliza swali la kizushi Ommy dimpoz kuhusu viatu vyake alivyo vaa..

nahiki ndicho alichoandika... B12 nakuweka picha ya viatu hivyo..

"Hivi ndo Viatu Vya dimpoz, si kwa ubaya tunaomba ufafanuzi ni Vya kike au kiume?"

We unaonaje Msomaji?

Harusi ya Baby Madaha na Manager Wake Joe Yanukia

$
0
0
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha na meneja wake, Joe Kariuki wanatarajia kufunga ndoa Novemba, mwaka huu nchini Kenya jijini Nairobi.

Akizungumza na mapaparazi wetu, Meneja wa Baby Madaha, Joe alithitisha mipango hiyo na akasema sasa wanafanya kazi nyingi za muziki mpaka zifike nyimbo 20 ambapo baada ya kuoana zitaanza kutoka mojamoja kwa muda wa miaka minne.

“Ni kweli tumepanga kuoana, kikubwa ninaandaa nyimbo nyingi ili baada ya ndoa nitasimama muziki na badala yake nitakuwa naachia nyimbo tu,” alisema Baby anayetamba na Wimbo wa Nawaponda.

Miss IFM 2014 ilivyokua na huyu mshindi kutangazwa

$
0
0
Chuo cha usimamizi wa Fedha IFM usiku wa mei 09 walikua wakimtafuta Miss Ifm ambayo kwao ni kama kumtafuta mwakilishi wao ambaye atakwenda kuwawakilisha kwenye ngazi zinazofuata za mashindani haya ya urembo.
Mgeni rasmi katika mashindano haya alikuwa ni Lawrence Masha,burudani toka 254 ilihusishwa ambapo Cmb Prezzo ameburudisha watu wote waliokuwa ukumbini usiku huo na katika mashindano haya yamemalizika kwa Lilian Timoth kutangazwa kuwa ni Miss IFM 2014.
Wengine ni aliyeshika nafasi ya pili Miss IFM Evanice William na Miss IFM nafasi ya tatu ni Lilian Josephat

Fedha za IPTL Kaa la Moto

$
0
0
Tuhuma za ufisadi wa zaidi ya Sh200 bilioni katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonekana kuwa kaa la moto na jana zilitikisa Bunge na kuibua mvutano mkali.
Hata hivyo, suala hilo sasa limekabidhiwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kubaini ukweli wake.

Tuhuma hizo ziliibuliwa juzi na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ambaye alisema kashfa hiyo ni zaidi ya ile ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT iliyotokea mwaka 2005.

Kafulila alisema ufisadi huo unamhusisha Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gavana wa BoT na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme (Tanesco).

Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.

Hata hivyo, akihitimisha hotuba ya bajeti yake na kujibu hoja mbalimbali za wabunge, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alimwagiza CAG na Takukuru kuchunguza tuhuma hizo ili kubaini ukweli.

“Hoja iliyopo na inayoleta ubishani ni kuondoa pesa kutoka akaunti ya Escrow na kuzipeleka IPTL. Tunajiuliza kama ni ufisadi, ni ufisadi wa nini wakati fedha zile ni za IPTL?” alihoji Pinda.

Pinda alifafanua suala hilo lilipoandikwa kwa kirefu na gazeti dada la Mwananchi (The Citizen), CAG aliwasiliana na Katibu Mkuu wa Nishati, Gavana wa BoT na Mkurugenzi wa Tanesco ili kupata picha ya mchakato mzima.

“Wakati akiendelea hivyo, CAG akapata barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Nishati akimwomba afanye uchunguzi wa kina na wakati huo huo kamati ya PAC nayo ikamwelekeza kuchunguza jambo hilo.”

Waziri Mkuu aliongeza kusema: “Kwa tuhuma zenyewe zilivyo, itabidi tuwahusishe Takukuru nao wafanye kazi kwa upande wao ili kupata ukweli.

“Kwa maelezo na mtiririko ulivyo, kinachobaki ni tuhuma zinazojitokeza ambazo upo uwezo mkubwa wa vyombo hivi kuweza kuzibaini. Naliomba Bunge lako likubali CAG akubali kukamilisha kazi hiyo.”

Waziri Mkuu alisema wako viongozi wa Serikali ambao wametuhumiwa katika suala hilo hivyo ni vyema likachunguzwa kwa uzito wake ili wale watakaobainika wamekula rushwa washtakiwe.

Pinda: Chonde Ukawa rudini Bunge la Katiba

$
0
0
Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewasihi viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurejea katika vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyotarajiwa kuendelea tena kuanzia Agosti 5 mwaka huu.

Amesema kama tatizo la wajumbe wa umoja huo kususia vikao vya Bunge hilo wiki moja kabla ya kuahirishwa kwake ni kejeli na matusi kama ilivyoelezwa na Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe, jambo hilo linazungumzika.

Waziri Pinda alitoa kauli hiyo jana wakati wa kuhitimisha na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2014/15.

Mei 7 mwaka huu, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati akitoa hotuba yake kuhusu Bajeti ya Waziri Mkuu, alisema wajumbe wa Ukawa hawatarejea katika Bunge la Katiba mpaka watakapohakikisha kuwa maana halisi ya uwepo wa Bunge hilo unafuatwa.

Alisema kama lengo ni kutumia mwamvuli wa Bunge Maalumu la Katiba ili kuendeleza mfumo wa kikatiba na muundo wa muungano uliopo sasa, wajumbe wa Ukawa hawatakuwa sehemu ya usaliti huo kwa Watanzania, huku akisisitiza kukerwa kwake na lugha za matusi na kejeli dhidi yao zilizokuwa zikitolewa na wajumbe kutoka chama tawala.

Hata hivyo Pinda jana alisema “Kauli zilizotolewa na Mbowe zilikuwa kali na zilinitisha kidogo. Nadhani  tusianze kutoa picha kwa Watanzania juu ya  hali ya kutokuwepo kwa amani katika siku zijazo kwa sababu jambo hili siyo zuri,” alisema Pinda na kuongeza;

“Nadhani kubwa hapa ni kuendelea kuzungumza juu ya uwezekano wa namna ya kufikia hatima nzuri juu ya mchakato wa Katiba.”

Pinda alisema sababu za lugha za kejeli na matusi zilizotolewa na Mbowe siyo sababu ya msingi ya kuwafanya wajumbe wa Ukawa kususia vikao vya Bunge hilo.

 “Hata kama tungefikia mahali tukavutana sana, suluhu haikuwa kutoka nje ya Bunge. Hata kama mngesema liahirishwe ili tukajadiliane na kukubaliana na kisha kurejea na kuendelea na mjadala, sidhani kama lingekuwa tatizo.”

 Waziri Pinda alisema Rais Jakaya Kikwete hakuwa chanzo cha kuvuruga mchakato wa Katiba kama ilivyoelezwa na Mbowe na kufafanua kuwa Rais Kikwete kama wananchi wengine naye alikuwa akitoa maoni yake na kwamba alieleza wazi kuwa wabunge ndiyo wenye uamuzi wa mwisho.

 Huku akiwataja wajumbe kadhaa wa Ukawa, Pinda alisema: “Bado naamini Mbowe, James Mbatia, John Cheyo na Profesa Ibrahim Lipumba tunaweza kuzungumza, maana kama hoja ni matusi na kejeli, hivi tukikubaliana si tunarudi na kukubaliana kutokuwapo kwa vitu hivyo.”

 Alisema kuwa anaunga mkono kauli ya Mbowe ya kukutanisha makundi yote yanayopingana ili kuzungumza ili yaweze kukubaliana.

Tusikubali Bunge Kuwa Sehemu ya Kuficha Wezi.

$
0
0
Nimejitokeza kuweka post ihi kimsingi tujadili mambo ya nayoendelea mjengoni, sasa tujadili jambo lililo ibuliwa jana na ndg kafulila,juu ya utafunwaji wa zaidi ya bilioni 200 benki kuu, ni ukweli usiofichika kwa sasa ugonjwa unaolitafuna taifa ili ni ufisadi, unaoratibiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi, na sema haya kwa sababu zifuatazo,wote tulishuhudia, bwana luhanga mpina, akijaribu kuzima hoja ya bw Kafulila, akisaidiwa na spika Anne Makinda.
Sote ni mashaidi kwamba mambo haya ya zima zima hayakuanza leo, nakumbuka dk wilbod slaa alipoibua tuuma za EPA bungeni, spika wa kipindi kile bw samweli 6 alitishia kumchukulia hatua za nizamu Dk Slaa, kwa kuongea uongo bungeni, mwishowe ikaja kuthibitika ni ukweli fedha zilichotwa kwenye akaunti ya EPA, likaja la richmond demo ikawa ihi ihi mwishowe ukweli ukathibitika, sasa kunataarifa za CAG na takukuru kupewa kazi ya kuchunguza jambo hili.

Ukweli ni kwamba CAG na takukuru katika tuhuma zilizopiti wali wasafisha EPA na Richmond kabla ya kuja kamati teule ya bunge na ripoti ya wizi hambao CAG na TAKUKURU uliubariki.

Kimsingi hapa zitakuja ripoti za safisha safisha kubariki wizi uhu wa fedha ambazo zingetumika kununulia madawati na madawa hospitalini.

Wito wangu kwa viongozi wa chama cha mapinduzi siku zao za kubakia madarakani zinaesabika, na yote walio yafanya wakiwa madarakani na kulindana watawajibika, waliotenda mema watapata thawabu yao

CHADEMA, Wakati Umefika wa Kuwasamehe Zitto na Wezake

$
0
0
CHADEMA sasa inapaswa kupitia upya na kufanya masahihisho. kwa maamuzi yote magumu yaliyo wahi kuchukuliwa na vikao vya chama hasa KAMATI KUU.kwakuwa imeweza kutengua msimamo wake na kuvunja serikali kivuli bungeni na kuunda serikali ya pamoja inayo wakilisha upinzani bungeni na kuvishirikisha,vyama vya NCCR na CUF.umefika wakati sasa kupitia upya yale maamuzi magumu na kuwa samehe na kuwa rudisha akina zito kabwe,dr kitilia mkumbo na samson mwigamba katka chama.kuwarudisha akina mtela mwampamba,juriana shonza na habibu mchange. haiingii akilini kama unaweza shirikiana na CCM (B) Kwa undani eti ushinde kushirikiana na alie itwa anatumika na CCM. MBOWE,SI LAA NA WAJUMBE WOTE WA KAMATI KUU kwa pamoja au kwa kila mmoja kwa wakati wake amuweni kuruhusu fikira hii mpya kwenu.huku mkitafakali faida na hasala ktk hili.
By Ally makwilo.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images