Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

UKWELI Mchungu...Askari Hawapaswi Kutishia Watu Lakini Swali Maarufu la "Unajua Mimi Nani?'' Huwa Linanikera Sana..!!!

$
0
0

Wakuu katika kuheshimu Mamlaka Viongozi na hasa Viongozi wastaafu wako nyuma sana mtu unamuuliza kwanini imefanya kitendo hiki hakikubaliki yeye anakimbilia Kusema "Unajua unaongea na Nani?'' Au "Unajua Mimi nani?'' 

Kwanini hutaki kujieleza kama Raia wa Tanzania unayefuata Sheria Ni vema Kufuata Utaratibu wa Kisheria kuna Askari wengine hata kiumri wadogo hata hawàjui Kua Lytonga Mrema alikuaga Waziri wa Mambo ya Ndani.

Suala la Parking linaongeleka Mimi mwenyewe huwa nakuta Lim/tairi limefungwa na Mnyororo lakini najishusha jamaa wanatoa mnyororo halafu maisha yanaendelea.

Nimechukulia Mfano wa Viral iliyoenea ikimuonesha Malima akitishiwa na Askari Katika Video ile Nimesikitishwa Kusikia hata Raia wa Pembeni wakishabikia Unajua unaongea na Nani huyo.

Kitendo hicho ni kumu intimidate askari asitimize wajibu wake unavyojitambulisha usihojiwe kama Mtanzania Unaeishi kwa Kufuata Sheria za Nchi.

Siungi Vitendo vya Matumizi ya Silaha ila watanzania tufuate Sheria ikiwa Pamoja na Kua cha tabia ya Kutishia unajua Unaongea na nani? Yaani hata Mimi hiyo kauli huwa inaniboa sana.

RAIS Magufuli Awasamehe Waliosimamishwa TBC kwa Kosa la Kusema Trump Kamsifia Rais Magufuli..!!!

$
0
0

Rais John Magufuli amewasamehe wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), waliosimamishwa kazi kwa kosa la kutangaza habari ya uongo iliyomhusu. Wafanyakazi hao waliosimamishwa Machi 14, walirusha taarifa kwenye Televisheni ya TBC ikidai kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amesifu utendaji wa Rais Magufuli hasa vita dhidi ya dawa za kulevya ilhali siyo kweli.

Taarifa hiyo ambayo ilirushwa Machi 10, inadaiwa ilikuwa imeandikwa kwenye tovuti ya Fox Channel.com. Hata hivyo, baadaye iligundulika tovuti hiyo haikuwa ya Fox na kwamba, taarifa iliyokuwa imeandikwa ni ya uongo.

Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi wa TBC, Dk Ayub Rioba aliwasimamisha kazi wafanyakazi hao waliohusika na uandaaji na utangazaji wa habari hiyo. Hata hivyo, Rais Magufuli ambaye jana alifanya ziara ya kushtukiza ofisi za TBC pamoja na mambo mengine alitoa msamaha kwa wafanyakazi hao. Baada ya kufika alitembelea chumba cha kurushia matangazo na chumba cha habari na kukalia kiti cha watangazaji, huku akiigiza kama mtangazaji wa habari, alitumia fursa hiyo kuzungumza na wafanyakazi.

Akizungumza kwa njia ya simu, Dk Rioba alisema Rais alifika katika ofisi hizo kwa lengo la kuwatembelea na kuzungumza na wafanyakazi, kisha alitoa msamaha huo. Aliwataja waliosamehewa kuwa ni Gabriel Zackaria, Elizabeth Mramba, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai. 

UTATA na Historia ya Salum bin Almasi Aliyeuawa Kurasini Akituhumiwa ni Jambazi..!!!

$
0
0

Salum Mohamed Almasi alizaliwa mwaka 1989 ni mjukuu wa sheikh Muhammad bin Abdurrahman Ashadhuly. Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Kivinje iliyopo Kilwa Kivinje darasa la kwanza mpaka la nne akahamia Masasi kwa mjomba wake Dr. Tondwa na kuendelea hadi kumalizia elimu ya msingi shule ya msingi Mkomaindo iliyo Masasi akaendelea na elimu ya sekondari Masasi day kidato cha kwanza hadi cha nne akachaguliwa kidato cha tano Ndanda high school na akahamia Tambaza high school kidato cha 6 mchepuo wa PGM. Aka dahiliwa katika chuo cha Saint Joseph college of engeering campus ya Songea course ya computer science lakini alishindwa kuendelea kwakukosa mkopo na kua ametoka katika familia isokua na uwezo wa kifedha akakaa nyumbani. Mwaka jana alijiunga na university of Dar es salaam computing centre UCC akisoma course ya ICT in networking ngazi ya stashahada mpaka unamfika umauti alikua ni mwanachuo mwaka wa pili UCC huku akiwa anakaa na kaka yake wa baba mmoja mama mmoja aitwae Alfi Mohammed Bin Almasi

Picha ya kijana aliyejifunika kashida @ kilemba ni SALUMU Mohammad enzi ya uhai wake picha ya nyeusi ni Sheikh Muhammadi Bin Abdulrahamani Alshazily babu wa marehemu nae enzi ya uhai wake picha ya mwenye joho la blue ni Sheik Nurudin Hussein Alshazily pia ni miongoni mwa mababu wa marehemu Salumu Mohammed Bin Almasi.

Unapouzungumzia uislamu wazee hawa ni miongoni mwa waliofanya kazi kuimarisha uislamu na kudumisha amani na upendo hivyo Salumu Mohammed nae alikua Imamu kwa historia ya kuzaliwa katika familia ya manguli wa Elimu ya dini ya kislamu ndani ya ukanda wa Africa Mashariki na kati huku wazee wake hawa wakiwa wamejipatia elimu ya dini kutoka nchi mbali mbali huku wakitokea Kilwa Pande. 

Kwa uwezo wa Allah wameijenga Kilwa kua na uimara wa watu wenye kumjua Mungu na kuchukua kua Dini ndiyo utamaduni wao wa maisha hata mavazi yao kua ni yakidini popote wanapokuwepo na kudumisha Amani na Upendo.

Kuvaa kanzu msuli Kilwa na kutembea na Yasin au msahafu ni sawa na Mmasai kufunga rubega au kutembea na sime ingawa kunatofauti kubwa ya kumfananisha Mmasai na mtu wa Kilwa Pande vile haijawahi Kilwa kutokea aina yeyote ya machafuko kama yatokeavyo huko kwenye jamii ya wafugaji.

Tumeamua kuweka picha za masheikh wetu hawa wawili waliotangulia mbele ya haki ili kuweka kumbukumbu sawa juu ya marehemu wetu huyu Salumu Mohammed Bin Almasi kujua ni mtu alotoka katika familia gani na kuonyesha kazi za kidini zilizofanywa na walimu wake hawa ndani na nje ya nchi hii bila kuhitirafiana na serikali au taasisi nyingine binafsi na za kidini.

Katika historia ya nchi hii watu wa Twarikat Shazily hawajawahi kuhitilafiana na serikali vile hufundisha watu Dini ili wajue kumuabudu Muumba wao.

Marehemu Salimu Mohammed Bin Almasi alishika dini na kushiriki ibada kama ilivyokua inafanywa kabla yake huku babu yake mzaa mama alofariki miaka ya 1990/91Sheikh Muhammad Bin Abdurahman Alshadhiry aliacha watoto wake na wajukuu zake WOTE kua walimu wa dini popote wanapokuwepo katika ardhi hii ya Mwenyezimungu.

Sifa ya shazily huwa anaweza kuipandisha ah'wal @ moli lakini hutokea pale tu anapokua katika dua.

Kifo cha Salimu Mohammed Bin Almasi kinaweza kuacha DOA kubwa ndani ya Shazily endapo uchunguzi hautofanyika na kupatikana majibu kwakua ni jamii iliyojijengea heshima kubwa ya uadilifu na ukalimu popote wanapokuwepo.

Njia zote za umauti hupangwa na Allah ila tukio lenye mashaka hata likileta umauti kwa mwanadamu lapaswa kubainishwa na kuondolewa shaka waziri na jeshi la polisi mutuambie kinaga ubaga ili kama tunakasoro tujirekebishe baada ya kufanya uchunguzi na si kuruhusu maiti izikwe tu na familia yake.

Narudia kidogo makala ya mchana sijawahi sikia familia ya sheikh Muhammad Bin Abdurahani ameiba hata pensel au rula darasani kama hana atakuomba umsaidie vile hana kwakua Allah amewajaalia utajiri wa imani na kusimamisha Dini ya uislamu na si fedha haya nimeyashudia tukiwa darasani na kila mwaka mwana familia yao anekuja kuanza shule kutoka familia hiyo lazima awe mwalimu wa Dini au Imamu hii Polisi pitieni kumbukumbu za familia hii katika shule walizosoma Kilwa secondary, Ndanda, Chidiya, Songea boys, Mtwara technical nk

Kubwa tunawaombea kwa Allah awaongoze KATIKA njia iliyonyooka na kuifikia pepo ya Firdausi awasamehe kwa yale yenye hitilafu ya kibinadamu.

Ndugu watanzania ifike muda tutambue Tanzania ni kubwa ina makabira mengi tamaduni nyingi hata dini pia.

Sisi watu wa Pwani ya Kilwa tumekua mfano wa kutokua na makabila huku tukitambua utaifa wetu tu na dini yetu kua hata ndiyo mila yetu na ni nguzo yetu kitaifa.

Tupeane pole wana Kilwa wote na twarikat shadhily.

Naimani kama leo masheikh wetu hawa wagekua hai ndiyo wangekua wasemaji wa hili Allah awarehemu Sheikh Nurudin Hussein Alshadhiry na Muhammad Bin Abdurahami Alshadhiry.

Pole sana Alfi Mohammed Bin Almasi najua umeumia sana kwa kuondolewa na ndugu yako ulokua unalalanae kitanda kimoja akiwa umetoka Kilwa kuja kutafuta elimu.

Allah Aqbal
Allah Aqbal
Allah Aqbal

ZITTO Ulitaka Bunge Limchague Masha, Umesahau Haya Maneno Yako..!!!

$
0
0

Nilishangaa sana baada ya kusoma ujumbe wa Zitto akidai anajuta kuzaliwa Tanzania kwa sababu wabunge hawakumchagua Lawrence Masha kuwa Mbunge wa EALA.


Zitto amesahau kuwa miaka tisa iliyopita alimtuhumu Masha akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa anapanga mkakati wa kumfilisi Mzee Reginald Mengi kwa sababu Media zake zilikuwa zinaandika habari za kupinga ufisadi.

Zitto huyu huyu leo eti anajuta kwa nini wabunge hawakumchagua Masha kuwa Mbunge.

Wanasiasa wa Tanzania ni viumbe wa ajabu kweli.

Ninaambatanisha maneno ya Zitto aliyoyasema mwaka 2008 kuhusu Lawrence Masha.

Zitto apasua jina la waziri kijana.
2008-12-07 13:37:18 

Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema ana ushahidi kuwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ndiye aliyepeleka hoja ya kumhujumu Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi katika vikao vya juu na kwamba taarifa hizo alithibitisha kuzipata jana.

Akiongea na Nipashe Jumapili jana, Zitto alisema waziri huyo, kwa taarifa alizonazo za kuaminika, alitoa hoja kuwa vyombo vya habari vya IPP vimekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi na hii inailetea matatizo serikali.

Hivyo, aliomba serikali ipange mikakati ya kumfilisi Mengi, kitendo ambacho kitasababisha kudhoofishwa kwa vyombo vyake vya habari ambavyo vitashindwa kuendelea kuupinga ufisadi.

Zitto alisema yeye hana sababu ya kumtetea Mengi ila hawezi kunyamaza kuona Mtanzania anayeipenda nchi yake na kulazimika kupinga ufisadi anafanyiwa hujuma.

Aidha, Zitto aliliambia Nipashe Jumapili kwamba, vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kuanika maovu ya ufisadi na vyombo hivyo lazima vilindwe na Watanzania wote wazalendo.

Akijibu hoja ya Mengi iliyotolewa jana kuwa yupo tayari kutupwa jela ikithibitishwa kuwa amedanganya na kumwomba Masha pia aseme kama atakuwa tayari kujiuzulu iwapo ukweli wa maneno ya Mengi yatathibitishwa, Masha aliliambia Nipashe Jumapili kuwa hawezi kujiuzulu kwa sababu nia yake ya kuwaagiza polisi kufanya uchunguzi ni kumlinda Mengi.

Alisema kutokana na taarifa ambayo Mengi aliipeleka kituo cha polisi cha Oysterbay, polisi wameamua kuifanyia uchunguzi ili kuhakikisha maisha yake yanakuwa salama.

``Nia ya serikali ya kuchunguza tuhuma zilizotolewa na Mengi ni kuhakikisha kuwa tunamlinda,`` alisema Masha na kuongeza kuwa hana tatizo na maneno yaliyotolewa na Zitto ili mradi awe na ushahidi.

Amesema, hata kama hawamuamini, basi waupeleke huo ushahidi kwa Rais au Waziri Mkuu kuuonyesha na kama ikibainika kama ni kweli yeye ndiye anayemhujumu Mengi, basi atajiuzulu.

Akasema kuwa yeye hakusema kuwa atamshughulikia Mengi kama alivyonukuliwa kwenye baadhi ya magazeti ila alisema kuwa sheria itachukua mkondo wake kama ikibainika kuwa tuhuma zilizotolewa ni za kweli.

Akiongea na TBC1 juzi, waziri Masha, alisema kuwa kama Mengi ana ushahidi wa tuhuma alizotoa, serikali haitapata shida ya kuhangaika na ushahidi na imemtaka apeleke ushahidi huo.

Kuibuka kwa sakata hilo kunatokana na Mengi kumtuhumu waziri mmoja kuwa ameagiza abambikiwe kodi bandia ya kiasi kikubwa atakachoshindwa kulipa ili hatimaye afilisiwe.

Alimtuhumu waziri huyo kuwa amekuwa akimtumia ujumbe wa vitisho kutokana na vyombo vyake vya habari kuwa mstari wa mbele katika kupigia kelele ufisadi.

Akifungua kongamano la kuwajengea uwezo vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa vijana wa chama hicho, John Mnyika, aliwataka vijana kuendeleza vita ya ufisadi na kutokatishwa tamaa na vitisho vinavyotolewa na baadhi ya watu.

Aliwakumbusha vijana kuwa ni wajibu wao kupigania haki zao kwa manufaa ya taifa na kwamba wanapaswa kukosoana pindi mwenzao anapofanya vibaya.

``Kwa maoni yangu naona kama kauli ya Masha ya kumtaka Mengi awasilishe ushahidi ndani ya siku saba ni ya kukurupuka kwa kuwa mbona nilipotuhumiwa na Mtikila kwamba nimeshiriki kumuua Chacha Wangwe hakusema lolote hadi leo?

Tunashangazwa sana na kauli ya Masha, tulidhani labda angechunguza kwanza kabla hajazungumza na katika hili nawaomba vijana muwe makini na vijana kama hawa na muwakosoe waziwazi,`` alisema.

Alionya kuwa iwapo vijana hawatakosoana jamii itapoteza imani juu ya utendaji wao na kuondoa matumaini ya taifa kuhusu umuhimu wa vijana.

Hata hivyo,alisema vita dhidi ya ufisadi bado ni kubwa kwa kuwa ni asilimia 10 tu imetekelezwa.

``Msibweteke na ushindi huu, ufisadi unaozungumziwa ni wa utawala wa Mkapa, katika awamu ya nne kuna ufisadi kama wa Richmond na Buzwagi kwa hiyo tunapaswa kupambana zaidi,`` alisema.

SOURCE: Nipashe

UMESHAWAHI Kujiuliza kwa Nini Tende ni Muhimu Mno Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani..Hili Hapa Ni Jibu..!!!

$
0
0

Ndugu zetu waislam hivi karibuni watakuwa wakiingie kwanye mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo mara  nyingi soko la tende limekuwa likiongezeka sasa hapa naomba tufahamu kwanini tende hutumika zaidi katika kipindi hiki.

Ikumbukwe kwamba Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alisema, “Fungueni swaumu zenu kwa tende, au, vinginevyo, basi fungueni kwa maji, kwani ni twahara.” (Abu Dawud na Tirmidh).

Hivyo chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Hii inaendana na Sunna ya Mtume, swallalllahu alayhi wa Sallam. Baada ya kushinda kutwa nzima na swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo huhitajika kurejeshwa upya.

Ingawaje tende si chakula cha kushibisha kwa upesi, lakini huaminika kuwa ndicho chakula kisicho na mafuta, na ni chanzo madhubuti cha sukari na hivyo kurejesha kwa haraka sukari iliyopungua mwilini.

Ifahamike kuwa nusu ya sukari zitolewazo na tende ni kwa ajili ya glukosi pekee, lakini mbali ya glukosi, tende pia ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi ambazo husaidia kuboresha michakato mzima wa umeng’enyaji chakula mwilini.

Pamoja na  hayo, tende ni chanzo kizuri cha madini ya potasiamu ambayo ni muhimu kwa usawazishaji wa maji ndani ya mwilini.

HAYA Hapa Maajabu Saba ya Mbegu za Maboga Ambayo Watu Wengi Hawayajui..!!!

$
0
0

Mbegu za maboga hutokana na tunda liitwalo boga, tunda ambalo asili yake haifahamiki vizuri ni wapi, ingawaje baadhi ya tafiti zinasema kuwa asili yake ni Amerika ya kaskazini.

1. Huimarisha moyo na mifupa

Mbegu za maboga huwa na kiwango kingi cha madini aina ya magnesium, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja na mishipa ya damu sambamba na kuongeza ufanisi wa utumbo mpana . Magnesium inaonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshtuko wa moyo na kiharusi.


2. Kinga ya mwili

Mbegu za maboga zina kiwango cha madini aina ya zink, ambayo pia yana faida nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na na uimarishaji wa kinga mwilini , ukuaji wa seli, macho na ngozi ya mwili. Hali kadhalika zinki huimarisha nguvu za kiume.


3. Saratani ya kibofu

Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha zinki, tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.


4. Ugonjwa wa ini

Mbegu za maboga pia zina kamba lishe na kinga kubwa ya kupambana na magonjwa nyemelezi. Mbali na hayo mbegu hizi zina virutubisho vinavyotoa kinga dhidi ya magonjwa ya ini na moyo.


5. Usingizi

Kwa watu wenye matatizo ya kukosa usingizi, wanashauriwa kula punje kadhaa pamoja na tunda lolote muda mfupi kabla ya kupanda kitandani, utafiti umeonesha kwamba mbegu za maboga zina kirutubisho kinachohamasisha uzalishaji wa homoni za usingizi kwa wingi

6. Uvimbe

Mbegu za maboga zimeonesha kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa yote ya uvimbe mwilini, ikiwa ni pamoja na kuvimba miguu, vidole na hata majipu.


7. Mambo ya kuzingatia

Hakikisha unakula mbegu ambazo hazijaoza na zilizo safi na ambazo hazijakaa muda mrefu, lakini pia tumia mbegu hizo kwa usalama zaidi ikiwa ni sambamba na kuziosha na maji safi na salama kisha zianike na inapendeza zaidi ukila bila kukaanga, lakini ukila pia baada ya kukaanga bado utapata faida zake. Isipokuwa hakikisha haziungui wakati unapozikaanga unaweza kutumia dakika 10 tu katika zoezi hilo la kuzikaanga.

ETI Wanaume Ma Handsome Hawana Lolote Kitandani Zaidi ya Kulamba Lips

$
0
0

Kundi la kwanza: Ma-handsome boys, hawa kitandani ni hovyoo kabisa, wanadhani watapendwa kwasababu ya sura zao pekee na si kugegeda.


Kundi la pili.....


Wanaume wenye pesa, hawa wanadhani watapendwa kwa pesa zao hivyo hawana time ya kutumia nguvu zao nyingi kwenye kugegeda, pesa inaongea.


Wanawake wengi wanaotembea na makundi hayo hapo juu huchepuka kwa lengo la kutafuta kuridhishwa kimapenzi.


Wanaume hawa kwakuwa hawana pesa wala si ahandsome hivyo wao silaha yao ni kugegeda tu, hapo ndipo wanapochukua marks zao za bure. Wanawake wanaogegedwa na hili kundi la hawa jamaa mara nyingi huchepuka kutafuta mabwana wa kupiga nao picha na wenye pesa.


Ila kwa kugegeda hili ndio kundi linaloongoza Tanzania na Africa mashariki na kati

Dogo Janja aingilia kati mapenzi ya Harmonize na Wolper

$
0
0

Msanii kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amesema licha ya kuwaimba Harmonize na Wolper katika wimbo wake wa Kidebe, hajawahi ‘kuvutiwa’ na mahusiano yao.

Dogo Janja amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa msanii akishakuwa kwenye mahusiano na mtu maarufu ni lazima akubali mapenzi yake kufuatiliwa na watu wengi.

“Ukishakuwa na mpenzi staa hiyo ni flamu tayari, maisha yenu ni filamu watu wanafuatilia. Kingine mapenzi yao yalivyokuwa yananza watu walikuwa wanachukulia kama Drama lakini mwisho wa siku unakuja kuona kama wapo serious, kwa hiyo ni vitu kama hivyo.

“Mimi kama mimi siko interested nao sana, ni verse tu zile, siko interest nao kwa vile na mimi nina mapenzi yangu , kila mtu ana mitikasi yake” amesema Dogo Janja.

Siku za hivi karibuni kuliibuka uvumi kuwa wawili hao wameachana lakini baadae Harmonize alikuja kuthibitisha ukweli kuwa hawapo tena pamoja.

AINA 5 ya Vyakula Vyakuamsha Hisia za Mapenzi Zilizopotea..!!!

$
0
0

Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na mmoja wa wanandoa kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa bila kujua kuwa vipo vyakula tunavyokula vinavyoweza kuchangia rekebisha tatizo hilo ndani ya  miili yetu .

Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na hivi hapa chini vifuatavyo:

1. Karanga

Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya. Mzunguko mzuri wa damu katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri na kulifurahia.

Pamoja na hayo, karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume.

2. Tangawizi

Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi inasifika kwa kuwa na uwezo wa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume.

3. Asali

Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.

4. Pilipili

Pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamsha haraka hisia za mapenzi na pia usaidia mwili kuwa na hisia za haraka zaidi kwa kuguswa na kadhalika.

5. Matunda & mboga za majani

Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi.

Zifahamu Mbinu Chafu Na Sababu Za Rafiki Msaliti Kumchukua Mpenzi Wako

$
0
0

Mstari unaotenganisha ‘penzi na urafiki’ ni laini zaidi ya uzi wa buibui, hivyo unahitaji heshima ya hali ya juu, uaminifu wa dhati na utulivu halisi ili usikatike na kuleta maafa ndani ya nyoyo za wahusika.
Kama utairudia vizuri aya hapo juu na kutafakari, unaweza kutumia lugha hiyo ya picha kuunganisha kile ulichowahi kusikia ama kushuhudia pale marafiki tena waliotoka mbali, wanapofikia hatua ya kugeuka kuwa maadui wakubwa kutokana na kusalitiana na kuibiana penzi.
Leo nitawalenga zaidi marafiki wa kiume dhidi ya mrembo wa mmoja kati yao.
“Wanavunja urafiki kwa uzuri wa shemeji zao,” huo ni msemo uliozoeleka unaoonesha madhara ya usaliti wa aina hiyo.
Lakini, wapo marafiki ambao wamefikia hatua ya kuuana kwa visu, kuendeana kwa ‘Kalumanzila’ au hata wenye roho nyepesi kujinyonga kwa hofu ya kuondoa aibu mbele ya dunia.
Kutokana na usaliti huo uliokubuhu, ni dhahiri kuwa wapo pia baadhi ya watu hata wamefikia hatua ya kulea watoto wanaodhani kuwa ni wa kwao na kumbe ni watoto wa rafiki zao wa karibu sana na wanaowaamini. Hiyo ni kwa upande wa wanaume.
Chanzo cha tatizo hilo kubwa la usaliti wa penzi, kwa hakika ni tamaa iliyofungwa kwenye kifurushi cha ukosefu wa heshima, haya, na ukosefu wa hofu ya Mungu kati ya wawili wanaokubaliana kuupasua moyo wa mtu wa tatu anayewaunganisha kama ‘Mashemeji’.
Chanzo kingine ni visasi kutokana na maudhi ambayo huenda yasiendane kabisa na mapenzi. Kwa mfano, mtu anaweza kuamua kufanya usaliti huu kutaka kumkomesha rafiki aliyemdhulumu au aliyemchonganisha na mtu fulani.
Lakini wengine, ni hulka ama uhamasishaji usio wa moja kwa moja kwenye jamii fulani kama uwepo wa misemo maarufu inayotukuzwa katika baadhi ya maeneo kuwa ‘hainaga ushemeji’. Hivyo, wasaliti wanachukulia kama kutembea na shemeji ni jambo la kawaida tu!
Hata hivyo, kwakuwa hata ajali ingawa haina kinga huwa na tabia ama dalili zinazoweza kutajwa, ndivyo ambavyo tabia ama alama za uwezekano wa rafiki kumgeukia mpenzi wako zinaweza kubainika.
Kwanza, baadhi ya marafiki wasio waaminifu, hutumia nafasi ya malalamiko wanayopewa na shemeji zao kuhusu rafiki husika, kuanza kujipenyeza na kuonesha jinsi ambavyo wao ni wema zaidi.
Pili, kwakuwa marafiki hao wasio waaminifu huwa na nafasi ya kusikiliza pande zote mbili, hujikuta wakiyajua vizuri mapungufu ya pande zote mbili na kuanza kampeni chafu inayoongozwa na tamaa, kuanza kuonesha namna wanavyoweza kuziba pengo la udhaifu husika.
Tatu, rafiki mnafiki na mwenye tamaa, huanza kutafuta namna ya kuanza kufanya mawasiliano na shemeji anayemtamani, mawasiliano ambayo yanaweza kuwa hayatiliwi shaka hata kidogo na rafiki husika, lakini yana sumu kali zaidi ya joka ‘cobra’. Lakini kadiri siku sinavyoenda, kwa kutegemea mwitiko wa upande wa pili, hujikuta mawasiliano husika yanaanza kuwa na usiri yakibeba nia ovu.
Kwakuwa rafiki huyo mnafiki anajua mbivu na mbichi kati ya wawili hao, hutumia uongo unaofanana na ukweli uliopitiliza kulaghai na kuidhinisha dhambi yake ya usaliti bila kujali hatari kubwa ya mauaji ya ‘moyo’ wa urafiki inayomkabili, kisa starehe ya muda mfupi.
Kwa upande mwingine wa shilingi, usaliti huo husababishwa kwa makusudi na mwanamke ambaye anaweza kuwa na tabia za kumshusha mpenzi wake mbele ya rafiki zake (rafiki wa mwanaume).
Mwanamke huyo anaweza kuzungumzia udhaifu wa mpenzi wake mbele ya rafiki aliyetambulishwa kwake, kuvaa mavazi au mikao inayoonesha ‘mitego’ kwa shemeji zake na kuomba ‘ofa’ kwa shemeji zake pasipo kumhusisha mpenzi au mmewe.


Hivyo, hupelekea watu wenye tamaa na macho ya ‘kiokote’ kuanza kampeni za kumshawishi kwani huamini ni mtu rahisi wa kutumika kutokana na tamaa iliyomjaa.
Kwa upande mwingine, mwanamke asiye mwaminifu huchukua maamuzi hayo kama sehemu ya kulipa kisasi kwa mpenzi wake akiamini kuwa kwa kutembea na rafiki wa mpenzi wake atakuwa amemuumiza kwa kadiri iwezekanavyo mpenzi wake.
Hata hivyo, kwakuwa Mungu huichukia na kujibu kwa nguvu zote dhambi ya usaliti, wawili hao hawaishi bila kuumbuka hata kama ni mabingwa wa kuficha siri. Na hapo ndipo dhambi ya usaliti huo hugeuka machungu ya kudumu maishani na majuto kwa wahusika.
Kwa mantiki hiyo, ingawa usaliti na uaminifu ni suala linalotoka ndani ya moyo wa mhusika, unapaswa kuchora mstari wa maana kati ya rafiki zako na mpenzi wako.
Hakikisha habari za marafiki zako muwapo kwenye maeneo yenu hazigeuki kuwa habari za kumsimulia mpenzi wako kila kukicha. Mpe habari zako, zenu au mipango ya kupiga hatua.
Tengeneza urafiki wa heshima kati yao na siku zote hakikisha unakuwa mwaminifu pia ili dhambi nzito ya usaliti wao dhidi yako isiwe na uhusiano wowote wa kusababishwa na wewe.
Usimgeuze rafiki kuwa adui mkubwa wa kudumu kwa tama za mwili zitakazoisha ndani ya muda mfupi.

Alinipiga Mpaka Kuniharibu Kizazi Kisha Akaniacha Kwasababu Siwezi Kumzalia

$
0
0

Tafadhali naomba ficha jina ila lakini naomba ushee kisa changu kwani naamini itasaidia wasomaji wako kujifunza kutoka kwangu. Mimi ni mwanamke wa miaka 27, niliolewa kama miama miwili hivi iliyopita na mwanaume ambaye tulidumu katika mahusiano kwa takribani miaka minne hivi kabla ya kufunga ndoa. Wakati tunakutana mimi nilikuwa chuo mwaka wa kwanza na yeye tayari alikuwa anafanya kazi.

Kusema kweli nilimpenda sana mume wangu kabla na baada ya ndoa na hata lakini kitendo alichonifanyia siwezi kukisahau katika maisha yangu. Mwanzo wa mapenzi yetu alikuwa mstaarabu sana, akinihudumia kwa kila kitu, akijali hisia zangu na kila mara kunionyesha kuwa ananijali na wakati wote tangu mwanzo alikuwa akisema kuwa mimi ndiye mwanamke ambaye angapenda kunioa.



Ingawa nilimpenda sana na alikuwa akionyesha kweli kuwa anamaanisha sikumuamini sana kwani nilijua wanaume wote ni waongo. Lakini kweli alionyesha kunipenda, tatizo lake alikuwa na wivu na hasira sana, yaani kila mara alitaka kuwa na mimi, hakutaka niwe na marafiki wa kiume. Kila rafiki aliyekuwa akiniona naye alihisi natembea naye na hilo lilinikwaza sana.

Nakumbuka wakati mmoja nikiwa niko ‘Discussion’ na wanafunzi wenzangu alinipigia simu nikachelewa kupokea, kwahiyo akawa amepiga kama mara mbili hivi, akaniuliza uko wapi nikamuambia nipo kwenye ‘discussion’ aliwasha gari na kuja mpaka chuo, alinikuta nipo na wakaka watatu ambao tulikuwa tunafanya ‘assigment’ alinichomoa katikati yao na kunipiga makofi mbele yao, kisha akanichukua mpaka kwenye gari lake na kuondoka na mimi.

Kitendo kile kilinikera sana kwani mbali na kuniumiza kimwili lakini alinidhalilisha pia, lakini nilikuja kumsamehe baada ya kuniomba sana msamaha. Madai yake iilikuwa kwanini niwe na ‘discussion’ na wanaume pekee, ukweli nikuwa group letu lilikuwa la watu sita wanaume watatu na wanawake watatu lakini rafiki zangu wawili walichelewa mjini hivyo sisi tukawa tumeamua kuendelea.

Hilo lilipita na kuahidi hatarudia tena, mambo yaliendelea vizuri akarudisha mapenzi lakini hakupunguza wivu, aliniminya sana mpaka kunifanya kuwatenga marafiki zangu wengi ili tu kumridhisha kwani sikutaka migogoro na yeye. Pamoja na yeye kuwa na wivu namna hiyo na kunichunga sana lakini mara kadhaa nilifumania meseji za wanawake wake wengine katika simu yake na nilipomuuliza ulikuwa ugomvi ambao ulipelekea hata kunipiga.

Kwasababu hiyo niliamua kutokumuuliza, hata nilipomkuta na mwanamke katika mazingira tata nilijifanya kipofu kwani nilimpenda sana na nilivumilia nikiamini kuwa iposiku atabadilika. Baada ya kumaliza chuo nilipata kazi hivyo kitu ambacho kilikuwa kimebakia ilikuwa ni ndoa tu. Kusema kweli nilikuwa na hamu sana ya ndoa kwani nilikuwa nikimpenda sana na kubwa kabisa nilijua baada ya kuoana atabadilika.

Niliamini kuwa baada ya kuniweka ndani hatakuwa na wivu tena na hatakuwa akinipiga kwani tayari atakuwa akinimiliki. Kichwani nilikuwa nikiamini sababu za wivu wake nikutokana na upendo wake kwangu na hofu ya kunipoteza, niliamini baada ya ndoa itakuwa rahisi kwangu kumbadilisha.

Niliongea naye kuhusu ndoa lakini aliniambia nisubiri “Unaharaka gani ya kuolewa?” Lilikuwa ndiyo jibu lake na kwakuwa nilimfahamu kama mtu wa hasira basi nilikaa kimya ili nisimuuzi. Siku moja nilichelewa kidogo kutoka kazini na wakati naondoka mfanyakazi mwenzangu ambaye yeye alikuwa na gari na alikuwa akikaa mtaa wa jirani na nilipokuwa nimepanga aliamua kunipa lifti.

Mara kadhaa hunipa lifti lakini anapofika kwake hunishusha na mimi kutembea kwa miguu mpaka kwangu kwani hakukuwa mbali sana, lakini siku hiyo kwakua nilichelewa sana aliamua kunifikisha mpaka getini. Alinishusha na kuondoka zake, niliingia ndani nikakuta mlango haujafungwa nikajua tu mpenzi wangu yuko ndani kwani alikuwa na funguo zangu na alikuwa na kawaida ya kuja bila taarifa.

Nilipoingia tu nikiwa sina hili wala lile nilikutana na kofi ambalo lilifuatiwa na teke lilionidondosha chini, kabla hata sijajiuliza ni kitu gani mtu alinikanyaga mguu na nikasikia ‘kaaaa’ mguu ulikuwa umevunjika. Hakujali aliendelea kunipiga kisha akaondoka kwa hasira, wakati akinipiga alikuwa akinitukana kuwa mimi ni Malaya na nimefikia hatua wanaume wangu wananileta mpaka nyumbani.

Aliniacha pale nikiwa katika maumivu makali, nilijaribu kunyanyuka lakini nilishindwa, kwa bahati nzuri kumbe wakati ananipiga majirani walisikia na alipotoka kwa hasira walimuona na waliposikia nalia kwa maumivu waliingia ndani na kuniona katika ile hali wakaamua kunipeleka hospitalini kwa kunipitishia Polisi kwanza. Ingawa nilikataa kupitia Polisi nikihofia kuwa mpenzi wangu atafungwa lakini waligoma wakisema siwezi kutibiwa bila PF3.

Kweli mguu ulivunjika nikafungwa POP, kule Polisi baada ya kuandika maelezo walitaka kufungua kesi lakini niligoma kutoa ushirikiano, hiyo ni baada ya kuniomba msamaha na kunivalisha pete nikiwa bado hospitalini. Ndugu zangu walinisihi sana kuachana naye lakini sikusikia, aliniambia ni shetani alikuwa amempitia na nilimuamini, aliomba msamaha sana akiahidi kubadilika.

Baada ya mimi kutokutoa ushirikiano na yeye kutoa pesa Polisi kesi ilifutwa kabisa na nikiwa bado na POP langu alijitambulisha kwetu rasmi ingawa walikuwa wanamjua akatoa mahari na mipango ya ndoa ikaanza kufanyika. Kama miezi minne hivi mguu ulishapona vizuri nikaweza kutembea bila msaada wa magongo na mwezi wa tano baada ya kile kipigo tulifunga ndoa.

Miezi ya mwanzo ya ndoa yetu ilikuwa mitamu na haikuchukua muda sana ndoa ilijibu, nilipata ujauzito kitu ambacho kilizidisha furaha, akawa mtu wa furaha, akapunguza wivu na hakukuwa na vipigo tena. Nilimshukuru Mungu kwa mabadiliko yale kwani nilikuwa na furaha tena na mume wangu alikuwa akijua kujali kwa vizawadi, outing za kutosha na vacation za hapa na pale.

Kusema kweli mambo yalikuwa mazuri mpaka mimba ilipofikisha miezi minne, hapo ndipo alipobadilika na kuanza kusema kuwa hataki nifanye kazi, mara ofisi yenu ina wanaume wengi, wivu ukarudi na kelele zikawa haziishi. Nilimgomea kuacha kazi kwani sikutaka kuwa Mama wa nyumbani, isitoshe kazi yenyewe ni nzuri na ina maslahi makubwa hivyo sikuona sababu ya kuacha kazi na kubaki kuwa mama wa nyumbani.

Mwanzoni sikujua nikwanini suala la kucha kazi limekuja ghafla wakati hapo awali alikuwa haliongelei, lakini nilipokuja kuchunguza ndipo nilipogundua kuwa kumbe alikuwa akitembea na dada mmoja pale ofisini kwetu na hakutaka mimi nijue ndipo akaona nibora niache kazi.

Siku moja wakati mimba ikiwa na kama miezi mitano hivi alikumbushia suala la mimi kucha kazi. Ingawa sikutaka kuzungumzia kuhusu yule dada kwani namjua hasira zake na nilishakubali kuishi naye hivyo hivyo hata kama anachepuka lakini nilipandwa na hasira na kuamua kumpasha ukweli kuwa sababu za kutaka mimi kuacha kazi ilikuwa ni yule dada wa ofisini.

Huwezi amini ilikuwa ni kama mimi ndiyo ninachepuka, aliwaka na kuanza matusi, alinitukana sana, kwakuwa najua hasira zake niliamua kukaa kimya na hilo pia lilikuwa kosa, alianza kunipiga akisema kuwa nina dharau, alinipiga sana sehemu mbalimbali bila kujali kuwa nilikuwa mjamzito, mimi sikufanya chochote kila mara nilijikunja ili kuzuia kupigwa tumboni.

Baada ya kumaliza kunipiga alinichukua na kwenda kunifungia stoo kisha yeye akaenda kulala. Kusema kweli nilipatwa na maumivu makali ambayo katika maisha yangu nilikuwa sijawahi kuyapata hasa eneo la tumbo na chini ya kitovu, damu zilianza kutoka na hapo ndipo nilijua kuwa nimempoteza mwanangu, nilijaribu kupiga kelele kumuambia mimba imetoka lakini hakusikia mpaka asubuhi ndipo alinifungulia.

Alinikuta nikiwa nimeshapoteza fahamu, mabonge bonge ya damu yapo chini. Alinichukua kunipeleka hospitali lakini kwa uoga alinipeleka katika kliniki tu ya rafiki yake ambaye alimuambia kuwa mimba imetoka, nilisafishwa na bila kumuambia mtu yeyote alinirudisha nyumbani. Siku nzima alikuwa akiniomba msamaha lakini sikuwa tayari kumsamehe, kila nilipowaza mtoto wangu hasira zilinipanda nakuwa mtu wakulia tu.

Wiki nzima alinihudumia yeye mwenyewe, nilianza kupata nafuu, sikumuambia mtu yeyote hata ndugu zangu kwani walishanikataza kuolewa na yule mtu, kuhusu mimba niliwaambia tu nilidondoka ghafla na mimba ikatoka. Wiki mbili baadaye nikiwa bado nyumbani kwakuwa kazini walijua mimba yangu imetoka tumbo lilianza kuuma tena, zamu hii kwa nguvu zaidi na vitu vyeusi kama uchafu kuanza kunitoka ukeni.

Nilimpigia mume wangu ambaye alikuja na kunikuta nimezidiwa, alinirudisha kwa yule yule daktari wake ambapo nilikaa huko siku mbili na hali ilipokuwa mbaya zaidi ndipo aliponipeleka Muhimbili, aliwambia kuwa nilipata ajali mimba ikatoka nakwenda kusafishwa, waliponichunguza ndipo waliposema kuwa nilisafishwa vibaya na kizazi kuguswa na kilishaoza ndiyo maana natokwa na uchafu na maumivu.

Hawakuwa na namna zaidi ya kukitoa kabisa na kunisafisha kwani kilishaharibika sana. Ilikuwa ni huzuni sana, nililia na kuzimia mara tano baada ya zile habari. Ndoto yangu ya kuwa Mama ilikuwa imesishia pale, mume wangu alijaribu kunituliza na kunifariji lakini haikusaidia, alinipa moyo kuwa alikuwa akinipenda mimi na si mtoto lakini wapi bado niliumia na sikuwa na mtu wa kumuambia maumivu yangu.

Nilikaa hospitalini kwa wiki moja na nilianza kujisikia vizuri kimwili nikaruhusiwa, nilitamani kuachana na mume wangu lakini nilishindwa. Kuna mambo mawili ambayo yalinizuia, kwanza ilikuwa ni namna ya kuwaambia ndugu zangu sababu za kuachana na mume wangu wakati walijua kuwa ndoa yetu inafuraha na kilichotokea ni ajali tu ya kawaida, hasa ikizingatiwa hawakujua kwamba nimepoteza kizazi.

Pili niliwaza ni mwanaume gani angeweza kunioa hasa akijua kuwa siwezi kumpatia mtoto? Nilijua kuwa hakuna mwanaume ambaye angeweza kunivumilia tofauti na mume wangu hasa ikizingatiwa kuwa yeye ndiyo alinisababishia lile tatizo. Nilivumilia na maisha yaliendelea furaha ilirejea kwa muda mchache mpaka nilipogundua kuwa amempa mimba  mwanamke mwingine tofauti kabisa na yule wa ofisini.

Nilinyamaza tu kwani nilijua kama ningeongea ingeleta shida, ingekuwa kipigo isitoshe sikutegemea kama angekaa tu na mimi bila kutafuta mtoto sehemu nyingine, hata mimi nilitamani awe na mtoto nilitamani kulea na nilijipa moyo kama angenileteea basi ningemlea bila kinyongo chochote. Lakini haikuwa hivyo bila ugomvwi wowote bila kutegemea siku moja  tu aliniambia.

Siwezi kuishi na mwanamke ambaye hazai, nimevumilia lakini nimeshindwa, sasa hapa kwangu utakuwa unafanya nini? Kungekua na shida nyingine labda mirija imeziba tungehangaika pamoja ila huna kizazi na huwezi kupata mtoto, tutaishi hivi mpaka lini. Mimi tayari nina mtu ana mimba yangu hivyo anataka kuja kuishi humu.

Najua nimechangia wewe kuwa hivyo lakindi ndiyo ishatokea sina chakufanya, siwezi kukurudishia kizazi chako lakini pia siwezi kukudanganya kuwa sitaki mtoto, namhitajisa na na nahitaji kuwa na familia. Mimi naona tu uondoke, sinakinyongo na wewe lakini siwezi kuishi na wewe tena, siwezi kuigiza tena.

Aliongea taratibu sana, macho yake yalionyesha kuwa alikuwa anamaanisha alichokuwa akikiongea na hakuwa tayari kurudi nyuma. Nnilimuangalia mara mbili nikajua hakuna kitu ambacho ningesema kitakachoweza kubadilisha maamuzi yake. Nilijikuta nasema tu “Sawa” basi sikuonge aneno lolote, hata alipotaka kugawana mali, sijui kunipa gari na vitu vingine nilimuangalia tu.

Akili yangu nika ilifunga, sikutaka kuchukua chochote. Siku iliyofuata nilikusanya kila kitu nilichokuwa nimenunua na hela yangu na kuondoka, alijaribu kunisihi tugawane kila kitu lakini nilikataa, nilitaka kuanza maisha yangu upya bila yeye. Sasa hivi naishi mwenyewe na nina jaribu kutafuta furaha tena, sihitaji tena mwanaume najikita kwenye kazi.

Tupo kwenye mchakato wa talaka rasmi ya kiserikali, ndugu hawajui sababu lakini wanahisi tu labda yeye ndiyo alinipiiga ingawa nawakatalia. Nimeamua kumsamehe kwaajili ya amani yangu mwenyewe na namuombea Mungu furaha katika mahusiano yake mapya, namuombea mwanamke mwenzangu yasijekumkuta kama yangu na naamini kama ana akili amejifunza hawezi kupiga mwanamke tena.

Najua siwezi kuzaa lakini hiyo haimaanishi kuwa siwezi kuwa Mama, kuna watoto yatima wengi wapo mitaani wanatafuta wazazi na mipango yangu sasa ni kutafuta pesa ili nikifikisha miaka 33 niwe na nyumba yangu na maisha mazuri ya kuweza kulea watoto wawili ambao nina mpango wa ku wa ‘adopt’ kuwa wangu kabisa.

Kuhusu wanaume nadhani kwa sasa sina hisia kabisa, nikiwaona nawaona kama wanawake wenzangu tu, siwachukii lakini sina hamu nao. Sababu ya kuamua kushea maisha yangu ni ili mabinti wadogo wajifunze kuwa huwezi tu kumbadilisha mtu tabia, vumilia kila kitu ila kama anakupiga usivumilie, usiingie kwenye ndoa ukadhani unaweza mbadilisha mwanaume ni ngumu, mwanaume hubaidlika pale anapoamua kubadilika yeye mwenyewe.

Najua unapokuwa katikati ya mapenzi huoni, macho hufungwa na kujipa moyo kwa kuangalia mazuri yamwenza wako ila usiwe kipofu kuona yaliyowazi. Ana wanawake wengi unamvumilia tena anakuonyesha na haoni kama ni kitu kibaya, anakupiga unavumilia, siku akikuvunja mguu au kukupa ulemavu wa kudumu ndipo utajutia kama mimi atakucha kwakuwa hutakuwa na vigezo ulivyokuwa navyo awali vilivyomfanya akupende.

MAMBO Makubwa Mawili Yenye Nguvu Ya Ajabu Katiba Kuyabadili Maisha Yako...!!!

$
0
0

Maisha yako ili yazidi kuimarika kila wakati yanahitaji kuwa na mtiririko ambao unaeleweka kila wakati. Kama hakutakuwa na mtiririko ambao unaeleweka huwa ni sawa na kuvaa kiatu kwanza kisha  uvae soksi, hii ina maana hauna mtiririko ambao unaeleweka, na kufanya hivyo kuandaa makao ya kufa maskini.

Hivyo katika maisha yako ili uweze kuona mabadiliko kila wakati unahitaji kuwa na mambo makubwa mawili ambayo yatakusaidia kufika mbali zaidi. Na mambo hayo ni lazima uweze kuyafanyia kazi kwa ufasaha na ufanisi wa kutosha. Na mambo hayo ni;-

1. DIRA.

Dira ni alama ambayo husaidia kuonesha uelekeo hii ni kwa mujibu wa mwalimu wangu wa somo la maarifa ya jamii. Ambapo mwalimu wangu alisema dira hii husaidia kuonesha pande nne za dunia ambazo ni mashariki, kusini, magharibi na kaskazini.

Baada ya kutufundisha hivyo niligundua ya kwamba kumbe dira ni ya muhimu sana kwani inatusaidia kujua uelekeo ni wapi ambapo tunaelekea, na nikawaza kumbe bila ya kuwepo kwa dira watu wengi tungekuwa tunapotea sana.

Kwa kutumia mfano kifaa hicho hicho cha DIRA kinachotusaidia kujua ni wapi ambapo tunaelekea, nimegundua kifaa hiki ni lazima kila mwanadamu aweze kukiweka katika fikra zake ili kimuoneshe ni wapi ambapo anaelekea katika kupata mafanikio ya maisha yako na jamii kwa ujumla.

Wengi wetu hatuna kifaa hiki katika fikra zetu, wengi hatujui ni wapi ambapo tunaenda, pia wengi hatujui tunataka nini katika maisha yetu. Kutukujua ni nini ambacho tunakitaka na wapi ambapo tunaekekea huko ndiko kutojua thamani ya  "dira".

Wengi wetu tumekata tamaa kabisa, na ndio maana tukiulizana mwenzangu unataka kufanya nini kwa sasa? Ambacho kitakutoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine wengi husema mimi nitafanya chochote, bila shaka kwa muktadha huo utagundua ya kwamba bila shaka hutujuai ni kitu gani ambacho tunakitaka, kwa maneno mengine tunaweza kusema hutuna DIRA.

Najaribu kuwaza kwa sauti ni kwa nini hatuna dira ambayo itasaidia kufika mbali zaidi? Nichokuja kugundua ni kwamba hatuna dira ya maisha kwa kuwa hatujui tunataka nini katika maidha yetu.

Hivyo ni wakati mwafaka kwako kuweza kujitengenezea kifaa hicho katika fikra zako kwa kujua ni nini ambacho unataka? baada ya kujua nini ambacho unakitaka unachotakiwa kufanya ni kuwaza je! unawezaje kufika huko ambako unataka kwenda? Baada ya kupata majibu anza kuweka mipango mikakati ambayo itakufanya uweze kufika huko ambako unataka.

2. KANUNI.

Baada ya kuona jambo la kwanza ambalo ni muhimu kulifahamu, jambo la pili ambalo ni muhimu kulifahamu ni kwamba unatakiwa kuwa na kanuni za mafanikio, kanuni ndiyo msingi wa kufikia dira. Bila kujua kanuni na misingi kufikia dira ya mafanikio itakuwa ni ngumu. 

Hivyo kanuni ndiyo njia sahihi ya kupata jawabu la changamoto fulani, hivyo kama kuna changamoto ni lazima uweze kutafuta kanuni ambazo zitakusaidia kuweza kutatua changamoto.

Kwa maneno mengine tunaweza tukasema ya kwamba kanuni ndio msingi wa maisha yako, na dira ndio ukuta wa mafaniko yako.

Roma Mkatoliki Afunguka

$
0
0

Rapa staa Roma Mkatoliki ambaye ali-make headlines kwenye mitandao mbalimbali baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana na kushikiliwa kwa siku kadhaa amesema bado hajakaa sawa tangu tukio hilo ingawa analazimika kufanya kazi ili apate riziki.

Akizungumza kwenye XXL ya Clouds FM May 17, 2017 Roma amesema waliathirika zaidi baada ya vifaa kuchukuliwa kwenye Studio za Tongwe Records huku yeye akipoteza album nzima na kushindwa kurejea kwenye muziki kwa sasa kwa sababu muziki ni hisia, hivyo anatakiwa kutuliza akili kwanza kabla hajaandika wimbo.

“Hatuko poa sana, lakini lazima tutoke tufanye kazi. Tulipata madhara makubwa kwenye Studio yetu Tongwe Records, baada ya kuchukuliwa vifaa vyetu. Nimepoteza album nzima na muziki ni hisia. Hivyo mpaka nitulie ndio nitaandika ngoma nyingine. Kwa sasa naomba msupport zilizopo. Mdogo wangu Moni Centrozone ana ngoma kali ametoa, inaitwa Tunaishi nao.” – Roma Mkatoliki.

SHIRIKA la Fedha Duniani (IMF) Lamshushia Pongezi Rais Magufuli..!!!

$
0
0

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Dk Tao Zhang amempongeza Rais John Magufuli kwa jitihada zake za kupiga vita  rushwa, ufisadi  na ukwepaji kodi.

Dk Zhang amesema uchumi wa taifa lolote unategemea kwa kiasi kikubwa makusanyo ya kodi kinyume na hapo ni vigumu kufikia maendeleo.

Naibu huyo amesema ili kukabiliana na changamoto za rushwa ni muhimu vyombo na taasisi za Serikali kuwa imara na kufanya kazi kwa ufanisi.

"Najua hii ni mada nyeti kwa mataifa mengi, ila natumai wote tunafahamu namna rushwa na ukwepaji kodi vinavyokwamisha kukuza uchumi wa nchi,"amesema.

BARABARA ya Mwenge Hadi Morocco Ilojengwa kwa Fedha za Uhuru Yaanza Kuharibika..!!!

$
0
0

Rais Magufuli aliamuru Sh bilioni 4 zilizopaswa kutumika kugharamia sherehe za sikukuu ya Uhuru, ambazo zingefanyika Desemba 9, 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco yenye Kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami. Kazi lifanyika mara tu tangazo kutoka, inasemekana hata tenda haikutangazwa. Bali Mkandalasi aliingia site mara moja na kuanza kutengeneza.

Leo nlipofika Dar es Salaam Mwaka mmoja baada ya Ujenzi, Nimeshangaa Kukuta barabara ina mawimbi na imeanza kuharibika. Nmesikitika sana sema sina la kufanya.

Nlitegemea kwa kuwa ilikuwa ndo barabara yake ya Kwanza tangu awe Rais basi ingekuwa ya kiwango cha juu na Mfano kwa barabara nyingine. Kwanza alama za barabara hazieleweki. Na ndicho kilinifanya nianze kuikagua. Au bado haijakabidhiwa? Kama bado isipokelewe.

Katika Barabara za Dar es Salaam ni barabara moja tu ya Sam Nujoma ambayo nimeona angalau inakidhi haja. Naomba Rais Magufuli aendelee kutumbua Majipu hadi nchi ikae sawa. Hivi walitaka rais Magufuli ndo aingie site kusimamia Ujenzi wa barabara?

Tumechoka ubabaishaji.

UKWELI Mchungu ..Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Analima Lakini Graduates Kutwa na Bahasha za Khaki Kutafuta Sehemu za Kujitolea..!!!

$
0
0

Tuamke tukaanze Kilimo wakuu hali ni mbaya siyo lazima wote mkaajiriwa. Mimi Roho huwa inaniuma Mtu anavyotaka Sehemu ya Kujitolea bila Malipo hebu Imagine Sehemu hiyo unayojitolea vipi kama ungekua umeanzisha Kilimo cha Ekari Mbili za Vitunguu au ungekua unamiliki mgahawa kwa Pesa ulivyotumia kununulia Galaxy S7 


Si sifa Asubuhi kuvaa Kiminini na high heels au Kuchomekea shati tayari kwenda kutumwa tena bure kuna Projects ulipiga Mara Mbili Kipato cha Mfanyakazi wa Halimashauri anayeanza Kitakua Mara Mbili 

Nakumbuka mwaka 2016 Mfanyakazi wa Halimashauri mwenye Degree za Kawaida kama Uhasibu, Sheria ilikua ni 716,000/= before statutory deductions 

Hapo Piga 
NSSF= 10%
NHIF=3℅
Workers Comp=1℅
HESLB=15℅
Tax=25 Plus 14℅ ya Level 3 

Aisee huyu Jamaa anaweza Kujikuta kwa Mwaka anapokea Tsh. 6,500,000 kwa mwaka kama Mshahara 

Kuna Project sitazitaja ukizikodolea Macho unaweza kupiga Mara 3 ya hizo Pesa kwa mwaka wa 1.


Mimi mwenyewe nataka Niache Kazi tukapambane nimechoka Kutumwa.

Leo Rais Jakaya Kikwete alikua anakagua shamba lake Msoga.

BAADA ya Kuzuiwa Kuchchua Mchanga wa Madini Nnje ya Nchi..Acacia Waanza Mchakato wa Kufunga Mgodi..!!!

$
0
0

Uongozi wa kampuni ya Acacia, inayomiliki mgodi wa Buzwagi, jana ulitoa taarifa ya kupunguza wafanyakazi zaidi ya 100 wakati ikijiandaa  kufunga mgodi huo ifikapo mwaka 2020.

Meneja mahusiano wa kampuni hiyo, Nector Foya alisema kuwa taarifa ya kupunguza wafanyakazi ilitolewa baada ya meneja mkuu wa Buzwagi, Stewart Hamilton kuzungumza na wafanyakazi wa mgodi huo jana.

“Ni kweli taarifa hiyo imekuja baada mkurugenzi kuzungumza na wafanyakazi wa mgodi leo (jana),” alisema Foya.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa wafanyakazi 100 watapunguzwa baada ya kufanyika vikao mbalimbali katika wiki mbili, kuanzia jana ikiwa ni pamoja na kujibu maswali mbalimbali.

Mbali na upunguzwaji huo, taarifa inaeleza kuwa wafanyakazi hao watatoka katika idara zinazotoa msaada na huduma.

“Tutaanza mawasiliano na jamii zetu na kulenga matumizi yetu katika mradi endelevu ya jamii inayoweza kuchangia katika kuifanya jamii iweze kujitegemea baada ya 2020,” inaeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa inaeleza kuwa uchimbaji wa mgodi huo utaanza kumalizikia katika robo ya nne ya mwaka na uchimbaji utaishia mwisho wa Desemba 2017 na uchenjuaji utaisha 2020.

WAPINZANI Kenya Watishia Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu..!!!!

$
0
0

Mzozo mpya umeibuka kati ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, na vinara wa mrengo wa upinzani wa NASA kuhusu utangazaji wa matokeo rasmi ya kura za Urais.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ‘IEBC’ imeijibu mrengo wa upinzani wa NASA kufuatia vitisho vyake vya kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itafaulu kwenye rufaa iliyowasilisha mahakamani dhidi ya uamuzi wa mahakama ulioruhusu matokeo ya kura za Urais kutangazwa katika kituo cha kupigia kura.

Hii ni baada ya viongozi wa upinzani kuishauri IEBC dhidi ya kusaka njia za kubadili mipango hiyo ili kutangaza matokeo ya kura za Urais katika kituo cha kitaifa jinsi ilivyokuwa matokeo ya miaka iliyopita.

Tume hiyo kupita mwenyekiti wake Wafula Chebukati, imeeleza kuwa haitobadili msimamo wake wa kukata rufaa na kuwaambia viongozi wa upinzani kuheshimu mahakama na kutumia njia za kisheria kutatua malalamiko yao.

Viongozi wa mrengo wa upinzani wakiongozwa na Mgombea wa Urais, Raila Odinga, walitishia kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itakata rufaa na kuruhusu matokeo ya Urais kutoka kila kituo kutangazwa kitaifa.

Taifa la Kenya linatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais baadaye mwaka huu huku ushindani mkali ukitarajiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta anayewania kiti hicho kupitia mrengo wake wa Jubilee na Raila Odinga, anayebeba bendera ya mrengo wa Upinzani wa NASA.

TAKUKURU Wamuhoji Makonda Sakata la Vyeti Feki..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 18/5/2017..!!!

NAPE Azidi Kuichachafya Serikali Bungeni..Adai Mikoa ya Kusini Hawataikubali Kamwe Serikali ya CCM ..!!!

$
0
0

Mbunge Nape Nnauye ljana bungeni wakati akichangia katika  bajeti ya Wizara wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji amesema Wanakusini hawatakubali kuona ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi unakwama kutokana na vita iliyopo kati ya mataifa makubwa.

Nape Nnauye amemtaka Waziri Mwijage asikubali kuona vita ya mataifa hayo inaendelea kuwaumiza wananchi wa Kusini na kusema kama atafanya hivyo  wao hawatakubali hilo jambo.

"Mwijage viwanda ni ukombozi hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa sababu bado ni masikini sana na ukombozi wowote una vita, hasa kwa wale ambao wanafaidika na mfumo wa kutokuwepo kwa viwanda. Na hapa nitatoa mfano. Tumekuwa tukizungumza juu ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi, Kilwa pale ila taarifa tulizonazo mataifa makubwa yenye 'interest' na mbolea katika nchi hii yanapambana kuhakikisha kiwanda hicho hakijengwi. Katika jambo ambalo hatutakubaliana nalo Mwijage ni pamoja na hili, kuruhusu vita hii iendelee kutuumiza wanakusini" alisema Nape Nnauye 

Nape Nnauye aliendelea kusisitiza

"Mataifa hayo yanapigana kwa maslahi yao na kama serikali mtayumba kwenye hili basi Wanakusini hatutokubali, tulishalizungumza, mlishakubaliana, mwekezaji alishapatikana na utaratibu uko wazi, sasa vita hii ya wakubwa isituumize sisi wakapiganie nje ya Lindi lakini tunakitaka kiwanda cha mbolea Lindi" alikazia Nape Nnauye 
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images