Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Kosa Kubwa Ni Kumuoa Huyu Mwanamke

0
0

Hii siyo habari ya kutunga ni ukweli ninaoupitia katika maisha yangu.

Ilikuwa mwaka 2010 nilipotoka kwetu Nyegezi Mwanza kwenda Mbeya kikazi, ilikuwa ni kazi ya miezi miwili tulifikia katika hotel ya Mt. Livingstone. Wiki la pili tulitakiwa kuwa Kyela kwa ajili ya kazi kwa wiki nzima ambapo tulifikia Matema Beach hotel. Tulifanya kazi zetu kila siku asubuhi hadi mchana na tulipumzika hadi kesho yake.

Siku moja jioni tukiwa tumejipumzisha alitokea binti pale akawa amekaa akinywa vinywaji, ni binti mzuri sana ambaye ngozi yake ilikuwa kama chocolate mweupe kiasi, alikuwa amejazia vizuri sana na akionekana mwenye furaha na mzuri sana. Nilijisogeza karibu na kuanza kupiga naye story huku tukinywa vinywaji visivyo na kileo.

Tulitambulishana na hatimaye kubadilishana namba za simu. Tulichat mara kwa mara hasa mida niliyokuwa nimetulia. Binti alisema yeye amesoma mambo ya uhasibu lakini bahati mbaya hakuwa amepata kazi. Siku ya mwisho kufanya kazi pale Kyela alikuja tena jioni tulikunywa vinywaji na chakula cha usiku na kuagana. Niseme tu kweli kuna wanawake ni wazuri jamani siyo mchezo. Nilitamani sana ningepata muda wa kuwa naye lakini mazingira hayakuruhusu.

Niliporudi Mbeya mjini niliendelea na kazi zilizotuleta kwenye mkoa huu wa baridi, huku nikiendelea kuwasiliana na huyu mwanadada hatimaye nikamualika aje Mbeya siku moja. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Jumamosi ambapo aliamkia safari kuja na kufika saa nne asubuhi alikuwa amefika, nilipokea na tukawa pale hotelini. Tulishinda siku nzima pale tukipiga story na kubadilishana mawili matatu. Ilipofika mida ya jioni tulienda kupasha kwenye kauwanja flani wanacheza mpira wa mikono karibu na TRA.

Yeye alikaa tu na kuniangalia baadaye tukarudi wote na kuingia hotelini. Nilioga nayeye akaoga kisha tukala chakula na kulala. Usiku ule ulikuwa wa ajabu sana, msichana huyu alijua sana mapenzi jamani aliniacha asubuhi akarudi Kyela nikiwa mwepesi na mlaini sana kiasi hata kwenda kutubu dhambi kanisani nilishindwa.

Penzi likakolea na kunoga, hata niliporudi Mwanza alikuja kama mara tatu hivi hatimaye tulioana kwa ndoa kubwa ya mbwembwe sana. Siku hiyohiyo ya ndoa usiku tuliporudi ndani nilishituka sana kwani nilimuona kama hana amani akiwa amekaa kimya, nikamuuliza kuna tatizo akasema hakuna yupo kawaida. Hali hii iliendelea, akawa anakaa kimya kununa hata kwa wiki nzima bila sababu kabisa. Ukimuuliza hasemi chochote anajibu kwa kifupi tu hakuna tatizo.

Kwakweli ghafla nilikuwa nimeingia kwenye tundu la simba bila kujua kwani ilikuwa kununiwa mwanzo mwisho, hakuna amani na furaha kabisa ndani, maneno makali. Nilijitahidi sana kujitathimini wapi nimemkosea na kujikuta sioni popote huku yeye akisema hakuna kitu. Ulifika wakati nikamwambia naomba nikupeleke nyumbani ukapumzike utarudi ukiwa okey alikataa katakata.

Mpaka leo hii tuna watoto wawili ndoa yangu na mke wangu huyu ni mateso tu. Tumekaa vikao vya familia sana akiulizwa anasema simtunzi wakati nimefungulia supermarket ya ukweli tu pale jijini kati na nimemwambia be free hakikisha biashara yako haifi, tunza ndugu zako na wewe mwenyewe.

Vikao vyote mpaka kwa wachungaji havijmsaidia kitu. Namuona kama simba ndani, hakuna amani kabisa. anaweza kucheka sana na rafiki zake lakini wakitoka tu anabadilika rangi kama simba, sina tena hamu ya tendo la ndoa na yeye nimekuwa mtu msongo wa mawazo sana hamu ya ngono muda mwingi imepotea.

Siku ambazo nimekuwa ninahamu kali ya kufanya mapenzi nimekuwa nikiteseka sana, hali hii imeniletea tabia mbaya sana maana hali hii ikinitokea nikiwa safarini nimekuwa nikilala sana na watoto wa mapokezi kwenye mahotel ninayofikia. Mfano nikienda Dar hotel yoyote kubwa nikifikia nikimkuta binti mapokezi huyo imekula kwake, usiniulize huwa unawapataje hawa kila mtu na ujanja wake.

Sina hamu kabisa ya kufanya naye mapenzi kwa vile ni kama mmekaa maadui na hali hii imetokea baada ya tabia yake kuzidi kuwa tishio. Sitaki kuwa na mchepuko pamanenti wala demu pamanenti niko radhi nilale na mdada ninaye mpenda na nimlipe kisha baada ya hapo tuachane.

Sasa nimechoka haya maisha, nimeamua niache kazi na nitoroke niiache familia yangu. Watoto wote nimewafungulia akaunti na zina pesa za kutosha kusoma mpaka chuo kikuu kwa kila mmoja na maelekezo ya kuzitoa ni hivyohivyo mpaka watakapomaliza shule. Nataka nikimbilie Zanzibar nikajaribu kuanza maisha mapya huko bila wao kujua. Nitabadili kila kitu na nisipatikane kabisa kwa ndugu wote.

Wanawake wa wengine ni simba waliovaa ngozi ya kondooo hawafai kwa ndoa.

 

Mbwana Samatta Aihamishia Mazembe Ubelgiji

0
0

Ubelgiji .Wakati mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe, Mbwana Samatta akitamba na Genk, klabu ya Standard Liege imebadilisha uhamisho wa mkopo wa wachezaji watatu wa TP Mazembe na kuwasajili kwa mkataba wa kudumu.

Samatta alinunuliwa na Genk akitokea Mazembe mwaka jana amekuwa mwenye mafanikio katika klabu yake jambo lililowavuta mabingwa wa Ubelgiji kujitosa DR Congo kuchukua nyota wengine.

Jonathan Bolingi, Merveille Bope na Christian Luyindama wote wamejihakikishia maisha katika klabu ya Standard Liege.

Nyota hao watatu walijiunga na klabu hiyo ya Ubelgiji kwa mkopo wa muda mrefu wakitokea kwa mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika,  TP Mazembe, lakini sasa umekuwa uhamisho wa kudumu.

Mshambuliaji Bolingi (22), amecheza mechi 10 za timu ya taifa DR Congo 'Leopards' na amecheza michezo sita akiwa na Standard.

Kiungo mzoefu Bope (24), amecheza mechi mbili, lakini ameichezea timu ya taifa ya DR Congo mechi nane.

Beki Luyindama (23), amecheza mechi tano na mabingwa hao wa Ubelgiji na kufunga bao moja.

Hizi Ndizo Timu 3 zilizoshuka Daraja Msimu huu...Yanga Rasmi Bingwa

0
0

Ligi kuu Tanzania bara imemalizika Leo jioni Yanga ikitangazwa Rasmi kuwa Bingwa

Hizi Ndizo Timu 3 zilizoshuka Daraja Msimu huu...

JKT Ruvu
Toto Africans
African Lyions

MREMBO Auawa na Kuzikwa Kama Mbwa....

0
0

Dada mrembo kutoka Kenya Nairobi Claire Njoki Kibia aliyekuwa akifanya kazi ya ujambazi Kwa kutumika ktk kutega wanaume na wakati mwingine yeye mwenyewe kwenda frontline, ktk kufanya ujambazi, aliuawa mapema wiki hii na kuzikwa Kama mbwa. 

Mrembo huyo alisumbua Sana enzi za uhai wake, hakuna mkenya ambaye hakuwa anajua habari za Claire.

Inadaiwa marafiki zake wengi waliogopa kwenda Kwa hofu ya kukamatwa na police maana rafiki zake wengi ni majambazi Sugu.

Inasemekana hata waliohudhuria msiba huo hawakuwa na uchungu wowote na wengi walikuwa majirani. 

Mara baada ya mazishi ,baadhi ya waombolezaji ambao walisemekana kuwa ni majambazi wenzake na Claire walikamatwa na askari kanzu waliokuwa pale msibani wakijifanya Kama waombolezaji wengine. 

"Laleni chini au la tunawapiga risasi "
Police mmoja aliyekuwa kavaa kiraia alisikika akitoa amri huku akiwa kawanyoshea bastola watuhumiwa.

JPM Akabidhi Rasmi Kofia ya Uenyekiti EAC kwa Rais Museveni..!!!

0
0

Rais John Magufuli leo (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni.

Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia madarakani.

“Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana.

Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake.

“Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema.

Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu na uwezo wake wote.


WATOTO Wawili Wafa Maji Tanga..Walidumbukia Kwenye Dimbwi la Maji ya Mvua Yaliyotuama..!!

0
0

Watoto wa wawili wa familia moja  wa kijiji cha Moa wilayani Mkinga, mkoani hapa, Kijiti Mohamed na Omari Maazizi (10) wamekufa maji baada ya kuzama katika dimbwi la maji ya mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia jana.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema kuwa watoto hao wamekufa maji leo (Jumamosi) mchaka katika kitongoji cha Mwakamba.

Wakulyamba amesema aliyeanza kuzama ni Omari ndipo dada yake akaamua kwenda kumuokoa ambapo hakuweza kufanikiwa, wakazidiwa na

kunywa maji yaliyosababisha kukosa pumzi hivyo kupoteza maisha.

“Watu waliokuwa karibu waliwatoa na kujaribu kuwapa huduma ya

kwanza lakini hawakuweza kufanikiwa sababu walishakuwa

wamekufa,”alisema Wakulyamba.

Ofisa elimu ya Sekondari wa Wilaya ya Mkinga, Omari Kombo amewataka

wazazi kuwa waangalifu kwa watoto katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha kwa sababu maeneo mengi yameharibika.

SBL yazindua bia mpya iitwayo Serengeti Premium Lite

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (wa kwanza kulia) akimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika hafla ya uzinduzi wa bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta pamoja na mjumbe wa Bodi ya SBL, Christopher Gachuma wakishuhudia uzinduzi huo.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi, Mjumbe wa Bodi ya SBL, Christopher Gachuma na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta wakionesha bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' mara baada ya kuzinduliwa bia hiyo itauzwa kwa shs 1500/-.
Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (wa kwanza kulia), Mjumbe wa Bodi ya SBL, Christopher Gachuma (katikati) na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta wakionja bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' mara baada ya kuzinduliwa.
Duh...inaradha ya kuvutia eehh! Meza kuu ikifurahia mara baada ya kuonja bia hiyo.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiwakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi amezinduwa bia mpya ya Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), inayojulikana kama 'Serengeti Premium Lite'.
 
Akisoma hotuba ya Waziri Mwakyembe katika uzinduzi huo, Bi. Kihimbi alisema wizara inaipongeza kampuni ya SBL kwa kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania yaani jina la Hifadhi ya Taifa Serengeti kupitia bia yao. Alisema Bia mpya ya Serengeti Premium Lite iliyopikwa kisasa iliyozinduliwa na SBL inaendelea kulitangaza hifadhi ya Serengeti hivyo kuwataka wananchi wapenzi wa kinywaji hicho kuitumia ili kutangaza nchi.
 
“Programu za jamii zinazoendeshwa na SBL katika sekta ya elimu, kilimo na ujasiriamali zimewezesha vijiji vingi hapa nchini kupata maji safi, watoto kupata elimu ya juu na mamia ya wakulima kupata masoko kwa ajili ya kuuza mazao yao ambapo SBL hununua mazao yao kama malighafi inayotumika kuzalishia bia,” alisema Mwakyembe.
 
Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta alisema SBL, ikiwa ni mojawapo ya kampuni kubwa zinazozalisha bia hapa nchini, imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa ni muendelezo wa bia mama ya Serengeti Premium Lager iliyoko sokoni kwa zaidi ya miaka 20.
 
“Bia ya Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa namna ya kipekee kwa kutumia utaalamu wa kisasa wa uzalishaji bia. Ina ladha kamili inayoburudisha zaidi ya bia za aina ya lite ambazo kwa sasa huuzwa reja reja sokoni,” alisema Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa kwa Sh.1,500 kwa chupa na kwamba inatarajiwa kuteka soko na jumuia ya wanywaji wake ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitafuta bia halisi ya Kitanzania. “Pamoja na kuwa na furaha kubwa usiku huu ambapo tunashuhudia uzinduzi wa biaya Serengeti Premium Lite, niseme kuwa ni bia halisi ya kitanzania yenye kiburudisho na ladha nyepesi.
 
Huu ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii kwa muda mrefu. Tuna amini kuwa bia hii ya Serengeti Premium Lite, ambayo imebuniwa na kutengenezwa na wazalishaji bia (bremasters) wa kitanzania kwa watanzania, itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri watakapo kuwa wakifurahia urithi wetu wa aina hii ya bia”, alisema Mehta.
 
Aliongeza kuwa, “Bia ya Serengeti Premium Lite ina ubora ule ule wa kimataifa sawa na bia mama ya Serengeti Premium Lager ambayoimepokea zaidi ya medali 10 za ubora wa kitaifa na kimataifa.”

Mjumbe wa Bodi ya SBL, Christopher Gachuma (kulia) akifurahia bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki katika hafla ya uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Masoko, Ceaser Mloka (wa kwanza kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kuzungumzia uzinduzi wa bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite'. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa SBL, Anitha Msangi  na Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta.

Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (kushoto) kwenye uzinduzi rasmi wa 'Serengeti Premium Lite'.

Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi (wa kwanza kulia) akigonganisha glasi na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti, John Wanyancha (kushoto) mara baada ya kuzinduliwa.

Wageni mbalimbali wakionja na kufurahia bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' mara baada ya kuzinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Wageni mbalimbali wakionja na kufurahia bia mpya ya 'Serengeti Premium Lite' mara baada ya kuzinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Watanzania 11 Watiwa Mbaroni Afrika Kusini Wakituhumiwa Kumbaka Mwanamke Mjamzito

0
0
Wanaume 11 ambao ni raia wa Tanzania wamekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani wiki hii Johannesburg Afrika Kusini .

Radio na Mtandaoni Johannesburg wiki hii kumeripotiwa kuwa kosa lililofanya Wanaume hao 11 kukamatwa na Polisi ni kumbaka Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 22 aliyekua akitoka kazini saa kumi na moja alfajiri.

Mwanamke huyo alikua akitoka kazini na Mfanyakazi mwenzake ambaye ni Mwanaume ambapo ghafla walivamiwa na kundi la Wanaume wenye silaha za moto na wakamvuta Mwanamke huyo kabla ya kumpiga Mfanyakazi mwenzake ambae baadae alifanikiwa kutoroka.

Baada ya Mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu Polisi na wakafanikiwa kuwahi eneo la tukio na kukuta Wanaume hao wakimbaka kwa zamu Mwanamke huyo mwenye ujauzito wa miezi mitatu.

Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo tukio lilikofanyika na kumuokoa Mwanamke huyo aliyekua kwenye hali mbaya ambapo walimpeka Hospitali huku Watuhumiwa wakichukuliwa na kupandishwa Mahakamani siku ya Jumatano.


Alichoandika Manara Baada ya Ubingwa wa Yanga na Kuhusu FIFA

0
0
Saa kadhaa baada ya Yanga kukabidhiwa kombe kama Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2016 – 2017, Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano Simba Haji Manara ameamua kuwakumbusha Yanga kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

May 20, 2017 Haji Manara ametumia ukurasa wake kuwaeleza Yanga kuwa Simba hawajakata tamaa kuhusu kudai Point zao 3 walizokuwa wamepewa na baadae kupokonywa kwenye ishu ya mchezaji aliyecheza akiwa na kadi tatu za njano, huku akisisitiza kuwa Yanga watalipeleka Kombe msimbazi kwa magoti…
”Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa mmenielewa,,soon tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA.
“Hivi unadhani FIFA wana figisu guys? kadi tatu za njano ni kukosa game inayofuata tu no way out!! ukizingatia reppti za mwamuzi na kamisaa na bodi inayosimamia ligi, sasa mjiandae kisaikolojia kulileta kombe kwa magoti! @Yangasc @simbasctanzania” – Haji Manara


Sababu za Issa Makamba wa Serengeti Boys kurudishwa Tanzania

0
0
Tumepata nafasi ya kuongea na Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas akiwa Gabon kuhusiana na nahodha wa timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys Issa Abdi Makamba.

Makamba akiwa mazoezini aliumia siku tatu kabla ya kuanzia kwa mashindano ya AFCON U-17 hivyo jina lake likaondolewa katika orodha ya Wachezaji wa Serengeti Boys watakaoshiriki michuano hiyo japokua aliendelea kubaki kambini na timu.

Taarifa za uhakika ni kwamba leo amerudishwa Tanzania licha ya kuwa awali viongozi walisema atakuwa na wenzake hadi mwisho wa mashindano, ni nini kilichofanya arudishwe Tanzania? afisa habari wa TFF Alfred Lucas ameongea haya:

“Ni kweli amerejea nyumbani na kilichofanya arudishwe ni sababu kuu mbili za Madaktari watatu, CAF walileta mchezo mmoja Port Gentil na yeye kwa hali yake haipaswa asafiri hivyo inakua kama kumsumbua zaidi” 

‘Sababu nyingine ni kwamba anapoendelea kubaki na Wachezaji wenzake na kuhudhuria mechi akiwa benchi inazidi kumuumiza zaidi sababu anatamani angekua anacheza, Madaktari wameshauri arudishwe tu Tanzania’

Majasusi wa Marekani CIA Wauwawa na China

0
0
Gazeti la New York Times limeripoti kuwa China, imewauwa au kuwafunga jela majasusi kati ya 18 au 20 hivi wa CIA, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kulemaza kabisa shughuli za Marekani za kuichunguza China.

Afisa mmoja mkuu wa Marekani ameliambia gazeti hilo kuwa, hiyo ni mojawepo ya ukiukaji mkubwa wa usalama, kwa miongo kadhaa na kufananishwa na usaliti wa kutoa siri kwa Urusi na Aldrich Ames (wa CIA) na Robert Hanssen (wa FBI).

Baadhi ya watu sasa wanadhani kuwa China, ilidukua mfumo wa mawasiliano wa CIA, ambayo hutumiwa katika mazungumzo ya kisiri.

Lakini kunao wengine wanaoamini kuwa, mdukuzi alisambaratisha kizuizi cha siri cha wapelelezi wa Marekani, mnamo mwaka 2010.

Majasusi hao walianza kutoweka mmoja baada ya mwingine, kuanzia mwanzo wa 2011 (huku mmoja wao akipigwa risasi mbele ya wenzake katika eneo la kubarizi, kwenye jumba la serikali).
Idara ya ujasusi CIA, imekataa kuzungumzia swala hilo.

Halima Mdee Awapa Somo CCM

0
0
Mbunge Halima Mdee leo akiwa bungeni amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi vijana hata wale watu wazima lakini hawana muda mrefu bungeni wasome vizuri Ilani ya Uchaguzi ya CCM na mpango wa maendeleo kabla ya kusimama bungeni na kuanza kutoa sifa.

Halima Mdee amesema hayo bungeni leo wakati akichangia katika bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi baada ya wabunge wengi wa Chama Cha Mapinduzi kusimama na kuanza kusifia Wizara hiyo kuwa imepiga hatua baada ya kufuta tozo nyingi jambo ambalo Halima Mdee anasema ni jambo dogo sana ukilinganisha na changamoto ilizonazo Wizara hiyo ambayo kila mwaka imeonekana kushuka katika sekta ya kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa taifa.
Kufuatia jambo hilo Halima Mdee amewataka wabunge wa CCM kusoma vizuri Ilani ya Uchaguzi waone inasema nini na inataka nini lakini pia wasome na mpango wa maendeleo ili kuona changamoto ambayo Wizara hiyo inayo.

"Nimeona wabunge wengi vijana hata wale watu wazima wakisimama na kutoa pongezi kwa Waziri kisa tu amepunguza tozo, lakini ndugu zangu tozo pekee ni kitu kidogo sana lakini hata Waziri alitumia muda wake mwingi jana kuhusiana na tozo tu, ndugu zangu Wabunge wa CCM mkasome vizuri Ilani ya Uchaguzi ya CCM, mkasome na mpango wa maendeleo, hapa hatutafutiani ubaya kwani mafanikio yenu nyinyi ndiyo mafanikio yetu sisi pia, kwa hiyo tusichukiane tunasema haya kwa dhamira njema, ukichukua kitabu cha Wizara ya Kilimo na kile cha Wizara ya Viwanda haviendani yaani ni kama mbigu na dunia" alisema Halima Mdee

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo

Wadada Hivi Mnaenjoy Kubambiwa Kwenye Mabasi ya Mwendokasi au?

0
0
Leo nimeshuhudia kitendo ambacho hadi sasa nahisi kuchanganyikiwa. Nimepanda mwendokasi natoka Kariakoo kwenda Ubungo kiti chanyuma. Magomeni kaingia mtoto mzuri hatari alafu ana shepu balaa tako, hips hatari kavaa suruali na kitop nyuma mgongo uko wazi mabegani. Mlangoni kuna jamaa kasimama kaegemea chuma. Msichana kaingia kasimama kampa jamaa mgongo walah! Vituo viwili mbele naona jamaa Kahama kabisa hata haegemei chuma kamuegemea msichana mgongoni.

Nimekaa nacheki tu mchezo. Kituo kinachofuata kuna abiria wakashuka, msichana ikabidi atoke nje kupisha abiria wapite mlangoni kisha kaingia ndani akapitiliza ndani mbali na aliposimama jamaa mlangoni. Jamaa kuona msichana anapitiliza ndani naye kafuata nyuma. Msichana kaegemea kwenye viti jamaa kawahi nyuma yake kaegemea mgongo zero distance. Gari inavyozidi kwenda jamaa naona anazidi kuegemea nikiangalia mikono jamaa kashika chuma inatetemeka jicho jekundu.

Msichana anageuka nyuma kumcheki jamaa na kujaribu kugeuka kidogo jamaa nae anageuka nae mgongoni. Nikimcheki jamaa kawa kama hajitambui kabisa na kibaya zaidi msichana yuko kimya anageuka shingo kidogo alafu anakaa kimya. Kufika Ubungo msichana akashuka na mimi ndo nikawa nashuka ghafla yule jamaa kama kazinduka naye akashuka. Sasa mimi niko nyuma ya yule msichana naona anapitisha mikono nyuma kama kujikagua kama kachafuka au la. Nikamcheki karudia mara kadhaa kiaina anapitisha mikono nyuma anafutafuta hivi huku anaondoka.

Kumcheki yule jamaa namuona kaenda upande wa pili anasubiri gari la kurudi town. Nikashangaa huyu jamaa kapanda gari toka Kariakoo kafika Ubungo anasubiri gari tena la kurudi town? Mhh. Kitu kinachonishangaza ni yule msichana, bonge la msichana ana ngozi ya shombeshombe hivi na bonge la shepu nilivyomfatilia niligundua ni mwanafunzi wa Dar nimeshangaa imekuwaje anabakwa hivi hivi na anakaa kimya mwishowe anaishia kujikagua kama kachafuka au vipi. Alafu jamaa mwenyewe aliyekuwa anambaka ni jamaa moja wa hovyo hovyo kama mlevi wa mataputapu.

Au wakina dada huwa mnapendaga kubambiwa hivi kwenye mabasi? Na unahisi kabisa kuna mtu nyuma yako na dudu kasimamisha kwenye bonde lako la ufa.

Source:JF

Amber Lulu ni Mpenzi Wangu Kabisa Najilia Bure- Harmorapa

0
0
Msanii Harmorapa amefunguka na kusema hakumlipa Amber Lulu ili wapige picha bali walikuwa pamoja sehemu ambapo matukio hayo yalitokea kwa kuwa wao ni watu wa karibu sana

Harmorapa anasema kuwa hakuwa na sababu ya kumlipa msanii huyo kwa kuwa wao ni wapenzi , hivyo walipiga hizo picha wakiwa katika mambo yao ya kawaida yanayowakutanisha.

"Amber Lulu mimi sijamlipa kwanza na wala sikumtafuta ili kutengeneza kiki, bali nilikutana naye katika mazingira tofauti, mimi Amber Lulu ni mtu wangu (mpenzi wangu)" alisema Harmorapa



KUTANA NA SHEKH SHARIFU SIMBA Mtabibu wa Nyota na Tiba za Asili Tanzania na Duniani Kote

0
0

KUTANA NA SHEKH SHARIFU SIMBA mtabibu wa nyota Tanzania na duniani kote,

✨SHEKH SHARIFU SIMBA anatoa shukrani kwa wote mnaopiga simu mlioko ndani na nje ya Tanzania, wanatoa shukrani na wale wenye matatizo, pia anawashukuru wote wanaomshirikisha na kutoa shuhuda jinsi tiba zake zinavyo wasaidia.
✨Bado ujachelewa piga simu na uweze kusaidiwa, SHEKH SHARIFU SIMBA yupo kwaajili ya kutatua matatizo yote yanayo wakabiki wanadamu,

🦅SHEKH SHARIFU SIMBA ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili anatumia kitabu cha QUR'AN, dawa za asili, dawa za kiarabu na majini,

✨je umeachwa na Mme/ mke, mchumba au umpenzi wako? SHEKH SHARIFU SIMBA anauwezo wa kurejesha mahusiano yako ndani ya masaa (72)
✨je umahangaika kupata mtoto bila mafanikio?
✨je mikosi inakuandama na umekuwa mtu wa kilia kila siku bila kupata msaada wowote?
✨je madeni yanakuandama?
✨je umesimamishwa kazi au kushushwa cheo bila sababu? SHEKH SHARIFU SIMBA anatoa kisomo na kusafisha NYOTA na kung'arisha, ili ung'ae upya kwa kila mtu na mahali popote,
💍SHEKH SHARIFU SIMBA anatoa Pete za bahati zilizoambatana na jini Mali,
✨Anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume chango kwa kina mama, ngizi na n.k, pia anatibu miguu kuuma na kufa ganzi, tumbo kujaa gesi na kuunguruma na magongwa mengine ya siri,
🇺🇸pia anatibu kwa njia ya simu kwa wale walioko mbali au nje ya nchi,
📞SHEKH SHARIFU SIMBA anapatikana BAGAMOYO, kwa wale walio nje ya nchi tumia WhatsApp no +255 719361792, kwa wale wa ndani ya nchi piga simu no: 0719-361792 au 0689-476132 na 0745-281712.

Huu Ndio Utapeli wa "Prophet Bushiri" Anayemtishia Lowassa Kuwa Atakufa

0
0
Nilisikiliza Madai ya Askofu Gwajima Dhidi ya Tapeli mmoja aitwaye Prophet Bushiri. Jinsi ambavyo anatumiwa Kutabiri ati Lowassa atakufa.
Wasichojua watu wengi Ni kuwa Wengi wa wanaoitwa Watumishi wa Mungu, Kiasi kikubwa ni Mbwa mwitu Matapeli wa Kutisha.

Nitaweka Mambo Kadhaa ya Kitapeli anayofanya Bushiri. Mojawapo ni Kujifanya alitabiri kuhusu Tetemeko, hawa wanachofanya ni Kungojea Tukio kubwa linatokea, halafu wanatengeneza Video inayoweka sauti yake juu ya Video nyingine ya zamani kabla ya Tukio na Wanasuparimpose maneno mapya (lipsing) juu ya hiyo video ya zamani ili isikike kana kwamba alikuwa akitabiri Tukio hilo, ilihali katika video ya awali, alikuwa akiongelea mengine kabisa!

Mengine ni Kutengeneza Mazingaumbwe ya Michezo ya Kitoto mfano kama huu. Bushiri akijifanya anashusha moto toka mbinguni Kuchoma hirizi. Ukweli ni kuwa ameweka kemikali yenye kutoa moto na akaongezea kiberiti juu yake ili kikipata joto la kemikali kilipoke moto!


Angalia kwa makini.

Na hii Video nyingine anachukua Video ya Zamani ambayo watu walikuwa wakiomba, anaiedit na kusema wanaona Malaika halafu ukisikiliza jibu analopewa ni la mtu wa studio maana halaiki ya watu wale haikuwa naye wakati akiongeza hiyo sauti mpya na ukungu wa malaika.



Sasa Ukiona Mtu anaweza Kudanganya Maelfu ya Watu Kiasi hiki, Hata kuua mtu hatasita! Nimemsikia Katika Video Fulani akisema alimwombea Mchungaji mmoja afe, na akafa sasa, ni wazi Tapeli wa Aina hii anaweza hata kumtumia mtu Majambazi ili wamuue kisha ajidai Utabiri wake umetimia




Gwajima asidanganyike Bushiri haombei afe, Bali Bushiri anaweza hata Kumtumia Majambazi! Gwajima.

Samatta azidi kuwika KRC Genk

0
0

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza vizuri kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Lokeren Uwanja wa Daknam mjini Lokeren, Ubelgiji kwenye mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League mwakani.

KRC Genk walitangulia kwa bao la penalti la kiungo mkongwe wa umri wa miaka 33, Mbelgiji Koen Persoons aliyejifunga dakika ya nne, kabla ya mshambuliaji mwenye umri wa miaka 31, Mbelgiji pia Tom De Sutter kuisawazishia Lokeren dakika ya 57.

Pamoja na sare hiyo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B katika mchuano wa kuwania tiketi ya Europa League mwakani kwa kufikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi tisa na Samatta jana ameichezea Genk mechi ya 58 tangu ajiunge nayo Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC akiwa amefunga mabao 19.

Kati ya mechi hizo 58, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 40 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 36 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 26 msimu huu.

Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu uliopita.

Kikosi cha Lokeren kilikuwa: Verhulst, Skulason, Single, De Sutter/Enoh dk65, Terki, Huppert/Rocketman Stra dk76, Ticinovic, Rassoul/Martin dk63, Miric, Knight na Monsecour.

KRC Genk : Ryan, Nastic, Wouters, Seigers, Castagne, Berge, Kumordzi/Heynen dk61, Sabak/Writers dk76, Naranjo, Buffalo/Vermijl dk45 na Samatta.

Saimon Msuva Tena.......

0
0

Kiungo wa Yanga Saimon Msuva amefanikiwa tena kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kufikisha mabao 14 yaliyosaidia kwa kiasi kikubwa timu yake kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo.

Msuva ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliocheza kwa kujituma zaidi msimu huu amefanikiwa kuwakimbia wenzake waliokuwa wakimfukuzia kwa karibu nafasi hiyo ambao ni Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting aliyebaki na mabao 13.

Wengine ni Shiza Kichuya wa Simba, Obrey Chirwa wa Yanga na Mbaraka Yusuph ambao wote wamebaki na mabao 12 kila mmoja.

Msuva ni sehemu ya safu kali zaidi ya ushambuliaji msimu huu ambayo ndiyo iliyofunika katika upachikaji mabao ikiwajumuisha Obrey Chirwa, Amis Tambwe na Donald Ngoma ambao pamoja na wengine wameifanya Yanga ipate ubingwa msimu huu kwa tofauti ya mabao licha ya kulingana point na wekundu wa Msimbazi Simba.

Yanga imemaliza ligi ikiwa na mabao 43 ambayo ni tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakati Simba ikiwa na mabao 33 kama tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, na hivyo kuipiku Simba kwa jumla ya mabao 10 ya kufunga.

Hii ni mara ya pili kwa kiungo huyo machachari wa pembeni kuibuka kinara wa ufungaji katika ligi hiyo, ambapo katika msimu wa 2014/15 aliibuka pia mfungaji bora.

Tofauti na misimu iliyopita, katika msimu huu, wachezaji wa kitanzania wamefanikiwa kufanya vizuri katika ufungaji, kwani katika wachezaji watano waliofanya vizuri zaidi, ni Obrey Chirwa pekee ndiye mchezaji wa kigeni aliyepenya katika orodha hiyo.

Riyama Alia na Umaskini wa Bongo Movies

0
0

Msanii wa bongo movie Riyama Ally amefunguka na kusema licha ya kufanya kazi ya filamu kwa miaka zaidi ya 15 lakini hajapata mafanikio yale ambayo watu wanategemea angekuwa nayo kutokana na uwezo wake wa kuigiza.

Rihaya Ally alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live na kusema hakuna kitu kinaumiza kama unapofanya biashara na kulipa kodi halafu mshindani wako ambaye anafanya biashara hiyo hiyo anafanya mambo kinyume halipi kodi, kazi yake ni kufyatua tu filamu na kuziingiza sokoni.

"Kikawaida changamoto katika biashara ni nyingi na hakuna biashara ambayo haina leseni au haulipi kodi, na kikawaida kila jambo linafanyika katika misingi ya sheria hatuwezi kufanya kitu kinyume cha sheria, kwa hiyo sisi tunalipa kodi halafu wenzetu inakuwa tu wanafyatua filamu bila kulipa kodi, hiyo inaumiza sana sababu mimi nipo kwenye game kwa zaidi ya miaka 15 sina baiskeli, sina bajaji, sina gari sina chochote" alisema Riyama Ally

Mbali na hilo Riyama Ally anasema wasanii wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na mambo kama hayo, ila anawataka wasanii wa bongo kujipanga na kutengeneza filamu ambazo wananchi wanazihitaji na kusema kuzuia filamu za nje zisiingie ni jambo la ajabu

"Kutokana na mambo hayo hayo wasanii wengi wanashinda kufanikiwa lakini kama wenzetu wangekuwa wanalipa kodi kama sisi basi hakuna tatizo, kama ukiwa msanii mzuri na unakidhi mahitaji ya jamii huwezi kuhofia kazi za nje maana hizo ndiyo kioo chetu sisi, wenzetu wametutangulia sana inabidi tujifunze kupitia wao, kwa hiyo zinatakiwa kuendelea kuingia lakini kwa kufuata utaratibu ili na kazi zao nao zilipiwe kodi nchini" alisisitiza Riyama
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images