Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

TRUMP Adhihirisha Ubabe Wake Mbele ya Mfalme wa Saud Arabia..Azikataa Taratibu na Protoko Alizoandaliwa na Wenyeji Wake..!!!

$
0
0

Katika ziara itakayomoeleka Donald Trump katika mataifa kadhaa matano kuanzia Saud Arabia mpaka Brussels, Jerusalem ikiwamo imeonekana kupokelewa kwa mtazamo tofauti ukilinganisha na msimamo wake juuya uislamu na namna Saud Arabia ilivyompa heshima ya hali ya juu hasa wengi wakiilinganisha na ziara ya Obama aliyoifanya mara ya mwisho akiwa madarakani. 

Mambo yaliyoteka mijadala mitandaoni ni pamoja na 

Heshima Trump anayoonekana kuipata kutoka kwa taifa la Saud Arabia kuanzia kwenye mapokezi ambayo Obama hakuwahi kuyapata.

Kitendo cha Trump kumuweka mwanamke kama translater wa mazungumzo yao na mtazamo wa Arab kuhusu uhusika wa wanawake katika masuala nyeti katika jamii.

Swala la Melanie Trump kutokuvaa head scarf kama ilivyozoeleka kwa Hillary Clinton, Condoleezza Rice na Michelle Obama pamoja na staff wao waliokua wakivaa head scarfs kuenzi utamaduni wa Arab

Msisimko wa mji wa Riadh katika ziara hii ya Donald Trump ambapo wananchi wa Saudia wameonekana kuvutiwa na kumpokea Mr President kwa upendo bila kujali misimamo ya Donald Trump kuhusu Uislamu ambayo ndio dini ya Saudis

KWA Mwendo Huu Ninamhurumia Maalim Seif na CUF Zanzibar!..!!!

$
0
0

Mzee Kikwete hupenda kusema, ‘’akili za kuambiwa, changanya na zako’’.

Maalim Seif na wapambe wake wa Zanzibar walikubali akili za kuambiwa lakini hawakuchanganya naza kwao.

Maalim Seif hakufahamu kuwa washauri wake wakubwa ni CCM B ambao hawakumtakia mema na kama alifahamu basi alitakiwa achukue ushauri wao na kuchanganya na akili zake.

Kama angechanganya na akili zake kwa sasa CUF isingekuwa katika hali iliyopo kwa sasa. CUF ya kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015 sio hii ya leo ambayo inagawana vito kila siku.

Kwa sasa amezunguka dunia nzima akipiga kelele kuhusu kuibiwa kura huku akiwaaminisha wapambe wake yuko mbioni kuingia Ikulu ya Zanzibar kabla ya 2020 lakini ukweli unazidi kumsuta kila siku.

Baada ya kuzunguka dunia nzima kwa sasa amehamia mpaka kwa wachungaji kama Josephat Gwajima kama mentor wake. Hii ni dalili inayoonyesha desperation and kicking a dead horse.

This is an enormous leap for Maalim Seif, catapulting him to a new level of obscurity.

Kinachofanywa kwa sasa na UN, EU wakisaidiwa na Marekani kinatoa maandiko ukutani kuwaambia wale ambao wanadhani Maalim Seif ataingia Ikulu ya Zanzibar kabla ya Uchaguzi Mkuu 2020 wasipoteze muda wao.

Ieleweke kuwa fimbo ya kuichapia serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa ni kuinyima misaada au kuweka shinikizo kubwa kwa serikali ya Tanzania. Kinachofanyika kwa sasa ni kinyume chake kwa maana nyingine, Wazungu wanamwambia Maalim Seif, Let bygones be bygones.

Ninatumaini Uchaguzi Mkuu ujao, Maalim Seif atachangaza na akili zake baada ya kura kuanza kuhesabiwa.

Hii sio dalili nzuri kwa Maalim Seif na CUF Zanzibar.

Waingereza husema, ‘’Sometimes you’ll never know the value of what you have until it’s gone’’.

Nimalize kwa kusema, A Chinese military general, strategist and philosopher, Sun Tzu once said, If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle.

Source - Jf

HILI Ndio Jina Jipya la Ali Kiba lAlilopewa na Jay Z..!!!!

$
0
0

Mtandao mkubwa wa kuuza muziki wa TIDAL ambao upo chini ya rapa Jay Z umempa jina jipya msanii kutoka Bongo Alikiba na kumtambua kwa jina la 'The unstoppable' yaani mtu asiezuilika kwa kitu akifanyacho. 

"The unstoppable AliKiba is live right now in London" mtandao wa TIDAL uliandika wakati Alikiba akifanya yake kwa steji usiku huo. 

Alikiba alipewa jina hilo wakati akishiriki katika moja ya tamasha la muziki ambalo lilifanyika mwisho wa wiki nchini Uingereza ambalo lilikusanya mastaa kibao akiwepo Cassper Nyovest, P Square, Davido, Awilo Logomba, Sarkodie, Tekno , MI na wasanii wengine wengi huku bongo ikiwakilishwa na 'King' Alikiba ambaye alipata nafasi ya kufanya 'performance' ya ngoma zake kama Mwana, Unconditionally Bae na Aje.

Mashabiki wengi wameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo ya Alikiba kushiriki katika tamasha hilo kubwa huku akiwa na wasanii wakubwa kibao, kwani wanaamini jambo hilo linazidi kumjenga na kufungua njia zaidi katika kazi yake hiyo ya muziki. 

JPM na Museven Wasaini Mkataba wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta..!!!

$
0
0

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uganda jana wamesaini mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka Tanga Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Yoweri Museveni ikulu jijini Dar es salam.

Akizungumza baada ya kutia saini tamko hilo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Museveni kwa hatua ambayo Tanzania na Uganda zimefikia katika mradi wa bomba la mafuta la Hoima – Tanga na ameeleza kuwa mradi huo ni matokeo ya urafiki na undugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili.

“Kwa hiyo mimi nakushukuru sana Mhe. Museveni na kwa niaba ya Watanzania wote tumefurahi sana, umetengeneza historia ya Tanzania na Uganda na pia umeimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu, Watanzania hawatakusahau” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wa Rais Museven ambaye ni mmoja wa wafuasi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyepigania ukombozi wa nchi mbalimbali za Afrika na aliyekuwa na ndoto ya kuiunganisha Afrika nzima zao ili kujipatia manufaa ya kiuchumi, ametoa wito kwa viongozi hasa vijana kuendeleza misingi ya umoja na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

"Nimefurahi sana leo, najua kuna kazi kubwa imefanyika hadi kufikia hatua hii, lakini hii pia imeonesha kuwa na sisi tunaweza” amesema Mhe. Museveni.

Tanzania na Uganda (Inter-Governmental Agreement–IGA) ambao umepangwa kukamilika katika kipindi cha wiki moja, na baada ya hapo taratibu za kuweka jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zitafanyika.

Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima – Tanga wenye urefu wa jumla ya Kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania utagharimu Dola za Marekani Bilioni 3.55, unatarajiwa kusafirisha mapipa laki 2 ya mafuta kwa siku na wakati wa ujenzi unatarajiwa kuzalisha ajira kati ya 6,000 na 10,000.

NCHEMBA: Sitavumilia Kibiti Igeuke Kuwa Somalia..!!!

$
0
0

Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amesema serikali haiwezi kuvumilia mauaji ya mara kwa mara kama yanayotokea Somalia.

 Akizungumza katika jiji cha Bungu, Kibiti  ilipo kambi ya Polisi wanaotunza amani, na kuwataka polisi hao kusonga mbele katika mapambano ya  kuwasaka wauaji.

 Amesema wauaji na wanaoshirikiana nao wapo hapa hapa Kibiti na hivyo waziri huyo aliagizwa wote wakamatwe.

“Kibiti haiwezi kuwa kama Somalia hata siku moja. Wauaji wamejichanganya na raia wema na sasa tuwamulike hadi wapatikane,” amesema

 Amesema umefika wakati tuondokane na dhana kuwa wauaji wamekimbilia mahali pasipojulikana ilhali wapo hapa hapa Kibiti

Alberto Msando Afunguka Kuhusu Video Iliyosambaa Akimshika Gigy Money Ikulu

$
0
0
Mwanasheria Alberto Msando amejitokeza na kuongelea kuhusu video iliyosambaa akimshika Gigy money sehemu za Kiuno, Amesema haya:

From @albertomsando - Nikikaa kimya nitakua mnafiki. Nimekosea. Kilichotokea hakikupaswa kutokea. I will be a man enough and say sorry kwa wote ambao nimewakwaza na kuwaangusha. Am so sorry. But the beauty of all this is we all are human. Kuna watu ambao wamekuwa wepesi kuhukumu. Siwalaumu. Ni sawa na ni haki yao. I made a stupid mistake. I take full responsibility. Mwisho wa siku maisha lazima yaendelee. It could have been worse. And to all those who took time to text I appreciate. Thats friendship. #TheDon #Hennessy #TheClip

DIALLO Aahidiwa Ukatibu Mkuu CCM..Siri ya Mkakati Wake na Bashite Yaanikwa..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 22/5/2017..!!

Polisi yabaini ubovu magari ya wanafunzi

$
0
0

MAGARI matano kati ya 16 yaliyofanyiwa ukaguzi mwishoni mwa wiki na askari wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Kipolisi Tarime-Rorya wakati ukaguzi wa magari ya kubebea wanafaunzi yamebainika kutokuwa na ubora na viwango vya kubeba wanafunzi.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Tarime-Rorya, Joseph Bukombe alisema kasoro zilizobainika ni pamoja na kuwa na ubovu mkubwa na mengine yanadaiwa kutoka nchi ya jirani ya Kenya na kuingia Tarime kubeba wanafunzi, huku yakikwepa kodi.

“Tumeamua kuwaita wamiliki wa shule katika wilaya zetu hizi wenye magari ya kubeba wanafunzi kuleta magari yao hapa kwa ajili ya ukaguzi ambapo magari tano kati ya 16 tuliyoyakagua hapa leo (jana), yamebainika kuwa yana ubovu mkubwa yakiwemo yaliyofungwa kamba kwenye injini na giaboksi, yaliyooza bodi zake , kutokuwa na taa , wepa , matairi mabovu , viti vilivyochakaa,”alisema.

Alisema walikuta gari lingine likiwa na namba za usajili wa Kenya, likiwa limechakaa bodi yake tumeyatoa namba zake na mengine ambayo yamebainika na ubovu mdogo yatapigwa faini na kwamba wengine wamewaonya ili wayafanyie magari yao matengenezo.

Alitaja magari matano yaliyofanyiwa ukaguzi na kubainika kuwa yana ubovu mkubwa kuwa ni lenye namba za usajili T 277 APU la Shule ya Mwera Vision iliyopo Tarime mjini, lenye namba T 721 BFH kutoka shule ya sekondari Angel House na lenye namba T 444 AAR la shule ya ST Jude ya Buhemba, Tarime.

Gari lingine ni lenye namba za usajili T 861 DHM la shule ya awali na msingi ya Maryo, Nyamongo na gari lenye namba za usajili wa Kenya K AZ 088 R aina ya Nissan UD ambalo bodi yake ni mbovu, imechakaa huku likiendelea kutumia namba za usajili za nchi hiyo bila kubadilishwa.

Magari mengine yaliyokaguliwa na kukutwa na ubovu kidogo na kupigwa faini ni lenye namba za usajili T 652 DBV kutoka Shule ya Angel House, T 199 CRW kutoka Shule ya Remagwe, T 125 ZCU kutoka Shule ya Gwitiryo , T 903 BGM kutoka shule ya Msati Hill ya mjini Tarime, T 981 DFB kutoka shule ya Bustani RC Tarime , T 938 DFQ kutoka shule ya Elizabeth Memoriam , T 378 DEH kutoka Shule ya MT Mikael Maria Gamasara na T 422 DHV kutoka Shule ya Msati Hill Crest ya mj

ZITTO Kabwe Tanzania ni Masikini kwa Sababu Tumedharau Kilimo..!!!

$
0
0

Mheshimiwa Spika,
Serikali yeyote makini lazima ihangaike na masuala yanayowahusu wananchi wake walio wengi, na hapa Tanzania watu hao (walio wengi) ni Wakulima. Hivyo basi, kipimo kikuu cha kuondoa umasikini wa Watanzania ni kuondoa umasikini wa wakulima.

Sekta ya kilimo ndio msingi wa Uchumi wa watanzania. Waziri wa kilimo katika hotuba yake hapa ametuambia kuwa 65.5% ya watanzania wameajiriwa kwenye kilimo au wanategemea kilimo kwa kipato chao cha kila siku, kwamba 100% ya chakula nchi inategemewa kutoka kwenye sekta hii. Kilimo kinachangia 29.1% ya pato la taifa (GDP), karibia theluthi moja ya thamani yote ya shughuli za Uchumi nchini kwetu.

Hivyo basi, unapowekeza kwenye sekta ya kilimo unawekeza kwa theluthi mbili ya watanzania. Unapokuza kilimo unakuza uchumi wa theluthi mbili ya watanzania, na unapoacha kilimo kishuke maana yake umewafukarisha theluthi mbili ya Watanzania.

Kwa mujibu wa wataalamu wa Uchumi, ili kupunguza umasikini Tanzania kwa kiwango kikubwa, sekta ya kilimo inapaswa kukua kwa asilimia zaidi ya 8% angalau kwa miaka mitatu mfululizo, na ukuaji huo uendelee kukua kwa wastani wa 6% kwa muda miaka kumi mfululizo.

Hali ikoje nchini? Kwa mujibu wa hotuba ya Waziri wa Kilimo, kwa miaka hii mitatu mfululizo ukuaji wa Kilimo umekuwa ukishuka nchini (Na hivyo ukuaji zaidi wa umasikini). Mwaka 2014 sekta ya Kilimo ilikua kwa 3.4%, Mwaka 2015 Kwa 2.3% na Mwaka 2016 Kwa 2.1%.

Taarifa ya ya robo mwaka ya Benki Kuu nchini (BOT quarterly economic bulletin) inayoishia Disemba 2016 inaonyesha tofauti na anachosema Waziri. Kwa mujibu wa tarifa ya BOT ni kuwa sekta ya Kilimo ilikua kwa kasi ya 0.6% tu kutoka ukuaji wa 2.3%. 65.5% ya Watanzania wote wamejiajiri katika sekta ya Kilimo, hivyo mdororo huu ya sekta ya Kilimo kutoka ukuaji wa 2.3% mpaka ukuaji wa 0.6% ni ishara mbaya mno kwa ustawi wa zaidi ya robo tatu ya Watanzania.

Kwa Vijijini 78% ya Watanzania wanajihusisha na Kilimo. Hii maana yake ni kwamba wananchi wengi vijijini hawafanyi uzalishaji, jambo hili ni hatari sana, ni dalili kuwa ufukara wa watu wetu unazidi. Ni kwa sababu hii, pamoja na uchumi wetu kukua kitakwimu, 7% kwa mwaka, lakini bado wananchi wetu walio wengi wanaishi kwenye dimbwi la ufukara. Maana ukuaji huo wa Uchumi hauhusishi kilimo, hauhusishi zaidi ya robo 3 ya Watanzania.

Tunajenga uchumi unaowaacha pembeni theluthi 2 ya watanzania wote. Ukuaji huu mdogo wa Kilimo unapaswa kuishtua Serikali kwani ni hatari sana, ni hatari mno. Maana unajenga uchumi unaowaacha karibu zaidi ya robo 3 ya Watanzania kwenye ufukara huko vijijini, ni uchumi unaopanua matabaka ya mafukara na matajiri. Ndio msingi wa umasikini wa wananchi wetu miaka 50 baada ya Uhuru.

Tatizo hasa ni nini? Kwanini ukuaji wa kilimo unashuka na hivyo umasikini wa Watanzania kuzidi? Tatizo kubwa ni sera za Serikali pamoja na utekelezaji wake. Serikali haiwekezi vya kutosha kwenye kilimo, Na hata ikipanga mipango juu ya kilimo haitekelezi kabisa mipango husika.

Katika bajeti ya mwaka 2015/16, bajeti ya mbolea ya Ruzuku katika Wizara hii ilikuwa ni shilingi bilioni 78. Bajeti ya kwanza ya Serikali ya awamu ya tano ilishusha fedha za ruzuku ya mbolea mpaka Shilingi bilioni 10 katika mwaka wa Fedha wa 2015/16. Hii ilikuwa ishara ya dhahiri ya kukipuuza kilimo, kuwapuuza 65.5% ya Watanzania wote, kutokujali chanzo cha 100% ya chakula chote cha Watanzania, kupuuza sekta inayochangia theluthi moja ya uchumi wa Taifa.

Si hivyo tu, katika bajeti ya mwaka 2016/17, Bunge liliidhinishia Wizara hii fedha za miradi ya maendeleo katika kilimo kiasi cha bilioni 100.53. Waziri amelieleza bunge hapa kuwa mpaka Mei 4, 2017 Wizara imepokea shilingi bilioni 3.34, sawa 3.31% ya fedha zote za maendeleo ya kilimo. Jambo hili linasikitisha mno, ni jambo linaonyesha kuwa hatuwajali wanyonge wa Taifa hili.

Watanzania wanyonge walikuwa na matumaini makubwa sana na Serikali hii, Rais Magufuli alisema yeye ni rais wa wanyonge. Wanyonge nchi hii ni wakulima. Matendo ya Serikali anayoiongoza yanaonyesha tofauti, Serikali haiwajali wanyonge, inapuuza uchumi wa 65.5% ya wananchi wetu. Ni vigumu kuondoa umasikini nchini ikiwa tutaendelea kuwadharau wakulima.

Kwetu sisi ACT Wazalendo tunaofuata Ujamaa wa Kidemokrasia, Kilimo ndio sekta ya msingi, ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa, ni sekta nyeti ambayo hatutaacha kuisemea. Hivyo pamoja na kuonyesha kasoro zote hizo za serikali, tutatumia pia nafasi hii kutoa njia mbadala za kuondoa kasoro hizo ili kuhakikisha uchumi wetu hauwaweki kando wananchi wetu wengi.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Bungeni Dodoma
Mei 20, 2017

SUMAYE - Nimejiuzulu CRDB Bank Baada ya Familia Yangu Kufuatwafuatwa na Kuandamwa Kila Muda..!!!

$
0
0

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amejitoa katika Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB kwa madai kuwa familia yake inafuatwafuatwa hivyo kuhofia kuwa anaweza kuathiri benki hiyo.

Baada ya kujitoa kama mmoja wa viongozi wa benki hiyo kubwa nchini, Sumaye amesema kuwa ataendelea kuwa mwanahisa wa benki hiyo ya biashara.

“Sitaki msimamo wangu wa kisiasa uhusishwe na benki yetu” alisema Sumaye ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani.

Sumaye alisema kuwa huenda majukumu yake ya kisiasa yakambana na akashindwa kuhudhuria baadhi ya vikao muhimu vya benki hiyo ambavyo ni muhimu kwa ufanisi na ustawi wa benki.

Akiwa nje ya mkutano huo Sumaye alisema kuwa, familia yake imekuwa ikifuatwafuatwa na serikali na kwamba tayari mtoto wake amepokwa shamba.

Serikali pia alimnyang’anya Sumaye shamba lake lililokuwa Mabwepande kwa madai hakuliendeleza, huku yeye akisema uamuzi wa yeye kupokwa shamba ulikuwa ni wa kisiasa. Sumaye alieleza kwamba hakuweza kulima shamba hilo kutokana na serikali kupiga kilimo jijini Dar es Salaam.

Sumaye amesema uamuzi wake aliuchukua ili CRDB iweze kuendeshwa na watu walioko huru mbele ya jamii kuepusha hisa za wafanyabishara wengine kuathiriwa.

Sumaye anamiliki zaidi ya hisa milioni 7.4 za benki hiyo.

NAPE Nnauye Aongoza Kundi la Mawaziri Waliotemwa Serikalini Kuichana Serikali ya JPM..Wadai CCM Itaanguka Mwaka 2020...!!!

$
0
0

Mawaziri  wa zamani, Nape Nnauye na Charles Kitwanga, wamegeuka kuwa mwiba kwa kutoa hoja za kukosoa utendaji wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli.

Mwenendo wa makada hao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuikosoa Serikali, umeanza kuibuka siku za hivi karibuni baada ya wote kwa nyakati tofauti kuenguliwa katika nafasi zao za uwaziri.

Kwa hatua yao ya sasa, wanasiasa hao wanadhihirisha ukweli kwamba wabunge wengi hushindwa kueleza matatizo ya majimbo yao pindi wanapopewa nyadhifa serikalini na wanapotenguliwa wanadai wanapata nafasi zaidi za kuwatumikia wapigakura wao.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa siasa wanadai kuwa makada hao walikosa ujasiri wa kuikosoa Serikali walipokuwa wanashikilia nyadhifa zao kutokana na kubanwa na hoja ya uwajibikaji wa pamoja.

Nape Nnauye
Nape ambaye alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla uteuzi wake kutenguliwa Machi, mwaka huu baada ya kupokea ripoti ya tukio la kuvamiwa kwa Kituo cha Televisheni cha Clouds, amesikika mara kadhaa nje na ndani ya Bunge akiikosoa Serikali.

Akiwa jimboni kwake Mtama alikoenda kuzungumza na wapigakura wake baada ya kutenguliwa, alisema kama matukio ya kuteka watu yataachwa yaendelee, basi CCM itakuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Nape alitoa kauli hiyo wakati huo kukiwa na tukio la kutekwa kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ibrahim Mussa maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki.

Wakati akichangia hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wiki iliyopita, Nape alisema kuwa kama CCM isipotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kutowapatia maji wananchi, inaweza kuondoka madarakani.

Kauli nyingine ya Nape aliitoa wiki hii alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, aliposema kuwa wananchi wa mikoa ya Kusini hawatakubali kuona ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi unakwama kutokana na kile alichodai vita iliyopo kati ya mataifa makubwa.

Aliitaka Serikali isikubali kuona vita hiyo inaendelea kuwaumiza wananchi hao na kuongeza kuwa kama itashindwa kusimamia, wao hawatakubali.

Pia kupitia kurasa zake za mtandao wa kijamii wa twitter, Nape, amekuwa akiandika baadhi ya kauli zenye mwelekeo wa kuikosoa Serikali

Charles Kitwanga
Kitwanga aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alianza kuikosoa Serikali baada ya kutenguliwa mwaka jana, kutokana na ununuzi wa ndege mbili mpya aina ya Bombardier kutoka Canada ili kufufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Alisema ndege hizo, si tu hazina mwendo, lakini pia ilikuwa ni ajabu kununuliwa kwa fedha taslimu wakati duniani kote ndege hununuliwa kwa kulipa kidogo kidogo wakati mteja akiendelea kuzitumia.

Kitwanga aliibuka tena wiki iliyopita wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Gerson Lwenge kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, akisema atawahamasisha wapigakura wake wakazime mtambo ulioko katika chanzo cha maji cha Iherere.

Alisema jimboni kwake hakuna maji ya uhakika na tangu mwaka 2008 wananchi wamekuwa wakiyasubiri bila mafanikio.

“Kwa hiyo, nitakachokifanya safari hii, sitatoa shilingi kwenye bajeti, bali nitakwenda kuwahamasisha wananchi wa Misungwi wapatao 10,000, twende tukazime mtambo katika kile chanzo cha maji ili wote tukose.

 “Mshukuru nilipokuwa waziri nilikuwa siwezi kusema kitu, sasa nimetoka, tutapambana kwa sababu lazima tuwe na mipango mizuri ya kuwapelekea wananchi wetu maji kama inavyofanyika katika umeme kupitia REA (Wakala wa Umeme Vijijini),” alisema.

Kauli hiyo iliibua hasira za Waziri Lwenge wakati akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, ambaye aliita kuwa ni sawa na uasi.

Kutokana na kauli hiyo, alimtaka ahame chama kama haoni jitihada za kupeleka maji jimboni kwake zinazofanywa na Serikali.

“Kitwanga anaposema atakwenda kuhamasisha wananchi wakabomoe mtambo wa Iherere maana yake analeta uasi au hathamini kazi iliyofanywa na chama chake?

“Kama ni hivyo, sasa ajitoe kwenye chama kwa sababu Serikali imepeleka fedha na kwa maendeleo yaliyofanyika, ni lazima tuwahamasishe wananchi kutunza miundombinu iliyopo badala ya kwenda kuibomoa.’ alisema.

Khamis Kagasheki
Mbali na kina Kitwanga, baadhi ya waliokuwa mawaziri katika Serikali ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete nao pia wamegeuka kuwa wakosoaji wa Serikali.

Mmojawapo ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, anayeikosoa Serikali kupitia akaunti yake ya twitter.

Kagasheki aliyeangushwa katika ubunge wa Bukoba Mjini na mpinzani wake wa siku nyingi, Wilfred Lwakatare (Chadema), aliwahi kusema kuwa kama nguvu ya Ukawa ingemchagua mgombea makini, basi CCM ingekuwa na kazi ngumu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi.

Kada huyo wa CCM aliyejiuzulu nafasi yake kutokana na sakata la Operesheni Tokomeza, aliwahi kuandika katika ukurasa wake wa twitter: “Kuikosoa Serikali yoyote ile ni jambo la kawaida. Ni vema kuchagua maneno na kulenga hoja bila matusi.”

Philip Mulugo
Naye Philip Mulugo aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati wa utawala wa Kikwete, pia amekuwa akiikosoa Serikali ya Magufuli.

Mulugo ambaye kwa sasa ni mbunge wa Songwe, amesikika bungeni wiki iliyopita akiikosoa Serikali alipochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.

Akichangia bajeti hiyo, Mulugo aliishangaa Serikali kuruhusu vitabu vyenye makosa vitumike shuleni wakati kuna uwezekano wa kuviondoa.

Katika maelezo yake, Mulugo alivitaja vitabu vya jiografia vya kidato cha tatu na kiingereza kidato cha nne, kuwa vina makosa yanayoweza kuharibu misingi ya wanafunzi.

“Haiwezekani mbili mara mbili mtu aseme ni sita wakati sisi tunajua ni nne. Kwa hiyo, hili suala la vitabu mliangalie vizuri kwa sababu haliko vizuri,” alisema Mulugo.

Pamoja na hayo, Mulugo alizungumzia michango inayotozwa na Serikali katika shule binafsi na kusema ni mingi na kwamba inatakiwa kupunguzwa kwa kuwa inawakatisha tamaa wamiliki wa shule hizo.

GAMBO Atangaza Kusitisha Kupokea Pesa za Rambirambi za Msiba wa Wanafunzi wa Arusha..!!!

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAPATO NA MATUMIZI YA MSIBA WA AJALI YA LUCKY VINCENT MKOANI ARUSHA
TAREHE 21 MAY 2017
Mnamo tarehe 19 May 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha ilitoa taarifa ya mapato na matumizi kuhusu michango ya Rambirambi ya ajali ya basi ya shule ya Lucky Vincent iliyotokea Wilayani Karatu eneo la Rhotia. Ajali hiyo ilitupotezea wapendwa wetu 35, wakiwemo wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1.

Aidha, ajali hiyo pia ilitubakishia Majeruhi 3 ambao hali zao zilikuwa ni mbaya sana. Tunaamini Mwenyezi Mungu ana makusudio yake kuwaacha hai hawa Majeruhi 3 kwenye ajali mbaya kama ile.

Baada ya Serikali na wadau mbalimbali nchini kushilikiana kufanikisha kuihifadhi miili ya wapendwa wetu ikiwa ni pamoja na kutoa fedha taslimu za rambirambi kiasi cha shilingi 3,857,000 kwa kila familia iliyofiwa kwa familia zote 35. Kwa ujumla tumeona ni vema sasa nguvu kubwa ikapelekwa kwenye kuwahudumia majeruhi ili waweze kupona na makusudio ya Mungu yaweze kutimia.

Tunapenda kuujulisha Umma kuwa hadi Ijumaa ya tarehe 20 May 2017 kutokana na wadau kuendelea kuchangia tumebakiwa na kiasi cha Shilingi 67,993,885. Kwa mantiki hiyo busara imeelekeza kuwa nguvu kubwa sasa ipelekwe kwenye kuwahudumia majeruhi, maana hata tufanyeje kwa wale ambao Mungu kwa mapenzi yake amewachukua hatuna namna tena ya kuwarudisha.

Hivyo, tunapenda kuujulisha Umma kuwa Jumatatu tarehe 22 May 2017 tutazitumia familia za majeruhi pamoja na Madaktari wetu waliojitoa kuwasindikiza majeruhi kiasi cha Dola za kimarekani 20,000 (Sawa na 44,720,000 kwa Exchange rate ya 2,236 , kila familia itapata Dola 5,000 (Jumla ni Dola 15,000 kwa familia 3), Daktari Dola 2,500 na muuguzi Dola 2,500 kama sehemu ya kuendelea kuwafariji na kuwapunguzia changamoto huko ugenini.

Kwa ujumla baada ya yote hayo tutabakiwa na kiasi cha shiliingi 23,273,885 huku tukiendelea kuangalia hali za majeruhi wetu. Kiasi cha fedha kilichobaki kitaendelea kuwekewa utaratibu kupitia timu ya wafiwa 4 walioteuliwa na wafiwa wenzao kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha mapato na matumizi ya suala hili yanaeleweka vema kwa Umma.

Pia tunapenda kuuhabarisha Umma kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha imehitimisha rasmi zoezi zima la kupokea rambirambi ili ipate muda zaidi wa kufuatilia Mustakabali wa Majeruhi wetu walioko haspitalini nchini Marekani.

Imetolewa na:
Mrisho Mashaka Gambo
Mkuu wa Mkoa Arusha

BEN Pol Amefunguka Haya Baada ya Watu Kumtukana kwa Kupiga Picha Nusu Uchi na Kuzisambaza Mitandaoni..!!!

$
0
0

Ben Pol amefunguka kwa mara ya kwanza tangu picha yake inayomuonyesha akiwa utupu kusababisha maneno mengi mitandaoni.

Muimbaji huyo amerudi tena kupitia mtandao wa Instagram kwa kuweka video ambayo inamuonyesha akiwa mtupu huku ukisikika wimbo ukiimba na kuandika, “Usi-judge kitabu kama hujakisoma ndani 🤔.”

Hata hivyo imeonyesha kuwa picha hizo zilizozua utata mkubwa mapema wiki hii ni ujio wa nyimbo yake mpya ya Ben ambayo imedaiwa kupewa jina la ‘Mateka’ na ndani yake amemshirikisha rapper Darassa.

Wimbo huo pia umetayarishwa na Tiddy Hotter ambaye alitengeneza wimbo mwingine wa Phone wa Ben.

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidiWhatsapp +255 674 835107 -calls +255746757102
Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..

Mabinti Wengi Wanakosa Bahati Kwa Kupiga Mizinga Bila Malengo

$
0
0

NENO KUPIGA KIZINGA NI NENO LA KAWAIDA ILA USICHOJUA UPIGAJI WA VIZINGA NI HATARISHI KWA MAHUSIANO HASA VIZINGA VISIVYO NA MSINGI.
Mabinti wengi wanajisahau sana katika hili na ndio mana unaweza shangaa mwanaume wako ghafla anaanza kukukimbia unajiuliza nimekosea wapi kumbe umekosea kwenye vizinga kuomba vitu vya ajabu ajabu.Unaweza shangaa ulikuwa na mwanaume unaomba hela za ajabu ajabu anakupa ila ukashangaa kakuacha kawa na mtu mwingine wamekaa baada ya muda unashangaa mwenzio ambaye kachukua nafasi yako amepewa kitu cha thamani ambacho hukuwahi hata kukiwaza.

Acha nikuambia vizinga vya kipuuzi ni vipi hasa.Mmeanza mna wiki mbili tu ushaanza baby mwenzangu yani hili wigi nishalichoka naomba hela nikasuke baby wangu,mara jamani baby mwenzio kuna gauni nimeliona nimelipenda bei yake 17,000 naomba baby wangu nikanunue,Hajakaa vizuri boo nikuambie kitu wiki ijayo kuna birthday ya rafiki yangu nataka nimnunulie keki japo ya 20,000 plz baby nisaidie hivi ndio vizinga vya kipuuzi na vingine vingi.Leo hii kirahisi unapiga vizinga vya vocha kila wiki mtu akuungie bando ndio vizinga vyako.Acha nikuambie binti hakuna mwanaume ambaye anapenda kuwa na mwanamke ambaye ni omba omba hasa wa vitu ambavyo havina msingi.
Mwanamke shujaa mwenye kujielewa haombi ovyo bali anapotaka kuomba kitu anaomba kitu ambacho kina direct impact katika maisha na ambacho kimeshiba na sio kukiomba kila mara.Unaweza kuwa na mwanamke ukashanga mna muda na hakuombi vitu hovyo the day anakuja kukuomba anakuomba kitu ambacho hata mwenyewe ukipima kumsaidia kwake namna moja utakuwa na wewe umejipa msaada katika maisha yako kama wapenzi.

Halafu acha niwape siri ukiomba mwanaume wako kitu usikurupuke kaachini uandae kama proposal kabisa yani unampa uchanganuzi wa kile unachoomba na kwanini unaomba ili kuonesha wazi huombei tamaa.

NAOMBA NIKUAMBIE KABISA BINTI HIVYO VIZINGA VYA MABANDO NA HELA ZA MAWIGI ZA KILA WIKI ZITAKUFANYA UKIMBIWE.JIFUNZE KUJIZUIA KWA VITU AMBAVYO HAVINA MSINGI NA UNAPOTAKA KUOMBA KITU OMBA KITU AMBACHO KINAONEKANA KINA IMPACT NA MAISHA.

UTASHANGAA UMEKAA NA MWANAUME MIAKA SIKU UNAACHWA HUNA CHOCHOTE ULICHOPATA ZAIDI YA KUBADILI STYLE ZA MAWIGI TU.

#TheOceanOfLove

Askofu Gwajima Ataja Njia Mbadala ya Kuwabaini Wahusika wa Mauaji Kibiti

$
0
0

Askofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema Serikali inapaswa kuwashirikisha viongozi wa dini katika kupambana na mauaji ya Polisi na raia yanayoendelea kutokea katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani.


Akihubiri katika Ibada ya Jumapili jana kwenye kanisa lake lililoko Ubungo jijini Dar es Salaam, Askofu Gwajima alisema mauaji hayo ni roho kamili ambayo pamoja na sheria za nchi, inapaswa kuondolewa kwa maombi.


Alifafanua kuwa Jeshi la Polisi nchini na dola wanazuia uhalifu kimwili, lakini viongozi wa dini wanazuia ki roho, hivyo wote wanatakiwa kushirikiana ili kukomesha matukio hayo ya mauaji yanayoleta hofu kwa watu.


"Kiongozi wa dini anaweza kwenda Kibiti na kuwaambia walioua polisi na kuendeleza mauaji wajitokeze na kusalimisha silaha na wakaja, lakini watu hao wakiitwa na Polisi walete silaha hawatatokea,' alisema.


Akitumia mfano wa mahubiri aliyosema kuwa aliwahi kuyatoa mwaka 1995 eneo la Kibiakali, Gwajima alisema viongozi wa dini wana nguvu ya ziada kupambana na uhalifu.


"Mimi nimewahi kuhubiri mwaka 1995 huko Kibiakali na kusema kuwa waliokuwa wanamiliki silaha walete kwa jina la Yesu na nilifanikiwa kukusanya SMG  nane ambazo walileta kwa mikono yao," alieleza.


"Hivyo, tunaomba (viongozi wa dini) Serikali itupatie nafasi ya kuhubiri ili kuweza kupambana na roho hizo za mauaji. Pia huu ni wakati wa Kanisa kulia na kusali ili kuweza kupambana na vita hivi vya kiroho ambayo inahitaji nguvu ya rohoni kukamata wahalifu.


Katika hatua nyingine Askofu Gwajima alisema Tanzania ni nchi iliyobarikiwa, hivyo siyo vyema watu wakaitabiria mabaya.


Ameyasema hayo jana wakati wa Ibada ya Jumapili kanisani kwake Ubungo. Alisema kuna jambo ambalo Mungu atafanya ambalo litaonyesha dhahiri kuwa  Tanzania ni nchi tajiri.


"Watanzania ni makuhani wa nchi, tumezaliwa nchi hii tumekunywa maji katika nchi hii, hivyo hatupo radhi kuona  watu wanatabiri vitu ambavyo havipo katika utabiri."


Aliendelea "Wiki iliyopia nilisema baadhi ya watu ambao walikuwa  wanafanya Tanzania shamba  la bibi kwa kila mtu kuilani nchi hii, wanatakiwa kujua kuwa Tanzania ni nchi iliyobarikiwa.


Pia  itafika wakati  mataifa yatajua kuwa nchi hii ni tajiri hivyo viongozi wa dini na waumini wanatakiwa  kuiombea ili mpango wa Mungu uweze kutimia.


"Na ndio maana hivi karibuni nimekuwa mkali kwa baadhi ya manabii wanaotabiri mabaya katika Taifa hili  sipo radhi kuona watu wanatabiri mambo ambayo hayaendani na nchi hii kwani hivi karibuni Mungu atajidhirisha katika nchi hii  ambayo ipo kwa makusudi yake"alisema.


Aliongeza kuwa wapo watu ambao wataona aibu nchi hii siku ambayo Mungu atajidhihirisha na kuiweka juu,  hata hivyo waumini na viongozi wanatakiwa kuitabiria mema nchi na kuiombea ili baraka zake zishuke.


"Mungu alimwambia Sauli toka uende, na utakapokuwa unakwenda utakutana na manabii watakao kuwa wanatabiri roho ya Bwana atashuka na kuwa mtu mwingine, Leo hii waumini mbalimbali wametoka sehemu tofauti na kuja kusikia utabiri  huu. Sisi ni mabalozi wa Mungu hapa duniani.


Alifafanua kuwa Kanisa halitakiwa kulilia demokrasia bali linatakiwa kulilia Ufalme kwamba ule ushawishi wa mbinguni  Mungu akisema ndio hakuna wa kupinga, bali mtafuata tu hata kama wengi wanasema lakini watafuata tu.


Baadaye sheria ijae Katiba ya Mungu, Sheria ya Mungu na tusimame katika mlima Kilimanjaro na kutangaza neema na ufalme wa Mungu.


Gwajima alisema wanasiasa hawaaminiki na kuwataka Watanzania kuweka tumaini lao kwa Mungu ambaye ndiye anayeweza kuwapa msaada wa kweli.


"Unafikiri wanasiasa wanaweza kuibadili nchi? Je, una mtazamo huo? Ukimtembelea mwanasiasa mmoja na mwingine ni kama leo unamtembelea chui na kesho simba. Usiweke tumaini juu yao, weka tumaini lako kwa Mungu"

Paul Makonda " Ruge Inabidi Aombe Msamaha Kwa Kuwatapeli Watanzania Kuwa Nilivamia Clouds TV"

$
0
0

Baadhi ya Maneno Aliyokaririwa akisema Paul Makonda katika mahojiano yake na Star TV Leo...

'Ruge Anapaswa awaombe msamaha Watanzania kwa kuwatapeli kuwa Nilivamia Kituo chake'

'Tukio linaloitwa uvamizi kwangu ni igizo la Uvamizi'

'Clouds nilikuwaga naeda kula ugali na Maharage'

'Gwajima anajiita Askofu lakini sio Askofu kamili'

'Nimeuona uongo wa Ruge hadharani, Nimeouna utapeli wa Ruge Hadharani'

'Ruge ana akili ya kutunga nyimbo za mapenzi na Ng'onjera sio maendeleo ya Dar as salaam'

WATUHUMIWA wa Mauaji ya Polisi 8 na Raia Zaidi ya 30 Kibiti Mkoani Pwani Wapatikana..!!!

$
0
0

Jeshi la polisi nchini limetoa orodha ya majina 12 ya wanaotuhumiwa kuratibu na kuendesha harakati na mauaji ya viongozi wa serikali za vijiji katika wilayani Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amesema kupatikana kwa watuhumiwa hao pamoja na picha ni kutokana na oparesheni inayoendelea na vyombo vya ulinzi katika Wilaya hizo.

“Tumeweza kuwa baini Watuhumiwa wa mauaji hayo, Watuhumiwa hao wameweza kubainika kwa majina na picha kwa baadhi yao ni matokeo ya oparesheni inayoendeshwa na vyombo vya ulinzi, Mtuhumiwa wa kwanza ni Faraji Ismail Nangalava, Anaf Rashid kapera, Said Ngunde, Omary Abdalla Mandimbwa, Shaban kinyangulia, Haji Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Njame, Rashid Salum Mtulula, Shekhe Hassan Nasri Mzuzuzi, Hassan Uponda,” alisema Kamanda Lyanga.

“Jeshi la polisi limebaini haya kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi,” aliongeza.

Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kufichua kwa siri watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama katika mkoa huo.

BAADA ya Kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki..Museveni Ajipa Ziara za Ulaya..!!

$
0
0

Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (EPA) baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Nchi za Umoja wa Ulaya (EU), bado halijapatiwa ufumbuzi mpaka hivi sasa.

Baada ya Tanzania na Uganda kugoma kusaini mkataba huo wa ushirikiano ambao baadhi ya viongozi wanaufananisha na ukoloni mambo leo, viongozi hao wamekubaliana kutuma ujumbe mjini Brussels, Ubelgiji yaliko makao makuu ya EU ili kujadili kwa kina juu ya EPA na kufikia ufumbuzi.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni atakwenda huko ili kujadili nafasi ya kiuchumi ya EAC na pia kuzungumzia suala la kutoiadhibu Kenya kutokana na nchi wanachama kutosaini mkataba huo.

Akizungumza katika mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za EAC mara baada ya kukabidhiwa kijiti cha kuiongoza jumuiya hiyo na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Museveni alisema, ataongoza ujumbe huo ndani ya mwezi kuanzia jana na kwamba EU haipaswi kuiadhibu Kenya kwa nchi wanachama kutosaini mkataba wa EPA.

“Tutawezaje kujadili na kusaini mkataba hali ya kuwa mwanachama wetu mmoja amewekewa vikwazo na EU ? bado tunahitaji ufafanuzi juu ya mambo kadhaa yaliyomo kwenye mkataba wa EPA,” alisema Museveni.

Museveni ameeleza pia kutofurahishwa na hatua ya Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo Burundi bila kushauriana na viongozi wa jumuiya hiyo. Alisema Burundi ni tatizo la jumuiya hiyo, hivyo wanaweza kulimaza wenyewe.

SNOOP Dogg Ajipanga Kutoa Albamu ya Nyimbo za Injili..!!!

$
0
0

Snoop Dogg ameushangaza ulimwengu kwa kuahidi albamu yake inayofuata itakuwa ya nyimbo za injili.

Akiongea katika kipindi cha The Pharmacy, rapper huyo amesema, “I’m working on a gospel album. It’s always been on my heart. I just never got around to it because I always be doing gangsta business or doing this or doing that. I just felt like it’s been on my heart too long. I need to do it now.”

Snoop amelitaja jina la albamu yake hiyo ya 16 itaitwa ‘Neva Left’.

April 17 ya mwaka jana msanii huyo alianza kuonyesha kuvutiwa na muziki huo baada ya kuandika katika mtandao wake wa Instagram, “Silver n gold. @dashradio Cadillac music Sunday gospel mix.”
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images