Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

Simon Msuva: Kiba anaitendea haki Tanzania

$
0
0

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ambaye msimu huu ameifungia klabu yake jumla ya mabao 14 amefunguka kwamba, msanii Alikiba anaitendea haki nchi yake ya Tanzania kwa kazi ya muziki ambapo amekuwa akifanya kazi bora zinazoleta sifa kwa nchi.

Msuva amesema hayo leo kupitia kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusema yeye anamkubali sana msanii huyo kutokana na uwezo wake kimuziki na namna anavyoweza kuimba vizuri kila apatapo nafasi.

"Kwanza naupenda sana ule wimbo wa wale jamaa wa Kenya wameshirikisha Alikiba 'Unconditionally Bae', naukubali ule wimbo sababu watu wamepangilia sana kazi yao mle ndani na unayasikia kabisa, nimependa mavazi ya mule jinsi walivyovaa ni mavazi fulani ambayo yanawakilisha Afrika japo hata watu wa Ulaya wanavaa lakini naona Afrika watu wanapenda sana kuvaa vile" alisema Msuva

Msuva aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya wimbo huo na uwezo wa Alikiba
"Ukisikiliza ule wimbo unaona jinsi ambavyo Alikiba amefanya vizuri yaani ameitendea haki Tanzania maana ametuwakilisha vizuri Tanzania yetu, kuwa tunaweza kuimba pia tunaweza hata kuwashirikisha nyinyi wenyewe mkaja kucheza nyimbo zetu huku Tanzania"- alisema Simon Msuva.

MAMBO 6 Ambayo Ukiyafanya Kamwe Hutapata Ugonjwa wa Kuhara..!!!

$
0
0

Kuharisha ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea (bacteria) ambao huenezwa na hali ya uchafu (inzi). kwa hiyo kama  kama utafanya yafutayo basi huwezi pata tatizo hilo.

1. Kuzingatia usafi wa choo

2. Kunawa mikono kila baada ya kutoka chooni

3. Kuosha vyombo vizuri na kuvihifadhi sehemu safi

4. Kuosha matunda kabla ya kula

5. Kunywa maji safi na salama (yaliyochemshwa)

6. Kunawa mikono kila unapohitaji kula chochote

TABIA 4 Zinazoharibu Kinga Zako za Mwili Bila Kujijua..!!!

$
0
0

Kinga ya mwili ni ile hali ya mwili kuwa na uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi mbalimbali. 

Mtu anapokuwa na kinga imara za mwili, huepuka kuugua mara kwa mara na kwa kifupi unaweza kusema kwamba kinga ya mwili ndiyo kila kitu katika afya ya binadamu. 

Kuumwa mara kwa mara ni dalili tosha kuwa kinga yako ya mwili imeshuka na hivyo unahitaji kuchukua hatua za kuziimarisha.

Kwa  kawaida Mungu alituumba miili yetu ikiwa na uwezo wa kujikinga na magonjwa yote, laikini mwili utaweza kufanya hivyo endapo tu utapatiwa vyakula vinavyohitaji ili kuimarisha kinga zake.


Leo tuangalia aina ya vyakula vya kuepuka ili kuzifanya kinga za mwili kufanya kazi zake vizuri.

1. Mhusika anapaswa kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi

Sukari siyo nzuri kwa afya yetu hasa inapotumiwa kupita kiwango. Kiwango cha kawaida cha sukari kinachoruhusiwa kutumiwa ni kijiko kimoja kidogo (teaspoon), kinapozidi hapo huwa kinachangia kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili. Inaelezwa kuwa chupa moja ya soda ina karibu vijiko 6 vya sukari. Hivyo kama wewe ni mnywaji mkubwa wa soda na vinywaji vingine vya aina hiyo, utaona ni kiasi gani unachangia kuharibu kinga zako za mwili.

2. Epuka unywaji wa vileo

Unywaji wa pombe kupita kiasi ni sumu  ndani ya miili yetu. hivyo si nzuri pia kwani huweza kuchangia kudhoofisha kinga za mwili.

3. Epuka matumizi ya vyakula vya kukaanga

Vyakula vya kukaanga kama vile chips na vinginevyo, pamoja na vyakula vya kuoka huwa na mafuta mabaya ambayo huwa na tabia ya kutengeneza magonjwa mwilini (fee radicals) ambayo huathiri mfumo wa kinga ya mwili pamoja na chembechembe za nasaba (DNA). Vyakula hivi vinapaswa kuliwa kwa nadra sana au kuepukwa kabisa ikiwezekana.

4. Epuka vyakula vya viwandani (vyakula vya makopo)

Epuka ulaji wa vyakula vya kwenye makopo na badala yake pendelea kula vyakula halisi‘fresh’ na vya asili. Ulaji wa vyakula vya asili, hasa vyakula vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa, huwa na idadi kubwa ya vitamini, madini na kamba-lishe ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili.

UTAFITI Mpya: Pombe ni Hatari kwa Moyo Wako, Fahamu Kiasi Usichopaswa Kuvuka..!!!

$
0
0

Ingawa tafiti kadhaa zilizopita ziliwahi kueleza kuwa ni vyema kunywa kiasi fulani cha pombe kwa afya yako, utafiti mpya umebaini kuwa pamoja na hayo, kuna hatari kubwa ya kuvuruga mwendo wa mapigo ya moyo kwa kunywa pombe.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na timu ya wataalam wa sayansi wakiongozwa na Profesa Peter Kistler wa Hospitali ya Alfred iliyoko Melbourne nchini Australia, pombe ina madhara mengi kwenye mwili wa binadamu ambayo yanaweza kuchangia katika kuvuruga mwendo wa mapigo ya moyo.

Imeeleza kuwa hali hiyo inaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya moyo pamoja na stroke (kupooza).

Imeeleza kuwa kunywa pombe kunaweza kusababisha udhaifu katika moyo na inaweza kuharibu mfumo wa mawasiliano unaoweza kusaidia seli za misuli ya moyo pamoja na mfumo wa fahamu ambao unasimamia kazi nyingi za mwili.

Watafiti hao wamewashauri watu ambao hunywa pombe lakini wamekuwa wakisikia mwendo wa mapigo ya moyo hauko vizuri wasitishe ama kupunguza kwa kasi kubwa matumizi ya vilevi.

Wakizungumzia kiwango cha pombe ambacho kinamfaa mtu ambaye ameanza kusikia mapigo ya moyo hayako sawa, apunguze hadi chupa moja ya pombe yenye kilevi cha kawaida na ahakikishe anapata siku mbili kwa kila wiki kutotumia kabisa kilevi.

Kazi hiyo ya watafiti hao iliyochapishwa kwenye jarida la American College of College of ardiology, ilifanya marejeo ya tafiti zaidi ya 100 na iliwahusisha takribani watu 900,000.

LIST ya Vyakula Asili Vyakuongeza Urembo kwa Wanawake..!!!

$
0
0

Vifuatavyo ni vyakula vinavyoweza kusaidia kuimarisha afya ya ngozi:-

Asali ambayo hutengenezwa na nyuki huwa na viambato asilia na ni moja ya chakula muhimu kwa ajili ya kuimarisha afya ya ngozi . Asali husaidia kutunza na kuhifadhi unyevu kwenye ngozi na ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambazo huzuia vijidudu wanaozaliana kwenye ngozi.

Tumia asali kwa kupaka wakati wa kuoga, kisha acha kwa muda na ioshe. Kufanya hivyo husaidia kuinawirisha ngozi.

Mayai pia ni muhimu kwa afya ya ngozi yako, kiini cha yai huwa na vitamini A na B, huku sehemu yenye ute ikiwa na protini nyingi ambayo ni muhimu pia kwa ngozi, ute wa yai ni muhimu katika kuifanya ngozi kuwa nyororo na yenye kung'aa na pia husaidia ngozi kujilinda vizuri na mionzi ya jua.

Matunda nayo ni muhimu pia hususani chungwa na limao ambayo husaidia kuimarisha afya ya ngozi, kwa sababu husaida kutengeneza collagen, ambayo ni aina ya protini inayotengeneza ngozi. 

Ndani ya matunda hayo huwa na Vitamini C , ambayo husaidia sana kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi na hivyo kuilinda ngozi isizeeke mapema.

Mboga za majani pia ni muhimu kwa afya ya ngozi kama tujuavyo zimesheheni vitamin na virutubisho vya aina mbalimbali vyenye faida kubwa kwa ngozi na mwili kwa ujumla. Mboga hizi za majani kwani husaidia ngozi kuzalisha seli mpya na kuondoa zile zilizokufa, hivyo kupunguza ukavu na kutunza ngozi na kuifanya ing’are na kuvutia.

Vyakula vya baharini kwa ujumla ni vizuri kwa afya ya ngozi. Vyakula vingi vya baharini vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu kwa siha ya ngozi. Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi na husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi.

Anza kupenda kula vyakula vyenye lishe bora kwa kuwa na ngozi bora zaidi.

HOJA Chonganishi: Star TV Ifungiwe Mara Moja,Imemdhalilisha Bashite..!!!

$
0
0

Kitendo cha Star TV kurusha matangazo ya mahojiano yenye mvurugano hakivumiliki. Mahojiano yasiyo na uwiano yalilenga kudhalilisha. Yalilenga kumuanika na kumfanya kuaibika RC wa Dar, Daudi Albert Bashite aka Paul Makonda.

Mahojiano yamemuacha Bashite peupe na akiwa amesawajika kiuhakika. Ubovu wa majibu; kukosa umakini na kubabaikababaika kwa Bashite kumemuacha Bashite katika hadhara ya hasara. Mahojiano yamekuwa ugonjwa wa jino. Maumivu makali kama kabali.

TCRA fungieni Star TV na wanyang'anyeni leseni. Ni katika kumlindia heshima Bashite. Mahojiano yamekoleza manjano kwenye tuhuma. Tuhuma za kubuma katika kusoma. Mahojiano yalipaswa kupangwa na kupangika kiuhakika. Si vile. Hayakufaa.

Nafasi haikutumika,nanasi limeharibika. Majivuno yameleta miguno ya kukataa kuambiwa uongo hata kwa hongo. Bashite ameumbuka. Bashite amedhalilishwa. Nani aliwatuma Star TV?

Rambirambi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Songea,Ruvuma)

Chanzo Jf

PROF. Ndalichako: Baada ya Vyeti Feki Tunahamia kwa Wenye Elimu Feki..!!!!

$
0
0

 Waziri wa elimu prof Ndalichako amesema serikali italazimika kupitia elimu za watumishi wake kwani wengi wao licha ya kua na vyeti vizuri lakini kilichomo vichwani mwao ni duni sana ukilinganisha na vyeti source waziri akiwa tbc.

Credit Jf

NAPE: Wabunge Waache Kuisifia na Kuipigia Makofi Serikali Sio Kazi Yao..!!

$
0
0

Nape alikuwa akijibu maswali mbalimbali aliyokuwa akiulizwa na mojawapo kuhusu bunge amesema bunge mkutano wa wananchi, wabunge wapo pale kwa niaba ya watanzania majimboni na kazi yao ni kuisimamia na kuishauri serikali na sio kuipigia makofi na kuipongeza kila kitu na wakifanya hivyo basi tutapiga hatua

Amesma pia vyombo vya dola visitumie mabavu kwani hii italeta chuki kwa vyombo hivyo na kwa rais na kusema Tanzania hatujazoea mabavu akatolea mfano wa tukio la Malima na kusema yeye alikua akiulizia tu ajabu polisi akamtishia vile

Pia amesema sasa yupo huru zaidi baada ya kuacha uwaziri na anafurahia maisha

DIAMOND - Nikipost Kumjulia Hali Ivan Nitaonekana Natafuta Kiki ..!!!

$
0
0

Msanii wa muziki, Diamond Platnumz amedai ameshindwa kupost chochote kumtakia hali aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Zari, Ivan ambaye amelazwa hospitali, kwa madai ataonekana anatafuta kiki.

Muimbaji huyo amedai amekuwa akimhimiza mpenzi wake Zari kwenda kumtakia hali mzazi mwenzake huyo.

“Ni kweli mzazi wake Zari anaumwa, na yuko serious. Na kila siku huwa namuhimiza Zari akamuone mzazi mwenzie kwasababu najiuliza asingekuwa anaenda familia yangu ingemuonaje, kwa hiyo maskini dada wa watu kila siku huwa anaenda,” Diamonda alikiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Aliongez, “Sijawahi mpigia simu kwasababu yuko serious sana na pia sikuweza kumpost kwasababu watu waneanza kusema labda natafuta kiki maskini ya Mungu kumbe wala,”

Hivi karibuni Zari alionekana katika picha akimjulia hali ex wake Ivan Ssemwanga ambaye anadaiwa kulazwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini baada ya kupata matatizo ya moyo.

Mitandao ya Uganda inadai kuwa Ivan anasumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease).

KAMANDA Sirro Awajibu Waliosusia Maiti ya Kijana Aliyeuawa Akihisiwa Kuwa Jambazi...!!!

$
0
0

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetolea ufafanuzi malalamiko yaliyotolewa na ndugu za kijana aliyeuliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za ujambazi wiki moja iliyopita akidaiwa kujaribu kumpora askari silaha.

Kamishna Simon SirroKamanda wa jeshi hilo Kamishna Simon Sirro amewataka ndugu wa marehemu huyo wakatembelee eneo la tukio kusikia wananchi wanasema nini kuhusiana na kitendo cha kijana huyo ambaye aliuawa na polisi baada ya wenzake kukimbia kusiko julikana.

Amesema katika eneo la tukio palikuwa gari la kubebea fedha lililokuwa likisambaza fedha katika mashine za ATM za CRDB kiasi cha Tsh. 320, 000,00 ambapo mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na wenzake alidaiwa kutaka kufanya tukio la uvamizi katika gari hilo, kabla ya askari kumuwahi na kumuua.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, ndugu wa marehemu huyo wamegoma kuchukua mwili wake kwa ajili ya maziko wakidai kuwa ndugu yao ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi wa UDSM hakuwa muhalifu, huku wakitaka jeshi hilo liombe radhi kwa kudai kuwa ndugu yao alikuwa mhalifu.

MAKONDA Atema Nyongo...Alikana Jina la Bashite Hadharani..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo Jumanne 23/5/2017

JPM Amwagiwa Sifa kwa Kufanya Mapinduzi Makubwa Kwenye Elimu..!!!

$
0
0

Rais Magufuli ametajwa kuwa rais wa kwanza mwenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu nchini baada ya kuruhusu serikali yake kutumia zaidi ya shilingi bilioni 18 kila mwezi kugharimia elimu ya msingi na sekondari

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wazazi wa shule sita za msingi katika kata ya Ihyela, Mbeya baada ya kukusanyika kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi 10 wa darasa la saba ambao wamefanya vizuri mtihani maalum wa majaribio wa maandalizi ya mtihani wa taifa unaotarajiwa kufanyika miezi michache ijayo.

Akizungumza kwa niaba ya walimu, Mratibu wa elimu kata ya Ihyela Dickson Sinkwembe, ameahidi kuwa walimu watahakikisha wanafunzi 10 ambao wamefanya vyema mtihani huo wa maandalizi, wanapata matokeo mazuri kwenye mtihani wa taifa na kuiletea heshima kata hiyo, huku akiwataka wazazi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa walimu.

Pamoja na hayo, mdau wa elimu katika kata hiyo, Bw. Ndele Mwanselela amewapatia zawadi wanafunzi hao ya fedha taslimu huku akiwataka wananchi kumuunga mkono Rais JPM kutokana na uamuzi wa serikali yake kutumia zaidi ya Shilingi bilioni 18 kila mwezi kwa ajili ya kugharamia elimu.

HUYU Ndiye JPM Mzee wa Kuteua na Kutengua..Huyu Hapa Bosi Mpya wa TRA Aliyemteua..!!!

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA .

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema, uteuzi wa Bw. Ndunguru umeanza mara moja .

Kabla ya uteuzi huo Bw. Ndunguru alikuwa Kamishna wa Sera, katika Wizara ya Fedha na Mipango.

Bw. Adolf Ndunguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.

WANAFUNZI 24 Wazama Ziwa Victoria..!!!

$
0
0

Wanafunzi 24 wa shule ya msingi Butwa iliyopo kata ya Izumacheli, mkoani Geita wamezama katika kisiwa cha Butwa katika Ziwa Victoria walipokuwa wanatoka shuleni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Geita, Herman Kapufi, kati ya wanafunzi hao 24 waliozama wakiwa ndani ya mtumbwi, 21 wameokolewa jana usiku lakini watatu bado wanatafutwa.

Taarifa zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 10 jioni baada ya mtumbwi huo kupinduka katika Ziwa Victoria.

Hata hivyo, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga imeelekea kwenye eneo la tukio kushiriki zoezi la uokoaji.

SAKATA la Mauaji ya Kibiti ..Polisi Waja na Mbinu ya Kuwajaza Watu Mamilioni Ili Kuwafichua Wahusika..!!!

$
0
0

JESHI la Polisi mkoa wa Pwani limetangaza zawadi ya Sh. milioni tano kwa mwananchi ambaye atafanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 12 ambao limedai wanajihusisha na mtandao wa mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Onesmo Lyanga, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Jeshi hilo linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao.

Alisema Polisi imepata picha za baadhi ya watuhumiwa na fununu za mahali wanapopenda kutembelea mara kwa mara.

MAJINA YA WATUHUMIWA

Kamanda Lyanga aliwataja watuhumiwa hao pamoja na mwanzilishi wa mtandao huo wa mauaji kuwa ni Abdurshakur Ngande Makeo, Faraj Ismail Nangalava, Anaf Rashid Kapera, Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa.

Wengine ni Shaban Kinyangulia, Haji Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Uponda, Rashid Salim Mtulula, Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame.

“Jeshi letu limewabaini watuhumiwa hao kwa kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi," alisema Kamishna Lyanga.

Alisema polisi imegundua kuwa watuhumiwa hao hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga, kisiwa cha Saninga katka kijiji cha Nchinga na kijiji cha Mfesini kata ya Nyamisati pamoja na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga.

Kamishna Lyanga aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwafichua watuhumiwa wote wa mtandao ambao unahatarisha hali ya usalama mkoani hapa.

Credit - Nipashe

NOMA Sana..Wasira Naye Aaanza Kurusha Madongo Serikalini..Akosoa Ndoto ya Magufuli ya Tanzania ya Viwanda..!!!

$
0
0

Imeelezwa kuwa Tanzania haijawekeza vya kutosha katika kilimo ili kukifanya kiweze kuendesha viwanda nchini.

Mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika Serikali ya Awamu ya Nne, Stephen Wasira amesema hayo na kuongeza kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kilimo na viwanda kwa sababu kilimo kinazalisha malighafi za kulisha viwanda na viwanda navyo, vinazalisha bidhaa au pembejeo za kukuza kilimo.

Katika mwaka wa fedha 2017/18, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaomba Bunge kuiidhinishia Sh267.86 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo.

Kati ya fedha hizo, Sh156 bilioni ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na Sh103 bilioni ni matumizi ya kawaida.

Wasira amesema Tanzania haiwezi kuendelea kiviwanda kama kilimo kitaendelea kuwa nyuma kama kilivyokuwa miaka mingi iliyopita.

 Amesema kitu kikubwa kinachokwamisha ukuaji wa kilimo nchini ni teknolojia duni.

“Kilimo chetu kinakabiliwa na teknolojia duni, kwa mfano unaona watu bado wanavua kwa kutumia ndoano. Ilitakiwa tuanze kuvua kwa kutumia boti za kisasa ili kuongeza mazao ya samaki, kwenye kilimo hivyo hivyo,” amesema Wasira.

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika

Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote

..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.

Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14.

Na mengi zaidiWhatsapp +255 674 835107 
Calls +255746757102

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..

VIDEO: Kala Jeremiah Aumendea Urais

$
0
0
Msanii wa hip hop ambaye anafanya vizuri na hit ya Wananduto Kala Jeremiah amefunguka na kusema hawezi kugombea ubunge kwani tayari ameshafanya kazi hiyo kwa miaka mingi na sasa anasubiri muda ufike aweze kugombea nafasi ya Urais.

Mbele ya kamera za eNewz Kala amesema kuwa kwa muda mrefu ameshaombwa na wanasiasa mbali mbali pamoja na wananchi ashiriki kugombea nafasi hiyo nzito ya kuwakilisha wananchi lakini bado kwa upande wake haitoshi kwani ameshiriki kuwawakilisha wananchi tangu alipotoa wimbo 'Wimbo wa Taifa'.

"Nilishaombwa sana kuwa mgombea wa ubunge lakini ukweli tayari nimeshakuwa mbunge kwa miaka mingi lakini kusema tena niende kugombea ubunge haitoshi. Nafasi ya Urais ndiyo nayoitaka lakini siwezi kusema ni lini ila jua ipo siku mimi nitagombea nafasi hiyo"- Kala alifunguka.

Mtazame hapa Kala Jeremiah akifunguka.

Taarifa ya Yusuf Manji Kutangaza Kujiuzulu Yanga, Tamko Rasmi la Klabu Hili Hapa

$
0
0
Baada ya taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kueleza kuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji ameachia ngazi kuiongoza Yanga, tamko rasmi limetolewa juu ya ukweli wa suala hilo.

Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa ametoa tamko kwa kusema kuwa hajapata taarifa rasmi juu ya ukweli wa suala hilo lakini amethibitisha kuwa bado hajawasiliana na Manji kama kweli amechukua uamuzi huo.

Akizungumza juu ya taarifa hizo, Mkwasa alisema: “Sijapata taarifa hizo rasmi, mimi ndiyo mtendaji mkuu wa klabu, bado sijakabidhiwa barua kwa kuwa sifanyi kazi kwa kutumia mitandao.

“Tunajua kuwa mitandaoni kuna taarifa nyingi ambazo siyo za kweli na zipo nyingine ambazo zimesababisha baadhi ya wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, hivyo nasubiri kuona kama ni kweli, basi nitapatiwa barua rasmi na nitatoa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo.”

Alipoulizwa kama amewasiliana na Manji hivi karibuni, alisema: “Nimekuwa nikiwasiliana naye kwa njia ya barua pepe kwa masuala ya kiofisi lakini sijakutana naye siku mbili hizi.”

Tangu mapema leo Jumanne kumekuwa kukisambaa barua ambayo inaonekana imesainiwa na mwekiti huyo akielezea uamuzi wake wa kutangaza kujiuzulu. Barua yenyewe inayosambaa hii hapa:


Mapenzi Yanawazidi Nguvu Izzo Buzness na Abela Music

$
0
0
YAWEZEKANA kukawepo maneno mengi ya kuzungumza juu ya ukaribu wa wanamuziki wawili Emmanuel Simwenga ‘Izzo Buzness’ na mwanadada anayefahamika zaidi kwa jina la Abela Music, lakini kubwa ni juu ya kuhusishwa kwa wawili hawa kuzama kwenye dimbwi la mahaba. Tetesi juu ya mkali huyu wa michano Bongo kutoka na Abela zilianza kusambaa muda mfupi tu baada ya yeye kumdaka mwanadada huyo kutoka Ughaibuni alikokuwa anaishi kwa ajili ya masomo na kuunda kundi wakijiita The Amaizing.

BUZNESS AKANA UHUSIANO

Hata hivyo tetesi hizo za kutoka na Abela, ‘mzee baba’ Buzness amezikanusha mara kadhaa. Muda mwingine amekuwa mkali na kudai watu wanashadadia kitu ambacho si kweli. Kwamba yeye na Abela wapo kwa ajili ya kazi tu na baada ya hapo kila mmoja wao ana maisha yake mengine, jambo ambalo linapingana na vitendo pamoja na mienendo yao.



VITENDO VYAWAUMBUA

Mbali na Buzness kukanusha kutoka na Abela vitendo vinawaumbua. Ukweli ni kwamba wawili hawa ni kama kumbikumbi. Muda mwingi wanakuwa pamoja.

Katika kazi na sehemu tofautitofauti wakila bata na wanaowafahamu zaidi wanasema hata anapoishi Buzness mitaa ya Sinza B, mwanadada huyo anaonekana mara kwa mara jambo ambalo linazidi kuzua maswali zaidi. Acha na hayo, hivi karibuni Buzness na mwanadada huyo walikuwa kwenye shoo ya mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Fid Q pale kwenye Ukumbi wa Next Door, Masaki Dar. Wakiwa pale walionekana kuwa karibu mno.



Lakini kilichowafanya watu wapigie mstari tetesi juu ya wawili hao ni namna Izzo alivyokuwa anamkumbatia na hata alivyopanda jukwaani alipokaribishwa kuwasalimia mashabiki. Buzness alimpandishi mwanadada huyo pia jukwaani na kumtambulisha kuonyesha mahaba ‘live’ akimkumbatia na kuwauliza mashabiki walikuwa wanawaonaje.



MAPENZI YAWAZIDI NGUVU

Kutokana na hali halisi hivi ndivyo unaweza kusema. Inawezekana kabisa Buzness anajaribu kuficha juu ya uhusiano wake na Abela kwa masilahi fulani.

Lakini ukweli ni kwamba mapenzi yamewazidi nguvu na kama walivyosema Waswahili mapenzi ni kama kikohozi huwezi kuficha, limekuwa ni suala gumu kwa mkali huyo kuendelea kuwapiga kamba watu kuwa habanjuki kimalavidavi na Abela

MAKALA: BONIPHACE/GPL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live




Latest Images