Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mange Kimambi " Nimekuheshimu Sana Alberto Msando Kwa Maamuzi Magumu Uliyochukua"

$
0
0

Baada ya Taarifu kuwa Alberto Msando amejiuzulu nafasi yake ACT Wazalendo kwa kashfa ya Video Chafu na Gigy Money Mange Kimambi ameandika haya:

From @mangekimambi_ - I wish CCM kungekuwa na viongozi wenye courage hii ya kuwajibika wanapotenda Makosa! Huko CCM kiongozi ameshajulikana ana vyeti feki ila bado anang'ang'ania madaraka na anagoma kuwajibika, kiongozi amekutwa anatumia jina feki meaning alikula kiapo cha Rais kwa kutumia jina feki still hawajibiki! Kiongozi imejukikana anajenga mansion la mabilioni kisirisiri huko Mwanza na ushahidi umewekwa still hatuoni uwajibikaji wowote ule, kiongozi imejulikana anatumia magari ya Watu aliowatuhumu kuwa wauza unga still hawajibiki, kiongozi kaonekana akivamia studio kwa mitutu still hawajibiki, why??? .
.
We are all human and we make mistakes! Ila unapokuwa kwenye nafasi ya uwongozi second chances are hard to come about! Kusema kweli alichofanya Alberto sio kitu ambacho wanaume wa TZ hawafanyi tena they do worse alichokosea yeye ni ku-Allow ile recording! That's the only thing nimeshindwa kuelewa, how did he allow that to happen??? Kusema kweli Mimi Hata nikiwa napiga story tu na Watanzania huwa nataka simu zote nizione mezani Maana mtu hachelewi hata kuwa anakurekodi!
.
.
Alberto nimekuheshimu kwa maamuzi haya uliyoyafanya! Ingekuwa ni kiongozi wa CCM asingewajibika ingepita tu as if hajafanya kitu! angeendelea na maisha yake
.
.
Ila nna swali so Alberto siasa ndo basi tena?? Au? Kwani hawezi kuingia kwenye chama kingine akaanza mpya?? Aiseee Giggy Money umetupotezea kichwa tulichokuwa tunakihitaji sanaaaaaa!
.
.
Kaka Alberto we Love you na hatutosahau ulichowafanyia Wema Sepetu na wale wasaniii wengine baada ya Bashite kuwabambikia makesi, nchi Ina wanasheria maelefu Ila ni wewe peke yako uliejitoa kuwawakilisha wasaniii wale tena bureeee! .
.
Wewe ni binadamu hujakamalika, if anything Leo ume prove wewe unafaaa kuwa kiongozi na unajua nini Maana ya uwongozi sababu umeona kosa lako, ingekuwa ni maViongozi ya CCM yangebebana na wala hakuna ambae angejiuzuru!! Tuangeambia tu ' Mimi Sipangiwi'
.
.
.
#Repost @jamiiforums (@get_repost)
・・・
Mshauri Mkuu wa ACT Wazalendo, Wakili Albert Msando amejiuzulu nafasi hiyo na kueleza kuwa anawajibika kwa kosa la kukiuka maadili.
.

Uongozi wa Chama wapokea barua na wakubalina na hatua hiyo ya kuwajibika kw

Madam Flora: Mume wangu ni shujaa

$
0
0

Msanii wa nyimbo za injili nchini, Madam Flora amefunguka na kusema mume wake wa sasa Daudi Kusekwa ni mwanaume shujaa kwani ni mtu aliyevumilia mengi.

Madam Flora alisema hayo siku ya kuzaliwa kwa mume wake huyo ambayo ilikuwa Jumapili  huku akimtakia maisha marefu na mafanikio mema

"Hongera mume wangu Daudi Kusekwa kwa kuzaliwa, Mungu akupe maisha marefu na yenye amani na furaha tele. Wewe ni mwanaume shujaa, nakupenda sana Daudi wangu na ninakuombea ufanikiwe zaidi kiroho na kimwili. Furaha yako ni furaha yangu" aliandika Flora.

Kwa upande wake Daudi Kusekwa aliitumia siku hiyo pia kumshukuru Madam Flora na kudai amepata mke mwema mwenye mapenzi ya dhati na yeye

"Napenda kumshukuru Mungu wangu kwa kunipa mke mwema na mzuri, anayenipenda kwa dhati"- alisema Daudi Kusekwa

Gwajima kumuanika tena Bashite, adai 'ameliamsha Dude'

$
0
0

Gwajima kumuanika tena Bashite, adai 'ameliamsha Dude'

Watu wengi wameonekana wakishabikia mitandaoni na kudai kuwa wanasubiria jumapili inayokuja kwa hamu

Unajua Athari za Kuitana Sweet, Dear na Baby Kwa Watu Ambao Sio Wachumba ama Mke na Mume?

$
0
0

BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby!

Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine).

Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji.

HUTUMIKA WAPI HASA?
“Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.”

Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha penzi la dhati lililopo moyoni mwa mhusika kwenda kwa mpenzi wake.
Husisimua na kuongeza ladha ya mapenzi ya kweli. Kumuita mpenzi wako kwa majina ya kimapenzi 

huongeza zaidi upendo na msisimko wa moyo. Mwenzi hujiona wa kipekee na mapenzi huzidi kukua.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile, ila iwe inatambulika vizuri na anayetamkiwa.

ATHARI SASA!

Kwa upande mwingine kuna athari za kutumia maneno hayo. Zama hizi, maneno hayo yanaonekana ya kawaida tu. Mtu yeyote anaweza kumuita yeyote mpenzi, honey, baby n.k. Hapo ndipo kwenye tatizo lenyewe.

Kwa ujumla wanawake ndiyo wanaongoza zaidi kuitana majina hayo. Wakati mwingine huenda mbali zaidi na kuwaita hata wanaume majina hayo ya kimapenzi. Si rahisi kuona athari zake kwa haraka na moja kwa moja, lakini zipo na wengi zimewasababishia matatizo. Ngoja tuone..

HUPUNGUZA THAMANI

Kama nilivyotangulia kusema awali, maneno 
niliyotaja hapo juu husisimua na kuongeza mapenzi. Kwa kuyatumia vinginevyo, basi kwa kiasi kikubwa huanza kukuathiri na kupunguza thamani ya neno lenyewe.

Kama unaweza kumwita mfanyakazi mwenzako dear, mtu wa jinsi sawa na wewe sweet ni wazi hata utakapomuita mpenzi wako au wewe kuitwa na yeye, halitakuwa na nguvu sana ya mapenzi kwa sababu ni neno ulilolizoea kila wakati.

HUKARIBISHA USALITI
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Veronica, mfanyakazi wa saluni moja ya kiume iliyopo Sinza, Dar alitoa ushuhuda ufuatao:
“Mimi naishi na mchumba wangu, tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu. Nafanya kazi saluni. 

Tangu nimeanza hii kazi, nimejifunza kutumia maneno matamu ya kumfurahisha mteja na wakati mwingine kumfanya akupe tipu baada ya kumaliza kazi.

“Kuna kaka mmoja nilizoeana naye sana. Kama kawaida, huwa namkaribisha kwa kumuita dear au sweet. Wakati nikiendelea kumfanyia scrub, mazungumzo yetu hutawaliwa na dear, sweet, nikajikuta nimezidi kumzoea.

“Kwa sababu tulibadilishana namba, mara akaanza kuwa na mazoea ya kunitumia meseji, akija ananipa pesa, anaondoka. Mazoea yakazidi. Nikajikuta nimemzoea na kuna siku ambayo siwezi kuisahau kabisa.

“Ni siku niliyomsaliti mchumba wangu...mbaya zaidi na huyo jamaa naye ana mke wake. Niliumia sana, lakini naamini kama nisingekuwa na mazoea ya kumuita majina ya kimapenzi nadhani nisingeingia mtegoni. Moyo wangu unauma sana, najuta kumsaliti mpenzi wangu.”

Unaweza usione athari hii moja kwa moja, lakini ndugu zangu chukua jambo hili leo; wanaume wengi wakiitwa kwa majina ya kimapenzi husisimka sana – hujiona wenye bahati na mara hushawishika kuingia mapenzi.

Kama mwanamke hatakuwa makini atajikuta ametumbukia. Ya nini yote hayo, wakati unaweza kubadilisha mazoea hayo? 

ANGALIA TOFAUTI
Rafiki zangu, kati ya maneno niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na wasio na uhusiano lakini wawe na undugu wa damu. Mathalani baba, mama, kaka, dada, shangazi nk.

Hakuna tatizo kumuita mtu mpendwa, lakini siyo baby, sweet, mpenzi na mengine yenye maana ya moja kwa moja ya kimapenzi. Umenipata? Akili za kuambiwa, changanya na zako kisha unazifanyia kazi! Chukua kinachokufaa!
Hadi wiki ijayo kwa mada nyingine. Wewe ni muhimu sana kwangu.

Soma Mambo Haya Utagundua Kama Unampenda au Unajilazimisha

$
0
0

Watu wengi wako kwenye uhusiano wa kimapenzi bila kujua kama kweli wanapenda kwa dhati au wanajilazisha? Ili kutambua upendo wako jipime kwa maswali yafuatayo:

1 - Unapoamka asubuhi wazo la kwanza kukujia linamhusu mpenzi wako au unafikiria zaidi kazi na mambo mengine? Una msukumo wa kutaka kumsalimia na pengine kumuuliza anapenda afungue kinywa kwa chakula gani? 

2 - Je umekuwa mwepesi na mwenye furaha kubwa kuwaambia rafiki zako wa karibu juu ya hisia zako kwa mpenzi wako? Unajisikiaje wanapokushawishi vibaya kuhusu yeye?

3 - Je, anapokwambia anakuja kukutembelea huwa unajisikia hamasa moyoni kiasi cha mwili kusisimka?

4 - Unapokuwa peke yako mawazo yako yanatawaliwa na yeye au unafikiria kucheza gemu kwenye simu yako na kujifariji kwa vitu vingine?

5 - Unapompima kwa kumlinganisha na wengine anachukua nafasi ya kwanza au anazidiwa?

6 - Je, unapomfikiria na kupata kivutio fulani ndani ya moyo wako kuhusu ucheshi na utani wake huwa unatabasamu hata ukiwa peke yako? 

7- Unajisikiaje wazo la kusalitiwa linapokujia, unaona ni sawa au unahuzunika kiasi cha kupoteza furaha na kutamani uambatane naye kila aendako ili usiibiwe?

8 - Hebu jiulize ni mara ngapi umekuwa ukishawishika kumnunulia mpenzi wako nguo, mapambo au vitu kwa lengo la kumfanya avutie au ndiyo umemtelekeza na kumwacha aonekane mchafu na asiyevutia mbele za watu?

9 - Je, umekuwa mtu wa kujijali mwenyewe kwa mavazi na mwonekano wako kwa lengo la kumfanya mwenza wako afurahie kuwa na wewe au ndiyo unajiweka katika mazingira ya ovyo yanayomtia aibu kwenye jamii?

10 - Unapoota ndoto za kimapenzi usiku, amekuwa akikutokea yeye au kuna wanaume/wanawake wa pembeni ndiyo wanajitokeza katika kuota kwako?

11- Unaposikiliza nyimbo za kimapenzi huwa unahisi ujumbe huo ni kwa huyo umpendaye au unauelekeza kwa mtu mwingine?

12 - Je, marafiki wa karibu wa mpenzi wako wamekuwa wakikupa kipaumbele au wanakudharau na kutopenda kukutana na wewe?

13 - Unajisikia furaha kuwa naye au huwa unapenda ubaki mwenyewe nyumbani ili ufanye mambo yako unayodhani uwepo wa mpenzi wako ni kikwazo?
14 - Je, umekuwa ukitafuta kwa nguvu nafasi za kukutana na mwezako au ndiyo kila siku uko bize na kazi?’

15 - Unapomtathmini mpenzi wako unajiona umepata au umejishikiza wakati ukitafuta mwingine?

16 - Umekuwa mwepesi kiasi gani kukumbuka ahadi zako kwake au kila unachopanga kumfanyia unasahau? Kumbuka kuhusu kumpigia simu, umekuwa ukijikuta ukisahau mara kwa mara?

17 - Vipi mpenzi wako anapopata nafasi ya kukushika sehemu yoyote mwilini wako, huwa unahisi msisimko mkali au mpaka ulazimishe hisia?

18 - Je, uko tayari kumwamini kiasi cha kumwekea dhamana?

19 - Kama utasikia mpenzi wako anakusifia kwa wenzake au kukuthamini kwa lolote utajiona mwenye bahati duniani? 

20 - Unapofikiri hadhi yako unaona inalingana na mwenzako au unahisi umemzidi na kwamba mapenzi yako ni kama umemsaidia kumweka juu?

21 - Unapopata siku ya kupumzika, mtu wa kwanza kumpa kipaumbele cha kujumuika naye ni huyo mpenzi wako au unapenda kufanya mambo mengine?

22 - Je, umekuwa ukitamani kumpigia simu kwa lengo la kusikia tu hata sauti yake na ukahisi furaha?
Mpenzi msomaji wangu, haya ni baadhi ya maswali ya msingi ambayo majibu yake yanaweza kukusaidia kujua kama unampenda au unaulazimisha moyo wako. Naomba ukae peke yako na ujibu maswali haya ambayo mengi yako kwenye msingi wa jibu la ndiyo au hapana.

Vyakula vinavyoongoza kwa kuongeza akili kwenye ubongo

$
0
0

Katika mwili wa mwanadamu hakuna kitu chenye umuhimu mkubwa kama ubongo, ubongo ndio ambao humsaidia mwanadamu katika kufanya mambo mbalimbali, hata hivyo inaelezwa ya kwamba ubongo wa mwanadamu ndio humfanya mwanadamu kuonekana hivyo alivyo.

Hivyo inaelezwa ya kwamba ili mwanadamu aweze kuongeza akili, katika kufikiri na kutenda mambo mbalimbali anatakiwa kula vyakula vifuatavyo:

1. Mafuta ya samaki.
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama sangara na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

2. Ulaji wa mbegu za maboga.
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama
karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, huweza kusaidia kuweza kuongeza akili.

3.Pilipili kali.
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa. Hivyo unaweza ukatumia pilipili kali kama vile pilipili kichaa, pilipili mbuzi kwani hizo ni mifano ya pilipili kichaa.

4.Nanasi.
Utumiaji wa nanasi pia ni miongoni mwa matunda ambayo husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongezea uwezo wa kiakili.

5. Nyanya
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.

6.Karanga
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

7. Mayai ya kienyeji.
Mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

MSHAURI wa ACT Wazalendo Albert Msando Ajiuzulu Baada a Video Yake Chafu Kusambaa Akifanya Mapenzi na Gigy Money..!!!

$
0
0

Wakili Alberto Msando amejiuzulu nafasi yake ya ushauri wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Taarifa iliyotolewa jana, Jumanne na kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe imeeleza kuwa Msando ameandika barua ya kujivua wadhfa huo ambayo imepokelewa na chama hicho.

“Ndugu Msando anawajibika kwani anapaswa, nanukuu  ‘kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka.’Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama,”amesema Zitto.

Zitto amesema Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya ACT.

“Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake. Msando ameomba msamaha kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba,”amesema Zitto.

NOMA Sana ..Wabunge wa Afrika Mashariki Waibua Hoja ya Ufisadi Upya..!!!

$
0
0

Bunge la Afrika Mashariki (Eala) lililoanza kikao chake cha siku 14  jijini hapa na cha mwisho kwa Bunge la Tatu linalofikia ukomo Juni 4 limelitaka Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki kuharakisha uchambuzi wa kikosi kazi kilichoundwa kuchunguza ufisadi katika Sekretariati ya EAC.

Baada ya dua jana (Jumanne), Abubakar Ogle alisimama kwa kutumia kanuni za Bunge ibara ya 30 (l) inayompa mbunge uwezo wa kuwasilisha hoja mahsusi yenye masilahi kwa umma na kwa haraka, na baada ya kupewa nafasi alitaka Bunge lijadili mustakabali wa EAC baada ya taarifa ya uchunguzi kubaini ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Amesema kikosi kazi kilichoundwa licha ya kujiridhisha na tuhuma zilizojitokeza kulingana na taarifa ya mtumishi wa EAC aliyemaliza muda aliyedai kuna ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za jumuiya, pia kilibaini mambo zaidi ya yaliyotarajiwa ambayo yanafanya uhai wa EAC kuwa shakani.

Spika wa Bunge la Eala, Daniel Kidega alimtaka mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki ambaye ni Naibu Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda, Julius Maganda kujibu hoja hiyo.

Maganda amesema uchunguzi umekamilika ila bado haujawasilishwa kwenye baraza.

"Mheshimiwa Spika naliomba Bunge  liwe na subira, tutakapokuwa tumepata taarifa kamili ya uchunguzi tutaifanyia kazi kwa kutoa mapendekezo kwa wakuu wa nchi za EAC," amesema Maganda

Wabunge walichangia hoja hiyo ni Bernard Mulengani, Dora Byamkama, Sarah Bonaya, Agnes Mumbi na Nancy Abisai, ambaye alionyesha hofu juu ya mustakabali wa jumuiya katika mazingira yanayoendelea katika Sekretariati ya EAC.

Patricia Hajabakiga, amesema vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi haviwezi kukubalika na jukumu la Bunge ni kusimamia mihimili mingine ili kuhakikisha utawala bora unakuwapo.

MAGUFULI Aifikiria Tanzania ya Kuzalisha Umeme wa Megawatts 10000 kwa Siku..!!!

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Tanzania imejiwekea malengo ya kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka Megawatts kati ya 1,500 na 1,800 zinazozalishwa hivi sasa hadi kufikia Megawatts 10,000.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CNMIF na Mbunge wa Bunge la Wananchi wa China Bw. Zhan Xin na kuongeza kwamba ili kufikia malengo hayo wawekezaji wanakaribishwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vilivyopo kama vile gesi, makaa ya mawe na jua.

Amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Shirikisho la Taifa la Utengenezaji wa Mitambo ya Viwanda la China (China National Machinery Industry Federation - CNMIF) kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawapa ushirikiano wa kutosha katika mpango wao wa kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme, viwanda na kilimo hapa nchini.

“Kwa hiyo Ndg. Zhang Xin kawaambie wawekezaji wenzako wa China waje Tanzania, nchini zetu ni ndugu na marafiki wa miaka mingi, itakuwa jambo jema wakija kuunga mkono juhudi zetu za kujenga viwanda kwa kuzalisha umeme mwingi na pia kushiriki katika miradi mingine ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara” amesema Mhe. Rais Magufuli.

MVUA ya Siku Sita Yasababisha Vifo vya Watu 10 na Kuharibu Nyumba 262 za Makazi ya Watu..!!!

$
0
0

Tathmini ya madhara yaliyotokana na na mvua zilizonyesha kwa siku sita mfululizo wiki iliyopita mkoani hapa zimeonyesha kuwa hadi sasa watu 10 wamekufa huku  nyumba 44 zikibomoka na nyingine 218 zikizingirwa na maji.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba ametoa  taarifa ya tahmini hiyo jana, Jumanne wakati akizumgumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Wakulyamba amesema katika yaliyotokena na mvua hizo, watu 10 walimepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, kuangukiwa nyumba na kutumbukia kwenye mashimo  ambapo  saba kati yao  walikuwa wakazi wa Wilaya ya Korogwe, wawili Muheza na mwingine ni mkazi wa Jiji la Tanga huku 20  wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, nyumba 44  ziliezuliwa paa, 218 zilizingirwa na maji, 12 zikisombwa na mafuriko.

Amesema wilaya zilizoathirika zaidi ni Korogwe,Tanga na Lushoto huku Pangani,Mkinga na Handeni zikipata athari  ndogo.

Kamanda huyo alisema katika mafuriko hayo,barabara zilizopo katika za Wilaya mbalimbali mkoani Tanga,zimeathirika kwa kubomoka,kuvunjika makaravati pamaoja na madaraja.

"Kama mnavyoona mvua bado zinaendelea, nawatahadharisha wanaokaa kwenye nyumba zilizopo mabondeni wasisubiri maji yaingie ili waokolewe, kuna wakati mwingine uokoaji unaweza kutofanikiwa na kujikuta mnaangamia,"amesema Wakulyamba.

BAADA ya Kuachana na Kuimba Taarab..Mzee Yusuph Aaamua Kuja Kivingine kwa Staili Hii ya Kusaka Pesa Mjini..!!!!

$
0
0

Aliyekuwa muimbaji wa muziki wa taarab nchini na mmiliki wa bendi ya Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf ambaye aliamua kuachana na masuala ya muziki na kumrudia Mungu ameibuka sasa kwa kuanza kufanya biashara ya tofali. 

Mzee Yussuf anasema ameamua kufanya biashara hiyo ya tofali za kujengea nyumba kwa kuwa Mungu ndiye amemtaka afanye biashara hiyo na si kitu kingine chochote

"Kwa hakika hii ndio biashara 'Allah' ametaka niifanye na mimi nimeanza kuizowea 'Alhamdulilaah' ukimtegemea 'Allah' hujutii licha ya majaribu na mitihani. Tupo chanika Taliani weka oda yako popote nakuletea"- alisema Mzee Yussuf. 

NAPE Kung'olewa CCM..Vigogo wa Chama Wachukizwa na Jinsi Anavyoikosoa Serikali..Habari za Magazeti ya Leo 2/5/2017..!!!

Natamani Mpenzi Wangu Achepuke na Wanaume Wengine....

$
0
0

Niko kwenye mahusiano na binti mmoja kati ya wengi nilionao.
.
Kiukweli natamani huyu binti achepuke kwa mwanaume mwingine, huyu binti niko nae kwenye mahusiano zaidi ya mwaka mmoja sasa. Natamani achepuke labda huko atapata mwanaume atakaemfaa katika maisha yake
.
Huyu binti ni mwema sana kwangu kiasi kwamba wema wake unageuka kua kero kwangu, mimi ndie mwanaume wake wa kwanza, nina uhakika hajawahi kutoka na mwanamume mwingine kabla yangu na baada yangu.
.
Nikiri kua nilitumia muda mwingi na gharama nyingi kumshawishi huyu binti kua mimi ndie mwanaume sahihi aliekua amemtunzia mwili wake hadi akakubali kuniruhusu kuchana nyavu.
.
Natamani achepuke maana huko aanaweza kupata mwanaume mwingine mwema kwake,kwa kweli hutu binti hastahili kua na mimi, ni mwema kiasi kwamba hadi namuonea huruma, anaomba radhi kwa makosa ambayo hakufanya au nimefanya mimi.
.
Nashindwa huyu binti namuachaje ili aende huko apate mtu anaestahili, namuonea huruma kwamba ameangukia sehemu isiyo salama, nina uhakika kuna watu wengine huko wanaostahili penzi na wema wa huyu binti mimi sistahili

Nape Nnauye Amvaa Tena Mkuu wa Mkoa Sakata la Kuvamia Clouds Media

$
0
0

IKIWA ni miezi miwili imepita tangu kutokea tukio la uvamizi wa kituo cha Clouds Media Group na kuundwa kwa kamati ya kuchunguza tukio hilo, hatimaye aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye  amemvaa  tena  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusema kwamba hakuunda kamati ya kumchunguza yeye, bali aliunda kamati ya kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa kituo cha utangazaji cha Clouds Media Group.
“Niliunda kamati kuchunguza tukio la kuvamiwa kituo cha utangazaji sio kumchunguza RC. Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, hayuko juu ya sheria,” ameandika Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Alipoulizwa kwanini Waziri wa Habari aunde kamati ya uchunguzi wa tukio la uvamizi badala ya kamati hiyo kuundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Nape alijibu kwa kuuliza swali kama kila kamati inaundwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Majibu haya ya Nape yamekuja ikiwa ni saa chache baada ya kuulizwa ni yapi maoni yake kuhusu kauli ya Makonda kwamba hakuwa akifahamu mipaka yake ya kazi ndio sababu alikwenda kuunda tume ya kumchunguza.

Kauli ya Nape kuhusu kuunda kamati imekuja ikiwa ni takribani saa 24 tangu Makonda aliposema kuwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliunda kamati ya kumchunguza.
Makonda alisema hayo jana, ambapo alidai kuwa kamati iliyoundwa na Waziri isingeweza kumhoji kwa sababu haikuwa na uwezo huo kutokana na wajumbe wa kamati hiyo kutofahamu mambo yanayohusiana na masuala ya uvamizi.

MAHAKAMA Yatupa Ombi la Cuf Upande wa Maalim Seif la Kutaka Sakaya na Wenzake Kuzuiwa Uongozi Ndani ya Chama..!!

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali maombi yaliyofunguliwa na Bodi ya wadhamini ya CUF dhidi ya   Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya(CUF), Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma(CUF) na wenzao sita yakuomba mahakama iwazuie kwa muda kujihusisha katika masuala ya uongozi na kufanya mikutano ya chama.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo baada ya kusikiliza pande zote mbili.

Hakimu Mashauri amesema Joram Bashange ambaye aliapa katika kiapo kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini  ya CUF aliapa uongo kwa sababu bodi hiyo ilikwisha muda wake.

Hivyo, Bashange kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF ni uongo  na kwamba yeye binafsi atabeba gharama   za kesi.

Katika kesi hiyo Sakaya na wenzake walikuwa wakiwakilishwa na Wakili, Mashaka Ngole huku bodi ya wadhamini ya CUF ikiwakilishwa na Wakili Hashimu Mziray.

Baada ya Mwakyembe Kutaka Wasanii Waimbe Mapenzi Tu..Kala Jeremiah Ameibuka na Kumjibu Haya Mazito..!!!

$
0
0

Msanii wa hip hop, Kala Jeremiah amemuomba Waziri Mwakyembe kutengua kauli yake ya kuwataka wasanii waache kuimba nyimbo zinazohusu siasa, kwa madai kuwa ni kuwatenga mbali na jamii inayotegemea wasanii kuwasemea mahitaji yao.

Akizungumza kwenye 'story' tatu ndani ya Planet Bongo, Kala amesema kuwa kauli ya  Mh. Mwakyembe haiko sawa kwani inatengeneza 'gap' kubwa kati ya jamii na wasanii na kuongeza kwamba siasa zinazoimbwa na wasanii ndizo ambazo zinasaidia jamii na wakati mwingine zinasaidia serikali kutopoteza pesa.

Aidha Kala amendelea kufunguka kwamba yeye kama msanii anayeimba harakati kwa ajili ya kusaidia jamii yake kauli ya Waziri ni kama inamlazimisha kuimba nyimbo za mapenzi kitu ambacho kwake hakitampa tatizo lakini hasara itakuwa kwa jamii inayohitaji kusemewa.

 Pamoja na hayo Kala amefunguka na kusema wimbo wake alioimba kuwasemea watoto yatima 'Wanandoto' umempatia sifa kubwa kutoka kwenye mashirika mbalimbali yanayojihusisha na kusaidia watu wenye matatizo na kumpongeza kwa kuweza kufikisha ujumbe mzito pasipo kutumia gharama kubwa sana.

Madamu Flora na Mume Wake Mpya Waonyeshana 'Mahaba Niue' Mazito Hadharani.

$
0
0

Msanii wa nyimbo za injili nchini, Madam Flora amefunguka na kusema mume wake wa sasa Daudi Kusekwa ni mwanaume shujaa kwani ni mtu aliyevumilia mengi. 

Madam Flora alisema hayo siku ya kuzaliwa kwa mume wake huyo ambayo ilikuwa Jumapili  huku akimtakia maisha marefu na mafanikio mema 

"Hongera mume wangu Daudi Kusekwa kwa kuzaliwa, Mungu akupe maisha marefu na yenye amani na furaha tele. Wewe ni mwanaume shujaa, nakupenda sana Daudi wangu na ninakuombea ufanikiwe zaidi kiroho na kimwili. Furaha yako ni furaha yangu" aliandika Flora.

Kwa upande wake Daudi Kusekwa aliitumia siku hiyo pia kumshukuru Madam Flora na kudai amepata mke mwema mwenye mapenzi ya dhati na yeye 

"Napenda kumshukuru Mungu wangu kwa kunipa mke mwema na mzuri, anayenipenda kwa dhati"- alisema Daudi Kusekwa 

Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini Afikishwa Mahakamani akiwa na Pingu Mikononi

$
0
0

Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kujibu mashtaka yanayomkabili, tangu alipokamatwa mwezi Machi mwaka huu.

Mwanasiasa huyo aliyeondolewa madarakani kwa kashfa nzito, anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwa ni pamoja na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na kuvujisha siri za Serikali. Hata hivyo, Park aliyefikishwa mahakamani hapo na gari la magereza akiwa amefungwa pingu mikononi alikana mashtaka yote dhidi yake.

Park anatuhumiwa kushirikiana na rafiki yake, Choi Sonn-sil, kuchota fedha kinyume cha sheria kutoka kwa makampuni makubwa ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kampuni ya Samsung, kwa malengo ya kupata mrejesho wa faida ya kisiasa.

Choi Soon-sil ambaye pia anakabiliwa na mashtaka alifikishwa mahakamani pamoja na mwanasiasa huyo lakini pia alikana mashtaka yote dhidi yake.

Kiwango cha juu zaidi cha adhabu kwa kosa la kupokea au kutoa rushwa nchini Korea Kusini ni kifungo cha maisha jela.

Diamond Platnumz - Ili Uwe na Sifa ya Kujiunga na WCB Lazima Uwe na Uwezo wa Jambo Hili

$
0
0

Rais wa lebo ya WCB Diamond Platnumz amefunguka na kusema ni vigumu kwa msanii kujiunga na lebo yake hiyo kama hajui kuandika nyimbo.

Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa wimbo unapoandikwa ndani ya lebo hiyo mara zote unakaguliwa na watu wote ili kubaini kama kuna makosa na kuelekezana.

“Kwanza Rich Mavoko ndiye mgumu kwenye kupitisha nyimbo, ikitoka hapo Ravvanny aipitishe, Queen Darleen aipitishe, ikitoka hapo niipitishe mimi, iende kwa Mkubwa Fella na Babu Tale waipitishe na Sallam aipitishe, ukitoka hapo wewe ni mwanaume haswa,” amesema Rich Mavoko na kuongeza.

“Kwa hiyo wengi wanakuwa na uwezo mkubwa. Labda unaweza ukaja ukasikia kitu kidogo, ukasema ukiweka hapa kitu flani itakuwa poa zaidi, yaani ukiandika unaandika haswa,” ameeleza Diamond.

Nay Wa Mitego Amjibu Waziri Mwakyembe Kuhusu Kutoimba Siasa

$
0
0
Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kumtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kutoa ufafanuzi juu ya kauli yake aliyotoa kuwa wasanii wasijihusishe na masuala ya siasa.

Nay wa Mitego akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio, amesema kuwa yeye anaamini muziki ni siasa na siasa ni muziki hivyo ni ngumu kutofautisha vitu hivyo viwili, hivyo amemuomba Waziri mwenye dhamana kutoa ufafanuzi juu ya kauli hiyo na kudai yeye hajawahi kuimba wimbo wa siasa bali anaimba mambo yaliyopo kwenye jamii.

"Nachoamini mimi muziki ni siasa na siasa ni kama muziki, siasa ni maisha ya watu ambayo wanaishi kila siku na muziki pia ni maisha ya watu ambayo wanaishi kila siku kwa hiyo anahitaji kutoa ufafanuzi wa kutosha juu ya hili. Siasa ni maisha ya watu na muziki ni maisha ya watu, mimi binafsi naamini sijawahi kuimba wimbo wa siasa hata siku moja bali ninaimba maisha ya watu ambayo yanaendelea kila siku na ndiyo maana wengi wanathubutu kusimama upande wangu endapo linatokea tatizo lolote" alisema Nay wa Mitego.

Mbali na hilo Nay aliendelea kusisitiza kuwa kuna haja Waziri kutoa ufafanuzi wa jambo hilo

"Mh. Waziri anatakiwa kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili ili watu wajue kipi hawatakiwi kuimba na kipi wanatakiwa kuimba sababu siasa ni maisha ya watu ya kila siku na muziki wa Hip hop ni maisha ya watu ya kila siku, kwangu mimi muziki wangu hauwezi kubadilika zaidi nitazidi kuongeza vitu ili nisiwaudhi watu na nizidi kuongeza idadi ya mashabiki" alisisitiza Nay wa Mitego
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>