Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live

Nape Aundiwa Zengwe CCM...Yafichuka Kikao Kizito Kinaandaliwa Dhidi Yake..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 25/5/2017..!!!


Alichokisema Nape Nnauye Baada ya Rais Magufuli Kumtengua Uwaziri Prof Muhongo..!!!

$
0
0

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amempongeza Rais John Magufuli kwa kazi iliyofanywa na tume ya uchunguzi wa sakata la mchanga.

Nape anaungana na baadhi ya wabunge ambao pia wamempongeza Rais Magufuli kutokana na kazi aliyofanya kupitia tume hiyo.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Nape ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Machi mwaka huu, ameandika, “hili la mchanga...big up!”

Baada ya kundolewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo nafasi hiyo sasa inashikiliwa na Dk Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Lipumba Amgalagaza Maalim Mahakamani..CUF Yake Yaiangusha ya Maalim Kuhusu Bodi ya Wadhamini *Sasa Yajipanga Kudai Gharama za Usikilizwaji wa Kesi Yao..!!!

$
0
0

CUF kambi ya Profesa Ibrahim Lipumba imeibuka kidedea mahakamani dhidi ya ile ya Maalim Seif Sharif Hamad katika kesi iliyohusu uteuzi wa Bodi ya Wadhamini wa Chama hicho kwa kutupwa kwa ombi la Maalim Seif na kuridhia uamuzi wa Lipumba.

Kwa uamuzi huo wa Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam juzi, upande wa Lipumba umesema utadai upande wa Maalim Seif urejeshe gharama ilizotumia wakati wa usikilizwaji wa kesi na kwamba unaendelea na shughuli za chama.

Uamuzi huo wa Mahakama unaweza kufasiriwa kuwa ni ushindi unaoipa nguvu kambi ya Lipumba katika uendeshaji wa CUF ambayo imekuwa kwenye mgogoro wa uongozi, tangu Mwenyekiti huyo atangaze kurejea kwenye nafasi yake.

Lipumba alitangaza kujiuzulu nafasi yake muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu, mwaka juzi akidai kupinga Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumpitisha Edward Lowassa, kuwa mgombea urais kupitia umoja huo akisema ni usaliti.

Hata hivyo, upande wa pili ulieleza kushangazwa na Lipumba ukisema ni mmoja wa walioshiriki kumshawishi Lowassa kujiunga na Ukawa ili awanie urais.

Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya jana aliwajulisha wanachama na Watanzania kuhusu uamuzi wa Mahakama katika kesi hiyo namba 45/2017 iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini kutoka upande wa Maalim Seif ukiongozwa na Joram Bashange kuwa imefutwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

“Kesi hiyo ilifunguliwa kwenye Mahakama ya Kisutu na upande unaomtii Maalim Seif dhidi ya upande unaosimamia Katiba ya CUF unaoongozwa na Profesa Lipumba, ukiiomba Mahakama kutoa amri kwa Magdalena Sakaya, Abdul Kambaya, Thomas Malima, Masoud Mhina, Zainab Mndolwa na Salama Masoud, kutojihusisha na shughuli za chama,” alisema. 

Alisema kesi hiyo ilisababisha shughuli za chama kusimama kutokana na baadhi ya viongozi waliopachikwa, ambao si wana CUF kufanya shughuli za chama, huku viongozi wengine wakitangazwa kusimamishwa uanachama na timu ya Maalim Seif.

Alisema baada ya maombi hayo kutupiliwa mbali, walalamikiwa waliruhusiwa kupeleka madai ya kufidiwa gharama za kesi.

“Kwa hiyo waheshimiwa wanachama na wananchi kwa ujumla, tunapenda kuwajulisha kuwa kesi hiyo imekwisha na sisi viongozi wenu tunaendelea kufanya kazi za CUF na tutachukua hatua stahiki, ikiwamo kudai kurejeshewa gharama za chama zilizotumika wakati wa usikilizwaji wa kesi husika,” alisema.

Uamuzi
Juzi, wakili Mashaka Ngole aliweka pingamizi dhidi ya mashitaka hayo, akimwomba Hakimu kuyatupilia mbali.

Kwa mujibu wa Ngole, hatua hiyo ilitokana na vifungu vya Katiba ya CUF kueleza kuwa kesi za kushitaki au kushitakiwa hufunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF, lakini wakati kesi ilipofunguliwa, chama hakikuwa na Bodi hiyo.

Alisema wakati kesi ilipofunguliwa, pande zote ndio kwanza zilikuwa zimewasilisha maombi ya usajili wa Bodi mpya na RITA haijasajili upande wowote ule kati ya pande hizo mbili.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Wilbert Mashauri mbele ya mawakili wa pande zote mbili, wa walalamikaji, Hashim Mziray na wa walalamikiwa Ngole, alisema ameridhika na pingamizi lililowasilishwa na walalamikiwa dhidi ya walalamikaji.

Hakimu Mashauri alisema waliofungua kesi hawakuwa na sifa zilizoainishwa kwenye Katiba ya CUF kama zinavyoelezwa kwenye Sheria namba 5 inayozungumzia masuala ya uanzishwaji wa vyama vya siasa kuwa lazima viwe na bodi iliyosajiliwa na RITA.

Alisema kwa kuwa RITA haijasajili bodi yoyote, ni dhahiri kuwa walalamikaji hawakuwa na sifa za kisheria kufungua shauri hilo.

Machi 19 kikao cha Baraza la Uongozi la Taifa la CUF upande wa Maalim Seif kilichofanyika Zanzibar, kilipitisha majina ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini na kuyapeleka RITA.

Baada ya kupeleka majina hayo, walipata taarifa kuwa upande wa Profesa Lipumba nao ulishapeleka majina yao RITA.

Aprili 10, Maalim Seif aliituhumu ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania kuwa inashinikiza RITA ipitishe majina ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini yaliyopelekwa na upande wa Lipumba.

Maalim Seif alisema RITA ikipitisha majina hayo, iwe tayari kubeba dhamana kwa yatakayotokea ndani ya chama.

Wamiliki wa Mgodi wa Acacia Wadai Hawajashirikishwa Katika Ripoti Aliyokabidhiwa JPM..!!!

$
0
0

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia imetoa taarifa kwa umma na kueleza kuwa kamati iliyofanya uchunguzi kuhusu mchanga wa madini  haijawapa ripoti ambayo Rais John Magufuli amekabidhiwa jana.

Katika taarifa hiyo, Acacia wamesema hawajui ni kwa kiasi gani ripoti hiyo itakuwa imeizungumzia kampuni hiyo lakini waliipa ushirikiano kamati hiyo wakati ikifanya uchunguzi.

Hata hivyo Acacia wamesisitiza kuwa huwa inatoa taarifa kamili ya kila kitu chenye thamani ya kifedha ambacho wanazalisha na huwa wanalipa kodi zote stahiki kwa kila madini yanayotakiwa kulipiwa.

Kimenukaaa...Wanasheria Wajitokeza Kumpinga Makonda....!!!

$
0
0

BAADA ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusema aliyekuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, hakuwa na mamlaka ya kuunda kamati kuchunguza tukio lake la kuvamia kituo cha Clouds Media, wanasheria nchini wamesema kiongozi huyo anapotosha umma.

Wamesema kauli ya Mkuu huyo wa Mkoa kuwa ana mamlaka sawa na waziri kutokana na kuteuliwa na Mamlaka moja ya uteuzi si sahihi, wakibainisha kuwa licha kuwa wakuu wa mikoa huteuliwa na Rais kama ilivyo kwa mawaziri, Nape aliunda kamati kuchunguza tukio lililotokea katika eneo linalosimamiwa na wizara yake, na si kuchunguza mwenendo na utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa.

Kiongozi huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa kauli hiyo juzi, wakati akihojiwa na kituo cha luninga cha Star Tv kwenye kipindi cha Tuongee Asubuhi, huku akikwepa baadhi ya maswali kuhusu elimu yake na jina lake halisi kwa kivuli cha “kuandamwa na wauza dawa za kulevya”.

“Hata kwa akili ya kawaida tu, unaweza kutofautisha mamlaka zao. Mkuu wa Mkoa ni kiongozi wa mkoa tu, ila waziri ni kiongozi wa nchi nzima kwa eneo analosimamia au kuongoza,” alisema Profesa Abdallah Safari.

Katika kipindi hicho, Bashite aliponda uamuzi wa Nape kuunda kamati ya kumchunguza baada ya kuvamia ofisi za Clouds Tv, akiwa na askari wenye silaha za moto na kulazimisha sehemu ya kipindi cha Shilawadu kurushwa hewani.

“Matukio kama haya hutokea nchi inapotaka kupinduliwa, lakini kama Rais yupo na nchi haijapinduliwa, basi kuingia ndani ya chombo cha habari na silaha, huku ni sawa na kunajisi uhuru wa habari,” alisema Nape.

Wakati akipokea ripoti ya kamati hiyo baada ya kupita saa takribani 24, Nape alisema ataifikisha kwenye Mamlaka za Uteuzi juu yake kwa maelezo kuwa yeye hana mamlaka ya kumchukulia hatua Mkuu wa Mkoa.

Hata hivyo, Nape aliachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais John Magufuli saa 12 baada ya kupokea ripoti hiyo iliyokuwa na timu ya watu sita.

Wanasheria

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk James Jesse alisema: “Nape hakuandaa mamlaka ya kumchunguza Makonda, yeye alichunguza jambo lililotokea katika wizara yake, alichunguza jambo si mtu.

“Kama angemchunguza Mkuu wa Mkoa, kweli angekuwa hana mamlaka hayo. Lile ni tukio na ili upate picha ni lazima uhoji watu wote ambao walihusika kwenye hilo tukio,” alisema.

Kuhusu mamlaka zao, alisema: “Katiba haisemi kuhusu mamlaka, lakini ukitazama tu, mmoja anaongoza wizara ambayo ni mamlaka ya kitaifa na huyu mwingine anaongoza mkoa. Hivi utasema wote wanalingana kwa mamlaka kweli?”

Alisema ukubwa au mamlaka ya kiongozi hayatokani na ukubwa wa bajeti aliyonayo katika eneo analoongoza, “watu huangalia unaongoza mkoa, wilaya au wizara.”

Katika ufafanuzi wake, Profesa Safari alisema: “Kazi zao zinatofautiana sana. Waziri ni wa nchi nzima na mkuu wa mkoa ni wa mkoa tu. Waziri ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri na katika kutekeleza wajibu wake, waziri ana wajibu wa kuunda tume kuchunguza jambo chini ya wizara yake.”

Aliongeza: “Kama huyo mkuu wa mkoa hataki kukubali kuhusu mamlaka ya waziri sijui anawaza nini, maana hili liko wazi na wanasheria tumelieleza kiundani zaidi. Kama hatambui hilo anashangaza, huko ni kujinyanyua tu.”

Alisema Nape alikuwa na lengo la kutaka kujua ukweli wa tukio lililotokea Clouds Tv, na si kumchunguza mkuu wa mkoa.

Mhadhiri mwingine wa Chuo hicho, Dk Onesmo Kyauke huku akichambua sheria inayoongoza utendaji katika mikoa (The Regional Administration Act), alisema waziri anaweza kutoa mapendekezo dhidi ya mkuu wa mkoa kwa Mamlaka ya Uteuzi ambayo ni Rais.

 “Kama mkuu wa mkoa akifanya kosa, nafikiri waziri anapaswa kuwasilisha malalamiko yake kwa Rais… mkuu wa mkoa anashughulikia mkoa wake tu, lakini waziri anashughulikia majukumu yanayohusu wizara yake kitaifa, yaani nchi nzima, ila tatizo ni kuwa mkuu wa mkoa hayuko chini ya waziri.”

Katiba

Kwa mujibu wa Ibara ya 61 (2) ya Katiba ya Tanzania; wakuu wa mikoa Tanzania Bara watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.

Kifungu kidogo cha (4) kinasema; Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (5), kila Mkuu wa Mkoa, atakuwa na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa kazi na shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mkoa aliokabidhiwa; na kwa ajili hiyo, atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria, au kwa mujibu wa sheria kama hizi au shughuli za mkuu wa mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

Mawaziri

Ibara ya 55 (1) inasema; Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri Mkuu.

Kifungu kidogo cha (2) kinasema; Pamoja na mawaziri waliotajwa katika ibara ndogo ya (1), Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuteua naibu mawaziri. Naibu mawaziri wote hawatakuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri.

(3) Rais aweza kuteua idadi yoyote ya naibu mawaziri ambao watawasaidia mawaziri katika utekelezaji wa kazi na shughuli zao. (4) Mawaziri na naibu mawaziri wote watateuliwa kutoka  miongoni mwa Wabunge.

(5) Bila kujali masharti ya ibara ndogo ya (1), ikitokea
kwamba Rais anahitajika kuteua waziri au naibu waziri baada
ya Bunge kuvunjwa, basi aweza kumteua mtu yeyote ambaye
alikuwa mbunge kabla ya Bunge kuvunjwa.

Sport Pesa Yazikutanisha Tena Simba na Yanga Dimbani..!!!!

$
0
0

Vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga watachuana na timu za Kenya kusaka bingwa wa Ligi ya SportPesa Super Cup.

Ligi hiyo itaanza Juni 5 ambapo Yanga itafungua dimba na bingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Tusker siku hiyo pia kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na AFC Leopards.

Juni 6, Simba itaonyeshana uwezo wa soka na Nakuru All Stars wakati na Gor Mahia itacheza na Jang'ombe ya Zanzibar, mechi zote zikichezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Abass Tarimba alisema mashindano hayo yataendeshwa kwa mtindo wa mtoano na fainali itachezwa Juni 11.

"Bingwa ataondoka na kitita cha Dola 30,000  na mshindi wa pili Dola 10,000 na timu zitakazoingia nusu fainali kila moja itapewa Dola 5,000 na timu zote zitakazoshiriki zitapewa kifuta jasho cha Dola 2,500 kila moja," alisema Tarimba.

JE Dada Unapenda Kuwa Mrembo? Na Kaka Unapenda Kuwa Mtanashati na Kurudisha Heshima ya Ndoa?

$
0
0
JE, DADA UNAPENDA KUWA MREMBO? NA KAKA UNAPENDA KUWA MTANASHATI NA KURUDISHA HESHIMA YA NDOA? Tumia Bidhaa halisi za MARKSON kwa mafanikio ya uhakika na bila madhara. 
Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kuthibitishwa kiafya. 
🍉🌿🍓🍒🎄🍍🍀🍓🍉
Pata hizi 👇👇👇👇👇👇

1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @120,000/=
2. Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa (a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge @180,000/=
3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @120,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa :- 
(a) Gely ya kupaka @130,000/= 
(b) Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @130,000/= (c)Handsome up (mashine) original @200,000/=
6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @120,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula @120,000/=
8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/= 
(b)Mkanda wa kawaida @100,000/= 
(c)Mkanda wa umeme @200,000/=
9 .Kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @120,000/=
10.Kushepu miguu na kuwa minene na kuondoa migimbi @120,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @100,000/=
12.Kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @120,000/= 

NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. 
Wasiliana nasi :-
(+255) 0767447444 na
0714335378
👉🏻Ili kuona bidhaa zetu na baadhi ya shuhuda za waliotumia bidhaa zetu

Mpambe wa Diamond Platnumz Afukuzwa WCB...Zari Ahusika

$
0
0
Aliyekuwa mwanamitindo wa Diamond Platnumz na timu ya WCB, Q Boy Msafi amethibitishwa kutokuwapo ndani ya lebo hiyo baada ya kufutwa kazi kutokana na kosa alilofanya.

Q Boy amesema kuwa alifanya kosa ambalo linahusu gari la Zari (mpenzi wa Diamond Platnumz) na licha ya kuwa kosa lile ni la kibinadamu kwamba yeyote angeweza kulifanya, lakini uongozi wa WCB uliamua kumfuta kazi.

Q Boy alitoa kauli hiyo akifanya mahojiano na kituo kimoja jijini Dar es Salaam ambapo alisema kwa sasa anajikita zaidi katika kazi zake za muziki, na pia anawashukuru mashabiki kwa kumpokea vizuri.

Akizungumzia uhusiano wake na WCB, Q Boy amesema wale ni kama ndugu zake, hana ugomvi nao na kuwa wamekuwa msaada kwake hata baada ya yeye kutoka.

Amefafanua kwamba, hata alipotoa wimbo wake, timu ya WCB haikusita kumsaidia katika mambo mbalimbali. Lakini pia aliweka bayana kwamba yeye ndio anaanza muziki, na anategemea msaada wao sana ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wasanii wa WCB kama Rayvanny, Rich Mavoko, Harmonize hivyo hawezi kuwa na ugomvi nao.

Aidha, Q Boy amesema kuwa uongozi wa WCB umemtaka aendelee na kazi zake za muziki, na endapo patakuwa na uhitaji wowote wa masuala ya mitindo basi watamtafuta.

Mimi na Diamond Tuna Mahusiano zaidi ya Kimapenzi – Jackline Wolper

$
0
0
Muigizaji Jackline Wolper amesema yeye na msanii Diamond Platnumz wana uhusiano wao ambao ni kiwango cha juu kwani wamekuwa wakishirikiana katika mambo mengi.


Katika segment ya kikaongoni inayorushwa na EATV (facebook) inayotoa fursa kwa watu kumuuliza mgeni maswali, moja ya swali lilitaka kujua ni iwapo Wolper alishakuwa na uhusiano wa kimapenzi na Alikiba, Jux, Ray Kigosi na Diamond Platnumz.

“Alikiba ndiyo, Jux alikuwa rafiki yangu wa karibu, Ray Kigosi yule ni kaka yangu namuheshimu sana, Diamond tuna mahusiano zaidi ya kimapenzi, yaani kikazi.

“Diamond tuna mahusiano mengi sana zaidi hata ya kimapenzi, ni bosi wangu, rafiki yangu, mshauri wangu, yaani na mahusiano nae mengi, umenielewa?, kikazi na vitu vingi,” amejibu Wolper.

Katika hatua nyingine muugizaji huyo amesema kinachomzuia kufanya movie na wasanii wa nje ni kutojua kingereza kwa ufasaha zaidi kitu ambacho ameanza kukifanyia kazi.

“Na wish kufanya hivyo lakini kidogo lugha gongano, ndio maana kuna mwalimu wangu huwa anakujaa kila saa 10 pale ofisini kwa hiyo sasa hivi kidogo naprove, kujua lugha kikweli hiyo ndio dream yangu sana kwa sababu kuna wasanii wa nje nawapenda na ninaamini naweza kufanya nao kazi, kwa hiyo nikiwa kwenye zile level zile za juu nitafanya,” ameleeza Wolper.

Gigy Money: Wema Sepetu ni Mwanamke Feki (Video)

$
0
0
Gigy Money ameendelea kuchafua hali ya hewa na safari hii amemchana Tanzanian sweetheart Wema Sepetu kuwa ni feki.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Gigy amedai japo mwanzoni alitamani sana kuwa kama Wema na kukiri kuwa muigizaji huyo alishawahi kuwa role model wake lakini kwa sasa hataki tena anamuona anaishi maisha ya kuigiza.

“Wema ni mtu ambaye she is fake, Yaah! She is fake. Ukimuona WQema hivi live na ukimuona mtandaoni unaweza ukavurugwa, watu wengi ambao hawajawahi kumuona Wema hivi live wanachanganyikiwa, sio kama mimi sasa hivi. Mimi nilikuwa navurugwa magazeti kila siku nikiensda shule napitia Wema kafanya nini? Sasa hivi naishi hayo maisha sasa huwezi kuniambia Wema she is real,” alisema Gigy.

“Mimi naishi hayo maisha by real sasa ndio maana kwake inakuwa changamoto, atafanya nini. Mimi ni changamoto kubwa sana kwa kila mtu ambaye yupo kwenye industry hii, maana sasa hivi unaweza ukaenda kwenye interview ukamfanyia msichana anayekuja interview akamtaja Gigy from nowhere pia. Mimi sifanyi kwaajili nashindana, nafanya kwa ajili yangu,” ameongeza.



Model huyo wa video za muziki, amesisitiza kwa kusema, “Mimi ukweli zamani nilikuwa natamani kuwa kwenye Bongo Movie niwe kama Wema Sepetu, nilikuwa naamini Wema ni msichana mzuri hakuna, nilikuwa naona kukaa hata na Wema na mimi ninaweza nikawa hata mtu kumbe wee! No, mimi ni Gigy Money na watu watataka kuwa Gigy Money soon. Kila mtu ana brand yake na ana nyota yake, usitamani kitu cha mtu, Yule ni Wema hamuwezi kumpambanisha na mtu yoyote.”

Gigy ameendelea kwa kuwataka mashabiki wampe nafasi na vyeo vyake ili awe top na wamthamini kama wanavyofanya kwa madam Sepenga. Akiendelea kufunguka kuhusu Sepetu Gigy amesema, “Last time nimekutana naye hawezi kupiga stori na mimi tena, nimekutana naye kwenye birthday ya Sallam, nilicheza sana lakini nilikuwa ba bae Dangote.”

“Alinuna kweli na alikuwa ananiangalia vibaya lakini unajua ni mtu ambaye alishakuwa inspiration kwangu kwa hiyo siwezi kuonyesha action yoyote kwangu na kiukweli am the first person nilimwambia umependeza, wakati anaingia, am real. Ni kweli alivaa kizamani na umbo lake lilivyokubwa mashallah, alipendeza lakini nilivyopingia ndani tena sasa nilivyoitwa na Dangote kisa kuna Wema tena, niacheni kidogo siwezi kuvumilia. Sasa nikawa nacheza mimi na Dangote akawa ananiangalia mimi,” ameendelea.

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika

Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote

..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.

Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14.

Na mengi zaidiWhatsapp +255 674 835107 
Calls +255746757102

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..

Imefichuka:Wajumbe wa Kamati Iliyomng'oa Muhongo Walitishwa

$
0
0

RAIS Dk. John Magufuli amebainisha kuwa licha ya kamati ya Kuchunguza Makontena ya Mchanga wenye Madini (makinikia) kupewa ulinzi mkali, kulikuwapo vitisho na hata baadhi ya wajumbe kutaka kuhongwa.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi na kamati hiyo, Rais Magufuli alisema vilijitokeza vitisho na watu kuzungumza kwa lengo la kupotosha huku ikionyesha kuwa wamelipwa fedha kufanya hivyo.

 “Tulitumia vifaa vyote vinavyowezekana katika ulinzi, pamoja na hatua hizo wapo waliojitokeza kutaka kuingilia uchunguzi huu. Kwa bahati nzuri majina yao tunayo, wapo waliojitokeza hadharani baada ya kupewa fedha. Kuna mtu anajiitaga Profesa wakati ni Daktari alihongwa fedha mbele ya kamera,” alisema na kuongeza:

“Akaanza kuzungumza ambayo hayajui, nimesikia wengi wakibwatuka wengine kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ya jeuri ya fedha walizopewa. Hatuna ushahidi ila ukishaona mtu anabwatuka kwa suala la maslahi ya taifa, hafanyi bure bali kuna kitu kimempa kiki.”

Rais alisema Watanzania wanatakiwa kutambua kuwa nchi iko kwenye vita ya uchumi ambayo ni mbaya sana.

Alisema mabilioni ya fedha yaliyopotea ni dhahabu tani 7.8 hadi 13.16 kwa makontena 277, ambazo kwa mujibu wa Rais, ni sawa na tani 15.5 za dhahabu ambazo kwa lugha rahisi ni sawa na malori mawili ya tani saba na landrover moja ya tani moja.

 “Hii ni kwa makontena 277, ninajua kuna Tume itatueleza ni makontena mangapi yaliyosafirishwa, ila ninachojua wanasafirisha makontena 250 na zaidi ya 300 kwa mwezi, kwa mwaka ni zaidi ya makontena 3,600 maana yake ni tani 171 hadi 200 za dhahabu, ukizidisha kwa miaka 17 utajua ni tani kiasi gani na trilioni kiasi gani, hii ndiyo Tanzania,” alisema.

“Tunasubiri kamati nyingine itakuja na hesabu kamili na hapo ndipo ripoti yote ya wataalamu itakuwa imekamilika, hiki ni kitu cha kuumiza mno, ni aibu sana, nilifikiri katika hili Watanzania tushikamane.

“Unapoenda kwenye hospitali watu wanakosa dawa, vitanda, mashuka, madarasa hayatoshi, madawati lazima tuchangishane, miundombinu tunahangaika kutafuta hela za kujenga treni mpaka tukope, tujibane, kumbe kuna hela zinamwagika hapa,” alisema.

“Wapo Watanzania tuliwapa wajibu wa kusimamia, hawajali na hilo linauma sana!”

Nyepesi Nyepesi....John Boko Atua Simba

$
0
0
Klabu ya Simba imemsainisha John Boko Mkataba wa  Miaka miwili

Taarifa zinaeleza mkataba huo ni wa awali na inaonekana Bocco ameamua kutua Simba baada ya makubaliano yake na Azam baada ya mkataba wake kwisha, kuonekana unakwenda kombo.

Hata hivyo, Bocco amekuwa hapokei simu ili kulithibitisha hilo suala ingawa hivi karibuni alikanusha kila kilichoandikwa kwenye akaunti yake ya Instagram kuhusiana na kwamba ana mpango wa kuondoka Azam.

Alidai akaunti yake ilikuwa imetekwa lakini hali halisi ilionyesha kwamba hakuwa amezungumza lolote.

Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi yeye alisema walikuwa katika mazungumzo na Bocco baada ya mkataba wake kufikia tamati.

SBL yatoa Zawadi ya Gari Aina ya Heicher ya shs 50m/- Kwa Msambazaji Bora

$
0
0
Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo (wa kwanza kushoto) akimkabidhi nyaraka za gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika,  ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza  katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka  huu wa fedha 2017.wanaoshuhudia katikati ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,na Baraka Kilimba Meneja Mauzo Baraka Kilimba na mwishoni ni Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha
Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo Akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu zawadi ya msambazaji bora ambapo MM Group kutoka Mpanda aliibuka mshindi ,kulia kwake ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy na kushoto kwake ni Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo wa kutangaza mshindi mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangaza mshindi wa shindano la msambazaji bora ambapo MM Group toka Mpanda aliibuka mshindi ,anayefuatia katikati ni Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo na mwishoni kulia ni ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika akijaribu gari lake mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuibuka kama msambazaji bora ,Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.


Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.


Dar es Salaam, Mei 24, 2017-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetoa zawadi ya gari aina ya Heicher  lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa MM Group,  ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza  katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka  huu wa fedha 2017.
Kampuni ya MM Group ambayo  ina makao yake  wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi iliwashinda wasambazaji wengine 85 walioshiriki kwa ajili ya kupata zawadi hiyo  ya kipekee.
Akiendesha  hafla hiyo ya makabidhiano  iliyofanyika katika makao makuu ya SBL Temeke, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo  alimpongeza mshindi  huku akithibitisha kujikita kwa kampuni  hiyo ya bia katika kutambua  juhudi zinazofanywa na wateja wake  katika kuunga mkono ukuaji kwa kampuni.
“Wakati tunapongeza  mchango wa MM Group kwa kuongoza na kushika nafasi ya juu  katika kipengele chake kulikomwezesha kupata zawadi hii, tunatambua pia  kazi nzuri inayofanywa na  wasambazaji wengine, wateja na hali kadhalika wadau wetu. Kupitia uungwaji mkono huu wa dhati, SBL imekua katika uzalishaji  na kufikia kiwango cha juu  katika sekta ya uzalishaji bia  ndani   ya nchi na hata katika ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema Tayo.
Akitoa wito kwa wasambazaji wengine wa SBL kuiga mfano wa MM Group, Tayo aliwahahakishia washirika wa SBL kibiashara wakiwamo wasambazaji na wateja kwamba SBL itaendelea kuwaenzi na kusikiliza mahitaji yao.
“Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuzingatia kwamba  wamekuwa pamoja nasi katika katika safari yetu ndefu na ya mafanikio kibiashara”, alibainisha Tayo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika, wakati akiishukuru SBL kwa zawadi hiyo,  aliwapa changamoto wasambazaji wengine kuendesha na kuenenda na ukaribu wa SBL kwa kufanya kazi kwa bidiii ili kufuzu kwa ajili ya tuzo kama hiyo.

“Naishukuru sana SBL  kwa kuheshimu ahadi yake  na kunituza gari hili Heicher. Hili gari ni zana  muhimu katika biashara yangu ambayo itaniwezesha kukuza shughuli zangu za usambazaji wa bidhaa za SBL,” alisema Bw Joseph Chanika kwa bashasha.

Maneno ya Wema Sepetu baada ya kifo cha Mzazi mwenzake na Zari

$
0
0
Kifo cha mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mume wa Zari The Boss lady, Ivan Semwanga ni moja kati ya habari zinazozungumzwa sana kwenye mitandao ya kijamii kwa kugusa hisia za wengi.

Baada ya Zari kuthibtisha kifo cha aliyekuwa mume wake, watu mbalimbali wamekuwa wakituma salamu zao za pole kwa familia wakionesha kusikitika kwa kuguswa na msiba huu ambapo miongoni mwa watu hao ni Miss TZ 2006 Wema Sepetu.

Wema aliandika kwenye account yake ya Instagram
“Broken hearted…💔💔💔… Rest In Peace Ivan… 🙏🏼🙏🏼🙏🏼 … SHOCKING NEWS kwakweli… rambirambi zangu kwa familia nzima… Mungu awatie nguvu wale watoto jamani… 😔 bado ni wadogo mno… na Mungu amtie nguvu Mama watoto wako…  utakua wakati mgumu kwenu lakini itapita”


Post ya Mwisho ya Mume wa Zamani wa Zari “Ivan The Don”

$
0
0

Leo May 25, 2017 zimeripotiwa taarifa za kifo cha Ivan Semwanga “Ivan Don” mfanyabiashara maarufu kutoka nchini uganda na aliyekuwa mume wa mrembo Zari the Boss Lady, ambaye amefariki baada ya kuugua ghafla takriban wiki moja sasa.

Taarifa za kifo cha Ivan zimethibitishwa na Zari ambaye alizaa naye watoto watatu wa kiume, alikuwa akijulikana zaidi kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kifedha, aina ya maisha aliyokuwa akiishi ikiwemo kutoa misaada ya fedha kila mwezi kwa watu wenye matatizo mbalimbali.

Nimekuwekea post ya mwisho ya Ivan aliyoiweka Instagram muda mfupi kabla ya kuanza kuumwa hadi kifo kinamkuta.

A post shared by Richgang President (@ivandon) on

Mohamed Thabalala wa Simba Anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligu Kuu Msimu wa 2016/17..!!!

$
0
0

Beki wa kushoto wa kutumainiwa wa klabu ya Simba, Mohamed Hussein Hussein 'Tshabalala' a.k.a Zimbwe Jr. amefanikiwa kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika wa 2016/17.

Zimbwe amewashinda Aishi MANULA (Azam) na Saimon MSUVA (Yanga na ameondoka na kitita cha shilingi milioni 10.

Beki huyo ambaye amecheza michezo yote ya Simba ya ligi kuu msimu huu kwa dakika zote 90 kwa kila mchezo ametangazwa rasmi katika sherehe zilizofanyika usiku wa jana Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mbali na tuzo hiyo ambayo ndiyo kubwa, tuzo nyingine zilizotolewa ni kama ifuatavyo... 

Tuzo ya Goli Bora la Msimu inakwenda kwa Shiza Kichuya, bao alilofunga Feb. 25 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga. Kichuya, amewashinda Peter Mwarianzi na Zahoro Pazi

Tuzo ya Heshima inakwenda kwa Kitwana Manara mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars aliyewika miaka ya 1960 hadi 1970

Tuzo ya Ismail Khalfan (U-20) inakwenda kwa Shaaban IDD (Azam) akiwashinda Abdalah MASOUD (Azam) na Mosses KITAMBI (Simba)

Mchezaji Bora Chipukizi ni Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), akiwashinda Shaaban IDD (Azam) Mohammed ISSA (Mtibwa)

Mchezaji Bora wa Kigeni ni Haruna NIYONZIMA (Yanga), akiwashinda Method MWANJALE (Simba) na Yusuph NDIKUMANA (Mbao FC)

Tuzo ya Kipa Bora imekwenda kwa Aishi MANULA (Azam) akiwashinda Owen CHAIMA (Mbeya City) na Juma KASEJA (Kagera Sugar)

Tuzo ya Kocha Bora imekwenda kwa Mecky MEXIME (Kagera Sugar) akiwashinda Joseph OMOG (Simba) na Ettiene NDAYIRAGIJE (Mbao FC)

Tuzo ya mwamuzi bora imekwenda kwa Elly SASII (DSM) miaka 29, amewashinda Shomari LAWI (Kigoma) na Hance MABENA

Tuzo ya mfungaji bora imekwenda kwa Saimon Msuva (Yanga) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), zawadi yao ni Tsh. mil 5.8

KIKOSI BORA (4:4:2): Manula (Azam), Kimenya (Prisons), Tshabalala (Simba), Yakub (Azam), Mwanjale (Simba), Kenny Ally (Mbeya City), Msuva (Yanga), Niyonzima (Yanga), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), Mbaraka (Kagera Sugar), Kichuya (Simba)

Baraka The Prince - Ben Pol Kaimba Upumbavu ..!!!

$
0
0

Baraka The Prince amemchana msanii mwenzake, Ben Pol kwa kumwambia hakuna chochote alichokifanya katika kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Tatu' licha ya kutengeneza kiki kubwa mitandaoni.

Baraka amesema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Istagram huku akilalamika kwa kusema hakutegemea kuona kazi hiyo kwa jinsi alivyojitoa msanii huyo kwa kuweka picha zenye utata katika mitandao na kuwafanya watu kuwa na shauku kubwa kujua ni jambo lilipelekea vile.

"Nimekuwa 'disappointed' sana huu wimbo...Kwa jamaa alivyojitoa nilidhani ni kitu kikubwa kumbe upumbavu..'Save our music".Ameandika Baraka 

Hivi Ndivyo Taifa Linavyoibiwa Madini Mchana Kweupee..!!!

$
0
0

Kamati iliyoundwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuchunguza mchanga wenye madini aliokuwa ameuzuia kusafirishwa nje ya nchi, hii ljana imewasilisha taarifa ya uchunguzi ilioufanya ikiwa na mambo 8 pamoja na mapendekezo 9.

Kamati hiyo imebaini mambo makuu 8 kama ifuatavyo......

1. Dhahabu

Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi. Viwango hivyo ni kati ya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t. Wastani huu ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni 676 (USD 307,292,720).

Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,146,860,330,000 (USD 521,300,150).

Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.

Taarifa tulizopata kutoka kwa wazalishaji pamoja na Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa takriban 200 g/t. Kiwango hiki ni sawa na kilo 4 za dhababu kwenye kila kontena. Hivyo, makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na tani 1.1 za dhahabu. Kiasi hiki cha dhahabu kina thamami ya TZS bilioni 97.5 (USD 44,320,000).

Thamani hii ni ndogo sana ukilinganisha na thamani halisi iliyopatikana katika uchunguzi huu ya kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147. Kutokana na tofauti hii kubwa kati ya viwango vya dhahabu vilivyopo kwenye taarifa za usafirishaji na vile ambavyo Kamati imevibaini, ni dhahiri kuwa Taifa linaibiwa sana kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.

2. Pamoja na viwango vikubwa vya dhahabu kwenye makinikia, Kamati ilipima na kupata viwango vikubwa vya madini ya copper (kiwango cha 15.09% hadi 33.78%, wastani wa 26%), silver (kiwango cha 202.7 g/t hadi 351 g/t, wastani wa 305 g/t), sulfur (kiwango cha 16.7% hadi 50.8%, wastani wa 39.0%) na iron (kiwango cha 13.6% hadi 30.6%,wastani wa 27%).

Copper

Wastani wa kiwango cha copper kilichopatikana ni tani 5.2 na kiwango cha juu kilichopimwa ni tani 6.75 kwenye kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa copper kwenye makontena 277 ni tani 1,440.4 ambazo thamani yake ni TZS bilioni 17.9 (USD 8,138,260) na kiasi cha juu ni tani 1,871.4 ambazo zina thamani ya TZS bilioni 23.3 (USD 10,573,478). Hivyo, thamani ya copper katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 17.9 na bilioni 23.3.

Wolper - Pamoja na Kuwa Mimi ni CCM..2020 Lowassa Akigombea Tena Nitampigia Kampeni Buree..!!!!

$
0
0

Msanii wa filamu nchini, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema endapo mwaka (2020) Mh. Edward Lowassa atagombea Urais basi yeye atajitoa moja kwa moja kumsapoti katika kampeni zake kwani yeye ni shabiki mkubwa sana wa Waziri huyo Mstaafu.

Wolper amesema hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV na kudai kuwa yeye anampenda sana Lowassa pamoja na mkewe na kusema hata kampeni za mwaka 2015 alijitoa kumsapoti Lowassa kutokana na mapenzi yake kwani hakuwahi kulipwa hata elfu kumi.

"Kama Edward Lowassa atagombea urais mwaka 2020 Mungu wangu nitampa sapoti yangu moja kwa moja, mimi nampenda sana Lowassa na mkewe na nilianza kumpenda Lowassa toka kanisani maana kila harambee alikuwa anakuja, kwa hiyo mimi ni shabiki wa Lowassa na mkewe nilifanya kampeni kwa ajili ya kumsapoti Mh. Lowassa na sijawahi kuchukua pesa yoyote lakini watu wake walinitelekeza ndiyo maana nilikwenda CCM" -alisema Wolper.
Viewing all 104702 articles
Browse latest View live


Latest Images