Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Wasanii Watatu Wanao Amini Mambo ya Waganga na Ushirikina Watajwa

$
0
0

Meneja wa wasanii wa bongo fleva maarufu kwa jina la Meneja Maneno, amefunguka na kusema wapo wasanii wengi Bongo wanaamini ushirikina na kukiri kuwa wapo wasanii wengine ambao yeye mwenyewe aliwapeleka kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kuroga.
.
.
Meneja Maneno aliyewahi kuwa meneja wa Diamond Platnumz, Rich Mavoko, Sam wa Ukweli na Nay wa Mitego, amefunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kuwataja wasanii ambao aliwahi kuwapeleka kwa waganga na ambao wanaamini sana ushirikina kuwa ni pamja na Rich Mavoko, Sam wa Ukweli huku akisema katika wote Diamond Platnumz ndiyo zaidi yao. "Ndele ni sehemu ambayo baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema 'Yes' ni 'Yes' tu kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa waganga kuroga ni pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko Kigamboni ndani ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi katikati yaani usiku ule unajifanya chizi kama umevurugwa" alisema Meneja Maneno.
.
.

Meneja Maneno aliendelea kutoa orodha ya wasanii hao ambao kwao shiriki ni kitu ambacho wanakiamini na kukiri kwenda nao huko na kufanya mambo hayo "Hata Sam wa Ukweli siwezi kukataa, ni watu ambao imani yao iliwapeleka huko lakini mimi nakumbuka kazi yangu niliyokuwa nafanya sikutaka kwenda kwa waganga.... ila sasa huyu Mondi sasa nimepata taabu naye, mara leo twende kwa mjomba, tunapeleka unga, leo tunapeleka mchele na mganga alivyo mshenzi hajawahi kuagiza samaki, yeye ni jogoo, mbuzi" alisisitiza Meneja Maneno .
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Shekhe Aomba Vyakula Visipande Bei Ramadhan..!!!

$
0
0

SHEKHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salim, amewaomba wafanyabiashara wasipandishe bei ya bidhaa katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Alitoa maombi hayo jana kutokana na alichosema ni tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa zao wakati wa Mfungo huo ili kujinufaisha binafsi.

“Vyakula vinapanda katika kipindi cha Mfungo na kuwasababishia baadhi ya wafungaji kutomudu hali hiyo, vitu vinakuwa na bei kubwa kuliko miezi ya kawaida,” alisema Salim.

Alisema ni vema Waislamu kujianda katika kipindi cha kuikaribisha Ramadhan kwa kutenda yaliyo mema na kuacha mabaya yasiyompendeza Mungu.

“Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni wa kila Mwislamu, kila mmoja anatakiwa kutii kwa kufunga na wala si jambo la hiyari ni lazima, kwa kila mwumini mwenye uwezo na vigezo vya kufunga,” alisema Alhad.

Aliwataka Waislamu kuwasaidia wasiojiweza kama kukaa na yatima na kuwalisha vyakula akisema hali hiyo itawajengea misingi bora katika kumsaidia asiye na kitu.

Katika hatua nyingine, aliwataka Waislamu kuliombea amani Taifa na watu wa mkoa wa Pwani waliokabiliwa na matukio ya mauaji ya kutumia silaha akisema:

“Nawaomba Waislamu tuiombee nchi yetu ya Tanzania amani hasa wenzetu wa mkoa wa Pwani kwa majanga yaliyotokea na tuombee vyombo vyetu vya ulinzi kuimarika ili kulinda na kudumisha amani ya nchi yetu.”

Rasmi..Azam Fc Watangaza Kuachana na John Bocco..!!!!

$
0
0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC ya Tanzania John Bocco ameachana rasmi na klabu yake hiyo aliyoitumikia kwa muda mrefu kwa mafanikio makubwa.

Nahodha huyo wa zamani wa Azam FC na taifa Stars ameondoka Azam FC akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na matajili hao wa jiji la Dar es Salaam wakitumia dimba la Azam Complex.

Kwa mujibu wa uongozi wa Azam FC kupitia kwa afisa habari wa timu hiyo Jafar Idd Maganga wamethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo kwani hawakuwa na mkataba naye tena.

Amesema "Kimsingi Azam FC inatangaza rasmi kuwa kuanzia hii leo Bocco siyo mchezaji tena wa Azam FC", Lakini watamkumbuka kwa mengi mazuri aliyoifanyia timu hiyo mpaka ilipofikia.

Maganga maarufu kama mbunifu amesema Bocco yuko huru kujiunga na timu yoyote hii ni baada ya kumalizika kwa mkataba na hata mazungumzo baina yao kutofanikiwa hivyo wao wanamtakia kila la kheri huko aendako.

Tayari kumekuwa na taarifa za mchezaji huyo mrefu kusajiliwa na Simba taarifa ambazo bado yeye na hata viongozi wa Simba hawajawa tayari kuzungumzia.

Mrema - Gerezani Sio Hotelini Jamani...!!!

$
0
0

Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa Mh. Augustino Lyatonga Mrema amewaonya wananchi kuacha kutenda makosa yatakayo wafanya kukataliwa kurudi kwenye jamii pindi watakapohitaji kupata msamaha 'Parole' na kusisitiza gerezani siyo hoteli.

Mapema wiki akifanya mahojiano EATV, Mhe. Mrema ameweka wazi kuwa hakuna mfungwa anayeweza kupatiwa msamaha na bodi ya Parole ikiwa tayari jamii yake haimtaki na kuongeza kuwa mfungwa atalazimika kutumikia kifungo chake.

Aidha Mrema ameongeza kwamba watu wamekuwa wakifanya makosa makubwa kwenye jamii hali ambayo inawanyima nafasi za misamahaa ambayo ni haki yao na kwamba tatizo linakuja wakati wakupata ruhusa kwa jamii anayoishi kukataa kutoa ruhusa.

"Huwa tunaauenda eneo analoishi au alipozaliwa kuwaeleza watu juu ya msamaha wanaotaka kuutoa na kama wakikataa kwa sababu na wao haki yao kukubali aua kukataa basi mtuhumiwa utarudishwa tu magereza. Nataka kuwaasa acheni kufanya mambo yatakayowafanya mkatliwe, jiepusheni na makosa yatakaowafanya mkose haki yenu labda itokee bahati mbaya" Mh. Mrema alifunguka.

Pamoja na hayo ameongeza kwamba jamii haipaswi kuwakataa watu wao walipo magereza kwani baada ya kumaliza kifungo watarudi kwenye maeneo yao na hawatakuwa na uwezo wa kuzuia waendelee kukaa magereza.

"Jamii inatakuwa ifahamu hawa watu waliopo magereza ni bdugu zao na ni watu wao. Tengezenezeni mahusiano mazuri na siyo kwamba mtu akishafungwa ndio anageuka mnyama mnatakiwa mtambue ni binadamu na ana haki zake zote za kimsingi" aliongeza Mrema.

Watu 1,945 Wafariki Katika Ajali ya Pikipiki Ndani ya Miaka Miwili..!!!

$
0
0


Jumla Watu 1,945 wamefariki dunia katika ajali za bodaboda 5,418 tangu mwaka 2015 hadi Februari mwaka 2017 hivyo serikali imeanzisha mikakati kabambe ya kupunguza ajali hizo ambazo zinapoteza nguvu kazi ya taifa licha ya kutoa ajira nyingi kwa vijana

Akitoa mikakati ya Serikali jana Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kati ya mikakati hiyo ni kupitishwa kwa kanuni ya leseni ya pikipiki na bajaji pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni pamoja na vyombo vya habari.

Mhe. Mwigulu amesema kuwa mikakati mingine ni kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa waendesha bodaboda, kuimarisha usimamizi wa sheria za barabarani pamoja kusisitiza matumizi ya kofia ngumu ili kupunguza madhara pindi ajali zinapotokea.

Aidha Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuwa Serikali kupitia wadau mbalimbali nchini pia wanaendesha semina mbalimbali kwa waendesha bodaboda hao ili kupunguza ajali lakini pia amelitaka suala hilo lianzie kuelimishwa kuanzia ngazi ya jamii ili kulidhibiti kabisa.

Kocha wa Uingereza Afunguka Sababu za Kumtema Rooney Kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa..!!!

$
0
0

Wayne Rooney ameachwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uingereza kwa sababu, kuna wachezaji wengine wana viwango zaidi yake, anasema kocha wa Uingereza Gareth Southgate.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United hajajumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 kilichotangazwa leo kwa ajili ya michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu za Scotland na Ufaransa mwezi ujao.

Rooney pia aliachwa kwenye cha Uingereza, mwezi Machi kwa sababu ya kukosa kucheza mechi nyingi za kucheza kwenye klabu yeka ya Manchester United, na mara ya mwisho kucheza kwenye kikosi cha Southgate, ilikuwa Novemba mwaka jana dhidi ya Scotland.

Kuanza kutemwa kwa Rooney kwenye kikosi, kunaleta shaka juu Nahodha huyo mwenye mabao 53 kwa timu ya Taifa na kuwa mfungaji wa muda wote akiipiku rekodi ya Sir Robert "Bobby" Charlton ya mabao 49 , huenda akashindwa kucheza kwenye michuano ya kombe la Dunia, nchini Urusi mwakani.

"Mara ya mwisho nilisema kuwa amekosa mechi za kucheza, na sasa hivi amecheza kidogo lakini, tumepata wachezaji wanaocheza vizuri, vizuri sana, vizuri kwetu kama Adam Lallana na Dele Alli". Alisema Southgate.

TLS chini ya Lissu Kama Kweli Wanaitakia Mema Tanzania Waungane Kuzima Wizi wa Acacia

$
0
0
Tumesikia mengi kuhusu Acacia kutuibia Watanzania kwa kutumia mikataba, tena iliyoandaliwa na Watazania wenzetu. Kama taifa, hatuwezi kuendelea kulalamika na kunyoosheana vidole, ni lazima tuchukue hatua. Sheria sio Misahafu. Sheria zimewekwa na binadamu na zinaweza kufutwa au kurekebishwa na binadamu pia.

Pamoja na nguvu ya kifedha waliyonayo Acacia Watanzania wakiungana tutashinda hii vita ya kiuchumi. Sasa, TLS kama kweli wanaitakia mema Tanzania waungane na kusimamia mabadiliko ya sheria ili kufuta vifungu vya kinyonyaji na kuhakikisha kila kinachovunwa kwenye ardhi ya Tanzania kinalipiwa kwa haki, na sio kutumia huu ujanja wa 'commercially viable'.

Ni wazo tu
By Hekima Kwanza

Je Mdau Unaonaje Hapo?

Chin Bees Afunguka, 'Navy Kenzo Wanamaisha Mazuri Kwasababu ya Nyimbo Zangu Nilizowatungia'

$
0
0
Mwimbaji staa wa Bongofleva Chin Bees amefunguka kuhusu mahusiano yake na kundi la Navy Kenzo pamoja na mambo mengine ya kimuziki.

Chen Bees amedai kuwa tofauti kwa sababu anafanya kazi kubwa ukilinganisha kipindi cha nyuma ambapo alikuwa anafanya kazi nyingi za watu huku akiushukuru uongozi wa sasa kwa kutoa ushirikiano unaomfanya aendelee kufanikiwa.

Mbali na hayo Chin Bees amezungumzia mahusiano yaliyopo baina yake na Navy Kenzo:
“Kamatia chini mimi ndio niliandika. Verse ya kwanza mimi ndio nilishiriki mpaka ule wimbo kufikia pale lakini watu wanafanikiwa kwa kutumia ubunifu wako kitu ambacho siyo kizuri. Zipo nyingi kama Never ever na Game zote zile nilihusika.” – Chin Bees.

Itazame full video hapa chini kwa kuponyeza Play:

Nina Kipaji cha Kukomolewa Kwenye Mapenzi – Wolper

$
0
0
Malkia wa filamu, Jacqueline Wolper amefunguka kueleza moja na sababu ya mahusiano yake na wanaume wengi kushindwa kudumu kwa muda mrefu.


Muigizaji huyo ambaye ameachana na msanii Harmonize miezi kadhaa iliyopita, amedai kuna baadhi ya wasichana wanaingilia mapenzi yake ili kumkomoa.

“Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipendae” alisema Wolper.

Licha ya Wolper na Harmonize kutoweka wazi sababu ya kuachana, lakini stori ambazo ziko mtaani zinadai Harmonize amemuacha muigizaji huyo baada ya kupata mwanamke wakizungu.

Diamond Amfariji Zari Kufuatia Msiba Mzito Alioupata

$
0
0
Diamond Platnumz ametuma ujumbe wa kumfariji mama watoto wake wake, Zari, kufutia msiba mzito wa Ivan ambaye ni baba watoto watatu wa Zari.

Diamond akiwa na Zari pamoja na watoto wa marehemu, Ivan. Picha hii ni yazamani

Kumekuwa na mengi yanazungumzwa kwenye mitandaoni ya kijamii kuhusu Zari, Ivan na Diamond Platnumz na mengine yamepelekea kuwakera baadhi ya mashabiki wao wa damu.

Diamond ameandika ujumbe wa kumtia moyo Zari The Boss Lady na kuonyesha yupo naye pamoja katika kipindi hicho kigumu anachopitia.

“Natamani ningekukumbatia badala ya kukutumia sms,najua upo kwenye wakati mgumu na ni mpweke, jua kwamba hauko mwenyewe, niko na wewe hapa usiku na mchana,” aliandika Diamond Instagram.

Ivan amefariki dunia Alhamisi hii nchini Afrika Kusini baada ya kuugua ugonjwa wa moyo kwa wiki kadhaa.

Steve Nyerere, Faiza Wazungumzia Kifo Cha Ivan Don

$
0
0

Waigizaji kutoka Bongo Movie, Steve Nyerere na Faiza Ally kwa nyakati tofauti wamezungumzia kifo cha aliyekuwa mume wa zamani wa  Zari ‘Ivan’ aliyefariki hapo jana.
 

Waigizaji hao kila mmoja amedai amejifunza kitu kutoka katika maisha ya Ivan.



Steve Nyerere ameandika,
“Alikuwa na pesa nyingi, alikuwa na uwezo wa kufanya chochote, alikuwa na uwezo wa kununua chochote lakini ameshindwa kununua uhai. Nimejifunza kitu kupitia wewe, tuishi vizuri na watu maana hakuna ajuaye kesho,”.

Kwa upande wake Faiza Ally ameandika ujumbe mrefu usemao,

“Binaadamu akikuchukia hata zuri kwake ni baya na ndio maana huwa na maisha yangu tu kama mimi bila kutaka kuwa yoyote, hakuna zuri mbele ya mtu mbaya. Unajua nini wala sijali naona upuuzi tu kama ya kipuuzi mengine yote yalio pita..Maisha yangu na wanangu yako kwenye mikono salama hata kushinda mikono yangu, yako kwenye mikono ya Mungu mwingi wa rehma. Leo Ivan na matajiri wengine wako wapi? Mali sio kila kitu kwenye maisha yetu tunahitaji amani, mapenzi, maelewano makubaliano.
Nimetoka kwenye kutokua na mlo mpaka sasa namiliki milo, huo ni utajiri mkubwa maana kwanza ni kushiba akili ikae sawa ndio upange habari zingine, so at the end my heart is pure and that what give me amani ya moyo, hayo mengineyo tena yako nje ya uwezo wangu ni mipango ya Mungu"

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika

Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote

..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.

Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14.

Na mengi zaidiWhatsapp +255 674 835107 
Calls +255746757102

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote.

Mjane Aangua Kilio Hospitali Baada ya Kujifungua Mapacha 4, Asema Hawezi Kuwalea

$
0
0
Hali ya umaskini pamoja na kufikiria namna ya kuwalea watoto wanane baada ya kujifungua wanne jana imemtoa chozi mkazi wa Yombo, Ashura Shaibu (37).

“Lakini nilipatwa na mshtuko baada ya kujifungua watoto wanne kwani ni jambo ambalo sikulitegemea,” alisema

Ashura alijifungua watoto hao katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke, lakini mzazi huyo hakufurahia tukio hilo kwa kuwa haikuwa matarajio yake ikizingatiwa kwamba familia yake ni maskini.

“Nilifurahi kusikia nimejifungua watoto wanne ingawa mume wangu amekwishafariki na sina mtu wa kunisaidia kwani hata mama yangu anaishi mbali na mimi na wazazi wa mume wangu wamekwishafariki,” alisema Ashura.

Mume wa mama huyo alifariki Desemba mwaka jana wakati akiwa mjamzito.

Alisema hali yake kiuchumi si nzuri kwani kabla ya kupata ujauzito, alikuwa akijishughulisha na biashara ndogo ndogo katika eneo la nyumba yake lakini mimba ilipofikisha miezi minne, alichoka na kushindwa kumudu shughuli zake na biashara.

“Nina maisha magumu, nina watoto wanane, sijui namna nitakavyowalea,” alisema.

Muuguzi katika wodi ya watoto wenye upungufu wa uzito Hadija Kamote anasema mama huyo alijifungua kwa njia ya kawaida ila watoto walionekana kuwa na uzito pungufu.

“Watoto wamezaliwa wa kiume watatu na wa kike mmoja. Wa kwanza ana uzito wa kilo 2 na gramu 300,wa pili ana uzito wa kilo 1 na gramu 900, wa tatu ana uzito wa kilo 1 na gramu 700 na mtoto wa nne ana uzito wa kilo 1 na gramu 300,” alisema Kamote.

Muuguzi Mkuu katika Hospitali ya Temeke Deodata Msoma alisema mama huyo baada ya kujifungua alionekana kukata tamaa na kuanza kulaumu kwanini amepewa watoto hao.

“Ilibidi tufanye kazi ya kumtuliza na kumtia moyo kuwa asikate tamaa na kumuambia wapo watu watakaomsaidia huku tukijaribu kufanya vitu vitakavyo mfurahisha na kurudisha tabasamu usoni kwake,” alisema Deodata. Atakayeguswa kumsaidia Ashura afanye hivyo kwa kutumia namba 0783- 287929.

Chanzo: Mwananchi

Rais Kagame Kung'atuka Madarani

$
0
0
Rais Paul Kagame wa Rwanda, ametangaza azma yake ya kun'gatuka madarakani baada ya mwaka 2024.


Rais Kagame amethibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa Jeune Afrique kuwa awamu hii ya miaka saba ndiyo ya mwisho na Wanyarwanda wanatakiwa waanze kufikiria mtu mwingine atakayewaongoza baada ya mwaka 2024.

Rais Kagame ameuambia mtandao wa Jean Afrique, kwamba, muda muafaka wa kupumzika umewadia na amewaomba raia wa nchi hiyo waanze kufikiri nje ya mimi baada ya miaka saba.
Kwa sasa hakuna shaka yoyote kuwa Rais Kagame atashinda uchaguzi wa urais wa Agosti 3 mwaka huu na ni ushindi ambao umekuwa ukitabiriwa kwa muda mrefu na Wanyarwanda.

Mwaka 2015 Wanyarwanda wapatao milioni 4 ambao ni zaidi ya asilimia 70% ya wapiga kura, walipaza sauti zao kulitaka Bunge lirekebishe Katiba ili RaisKagame apate nafasi ya kuendelea kutawala.

Bunge lilifanya hivyo ili kumruhusu Rais huyo ambaye ana umri wa miaka 59 kuwania muhula mwingine..

JE Dada Unapenda Kuwa Mrembo? Na Kaka Unapenda Kuwa Mtanashati na Kurudisha Heshima ya Ndoa?

$
0
0
JE, DADA UNAPENDA KUWA MREMBO? NA KAKA UNAPENDA KUWA MTANASHATI NA KURUDISHA HESHIMA YA NDOA? Tumia Bidhaa halisi za MARKSON kwa mafanikio ya uhakika na bila madhara. 
Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kuthibitishwa kiafya. 
🍉🌿🍓🍒🎄🍍🍀🍓🍉
Pata hizi 👇👇👇👇👇👇

1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @120,000/=
2. Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa (a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge @180,000/=
3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @120,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa :- 
(a) Gely ya kupaka @130,000/= 
(b) Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @130,000/= (c)Handsome up (mashine) original @200,000/=
6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @120,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula @120,000/=
8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/= 
(b)Mkanda wa kawaida @100,000/= 
(c)Mkanda wa umeme @200,000/=
9 .Kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @120,000/=
10.Kushepu miguu na kuwa minene na kuondoa migimbi @120,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @100,000/=
12.Kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @120,000/= 

NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. 
Wasiliana nasi :-
(+255) 0767447444 na
0714335378
👉🏻Ili kuona bidhaa zetu na baadhi ya shuhuda za waliotumia bidhaa zetu

Hii Ndiyo Sababu ya Rapa Stamina Kuanza Kuimba Mapenzi na 'Kupiga Chini' Ngoma za 'Mashairi Magumu'

$
0
0
Rappa Stamina anaye-hit kwa sasa na ngoma ya 'Love Me' amefunguka na kudai ameamua kuimba wimbo wa mapenzi, siyo kwa sababu nyimbo zake ngumu zimebuma bali amebadilika kidogo ili kuimba vitu vilivyopo kwenye jamii kwa kuwa yeye ni msanii.

Stamina amefunguka hayo mbele ya kamera za eNewz na kudai kwamba ujio wake mpya na kusema ameamua kuimba maisha yaliyopo kwenye jamii inayomzunguka na kuongeza kuwa hajatoa kwa sababu ameumizwa kimapenzi bali yeye kama msanii ni wajibu wake kwa kuwa mapenzi ni maisha yaliyopo kwenye sehemu jamii.

Akizungumza kuhusu kuimba mapenzi kitu ambacho siyo kawaida yake, Stamina amesema "Hakuna kitu kigumu mbele ya mapenzi kwani hata wao waimba hip hop wana hisia kama watu wengine. Sijatoa Love me kwa sababu nimetendwa ila nimeimba kuwasilisha kazi ya sanaa kwa sababu mimi ni msanii. Mwana hip hop akitoa nyimbo ya mapenzi watu wanamsahangaa kwa nini sisi ndio hatuna wapenzi? mapenzi ni shemu ya maisha" Stamina alifunguka.

Kwa upande mwingine rappa huyo ambaye amemshirikisha  Maua Sama  katika wimbo wake mpya amefunguka na kusema kwamba hakuna wimbo wowote duniani unaobuma kwenye game bali mapokezi ndiyo husababisha kazi kuwa hit au kuonekana kawaida.

"Hakunaga ngoma inayobuma duniani, kwa sababu ngoma wewe unayohisi imebuma kwako kwa mtu mwingine ni kali sana na kwenye simu yake utakuta ndiyo anaisikiliza sana. Ila kinachotokea ni ngoma kushindwa kufika mahali palipotarajiwa na wakati mwingine siyo lazima zote zifike. Kitu kama hit inatokeaga tu kutokana na mapokezi ya watu' Stamina aliongeza.

Wolper Akana Kuwahi Kubadili Dini na Kuwa Muislamu..Adai Ile Ilikuwa ni Maigizo Tu..!!!

$
0
0

Muigizaji Jacquline Wolper amekanusha vikali kuhusu suala la kuwahi kubadilisha dini kwa shinikizo la mapenzi na kwamba yote yaliyowahi kuonekana au kusikika huko nyuma ni mambo ya sanaa.

Wolper amefunguka hayo na kudai kwamba yeye kama msanii kuna mambo anaweza kufanya ya kisanii lakini watazamaji wasijue kama ni sanaa lakini ukweli ni kwamba hajawahi kuhama ukristo na kwenda kwenye dini ya kiislamu.

"Sijawahi kubadilisha dini mimi, Sisi wasanii ndiyo tunajua tunafanyaga mimi mpaka watu wanaamini vitu kama kubadilisha dini. Ukweli wa dini yangu naujua mimi peke yangu lakini mengine yanayoonekana ni kazi ya sanaa" -Wolper alifunguka.

Akizungumzia suala la mapenzi Wolper amesema kwamba amekuwa na changamoto mbalimbali sana za kushindwa kudumu kwenye mahusiano kwa kuwa wanawake wenzake hupenda kumuingilia kwenye mahusiano yake kitu ambacho amekiita kipaji cha kukomeshwa.

"Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipende" aliongeza Wolper.

Niyonzima - Nitawaaga Mashabiki wa Yanga kwa Amani na Heshima Zote..!!!

$
0
0

Kiungo wa kimataifa wa Rwanda anayekipiga katika klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) Haruna Niyonzima amefunguka na kusema yeye atawaaga wana Yanga kwa amani wakati huo utakapofika kwa kuwa ameishi nao kwa muda mrefu kwa upendo na amani.

Niyonzima alisema hayo baada ya tetesi kuzuka kuwa msimu ujao hatakuwa tena Yanga na kuwa atakwenda kukipiga katika klabu nyingine ndipo hapo aliposema kwa sasa hayupo kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia jambo hilo ila kama litatokea basi ataagana vizuri na klabu hiyo ambayo ameichezea kwa muda mrefu.

"Hilo suala siwezi kulizungumzia sana unajua Yanga ni timu ambayo nimekaa nayo na ninaiheshimu, ni timu ambayo nimeweza kudumu kwa miaka mingi hivyo naamini nikija kupata fursa ya kutoka au kuondoka kwenda sehemu nyingine naamini wana Yanga nitawaaga kwa amani na vizuri kabisa lakini kwa sasa siwezi kuzungumza chochote" alisema Niyonzima 

Katika msimu wa ligi ambao umemalizika wiki iliyopita Haruna Niyonzima aliyanyakua tuzo ya mchezaji bora wa kigeni. 

Undani wa Kifo Cha Mume wa Zari Nyuma ya Pazia..A - Z ya Jinsi Ilivyokuwa Wiki Mbili Nyuma Kabla ya Kufariki..!!!!

$
0
0

Kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’, raia wa Uganda, mwenye maskani yake Johannesburg na Pretoria, Afrika Kusini, kimeibua simulizi nzito nyuma ya pazia.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda, katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo usiku wa kuamkia juzi.

MARA YA MWISHO KUONEKANA

Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pati ya Blankets and Wine iliyofanyika huko Kampala, Uganda wiki mbili zilizopita. Ilielezwa kuwa, rais huyo wa Kundi la Rich Gang, mwenye umri wa miaka 39, alionekana aliyedhoofu na asiyekuwa na furaha kama kawaida yake huku akinywa soda na kula samaki, tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa kupiga vinywaji vikali, tena vya bei mbaya. “Nyuma ya hali yake kiafya alionekana dhahiri mwenye matatizo yaliyosababisha hata kula yake kuwa ya kusuasua na kusababisha hali kuwa mbaya zaidi,” kilikaririwa chanzo hicho.

CHANZO CHA UGONJWA

Chanzo hicho kilidai kuwa, chanzo cha Ivan kupatwa na ugonjwa huo ni pale alipotokea Sauzi na kwenda kuangalia moja ya mali zake (mashamba makubwa) zilizopo Kampala na kukuta kuna watu wamebadilisha umiliki bila yeye kujua. Ilisemekana kuwa, kuna wakazi waliotengeneza nyaraka na hati za kumiliki ardhi ya jamaa huyo ambayo ilionesha walikuwa wamiliki wapya ilihali ni mali ya jamaa huyo.

Wakati watu hao wakifanya hivyo, Ivan hakujua kilichokuwa kikiendelea. Ilielezwa kwamba, ishu hiyo ilimsababishia Ivan mshtuko wa moyo na maumivu makali ya kichwa ambayo pia yaliathiri utendaji wake wa kazi wa kila siku.

Mbali na hilo, pia, kuliibuka taarifa za kuuzwa kwa nyumba yake na watu wasiojulikana ambapo alitumia nguvu kubwa kukanusha taarifa hizo na kueleza kuwa kwa utajiri alionao hawezi kuuza nyumba yake ya kifahari iliyopo Munyonyo, Kampala.

“Mwishowe, alipoona hali yake kiafya inakuwa mbaya kutokana na mshtuko uliotokana na mambo hayo, Ivan alichukua ndege na kwenda Afrika Kusini kisha kuripoti mwenyewe katika Hospitali ya Steve Biko Academy iliyopo Pretoria. “Vipimo vilionesha kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo ambao ulisababishwa na kuganda kwa damu kwenye mishipa,” alisema sosi huyo wa jijini Kampala. Mwishoni mwa wiki iliyopita, baba huyo wa watoto watatu aliozaa na Zari alielezwa kuwa hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi hivyo kufanyiwa operesheni kubwa ya kichwa.

ZARI ATHIBITISHA

Kupitia ukurasa wake Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Zari alithibitisha kifo cha mumewe ambapo aliandika

waraka wa simanzi: “Mungu huwapenda wale ambao ni maalum kwake ndivyo ulivyokuwa, umewagusa na kuwasaidia maelfu, ulifanya mengi ya kushangaza na nakumbuka maneno yako ‘maisha ni mafupi mno, acha tuishi kwa ukamilifu’. Hii ni saa ya giza, sasa naelewa kwa nini ulikuwa ukisema maneno hayo kwangu. “Kwa wanao, umekuwa shujaa -aina fulani ya superman. Mtu yeyote ambaye amewahi kuwa karibu yako anajua wewe ni mtu wa aina gani, anajua ucheshi wako.

Watu watakumisi na kukumbuka sana kwa namna nyingi…Ulikuwa IVAN DON.

Baadhi ya mastaa wa Uganda walieleza ni namna gani walivyoshtushwa na kifo cha Ivan. Bebe Cool –Natoa rambirambi zangu za dhati kwake na familia yake. RIP kaka IVAN. Jose Chameleone -Mungu anaumba na kuchukua kilicho chake! Mungu akurehemu rafiki yangu na kuimarisha familia yako na sisi rafiki zako. Pumzika kwa amani Ivan. Ed Cheune –Ulieneza furaha miaka yote ulipokuwa nasi wote, sasa ni zamu ya Mungu kukupa furaha yote katika kurudi kwako kwake.

Pumzika kwa amani ndugu yangu mpendwa Ivan Semwanga. Baadhi ya mastaa wa Kibongo walioandika mitandaoni kumlilia Ivan ni pamoja na Wema Isaac Sepetu, Emmanuel Mbasha, Ali Kiba, Ester Kiama, Shilole na wengine wengi kutokana na ukaribu wake na wao. Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, bado utaratibu wa mazishi ulikuwa haujawekwa wazi. Ivan alipata umaarufu Afrika Mashariki kutokana na biashara zake kubwa ikiwemo umiliki wa vyuo mbalimbali nchini Afrika Kusini huku akisifika kwa kusaidia shughuli za kijamii nchini Uganda.

Maisha Ya Mke wa Deo Filikunjombe Baada ya Miaka Miwili ya Kifo Cha Mumewe..!!!

$
0
0

MAMA shujaa! Ikiwa imebaki miezi minne na siku kadhaa itimie miaka miwili kutokea kwa kifo cha aliyekuwa kada muaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, mkewe Sarah Filikunjombe (Pichani) amethibitisha ushujaa kwa kuendelea kupambana na changamoto za kimaisha na kufikia vilele mbalimbali vya mafanikio, Ijumaa limemfungia kazi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii, kwa siku tatu tofauti, waandishi wetu walijipa kazi ya ziada ya kumtafuta Sarah ili kujua nini kimeendelea katika maisha yake baada ya kuondoka kwa mumewe ambapo walibaini mambo mengi mazuri yenye kutia moyo, ambayo mama huyu licha ya kuonekana sistaduu, ameyafanya kwa ujasiri wa kipekee.

IJUMAA NYUMBANI KWAKE

Hatimaye Jumanne mchana, gazeti hili lilifika nyumbani kwake, Kijichi Mbagala jijini Dar na kufanya naye mahojiano ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha na kufunguka mengi juu maisha yake tangu kuondokewa na mumewe.

BAADA YA KIFO CHA MUMEWE

“Kufiwa ni kovu la milele maishani, kifo cha mume wangu kiliniumiza sana na hata sasa sijapona jereha hilo, nililia, nilihuzunika na bado nahuzunika lakini ilikuwa lazima maisha yaendelee. Aliniacha na watoto ambao bado ni wadogo hivyo wanahitaji uangalizi wa hali ya juu, kwa hiyo ilinibidi nijipange upya namna ya kuwatunza,” alisema Sarah na kuongeza; “Ukiondoa nyumba na miradi mingine, mume wangu aliacha Kampuni ya Jumbo Camera House inayojishughulisha na uuzaji wa kamera za kisasa, iliyopo Posta Mpya, kwenye Jengo la Benjamin Mkapa, lakini sikutaka kabisa kutegemea kitu hicho pekee, niliamua kuangalia njia nyingine za kuingiza kipato ili nikikusanya huku na huku, maisha yanasonga kwa wepesi.

“Hivyo, nilianza kujishughulisha na kilimo na ufugaji ambapo nafuga kuku wa kisasa na pia nina mabwawa ya kufuga samaki aina ya kambale, vyote hivyo viko wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani, pia nimewekeza kwenye vinywaji ambapo nimefungua baa iliyopo Vianzi hukohuko Mkuranga na vilevile niko kwenye hatua ya mwisho kukamilisha mradi wa kuuza unga wa sembe ambao nitakuwa naufunga kwenye viroba, yote hayo yako chini ya Kampuni ya Tripple L, ambayo inawakilisha majina ya wanangu wapendwa watatu, Lee, Levis na Larry ambapo hata nembo ya viroba vya unga itakuwa na picha yetu wote wanne,” alisema Sarah.

MARAFIKI WAPO PAMOJA NAYE?

“Idadi imepungua kwa kweli, hata wale marafiki waliokuwa karibu na mume wangu hawana tena ule ukaribu kama ilivyokuwa zamani, lakini huwezi kulaumu maana majukumu yanabana na kila mtu anapambana kukimbiza ndoto zake maishani.

“Hata marafiki zangu wamebaki wachache sana, wengi walidhani ningekuwa tegemezi na niseme bila kuficha walikuwa karibu na mimi kipindi mume wangu akiwa hai, wakitarajia msaada wa haraka . Sasa mambo yamebadilika, ingawa mimi nipo na ninapigana na maisha, simtegemei mtu zaidi ya Mungu na wale wanaokuwa karibu yangu maana sasa nina marafiki wapya kabisa,” alisema Sarah.

KUNA HILI LA MADENI “Katika mzunguko wa kutafuta mafanikio maishani, hususan kwa wafanyabiashara jambo la madeni halikwepeki, iwe kudai au kudaiwa. Sisi tunadaiwa na duka moja kule Dubai, wakati mume wangu akiwa hai, alikopa mzigo na alifariki tukiwa bado hatujakamilisha lakini Mungu yu mwema ulipaji utakamilika na pia tuna pesa tunadai, siwezi kusema ni wapi lakini ieleweke tu kwamba kuna mahali tunadai na vilevile matarajio ya kulipwa ni makubwa,” alisema.

SUALA LA MIRATHI LIKOJE?

“Kuna watu wanashughulikia jambo hilo, hivyo siwezi kulisemea chochote.”

ANASAIDIA NYUMBANI KWAO?

“Japo si kwa haraka kama ilivyokuwa zamani, sasa hivi wakihitaji msaada kutoka kwangu, lazima niwaambie wasubiri kwanza nijikusanye au kuangalia kilichopo kwa wakati huo, unajua kwenye familia yetu ni mimi na dada yangu ndiyo tumejaaliwa kuwa na unafuu wa kimaisha hivyo familia yetu ni ya kawaida sana kwa maana ya kipato,” alisema Sarah.

MSAADA KWA WANAWAKE WENZAKE

“Sitaki kujisifia juu ya hilo, lakini kwa kidogo nilichojaaliwa kwa maana ya mawazo ya kimaisha, huwa nashirikiana sana na wanawake wenzangu, hususan wajane kama nilivyo, kuna kipindi nilikuwa naendesha mafunzo ya namna ya kufuga samaki bure na elimu ya kufungua miradi mbalimbali, sikutaka malipo yoyote na hata sasa huwa nawafundisha, nikitarajia malipo kutoka kwa Mungu,” alisema Sarah.

VIPI KUHUSU MRITHI WA DEO?

“Hapana, kwa sasa nimeelekeza nguvu na akili yangu yote kwa wanangu, nawapenda mno, zaidi ya neno lenyewe na hata wao wanajua kuwa nawapenda, napambana kuhakikisha wanapata mahitaji yao yote kwa wakati, sitaki kujiingiza kwenye mambo ya kuwekeana msongo wa mawazo na mwanaume mwingine, pia hayupo wa kuziba pengo la marehemu mume wangu mpendwa, ameacha nembo ya milele maishani mwangu, kwa hiyo siwezi kuwaza kuwa na mtu kwa sasa,” alisema.

NENO LAKE KWA WAJANE NA WANAWAKE KWA UJUMLA

“Kufiwa ni jambo moja, lakini haipaswi kulia tu
bila kutenda jambo. Kama nilivyosema mwanzoni, kovu la kufiwa lina maumivu ya kuvuka kiwango cha kutamkwa, lakini lazima mwanamke asimame na kupambana na maisha, wapo wanawake wengi walifiwa na wanaume zao na kuwaacha mikono mitupu kabisa, wakati mwingine kunyang’anywa kila kilichokuwepo na baadhi ya ndugu, lakini leo hii wamesimama na kufanikiwa zaidi ya ilivyokuwa awali. “Nguvu ya mwanamke ni kubwa, mwanamke ni kiumbe wa pekee mno akiamua kufanya jambo kwa kuielekeza akili na nguvu yote kwenye jambo husika, lazima lifanikiwe ndiyo maana kuna ule msemo kwamba nyuma ya mafanikio ya kila mwanaume kuna mwanamke, hivyo sisi ni Generation point (chanzo cha uzalishaji) ya mafanikio, Mungu ameweka nguvu kubwa mno maishani mwetu, wanawake tuamke na tuzidi kupambana huku tukimuweka Mungu kama nguzo muhimu maishani,” alisema Sarah.

ANAO MPANGO WA KUJITOSA KWENYE SIASA?

“Sifikirii, nina mambo mengi sana kuhusu maisha na siasa inahitaji muda wa kutosha katika kuwahudumia wananchi, nilikuwa naona wakati wa mume wangu, jinsi alivyokuwa akijitoa kwenye siasa na wakati mwingine zaidi ya ilivyokuwa kwa familia, kwa hiyo sina wito wa siasa, mimi napambana na maisha tu,” alisema Sarah Filikunjombe katika mahojiano hayo maalum.

NI MAUMIVU KUKUMBUKA, LAKINI TURUDI NYUMA KIDOGO

Marehemu Deo Haule Filikunjombe alifariki dunia Oktoba 15, mwaka 2015 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, katika ajali ya chopa ilikuwa na usajili namba 5Y-DKK ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Selous, ambapo watu wengine watatu walifariki, akiwemo rubani William Silaa, aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Egdi Mkwera na aliyekuwa mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Vitalis Blanko Haule
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images