Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Sayari ya Mars Ilikuwa na Sifa ya Kuishi Viumbe Hai Vyote kwa Miaka Bilioni 3 Iliyopita..!!!

$
0
0

MIAKA bilioni kadhaa iliyopita, sayari ya Mars ilikuwa ni sehemu nzuri ambayo viumbe hai wangeweza kuishi kutokana na uwapo wa maji ya kutosha pamoja na udongo wenye rutuba.

“Tumegundua mazingira ambayo yangeweza kufaa kwa maisha ya viumbe hai ikiwamo uwapo wa maji ambayo kama yangekuwapo duniani tungeweza kuyatumia kwa ajili ya kunywa na shughuli nyingine,” anasema John Grotzinger ambaye ni Profesa katika taasisi ya Teknalojia ya California nchini Marekani na ambaye pia ameshiriki katika utafiti kuhusu Mars kupitia Kituo cha Anga cha Marekani (NASA).


 Kupitia roboti aliyetumwa kufanya utafiti kwa kupasua mwamba na kuteta taarifa zake duniani, wanasayansi wanasema uwapo wa matope kati kati ya miamba ni ushahidi tosha kuwa miaka iliyopita sayari hiyo ilikuwa na maji ya kutosha

pamoja na maji, wanasayansi waligundua madini kama, sulfur, nitrogen, hydrogen, oxygen, phosphorus na carbon kwenye miamba ambayo ni muhimu kwa maisha.

Profesa Grotzinger anasema madini hayo ni kama betri na ni muhimu kwa maisha kwa kuwa ni chanzo cha nishati kwa mwili.

Ugunduzi mwingine muhimu ni pamoja na udongo wa mfinyanzi ambao mara nyingi hupatikana sehemu sehemu zenye maji

“Kitu muhimu ambacho tumeweza kujifunza ni kuwa, katika kipindi cha miaka 20 iliyopita baadhi ya viumbe wadogo wadogo wangeweza kupata nguvu kwa kula kupita miaka ambayo ilikuwa na madini muhimu kwa maisha,” anasema Grotzinger

Hata hivyo, wanasayansi wanasema takribani miaka bilioni tatu iliyopita, hali katika Sayari ya Mars ilibadilika. Mabadiliko hayo yalihusisha kupoa kwa hali ya hewa pamoja kusimama kwa ulipukaji wa volacano. Maji yaliganda au kutoweka kwa njia ya mvuke na kuifanya sayari hiyo kuwa kavu na yenye baridi.

Leo hii uso wa sayari hiyo ni baridi na mkavu huku ukiwa na mionzi inayotokea angani. Lakini wanasayansi wanaamini kuwa miaka bilioni tatu iliyopita ilikuwa ni sehemu nzuri kwa maisha kwa kuwa hali ya hewa ilikuwa ya baridi ya wastani pamoja na maji yaliyokuwa yakitiririka.

Ujumbe wa NASA ulioenda Mars haukuwa na chombo chenye uwezo wa kutambua kama kuna kiumbe aliwahi kuishi kwenye sayari hiyo lakini iliweza kutambua baadhi ya madini ambayo kimsingi ni muhimu kwa maisha.

Ninayo picha sasa ya kitu kama ziwa la maji baridi pamoja na hali ya hewa ya wastani kwa ajili ya maisha,” anasema John Grunsfeld, mmoja kati ya timu inayofanya utafiti juu ya Mars kutoka NASA.

Sayari ya Mars ni ya nne kwenye mfumo wa jua na ni ya pili kwa udogo. Jina la Mars lilitokana na mungu wa vita wa dola ya Warumi ya zamani. Sayari hii wakati mwingine huitwa Sayari Nyekundu kutokana na kuwa na muonekano wenye rangi nyekundu.

Pamoja na utafiti wa miaka mingi ya utafiti, hakuna binadamu aliyeefanikiwa kufika katika sayari hii kutoka na sababu mbalimbali ikiwamo hali ya hewa ya baridi pamoja na hewa na carbon dioxide.

Kama binadamu akifanikiwa kufika kwenye sayari hii, atajikuta akiwa na uzito mdogo kuliko uzito wake halisi kutokana na nguvu ya gravity. Endapo ana kilo 45 akifika Mars atajikuta akiwa na kilo 17

Kama ilivyo kwa dunia, Mars ina majira aina nne lakini kwa saizi ni ndogo ukilinganisha na dunia.

Sayari hii pia ina mlima mkubwa zaidi unaoshikilia nafasi ya pili katika mfumo wa jua unaoitwa Olympus Mons ambao ni mrefu kuliko mlima wowote uliopo duniani. Mlimma huu unaaminika kuwa ulikuwa na volcano lakini kutokana na mabadiliko ndani ya sayari, Volcano hiyo imegeuka kuwa mfu.

Abdi Banda Awaaga Mashabiki na Wapenzi wa Simba..Adai Ataikumbuka Simba Daima..!!!

$
0
0

Beki wa timu ya Simba SC Abdi Banda ameaga rasmi jana baada ya timu yake kushinda Kombe la Shirikisho kwa kuipiga bao 2 kwa moja Mbao FC katika mchezo uliofanyika mjini Dodoma 

Abdi Banda anasema imefika wakati sasa anapaswa kutafuta maisha mengine nje ya klabu hiyo au sehemu nyingine huku akisema atakumbuka mambo mengi mazuri katika klabu hiyo 

"Ahsante Mungu nashukuru kwa hiki ulichotujaalia. Zawadi ya mashabiki wa Simba nawaachia acha na mimi nitafute maisha sehemu nyingine. Nitamiss vitu vingi hasa 'support' yenu na moyo wenu wa uvumilivu ahsanteni sana na kwaherini" aliandika Abdi Banda 

Rais Magufuli Amtembelea Mzee Aliyechora Nembo ya Taifa Hospitalini Muhimbili Leo..!!!

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe wamewatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwashukuru Madaktari na Wauguzi kwa juhudi kubwa wanazofanya kunusuru maisha ya watu.

Miongoni mwa wagonjwa waliojuliwa hali ni Mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) aliyelazwa katika chumba namba 310 na Mtoto Shukuru Musa Kisonga aliyelazwa katika chumba namba 312 ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuugua ugonjwa usiofahamika uliosababisha aishi kwa kunywa mafuta ya kula, sukari na Maziwa.


Rais Magufuli na Mama Janeth Magufuli wamefanya matembezi hayo leo majira saa moja ya asubuhi wakiwa wanatokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro liliopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ambako walihudhuria ibada ya Jumapili.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali itaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo pamoja na zile zinazowakabili madaktari na wauguzi hao.

“Jamani, Madaktari tunawashukuru sana, mnafanya kazi nzuri, Madaktari wote nchini pokeeni pongezi zangu, sisi serikali tutaendelea kuzikabili changamoto hizo na siku moja zitakwisha. Kikubwa ni kumtanguliza Mungu mnapofanya kazi ya kuokoa maisha ya watu kwa juhudi kubwa, mnafanya kazi ya Mungu” alisema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ameweza kumshukuru Rais Mgufuli kwa kuwatembelea huku akisisitiza kuwa tayari madaktari wamegundua magonjwa yanayomkabili Ngosha pamoja na Mtoto Shukuru.

Aidha, Prof. Museru amesema hospitali hiyo imepiga hatua kubwa ya kujenga uwezo wa kutibu magonjwa ambayo wagonjwa walilazimika kwenda kutibiwa nje ya nchi na hivyo kuokoa fedha nyingi za serikali.

“Mhe. Rais hospitali yetu sasa imeanza kufanya upasuaji na kutoa tiba ya magonjwa ambayo yalilazimu wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, mfano hivi sasa tunatoa huduma ya kusafisha figo kwa wagonjwa takribani 250, na kuanzia mwezi Julai mwaka huu tutaanza kupandikiza figo.Huduma hii hugharimu kati ya Shilingi Milioni 60 na Shilingi Milioni 70 kwa mgonjwa mmoja anayekwenda kutibiwa nje ya nchi, lakini hapa nchini gharama zinashuka hadi Shilingi Milioni 21” alisema Prof. Museru.

Kwa upande mwingine Prof. Museru amesema kuwa hospitali ya Muhimbili imejipanga kuanza kutoa huduma ya matibabu kwa watoto wenye matatizo ya usikivu ambao wapo hatarini kuwa viziwi ili kuweza kuokoa fedha nyingi zinazokazo kwenda kuwatibu nje ya nchi, kutoka Shilingi Mil 90 hadi Mil 30.

Gwajima Atema Cheche Sakata la Mchanga wa Madini...Ampa Makavu Live Tundu Lissu Juu ya Kuitisha Nchi ...!!!

$
0
0

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na kusema Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu ambacho kinaweza kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa nyuma. 

Mchungaji Gwajima amesema hayo leo wakati akitoa mahubiri yake kwenye kanisa lake na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana maandamano na vitu visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema Tanzania ina vitu na mali nyingi 

"Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima 

Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais ashikirie hapo hapo 

"Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna kwenda" alisema Gwajima 

Huu Ndio Ukweli Sasa..Magufuli "Nchale!" - Usiteme, Usimeze wala Usimumunye..!!!!

$
0
0

Unajua mnisamehe kidogo; kuna hisia mbaya sana ya uduni (acute sense of inferiority complex). Kwanza, tunaamini tutashindwa kama kes itatokea kati ya serikali na Acacia. Tutashindwa kwa sababu hatuwezi kushinda! Lakini kuna kitu kingine pia kinajionesha. Chukulia kwa mfano hoja ya "mikataba"; sote tunajua jinsi gani suala la mikataba mibovu limeisumbua nchi yetu na jinsi ambavyo ukweli kabisa upinzani ulifanya kazi kubwa sana kuonesha. Sasa unajiuliza; kama kuzuia makontena 277 tu tunaambiwa tutalizwa na tutalipishwa vibaya itakuwaje kama tukigusa mikataba? 

Ndugu zetu katika woga wao wanasema "tusifanye lolote kwa sababu itatugharimu"; Wanasahau kuwa wakati mwingine mtu inabidi uchukue maamuzi ya kutetea maslahi yako hata kama itakuja gharama kubwa. Kuna watu wanaamua kuachana katika ndoa wakijua kabisa kuwa kwa kufanya hivyo (ni mkataba huo) watatakiwa kulipa gharama kubwa sana kwa yule mwingine. Lakini watafanyaje sasa? Abakie kwenye uhusiano ambao unahatarisha afya yake ya akili na mwili au atoke ili atafute ahueni kwingine hata kama kwa kufanya hivyo atatakiwa kulipa gharama ya matunzo kwa yule mwingine au atalazimika kugawana mali walizochuma pamoja? Kwa wengine, huo siyo uamuzi mgumu kivile.

Katika mahusiano ya biashara ya kimataifa hili pia si jambo geni; nchi, makampuni na hata watu binafsi wanaweza wakafika mahali wakaona kuwa hali iliyopo (status quo) haiwezi kuendelea na watatafuta namna ya kutatua tofauti zao lakini kama ikibidi wataenda mahakamani kutafuta judicial intervention (mahakama iingilie kati). Wanapofanya hivyo ina maana wanakuwa tayari kwa matokeo yoyote lakini hofu ya gharama peke yake haiwezi kuwa sababu ya kutokuchukua maamuzi yenye maslahi kwa upande husika. 

NImewasoma ndugu zangu wengi wakitolea mfano wa mambo mbalimbali ambayo yamewahi kufanywa chini ya Magufuli na kuwa yamekuja kuligharimu taifa. Lakini kama ni gharama ya lazima kwanini tusilipe? Ni kweli kuna haja ya kuwa waangalifu; lakini uangalifu usije kugeuka kuwa woga! Jambo jingine la kuzingatia hapa ni kuwa katika sakata hili la makontena ya michanga mwenye maslahi makubwa ni taifa na siyo kampuni; hivyo kama taifa ni lazima tuangalie maslahi yetu lakini kama maslahi yetu yanatishiwa sana ni jukumu letu kuyatetea kwa umakini, weledi na uangalifu. Lakini kamwe tusisite kuyaangalia maslahi yetu kwa sababu tunaogopa wakubwa wanaweza kutushtaki au wanaweza kuamua kuondoa uwekezaji wao. 

Mikataba hii ambayo tunasema "tuipitie" na tumeshadai kuwa ipelekwe Bungeni; lengo litakuwa ni nini? Je, tukiipitia au tukiipeleka Bungeni tutataka tuifumue tu tuifute au tuijadili upya? Vipi kama hao "wakubwa" wakigoma kupitiwa tena mikataba yao na wakikataa tusiiguse kwa sababu ni mikataba halali? Je, kama tukifanya hivyo kwa maamuzi yetu wenyewe (unilaterally) siyo kwamba watatupeleka kwenye arbitration ambako tutaweza kupoteza kama tulivyofanya kwenye Dowans? na kesi nyingine? 

Wanaosema "tupitie mikataba" - jambo ambalo wengi tunalikubali na tumelipigia kelele miaka nenda rudi - hawajui kuwa wakubwa hawa kama kuna kitu watatubana nacho sana na hawako tayari kukiona ni kupitiwa mikataba hii. Sasa, Magufuli akiamua kusitisha mikataba na kuipitia yote (na ninatabiri hili itakapokuja ile kamati nyingine na matokeo yake) je, tutamuunga mkono au tutahamisha magoli tena na kusema "kwanini anaingilia mikataba halali!? hajui watatunyoa na mchanga!"? 

Kwa sababu baada ya ile Kamati Magufuli anaweza kuleta usitiswhaji wa muda (Moratorioum) ya hata miezi sita ili kulipa taifa na wataalamu wake kupitia mikataba hiyo. Je, tutakubali na kuunga mkono au tutakimbia tena na kusema "mamaaa wee kagusa mikataba sasa, nchi itakimbiwa"? 

Matokeo yake ni kana kwamba tunaambiwe kile alichoambiwa yule mwizi kwenye simulizi fulani 'ukisimama nchale, ukikimbia nchale, ukizungumza nchale, ukiguna nchale, usimeze, usiteme, wale usimumunye"! Ndio maana unaona kuwa Magufuli amefanya kile ambacho Wasambaa wanasema kama ni 'mbwai na iwe mbwai'!

Nawatakieni Mfungo Mwema wa Mwezi wa Ramadan.

Samatta Azidi Kuwashangaza Wazungu..Atupia Goli na Kuweka Rekodi Hii..!!

$
0
0

Streika wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameonesha ubabeb usiku wa jana kwa kuifungia klabu yake bao moja pale timu hiyo iliposhinda  3-0 dhidi ya Sint-Truiden.

Bao hilo linakuwa bao lake la 20  katika mechi 59 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC. 

Kati ya mechi hizo 59, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 41 msimu huu na kati ya hizo, ni michezo 37 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 27 msimu huu.

Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, 8 msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu uliopita.

Askofu Gwajima Afunguka Mazito Sakata la Madini Katika Mchanga

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na kusema Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu ambacho kinaweza kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa nyuma.

Mchungaji Gwajima amesema hayo leo wakati akitoa mahubiri yake kwenye kanisa lake na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana maandamano na vitu visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema Tanzania ina vitu na mali nyingi

"Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima

Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais ashikirie hapo hapo

"Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna kwenda" alisema Gwajima

CHADEMA Wamtupia Lawama Mkapa na Kikwete sakata la mchanga wa madini

$
0
0
Mwenyekiti  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete, wanahusika na sakata la mchanga wa madini (makinikia) unaosafirishwa nje ya nchi.

Pia amesema Mkapa na Kikwete hawawezi kukwepa lawama juu ya mchanga huo kwa kuwa mikataba kati ya Serikali na wawekezaji wa migodi inayotajwa, ilisainiwa kwa nyakati tofauti wakati wao wakiwa madarakani.

Kauli hiyo aliitoa mjini Dodoma  jana alipozungumza katika mkutano wa Baraza Kuu la Chadema uliokutanisha wajumbe 332, kati ya 370 waliotakiwa kuhudhuria.

 “Kama kuna kitu kinaangamiza nchi, ni pale unapomwambia mfalme umevaa suti wakati unaona yuko uchi. Katika sakata hili la mchanga, sisi kama chama cha siasa, tumekaa na wataalamu wetu na kukusanya taarifa kwa sababu wengi wanalizungumzia kwa kauli tofauti,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Kwanza kabisa inabidi tuelewe kwamba mchanga wa madini umekuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi kutoka kwenye migodi yetu miwili ya Bulyanhulu kuanzia mwaka 2001 na Buzwagi kuanzia mwaka 2008.

“Eleweni kwamba leseni za kusafirisha mchanga kwenda nje zilitolewa na Serikali hii hii ya CCM na katika mikataba hiyo, kunatambulika kuna madini mengine mbali na dhahabu katika migodi hiyo.

 “Pia makontena ya madini yanapokuwa bandarini kabla ya kusafirishwa, watu wa TRA, TMAA, lazima wahakiki makontena yenye mchango huo ili kujiridhisha na kilichomo.

“Wakati mikataba hii inasainiwa, Rais Dk. John Magufuli alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri na pia Mkapa na Kikwete, wanayajua haya kwa sababu mikataba ilisainiwa wakati wao wakiwa madarakani kwa nyakati tofauti.

“Nasema hivyo kwa sababu enzi za Mkapa, mikataba mingi ya madini ilisainiwa na hata Kikwete alipokuwa Waziri wa Nishati, kuna mkataba aliusaini.

 “Kibaya zaidi, CCM wamekuwa wakitumia wingi wao vibaya bungeni kupitisha sheria mbovu kwa sababu hata mwaka 1997, Bunge lilipitisha kwa siku moja sheria mbili za madini chini ya hati ya dharura na mwaka 1998, Bunge lilipitisha sheria nyingine ya madini inaweka utaratibu wa uchimbaji wa madini na kuruhusu wawekezaji kutoa mrabaha wa asilimia tatu ingawa baadaye mrabaha huo ulibadilishwa na kuwa asilimia nne, huku sheria hiyo ikiruhusu mchanga usafirishwe kwenda nje ya nchi.

“Yaani, hata mikataba yetu inaruhusu wawekezaji kupewa misamaha ya madini wakati sheria haisemi hivyo. Kwa hiyo, kinachotokea sasa ni matokeo ya CCM kutufikisha tulipofika.”

Kutokana na hali hiyo, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuna uwezekano mkubwa Kampuni ya Acacia inayomiliki migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ambako mchanga huo ulipatikana, ikafungua mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro.

“Jana nilikuwa nasoma Gazeti la Telegraph la Uingereza ambapo wanasema tatizo sio wawekezaji bali ni Waafrika wanaoingia mikataba ya uwekezaji na wanasema kwa mujibu wa mkataba wetu, mchanga sio mali ya Tanzania bali ni mali ya wawekezaji.

“Kwa hiyo, kinachoonekana sasa ni kwamba nchi inaingia katika mgogoro wa kidiplomasia na wawekezaji na kama wakiamua kwenda mahakamani, hatutashinda kesi kwa sababu mikataba tuliisaini vibaya.

“Kibaya zaidi, ni kwamba kesi haitakuwa Kisutu, Kinondoni, Mwanza au Kigoma, bali itafanyika huko huko kwao,” alisema.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alisema kwa kuwa uwezo wa Tanzania ni mdogo katika uwekezaji wa miradi mikubwa, Serikali inatakiwa kuwa makini kwa sababu si kweli kwamba wawekezaji wote ni wezi na pia si kweli kwamba wote ni waaminifu.

Akizungumzia hali ya kisiasa, Mbowe alisema katika uzoefu wao kisiasa, Serikali ya awamu ya tano ndiyo ngumu katika harakati zao kwa sababu Rais Magufuli anakandamiza demokrasia.

Kwa mujibu wa Mbowe, alisema serikalini kuna baadhi ya viongozi wanaamini njia pekee ya kuwaweka madarakani ni kuvunja sheria na kuminya demokrasia, jambo ambalo wamelivumilia kwa muda mrefu na kuwafanya viongozi hao waamini Chadema ni waoga.

Alitoa mfano wa matukio aliyosema ni uminywaji wa demokrasia nchini ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa, kukamatwa kwa wanasiasa wa upinzani na kufikishwa mahakamani bila sababu na kupotea kwa kada wa Chadema, Ben Saanane.

 “Awamu hii ya tano ni ngumu sana kisiasa, lakini pia inatoa fursa kwetu kwa sababu wananchi wana maisha magumu kweli kweli kuliko Serikali yoyote katika nchi yetu.

“Rais lazima ajue kwamba matendo yake yanaathiri Watanzania milioni 50 na ajue sisi tunahitaji pia aliyeko madarakani alete amani kwa sababu nchi ni yetu sote.

“Kwa kifupi, nchi yetu kwa sasa haiko salama, kisiasa, kiuchumi na wala kijamii, kwa sababu kila mmoja anashuhudia jinsi watu wanavyouawa Rufiji na Mkuranga.

“Pamoja na hayo, eleweni kwamba haki haipatikani kwa kuombwa bali kwa mapambano. Kwa hiyo, lazima katika kikao chetu hiki tutoke na uamuzi mgumu ili watawala wa nchi hii waelewe salama ya nchi ni kusimamia haki kwa watu wote na sio kwa wana CCM peke yao, kama mbwai na iwe mbwai,” alisema Mbowe.

Breaking Newz: Nahodha wa Simba Jonas Mkude apata ajali mbaya

$
0
0

Baada ya jana kuiongoza timu yake ya Simba SC kurejea katika anga ya kimataifa kwa ushindi wa kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mbao FC, kiungo wa Simba Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali mbaya akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma.


Nahodha huyo wa Simba amepata ajali hiyo maeneo ya Mitibora, Dumila mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam kuiwahi Taifa Stars. Taarifa za awali zinasema ameumia maeneo ya shingoni, amekimbizwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wenzie ambao baadhi wana halimbaya.

Kwenye gari ambayo Mkude amepata nayo ajali walikuwepo watu 6, na kilichopelekea ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la nyuma. Majeruhi mmoja yuko mahututi.

Tutaendelea kujuzana hali yake na majeruhi wengine kadri taarifa zitakavyokuwa zinatoka.

Picha ya Shabiki wa Simba aliyepoteza maisha katika ajali aliyokuwemo Jonas Mkude

$
0
0
Shose Fidelis ndiye aliyepoteza maisha katika ajali ya gari ambalo alikuwamo Nahodha wa Simba, Jonas Mkude.

Mkude ni katika ya majeruhi watatu na Shose ambaye aliambatana na wenzake kwenda kuishangilia Simba ikipambana kuwania Kombe la Shirikisho, amepoteza maisha.

Shose amekuwa katika ya mashabiki wakubwa wa Simba na amekuwa akionekana pamoja katika lile Kundi la Wapenda Soka ambalo linaundwa na mashabiki wa Simba.

Mkude alikuwa njiani kutoka Dodoma kurejea Dar es Salaam baada ya jana Simba kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho.

Mkude alikuwa katika gari na baadhi ya mashabiki wa Simba na gari lilipasuka tairi na kuanguka. Mtu mmoja amefariki dunia.

BREAKING: Rais Magufuli amwondoa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)

$
0
0

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP).



Taarifa iliyotolewa na Ikumu muda mfupi uliopita inasema aliyekuwa IGP, Ernest Mangu, atapangiwa kazi nyingine.


Taarifa iliyotolewa na katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, inaeleza kuwa Sirro ataapishwa kesho Jumatatu ya Mei 29, 2017 saa 3.00 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.


Taarifa ya leo Mei 28, kumuhusu Ivan aliyekuwa Mume wa Zari

$
0
0

IVAN SEMWANGA, aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘The Bosslady’ ambaye sasa ni mpenzi na mzazi mwenzake wa mwanamuziki wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnum’, atazikwa Jumanne (Mei 30) wiki ijayo  nyumbani kwao Kayunga, Uganda.


Mwili wa mwananchi huyo wa Uganda aliyefariki nchini Afrika Kusini kutokana na matatizo ya moyo, umewasili leo nchini Uganda ambako leo utafanyiwa mkesha maalum na Jumatatu kufanyiwa ibada maalum ya wafu katika Kanisa la Namirembe siku ya Jumatatu.


Semwanga alijipatia umaarufu mkubwa tangu nchini mwake Uganda hadi Afrika Kusini ambako ameacha utajiri mkubwa uliomfanya kuwa mmoja ya watu matajiri nchini humo kabla ya kufikwa na mauti.

Kama Hujui..Viazi Vitamu Ni Moja ya Tiba ya Uhakika ya Nguvu za Kiume..Pitia Hapa Ujue Jinsi Vinavyofanya Kazi..!!!

$
0
0

JE WAJUA KUWA VIAZI VITAM HUONGEZA
HAMU YA KUFANYA MAPENZI NA KUSAIDIA
KUCHELEWA KUFIKA KILELE?

JINSI YA
KUTUMIA

(1) Chukua viazi vitamu vyembamba
vyenye rangi nyekundu 

(2) usivimenye bali vioshe na uvichemshe kama vilivyo ... Hakikisha vimeiva na uviepue. 

(3) Hakikisha unakula na maganda bila kutumia
kinywaji chochote!!

(4) Baada ya hapo tambua kuwa mapenzi ni hisia zako hivyo umejifunza kupika viazi vitamu na siyo tiba maana macho yalikutoka kama una tatizo hilo muone Doctor.

(5) Usijione mpuuzi utakuwa umejifunza kitu si kila tiba unataka kujaribu
utakunywa Sumu fala wewe!

Polepole aonywa kauli yake ya Mauaji Kibiti

$
0
0


Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amemuonya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza matukio ya kuuawa Watanzania katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kuyageuza kama mtaji wa kisiasa kwa CCM ili CCM ionewe huruma na kuvichonganisha vyama vingine na wananchi.



Mgeja alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa mkoani Morogoro akitokea Dar-s-Salaam.


Mgeja alisema kila mpenda amani nchini amesikitishwa na kauli yenye ukakasi alizotoa Polepole hivi karibuni akisema CCM inakemea na imekuwa ikikemea maafa hayo lakini vyama vya upinzani vikikaa kimya.


Mwenyekiti huyo amemshangaa Polepole kwa maneno yake akimtaka atambue kila Mtanzania mpenda amani kwa matukio yanayotokea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani yanawagusa moja kwa moja bila kujali dini zao, ukabila wao wala vyama vyao vya siasa.


“Tumesikitishwa kwa kauli za Polepole za kwake bila kujali msingi na wala siyo kipindi muafaka wakati taifa lina majonzi makubwa,"alisema.

Mgeja Amnyooshea Kidole Polepole kwa Kauli Aliyoitoa Kuhusu Mauji ya Wananchi Pwani..!!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amemuonya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza matukio ya kuuawa Watanzania katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa kuyageuza kama mtaji wa kisiasa kwa CCM ili CCM ionewe huruma na kuvichonganisha vyama vingine na wananchi.

Mgeja alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa mkoani Morogoro akitokea Dar-s-Salaam. Mgeja alisema kila mpenda amani nchini amesikitishwa na kauli yenye ukakasi alizotoa Polepole hivi karibuni akisema CCM inakemea na imekuwa ikikemea maafa hayo lakini vyama vya upinzani vikikaa kimya.

Mwenyekiti huyo amemshangaa Polepole kwa maneno yake akimtaka atambue kila Mtanzania mpenda amani kwa matukio yanayotokea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani yanawagusa moja kwa moja bila kujali dini zao, ukabila wao wala vyama vyao vya siasa.

 Tumesikitishwa kwa kauli za Polepole za kwake bila kujali msingi na wala siyo kipindi muafaka wakati taifa lina majonzi makubwa,"alisema.

Mataifa 7 Yenye Nguvu Duniani Yampiga Mkwara Trump..!!!

$
0
0

Mataifa saba yenye nguvu za kiuchumi duniani maarufu kwa jina la G7 yametofautiana na Rais wa Marekani, Donald Trump kuhusu makubaliano ya Paris ya mabadiliko ya Tabia ya nchi ambayo yamelenga kupunguza hewa chafu duniani.

Viongozi wa G7 wametoa msimamo wao kuhusu Marekani kuwa endapo Trump hatokubaliana na makubaliano hayo basi Marekani itakuwa imejiondoa katika umoja huo wa G7.

Hata hivyo, katika taarifa iliyotolewa na umoja huo imesema kuwa Marekani haitaungana na mataifa hayo yenye nguvu duniani katika makubaliano ya mabadiliko ya Tabia nchi.

Mbowe: Tunajiandaa Kukamata Dola Mwaka 2020...!!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema wamebadili msingi wa uongozi wao ikiwamo kufanya mfumo unaoendana na mwaka wa Serikali ambao unaanzia Julai Mosi hadi Juni 30.

Kwa mujibu wa Mbowe, Chadema imefanya hivyo kutokana na maandalizi yao ya kushika dola mwaka 2020 na kuwa ndiyo maana wameanza kufanya hivyo mapema.

Akifungua mkutano wa Baraza Kuu mjini Dodoma jana, Mbowe aliwataka wajumbe na wanachama kukubaliana na mabadiliko hayo kutokana na hali ilivyo kwa sasa baada ya kuona chama kinakwenda vizuri na kinazidi kukua kila kukicha.

“Nasisitiza kuwa, lazima chama hiki tukilinde na kukijenga kwa gharama zote, tumepita milima na mabonde lakini ukweli hata ninyi mnajua kuwa tuko mahali salama sasa,” alisisitiza.

Awali, Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vicent Mashinji alisema chama kinakua kwa kasi ya ajabu ambayo wengi wanashindwa kuijua.

Alisema kwamba mpango walionao ni kuhakikisha kuwa mwaka 2020 wanashika dola au kugawana wabunge nusu kwa nusu na chama tawala na akaomba Watanzania kutumia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuomba safari ya kushika dola iwe njema. Jumla ya wajumbe walioshiriki mkutano walikuwa 332 kati ya wajumbe halali 370.

Prof Maghembe Awashukuru Waliovamia Hifadhi za Misitu..!!!

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amewashukuru wavamizi  wa Msitu wa Hifadhi wa Isawima wilayani Kaliua ambao wameamua kwa hiari yao kubomoa makazi na kuondoka wao na mifugo yao katika eneo hilo ambalo ni miongoni mwa vyanzo vya maji ya Ziwa Tanganyika 
.
Ameyasema hayo Wilayani Kaliua mara baada ya kusomewa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa Wavamizi hao katika Msitu wa Hifadhi na kutembelea eneo walipoondolewa wavamizi na kisha kupata fursa ya kuongea na wananchi.

Amesema kuwa Serikali imefurahishwa na uamuzi huo uliochukuliwa na watu hao baada ya kupata elimu kuhusu athari za kimazingira za wao kung’ang’ania kuendelea kuishi katika maeneo yaliyohifadhiwa na kuamua kuondoka bila kushurutishwa.

“Serikali haina shida ya kumuonea  mtu na ndio maana tumekuwa tukiitumia zaidi elimu jambo ambalo limeleta mafaniko makubwa katika eneo la Hifadhi hii ambapo zaidi ya asilimia ya 70 ya watu waliokuwa wamevamia wameondoka,”amesema Prof. Maghembe

Simba Walipeleka Kombe la Azam FA Cup Bungeni Leo..!!!

$
0
0

Siku mbili baada ya klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho, imepata mwaliko bungeni.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza, bao lililopatikana ndani ya dakika ngumu 120 katika mchezo uliopigwa jana Jumamosi makao makuu Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Kwa matokeo hayo, Simba imekata tiketi ya kupanda ndege na kuungana na watani zao Yanga. Simba watawakilisha Taifa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Pia, baada ya kupeleka kombe hilo bungeni, itakwenda Kondoa kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki na Kondoa Kombaini.

Baada ya kukamilisha ratiba hiyo, itasafiri kwa basi kurudi Dar es Salaam tayari kujiandaa na mashindano ya Ligi ya Sportpesa.

Siri Nzito Kung'ota kwa IGP Mangu Yaanikwa..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo Jumatatu ya 29/5/2017..!!!

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images