Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Uncle wa IVAN( baba) Aomba Msamaha Kwa Zari Kwa Maneno Aliyoshusha

$
0
0
Siku chache baada ya aliekiwa mume wa Zari kufariki aliibuka mzee herbet Lunyinda uncle wa IVAN na kujitambulisha kama baba wa ivan huku akisema hawamtambui zari na hausiki na chochote
Lakini leo wakati wa kuaga mwili wa kanisani alimuomba zari msamaha na watu wote.
katika misa hiyo zari alipewa muda wa kutoa speech na kuahidi kuwalea watoto wake vizuri na kuendeleza mali zote na kuhakikisha legacy ya marehemu haipotei

Uncle Apologises
In a twist of events, Semwanga’s uncle Herbert
Luyinda took the opportunity of the requiem
mass to apologise for dividing the deceased’s
family.
Last week, Luyinda told journalists that
Ssemwanga’s children will be taken for DNA
tests to prove they belonged to him, raising dust
among family members.
The deceased’s uncle also claimed Zari doesn’t
have any shares on Ivan’s property accusing her
of leaving their marital home and got married to
another man.
However on Monday, the deceased’s uncle
apologized for the statements he had earlier
made in public.
“I apologise for any mistakes that I made. Let us
stay together, ” Ivan’s uncle said during the
requiem mass at Namirembe cathedral.

The mother of Ivan Semwanga’s children, Zari
Hassan has promised to look after the kids.
Speaking during Semwanga’s Church service at
Namirembe Cathedral, Zari said she is a strong
lady who is willing and ready to take care of her
children.
“I have cried since he was hospitalized. I am now
strong,” Zari said.
“My mother raised me single-handedly and
taught me to be strong. I will do the right thing
for him and the boys.”
Zari, who is now married to Tanzanian singer
Diamond Platnumz said Ivan’s 3 children are her
own blood that she can’t leave to wander in the
world.

Maneno ya Idriss Sultan Kwa Mrembo Jokate Mwegelo Baada ya Kutajwa na Forbes

$
0
0

Ndani ya miaka 5 she has done so much more than any celebrity in Tanzania kwenye jamii.

Naomba nihamishie upepo kwake kwa shukrani zote kwa yote aliyoyafanya kuinyanyua jamii ya watanzania na naomba msamaha kwa niaba ya watanzania kwani tulikua busy tunaangalia nani anatoka na nani na nani kagombana na nani na nani kaposti uchi leo, tukasahau kua umebadilisha maisha ya vijana zaidi ya laki 5 ndani ya miaka miwili tu.

Ingekua muamuzi ni mimi ungekua Forbes because ni celebrity pekee uliyesimamisha brand product yako kwa jina lako and yes African boy ya Jux inakuja pia. Uliyoyafanya kwenye jamii yako bila kulazimishwa ni zaidi ya baadhi viongozi tuliowachagua kufanya kazi hizo tunazowalipa kufanya.

If am allowed may I please say you are "THE FLOWER  OF TANZANIA" if you ask me why its because you are beautiful and you make us smell good werevaa you go.

Idriss Sultan

Zari Kusimamia Shule na Vyuo Vyote vya Ivan Vilivyopo South Africa

$
0
0
Baada ya maziko siku ya Jumanne nchini UGANDA ya aliyekuwa mume wa Zari.
Mwanamama huyu ataanza kazi rasmi ya kusimamia na kuendeleleza vyuo na shule zilizoachwa na Ivan.

Kaka wa Ivan na aliekuwa mtu wa karibu yake Pinto amesema hayo.Pinto amesema tatizo la moyo ni ugonjwa uliopo kwenye familia yao na kitendo cha Zari kuwa na watoto 3 wa Ivan tayari amequalify kuwa msimamizi wa mali hizo kwa ajili ya future ya watoto ikizingatiwa wazazi wote wawili wa IVAN walishafariki.

Pinto amekanusha habari zinazombaa kwamba wana ndugu wanagombania mali huku akisema pesa kwenye familia yao sio tatizo ni kitu kipo kwenye blood.

Zari To Manage Ivan Ssemwanga’s Schools In S.A

A few hours after Zari managed to secure her deceased ex hubby ’ s will, sources revealed that the Ugandan socialite will take over managerial duties for all schools Ivan had established in South Africa. This exclusive information was released by one of Ivan ’ s close family members only identified as Sir Pinto.

Ivan left behind Brooklyn College that has over 7 campuses spread allover South Africa. After revealing that both of Ivan ’ s parents died in his infant stages, Pinto also added that high blood pressure is very common in their family and Ivan’ s life is not the first to be taken among them . Pinto also disagrees with people who have been claiming that his family is fighting for the deceased property as he trashed the claims by saying their family has enough money.

His reply follows claims that have been making rounds on various news platforms that Zari, family members and other close friends were fighting for the deceased’ s property . Being the mother of Ivan ’ s three young sons , Zari qualifies more than any other person to protect the kids property from greedy people likely to take advantage of the business man ’ s death .

It should be noted that Zari also worked hard with Ivan to establish most of these businesses before she dumped him for a younger Tanzanian musician commonly known as Diamond Platinumz .

Kutana na Mtaalamu wa Tiba Asili Ostadh Khamis Kutoka Mombasa..Yupo Tanzania....Anatibu Magonjwa Yafuatayo

$
0
0

Kutana na OSTADH khamis kutoka Mombasa Kenya kwa sasa yupo Tanzania nibingwa watiba za asili:

Miguu kuuma miguu kufagazi nakuwaka moto
Unashida na mchumba au pesa haikai muone haraka 
Kurudisha mpenziwako alie kukimbia ndani ya siku (3)
Dawa ya ( LIMBWATA) kumtawala mpenzi wako kwasababu maalumu   
Pete ya bahati inayo endana nanyota yako itakayo kuletea pesa bila mashart yeyote
Kuongeza uume saizi uipendayo 
Dawa ya ulijali 
Dawa yakuongeza hips
Kumuliki Mali isiokuwa namasharti yeyote 
Kurudisha Mali iliopotea au kudhurumiwa ndani yasiku(3) 
Napia OSTADH KHAMIS anafunga kesi nakupata hakiyako kwa haraka 
Dawa ya mvuto pia inapatikana mvuto Wa biashara kuuza Mali yako kwa haraka 
Kuzuiya chuma ulete na kupandishwa cheo kazini PAMOJA na kusafisha nyota njoo ufunguliwe vifungo ulivyo fungwa

Call+255718746825 au +255754765246 WhatsApp IMO +255783708487

Full Ripoti: Daktari Afichua Mume wa Zari alipewa Sumu

$
0
0
KAMPALA: Imefichuka! Nyuma ya msiba ulioacha historia wa aliyekuwa mzazi mwenza wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ivan Ssemwanga ‘The Don’ aliyepatwa na umauti wiki iliyopita akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Steve Biko, Pretoria nchini Afrika Kusini, kuna mengi yanayosemwa, Wikienda liko bega kwa bega na kinachojiri.

Miongoni mwa yanayosemwa ni madai ya jamaa huyo kupewa sumu iliyomdhuru moyo hivyo kusababisha kifo chake.

MADAI YA SUMU

Chanzo cha ndani ya familia ya Ivan kililieleza gazeti moja maarufu nchini Uganda kuwa, Ivan alilishwa sumu na watu ambao hawakuwataja na kwamba mara ya mwisho alikuwa akipata chakula na ndugu zake kabla ya hali yake kuanza kuwa mbaya kisha siku chache baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Steve Biko.

Gazeti hilo lilimkariri mtu huyo akieleza kuwa, Ivan hakufa kwa shambulio la moyo wala moyo kushindwa kufanya kazi bali aliwekewa sumu kali kwenye chakula.

MAUMIVU MAKALI

Sosi huyo alisema kuwa, baada ya sumu hiyo, muda mwingi Ivan alikuwa akilalamika maumivu makali ya tumbo na kuomba kuwahishwa hospitalini.

Hata hivyo, mbali na madai hayo, taarifa za kitabibu zilieleza kuwa, Ivan alifariki dunia kutokana na shambulio la moyo bila kuweka bayana kama alipewa sumu au la.

Katikati ya mkanganyiko huo, Wikienda lilizungumza na daktari wake aliyekubaliana na maelezo kuwa inawezekana sumu hiyo ndiyo iliyomdhuru moyo na kumsababishia tatizo la Atrial Fibrillation.

ATRIAL FIBRILLATION NI NINI?

Daktari huyo alisema kuwa, Atrial Fibrillatoni ni ugonjwa ambao huufanya moyo badala ya kuwa unadunda kama ilivyo kawaida, uwe unatetemeka na kusababisha shida katika mfumo mzima wa upumuaji na usukumaji wa damu.

“Tatizo hili, huwa linatokea kwenye chemba za juu za moyo (Atria) ambazo kimsingi misuli yake ndiyo inayosababisha moyo kudunda.

“Misuli hii inapoishiwa nguvu, hushindwa kuzalisha nguvu ya kutosha kusukuma damu na badala yake, hutetemeka na matokeo yake, damu huanza kuganda kwenye mishipa (blood clotting) kwa sababu ya kukosekana kwa presha ya kuisukuma na kuifanya izunguke mwili mzima kisha kurudi tena kwenye moyo.

“Kwa baadhi ya watu, tatizo hili hutokea mara moja na kuacha au kwa kitaalam Sporadic Fibrillation na kwa wengine, ikitokea mara moja huendelea bila kupata ahueni yoyote au kwa kitaalam Persistent Fibrillation.

NINI CHA KUFANYA?

“Unapoona hali ya aina hiyo ni muhimu kuwahi hospitalini baada ya kuona dalili za ugonjwa huu kwani ukichelewa, husababisha damu kuganda kwenye viungo muhimu katika mwili, hasa kwenye ubongo.

“Pia inapotokea damu imeganda kwenye ubongo, husababisha mifumo mingine ya mwili kama upumuaji na mfumo wa fahamu kuwa kwenye hatari ya kushindwa kufanya kazi, jambo ambalo ni hatari kwa maisha.

“Inapotokea damu imegandia kwenye ubongo kutokana na tatizo hili, madaktari ni lazima wafanye kwanza upasuaji wa kuondoa damu hiyo kwenye ubongo kisha baada ya hapo ndipo waendelee na kutibu chanzo cha tatizo, ambacho huwa ni kwenye moyo.


“Mara zote, Atrial Fibrillation husababisha mgonjwa apatwe na ‘stroke’ na endapo tatizo hili likiwa ni lile la kuendelea, Persistent Fibrillation, uwezekano wa mgonjwa kupona huwa mdogo.

NINI KINASABABISHA?

“Yapo mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha tatizo la Atrial Fibrillation, miongoni mwa hayo ni matatizo ya shinikizo la damu ya muda mrefu, kuziba kwa mishipa ya damu kunakoweza kusababishwa na mwili kuwa na mafuta mengi (cholesterol). “Hii huwapata zaidi watu wanene. Pia matatizo katika valvu za moyo, huweza kusababisha tatizo hili.

“Atrial fibrillation inaweza pia kusababishwa na kuumia kifua au upasuaji wa kifua ambao haukwenda vizuri. Wapo pia watu waliopatwa na tatizo hili kwa sababu ya kunywa sana pombe kupita kiasi.

UWEZEKANO MDOGO WA KUPONA

“Tiba za muda mrefu huweza kusababisha mgonjwa akapona ingawa nafasi ya kupona kwa wagonjwa wanaopatwa na Persistent Fibrillation huwa ni ndogo,” alisema daktari huyo.

ZARI, MASHEMEJI ZAKE PACHIMBIKA

Hata hivyo, wakati Ivan akiagwa leo nchini Uganda kisha kuzikwa kesho, kuna taarifa zilizoenea mno wikiendi iliyopita zikionesha kuwa, katika kipindi cha kuuguza, Zari alikuwa ‘bize’ akisuguana na kaka wa Ivan pamoja na mashemeji zake akiwemo King Lawrence juu ya mali alizoacha marehemu.

IVAN AMEACHA NINI?

Ivan ameacha shule sita nchini Afrika Kusini, hoteli mbalimbali pamoja na majumba nchini Uganda. Ameacha pia watoto watatu, Pinto, Raphael na Quincy.

Yule Mchoraji wa Nembo ya Taifa, Mzee Francis Kanyasu (Ngosha) Amefariki Dunia

$
0
0
Mzee Francis Kanyasu aliyechora Nembo ya Taifa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye matibabu Muhimbili Hospital

Soma Nafasi za Ajira Mbali Mbali Zilizotangazwa Leo

Mwanamke Wangu Hataki Nione Nyeti zake

$
0
0
Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza , Mimi sijaoa  ila nina mpenzi sasa mpenzi wangu huyu mpya ananishangaza sana, tukiwa faragha mimi huwa sio mtu wa kujifichaficha huwa najiachia tu kama nilivozaliwa siogopi wala kuona aibu maana tunakuwa wawili tu , ila yeye sijawahi kumuona uchi wake kiukweli, kwanza hapendi tuonane mchana na usiku anataka nizime taa nashindwa kuelewa sababu ni nini?

Akilala kwangu asubuhi anavaa chupi akiwa kajifunika shuka, kifupi anajiziba ili nisione nyeti zake jambo hilo linanipa mawazo sana.

JE sababu ni nini?
Mwanzo nilidhani labda ni aibu ya upya hajanizoea ila ni mwezi wa tatu huu tangu tuanze mapenzi na huwa tunado karibia mala mbili kwa wiki anakuja jumamosi home na anakuja na jumatano,   hivyo kama ni kunizoea basi kanizoea sana na viutani vya kutosha vipo sana ila suala la kuona uchi hapo kwake ni pagumu, sasa ningetaka kujua hivi inaweza ikasababishwa na nini hiyo kitu ?

Ushauri Tafadhali

Korea Kaskazini Yaichafua Japan kwa Kombora, Yazidi Kuivuruga Marekani..!!!

$
0
0

Korea Kaskazini imeendelea kuonesha ukaidi dhidi ya makatazo ya Marekani na Umoja wa Mataifa kwa kufanya majaribio mengine ya makombora ambayo yamethibitika kufanikiwa.

Kwa mujibu wa BBC, makombora yaliyofyatuliwa na Korea Kaskazini mara tatu mfululizo yalienda umbali wa kilomita 450 juu kabla ya kutua kwenye maji ya bahari ya Japan ndani ya dakika sita, hali iliyosababisha Japan kupinga vikali kitendo hicho.

Katibu wa Baraza la Mawaziri la Japan, Yoshihide Suga ameviambia vyombo vya habari kuwa makombora hayo yalitua katika maeneo kati ya Sado na visiwa vya Oki, maeneo ambayo ni kanda muhimu za kiuchumi.

Wataalam wameeleza kuwa majaribio hayo ya hivi karibuni yanaonesha dhahiri kuwa Korea Kaskazini inapiga hatua nzuri katika kufanikisha makombora yake kubeba vichwa vya nyuklia.

Marekani imeendelea kuionya Korea Kaskazini ikiitaka isijaribu kucheza na moto kwani haitavumilia. Rais Donald Trump alilaani na kutoa onyo kwa tamko la Korea Kusini kuwa makombora yake ya nyuklia yanaweza kufika katika baadhi ya sehemu za dunia ikiwa ni pamoja na majimbo kadhaa ya Marekani.

Korea Kusini imekuwa ikijitetea kuwa program yake ya silaha ni muhimu dhidi ya vitendo vya ukandamizaji vya Marekani.

Diamond: Sitaki Tiffah Awe Msanii, Naogopa Ataliwa Sana na Wanaume...!!!

$
0
0

Diamond Platnumz amefunguka kwa kudai kuwa hataki mtoto wake wa kike Tiffah awe msanii kwa madai akiwa msanii atatembea kimapenzi na wanaume wengi.

Muimbaji huyo amedai mtoto wake huyo akiwa msanii, wanaume wengi watamiminika kumtaka kimapenzi.

“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana,” alisema Diamond weekend iliyopita  akiwa katika kipindi KTN nchini Kenya. 

“Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha,”

Aliongeza, “Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na kweli nimetulia,”

Muimbaji huyo Jumanne hii anatarajia kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zazi, Ivan aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika Kusini kwa ugonjwa wa moyo.

WCB Yawapiga Marufuku Wasanii Wake Kwenda Club Usiku..!!!

$
0
0

Kama wewe ni mtembeleaji mzuri wa kurasa za mitandao ya kijamii ya wasanii wa lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz, bila shaka umekutana na uhaba mzito wa picha zinazowaonesha wakiwa klabu za usiku. Hii imetokana na marufuku inayowakabili!

Mpishi rasmi wa muziki wa WCB ndani ya Wasafi Records, mtarishaji Laizer amesema kuwa moja kati ya sera za lebo hiyo, zinakataza wasanii pamoja na mtayarishaji huyo kwenda kwenye klabu za usiku kula bata.

“Moja kati ya vitu ambavyo tunakatazwa ni kwenda klabu za usiku, hii hairuhusiwi kabisa,” Laizer aliiambia Twenzetu ya Times Fm. “Nadhani ni kwa sababu ya brand, haitakuwa kitu kizuri kuona brand inazurula tu usiku kwenye klabu na kama unavyojua klabu za usiku zina mambo mengi,” 
aliongeza.

Hata hivyo alisema kuwa wasanii hao wanaruhusiwa kuingia klabu kama kuna kazi au kuna mwaliko maalum utakaowasilishwa kwenye menejimenti kama mwaliko rasmi.

Endelea kubang tu na ngoma za WCB kwenye klabu ya usiku unayoikubali zaidi, lakini usitegemee kumuona Harmonize, Rich Mavoko, Raymond, Lava Lava hata bosi mwenyewe Chibu Dangote wakila bata karibu na wewe ndani ya klabu hizo bila mualiko maalum.

Banda Afunguka Sababu ya Kuondoka Msimbazi..Awataja Viongozi ..!!!

$
0
0

Mlinzi kiraka wa klabu ya Simba Abdi Banda amesema anaondoka klabuni hapo kwa kuwa makataba wake umeisha na hakuna mazungumzo yanayoendelea kati yake na uongozi wa wekundu hao, hadi sasa.

Banda, aliwashukuru mashabiki wa Simba na kuwaaga kwenye ukurasa wake wa Instagram, mara baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbao na kutwaa kombe la TFF Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Jumamosi iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dodoma, Banda amesema viongozi wa Simba hawaoneshi kumuhitaji kwani hawajazungumza naye hadi sasa.

"Ni kweli naondoka kwa sababu mkataba wangu umeisha na hakuna kiongozi aliyezungumza na mimi kuhusu mkataba mpya, na ndo maana niliwaaga mashabiki wa Simba kwenye Instagram". Alisema mlinzi huyo wa zamani wa Coastal Union.

Kuhusu wapi anaelekea kwa maisha mapya ya soka, Banda alisema kuwa anataka kuelekea Afrika Kusini kucheza soka huko.

Mangu Amsukumia Sakata la Mauaji Mkoani Pwani IGP Sirro..!!!

$
0
0

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.

Mangu ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Sirro kuwa IGP mpya wa kuliongoza jeshi la polisi nchini.

Kuhusiana na hali inayoendelea mkoani ][Pwani, Mangu amesema "Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano" - Mangu alifunguka

Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine amesema anamfahamu Sirro kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani

Hakimu Ajitoa Kusikiliza Kesi ya Godbless Lema

$
0
0
Hakimu  Mkazi, Desderi Kamugisha, amejitoa kuendelea kusikiliza moja ya kesi za uchochezi zinazomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema).

Katika kesi hizo, Lema anadaiwa kutoa matamshi yenye chuki na kuibua nia ovu kwa jamii.

Hakimu Kamugisha amejitoa katika kesi ya jinai namba 441/2016 ambayo Lema anadaiwa kutoa matamshi hayo Oktoba 23, mwaka jana wakati wa mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa.

 “Kiburi cha Rais kisipojirekebisha, Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, mwaka 2020 haitafika Mungu atakuwa ameshamchukua maisha yake.

“Rais ana kiburi, Rais kila mahali watu wanaonewa, wafanyakazi wa Serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana amani, watu wananyanyaswa,” Lema alinukuliwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Martenus Marandu.

Hakimu huyo sasa ataendelea kusikiliza kesi nyingine ya jinai namba 440/2016 ambayo pia inamhusu Lema anayedaiwa kutoa maneno ya uchochezi yenye kuleta tabaka miongoni mwa jamii Oktoba 22, mwaka jana maeneo ya Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro wakati wa mkutano wa hadhara.

Miongoni mwa maneno ambayo Lema anayodaiwa kuyatoa ni: “Rais Magufuli akiendelea na tabia ya kudhalilisha demokrasia na uongozi wa upinzani, iko siku taifa litaingia kwenye umwagaji wa damu.

 “Rais yeyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, mipaka ya katiba, ataingiza taifa katika majanga na umwagaji damu, watu watajaa vifua, wakiamua kulipuka polisi hawa wala jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu utakaojitokeza.”

Jana kesi hizo mbili zilipangwa kutajwa mbele ya Hakimu Kamugisha katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, lakini Wakili wa Serikali, Alice Mtenga, alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi umekamilika, hivyo wanaomba kupangiwa tarehe ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Lakini Hakimu Kamugisha alisema haoni busara kuendelea kusikiliza kesi zote wakati kuna mahakimu wengine.

“Nilikuwa na kesi nne za mshtakiwa huyu huyu, sasa zimebaki mbili. Kwangu sioni kama itakuwa busara  kusikiliza kesi zote wakati kuna mahakimu wengine wanaweza wakasikiliza, najiondoa kwenye kesi namba 441, nitaendelea na kesi moja namba 440.

“Ukiangalia nature ya kesi ni ile ile moja, mshtakiwa yule yule, kwa hiyo tutaenda kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi ili apangiwe hakimu mwingine wa kusikiliza kesi hiyo ili tarehe ya kusomwa maelezo ya awali itakayopangwa, asikilize hakimu mwingine,” alisema.

Katika kesi hizo, Lema anawakilishwa na Wakili Sheck Mfinanga.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo hakuweza kufika mahakamani hapo jana kwa madai kuwa hawakuwa na taarifa za kesi hizo kupangwa.

“Nilikuwa nimesimama kwenye korido ya mahakama asubuhi nikamuona RCO, nikamuuliza kuna nini akanijibu amekuja kwenye hizi kesi, ndipo nikaamua kuja mahakamani ila Lema au wadhamini wake hawakufika,” alisema Mfinanga.

Lema alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Kamugisha Novemba 8, mwaka jana, akikabiliwa na kesi hizo.

Novemba 11, mwaka huo huo, alishindwa kupata dhamana baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha kwa njia ya mdomo kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kupinga uamuzi wa dhamana uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Lema alikaa mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo kwa zaidi ya miezi minne kutokana na kukosa dhamana kuanzia Novemba 11 mwaka jana kabla ya kuachiwa kwa dhamana Machi 3, mwaka huu na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Mchanga wa Madini Walivuruga Bunge....... Tundu Lissu na Godbless Lema Wanapinga Kitendo cha Serikali Kuuzuia

$
0
0

Mchanga  wa dhahabu uliozuiwa katika makontena Bandari ya Dar es Salaam, umezua mjadala bungeni baada ya wabunge wa CCM na Chadema kupingana juu ya uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli kuyazuia kusafirishwa nje ya nchi.

Hayo yalitokea jana wabunge walipokuwa wakichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2017/18, iliyowasilishwa na Waziri Balozi Augustine Mahiga.

Wakichangia bajeti hiyo, wabunge wawili wa Chadema, Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Godbless Lema (Arusha Mjini), walisema uamuzi wa Rais Magufuli utalisababishia taifa hasara na kuwafukuza wawekezaji wa nje.

Naye Lema alisema amepata taarifa kwamba wamiliki wa mgodi wa Acacia ambao makontena yao yamezuiwa, wamefungua kesi katika Mahakama ya London, Uingereza, kulalamikia uamuzi huo wa Serikali.

“Katika hatua ya kulinda rasilimali ya nchi, ni mwendawazimu anayeweza asipongeze, lakini lazima tujue ni namna gani unalinda rasilimali hizo bila kuligharimu taifa.

“Wote tunafahamu taifa letu lina mgogoro na Acacia Minning ambao kwa sura ya kwanza, mgogoro huo unajenga hisia za siasa ndani ya nchi na sura ya pili ya mgogoro huo unapunguza kasi ya wawekezaji wa nje kuja kuwekeza nchini.

“Leo (jana) tunapongeza alichokifanya Rais, tuelewe wakati Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anaanza sera ya kunyang’anya watu mashamba na kuwakandamiza wawekezaji, alipigiwa makofi na watu wake kama ambavyo sisi tunapiga makofi leo.

“Matokeo yake leo Zimbabwe hawana noti yao, hawana fedha yao na ni taifa ambalo halina ‘identity’.

“Katika suala hili ni muhimu mumshauri Rais kwa sababu  gharama za uamuzi wake ni kubwa, ikizingatiwa Acacia leo wamekwenda mahakamani London na kwa hali ya kawaida, taifa hili litaingia kwenye gharama kubwa kama tulivyoingia kwenye minofu ya samaki,” alisema Lema.

Tundu Lissu alisema amekuwa akipinga sera mbaya za uwekezaji tangu mwaka 1999 na kwamba uamuzi alioufanya Rais Magufuli si mzuri na ataupinga kama ambavyo amekuwa akipinga sera zote ambazo zimelifikisha taifa pabaya.

Alisema uamuzi wa kuzuia makontena hayo unalichafua taifa kimataifa na kuwaogopesha wawekezaji wa nje.

“Suala siyo Acacia watafanya nini, suala ni watu wote tunaohusiana nao kwenye uchumi kama Wachina ambao ndiyo taifa kubwa duniani kwa uwekezaji watafanya nini.

“Fikiria, Jumuiya ya Ulaya, Japan na Marekani watafanya nini kwa sababu ya kuwanyang’anya mchanga wa dhahabu Acacia.

“Sisi tunazungumza masuala ya diplomasia ya uchumi wakati hatujui lolote kuhusu diplomasia ya uchumi, ndiyo maana tunafanya haya tunayoyafanya. Kwa hiyo, waziri nakuomba usikubali hizi kelele kwa sababu hivi sasa nchi yetu ina hali mbaya kwenye diplomasia.

“Tulichokifanya ni makosa katika sheria, mikataba ni makosa kwa mujibu wa sheria za mataifa. Kwa taarifa yenu, gharama tutakazolipa katika jambo hili ni kubwa kuliko huo mchanga wa Acacia.

“Tutakuwa na kesi kama Zimbabwe, tusishabikie uamuzi uliofanyika kwa sababu tu umefanywa na Rais,” alisema Lissu.

Hatua hiyo ilimfanya Mnadhimu Mkuu wa Serikali, Jenister Mhagama, aombe mwongozo kwa mwenyekiti wa Bunge kutokana na lugha kali aliyokuwa akitumia mbunge huyo (maneno hayo makali hatukuyaandika).

Akijibu mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, alimtaka Lissu afute maneno hayo makali, jambo ambalo alilikubali ingawa alisisitiza kupingana na uamuzi wa Rais Magufuli.

Wabunge wa CCM nao waliamua kujibu mapigo kwa kusema uamuzi uliofanyika ni sahihi kwa kuwa nchi ilikuwa ikiibiwa.

Mbunge wa Viti Maalumu, Juliana Shonza, aliwashamnbulia Lema na Lissu akisema hawaaminiki kwa kuwa walikuwa wakimsema vibaya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa ni fisadi, lakini alipohamia Chadema wakampigia kampeni wakati wa Uchaguzi Mkuu.

“Wewe Lissu na Lema, mlikuwa mkimsema vibaya Lowassa ni fisadi, alipokuja kwenu mkaanza kumsafisha. Je, huo siyo uamuzi mbaya?

“Yaani nyie kila kinachofanywa na Serikali mnaponda kwa sababu mmejipa vyeo vya mtoto wa kambo. Eleweni nchi hii inahitaji Rais kama Magufuli, nyie wenzetu endeleeni kutetea wezi, sisi tumeshawazoea.

“Tunamuomba Mheshimiwa Rais aendelee kuchapa kazi, nyie wenzetu muendelee kulalamika, sisi hapa kazi tu,” alisema Shonza.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba, alisema uamuzi uliofanywa na Rais Magufuli ni sahihi na utaigwa na mataifa mengine duniani.

Alisema kuna haja ya Watanzania kushirikiana katika uamuzi huo kwa masilahi ya taifa.

Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi, aliwatoa hofu Watanzania kwa kusema kama Acacia watakwenda mahakamani, Serikali itakwenda pia kwa kuwa jambo hilo linawezekana.

“Tutabishana hapa kutafuta umaarufu kwa sababu kama ni mahakamani tutakwenda pia. Hata mtu wa kawaida ukimwambia jambo hilo alilofanya Rais atakuunga mkono na nawaomba tusipinge kila kitu kwa sababu ya itikadi zetu,” alisema Chumi.

Wengine waliounga mkono uamuzi wa Serikali huku wakitaka Watanzania washirikiane katika jambo hilo, ni Mbunge wa Viti Maalumu, Mary Mwanjelwa, Ester Mahawe na Rose Tweve.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, aliwataka wabunge wasishabikie suala la wawekezaji hao kwenda mahakamani kwa sababu wakienda huko hawataishtaki CCM bali wataishtaki Tanzania.

“Nawaomba waheshimiwa wabunge muiunge mkono Serikali katika jambo hili kwa masilahi ya Taifa, nchi ikishtakiwa, haitashtakiwa CCM.

“Kilichofanyika hakina makosa kwa mujibu wa sheria kwa sababu mkataba una kipengele kinasema unaweza kupitiwa upya baada ya miaka mitatu, kwa hiyo nawaomba tushirikiane,” alisema Masaju.

Wabongo ni Kiboko Nimewavulia Kofia Instagram - Shamsa Ford

$
0
0
Msanii wa filamu bongo, Shamsa Ford amefunguka mapya kwa kudai laiti watu wangekuwa wanaitumia vizuri mitandao ya kijamii basi wangekuwa wamefika mbali kimaendeleo lakini wamebakia katika kutengenezea mambo ya uongo tu.

Shamsa amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kukerwa muda mrefu na watu wanaopenda kutumia mitandao ya kijamii kuanzisha mijadala ambayo haina ukweli wowote wala kuwa na taswira nzuri katika jamii.

"Nina imani hii mitandao tungeitumia vizuri tungekuwa na maendeleo makubwa,ila unavyotumika jamani ni kero. Sisi wabongo ni kiboko aise, wabongo wa instagram ni kiboko Wallah, mtu anaweza akatengeneza jambo likafanana na ukweli mpaka mwenyewe ukachoka. Wabongo tuna vipaji"aliandika Shamsa.

Walemavu Walioungana Wampata Kijana wa Kuwaoa

$
0
0

Kwa yeyote aliyewahi kukutana nao, mapacha wawili ambao ni walemavu walioungana matumbo, Maria na Konsolata hatabisha kwamba pamoja na hali yao, watoto hao ni wacheshi, wakarimu na wanaoweza kukufanya utabasamu hata kama moyoni mwako, ulikuwa na huzuni.

Wiki hii walifanyiwa mahojiano na Gazeti la Mwananchi na kufunguka mengi kuhusu maisha yao pamoja na ishu yao ya kufikiria kuolewa.

Si rahisi kufikiria maisha ya ndoa ya Maria na Consolata kwa jinsi walivyo, lakini pacha hawa walioungana wako wazi kuhusu matamanio yao ya maisha ya ndoa.

Katika mazungumzo yao na gazeti hili, Maria na Consolata waliweka bayana mipango yao ya ndoa mara watakapomaliza elimu ya chuo kikuu.

Ingawa ni kitu cha kushangaza, Maria na Consolata hawatakuwa mapacha wa kwanza katika maisha ya ndoa. Chang na Eng Bunker ni pacha wanaume waliozaliwa mwaka 1811 nchini Thailand ambako zamani kuliitwa Siame.

Tofauti na mapenzi ya akina Maria na Consolata, pacha hao kila mmoja alioa mke wake na kufanikiwa kupata watoto.
Kama ilivyokuwa kwa pacha hao, Maria na Consolata wanatamani kuwa wanandoa na ndoto zao ni kuolewa na mwanaume mcha Mungu na atakayewajali.

“Ndoa ni sakramenti takatifu, tukishamaliza masomo yetu ya chuo kikuu tunatamani kuja kuwa wanandoa,” anasema Maria.

Kwa namna walivyo, si rahisi kwao kuolewa na wanaume tofauti isipokuwa mume mmoja na wanalijua hilo.

Haya ndio yalikuwa mahojiano baina yangu na wao kufuatia ndoto hiyo.

Mwandishi: Baada ya masomo, nini ndoto zenu?

Maria: Ndoto zetu ni kuwa wanandoa. Zamani tulikuwa tunapenda tofauti, lakini kwa sasa tumempenda mtu mmoja.

Tumegundua tuna hisia moja.

Mwandishi: Tayari kuna mtu mmempenda nini?

Maria na Consolata kwa pamoja: Ndio tumempenda mtu mmoja.

Mwandishi: Nani alimwambia mwenzake kwanza kuhusu hisia za kupenda?

Consolata: Sisi ndio tuliomwambia kwamba tunampenda, naye alitusikiliza.

Mwandishi: Aliwajibu nini?

Maria: Yupo kwenye tafakari, hawezi kusema akurupuke na kuingia bila tafakari. Lazima tumpe muda wa kutafakari.
Mwandishi: Ni mwanaume wa aina gani mnayempenda?

Consolata; Tunapenda kuolewa na mwanaume wa kawaida, mwenye tabia njema na mcha Mungu asiwe tajiri. Ikiwa tutamaliza masomo yetu, huyu tuliyempenda anafaa kuwa mume wetu. Kihalisia tunatamani mwanaume mcha Mungu, mwenye upendo na ambaye atathamini utu wetu.

Mwandishi: Kwa nini hampendi kuolewa na tajiri?

Consolata: Ni kwa sababu matajiri wengi huwa wanathamini pesa zao sio utu. Samahani hapa sio matajiri wote, ila wengi wao kwa hiyo sisi tunataka mtu anayeweza kuthamini utu.

Mwananchi: Ndoa ni mume na mke mmoja kwa Wakristo. Mmewahi kutafakari hilo?

Consolata; Ndio, Biblia inasema kwamba Mungu aliweka agano kati ya mume na mke mmoja. Sasa kwa kuwa sisi tumeungana wawili na tuna hisia moja, hatuwezi kuolewa na wanaume tofauti. Tutaolewa na mume mmoja.

Tunatamani sana kumtumikia Mungu kupitia sakramenti ya ndoa. Mungu akitujalia tumalize masomo yetu basi tunataka kuolewa ili tumtumikie Mungu katika huo wito vizuri.

Pacha hao waliweka bayana jina la kijana waliyempenda, ingawa kwa sababu za kimaadili tunalihifadhi. Hata hivyo, baba mdogo wa kijana huyo alikuwa tayari kuzungumza na gazeti hili.

Baba huyo mdogo alisema ana taarifa za kijana wao kupendwa na pacha hao.

“Unajua nilishangaa kuona watu wananiita baba mkwe wa akina Maria na Consolata. Baadaye ndio nikajua kuwa kuna mahusiano baina yao (kijana na mapacha hao), japo wote wanaendelea na masomo. Kupenda ni moyo na kama ikitokea wakafikia ndoto hizo huko baadaye, basi itakuwa hivyo,” anasema.

Mwalimu mkuu wa Shule ya Maria Consolata, Jefred Kipingi anasema hisia za kuolewa kwa mabinti hao ni jambo la kawaida na kwamba, wanapenda kuishi maisha ya kawaida kama walivyo watu wengine.

“Uzuri wake ndoto yao ni kuwa walimu na wanasema wataolewa wakishamaliza masomo yao. Jambo hilo ni jema na hapo Mungu ndipo atadhihirisha utukufu wake zaidi,” anasisitiza.

Ingetegemewa kwamba katika dunia ya utandawazi, taarifa za kuzaliwa kwa pacha walioungana zingetapakaa kila mahali zikipamba magazeti, redio, luninga na hata mitandao ya kijamii.

Lakini haikuwa hivyo kwa Maria na Consolata. Hakuna chombo chochote kilichopata taarifa ya kuzaliwa kwa pacha hao wa kipekee.

Ulemavu wao ulisababisha wafichwe hadi walipofikisha umri wa kuandikishwa elimu ya msingi katika Shule ya Ikonda na kutafutiwa mlezi wa kuwaangalia, baada ya wazazi wao kufariki dunia wakiwa wadogo.

Habari zao zilianza kufahamika baada ya kuandikishwa darasa la kwanza na kutafutiwa mlezi aliyewalea hadi wakati walipofaulu vizuri mitihani yao ya darasa la saba mwaka 2010.

Mlezi wao, Bestina Mbilinyi alikuwa alifanya hivyo chini ya wamisionari lakini, alikuwa akiishi nao nyumbani kwake Ikonda.

“Niliombwa niishi na watoto hawa kwa sababu kutoka kwangu hadi shuleni sio mbali, nilijengwa choo kinachokidhi maumbile yao na niliishi nao hadi wanamaliza darasa la saba,” alisema wakati akizungumza na Mwananchi wakati walipomaliza darasa la saba

Ivan Kuzikwa leo, Zari aahidi Kuwaangalia Watoto

$
0
0
Baada ya Jumatatu hii mwili wa Ivan Ssemwanga kuagwa na kufanyiwa ibada takatifu, aliyekuwa mke wa zamani wa marehemu, Zari Hassan alipata fursa ya kuzungumza kwa mara ya kwanza.

Katika misa ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Namirembe mijini Kampala, Uganda Jumatatu hii, Zari alionekana akiwa ametulia na akizungumza na wanae.

Alipoitwa kuzungumza madhabahuni, watu waliohudhuria walijianda kumsikiliza atakachosema.

“Sitomhuzunikia Ivan,” alisema. “Nitasherehekea maisha yake. Muda mrefu, tulitengana kwasababu ya tofauti ambazo sote tulizijua. Nilisonga mbele na maisha yangu, lakini si Ivan. Ivan alijua kile nilichoweza kufanya. Alijua kile nilichoweza kufanya na kile nisichoweza. Alijua kuwa ningewaangalia vijana vyema na aliniamini. Kwa hali hiyo, naahidi ntawaangalia vijana hadi nitakapoungana naye.”

Ivan anatarajiwa kuzikwa leo ambapo Diamond aliyezaa na Zari watoto wawili naye aliahidi atahudhuria.

Msanii siyo Malaika Tuna Mioyo Pia- Irene Uwoya

$
0
0
Malkia wa filamu Bongo, Irene Uwoya amefunguka kwa kusema anachukizwa na tabia za baadhi ya mashabiki waliopo mitandaoni kushindwa kutoa ushauri kistaarabu na badala yake kuanza kuwashambulia kwa kuwatukana.

Uwoya ameeleza hayo baada zile kelele za wasanii wengine kudai mashabiki zao ndiyo wamekuwa vinara katika kuwakosoa pindi wanapokuwa wame-post kazi zao hata muda mwingine maisha yao binafsi wakiwa sehemu wana-enjoy na marafiki zao.

"Mashabiki zetu wapo katika nafasi nzuri ya kusema kama tunakosea au tunapatia lakini njia wanayoitumia kutuelewesha siyo nzuri, wanatumia matusi badala ya kumwambia mtu taratibu akaelewa. Wanasahau kwamba wasanii ni binadamu kama binadamu wengine so tunavyoishi tunaishi kama watu wengine tu. Msanii siyo malaika, saa zingine hawajui mtu unakuwa katika hali gani, labda umefiwa au unaumwa wao wanatukana tu."alisema Uwoya.

Simba na Yanga Wahamishia Bifu lao Kimataifa

$
0
0
BAADA ya kushuhudia upinzani mkali kwenye kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Kombe la FA, ushindani na upinzani wa Simba na Yanga sasa umehamia kwenye michuano ya kimataifa.

Hatua hiyo inakuja baada ya Yanga kufanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Simba ikikata tiketi ya kushiriki Kombe Shirikisho barani Afrika.

Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, aliliambia Nipashe jana kuwa kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika haitoshi na badala yake wanataka kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi.

"Lazima Simba ionyeshe utofauti... tunataka kurejea kwa kishindo kwenye michuano ya kimataifa kwa kuhakikisha tunafika mbali," alisema Mayanja ambaye juzi alikuwa pamoja na kikosi cha timu hiyo Bungeni mjini Dodoma.

Aidha, Meneja wa Yanga, Hafidh Salehe akizungumza na Nipashe juzi, alisema ushiriki wa Simba na Yanga utaleta ushindani mkubwa kwao kwenye michuano ya kimataifa.

Alisema kila timu itataka kuizidi nyingine kwenye michuano ya kimataifa na hiyo itasababisha kujipanga zaidi kuelekea kwenye ushiriki wa michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

"Hii italeta changamoto kuhakikisha kila mmoja anamzidi mwenzake, michuano ya kimataifa ni migumu, lakini naamini maandalizi mazuri yanatoa msaada mkubwa kwenye kufanya vizuri," alisema Saleh.

Simba na Yanga zilionyesha mchuano mkali kuelekea mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kukabana koo hadi dakika ya mwisho kwa kufungana pointi 68 kila moja kileleni.

Hata hivyo, Yanga ilitangazwa mabingwa wa ligi hiyo kufuatia kuwa na tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo kukata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika hapo mwakani.

Simba yenyewe ilipata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuichapa Mbao FC mabao 2-1 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA iliyopigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma Jumamosi iliyopita.

Katika kujiimarisha na michuano hiyo pamoja na Ligi Kuu Bara msimu ujao, klabu hizo kila moja imeanza kuendesha mkakati wa usajili kimyakimya, huku viongozi wao wakikataa kuweka wazi majina ya nyota wanaowahitaji.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images