Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live

Polisi Moshi Yazuia Jeneza la Mwili wa Ndesamburo Kupitishwa Barabarani..!!!

$
0
0

Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa hiyo, mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu Philemon Ndesamburo .

Majibu ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali zinazoendelea.

Sababu ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha usumbufu kwa watumiaji wengi wa barabarani.

“Ofisi ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli zote za kutoa heshima za mwisho.

Jana mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu aliliambia Mwananchi kuwa mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.

Credit- Mwananchi

Hivi Ndivyo Gwajima Alivyotua Kilimanjaro kwa Ajili ya Kazi ya Kuuaga Mwili wa Ndesamburo..!!!

$
0
0

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewasili katika viwanja vya Majengo, Moshi kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Chadema, Phillemon Ndesamburo.

 Tayari mwili wa Ndesamburo umewasili katika viwanja vya Majengo na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa Chadema.

Mwili wa Ndesamburo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini,utaagwa katika viwanja hivyo na leo saa 10 jioni utapelekwa nyumbani kwake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

 Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chadema, akiwamo muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, Frederick Sumaye wapo uwanjani hapo kwa ajili ya kumuaga Ndesamburo

Kajala Aibuka na Haya Kuhusu Wema Sepetu..Adai Hata Mwanae ni Shahidi..!!!

$
0
0

TASNIA ya filamu nchini imepambwa na wasanii wa kike wenye urembo unaovutia macho na hakika kwenye orodha ya waingizaji wenye kipaji, uwezo na mvuto huwezi kumuacha, Kajala Masanja.

Huyu ndiyo bosi wa kampuni ya Kajala Entertment,  ambayo imetengeneza filamu nyingi ikiwemo ile ya Sikitu ambayo chini ya mpicha Farid Uwezo iliweza kufanikiwa  kuliteka soko hilo la filamu.


Juma3tata wiki hii lipo na mrembo huyu, mpenzi wa chakula aina ya ndizi na samaki sato ambapo amefunguka mambo kadha wa kadha yanayohusu maisha yake ya ustaa na yale ya kawaida.

MKASA WA JELA WAMFUNZA

“Nina mfano halisi kabisa katika maisha na nitahakikisha namfunza mwanangu Paula asije akakutana na mkasa ulionikuta mimi na kufanya niingie jela kwa kuwa nilimsapoti mtu hata kwa yale yasiyostahili kisa nilikuwa nampenda,” alisema Kajala.

HATAKI KUFANYA TENA KOSA

Kajala amezidi kulifahamisha Juma3tata kuwa hapendi kulikumbuka tukio lile lililomfanya akae jela kwa muda wa mwaka mmoja na kumwacha mtoto wake kwenye wakati mgumu na hataki tena kufanya uzembe uliosababisha kosa lile.

 “Naweza sema ni uzembe ambao nilijitakia mwenyewe,  kumwamini mtu wakati kabisa najua ananiingiza shimoni ni kitu ambacho hakitafutika maishani mwangu, sitafanya kosa tena” anasema Kajala.

AWAONYA WAREMBO WENGINE

“Nataka wasichana wenzangu wajifunze kupitia mimi yaani hata kama unampenda mtu, usikubali akushawishi uvunje sheria za nje, jitahidi ujinasue kwani mwisho wake ni mbaya sana,” anasema.

HATASAHAU HURUMA YA WEMA SEPETU

Mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 au faini ya shilingi milioni zaidi ya kumi, Kajala na ndugu zake  waliingiwa na hofu kwani fedha hiyo ilikuwa ni kubwa kwao na hapo ndipo Wema Sepetu alipoibuka shujaa.

“Kama asingekuwa Wema Sepetu kunilipia zile  pesa sijui sasa hivi ningekuwa wapi, kwani hata ndugu zangu walichanganyikiwa kusikia kiasi kikubwa kile cha fedha ila moyo wa huruma wa Madame ulisababisha nitoke, siachi kumwombea katika sala zangu mwanangu pia analijua hilo,” anasema Kajala.

AZIPONDA TIMU MTANDAONI

Aidha aliweka wazi kusikitishwa timu katika mitandao ya kijamii zinazoibua maneno ya kuchochea ugomvi kati yake na Wema kitu kinachomuumiza kwani kwake ni mtu wa thamani mno.

KUFA KWA SOKO LA FILAMU

Katika hatua nyingine  mrembo huyo  alizungumzia anguko la filamu huku akikanusha taarifa hizo kwa kuwa wasanii wa bongo bado wanapiga kazi huku wengine wakishirikishwa na wasanii wa mataifa mengine.

“Kama soko la filamu limekufa basi wasanii wasingepata kazi za nje, sasa hivi wasanii tunaitwa kufanya filamu nchi za nje kwa malipo mazuri, tamthilia zetu pia zinaruka kwenye ving’amuzi mbalimbali, nchi nyingi zinazojifunza Kiswahili zinategemea filamu zetu kwa hiyo tunazidi kuvuka mipaka na kufanya vizuri,” anasema Kajala.

AWACHANA WASAMBAZAJI

Kajala amewataka wasambazaji kuwalipa wasanii kwa wakati mara wanapowekeana saini mikataba ya kusambaza filamu zao na siyo kuwalipa wasanii kwa awamu kitu kinachowafilisi wasanii.

 “Wasambazaji wa Kihindi waache  kutuzungusha kwenye malipo, kingine waache kubagua wasanii, waache kuangalia staa gani yupo ndani ya filamu ndiyo wanunue, waangalie ubora wa kazi na siyo sura,” anasema.

ANAAMINI KWA WASANII WACHANGA

Staa huyu wa filamu amesema anaamini katika vipaji vya wasanii wachanga, anaamini kuna kazi nzuri zinatengenezwa na wasanii wachanga lakinni wasambazaji huzikataa kwa sababu hawana ustaa.

Hii Ndio Yanga Bana..Yatenga Bilioni 2 za Kufanya Usajili wa Kishindo..Chuji Aomba Kurudi Yanga Kukipiga Msimu Ujao..!!!

$
0
0

SASA Yanga kumekucha. Baada ya kumaliza pilikapilika za kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, sasa klabu hiyo inataka kuanza kazi ya kuunda kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao.


 Kamati ya Utendaji wa Yanga imeunda kabineti ya watu watano na kuwakabidhi Sh bilioni 2 kwa ajili ya kufanya mazungumzo na nyota wao wanaomaliza mikataba mipya na kufanya usajili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Mwenyekiti wa kabineti hiyo ni Hussein Nyika, makamu wake ni Mustapha Ulungo, huku wajumbe wakiwa ni Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa na kocha wa klabu hiyo, George Lwandamina.

Moja ya majukumu yatakayowakabili ni kuhakikisha wananasa saini za wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na klabu hiyo, ambao ni Salmin Hoza, Yusuph Ndikumana, Mbaraka Yusuph, Jamal Mwambeleko, Michael Gradiel,  Raphael Daudi, Mrisho Ngassa, Youth Rostard, Said Ndemla, Ibrahim Ajib na Jonas Mkude.

Ili kupata nafasi ya kuwasajili wachezaji hao, klabu hiyo imepanga kuacha nyota wao 15, ambao hawakuwa na nafasi katika kikosi hicho na kusuka upya timu kwa ajili ya msimu ujao.

“Kamati imeazimia kusajili wachezaji wengi vijana ambao wana uwezo na wenye ubora wa kucheza Yanga na kuwaacha wachezaji 15 ambao walikuwa hawana nafasi ya kucheza, wamedhamiria kujenga timu imara yenye hadhi na mashindano ya kimataifa, ndiyo maana wametenga fungu hilo la fedha,” alisema mjumbe huyo.

Aliongeza kuwa, mbali na kufanya usajili huo wa nguvu, lakini kamati hiyo leo inatarajia kuanza mazungumzo na wachezaji Deus Kaseke, Donald Ngoma, Amis Tambwe, Haji Mwinyi, Thaban Kamusoko, Vincent Bossou na wengine ambao mikataba yao ya kuichezea timu hiyo imemalizika hivi karibuni na kupendekezwa na Kocha Lwandamina kuendelea kuwa nao.

Mmoja wa wajumbe wa kabineti hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema: “Kesho (leo) Jumatatu tutaanza kazi ya kuzungumza na wachezaji wote ambao walimalizia mikataba yao, ambao wamependekezwa kubaki na kocha Lwandamina, baada ya hapo itakuja zamu ya wachezaji wapya ambao watakuwa wameorodheshwa kwenye ripoti ya kocha wetu.”

Kwa upande wake Mkwasa, alisema Yanga ni timu kubwa na wamejipanga kufanya usajili wa nguvu wenye tija utakaowezesha kutetea ubingwa wao msimu ujao.

“Tumejipanga kila eneo ili kufanya usajili wa nguvu wenye tija ambao utazingatia vigezo vyote na mimi ndio nitaongoza jahazi hilo,” alisema Mkwasa.

Katika mipango yao ya usajili, Yanga wanadai kuwa na mpango na kuanza na beki wa kushoto wa Azam, Gadiel Michael, ili kucheza pamoja na Haji Mwinyi kwenye klabu hiyo.

Naye kiungo wa zamani wa timu hiyo, Athumani Idd  ‘Chuji’, ameomba kurejea tena kundini kuvaa viatu vya Justine Zullu ‘Mkata Umeme’ na kusema uwezo wa kuitumikia timu hiyo ya Jangwani bado anao kama akipewa nafasi katika eneo la kiungo mkabaji.

“Nimeiangalia Yanga msimu uliomalizika, nimegundua bado ninao uwezo mkubwa wa kuichezea timu hiyo pamoja na umri wangu wa miaka 29, bila shaka ninaweza kulitibu tatizo la kiungo mkabaji ambalo limekuwa likiwasumbua Yanga kwa muda mrefu,” alisema ‘Pass Master’ huyo, Chuji.

Akizungumza kuhusiana na ombi hilo la Chuji kutaka kurejea tena Yanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Paulo Malume, alisema amelisikia suala hilo na atalipeleka mahali husika kwa ajili ya kulitolea maamuzi, lakini yeye hawezi kusema lolote.

“Nimelisikia suala la mchezaji huyo, kwa kifupi nitalipeleka mahala husika tuone nini watasema, kila mtu anamfahamu Chuji alikuwa ni mchezaji wetu, lakini muda mrefu umepita tangu aondoke, hivyo ngoja tuone watasemaje,” alisema Malume.

Mnyika Aaapa Kula Sahani Moja na Askari wa Bunge Aliyemsukuma Juzi Bungeni..!!!

$
0
0

Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika amesema atachukua hatua kwa kitendo cha kusukumwa kilichofanywa na askari wa Bunge mwishoni mwa wiki.

Alisema atafanya hivyo mara baada ya kumaliza msiba wa mmoja wa waasisi wa chama hicho, Philemon Ndesamburo.

“Nitatoa tamko na kuchukua hatua nikimaliza msiba, leo (jana) na kesho (leo) nipo msibani huku Moshi, lakini nitafafanua na kuzungumzia hilo nikimaliza,” alisema.

Mnyika alitolewa bungeni kwa nguvu na askari wa Bunge baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwaamuru kumtoa ndani akidaiwa kukiuka kanuni za Bunge wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini.

Pia, mbunge huyo alipewa adhabu ya kutohudhuria vikao saba vya Bunge, huku askari hao wakimtoa ndani kwa nguvu na kumsukuma.

Perez - Zidane Anaweza Kuifundisha Madrid Hadi Mwisho wa Maisha Yake..!!!

$
0
0

Kocha Zinedine Zidane huwenda akaifundisha klabu ya  Real Madrid maisha yake yote kwa mujibu wa rais wa klabu hio, Florentino Perez ikiwa ni siku chache baada ya kocha huyo Mfaransa kuchukua kombe la  Champions League kwa miaka miwili mfululizo, baada ya ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Juventus.

Meneja huyo ambaye pia alikuwa na mafanikio makubwa katika kucheza soka duniani, alikuwa akibezwa hukusu uwezo wake wa kufundisha soka.

Ubingwa huo umeweza kuifanya klabu hiyo kuvunja rekodi ya kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo pamoja na kuwa klabu iliyochukua kombe hilo mara 12.

Rais wa klabu ya Real Madrid ameiambia radio ya Spanish Cadena Ser “Zidane can stay at Real Madrid for the rest of his life. Every Real Madrid fan is so grateful to him, he lifted our level of talent when he arrived in 2001 and was the best player in the world,”

Kwa upande wa Zidane baada ya mafanikio hayo alisema, “I can’t say whether I’ll stay for the rest of my life but I’m so grateful for the club for everything it has given me,”

“I played here for a long time and I feel part of the furniture. I’m also lucky to be part of this club and with this squad. Every player in the squad has played their part, and that’s been the key factor this season.” Zidane aliviambia vyombo vya habari.

Okoa Ndoa Yako Sasa..Ongeza Maumbile, Nguvu na Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0

OKOA NDOA YAKO SASA. ONGEZA MAUMBILE, NGUVU NA HAMU YA TENDO LA NDOA HATA KWA WENYE KISUKARI.
Tatizo la maumbile madogo, nguvu za kiume na ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa limekuwa likiwasumbua wengi na kusababisha kushindwa kujiamini ktk tendo hivyo kusababisha ndoa nyingi kuvunjika pamoja na mahusiano. Upungufu wa nguvu na hamu ya tendo husababisha mambo kama:-
(a)Uume kulegea wakati wa tendo
(b)Kukosa hamu ya tendo la ndoa
(C)Kuwahi kufika kileleni
(D)Uume kuchelewa kusimama baada ya round ya kwanza.
(E)Kuchoka sana baada ya round moja n.k
@Markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo kwa kutumia bidhaa zilizotengenezwa kwa mimea na matunda zisizo na kemikali wala madhara na kuthibitishwa kiafya. Pata hizi👇👇👇👇
🍉 🌿🍅🍒🍍🍓🍉🍎🍀
1.HANDSOME UP ni kifaa chenye uwezo wa 99 % kuongeza uume (size unayohitaji) na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6.5 @130,000/=
3.Vidonge maalum kwa ajili ya nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @130,000/=
4.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kuweza kurudia tendo hata mara 3 @130,000/=
Kwa Bidhaa hizi na nyingine kama:-
5.Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi @130,000/=
7.Kutengeneza shepu (hips, makalio na mapaja) @200,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni @120,000/=
9.Kuwa mweupe na soft mwili mzima bila kuacha sugu 120,000/=
10.Kurudisha usichana (bikra) @120,000/=
11.Kupunguza au kuongeza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @120,000/=
Wasiliana nasi kwa (+255)
0767447444 au 0714335378.
NB: Matokeo ni uhakika na garantii na upate risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii.
Follow us
@Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr

Askari wa Bunge Wapangiwa Vituo Vingine vya Kazi kwa Kusuasua Kumtoa Nnje ya Bunge Mnyika..!!!

$
0
0

Askari walioagizwa kumtoa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika bungeni Ijumaa iliyopita, wamepangiwa vituo vingine vya kazi kwa kuchelewa kutekeleza agizo la Spika.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema aliwashangaa askari hao kwa jinsi walivyokuwa wanambeleza mbunge huyo wa Kibamba kutoka nje.

"Askari hawa wataendelea kuhamishwa mpaka pale tutakapowapata wanaofaa," amesema Ndugai.

Mnyika alitolewa bungeni Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa wabunge kusema ‘Mnyika mwizi’ akimhusisha na wizi wa madini.

Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua dhidi ya mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika alisema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi.

Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayawezi kwenda hivyo. 

Baada ya majibizano kati yao Spika aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge

Ndugai: Askari Nikisema Mbunge Atoke Akikaidi Mpigeni Nawaruhusu..!!!

$
0
0

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amewapa maelekezo askari wa Bunge wampe kipigo Mbunge yeyote atakayeagiza atolewe nje ya Bunge na kukaidi, ili iwe mfano kwa wabunge wengine.

Zari Achaguliwa Kuwa Msimamizi Mkuu wa Mali za Marehemu Ivan Ssemwanga..!!!

$
0
0

Kamati ya watu 4 yachaguliwa kusimamia mali za marehemu Ivan Ssemwanga mpaka watoto wake watakapofikisha miaka 18. Zari Hassan yumo. 

Wengine waliochaguliwa ni Ritah Ssemwanga(Dada wa Ivan), Lawrence Muyanja(Maarufu kama King Lawrence) na George Ssemwanga ambae ni kaka mkubwa wa Ivan.

Zari ametakiwa kusimamia shule za Ivan zilizoko Afrika Kusini kikiwemo chuo cha Brooklyn na pia nyumba mbili za Ivan zilizoko Sandton na Pretoria. 

Zari pia ametakiwa aishi na watoto wake wote kwenye nyumba moja na nyingine ipangishwe.

Eh..Kumbe Mrisho Ngasa Yupo Yanga kwa Makubaliano Haya Eti..!!!

$
0
0

WINGA aliyekipiga Mbeya City msimu uliopita, Mrisho Ngassa, amerejea kwenye klabu yake ya zamani ya Yanga na leo amejumuishwa kwenye kikosi hicho kilichocheza na Tusker kwenye michuano ya Super Cup, katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

 Ngassa, ambaye mkataba wake na Mbeya City umemalizika baada ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha klabu hiyo ya Jangwani katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Dar es Salaam.

Taarifa ambazo BINGWA imezinasa jana kwenye mazoezi hayo, ni kwamba Ngassa ameagizwa kujiweka fiti ili kuangaliwa uwezekano wa kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.

“Ngassa ameomba kurejea Yanga na benchi la ufundi kupitia uongozi limempa masharti ya kuhakikisha anajifua na kurejesha kiwango chake ili waangalie uwezekano wa kumpa mkataba,” kilisema chanzo hicho.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, alisema michuano hiyo haimzuii mchezaji kutoka timu nyingine kushiriki, bali kikubwa ni kufuata kanuni zao walizoweka.

“Kwa sasa Ngassa yupo na timu yetu akifanya mazoezi na ikibidi anaweza kutumika pia katika michuano hiyo, suala la kumsajili itategemeana na mapendekezo ya kocha, akimhitaji tutampa mkataba,” alisema Mkwasa.

Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema anachofahamu yeye kuhusu Ngassa ni kwamba amekwenda Yanga kwa ajili ya kufanya mazoezi ili ajiweke fiti na wapo wengine wengi.

“Siyo Ngassa pekee anayefanya mazoezi na Yanga, wapo wachezaji wengi ambao huwezi kuwazuia wala kuwauliza wamefuata nini, kwani kazi yangu ni kufundisha, jukumu la kuuliza nani yupo kwa sababu gani ni la uongozi wa juu,” alisema.

Mbali na Ngassa, wachezaji wengine waliojiunga na kikosi hicho kwenye mazoezi ya kujiandaa na michuano hiyo ya Super Cup ni Babu Ally wa Kagera Sugar, Zahora Pazi (Mbeya City), Haruna Chanongo aliyecheza Mtibwa Sugar msimu uliopita, Emmanuel Kichiba na mshambuliaji mmoja wa Ghana.

Issue ya John Bocco na Okwi Kusaini Simba...Hans Poppe Aanika Mambo Yote Hadharani..!!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho nchini Simba SC, Zakaria Hans poppe amekanusha timu yake kuwasajili wachezaji Aishi Manula, John Bocco, Shomari Kapombe pamoja na Emmanuel Okwi na kusema taarifa hizo ni za uongo.

Hans poppe amebainisha hayo baada ya kuenea kwa tetesi kuwa timu hiyo imeshawasajili wachezaji hao baada ya msimu 2016/2017 kuisha hivi karibuni.

“Ni uongo kusema kuwa sisi tumeshaingia mkataba na mchezaji yoyote maana hadi sasa mikataba ya wachezaji bado haijamalizika, tukisajili mtu sasa itakuja kuwa kama suala la Kessy ambalo tuliwaambia Yanga lakini wakajifanya wajuaji, matokeo yake wametema milioni 50 tena kwa huruma yetu” alisema Poppe.

Pamoja na hayo, Hans poppe amesema kwa sasa hawezi kusema chochote kama wameanza mazungumzo na wachezaji hao wanaotajwa zaidi.

Rasmi...Mbowe Avunja Ukimya..Aanika Mahusiano Yake Hadharani na Wema Sepetu..!!!

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema clip ya sauti inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye na Wema Sepetu si ya kwake na hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mrembo huyo.

Kiongozi huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, kuwa yeye anachukulia clip hiyo kama taarifa za kawaida za majitaka ambazo zinasambazwa wala hazina ukweli wowote.

“Kitu ambacho naweza kukisema kwa sasa hizo taarifa sio za kweli na timu yangu ya mtandao inajaribu kufuatilia kujua, na ukweli utajulikana muda sio mrefu,” amesema Mbowe.

Alipoulizwa kama anawajua waliofanya kitendo hicho, Mbowe amesema akizungumza sasa atakuwa anaharibu uchunguzi wao.

Pia ameongeza kuwa hajawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Wema Sepetu kama inavyosikika kwenye clip hiyo ya sauti.

“Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana kwamba ni mwanachama wetu aliyejiunga na chama chetu, na wapo wanawake, wasichana, wapo watu wengi kwenye chama chetu ni kwamba kuna mahusiano si kweli ni taarifa tu za upotoshaji,” ameeleza Mbowe.

Steven Nyerere - Nimeanzisha Kundi Langu la Wenye Akili..Siwezi Kukaa na Wasanii Masikini Amabo Hata Milioni 3 Hawana..!!

$
0
0

Baada ya kutoonekana katika maandamano ya kupinga filamu za nje, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameamua kuweka wazi juu ya  kundi jipya alilolianzisha.

Steve ameeleza kuwa “niliamua kujitenga na baadhi ya wasanii wenzangu wa Bongo Muvi kwa sababu siwezi kukaa nao ndiyo maana nimeamua kuanzisha kundi langu la watu wenye akili wanaoweza kufanya mambo ya maana na kuleta mafanikio”.

Mchekeshaji huyo alizungumza maneno hayo na gazeti la Wikienda, na kusisitiza kuwa angeendelea kujumuika na waigizaji hao basi angekuwa mjinga kama wao.

“Kwanza mimi ndiye maarufu kuliko wao maana nina kipaji cha kuzaliwa, lakini wao wamejifunza, maisha yangu ni mazuri tofauti na wao ambao hata milioni tatu kwao kupata ni shida,” amesema Steve.

Rais Magufuli Aishukuru Serekali ya Kuwait kwa Kuchangia Bilioni 110 za Ujenzi wa Barabara..!!!

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameishukuru serikali ya Kuwait kwa kutoa shilingi bilioni 110 kujenga barabara ya Chaya – Nyahua mkoani Tabora yenye urefu wa Kilometa 85 ambayo itaunganisha mawasiliano ya barabara kati ya mkoa wa Singida na Tabora.

Rais Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea Ikulu jijini Dar es salaam



Upande wa Alikiba hawataki kuwa karibu na mimi – Dully Sykes

$
0
0
Msanii wa muziki, Prince Dully Sykes amedai kuwa upande wa Alikiba hawataki kuwa karibu naye ila upande wa Diamond wanamuonyesha upendo ndiyo maana yupo karibu nao.

 

Dully amesema kuwa “Upande wa Alikiba hawataki kuwa karibu na mimi ila upande wa Diamond wapo karibu na mimi, sababu hao wapo karibu na mimi na wao wananionyesha upendo ndio maana nipo karibu nao na sina tatizo na AliKiba wala Diamond,”

Dully alisema hayo wakati wa mahojiano na kipindi cha 180 Power cha Sibuka Fm, alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho Byno, kuwa baada ya kufanya kazi na Harmonize, watu wanahisi unaupendeleo na upande huo na umeuacha upande mwingine ambao ni Alikiba.

Hits maker huyo wa ‘Yono’ pia alifunguka juu ugomvi wa Diamond na Alikiba na kusema kuwa yeye hawezi kujiingiza katika hilo, yeye ni mtu mzima na ugomvi wao ni wakitoto.

Porojo za Dodoma Haziniumizi Kichwa – Halima Mdee

$
0
0
Baada ya taarifa kuenea kwenye vyombo vya habari kuwa Mh.Halima Mdee na Ester Bulaya, kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge hadi 2018/19, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ametoa kauli yake ya kwanza.



Mdee ambaye yupo mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Moshi, Philemon Ndesamburo, amedai haumizwi kichwa na tukio lililotekea bungeni.

Tunamsindikiza jemedari wa MAGEUZI MHE PHILEMON NDESAMBURO kwenye nyumba ya milele!Porojo za DOM haziniumizi kichwa!

alitweet Mdee.



Halima Mdee na Bulaya wanaadhibiwa kwa kosa la kudharau mamlaka ya Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MFANO HALISI: Road License inavyoikosesha Serikali Mapato

$
0
0
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

By Ntate Mogolo

Ndugai: Ningeamua Ningeamuru Bulaya na Halima Wakamatwe Huko Moshi Waletwe Hapa Kwa Usafiri Wowote

$
0
0
Amaeyasema hayo leo Bungeni wakati akichangia maazimio ya kamati(Nasema akichangia maana leo aligeuka mchangiaji kwa kujibu hoja za walioonekana kuwatetea akina Halima dhidi ya adhabu ile kubwa)!

Akasema angeamua angeamuru wakamatwe huko Moshi kwa pingu na wafikishwe mbele ya kamati kwa usafiri wowote!

Huyu Spika amenishangaza!

Mbowe Aikana Sauti Inayosambaa Mitandaoni Ikidai Wema Sepetu ni Mpenzi Wake

$
0
0
Habari inayotikisa mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile Audio  (voice note/Sauti) inayodaiwa kuwa ya Muigazaji Wema Sepetu na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe inayoashiria kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.

Leo kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM  Mbowe ameielezea sauti hiyo akisema taarifa hizo anazichukulia kama majitaka:

Mimi nalichukulia kama taarifa za kawaida za maji taka zinasambazwa. Taarifa ambazo zinatengenezwa hazina ukweli wowote ndio kitu ninachoweza kusema kwa sababu siyo za kweli.

“Timu yangu ya mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo limetengeneza kutuchafua kwani tupo kwenye msiba, kwenye maombolezo na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu. 

"Sauti siyo ya kwangu. Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana ni mwanachama wetu na kwamba, kama kuna mahusiano sio kweli, ni taarifa za upotoshaji tu."
Viewing all 104694 articles
Browse latest View live




Latest Images