Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mnyika awaponza askari wa Bunge......Ndugai Kaamua Kuwahamisha

$
0
0
Askari walioagizwa kumtoa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika bungeni Ijumaa iliyopita, wamepangiwa vituo vingine vya kazi kwa kuchelewa kutekeleza agizo la Spika.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema aliwashangaa askari hao kwa jinsi walivyokuwa wanambeleza mbunge huyo wa Kibamba kutoka nje.

"Askari hawa wataendelea kuhamishwa mpaka pale tutakapowapata wanaofaa," amesema Ndugai.

Mnyika alitolewa bungeni Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa wabunge kusema ‘Mnyika mwizi’ akimhusisha na wizi wa madini.

Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua dhidi ya mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika alisema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi.

Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayawezi kwenda hivyo.

Baada ya majibizano kati yao Spika aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge.

Waziri Lukuvi Kutunukiwa Tuzo ya Uwajibikaji na Utendaji Bora

$
0
0
Viongozi wa Dini wanajiandaa kumpa tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kwa utendaji mzuri uliojaa ubunifu na uwajibikaji.

Hayo yameelezwa katika mahojiano maalum jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Dini zote Tanzania, Askofu William Mwamalanga.

Askofu Mwamalanga amesema kuwa Waziri Lukuvi amekuwa kiongozi imara katika kufuatilia masuala yanayohusu ardhi ikiwemo utatuzi wa migogoro ambayo imedumu kwa muda mrefu.

“Lukuvi ameing’arisha Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli, hakika amevaa viatu vya Magufuli, hivyo tumeamua kumpa tuzo maalum kwa ajili utendaji wake”, alisema Askofu Mwamalanga.

Ameeleza kuwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanya jambo zuri kwa kutoa elimu ya ardhi kiasi kwamba karibu kila mtu amefahamu matumizi ya ardhi na umuhimu wake.

Askofu Mwamalanga amesema kuwa ardhi imefanywa kuwa lulu na kufanya sura mpya ya ardhi kuonekana ambapo takriban asilimia 85 ya Watanzania wameiona kuwa ni mali.

Mhe. Lukuvi amewapa nafasi ya kwanza wananchi kuliko Sheria jambo ambalo limewafanya Watanzania kujisikia kuwa wanathaminiwa na Serikali yao, aliongeza Askofu Mwamalanga.

Yanga Yawarudisha Wakenya Kwao.....

$
0
0
Yanga imetinga nusu fainali ya Sports Pesa Super Cup kwa mikwaju ya penalti.

Yanga imeing'oa Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila bao.

Kipa wa Yanga, Deo Munishi maarufu kama Dida alichangia kung'olewa kwa Tusker baada ya kupangua moja ya mikwaju ya Wakenya hao.

Sasa Yanga itakutana na Wakenya wengine, safari hii ni AFC Leopards ambao wameing'oa Singida United kwa mikwaju ya penalti pia.

Aweka Sumu Ukeni ili Kumuua Mumewe Akizima Chumvini....

$
0
0
Mwanamke mmoja wa nchini Brazili amefikishwa mahakamani kufuatia jaribio lake la kumuua mumewe kwa kuweka sumu kwenye sehemu zake za siri na kisha kumtaka mumewe azamie kuziramba sehemu zake za siri kabla hawajafanya tendo la ndoa. Mume wa mwanamke mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa mji wa Sao Jose do Rio Preto nchini Brazili aliamua kumfikisha mahakamani mkewe baada ya kunusurika jaribio la kuuliwa kwa sumu iliyowekwa kwenye sehemu za siri za mkewe.
Soma Zaidi Chini:

Taarifa zilisema kuwa mwanamke huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni, alipakaza sumu kwenye sehemu zake za siri na kisha kumhadaa mumewe wafanye mapenzi.

Mwanamke huyo ili kukamilisha azma yake ya kumuua mumewe alimtaka mumewe azirambe rambe sehemu zake za siri kabla hawajaanza tendo la ndoa.

Lakini mumewe akiwa kwenye jaribio la kukamilisha ombi hilo la mkewe alishtuka kusikia harufu ya ajabu ikitokea kwenye sehemu za siri za mkewe.

Alikatisha zoezi hilo na kumchukua mkewe na kumpeleka hospitali ambapo madaktari walimfanyia vipimo na kugundua kuwa mkewe alijipakaza vitu vyenye sumu kali kwenye sehemu zake za siri.

Mume wa mwanamke huyo amemfungulia kesi mkewe mahakamani kufuatia jaribio lake hilo la kumuua.

Lowassa Afunguka Mazito Kwenye Msiba wa Ndesamburo..Agusia Sakata la Polisi Kuinyanyasa Chadema..!!!

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA, Mh. Edward Lowassa amempongeza muasisi wa Chama hicho Mzee Mtei kwa kukutana na Mzee Ndesamburo na kutengeneza chama imara, huku akitoa ahadi ya chama hicho kuongoza mwaka 2020.

Akizungumzaa kwenye ibada ya kuuaga mwili wa Mzee Ndesamburo, Mh. Lowassa amesema kwamba  waasisi hao wameacha  chama chenye nguvu sana na ambacho kinafanya nzuri na kwa weledi.

"Nakupongeza Mzee Mtei kwa kukutana na Ndsamburo. Nakupongeza wewe zaidi kwa sababu umetuachia chama chenye nguvu. Pale nilikuwa namnong'oneza Mzee Mtei kwamba mwaka 2020 tutachukua ushindi,pamoja na jitihada zao mungu atatuongoza na tutaweza" - Mh. Edward Lowassa.

Akizungumzia kuhusu suala la polisi kuzuia eneo la uwanja wa Mashujaa kutumika kumuaga Mzee Ndesamburo, Mh Lowassa amefunguka kuwafariji wafiwa, wanachama na wananchi kwa kuwataka wasamehe yaliyotokea.

"Wamewakatalia uwanja wa Mashujaa lakini hapa kwenye uwanja wa majengo ndo pamega zaidi.Tuwasamehe bure au tuwaachie maneno ya biblia kwamba , Waacheni wafu wazike wafu wao maana hupimi watu kwa uwanja kujaa bali kwa mioyo yao na waliopo hapa ni wale waliompenda na kumuheshimu Mzee wetu" - Mh. Lowassa alifunguka. 

Mbunge wa CCM Ataka Bunge Lipitishe Sheria ya Kuwapima Wabunge Matumizi ya Madawa ya Kulevya..!!!

$
0
0

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekea kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara.

Keissy amesema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge. 

"Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale" - alisema Keissy.

Aidha, Mbunge huyo aliendelea kwa kusema kuwa "Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara hatutaki mchezo mchezo namna hii ya kutukana. Spika kwanza anawazidi umri pamoja na cheo" aliongezea Keissy.

Mchungaji Aliyekuwa Anawalisha Waumini Wake Nyoka na Panya Akimbilia Kuombewa kwa TB Joshua..!!!

$
0
0

Mchungaji wa Afrika Kusini ambaye miaka miwili iliyopita alivuma kwa kitendo chake cha kuwalisha waumini wake nyoka, panya , na nywele amejitokeza katika kanisa la mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua.

 Mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mnguni amekaririwa na gazeti la Afrika Kusini la Citizen akidai kuwa moyo wake ulibadilika hasa baada ya kukamatwa na kuachiwa na jeshi la polisi, na kwamba alijisikia kumrudia Mungu wa kweli.

“Nilianza kuangalia Emmanuel TV, kumsikiliza TB Joshua, nikabaini kuwa nilikuwa nafanya kitu ambacho sio cha kiroho. Nilibaini kuwa lile lilikuwa shambulizi dhidi yangu. Nimekuja kwa TB Joshua ili niokolewe,” alisema.

Mnguni alifunguliwa mashtaka na jamii kwa kosa la kufanya ukatili dhidi ya wanyama. Hata hivyo, mashtaka yote yalifutwa baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Siku Chache Baada ya Kifo cha Ivan..Zari Kulipwa Mabilioni ya Pesa na Kampuni za Bima..!!!

$
0
0

Wakati wanafamilia wakiwa bado katika majonzi kufuatia kifo cha mpendwa wao, Ivan Ssemwanga ‘The Don’ aliyezikwa wiki iliyopita huko Nakalilo nchini Uganda, imebainika kuwa aliyekuwa mkewe, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ atalipwa mabilioni ya fedha kutokana na bima na mikataba mingine mingi aliyoingia jamaa huyo enzi za uhai wake.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya nchini Uganda, Zari ndiye mtu pekee atakayesimamia mali zote zilizoachwa na Ivan, hasa kutokana na ukweli kuwa ana watoto wake watatu wa kiume na ndiye aliyeanza kutafuta mali wakiwa wote mwanzoni mwa miaka ya 2,000.

KULIPWA NA KAMPUNI YA BIMA

Kwa mujibu wa habari hizo, Zari ambaye alishiriki mwanzo mwisho msiba wa mumewe huyo wa zamani, atapata fedha ambazo Ivan alilipia bima yake ya maisha ambazo hata hivyo, mama huyo wa watoto watano hakuweza kutaja jina la kampuni hiyo ya bima wala kiasi cha fedha atakazolipwa zaidi ya kusema tu ni mabilioni.

“Ivan ameacha mali za kutosha na of course pia alikuwa na bima ya maisha ambayo alikuwa akilipa fedha kila mwezi, kwa hiyo kwa kuwa amefariki dunia, basi nina uhakika wa kupewa fedha hizo ambazo ni nyingi, sina uhakika ni ngapi kwa sababu bado sijapiga hesabu, lakini ni a lot of money,” alikaririwa mwanamama huyo.

BIMA YA MAISHA NI NINI

Bima ni mfumo wa kulipa kiasi cha fedha katika kampuni ya bima ili kujiinua au kujilinda na madhara ya tukio lolote baya litakalotokea katika kitu ulichokatia bima. Kampuni ya bima inachukua jukumu la kurudisha hali iliyochafuka kuwa safi katika mazingira yoyote ya mtu aliyekata bima kwao.

Baadhi ya kampuni zinazotoa bima hiyo ya maisha, mteja huweza kuwa na nafasi ya kukopa baada ya mwaka wa tatu wa ulipiaji wa bima hiyo na bima hukomaa baada ya muda uliolengwa kufikia (mfano endapo mteja alikata bima ya maisha ya miaka 15, tuseme shilingi 150,000 kwa kila mwezi) baada ya muda huo kufika atalipwa kiasi chake chote cha fedha alizoweka, pamoja na faida isiyopungua asilimia tano kutegemea na kampuni.

Endapo mteja atafariki dunia kabla ya muda huo kufika na bila kupatwa na madhara mengine yaliyo katika ulipiaji wa bima, mrithi wake ndiye atapaswa kupewa fedha hizo pamoja na faida.

AMEJIPANGAJE NA MAISHA YAKE?

Zari alisema kuwa, anaamini atapambana kiasi cha kutosha kuweza kuwapa watoto wao watatu vitu muhimu katika maisha yao, ikiwemo elimu, afya, chakula na malazi.

“Kuna vitu vya msingi ambavyo watoto ni lazima wavipate na watavipata kwa sababu baba yao ameacha urithi wa kutosha tu. Mimi siyo aina ya mwanamke ambaye baada ya hili jambo kutokea labda nitahitaji magari au nini sijui, nitahakikisha wanapata elimu nzuri kama baba yao alivyopania kuwapa.

“Uzuri ni kwamba baba yao alishawawekea misingi ya maisha yao kwa hiyo halitakuwa jambo geni kwangu wala kwao. Ninamuomba Mungu tu abariki kila jambo liende vizuri na kwa kweli tunaomba sana.

MALI ZINGINE ZITAKAZOBAKI MIKONONI MWA ZARI

Kwa mujibu wa Zari, aliyenukuliwa na mitandao ya nyumbani kwao Uganda, yeye ndiye atakuwa msimamizi mkuu wa vyuo na shule zote zilizoko Afrika Kusini, ambazo zilikuwa zikimilikiwa na Ivan.

“Kuna manenomaneno mengi yanasemwa na watu, akiwemo baba mdogo wa Ivan, wanasema mimi ninagombea mali, siyo kweli, kwa nini nigombee, wasichojua ni kwamba mimi ndiye nilianza kutafuta mali nikiwa na Ivan hadi tukapata na hawajui kuwa hata baada ya kutengana, bado alikuwa kila siku akitaka nirudi ili nisimamie mali maana aliona zinaanza kupotea.

“Kuna nyumba moja ambayo tulijenga ikiwa na majina yetu mimi na yeye na nyingine ilikuwa na jina lake kila kitu. Hivi vitu vyote vitakuwa chini ya usimamizi wangu kwa ajili ya watoto hawa ambao wanahitaji kupata mambo yote muhimu,” alisema Zari.

ANA MATATIZO NA FAMILIA YA IVAN?

“Sijawahi kuwa na wala hakutakuwa na matatizo kati yangu na familia ya Ivan, kule kuna wajomba, shangazi, dada na kaka za watoto wake, ninahitaji sana kuwa nao karibu na nitahakikisha kila jambo ninawashirikisha.

“Ikitokea nikashindwa kulipa ada ya watoto nitawaambia jamani nisaidieni nimeshindwa. Lakini siyo hivyo tu, hawa watoto wanahitaji mtu wa kuwasimamia katika baadhi ya mambo, kwa mfano watahitaji kuoa, sasa lazima baba zao wakubwa na wadogo wajue na washiriki.

“Huenda huko mbele wanaweza kuwa watu wa kunywa pombe kupita kiasi, nitawahitaji ndugu wa baba yao ili aweze kuwakemea, so hawa ni watu muhimu sana katika maisha yangu na watoto wa Ivan na sitarajii kugombana nao,” alisema Zari.

Credit - Global Publisher

Kimenukaa..Gwajima Amkaanga Mrisho Gambo Kwenye Msiba wa Ndesamburo..Amchana Live Juu ya Tabia Yake ya Kuleta Siasa Misibani...!!!!

$
0
0

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa msibani Moshi amemshukia Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuleta siasa msibani huko Arusha ambapo alimzuia mbunge wa jimbo hilo Godbless Lema kutoongea.

Aidha Gwajima amesema jambo lililofanywa na viongozi wa serikali kukataza Uwanja wa Mashujaa kutumika kuaga mwili wa Marehemu Ndesamburo siyo jambo la busara hata kidogo huku nakimlaumu mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kile alichokisema ni tetesi alizosikia kuwa alitoa maelekezo uwanja huo usitumike na badala yake vitumike Viwanja vya Majengo.

Rose Muhando Akamatwa na Polisi Singida..Chanzo Ni..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 6/6/2017..!!!

ACT-Wazalendo Kwafukuta, Wamtaka Anna Mghirwa Kukataa Uteuzi..!!!

$
0
0

Hali ya sintofahamu imekikumba chama cha ACT-Wazalendo baada ya Mwenyekiti wa chama hicho kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Hayo yametokea mara baada ya Afisa Habari wa chama hicho, Abbdallah Khamis kushindwa kuelezea undani wa tukio hilo huku ikisemekana baadhi ya wanachama kutoa shinikizo la kukataa uteuzi huo alioteuliwa na Rais.

“Uteuzi huo hata sisi tumeusikia kwenye vyombo vya habari, hivyo chama kitakaa kikao na Mwenyekiti wetu ili tuweze kuzungumza nae, kani kwasasa siwezi kuzungumzia chochote kwasababu muhusika yupo safarini, hata Zitto naye kasikia kwenye vyombo vya habari hivyo baada ya kikao chama kitatoa tamko,”amesema

Madai Ya Kufulia, Kuuza Ghorofa Na Kukimbia Jiji… Vicky Kamata Abanwa, Awaka!

$
0
0

Nini? Victoria Paschal Kamata ‘Vicky Kamata’ ni Mbunge wa Viti Maalum akiwakilisha Mkoa wa Geita kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katikati ya wiki iliyopita, aligeuka mbogo na ‘kutoa povu ambalo siyo la nchi hii’ kufuatia swali aliloulizwa na Wikienda juu ya madai ya kufulia, kuuza baadhi ya mali zake ikiwemo lile ghorofa lake kisha kutimkia mkoani Geita kutengeneza makazi mapya.

Habari kutoka kwa chanzo ambacho ni mbunge mmoja ambaye aliwahi kuwa rafiki wa karibu na Vicky, zilieleza kuwa, kwa sasa mwanasiasa huyo ameamua kuuza baadhi ya vitu vyake ikiwemo magari na kujikita kwenye kilimo.

Siku za nyuma, mwandishi wetu aliwahi kuwasiliana na Vicky ambaye alimjuza kuwa yupo mkoani Morogoro ambako anasimamia kilimo cha mazao ya tikiti-maji na kumtania mwandishi amtafutie wateja, jambo ambalo liliishia kwenye vicheko kwani yalikuwa ni mazungumzo ya kawaida.

Kama aya ya kwanza inavyojieleza vyema, baada ya madai ya ‘kulikimbia jiji’, mwandishi alimtafuta tena Vicky na kumtaka afafanue kwa kina juu ya manenomaneno hayo ili kuondoa ukakasi kwani nyuma yake kuna wadau na wapenzi wengi wa kazi zake kama mbunge, msanii na Mkurugenzi wa Taasisi ya Victoria Foundation.

“Unajua wewe (akilitaja jina la mwandishi), mimi na wewe tunafahamiana, tena ni mdogo wangu, sasa mimi nataka nikuulize swali dogo sana, ulipoambiwa maneno hayo, kabla hata ya kunipigia simu na kuniuliza ulipima na kuona kama yanafanana na mimi kweli unayenijua? “Sikutarajia kwa kweli ninavyokuamini kama ungethubutu kuniuliza jambo la kama hilo.

“Hivi unatarajia mimi niolewe na kiongozi mkubwa mwenye wadhifa na maisha yake mazuri (aliyekuwa Katibu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk  Servacius Likwelile) halafu nimhamishe aje nimuoe na kuishi naye nyumbani kwangu?

“Sawa, inaweza kutokea lakini kama sijafanya hivyo? Mambo mengine yanatia hasira sana,” aliwaka Vicky.

Huku akitweta kwa hasira, Vicky aliongeza: “Sikiliza mdogo wangu, kuna watu wanaomba kila kukicha niishiwe na kufilisika, okey, kwani wanaoishiwa si ni binadamu kama mimi? Nenda pale Sinza ukaone Victoria Foundation inavyozidi kufanya kazi.

“Nataka niwaambie hivi, wanaoombea niuze kila kitu, watauza wao na hatimaye kujiuza na wao na Vicky ataendelea kudunda kwa kumtegemea Mungu,” alisema Vicky.

Ubuyu wa Moto Moto..Idris Sultan Afilisika Milioni 500 Alizoshinda Big Brother..Ashindwa Kulipia Kodi ya Ghorofa Alilokuwa Anaishi..!!!

$
0
0

Wapenda ubuyu wanakuambia hakuna kinachodumu milele duniani! Ndiyo maneno unayoweza kusema kutokana na maisha ya Mshindi wa Big Brother Africa (BBA) mwaka 2014, Idris Sultan ambayo anaishi kwa sasa.

Kwa mujibu wa watoa ubuyu, mai­sha ya jamaa huyo ni tofauti kabisa na matarajio ya wengi kutokana na mshiko aliovuta BBA wa zaidi shilingi milioni 500 za Kibongo.

NDIYO CHOKA MBAYA?

Inasemekana kuwa, ishu hiyo ndiyo ilizua maswali kwa watu wake wa karibu wakihoji ndiyo jamaa amekuwa choka mbaya? Vyanzo makini vilil­iambia Wikienda kuwa, kwa sasa Idris anaonekana amechoka mbaya kwani anadaiwa kuhama kwenye jumba la ghorofa alilokuwa akiishi Mbezi-Beach jijini Dar na kuhamia kwenye chumba kimoja maeneo ya Mbezi-Chini, Dar.

“Kiukweli maisha anayoishi Idris yanashangaza sana na inaonekana ameshamaliza zile shilingi milioni mia tano alizoshinda BBA.“

Inaonekana zimekata maana siyo wa kwenda kupanga chumba kimoja waka­ti mwanzoni kabisa baada ya kushinda alikuwa anaishi kwenye ghorofa na maisha yake yalikuwa ya mwendokasi (kufuru ya fedha) kwa kuwa mkwanja ulikuwepo.

“Kwa sasa anaishi maisha ya kawaida kama vile hajawahi kupata fedha nyingi kiasi kile. “Sasa sijui alizimalizia wapi fedha zote zile au aliendekeza sana bata maana vijana wengi wa Dar wanapenda kujiachia wanapopata fedha huku wakiendekeza tabia ya kubadilisha totozi kila kukicha,” kilisema chanzo chetu kwa sharti la kutotajwa gazetini.

OFM WAMFUNGIA KAZI

Baada ya kupata ubuyu huo, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilicho chini ya Global Publishers kilimfungia kazi Idris am­bapo walifika Mbezi-Chini anakodaiwa kuishi kwenye chumba kimoja.

MAJIRANI WAFUNGUKA

Walipofika anakoishi, OFM walijifanya wageni wake, lakini wapangaji wenzake walidai kuwa alitoka. Hata hivyo, jibu hilo liliwathibitishia OFM kuwa Idris anaishi pale ambapo walipata fursa ya kuoneshwa mlango cha chumba chake.Mazingira ambayo OFM ilishuhudia ni tofauti na maisha aliyokuwa akiishi awali ambapo ilibidi kufotoa picha kadhaa.“Ni kweli hapa ndipo anapoishi Idris kwa upande wa mbele wa nyumba hii lakini kwa sasa hayupo, naona ameenda kazini (kwa sasa ni Mtangaz­aji wa Choice FM na ni msanii wa vichekesho,” alisema jirani mmoja aliyeomba hifadhi ya jina ili asije akaonekana ‘mnoko’ na kutibua ujirani mwema na staa huyo na kuongeza:

“Lakini ni mtu mzuri na tunafurahi kuishi na staa.”

IDRIS ASAKWA

Baada ya kumkosa nyumbani hapo, OFM walimsaka Idris kwa njia ya simu lakini iliita bila kupokelewa.

Hata hivyo, baadaye ali­tuma ujumbe mfupi kwamba atumiwe meseji ambapo mazungumzo yalikuwa hivi;

OFM: Kuna habari kwamba kwa sasa ume­filisika na unaishi kwenye chumba kimoja, tofauti na mwanzo ulivyokuwa unaishi kwenye ghorofa la ukweli, hii ishu ikoje?

Idris: Haahaaa..! Hivi nina endorsements (mi­kataba ya madili) ngapi? Ukipiga hesabu ukakadiria utakuwa unajua nina thamani gani. Ila unaruhusiwa kuhisi vingine.

OFM: Sawa, lakini sisi ni vijumbe tu. Mashabiki wako wanataka uweke wazi kuhusu fedha ulizopata ziliishia wapi ili kumaliza maneno yanayozungumzwa?

Idris: Huwezi kuzuia watu kuzungumza ndugu yangu. Nikianza kuwaza mangapi ya kuyaweka wazi, nitajikuta ninajieleza kutwa kucha.

NENO LA MHARIRI

Sisi kazi yetu ni kumfikishia ubuyu mhusika na ndicho tulichokifanya lakini ni vizuri Idris akaweka mambo hayo wazi kwa sababu shilingi milioni 500 kukata kwenye mazin­gira kama hayo kunazua maswali mengi.

Isalmic State Yakiri Kuhusika na Shambulizi la London Uingereza,,!!!

$
0
0

Kundi la wanamamgambo wa Islamic State wamekiri kuhusika katika shambulio lililotokea jijini London nchini Uingereza na kuuwa watu saba huku wengine 48 wakijeruhiwa na kupelekwa hospitali.

Aidha, katika shambulio hilo Polisi nchini humo imesema kuwa imewakamata watuhumiwa 12 ambao wanadaiwa kuhusika katika shambulio hilo la kigaidi  ambalo ni baya kutokea kwa nchi ya Uingereza.

Hata hivyo, ulinzi umeimarishwa na msako mkali dhidi ya wahusika unaendelea jiji humo huku bado kukiwa na hofu kubwa ya mashambulizi mengine kutoka kwa magaidi hao jijini London.

Masikini Johari wa Bongo Movies...Apata Piga la Maisha

$
0
0

Pole! Staa wa kitambo wa sinema za Kibongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ amepata pigo ‘hevi’ baada ya kufiwa na shangazi yake aliyemlea tangu akiwa mtoto, kumsomesha na kumfundisha maisha hivyo kuondoka kwake kumemuachia maumivu na pigo kubwa.

Johari, akiwa nyumbani kwao mkoani Shinyanga kuhudhuria msiba huo aliliambia Wikienda kwa njia ya simu kuwa, aliumia mno alipopata taarifa za kifo cha shangazi yake huyo aliyekuwa nguzo muhimu maishani mwake.

“Nimekuja Shinyanga kumzika shangazi yangu, tumeshamzika, lakini kwa kweli ameniacha mpweke sana maana ndiye aliyenilea, kunisomesha na kunifundisha maisha, kiukweli ni pigo kwangu,” alisema Johari.

Mume Ashtukia Mke Wake Unaliwa na Bosi Wake...Hichi Ndicho Alichoamua Kufanya

$
0
0
Huko nchini Kenya jamaa mmoja aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi wake ambaye ni mke wa mtu ameadhibiwa kwa style ya aina yake. Inaelezwa kuwa mwanamke huyo aliyekuwa akitembea na bosi wake alishtukiwa na mumewe na kuonywa lakini hakusikia. Kilichofuata ni mumewe kuvizia gari la bosi huyo na kuliandika kwa maandishi makubwa ya rangi nyeupe maneno yasemayo ‘Achana na mke wangu’.

Hii imekaaje?

Biashara ya Kuuza Pombe Yawa Kimeo...Duniani Kote Wafanyabiashara Walia

$
0
0
Idadi ya watu wanaojivinjari kwa mvinyo imepungua, kulingana na ripoti ya shirika mpya linalofuatilia unywaji wa pombe duniani.

Uuzaji wa pombe uliendelea kudidimia mwaka jana huku pombe ya Cider iliyoanza kupata maarufu sasa hainunuliwi kama hapo mwanzoni.

Soko la kimataifa la pombe lilipingua kwa asilimia 1.3 mwaka wa 2016, hali iliyosababishwa na kushuka kwa ununuzi wa pombe kwa asilimia 1.8.

Uuzaji wa pombe ya Cider ulishuka kwa asilimia 1.5 baada ya miaka kadhaa ya kufanya vizuri.

Kulingana Shirika la fedha duniani, kukua kwa uchumi wa nchi huwa inaachangia kuongezeka kwa unywaji wa pombe.

Uuzaji wa pombe nchini China ulishuka kwa asilimia 4.2, huku nchini Brazil na Urusi ukishuka kwa asilimia 5.3 na 7.8 mtawalia.

Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid, Je? Unapata Pesa Haikai? Umeachwa na Mpenzi, Mke au Mme Anakusumbua?

$
0
0


MIUJIZA YA SHEKH SHARIFU RASHID KUTOKA BAGAMOYO PWANI. (RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 72 TU) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU SHEKH SHARIFU RASHID KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI: 

SHEKH SHARIFU RASHID ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, anatumia kitabu cha quran dawa za asili dawa za kiarabu, na njiwa, Anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango kwa kina mama, ngiri maji na n.k, anakuvutia mali zilizo potea au kudhulumiwa, pia anatoa Pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali, Wenye matatizo ya uzazi, jini mahaba, mapepo ya kichawi, vifungo vya kimaisha, ndoto mbaya za usiku, uelewa mdogo wa ufahamu shuleni kwa watoto wote, pia anauwezo mkubwa wa kumaliza kazi zilizoachwa na wataalamu wengine ndani ya masaa 48 tu, Pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo. WASILIANA NAE KWA WhatsApp na SIMU NO: +255 718-668347 na +255 767-204308 , +255 685-224047 Email shekhsharifurashidi@gmail.com.

USHAURI: ni vyema kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate huduma kwa haraka.

Irene Paul wa Bongo Movies Abarikiwa Mtoto wa Kike Tarehe na Mwezi Baba yake Aliyofariki

$
0
0

Msanii Maarufu wa Bongo Movies Irene Paul  amejifungua mtoto wa kike Leo tarehe 6 mwezi
wa 6, 2017, Irene ameona ni maajabu kwasababu tarehe na mwezi ambao baba mzazi wake alifariki mwaka 1996 dio mtoto wake kazaliwa


Irene Ameandika haya:

From @irenepaul001 - Nilimuona Mungu akinipigania na kunipa heshima mbele ya ma taifa, NIMEBARIKIWA,NIMEBADILISHWA JINA☺eti siku babangu aliyoenda 6.6.1996 ndio siku wewe uliyokuja 6.6.2016,umekuja na mengi ila kubwa kuliko yote ni UPENDO KAMA JINA LAKO😆😆MUNGU UNAISHI,MUNGU LITUKUZWE JINA LAKO,BABA YANGU UTUKUFU HESHIMA NA MAMLAKA VINA WEWE,WEWE NI MKUU NA UKUU WAKO HAUNA MWISHO,NAKUSHUKURU YARABI....MIKONO YANGU NI MIDOGO KUBEBA ZAWADI HII ILA KWA HURUMA YAKO NISAIDIE BILA WEWE HATUWEZI/SIWEZI.....HAPPY BIRTHDAY BABY WENDO-ISABEL 6.6.1Y

Msanii Ebitoke Alia Hadharani Akimtaka Ben Paul Kimapenzi- VIDEO

$
0
0
Msanii wa vichekesho Anna Exavery a.k.a Ebitoke amefunguka na kusema yupo serious akimtaka Ben Paul awe mpenzi wake

Amedai ameanza kumzimia kitambo kabla hajawa maarufu ial hkuweza kuonana nae kwa kuwa alikuwa hafahamiki

Ameongezea ujumbe wake akimuonyesha mtoto wake umemuumiza sana kwakuwa alikuwa anasubiria jibu kutoka kwake,
Pia kuna siku alipost picha na kuandika ujumbe wake kisha Ben Paul akamjibu na kumuonyesha alama za love akadhani amemuelewa ila kuja kuona kwenye akaunt yake akashangaa kuona picha ya mtoto wake lakini mtoto wake anaweza kuishi nae akamlea,

Amedai ameongea akilia kwa sababu anaumia na skendo yake ya kupakwa mafuta haijali sababu anampenda mnoo Mtazame Akilia Kwa Machozi:
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images