Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Mwalimu Aliyekufa Kifo Tata, Mkewe Afichua Mazito...!!!

0
0

MARA: Wiki mbili baada ya aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Kukirango iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Julius Chacha Marinya (29) kukutwa akiwa amefariki dunia katikati ya barabara eneo la Baruti Musoma Mjini, mkewe Mukomkama Rwechungura amefunguka mazito juu ya kifo cha mumewe.

Mwanamke huyo ambaye ni mwalimu katika Shule ya Msingi Nyamisisi iliyopo pia katika Halmashauri ya Butiama, amesema kwamba, tangu aolewe na mumewe huyo mwaka 2013 na kufunga ndoa ya Kikristo kwenye Kanisa Katoliki walikuwa wakiishi vizuri katika ndoa yao hadi mwanzoni mwa mwaka huu mumewe alipoamua kuasi ndoa yao na kumchukua mke wa mtu na kumhamishia Musoma kutoka Kiabakari.

Mwalimu Mukomkama amefafanua kuwa, mara baada ya mumewe kufanya mapenzi na mwanamke huyo ambaye ni nesi (jina tunalihifadhi) wilayani Butiama, mumewe alibadilika ghafla na kuhama nyumbani kwake kwa kumhamisha mwanamke huyo kwenda Musoma kutoka Kiabakari licha ya kuendelea kufanyia kazi Butiama ambapo amesema mbaya zaidi ni kwamba kila siku za kazi mumewe akiwa amelala nyumbani kwake alikuwa akimfuata asubuhi nesi huyo kutoka Musoma kwenda kazini, baada ya kazi jioni alimrudisha tena Musoma.

“Nilipokuwa nikimsihi aache mambo ya mwanamke huyo ili tulinde ndoa yetu kama tulivyoapa siku ya kufunga ndoa, alikuwa akinijia juu na kunipiga na mabapa ya mapanga na kunitishia kuwa

 kama ningeendelea kumfuatilia angeniua,” alisema mwalimu huyo kwa huzuni huku akitokwa na machozi.

Aidha, alilieleza Uwazi kwamba, mapema mwezi uliopita alijaribu kumbembeleza mumewe akae nyumbani, atulie walee watoto wao lakini cha kushangaza alimpiga kwa mabapa ya panga kisha akavua pete ya ndoa na kuirusha chini akiashiria kuwa hamtambui tena kuwa ni mkewe na kwenda kwa huyo hawara yake.

“Chanzo cha kifo cha mume wangu naamini kuwa ni huyo mwanamke kwani bila yeye mume wangu asingetangatanga kwenda Musoma,” alisema kwa masikitiko Mukomkama na kuongeza kuwa;

“Hata kabla ya mume wangu hajakutwa na mauti aliondoka hapa nyumbani Mei 12 bila kuaga na hakurejea hadi mwili wake ulipokutwa barabarani Mei 14, mwaka huu saa 2.00 usiku,” alisema.

Mjane huyo aliongeza kuwa, kufuatia mgogoro huo wa ndoa aliondoka nyumbani kwake kwa siku kadhaa kwa hasira, lakini alirudi kwa ajili ya kulinda nyumba.

Mwili wa Mwalimu Chacha uliokotwa barabarani eneo la Baruti Musoma mjini Mei 14, saa 2.00 usiku pembeni kukiwa na pikipiki yake na baadaye alitambuliwa baada ya picha yake kurushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hatma ya Mhe Anna Mghwira Kuendelea na Uenyekiti wa ACT Wazalendo Kujulikana Leo..ACT Wakutana Kumjadili..!!!

0
0

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amekula kiapo Ikulu jijini hapa jana, Jumanne Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kitajadili utekelezaji wa majukumu yake mapya na ya uenyekiti wa chama hicho.

ACT imesema ilipokea taarifa ya uteuzi huo wakati Mghwira akiwa nje ya nchi hivyo baada ya kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho pamoja na yeye walifanya mazungumzo kuhusu uteuzi huo.

Mghwira aliteuliwa nafasi hiyo Juni 3, mwaka huu na Rais John Magufuli kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Saidi Meck Sadick aliyeamua kuachia ngazi ili vijana waendelee kufanya kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Jumanne na kuthibitishwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT, Ado Shaibu ni kuwa kufuatia uteuzi huo na uenyekiti na majukumu ya Mkuu wa Mkoa kamati ya uongozi wa chama itakutana leo kwa ajili ya mazungumzo.

Pamoja na mambo mengine chama kitajadili namna ambavyo Mghwira atatekeleza wajibu wake wa uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya.

 “Chama kinatoa wito kwa wanachama wake kuendelea na utulivu wakati wa vikao vyake vya chama vinachukua hatua stahiki kuhusu jambo hilo,”imesema taarifa hiyo.

Wabunge Walilia Bei ya Bia na Soda Zisipande Bei Kwenye Bajeti Kuu ya Serikali Itakayosomwa Kesho..!!!

0
0

WAKATI Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18 ikitarajiwa kuwasilishwa bungeni kesho, baadhi ya wabunge wametoa maoni yao wakisisitiza haja ya sekta ya maji na sekta ndogo ya umeme kupewa fedha nyingi.

Aidha, Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) amependekeza kupunguzwa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), na kuondolewa kwa kodi hiyo katika malighafi za kilimo zinazozalishwa nchini, na kusiwepo upandishaji wa ushuru wa vinywaji baridi na bia.

Wabunge wametoa maoni hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ikiwa katika mashauriano na serikali kwa siku ya tatu kuhusu hoja zilizojitokeza wakati wa kujadili bajeti za kisekta bungeni.

Kamati hiyo ya Bajeti chini ya Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (CCM), imekuwa katika majadiliano hayo na serikali ili kuboresha maeneo ambayo wabunge walitaka yafanyiwe kazi kabla ya Bajeti ya Serikali kusomwa kesho.

Kesho asubuhi, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango atawasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi nchini kabla ya jioni kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/18.

Akizungumza na gazeti hili, Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM) alisema suala la maji ni muhimu, hivyo serikali haina budi kuongeza fedha badala ya kupunguza, kama ilivyofanya bajeti ya wizara hiyo kutoka zaidi ya Sh bilioni 900 hadi zaidi ya Sh bilioni 600.

Aidha, Chumi alilitaja eneo jingine ambalo serikali inatakiwa kulitazama ni kuchangia katika ujenzi wa maboma ya zahanati, vituo vya afya na madarasa. “Serikali ilihamasisha wananchi wajenge maboma hayo na wao watamalizia, kazi hiyo imefanyika lakini serikali haijaweka fedha katika maeneo mengi, hii inaweza kukatisha tamaa wananchi siku nyingine watakapoombwa kuchangia,” alieleza Chumi.

Lakini, pia alitaka serikali itenge fedha kwa ajili ya Mfuko wa Mazingira hasa baada ya hali ya sasa ya mabadiliko ya tabianchi, ambayo yameathiri maeneo mengi nchini. “Fedha hizi zitasaidia katika kutoa ruzuku kwa maeneo yenye kufanya vizuri katika uhifdhi wa mazingira na hivyo kuchochea watu wengine kupanda miti kwa wingi na hivyo kurejesha hali ya kijani,” aliongeza Chumi.

Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM), alitaka kuwapo kwa msamaha wa kodi kwa watu wenye ulemavu hasa katika vifaa vyao. Mollel alisema mbali ya msamaha huo, pia serikali kuimarisha Mfuko wa Watu wenye Ulemavu hasa baada ya kuunda Baraza la Watu wenye Ulemavu nchini.

Aidha, Mollel alipendekeza kwa serikali kutenga asilimia mbili kutoka katika asilimia 10 iliyotengwa katika halmashauri kwa ajili ya mifuko ya vijana na wanawake, iende kusaidia watu wenye ulemavu.

Mbali ya hayo, alitaka wizara nyeti ikiwamo ya Nishati na Madini kuongezewa fedha hasa wakati huu, ambao amesema Rais John Magufuli anapambana kuhakikisha rasilimali za Taifa yakiwamo madini yanawanufaisha Watanzania badala ya wachache kunufaika.

Kwa upande wake, Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), alisema maji na nishati ya umeme ni muhimu na akapendekeza kuundwa kwa Mfuko wa Maji Vijijini. Ndassa alisema kama ilivyo kwa umeme ambako kuna Wakala wa Umeme Vijijini (REA), ni muhimu kuwa na Mfuko wa Maji Vijijini ambao utawezeshwa na tozo ya mafuta kupandishwa kutoka Sh 50 hadi 100.

“Fedha hizi zitakazopatikana ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 360 ziwekwe zisiguswe kwa kazi nyingine, zitumike kwa ajili ya Mfuko wa Maji Vijijini, maji ni muhimu pengine kuliko umeme,” alieleza Ndassa.

Alishauri serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri ya ukusanyaji wa kodi na kuwa na vyanzo vyake vya kuaminika vya mapato ili Taifa lijitegemee lenyewe. Mbunge wa Bukombe, Dotto Biteko (CCM) pia alikazia suala la maji, umeme, kilimo na ardhi, akisisitiza fedha nyingi zielekezwe katika miradi ya maji nchini kwani maji ni muhimu kwa matumizi ya binadamu na kilimo.

Biteko alisema kuwapo kwa maji ya kutosha yatawezesha kufanyika kwa kilimo cha umwagiliaji, hivyo kuzalisha malighafi nyingi kwa ajili ya Tanzania ya viwanda. Katika kilimo alipongeza serikali kwa kuondoa tozo zilizokuwa na kero kwa wananchi, kama ilivyofanya katika ardhi, hivyo kuwataka wananchi watumie fursa hiyo kujiongezea uzalishaji wao na kujiletea maendeleo.

Kuhusu umeme, alisema serikali imeahidi kuvipatia umeme vijiji vyote nchini mwaka huu, hivyo akataka Bajeti ya Serikali itenge fedha kuharakisha azma hiyo. Hoja ya umeme na maji pia ilitolewa na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), akisema maji ni kila kitu, ni vyema kuongeza fedha katika sekta hiyo na umeme.

Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM) pia alizungumzia suala la maji, akisema maenep mengi nchi yana tatizo kubwa la maji, hivyo akashauri fedha za bajeti ziongezwe ili kuhakikisha miradi mingi ya maji inaanzishwa au inakamilishwa kwa haraka.

Nkamia pia alitoa pendekezo la kuanzishwa kwa dirisha maalumu la serikali katika Bandari ya Dar es Salaam ili kurahisisha utoaji wa vifaa vya serikali bandarini. Kwa upande wake, Bashe alipendekeza katika bajeti ya kesho serikali ipunguze VAT hadi kufikia asilimia 16 kutoka 18 ya sasa na iondoe kodi hiyo katika bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.

Bashe pia alitaka VAT iondolewe katika malighafi za mazao yanayozalishwa nchini, na kusiwapo na ushuru wa bidhaa katika pembejeo za kilimo. “Kwa kufanya hivyo, uzalishaji utaongezeka, serikali itapata kodi nyingi (kodi ya makampuni, VAT na kodi ya ushuru wa forodha).

Hii pia itaongeza ajira na hivyo kusaidia kupata kodi ya PAYE,” alieleza Bashe. Akijibu swali bungeni juzi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alieleza kuwa serikali itawasilishwa katika bajeti yake mapendekezo ya kufuta misamaha ya kodi isiyo na tija.

Dk Kijaji alisema mpango wa serikali ni kuhakikisha misamaha ya kodi inashuka mwaka hadi mwaka na katika mwaka ujao wa fedha, serikali italeta mapendekezo ya marekebisho ndani ya bajeti itakayosomwa kesho.

Machi 29, mwaka huu, Dk Mpango alisoma mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa 2017/18. Kwa mujibu wa Dk Mpango, serikali katika bajeti hiyo inatarajia kuwa na ukomo wa Sh trilioni 31.6.

Katika fedha hizo, za maendeleo zimeongezeka kutoka Sh trilioni 11.8 katika mwaka 2016/17 hadi Sh trilioni 11.9 katika mwaka wa bajeti 2017/18. Ongezeko hilo ni kiasi sawa na asilimia 38 katika bajeti hiyo tarajiwa.

Credit -Habari Leo

Sababu 4 Zilizoifanya Qatar Kutengwa na Mataifa ya Kiarabu

0
0
Taharuki ya Qatar na majirani zake, inaendelea kuongezeka, licha ya wito wa mazungumzo kutolewa.
Safari za ndege zinazotoka Qatar kuelekea Saudi Arabia, Misri na Bahrain zimefutiliwa mbali kuanzia siku ya Jumanne.

Mataifa kadhaa tayari yamekomesha uhusiano wao na kidiplomasia na taifa hiolo lililoko katika rasi ya Arabia, huku yakililaumu kwa "kuunga mkono ugaidi". Doha inakatalia mbali shutma hizo.

Mwaandishi wa BBC wa idhaa ya Kiarabu Amir Rawash, anatathmini namna taharuki kati ya Qatar na majirani zake imefikia kiwango cha kutamausha.

Baraza la ushirikiano wa mataifa ya ghuba, yanasema kuwa Qatar iliunga mkono upinzani wakati wa vuguvugu lililotokea kwa mataifa ya kiarabu.

Doha, ilionekana kama muungaji mkono wa makundi ya kiislamu, ambayo ilitaka kupata umaarufu katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.

Kwa mfano, baada ya kuondolewa kwa Rais wa Misri Mohamed Morsi - kinara mkuu wa Muslim Brotherhood - ambaye alitimuliwa mamlakani mwaka 2013, Qatar iliwapa hifadhi wanachama wa kundi hilo ambalo limepigwa marufuku na utawala wa Misri.

Saudi Arabia na Milki za kiarabu UAE pia zilitaja Muslim Brotherhood kama kundi "la kigaidi".
Katika taarifa iliyochapishwa katika mtandao rasmi wa habari za utawala wa serikali ya Saudia, Qatar ililaumiwa kwa "kuzikubalia makundi kadhaa ya kigaidi na makundi yenye itikadi kali yenye nia ya kuyumbisha amani katika kanda ya mataifa ya kiarabu, kwa pamoja na makundi kama la Muslim Brotherhood, Daesh (Isis) na Al-Qaeda".

Hata hivyo, Wizara ya nchi za nje ya Qatari, ilisema kuwa hatua zilizochukuliwa na Riyadh, Abu Dhabi na Manama "hazikuridhisha na yanaegemea madai yasio na msimamo kabisa wala ukweli".
TTaaarifa hiyo aidha inasisitiza kuwa, Qatar inafaa "kujitolea " chini ya mkataba wa GCC na "kutekeleza majukumu yake ya kukabiliana na ugaidi na itikadi kali".

Mbinu ya Iran
Mzozo wa sasa ulianzishwa na taarifa iliyokataliwa iliyomnukuu Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, akikosoa "uadui" wa Marekani dhidi ya Iran.

Qatar ilisema kuwa wadukuzi wanatazamiwa kuchapisha maoni hayo katika shirika lake la habari la taifa.

Saudi Arabia, mpinazi mkuu wa taifa hilo la kiislamu, limekuwa likitatizwa kwa muda mrefu na umaarufu wa Iran katika kanda hiyo.

Mzozo nchini Libya
Libya imekuwa katika lindi la mzozo tangua kuangushwa kwa utawala wa Rais wa nchini Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Kiongozi mkuu wa jeshi ya Libya Khalifa Haftar, ambaye alipata uungwaji mkubwa kutoka Misri, Milki za kiarabu UAE na Qatar, aliilaumu Qatar kwa "kuunga mkono ugaidi".

Haftar anaongoza serikali iliyoko mashariki mwa Libya katika mji wa Tobruk. Ilihali Qatar inaunga mkono serikali pinzani iliyoko katika mji mkuu Tripoli.

Mzozo wa vyombo vya Habari
Mara tu taarifa tatanishi ilipotolewa ikimnukuu Emir wa Qatar mnamo Mei 23, vyombo vya Habari huko UAE, Saudi Arabia, Bahrain na Misri yalianzisha ukosoaji mkubwa dhidi ya familia inayotawala Qatar.

Mataifa hayo manne yaliamua kwa kauli moja kuzima mtandao wa habari wa Qatar.
Jumanne jioni Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuwa kushindwa kwa Qatar, itakuwa mwanzo wa kumalizika kwa makundi ya kigaidi duniani.

Mashambulizi London: Mshukiwa wa Tatu Atajwa

0
0
Mshambuliaji huyo wa tatu katika shambulio lililotokea mwishoni mwa juma eneo la London Bridge, Uingereza, ametajwa kama Youssef Zaghba mwenye asili ya asili ya Morocco na Italia.

Mzaliwa wa Pakistan Khuram Butt aliye na umri wa miaka 27, na Rachid Redouane mwenye umri wa 30 ambao wote wawili ni wa kutoka katika eneo la Barking, walikuwa miongoni mwa washambulizi wa tukio hilo.

Wakati huo huo, mhasiriwa mwingine ametajwa kama Kirsty Boden, ambaye ni muuguzi kutoka Australia, mwenye umri wa miaka 28, ambaye familia yake imesema kuwa alikuwa amekimbia akielekea katika daraja hilo kuwasaidia watu.

Watu saba waliuwawa na 48 kujeruhiwa katika shambulio hilo la Jumamosi usiku ambapo washambuliaji hao watatu walipigwa risasi na kuuliwa na polisi.

Zaghba, Butt na Redouane waliwagonga watu waliokuwa wanatembea kwa miguu katika daraja la London, wakitumia gari walilolikodisha majira ya saa tano na dakika 58 usiku, saa za Afrika Mashariki, kisha wakashuka na kuwadunga visu watu wengi katika eneo lililokuwa karibu na soko la Borough.

Maafisa waliokuwa wamejihami kwa silaha waliwauwa wote watatu dakika 8 baada ya kupokea wito wa dharura.

Katika matukio mengine:
Waziri muu Bi Theresa May, amesema kuwa anatarajia uchunguzi wa wataalamu, utazinduliwa na polisi pamoja na vyombo vya usalama kufuatia shambulizi hilo licha ya kuwepo malumbano kuhusu idadi ya polisi.

Idara tya Polisi wa katikati wa jiji la London, inasema kwamba mshukiwa mwenye umri wa miaka 27, alishikwa katika eneo la Barking siku ya Jumanne kuhusiana na uchunguzi.

Msako pia ulifanywa na polisi katika nyumba iliyo katika eneo la Ilford, mashariki mwa London, mwendo wa saa tisa unusu masaa ya Afrika Mashariki, lakini hakuna aliyeshikwa, polisi walisema.
Charles Phillip na Camilla Rosemary kutoka jamii ya kifalme jijini London watawatembelea manusura katika hospitali ya Royal London.

NHS England inasema watu 36 wangali wamelazwa hospitalini, 15 kati yao wakiwa katika hali mahututi.

Ukimya wa dakika moja kwa taifa zima ulifanyika ili kuwakumbuka waliouwawa
Washukiwa wote 12 walioshikwa siku ya Jumapili baada ya shambulio hilo wameachiwa huru bila kushtakiwa.

Kundi linalojiita Islamic State (IS), limesema kuwa "wapiganaji wake" walitekeleza shambulio hilo.
Duru kutoka kwa polisi nchini Italia zimethibitishia BBC kuwa Zaghba, ambaye alikuwa akiishi mashariki mwa London, amekuwa katika orodha ya uchunguzi wa wapelelezi, ambayo husambazwa kwa mataifa mengi likiwemo Uingereza.

Mnamo Machi mwaka 2016, afisa mmoja wa usalam nchini Italia, alimsimamisha Zaghba katika uwanja wa ndege wa Bologna na kumpata na baadhi ya vitu vinavyohusiana na IS kwenye simu yake ya mkononi na akazuiwa kuendelea na safari yake kuelekea mjini Istanbul.

Butt alishirikishwa katika filamu iliyofanywa na Channel 4 mwaka jana kuhusu waislamu wenye itikadi kali walio na uhusiano na mhubiri aliyefungwa Anjem Choudary iliyoitwa "The Jihadis Next Door".

Butt ambaye ameoa na ni baba ya watoto wawili, alipokea mafunzo kama msaidizi wa kutoka huduma kwa wateja London Underground kwa takriban miezi sita mwaka jana, anaonekana kwa filamu akibishana na polisi mitaani,baada ya kuonyesha bendera inayotumika na linalotajwa kama "Islamic State" katika bustani moja jijini London.

Watu wawili katika eneo la Barking, mashariki mwa London, pia walikuwa wameelezea wasiwasi wao kumhusu Butt, mwanahabari wa BBC wa masuala ya ndani ya uingereza, Dominic Casciani alisema.

Mtu mmoja alipiga simu katika kitengo cha kupambana na ugaidi mwaka wa 2015, na mwanamke mmoja alienda kwa polisi kwa kuhofia kwamba Butt alikuwa akiwafunza wanawe itikadi kali.

Naibu mkuu wa Polisi wa Metropolitan Mark Rowley alisema uchunguzi wa Butt ulianzia mwaka wa 2015, lakini "hakukuwa na habari ya kindani kuonyesha kuwa shambulizi hili lilikuwa linapangwa na uchunguzi ulipewa kipao mbele ilivyofaa"

Alipoulizwa ikiwa ulikuwa uamuzi mbaya, bwana Rowley alisema hakuona chochote cha kubainisha hayo.


Kuna takriban uchunguzi 500 ya visa vya ugaidi yanayohusu watu 3,000 wanaoshukiwa kuhusika.
Bwana Rowley alisema kuwa kazi ilikuwa inaendelea ili kuelewa mengi kuhusu washambuliaji hao, "wanaohusiana nao na iwepo walisaidiwa na watu wengine".

Redouane alikuwa mpishi aliyetumia jina Rachid Elkhdar na polisi walisema alidai kuwa wa asili ya Morocco na Libya. Alimuoa mkewe ambaye ni muingereza jijini Dublin mwaka wa 2012 na kuishi mjini Rathmines.

Kwa sasa tatu kati ya waliouwawa katika shambulizi hilo wametajwa.
Bi Boden alifanya kazi kama muuguzi katika hopitali za Guy na St. Thomas jijini London. Familia yake imemtaja kama alipenda kuzuru kwengi na mkarimu " Tunamsherekea Kristy kwa ujasiri wake ambayo yaonyesha alivyojali watu, sio kwa usiku huo pekee, lakini katika maisha yake yote" waliongeza.

Hospitali alikofanyia kazi ilisema kuwa Bi Boden alikuwa muuguzi wa kipekee aliyefaa sana katika vyumba vya kupona baada ya upasuaji.

Mwenyeji wa Canada Chrissy Archibald, mwenye umri wa miaka 30, alikuwa nusura wa kwanza kutajwa. Familia yake inasema kuwa alifariki katika mikono ya mchumba wake baada ya kugongwa na gari la washambulizi hao lilipopita kwa kasi.

Nayo famili ya James McMullan, mwenye umri wa miaka 32 kutoka eneo la Hackney, Mashariki mwa London, wmeisema kuwa wanaamini pia yeye alifariki.

Dadake McMullan anaaminika kuwa kati ya waliofariki, baada ya kadi yake ya benki kupatikana kwa mwili mmoja katika eneo la tukio.

Mfaransa mmoja pia aliuwawa kwenye shambulizi hilo, kulingana na waziri wa kigeni Jean-Yves Le Drian.

Polisi wametoa nambari 0800 096 1233 na 020 7158 0197 za kupigwa na familia na marafiki walio na wasiwasi kuhusu jamaa zao.

Msajili wa Vyama Azungumzia Sakata la Maalim Seif Kufungua Ofisi Mpya za CUF

0
0
Kutokana na Chama cha Wananchi (CUF) kufungua ofisi mpya za chama hicho katika eneo la Mtaa wa Idrisa Kata ya Mzimuni, Magomeni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Msajili wa Vyama vya Siasa amesema anaamini chama hicho kinafanya mambo yake kwa kuzingatia sheria.

Jana  Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alisema hajapata taarifa yoyote ya chama hicho, kufungua ofisi mpya zaidi ya kuona katika vyombo vya habari.

Ukiondoa taarifa za kwenye media sijapata taarifa yoyote kutoka CUF labda wawe wameleta leo (jana), lakini naamini chochote wanachofanya wanaelewa taratibu wataleta taarifa,“ alisema Jaji Mutungi.

Jaji Mutungi alisema sheria inawataka wanapofungua ofisi watoe taarifa ndani ya siku 14, ambazo hazijaisha hivyo anaamini wanajua hilo.

Upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad wamefungua ofisi hizo, baada ya tukio la kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Buguruni na kundi la Profesa Ibrahim Lipumba.

Jaji Mutungi alisema atakapopokea taarifa rasmi ataangalia kama taratibu zilifuatwa kwani ufunguaji wa ofisi mpya una taratibu zake.

Nikiletewa taarifa ndio nitajua kama walifata taratibu au la, ufunguaji wa ofisi una taratibu zake najua wanazijua pia,“ alisema Jaji Mutungi.

Alisema taarifa hiyo ataipata kutoka kwa mwenyekiti au msemaji wa chama, ambaye ni katibu mkuu ambao wanatambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Akizindua ofisi hiyo Juni 4 mwaka huu, Maalim Seif alisema ofisi hiyo imetolewa na wabunge 40 wa CUF.

Alisema uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni kitendo cha kiungwana na kiungwe mkono na wanachama wote.

Alisema kwa miezi 10 sasa, wamekuwa wakishindwa kufanya kazi kwa upande wa Tanzania Bara, jambo ambalo limewaathiri hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu bila hofu yoyote.

Katibu huyo alisema ana imani na mahakama kuwa itawapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.

Miujiza ya Shekh Sharifu Rashid, Je? Unapata Pesa Haikai? Umeachwa na Mpenzi, Mke au Mme Anakusumbua?

0
0

MIUJIZA YA SHEKH SHARIFU RASHID KUTOKA BAGAMOYO PWANI. (RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 72 TU) ASANTE KWA KUENDELEA KUMPIGIA SIMU SHEKH SHARIFU RASHID KWA WALE WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA SHUKRANI: 

SHEKH SHARIFU RASHID ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili, anatumia kitabu cha quran dawa za asili dawa za kiarabu, na njiwa, Anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango kwa kina mama, ngiri maji na n.k, anakuvutia mali zilizo potea au kudhulumiwa, pia anatoa Pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali, Wenye matatizo ya uzazi, jini mahaba, mapepo ya kichawi, vifungo vya kimaisha, ndoto mbaya za usiku, uelewa mdogo wa ufahamu shuleni kwa watoto wote, pia anauwezo mkubwa wa kumaliza kazi zilizoachwa na wataalamu wengine ndani ya masaa 48 tu, Pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo. WASILIANA NAE KWA WhatsApp na SIMU NO: +255 718-668347 na +255 767-204308 , +255 685-224047 Email shekhsharifurashidi@gmail.com. 

USHAURI: ni vyema kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate huduma kwa haraka.

Ewura Yapandisha Bei ya Mafuta Kuanzia Leo Jun 17

0
0
Mamalaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini (EWURA) imetangaza bei mpya elekezi za mafuta zitakazoanza kutumika maeneo yote nchini kuanzia leo Juni 7, 2017.

Katika bei hizo mpya zilizotolewa jana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa EWURA, Titus Kaguo alisema kuwa kunaongezeko la bei katika mafuta ya petroli na dizeli huku mafuta ya taa yakishuka bei.

Kaguo alisema kuwa, ongezeko hilo la bei linatokana na sababu ya mabadiliko ya bei ya mafuta katika soko la dunia sambamba na kuimarika kwa thamani ya dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania.

Kwa upande wa mafuta ya dizeli yameongezeka Tsh 43 kwa lita huku mafuta ya petroli yakiongezeka Tsh 25 katika kila lita moja.

Aidha, afisa huyo alisema kuwa, bei hizo mpya haziwahusu wateja kutoka mkoa wa Tanga ambao wao wataendelea kutumia bei za mwezi uliopita kutokana na mkoa huo kuwa na bandari inayotumika kushushia na miundombinu ya kuhifadhi mafuta kiasi cha kuwa na akiba kubwa ya mafuta yaliyoingia nchini mwezi uliopita.

Steve Nyerere Ataka Asihusishwe na ishu ya Audio ya Wema na Mbowe

0
0
Mchekeshaji Steve Nyerere mwenye vipaji vya kuigiza sauti mbalimbali za viongozi, amewataka Watanzania kuacha kumuhusisha kwenye sakata la kutengeneza audio ambayo anasikika malkia wa filamu, Wema Sepetu akizungumza mambo ya faragha na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Freeman Mbowe.


Mwenyekiti huo wiki hii, aliikataa audio hiyo kwa kusema siyo yake huku akiwataka Wanzania kutulia wakati timu yake ikifanya uchunguzi juu ya sakata hilo.

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Steve Nyerere amedai kila mtu anajua hawezi kufanya kitendo kama hicho kwaajili ya kumchafua mtu.

“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile,” alisema Steve. “Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,”

Alisema hataki kulizungumzia zaidi sakata hilo kwa kuwa anaweza akaanzisha mjadala mpya kitu ambacho hapendi kitokee.

Muigizaji huyo alihusishwa kwenye tukio hilo baada ya kusikika mtu anayedaiwa kuwa ni Wema akitaja jina lake.

Katuni Aliyochorwa RC Anna Mghwira, Baada ya Kuapishwa

0
0
Rais John Magufuli akimuapisha Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo.

Kauli ya Mkwasa Kuhusu Hatma ya Ngoma

0
0
Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema Ngoma bado ni mchezaji wa Yanga na amemuaga anakwenda kutibiwa huku Mkwasa akiongeza kwamba bado hawajapokea ofa kutoka klabu yoyote kuhusu kumtaka Ngoma.

Suala lake lina zungumzika vizuri tu, bado anamajeruhi na ameniomba ruhusa anakwenda kupata matibabu lakini bado tupo naye na anapenda bado awe na sisi lakini ana suala lake kubwa ambalo linamsimu kama unakumbuka muda mrefu hajacheza kutokana na maumivu yanayomkabili.”

“Amekwenda kwa ajili ya ‘deep treatment’ kwa hiyo atakapokuwa amepona tutakuwa nae, kwa mujibu wa mkataba bado ni mchezaji wa Yanga kwa sababu hatujapata ofa kutoka sehemu yoyote na tunachofahamu sisi ni kwamba anaendelea na matibabu kwa hiyo hatuwezi kusema chochote.

Ngoma hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara huku kukiwa taarifa ambazo si rasmi zikidai kwamba mchezaji huyo anaweza kuihama Yanga na kwenda kucheza soka nchini Afrika Kusini.

Umeipata Hii Mpaya ya Mama Kanumba na Mama Lulu?

0
0
Baada ya kuwa katika mgogoro kwa muda mrefu, wazazi wa kike wa waigizaji marehemu Steven Kanumba na Elizabeth Michael ‘Lulu’ hatimaye wamemaliza bifu lao na hivi sasa, hakuna mwenye kinyongo tena. Wazazi hao, Lucresia Karugila wa Lulu na Flora Mtegoa wa marehemu Kanumba, awali walikuwa mashoga wakubwa, kabla ya upepo kubadilika na baadaye kukosekana kwa maelewano baina yao. Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na wawili hao, hivi sasa wazazi hao wana mawasiliano kama ilivyokuwa zamani.

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mama mzazi wa Lulu ambaye baada ya kuulizwa kuhusu habari hizo njema, alikiri ni kweli wamerejea katika uhusiano wao kama zamani. “Mimi sina ugomvi na mama Kanumba kabisa, niko naye vizuri, tatizo maneno ya watu ndiyo yanatuharibia,” alisema kwa kifupi. Kwa upande wake, mama Kanumba alipotafutwa alijibu kwa kifupi tu; “Siku zote huwa nasema kila kinachotokea Mungu ameshapanga hivyo, sina tatizo na mama Lulu.”

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa leo Katika Magazeti

Anna Mghwira: Mpaka sasa mimi ni Mwenyekiti wa Chama

0
0
"MPAKA sasa mimi ni mwenyekiti wa chama, nitakaa na wenzangu tuangalie mazingira ya chama chetu jinsi kilivyo kutokana na majukumu yangu nitakuwa Kilimanjaro kwa muda mwingi uwenyekiti wangu itakuaje"

Ni kauli ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Anna Mgwira alipokuwa kwenye mahojiano na Azam Tv jana mara baada ya kuapishwa kwenye nafasi ya ukuu wa Mkoa huo, ambapo amesisitiza kuwa yeye bado ni Mwenyekiti wa Chama cha Act-Wazalendo.

amesema kuwa uenyekiti wa chama chochote nchini ni shart uwe  Makamu Mwenyekiti Bara na Zanzibar na makamu wangu wote wanaimudu nafasi ya umakamu.

" Ilani ya chama cha mapinduzi ni lazima niitekeleze, napotekeleza Ilani nikiona ina mapungufu namuona Mwenyekiti wa chama na Katibu wake kwamba Ilani hii haitekelezeki.
"Wakati mwingine hizi Ilani watu wanaongea tu maneno hawazisomi, Ukiisoma Ilani ya kila chama cha Tanzania zote ni nzuri,"

Wabunge Wapongeza Kuwajibishwa kwa Halima Mdee na Ester Bulaya..!!!

0
0

MHADHIRI Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Banna, amesema adhabu iliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na Ester Bulaya ya kufungiwa shughuli za Bunge kwa takriban mwaka mmoja ni sahihi.

Wabunge hao walipewa adhabu hiyo juzi kwa kosa la utovu wa nidhamu katika kikao cha Bunge na kukidharau Kiti cha Spika, Ijumaa iliyopita. Wabunge hao walionesha utovu huo wa nidhamu bungeni, wakipinga Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kutolewa nje ya Bunge kwa agizo la Spika wa Bunge Job Ndugai.

Kutokana na Mnyika kukaidi amri ya Spika ya kumtaka akae huku Mnyika akitaka ombi lake la utaratibu bila kujali maelekezo ya Spika, Ndugai aliagiza askari kumtoa nje ya Bunge na kutohudhuria vikao vya Bunge kwa wiki moja.

Wakati askari wakimtoa Mnyika ukumbini, Halima ambaye ni mbunge wa Kawe na Bulaya wa Jimbo la Bunda Mjini, waliinuka katika viti vyao na kuelekea upande wa askari waliokuwa wakimtoa nje Mnyika huku Bulaya akihamasisha wabunge wengine wa upinzani kuondoka na kususa Bunge.

Kutokana na hali hiyo, Ndugai aliiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujadili adhabu mwafaka na ndipo baada ya mjadala, Bunge likaridhia wabunge hao kutoshiriki shughuli za Bunge vikiwamo vikao vya Bunge na safari na vikao vya Kamati za Kudumu hadi mwezi Aprili mwakani katika Bunge la Bajeti mwaka 2018/ 2019.

Akizungumza na gazeti hili, Dk Banna alisema wabunge hao walidhalilisha Bunge, wapiga kura na wananchi katika majimbo yao. Alisema wabunge wanapaswa kuheshimu kanuni za Bunge na kuzifuata ili kufanya uwakilishi mzuri kwa wananchi.

“Kuna gharama ya kuwa Mheshimiwa na hiyo ni kuwa na hekima kwa kuwa chochote kinyume na hapo ni kosa tena kubwa na wabunge hao wamevuna kile walichokipanda,” alisema.

Mbunge wa Kaliua wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya alisema kuwa adhabu hiyo ni mwafaka kwa wabunge hao kutokana na kuwa walikwishaonywa. Alisema, Bunge linatakiwa kuheshimiwa na wabunge hao wamekuwa watata mara kwa mara katika kufuata kanuni zilizowekwa.

Alisema, wabunge wanatakiwa kuwa na nidhamu, uvumilivu na hekima ya hali ya juu kipindi chote wakati Bunge likiwa linaendelea. Alisema kwa upande wa Mdee, ndani ya kipindi kifupi amefanya makosa kadhaa ya utovu wa nidhamu.

Alisema, mbunge huyo aliitwa kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu mwezi Aprili baada ya kudaiwa kumtukana Spika Ndugai na alipewa karipio kali la kumtaka asirudie kosa. Alisema wakati wakiwa kwenye kikao hicho, aliambiwa wazi kuwa iwapo atarudia tena kosa, atapewa adhabu kali zaidi na kwa sasa anatumikia kile alichoonywa.

Jay Moe Amkana Producer T-Touch

0
0
Msanii wa mkongwe wa ' hip hop' mwenye hit ya 'Nisaidie kushare' Jay Moe amefunguka kwa kusema hawezi kusainiwa na mtu yoyote yule akidai yeye mwenyewe ana label yake ya So Famous na kuna wasanii wanamtegemea.

Jay Moe amefafanua hayo baada ya kuenea tetesi zilizokuwa zikiwaaminisha watu kuwa huenda akasainiwa na Mr T-Touch ili aendelee kutoa nyimbo chini ya uongozi wa 'Producer' huyo.

"Mimi ni C.E.O wa so Famous entertainment kwa hiyo siwezi kusainiwa na mtu mwingine wakati mimi mwenyewe nataka kusaini watu, mimi sipo kwa T-Touch wala sipo tayari kusainiwa na 'record label' yoyote kwa sababu nina label nataka niikuze nisaidie wengine ambao wapo nyuma yangu, wanataka waone mafanikio yangu ili na wao yawanufaishe" - alisema Jay Moe

Lukuvi Azua Tafrani Kwenye Msiba wa Ndesamburo..Atinga Kanisani Akiwa na Lundo Polisi Wenye Silaha..!!!

0
0

Katika hali isiyo ya kawaida Waziri Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi jana alizua taharuki baada ya kuwasili katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi Mjini Philemon Ndesamburo akiwa ameongozana na magari mawili ya polisi waliobeba silaha.

Ibada hiyo ilifanyika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Kiboriloni mjini Moshi jana.

Hali hiyo ilisababisha hofu kwa wananchi wengi waliokuwa nje ya kanisa hilo na baadhi wakishindwa kuingia kanisani katika ibada iliyokuwa inaendelea ndani.

Hata hivyo ni kawaida kwa waziri kuongozwa na vyombo vya usalama wakati wa msongamano wa watu.

Sura Mbili za Spika Ndugai Bungeni..!!!

0
0

Wakati wa Bunge la Bajeti la mwaka 2016/17, wabunge kutoka vyama vya upinzani walisusa vikao kila walipomuona Naibu Spika, Dk Tulia Ackson akiingia ukumbini.

Walisema Dk Tulia, ambaye alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu kabla ya kuteuliwa kuwa mbunge na baadaye kupitishwa na CCM kuwa mgombea nafasi ya Naibu Spika, alikuwa na uozefu mdogo na kutumia cheo chake kukandamiza upinzani.

Wakati huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alikuwa nje ya nchi kutibiwa na wengi walisikika wakisema kuwa kama mbunge huyo wa Kongwa angekuwepo, mambo yasingeweza kwenda kama yalivyokuwa yakiendeshwa na Dk Tulia.

Na baada ya kurudi nchini, Ndugai alihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam na kusema kile wapinzani walichokitarajia.

Katika mahojiano hayo, Ndugai alisema kikao kilichokuwa kinafuata ambacho kilianza Septemba 6, 2016 angekitumia kufanya majadiliano kati ya Spika na Naibu Spika, wenyeviti wa Bunge pamoja na wabunge wa upinzani.

“Katika Bunge hili tuna malengo mengi kama changamoto ya kujenga Bunge moja na si vipande vipande. Kwa sasa ushirikiano umepungua bungeni, yaani kuna uvyama na migogoro imezidi, hii hali haiwapi raha Watanzania,” alisema Spika Ndugai akitoa matumaini kwa wapinzani.

Alifikia hata kuahidi kuwa ataazima kanuni za Bunge la Katiba lililompa mwenyekiti mamlaka ya kuunda kamati ya maridhiano ambayo ingefanya kazi ya kutafuta suluhisho kunapotokea matatizo.

“Kutoka nje ya bunge, si kosa ni haki ya kidemokrasia, lakini zipo njia mbalimbali za kufikisha ujumbe kwa mujibu wa kanuni zetu,” alibainisha.

“Mbunge wa upinzani anakatisha ruti (njia) ngumu kuliko mbunge wa CCM huko mtaani katika kugombea. Hukumbana na polisi na kupita sero, sasa anapofika pale bungeni subira inakuwa ndogo. Na akiguswa kidogo kumbukumbu yake inakuwa vile vile kuwa alah kumbe na huku ni walewale,” alisema Ndugai.

Takriban mwaka mmoja sasa, wapinzani wanaanza kuona sura tofauti ya Spika Ndugai. Sasa hawaoni uzoefu, kuwajali na wala kutenda haki sawa kwa wabunge wote.

Agizo lake la kutaka mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika atolewe kwa nguvu bungeni, kimeshawafanya wabunge wa upinzani kutathmini upya imani yao kwa Ndugai kulinganisha na ilivyokuwa miezi michache iliyopita na mwaka mmoja uliopita.

Miezi miwili iliyopita, Spika Ndugai alitumia maneno makali wakati akiagiza mbunge wa Kawe, Halima Mdee akamatwe kwa kosa la kumtukana, huku akiwaeleza wabunge kuwa chombo hicho kimeongeza uwezo wake wa kung’amua wakorofi ndani na nje ya ukumbi.

“Waheshimiwa wabunge, tumeimarisha sana masuala ya kujua mwenendo wa kila mmoja wetu ndani ya jengo hili na hata katika viwanja vyote vya Bunge, labda isipokuwa vyooni peke yake,” alisema Ndugai Aprili 6 mwaka huu.

“Lakini maeneo yaliyobaki mengine yote tuko imara na tuko vizuri sana, ningeliomba niwahakikishie waheshimiwa wabunge.

“Na yote hii ni kwa sababu ya usalama wenu na ulinzi wenu.

“Kwa hiyo ukiwa hapa ni vizuri ujue kuwa hauko jimboni wala mahali pengine. Bali mahali ambapo unapaswa kujiheshimu kibunge.”

Alikuwa akizungumzia tukio lililotokea Aprili 4 wakati wa kujadili uchaguzi wa wagombea wa nafasi tatu za upinzani katika Bunge la Afrika Mashariki, mjadala uliotawala na mhemko na hasira.

Katika mjadala huo, Mdee alisikika akisema neno “fala”, akilielekeza kwa Spika, hali iliyomfanya Ndugai kueleza jinsi walivyojizatiti kukabiliana na wabunge wanaozomea au kutoa lugha chafu.

“Niwaambieni nyinyi mnaomzomea Spika kwa mara nyingine na sitachoka kuwaambieni, tuna miezi hii, mitatu. Tutashughulika na kila mmoja ambaye anayedhani kwamba yeye kujifanya hapa ana (uwezo wa kufanya) vurugu,” alisema Ndugai.

Miezi miwili baadaye, Ndugai amekumbana tena na wabunge wanaozomea, lakini safari hii hawajakizomea kiti, bali Mnyika.

Akiomba mwongozo kwa Spika kuhusu madai ya mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde kuwa wapinzani wanatetea wezi katika suala la kuzuia mchanga wa madini kusafirishwa nje, Mnyika aligeuzia suala hilo kwa chama tawala akisema ndicho kilichoingia mikataba ya wizi na bado dhahabu inaendelea kusafirishwa nje.

Wakati Ndugai alipomtuliza kwa kumwambia hoja yake imesikika, sauti ilisikika kwenye kipaza sauti ikimuita Mnyika kuwa “mwizi” na mbunge huyo wa Kibamba akataka hatua zichukuliwe.

Lakini Spika hakutaka kuzungumzia sauti hiyo.

“Mheshimiwa Mnyika ulikuwa unaongea ukimuelekezea Mheshimiwa Lusinde. Mtu mwingine yeyote anayeongea kitu kingine hapa, mimi sina habari nacho. Mheshimiwa Lusinde endelea,” alisema Ndugai.

Lusinde alipotaka kuendelea, Mnyika naye alisimama na kuendelea kupaza sauti akitaka aliyesema neno hilo achukuliwe hatua, na ndipo Ndugai alipoamuru mbunge huyo wa Kibamba aondolewe kwa nguvu ukumbini.

Hadi jana hakukuwa na hatua zozote za kumtafuta mbunge aliyetoa neno hilo kwa kutumia mitambo ambayo Ndugai alisema ina uwezo wa kumtambua mbunge akiwa ndani au nje ya ukumbi wa Bunge.

Kitendo hicho kimewaudhi wapinzani na wanaona kuwa Spika ana sura mbili tofauti inapofikia masuala yanayowahusu wabunge wa CCM na wa upinzani.

“Ukiona wameungana na upinzani ujue wameguswa wao pia, lakini jambo likiwagusa upinzani pekee halina majibu mazuri zaidi ya dhihaka na majibu ya kuumiza upande mmoja,” alisema mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali.

“John Mnyika alipoitwa mwizi, (Spika) alikuwa hana masikio 100, lakini alipotukanwa yeye alikuwa na masikio 1,000 ya kusikia. Halikuwa kwenye hansard (kumbukumbu za Bunge) kama ambavyo wanapenda kujitetea, lakini kalisikia kwenye mitandao na akalitolea maamuzi.

“Lakini la Mnyika kuitwa mwizi hadharani tena kwa sauti ya wazi, halijatolewa maelezo zaidi ya aliyetukanwa kuonekana ana makosa na kutolewa nje. Kazi ya kututetea upinzani inabaki kwa wananchi.”

Hata hivyo, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema kuangalia kwenye kamera kujua aliyetamka maneno “Mnyika mwizi” si busara, ingawa hakuunga mkono uamuzi wa Spika Ndugai.

Alisema angetumia ushawishi wake kulishauri Bunge kuchukua uamuzi tofauti kuliko chombo hicho kuwafungia wabunge wawili ambao wamechaguliwa na wananchi.

“Angeamua kwa busara hata kwa kusema aliyesema ameropoka na Mnyika atulie taratibu nyingine ziendelee badala ya kujibu kuwa hana masikio 100 ya kusikiliza huku na huku,” alisema Mbunda.

Alisema wakati mwingine nguvu hazihitajiki katika masuala ambayo yanaweza kumalizwa kwa kutumia busara, kama lilivyokuwa suala la Mnyika.

“(Mnyika) Ametukanwa na bado ametolewa nje na kadhia kadhaa zimetokea,” alisema Mbunda.

Kauli ya Mbunda inalingana na ya mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa aliyesema maamuzi hayakuwa ya haki kwa sababu Bunge lina uwezo wa kubaini aliyemtukana Mnyika.

Alisema hekima na busara vimekosekana katika Bunge badala yake utashi, uoga ndiyo vimetawala na kusababisha kinachosemwa kukinzana na kinachotendwa.

“Spika analinda heshima yake badala ya kulinda heshima na nidhamu ya mhimili wa Bunge kwa kuzingatia matakwa ya kidemokrasia,” alisema mchungaji huyo wa Kanisa la Vineyard.

“Vitisho wanavyopata kutoka kwa viongozi wao wa chama wanavileta hadi bungeni. Wanafanya kazi na kutoa maamuzi kwa uoga na kusahau haki.”

Msigwa alisema wakati mwingine kuwa wabunge ni kutumia vibaya fedha za wananchi kwa sababu kinachofanyika ni vurugu.

“Kwa mwenendo uliopo na unaoendelea wa kutisha wapinzani, kuwakatisha tamaa haina haja ya kuwa na Bunge,” alisema Msigwa.

Alieleza kuwa haina haja ya kuwa na kamera kama watu wanasema maneno ya kukera kwa wenzao na uwezekano wa kuwabaini upo, lakini haifanyiki.

“Kwa sababu aliyekerwa ni wa upinzani kamera hazina kazi na hazina maana kuwepo, lakini angekerwa wa chama tawala zingefanya kazi na kutegua kitendawili cha Mnyika,” alisema.

Ndugai na hasira

Pamoja na kuonyesha sura mbili, Ndugai anaonekana kuwa mtu mwenye hasira za karibu kwa jinsi alivyokuwa akizungumza katika matukio hayo mawili na mengine.

Wakati wa kura za maoni ndani ya CCM kuwania ubunge wa Kongwa, Ndugai aliingia kwenye mzozo na mgombea mwenzake kiasi cha kumpiga na fimbo aliyokuwa akitembelea wakati huo.

Alimshambulia kwa fimbo, Dk Joseph Elieza Chilongani katika mkutano uliofanyika Kitongoji cha Ugogoni.

Wakati mmoja wa wagombea akijinadi katika mkutano huo, alidai kuwa jimbo la Kongwa halijafaidika chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini, jambo lililomuudhi Ndugai aliyekuwa amekaa kusubiri zamu yake na kumtaka mgombea huyo anyamaze kwa kuwa alikuwa anaongea upuuzi.

Wakati wawili hao wakiendelea kujibizana, Ndugai aligeuka na kugundua kuwa Dk Chilongani alikuwa akirekodi tukio hilo.

Ndugai aliamka huku akisema kuwa alikuwa akimtafuta siku nyingi Dk Chilongani na kwamba angemtambua kwa kurekodi tukio hilo.

Ndipo alipompiga kwa fimbo hiyo na baadaye kumshambulia, kabla ya kuamuliwa na baadaye Dk Chilongani kupelekwa hospitali kwa matibabu.

Wakati akitangaza uamuzi wa kumpeleka Mdee mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge, Ndugai alidokeza jinsi alivyojizuia hasira zake wakati akitukanwa.

“Watanzania wengi sana wameniandikia, wamesikitishwa sana, sana, sana na jambo hili. Na huu si utamaduni wa Watanzania, lakini kwa kuwa wenzetu wamefika hapo,” alisema.

“Na hii si mara ya kwanza kwa Halima na hata juzi nilivumilia sana. Yaani nilivuta, nikamuomba Mungu anisaidie. Nikanyamaza kimya.”

Kutenda haki

Spika Ndugai pia ameonyesha kutenda haki katika baadhi ya matukio.

Aliwahi kumtimua ukumbini mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine Ndungulile kwa kosa la kumuita Mdee kuwa ni kituko.

Pia mapema mwaka huu alikemea vitendo vya kukamatwa ovyo kwa wabunge akisema jambo hilo ni kinyume cha sheria na utaratibu. Akihitimisha Mkutano wa Sita wa Bunge, Ndugai alisema kama kuna kiongozi yeyote wa Serikali anamuhitaji mbunge, anapaswa kutoa taarifa kwake kwanza badala ya kwenda moja kwa moja kumkamata.

Ilikuwa ni baada ya wabunge kama Tundu Lissu na Godbless Lema kukamatwa na kusafirishwa kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka, huku Zitto Kabwe akiamua kugomea ndani ya viwanja vya Bunge ili asikamatwe.

Habari ya ziada na Kalunde Jamal (kjamal@mwananchi.co.tz)     

Mhe Mghwira Siachii Uenyekiti wa ACT Ng'oo,Mbona Mbowe Ni Mwenyekiti wa Chama na Pia ni Mbunge...!!!!?

0
0

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema hana mpango wa kuachia nafasi yake ya uenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo.


Mghwira alitoa msimamo huo baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais Dk. John Magufuli Ikulu, Dar es Salaam jana.

Alisema kwa sasa anachokiangalia ni kusimamia shughuli za maendeleo kwa faida ya Watanzania.

Juni 3, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli alimteua Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, uteuzi ambao ulizua maswali na mshtuko mkubwa katika tasnia ya siasa.

Mjadala mkubwa uliibuka kutokana na cheo alichopewa, kuwa ni tofauti na kile cha ubunge, huku wengine wakienda mbali zaidi huenda kuna usaliti.

Mghwira ambaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka juzi, aligombea urais kupitia ACT- Wazalendo, sasa atalazimika kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM.

Mbali na hilo, pia atabeba jukumu la kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

MGHWIRA

Akizungumza jana, Mghwira alieleza kushangazwa na namna watu wanavyohoji endapo ataachia uenyekiti wa ACT-Wazalendo, wakati kuna mambo ya msingi.

“Sasa unataka niseme nini wakati leo (jana) ndio nimeapishwa? Hakuna vitu vya msingi vya kuhoji?  Mimi sitazami hizo nafasi.

“Mimi ni mwenyekiti wa chama na kama unakumbuka wakati Magufuli aliposhinda urais, nilimkabidhi ilani ya chama chetu na hata leo (jana) wakati ananikabidhi ya CCM nilimkumbusha kuwa hata mimi nilimpatia ya ACT akasema kweli anayo.

“Lakini kwani tatizo liko wapi? Mbona Mbowe (Freeman) ni Mbunge wa Hai halafu ni Mwenyekiti wa Chadema sasa tatizo liko wapi kwangu?” alihoji.

Alipoelezwa na mwandishi kuwa upo utofauti wake na Mbowe kwa kuwa yeye anakwenda kutekeleza ilani ya CCM, alisema. “Bungeni wanatekeleza ilani ya chama gani? Waziri Mkuu na wengine wote wanatekeleza ilani ya chama gani?

“Nikwambie tu, wengine ni maneno tu hawasomi hata hii ilani ya CCM na kwamba ilani yao si mbaya kinachotakiwa ni utekelezaji tu,”alisema.

Alisema chama chochote kinapoingia madarakani hakuna mbadala zaidi ya kutekeleza ilani yake.

“Mara nyingi tumekuwa tukilalamika ooh tunaonewa, tukipewa huo uhuru tena tukatae? Tujikite kwenye masuala ya msingi,”alisema Mghwira.

Kuhusu kipaumbele chake katika Mkoa wa Kilimanjaro, alisema ataanzia pale alipoishia Said Meck Sadick na kwamba ataripoti eneo lake la kazi ndani ya wiki hii.

Alipoulizwa endapo kabla ya kuapishwa amekutana na viongozi wa chama chake, alisema. “Jana tumeongea sana na viongozi wangu na leo (jana) tutaonana,” alisema.

Credit - Mtanzania

Mtukutu Mario Balotel Kutua Borussia Dortmund..!!!

0
0

Wakala Mino Raiola anayemsimamia Mario Balotelli, amesema nafasi kubwa ya mchezaji huyo ni kutua Borussia Dortmund msimu ujao.

Sababu za klabu hiyo ya Dortmund kuwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo wa timu ya Nice, ni kutokana na kuwapo taarifa za msambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang kuhitajika Paris Saint-Germain.

Riola alifanya mazungumzo ya awali na uongozi wa klabu hiyo jana Jumanne, huku akisema ana uhakika mchezaji huyo atakipiga Dortmund msimu ujao.
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images