Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Dk. Slaa Aibuka Aandika Waraka Mzito Kufuatia Kifo cha Mzee Ndesamburo

$
0
0
Dr Slaa
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa amesema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha Mzee Philemon Ndesamburo na kueleza namna ambavyo walikijenga chama pamoja.

Dk. Slaa amesema kuwa licha ya Ndesamburo kuwa na utajiri mkubwa, lakini hakuuona kuwa ni kitu bali ni nyenzo ya kuwakomboa wananchi katika sekta mbalimbali.

Dk. Slaa ameitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa miaka 15, Mzee Philemon Ndesamburo alipozikwa nyumbani kwake KDC Moshi baada ya kufariki wiki iliyopita alivyopata matatizo ghafla akiwa ofisini kwake.

Dk. Slaa ambaye sasa anaishi Toroto nchini Canada baada ya kujiuzulu  wadhifa wake na kuachana na siasa tangu mwaka juzi, alisema kuwa ameshtushwa sana na kifo cha ghafla cha kiongozi huyo tegemeo. Alieleza kuwa licha ya wao kubaki na majonzi, lakini anaamini kazi ya Mungu haina makosa wala haihojiwi.

Ni kweli nimefanya kazi na Ndesamburo, tumejenga CHADEMA kwa pamoja hasa kipindi cha mwaka 2003 hadi 2005 ambapo tulizunguka nchi nzima, alisema Dk. Slaa. Licha ya mazingira magumu waliyokutana naye kwenye harakati za kukitangaza chama hicho, Mzee Ndesamburo hakulalamika alipotakiwa kulala chini, lakini aliona hizo ni changamoto za kutafuta ukombozi.

Aidha, Dk. Slaa alisema kuwa Mzee Ndesamburo alikuwa msikivu na mwenye kuelewa na kuwa tayari kuwasaidia wengi kwa hali na mali kwani mara kadhaa alitoa mali zake kuwasaidia wagombea wa CHADEMA na hata yeye mwenyewe kwenda kuwapigia kampeni bila kujali umbali aliotakiwa kwenda.

Akizungumzia kifo chake, Dk. Slaa alisema kuwa kifo hicho ni cha kusikitisha kwa sababu alifariki ghafla, hakupata nafasi ya kuagana na ndugu jamaa na marafiki. Wakati mwingine afadhari mtu akiugua mnajiandaa kisaikolojia, ila akifariki ghafla tu, huwa ni kazi ngumu kuipokea ile hali.

Kazi kubwa iliyobaki kwa watanzania sasa ni kutekeleza yale yote ambayo Mzee Ndesamburo amewaachia huku tukimuombea Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Dk. Slaa aliondoka nchini mwaka 2015 baada ya kujiuzulu wadhifa wake kufuatia chama chake kumpokea na kumpa nafasi ya kugombea urais, aliyekuwa kada nguli wa CCM, Edward Lowassa.

CREDIT: TanzaniaDaima

Ndege ya Jeshi Yapotea na Watu 100 Ndani

$
0
0

Ndege ya Jeshi
BBC,Burma. Ndege ya jeshi la Burma, iliyokuwa imewabeba zaidi ya watu 100, imetoweka.

Taarifa zilizotolewa na viongozi wa kitaifa wa Burma, zimeeleza kuwa ndege hiyo ya kijeshi, ilikuwa imeruka kati ya Yangon (Rangoon) na mji ulioko Kusini mwa nchi hiyo wa Myeik. Shughuli za kutafuta ndege hiyo.

"Tulipoteza mawasiliano na ndege hiyo kuanzia saa 4:35 leo asubuhi (saa za Afrika Mashariki),   ndege hiyo ilipofika maili 20 Magharibi mwa Mji wa Dawei," jeshi la Burma limetoa taarifa hiyo

Inaelezwa kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria 105 na wafanyakazi 11.

Ndege za wanajeshi pamoja na helikopta zimetumwa katika eneo hilo katika shughuli za kuwatafuta manusura au mabaki ya ndege hiyo ambayo mpaka sasa inaaminika kuwa imeanguka.

Taarifa zinaongeza kuwa, ndege hiyo ilikuwa angani ikivuka bahari ya Andaman dakika chache baada ya kutoweka.

Vita vya Mimba Havijawahi Kumuacha Diamond Platnumz Salama

$
0
0
Mimba

Kila kukicha kuna tetesi za wadada wa mujini mfano irene(Queen video wimbo wa kwetu),hamisa mabeto(queen video wimbo wa salome),penny(ex girlfriend wa dai) kubeba ujauzito wa msanii diamond ila cha kushangaza ni mwanamke mmoja pekee aliyetangaza ana mimba ya dai na akajifungua mara mbili. Ila wadada wengine mimba zao sijui huwa wanazipeleka wapi. kwa sasa insta kumechafuka kwa tetesi,hadi kufikia january matokeo ya mimba hizo yatakua hadharani

SOMA HII HAPA CHINI:


Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma Leo Juni 8, 2017

$
0
0
Bungeni

Fuatilia hapa matangazo ya moja kwa moja kutoka Bungeni Dodoma, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Juni 8, 2017..


 Asuhi hii, Waziri wa Fedha Dk Mpango atawasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi ya nchi, ambayo itajikita katika kueleza mipango ya maendeleo kwa mwaka ujao.

Tazama Hapa Chini:

 

Wema Sepetu Kusomewa Kisomo cha Kufa Mtu

$
0
0
Wema Sepetu
Wema Sepetu Akilia
Kufuatia mabalaa mbalimbali ambayo yamekuwa yakimuandama Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Shehe Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amejipanga kumsomea kisomo maalum ndani ya Mwezi Mtukufu ili kumuepushia yale yote ya shari.

Shehe Mkuu amefikia hatua hiyo kufuatia mdada huyo ndani ya kipindi kifupi kuandamwa na majanga ambayo yamekuwa yakimkosesha amani. Miongoni mwa mabalaa ambayo yememkumba Wema siku za hivi karibuni ni pamoja na lile la kutajwa kwenye listi ya mastaa wa madawa ya kulevya na hili la juzi la kutengenezewa sauti akiongea kimahaba na kiongozi wake, Freeman Mbowe.

Akizungunza na Amani juzi, shehe huyo alisema kuwa, amepanga kumfanya kisomo hicho ndani ya mwezi huu endapo Wema na mama yake watafika katika ofisi zake zilizopo Lumumba jijini hapa kwa maelezo zaidi.

MSIKIE SHEHE MKUU

“Unajua Wema amekuwa akikutana na misukosuko mingi, ninachoweza kusema iwe kweli au si kweli Wema anatakiwa kufanyiwa kisomo maalum. Maana kumbukumbu zinaonesha hapitwi na mabaya mara kwa mara, kwa Rehema ya Mwenyezi Mungu amuepushie, kisomo nitakiandaa mimi mwenyewe. “Kuhusu sehemu na siku ya kufanya kisomo hicho bado haijafahamika kwa sababu hadi Wema na mama yake watakapokuja na kupanga nami kama ni nyumbani kwao lakini ni vyema wakaja ofisini kwangu. Ninafikiria kisomo hiki kukifanya

ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,” alisema Shehe Mkuu. Baada ya kumsikia shehe huyo, gazeti hili lilimtafuta Wema na mama yake ili kusikia wana lipi la kusema kuhusiana na uamuzi huo wa heri wa kiongozi huyo wa dini lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kupatikana. Hata hivyo, kwa kuwa ni jambo jema, gazeti hili linamshauri staa huyo kumtafuta Shehe Alhad ili kufanyiwa kisomo hicho kinachoweza kumuepusha na mabalaa.

Maaskofu Walaani Kuibwa Kwa Mabaki ya Ubongo wa Mtakatifu Bosco

$
0
0
Askofu wa Kanisa Katoliki

Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania, wamelaani kuibwa mabaki ya ubongo wa Mtakatifu John Bosco wa Italia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, walishangazwa iweje mtu mwenye akili timamu na nia thabiti ya kuhiji na kuomba baraka kutoka kwa watakatifu aibe mabaki hayo.

Kauli hiyo imetolewa baada ya mtu aliyejifanya hujaji kuiba kisanduku kilichokuwa na mabaki ya ubongo wa Mtakatifu John Bosco uliokuwa umehifadhiwa katika Kanisa la Casstelnuovo jijini Turin.

Kutokana na wizi huo, polisi wa Italia wameweka vizuizi katika mipaka kaskazini mwa nchi hiyo ili kumsaka mhusika.

Mtakatifu John Bosco aliyezaliwa Agosti 16, 1815 na kufariki dunia Januari 31, 1888 alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mwanzilishi wa Shirika la Mtakatifu Fransisko wa Sales (Salesian Congregation).

Gazeti la USA Today liliandika kuwa mwizi huyo aliingia katika Kanisa la Castelnuovo lililopo jirani na mji wa Turin Ijumaa iliyopita na kuiba mabaki ya ubongo huo.

Kwa kawaida waumini hufika kanisani hapo kusali mbele ya mabaki hayo ambayo huwekwa nyuma ya altare.

Namuomba yeyote aliyeuchukua aurudishe haraka, bila masharti ili tuufunge ukurasa huu na tuendelee kuadhimisha kumbukumbu ya Don Bosco vizuri,” alisema Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Cesare Nosiglia.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi alisema anachoamini ni kuwa, aliyeiba mabaki hayo atakuwa na kasoro kichwani.

Naye Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Jude Thadeus Ruwa’ichi alisema waliofanya kitendo hicho inawezekana imani yao ni tofauti na waliokwenda kuhiji.

Steve Nyerere: Mimi Sijaigiza Sauti za Mbowe na Wema, Sio Kwa Kiingereza Kile..

$
0
0
Mchekeshaji Steve Nyerere
Steve Nyerere
Steve kakanusha kuhusika na uigizaji wa sauti za mtongozo zilizovuma baina ya watu wanaodaiwa kuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mrembo Wema Sepetu wa Bongo Movie..

Kwanza mimi toka nimeanza kuigiza sauti sijawahi kuigiza sauti za viongozi wa chama fulani, Pili, kutongoza napo sio dhambi, ni sunna (akimaanisha ni jambo jema tu kwa mwanaume yoyote kulifanya). 
Tatu, sio kila kitu ambacho kimefanywa na familia fulani basi Steve anahusika. 

Limenikera na kuniumiza sana. Pia sio kwa Kingereza kile cha kubembeleza vile, nina uwezo huo? Na pia sio mimi peke yangu ninayeweza kuigiza sauti za watu, waigizaji wapo wengi.” alinukuliwa akisema Steve Nyerere.

WanaCCM: Tunaburuzwa na Rais Magufuli. Wapinga Uteuzi wa Mghwira..!!!

$
0
0

Rais kuteua wakuu wa mikoa toka vyama vya upinzani alipaswa kupata baraka za chama. Na ikibidi hata kubadilisha vifungu vya katiba ya ccm. 

Nafasi ambazo rais huteua kwa matakwa yake bila ya kufungwa na katiba ya chama chake ni zile nafasi kumi za ubunge. Lakini kamwe siyo ukuu wa mikoa na wilaya. Hawa ni watekelezaji wa ilani ya chama kwa mujibu wa katiba ya ccm. Hivyo wanapaswa kuwa wafuasi ama wanazi wa ccm. 

Huyu rais hana uchungu na chama na ni kwasabb hajawahi kukitumikia chama na hivyo hajui machungu ya kujenga chama. Kuna kila sabb ya kumpinga kwa nguvu zetu zote tutakapokutana ktk vikao vijavyo. 

Haya yanaelezwa kwa uchungu sana na wanaccm, wazee kwa vijana wa sehemu mbalimbali nilikotembelea ili kupata maoni yao kufuatia uteuzi wa m/kiti wa chama cha ACT kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro. 


Kifo cha Mzee Ndesamburo Chamfanya Dk Slaa Kugunguka Mengine Mapya Kuhusu Chadema..!!!

$
0
0

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa amesema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha Mzee Philemon Ndesamburo na kueleza jinsi walivyokijenga chama pamoja.

Dk. Slaa amesema kuwa licha ya Ndesamburo kuwa na utajiri mkubwa, lakini hakuuona kuwa ni kitu bali ni nyenzo ya kuwakomboa wananchi katika sekta mbalimbali.

Dk. Slaa ameitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa miaka 15, Mzee Philemon Ndesamburo alipozikwa nyumbani kwake KDC Moshi baada ya kufariki wiki iliyopita alivyopata matatizo ghafla akiwa ofisini kwake.

Dk. Slaa ambaye sasa anaishi Toroto nchini Canada baada ya kujiuzulu  wadhifa wake na kuachana na siasa tangu mwaka juzi, alisema kuwa ameshtushwa sana na kifo cha ghafla cha kiongozi huyo tegemeo. Alieleza kuwa licha ya wao kubaki na majonzi, lakini anaamini kazi ya Mungu haina makosa wala haihojiwa.

"Ni kweli nimefanya kazi na Ndesamburo, tumejenga CHADEMA kwa pamoja hasa kipindi cha mwaka 2003 hadi 2005 ambapo tulizunguka nchi nzima," alisema Dk. Slaa na kuongeza kuwa licha ya mazingira magumu waliyokutana naye kwenye harakati za kukitangaza chama hicho, Mzee Ndesamburo hakulalamika alipotakiwa kulala chini, lakini aliona hizo ni changamoto za kutafuta ukombozi.

Aidha, Dk. Slaa alisema kuwa Mzee Ndesamburo alikuwa msikivu na mwenye kuelewa na kuwa tayari kuwasaidia wengi kwa hali na mali kwani mara kadhaa alitoa mali zake kuwasaidia wagombea wa CHADEMA na hata yeye mwenyewe kwenda kuwapigia kampeni bila kujali umbali aliotakiwa kwenda.

Akizungumzia kifo chake, Dk. Slaa alisema kuwa kifo hicho ni cha kusikitisha kwa sababu alifariki ghafla, hakupata nafasi ya kuagana na ndugu jamaa na marafiki. 

"Wakati mwingine afadhai mtu akiugua mnajiandaa kisaikolojia, ila akifariki ghafla tu, huwa ni kazi ngumu kuipokea ile hali.Kazi kubwa iliyobaki kwa watanzania sasa ni kutekeleza yale yote ambayo Mzee Ndesamburo amewaachia huku tukimuombea Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi."

Dk. Slaa aliondoka nchini mwaka 2015 baada ya kujiuzulu wadhifa wake kufuatia chama chake kumpokea na kumpa nafasi ya kugombea urais, aliyekuwa kada nguli wa CCM, Edward Lowassa.

Kwa Mara ya Kwanza Membe Atoka Hadharani na Kuzungumza Haya Msibani..!!!

$
0
0

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amemsifu marehemu Abdul Mtiro kuwa alikuwa hodari, mchapakazi na mtiifu.

Mtiro maarufu Cisco amewahi kuwa Mkuu wa Itifaki katika Serikali za awamu ya nne na Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.

 Mtiro aliyefariki dunia Jumatatu, alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Membe aliyekuwa pamoja na viongozi wengine wakiwamo marais wa awamu ya pili na ya nne, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete alisema umati huo wa watu unaonyesha tafsiri ya utumishi uliotukuka wa kiongozi huyo.

 Membe aliwahi kuwa bosi wa Mtiro wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

 “Balozi Cisco alikuwa anaijua dunia kama anavyoijua Tanzania, Tunamkumbuka kwa uhodari katika kazi na utiifu,” alisema.

Alisema marehemu Mtiro alikuwa mwalimu mzuri kwa maofisa wa mambo ya nje hasa kwenye masuala ya itifaki.

Tibaijuka - Nilitolewa Kafara Kwenye Sakata la Escrow..!!!

$
0
0

WAZIRI wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amefunguka na kusema alitolewa mbuzi wa kafara katika kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Amesema  wabaya wake walijikita kuhoji matumizi ya Sh milioni 10, badala ya Sh bilioni 1.6 alizopokea.


Profesa Tibaijuka ameyasema hayo ikiwa ni miaka miwili na nusu tangu  avuliwe uwaziri  kwa sababu ya kashfa hiyo.

Katika kashfa hiyo, Profesa Tibaijuka ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini, ni mmoja wa watu waliopata mgao wa fedha hizo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira.

Rugemalira    alikuwa mbia wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.

Akizungumza na gazeti hili Dodoma jana, alisema baadhi ya mambo kuhusu suala hilo kama atayaweka wazi yanaweza kuingilia kitabu anachotaka kuandika.

Alisema wakati wabaya wake wakimsakama kwa kauli yake aliyosema kuna Sh milioni 10 alitoa kwenye akaunti yake  akisema zilikuwa ni za mboga, vita hiyo ilimsaidia kumuinua badala ya kumuangusha kama walivyotarajia.

“Hili ni swali zuri na kweli sijawahi kufafanua maana yangu ilikuwa nini kusema Sh milioni 10 ni hela ya mboga. Niliona kwamba nilishatolewa mbuzi wa kafara kwa hiyo niachie Mungu.

“Kama akipenda na kunivusha nitapata nafasi ya kueleza jinsi nilivyokumbwa na kadhia hiyo .

“Kumbuka hivi sasa watu wanatumbuliwa kila siku lakini mimi nadhani naingia katika historia ya Tanzania kama mtu pekee aliyetumbuliwa katika Serikali ya Awamu ya Nne, wengine walijiuzulu,” alisema Profesa Tibaijuka.

Alisema pamoja na hali hiyo kwa sasa wana CCM katika  jimbo lake hawataki ujinga kwa sababu  waliweza kumsimamia na kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kura nyingi.

“Bahati nzuri pia tukampata Rais mkweli ambaye naye hataki ujinga na utani usio na maana kuingoza Serikali ya Awamu ya Tano.

Credit - Mtanzania

Conte Amfukuza Costa Chelsea kwa Njia ya Meseji ya Simu ya Mkononi..!!!

$
0
0

 Mshambuliji wa Chelsea, Diego Costa amesema ametumiwa ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa kocha Antonio Conte akitakiwa kutafuta maisha sehemu nyingine.

Ndoto za Costa kubaki kwenye Uwanja wa Stamford Bride zimezimwa na kauli hiyo ya kocha ambaye hivi sasa yupo kwenye harakati za usajili kwa ajili ya kukisuka kikosi chake.

Taarifa za mchezaji huyo kuondoka kwenye klabu hiyo mabingwa wa England msimu ulioisha, ziliaanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kabla hata ligi hiyo kumalizika.

Costa alikuwa anahusishwa kuhamia Ligi Kuu ya China hata hivyo hivi karibuni alibadili mawazo na kutanga kwamba angependa kuendelea kubaki England.

Nafasi yake kubaki Chelsea imekuwa ndoto kutokana na uongozi huo kuongeza kasi kumsajili mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku.

Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amepewa taarifa za kutokuwapo kwenye mipango ya Conte jambo lililomfanya kuiwa njiapanda.

“Nimetumiwa ujumbe mfupi kwenye simu kutoka kwa Conte akisema sipo kwenye hesabu zake za msimu ujao” alisema Costa alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari wakati timu yake ya Hispania ilipotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Colombia jana Jumatano.

Costa alisema huenda kocha wake amechukua uamuzi huo kutokana na kufanyua vibaya msimu uliopita

VIDEO:Tundu Lissu Afunguka Mazito Asema ACT Wameanzishwa Kuua Upinzani

$
0
0
Tundu Lissu Bungeni

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki amefunguka kwa kusema chama ACT-Wazalendo kinatumiwa katika kuvunja upinzani uliopo nchini na serikali ya CCM.

Lissu amebainisha madai hayo baada ya Rais Magufuli kumteua aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyeapishwa jana katika viunga vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

"Hao siyo wapinzani hawajawahi kuwa wapinzani, walianzishwa kwa kazi maalumu ya kuua upinzani imeshindikana sasa wanapewa zawadi. ACT na Anna Mghwira walikuwa wakabariane na Lowassa nasiyo CCM walipata kura chache hata laki moja hazikufika. Huu ukuu wa Mkoa ni zawadi tu, Ukatibu Mkuu wa Kitila Mkumbo ni zawadi tu wanawazawadia watu wao hawa siyo wapinzani" alisema Lissu.

Aidha, Lissu amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi haijawahi kuwa na shida ya aina yeyote na viongozi wa ACT bali shida yao kubwa ni CHADEMA na CUF.

"Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), haijawahi kuwa na shida na ACT wala Kitila Mkumbo, haijawahi kuwa na shida na Anna Mghwira na hao wanaojiita wapinzani wote, shida yao kubwa ni CHADEMA na CUF ndiyo wapinzani wengine wote hawa ni wana CCM" alisisitiza Lissu.

Pamoja na hayo, Lissu amesema haitoweza kuja kutokea kwa Rais Magufuli kuja kumteua yeye kwa nafasi yeyote na endapo itatokea hivyo basi atamtaka kwanza abadilishe katiba mpya ili waweze kutengeza nchi mpya.

Msanii Rayuu Afunguka Sababu za Kutokufunga Mwezi Mtukufu

$
0
0
Rayuu
MSANII kutoka Bongo Muvi, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kuwa ugonjwa wa vidonda vya tumbo unaomsumbua umemfanya ashindwe kufunga kama alivyokuwa akifanya miaka ya nyuma.

Akizungumza na 3 Tamu, Rayuu amedai kuwa anaumia sana kutotimiza nguzo hiyo muhimu ya dini yake na anafanya kila awezalo kuhakikisha anautibu ugonjwa huo ili siku zijazo aweze kufunga.

“Nimekuwa nikijaribu kufunga lakini kabla siku haijaisha vizuri, vidonda vinatibuka hatari hivyo najikuta nikifungulia njiani, naumia sana kwa hali hii kwani napenda kufunga ila ndo hivyo sina jinsi,” alisema Rayuu

Serikali Yajigamba Kudhibiti Mfumuko wa Bei Kwa Miaka Minne Mfululizo..!!!

$
0
0

Tanzania imeendelea kudhibiti kiwango cha mfumuko wa bei katika kipindi cha miaka minne mfululizo huku kukiwa na matumaini  ya hali hiyo kuendelea kupungua kutokana na mikakati inayoendelea kuchukuliwa na Serikali.

Akisoma hali ya uchumi nchini bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi, Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Philip Mpango ameeleza kuwa kiwango cha mfumuko huo katika kipindi cha mwaka 2016 kilikuwa asilimia 5.2, kikiwa kimeshuka kwa alama chache ikilinganishwa na kile kilichorekodiwa mwaka mmoja nyuma (2015) kilichokuwa asilimia 5.6.

Amesema kuimarika kwa kiwango hicho kulichangiwa na mambo kama  kukua kwa biashara ya mafuta katika soko la kimataifa, kuwepo kwa uhakika wa chakula na sera madhubuti zinazotekelezwa na Serikali.

Hata hivyo, Dk Mpango amesema hali ya mfumuko wa bei iliongezeka na kufikia asilimia 6.4 katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ikichangiwa na ukosefu wa mvua.

“ Wananchi wengi waliingiwa na hofu kwamba kungekuwa na tatizo la ukosefu wa chakula hali ambayo ilisababisha kuwepo kwa ongezeko la mahitaji ya chakula,” amesema.

Hata hivyo, amesema kiwango hicho cha mfumuko wa bei kimeshuka kuanzia Mei na kufikia wastani wa asilimia 6.1.



Jezi ya Bocco Simba Yazua Kizaa Zaa..!!!!

$
0
0

JOHN Bocco alipokuwa Azam FC alikuwa akitumia jezi namba 19, lakini sasa ametua Simba ambapo jezi hiyo inatumiwa na kiungo mwenye uwezo mkubwa, Mzamiru Yassin, ambaye inadaiwa kuwa hataki kusikia akipokwa namba hiyo.

Mzamiru, ambaye amesajiliwa na Simba kutoka kwa Wakata Miwa wa Mtibwa Sugar, amekuwa akiitendea haki jezi hiyo yenye namba 19, kutokana na uwezo wake wa kusimama vema dimba la katikati, huku pia Bocco naye akifanya hivyo huko anakotoka.

Baada ya kusajiliwa Simba ndipo zikaanza kuzagaa taarifa kwamba huenda Straika huyo akakabidhiwa jezi aliyoizoea namba 19, lakini taarifa kutoka kwa watu wa karibu na Mzamiru zinadai kuwa, anaipenda jezi yake na hana mpango wa kuitoa kwa mtu mwingine.

“Sidhani kama Mzamiru atakubali kuachana na namba 19, kwani anaipenda sana, ngoja tuwaachie wenyewe, japo hakuna linaloshindikana kama wakikaa na kukubaliana,” alisema mchezaji mmoja wa Simba ambaye ni swahiba na Mzamiru.

DIMBA Jumatano lilikwenda mbali zaidi na kumtafuta Mzamiru, ambaye yupo kambini na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, nchini Misri, ambapo aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuiachia jezi hiyo.

“Ni ngumu sana kulizungumza hili jambo, kama nitaendelea kubaki basi haitakuwa rahisi kuiacha, labda niwe nimeondoka katika kikosi cha timu hiyo,” alisema kiungo huyo.

Hata hivyo, taarifa nyingine kutoka Simba zinadai kuwa, wamemuandalia Straika huyo ambaye ameifanyia makubwa Azam FC, jezi namba 29 kama Mzamiru akikomaa na namba 19.

“Tumemuandalia jezi namba 29, kama ataipenda na kuridhika, kwani inawezekana Mzamiru akakataa kuachia namba 19, nadhani hakuna kitakachoharibika,” alisema kigogo mmoja wa Simba.

Credit - Dimba

Ongeza Hips, Makalio, Mapaja, Miguu, Uume na Nguvu za Kiume , Punguza Unene, Kuwa na Mweupe Bila sugu na Products za Markson

$
0
0

ONGEZA HIPS, MAKALIO, MAPAJA, MIGUU, UUME NA NGUVU ZA KIUME. PIA KUPUNGUZA UNENE, KUWA MWEUPE BILA SUGU NA KUONDOA MADOA.
@Markson_beauty_pr Tunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa kiafya.
🍉🌿🍅🍍🍒🍉🍓🍅🍒
NB÷ Matokeo ni uhakika na garantii. Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
BIDHAA ZETU:-

1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @120,000/=
2. Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @ 150,000/=
3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-
(1)Mafuta @120,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a) Gely ya kupaka @130,000/=
(b) Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @130,000/=
(C)Handsome up original @200,000/=
6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @120,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula @120,000/=
8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/=
(b) Mkanda wa kawaida @100,000/=
(c) micro-computer belt wa umeme @170,000/=
9 .Kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @120,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @120,000/=
11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120,000/=
12.Kurudisha usichana (bikra) @120,000/=
Wasiliana nasi :- (+255)
0767447444au 0714335378
👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
Follow us on instagram @Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

Zitambue Hasara za Kuzama Chumvini Kwa Mwanamke

$
0
0

Tafiti zimeonyesha kuwa,mdomo wa binadamu ki bacteriologia (bacteriologically) ni mchafu maradufu kuliko sehemu ya uke(vagina).
Ni vema kufahamu kuwa,katika hali ya afya,binadamu wote tunaishi navimelea(microorganisms) katika sehemu nmbalimbali za miili yetu, wakiwa na lengo la kutulinda, kitaalamu wanaita normal flora hawa wanakuwa hawana madhara katika mwili.Hivyo ni kweli kuwa vagina kama ilivyo mdomo una normal flora. 


sasa baadha ya vitendo huweza kuondoa normal flora na kukaribisha magonjwa,mfano kinamama kujiosha ukeni na maji ya ndimu,limao,Shabu etc huweza kuondoa Normal flora na kukaribisha magonjwa,kama ambavyo matumizi ya sabuni zenye kemikali zinavoweza kuua normal flora kwenye ngozi na kusababusha magonjwa ya ngozi.Hivyo kwa mwanamke mwenye afya,uke ni mahali salama kufanya upendalo(kama vile kwenda chumvini).
Hata hivyo, nionye kuwa hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa kinywani kama vile Gonnorhea, Syphilis, candidiasis (fungus), HIV n.k ipo pale pale kama ambavyo mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya kawaida ya kujamiiana.
Mwisho, kama wewe ni mgonjwa wa kwenda chumvini, hakikisha unafanya mchezo huo nampenzi/mke aliye salama.

Mwenyekiti wa kijiji Atekwa Ikwiriri, Mwingine Aokotwa Mtoni

$
0
0

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kati, Ikwiriri, Athuman Mtoteka anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana akiwa  nyumbani kwake.


Mwenyekiti huyo ambaye anawakilisha chama cha Wananchi CUF, anadaiwa kutekwa jana kati ya saa moja na mbili usiku.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema  watu wasiojulikana walifika nyumbani kwake kwa miguu kisha kumchukua na  kwenda naye kusikojulikana.


Amesema taarifa za tukio hilo zilitolewa katika kituo cha Polisi Ikwiriri leo Alhamisi asubuhi na mkewe.


Lyanga ameeleza kuwa baada ya kutolewa kwa taarifa hizo kituoni hapo, Polisi tayari wamefungua jalada la uchunguzi dhidi ya tukio hilo.


"Tumepokea taarifa hizo toka kwa mkewe akielezea mumewe kuchukuliwa na watu wasiojulikana na kuondokanae kusikojulikana" amesema Lyanga.


Kadhalika taarifa toka kwa majirani wa mwenyekiti huyo zinaeleza kuwa waliwaona  watu watano waliofika nyumbani hapo wakitembea kwa miguu kisha kumkamata na kuondoka naye.


Katika tukio jingine, maiti ya mtu mmoja ambaye hajatambulika jina lake imekutwa ikielea ndani ya Mto Rufiji,  Kitongoji cha Ngwalo kilichopo katika Kijiji cha Mtunda A, wilayani Kibiti.


Kamanda Lyanga amesema uchunguzi wa daktari juu ya maiti hiyo ulionyesha marehemu alikuwa na jeraha moja kichwani lililotokana na kupigwa risasi.


Lyanga amesema marehemu alikuwa amefungwa kamba katika mikono yake yote na maiti hiyo  ilikuwa imeanza kuharibika  kutokana na kukaa majini kwa muda mrefu.


Amesema kutokana na maiti hiyo kuanza kuharibika waliuruhusu uongozi wa kijiji hicho kuizika jana Jumatano.


Amesema baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliiona maiti hiyo ikielea majini kwenye mikondo ya maji ya Mto Rufiji kisha kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji hicho nao waliotoa taarifa Polisi.


Kutokana na matukio hayo, Jeshi la Polisi mkoani Pwani kupitia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Onesmo Lyanga  limetoa wito kwa wananchi waishio katika wilaya za Kibiti na Rufiji kuchukua tahadhari dhidi ya vitendo vya mauaji yanayozidi kutokea katika wilaya hizi mara kwa mara.

Nchemba: Polisi Hawajazuia Chadema Kufanya Mikutano na Kuwapendelea CCM..!!

$
0
0

Akijibu swali la Mh Mchungaji Peter msigwa mbunge wa Iringa mjini amesema kwamba serikali haiwezi kjwapendelea CCM (Chama cha mapinduzi) na kuwazuia chadema ila tu tunataka sheria na utaratibu ufatwe.

Sheria zote zipo na kila chama kinatakiwa kujua hilo na sio kujiamulia tu kufanya kila chama kinatakiwa kuomba kibali cha kufanya mikutano ya hadhara na sio vinginevyo
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images