Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

SOMA Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato Cha Tano na Vyuo Vya Ufundi 2017

$
0
0
Matokeo Kidato cha Tano
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa.

Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.

Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.

Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.

Simbachawene alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.

Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.

"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.

Kuangalia majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa

==> BOFYA HAPA


EXCLUSIVE: Mchekeshaji Ebitoke aahidi kujitunza kwa ajili ya Ben Pol

$
0
0
Ebitoke
Moja ya story kubwa hivi sasa ambayo ina-make headlines ni kuhusu Mchekeshaji Ebitoke kuweka wazi akieleza hisia zake kuwa siku moja anatamani kuwa mke wa staa wa RnB Bongo Ben Pol.

Kwenye EXCLUSIVE Interview na Ayo TV na millardayo.com Ebitoke ameeleza kila kitu kuhusu anavyohisi kila anapomuona Ben Pol na namna alivyojiweka tayari kuwa mke wa staa huyo Bongofleva akidai kuwa hakuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote kwa ajili ya Ben Pol akisema ameumia baada ya kujua ana mtoto.

WABUNGE Wenye Hali Mbaya "Uchaguzi 2020"

$
0
0
Bungeni leo
"TATHMINI MAJIMBONI"

Mpaka tulipo fika sisi kama wananchi ni hakika kua tunaweza kutathmini hali halisi ya Utendaji wa Wabunge kwmye Majimbo yetu na hata Bungeni .

Embu kwa pamoja tujaribu kuyapitia majimbo ya wabunge ambao wapo kwenye Possibility kubwa ya kutokushinda tena 2020.
Na ni sababu vipi zitawafanya wabunge hao kupoteza majimbo yao ? .
Lengo.

1.Kuwapa Alert Wabunge husika kua active.(bado wana kamda)

2.Kuaanda watu wenye nia ya kugombania Ubunge 2020 kuyafahamu majimbo dhaifu mapema.

Ahsanteni.
By Mandella/JF

PEDESHEE Ndama Ahukumiwa Jela Kesi ya Kutakatisha Fedha

$
0
0
Pedeshee Ndama
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kulipa faini ya Sh200 milioni mfanyabiashara, Ndama Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng’ombe baada ya kulikubali na kutiwa hatiani katika shtaka la sita la kutakatisha dola za Marekani 540,000.

Akitoa hukumu hiyo jana Ijumaa, Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa amesema endapo mshtakiwa huyo atashindwa kulipa kiasi hicho cha fedha atatumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Hukumu hiyo ya shtaka la sita la kutakatisha fedha ilitolewa baada ya Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa kumsomea maelezo ya awali (PH) Ndama na kuyakubali maelezo yote yanayounda shtaka hilo la kutakatisha fedha, akapatikana na hatiani na kupewa adhabu hiyo.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili Msigwa aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa amekubali shtaka la sita la kutakatisha fedha na maelezo yanayounda shtaka hilo.

Hatuna kumbukumbu za nyuma za makosa dhidi ya Ndama ila ni rai ya upande wa mashtaka kuwa wakati mahakama ikitoa adhabu izingatie matakwa ya kifungu cha 13(a) cha sheria ya kuzuia utakatishaji fedha,” imesema hati ya hukumu.

Alisema pia mahakama ibebe dhana ya sheria hiyo ambayo lengo lake ni kuzuia makosa ambayo yanalenga kudidimiza uchumi wa nchi na uzito wa kosa ambalo mshtakiwa amelifanya.

Kwa upande wa Wakili Wabeya Kung’e anayemtetea mshtakiwa huyo kwa kushirikiana na Jeremiah Mtobesya, Kung’e aliiambia mahakama kuwa ni wazi mshtakiwa amekiri kosa baada ya kusomewa maelezo ya awali hivyo mahakama isitoe adhabu kali kwa mshtakiwa.

Aliiomba mahakama izingatie maombi yao kwa sababu mshtakiwa huyo hilo ndiyo kosa lake la kwanza, kitendo chake cha kukiri kosa kinaonyesha kusikitikia kosa alilolitenda na kwamba anayo familia ambayo inamtegemea ambao kwa kipindi cha mwaka mmoja ambacho amekaa ndani imepata shida kwa kukosa huduma yake.

Kwa kuzingatia kifungu cha 13(a) cha sheria ya kutakatisha fedha ni rai yetu mahakama tukufu isitoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa sababu amejutia kosa alilolitenda,” alisisitiza Kung’e. Hivyo Ndama alihukumiwa kulipa faini ya Sh 200 milioni ama akishindwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Juni 6, 2017 Ndama aliiomba mahakama akumbushwe shtaka, akakumbushwa na Wakili wa Serikali, Esterzia Wilson na akalikubali shtaka hilo.

Akisomewa maelezo ya awali mahakamani hapo, Ndama alikubali maelezo ya awali aliyosomewa ikiwamo nyaraka zilizotumika kufungua akaunti iliyotumika kuingizwa fedha hizo, hundi 18 zilizotumika kutolea fedha hizo, maelezo ya benki ‘bank statement’ na Swift massage.

Iwapo atakamilisha kulipa Sh200 milioni atakuwa huru kuendelea katika mashtaka matano mengine yanayomkabili mahakamani hapo ambayo upelelezi wake bado haujakamilika.

Ndama anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na atoe fedha taslimu kiasi cha Dola za Marekani 270,200 ambacho ni sawa na zaidi ya Sh600 milioni mahakamani hapo na mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

INASIKITISHA:Mwanafunzi wa Miaka 13 Abakwa Korongoni Hadi Kufa

$
0
0
Mwanafunzi Abakwa
Mwanafunzi  wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13 anayesoma Shule ya Msingi Kipanga wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, amebakwa hadi kufa na watu wasiojulikana, ambao waliutupa mwili wake korongoni.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benedict Mapujila alisema kitendo hicho cha kikatili ni cha juzi ya saa 11:30 kijijini humo . Alisema siku ya tukio hilo, mwanafunzi huyo wa kike aliondoka nyumbani kwao kama kawaida yake kwenda shule.

Hata hivyo, hakurudi tena kwao na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa wazazi wake, kwa kuwa hakuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani.

Wazazi wake walikuwa na wasiwasi mkubwa kwa binti yao kuchelewa kurudi nyumbani, hivyo waliamua kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji chao.

Viongozi hao wa kijiji na wananchi, walianza kumsaka binti huyo kwenye maeneo mbalimbali bila kukata tamaa.

Ilipofika saa kumi na moja na nusu ya jioni waliukuta mwili wa mwanafunzi huyo ukiwa umetupwa korongoni na kubaini kuwa alikuwa amebakwa huku sehemu zake za siri zikiwa zimeharibika vibaya,“ alisisitiza .

Alisema chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo wa kike, kilisababishwa na kuvuja kwa damu nyingi baada ya kufanyiwa ukatili huo na watu ambao hawajafahamika.

Kamanda huyo alisema hakuna aliyekamatwa kuhusu tukio hilo na jeshi la polisi linaendelea kusaka wahalifu hao.

Alisema baada ya kuufanyia uchunguzi wa kitabibu, mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maandalizi ya maziko yake.

KIMENUKA..Zari Aamuliwa Kuishi na Watoto Wake Katika Nyumba ya Marehemu Ivan...

$
0
0
Zari, Diamond na IVAN Don
KAMATI ya watu wanne walioteuliwa kushughulikia namna ambavyo mali za marehemu Ivan Ssemwanga zitasimamiwa, imempa mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zari Hassan, moja ya nyumba za marehemu huyo iliyopo nchini Afrika Kusini ili aishi na watoto wake.

Kwa mjibu wa mtandao wa Kenya moja, kamati hiyo iliwajumuisha Ritah Ssemwanga (dada wa Ivan), George Ssemwanga Pinto (kaka wa Ivan), Lawrence Kiyingi Muyanja maarufu King Lawrence (rafiki mkubwa wa Ivan) ambaye pia ni kiongozi wa kundi la matajiri wanaojiita (Rich Gang) na Zari Hassan (mke wa Ivan). Kwa pamoja kamati hiyo imekubaliana kwamba licha ya kumpa Zari nyumba hiyo, pia imempa madaraka ya kusimamia chuo cha Ivan cha Brooklyn, kilichopo Afrika Kusini.

Pia Zari ameamliwa kuishi na watoto wake katika moja ya nyumba za Ivan zilizopo Afrika Kusini na nyingine itapangishwa ili kusaidia familia hiyo kiuchumi, huku kamati hiyo ikiendelea na usimamizi wa jumla hadi watoto hao watakapofikia umri wa kujitambua wa miaka 18.

Kutokana na hilo, Zari ameondoka Uganda na kuelekea Afrika Kusini, ingawa bado haijajulikana kama ataishi katika moja ya nyumba za Ivan huko Pretoria, Afrika Kusini au ataishi na watoto wake kwenye nyumba ya mpenzi wake, Diamond Platnumz, aliyonunua jijini Johannesburg.

TOA MAONI YAKO HAPA

Mwanafunzi Darasa 6 Abakwa Hadi Kufa,,,!!!

$
0
0

MWANAFUNZI wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13 anayesoma Shule ya Msingi Kipanga wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, amebakwa hadi kufa na watu wasiojulikana, ambao waliutupa mwili wake korongoni.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benedict Mapujila alisema kitendo hicho cha kikatili ni cha juzi ya saa 11:30 kijijini humo juzi. Alisema siku ya tukio hilo, mwanafunzi huyo wa kike aliondoka nyumbani kwao kama kawaida yake kwenda shule.

Hata hivyo, hakurudi tena kwao na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa wazazi wake, kwa kuwa hakuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani. Wazazi wake walikuwa na wasiwasi mkubwa kwa binti yao kuchelewa kurudi nyumbani, hivyo waliamua kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji chao.

Viongozi hao wa kijiji na wananchi, walianza kumsaka binti huyo kwenye maeneo mbalimbali bila kukata tamaa. “Ilipofika saa kumi na moja na nusu ya jioni waliukuta mwili wa mwanafunzi huyo ukiwa umetupwa korongoni na kubaini kuwa alikuwa amebakwa huku sehemu zake za siri zikiwa zimeharibika vibaya,“ alisisitiza .

Alisema chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo wa kike, kilisababishwa na kuvuja kwa damu nyingi baada ya kufanyiwa ukatili huo na watu ambao hawajafahamika. Kamanda huyo alisema hakuna aliyekamatwa kuhusu tukio hilo na jeshi la polisi linaendelea kusaka wahalifu hao. Alisema baada ya kuufanyia uchunguzi wa kitabibu, mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maandalizi ya maziko yake.

Serikali Yaokoa Bilioni 53 Katika Rushwa...!!!!

$
0
0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kuokoa Sh bilioni 53.9 kutokana na uchunguzi na operesheni mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika mwaka 2016/2017.

Amesema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa mno, ikilinganishwa ni Sh bilioni 7 tu zilizookolewa katika mwaka 2015/2016. Alisema hayo jana wakati akifungua semina ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika walio katika Mapambano ya Rushwa (APNAC) Tawi la Tanzania kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma.

Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa, alisema Serikali imeanza kupata mrejesho mzuri kwamba watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo na vitendo vya rushwa vinaendelea kupungua.

“Baadhi ya hatua tulizochukua ni pamoja na kuimarisha taasisi yetu ya TAKUKURU; kuimarisha matumizi ya mashine za kielektroniki ili kupunguza mianya ya kupoteza mapato; kuanzisha mahakama ya mafisadi; kusimamia nidhamu katika utumishi wa umma na kuchukua hatua za haraka za kinidhamu na za kisheria dhidi ya watuhumiwa wote wa rushwa na ufisadi,” alisema.

Aliwaomba wabunge waendelee kuiunga mkono Serikali, kwani haina mzaha kwenye mapambano hayo. “Serikali haina mzaha kwenye mapambano dhidi ya rushwa na tutaendelea na mapambano hayo.

Hivyo, ninaomba waheshimiwa wabunge muendelee kutuunga mkono katika mapambano haya, twende kwa wananchi tukatoe wito kwao watuunge mkono kwenye vita hii,” alisisitiza.

“Tayari tumefanya tathmini na kubaini mianya ya rushwa katika sekta za ardhi, uchukuzi, biashara na maji na hivyo kuziba mianya hiyo. Tutaendelea kuiwezesha TAKUKURU ili iendelee na kazi nzuri waliyoianza ya kubaini mianya na kutoa ushauri wa kuziba mianya hiyo ya rushwa.

Lengo letu ni kuwekeza zaidi kwenye kuzuia, kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba”. Mapema, akizungumza katika semina hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alisema Takukuru kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini yake, wako njiani kuanzisha mtaala wa somo la rushwa ili ifundishwe tangu shuleni.

“Napenda kuwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba Serikali ya awamu ya tano haitakubali kuona rushwa ikiota mizizi. Tunaamini wanafunzi wakijengewa uwezo tangu utotoni, watachukia rushwa na hatimaye tutakuwa na Taifa lenye watu waadilifu,” amesema.

Alisema kutokana na kazi ya kupunguza watumishi hewa, hadi kufikia Aprili mwaka huu, Serikali imekwishapokea Sh bilioni 1.2 kwenye akaunti maalumu ya Takukuru iliyoko Hazina ambazo zinatokana na makusanyo kutoka kwa waliokuwa watumishi hewa.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Godfrey Mulisa alisema wataendelea kushirikiana na Bunge katika miradi mbalimbali ikiwemo shughuli zinazofanywa na APNAC.

Awali, Mwenyekti wa APNAC tawi la Tanzania, George Mkuchika alisema hadi sasa wabunge wapatao 148 wamekwishajiunga na mtandao huo. Kwamba anaamini hadi Bunge hili litakapomaliza muda wake, zaidi ya robo tatu ya wabunge watakuwa wamejiunga

Christian Bella Afunguka Ugonjwa Uliomfanya Alazwe Ghafla Congo..!!!

$
0
0

Baada ya wiki iliyopita kusambaa picha mitandaoni za muimbaji Christian Bella zikimuonyesha akiwa amelazwa hospitali nchini Congo na kuzua hofu kwa mashabiki wa muziki wake, muimbaji huyo amefunguka kuzungumzia kitu ambacho kilimsibu.

Akiongea Ijumaa hii, Bella amesema alikimbizwa hospitali baada ya kuishiwa nguvu ghafla.

“Namshukuru Mungu anaendelea vizuri, nililazwa kwa muda mfupi kutokana na uchovu lakini baada ya kufanyiwa vipimo nilikutwa nimechoka tu. Kwahiyo baada ya kupumzika niliruhusiwa lakini niliambiwa natakiwa nitenge muda wa kumpumzika kwa sababu nilikuwa na tour ya muda mrefu kwa hiyo mwili ulikuwa umechoka sana,” alisema Bella.

Muimbaji huyo ambaye ni raia wa Congo, kwa sasa amerejea nchini Tanzania kwaajili ya kuendelea na shughuli zake za muziki baada ya kuwa na tour kubwa ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kati.

Dully Sykes - Waganga Watamaliza Pesa Zangu..!!!

$
0
0

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Prince Dully Sykes amefunguka na kusema kwamba wasanii au watu wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji ili kufanikiwa wanaongozwa tu na tamaa na kutoridhika na kile wanakichopata

Dully amefunguka hayo alipokuwa kwenye  Planet Bongo ya East Africa radio ikiwa ni siku chache baada ya Meneja Maneno kufunguka na kudai wasanii wengi wanaaminmi ushirikina na kusema kwamba yeye hawezi kufanya hivyo kwani anaridhika na maisha yake kwa kila akipatacho.

“Mimi maisha yangu naridhika nayo japo si makubwa kiivyo, naridhika na kagari ambacho naendesha, naridhika na mahali ninapolaza ubavu wangu, naridhika na chakula ninachopata, 

ninaridhika na kipato ninachopata japo ni kidogo ila nagawana na wenzangu, watoto na familia,” amesema Dully Sykes.

Dully ameongeza kuwa “Sifikirii kama kuna mganga ambaye anaweza kufanya mimi nikapata hela zaidi ya hapa, sana sana watanimaliza hela zangu,” ameongeza.

Walimu 261 Arusha Wabainika Kuwa na Vyeti Feki..!!!

$
0
0

WAKATI mkoa wa Arusha ukiwa na upungufu wa walimu 788 sawa na asilimia 58.85 ya mahitaji ya walimu mkoani hapa, imebainika kuwa, walimu 261 wamebainika kuwa na vyeti feki.

Mkoa wa Arusha wenye shule za sekondari za serikali 162, una upungufu wa walimu 197 wa Fizikia, 243 wa Kemia, 85 wa Bayolojia na 263 wa hisabati. Kwa mujibu wa Ofisa Elimu-Taaluma wa mkoa wa Arusha, Eugene Shirima kazi ya kubaini walimu wenye vyeti feki mkoani humo imethibitisha kuwepo na walimu 261 vyenye vyeti feki hadi sasa wakiwemo walimu wa masomo ya sayansi na baadhi yao wamelazimika kujiondoa kazini.

Hata hivyo, Shirima amefafanua baadhi ya walimu wamelazimika kukata rufaa Baraza la Mitihani la Taifa na Idara ya Utumishi kupinga hatua ya kuwaondoa kazini. Amesema mbali na walimu hao kubainika kuwa na vyeti feki baadhi ya walimu wamelazimika kujiondoa wenyewe bila hata kutoa taarifa kwa mwajiri wao katika halmashauri za wilaya ama kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha.

BARAKA The Prince Aongoza Kwa Kukosa Heshima Kwa Wasanii Wenzake...List Aliyowakosea Adabu Hii Hapa

$
0
0

baraka The Prince


MOJA YA SIFA MUHIMU KATIKA MAFANIKIO NI NIDHAMU NA HASA KUHESHIMU WAKUBWA AMBAO WAMEKUTANGULIA.

Nadhani tunaweza muona msanii @barakahtheprince_ toka ameanza muziki tunakuwa tunamuona kama anaenda mbele kimataifa lakini mwisho wa siku anabaki hapa hapa.Sawa tuseme labda ngoma zake hazijawa na nguvu kwenda kimataifa ila nje ya hapo kuna maswala ya msingi ya kuangalia.

Nadhani moja ya kitu ambacho @barakahtheprince_ kitakuja kumfelisha ni kutowaheshimu wasanii wenzake ambao ni wakubwa kwake na hata wamemtangulia kwenye game.

@barakahtheprince_ ashawahi kuingia kwenye mzozo na @naytrueboy na kuongea mambo mabovu zaidi kwa ney lakini mwisho wa siku nay alikuja akaona huyu ni mtoto na akaepusha malumbano.

Lakini pia @barakahtheprince_ ashaingia kwenye mzozo na @msamibaby na alimtukana msami maneno mabovu lakini kumbe msami alichofanya alimtania tu kuhusu najma mwisho wa siku barakah akamtukana msami bila sababu.

Lakini ni @barakahtheprince_ huyu huyu leo anamuongelea maneno mabaya @iambenpol na kumuambia sijui katoa wimbo mbaya sijui kajidhalilisha.Kwa mtu kama barakah anatakiwa kumuheshimu benpaul mana kwanza ni kama kaka yake na pia kamtangulia kwenye game na bado uwezo wa benpaul ni mkubwa kuliko barakah na pia benpaul ni mtu mwenye nidhamu ambaye sikutegemea mtu kama barakah atamuongelea maneno hayo.

Ila ni huyu huyu @barakahtheprince_ ambaye alishindwa hata kumuheshimu msanii wa mkoa wake @youngkillermsodokii na kusema wazi hajawahi kuwa shabiki wake na wala hajawahi penda wimbo wake wowote ki hekima sio jambo zuri hasa ukizingatia anatoka naye mkoa mmoja.

Ila ni barakah huyu alimdhihaki @diamondplatinumz na kusema kuwa alijua simba ni mnyama mkali kumbe ni kamnyama kadogo tu kaoga akimlenga diamond sababu anajiita simba.

Haya yote ukiyaunganisha unagundu ndio msanii anaongoza kwa kutokuwa na nidhamu na wasanii wenzie.

SIKU ZOTE MSINGI MKUBWA WA MAFANIKIO NI NIDHAMU.UKIKOSA NIDHAMU HATA YULE ALIYEKUWA ANATAMANI KUKUSAIDIA ATAHISI BADAE UTAKUJA KUMKOSEA HESHIMA.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Siku ya Leo......

$
0
0

SASHA Akerwa Sauti Yake Kufananishwa na ya Wema Sepetu

$
0
0
Shasha Kassim
MWA­NA­MITINDO, Sasha Kas­sim ameibuka na kusema kuwa hapendi sauti yake kufananishwa na ya Wema Sepetu kwani inaanza kumletea matatizo am­bayo hakuyatarajia kwa maana ya usumbufu.

Wema Sepetu


Sasha alion­gea hayo baada ya kuandam­wa na watu aki­daiwa kuhusika na utengenezaji wa sauti iliyokuwa ikisambaa mtandaoni kitendo ambacho alikana kukifanya na kudai kuwa hana mazoea wala maisha hayo ya kujianika kwa kutafuta kiki.

Dah mimi sija­husika na sauti yoy­ote na wala sidhani kama sauti yangu inafanana kiasi hicho na Wema kwamba naweza ku­muigiza mimi si wa hivyo jamani ki­tendo cha kuhusishwa na sauti hiyo kimeni­kera na naomba watu waache mara moja,” alisema Sa­sha.

GPL 

CHID Benz Aibuka, Afunguka Mazito …Baada ya Kuacha Kutumia Madawa ya Kulevya

$
0
0
Chid Benz
BAADA ya Mwanamuziki Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ kupotea kwa muda mrefu kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, kufuatia kutopea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, hatimaye ameibuka na kufunguka mambo kibao.

Akizungumza na Risasi Jumamosi hivi karibuni, Chid Benz ambaye kwa sasa yupo jijini Dar akitokea Zanzibar alikokuwa amekwenda mapumzikoni baada ya kutoka mkoani Iringa alikokuwa kwenye kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya, amesema kwa sasa yupo fiti kiafya na kiakili na anachowaza ni muziki na maisha tu.

Hatarudia madawa Chid Benz aliendelea kufunguka kuwa anamshukuru Mungu kwa kumsaidia mpaka amefanikiwa kutoka ‘kuzimu’ kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya na kwamba hawezi kurudi nyuma wala kuthubutu kurudia kutumia dawa hizo za kulevya.

Kwanza sipendi kuzungumzia maisha niliyopitia nyuma. Kwa sasa nahitaji kuzungumzia muziki tu. Lakini kwa kifupi namshukuru Mungu kunitoa nilikokuwa na kunifanya mtu mwingine. Wakati ule nilikuwa sihitaji hata kuonana na watu kutokana na muonekano wangu lakini kwa sasa ninaonana na kila mtu,” alisema Chid Benz.

Amerudi nyumbani kwao Chid aliendelea kuongeza kuwa, tofauti na wakati wa nyuma alipokuwa anaishi mitaani kwenye ‘mageto’ ya washikaji zake, kwa sasa amerudi nyumbani kwao na anaishi na familia yake na maisha yametawaliwa na furaha.



Wakati natumia dawa za kulevya nilikuwa naishi kwenye mageto ya washikaji mitaa ya Kinondoni, sikuhitaji kukaa nyumbani kwa sababu mazingira hayakuwa r a f i k i k w a n g u katika kutumia madawa hayo,” alifunguka Chid na kuongeza kuwa; “Mama yangu kwa sasa anafuraha sana, lakini nina mpango wa kuiunganisha familia yangu pamoja, namaanisha watoto wangu ingawa katika hili naomba niishie hapa, nisiingie ndani zaidi maana si vizuri kuzungumza kila kitu.”

Alipokuwa Zanzibar alifanya nini? Akifunguka kuhusu maisha yake ya Zanzibar, Chid Benz alisema kuwa kikubwa ilikuwa ni kupumzika na kutumia muda mwingi kufikiria maisha yake, alikotoka na anakoelekea. Tofauti na hivyo alisema alikuwa anatembelea studio za washikaji zake wa zamani ambao alikuwa nao karibu kabla hajaingia kwenye matumizi hayo ya madawa ya kulevya. Kapika dude na Q-Chillah “Nimeingia studio pale Kill Records na kufanya kazi na mkongwe mwenzangu Q- Chillah ambayo itatoka soon.

Menejimenti yangu inajipanga kwa sasa juu ya kufanya video kali na kila kitu kikikamilika nitaachia ngoma hewani,” alisema Chid Benz.

Hata hivyo alipoulizwa juu ya nani anayemsimamia katika kazi zake kwa sasa Chid Benz hakutaka kuweka wazi kwa kudai kuwa, ana sababu maalumu za kufanya hivyo. Alipoulizwa kuhusu kufanya kazi na msanii mwenzake Shetta kutokana na video iliyoonekana kwenye mitandao ya kijamii wakiwa pamoja, Chid alisema: “Shetta ni mdogo wangu. Tulikutana tu na tukafurahi na kurekodi kile kividio, lakini hakuna kitu chochote kati yetu ambacho kinaendelea kama kazi ikiwepo nitafunguka pia.



Kila kitu kwenye maisha yake ni miujiza Chid alimalizia kwa kusema kuwa, kila kitu katika maisha yake ni mfano wa miujiza ama muvi na haamini kuwa ameweza kufanikiwa kuachana na unga na kuwa mtu safi. “Ni jambo la kumshukuru Mungu. Ilikuwa ni vigumu kuamini kuwa ningeweza kurudi kama nilivyo leo n a kumiliki tena usafiri na maisha yakasonga mbele, niseme tu mambo ya nyuma yamepita na sasa ninasonga mbele tu,” alimaliza Chid.

IMETIAMIA...Cristiano Ronaldo na Zidane Wanyakua Tuzo La Liga..

$
0
0
Cristiano Ronaldo na Zidane

Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Mei wa ligi ya Hispania (La Liga) huku Zinedine Zidane akishinda tuzo ya meneja bora.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 ameshinda tuzo hiyo, baada ya kufunga mabao matano katika michezo minne ya mwisho na kuisaidia Real Madrid kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa La Liga baada ya miaka mitano.

Zidane ametangazwa kuwa meneja bora wa mwezi Mei, baada ya kuiongoza Real Madrid kushinda michezo ya mwezi huo na kuwapiku wapinzani wake Barcelona kwenye mbio za ubingwa wa La Liga.

Wawili hao wanaendelea kuchagiza furaha ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid, ambayo iliendelezwa mwishoni mwa juma lililopita, kwa kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, kwa kuifunga Juventus mabao manne kwa moja.

SPORT Pesa Kuzifikiria Upya Yanga, Simba kwa Everton..

$
0
0

KAMPUNI ya bahati nasibu ya SportPesa imesema inafikiria uwezekano wa Simba na Yanga kucheza mechi dhidi ya timu ya Everton inayocheza Ligi Kuu England ili kutoa fursa kwa wachezaji wake kujiuza.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni hiyo, Abbas Tarimba alisema jana Dar es Salaam kuwa, ni jambo linalosikitisha timu za Tanzania kutolewa mapema katika michuano hiyo yenye dau kubwa zikionyesha wazi hazikuwa makini.

Timu za Tanzania zilizoshiriki michuano hiyo ni Yanga, Simba, Singida United na Jang’ombe Boys zilizoshindwa kutamba kwa timu za Kenya, Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker. Simba ilitolewa hatua ya mtoano kwa penalti 5-4 dhidi ya Nakuru All Stars baada ya kutoka suluhu dakika 90.

Singida United ilitolewa na AFC Leopards kwa penalti 5-4 baada ya sare ya bao 1-1. Yanga iliwatoaTusker mchezo wa kwanza kwa penalti 4-2 baada ya kutoka suluhu 0-0 lakini ikatolewa nusu fainali na AFC Leopards kwa penalti 4-2 zilipotoka 0-0.

Akizungumza uwezekano wa kuzisaidia Simba na Yanga kucheza na Everton, Tarimba alisema ni mapema mno kulisemea hilo lakini wataangalia cha kufanya. “Hatukutarajia timu zetu zingetolewa mapema. Kwa kweli imetushangaza.

Tumeshindwa kucheza kwa kiwango cha juu jambo ambalo limetuhuzunisha. Inawezekana kabisa hazikufanya matayarisho,” alisema Tarimba. Alisema wachezaji wenyewe hawakuwa makini kwani ni kama walichezea bahati.

Alisema huenda hazikufanya matayarisho mazuri ingawa zilipewa taarifa mapema. Alisema hakubaliani na visingizio vya timu hizo kuwa wachezaji wao walikwenda kujiunga na timu ya Taifa, Taifa Stars kujiandaa na mechi ya AFCON dhidi ya Lesotho inayoanyika Chamazi, leo usiku.

Alisema hata Gor Mahia ina wachezaji wengi wanaocheza timu ya taifa Kenya na bado waliopo walicheza kwa kiwango cha juu na kufunga magoli katika mechi zao. Tarimba alisema ni Singida United tu iliyothubutu kufunga goli lakini si Simba, Yanga wala Jang’ombe iliyoweza kufanya hivyo zikionyesha udhaifu katika ufungaji.

Alisema lengo lao ni kusaidia soka la Tanzania na hasa wachezaji kufika mbali ndio maana walitoa fursa ya michuano hiyo ili wachezaji waitumie kuonyesha uwezo. Timu zilizotinga fainali ni Gor Mahia na Leopards zote za Kenya ambazo kesho zitacheza fainali na atakayeibuka bingwa atacheza na Everton Julai 13, mwaka huu.

JAKAYA Kikwete Alia Uhaba wa Soko la Mananasi..Adai Wakulima Akiwamo Yeye Wanadhulumiwa na Wateja..

$
0
0
Jakaya Kikwete Akiwa Shambani Kwake

 Rais mstaafu, Jakaya Kiwete amezungumzia shughuli za kilimo anazozifanya huku akianika changamoto mbalimbali zinazomkabili.

Akizungumza jana Ijumaa muda mfupi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani hapa, amesema ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.

"Nilianza kilimo miaka mingi sana na mpaka nastaafu nilikuwa naendelea na kilimo, lakini changamoto kubwa katika kilimo ni suala la palizi hususan haya mananasi unaweza palilia zaidi ya mara tatu," amesema.

Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.

"Hata kama viwanda vitajengwa kwa wingi lakini ili mkulima apate faida ya juu ya kilimo hasa cha mananasi ni lazima kuwe na bei nzuri, lakini kama wanunuzi watakuwa wananunua bei isiyo na masilahi hakutakuwa na maendeleo kwa wakulima,"amesema.

Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.

Chanzo: Mwananchi

TID Aiomba Serikali Imnunulie Vyombo vya Muziki Apambane na Watumia Madawa ya Kulevya

$
0
0
Mwanamuziki TID

Amesema vyombo vya band yake vya awali alivinunua kwa shilingi milioni 18 lakini kwa sasa hana uwezo. Hivyo anamuomba MTU yeyote mwenye mapenzi mema ikiwemo serikali waweze kumsaidia. Amesema atatumia vyombo hivyo kupambana na vita ya utumiaji madawa ya kulevya akilenga kuielimisha jamii kupitia muziki.Source Mahojiano mubashara TBC tv

JE, Wanaoshangilia na Kupongeza Bajeti Wanajua Wanashangilia Nini?

$
0
0

Kwanza naomba na mimi nianze kwa kuipongeza bajeti na kuishangilia kwasababu tuu watu walipiga makofi, as when you are in Rome, lakini naomba kukiri kuwa mimi sio mchumi, hivyo sijui hata watu walikuwa wakishangilia nini!. Hivyo nimekuja hapa na swali kuhusu bajeji ambalo haliko based kiuchumi bali ni swali kuhusu failures za utekelezaji wa bajeti tunazopanga kwa kutumia kitu kinachoitwa a common sense logic.

Tangu kutangazwa kwa bajeti mpya ya serikali, nime note watu wengi wakiishangilia na wakipongeza bajeti hii, mimi ambaye sio mchumi ninajiuliza hivi washangiliaji hawa wanajua wanashangilia nini au wanapongeza nini? . Unawezaje kuishangilia bajeti mpya kubwa kuliko bajeti ndogo iliyotangulia ambayo imeshindwa kutekelezwa?!. Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, ukitokea wengi wa washangiliaji wakawa hawajui wanashangilia nini, ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia ujinga?. Yaani itoke bajeti hewa ya kwanza ishindwe kutekelezwa halafu inaletwa bajeti kubwa zaidi halafu watu wanashangilia?!. Wachumi wetu humu tusaidieani akina sisi tusiojua uchumi kwa kutuelimisha kuhusu bajeti hii, ili kama ni kuishangilia, tujue tushangilie nini?.

Naunga mkono kwenye mazuri kupongeza hivyo ni haki ya wabunge kupongeza mazuri yaliyoletwa katika bajeti hii, lakini kama hatujiulizi pale tuliposhindwa tulishindwa nini na badala yake kuja na bajeti mpya kubwa zaidi bila mipango madhubuti ya kuonyesha tutapata wapi fedha za kuitekeleza, huku kuishangilia bajeti nakuita ni kuishangilia ujinga!.

Namalizia kwa kulirudia hili swali la msingi la uzi huu,;Jee Wanashangilia Bajeti, Wanajua Wanashangilia nini au ndio yale yale ya Kushangilia Chochote Bungeni.

Keshokutwa Jumatatu, wabunge wetu wanaanza kuchangia bajeti, natoa rai kwa Bunge letu tukufu kuruhusu matangazo ya moja kwa moja wakati wabunge wakijadili bajeti, kama waliweza kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya bajeti, pia tupate fursa ya kuwasikia wawakikishi wetu wakichangia bajeti hiyo hivyo kututendea haki sisi wananchi

Jumamosi njema
Paskali
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images