Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Kifungu cha 9(3) cha Sheria ya Madini (2010) ni Msumari wa Moto Lakini Wala Hakikutajwa na Kamati ya Pili ya Mchanga wa Madini...!!!!

$
0
0

Labda tujiulize hivi kwanini kamati ya pili haikujiridhisha na kifungu cha 9(3) cha sheria ya madini ya mwaka 2010?

Kifungu tajwa kinamwondelea Mchimbaji wa madini aliyesajiliwa uhaja wa kusajili tena kampuni tanzu katika kufanya kazi za uchimbaji, usafirishaji wa madini.

Kwa lugha rafiki, baada ya African Barrick Gold Ltd kusajiliwa kuwa ni mmiliki wa North Mara Gold mine Ltd, Bulyanhulu Gold mine Ltd na Pangea Minerals Ltd ambapo migodi yote imesajiliwa hawakuwa na uhaja tena wa kusajili kampuni tanzu yake ya Acacia.

Sasa sijui walimeza maharagwe ya wapi hii kamati ya pili ya Makinikia kudai Acacia ilipaswa isajiliwe wakati sheria ya madini (2010), kifungu na. 9(3) kinawazuia wasisajili tena kampuni tanzu.

Chanzo JF

Ukweli Huu Hapa...Acacia Iliwahi Kuhukumiwa kwa Kosa la Kuiibia Serikali ya Tanzania Lakini Haikulipa Hata Sent Moja..!!!

$
0
0

Kampuni ya BARRIC iliwahi kuhukumiwa kuhusika katika ukwepaji wa kodi ya takribani $40-million usd kwa kile kichobainishwa na mahakama kama a “sophisticated scheme of tax evasion” 
Katika kipindi cha mwaka 2010 - 2013 kampuni ya BARRIC iliwalipa wanahisa wake zaidi ya $400-million kama gawio,lakini kampuni hiyo haikuilipa serikali ya Tanzania kodi yoyote kwa madai ya kupata hasara.The tribunal ordered the company to pay $41.25-million in taxes to the Tanzanian government.

Barrick Gold subsidiary evaded Tanzanian taxes, tribunal rules.

GEOFFREY YORK
JOHANNESBURG — The Globe and Mail
Published Tuesday, Apr. 05, 2016 5:50PM EDT

The African subsidiary of Barrick Gold Corp. has engaged in a “sophisticated scheme of tax evasion” to dodge more than $40-million (U.S.) in corporate taxes, a Tanzanian tribunal has ruled.

The tribunal, headed by a High Court judge, said the subsidiary of the Toronto-based company had failed to pay any corporate taxes in Tanzania from 2010 to 2013 while still paying more than $400-million in dividends to its shareholders from its gold-mining profits in the East African country.

The tribunal ordered the company to pay $41.25-million in taxes to the Tanzanian government.

The ruling is the latest sign of growing scrutiny of the tax arrangements of foreign investors worldwide, including Canada’s mining companies. The leaked documents known as the Panama Papers are another example of the mounting controversy over alleged tax avoidance.

The Barrick subsidiary said it would appeal the tax ruling to Tanzania’s highest court, calling it a “fundamentally flawed” decision. It denied any wrongdoing, and said it was merely following the terms of its investment agreement with the Tanzanian government.

The London-based subsidiary, formerly known as African Barrick Gold (ABG) and now known as Acacia Mining, is the biggest mining company in Tanzania and operates three major gold mines there.

The Tax Revenue Appeals Tribunal, in a ruling on March 31, said the company’s explanation for its lack of corporate tax payments was “far from plausible.” It accepted the government’s argument that the company’s transactions were “aimed at tax evasion.”

It noted that the company’s three Tanzanian gold mines were its only source of profits for the dividend payout.

“Ultimately, the fact that none of ABG’s subsidiaries is declaring any profit that could provide its holding company with such huge net profits sufficient to distribute to its shareholders four years in a row is what in our respectful opinion constitutes the evidence of a sophisticated scheme of tax evasion,” the tribunal said.

The tribunal’s ruling has sparked much publicity in Tanzania, adding to the growing concerns about foreign miners. “Mining companies have long been suspected of being tax cheats, causing the government to get less than its fair share of revenues from the sector,” one Tanzanian newspaper, The Guardian, said on Monday.

But the Barrick subsidiary sees itself as the victim of a flawed understanding of its tax agreements. It calculates that it has invested about $3-billion in Tanzania and it says the government has agreed that this investment can be deducted from its corporate taxes.

It believes it will be another three years before its corporate tax obligations will outweigh its remaining deductions from those investments. But as a goodwill gesture last month, it agreed to make an advance payment of $20-million on its future corporate tax obligations “to demonstrate our commitment to Tanzania.”

It says it has paid a further $372-million in other taxes and royalties over the past three years.

“Acacia and its subsidiaries fully comply with all international and domestic tax legislation and have not and never will undertake any form of tax evasion or tax avoidance schemes,” the company said on Tuesday in response to the tribunal’s ruling.

Jamie Kneen, a researcher at Ottawa-based civil society group MiningWatch Canada, said many governments in Africa are becoming convinced that the taxes paid by mining companies are insufficient.

“The whole mining sector has been increasingly under the microscope around the world as the public realizes how little it contributes to public accounts in exchange for depleting non-renewable resources and leaving behind massive public liabilities in health and the environment,” he said.

“Tanzania is just one of many countries where tax holidays, sweetheart deals with mining companies and tax evasion have been the subject of heated debate.”

Canada, indeed, has pledged to tackle tax avoidance in the mining sector. In 2013, the federal government promised to help Tanzania and other developing countries to improve their tax-reporting and royalty-collecting systems in the mining and energy sectors.

TAYARI WALISHAHUKUMIWA MWAKA MMOJA ULIOPITA,WANAENDELEA KUKATA RUFAA ZISIZO ISHA HAWATAKI KUUKUBARI UKWELI.
MAGUFULI ALIKUWA ANATAFUTA PA KUANZIA.

Kumbukumbu: Ni Kipi Kiliwafanya Barrick(Acacia) Kumpa Mkapa Kinyago cha Dhahabu..!!!?

$
0
0

Wakati akiwa madarakani alipotembelea mojawapo ya mgodi wa Barick gold mine alipewa kinyago cha dhahabu. Ni kipi kiliwafanya Barick kumpa zawadi ile ya kinyago cha dhahabu Mkuu? Je Mkulu aliwafanyia nini hawa jamaa mpaka wakampa zawadi ya thamani kiasi hicho?

Tuache siasa tuongee ukweli tupu.

Chanzo JF

Kwa Kupitia Ibara ya 46(3): Jakaya Kikwete Anaweza Kushitakiwa Vizuri Tu..!!!

$
0
0

Nimeona kwenye mitandao ya kijamii  baadhi ya wachangiaji wakimdhihaki Tundu Lissu kwamba anachemka kusema Kikwete ahojiwe. Wapingaji hawa wanashangaa uanasheria wa Tundu Lissu kwamba iweje hajui kama Kikwete ana kinga. Tundu Lissu. Wabongo wavivu kusoma, naomba niweke Ibara ya 46 na Ibara ndogo zake tujadili namna ya kumdaka Jakaya Kikwete


46.-(1) During the President’s tenure of office in accordance with this
Constitution it shall be prohibited to institute or continue in court any criminal proceedings whatsoever against him.

(2) During the President’s tenure of office in accordance this Constitution, no civil proceedings against him shall be instituted in court in respect of anything done or not done, or purporting to have been done or not done, by him in his personal capacity as an ordinary citizen whether before or after he assumed the office of President, unless at least thirty days before the proceedings are instituted in court, notice of claim in writing has been delivered to him or sent to him pursuant to the procedure prescribed by an Act of Parliament, stating the nature of such proceedings, the cause of action, the name, residential address of the claimant and the relief which he claims.

(3) Except where he ceases to hold the office of President pursuant to the provisions of Article 46A(10) it shall be prohibited to institute in court criminal or civil proceedings whatsoever against a person who was holding the office of President after he ceases to hold such office for anything he did in his capacity as President while he held the office of President in accordance with this Constitution.

UFAFANUZI
Ibara hii inazungumzia Kinga anayopewa Rais. Ibara ya 46 ibara ndogo ya 3, inasisitiza hatashitakiwa kwa makosa aliyofanya katika kipindi akiwa Rais na si vinginevyo. Hivyo Kikwete anaweza kudakwa kwenye makosa aliyofanya akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

NYONGEZA
Kwa hiyo hata kwa katiba hii,hata Rais Magufuli akitolewa madarakani 2020 tunaweza kumuundia kamati na kumshitaki kwa makosa ya MV Dar es Salaam na uuzwaji wa nyumba za serikali.

MY TAKE
Nadhani Magufuli hakujua kama wale ''wahuni'' kina Tundu Lissu watamfikisha huku, matokeo yake anaweza kurudi nyuma ikawa kama zile kamati zingine zilizopita

Zitto: Wabunge wa CCM Akiwemo Magufuli Waliniadhibu kwa Kuibua Sakata la Madini Mwaka 2007..!!!

$
0
0

Zitto Kabwe akihojiwa na Azam Tv amesema ripoti kamati iliyoongozwa na Prof. Osoro iliyowakilishwa kwa Magufuli haina mapendekezo mapya tofauti na kmamati ya Jaji Bomani ya Mwaka 2008 ambayo yeye alikuwa ni mjumbe pia wa kamati hiyo, tofauti ya sasa na kipindi kile ni rais kuthubutu kufanyia kazi mapendekezo hayo

Pia amesema mwaka 2007 aliibua suala hilo bungeni ila aliambiwa anakimbiza wawekezji ni mchochezi na akaadhibiwa kutohudhuria vikao vya bunge Magufuli akiwa ni mmoja wa watu waliomuadhibu

South Africa Wanataka Kubadili Jina la Nchi Yao..Wanataka Nchi Yao Iitwe Azania..!!!

$
0
0

Habari iliyopo South Africa ni kwamba wanataka kubadilisha jina la nchi yao, wakidai jina South Africa sio jina bali linaeleza mahali nchi ilipo katika bara la Afrika. Kimsingi wanasema South Africa ni nchi ambayo haina jina.

Wanasema kwamba walipaswa waige mfano wa nchi kama Zimbabwe na Namibia, zilizobadili majina mara baada ya kupata uhuru.

Wazo hili limekuwa likiungwa mkono na vyama mbalimbali vya siasa nchini humo, na maoni ya ANC, chama tawala nchini humo, ni kwamba linapaswa kujadiliwa rasmi katika ngazi za juu za chama.

Kumekuwa na mapendekezo na upendezi kwamba South Africa ibadili jina na kuitwa Azania, jina ambalo huko nyuma lilitumika na vyama kama Pan African Congress (PAC).

Ikiwa South Africa itabadili jina na kuwa Azania, basi itazidi kufanana na Tanzania katika jina, bendera na wimbo wa taifa. Sijui hili limetokeaje.

Source: The Mercury, South Africa

Breaking News... Habari Zilizotufikia Muda Huu Zinasema Kwamba.....!!!

$
0
0

Ndani ya Saa chache au siku mbili au tatu tu zijazo Mchezaji mahiri wa Kiungo wa Yanga FC Haruna Niyonzima anategemea Kusaini kandarasi ya kuichezea Klabu ya Simba SC kwa miaka miwili ( 2 ) kwa ada ambayo itavunja rekodi nchi nzima.

Nawasilisha.

Picha: Watu Wafariki, Wanasa Kwenye Jengo Linalowaka Moto London

$
0
0

 Jengo hilo liliteketea kutokana na kile kilichodaiwa friji bovu, japokuwa kikosi cha zimamoto hakijathibitisha ripoti hiyo.

WATU kadhaa wamethibitika kufariki baada ya moto mkubwa kutokea usiku wa manane katika jengo moja magharibi mwa Jiji la  London, Uingereza, ambao unasemekana ulisababishwa na friji mbovu.

Familia zinazokaa katika jengo hilo, zilisikika zikipiga kelele kuomba msaada, wakati wengine wanenasa sehemu mbalimbali ndani ya jengo hilo lenye ghorofa 27 linaloteketea na kutishia kuanguka.

Zaidi ya wakati 600 jengoni humo walijaribu kujiokoa ambapo huduma za magari ya wagonjwa zimesema watu 50 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali za jiji hilo.

Habari zaidi zinasema watu walionasa ndani yake walifunga mashuka yao na kuyatumia kama kamba na kujirusha kupitia madirishani ili kujiokoa.

Mashuhuda wamesema waliwaona watu wengine wakiruka kutoka kahtika ghorofa ya 15 ili kujiokoa na wengi wao wakipiga kelele huku vikosi vya waokoaji vikiwatoa wengine katika miali ya moto.

Wakazi zaidi ya 600 waliokuwa wakiishi katika jengo hilo walijaribu kujiokoa kwa njia mbalimbali.
Tukio hilo la moto limeelezwa kuwa ni kubwa zaidi ambalo halijawahi kutokea jijini London katika miaka ipatayo 30 iliyopita






Wameumbukaa..Lissu na Wenzake Waliokuwa Wanampinga JPM Wameumbuka Baada ya Ujio wa Bosi wa Barrick Mabye Amekiri Makosa na Kuhaidi Kulipa Tanzania Mabilion ya Fidia..!!!

$
0
0
Rais John Pombe Joseph Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton Ikulu jijini Dar es salaam. Katika mkutano huo, uliohudhuriwa pia na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles umemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo pande zote zimekubaliana kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya madini. Habari kamili yaja punde




ACACIA waelezea usajili wao

$
0
0

KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Acacia, imesema kuwa inafanya kazi nchini kwa misingi ya sheria na Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CMSA) inatambua uwepo wake.

Kauli hiyo imekuja baada ya juzi taarifa ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa mchanga wa madini katika makontena yalizuiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi, kubainisha kuwa kampuni hiyo haina kibali na inafanya kazi kinyume na sheria.

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jana pia imesema kuwa Acacia itafanya mkutano na wanahisa wake kesho kutoa ufafanuzi zaidi juu ya sakata zima.

Kampuni hiyo ilieleza kuwa migodi yake ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inaendeshwa kisheria.

“Acacia inapenda kuthibitisha kwamba inaendelea kufanya kazi katika migodi yake mitatu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.

“Migodi hii yote inamilikiwa na kuendeshwa na makampuni ambayo yamesajiliwa Tanzania kisheria; Bulyanhulu Gold Mine Limited, Pangea Minerals Limited na North Mara Gold Mine Limited ambayo yana leseni maalumu kwa kila mgodi,” inasomeka sehemu ya taarifa katika tovuti ya Acacia ambayo gazeti hili iliiona jana.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza: “Kampuni hizi zinamilikiwa na Acacia ambayo imesajiliwa nchini Uingereza ingawa umiliki huu si wa moja kwa moja (indirectly owned).

“Muundo huu ni wa uwazi, upo kisheria na huwekwa wazi katika taarifa zetu za hesabu za mwaka ambazo hukaguliwa kwa mujibu wa taratibu za kimataifa.”

Taarifa hiyo iliendelea kufafanua kwamba utaratibu huo wa umiliki uliwekwa wazi kwa CMA wakati Acacia ikijioredhesha katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) mwaka 2011.

“Muundo huu ni sehemu ya taarifa ambayo ilipitishwa na CMSA kwa ajili ya kujiorodhesha DSE. Tangu kujisajili DSE kilichobadilishwa ni jina la Acacia kutoka African Barrick Gold Plc kuwa Acacia Mining Plc,” inasema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Acacia wametangaza kufanya mkutano na wanahisa wake kwa mtandao kesho kutoa ufafanuzi zaidi juu ya sakata zima.

Walipofuatwa DSE kutoa maelezo ni kwa vipi kampuni ambayo haina usajili kuweza kujiorodhesha na kuuza hisa, walisema wao si wasemaji kwa kuwa mchakato wa kujiorodhesha huongozwa na kusimamiwa na CMSA na hivyo kumshauri mwandishi awasiliane nao.

Mwandishi alipowasiliana na  Ofisa Habari wa CMSA, Charles Shirima, alisema mtu aliyekuwa akishughulikia suala hilo alikuwa safarini Dodoma na kumtaka mwandishi awasiliane naye leo.

John Heche: Ndege za ACACIA kupigwa mawe

$
0
0

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amefunguka na kusema kwa kuwa Rais Magufuli kupitia ripoti ya pili ya mchanga amesema kampuni ya ACACIA ni feki na haipo basi yeye anawaambia wananchi wa jimbo lake wajiandae kuingia mgodini kuchukua kila kitu.

Heche amesema hayo bungeni jana na kudai kuwa atasimamia zoezi hilo na kuhakikisha kuwa ndege za kampuni hiyo zikitua mgodini kwa ajili ya kubeba madini basi zinapigwa mawe kwa kuwa wananchi wa jimbo lake la Tarime ambapo hiyo migodi ipo wameumizwa sana kusikia hiyo kampuni inayochukua mali zao ni feki na hewa.

"Kampuni ile ya ACACIA Rais amesema feki na hakuna 'formula' ya kukamata mwizi mlisema wenyewe, formula ya kukamata mwizi ni kupambana naye sisi hatutaruhusu madini yatoke pale ndege ikitua itapigwa mawe, magari yao tutayakamata kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime. Mhe. Spika sisi tulitegemea Mhe.

Rais aseme madini yasiondoke nchini mpaka mambo hayo yote yapitiwe, tutazuia mchanga madini yanaondoka. Rais amesema ACACIA ni mwizi wewe unataka utaratibu wa kukamata mwizi Tarime, sisi watu wetu wameumia sana na maji ya sumu, ng'ombe wamekufa, watu wamepigwa risasi kwa mujibu wa ripoti ya Waziri wa Nishati na Madini watu wa Tarime zaidi ya 64 wameuawa pale mgodini" alisema Heche

Mbali na hilo John Heche amesema kuwa kama serikali itamkamata kwa maamuzi ambayo atafanya basi Watanzania watajua kuwa serikali haipo tayari kupigana vita hii ya kupigania rasilimali za nchi hii, hivyo amewataka watu wa jimbo la Tarime wajiandae na kuanza maandalizi ya kupigania rasiliamali zao ili waone kama serikali itapeleka jeshi la polisi kulinda mali za wezi hao.

JISAJILI USHINDE GARI LA BUREEEEE KABISA

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote... Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...

CHAKUFANYA NI Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Bonyeza Hapa >>> SHINDA GARI YA BURE <<< Kujisajili ni Bure tu...

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Bunge Latoa Azimio La Kuitaka Serikali Ichukue Hatua KALI Kwa Wahusika Wote wa Mikataba Mibovu ya Madini..!!!

$
0
0

Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaothibitika kuhusika kuliingizia Taifa hasara na kuwakosesha Watanzania fursa ya kufaidika na rasilimali za madini.

Hoja hiyo imetolewa leo Jumatano bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana na Spika Job Ndugai kupata maoni ya namna Bunge linavyoweza kuunga mkono juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais John Magufuli kukabiliana na udanganyifu unaofanywa kwenye sekta hiyo.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika baada ya kukamilisha taratibu zote, imetoa maazimio matatu ambayo yamepitishwa na Bunge.

"Bunge linamuunga mkono Rais John Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha juhudi hizi hazipotei bure na sekta ya madini inachangia maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla," amesema Mkuchika.

Kukubaliana na kinachofanywa na Rais Magufuli maazimio matatu yametolewa ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono kwa hatua anazochukua, kumhakikishia ushirikiano wakati wowote atakapohitaji na kushauri kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kushiriki kulitia taifa hasara kutokana na kuidhinisha mikataba mibovu na wizi uliofanywa.

Beaking News..Mzee Akilimali Ajitokeza Kuwania Uenyekiti wa Yanga..Awataka Wanayanga Waachane na Kumpigia Magoti Manji..!!!

$
0
0

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu ya hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.

Hivi karibuni Manji alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo ili aweze kupumzika kutokana na matatizo mbalimbali aliyokumbana nayo siku chache zilizopotia.

Lakini pia maamuzi hayo ya Manji  yalikuja ikiwa ni muda mfupi tu umepita tangu alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka 10, lakini akakukumbana na changamoto kibao kutoka kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo na kuamua kusitisha mpango wake huo.

Akilimali alisema anaamini amefikia uamuzi huo ili aweze kuleta mabadiliko makubwa ya ndani ya klabu hiyo kuanzia pale Manji alipoishia.

Alisema licha ya kutokuwa bilionea kama ilivyokuwa kwa Manji lakini anaamini kwa kutumia utajiri wake wa hekima na busara alizonazo ataiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, kwa hiyo amewataka wanachama kutulia.

“Manji keshaondoka Yanga akapumzike kutokana na matatizo yaliyompata hivi karibuni kwa hiyo siyo vizuri kuanza kuumiza vichwa kuwa mambo yatakuaje bila ya yeye.

“Yanga ni timu kubwa, jina lake na nembo yake tu chanzo kikubwa cha kuingizia mapato endapo atapatikana kiongozi mwenye uchungu na maendeleo ya Yanga na asiwe mpigaji.


“Kwa hiyo, katika uchaguzi ujao ambao utafanyika ili kuziba nafasi iliyoachwa na Manji, nitagombea nafasi hiyo kwani uwezo wa kuipa Yanga mafanikio ninao,” alisema Akilimali.

Mayanga Aita Wachezaji 22 wa Taifa Stars kwa Ajili ya Michuano ya Kombe la Cosafa..!!!

$
0
0

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga, leo Jumatano Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, inatarajiwa kuanza kambi rasmi kesho Jumapili Juni 18, mwaka huu. Kambi hiyo itakuwa kwenye Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu. Michuano hiyo, inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania - mwanachama wa Cecafa, imepata mwaliko kushiriki.

Tanzania imepangwa kundi A ambako wapinzani wake ni Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.

Kwa mujibu wa Mayanga, kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Salum Manula  (Azam FC), Benno David Kakolanya  (Young Africans SC) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Salum Kapombe    (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young Africans SC) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans FC).

Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.

Kadhalika wako viungo wa kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).

Katika safu ya ushambuliaji wamo Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).

Imefichuka...Jakaya Kikwete Kama Waziri wa Nishati na Madini Alishasafishwa na Ripoti ya 2 ya Tume ya Uchungizi wa Madini,Ushahidi Huu Hapa...!!!!!!

$
0
0

I love this country!!!

Kwa bahati mbaya sana siku inasomwa Ripoti ya 2 sikupata fursa ya kuisikiliza!! Anyway, labda niseme sikutaka kuisikiliza! Binafsi huwa nasubiria ripoti kamili ili niisome kituo kwa kituo!!!

Baada ya kuisoma ripoti hiy kituo kwa kituo, nikagundua kwamba, wakati tunafikiria JK nae ana hatia kwa kusaini hiyo mikataba kama Waziri wa Nishati na Madini, kumbe Ripoti ya Profesa Osoro ilishamsafisha kitambo!!!!

Sehemu ya 5 ya Ripoti ya Profesa Osoro (Ripoti ya 2) inazungumzia Mikataba ya uchimbaji madini (Mining Development Agreements-MDAs).

Kipengele hiki kinaanza kwa kusema:
Mheshimiwa Rais,

Mikataba ya uchimbaji wa madini inafanyika chini ya kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini, Sura 123. Kwa mikataba iliyoingiwa mwaka 1994, mikataba hiyo ilifanyika chini ya kifungu cha kifungu 15 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1979 na kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 .
Hiyo mikataba ya 1994 ndiyo ambayo ilisainiwa na JK!!!

Na kwa maana nyingine, Profesa Osoro na timu yake ni kama wanataka kutuambia tusimsumbue sumbue JK kwani yeye alisaini kwa kutumia sheria ya Nyerere isiyo ya kifasadi!!

Nadhani hiyo wakaona haitoshi, wakaamua kumpamba lakini bila kumtaja jina! Hawa hapa tena:
Mgodi wa Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Kahama Mine Corporation Limited). Katika mkataba huu, Waziri wa Nishati na madini kwa jitihada kubwa alifanikiwa kujadiliana na kampuni hii na kuiwezesha Serikali kupata asilimia 15 za hisa katika kampuni za uchimbaji. Hata hivyo, mkataba huoulifanyiwa marekebisho mwezi Juni, 1999 na kusainiwa na Waziri wa Nishati na Madini aliyefuata, Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda.

Hapo Profesa Osoro naona anajaribu kutuambia ni namna gani waziri asiye na jina jinsi alivyokuwa "ame-figh"t kweli kweli kuhakikisha serikali inapata 15%!!!

Katika hali ya ajabu kabisa, akaja waziri mwingine ambae ametajwa LIVE kwamba ni Dr. Abdallah Kigoda! Huyu bila kujali "fight" za waziri asiye na jina akaamua kuhujumu "struggles" za waziri waliyeshindwa kumtaja!!!

Itoshe tu kusema kwamba, mawaziri wooooooooooooooooote waliopita nishati including Muhongo wa juzi juzi; hawa wametajwa kwa majina yao kasoro waziri mmoja tu... aliyesaini mkataba wa Bulyanhulu!!!

Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, ni JK ndie alisaini mkataba wa Bulyanhulu (am ready to be corrected). Kwahiyo waziri asiye na ajina ambae ali-struggle kweli kweli ni JK!!!!

Shikamoo JPM!!! Ama kweli hakuna kufukua makaburi hapa!!!!!

Chanzo JF

Okoa Ndoa yako Sasa, Ongeza Maumbele, Nguvu na Hamu ya Tendo la Ndoa Hata Kwa Wenye Kisukari

$
0
0


OKOA NDOA YAKO SASA. ONGEZA MAUMBILE, NGUVU NA HAMU YA TENDO LA NDOA HATA KWA WENYE KISUKARI.
Tatizo la maumbile madogo, nguvu za kiume na ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa limekuwa likiwasumbua wengi na kusababisha kushindwa kujiamini ktk tendo hivyo kusababisha ndoa nyingi kuvunjika pamoja na mahusiano. Upungufu wa nguvu na hamu ya tendo husababisha mambo kama:-
(a)Uume kulegea wakati wa tendo
(b)Kukosa hamu ya tendo la ndoa
(C)Kuwahi kufika kileleni
(D)Uume kuchelewa kusimama baada ya round ya kwanza.
(E)Kuchoka sana baada ya round moja n.k
@Markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo kwa kutumia bidhaa zilizotengenezwa kwa mimea na matunda zisizo na kemikali wala madhara na kuthibitishwa kiafya. Pata hizi👇👇👇👇
🍉 🌿🍅🍒🍍🍓🍉🍎🍀
1.HANDSOME UP ni kifaa chenye uwezo wa 99 % kuongeza uume (size unayohitaji) na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6.5 @130,000/=
3.Vidonge maalum kwa ajili ya nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @130,000/=
4.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kuweza kurudia tendo hata mara 3 @130,000/=
Kwa Bidhaa hizi na nyingine kama:-
5.Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi @130,000/=
7.Kutengeneza shepu (hips, makalio na mapaja) @200,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni @120,000/=
9.Kuwa mweupe na soft mwili mzima bila kuacha sugu 120,000/=
10.Kurudisha usichana (bikra) @120,000/=
11.Kupunguza au kuongeza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @120,000/=
Wasiliana nasi kwa (+255)
0767447444 au 0714335378.
NB: Matokeo ni uhakika na garantii na upate risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii.
Follow us
@Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr

Acacia Wakubali Kulipa Fedha Wanazodaiwa

$
0
0
John Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Prof. John L. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) ambao ripoti zimekabidhiwa kwake na kamati hizo.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017

Kauli ya Mbowe Baada ya Serikali Kuharibu Miundo Mbinu ya Shamba Lake

$
0
0
Shamba la Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe amethibitisha shamba lake kuvamiwa na viongozi wa serikali ya Wilaya na kuharibiwa miundombinu ya shamba hilo huku akidai anajua yote hayo yanafanyika kutokana na misimamo yake ya kisiasa na kudai hawawezi kumbadili.

Freeman Mbowe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii huku akikiri wazi kuwa siku ya Alhamisi ya tarehe 7 mwaka huu walipokea barua kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira -NEMC ambayo ilikuwa inadai kilimo wanachofanya kilikuwa kinaharibu mazingira hivyo hawapaswi kuendelea na kilimo hicho.

"Ni kweli nimepata taarifa ya kuwa mkuu wetu wa wilaya ya Hai, akiambatana na askari wa mgambo akiambatana na watu wengine ambao sijaweza kuwafahamu wakiwemo vile vile waandishi wa habari, walikwenda kwenye mradi wetu wa Kili Vegies ni mradi wa kilimo cha kisasa cha mboga mboga (Green house), tukilima mboga na matunda, tukilima mboga kwa sababu ya 'local market' na wakaanza kuharibu miundombinu, ikiwemo kuharibu 'Green houses', kukatakata mabomba , kuharibu mimea na uharibifu mwingine mwingi" alisema Mbowe n kuongeza;

"Ni kweli tulipokea barua ya NEMC siku ya Alhamisi tarehe 7, iliandikwa tarehe 7 lakini tuliipata tarehe 8, tulijibu hiyo hoja ya NEMC, kwamba tunaamini wamekosea sheria kwa sababu kilimo chetu hakiharibu mazingira wala shutuma zilizotolewa kwamba ni kwenye chanzo cha maji sio kweli, wanadai kwamba shamba hilo limeanzishwa kwenye chanzo cha mto Weruweru jambo ambalo sio kweli, mto unaoitwa Weruweru unaanzia mlimani kabisa National Park Kilimanjaro"
Shamba la Mbowe

Mbowe anasema kitendo hicho kilichofanywa na viongozi hao ni kitendo cha kufedhehesha na cha kukatisha tamaa hivyo anasikitishwa sana na kitendo hicho, huku akisema anatambua kuwa yote hayo anayofanyiwa ni kutokana na misimamo yake kisiasa, na misimamo ya chama anachokiongoza.

"Najua haya yanatokea kwa sababu ya misimamo yangu ya kisiasa kwa sababu wa muelekeo wangu wa kisiasa na uthabiti na uimara wa chama ninachokiongoza, sasa mimi siwezi kuwa kondoo, nimesema siku zote, haya mambo ya duniani anayeyalipa ni Mungu,hawatabadilisha mawazo yangu kwa kuharibu mali zangu, wanaweza kuharibu zote hata wakitaka roho yangu waichukue, waichukue tu lakini haitanisababisha nibadili msimamo wangu katika kuamini ninachokisimamia, ninachokipigania katika Taifa" alisisitiza Mbowe

Mbali na hilo kiongozi huyo amedai kuwa hakuna wingi wa mali zake zinaweza kuharibiwa zikamfanya yeye akapige magoti kama watu wengine wanavyofanya, anadai yeye hawezi kupiga magoti bali atasimama kwenye ukweli na haki siku zote.

Hili ni tukio la pili kwa mwaka huu kutokea kwenye shamba hilo, mwezi wa kwanza mwaka huu serikali ilimtaka kiongozi huyo kusimamisha kilimo kwenye shamba hilo ikidai kuwa lipo kwenye chanzo cha maji.

Bunge Latoa Azimio La Kuitaka Serikali Ichukue Hatua KALI Kwa Wahusika Wote wa Mikataba Mibovu ya Madini

$
0
0
Bunge
Bunge limeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wote watakaothibitika kuhusika kuliingizia Taifa hasara na kuwakosesha Watanzania fursa ya kufaidika na rasilimali za madini.

Hoja hiyo imetolewa leo Jumatano bungeni baada ya kamati iliyoundwa jana na Spika Job Ndugai kupata maoni ya namna Bunge linavyoweza kuunga mkono juhudi binafsi zinazochukuliwa na Rais John Magufuli kukabiliana na udanganyifu unaofanywa kwenye sekta hiyo.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Newala Mjini, George Mkuchika baada ya kukamilisha taratibu zote, imetoa maazimio matatu ambayo yamepitishwa na Bunge.

"Bunge linamuunga mkono Rais John Magufuli na lipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kadri itakavyohitajika kuhakikisha juhudi hizi hazipotei bure na sekta ya madini inachangia maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla," amesema Mkuchika.

Kukubaliana na kinachofanywa na Rais Magufuli maazimio matatu yametolewa ambayo ni kumpongeza na kuunga mkono kwa hatua anazochukua, kumhakikishia ushirikiano wakati wowote atakapohitaji na kushauri kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kushiriki kulitia taifa hasara kutokana na kuidhinisha mikataba mibovu na wizi uliofanywa.

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images