Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

Vanessa Mdee na Navio si Siri Tena.....

0
0


Navio na Vanessa Mdee
Ulijua baada ya kukutana kwa Vanessa Mdee na Navio kutoka Uganda ndio imeishai pale? Basi kaa tayari kwa wimbo mpya kutoka kwa wasanii hao.



Wawili hao wameonekana tayari kuna kitu wameshakiandaa kwa ajili ya mashabiki wao kutokana na baadhi ya picha walizoziweka kwenye mitandao yao ya kijamii.

Vanessa ambaye wiki iliyopita alionekana akiwa nchini Uganda na kukutana na rapper huyo, ameweka picha kadhaa kwenye mtandao wake wa Instagram zikiwaonyesha wakiwa location wakishoot video ya wimbo wao huo.

Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha wawili hao wakiwa wanashoot video hiyo.


TANESCO Yawatahadharisha Wanaoomba Ajira

0
0
TANESCO Yawatahadharisha Wanaoomba Ajira
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO), limetoa tahadhari juu ya matapeli waajira ambao wamekuwa wakiwatapeli watu kuwa watawapa ajira kwa kuwalipa viwango mbalimbali za fedha kulingana na walizoomba Tanesco.



Soma taarifa kamili:

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Tundu Lissu Amkuna Bashe

0
0
Tundu Lissu
MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), ameeleza kukunwa na nyaraka na maandiko ya Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, yanayohusu madini ya Tanzania.

Akichangia mjadala wa mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha bungeni mjini hapa jana, Bashe alisema kuwa baada ya kusoma maandiko hayo hadi usiku mnene, alibaini Tanzania imeibwa vya kutosha kwenye sekta hiyo.

“Jana (juzi) wakati Lissu nilienda kumwomba anipe yale maandiko yake na alinipa… nimeyasoma sana na hadi saa tisa usiku nilikuwa nayasoma maandiko yale," Bashe alisema.

"Ukisoma maandiko ya Jaji Bomani na kesi ambayo yeye Lissu aliisimamia mwaka 2006, nchi hii imeibiwa kwa muda mrefu sana.

Bunge limefanya makosa na huko nyuma tumefanya makosa, sasa tumepata mtu (Rais John Magufuli) wa kupambana na rasilimali za nchi hii tumuunge mkono Watanzana," alisema.

Alisifu jitihada za Rais Magufuli katika kulinda rasilimali za umma hasa madini na kuwaomba wabunge na Watanzania wote wamuunge mkono.

Bashe alisema kwa kuwa Rais ndiye mlinzi mkuu wa rasilimali za taifa, kuna umuhimu kwa kila Mtanzania kuona kuwa vita hii inamhusu badala ya kumwachia Rais Magufuli peke yake.

Bashe alimtaka Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medad Kalemani, aliambie Bunge jinsi serikali itakavyozipata Sh. bilioni 10 ambazo kampuni hiyo iliondoka nazo.

“Mimi natoka Nzega, sasa kama Mbunge wa Nzega Mjini, naliambia Bunge kuwa tumeibiwa, tumeibiwa sana na kama alivyosema (John) Heche (Mbunge wa Tarime Vijijini -Chadema) jana (juzi), na mimi narudia leo (jana), Resolute wameondoka na fedha za 'Service Levy', lakini Kampuni yake tanzu imepewa leseni, mimi sitajali matokeo, nitawaongoza wananchi wangu kubomoa mabati ya chuo cha serikali,” alisema Bashe.

Alisema wawekezi hao wa madini wameacha mahandaki yenye urefu wa zaidi ya mita 1,000 ambayo walielezwa kuwa yatajaa maji baada ya miaka 200.

Bashe alisema pamoja na wizi uliofanywa na kampuni ya Resolute kwa kuondoka na fedha za halmashauri, kampuni yake tanzu imepewa leseni ya kupata maeneo ya uchimbaji maeneo hayo hayo ya Nzega.

Alisema Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangalla, alipigwa na kuumizwa alipokuwa akipambana kutaka wananchi wake wapate haki yao kwenye mgao wa madini, lakini

Roma Aamua Kurudi Kufundisha Shule

0
0
roma
MKALI wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ anatarajiwa kuwa mwalimu wa muda wa somo la hisabati leo (Juni 15) katika Shule ya Msingi, Mchikichini iliyopo Mbagala-Kibondemaji jijini Dar.

Akizungumza na Showbiz Xtra , Roma anayebamba na ngoma kibao ikiwemo Viva R.O.M.A Viva, K, Ivan na Kaa Tayari alisema kuwa, ameamua kuchukua nafasi hiyo kwanza kujikumbushia kazi yake ya ualimu aliyokuwa akiifanya zamani ambapo alikuwa mwalimu mzuri wa somo la hisabati.

“Somo la hisabati ni miongoni mwa masomo yanayotengwa sana na wanafunzi wengi hivyo basi nikiwa kama mwalimu niliyepitia kufundisha somo hili, nimeona vyema kuhamasisha wanafunzi walipende na kuliamini. “Nitagawa vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba na pia kuwafundisha somo hilo. Kila mmoja nitahakikisha amehamasika na somo hili na kulipenda kama masomo mengine,” alisema R.O.M.A.

Kesho kufutuRisha Mbali na R.O.M.A kutembelea shule hiyo ya Mchikichiki, kesho (Juni 16) mkali huyo ataelekea katika Kituo cha Watoto Yatima cha Nira ambapo atatoa msaada sambamba na kufuturisha.

Shoo ya Dar Live sasa Naye Meneja na Mratibu wa Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, Juma Mbizo alisema baada ya R.O.M.A kufanya yote hayo ya kijamii, mashabiki wake wote waliommis jukwaani watarajie shoo ya nguvu katika Sikukuu ya Idd Mosi.

“Shoo itatambulika kama Nishushe Dar Live ambapo Roma akiwa na wasanii kibao wakiongozwa na Mr. Blue wataliamsha dude ndani ya Dar Live na kugonga nyimbo zake zote zinazobamba. “Nikukumbushe tu mara ya mwisho kwa R.O.M.A kupiga shoo ya kihistoria ilikuwa mwaka jana katika Mkesha wa Mwaka Mpya ambapo alipanda jukwaa moja na mkali, Darassa na kuzoa kijiji. sasa safari hii jibu utatoa mwenyewe akishuka jukwaani,” alisema Mbizo.

WENGINE SASA
Mbizo aliongeza listi kuwa mbali na Mr.Blue na R.O.M.A mashabiki wategemee jukwaa kufunikwa na wakali wa Hip Hop kama Darassa na Stamina huku Snura akiwarushia vyura jukwaani.

Shoo ya watoto nayo ndani Mbizo aliongeza kuwa, mbali na shoo hizo pia pazia la burudani litafunguliwa Sikukuu ya Idd Mosi mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa kundi la sarakasi lisilo na mpinzani Bongo, Wakali Dancers pamoja na wakali wa nyimbo za Asili, Makhirikhiri kutoka Tanzania ambao wataliamsha kwa kutoa burudani kwa watoto.

“Kutakuwa na michezo mingi ya watoto kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea, kucheza ndani ya ndege na mingine mingi.

“Katika kunogesha burudani kwa watoto, kwa mara ya kwanza mkali wa vichekesho anayebamba katika Kipindi cha Ze Comedy, Bambo atakuwepo kuvunja mbavu za watoto wote watakaojitokeza huku akigawa zawadi ndogondogo kwa watakaotoka chicha.

Zanzibar Stars kuibuka Baada ya kupotea kwa muda, kundi kongwe la Muziki wa Mwambao, Zanzibar Stars linatarajiwa kuibuka kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live likiwa na vichwa hatari kama Bi. Mwanahawa, Sabaha Mchacho, Jokha Kassim, Mosi Suleiman, Ally Jay, Zubeda Mlamali na wengine kibao. Mtonyo sasa! Mbizo alimaliza kwa kutaja kiingilio kwa siku hiyo kuwa, burudani kwa wakubwa itakayoanza saa 2:OO usiku itakwenda kwa shilingi 7,000 huku watoto ikiwa shilingi 3,000 tu!

Utafiti wa Twaweza..Kukubalika kwa JPM kwa Shuka Kutoka 96% hadi 71%..CCM Yazidi Kupendwa na Wasiosoma na Wazee..!!!

0
0

 Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Twaweza umebaini kuwa asilimia 71 ya Watanzania wanaukubali utendaji kazi wa Rais John Magufuli ingawa kiwango hicho kimeshuka kutoka asilimia 96 ikilinganishwa na utafiti huo ulipofanyika Juni mwaka jana.

Matokeo haya yametolewa leo Alhamisi na Twaweza katika utafiti wake uitwao ‘Matarajio na matokeo; Vipaumbele, utendaji na siasa nchini Tanzania.’

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze, amesema:

 “Idadi kubwa ya wananchi inaendelea kuukubali utendaji wa Rais Magufuli. Lakini kushuka kwa viwango vya kukubalika kwake, pamoja na vile vya wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa, ni ujumbe mzito kutoka kwa wananchi wanaohisi kuwa, tofauti na matarajio yao, wameangushwa na utendaji wa Serikali katika kuzitatua shida zao moja kwa moja. Wananchi wana hofu na vitu vya msingi – kipato na chakula - na wanatuma ujumbe mzito kwa viongozi wao."

"Lakini utafiti unabainisha ujumbe mwingine kutoka kwa wananchi. Katika orodha ya matatizo makubwa matatu yanayowakabili, afya, elimu na maji zimeshuka ngazi,” ameongeza.

 Amesema Sekta hizo kwa miaka mitatu mfululizo zilichukua nafasi za juu kama changamoto kuu zilizotajwa na wananchi na hivyo utafiti huu unaashiria kuwa wananchi wanayaona mabadiliko katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Utafiti huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

 Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa Aprili mwaka 2017 kutoka kwa wahojiwa 1,805 katika maeneo mbalimbali Tanzania Bara.

Pamoja na kukubalika kwa Rais Magufuli, lakini kukubalika kwa viongozi wengine kama wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji na wa mitaa.

Kwa mfano, kukubalika kwa utendaji wa wabunge, kumeshuka kutoka asilimia 79 (Juni 2016) hadi asilimia 58 (Aprili 2017).

Kukubalika kwa utendaji wa madiwani, kumeshuka kutoka asilimia 74 hadi asilimia 59 na kukubalika kwa utendaji wa wenyeviti wa vijiji/mitaa kumeshuka kutoka asilimia 78  hadi asilimia 66.

Kukubalika kwa vyama vya siasa

Kadhalika utafiti huo ulibaini kuwa CCM imeendelea kuimarika kwa kukubalika kwa kati ya asilimia 54 na 64 kati ya mwaka 2012 na 2017.

“Mwaka 2013 na 2014 kiwango cha kukubalika kilishuka na kilifikia asilimia 54 kutoka asilimia 65 ya mwaka 2012. Kukubalika kwa CCM kumeendelea kubaki katika kiwango hicho hicho cha asilimia 62 tangu uchaguzi wa mwaka 2015 na asilimia 63 mwaka 2017,” umesema utafiti huo.

Chadema yaporomoka

Kadhalika utafiti huo umebaini kuwa kukubalika kwa Chadema kumeshuka kutoka asilimia 32 mwaka 2015 hadi asilimia 17 mwaka huu.

Utafiti huo umebaini, CCM inakubalika zaidi miongoni mwa wazee (asilimia 80), ukilinganisha na asilimia 55 ya vijana. Wanawake (asilimia 68) wanaikubali CCM kuliko wanaume (asilimia 58), maeneo ya vijijini (asilimia 66) kuliko maeneo ya mijini (asilimia 57), na wananchi masikini (asilimia 69) kuliko matajiri (asilimia 53).

Wananchi wenye elimu ya sekondari, elimu ya ufundi au elimu ya juu wanaikubali CCM kwa asilimia 46.

Kukubalika kwa Chadema kwa ujumla kunafuata mtiririko tofauti: ni mkubwa miongoni mwa vijana, wanaume, watu matajiri na wenye kiwango kikubwa cha elimu.

Nafasi za Ajira zilizotangazwa Siku ya Leo

0
0

Bashe,Lugola na Heche Watema Nyingo Bungeni Kuhusu Sakata la Madini..!!!

0
0

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), amesema Serikali isipoifutia leseni ya uchimbaji madini Kampuni ya Mwabangu, ataungana na wananchi na kuwaruhusu wang’oe mabati katika Chuo cha Madini wagawane.

Wakati Bashe akisema hayo, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), amesema atahamasisha wananchi wakachukue kilicho chao kwenye mgodi wa Acacia, huku Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), akishangaa kwa nini hadi sasa polisi na jeshi hawajaenda kwenye mgodi huo.

Akichangia bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2017/18, Bashe alisema: “Naomba kuwaambia wabunge wenzangu, Watanzania wanapokwenda kuchagua viongozi na wanapokwenda kupiga kura ya kumchagua rais, wanamkabidhi dhamana juu ya uhai wao, usalama wao, anakuwa mlinzi wa rasilimali zao walizopewa na Mungu.

“Rais ameunda tume mbili na ametusomea matokeo ya tume, lakini nyuma marais waliotangulia nao waliunda tume mbalimbali, vita ya kupambania rasilimali za nchi hii si ya Rais Magufuli peke yake, ni ya Watanzania wote, hakuna kufanya kosa katika kufanya jambo jema.

“Bunge limefanya makosa, viongozi wetu wamefanya makosa, leo tumepata mtu wa kupigania rasilimali zetu, tumuunge mkono, akishindwa kutufikisha mwisho tumnyooshee mkono.

“Kule Nzega, Kigwangala alipigwa mabomu kwa ajili ya Mgodi wa Resolute, tumeibiwa. Kama alivyosema Heche, niungane naye, Kule Nzega Resolute kaondoka na Sh bilioni 10 za kodi ya huduma, wameacha mashimo… Serikali imeipa Kampuni tanzu ya Resolute, Mwabangu Mining leseni ya kuchimba madini, wallahi wabillahi nitaongoza wananchi bila kujali kitakachotokea kama leseni haitafutwa.

“Resolute wana mgogoro wa kodi na TRA, nataka katika majumuisho mniambie kuhusu Sh bilioni 10 za Nzega tutazipataje.

“Nitamuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake zote, kile chuo mlichofungua cha madini naenda kuwaambia wananchi wang’oe mabati wagawane.

“Rais kawa mstaarabu sana, angetangaza kufunga migodi, Mgodi wa Diamond William, pembeni kuna uchimbaji mwingine unaendelea wa Kampuni ya Hillary, wanachukua dhahabu Mgodi wa Mwadui wanaenda kuyatengenezea katika Mgodi wa Hillary,” alisema Bashe.

Kwa upande wake, Lugola alisema Magufuli wa leo si wa jana.

“Rais Magufuli wa leo tofauti na wa jana, Magufuli wa leo tunamzungumzia kikatiba, ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu, inakuwaje mtu anakuwa na mashaka na uamuzi wake na utendaji wake.

“Nilitegemea mawaziri waanze kazi kwa kwenda katika migodi kuzuia dhahabu, mnasubiri nini, mnahangaika na wawekezaji, mafisadi wamepatikana bado tunasota, eti tunajadiliana na wezi… tunajadiliana nini… mtakaa nao Bahari Beach Hotel katika kiyoyozi, mahakama ya mafisadi ipo hawapelekwi,” alisema Lugola.

Akichangia bungeni juzi, Mbunge wa Tarime Vijijini, Heche, alisema kwa sababu ripoti imeonyesha kuwa Kampuni ya Acacia haijasajiliwa nchini na hivyo haitambuliki, sasa ni muda wa kuhamasisha wananchi wakachukue kilicho chao katika mgodi huo.

“Kwamba Acacia ni kampuni feki, ni kampuni hewa ambayo haipo, lakini ipo Tarime na inawaibia wananchi wa Tarime, kuanzia leo nawaambia wananchi wa Tarime wajiandae tuingie mle mgodini tuchukue kila kilicho chetu.

“Na mimi hili nalisema humu, na nitalifanyia kazi na sidanganyi kwa sababu wananchi wa Tarime wameumizwa na kampuni ile.

“Sisi watu wetu (wananchi wa Tarime), mheshimiwa Spika unajua, wewe ukiwa Naibu Spika, wameumia na maji ya sumu, ng’ombe wamekufa, watu wamepigwa risasi, kwa mujibu wa ripoti ya Waziri wa Nishati na Madini.

“Watu wa Tarime zaidi ya 64 wameuawa na hao ni kwa mujibu wa ripoti ya waziri mwenyewe, wameuawa pale mgodini Serikali ikilinda hawa wezi wa Acacia, ndiyo maana tunasema watu wengine tuna machungu na tuna maumivu na hili,” alisema.

BAD NEWS: Aliyemfukuza Mwizi auawa yeye badala ya Mwizi DSM…kisa?

0
0
Moja ya story kubwa iliyonifikia leo June 15, 2017 ni tukio la kusikitisha ambalo limetokea maeneo ya Ubungo DSM ambapo mtu mmoja amepigwa hadi kufariki na watu wanaodhaniwa kuwa mateja baada ya kumfukuza mwizi.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo June 15, 2017 ambapo inadaiwa kuwa marehemu alikuwa katika juhudi za kumfukuza mwizi aliyepora mkoba wa mwananmke na kukimbilia vichakani na alipomfuata huko alishambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni mateja.

Video hii ina kila kitu kutokana na tukio hilo…Bonyeza Play hapa chini kutazama.

Gazeti la NEWAFRICAN: Heshima ya Tanzania Yaanza Kurudi

0
0
Naamini msimamo MKALI aliouchukuwa rais Magufuli wa KUITETEA nchi yake dhidi ya KUONEWA KIUCHUMI ambao wengine waliuona ni kama anakimbizana na upepo/Chasing after wind umeanza kuzaa matunda.

1. HESHIMA kama TAIFA inaanza KURUDI hatua kwa hatua. Hadi kumfanya mkuu wa migodi husika AJE YEYE mwenyewe KUIMBEMBELEZA Tanzania. Hilo tayari ni jambo linaanza kuipa HESHIMA nchi yetu.

2. Wawekezaji wa kweli itawafanya KUIHESHIMU nchi hii na HAKUTAKUWAPO tena ubabashiaji wa kutunyonya.

3. Badala ya kupewa vitisho vya aina mbalimbali sasa TUNABEMBELEZWA.

Ndo maana gazeti la mwezi huu wa June la New African: Linalosomwa kote duniani lilisema Katika front page yake huku likiwa na PICHA ya RAIS MAGUFULI nami nanukuu

 
AFRICA'S NEW RISING STAR President Magufuli""/Tanzania RAIS Magufuli NYOTA INAYOANZA KUNG'AA AFRICA".

Na katika makala hiyo, mmoja wa waandishi wa MASUALA ya kiuchumi Mr Neil Ford anasema si muda mrefu Tanzania itakuwa juu sana Kiuchumi na KUHESHIMIKA si Africa tu bali KOTE DUNIANI.

Akilinganisha na nchi zingine za Africa Mashariki Tanzania KUNA UNAFUU mkubwa wa MAISHA na hata bei ya BIDHAA ziko CHINI kuliko nchi zinazoizunguka.

Na si muda mrefu huenda UMASKINI UTATOKOMEZWA kabisa nchini Tanzania hivyo kuifanya nchi hii KUHESHIMIKA katika bara ZIMA la Afrika.

Rais Kwa Hili Weka Siasa Pembeni Umpe Lissu Nafasi

0
0
Magufuli
Kuna msemo unasema huwezi Kufanya kitu kile kile kwa akili zile zile utegemee matokeo tofauti.

Wahindi wakitaka kuendelea kibiashara na haswa kwenye sekta ya usafirishaji, huwa wanawagombanisha wafanyakazi wao ili kila mtu ajione Kama yeye ndo Bosi kwenye gari.

Tunakwenda kwenye mazungumzo na barrick juu ya kulipwa kipande chetu tunachowadai hao wadosi. Ni vyema kuamua kwa busara hata Kama hiyo busara inakuumiza. Weka siasa pembeni, muongeze Lissu kwenye hiyo tume ya majadiliano.
Anaweza kuwa hajui sana lakini anachokijua hata Kama ni kidogo, kinaweza kusaidia na haswa ukikumbuka historia yake na bulyankhulu...... Sisemi zaid.

Sisemi kwamba kabudi na hiyo timu yake hawana uwezo wa kung'amua mambo kwenye hayo mazungumzo na barrick... Ila nina waswas na ukweli kwamba hata ukiwa na madegree mangapi, ukishaingia CCM unakuwa Kama zuzu hivi.

Wacha Lissu aingie Huko ndani, wakigombana ndo utapata hela nzuri.... Ila ikiwa smooth sana watatulipa Kama wanautupa msaada hivi.

Kingine kwenye hayo majadiliano hao barrick waambiwe kabisa... Wakimaliza upuuzi wao wafukie mashimo. Wanatuachia miandaki isiyo na matumizi.

By Erythrocyte/JF

Mbunge Ataka Mawaziri Wafanyiwe ‘Interview’ Kabla ya Kuteuliwa

0
0

Mbunge Msukuma
Dodoma. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma, ametaka mawaziri kufanyiwa usahili kabla ya  kuteuliwa kushika  nafasi hizo kutokana na baadhi yao kuwa na elimu ya juu, lakini wanashindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Akichangia katika hotuba ya Bajeti Kuu leo Alhamisi bungeni mjini hapa, Msukuma amesema walioaminiwa na kupewa nafasi hizo wamekuwa wakitajwa kwenye kashfa kubwa.

"Wengine wamegushi vyeti, tukiangalia wana madigrii huenda wengine wana uwezo mdogo wanazidiwa na makaratasi makubwa,"amesema.

Mbunge Ahoji Uwanja wa Ndege Kujengwa Chato

0
0
Mbunge Ahoji Uwanja wa Ndege Kujengwa Chato
DODOMA: Mbunge wa Viti Maalum Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Salome Makamba amehoji bungeni sababu zilizoifanya serikali kujenga uwanja wa ndege wilayani Chato, ambako ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kuacha kufanya hivyo kwenye maeneo mengine mengi yenye fursa za kiuchumi.

Mhe. Salome ameyasema hayo bungeni wakati akichangia kwenye bajeti ya mwaka huu ambapo amesema sababu kubwa ya kushindwa kutekeleza kwa bajeti iliyopita, ni kwa sababu ya serikali kushindwa kusimamia mambo ya msingi.

Mbunge huyo ameenda mbele na kutaka kujua ni utaratibu gani umetumika kusimamia gharama za ujenzi wa uwanja huo, sambamba na kutaka kujua kuhusu ununuzi wa ndege uliofanywa na serikali.
Akataka ufafanuzi pia utolewe kwenye ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco jijini Dar es Salaam.

Source: Global Publisher

Wasanii Wawatupia Lawama Wanasiasa Kuiporomosha Sanaa

0
0
Wasanii Wawatupia Lawama Wanasiasa Kuiporomosha Sanaa

Wasanii walioto changia mada katika Kongamano la tisa la Kigoda cha Mwalimu Nyerere leo Alhamisi, wamesema wanasiasa ndiyo wanaoshiriki kubadilisha lengo na mwelekeo halisi wa sanaa ya Afrika.

Wasanii waliopata nafasi ya kutoa mchango wao katika kongamano hilo ni John Kitime, Carola Kinasha, Niki wa Pili na FID Q.

Nay wa Mitego naye alikuwa miongoni mwa wazungumzaji hao, lakini mpaka sasa bado hajawasili kwenye ukumbi wa Nkurumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lipofanyika kongamano hilo.

Akizungumza katika kongamano hilo  lililoendelea kwa siku ya tatu mfululizo leo, msanii Niki wa Pili ambaye amesema wasanii wanatumiwa na wanasiasa kwa propaganda za kisiasa bila kujali kuwa dhima ya sanaa ni ukombozi.

Naye Fid Q amesema wasanii hushiriki katika kampeni kwa ajili ya kujipatia fedha.

 "Fedha zenyewe ni nyingi kweli zina uwezo wa kutatua baadhi ya changamoto zinazozungumzwa katika majukwaa hayo,” amesema.

Mada kuu katika kongamano hilo la Kigoda cha Mwalimu mwaka huu ni nafasi ya viongozi wa siasa katika kuanguka na kuinuka kwa maendeleo ya Afrika.

Idadi ya wanaomkubali JPM yashuka

0
0

Idadi ya wanaomkubali JPM yashuka
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Twaweza umebaini kuwa asilimia 71 ya Watanzania wanaukubali utendaji kazi wa Rais John Magufuli ingawa kiwango hicho kimeshuka kutoka asilimia 96 ikilinganishwa na utafiti huo ulipofanyika Juni mwaka jana.

Matokeo haya yametolewa leo Alhamisi na Twaweza katika utafiti wake uitwao ‘Matarajio na matokeo; Vipaumbele, utendaji na siasa nchini Tanzania.’

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze, amesema:

 “Idadi kubwa ya wananchi inaendelea kuukubali utendaji wa Rais Magufuli. Lakini kushuka kwa viwango vya kukubalika kwake, pamoja na vile vya wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa, ni ujumbe mzito kutoka kwa wananchi wanaohisi kuwa, tofauti na matarajio yao, wameangushwa na utendaji wa Serikali katika kuzitatua shida zao moja kwa moja. Wananchi wana hofu na vitu vya msingi – kipato na chakula - na wanatuma ujumbe mzito kwa viongozi wao."

"Lakini utafiti unabainisha ujumbe mwingine kutoka kwa wananchi. Katika orodha ya matatizo makubwa matatu yanayowakabili, afya, elimu na maji zimeshuka ngazi,” ameongeza.

 Amesema Sekta hizo kwa miaka mitatu mfululizo zilichukua nafasi za juu kama changamoto kuu zilizotajwa na wananchi na hivyo utafiti huu unaashiria kuwa wananchi wanayaona mabadiliko katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Utafiti huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

 Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa Aprili mwaka 2017 kutoka kwa wahojiwa 1,805 katika maeneo mbalimbali Tanzania Bara.

Pamoja na kukubalika kwa Rais Magufuli, lakini kukubalika kwa viongozi wengine kama wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji na wa mitaa.

Kwa mfano, kukubalika kwa utendaji wa wabunge, kumeshuka kutoka asilimia 79 (Juni 2016) hadi asilimia 58 (Aprili 2017).

Kukubalika kwa utendaji wa madiwani, kumeshuka kutoka asilimia 74 hadi asilimia 59 na kukubalika kwa utendaji wa wenyeviti wa vijiji/mitaa kumeshuka kutoka asilimia 78  hadi asilimia 66.

Kukubalika kwa vyama vya siasa

Kadhalika utafiti huo ulibaini kuwa CCM imeendelea kuimarika kwa kukubalika kwa kati ya asilimia 54 na 64 kati ya mwaka 2012 na 2017.

“Mwaka 2013 na 2014 kiwango cha kukubalika kilishuka na kilifikia asilimia 54 kutoka asilimia 65 ya mwaka 2012. Kukubalika kwa CCM kumeendelea kubaki katika kiwango hicho hicho cha asilimia 62 tangu uchaguzi wa mwaka 2015 na asilimia 63 mwaka 2017,” umesema utafiti huo.

Chadema yaporomoka

Kadhalika utafiti huo umebaini kuwa kukubalika kwa Chadema kumeshuka kutoka asilimia 32 mwaka 2015 hadi asilimia 17 mwaka huu.

Utafiti huo umebaini, CCM inakubalika zaidi miongoni mwa wazee (asilimia 80), ukilinganisha na asilimia 55 ya vijana. Wanawake (asilimia 68) wanaikubali CCM kuliko wanaume (asilimia 58), maeneo ya vijijini (asilimia 66) kuliko maeneo ya mijini (asilimia 57), na wananchi masikini (asilimia 69) kuliko matajiri (asilimia 53).

Wananchi wenye elimu ya sekondari, elimu ya ufundi au elimu ya juu wanaikubali CCM kwa asilimia 46.

Kukubalika kwa Chadema kwa ujumla kunafuata mtiririko tofauti: ni mkubwa miongoni mwa vijana, wanaume, watu matajiri na wenye kiwango kikubwa cha elimu.


Hii Ndio Shule Anayofundisha Msanii Roma Mkatoliki

0
0
Hii Ndio Shule Anayofundisha Msanii Roma Mkatoliki
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Ibrahim Mussa (Roma Mkatoliki) amegeukiwa kufundisha ambapo jana aliibukia katika Shule ya Msingi Mchikichini iliyopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam na kufundisha wanafunzi wa darasa la saba somo la hisabati.

Msanii huyo akiongea na gazeti la MTANZANIA alisema kuwa anafundisha somo hilo kwa wanafunzi wa darasa la saba kwani wengi hufeli kutokana na kuwa na walimu.

“Mimi kitaaluma ni mwalimu wa hisabati, kutokana na kufeli mno somo hilo nimeanza kampeni ya kufundisha na kugawa vitabu kwa kuanza na shule hii kwa sababu pia nitakuja kufanya onyesho la muziki kwenye sikukuu ya Eid kwa mara ya kwanza,”  alisema Roma.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ramadhan Mashaka alisema kuwa msanii huyo amepata kibali cha kufundisha shuleni hapo.

“Nimekagua na kugundua kuwa Roma ni mwalimu mzuri wa hisabati hivyo tumemkaribisha afundishe wanafunzi bila hofu, tukiwa na imani kubwa kuwa wataelewa kwa sababu wanafundishwa na mtu wanayempenda na hii itaongeza morali ya wanafunzi shuleni hapa,” alisema Mwalimu Juma.

Licha ya kufundisha, atafuturisha watoto yatima wa Kituo cha Nira kilichopo Mbagala Chamazi na atatoa zawadi za sikukuu ya Eid.

NCCR- Mageuzi yaibuka Wataka CCM iombe Radhi Sakata la Mchanga wa Madini

0
0
Baada  ya Rais, Dk. John Magufuli kukabidhiwa ripoti ya mchanga wa dhahabu, Chama cha NCCR-Mageuzi kimekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwaomba radhi Watanzania.

Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Juju Danda, alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, kwamba ripoti hiyo ya mchanga imeanika uozo uliosababishwa na CCM kwa kipindi kirefu ilichokaa madarakani.

“Kwa maana hiyo, ni vema CCM wakakaa, wajiulize na kujipima kwa kuwaomba radhi Watanzania ambao wamekuwa wakiishi maisha magumu yaliyosababishwa na CCM.

“Kamati mbili zilizoundwa na Rais Dk. John Magufuli, zimethibitisha pasipo shaka, kuwa Watanzania wameibiwa tena kwa kiwango kikubwa ingawa mwaka 2007, Kamati ya Bomani ilitoa maoni na mapendekezo kadhaa yaliyohusu sekta ya madini ingawa maoni hayo hayakufanyiwa kazi,”alisema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kukiri kosa ni uungwana na kwamba CCM wanatakiwa kujitokeza hadharani na kuwaomba radhi Watanzania, kuwa hawakuwatendea haki kutokana wizi uliokuwa ukifanyika katika sekta ya madini.

Pamoja na hayo, Danda aliiomba Serikali kuhakikisha inachukua hatua za kisheria kwa yeyote aliyeshiriki katika kuangamiza uchumi wa Taifa kwa kusaini mikataba mibovu katika sekta ya madini.

 “NCCR-Mageuzi, tunafarijika kuona tuliyokuwa tukiyapigania kwa miaka mingi, yanaendelea kufichuliwa waziwazi  na ukweli unazidi kubainika kupitia kamati zilizoundwa na Rais.

“Pia ni muda muafaka wa kupitia upya sheria zote zinazohusu masuala ya madini na ni wakati muafaka wa wataalamu wazalendo kuipitia tena Katiba iliyopendekezwa kwa kuwa inatoa mwelekeo wa kuwadhibiti wabadhirifu,” alisema.

Tunda Asanukia Ishu ya Kitumbo Chake Baada ya Kusemekana Mjamzito

0
0

Muuza nyago machachari Bongo, mwenye kupenda kujiselfisha akiwa kwenye maakuli, Tunda Sebastian amesanukia ishu iliyoenea kwamba, ana kibendi akisema kuwa kilichotokea ni mpangilio mbovu wa menyu ndiyo unamfanya aonekane tumbo hilooo!

 Akibonga na 3 Tamu, amedai kuwa, kuna watu wanasema ana mimba, lakini hana cha mimba wala tumbo la mitungi bali ni mpangilio mbaya wa misosi.

 “Sina mimba wala kitambi cha ulabu, hili tumbo limejaa misosi tu si kingine, kuna kipindi nilikuwa na mpangilio mbaya wa menyu. Najitahidi kufanya mazoezi na kupunguza kufakamia misosi,” alisema Tunda.

Zari wa Diamond Akwaa Aibu 5

0
0
zari Hassan

KAMPALA: Katikati ya majonzi, yapata siku 15 tu tangu mumewe, Ivan Ssemwaga ‘Ivan Don’ azikwe huko Nakalilo nchini Uganda baada ya kufariki dunia ghafla, aliyekuwa mkewe, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, anadaiwa kuwatibua Waganda kufuatia kushiriki matukio matano (5) yanayotafsiriwa kuwa ni ya aibu, Amani linayo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya udaku nchini Uganda, tofauti na ilivyotarajiwa, kama ilivyo kwa baadhi ya tamaduni za Kiafrika, kuwa Zari angekuwa kwenye maombolezo kwa siku arobaini au hadi amalize eda kwa kufi wa na mume huyo, yeye amekuwa akijihusisha na ishu ambazo zinaacha watu midomo wazi.



AIBU YA KWANZA
Ilielezwa kwamba, siku mbili tu baada ya mazishi ya Ivan, Mei 30, mwaka huu, Zari alitupia video kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Snapchat ikimuonesha mwenye furaha tele huku akikata mauno ya hatari hivyo kushangaza wengi walioamini ni video ya zamani.
Ilisemekana kuwa, ili kuonesha video hiyo haikuwa ya zamani, Zari aliambatanisha na maneno yalioonesha alikuwa akijiachia ili kuondoa stresi za majonzi.

Zari ambaye alijirekodi video hiyo akiwa nyumbani kwa mama yake, Halima Hassan huko Munyonyo, Kampala aliandika: “Yote kwa yote ni kujifunza kudensi wakati wa majonzi.”
Kwa mujibu wa taarifa za tukio hilo, wengi walikasirishwa na kitendo hicho huku wakihoji kama ni Zari huyohuyo aliyefi wa na mumewe?


AIBU YA PILI
Achilia mbali kukata mauno, ilielezwa kwamba, tukio linguine la aibu ni pale alipotaka kuzichapa kavukavu na binamu wa Ivan, King Lawrence kwenye kikao cha familia ya jamaa huyo kilichomuhusisha Zari juu ya usimamizi wa mali za baba watoto wake huyo.

Ilidaiwa kuwa, katika tukio hilo, Zari alitia aibu kwa kushindwa kuwaheshimu waliokuwa wakwe zake na kuondoka kwenye kikao hicho kwa hasira akiwa na wanaye watatu wa kiume aliozaa na Ivan, Pinto, Raphael na Quincy.


AIBU YA TATU
Ilielezwa kuwa, tukio lingine la aibu kwa mwanamke huyo ni kitendo cha kushindwa kutulia na watoto hao wa marehemu kwa wakwe zake kasha kukimbilia nao kwao kabla ya kutimka nao nchini Afrika Kusini.

“Alitakiwa akae kwa wakwe au hata kwa mama yake hapa Munyonyo (Kampala) hadi angalau afi kishe arobaini, lakini ametimua na watoto kwa kuwa si mtulivu wala haoni aibu kuwa bado ni mapema kwa mfi wa kama yeye,” kilikaririwa hanzo kimoja na vyombo vya habari vya Uganda.

Hata hivyo, ilidaiwa kwamba, huko Afrika Kusini aliwafanya wanaye hao kuwa katika wakati mgumu kwani badala ya kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoachiwa ya Ivan ambayo watoto hao walikuwa wakiishi awali iliyopo Pretoria nchini Afrika Kusini, yeye aliwapeleka kwa mwanaume mwingine huko Johannesburg ambaye amezaa naye watoto wawili.

AIBU YA NNE
Aibu nyingine anayodaiwa kuifanya Zari katika kipindi hicho kifupi hata kabla ya arobaini ni pamoja na kuvujishwa kwa picha zisizokuwa na maadili zilizomuonesha akijiachia kimalovee na mwanaume mwingine kwenye bwawa la kuogelea.
Taarifa hizo zilieleza kwamba, kama hiyo haitoshi, kilichotibua mambo zaidi hadi kwa jamaa anayeishi naye ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, ni kitendo cha mwanaume huyo aliyekuwa akiogelea naye kumshika sehemu za nyuma za mwili wake ‘msambwanda’ hadharani bila kujali kuwa yupo kwenye kipindi cha majonzi na pia ni mama wa watoto watano.
Katika utetezi wake, Zari alidai kuwa, mwanaume huyo ni binamu wa mumewe na kwamba tukio la uchukuaji wa picha lilifanywa na mke wa jamaa huyo (wifi ye) aliyekuwa akiogelea naye.

AIBU YA TANO
Hata hivyo, ilidaiwa kwamba aibu ya nne ndiyo iliyozaa aibu ya tano kwani Zari alijikuta akiwaporomoshea matusi baadhi ya watu aliodai ndiyo waliosambaza picha za tukio hilo mitandano.
Ilielezwa kwamba, Zari alitumia tusi ambalo haliandikiki gazetini huku akiwaita punda na kuwataka kuacha kufuatilia maisha yake, jambo lililozidi kumtengenezea picha ya tofauti kwa baadhi ya watu wasiomjua tabia zake.

MSAADA WA KISAIKOLOJIA
“Kiukweli nimemfuatilia Zari tangu afi we na aliyekuwa mumewe, hayupo sawa, anahitaji msaada wa kisaikolojia maana anafanya vitu kwa kushindwa kujikontroo,” kilikaririwa chanzo kingine.
Ivan alifariki dunia Mei 25, mwaka huu ambapo tangu hapo kuliibuka mambo mengi hasa juu ya usimamizi wa utajiri mkubwa aliouacha huku Zari akiwa kinara katika mapambano hayo hadi alipoibuka kidedea kwa kumilikishwa sehemu ya utajiri huo ili alee watoto hao watatu aliozaa na Ivan.

Global/Amani

Mo Dewji Azidi Kufanya Kufuru Simba Sc..Awaambai Viongozi Wasajili Pesa Kwake Siyo Tatizo..!!!

0
0

SASA hii ni jeuri ya fedha, kwani baada ya Simba kufanikiwa kuzinasa saini za John Bocco, Shomari Kapombe na kipa Aishi Manula kutoka Azam FC, mwanachama maarufu wa Wekundu hao wa Msimbazi, Mohammed Dewji ‘Mo’, ameuambia uongozi utafute wachezaji wengine wazuri, kwani fedha kwake si tatizo.

Mbali na wachezaji hao watatu kutoa Azam FC, pia Simba imefanikiwa kuzinasa saini za mabeki wawili, Jamal Mwambeleko kutoka Mbao FC pamoja na Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans, zote za jijini Mwanza, na Mo amesema anataka waletwe wengine wenye uwezo mkubwa zaidi.

Gazeti la Dimba limenasa ujumbe wa Mo ukiwataka Wanasimba kuwa kitu kimoja, huku akisisitiza kwamba lazima ufanyike usajili wa nguvu ili timu irudishe heshima yake iliyopotea kwa misimu kadhaa.

“Narudisha heshima ya Simba SC iliyopotea ndani ya misimu mitatu, pesa si tatizo kwangu, usajili huu ni chachu ya Simba kuelekea kwenye mafanikio endelevu na kufanya vyema kimataifa, huu ni muda mzuri kwetu kuunganisha nguvu zetu zote kuona Simba SC inafanikiwa na kuliletea heshima taifa letu, Simba nguvu moja,” ulisomeka ujumbe huo.

Kauli hiyo ya Mo inaupa uongozi jeuri ya kuinasa saini ya mastraika hatari kutoka nje ya nchi, akiwamo yule straika wa Zambia, Walter Bwalya, ambaye ana njaa ya mabao kinoma.

Aidha, Mo, ambaye ameonekana kujiamini sana, amewahakikishia Wanasimba kwamba mbali na huyo, pia straika mwenye zali na Simba, Emmanuel Okwi, wanamalizana naye kila kitu ndani ya siku mbili hizi na atatua Msimbazi dakika yoyote kuanzia sasa, huku pia klabu hiyo ikikamilisha mazungumzo na straika wa AFC Leopards, Allan Kateregga, ambaye wamekuwa wakimfukuzia baada ya kuona uwezo wake katika michuano ya SportPesa, iliyomalizika hivi karibuni Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Kateregga, pia huo utakuwa mwanya kwa uongozi kumpelekea mapendekezo yao juu ya uhitaji wa wachezaji wawili kutoka Yanga, Donald Ngoma pamoja na Haruna Niyonzima, ambao wamekuwa wakiwafukuzia, hasa baada ya mikataba yao na Yanga kufikia ukingoni.

Uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi umekuwa kwenye mipango kabambe ya kutaka saini za Ngoma na Niyonzima, ila tatizo linakuja kwenye fedha wachezaji hao wanazozitaka za usajili, lakini sasa viongozi hao wanaweza wakampelekea Mo mezani kwake, ambapo atazungumza na mastaa hao na kumalizana nao kiutu uzima.

Anachokifanya Mo kinaendana na kile kikao kizito kilichokaliwa mjini Dodoma kati ya uongozi na baadhi ya wabunge na mawaziri wanaoshabikia Simba, baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la FA, ambapo Wekundu hao wa Msimbazi walifanikiwa kuwafunga Mbao bao 1-0, ambapo kikao hicho kwa kauli moja kiliafikiana kuifumua timu na kuijenga upya, hasa kwa kununua wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Vigogo hao walipendekeza usajili wao uzingatie uwezo wa mchezaji husika na kubwa zaidi mwenye uzoefu wa michuano ya Kimataifa, hiyo ikiashiria kuwa ni maandalizi ya kukijenga kikosi chao katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambayo watashiriki mwakani.

Wanachotaka kukiona Vigogo hao ni ile Simba ya mwaka 2003, iliyokuwa na mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi, hasa ikiweka historia ya kuwatupa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika waliokuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Zamalek ya nchini Misri.
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images