Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Rasmi..Ibrahim Ajib Ajiunga na Yanga kwa Miaka Miwili..Amesaini Mkataba Mchana Huu..!!!

$
0
0

Yanga imemalizana na mshambuliaji Ibrahim Ajibu Migomba.

Ajibu amejiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Taarifa kutoka Yanga zinaeleza Ajibu amemalizana na Yanga mchana huu baada ya kuwa wamefanya mazungumzo mfululizo tokea juzi.

"Tulikuwa hatujamalizana katika masuala fulani ya fedha, lakini sasa naona mambo yamekaa vizuri kabisa," kilieleza chanzo.

"Ukisema Ajibu ni mchezaji wa Yanga tayari, wala hautakosea," chanzo kilisisitiza.

Tetesi...Niyonzima Asaini Simba Sc Kwa Dau la Milioni 110..!!!

$
0
0

SIMBA imeamua kufanya kufuru katika usajili wake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo inasemekana wametumia dau la Dola 50,000 za Marekani (Sh mil 110) kwa ajili ya kumng’oa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima.

Niyonzima ambaye amemaliza mkataba wake na Yanga, yupo nchini kwao Rwanda alipokwenda kuungana na timu yake ya taifa ‘Amavubi’ kwa ajili ya mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).

Yanga imeshindwa kuwaongezea mikataba mipya baadhi ya wachezaji wake wa kimataifa kutokana na kile kinachodaiwa ni ukata ulioikumba klabu hiyo kwa sasa.

Kufuatia jambo hilo, uongozi wa klabu ya Simba ambao kwa muda mrefu walikuwa wakihitaji huduma na Mnyarwanda huyo, umefunga safari hadi nchini kwao kwa ajili ya kumalizana na mchezaji huyo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutokea Rwanda, mmoja wa wanafamilia wa mchezaji huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema tayari viongozi wa Simba wamemalizana na mchezaji huyo kwa dau la dola 50,000 za Marekani.

Alisema: “Ni kweli Niyonzima amemalizana na Simba na wamemfuata huku na hivyo kila kitu kimekwenda sawa.”

Kwa upande wake, Niyonzima licha ya kuthibitisha viongozi wa Simba kumfuata kwao nchini Rwanda, lakini alisema bado hajaingia mkataba rasmi na timu hiyo.

“Ni kweli viongozi wa Simba wamenifuata Rwanda, nimerudi juzi kutoka kuitumikia timu yangu ya Taifa, sijasaini mkataba nayo lakini tupo kwenye mazungumzo,” alisema Niyonzima ambaye ni nahodha wa Amavubi.

Hata hivyo, hivi karibuni mchezaji huyo alihojiwa na gazeti la New Times Sports la nchini kwao na kuweka wazi mipango yake akisema, ameshawaaga mashabiki wa Yanga na kwamba muda wake wa kuondoka ndani ya timu hiyo umefika.

Kimenukaa..CCM Yawageuka Kina Chenge na Wote Waliotajwa Kwenye Sakata la Madini..Yatoa Tamko Hili Dhidi Yao..!!!

$
0
0

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wote waliotajwa katika ripoti ya kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya mchanga wa madini, kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola vitakavyowahoji.

 Waliotajwa katika ripoti ya pili ni aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Profesa Sospeter Muhongo na na Nazir Karamagi.

Akizungumza na wanahabari leo (Alhamisi) katika ofisi za Lumumba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey   Polepole amesema ili vyombo vya dola viweze kufanya kazi yake kwa haraka na ufanisi, waliotajwa wanapaswa kutoa ushirikiano.

Polepole amesema chama hicho chenye Serikali kinaviagiza vyombo vya dola kuwahoji waliohusika kwa haraka ili Watanzania wajue ukweli wa yaliyotokea.

Amempongeza Rais John Magufuli kwa kuthubutu kudai rasilimali ambazo zimekuwa zikiibiwa.

Pia, amewataka wananchi kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi anayoifanya badala ya kugawanyika.

Mke wa Waziri Mkuu Auawa kwa Kupigwa Risasi Wakati Akiendesha Gari..!!!

$
0
0

Mke wa Waziri Mkuu mteule wa Lesotho, Lipolelo Thabane ameuawa kwa kupigwa risasi ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuapishwa kwa mume wake, Thomas Thabane.

Lipolelo ameuawa jana (Jumatano) wakati akiendesha gari karibu na nyumbani kwake, katika mji mkuu wa Maseru.

Taarifa zinaeleza kuwa Thabane ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, alitengana na mwanamke huyo tangu 2012.

Historia inaonyesha kuwa mwaka 2014 wanajeshi walijaribu kumpindua Thabane kutoka madarakani.

Uchaguzi uliofanyika nchini Lesotho mapema mwezi huu ni wa tatu katika kipindi cha miaka mitatu kutokana na migogoroy kisiasa.

Waziri Mkuu huyo ataapishwa Ijumaa.

Mbunge wa CCM Awafananisha Wabunge wa Upinzani na POPO..!!!

$
0
0

Mbunge wa Mkuranga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Ulega amewafananisha wabunge wa upinzani na popo kuwa hawaeleweki na kusema wamekuwa watetezi wa wawekezaji ambao wao wamewatuhumu kuwa ni wezi wa madini.

Mbunge huyo amesema hayo  bungeni akisema kuwa wapinzani hao leo limewashuka baada ya jana Rais Magufuli kukutana na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

"Popo hajafahamika kama ni mnyama au ndege mpaka hivi leo na hawa wenzetu hata sitaki kuwaita vinyonga naomba niwaite popo maanake hawajafahamika kama ndege au wanyama na leo limewashuka kwani walijigeuza kuwa mawakili wa wale ambao sisi tunawatuhumu kwamba ni wezi wetu na yule anayehusika Mkuu amewathibitishia mchana wa leo (jana) ameingia na amekiri mwenyewe kwa kinywa chake ya kwamba wapo tayari kulipa pesa ambazo tunawadai na tena lile lililokuwa linaonekana jambo gumu la kujenga kinu cha kuchenjua madini amelichukua na amesema yupo tayari kujenga" alisema Ulega

Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi na kesema bara la Afrika limekuwa na bahati mbaya kwani wapinzani wa Afrika wamekuwa wakitumika na mabeberu miaka yote na kusema wao kama Chama Cha Mapinduzi wanakila sababu ya kutamba kwa kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeweka sawa na kutamka namna nzuri ya kusimamia shughuli za madini. 

Spika Ndugai Aanika Taratibu Zitakazotumika Kumvua Chenge Uenyekiti wa Bunge..!!!

$
0
0

Katika ripoti ya pili ya Kamati ya kutathmini mchanga wa madini Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge ametajwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo kuwa alikuwa na mchango mkubwa wa kulisababishia Taifa hasara kubwa kutokana na kuandaa au kusaini mkataba mbovu wa madini unaoyaruhusu makampuni ya uchimbani kusafirisha mchanga huo kwenda nje ya nchi pamoja na kukubali viwango vidogo vya mrabaha kwa Taifa katika sekta ya madini.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa kwa Rais na Mwenyekiti wa kamati hiyo ni pamoja na kuwashughulikia viongozi na watendaji wote wa Serikali walioshiriki kusababisha hasara hii kwa zaidi ya miaka 19.

Rais Dkt. Magufuli akiongelea pendekezo hili aliagiza vyombo vinavyohusika viwaite watu wote waliotajwa ili wahojiwe.

Baada ya kauli hiyo ya Rais, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Chenge ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Bunge mpaka atakapoitwa na kuhojiwa kuhusu mchanga wa madini (makinikia). Spika Ndugai alisema hakuna kanuni inayomzuia Chenge kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bunge kwa sasa.

“Kwa sasa hapana. Ataachia nafasi hiyo atakapoitwa kuhojiwa; akishathibitika ndio atatoka kwenye nafasi ya Uenyekiti,” alisema.

Utaratibu unaeleza kwamba Ofisi ya Spika ikishapata taarifa ya Mbunge au kiongozi fulani wa Bunge kuhitajiwa na chombo cha dola na Spika akatoa ruhusa hiyo, Mbunge huyo ataachia madaraka yake na kubaki na ubunge tu.

Mwenyekiti wa kamati ya pili ya kuchunguza hasara iliyoletwa na kusafirisha mchanga wa madini, Profesa Nehemiah Osoro alisema kuwa wakati Taifa linapitisha Sheria na mikataba ya hovyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Andrew Chenge.

William Ngeleja : Kutuhumiwa Siyo Kukutwa na Hatia......Maisha Yanaendelea..!!!

$
0
0

Mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja, amesema kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia na maisha yanaendelea.

Ngeleja ambaye ni mmoja wa watuhumiwa waliotajwa kwenye Ripoti ya pili Rais ya kuchunguza Makinikia, ameyasema hayo leo alipokuwa akichangia Bajeti Kuu ya Serikali ya 2017/18.

Wakati akiendelea na mchango wake, aliwataka wabunge kusimama ili kuonyesha kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kupambana na wizi wa rasilimali za Watanzania ikiwamo dhahabu.

Wakati akiendelea na mchango wake huo, Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga, aliomba kutoa taarifa kwa mzungumzaji akimtaka Ngeleja kueleza uhusika wake kwenye kashfa hiyo kwa sababu kamati imemtaja.

Baada ya kauli hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, alimtaka Ngeleja kuendelea na mchango wake na kuwa alichotoa Mbunge Haonga siyo taarifa.

Hata hivyo kabla ya kuendelea na mchango wake, Ngeleja alisema ” kutuhumiwa siyo kukutwa na hatia na maisha yanaendelea”.

Makamu wa Rais Mgeni Rasmi Mchezo wa Everton na Gor Mahia, Aipongeza SportPesa..!!!

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amepongeza mipango na mikakati mizuri ya kampuni ya SportPesa ya kutaka kukuza vipaji vya wanamichezo hasa kwa mpira wa miguu kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Makamu wa Rais amesema hayo leo Juni 15, 2017  Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa kampuni hiyo inayojishughulisha na ubashiri wa michezo ya ‘Sports Betting’ nchini, Abbas Tarimba na Mkurugenzi Mtendaji wa hiyo, Pavel Slavkov.

Amesema kama malengo ya kampuni hiyo yatafikiwa Tanzania itakuwa bora katika mchezo wa mpira katika bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.

Aidha, Makamu wa Rais amekubali ombi la kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Everton ya nchini Uingereza na timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya ambayo ilitwaa kombe la michuano ya Sportpesa iliyofayika hivi karibuni hapa nchini

Pia amewahakikishia watendaji wa kampuni hiyo kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi na pindi wakikwama katika jambo lolote wawasiliane na ofisi yake ili tatizo linalowakabili liweze kutafutiwa ufumbuzi ili lisikwamishe shughuli za kampuni hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa ‘SportsPesa, Tarimba Abbas amesema kuwa kampuni hiyo ina malengo makubwa ya kufanya biashara hapa nchini kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchini.

Tarimba amesema katika mipango yao wanataka katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kampuni yao iwe ni moja ya kampuni bora nchini katika ulipaji wa kodi kwa Serikali kama wanavyofanya kwa sasa katika Serikali ya Kenya.

Pia, amemshukuru Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kukubali ombi lao na kuwa Mgeni rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Everton ya nchini Uingereza na timu ya Gor Mahia ya Kenya mchezo ambao unatarajiwa kufanyika Julai 13, 2017 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Majasusi wa Kimarekani Waendelea Kumchunguza Trump..Kisa Hiki Ni Sababu Hii Tu..!!!

$
0
0

Bundi la kuchunguzwa limeendelea kutua juu ya paa la Ikulu ya Marekani, ambapo mkuu wa nchi hiyo, Rais Donald Trump anakabiliwa na uchunguzi mwingine kwa tuhuma za kuzuia sheria isitekelezwe.

Gazeti la Washington Post limeeleza kuwa Trump anachunguzwa na jopo la wanasheria likiongozwa na mwanasheria maalum Robert Mueller, taarifa ambazo zilitolewa kwa gazeti hilo na maafisa wa FBI.

Muller pia anaongoza uchunguzi wa FBI kubaini kama Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani uliomuingiza madarakani Rais Trump, lakini pia unalenga kubaini endapo Trump alihusika katika suala hilo.

Wanasheria wa Trump wamelaani kitendo cha FBI kutoa taarifa hizo kwenye gazeti hilo, hatua ambayo gazeti hilo limedai kuwa ni hatua kubwa kwa uchunguzi ulioanzishwa.

Rais Trump anahusishwa na kuwa na uhusiano wa karibu na Urusi, ambapo ushirikiano kati ya nchi hizo zenye historia ya uhasimu ilikuwa moja kati ya ahadi zake wakati wa kampeni. Trump alieleza kuwa ili kukabiliana na kundi la kigaidi linalojiita Islamic States of Iraq and Syria (ISIS), ni muhimu nchi hizo kushirikiana.

Kwa mujibu wa Washington Post, maafisa wa FBI wamesema kuwa uchunguzi dhidi ya Trump juu ya suala hilo ulianza mapema baada ya kumfukuza kazi mkuu wa FBI, James Comey mwezi Mei mwaka huu.

Trump alidaiwa kumshawishi Comey kutoendelea na uchunguzi dhidi ya mshauri wake wa masuala ya usalama, Michael Flynn aliyekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano wenye utata na balozi wa Urusi.

VIDEO: Polepole Afunguka Kuhusu Sakata Makenikia, Asema Vita Hairudi Nyuma

$
0
0
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Kupitia Katibu wake  wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole  kimeweka wazi kuwa hakitarudi nyuma kwenye vita ya Uchumi iliyoanzishwa na Rais John Magufuli.


Amewataka Watanzania  kumuonga Mkono Rais John Magufului Kwenye vita ya Uchumi aliyoiizisha ili Wananchi kunufaika na rasimali za nchi.

Hatimaye Yanga Yafunguka Kuhusu Mchezaji Simon Msuva Kuhusu Kuvunja Mkataba

$
0
0
Klabu ya Yanga imetoa taarifa kuwa haiwezi kumzuia mchezaji wao Saimoni Msuva endapo kuna klabu yoyote ndani na nje ya nchi itamuhitaji licha ya kuwa wao bado wanamuhitaji sana katika kikosi chao.

Taarifa hiyo ya Yanga inasema wao bado wanamkataba na mchezaji huyo mrefu na kudai wanafahamu kuna klabu nyingi zimekuwa zikimuhitaji mchezaji huyo kutokana na ubora wake na kusema wao hawana pingamizi lolote.

"Tunafahamu kuna vilabu vingi vinamtaka mchezaji wetu kutokana na ubora wake na sisi kama klabu hatuna pingamizi. Klabu yoyote ndani ya nchi na nje ya nchi inayomtaka Saimoni Msuva inakaribishwa klabuni na kufuata taratibu zote sahihi za kumnunua mchezaji. Bado Msuva ni muhimu katika klabu yetu na sisi tunapenda sana kuendelea naye lakini hatuwezi kumzuia kutafuta riziki sehemu bora zaidi kuliko kwetu" ilisema taarifa ya Yanga

Mwisho kabisa Yanga wamekanusha taarifa zinazoenea kuwa mchezaji huyo amevunja mkataba na klabu hiyo na kusema bado ni mchezaji wao

Mzee Yusuph Afunguka Kilichosababisha Kuacha Muziki

$
0
0

Mzee Yusuph
Aliyekuwa mwimbaji wa muziki wa Taarabu Mzee Yusuph ambaye kwa sasa anafahamika kama Alhaj Mzee Yusuph amefunguka kuhusu kuacha kwake muziki na kufanya toba ili kurudi kuwa muumini na kutoa daa’wa.

Akizungumza kwenye Leo Tena ya Clouds FM leo June 15, 2017 Alhaj Mzee Yusuph amegusia pia jinsi maneno ya watu yalivyofuata baada ya kutangaza na hatimaye kuacha kabisa muziki huku akielezea namna alivyokuwa anakataza watu kwenye Kundi lake wasitende maovu.
“Mimi nimeacha muziki kwa sababu nataka kuwa Muumuni wa Dini ya Kiislamu na kumfuata Mtume Muhammad (SAW). Nilipopata nafasi ya kwenda kuhiji Makka na kushika Al Kaaba nilimuomba Mwenyezi Mungu anisamehe makosa yangu.

“Nilipoanza kubadilika nilikuwa nakataza pombe kwenye Band yangu. Siku nisiyowepo walikuwa wanasema Simba leo hayupo. Nilipokuwa nakataza haya mambo wengi walikuwa wakiniambia kwa nini nisifungue Madrasa. Kubadilika kwangu niliachana kwanza na starehe magoma kwanza maana ilikuwa ni kama kunywa maji tu unaposikia kiu.

“Nilizungumza mimi na Mungu wangu nikisema: ‘Wewe ndiye mwenye kutoa msamaha’. Nikafanya show ya mwisho Dodoma nikaachana na muziki. Nilimwambia kwanza mke wangu mdogo mimi nimeacha muziki. Kesho yake nikamuambia mke wangu mkubwa nimeachana na mziki, hawakuamini.” – Alhaj Mzee Yusuph.

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Alikiba Aombewa Kolabo Kwa Davido

$
0
0
Davido na Alikiba

Shabiki mmoja wa Alikiba ameamua kujitosa kumuombea kolabo msanii huyo kwa hitmaker wa ‘Fall’, Davido kutoka Nigeria.



Shabiki huyo ambaye anatumia jina la peter_allyson kwenye mtandao wa Instagram, amecomment kwenye picha ya Davido hiyo hapo chini kwa kuandika,
“Plz plz broe do collaboration with alikiba plz plz plz plz plz plz plz plz is me tz boy.”


Ni mara kadhaa mashabiki wa Kiba wamekuwa na mchango mkubwa katika muziki wa msanii huyo hivyo sio ajabu kwa shabiki kama huyo kutupa karata yake ya mawazo kwa Davido.

Wawili hao wote wapo chini ya usimamizi wa Sony Music japo Davido anasimamiwa na Sony Music International na Alikiba yupo chini ya Sony Music Africa.

Beka: Mkubwa Fella Hajatujengea Nyumba..!!!

$
0
0

BAADA ya kundi la Yamoto Band kusambaratika na wasanii wake, Enock Bella, Aslay, Beka na Maromboso kila mmoja kupata menejimenti yake mpya na kuanza kufanya kazi kama ‘solo artists’, hatimaye Beka 1 Flavour anayetamba na ngoma yake ya Libebe ameibuka na kujibu tuhuma zinazowakabili kuwa licha ya kupewa nyumba na meneja wao wa Yamoto Band, Mkubwa Fella,  bado wamemkimbia.

“Yamoto Band bado ipo isipokuwa Mkubwa mwenyewe ametupa ‘go ahead’ ya kufanya kazi kama ‘solo artists’  na kuhusu kupewa nyumba Mkubwa hajatugawia nyumba isipokuwa yale ni mavuno ya tulichokipanda baada ya kufanya shoo nyingi ndani na nje ya nchi na kuingiza mtonyo wa kutosha ndipo tukakaa na kujadili kwamba  badala ya kutugawia malipo yetu, kila mmoja tukaona ni bora atusimamie tuweze kusimamisha vibanda vyetu,”  amesema Beka1 Flavour.

Gazeti la Mawio Lafungukiwa kwa Miaka Miwili kwa Kosa la Kuchapisha Habari Kuhusu JK na Mkapa Kuhusika na Ufisadi wa Madini..!!

$
0
0

Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe imelifungia gazeti la Mawio kuchapishwa kwa miezi 24 kuanzia leo (Alhamisi).

Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbas imesema waziri amechukua hatua hiyo kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.

Amesema hatua hiyo inatokana na gazeti hilo katika toleo namba 196 la 15-21 Juni, 2017 kuchapisha katika ukurasa wa mbele picha za marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ikiwahusisha na sakata la mchanga wa madini.

Pia, katika ukurasa wa 12 wa gazeti hilo limechapisha makala iliyoandikwa Lissu: Mkapa, Kikwete wataponaje? Kuwatuhumu viongozi hao kuhusika katika sakata la madini wakati ukweli ni kwamba hawakuwa sehemu ya uchunguzi wa kamati za Rais John Magufuli na wala matokeo ya kamati hizo hayakuwatuhumu kwa kosa lolote.

Taarifa ya Waziri Mwakyembe kwa mhariri mkuu wa gazeti hilo imesisitiza kuwa, licha ya utetezi wao, habari hizo si tu zimekiuka agizo la Serikali lakini pia, zimekiuka vifungu vya 50(a), (b), (c), (d) na (e) vinavyokataza uandishi wenye dhamira hasi.

“Sina budi kulifungia gazeti lako na kukutaka usitishe kulichapisha kwa nakala ngumu au ya mtandaoni kwa kipindi cha muda wa miezi ishirini na nne 24 tangu tarehe ya barua hii kwa mamlaka niliyopewa chini ya sheria ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016 kifungu 59,” imesema taarifa ya Dk Mwakyembe kwenda kwa mhariri wa Mawio.

Waziri pia amevipongeza vyombo vingi vya habari ambavyo amesema kuanzia leo vimefuata weledi wa taaluma na misingi ya sheria, vikitii agizo la Serikali kwa kutowaingiza katika sakata hilo pasipo hoja za msingi viongozi wastaafu.


Je, Simu yako Inaisha Chaji Haraka? Tatizo sio Betri Epuka Mambo Haya

$
0
0
Je, Simu yako Inaisha Chaji Haraka? Tatizo sio Betri Epuka Mambo Haya
 
Kwa jinsi maisha yanavyokwenda kasi hususani utandawazi hakuna shaka yoyote kuwa mtu uppo radhi hata ugharamie pesa ili uchaji simu yako, hii yote usipitwe na habari, au dili nyingine ambazo kwa maisha ya sasa zinakamilishwa kupitia simu.



Nakumbuka mwaka jana nilifanya tafiti ndogo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDSM, UDOM na SAUT kuhusu maisha bila simu inawezekana? Asilimia 90% kati ya wanafunzi 120 walisema hawawezi kuishi bila simu wala kukaa mbali na simu zao, huku asilimia 10% tu ndiyo walisema wanaweza kuishi bila simu.

Hii ni ishara kuwa kwa ulimwengu wa sasa kama hauna simu huenda ukawa upo nyuma ya ulimwengu wa Teknolojia kwani vitu karibia vyote vinakamilishwa kupitia simu.

Je, changamoto gani ambayo inaumiza sana au inaboa watu wengi kwenye matumizi ya Simu? zipo changamoto nyingi kama ukosefu wa vocha lakini kubwa zaidi ni Changamoto ya CHAJI.

Nadhani hili ni tatizo kubwa sana kwani kwenye mikusanyiko mikubwa siku hizi kama kwenye sherehe au mikutano sio jambo la kushangaza kumuona mtu akikuomba Charger pengine hata kama hamjuani.

Je, tatizo nini mpaka kuwe na usugu wa tatizo hilo? jibu ni kwamba watumiaji wengi wa simu za mikononi hawasomi maelekezo ya jinsi ya kutunza betri za simu zao na kuishia kulalama kuwa betri zao ni FEKI.

Basi nakuhakikishia kuwa betri ya simu yako sio feki wala mbovu ila hujui jinsi ya kutunza Betri yako, Kwahiyo kama betri yako inakusumbua kwenye chaji usiamini kuwa betri yako ni FEKI fuatilia hatua hizi wakati wa kuchaji simu ili simu yako iweze kuhifadhi chaji muda mrefu.

1-Epuka kuchaji Simu mara kwa mara kwa kutumia kihifadhi Chaji (Power Bank).

Kumekuwa na kesi nyingi za watu kulalamika mara baada ya kutumia Power Bank wengi wao wakisema simu zao hazitunzi chaji, ukweli ni kwamba Power Bank huhifadhi chaji kama betri la simu lilivyo hivyo kitendo cha kuchaji betri lingine husababisha maambukizi ya mtiririko wa Chaji hivyo hufanya betri kupoteza nguvu ya kuhifadhi chaji kadri unavyozidi kutumia mara kwa mara.Hapa unashauriwa kutumia umeme wa moja kwa moja kutoka kwenye Soketi wakati wa kuchaji na sio vihifadhi chaji.

2-Epuka kutumia Program (App) zenye matangazo mengi.



Nadhani ushawahi kuliona hili kama ni mtumiaji mzuri wa App mbalimbali hususani zenye matangazo mengi wakati wa kutumia huwa simu inashika joto haraka sana, Ukweli ni kwamba kwenye majaribio mbalimbali yaliyofanywa na wataalamu wa mitandao yamebaini kuwa programu zenye matangazo mengi huchukua karibia asilimia 30% ya chaji pindi unapozitumia pata picha una App tano zenye matangazo ni kiasi gani cha chaji utapoteza kwa wakati unatumia? bila shaka umepata jawabu. Hapa unashauriwa kutoa kabisa kama sio kupunguza matumizi ya Program hizo.

3-Epuka kutumia ‘Charger’ tofauti tofauti,(Tumia charger sahihi).

Kutokana na kukosa uelewa wa kusoma maelekezo kumekuwa na desturi kwa watu wengi siku hizi kugongea charger hususani maofisini au hata kwenye maeneo mengine ya kazi basi usifanye hivyo tena.



Kila simu ukisoma kwenye betri yake kuna maelekezo yameandikwa kwa nyuma kuwa usitumie Charger nyingine mbali na ile uliyopewa na simu, hii maana yake ni nini? ni kwamba Charger zinakuwa na Voltage yake inayopita kuchaji simu na hii hutofautiana sana kutokana na ukubwa na aina ya simu  kwa hiyo kama simu yako inapitisha mfano Voltage 0.05 na ukatumia Charger inayopitisha voltage 0.5 lazima uharibu betri yako hivyo ni vyema ukajua charger ya simu yako inapitisha kiasi gani cha umeme kabla ya kutumia charger nyingine.

4-Epuka kuchaji simu au kuweka simu kwenye mazingira ya joto kali au baridi kali.



Simu nyingi hususani zile za kisasa haushauriwi kuziweka kwenye mazingira ya joto kali zaidi ya Celsius 50 kwani kwa kufanya hivyo kutafanya betri ya simu yako kupungua nguvu na hii pia ipo hata wakati wa kuchaji simu kama una tabia ya kuchaji simu ikiwa juani au sehemu yenye joto kali utaifanya simu yako ijae upesi lakini pia itawahi kuishana muda mwingine simu kulipuka au Betri kuvimba.



5-Chaji simu yako pale inapofikia asilimia kuanzia 16% hadi 10%.

Hapa wataalamu wengi wa masuala ya kielekroniki wanasema chaji simu yako pale tuu inavyoanza kulia mlio wa kuashiria betri yako inahitaji kuchajiwa.



Kwa bahati mbaya sana wameshauri kupunguza kabisa kama sio kuacha tabia ya kusubiri mpaka simu izime chaji ndiyo uanze kuchaji kwani kwa kufanya hivyo kutaathiri ions ambazo huhifadhi chaji na kwa muda mfupi sana utaona betri yako ikishindwa kuhifadhi kabisa chaji.

Ushauri kama utakuwa upo mbali na sehemu ya kuchaji simu yako na tayari imeshafika asilimia kati ya 10%-16% basi ni bora ukazima simu kabisa.

 6-Kushindwa kuchaji simu vizuri na kwa ufasaha.

Hii ni sababu kubwa na mbaya sana hususani kwa watumiaji wa Smartphone huwa ni wanashindwa kustahimili muda wa kuchaji hujikuta wanachaji simu huku wakitumia au kuitoa simu chaji hata kabla ya kujaa hilo ni kosa kubwa sana.


Unashauriwa uchaji simu yako bila kuitumia mpaka betri ijae yaani (Full Charge) kwa kufanya hivyo utaiongezea betri uwezo wa kutunza chaji tofauti na mfumo wa kuchaji bila mpangilio maalumu.

Kuna kesi kibao za vifo ambavyo vimetokana na simu kulipuka kutokana na kutumia simu huku ikiwa kwenye chaji.

7-Epuka kuchaji simu ikiwa hewani (Zima au weka Flight Mode).



Jitahidi unapochaji simu yako kuizima au kuweka flight mode ni vizuri zaidi kama ungeweza kuweka flight mode kwa kuwa simu inajaa chaji vizuri ikiwa imewaka lakini haitumiki.

8-Hakikisha betri la simu yako limekaa vizuri kwenye simu.



Hii ni kwa watu wangu wanaotumia simu ndogo za au zile zenye uwezo wa kutoa betri hakikisha betri ya simu yako imebana vizuri kwenye koili za chaji za simu yako kwani kuna kiwango kikubwa  cha chaji kinapotea kama simu yako imelega lega au kushikana vizuri na koili zinazotumika kuchaji simu yako.

Endapo utazingatia haya hakuna shaka yoyote uhai wa betri yako ya simu utaendelea kudumu na hautopata kamwe buguza za chaji kukata kata au kutembea na Power Bank kila sehemu.

By Godfrey Mgallah



Jenga Heshima kwa Jamii Kwa kufanya Mambo Haya Matatu

$
0
0

Hakuna ubishi wowote, heshima ni moja ya kitu ambacho karibu kila mtu anakitafuta katika maisha yake. Hakuna mtu ambaye hataki asiwe wa kuheshimika, heshima inatafutwa na watu wengi sana.

Ndio maana utakuta kuna watu wanatumia pesa au mbinu nyingi sana kuweza kujenga heshima. Hali hiyo yote inaonyesha kwamba heshima ni mojawapo ya kitu cha thamani na kinachokubalika sana katika jamii yoyote ile.

Pamoja na umuhimu wa heshima kwa wengi, sasa kitu ambacho tunatakiwa tujiulize mimi na wewe ni kwamba, je, kati yetu ni wangapi hasa wanajua namna ya kujenga heshima zao katika jamii?
Je, pesa peke yake ndio ina uwezo wa kujenga heshima? Au ni kitu gani ambacho unatakiwa uwe nacho ili kikusaifdie kuweza kujenga heshima kubwa katika jamii na kujikuta ukikumbukwa pengine vizazi na vizazi?

Kama nia yako ni kutaka kujenga heshima na ukawa mtu wa kuheshimika, fahamu mambo haya;-

1. Toa thamani.
Ili uweze kujenga heshima kubwa kwa jamii inayokuzunguka, toa thamani, fanya vitu ambavyo vinagusa maisha ya watu. Haijalishhi unafanya kitu gani lakini lilokubwa fanya kitu ambcho kinagusa maisha ya watu, kina mchango wa kubadili maisha ya wengine.

Siku zote haijalishi una pesa za kiasi gani, lakini je, kupitia hizo pesa wewe binafsi unatoa mchango gani kwa wengine kufanya maisha ya yakabadilika? Watu wote wanaotoa thamani na kuweza kubadili maisha ya wengine ni watu wa kuheshimika.

Kama unafikiri natania kuhusu hili angalia watu waliokuwa wakipagania uhuru, heshima zao zikoje katika jamii zao, utangudua heshima zao ni kubwa sana. Hivyo hiyo inatuonyesha njia mojawppo ya kujiwekea heshima toa thamani kwa kugusa maisha ya watu.

2. Wakubali watu.
Mbali na kutoa thamani, njia mojawapo nyingine ambayo inaweza kukujengea heshima ni kuwakubali watu. Kubali mawazo yao wanayotoa ila kama kweli yanasaidia kujenga jamii au kuwasaidia wengine.

Kama unahitaji kuwakosea, tafadhari usiwakosoe hadhari, jitahidi ukosoe kwa pembeni. Hiyo pia ni njia nzuri ya kukusaidia kujua au kutambua kwamba yapo makosa ambayo umeyaona na ni muhimu kurekebishwa.

3. Unapokosea, omba msamaha.
Hakuna mtu ambaye tunaweza tukasema yupo kamili kwa asilimia zote. Hivyo, unapokosea iwe kwa jamii yako au kwa watu wako wa karibu, hebu kuwa mwepesi wa kuomba msahamaha.

Msahama ni kitu kidogo sana lakini utakusaidia kukujengea picha kwa watu wengine kwamba una busara. Kwa sababu ya busara zako utajikuta ukiwa ni mtu wa kuheshimika karibu na watu wote.
Hizi ni mbinu miuhimu ambazo mtu yoyote anayataka kuheshimiak katika jamii yake anaweza akazitumia kama njia mjawapo ya kumsaidia kumjengea heshima kubwa katika jamii yake.

Kama Kweli Unataka kufanikiwa Wekeza Akili Yako katika Jambo hili

$
0
0
Kama Kweli Unataka kufanikiwa Wekeza Akili Yako katika Jambo hili
Kuna wakati mwingine watu hushindwa kulitekeleza jambo fulani sio kwa sababu hawajui jambo hilo au eti kwa sababu hawana uzoefu wa jambo hilo, la hasha huo si kweli watu wengi wanashindwa katika kulifanya jambo fulani kwa sababu wanakosa"umakini" juu ya kulitenda jambo hilo.

Na umakini ni ile hali ambayo ambayo mtu anakuwa nayo kutoka nafsini mwake katika kulitenda jambo fulani, lakini kulitenda jambo hilo bila kufikiri ni sawa na bure, hivyo kila wakati unahitaji kujenga umakini kwa kuwekeza nguvu na akili katika kufikiri na kutenda jambo hilo.

Kamwe hutoweza kufanikiwa kama utaendelea ile tabia ya kutofanya vitu kwa umaikini. Kwani siri kubwa ya kushindwa kufanikiwa kwako ipo katika jambo hilo. Nasisitiza swala hili la kutenda mambo kwa umakini kwani pindi mtu anaamua kuwa makini humsaidia mtu huyo kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa jambo husika na mara nyingine kutenda jambo kwa umakini huumfanya mtendaji wa jambo hilo kuepuka kurudia makosa katika kulitenda jambo hilo.

Hivyo umakini katika kila nyanya na masuala mbalimbali ya maendeleo yako binafsi na ya jamii kwa ujumla yanahitajika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama unataka kufanikiwa kwa kiwango kikubwa unatakiwa kuwa makini kwa kila jambo.

Mwisho jitahidi kuwa makini juu ya mambo haya;

1. Kuwa makini katika kuchagua mawazo ya mambo ambayo unataka kuyatenda.

2. Kuwa makini katika kubeba mawazo na ushauri wa watu mbalimbali ambao wanakuzunguka. Au kwa maneno mengine tunaeza kusema kuwa makini na wewe mwenyewe na watu wengine.

3. Jitahidi kadri uwezavyo kuwa makini katika katika kufanya upembuzi yakinifu ni wapi ambapo umetoka ni wapi ambao unaelekea.

4. Kuwa makini katika katika kuchagua marafiki wenye tija kwako kila wakati.

5. Kuwa makini katika kuwekeza mambo ambayo unajifunza mara kwa mara. Jiulize yana tija gani kwako.

6. Kuwa makini katika kutambua thamani ya muda na pesa.
Hayo ni baadhi ya maeneo machache kati ya mengi ambayo unatakiwa kuwekeza fikra katika kulitenda jambo fulani.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Jioni ya Leo

Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images