Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Chadema - Suluhisho la Ufisai Nchini ni Katiba ya Warioba na Si Vinginevyo..!!!

$
0
0

Chadema imesema iwapo Tanzania inataka kunufaika na rasilimali zake na kushinda vita vya kutetea utajiri wake inapaswa kwanza kurejesha katiba iliyopendekezwa na Jaji Joseph Warioba na si vinginevyo.

Akitoa msimamo wa chama kutokana na kile kinachoendelea baada ya kutolewa kwa ripoti mbili za Rais kuhusu mchanga wa dhahabu, leo (Ijumaa) Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji amesema suluhisho la kudumu katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za Taifa ni kurejea katika katiba ya wananchi.

“Chadema tunasema kuwa haya yote tunayoyapigia kelele itakuwa ni kazi bure iwapo haturejeshi hoja ya katiba mpya.

“Katiba ya Warioba iliweka mapendekezo ya jinsi ya kulinda rasilimali za taifa na kama tungefuata hayo yote hili la sasa halingepaswa kuwa na mjadala mkubwa kiasi hiki,” amesema wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho Kinondoni.

Pia, chama hicho kimeitaka CCM kujipima na kujitafakari kama kinafaa kuendelea kuaminika kuongoza dola kutokana kushindwa kutetea vyema rasimali za taifa kwa kuruhusu mikataba mibovu.

VIDEO: ACACIA Hawajakubali Kulipa Chochote -- Mbunge Lijualikali

$
0
0
Mbunge Lijualikali
Kwenye Exclussive Interview na Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali amesema kuwa Kampuni Mshirika wa Acacia (Barrick) haikukubali moja kwa moja kulipa Deni wanalodaiwa na Serikali kutokana na Makubaliano ya awali ya serikali na Kampuni hiyo.

Lijualika amesema kuwa ukifuatilia taarifa ya Kampuni hiyo imeeleza wazi kuwa Kampuni hiyo itakuwa ridhaa kulipa deni litakalopatikana baada ya kupitia kwa pamoja ripoti ya kamati, na kwamba kukubali kitendo cha kuipitia ripoti hiyo ni kwamba wana uhakika watashinda madai yote kwakuwa watakuwa wamepewa fursa ya kujieleza na Mwisho wa Siku hawatokubali... Video:

Video: Roma Apata Ulemavu wa Kidole, Kilivunjwa na Waliomteka

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop, Roma Mkatoliki amefunguka kuzungumzia hali yake ya afya ambapo amesema kidole chake kimoja ambacho kilikuwa kina kazi maalum kwenye muziki wake hakijakaa sawa, ni kile kilichovunjwa na watekaji. Rapa huyo na wenzake watatu walitekwa na watu wasiojulikana miezi miwili iliyopita wakiwa studio ya Tongwe Record iliyopo Masaki jijini Dar es salaam.


Godzilla Awatusi Nikki Mbishi na Wakazi

$
0
0
Nikki Mbishi na Godzilla
Msanii wa muziki wa hip hop nchini, Godzilla amefunguka kwa kuwachana wasanii wenzake wanaoishi Ukonga Jijini Dar es Salaam kwa kuwaambia ni miyeyusho japokuwa ni ndugu zake wa kipindi kirefu na bado anawalea.


Zilla amesema hayo baada ya kuulizwa chanzo cha ugomvi wake na msanii Nikki Mbishi pamoja na Wakazi.

“Nikki ‘is my friend’ tumefanya kazi kwenye nyimbo yake, ‘I don’t know’ sijui kitu gani kimetokea lakini ‘we still friend. Mimi sina tatizo kwa sababu kama ingekuwa chochote kimetokea watu tusingefanya kazi pamoja, lakini imekuwa ‘too much’,” Zilla alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

“Unajua watoto wa Ukonga wengi wanakuwa miyeyusho miyeyusho lakini ni ndugu zangu wakina Wakazi, Nikki tunawalea tutafanyaje wanetu hao” aliongeza.

Alichokisema Kikwete Baada ya Kukutana na Kardinali Pengo Nchini Dubai..!!!

$
0
0

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai leo.

Kikwete ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter leo(Ijumaa) na kueleza kuwa amemkuta Kardinali Pengo akiwa mwenye siha njema.

Ingawa hajaeleza amemkuta Kardinali Pengo nyumbani au Hospitali lakini askofu huyo mkuu wa jimbo la Dar es Salaam, amewahi kuripotiwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matibabu.

“Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.” Ameandika Kikwete

Kikwete amesema amemtembelea Kardinali Pengo wakati akiwa safarini kuelekea Canada. 

Wajue Vigogo wa Dunia Walio Nyuma ya Acacia Katika Sakata la Madini Ambao Watatua Nchini Kuikabili Kamati ya Magufuli..!!!

$
0
0

Wakati Serikali na kampuni ya Acacia zikiwa zinajiandaa kwa mazungumzo ya kumaliza mzozo wa usafirishaji mchanga wa madini nje ya nchi, taarifa zinaonyesha timu ya Tanzania itakuwa na kazi ngumu kukabiliana na upande wa pili.

Timu ya kampuni hiyo kubwa ya uchimbaji madini itaundwa na viongozi kutoka kampuni ya Barrick Gold Cooperation na Acacia.

Barrick inamiliki zaidi ya asilimia 63 za hisa za Acacia, ambayo inaendesha migodi ya Buzwagi, Bulyanhulu, inayozalisha mchanga unaosafirishwa nje kwa ajili ya kwenda kuuyeyusha kupata mabaki ya madini, pamoja na North Mara.

Mazungumzo hayo kwa upande wa Barrick yatahusisha vigogo 12 ambao ni wajumbe wa Bodi ya Kimataifa ya Ushauri, ambayo kwa mujibu wa tovuti yao imepewa jukumu la kutoa ushauri kwa Bodi ya Wakurugenzi na menejimenti kuhusu masuala ya ardhi na siasa na mambo mengine ya kimkakati yanayoathiri kampuni.

Vigogo hao ni pamoja na mawaziri wakuu wawili wa zamani, na mawaziri watatu wa zamani wa nchi nne tofauti zilizoendelea.

Mwenyekiti wa bodi hiyo ni Brian Mulroney, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada kati ya mwaka 1984 na 1993, Jose Maria Aznar, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Hispania (1996-2004), pamoja na aliyekuwa spika wa Bunge la Marekani Newt Gingrich (1995-1999) na ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Rais Donald Trump ndani ya chama cha Republican.

Wajumbe wengine wazito ni John R. Baird, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada (2011-2015) , William S. Cohen, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani (1997-2001) na Karl-Theodor zu Guttenberg aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani (2009-2011).

Mwingine ni Charles Powell, aliyekuwa mshauri wa mambo ya nje wa Margareth Thatcher (Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza na John Major (1990). Kwa sasa Powell ni mjumbe wa Bunge la Mabwenyenye na amekuwa mshauri wa kampuni za Rolls-Royce na BAE Systems.

Wajumbe wengine wa bodi hiyo ni Peter Munk, muasisi na mwenyekiti wa Emeritus, Barrick Gold Corporation, mshauri wa kampuni za Akin, Gump, Strauss, Hauer & Feld na L.L.P, Vernon E. Jordan Jr, Andrónico Luksic na Gustavo Cisneros, mwenyekiti wa Cisneros Group of Companies ya Jamhuri ya Dominica.

Mwenyekiti mtendaji wa Barrick, Profesa John Thornton, ambaye alikutana na Rais Magufuli Jumatano na kukubaliana kuanza mazungumzo ya kumaliza mzozo wa suala hilo, pia ni mjumbe wa bodi hiyo.

Kwa upande mwingine, bodi ya Acacia inaundwa na watu wanane, akiwemo Mtanzania Juma Mwapachu, ambaye alikuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mwenyekiti wa bodi hiyo ni Kelvin Dushnisky ambaye pia ni Rais wa Barrick. Mjumbe mwingine ni ofisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, Brad Gordon.

Wakati Rais Magufuli alisema baada ya kukutana na Profesa Thornton kuwa Acacia imekiri makosa na imekubali kulipa deni, kampuni hiyo juzi usiku ilitoa ufafanuzi kuwa licha ya kukubaliana kuingia katika mazungumzo, “hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa, lakini mazungumzo yatalenga kutafuta suluhisho kwa ajili ya maslahi ya pande zote mbili”.     

Credit - Mwananchi

Breaking News..CCM Kuwatimua Wote Waliotajwa Kwenye Ripoti ya Ufisadi ya Mchanga wa Madini..Yupo Chenge na Genge Lake..!!!

$
0
0

Ripoti ya kamati ya pili ya makinikia iliyowasilishwa mwanzoni mwa wiki, inawaweka katika wakati mgumu vigogo watano wa CCM, imefahamika.

Ripoti ya kamati hiyo iliyoongozwa na Profesa Nehemiah Osorro ilipendekeza vigogo waliohusika kuingia mikataba mikubwa ya migodi ya madini na kulitia hasara Taifa, wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Kitendo cha Rais John Magufuli kukubali mapendekezo yote 21 ya kamati hiyo, ikiwamo kuwachukulia hatua waliotajwa katika ripoti hiyo, kunafanya uhai wa vigogo hao ndani ya chama tawala kuwa shakani.

“Tutawashughulikia wote, ambaye hataguswa ni marehemu tu,” alisema Magufuli huku akiagiza vyombo vya dola kuanza kuwahoji wote waliotajwa.

Mbali na kauli hiyo ya Rais, jana Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alitaka vyombo vya dola viharakishe uchunguzi wao, huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, akishauri wahusika watimuliwe kutoka chama hicho tawala.

Miongoni mwa vigogo waliotajwa kuhusika kuingia mikataba hiyo ni mawaziri wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini; Dk Abdallah Kigoda (marehemu), Daniel Yona, Nazir Karamagi, William Ngeleja na Profesa Sospeter Muhongo.

Wengine ni wanasheria wakuu wa zamani na manaibu; Andrew Chenge, Johnson Mwanyika, Felix Mrema na Sazi Salula.

Mbali na hao pia wamo makamishna wa madini na wakuu wa idara ya mikataba wa zamani; Paulo Masanja, Ally Samaje, Dk Dalaly Kafumu, Maria Ndossi na Julius Malaba.

Lakini, ambao wanaweza kujikuta matatani ni wale walio kwenye ngazi za uongozi wa chama hicho tawala.

Vigogo hao wanaoweza kuchukuliwa hatua ndani ya chama hicho ni Profesa Muhongo, Karamagi, Ngeleja, Chenge na Kafumu ambao ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na baadhi ni wabunge.

Chenge ni mbunge na mwenyekiti wa Bunge na iwapo ataondolewa CCM atapoteza nafasi yake ya ubunge wa Bariadi Magharibi kama ilivyo kwa wengine wanaoshika nafasi hiyo.

Wabunge hao - Kafumu (Igunga), Profesa Muhongo (Musoma Vijijini) na Ngeleja (Sengerema) - wanaweza kujikuta wakipoteza nafasi za uwakilishi wa wananchi wao bungeni iwapo watavuliwa uanachama.

Karamagi, mfanyabiashara ambaye amewahi kuwa mbunge wa Bukoba Vijijini alishindwa katika mchujo wa chama chake kwenye uchaguzi wa 2010 ikiwa ni miaka miwili tangu ajiuzulu uwaziri wa nishati na madini kutokana na kashfa ya mitambo ya kufua umeme ya Richmond.

Akizungumza Machi 11 kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM mjini Dodoma, Polepole alisema chama hicho hakiwezi kuwavumilia wanachama na viongozi watakaokwenda kinyume na maadili.

“Wanachama na viongozi wa CCM, ambao kwa wakati wowote ule watakwenda kinyume cha maadili, watakihujumu Chama cha Mapinduzi, watajihusisha na rushwa, ubadhirifu na tabia zozote zile ambazo kwa asili yake zinakwenda kinyume na uongozi bora na uaminifu, (wataadhibiwa) kuhakikisha chama chetu kinakuwa ni mfano wa vyama vyote sio tu Tanzania, lakini Afrika nzima kwa ujumla,” alisema Polepole.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akitangaza kuwatimua wanachama 12, wakiwamo wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu, wenyeviti wanne wa mikoa, watano wa wilaya na mwenyekiti wa UWT kwa madai ya kukisaliti chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015.

Waliofukuzwa wakati huo ni pamoja na Sophia Simba, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UWT na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Wenyeviti wa mikoa waliotimuliwa ni Jesca Msambatavangu (Iringa), Ramadhani Madabida (Dar es Salaam), Erasto Kwilasa (Shinyanga) na Christopher Sanya (Mara).

Wajumbe wa Halmashauri Kuu waliofukuzwa uanachama ni Ally Sumaye (Babati Mjini) na Erasto Manga (Arumeru).

Ikiwa ni miezi mitatu tangu CCM ifanye uamuzi huo mgumu, suala hilo linaweza kujirudia tena, lakini safari hii kwa wanachama ambao tuhuma zao hazihusiani moja kwa moja na chama.

Jana, Polepole aliendelea kuwa na msimamo huohuo aliposema chama hicho kinasubiri makada hao wahojiwe na kwamba ikithibitika walihusika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

“Tunaomba vyombo vya dola vianze kazi ya kuwahoji watu hao haraka na makada waliotajwa watoe ushirikiano ili ukweli ujulikane ili chama kiwachukulie hatua za kinidhamu,” alisema.

Alisema chama hicho kinampongeza Rais John Magufuli kwa ujasiri aliounyesha katika kusimamia rasilimali za Watanzania.

“Tunamuunga mkono Rais Magufuli, tuko pamoja naye ameonyesha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano si ya kinyonge,” alisema.

Alisema Watanzania wanatakiwa kushirikiana katika kipindi hiki kumuunga mkono Rais ili apate nguvu ya kusimamia rasilimali nyingine.

“Wako watu wachache ambao wanataka kumkatisha tamaa, lakini tulio wengi tuendelee kushikamana kumpa moyo Rais wetu,” alisema.

“Katika Ilani ya CCM, kifungu cha 35 (k) tumeweka wazi kuwa tutarekebisha mfumo wa uendeshaji wa migodi ili kukomesha utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi,” alisema.

Alisema pamoja na ilani kuahidi hayo, kitendo cha Rais Magufuli kimewapa nguvu Watanzania ya kusimamia rasilimali za nchi.

“Tunaomba aendelee kutuongoza kusimamia madini mengine kama almasi na rasilimali nyingine za nchi,” alisema.

Msukuma akoleza moto

Suala hilo pia lilijitokeza bungeni, ambako Kasheku “Msukuma” alisema wakati akichangia mjadala wa bajeti ya mwaka 2017/18 kuwa wana-CCM waliotajwa katika sakata la mchanga wa madini wachukuliwe hatua.

Msukuma ambaye pia ni Mbunge wa Geita Vijijini, alisema: “Tufike mahali tuambiane ukweli tuache mizaha. Wote tumeangalia ripoti ya maprofesa, watu tusiosoma na wananchi wetu kule vijijini. Halafu wabunge mliotajwa kutoka CCM mnaanza kuweka kwenye twitter (mtandao) mimi sihojiwi mpaka nini?

“Hivi kweli wezi wana kinga? Kama kweli wametajwa ni wezi, hata kama wapo CCM hili sio suala la mizaha. Kuna maisha ya watu na watu tumeumia, watu mmetajwa wabunge wenzangu wa CCM humu. Halafu mzee wetu tunayemuheshimu humu ndani anasema hawezi kuhojiwa mpaka mahakamani, yeye ni nani?”

Msukuma alisema watu waliburuzwa sana miaka iliyopita na kwamba kuna watu walikwenda Ulaya wakasaini mikataba huko na wakawagawana fedha.

“Naomba kama kuna uwezekano hawa watu kama ni mbunge, kama ni nani wakamatwe. Wanaotusumbua humu ndani ni haohao wametajwa kwa Profesa Osorro, katajwa Kafumu, Ngeleja na Chenge,” alisema.

“Wanakinga gani kama wezi? Kwani magereza imewekwa kwa ajili ya kina babu Seya peke yao? Tufike mahali tulipiganie Taifa hili. CCM sio kichaka cha wezi. Kila mwaka kila tuhuma mtu anatajwa. Tufike mahali tuwe serious kwenye suala hili.”

Msukuma alimpongeza Rais kwa kumtumbua aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo na kisha akageuka na kuuliza, “Sijui kama yupo humu nina hamu naye kweli.

“Rais alisema aliamini vyeti, lakini vimemuangusha, halafu juzi tu alisema mara tatu PhD 17 za BoT (Benki Kuu Tanzania). Nilikuwa naishauri Serikali tuangalie uwezo wa mtu na ikiwezekana hata mawaziri hawa wawe wanafanyiwa interview.

“Haiwezekani unakuwa na watu wana PhD za kutisha. Tunapogundua wezi, haohao wenye PhD wanaanza kututisha sisi ambao hatuna digrii. Sasa yako wapi madigrii tunayoyategemea hapo?” alihoji.

“Tufanye kitu cha msingi kama wabunge hata kama kubadilisha sheria tusiamini haya madigirii na mavyeti makubwa. Kwa kuwa Katiba ilitamka elimu kubwa katika baadhi ya vyeo watu waliforge (walighushi), hivyo vyeti na matokeo yake tunayaona  leo hapa,” alisema.

Ngeleja, mmoja wa waliotajwa, aliposimama alielezea umuhimu wa kuangalia upya Sheria ya Madini akisema kuna kifungu kinaruhusu na baadaye kutaka Bunge limpe Rais heshima kwa kusimama na wabunge wakasimama wakipiga makofi.

Kitendo hicho kilimfanya mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga kusimama kumpa taarifa Ngeleja kwamba awaeleze Watanzania anahusikaje kwenye makinikia.

Lakini Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu alimzuia Ngeleja kujibu taarifa hiyo na kumruhusu aeendelee kuchangia.

Kabla ya kuendelea, Ngeleja alimjibu Haonga akisema: “Mdogo wangu Haonga anafahamu kutuhumiwa si kupatikana na hatia. Maisha yanaendelea na kazi inaendelea tunazungumzia masilahi ya Taifa.”     

Credit - Mwananchi

Wabunge wa CCM Wafunguka ya Moyoni Juu ya Sababu za Kushuka kwa Umaarufu wa JPM..!!

$
0
0

Wabunge wa chama tawala wameunga mkono ripoti ya Taasisi ya Twaweza inayoeleza kushuka kwa ushawishi wa Rais John Magufuli.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana na kubainisha kwamba umaarufu wa Rais huyo wa awamu ya tano umeshuka na kwamba anakubalika miongoni mwa maskini, wasio na elimu kubwa pamoja na waishio vijijini.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Lucy Mayenga amesema kilichoelezwa na Twaweza ni sahihi kwa sababu Rais amejielekeza kwa makundi hayo ambayo hayana mtetezi.

"Hao ndiyo watu wengi zaidi. Kiuchumi inakubalika," amesema Lucy.

Wakati Lucy akiendelea kutoa hoja zake, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega alitoa taarifa iliyopokelewa na mtoa hoja.

Uledi amesema: "Kwa muda wa utafiti, Rais alikuwa anapambana na vyeti feki, dawa za kulevya na mafisadi. Hao wote hawawezi kumpenda zaidi ya maskini ambao hawaguswi na mambo hayo."

Lucy ametoa maoni hayo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali unaoendelea bungeni.

JISAJILI USHINDE GARI LA BUREEEEE KABISA

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote... Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...

CHAKUFANYA NI Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Bonyeza Hapa >>> SHINDA GARI YA BURE <<< Kujisajili ni Bure tu...

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Shigongo amtolea uvivu Tundu Lissu

$
0
0

Mfanyabiashara na kada wa Chama Cha Mapinduzi, Erick Shingongo amemnyoooshea kidole Tundu Lissu na kusema anashindwa kuelewa kwanini Mwanasheria huyo amekuwa ni mpingaji wa mambo mazuri na kusema jambo hili linamshushia heshima.

Erick Shigongo amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema yeye kwanza anapongeza hatua alizochukua Rais Magufuli juu ya sakata la madini na kudai kuwa limekuwa na matokeo chanya kwani kiongozi wa Barrick amelazimika kuja Tanzania na kubembeleza yaishe.
"Namheshimu sana Lissu, sana tu.

Ni msomi wa sheria, tena mzuri tu! Lakini namshangaa, nashindwa kumwelewa kwa kitu kimoja kwamba kwa nini hawezi kukubali pale jambo jema linapofanyika? Mimi nadhani ni kujijengea heshima kubwa sana kuonyesha uzalendo pale nchi inapopambana na wizi wa maliasili ambazo hata hao Acacia wenyewe wameukubali, sasa kwa nini Lissu anaendelea kubeza kile kinachofanyika? Hakika hili linamshushia heshima" alisema Shingongo

Kauli ya Zitto Kabwe kufuatia kufungiwa kwa Gazeti la Mawio

$
0
0

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto kabwe amepinga vikali hatua ya kufungiwa kwa gazeti la MAWIO na kudai kuwa hatua hiyo inawanyima Wananchi mawazo mbadala.

==>Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto ameandika yafuatayo;

“Uamuzi wa kufungia gazeti la Mawio unapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia. Uhusika wa Marais wastaafu kwenye mikataba ya madini umesemwa na Rais Magufuli Mwenyewe sio Mawio.

"Hakuna mkataba ulioingiwa bila Baraza la Mawaziri kuidhinisha. Kitendo cha Kamati ya Rais kutuhumu Mawaziri wa zamani mbele ya Rais Magufuli na yeye Mwenyewe Rais Magufuli kusema hatapona mtu ilikuwa ni dhahiri kuwa Rais anawachimba watangulizi wake.

"Kwa sisi tuliofundishwa lugha ya Uongozi tuling’amua mapema kuwa Rais Magufuli alikuwa anawatuhumu wenzake. Hivyo Gazeti la Mawio lilitafsiri tu maelezo ya Rais. Kitendo cha Rais kuonya kuwa Marais wastaafu waachwe ilikuwa ni KUJISEMESHA tu na kufungia gazeti la Mawio ni ‘ panick ‘ ya Rais Magufuli baada ya kuwasema watangulizi wake.

"Kila wakati Rais analia kuhujumiwa na kutaka kuombewa; Adui wa Magufuli ni Magufuli mwenyewe.

"Serikali ifungulie Gazeti la Mawio mara moja bila masharti kwani kulifungia ni kuwanyima Watanzania mawazo mbadala kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea nchini kwetu.

na kumalizia kwa hashtag ya #PressFreedom #UhuruWaHabari.”

Wabunge wafunguka kushuka umaarufu wa JPM

$
0
0

Dodoma. Wabunge wa chama tawala wameunga mkono ripoti ya Taasisi ya Twaweza inayoeleza kushuka kwa ushawishi wa Rais John Magufuli.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana na kubainisha kwamba umaarufu wa Rais huyo wa awamu ya tano umeshuka na kwamba anakubalika miongoni mwa maskini, wasio na elimu kubwa pamoja na waishio vijijini.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Lucy Mayenga amesema kilichoelezwa na Twaweza ni sahihi kwa sababu Rais amejielekeza kwa makundi hayo ambayo hayana mtetezi.

"Hao ndiyo watu wengi zaidi. Kiuchumi inakubalika," amesema Lucy.

Wakati Lucy akiendelea kutoa hoja zake, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega alitoa taarifa iliyopokelewa na mtoa hoja.

Uledi amesema: "Kwa muda wa utafiti, Rais alikuwa anapambana na vyeti feki, dawa za kulevya na mafisadi. Hao wote hawawezi kumpenda zaidi ya maskini ambao hawaguswi na mambo hayo."

Lucy ametoa maoni hayo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali unaoendelea bungeni.

Picha ya Siku..Ujumbe Tosha kwa Wazee Wastaafu...!!!

Okwii Amalizana na Simba ..Hans Pope Amfuata Uganda na Kumsainisha Mchana Kweupee..!!!

$
0
0

Emmabuel Okwi amemalizana na Simba mjini Kampala, Uganda, leo hii.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amekutana na Okwi na kumalizana mjini Kampala.

Lazima Tuulizane Jamani ..Hivi Hii Tabia ya Simba Kudangnya Wachezaji Wameanza Lini..!!!?

$
0
0

Kuna hili suala limekuwa likitumiwa sana na Simba kwenye kulaghai wachezaji masikini wa Kitanzania.

Wenyewe wanasema "Ukicheza Simba ni sawa na kuwa njia panda ya ULAYA".

Nimemsikia yule beki wa kushoto aliyetoka Mbao FC someone Mlipili akihojiwa. Anasema kuwa amejiunga simba kwa kuwa unajua ni njia panda ya kwenda ULAYA.

Nikacheka na kujiuliza ' Hivi huyu dogo nani amemuaminisha kuwa ukicheza simba ndio una uhakika wa kuja kucheza Ulaya?. Hivi ni kweli ameahindwa kujiuliza yaliyomkuta Mgosi ambaye alijikuta akitupwa kwenye misitu ya DR Congo? Haoni jinsi Mkude anavyoendelea kuzeekea pale, amuoni Zimbwe JR na ubora wake wote hajawahi hata kuitwa Somalia akafanye trial?. Ni nani amemuaminisha kuwa akicheza pale simba kuwa yeye anaweza kufanikiwa kucheza soka la nje. Si watu wengine bali ni viongozi wa simba wanao walaghai hawa wachezaji.

Huwaga najiuliza ni wachezaji wangap ( kushinda Yanga SC) ambao Simba imewalea na kuwakuza mpaka wamefikia ubora wa kupata nafasi nje ya nchi? 

Okey! wengi wanasema Samatta amepata nafasi ya kwenda nje kwa sababu ya kucheza simba, ila ukweli halisi ni kwamba kwa kipaji alichonacho Jamaa ni dhahiri asingekaa Bongo hata kama asingechezea simba. Licha ya kuwa pale simba alipita tu kwa nusu msimu.

Kuna jamaa nimemuuliza maswali kadhaa, kwanza "ni mchezaji gani ambayo simba wanajivunia kapitia simba na kupata nafasi nje ya Nchi?"
Akajibu "Samatta."

Nikamuuliza "|akini mbona YANGA amepita mtu kama NONDA"?

Hakuweza kuendelea kujibu kwa hoja, lakini ki uhalisia unajiuliza kwanini simba wanajisifu kutoa wachezaji nje ya nchi ikiwa hawajatoa wachezaji kuizidi Yanga.? 

Wapenzi wengi wa simba hawawezi kujibu hili swali kwa ufasaha.

Hii inadhihirisha ni njama za ulaghai za baadha ya viongozi wa simba kuwafanya wachezaji waache kufuata ndoto zao za kutwaa MATAJI na kubaki simba wakiamini ipo siku watacheza ULAYA.

Kimenukaa..Makonda na Gambo Wapewa Onyo Bungeni..Ni Juu ya Tabia Zao za Kukamatkamata Watu Ovyo..!!

$
0
0

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia vibaya madaraka yao ya kukamata watu walio kwenye himaya zao.

Ametoa onyo hilo leo (Ijumaa) alipojibu maswali ya wabunge waliotaka kufanyika marekebisho ya sheria inayowapa mamlaka wakuu hao ya kuwakamata na kuwaweka ndani wananchi wanaowatuhumu kwa lolote.

Licha ya kubainisha kwamba sheria hiyo haina tatizo, waziri amesisitiza: "Ukamataji unatakiwa ufanywe kwa mtu aliyetenda kosa la jinai au anayehatarisha usalama. Isiwe kwa show-off tu. Na mhusika anatakiwa kufikishwa mahakamani mara moja, asishikiliwe tu."

Amesisitiza kwamba wakuu hao ni wawakilishi wa Serikali kwenye maeneo yao, hivyo hawatakiwi kutumia vibaya madaraka waliyokasimiwa.

Katika siku za karibuni wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakilalamikiwa kuwaweka watu kizuizini pasipo kuwa na sababu za msingi, miongoni mwao wakiwamo waandishi wa habari.

Thamani ya Mbappe Yawatisha Barcelona..!!!

$
0
0

Eric Abidal amesema haamini thamani ya mchezaji Kylian Mbappe imepanda hadi kufika Pauni 120 milioni huku akisema iwapo Barcelona inahitaji kusajili mshambuliaji wajielekeze kwa Osmane Dembele.

Thamani ya mchezaji uyo inaelezwa kupanda kutokana na timu vigogo za Ulaya kumhitaji.

Barcelona imeungana na Real Madrid, Manchester City, Arsenal, Manchester United pamoja na Liverpool kusaka saini ya mchezaji huyo.

Mbappe aliyeisaidia timu yake ya Monaco kutwaa ubingwa wa Ligue 1 msimu ulioisha ameweka rekodi kubwa zaidi ya uhamisho kumng’oa Uwanja wa Stade Louis II.

Mshambuliaji huyo amefunga mabao 26 katika mashindano iliyoshiriki Monaco.

“Kama tukifikiria kulipa zaidi ya Pauni 100 kama ilivyofanyika kwa Pogba wakati haendani na thamani halisi ya kiwango chake tutajikuta wachezaji wenye vipaji tunawanunua kwa Pauni 200 milioni,” alisema Abidal ambaye amestaafu soka kutokana na matatizo ya moyo.

Abidal alisema ni afadhari Barcelona ikaelekeza nguvu kwa Dembele kwa kuwa walionyesha nia ya kumhitaji tangu mwaka jana.

JISAJILI USHINDE GARI LA BUREEEEE KABISA

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote... Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...

CHAKUFANYA NI Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Bonyeza Hapa >>> SHINDA GARI YA BURE <<< Kujisajili ni Bure tu...

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Faida Utazozipata Mara Baada Ya kuacha kufanya Mambo Ya Msingi Kimazoea....!!!

$
0
0

Wakati nikiwa mdogo niliwahi kusikia wakubwa wangu wakisema ya kwamba mazoea yana tabu, kwa kipindi kile sikujua walikuwa wanamaanisha nini, ila kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kuelewa walikuwa wanamaniisha nini.

Nilichokuja kukigundua juu ya msemo huu ni kwamba mawazo ya binadamu ni mawazo ya mgando, naweza nikasema hivyo kwa sababu akili zetu tumezielekeza katika kufanya mambo katika mazoea. Kama mtu amezoea kula ugali muda wa mchana basi mtu huyo ukimpa wali muda wa mchana basi utamsikia mtu huyo akisema kwa kweli mimi kula wali mchana zijazoea.

Kwa mfano huo, angalia watu ambao wanafanya  biashara fulani ambazo hazilipi, ukimwambia wafanyabiashara hao wafanye biashara nyingine watakwambia ya kwamba hawawezi kufanya biashra ambayo hawaijaizoea. Kwa majibu ya aina hiyo ndipo nianapokubaliana na usemi ule usemao ya kwamba mazoea yana tabu, hii ni kwa sababu watu wengi tunashindwa kufanya vitu vingine tofauti na tulivyovizoea.

Lakini kama kweli unataka mafanikio ya kweli ni vyema kwa jambo lolote ambalo unalifanya acha mara moja tabia kufanya vitu kwa mazoea kwani mazoea ni dalili za uvivu, unashangaa huo ndio ukweli ambao upo wazi. Hivyo kwa kila jambo ambalo unalifanya hakikisha ya kwamba unatafuta mbinu nyingine za kuweza kuwa bora zaidi.

Lakini pia unashauriwa ya kwamba Ili kufikia mafanikio zaidi ya hapo ulipo, ipo haja na ulazima wa wewe kujituma na kufanya kazi kwa bidii sana nje ya yale mazoea uliyojiwekea. Kwa mfano, kama umezoea kufanya kazi kwa saa 8, ongeza masaa mengine manne ya ziada. Kama umezoea kuamka sa 12, anza kuamka saa 11 alfajiri. Fanya kitu ambacho kitakutoa nje ya mazoea yako yaani ‘comfort zone’. Kwa chochote kile unachokifanya, fanya nje ya mazoea yako.

Hivyo kila dakika na kila sekunde, kama kweli unataka kuondoka katika hali uliyopo kwa sasa unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuachana mara moja ile tabia ya kuishi katika misingi ya kimazoea (comfort zone) ambayo umeyazoea, na kufanya hivi  itakusaidia sana kujenga misuri mikubwa ya kukuwezesha kufika mbali  zaidi kimafanikio.

Endapo utandokana na hali ya kufanya vitu kwa mazoea tegemea kupata mambo makubwa ya fuatayo;

1   1. Utapata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi, hii ni kwa sababu utaongeza uwezo  na muda wako wa kufanya kazi.

 2. Lakini pia kama utaondokana na ile tabia ya kufanya kazi kwa mazoea basi jiandae kuwa mtaalamu kwa jambo ulifanyalo.

Hivyo tumalize kwa kusema ya kwamba unatakiwa kuachana mara moja tabia yako ya kufanya vitu kwa mazoe.

Tukushuru sana kila wakati kwa kuwa sehemu ya mafundisho  haya  kila siku, endelea pia kuwashirikisha wengine.

Imeandikwa na uongozi wa mtandao wa dira ya mafanikio,

Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
0713 04 80 35, 0652 015 024,
dirayamafanikio@gmail.com,
bensonchonya23@gmail.com,

Zifahamu Aina za Vyakula Vinavyoongeza Uhodari kwa Wanaume..!!!

$
0
0

Vyakula jamii ya nafaka ni miongoni mwa vyakula ambavyo vimejaa nishati nyingi ikiwa ni pamoja na nyuzinyuzi na sukari. Hivyo unaweza kuweka kwenye orodha ya vyakula anavyopaswa kula mwanaume.

Nafaka husaidia kuzalisha homoni ya testosterone kwenye damu hivyo kumuwezesha mtu kuwa na nguvu na hivyo kuepuka tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Ulaji wa vyakula vya nafaka visivyokobolewa ni muhimu zaidi kwani husaidia kutokupa mwili wa mafuta mengi kwani mafuta mengi ndani ya mwili huweza kuchangia kuharibu mishipa ya damu ikiwamo mishipa uume.

Moja ya viungo muhimu kwa wanaume ni pamoja na tangawizi ambayo husaidia kusisimua mfumo wa mzunguko wa damu mwilini ieleweke kwamba mzunguko wa damu unapokuwa vizuri ndani ya mwili husaidia hata damu kwenda vizuri sehemu za viungo vya uzazi pia (uume).

Aidha, ulaji wa karanga ni muhimu pia kwani ndani ya karanga kuna madini ya magnesium,zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za kiume pamoja na kuamsha hisia za tendo la ndoa.

Pia matumizi ya tunda la komamanga huweza kumsaidia mwanaume kujenga afya ya kimahusiano kutokana na tunda hilo kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na hivyo kumuongezea mtu uwezo wa kushiriki tendo hilo.

Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>