Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Fahamu Kazi 5 Muhimu za Mbegu za Tikiti Maji Zikiandaliwa Ipasavyo..!!!

$
0
0

Tikiti ni moja ya matunda ambayo hupendwa na watu wengi na yamekuwa na faida zake kiafya, lakini leo naomba tuzifahamu hizi faida za mbegu zake za tunda hilo.

1. Husaidia kulinda afya ya moyo.
Hii ni kutokana na kuwa na madini ya kutosha ya magnesium ndani ya mbegu hizo.

2. Husaidia kwa wenye chunusi
Unapotumia mafuta ya mbegu za tikiti huweza kuwasaidia wale wenye tatizo la chunusi. Ambapo mafuta hayo utapaswa kuyapaka kwa kutumia pamba kwenye sehemu zilizoathirika.

3. Husaidia kuimarisha kinga za mwili
Kutokana na kuwa na madini ya magnesium ya kutosha hiyo husaidia kuimarisha kinga zako za mwili na kufanya kutokumbwa na maradhi mara kwa mara.

4. Huboresha mfumo wa uzazi kwa wanaume
Wanaume wanaotumia mbegu hizi huwa katika hali nzuri kwenye tendo la ndoa na uzalishaji kwa ujumla.

5. Husaidia kuzuia tatizo la nywele kukatika
Mbegu hizi zina utajiri wa fatty acid ambayo husaidia kuboresha afya ya nywele

Aina Kubwa Tatu Za Watu Na Nafasi Zao Katika Mafanikio..!!!!

$
0
0

Wewe ni Mtu wa aina gani?

Hili ni swali ambalo kimsingi kila mmoja lazima ajihoji kwa wakati wake.

Ukisoma katika vitabu mbalimbali vya dini vinasema ya kwamba binadamu wote ni sawa, hii ikiwa na maana ya kwamba ukiangalia katika mfano wa vitu kijinsia, organi pamoja homoni.

Lakini ukija katika ulimwengu wa mafanikio binadamu hatufanani hata chembe na hii ndiyo maana kuna watu maskini na wengine ni matajiri, na nilichokigundua ni kwamba utofati wetu huanza rasmi katika fikra.

Fikra ndiyo inayotufanya tuweze kuwa tofauti.  Hivyo ili binadamu  tuweze kuwa sawa ni vyema kila mtu aweze kutafakari yeye ni mtu wa aina gani? Ukishapata majibu ndipo utapojua  wewe ni wa aina gani na unawezaje kusonga mbele kimasha.

Ili mkupata majibu ya swali hilo, siku ya leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kuweza kujua wewe ni mtu wa aina gani. Hivyo yafutayo ni makundi ya watu ambao wapo hapa duniani katika kuyasaka mafanikio.

Watazamaji.

Aina ya kwanza ya watu wanaopatikana katika duniani hii ni watazamaji. Tabia za watu hawa huwa kama ifuatavyo;

Wao ni waoga katika kujaribu kufanya kitu kipya.

Wao huamini zaidi katika kushindwa kuliko kufanikiwa.

Wao ni wazungumzaji wazuri kwa yale ambayo yanatokea katika jamii.  Watu hawa huzungumza zaidi masuala ambayo huwa hayawasaidii mfano wa mambo hayo ni mpira, siasa na matukio mbalimbali yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na mambo ya nje ya mitandao ya kijamii.

Lakini kubwa kabisa watu hawa  huwa hawana ubunifu wowote, na huwa wanaishi katika misingi ya kuwaangalia watu wanaopenda (role model), kwa misingi hiyo utagundua ya kwamba aina hii ya watu huishi maishi ya ganda la ndizi, kwa sababu husubiri mtu afanye jambo fulani ili na wao waanze kufanya.

Wapotezaji.

Kundi hili lina watu lukuki sana. Na watu ambao wapo katika kundi hili huwa wana tabia zifuatazo;
Kazi yao kubwa huwa ni kuwangalia watu wengine wanafanya nini katika maisha yao. Hata hivyo katika kundi hili, watu wengi huwa wapo kwa ajili ya kuwakosa wengine kwa yale wayafanyao, na katika kukosoa huko huwa ni katika kukatisha tamaa zaidi kuliko kujenga.

Watu ambao wapo katika kundi hili ni wale ambao wameathiriwa kwa kiwango kikubwa ugonjwa wa wa kuahirisha mambo ya msingi.

Washindi.

Kundi la tatu la mwisho ni kundi la washindi, kundi hili ndilo lenye watu wachache na wenye mafanikio. Na kundi hili lina watu wachache kwa sababu watu wengi wameng’angana’ katika makundi mengine ambayo nimekwisha yaelezea hapo awali.

Watu ambao ambao wapo  katika kundi hili huwa wanasifa zifutazo;

Wao hujua ni nini wanachokitaka katika maisha yao.

Wao hupanga na kukamilisha yale waliyoyapanga kwa wakati.

Lakini kubwa zaidi watu ambao wapo katika kundi hili huwa si wabinafsi kama walivyo makundi wangine, wao huwa wapo tayari kuwasaidia wengine.

Pia ni  watu ambao wamewekeza muda mwingi sana katika kujifunza na kutafakari.

Hayo ni machache kati ya mengi yaliyopo katika kundi hili.

Hayo ndiyo makundi matatu yaliyopo katika ulimwengu huu, Mara baada ya kuona makundi matatu ya watu yanayotufautisha hapa duniani. swali linakuja wewe mwenzangu na mimi upo kundi gani? 
Kama unahisi upo kundi ambalo hustahili, unachotakiwa kufanya ni kuhama mara moja na kuhamia katika kundi lenye mafanufaa kwako.

Asante kwa kuwa pamoja nasi kila wakati nikutakie siku njema na mafanikio mema.

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.

0757909942,
dirayamafanikio@gmail.com,

Pilipili Manga Inatumika Sana Wakati Huu wa Mfungo, Zifahamu Faida Zake 4 za Kiungo Hicho..!!!

$
0
0

PILIPILI manga ni mbegu ndogo ndogo ambazo ukiziangalia vizuri sana basi zinataka kufanana na mbegu za papai. 

Rangi yake ni nyeusi hivi na ladha yake ni mfano wa pilipili. 

Moja ya faida za kiungo hiki ni pamoja na kuwasaidia wale wenye matatizo ya upumuaji na kuongeza hamu ya kula, hivyo ni kiungo kizuri sana kwa wale wenye kukosa hamu ya chakula.

Aidha, pilipili manga pia inaelezwa kutoa ahueni kwa wenye matatizo ya tumbo pamoja na kusaidia kwa wale wenye tatizo la kuhara.

Kazi nyingine ya kiungo hiki mwilini ni pamoja na kupunguza uzito kwa wenye shida ya uzito mkubwa sambamba na kuboresha afya ya ngozi na kuifanya kuonekana vyema zaidi.

Mbali na hayo, kiungo hiki kuna wakati kinapotumika vizuri huweza kutoa ahueni kwa wenye tatizo la vidonda vya tumbo kutokana na kuwa antioxidants pamoja anti-inflammatory.

Zingatia.
Matumizi ya pilipili manga huweza kumsababishia mtumiaji kupiga chafya pia si nzuri kwa waliotoka kufanyiwa uparesheni hasa wa tumbo.

Mtanzania Akamatwa Uingereza kwa Kupost Picha za Maiti wa Ajali ya Moto Kwenye Facebook...!!!

$
0
0

Kweli jasiri haachi asili maana huku kwetu watu hukimbilia kupost picha maiti hata zikiwa uchi ili mradi waonekane wametoa breaking news,haya bwana mwaikambo enjoy your jail stay

A neighbour who posted pictures on Facebook of a dead victim believed to have leapt to his death from the Grenfell Tower inferno has been jailed for three months.

Omega Mwaikambo, 43, was hauled before the courts after posting the distressing picture of the body bag and then close ups of the male victim after opening it on Wednesday morning.

He posted one video and two pictures of the body bag with the man inside and then later five pictures of the victim's face and body after opening it to look inside.


Today at Westminster Magistrates Court he pleaded guilty to two counts of sending by a public communications network an offending, indecent or obscene matter.

Kesi ya Uhujumu Uchumi; Kitilya na Wenzake Wapokea Awamu ya Kwanza ya Vielelezo Kutoka Uingereza..!!!

$
0
0

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umeieleza mahakama kuwa wamepokea awamu ya kwanza ya vielelezo kutoka nchini Uingereza.

Hayo yameelezwa jana na wakili wa Serikali, Christopher Msigwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Msigwa ameiambia mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wanatarajia awamu ya pili ya vielelezo kuwasili nchini Tanzania wakati wowote kuanzia sasa.

Hata hivyo wakili wa utetezi, Mwanahamisi Adam ameuomba upande wa mashtaka kueleza muda muafaka ambao utatumika kwa vielelezo hivyo kufika nchini.

Aidha Hakimu Mkeha amewaambia upande wa mashtaka huo muda wowote wanaoutaja wahakikishe unaangukia ndani ya siku 14 na ikishindikana basi Juni 30 mwaka huu waeleze vielelezo hivyo vitafika ndani ya siku ngapi.

Miezi miwili iliyopita upande wa mashtaka uliieleza mahakama kuwa upalelezi dhidi ya kesi hiyo uliokuwa unafanywa ndani ya nchi umekamilika na kuwa bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.

Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza

Rais Magufuli Anaweza Kufanya Kama Botswana na Namibia Katika Madini...Inawezekana ni Jambo la Kuamua Tu!!

$
0
0

Nchi ya ya Botswana na Namibia waliweza kuwa na 50/50 shares Katika migodi ya nchi zao kwanini Tanzania tushindwe??

Ni kuamua tu kukaa meza ya majadiliano na wawekezaji na kufikia makubaliano ya kila mmoja anufaike na inawezekana kabisa.

Hapa hatutaki tena watu wa kujifungia ndani ya mahoteli makubwa na kujificha na mikataba.

Wakina Tundu Lissu,Prof Issa Shivji,Reginald Mengi,Prof Kabudi,Ester Matiko,Mzee Mpinga na wengine wengi tu kwa kuanzia ni muhimu ktk timu ya majidiliano

Tunaweza kufanikiwa kabisa kuwa shares 50/50 kama nchi zingine na tukanufaika na madini.

Sakata la Mchanga wa Madini..Wanasiasa Wageukia Mikataba Mikubwa..Wapinzani Wataka Juhudi za Magufuli Ziungwe Mkono..!!

$
0
0

WAKATI agizo la Rais John Magufuli kutaka liundwe jopo la kupitia sheria zote za madini na kuzipeleka bungeni ili zipitishwe likisubiri utekelezaji, baadhi ya wanasiasa wametaka mikataba yote mikubwa inayoingiwa na Serikali ipelekwe katika chombo hicho cha kutunga sheria.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, walisema Taifa limeingia mikataba mingi yenye utata inayoweza kuzua sintofahamu, kama ilivyokuwa kwa mikataba na sheria za madini wakitaka jambo hilo lifanyike mapema ili kukwepa wizi na unyonyaji unaofanywa na baadhi ya wawekezaji.

Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli alipokea ripoti ya pili ya Kamati aliyoiunda kuchunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu mchanga wa madini unaosafirishwa nje, kuagiza kupitiwa kwa sheriza zote za madini na kutaka zipelekwe bungeni, jambo ambalo limepongezwa na watu mbalimbali.

Tayari kampuni ya Acacia ambayo imetajwa katika ripoti hiyo kulitia hasara Taifa ya Sh trilioni 108.06 imekubali kukaa meza moja na Serikali na kufungua njia ya mazungumzo.

Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ambayo ni mmliki mkubwa wa kampuni ya Acacia, Profesa John Thornton,  juzi alikutana na Rais Magufuli, Ikulu na kukubali kukaa pamoja na Serikali kuzingatia maslahi ya pande zote na kuwa tayari kulipa fedha zote inazopaswa kuilipa Tanzania.

“Suala hapa si mikataba ya madini pekee. Anapaswa kuruhusu mikataba yote yenye maslahi ya nchi ipelekwe bungeni. Katika hili tunamwomba sana Rais kutekeleza, maana tayari ameshaonesha utashi wa kisiasa, anachokipigania ni malengo ya wengi, ikiwemo CCK,” alisema Constatine Akitanda, Mwenyekiti wa Chama Cha Kijamii (CCK).

Kwa mujibu wa ripoti ya Kamati hiyo, mikataba ya madini iliyoingiwa  tangu mwaka 1998 ndiyo iliyosababisha upotevu wa kiasi hicho cha fedha,  ambazo zingetumika katika bajeti ya miaka mitatu.

Kwa hali hiyo, ilitoa mapendekezo 21, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua Dk Abdallah Kigoda (marehemu), Daniel Yona, Nazir Karamagi, William Ngeleja na Profesa Sospeter Muhongo ambao waliwahi kushika nafasi za uwaziri wa nishati na madini kwa vipindi tofauti.

Wengine ni wanasheria wakuu wa zamani na manaibu; Andrew Chenge, Johnson Mwanyika, Felix Mrema na Sazi Salula.

Wamo pia makamishina wa madini na wakuu wa idara ya mikataba wa zamani; Paulo Masanja, Ally Samaje, Dk Dalaly Kafumu, Maria Ndossi na Julius Malaba.

Katika maelezo yake, Akitanda alisema: “Unakumbuka hapa watu walikunja twiga na kuwasafirisha bila ushahidi kupatikana, tumeona utayari wake, tuko tayari kumsaidia kwani maendeleo ni kwa watu wote, yapo mataifa yanamtukana ila kwa hili lazima Acacia watubu.”

Katibu Mkuu wa chama cha Tanzania Labour (TLP), Nancy Mrikaria alisema ni wakati mwafaka kwa mikataba yote kufika bungeni ili ipitiwe ili kunufaisha wananchi wote.

Alisema Rais Magufuli ameonesha utofauti tangu aingie madarakani, hivyo dhamira yake itaonekana zaidi kama atakubaliana na mapendekezo hayo kwani ni dhahiri mikataba ina changamoto nyingi.

“Ukiwa mpinzani si lazima upinge kila kitu, hivyo kwa hili linapaswa kupongezwa na ndiyo maana tunamshauri aruhusu mikataba yote ipite bungeni ili dhamira ya Rais iweze kuonekana kivitendo,” alisema.

Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Danda Juju alisema hatua anazochukua Rais kwa sasa ni ishara tosha kuwa ameanza kutekeleza madai ya wapinzani ambao wamekuwa wakililia Katiba mpya ambayo itaonesha aina ya uongozi wa nchi.

“Suala analofanya Rais ni sahihi na lisiishie hapo liende mbali kwa kuhakikisha mikataba kama ya maliasili ambayo inalalamikiwa, ifikishwe bungeni kwa maslahi ya nchi,” alisema.

Alisema kinachohitajika ni haki kutendeka kwa kila upande ambayo itakuwa inahusika katika mabadiliko hayo ili kuepusha mgogoro kwa pande zinazokinzana.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wananchi (JUKECUF), Severine Mwijage alisema mapendekezo ya Rais ndiyo wamekuwa wakiyapigania miaka yote, hivyo uamuzi huo ni sahihi ila isiwe mikataba hiyo pekee.

Mwijage ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, alisema yote yanayotokea sasa yanachangiwa na mikataba mibovu, ila kila wakati wamekuwa wakionekana kuwa wanapiga kelele za chura.

Alisema kimsingi suala la uvunjaji mikataba si jambo rahisi, lakini kupitia upya ni hatua muhimu kwa maslahi ya nchi, hivyo ikifika wataipitia ili iendane na hitaji la nchi.

“Mikataba yote ni mibovu hivyo anapaswa kuleta yote kama ana nia ya kusaidia Watanzania kupiga hatua kiuchumi, lakini kama anafanya propaganda hakutakuwa na tija,” alisema.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alisema pamoja na kupeleka mikataba bungeni, kinachohitajika ni kuwa na sera moja ambayo inazungumzia uvunwaji wa rasilimali za nchi.

Profesa Baregu alisema pia dhana hiyo itafanikiwa iwapo Katiba mpya hasa ile ya Jaji mstaafu Joseph Warioba ndiyo mkombozi wa rasilimali za nchi.

“Mimi nadhani upo umuhimu wa kuzungumzia sera ya uvunaji rasilimali za nchi upya na hili lipewe nguvu na Katiba kama Watanzania walivyokuwa wamependekeza katika Katiba ya Warioba,” alisema.

Alisema wananchi wamekuwa wakisisitiza uwepo wa sheria ambazo zinatunza na kulinda rasilimali za nchi na kutoa rai kwa wananchi kuachana na dhana ya kushambuliana.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa alisema anaamini kila sekta ina udhaifu, hivyo ni vema Rais akaangalia mikataba yote na isiwe ya madini pekee.

“Sisi ACT tumekuwa tukisema ukweli kila mara kuhusu rasilimali za nchi, naamini tukiwa hivyo wote hakuna kitakachoshindikana,” alisema.

Credit - Jambo Leo

Wamtaka Mbunge Wao Ajiuzulu kwa Kutajwa Kwenye Ripoti ya Mchanga wa Madini..!!!

$
0
0

BAADHI ya wananchi wa Jimbo la Igunga Mkoani Tabora wamemtaka Mbunge wao Dk Dalaly Kafumu ajiuzulu ubunge kwa walichodai ni kushindwa kutumia madaraka yake vizuri wakati akiwa Kamishna wa Madini.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti , baadhi ya wananchi hao, Oscar Thomas, Godfrey Batoba, Pius Roben na Regina Jackson, walisema ni vema mbunge wao akajiuzulu kwa kuwa miongoni mwa wanaotuhumiwa kuiingizia hasara nchi kwa kuingia mikataba mibovu ya madini na kujinufaisha.

Thomas alibainisha kuwa kazi anayofanya Rais John Magufuli ya kufuatilia rasilimali za wananchi inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake huku wakimwomba kutoonea huruma wahusika walioisababishia nchi hasara.

Mwenyekiti wa Wazee wa Wilaya, Kassim Ally akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, alisema walimwomba Rais Magufuli kutokatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu kwani wako nyuma yake wakimpa ushirikiano.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya, Costa Ollomi na wakem, Mwanamvua Killo walisema kazi anayofanya Rais Magufuli imeleta heshima ndani ya chama na Serikali na kuwataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati waliohusika wakihojiwa na vyombo husika.

Kuhusu Mbunge kujiuzulu alisema Ollomi alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa tayari Rais alishatoa maelekezo ya kuchukuliwa hatua kwa waliotajwa na Kamati.

 Dk Kafumu alitafutwa kupitia simu yake ya kiganjani   ili kuzungumzia matakwa hayo lakini hakupokea simu licha ya kupigiwa zaidi ya mara nne.

Credit - Jambo Leo

Raia Naigeria Afanya Harusi ya Bilioni 14.3 kwa Usiku Mmoja Tu..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo Jumamosi ya 17/6/2017..!!!

MAGAZETI YA LEO 17/6/2017

Zitto Afunguka Juu ya Kikao cha Bosi wa Barrick na JPM,,,Adai Hayatakuwa na Tija wala Jipya kwa Taifa..!!!

$
0
0

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) amesema suala la Serikali kukaa na wawekezaji si jawabu la tatizo lililotokea bali kinachotakiwa ni Katiba Mpya yenye kumilikisha utajiri wa nchi kwa wananchi.

Kauli hiyo ya Zitto imekuja siku moja baada ya Rais John Magufuli kukutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambaye ni mmiliki mkubwa wa Kampuni ya Acacia Mining Limited, Profesa John Thornton na kukubaliana kampuni hiyo kufanya mazungumzo na Serikali yake.

Pia Profesa Thornton alisema kampuni yake itakuwa tayari kulipa fedha ambazo Tanzania imepoteza kutokana na uendeshaji wa shughuli zake nchini ikiwa italazimika baada ya majadiliano.

Hatua ya kampuni hiyo kufanya mazungumzo na Rais Magufuli inatokana na taarifa  ya Kamati ya pili ya wachumi na wanasheria iliyopewa jukumu la kuchunguza mikataba ya madini na kiwango kilichopo kwenye makanikia yaliyosafirishwa nje na kwenye kontena 277 zilizozuiwa bandarini Dar es Salaam.

Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli alipokea taarifa ya Kamati hiyo ambayo ilieleza kuwa Acacia haijasajiliwa na haipo kisheria nchini, jambo ambalo liliibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mengine hususan kwa wanasiasa.

Lakini akizungumza Dar es Salaam jana, Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo alisema chama chake kilihadharisha jambo hilo katika kongamano lake la Rasilimali Madini lililofanyika Juni 3 Dar es Salaam.

“Tulihadharisha hili Juni 3 kwamba mwisho wa siku Serikali itakaa mezani, hivyo tuombe sana hoja za Serikali ziwe na ushahidi wa kutosha, vinginevyo tutaendelea kulia kuibiwa daima,” alisema.

Aliongeza kuwa jawabu la changamoto zilizojitokeza si mazungumzo na wawekezaji, bali ni Katiba mpya yenye kumilikisha utajiri wa nchi kwa wananchi wa Tanzania milele, ambao ndio rasilimali yao.

Juni 3 ACT-Wazalengo ilifanya kongamano la Rasilimali Madini la kujadili nchi inavyonufaika na sekta ya madini ambalo liliibuka na maazimio 10, likiwamo la kutaka mjadala mpana kulinda aina zote za madini nchini.

Watoa mada katika kongamano hilo lililenga kujadili kwa kina sekta hiyo baada ya hivi karibuni Rais John Magufuli kuunda Kamati ya Kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa nje na kutoa ripoti iliyoshitua Taifa.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT), Dk Rugemeleza Nshala, Mwenyekiti wa Taasisi ya ONGEA, Dennis Mwendwa na Nico Kajungu wa Numet.

Kamati iliyochunguza mchanga wa madini chini ya uenyekiti wa Profesa Abdulkarim Mruma, ilibaini kuwa kontena 277 zilizozuiwa katika bandari ya Dar es Salaam zina tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya kati ya Sh bilioni 676 na Sh trilioni 1.147.

Kiwango hicho kilikuwa tofauti na ambacho Kamati hiyo ilielezwa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) kwamba kontena hizo zilikuwa na tani 1.1 za dhahabu.

ACT-Wazalendo ilieleza kuwa mbali na kutaka uchunguzi ufanyike kwa madini yote, kongamano hilo lilibaini kuwa takwimu za Kamati zina walakini.

“Takwimu hizi zikikubaliwa kama zilivyo, zitaifanya Tanzania kuwa mzalishaji namba moja wa dhahabu Afrika. Hatuhitaji kupika takwimu au kuongopa, ili kushinda vita vya rasilimali.

“Kunapaswa kuwa na timu huru ya kupitia takwimu zilizotolewa na Kamati ya Profesa Mruma ili kuthibitisha uhalali wake. Kuwa na takwimu sahihi ni muhimu sana kwenye kupata majawabu,” lilieleza azimio la pili.

Azimio lingine ni kwamba katika mapambano ya kulinda rasilimali madini, ni lazima yafanyike mabadiliko ya sheria ya madini na Katiba, ili kufanya madini na maliasili zingine kuwa mali ya wananchi milele.

“Serikali ibadilishe mfumo wa kuchimba madini kwa kuhamia kwenye mfumo wa kugawana mapato ili kuondokana na mfumo wa sasa ambao kimsingi una njia nyingi za kukwepa kodi kwa mbinu halali kabisa,” kilieleza chama hicho katika azimio lake la nne.

Pia kilitaka sauti za wafanyakazi katika migodi ziheshimiwe, haki zao zilindwe na washirikishwe kikamilifu kwenye uamuzi kuhusu sekta ya madini.

“Mikataba ya madini izingatie kuwa kuna uharibifu wa mazingira kwenye uchimbaji madini. Mikataba iwe na vifungu imara vya kulinda mazingira.

“Watu wote walioshiriki kuingia mikataba ya madini na kufanya uamuzi unaolitia Taifa hasara wawajibishwe na kuchukuliwa hatua bila kujali vyeo vyao au lini makosa yalifanyika.”

Katika azimio la nane, kongamano hilo lilipendekeza kufanyika kwa usanifu wa madini ya tanzanite likisema: “Sisi ndio wazalishaji pekee wa tanzanite. Hivyo tuna ukiritimba unaotuwezesha kushawishi kampuni za vito vya tanzanite kujenga viwanda Tanzania.”

Pia lilitaka mikataba yote ya madini ipitiwe upya, kama ikihitajika kurekebishwa ifanyike hivyo ili kulinda maslahi ya umma, kwamba iwapo mikataba husika itabainika kuwa ya hovyo ivunjwe kama ilivyotokea katika nchi za Bolivia, Venezuela, Iran na Botswana.

“Mjadala wa rasilimali madini usiachwe mikononi mwa Serikali ya CCM ambayo ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo sasa,” lilieleza azimio la 10 la kongamano hilo.

“Wananchi wote kupitia asasi za kiraia, vyama vya siasa na umma kwa ujumla washiriki kuhakikisha mjadala juu ya rasilimali madini unafikishwa mwisho kwa maslahi ya umma.”

Kalapina Awataka Wale Waliomteka Roma Mkatoliki Wakamteke na Yeye Ili Awaonyeshe Kazi..!!!

$
0
0

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmoja wa Watu wanaoaminika kuwa ni Mbabe kama siyo Mtemi na Ngumi Jiwe wa kutukuka Kalapina jana wakati akihojiwa na Kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds fm aliamua kutema nyongo / kuvunja ukimya juu ya Kitendo cha Msanii mwenzake na mshikaji wake Roma Mkatoliki Kutekwa.

Kalapina ambaye anasifika mno kwa Usela / Uhuni na ukorofi ambao kiuhalisia kweli anauweza alianza kwanza kwa kumpa pole Roma Mkatoliki kwa yote yaliyomkuta ila hakusita pia kumlaumu kidogo Roma kwa kumwambia kuwa asingekubali kirahisi rahisi kubebwa na kuingizwa katika Gari na Kutekwa.

Ifuatayo ni nukuu Kuntu kabisa kutoka kwa Kalapina ambayo nadhani ni ujumbe tosha kwa Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba Beach ( Watekaji ) “ Nakuambia Mimi nina hamu sana hao Watekaji siku wakosee tu waje waniteke Mimi kisha wajue kuwa kuna Watu tumebarikiwa kwa Ukorofi na Ukorofi tunaujua. Mimi wakija kama 10 na kutaka kuniteka basi nakuhakikishia lazima wakati wanafanikiwa kuniingiza katika Gari lao na kuniteka basi tayari name huku nyuma nitakuwa nimeshawaua Watatu au Wanne huku waliobaki nikiwaachia maumivu ya Kutukuka kabisa. Mdogo wangu Roma ulilegea sana na siku nyingine usifanye hivyo ukiona Mtu anataka kukuteka au ana nia mbaya nawe usimcheleweshe na badala yake mpe Kipondo / Kipigo pale pale “ mwisho wa kumnukuu Kalapina.

Haya Watekaji ( Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba beach ) Kalapina huyo anawakaribisheni mkamteke na Yeye ili mkapate Kipondo / Kipigo ambacho inawezekana hata huko Chuoni Kwenu Wakufunzi wenu ama hawakuwafundisha au walisahau kuwafundisha.

Shikamoo Kalapina

Samatta Awaita Mbeya City Mezani..Adai Yeye ni Mchezaji Huru..!!!!

$
0
0

Mbeya City inamuwinda mshambuliaji wa Prisons, Mohamed Samatta katika kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao.

Samatta tayari imefanya mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na Prisons ingawa mwenyewe amesema mazungumzo hayo hayamzuii kupokea ofa nyingine.

Kocha wa Mbeya City, Mmalawi Kinnah Phiri alipendekeza usajili wa Samatta ambapo alisema kuwa mchezaji huyo atasaidia kuziba pengo la Kenny Ally aliyesajiliwa na Singida United kwa madai ya kwamba uwezo wao kisoka unafanana.

Samatta msimu uliopita ameifungia Prisons mabao matano katika Ligi Kuu Bara.

Samatta alisema mkataba wake na Prisons ulikuwa wa mwaka mmoja, amefanya mazungumzo na viongozi ambapo anaamini kwamba watafikia muafaka na anafurahia maisha ya hapo kwa kipindi chote alichoishi na Prisons.

"Kuhusu Mbeya City pengine wao wameniweka kwenye mipango yao ila bado hawajaniambia jambo lolote, nimemaliza mkataba na Prisons tumezungumza ila bado hatua ya mwisho hivyo sizuiliwi kupokea ofa kutoka timu nyingine kwani mimi ni mchezaji huru."

Benki ya Dunia Yaitabiria Tanzania Kuwa Nchi ya Tatu Yenye Uchumi Unaokuwa kwa Kasi Zaidi Afrika..!!!

$
0
0

Benki ya dunia imeitabiria Tanzania kuwa ya 3 kwa uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi Africa baada ya Ethiopia na Ghana. Uchumi wa Tanzania utakuwa kasi ya 7.2% nyuma ya Ghana 7.8% na Ethiopia 8.3

======= 

The World Bank (WB) has forecasted Tanzania as the third fastest growing economy in Africa next year after... 

The World Bank (WB) has forecasted Tanzania as the third fastest growing economy in Africa next year after Ethiopia and Ghana. In a brief report, Global Economic Prospects: Sub-Saharan Africa, the WB predicted Tanzania to grow 7.2 per cent behind Ghana 7.8 per cent and Ethiopia 8.3 per cent.

“Growth in non-resource intensive countries is anticipated to remain solid, supported by infrastructure investment, resilient services sectors, and the recovery of agricultural production,” WB said in a statement.

The report brief further said weather-related risks are elevated in East Africa. “Worsening drought conditions will severely affect agricultural production, push food prices higher, and increase food insecurity in the subregion,” the bank said.

On the Sub-Sahara outlook, the bank said growth in the area was forecast to pick up to 2.6 per cent in 2017 and to 3.2 per cent in 2018, predicated on moderately rising commodity prices and reforms to tackle macroeconomic imbalances.

Per capita output was projected to shrink by 0.1 per cent in 2017 and to increase to a modest 0.7 per cent growth pace over 2018-19. “At those rates,” World Bank said “growth will be insufficient to achieve poverty reduction goals in the region, particularly if constraints to more vigorous growth persist”.

Growth in South Africa, the second biggest economy in Africa, is projected to rise to 0.6 per cent in 2017 and accelerate to 1.1 per cent in 2018. Africa’s biggest economy, Nigeria, is forecast to go from recession to a 1.2 per cent growth rate in 2017, gaining speed to 2.4 per cent in 2018, helped by a rebound in oil production.

Growth is forecast to jump to 6.1 per cent in Ghana in 2017 and 7.8 per cent in 2018 as increased oil and gas production boosts exports and domestic electricity production

Source: WORLD BANK FORECASTS TANZANIA AS THE THIRD FASTEST GROWING ECONOMY IN AFRICA NEXT YEAR - Corporate Digest

Wabunge Watifuana Bungeni Kisa Sakata la Makinika na Mikataba ya Madini..!!!

$
0
0

BUNGE limeingia siku ya nne jana kujadili Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/18, huku wabunge kadhaa wakiraruana kuhusu ripoti ya pili ya kamati iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli, kuhusu mchanga wa dhahabau (makinikia) pamoja na mikataba ya madini.

Ripoti ya kamati hiyo pamoja na watu wengine  iliwataja baadhi ya vigogo wa Serikali kuhusika moja kwa moja katika kusaini mikataba mbalimbali ya madini na kupendekeza vyombo vya dola viwachunguze.


Waliotajwa na ripoti hiyo ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja  katika Serikali ya awamu ya nne kuanzia 2008 hadi 2012.

Mwingine ni aliyewahi kushika wadhifa wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, kuanzia mwaka 1993 hadi 2005 na Dk. Dalaly Kafumu aliyepata kuwa Kamishina wa Madini katika wizara ya Nishati na Madini kati ya mwaka 2006 na 2011.

Aliyekuwa wakwanza kuchafua hali ya hewa bungeni ni Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga (Chadema), aliyemkatisha Ngeleja wakati akichangia bajeti hiyo aliyewataka wabunge wanyanyuke kwenye viti vyao ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli katika kupambana na wizi wa rasilimali za taifa.

Wakati Ngeleja akichangia, Haonga alisimama na kuomba kumpa taarifa Ngeleja ambapo alisema. “Naomba kutoa taarifa, mheshimiwa Ngeleja yeye ni miongoni mwa wabunge waliotajwa katika kashfa hii ya makinikia, anapokuwa anachangia atuambie uhusika wake katika hili”.

Kabla Ngeleja hajasimama kujibu hilo, Mwenyekiti wa Bunge aliyekuwa akiongoza kikao hicho jana asubuhi, Mussa Zungu, alisema hiyo siyo taarifa na hivyo kumtaka Ngeleja kuendelea na mchango wake.

Hata hivyo Ngeleja kabla ya kuendelea alisema: “Haonga mdogo wangu anajua kutuhumiwa si kupatikana na hatia, maisha yanaendelea.

“Sisi Bunge tumetoa pongezi kwa rais kwa kazi kubwa aliyofanya, tumpongeze mheshimiwa rais, kwa hali tuliyofikia tunahitaji usimamizi wa sera, nimekuwa waziri kwa miaka mitano, tungeanza utaratibu wa kawaida kuboresha mikataba ya madini ingetuchukua miaka mingi kufikia hapa,” alisema.

Naye Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma (CCM), akichangia bajeti hiyo alipigilia msumari wa moto kwa kusema waliohusika wote wakamatwe kabla ya kuhojiwa.

“Nampongeza Rais na Profesa (Nehemiah Osoro- Mwenyekiti wa Kamati ya pili ya makinikia), aliwataja watu waliosababisha matatizo, wengine wako CCM, tusema ukweli tuache mzaha.

“Wengine wanaweka katika twitter eti sihojiwi mpaka mahakamani, wengine tunawaheshimu, mzee wetu humu ndani anatwitt eti hawezi kuhojiwa hadi mahakamani, kila mwaka, kila tuhuma anatajwa kwani yeye ni nani?

“Kama kuna uwezekano wakamatwe washtakiwe, wanaotusumbua humu ni hao hao waliotajwa….. katajwa Ngeleja, katajwa Chenge, katajwa Kafumu” alisema Msukuma na kuendelea:

“Nimefuatilia taarifa zote hata Rais Magufuli alipomtumbua aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,..sijui kama yumo humu….nina hamu naye.

“Rais Magufuli alisema aliyaamini ma – vyeti, tuangalie uwezo wa mtu ikiwezekana mawaziri wafanyiwe usaili kabla ya kupata nafasi.

“Tunaamini madigrii mwisho wa siku tunakuta wezi, tufanye kitu cha msingi, tusiamini haya madigrii, kuamini haya madigrii kunatuletea matatizo, zile Phd zimerudi kwetu,”alisema Musukuma.

Alisema watu wengi hawana vyeti, hawana elimu, Katiba inasema ukitaka cheo fulani inataka elimu kubwa sasa wamefoji hayo madigrii, uwezo ni mdogo makaratasi makubwa.

Kubenea

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), alisema wabunge wa CCM wamezungumza mengi kwamba wapinzani hawaungi mkono hoja ya kukomboa rasilimali.

Alisema wapinzani hawapaswi kuingia kwenye lawama hizo kwakuwa hawahusiki katika mikataba yote kwani hawajawahi kuingia katika Serikali na kwamba kazi hiyo ni ya CCM.

“Sisi hatuhusiki katika mikataba yote iliyofungwa, hatujawahi kuingia katika Serikali, hii ni kazi ya CCM…ni dudu lao wameliamsha wahangaike nalo.

“Imekuwepo hoja ya msingi kwamba eti tumeibiwa katika rasilimali zetu, tumeibiwa na watu waliokuja kuwekeza, mikataba ilifungwa kwa sheria zilizopo, walifunga mikataba… bahati mmoja wao kazungumza hakamatiki.

“Rais alikaa na aliyemwita mwizi jana, mlango wa Ikulu jana ulifunguliwa ukawa wazi mwizi akaingia Ikulu,” alisema.

Kafulila, Zitto waombwe radhi

Akichangia mjadala huo wa bajeti, Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida (CUF) alisema wabunge warudi majimboni wakaombe radhi wananchi kwani wao ndiyo walipitisha sheria za madini.

“Tuliapa kwa kushika kurani na biblia, kurani na biblia ni vitabu vya Mwenyezi Mungu havitakiwi kudanganya, huwezi kuapa kisha ukazungumza uongo, unashika kurani ama biblia alafu ukaja kubadilisha ukazungumza mengine, kila siku tunasema tumerogwa na nani, tumerogwa na kurani na biblia.

“Mara nyingi ukiwa mkweli hukubaliki, kuna wakereketwa na wanaharakati walionesha hali ya madini ngumu, Dk. Hamisi  Kigwangala ubunge wake ulikuwa wataabu kwa sababu alisimamia na kupinga madini haya yasiibwe hayachakachuliwi, alipigwa mabomu, aombwe radhi.

“David Kafulila ambaye alikuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) akaitwa tumbili, Zitto Kabwe alikuja na hoja nzito mwisho wa siku hapana ikawa ndio”alisema mbunge huyo.

JISAJILI USHINDE GARI LA BUREEEEE KABISA

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote... Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...

CHAKUFANYA NI Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Bonyeza Hapa >>> SHINDA GARI YA BURE <<< Kujisajili ni Bure tu...

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Donald Trump Akiri Kwamba Anachunguzwa Marekani

$
0
0
Rais wa Marekani Trump amethibitisha kwamba anachunguzwa yeye binafsi kutokana na hatua yake ya kumfuta kazi mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la Marekani FBI James Comey.

Kupitia Twitter, Bw Trump amekariri kwamba uchunguzi unaoongozwa na mwendesha mashtaka maalum kuhusu tuhuma kwamba maafisa wa Urusi waliingilia uchaguzi wa mwaka 2016 ili kumfaa Trump hauna msingi.

Ni mara ya kwanza kwa Bw Trump kuzungumzia taarifa kwenye magazeti kwamba anachunguzwa kwa tuhuma za kuhujumu mifumo ya haki kwa kumfuta kazi Bw Comey.

Awali, taarifa kwenye vyombo vya habari Marekani vilikuwa vimeripoti kwamba wasaidizi wake pamoja na watu waliojitolea kusaidia katika kundi lake la mpito wameamrishwa kuhifadhi nyaraka zote kuhusiana na uchunguzi huo wa madai kuhusu Urusi.

Taarifa zinasema mawakili wa maafisa hao wa Trump wametakiwa kuhifadhi nyaraka zote zinazohusiana na Urusi, Ukraine na washauri wengine kadha wa kampeni.

Kuna makundi kadha yanayofanya uchunguzi, kundi moja likiongozwa na mkurugenzi wa zamani wa FBI Robert Mueller, ambayo yanachunguza iwapo maafisa wa Trump walishirikiana na maafisa wa Urusi wakati wa kampeni.

Sababu iliyomfanya Cristiano Ronaldo Atake Kuhama Real Madrid

$
0
0
Staa wa soka wa Kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo licha ya kutetewa na club yake ya Real Madrid kuhusiana na tuhuma za ukwepaji kodi zinazomkabili, ameripotiwa kufikiria kufanya maamuzi magumu.

Cristiano Ronaldo ambaye ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha Real Madrid anatuhumiwa kukwepa kodi nchini Hispania katika kipindi kati ya 2011 hadi 2014 kiasi kinachotajwa kufikia pound milioni 13 ambazo ni zaidi ya Bilioni 35 za kitanzania.

Mtandao wa Sky Sports umeripoti kuwa staa huyo aliyeisaidia Real Madrid kutwaa mataji matatu ya UEFA Champions League anataka kuondoka Hispania kutokana na tuhuma zinazoendelea ambazo anaamini hafanyiwi haki.

Kama kuna timu itakuwa inamuhitaji Cristiano Ronaldo kumtoa Hispania na kumsajili katika timu yao basi italazimika kuilipa Real Madrid euro bilioni 1 ambazo ni zaidi ya trilion 2.5 za kitanzania, hiyo ni kwa mujibu wa kipengele kilichopoa katika mkataba wake na Real Madrid.

Katibu Mkuu Yanga Aunguka Kuhusu Ibrahim Ajib na Niyonzima Kwa Mara ya Kwanza

$
0
0
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ambae amekubali kujibu maswali  kuhusiana na kinachoendelea katika soka la Bongo hususani club yake.

Kuna stori kuwa Yanga wamemsajili Ibrahim Ajib wa Simba kimya kimya kwa dau la Tsh Milioni 50 na wamempa na gari aina ya Brevis ukweli upo ukoje kuhusu Ajib na kuhusu stori za Simon Msuva kuwa amepata club nje ya nchi na Yanga wamegoma kumruhusu?

Na hizi stori tunazosikia kuwa wameshindwana na kiungo wao wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima ili aongeze mkataba ni kweli, yaani wameshindwa kumpa dau analolitaka na kuna habari kuwa kajiunga na Simba.

“Siwezi kusema lolote kuhusu Ibrahim Ajib na mimi nasikia kama unavyosikia wewe naona kwenye mitandao lakini niseme kuwa kuwa sina taarifa yoyote, kuhusu Msuva amepata timu Egypty na Morocco lakini hatuwezi kumruhusu aende hadi tupate mualiko rasmi” Mkwasa

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika

Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.
Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,

HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp: +255 674 835107
Calls: +255746757102

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images