Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

WATU 25 wamefariki katika ajali ya moto nchini Ureno

$
0
0

Maafisa nchini Ureno wamesema kuwa, moto mkubwa wa msituni katika maeneo ya katikati mwa nchi hiyo, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 25 na kuwajeruhi wengine 20, wakiwemo maafisa kadhaa wa zima moto.

Awali watu waliofariki walikuwa 19, lakini sasa idadi hiyo imepanda na kufikia 25. Wengi wao walifariki pale walipokuwa wakiukimbia mji wa Pedrogao Grande, kilomita 50 kama (Maili 30) Kusini mashariki mwa Coimbra, kwa kutumia magari yao. Hayo ni kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.

Watatu kati yao walifariki baada ya kuvuta hewa yenye moshi mkali.

"Kwa bahati mbaya, hii inaonekana janga baya zaidi ambayo tumewahi kushuhudia katika miaka ya hivi karibuni, katika moto wa nyika," amesema Waziri mkuu Antonio Costa.

Waziri wa maswala ya ndani wa nchi hiyo João Gomes, amewaambia waandishi habari kuwa, waathiriwa 16 wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, pale walipokabiliwa na moto huo mkubwa katika Wilaya ya Pedrógão Grande barabara inayounganisha miji ya Figueiro dos Vinhos na Castanheira de Pera.

Moto "ulienea kwa kasi mno" katika maeneo manne, amesema Bw. Gomes.

Uhispania imetuma ndege mbili ya kuzima moto, ili kuweza kukabiliana na janga hilo.

Haijabainika kilichosababisha moto huo wa msituni, ambao umeteketeza nyumba nyingi katika maeneo hayo.

Awali, meya wa eneo hilo Valdemar Alves, aliwaambia wanahabari kuwa, kuna idadi ndogo ya wazima moto, kukabiliana na janga hilo la moto katika vijiji kadhaa ambavyo vinaungua kwa sasa.na na janga hilo la moto katika vijiji kadhaa ambavyo vinaungua kwa sasa.

VIDEO:Tazama Joti Akipata Shida Kuliingiza ZIGO Lake Geto

$
0
0
Hatimaye Babu Joti kapata zigo na kulipeleka nyumbani , kimbembe kinakuja kwenye kulipitisha maana mapo kwake ndo maskani ya vijana wake wa kitaa.

Mfanye Mpenzi Wako Unayempenda Achanganyikiwe Juu Yako Na Kukupenda Zaidi.

$
0
0

Kwenye mahusiano ya kimapenzi ni vizuri uzito wa mahusiano uwe pande zote mbili, mapenzi huwa matamu zaidi iwapo umpendae naye anakupenda kwa kiwango umpendacho wewe, na si vinginevyo maana tofauti na hapo mapenzi huwa kama kero au mzigo na hisia hukupelekea kujiumiza moyo na kujiharibu kisaikolojia".


Wewe ni mtu mzuri na unampenda sana msichana wako, kiasi kwamba unamkubali sana mpaka unampa dunia yako kumuonyesha unavyomjari, ndani ya muda mrefu mliopo kwenye uhusiano umeshajitoa kwa mengi, kimuda na hata kifedha, unamchukua kutoka kazini kila siku ndani ya juma ili tu asije kuchosha miguu yake mizuri na laini.

Unamsaidia kwa kila jambo analohitaji na umeacha kutumia muda wako na marafiki zako ili kusudi uwe na muda mwingi zaidi wa kutumia naye, umemnunulia gauni la gharama na vingine vingi ili apendeze bila kuchoka huwa unabadilisha ratiba zako ili ziweze kuendana na za kwake ili muwe pamoja na kumuonyesha jinsi gani alivyo na nafasi kubwa ndani ya moyo wako, na unafanya yote haya bila ya kumtaka kitu chochote kutoka kwake.

Na hata hivyo ni mara moja tu siku ule ulipokua unaumwa ambapo ulimuomba akupikie ugali na akakuchukulie mishikaki unayoipenda pale uswazi teki awei, ambapo alikataa kwa upole na kukwambia hajui kupika vizuri ugari na wewe ulikubali kwa roho safi maana hupendi kuwa kero kwake.

Sasa turudi kwenye uhalisia.

Rafiki sijui nikuambieje ili unielewe, kaka hapa unatiketi moja tu inayokwenda bila kurudi ambayo kupeleka kwenye nchi ya mvunjiko wa moyo ambapo wapo wapenzi wake wa zamani aliowaacha.
Ni muda wa kumuuliza, "Hivi ni kipi umenifanyia mimi hivi karibuni?".

Kila ukiwa unamfanyia kitu kizuri nahisi labda unaona kama unajiongezea pointi nyingine za ziada, lakini kiukweli ni kwamba kama yeye hatojihusisha na kuchangia kwa kukufanyia wewe hayo mambo mazuri unayomfanyia yeye kwenye uhusiano wenu, jua kabisa nguvu zako zitakua hazina faida yeyote ile, ni kama maji mtaroni yanayopita tu, na hapa ndipo kiumeni.com tunapokwambia kwanini!.

Kikawaida tunaweza kuwapa ushauri wanaume wengi wanaokutana na haya wavunje uhusiano tu pale mwanamke anapomtumia mwanaume bila kurudisha upendo wowote ule anaofanyiwa, hapa simaanishi yale mambo yetu mengine ya kitandani.

Lakini kama kweli umejiweka kwenye huu uhusiano kwa roho yote na unataka uhusiano uendelee kuwa wa muda mrefu lazima ufanye na yeye awekeze hisia zake na hata pesa zake kwenye huu uhusiano hata kama ni asilimia 50%.

Hapa haijarishi wewe ni tajiri kiasi gani, ni mzuri kiasi gani au ni mwanaume mwenye mahaba yote duniani kiasi gani, kama mwanamke hana kitu chochote alichowekeza kihisia, iwe ki muda au ki fedha lazima atakuacha iwapo mtu mwingine ambaye yuko zaidi ya wewe akitokea. Kama sheria za kiumeni.com zinavyosema(kama msomaji utakua unazijua), "Mtu mpya na ambaye ni zaidi yako huwa yuko nyuma anakuja, anasubiri ukosee kidogo tu", na kama hata jiwekeza kwako likija dili ambalo ni zaidi ya wewe unalompa lazima ataondoshwa tu

Bado hujaniamini tu?

Kama ukiwekeza kiasi fulani cha muda na fedha kwenye mpango flani, iwe kununua nyumba au kuanzisha biashara, utakua unajua uchungu na uzito wa kitega uchumi chako tofauti na ukiwa umepewa bure.

Sheria hizi hizi ndizo zinazofanya kazi kwenye mapenzi, ni ubinadamu kuona uzito na uchungu kwenye kitu ambacho umekiwekeza, sasa nini swali kwako, "Ni nani anayechangia sa kwenye uhusiano wenu?, ni wewe au ni malaika wako mrembo?
Fikiria kwa umakini maana uhalisia wa jibu lako tayari limeshafanya kazi kubwa kuutengeneza uhusiano wako jinsi ulivyo sasa.

Mwachie baadhi ya malipo afanye yeye...

Inabidi uwe kama vocha isiyorudishwa, fikiria kila saa msichana wako akienda kununua mahitaji yake, analipia kwa vocha na anapata muda wa maongezi, atafanya hivi kwa kipindi kirefu mpaka ndani ya muda atakuwa na muda wa maongezi ambao anaweza kuutumia kuongea kwa miaka mingi, sasa vipi kampuni nyingine ya vocha ikiingia na kumpa ofa nzuri zaidi?, kwa unavyofikiria anaweza kubadilisha kampuni?
Kama hata kuwa na muda wa maongezi mwingi na wewe, basi kuna nafasi kubwa atabadilisha kampuni bila kujiuliza na kwa upande mwingine kama atakua na muda wa maongezi mwingi wa miaka kumtosheleza maongezi yake kutokana na jinsi alivyowekeza, hawezi kubadilisha kampuni. Umeipata pointi yamgu, Rafiki?

Kazi yako...

Ni kazi yako kumfanya msichana wako awekeze muda na hela kwenye kampuni yako ya vocha ili ikija kampuni nyingine isiweze kumchukua akili kwa ofa nzuri itakazokuja nazo.
Kwa kuwa sasa hivi nimeshakuelewesha umuhimu wa kumfanya msichana wako awekeze kwenye uhusiano, sasa utafanyaje ili aanze kuwekeza?

Omba misaada: Kitu muhimu cha kuangalia sasa hivi ni misaada, kama akikupa msaada atajishauli amefanya hivyo kwa sababu unamvuto kwake na unastahili kufanyiwa hicho alichokifanya, acha sasa hivi akuhudumie vizuri, mwache sasa hivi akupikie, saa zingine mwombe aje akupitie kazini na mwache alipie baadhi ya vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wake.
Ukiishiwa vocha usione aibu kumtumia tafadhari niongezee salio mara moja moja.
Hii ni moja ya sababu hutakiwi kuweka mayai yote kwemye kapu moja, na ndio maana huwezi kumwacha mwanamke ambaye hakujali kwa sababu wanaume wengi wanakuwa wamewekeza muda mwingi na fedha kwa huyo mwanamke.

Muda ni pesa: unaweza kumwongezea hamasa zake kwako kwa kumfanya atumie muda mwingi na wewe kwa kufanya vitu unavyovipenda na sio anavyovipenda, hii itamuonyesha uzito wako kwake.
Sio mbaya kumbeba mwanamke kama dhahabu, ila hakikisha ndani ya uhusiano kila mmoja anawekeza na sio uhusiano uwe unaegemea upande mmoja tu, kama kweli anahisia na wewe basi hisia zakezitamwendesha na yeye akujali wewe kama ambavyo zinakuendesha wewe.

Ubalozi wa Tanzania Uingereza Wakana Kuwa na Taarifa za Mtanzania Aliyekamatwa Kwa Kuweka Picha za Marehemu Mtandaoni

$
0
0

Ubalozi wa Tanzania Uingereza umesema hauna taarifa za anayedaiwa ni Mtanzania, Omega Mwaikambo aliyefungwa kwa kuchapisha picha ya maiti.

CHADEMA wadai katiba mpya

$
0
0
Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa,  Dkt. Vicent  Mashinji amewataka wananchi kumuomba Rais Joseph Magufuli  kuitoa katiba iliyopatikana kupitia Jaji Joseph  Warioba ili kupunguza ushabiki wa kisiasa wa Wabunge, kufikia kupitisha mikataba mibovu bungeni.


Leo akizungumza na wanahabari, Dkt. Mashinji amesema kwamba kuna umuhimu mkubwa wa katiba ya Jaji Warioba kuanza kudaiwa maana itakuwa suluhisho la kudumu kuepusha matokeo ya wizi wa rasilimali serikalini kutokana na mapendekezo ya wananchi yaliyowekwa.
Dkt Mashinji amesema kuwa mikataba mibovu  inayopitishwa na wabunge haitokuwepo tena bungeni kwa kuwa katiba itakuwa inawabana kuwajibika kwa ufasaha la sivyo watawajibishwa na wananchi waliowapa dhamana ya uwakilishi.

"Ile Katiba ya Jaji Warioba ndiyo inatakiwa sasa hivi wananchi tuanze kumuomba Mh. Rais atupatie kwa sababu hata hii mikataba mibovu inayopitishwa ni kwa sababu wabunge wanafanya kazi kwa ushabiki. Ila kwa katiba ya Warioba watu watawajibika maana watajua wakiharibu wananchi watawawajibisha hata yale makofi yatapungua, na wabumge wataongeza ufanisi na  uwajibikaji" alisema Dkt Mashinji.

NIKKI Mbishi Amzodoa Godzillah Adai Ana Stress

$
0
0
Rapa Nikki Mbishi amedai Godzillah anaumizwa na 'stress' za kuporomoka kimuziki kitu ambacho hakukitarajia kutokea mapema kwenye maisha yake ndio maana amekuwa akitapa tapa kwa kumtolea maneno ya kashfa kwenye kila mahojiano anayofanya.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet bongo, Nikki amefunguka na kusema kwamba Mfalme huyo wa Salasala alibebwa na watu kwenye muziki na ndiyo waliomtupa na sehemu ambayo imemfanya ashindwe kuamka sababu inayomfanya hata kufikia kumtaja kwenye mahojiano mara kwa mara ili azidi kusikika.

"Zizi ameshushwa na waliompandisha bila yeye kutarajia hilo. Ametupwa halafu ameenda kuporomokea sehemu ambayo hata hajui atanyanyukaje, halafu ana watu wake anahitaji kuwasema ila anaona Nikki mwanangu nikiongea nitammudu fresh, kwanini awe muoga mbona mimi nawaambiaga,” Nikki alifunguka.

Aidha Nikki amejibu kauli ya Zillah kumuita 'Wack' na kusema kuwa haelewi ni sababu gani zimemfanya msanii huyo kutumia kauli hiyo huku akihoji labda kama anaishi maisha ya kuigiza kama msanii huyo ingekuwa sawa..

'Ukiniita mimi 'wack' kwa maana ipi, labda sijui kuandika, au 'wack' kama yeye hajui anachokifanya? anaishi maisha ya kuigiza, kujifanya wewe unaisha maisha ya Ulaya wakati upo Salasala unadanganya watu kuna all stars zimeninginizwa kwenye nyaya za umeme whichi is not true. Ana stress zake kaenda kwenye ufalme ambao sio wake sasa karudi huku ambako pengine alitakiwa awepo amekuta wafalme ni wengine na sio yeye tena,” Nikki aliongeza.

BARACK The Prince Afunguka Bifu Lake na Ali Kiba....

$
0
0

Msanii Baraka The Prince amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hana tofauti yoyote na Alikiba na kudai kuwa watu wa mitandaoni ndiyo wamekuwa chanzo cha kusambaza maneno hayo kuonyesha yeye ana tofauti na Alikiba.
Baraka The Prince amedai kuwa yeye hawezi kugombana na Alikiba na wala hategemei kuja kumkosea kwa kuwa ni moja kati ya watu ambao wanampenda sana yeye pamoja na sanaa yake. "Unajua ukidili wa watu wa Instgram wanaumiza sana kichwa kwa sababu mimi nipo kwenye label moja na Alikiba, hivyo Alikiba ni brother wangu na naishi naye kama kaka yangu kabisa, pia ni miongoni mwa watu ambao wananipenda sana, hivyo sitegemi kuja kumkosea au hata kugombana naye sitegemi kitu kama hicho, sema watu walianza kuongea hivyo baada ya kuona siongozinaye kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, watu wamezoea kuniona kila anapokwenda Alikiba niko naye kwa hiyo kuna sehemu zingine mimi sipo sababu sina sababu ya kuwepo, Alikiba amekuwa ni mtu ambaye hapa nchini hakai sana kwa kipindi hichi ndiyo maana wanakuwa hawaoni tupo pamoja" alisema Baraka The Prince
Mbali na hilo Baraka The Prince amesema kuwa mkali huyo wa Aje hivi sasa yupo kwenye maandalizi ya kuachia kazi yake mpya baada ya Aje kusumbua zaidi ya mwaka mzima.
Alikiba na Baraka The Prince licha ya kuwa chini la label moja ya  RockStar4000 wasanii hao pia waliachia kazi ya pamoja ambayo inafahamika kama 'Nisamehe'.

EBITOKE na Ben Pol Wameanza kuchati

$
0
0

Msanii Mchekeshaji Ebitoke baada ya kutamka mtandaoni kuitaka ndoa na msanii Ben Po lakini kubwa zaidi aliomba nafasi ya kukutana naye ili aweze kumueleza Ana kwa ana, Ben Pol alikubali la ombi hill la kukutana nacye.

Muungwna Blog na Tv imepiga stori na Ebitoke kutaka kujua kama tayari ameshaonana na Ben Pol? Amejibu kuwa Mpaka sasa hawajaonana Ila Wanachati sana na kupigiana simu!

MBWANA Samatta Asaini Dili Maalumu Kwaajili ya Watanzania

$
0
0

Nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubeligiji, Mbwana Samatta ameingia mkataba maalumu na Benki ya DTB na pia ataendesha kliniki ya soka kwa mamia ya vijana zoezi lililofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu Dar es Salaam.


Akizungumzia mkataba huo, Samatta alisema una lenga kuhamasisha vijana ili kuendeleza soka la Tanzania.


"Nitakuwa balozi wa DTB (Diamond Trust Bank), nikifanya kazi mbalimbali za kijamii na masuala ya kimichezo," alisema Samatta muda mfupi baada ya kumaliza kutoa mafunzo ya soka jana.

MABAHARIA 7 Wapatikana Wamefariki Katika Ajali ya Meli ya Jeshi la Marekani

$
0
0

Mabaharia saba wamepatikana wakiwa wamefariki dunia baada ya meli ya jeshi la Marekani ilipogongana na meli ya mizigo ambayo ilikuwa na bendera ya Ufilipino katika maeneo ya bahari ya Japan.

Maiti hizo zilipatikana ndani ya meli katika chumba cha kulala ambacho kiliharibika na kujaa maji.

Meli ya mizigo ilikuwa ni aina ya ACX Crystal iliyokuwa na urefu wa mita 222 na meli ya kijeshi ya Marekani ina urefu wa mita 154 ambayo pia huwa inatumika katika kuharibu makombora.

Mmoja kati ya makamanda wa jeshi la Marekani alijeruhiwa katika ajali hiyo na alikimbizwa haraka hospitalini usafiri wa helikopta.

CHRISTIANORonaldo huenda akajiunga na timu hizi

$
0
0

Baada ya kuipa mafanikio makubwa klabu yake ya Real Madrid ya Spain, Cristiano Ronaldo ameutaarifu uongozi wa klabu hiyo kuwa anataka kuondoka.


Gazeti la A Bola la Ureno limeripoti na kuzihusisha klabu za PSG na Manchester United kuwa ni timu ambazo huenda akajiunga nazo.


Hatua hii ya Ronaldo ambaye pia ni mshindi mara nne wa tuzo ya 'Ballon d'or' inakuja baada ya kupata kesi ya ukwepaji kodi.


Katika hatua nyingine gazeti la Marca limeripoti tetesi kuwa Real Madrid imeiambia Man United iandae Pauni 160 milioni, kama inamtaka mkali huyo. 

JE Unajua Athari za Kuitana Sweet, Dear na Baby Kwa Watu Ambao Sio Wachumba ama Mke na Mume?

$
0
0
BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby!

Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine).

Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji.

HUTUMIKA WAPI HASA?
“Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.”

Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha penzi la dhati lililopo moyoni mwa mhusika kwenda kwa mpenzi wake.
Husisimua na kuongeza ladha ya mapenzi ya kweli. Kumuita mpenzi wako kwa majina ya kimapenzi 

huongeza zaidi upendo na msisimko wa moyo. Mwenzi hujiona wa kipekee na mapenzi huzidi kukua.
Kwa maana hiyo basi, ni sahihi zaidi kwa wapenzi kuitana majina niliyotaja hapo juu na mengine yanayofanana na hayo kwa lugha yoyote ile, ila iwe inatambulika vizuri na anayetamkiwa.

ATHARI SASA!

Kwa upande mwingine kuna athari za kutumia maneno hayo. Zama hizi, maneno hayo yanaonekana ya kawaida tu. Mtu yeyote anaweza kumuita yeyote mpenzi, honey, baby n.k. Hapo ndipo kwenye tatizo lenyewe.

Kwa ujumla wanawake ndiyo wanaongoza zaidi kuitana majina hayo. Wakati mwingine huenda mbali zaidi na kuwaita hata wanaume majina hayo ya kimapenzi. Si rahisi kuona athari zake kwa haraka na moja kwa moja, lakini zipo na wengi zimewasababishia matatizo. Ngoja tuone..

HUPUNGUZA THAMANI

Kama nilivyotangulia kusema awali, maneno 
niliyotaja hapo juu husisimua na kuongeza mapenzi. Kwa kuyatumia vinginevyo, basi kwa kiasi kikubwa huanza kukuathiri na kupunguza thamani ya neno lenyewe.

Kama unaweza kumwita mfanyakazi mwenzako dear, mtu wa jinsi sawa na wewe sweet ni wazi hata utakapomuita mpenzi wako au wewe kuitwa na yeye, halitakuwa na nguvu sana ya mapenzi kwa sababu ni neno ulilolizoea kila wakati.

HUKARIBISHA USALITI
Wakati mwingine unaweza kujikuta umeingia kwenye usaliti bila kutarajia. Veronica, mfanyakazi wa saluni moja ya kiume iliyopo Sinza, Dar alitoa ushuhuda ufuatao:
“Mimi naishi na mchumba wangu, tuna mtoto mmoja mwenye miaka mitatu. Nafanya kazi saluni. 

Tangu nimeanza hii kazi, nimejifunza kutumia maneno matamu ya kumfurahisha mteja na wakati mwingine kumfanya akupe tipu baada ya kumaliza kazi.

“Kuna kaka mmoja nilizoeana naye sana. Kama kawaida, huwa namkaribisha kwa kumuita dear au sweet. Wakati nikiendelea kumfanyia scrub, mazungumzo yetu hutawaliwa na dear, sweet, nikajikuta nimezidi kumzoea.

“Kwa sababu tulibadilishana namba, mara akaanza kuwa na mazoea ya kunitumia meseji, akija ananipa pesa, anaondoka. Mazoea yakazidi. Nikajikuta nimemzoea na kuna siku ambayo siwezi kuisahau kabisa.

“Ni siku niliyomsaliti mchumba wangu...mbaya zaidi na huyo jamaa naye ana mke wake. Niliumia sana, lakini naamini kama nisingekuwa na mazoea ya kumuita majina ya kimapenzi nadhani nisingeingia mtegoni. Moyo wangu unauma sana, najuta kumsaliti mpenzi wangu.”

Unaweza usione athari hii moja kwa moja, lakini ndugu zangu chukua jambo hili leo; wanaume wengi wakiitwa kwa majina ya kimapenzi husisimka sana – hujiona wenye bahati na mara hushawishika kuingia mapenzi.

Kama mwanamke hatakuwa makini atajikuta ametumbukia. Ya nini yote hayo, wakati unaweza kubadilisha mazoea hayo? 

ANGALIA TOFAUTI
Rafiki zangu, kati ya maneno niliyoyataja, kuna ambayo yanakubalika kutumiwa na wasio na uhusiano lakini wawe na undugu wa damu. Mathalani baba, mama, kaka, dada, shangazi nk.

Hakuna tatizo kumuita mtu mpendwa, lakini siyo baby, sweet, mpenzi na mengine yenye maana ya moja kwa moja ya kimapenzi. Umenipata? Akili za kuambiwa, changanya na zako kisha unazifanyia kazi! Chukua kinachokufaa!
Hadi wiki ijayo kwa mada nyingine. Wewe ni muhimu sana kwangu

Kama Una Moyo Mwepesi Usisome Stori Hii, Wengi Wamelia Sana

$
0
0

Kama nilivyoanza mwanzo....usisome kama una machozi ya karibu...

“Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa.

Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi.

Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Mary.

Kwa kweli nilimdharau mke wangu!
Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu.

Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.
Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu kisawasawa.

Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.

Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Mary
Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika.

Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana.

Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu.

Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.

Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Mary tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya.

Nilimuweka chini nje ya nyumba.
Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.

Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.

Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.

Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Mary alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Mary, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’
Ikawa kama Mary alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenga
nisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.

Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.
Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema.
Mungu nisaidie Nisifike huku mimi.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika

Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote
..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.
Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,

HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp: +255 674 835107
Calls: +255746757102

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote..

Tambua Vitu Mwanaume Anavyokupima ili Akujue Unafaa Kuolewa Au Ni Hit And Run !

$
0
0

1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.

2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu".

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.

9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo.

Nchi Nyingine Ilivyojadili Upya na Barick Gold Mkataba wa Makinikia

$
0
0

SERIKALI ya Jamhuri  ya Dominica na kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick Gold ya Canada nao walifanya mazungumzo kumaliza mgogoro kuhusu mkataba wa makinikia kama Tanzania.


Habari kutoka Santo Domingo zinasema Rais wa Dominica, Danilo Medina, mwaka 2013 alisema kwamba  mkataba huo una hasara kwa nchi hiyo iliyoko eneo la Carribean na kwamba ujumbe wa kampuni ya Barrick umewasili nchini humo ili kufanya majadiliano mapya ya pamoja.


Serikali ilisema kwamba inataka mkataba huo ujadiliwe upya kwa faida ya pande zote mbili.


Mamlaka za ushuru nchini humo zilishikilia  kilo 1,264 za makinikia ambazo zilikuwa zisafirishwe kwenda nje na kampuni Barrick.  Makinikia hayo yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. Billioni 49 (Dola Millioni 22 za Marekani) yalikamatwa kwenye uwanja wa ndege kimataifa wa Las Americas, mashariki mwa jiji la Santo Domingo.


Dominica imekuwa ikiishutumu Barrick kwa kufanya udanganyifu wakati wa kujaza fomu za usafirishaji wa vitu mbalimbali nje ya nchi.


Kwa upande wake, kampuni hiyo ya Canada imesema imekuwa ikiendesha shughuli zake nchini Dominica kwa kufuata taratibu zote ambazo bidhaa zote zimekuwa zikikaguliwa na kupitishwa na mamlaka husika za ushuru.


Kampuni hiyo inaendesha shughuli zake katika mgodi wa dhahabu wa Pueblo Viejo katika mji wa Cotui, moja ya migodi mikubwa zaidi duniani ya dhahabu.  Kampuni hiyo inamiliki asilimia 60 ya mradi huo na ndiyo inaendesha shughuli zote katika mgodi huo ambapo uzalishaji wa kibiashara ulianza Januari 2013.  Kampuni la Goldcorp la Canada linamiliki asilimia 40 ya hisa zilizobaki.


Mnamo Machi mwaka huu, mamlaka za ushuru zilisimamisha usafirishaji wa makinikia  wa Barrick kwenda nchi za nje kutokana na madai ya kuvunja taratibu za ushuru.  Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Medina kudai hadharani  kwamba kampuni hiyo lazima ifanye majadiliano mapya kuhusu mgodi wa Pueblo Viejo ambao ulikuwa hauendani na maslahi ya nchi hiyo.

Kaburi la Baba mzazi wa Spika wa bunge Job Ndugai Lafukuliwa

$
0
0

Ikiwa ni miaka 25 tangu Yustine Ndugai ambaye ni baba mzazi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai azikwe katika Kitongoji cha Katente mkoani Geita, kaburi lake limefukuliwa na mabaki yake kuchukuliwa na ndugu zake ili kwenda kuzikwa upya katika Kijiji cha Ibagwe, wilayani Kongo mkoani Dodoma.


Mabaki ya mzee huyo aliyefariki dunia Mei 22, 1992 yalichukuliwa na wanaukoo juzi wakiongozwa na Spika Ndugai.

Mwenyekiti wa umoja wa wazee kitongoji cha Katente Namba Moja, Joseph Kitafuma alisema walimpokea mzee huyo kijijini hapo kama mchimbaji mdogo wa dhahabu mwaka 1986. Kitafuma alimuomba Spika Ndugai kuwajengea zahanati kwani aliyotibiwa baba yake wakati anaugua imechakaa sana na kusema zahanati hiyo itapewa jina la Ndugai, ombi ambalo kiongozi huyo wa bunge alilikubali.

Mbunge wa Bukombe, Dotto Biteko aliwataka wananchi kuona umuhimu wa kuwatunza wazazi na kuhamisha makaburi yao kwa kufuata mila na desturi za eneo husika. Alisema kuwa, kitendo kilichofanywa na spika ni cha kuigwa kwani kinaonyesha anatambua umuhimu wa wazazi si tu wakiwa hai lakini pia baada ya kufariki dunia.

“Sitasahau wema na utu walioonyesha wananchi wa Bukombe kutunza kaburi la baba yangu kwa miaka 25,” alisema Spika Ndugai huku akimtaka Mkuu wa Wilaya, Mbunge na Mkurugenzi wa Halmashauri kusimamia ujenzi wa zahanati kama walivyooomba wazee wa kijiji hicho.

Ufukuaji wa mabaki hayo ulifanyika baada ya kupata idhini ya mahakama.

Chanzo: Mwananchi

Fahamu : Madhara ya kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu

$
0
0

April mwaka jana, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TDFA) ilikamata makopo 1,526 ya vinywaji vya kuongeza nguvu katika soko la Tanzania ambavyo vilikuwa havikidhi viwango vya ubora na usalama kwa matumizi ya binadamu.


Vinywaji vya kuongeza nguvu, visivyo na kilevi, kisayansi vinaelezwa vina kiasi kikubwa cha kafeini, vitamini pamoja na kemikali za taurine, glucuronolactone.Wakati mwingine pia huongezewa dawa aina ya guarana pamoja na mitishamba aina ya ginseng kwa lengo la kusisimua akili na kuongeza nguvu za mwili.


Mtafiti wa madhara ya dawa za kulevya wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Stephen Nsimba anasema kwamba vinywaji hivi vina kiasi kikubwa cha kafeini ambayo ni dawa inayosisimua ubongo na kwa kuvichanganya na pombe athari zake kwenye mfumo wa fahamu za mwili huongezeka.

“Baada ya kuchanganya vinywaji hivi, kafeini katika vinywaji vya kuongeza nguvu, hupunguza athari za kilevi na kumfanya mtumiaji asibaini haraka kuwa amekunywa kiasi kikubwa cha kilevi. Hili ni jambo la hatari” ameonya Dk Nsimba.



Matokeo ya utafiti mmoja yaliyowasilishwa katika mkutano wa mwaka 2013 wa Chama cha Afya ya Moyo cha Marekani (American Heart Association) uliofanyika katika mji wa New Orleans, ilibainika kuwa kunywa kopo moja hadi matatu ya vinywaji vya kuongeza nguvu, kunaweza kusababisha maoigo ya moyo kudunde bila mpangilio na kuongeza shinikizo la damu, na kusababisha kifo cha ghafla.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa T. Van Batenburg-Eddes na wenzake uliochapishwa katika jarida la Front Psychology toleo la 5, mwaka 2014.

WAZIRI Mwigulu Nchemba Ashindwa Kuvumilia..Amvaa Tundu Lissu Sakata la Madini...Magazeti ya Leo Jumatatu June 19

KIMENUKA...Wananchi 400 Wavamia Mgodi wa North Mara...Nimekuwekea Video Hapa

$
0
0

Kundi la wananchi zaidi ya 400 kutoka baadhi ya kata zinazopakana na mgodi wa dhahabu wa North Mara wilayani Tarime wanaotakiwa kuhama kupisha shughuli za uchimbaji, wamevamia mgodi huo  leo (Jumapili) wakidai malipo ya fidia.

Wananchi hao ambao maeneo yao yalifanyiwa tathmini tangu mwaka 2014 bila kulipwa hadi sasa, wanadaiwa kuchukizwa na kitendo cha majina yao kukosekana kwenye orodha iliyotoka hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Andrew Sata amethibitisha kutokea kwa jaribio la kuvamia mgodi uliodhibitiwa na polisi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Hakuna aliyejeruhiwa wala kushikiliwa kwa tukio hilo. Habari kwa kina fuatilia mitandao ya MCL na magazeti yetu kesho.

Tazama Video:


Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images