Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

DAKTARI Feki Akamatwa Hospitali ya Muhimbili

$
0
0

#HABARI Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Abdallah Juma anayedhaniwa kuwa daktari feki amekamatwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

BREAKING: Wananchi Wavamia Tena leo Mgodi wa Acacia

$
0
0

Kundi kubwa la wananchi kutoka vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa Acacia North Mara wamevamia mgodi huo.


Taarifa kutoka eneo la tukio hivi sasa zinaeleza kuwa wananchi hao wanaendelea kukusanyika katika lango kuu la mgodi huo maarufu Boom Gate huku jeshi la polisi likijaribu kuwatawanya.


Hilo ni jaribio la pili kwa wananchi hao kutaka kuingia mgodini humo baada ya lile ya jana ambapo polisi walifanikiwa kulizima.


Taarifa zaidi kukujia.

BREAKING: TAKUKURU inawashikilia Waliotajwa kashifa ya Escrow

$
0
0

TAKUKURU inawashikilia Singh Sethi na Rugemalila(Waliotajwa kashifa ya Escrow ) kwa tuhuma za uhujumu uchumi

- Kupelekwa Mahakamani

TAKUKURU imesema inawafikisha mahakamani watuhumiwa, James Rugemarila na Harbinder Sethi kwa makosa ya uhujumu uchumi

Umoja Wa Vilabu Vya Waandishi Wa Habari Tanzania ( MCT, UTPC na THRDC) Walaani Vikali Serikali Kulifungia Gazeti La Mawio

$
0
0

TAMKO LA PAMOJA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MAWIO NA HALI YA UHURU WA HABARI NCHINI


UTANGULIZI
Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Umoja wa Vilabu vya Habari Tanzania (UTPC) kwa pamoja tunalaani vikali kufungiwa kwa Gazeti la Mawio na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe Juni 15,  2017. Gazeti limepigwa marufuku kuchapishwa na kuwekwa katika mzunguko kwa miaka miwili.

MAKOSA WANAYOTUHUMIWA KUFANYA
Gazeti la Mawio limefungiwa siku ya tarehe 15 Juni 2017, baada ya kutoa toleo lake lenye namba 196 la tarehe 15-21Juni, 2017.Waziri ametumia sheria mpya ya Huduma ya Vyombo vya Habari, 2016 kulifungia gazeti la Mawio kwa madai ya kukiukwa vifungu vya sheria hiyo na “Agizo la Mhe Rais” kuhusu kutowahusisha Marais wastaafu na sakata la uporaji wa rasilimali madini nchini. Gazeti hili limeshutumiwa kutenda makosa mawili; kosa la kwanza chini ya kifungu cha 50 na 59  cha Sheria ya Huduma za Habari Namba 2 ya 2016 na kosa la pili kukiuka  “ Agizo la Rais laTarehe 14/6/2017.. “ kama ifuatavyo;

(ii) Kuchapisha Picha za Marais Wastaafu
Waziri alidai kuwa, gazeti hilo limechapisha picha na majina ya marais waliopita kwa kuwahusisha na kashfa ya rushwa katika mikataba ya madini kati ya Serikali na wawekezaji.
Waziri anasema kuwa hawakufurahishwa na picha za marais wastaafu ambazo ziliwekwa kwenye ukurasa wa mbele.
(i) Kuchapisha Makala Kuhusu Uporaji wa Madini kinyume na Agizo la Rais
Kosa la pili ni kuchapisha makala ambayo ilichapishwa katika ukurasa wa 12 wa gazeti hilo kinyume na “Agizo la Rais la tarehe 14/6/2017.  Linalowataka watanzania kuacha kuwataja au kuwahusisha marais wastaafu na sakata la upoteaji wa rasilimali madini”.

Makala hiyo ni andiko lililosheheni historia ya jinsi viongozi mbalimbali walivyoshiriki katika usimamizi wa uwekezaji katika sekta ya raslimali madini.

UCHAMBUZI KUHUSU TUHUMA HIZI NA HATUA YA KULIFUNGIA GAZETI
Itambulike kuwa hii si mara ya kwanza kwa magazeti na vyombo vya habari kufungiwa na Waziri  katika nchi yetu kwa kutumia  sheria mbalimbali kandamizi hasa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 iliyofutwa mwaka 2016 na kuridhiwa na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya 2016. Magazeti kadhaa yalifungiwa katika siku za nyuma ikiwemo Mwananchi, Mawio, Mwanahalisi na Mtanzania.
Kwa upande wa Gazeti la Mawio hii ni mara ya pili kusimamishwa. Januari 15, 2016 gazeti hili lilipigwa marufuku kabisa kupitia Tangazo la Serikali (GN) Namba 55 la 2016. Hata hivyo gazeti hilo liliishtaki Serikali kwa mafanikio katika kesi namba. 15 ya 2016 na hatimaye likaweza kuendelea na machapisho yake.

 Itambulike  kuwa kwa muda mrefu tumekuwa tukipinga utaratibu wa kisheria wa kumpa Waziri mamlaka makubwa katika sekta ya habari.

Sheria iliyopita na ya sasa havina tofauti yoyote hasa katika mamlaka ya Waziri kulifungia gazeti pekee na kwa makosa atakayoyaona yeye ni kinyume na maslahi ya umma.  Sheria hii mpya imeendelea kumfanya Waziri awe Mhariri Mkuu, Mlalamikaji, Mpelelezi, Mwendesha Mashtaka na Hakimu kwa wakati mmoja.

Kifungu cha 59 cha sheria ya huduma za habari imetumika kulifungia Mawio kwa madai kuwa kuchapisha picha za viongozi wastaafu ni kinyume na maslahi ya umma.

 Kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania Watanzania wana uhuru wa kutoa maoni na kupashana habari kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusu maisha yao.

Kitendo cha kuzuia watanzania au vyombo vya habari visichapishe picha za viongozi wastaafu hasa katika mijadala ya kitaifa ambayo inahusu mambo yaliyotekea wakiwa madarakani ni kuwaziba watanzania midomo katika sakata la vita dhidi ya wizi wa madini Tanzania.

Katika kosa la pili gazeti hilo lilitumia makala ya Mbunge mmoja na mtaalamu wa sheria za madini nchini yenye maelezo juu ya mambo muhimu katika kumsaidia Mhe. Rais katika vita ya uporaji wa rasilimali madini.

 Vyombo vya habari kama watu wengine wana haki ya kutoa habari kama wanadhani ina maslahi kwa umma ilimradi hazikiuki sheria.  Tumeshangazwa kuona Waziri kitaaluma ni Mwanasheria ametumia Agizo la Rais Kama sheria kitendo ambacho ni hatari kwa mustakabali wa Taifa kama kila kitakachoagizwa na kiongozi mkuu kitachukuliwa kama ni sheria.

Hata hivyo kwa mujibu wa Mawio, Agizo la Rais kuhusu kuzuia marais wastaafu wasitajwe au kujadiliwa kwenye sakala la madini lilitoka wakati tayari gazeti hilo toleo la tarehe 15/6/2017 lilishakuwa limeshachapishwa na kusambazwa kwa mawakala nchi nzima tarehe 14/6/2017 wakati ambapo ndipo Agizo la Rais lilitoka tarehe hiyo hiyo 14.

Taarifa rasmi ya Mkurugenzi wa Idara ya habari-MAELEZO na msemaji mkuu wa Serikali ilinukuu Kifungu cha sheria cha 50 (a) (b) (c) (d) na (e) kuwa ndicho kifungu kilichokiukwa na gazeti la Mawio kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Dr. Harrison Mwakyembe. Aidha, kifungu kilichotumiwa na waziri kutoa adhabu hakiendani na kifungu kilichotamka kosa lililotendwa na gazeti la Mawio.

Kwa mujibu wa kifungu kilichotumika, mamlaka yenye uwezo wa kutoa adhabu ni mahakama baada ya kumsikiliza mtuhumiwa jambo ambalo katika maamuzi ya Waziri Mwakyembe halikufanyika ukiachilia mbali kwamba yeye sio mahakama.

Ikumbukwe kwamba, mamlaka pekee yenye uwezo wa kutoa haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mahakama kwa mujibu wa Ibara ya 107 (A) (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Hivyo waziri kutoa adhabu kama hii amekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kifungu alichotumia kutoa adhabu hakielezi kosa lililotendwa na gazeti la Mawio na kisheria adhabu haiwezi kutolewa bila kuwepo kosa (no punishment without law kwa kilatini Nullum Criminem Sine Lege). Waziri ametoa adhabu kwa gazeti la Mawio bila kufuata misingi ya sheria ili hali yeye mwenyewe ni mwanasheria.

Ikumbukwe mpaka sasa kwambakuzuia kujadili watu au juu ya masuala ambayo hayakuwekwa katika ripoti mbili za  kamati ya Mhe Rais  juu ya kashfa ya madini,  haiondoi haki na  wajibu  kwa watanzania kama ilivyoanishwa katika katiba ya nchi kama ifuatavyo;

• Kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake Ibara ya 18(a). Makala iliyochapishwa katika ukurasa wa 12 ni maoni ya mwandishi wa makala hiyo kwa mujibu wa kifungu hiki.

• Kila mtu amepewa haki wakiwemo waandishi wa habari kutafuta, kupokea na kutoa taarifa kama inavyoelezwa katika Ibara ya 18 (d) ya  Katiba. Wanahabari ni sehemu muhimu katika maendeleo ya taifa letu na wamekuwa kiungo kizuri cha utekelezaji haki hii.

• Kila Raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na shughuli muhimu kwa wananchi Ibara ya 18 (b).  Suala la Madini ni tukio muhimu kwa maisha ya Mtanzania na gazeti la mawio lilikuwa katika kufikisha taarifa mbalimbali zinazohusiana na sakata hili la madini.

• Katiba ibara ya 27 (1) imempa wajibu kila Mtanzania wajibu wa kulinda rasilimali asili za nchi. Hivyo pamoja na kuwa kuna  ripoti mbili za kamati, bado watanzania wengine wana wajibu wa kumsaidia Mhe. Rais katika kulinda rasilimali za nchi kama gazeti la Mawio lilivyofanya kwa kuruhusu watanzania watoe taarifa wanazoona ni muhimu kumsaidia Rais katika sakata hili.

Tumebaini pia hakukuwa na  utaratibu mzuri wa kuwasikiliza viongozi wa Mawio kwani Idara ya Habari iliwasiliana kwa njia isiyo rasmi na Mhariri wa Mawio bila ya kutoa barua yoyote ya kiofisi.  Pamoja na kwamba hakukuwa na mawasiliano yoyote ya kiofisi zaidi ya simu, Mawio waliandika barua ya kuelezea sababu za kuchapisha gazeti lao na taarifa husika.

 Moja ya sababu ni kuwa gazeti lilipishana na Agizo la Rais. Maanake Agizo liliwafikia wakati tayari gazeti limekwishachapwa na kusambazwa kwa mawakala.

Nguvu kubwa kama hizo alipewa Waziri pia katika Sheria ya Magazeti ya 1976 na sasa imeletwa  katika Sheria ya Huduma za Habari.

Waziri chini ya sheria hii mpya anafanya kazi kama mhariri mkuu, mlalamikaji, mchunguzi, mpeleka mashtaka na jaji.

Kwa mfano, Kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari inasema kwamba, "Waziri atakuwa na uwezo wa kuzuia au kuweka vikwazo kwa uchapishaji wa maudhui yoyote ambayo yanahatarisha usalama wa taifa au usalama wa umma."

 Hiki ni kipengele pekee ambacho Waziri anaweza kutumia kupiga marufuku gazeti. Kifungu hicho kinampa nguvu kubwa mno mtu moja kuamua makosa yanayofanywa chini ya Sheria ya Huduma za Habari na kuwa muamuzi wa makosa hayo pia.  Ni kinyume na misingi ya sheria za utawala bora.

Licha ya ukweli kwamba sheria hii ni mbaya sana na ni hatari kwa uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari kwa ujumla, tunaona hakuna uwezekano wowote kwamba machapisho hayo yameweza kuuweka "usalama wa taifa au usalama wa umma hatarini”.

Badala yake, uchapishaji wa picha za viongozi wastaafu wa nchi na makala iliyoundwa vizuri ikionyesha namna ambavyo sheria mbaya katika sekta ya madini zilipitishwa katika nchi yetu kipindi cha uongozi wao inaweza kutumika vyema na serikali, Bunge na wadau wengine ili kupata ufumbuzi sahihi katika usimamizi wa rasilimali zetu.

Kufungiwa kwa Mawio si tu kumekiuka sheria zetu kuhusu uhuru wa kujieleza lakini pia kimataifa imevunja Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) na Mkataba wa Afrika ambao Tanzania imeridhia.

 Kwa  uzuiaji huu idadi kubwa ya Watanzania wamenyimwa haki ya kupata taarifa na hivyo inapunguza kiwango cha uwazi kwa viongozi wa serikali kwa sababu waandishi wa habari na vyombo vya habari kwa ujumla ni waangalizi  wa utendaji wa serikali.

Kwa ujumla hatukuona sababu kubwa ya kulifungia gazeti hilo kwani tuhuma zote zilikuwa zinazungumzika lakini katika njia ambayo ingehusisha makundi kadhaa katika sector ya habari badala ya kumwachia Waziri awe mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mwamuzi kwa wakati mmoja.

WITO NA USHAURI WETU
• Serikali itengue uamuzi wake wa kulifungia gazeti la Mawio kwani umeenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 ambayo kimsingi haimpi mamlaka waziri kutoa adhabu aliyoitoa.

• Juhudi za serikali katika kuhakikisha uchumi unakua na juhudi za kupambana na rushwa lazima ziende sambamba na viongozi kuwa wavumilivu na kukubali kukosolewa kwa  mambo ambayo ni muhimu katika kufikia malengo na matarajio hayo.

• Ili kutimiza nia ya Rais wetu  ya dhati katika kukabiliana na watuhumiwa wote wa kashfa za madini, yampasa kuruhusu wananchi kuwajadili kwa uhuru wale wote wanaotuhumiwa kuhusika bila kujali kwamba wametajwa katika taarifa ya Kamati au la.

• Tunamshauri Rais atambue kuwa hiki kizuri anachokifanya leo katika kulinda rasilimali asili, kinaweza kuwafanya wananchi kwa nia nzuri kabisa kuhoji  viongozi wa zamani walifanya nini kwa kuwa walikuwa na jukumu kubwa katika kushawishi aina ya usimamizi wa rasilimali wakati wa uongozi wao.

• Ikumbukwe kwamba vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na Magazeti hufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hasa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Katiba inasema wazi chini ya Ibara ya 18 kwamba Watanzania wote wana haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari na maoni kwa njia yoyote.

• Kwamba serikali inapaswa kuondoa marufuku yake dhidi ya Mawio kuzingatia kwamba sheria hii inakiuka misingi ya kidemokrasia na inajenga picha hasi ya nchi yetu kwa jumuiya ya kimataifa.

• Ni wakati muafaka sasa kwa Sheria ya Huduma za Habari, 2016 kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha kwamba vifungu vyake vinaendana na matakwa ya  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatoa ukakika wa uhuru wa kujieleza.

• Tunamshauri Mhe Rais avione vyombo hivi vya habari kama wabia wazuri katika kupambana na rushwa nchini , na asikubali kuona wasaidizi wake wanachukua hatua za kuwajengea hofu waandishi wa habari katika kuhabarisha mambo yanayohusu ufisadi na uhujumu uchumi.

• Vyombo vyote vya habari na wanahabari waweke tofouti zao pembeni na waamke kupigania uhuru wao wa kufanya kazi zaao kama katiba ya nchi inavyotaka.

• Kwamba waandishi wa habari na wahariri wachukue kwa uzito masuala yenye maslahi ya Taifa na pia kusimamia maadili ya taaluma zao.

• Tunashauri Sheria ya Huduma za Habari ifanyiwe marekebisho ili kuondoa vifungu vinavyompa mtu mmoja mamlaka ya kufungia chombo cha habari na kuweka mfumo shirikishi utakaoshirika wadau wengine wa vyombo vya habari katika kufuatilia makosa yanayofanywa na vyombo vya habari

• Kutokana na kuwa hakuna sehemu yoyote ya kupeleka rufaa dhidi ya maamuzi ya Waziri katika sheria ya huduma za habari ya 2016,  endapo hakutakuwa na mazungumzo na waziri,  tutakwenda mahakamani kwa kushirikiana na Mawio kuonyesha haki zilizokiukwa katika kulifungia gazeti hili.

Imetolewa kwa pamoja kati ya MCT, UTPC na THRDC leo Juni 18, 2017
...............................................................
Pili Mtambalike
Kaimu Katibu Mtendaji  Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Onesmo Olengurumwa
Mratibu wa Taifa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)

Deogratius Nsokolo,
Rais – Umoja wa  Vilabu vya Waandishi Habari Tanzania-UTPC

MIMI Sio Shabiki wa Shilole, Nampenda ROSA REE – Gigy Money

$
0
0
MIMI Sio Shabiki wa Shilole, Nampenda ROSA REE – Gigy Money
Video Vixen, Gigy Money amefunguka na kusema yeye sio shabiki wa msanii wa Bongo Fleva Shilole na wala hajawahi kufikiria kumshirikisha katika muziki ambao anafanya kwa sasa.

Akipiga stori na kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, Gigy Money alieleza kuwa kati ya wasanii wa kike anaowakubali katika Bongo Fleva ni Rapper Rosa Ree.

“Sina hata mpango wala sitaki, sio fun wake (Shilole), labda Rosa Ree, tatizo la watu walio up wanasumbua, so hip hop its better, mimi ningepata mtu wa kuniandikia niwe nachana ningependa, I don’t love this kind of music ambayo nafanya, nafanya ili nipate hela, mimi napenda hip hop,” alisema Gigy Money.

By Peter Akaro

JINAMIZI la Kudanganya Umri Miss Tanzania Bado Lamtesa SITTI MTEMVU...Afunguka Haya

$
0
0
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amedai sakata la umri lililopelekea kuvuliwa taji la Miss Tanzania ni kitu ambacho kimebadili mfumo wa maisha yake kabisa huku akiwaahidi Watanzania siku moja kuweka wazi ukweli kuhusu umri wake.



Akiongea na Bongo5 wiki hii, Sitti amedai sakata hilo liliweza kubadili mfumo wake mzima wa maisha.

“Mamshukuru Mungu maisha yanaendelea vizuri kwa sababu lile sakata lilikuwa kubwa sana lakini baada ya kumalizika niliamua kurudi shule na namshukuru Mungu nimemaliza salama na sasa anaendelea na shughuli zangu za kawaida,” alisema Sitti. “Ishu ya umri wangu siwezi kuizungumzia kwa sasa tuombe Mungu siku moja nitaanika ukweli na kila mtu anatajua ni nini kilitokea,”

Mrembo huyo kwa sasa anaendelea kufanya bishara ya kitabu chache cha Chozi la Sitti ambacho alikiandika baada ya sakata hilo.

Sitti alisema kitabu hicho kitaweza kuwasaidia vijana wengi hasa wakike katika nyanja mbalimbali za maisha.

GODZILLA na Wakazi Katika Vita Nzito..Wachambana ya Nguoni Kupitia Mziki, Sikiliza Hapa Alafu Uniambie Nani Mkali

$
0
0
GODZILLA na Wakazi Katika Vita Nzito..Wachambana ya Nguoni Kupitia Mziki, Sikiliza Hapa Alafu Uniambie Nani Mkali
Bifu la Wanamuziki Godzilla na Wakazi limechukua sura mpya baada ya kuhamisha mipasho yao kwenye muziki....Embu sikiliza walivyochanana alafu uniambie nani kamfunika mwenzie

VIDEO (Wakazi)


VIDEO (Godzilla)

SIRI iliyojificha Kwenye Nazi, Muhogo na Karanga Mbichi

$
0
0

Umewahi kukaa kwenye foleni? Kama jibu ni ndiyo, je, umewahi kuwaona kina mama wanaouza nazi, muhogo na karanga mbichi katika mabeseni?

Kama jibu pia ni ndiyo, basi ukae ukijua kuwa bidhaa hizo sasa ndiyo habari ya mjini kwani muhogo, karanga mbichi na nazi vinatajwa kuwa vyakula vya kuongeza urijali na kulinda heshima ya baba nyumbani.

Ni kawaida siku hizi kuwaona kina mama wakiwa wamebeba mabeseni yaliyojaa, muhogo, nazi na karanga. Muhogo huwa umesafishwa vizuri huku gamba la juu likiachwa, lakini likikwaruzwa na kusafishwa hadi kuwa jeupe.

Karanga hufungwa kwenye vifuko vya plastiki na nazi (mbata) hukatwa vipande vidogo vidogo na kufungwa katika vifuko pia.

Muuzaji aghalabu hutembea na kisu chake kwa ajili ya kukata muhogo kwa sababu, kuna kipande cha Sh100, 200 hadi cha 500. Karanga mbichi huuzwa Sh200 kwa pakiti na nazi ni Sh100 kwa pakiti.

Wauzaji hawa ambao wengi wao ni wanawake, hutega wateja wao katika foleni za magari ambako madereva wa daladala na wanaume wengine wengi walio kwenye magari hununua kwa wingi bidhaa hizo.

Kadhalika, wanaume wenye biashara zao katika masoko makubwa kama Kariakoo, Tandika au Buguruni nao huichangamkia mihogo, karanga na nazi.

Lakini, swali ni kwa nini bidhaa hizi huuzwa kwa pamoja na kwa nini zinapendwa zaidi na wanaume?

Mwandishi wetu aliwatafuta wauzaji hao, ambao walikuwa wametingwa kuuza bidhaa zao katikati ya magari yaliyo kwenye foleni yakielekea Buguruni.

Akiwa amebeba beseni lake lililosheheni bidhaa hizo kichwani, Magdalena Mwombeki, alisema anauza karanga mbichi na mihogo kwa sababu ni vitu ambavyo wanaume wamekuwa wakivikimbilia kwa wingi.

“Zamani nilikuwa nauza matunda na muhogo mibichi, lakini wateja wakawa wanaulizia na karanga na nazi, nikaamua kuanza kuuza hivyo tu na kwa kweli vina wateja,” alisema.

Alisema baada ya kuanza kuuza kwa wingi aligundua wanaume wanapenda zaidi bidhaa hizo kwa sababu zinaongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa, “Wanaponiita wakitaka kununua, wanasema hebu tuletee karanga hizo tuongeze heshima ya ndoa.”

Alisema baadaye wateja wake wengi wakawa wanaulizia nazi na ndipo akaanza kuziuza lakini alisema anaikata vipande vidogo vidogo na kuvifunga katika mifuko ya plastiki.

Muuzaji mwingine, Shyrose Kamunguye alisema sasa hivi wanawake wengi wameacha kuuza matunda na wamekimbilia kuuza karanga mbichi, muhogo na nazi kutokana na wanunuzi wa bidhaa hizo kuwa wengi.

“Hata nikijaza matango na maembe kwenye beseni bado wateja wanaulizia muhogo mbichi na karanga na hawa wa nazi nao wanakuja kwa kasi sasa,” alisema.

Mtaalamu wa chakula na lishe katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Pazi Mwinyimvua alisema manufaa ya muhogo, nazi na karanga yameibuliwa na ujuzi wa asili.

“Binadamu mwenyewe amekula vitu hivi na akaona faida zake ndiyo maana unaona vinahitajika kwa wingi na wanaume. Ni ajabu kuona wengine wanakanusha kuwa vyakula hivi vinaongeza nguvu wakati hata sayansi inaonyesha hivyo,” alisema.

Alisema kwa mfano karanga, ina wingi wa protini na inazalisha seli nyingi kwa hali ya kawaida anayekula lazima atazalisha pia manii kwa wingi. “Kwa upande wa muhogo huu una wanga na nishati kubwa kwa hiyo ukila unakusaidia kukupa nguvu na joto na mtu ambaye hajala na hana nishati, hawezi kuwa imara katika tendo la ndoa,” alisema.

Mwinyimvua alisema nazi nayo ni muhimu zaidi kwa sababu ina protini na mafuta na yote kwa pamoja husaidia kuufanya mzunguko wa damu uende sawasawa, hivyo kumfanya mwanamume apate hamu ya tendo la ndoa na pia kuwa na nguvu zaidi.

“Hatuhitaji hata maabara kupima umuhimu wa muhogo, nazi na karanga katika kuongeza nguvu za kiume. Kwa sababu nguvu za kiume siyo miujiza ni namna unavyoishi na kile unachokula,” alisema.

Daktari wa uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Innocent Mosha alisema vyakula hivyo vinaongeza wingi wa mbegu za kiume kwa sababu vina mafuta na protini kwa wingi.

“Mafuta na protini vinazalisha seli na hivyo manii kuwa mengi. Kwa kifupi, hivi huweza kuongeza hamu ya tendo la ndoa, lakini kwa nguvu za kiume nadhani ni kwa sababu vyakula hivyo huongeza nguvu mwilini,” alisema.

Utafiti wa Mpemba

Mwandishi wetu pia alizungumza na Abeid Sultan Ghassani (81), mkazi wa Mjini Magharibi, Zanzibar ambaye kwa sasa anaishi Dar es Salaam.

Ghassani alisema wengi hawajui kuwa ili kuwa na nguvu za kiume huna haja ya kutumia dawa za hospitali, bali vyakula vya asili.

Ghassani ambaye ana wake watatu, alijisifu kuwa mpaka sasa ana nguvu za kutosha kwa kuwa katika maisha yake amekuwa akila muhogo, karanga, nazi na samaki vibua.

“Tunakula vyakula vya asili vilivyotoka shambani, muhogo mbichi na kila kitu hakijawekwa kemikali, kwa nini nisiwe imara kama simba?” alisema


Mwananchi

Imebaki Siku 1 Tu Jisajili Ushinde Gari La Bure, Shindano Hili Ni La Kweli Usipuuzie

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote... Basi hii Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...

CHAKUFANYA NI Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi wa Gari hilo..

Bonyeza Hapa >>> SHINDA GARI YA BURE <<< Kujisajili ni Bure tu...

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Meya wa Ubungo Boniface Jacob Amekamatwa na Polisi

$
0
0

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano hata hivyo sababu za kuchukuliwa kwake bado hazijawekwa wazi.

Tukio limetokea leo Jumatatu saa sita mchana katika makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Kibamba.

Askari wapatao wanne wakiwa katika gari aina ya Land Cruise walifika katika eneo hilo kisha kuzuia msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa tayari kuanza ziara ya kutembelea manispaa hiyo.

Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na viongozi wengie wa Ubungo na Kanda ya Pwani.

Baada ya kuzuia msafara huo, mmoja wa askari alishuka na kumfuata Jacob na kumweleza anamuhitaji kuambatana naye hadi Kituo cha Polisi cha Mbezi.

"Tunakuomba uongozane na sisi hadi kituoni tuna maongezi na wewe yasiyozidi dakika 10 tukiridhika tunakuachia uendelee na shughuli zako,"

Baada ya kumweleza hayo, ofisa huyo alikwenda moja kwa moja katika gari la Sumaye na kumweleza kuwa wanamuhitaji meya kwa dakika 10 kisha watamuachia.

Imetolewa Ruhusa Kuikosoa Serikali

$
0
0

Mkurugenzi wa Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbasi amefunguka na kusema hakuna chombo cha habari ambacho kitachukuliwa hatua na serikali kwa kuandika habari zenye mrengo wa kukosoa sera na utekelezaji wake na kusema watu wamekuwa wakipotosha umma.


Dkt. Abbasi amesema kuwa Sheria na 12 ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51 kinatoa ruhusa kwa chombo cha habari kukosoa kwa lengo la kuonyesha njia mbadala katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.


“Hakuna chombo cha habari kitakachochukuliwa hatua kwa kukosoa, haki hiyo ipo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51, tutaendelea kuthamini na kufanyia kazi ukosoaji huo,” alisema Dkt. Abbasi.


Mbali na hilo Dkt. Hassan Abbasi amedai kuwa kama serikali haitasita kuvichukulia hatua vyombo vya habari vyote ambavyo vitakiuka sheria na misingi ya maadili ya taaluma ya habari kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa. 


Dkt. Abbasi alisitiza kuwa ni vyema wamiliki wa vyombo vya habari wakatumia uhuru huo wa kisheria kuchapisha habari zenye nia njema kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi badala ya kueneza hofu miongoni ya mwa jamii.

Simu Tano Zakamatwa Zikiingizwa Gerezani Keko...

$
0
0

PICHA: Simu tano zimekamatwa leo zikiwa kwenye mchakato wa kuingizwa gereza la Keko zikiwa zimewekwa kwenye mapande ya nyama.

Toa maoni yako

Godbless Lema Atabiri Tena

$
0
0

Mbunge Godbless Lema amefunguka na kutoa utabiri mwingine mpya kuwa katika nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kila nyumba itakuwa na watu waliomaliza shahada ya kwanza na 'masters' lakini hazitakuwa na tija katika maisha yao na nchi kwa ujumla.


Godbless Lema amesema hayo alipokuwa katika mahafali ya Umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHASO) ambapo amewataka wanafunzi hao kuwa na maadili na maono katika maisha yao huku akisema hata katika vita ambayo nchi inapigana sasa, watu wanaoturudisha nyuma ni wasomi ambao wameshindwa kutambua wajibu wao.

"Ambalo mimi naliona ni vijana wenye vyeti lakini hawana 'moral authority' nchii hii baada ya miaka 15 au 20 kutoka sasa utakuta kila familia ina degree, kila familia ina masters lakini zisizona tija. Wasomi wasio na moral authority ni hatari kuliko wajinga wenye moral authority na gata ukiangalia kwenye haya mapambano wanaofanya kazi yetu inakuwa ngumu ni wasomi ambao wameshindwa kujua wajibu wao" alisema Godbless Lema 

Mbali na hilo Lema amesema wasomi wengi wa sasa ambao ni vijana wamekuwa ni watu wasiojali mambo ya msingi, wamekuwa wakijali sana mambo yasiyokuwa na tija katika nchi au taifa na kuikacha siasa ambayo ndiyo msingi wa kila kitu. 

"Vijana wa sasa hamjali mnajua mambo ya mipira, yaani vijana wasomi wa nchi hii wanajua zaidi mipira sijui 'Premier League' mimi siyajui vizuri hayo mambo, yaani 'commitment' yenu kwenye mambo ambayo hayawezi kuleta tija kwenye nchi imekuwa kubwa kuliko 'commitment' yenu kwenye mambo ya siasa" alisisitiza  Lema 

SABABU Zinazoweza Kupelekea Mwanamke Asiolewe Kabisa

$
0
0

Kuoa au kuoelwa ni jambo ambalo watu wengi hutamani kwani ni miongoni mwa hatua kubwa  katika maisha ya kila mmoja. Ukifanya utafiti kwa watu ambao hawajaoa wengi watakwambia wanatamani siku moja wawe na familia bora na yenye furaha, kwani kila mmoja anaamini hayo ni mafanikio kwenye maisha.

Licha ya kuwa kuolewa au kuoa ni jambo jema, baadhi ya watu huwa hawaoi au hawaolewi. Kuto kuoa au kuolewa kunaweza kuelezewa na sababu nyingi sana. Leo tutazungumzia suala la mwanamke kuolewa, na tutaweka bayana baadhi ya tabia chache ambazo zinaweza (zinachangia kwa kiasi kikubwa) mwanamke kuto kuolewa.

Utumiaji mbaya wa mitandao ya kijamii- Hili najua si kwa wanawake tu, lakini kwa sababu leo wao ni walengwa wa mada, tutazungumzia upande wao tu. Baadhi ya wanawake hutumia vibaya mitandao  ya kijamii ambapo huchati tangu asubuhi hadi jioni, wakiinua macho basi wanaangalia Tv na akimaliza channel hii atahamia nyingine, akimaliza mtandao huu atahamia mwingine. Kutwa nzima unakuta anafuatilia staa huyu alifanya nini usiku, huyu alipiga picha gani, kikapanda kikashuka.

Mwisho wa siku mwanamke kama huyu atakuwa hana cha maana alichojifunza kwenye mitandao au kutazama Tv zaidi ya kuanza kuiga yale aliyoyaona. Na hakuna mwanaume muoaji anayetaka mwanamke ambaye akili yake imetawaliwa na mitandao ya kijamii hakumbuki hata kufanya usafi ndani.

Kutokupenda kufanya kazi za nyumbani- Wanawake wengi wa ki-Afrika kwa vile wamekwenda shule wakatambua mambo ya haki sawa kwa wote na wengine kuona kwenye filamu wanaume wakifanya kazi ambazo mara nyingi hufanywa na wanawake, basi na wao ndio wameweka nukta kufanya kazi za nyumbani.

Kuto kana na hali hii, wanawake wamekua wakujiremba tangu mawio hadi machweo, ukitazama kucha zao zilivyondefu unajiuliza hutu anafua kweli? wengine wame amua kuajiri watu wa kuwafulia hadi nguo za ndani. Kwa hali hii isitarajie mwanaume akuoe kwa sababu anajua ni matatizo anapeleka nyumbani.

Kujipara hadi sura yako ya asili inasahaulika- Ni kweli wanaume hupenda mwanamke mrembo na mwenye kupendeza. Lakini hii haimaanishi ndio ujipodoe hadi uchukize. Kila kitu  kwa kiasi chake kwa sababu kitu chochote kikizidi huwa ni sumu.

Jirembe kwa kiasi, hili litavutia watu walio-serious kutaka kukuoa, lakini ukiwa ni wa kujiremba hadi ukapindukia, hakuna muoaji atakaye kuta. Tena ikumbukwe kuna baadhi ya wanaume wao hupenda mwanamke asiyejiremba (wenyewe huita natural)

Hizi ni baadhi tu, na wewe unaweza kuongezea ili kuwakumbusha wasichana wanaotaka kuolewa.

ZITTO Kabwe "Naipongeza Serikali kwa Kuchukua Hatua Juu ya Sakata la Escrow"

$
0
0

Naipongeza Serikali kwa Kuchukua Hatua Juu ya Sakata la Escrow

Kwa dhati kabisa naomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Chama changu kuipongeza Serikali kwa hatua hii ya kuwafikisha Mahakamani Watuhumiwa wa Sakata la Escrow kama ilivyoazimiwa na Bunge Septemba, 2014. Hii ni hatua muhimu sana katika mapambano dhidi ya Ufisadi nchini.

Nasikitika ndugu yangu Deo Fulikunjombe hayuko hapa kushughudia matokeo haya ya kazi kubwa aliyoifanya kwaajili ya Taifa.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Mikumi- Morogoro
Juni 19, 2017

Pendeza na Markson Beauty, Ongeza Hips na Makalio, Kuwa Mweupe na Softi na Ongeza Nguvu za Kiume

$
0
0

PENDEZA NA MARKSON BEAUTY. ONGEZA HIPS NA MAKALIO, KUWA MWEUPE NA SOFTI, ONGEZA MAUMBILE YA KIUME, NGUVU NA HAMU YA TENDO N.K
@Markson_beauty_pr Tunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa kiafya.
NB. Matokeo ni uhakika na garantii.
🍉🌿🍅🍍🍒🍉🍓🍅🍒
BIDHAA ZETU:-

1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @120,000/=
2. Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @ 150,000/=
3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-
(1)Mafuta @120,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a) Gely ya kupaka @130,000/=
(b) Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @130,000/=
(C)Handsome up original @200,000/=
6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @130,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula @120,000/=
8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/=
(b) Mkanda wa kawaida @100,000/=
(c) micro-computer belt wa umeme @170,000/=
9 .Kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @120,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @130,000/=
11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120,000/=
12.Kurudisha usichana (bikra) @120,000/=
Wasiliana nasi :- (+255)
0767447444 au.
0714335378
TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
F

NAPE Nnauye Awatetea Wapinzani...Adai Wasibezwe Sakata la Mchanga...

$
0
0

Nape Nnauye amepinga vitendo vinavyofanywa na CCM vya kuwabagua watu wa Vyama vya Upinzani na kuwaona ni Wasaliti katika hili swala la Madini na Mchanga unaoshikiliwa. Hili swala halifai na halitatufikisha popote kama taifa. Ni wakati wa kwenda pamoja kwenye hii vita ili tufanikiwe bila kudharau mawazo ya mtu yoyote.

Hii ni vita yetu sote, Tushikamane, hata kama wana hoja, wajibiwe kwa hioja sio matusi. Ameshauri Serikali iangalie kwa makini hili swala ili kuondoa Mashaka.

Amempongeza rais Magufuli kwa kuzuia Mchanga.

Amekosoa pia sela za mapato. nasema mipango yote inalenga kubana na kukamua walipa Kodi.

.
KUPATA HIZI STORI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KUTOKA PLAY STORE KWA KUBONYEZA LINK YA BLUE KWENYE BIO YANGU....

MWANAMKE adaiwa kumkata sehemu za siri mtoto wa jirani yake

$
0
0

Hekaheka ya leo June 19, 2017 kupitia Leo Tena ya Clouds FM imetokea Sinza DSM ambapo mwanamke mmoja anadaiwa kumkata sehemu za siri mtoto wa kiume wa jirani yake mwenye umri wa miaka minne akidai amembaka binti yake wa miaka miaka mitatu.


Inadaiwa kuwa watoto hao walikuwa wanacheza nyumbani kwa mama huyo ambapo alidai kuwakuta wakifanya hivyo hivyo kuamua kumkata sehemu za siri mtoto huyo wa jirani jambo lililopelekea kukimbizwa Hospitali na kufanyiwa tohara baada ya mzazi wake kutoa taarifa Polisi.

Cheen Beenz na Chuki Binafsi Kwa Navykenzo na Wasanii wa The Industry

$
0
0

Huyu msanii anayejiita Cheen Beez kila mara amekuwa akiojiwa na media tofauti akilalamika kuwa amewatungia Baadhi ya nyimbo Navykenzo na Wasanii wao Rosa ree na Vanessa Mdee na kuonyesha uchungu kuwa wanapiga hela ndefu kwa ajili yake.....

Ki ukweli mie hii hainingii akilini hata kama kweli aliwatungia hizo baadhi alizodai , kila mtu anajua Uwezo na Navykenzo, Vanessa Mdee na Rosa Ree wasanii anaodai aliwatungia viitikio alivyokuwa katika lebo hiyo....

Hawa wasanii ukiangalia tu kwa haraka haraka wanauwezo kuliko yeye na wanahit songs nyingi hata before yeye hajajulikana katika game ya music, nachoona kwake ni chuki binafsi alizonazo kutokana na mafanikio wanayopata kila siku zinavyoenda huku yeye akizidi kupiga jalamba na nyimbo zake ambazo hazieleweki huku akidai anauwezo mkubwa wa kutunga nyimbo..

Namshauri tu akae kimya kwani hizo ni kiki hewa tuu huku anaowashutumu hawana hata time ya kumjibu ...

Atumie huo uwezo wake kujitoa kwanza yeye mwenyewe naye apige hela kibao....la sivyo namtabiria hata hiyo lebo ya wanene siku si nyingi watampiga chini kwa kutoona mafanikio yake bali longo longo na kujidai tu

By Laikon

Chemical Afunguka" Sijapaniki Marapa Wengine wa Kike Kufanya Vizuri Bongo"

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Chemical amesema wimbo wake wa Queen of Dar es Salaam hajauandika kwa ajili ya watu fulani kama watu wengi wanavyodhani.



Rapper huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, kuwa yeye amerudia kile ambacho walifanya Sugu na Prof Jay alichoongeza yeye ni katika verse ya tatu.

“Verse ya mwiso ndio imeleta utata watu kuona Chemical anashindana na watu. Siwezi kusema imeleta chuki ila watu wameona kama Chemical kapaniki kuona marapa wa kike wanafanya fresh, hawajui hii ni sanaa sio ya kujisifia na ukiangalia sio ngoma moja mimi kufanya hivi, that its hip hop watu wasiichukulie too person,” amesema Chemical.

Wimbo wa Queen of Dar es Salaam Chemical amechukua verse moja moja pamoja na chorus kutoka kwenye wimbo wa  Prof Jay ‘Bongo Dar es Salaam’, na ile ya Sugu na Balozi ‘Dar DSM.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images