Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Timu Yakamilisha Uchunguzi Sakata la Pacha Temeke

0
0

Timu iliyoundwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuchunguza tuhuma za wizi wa mtoto pacha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke, imekamilisha kazi yake.

Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa timu hiyo, Profesa Charles Majinge zilieleza uchunguzi ulikamilika mwishoni mwa juma lililopita na wakati wowote ripoti itakabidhiwa kwa waziri.

Waziri Mwalimu aliunda timu hiyo Mei 29, mwaka huu baada ya familia inayodai kuibiwa mtoto kutoridhika na ripoti ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Grace Magembe iliyoeleza mlalamikaji hakuwa na pacha, bali watumishi wa hospitali hawakutimiza wajibu wao, hivyo kumfanya aamini alikuwa na pacha.

Waziri aliunda na kutangaza timu hiyo baada ya kukutana na familia inayodai kuibiwa mtoto ya Asma Juma na Abubakar Pazi.

Profesa Majinge aliliambia gazeti hili kuwa wameshakamilisha ripoti na wanasubiri maelekezo ya waziri ili kumkabidhi.

“Tumeshakamilisha ripoti yetu na kama waziri angekuwapo tungemkabidhi hata Ijumaa, kwa sasa nataka nifanye mawasiliano na katibu wake ili atueleze lini tumkabidhi,” alisema Profesa Majinge.

Timu hiyo ilitakiwa kufanya kazi kwa muda wa siku 14 kuanzia Mei 31 na kukabidhi ripoti Juni 14.

Timu hiyo ilikutana na walalamikaji Muhimbili Juni 3 na baadaye kuendelea na uchunguzi kwa kuwahoji walalamikiwa ambao ni madaktari waliohusika kumpasua mama huyo alipojifungua, wahudumu wengine wa afya katika Hospitali ya Temeke na zahanati ya Mbande alikokuwa akipata huduma za kliniki.

Pia ilifanya mahojiano na mtaalamu wa vipimo vya ultrasound katika zahanati ya Huruma iliyoko Mbande na kutembelea na kukagua zahanati na mashine hiyo.

 

Jokate ana kolabo na Rosa Ree?

0
0
Mrembo Jokate huwenda akandosha ngoma na hitmaker wa ngoma ya Up In The Air, rapper Rosa Ree ila haijajulikana ni lini hasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jokate ameandika, “Najua imekuwa muda mreefu saaana buh muda umewadia and we got a lil something for y’all. Rosa Ree X Kidoti #Get Ready To Be Entertained,”

Jokate amekuwa akifanya muziki na alishatoa wimbo na produza Lucci uitwao Kaka Dada, na amesikika kwenye kolabo kadhaa ikiwemo Kings and Queens na El Chapo zote za AY.

By Peter Akaro

VIDEO: Walemavu Waliopigwa na Polisi Kwenye Maandamano Wadai Fidia

0
0
Kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ulemavu Jijini humo, Abdallah Komboza ameeleza kuwa kitendo walichofanyiwa na Jeshi la Polisi Juni 16 Jeshi la Polisi hakikuwa cha kiuungwana na sasa wanataka walipwe fidia kutokana vipigo na majeraha waliopata

Juni 16 Mwaka huu, Walemavu hao walijikuta Mikononi mwa Polisi katikati ya Jiji la Dar es salaam kwa kile kilichoelezwa kuwa walifanya Maandamano yasiyo halali

VIDEO:

Davida Kafulila 'Wakati wa Sakata la Escrow Niliitwa Nyani na Kutishiwa Maisha ila Magufuli Alinipa Moyo Nikomae tu Mpaka Kieleweke'

0
0
Hatimaye imekuwa! Vinara katika ufisadi wa IPTL/ESCROW Singasinga Seth na Rugemarila watiwa nguvuni. Huu ni uamuzi mkubwa uliosubiriwa sana. Na siku zote sikujua kwanini Mhe Rais alikuwa anahofu kuagiza hatua hii.

Sikujua kwanini, kwasababu wakati wa mnyukano wa hoja hii, Mhe Rais alikuwa bungeni na alikuwa sehemu ya maazimio ya Bunge kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe na wahusika watiwe nguvuni..

Nakumbuka nikiwa kwenye kipindi kigumu hata kutishwa kuondolewa kichwa na kuitwa majina ya wanyama, yeye alikuwa miongoni mwa mawaziri 5, walionidokeza kwamba ESCROW ni dili nikomae tu mpaka kieleweke!

Nampongeza Mhe Rais kwa uamuzi huu muhimu uliosubiriwa siku nyingi kuamua hatma ya ufisadi huu uliomshinda vibaya mtangulizi wake.

Singasinga huyu alinifungulia kesi kunidai Sh300bn Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2014, Agust2015 nikamshinda lakini akaamua kunifungulia upya Mahakama ya Kisutu akidai Sh100m, zote akidai nimsafishe kuwa yeye na wenzake hawakuchota zaidi ya 300bn kifisadi.

Kifupi naomba PCCB na DPP wasituangushe watanzania. Nilipata kuwaza kumwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali anipe kibali niendeshe kesi na hawa majabali wa escrow kwani nina ushahidi wakutosha,Sasa nina furaha kwamba PCCB wameamua kuwaburuza.

Nashauri mambo machache;
1.Mali zote za wahusika hawa ziwekwe chini ya ulinzi kabla hawajahamisha umiliki kwani ni muhimu zikakamatwa kusubiri hukumu ya kesi hii ya Tanzania lakini pia kesi iliyopo Mahakama ya kimataifa ya International Centre For Settlement of Investment Disputes (ICSID). Ambako Septemba 2016, iliamuliwa tulipe Bank ya SCB-HK kiasi zaidi ya 400bn kwa kuwa ndio wamiliki halali wa IPTL na wenye share certificate za IPTL..

Mwaka huu TANESCO imekata rufaa. Najua TANESCO hawajakata rufaa kushinda kesi bali kuomba wapunguziwe hukumu ifanane na uamuzi wa ICSID wa Feb 2014.

Lakini kwakuwa Singasinga Seth alisaini hati na Benki Kuu ya Tanzania, kwamba deni lolote lotakalotokana na migogoro ya IPTL atawajibika yeye na wenzake wanaomiliki kampuni PAP, ndio maana nasisitiza Mali za watu hawa zishikiliwe.

2. Mtambo wa IPTL uwekwe chini ya TANESCO kama ilivoazimiwa na Bunge Nov 2014, tuachane kabisa na kulipa matapeli 7bn kila mwezi ambazo ni malipo ya capacity charges walizokuwa wanalipwa na serikali hii bila kujali IPTL imezalisha au haijazalisha umeme.

3. Mwisho watanzania watambue kwamba huyu Singasinga anaetambulishwa kama mmiliki wa PAP iliyopora 300bn za escrow kama mmiliki mpya wa IPTL, mpaka fedha hizo zinaporwa alikuwa anamiliki asilimia50% tu ya kampuni lakini asilimia 50 zilikuwa zikimilikiwa na kampuni ijulikanayo kama SIMBA TRUST, inayomilikiwa na watu wasiojulikana. Hawajawahi kutajwa popote kwenye report zote.

Nilijaribu kutaka majina yao kwenye Kamati ya Viwanda wakati tukiwahoji BRELA na hata baadae bungeni Serikali iliendelea kusisitiza kuwa majina hayo ni SIRI. Hawa ni wahusika muhimu sana wajulikane kwani inawezekana ndio msingi wa serikali ya awamu ya nne kuibeba IPTL kama mtoto!

Naam, hongera Mhe Rais kwa hatua hii, nazidi kuomba Mungu kesi hizi zifike mwisho kwani kwangu leo ni siku muhimu katika kumbukumbu zangu kuliko Aprili 28, 2015, siku niliyopewa tuzo kwa mapambano dhidi ya ufisadi kwa rejea ya sakata la ESCROW, kwani tuzo haina maana kama vita haifiki mwisho.

Mwisho nishauri asiwepo yeyote wakulindwa kwa Kinga yoyote kwani Katiba na Sheria vipo kwa ajili ya watanzania na sio watanzania kwajili ya Katiba na Sheria. Tusipofika huko vita ya UFISADI mkubwa itakuwa ngumu sana kufika mwisho.

David KAFULILA
JUNE19,2017

Ladies:Wanaume wa Kuoa Hawatafutwi Clubs na Sehemu za Starehe

0
0
Some ladies have lost their thinking caps. Some found it but unable to use it. Must you clock 35 before you stop partying here & there? You already know all Eateries/ Hotels in town! You even know the tastes of their various ice-creams, pepper-soups, shawamas, etc.
And you can tell the prices of their beers and wines offhand.

Funny, you're singing “No man is responsible.”

*Which responsible man drinks to stupour and clubs every weekend?

*Which responsible man samples you and your slutty friends randomly?

*Which responsible man sags with dog's chains on his neck and tattoos on his body?

Ask your self; “Is the guy I'm currently dating my dream man?”

Dear sisters,

If you are living your life as above, my dear, you are living a life of mirage. Be real! Humble yourself and so you will be raised.

The so called "responsible men" you are searching for are not in the clubs and hotels, you won't find them at the weekly birthday 'bashes', weekend beach crashing or pool-side jamborees loitering around women of easy virtues, drunkards and men of questionable characters.

They are busy; in the Universities, Polytechnics and Colleges studying hard for the life after school, and in the offices, workshops, and on business trips striving hard to make life better for their families and better than they've met it.

Use that brain Sweet Sisters!

It's for thinking.

Sheikh: Walaaniwe Wanaombeza Magufuli

0
0
Sheikh   wa  Mkoa  wa  Mbeya,  Mohamed  Mwansansu  amesema anayezibeza  juhudi za  Rais John Magufuli anapaswa kulaaniwa.

Sheikh Mwansasu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu) usiku alipokuwa akisoma dua ya kumuombea  Rais Magufuli kwenye kusanyiko la waumini wa Kiislamu wa mikoa ya Mbeya na Songwe.

Dua hiyo ilienda sambamba na  futari iliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust, kwa waumini wa dini ya Kiislam na kufanyikia katika Ukumbi wa Royal Tughimbe jijini hapa.

“Lazima kwa umoja wetu tuendelee kuungana na Rais wetu katika kupambana na wezi na mafisadi wa rasilimali zetu, na nitamshangaa mtu mwenye akili timamu anapinga juhudi hizi kwa sababu ya itikadi za chama chake  au mtu yeyote ni lazima aangamie mara moja,” amesema.

Amesema anachokifanya Rais Magufuli ni kwa  ajili ya masilahi ya Watanzania wote na siyo familia yake wala chama chake hivyo Watanzania kwa umoja wao wanapaswa kuungana  kwa pamoja katika kumuunga mkono ikiwa ni pamoja na kumuombea kwa Mungu kwani ndiye mlinzi mkuu.

Kuhusu futari hiyo amesema alichokifanya Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson kupitia taasisi yake  ni jambo la  thawabu hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati yeye ni Mkristo.

“Huu ni mfano mkubwa, Tulia kuwapa chakula Waislamu hivyo na sisi waislamu tuweze kufanya hivi kwa kuwaita jamii isiyo ya kiislamu na kukaa nayo pamoja zungumza na kufuturu pamoja,”amesema. Kaimu Sheikh  wa Mkoa wa Songwe,  Hussein Issah Batuzi, amesema uislamu ni kuitisha jamii tofauti tofauti kukaa pamoja na kuzungumza na kuleta amani  na utulivu badala ya kuleta shida, vurugu na patashika kwa jamii nyingine jambo ambalo mwenyezi Mungu anakataa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi  Mkoa wa Mbeya (CCM) Wilson Nkhambaku, ametoa rai kwa viongozi hao wa dini ya kiislamu na Watanzania wote bila kujali tofaui za kiitikadi kuendelea kuwaombea viongozi wa Serikali kwa kazi ngumu wanayofanya ya kupambana na mafisadi wa rasilimali za Taifa.

“Naomba muendelee kuwaombea vingozi wetu ili Mungu aweze kuwapa ujasiri mkubwa na upendo kwa manufaa ya Taifa letu na waendelee kusimamia uchumi wa nchi yetu kwani kufanya hayo kunahitaji ujasiri na ulinzi wa mwenyezi Mungu.”amesema.

Aliyetaka Kuingiza Simu Gerezani Afahamika

0
0
Ramadhan Nombo, mkazi wa Jiji la Dar jana amenaswa na askari magereza katika Gereza la Mahabusu la Keko akitaka kuingiza simu tano.

DAR ES SALAAM: Kijana mmoja, Ramadhan Nombo, mkazi wa Jiji la Dar jana amenaswa na askari magereza katika Gereza la Mahabusu la Keko akitaka kuingiza simu tano alizokuwa amezificha ndani ya mapande ya nyama yaliyorostiwa. Tukio hilo la ajabu limetokea jana baada ya Nomba kuwapelekea ndugu zake chakula.

Kwa mujibu wa chanzo, Nombo alipanga kuingiza simu tano ambazo alizipachika kwenye mapande ya nyama iliyorostiwa kisha kuwapelekea ndugu zake walioko gerezani hapo.  Hata hivyo, haikufahamika alikuwa anawapelekea kwa sababu gani, na wafungwa wa kesi zipi.

Mtandao huu ulimtafuta Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, ASP Lucas Mboje ili kuzungumzia tukio hilo ambapo alikiri kutokea na akaelekeza aonwe Mkuu wa Magereza wa Dar.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, DCP Augustine Mboje alipoulizwa alisema ni kweli kijana huyo amekamatwa.

Kama akikutwa na hatia atakuwa amevunja Kifungu cha 86 (1) cha Sheria za Magereza sura ya 58 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, inakataza kwa mtu yeyote kuingiza kitu chochote kisichoruhusiwa gerezani na atahukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita(6) au faini au vyote kwa pamoja.

Hadi sasa Nombo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mganga Aua, Aondoka na Kiganja Cha Mkononi

0
0
WATU watatu wamefikishwa mahakamani akiwemo mganga wa kienyeji kwa tuhuma za mauaji ya Elizabeth Charles (45), mkazi wa kijiji cha Tambalale kata ya Nsimbo wilayani hapa.

Waliofikishwa mahakamani hapo ni Juma Idd(25), Tatu Juma (20) wote wakazi wa kijiji cha Tambalale pamoja na mganga wa kienyeji, Shida Mwanansimbila (54) mkazi wa kijiji cha Kipungulu kata ya puge wilayani Nzega.

Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi wilaya, Mengo Kamangala alidai mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi, Ajali Milanzi kuwa Mei 25 mwaka huu majira ya saa 5:00 usiku katika kijiji cha Tambalale Tarafa ya Nsimbo wilaya hapa, washitakiwa wote kwa pamoja walimpiga kisha kumuua na kuondoka na kiganja chake cha mkono wa kulia.

Alisema washitakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo. Hata hivyo, washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 23 mwaka huu, itakapotajwa tena na washitakiwa wamepelekwa mahabusu.

Ben Pol "Wanawake Wajigonga Kwangu Wakijua Watakula Bata na Kwenda Clubs, Nikiwakubalia Wanakuta Tofauti na Kusepa"

0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema mahusiano yake yaliyowahi kudumu zaidi ni miezi tisa tu.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa sababu inayopelekea hali hiyo ni kwamba watu wanaoingia katika mahusiano na yeye huwa na matarajio makubwa na wanapokuta sivyo wanakimbia.

“Miezi tisa ndio longest relationship kwa sababu unajua yaani nimekutana na watu wa aina tofauti, watu ambao wanaokuwa na expectation kubwa zaidi kuhusu mtu flani, kwa hiyo akiingia kwenye maisha yako anakuwa ana vitu tayari ali-picture kwamba Ben Pol tutakuwa tunakula bata every weekend, tunakula bata milioni, tunaenda huku na kule,” Ben Pol ameiambia Choice FM.

“Kwa hiyo mtu anaingia kwenye maisha yako anakuta si mtu wa hivyo ni staa ndio lakini we don’t go to club mara kwa mara, we don’t do this, we don’t do that, kwa hiyo mtu anakuwa disappointed anatoka kwenye mahusiano ndio hicho nime-experience zaidi kwenye mahusiano yangu yaliyopita,” ameeleza Ben Pol.

Serikali Yaomba Radhi Walemavu Kupigwa Dar

0
0
Serikali imewaomba radhi walemavu na Watanzania wote kutokana na nguvu kubwa iliyotumika kwa walemavu waendesha bajaji wa Jiji la Dar es Salaam waliokuwa wakitaka kwenda kumuona Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameomba radhi leo (Jumanne) na kukiri kuwa pamoja na walemavu hao kuwa na makossa, lakini nguvu ya polisi ilipitiliza na akasema wameshawasilina na mkoa husika kupitia ustawi wa jamii.

Waziri alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu, Stella Ikupa ambaye alitaka kujua namna gani Serikali inavyoweza kuliona jambo hilo lililosababisha walemavu kupigwa, kuburuzwa chini na kudhalilishwa kwa kiasi kikubwa.

Sumaye Aiangukia Serikali, Oomba Kukivumilia Chadema

0
0
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amefunguka na kuitaka serikali ya awamu ya tano iwavumilie na itambue kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na viongozi wake ni chama halali kinafanya kazi kama CCM inavyofanya kazi zake.

Sumaye aliyasema hayo jana baada ya jeshi la polisi kuzuia msafara wao ambao ulikuwa na lengo la kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na CHADEMA.

"Hili si jambo la ajabu kwa sababu hata viongozi wa CCM kwa mfano hata Pole Pole anazunguka halmshauri zote nchini, ila wanapozunguka wao hakuna tatizo ila inapokuja viongozi wa CHADEMA kidogo tayari wanaanza mapambano, tunadhani huu ni uonevu tu unaendelea wa kujaribu kuwafanya watu wengine wajisikie kwamba hawana uhuru na nchi yao hili nafikiri si jambo jema.

"Serikali tunaomba ituvumilie ijue kwamba CHADEMA pamoja na viongozi wake ni chama halali kinafanya kazi kama CCM wanavyofanya kazi kwa hiyo mambo ya kuandamwa CHADEMA kila mahali inatusikitisha sana" alisema Sumaye

Mbali na hilo Sumaye anasema vitendo hivyo vinavyofanywa kwa viongozi wa CHADEMA ni kutaka kukatisha tamaa jitihada zozote zinazofanywa na viongozi wa chama hicho hivyo anadai ni kitu ambacho hakiwezi kuvumilika.

"Kwa jambo hili mimi nataka tu kuimbia serikali kuwa hawatafanikiwa kwani wataleta vurugu pasipo kuwa na sababu zozote zile, wawaache watu wafanye kazi zao hapa hakuna siasa zozote tunazofanya.

"Tunakagua miradi kwani halimashauri hizi ni zetu kama ambavyo wao wanatembea kwenye halimashauri zote nchini kuona namna Ilani yao inavyotekelezwa na sisi tunataka kujua viongozi wetu wa CHADEMA wanatekeleza vipi yale ambayo CHADEMA imewaagiza kufanya katika Ilani yake. Na miradi hii ni kwa wananchi wote" alisisitiza Sumaye   

Makubwa! Mpenzi Anataka Nyuma la Sivyo Ananiacha..Help

0
0
Kuna dada mmoja amenihadithia jambo akiomba ushauri anasema ana mpenzi wake wanaopendana sana wamekuwa pamoja kwa miaka mitano sasa, kila siku ya maisha yao haijawahi kutokea akajutia kuwa na huyo mpenzi wake..

kwa muda huo wote walikuwa wakikutana kimwili kwa njia ya kawaida tu ile ambayo inaruhusiwa kihalali na wala kulikuwa hamna tabu wala hamna mtu ambaye hakuridhika na starehe ambayo mwenzake anampa..

anachoshangaa yeye ni kwamba mwezi wa tatu huu sasa jamaa ananuna hataki hata kwenda nyumbani kwa huyo dada kisa jamaa amechoka kula mbele peke yake anataka kanga igeuzwe upande wa pili..

huyu dada alikataa na kumwambia hiyo siyo sahihi kwake, kitu mpenzi wake alichomjibu ni kwamba kwani wewe upo nji gani wasichana wenzako siku hizi wengi huwapa wapenzi wao upande wa pili kwa nini wewe hutaki kunipa? kama hutaki inamaana utaanza kumpa mtu mwengine ama unaona mimi sifai?

yule dada kwa uchungu anasemakila siku alikuwa anampigia simu mpenzi wake akilia akimuomba aachane na hayo mawazo, lakini kijana bado anadai anataka, anasema sasa umekuwa ugomvi mkubwa sana kati yao na anahisi wataachana kinachomuuma nikwamba anampenda sana mpenzi wake huyo, na mpenzi wake haelewi somo lengine kabisa huyu dada sasa hajui afanye nini...

akiomba ushauri kwa rafiki zake wengine wanamwambia ampe tu huyo mpenzi wake kwani atabadilisha wanaume wa ngapi? wengine wanamwambia hiyo ni dhambi kubwa lakini akitaka anaweza tu kumpa kwani dhambi ngapi amefanya tokea amezaliwa iwe hiyo moja? wengine humshauri kwamba siku hizi mpaka machangu wengi hutoa nyuma ama unataka aende akachukue kwao akileta magonjwa je?

I'm Pregnant For My Pastor, What Should I Do?

0
0
I am writing this note, not exactly because I regret my action of taking full control of a married Pastor, but because I have sensed something that is really not going to work for me in the most positive way, if I keep this pregnancy. I don’t regret my action because I understand that pastors too are human beings, and have the same feelings like the rest of us. He slept with me, got me impregnated; so what?

However, a little of the background will give you an insight into how it all started. I understand that as human beings, we cannot cheat nature. I’m one of the Choristers in the church, and there is this magnet that pulls the pastor and I together. It is like a magnetic force. However, he had explained to me in the most pathetic way one day on how the wife had starved him of sex for months all in the name of spirituality. He only said that passively anyway. He also complained bitterly, while I listened with superlative attention on how the wife hardly ever satisfy him on bed. I actually wanted to satisfy him, as I’m such an emotional and considerate person. I am very sure God won’t judge me negatively because of my kind gesture. I only tried to satisfy a man who was dying of hunger, he was been starved of sex and I had to leave spirituality behind to get him satisfied.

I remember how it all started, and like a Hollywood movie, the scenes reeled from one to the other and we had our fun in different hotels after every church meeting. I must always wait for the Pastor who will convey me to my house. After all, he is a pastor, and no one would suspect that any ‘dirty’ romance was going on between us. He confessed that I had made him feel like a woman, and I was just proud of myself. I will always node in exhilaration knowing very well that if I can satisfy another man, then I can satisfy my man. This is something every young lady should be proud of. I am not trying to patronize my action, but only being reasonable about some sensitive sexual matters.

Yes, we did, and since then, I have been excommunicated from the church. In fact, the whole thing remained secret until he got me impregnated, and I confronted him for an abortion. To my consternation, he refuted my suggestion; he wanted me to keep the baby. I had moved against it. I had given him reasons why I shouldn’t keep the baby. I don’t want to jeopardize my dream of getting married at the age of 26 which is just less than a year. I told him that I must get rid of the baby. But he has vowed to sue me if I do. He is happy that at least what he had waited for endlessly since he got married in 2000 has come to fruition as God has finally opened the doors through me. Yes, he never had a child since he got married, and age is really not on his side. I can’t get his words off my head; “ I want this baby like yesterday” he said.

This disagreement has put me in the public glare today as my close friends whom I divulged the situation to, had reported the matter to the church committee, and I have since been excommunicated. Everybody talks about me as if I have done something so strange. My concern really is not about what people are saying but to get a little piece of your advice on whether I should keep the baby against my wish, or go for an abortion. I know what I want but I still need your advice in order to justify the action I’m about to take. In the next five days, I should be able to take a major decision. Thank you for publishing my story.

Mapenzi ya Kuiba au ya Chap Chap ni Matamu ila Yana Madhara Makubwa...

0
0

Kula nanasi kunahitaji nafasi, wengi wamekuwa wakishawishika kufanya mapenzi katika eneo la kazi kutokana na kupendana ama vishawishi mbali mbali kutoka kwa kinadada hususani katika mavazi. Sina maana mbaya ninaposema kina dada kwasababu wengi wao ndio wanaoacha sehemu zao nyeti wazi, kwamfano kuvaa nguo fupi sana na kuvaa vitop vinavyoonyesha sehemu kubwa ya maziwa wazi.

Kwa asilimia miamoja watu wengi wanaofanya mapenzi kwa kuiba katika maeneo kama ya ofisini huwa hawakumbuki kuvaa kinga kutokana na mihemumko mikali na ya haraka kuliko kawaida wanayokuwa nayo kwa wakati huo. Ni vyema kujihadhali ma mihemuko hii kwani madhara yake ni makubwa.

Mihemuko hii huwakumba watu wote hata ambao wako katika ndoa, kutokana na vishawishi vya mwenzake basi anajikuta amezama katika saa za kazi. Tabia hii ikifanyika mara tatu huanza kuwa kama sehemu ya majukumu ya wezi hawa wa mapenzi. Kinadada wanaovaa nguo fupi katika makazi ya watu huenda wakawa wanafanya hivyo kwasababu ya fasheni, wengine kutafuta mvuto kwa wafanyakazi wenzie, lakini kwa wanaume huwa ni kishawishi kimoja kikubwa sana.

Kumbuka unapaswa kuishinda faragha yako na kujitambua kuwa hupaswi kufanya mapenzi na mke wa mtu au mume wa mtu. Unapoona vishawishi kama hivi jaribu kuwa bize na kazi, chukulia poa tu japokuwa wadada wengi huwa na njia mbali mbali za kukufanya ukanasa kirahisi kwa mfano kama mnakumbuka skendo ya Monica Lewinsky na aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo walichokifanya ofisini na baadae kuja kuwa ni skendo kubwa sana.

Hasara ya mapenzi hayo ya kiwizi wizi katika masaa ya kazi ni kupata maambukizi ya Ukimwi bila kufahamu kwani utakuwa umemzoea mfanyakazi mwenzio kwa jinsi alivyo smati katika kazi, hivyo hutafikilia kama anawatu wengine nje ya kazi. Pia kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo kwa wanawake hujificha kwa muda kabla ya kuonekana haraka kama wanaume.

Amenisomesha, Kaninunulia Gari Lakini Sina Mapenzi Naye! Nifanyeje?

0
0
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.

Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.

Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo pia ni sharo sio mshamba kama huyu wa zamani.

Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?

Marekani Yaishambulia na Kuiangusha Ndege isiyo na Rubani Nchini Syria

0
0
Ndege ya jeshi la Marekani imeangusha ndege isiyo na rubani inayoendeshwa na serikali ya Syria kusini mwa nchi, Ndege hiyo isiyo na rubani ilidaiwa kuwa na silaha na ilikuwa hatari kwa jeshi la Marekani ardhini.

Hiki ni kisa cha karibuni kabisa katika anga ya Syria, baada ya Marekani kuangusha ndege ya kivita ya Syria siku ya Jumapili na ndege nyingine isiyo na rubani mapema mwezi huu.

Katika taarifa nyingine jeshi la Marekani lilitangaza rasmi kuwa lilimuua kiongozi wa cheo cha ju wa kundi la Islamic State Turki al-Binali, wakati wa shambulizi lililofanywa na ndege nchini Syria Mwezi uliopita.

TAZAMA Jinsi Mbunge Waitara Alivyolianzisha na Kuamriwa Atoke Nje ya Bunge na Spika

0
0
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzaia Job Yustino Ndugai Amemtoa nje Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara kwa Kufanyafujo ndani ya Bunge wakati wa Kupitisha Bajet leo Jioni.

Kura ya Hapana yazua Mjadala Upitishaji Bajeti ya Serikali..Spika Ataka Waliopiga Hapana Wasipewe Pesa

0
0
Kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba waliopiga kura ya hapana wakati wa kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 wasipatiwe fedha na mawaziri kwa ajili ya miradi imeibua mjadala bungeni.

Aliyeanza kuhoji kuhusu kauli hiyo leo (Jumanne) ni Joseph Mbilinyi maarufu Sugu aliyetaka mwongozo wa spika kuhusu kauli yake.

James Mbatia, amesema ni bora kufanyike mabadiliko ya Katiba ili kuwe na chama kimoja kama Bunge haliruhusu mawazo tofauti.

David Silinde amesema kauli zinazotolewa zinaweza kulipasua Taifa, hivyo kuwataka wabunge kutojenga Taifa ambalo wanaweza kulipasua wenyewe.

Mchungaji Peter Msigwa amesema wapinzani hawako bungeni kwa bahati mbaya na kwamba waliowachagua wanajua misimamo yao, hivyo wanapopiga kura ya hapana si kwamba Serikali ipeleke fedha kama hisani kwa kuwa ni fedha za walipa kodi.

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amesema dunia imebadilika na kwamba zamani bajeti haikuwa shirikishi lakini sasa wabunge wanashirikishwa tangu mipango na maoni ya pande zote huchukuliwa kwa hiyo inashangaza kukataa.

Spika amesema upinzani si wa kusema hapana kwa kila jambo hata pale unaposhiriki na kwamba, unaposema sitaki halafu ukamfuata waziri kwa ajili ya fedha za miradi ataangalia akusaidie vipi. Amesema hapo baadaye itabidi kuangalia namna ya kufany

Madhara ya Kulala Ukiwa Umevaa Sidiria Kwa Mwanamke

0
0
Sidiria inavaliwa na mwanamke ili kusaidia kuyashikilia matiti, kuyapunguzia uzito na inasaidia kuongeza kujiamini mbele ya watu. Kwa mara moja inapovaliwa inabadili umbo na muonekano wa matiti, kama kuyainua (kubusti) ili kutengeneza muonekano ambao mwanamke mwenyewe anautaka. Katika miaka ya 1930, muonekano wa kiume kwa mwanamke ilikuwa ndio fasheni inayotamba, kwahiyo sidiria zilivaliwa ili kuficha kabisa maziwa na kuwafanya waonekane kuwa na kifua kama cha mwanaume. Kwa wanawake wenye maumbile makubwa, inawaongezea hali ya kuwa na amani zaidi. Hata hivyo, kumekuwa na mjadala mkali kuhusu madhara ya kuvaa sidiria, hasa wakati wa kulala.

Kutopumzisha matiti

Mara nyingi sidiria huwa zinawaumiza baadhi ya wanawake wanapozivaa wakiwa katika shughuli zao za kila siku, kwahiyo kulala wakiwa pia wamezivaa inaongeza maumivu haya. Wanawake wanaolalia mgongo wanaweza kupata maumivu sehemu ambayo ngozi inagusana na sehemu ya kufungia sidiria na kusababisha kero. Na waya wa upande wa chini wa sidiria unaoshikilia matiti unaweza ukawa na madhara kwa kuchimba sehemu ya chini ya tishu za matiti na kusababisha michubuko au kuvilia kwa damu. Madhara ya matatizo haya yatadumu usiku mzima na kumsababishia mvaaji kero isiyoisha.

Kutotengenezwa tishu zainazoweza kumudu kubeba uzito wa matiti

Ingawa wanawake huvaa sidiria ili kuyasaidia matiti yasizidiwe uzito, inaweza ikasababisha madhara ya kiafya kwa mwanamke. Kwa kuvaa sidiria, matiti yanakuwa hayatengenezi tishu ngumu zitakazouwezesha mwili kumudu kubeba uzito wa matiti. Kwa sababu hii, matiti yatadondoka mapema zaidi kama sidiria itakuwa inavaliwa mara kwa mara. Na kama itakuwa inavaliwa usiku na mchana, matiti hayatapata nafasi ya kutengeneza wala kutumia tishu hizi kabisa, jambo linalolikuza tatizo lenyewe.

Inasababisha Saratani ya matiti

Kitabu cha “Dressed to Kill,” kilichotolewa mwaka 1995, kinasema kwamba sidiria inaathiri uwezo wa mwili kunyonya majimaji, inaongeza joto kwenye matiti na kuathiri kiwango cha protini aina ya prolactin, inayotumika kutengeneza maziwa.

Kwa sababu hiyo, waandishi wa kitabu hicho Singer na Grismaijar wanasema kuwa hali hiyo inaongeza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti. Hata hivyo, Louise Brinton wa Taasisi ya Saratani nchini Marekani anasema kuwa hilo haliwezekani kisayansi kwakuwa haihusiani na kuathiri wingi wa homoni za endogenous, ambazo ndio zinahusiana na kutokea na kukua kwa saratani. Kwahiyo, ingawa wataalamu wanapingana kuhusu hili, watafiti wanaamini kuwa kuvaa sidiria kunaweza sababisha mwanamke kupata kansa ya matiti, na kuvaa kwa muda mrefu kunaongeza hatari hii kwa kiwango kikubwa.

Kutokwa jasho muda mrefu

Kutokwa jasho sana kwa mwanamke mara nyingine ni madhara ya kuvaa sidiria wakati wa kulala. Kitambaa cha ziada kilichetengenezewa sidiria kinazuia mzunguko wa hewa mwilini na kusababisha mwanamke atoke jasho kupita kiasi. Hii inaweza kusababisha muwasho na usumbufu kwa mvaaji. Wanawake wanaona ni lazima walale wakiwa wamevaa sidiria wahakikishe kuwa imetengenezwa kwa kitambaa kinachoiwezesha ngozi kupumua vizuri kama pamba.

Vimbe

Hizi ni vimbe zisizo na uhusiano wowote na saratani (kansa) ya matiti kwa mwanamke. Hizi ni vimbe zinazotokana na mkusanyiko wa tishu zinazoweza kutokea sehemu yoyote mwilini. Dkt. John McDougall akiandika kwenye program yake inayojulikana kama “The McDougall Program for a Healthy Heart” jinsi sidiria inavyoyazuia matiti inasababisha uvimbe kutokea na matiti kuwa na jasho muda mwingi. Hivyo, japokuwa hazina madhara yoyote kiafya, lakini vimbe zinaweza kutokea. Vimbe hizi zinaweza kusababisha ongezeko la hofu kwa mwanamke, na hofu hii ndio yenye madhara kwake.

Ukarimu Mwingine Kutoka Vodacom Unaoendelea Kuwafikia Watanzania

0
0
Ukarimu ni miongoni mwa mambo ambayo huwafanya watu kuishi kwa amani, upendo, ushirikiano na mshikamano siyo tu Tanzania bali popote katika Dunia hii.

Sio kila sehemu unaweza kuupata ukarimu lakini Vodacom Tanzania Foundation wameweza na wametusogezea Kampeni ya Ukarimu wa Vodacom kwa lengo la kuwaleta pamoja Watanzania katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan.

Kampeni ya Ukarimu wa Vodacom imendeelea kuwafikia Watanzania katika maeneo mbalimbali Tanzania ikiwa na lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku.


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ocean inayomilikiwa na Taasisi ya Marwa iliyoko Mtwara wakijiandaa kupata Futari mwishoni mwa Juma.


Watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima cha Mwinyi Baraka kilichopo Misugusugu Kibaha, Pwani, wakiwa na Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC Glori Mtui.


Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images