Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Alazimishwa Kunywa Maji ya Kisima na Wananchi

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amelazimika kula chakula na kunywa maji yaliyotoka kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu uliokataliwa na wananchi kwa hofu kuwa wakinywa maji hayo watakufa na wakipikia chakula kitabadilika rangi ya njano.

Mkuu huyo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho juzi alitaka kusikiliza kero za wananchi na kufahamu kwanini wanaendelea kutumia maji ambayo siyo safi na salama ikiwa mradi upo tangu mwaka 2014 hawajawahi kuyatumia.

Matiro aliyekuwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine na baada ya kusikiliza hoja hiyo walilazimika kuyaonja na kupika chakula kwa haraka na kubainika hayana chumvi wala chakula kilichopikwa kutokuwa cha njano ndipo ilipobainika kuwa walidanganywa kwa sababu za kisiasa.

Sababu Nyingine ya Watanzania Kufurahi Kutoka VODACOM Tanzania

$
0
0
Kwenye dunia sio kila mmoja anaweza ku-share furaha au unaweza kupata furaha kwa kukipata unachokitaka ama kupewa unachokitaka ili kukufanya uendelee kuwa na furaha na kulinda furaha yako kila mara bali furaha huandaliwa kwa misingi.

Sio kila mmoja anaweza kukufanya ukafurahi lakini VODACOM TANZANIA wameweza na kuileta karibu furaha kwa wateja wake wote Tanzania,  ni baada ya kuletewa huduma mpya ya RED ambayo unaambiwa ni mpango unaojumuisha vifurushi na kulipia kadri utumiavyo.

Naambiwa pia ukijiunga na huduma hii ambayo inapatikana kwa kununua kupitia USSD utafurahia pia huduma za SOKONI App BURE, Taarifa fupi ya M-Pesa BURE pale utakapoihitaji, Huduma ya kipekee pindi atakapowasiliana na huduma kwa wateja na Huduma ya kipekee, pindi utembeleapo maduka ya Vodacom.

Tazama hapa chini kwenye hii video!!!

Korea KASKAZINI Yaitia Jamba Jamba Marekani

$
0
0
Maafisa wa Marekani wanaamini kwamba Korea kaskazini ilitekeleza jaribio jingine la mashine ya kurushia makombora yake .

Jaribio hilo linadaiwa kutekelezwa siku ya Jumatano litakuwa jaribio la kwanza la mashine kama hiyo kutekelezwa na Korea Kaskazini tangu mwezi Machi.

Mashine hizo zinaweza kutumika katika kurusha satelaiti angani, lakini maafisa wa Marekani wana wasiwasi teknolojia hiyo inajaribiwa kutengeza kombora linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.

Mkuu wa UPELELEZI Asimulia Jinsi Alivyomkamata TUNDU Lissu

$
0
0
Mkuu  wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu (ZCO), Camilius Wambura kumtaka afanye hivyo.

Mgonja ambaye ni shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi inayomkabili Lissu, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, shahidi huyo alidai kuwa Juni 28, mwaka jana, Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika viwanja vya mahakama hiyo.

Alidai kuwa Juni 29 mwaka jana saa 7 mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo ya Tegeta wilayani Kinondoni, ambapo alimkamata na kumfikisha katika ofisi ya ZCO na kumkabidhi.

“Nilipewa amri na ZCO nikukamate hivyo kwa mamlaka hayo bila kuwa na hati ya ukamataji naweza kukukamata; kwani makosa yoyote ya jinai unaruhusiwa kukamata bila kuwa na hati hiyo,” alidai Mhonja.

Pia alidai kuwa kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya maneno aliyoyatoa, ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa kutumia lugha za kichochezi.

Katika mashitaka yake, Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi kuwa “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, ‘huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu’. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene.’’

ESCROW: Serikali yazuia mali za Seth SINGH na Rugemalira

$
0
0
Habari za kuaminika zilizotufikia ni kuwa serikali imezuia mali zote za Singh na Rugemarila . Mali zote zimewekwa chini ya ulinzi mkali na account za benki zimefungwa.

Pia imeelezwa orodha ya waliokwapua pesa za Escrow na kugawana imeongezeka wapo vigogo kutoka wizara ya fedha, taasis za dini, maaskofu, NGOs, na wataanza kuhojiwa kuanzia jumatatu ili nao wafikishwe mahakamani.

Imeelezwa kila aliyehusika atafikishwa mahakama bila kubagua wala kujali nafasi yake katika jamii.

Taarifa zaidi zinaeleza wanaotuhumiwa katika sakata hilo wanakaribia 30.

By Kiriba/JF

Ali KIBA ndo Kisha Potea Kabisa Au Tuendelee Kuvuta Subira?

$
0
0
Nahitaji jibu huyu jamaa yuko wapi siku hizi maana hasikiki kabisa au tayari kapuni na vipi zile show zake za ugaibuni kaisha maliza au ndo Sony wanampoteza hivyo, ikumbukwe baada ya Kiba Kuingia Sony watu wengi walitabiri anguko lake kutokana na historia ya wanamuziki Wengine waliojiunga na lebo hiyo kutoka Africa kuzikwa kabisa katika ramani ya Muziki...

Team Kiba njooni hapa mtujuze kunani na Kiba

SOMA Nafasi za Ajira Mbali Mbali zilizotangazwa LEO ijumaa

Hivi Ndivyo Ukarimu wa Vodacom Ulivyowafikia Watanzania Msimu wa Ramadhan

$
0
0

Vodacom Tanzania imefanikiwa kufikia Watanzania zaidi ya 20,000 katika msimu huu wa Ramadhan unaoelekea ukingoni ambapo jumla ya tende tani 4 zimegawiwa pamoja na maji chupa 25,000. Kampeni hiyo yenye lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku hadi sasa imewafikia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi Mtwara, Tanga na Zanzibar.

Ukarimu huu wa Vodacom unakwenda sambamba na kuwapatia wateja kifurushi kinachowawezesha kupata Qaswida, Mawaidha, Hadith, Facebook yenye picha na kuzungumza usiku wanaposubiri daku BURE kabisa. Huduma hii pia inawapatia muda wa maongezi, SMS na kuwawezesha kupiga simu BURE wakati wakisubiri muda wa kula daku, kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma hiyo inawakumbusha muda wa kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili kujiunga na huduma hii mteja anapiga *149*01# kisha anachagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha, kuna bando linalodumu kwa saa 24 na lingine linadumu kwa siku 7.




Shamsa Ford Aiweka Rehani Ndoa Yake!

$
0
0
STAA ‘upper class’ katika kiwanda cha filamu Bongo, Shamsa Ford ‘Chausiku’ amesema miongoni mwa mambo ambayo aliyabeba moyoni na kuyaombea dua maalum katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni pamoja na uhai wa ndoa yake, hivyo anamuachia Mungu atende sawasawa na maombi yake.

Katika mazungumzo na Star Mix msanii huyo mwenye uwezo wa ‘makinikia’ linapokuja suala la kuigiza, aliweka wazi kuwa kama mwanadamu haishiwi na mapungufu ambayo ameyatubu kwa Mungu.

“Kama binadamu siishiwi na makosa, lakini katika mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, yapo mengi ambayo niliyafanyia toba maalum, lakini kubwa sana ni uhai wa ndoa yangu, maana siko tayari kwa kweli kuvurugikiwa na kuvunjika kwa ndoa hii ambayo inamaanisha furaha ya maisha yangu, kwa hiyo naiweka ndoa yangu kwa Mungu na yote namuachia yeye,” alisema Shamsa.

Na Brighton Masalu | Ijumaa

USIBISHE.....John Pombe Magufuli ni Rais bora Afrika

$
0
0
Kwa muda mrefu haijawahi tokea katika Afrika kupatikana rais mwenye kuguswa na matatizo ya wananchi masikini kama rais wetu, John Pombe Magufuli.

Katika enzi za kupigania Uhuru Afrika palikuwa na wazalendo kama Mwl.Julius Nyerere , Patrick Lumumba, Kwame Nkuruma na wengine wengi.Wapigania Uhuru hawa walikuwa na moyo wa kizalendo wa hali ya juu katika nchi zao.

Wazalendo hawa walijitoa muhanga wa maisha yao kwa faida ya nchi zao na vizazi kwa vizazi.

Miaka ya sasa wazalendo kama hawa wako wachache sana.Libya alikuwepo Gaddafi, na Tanzania yupo rais John Pombe Magufuli.

Rais JPM amejitoa katika kuwatumikia wananchi maskini Tanzania.Hapati usingizi akiwafikiria kuwakomboa wananchi maskini.

Juhudi zake za kupinga rushwa, ufisadi na uwajibikaji wa viongozi ni kielelezo tosha rais huyu ana uzalendo uliotukuka.

Wananchi wa Tanzania wanabahati kubwa ya kumpata kiongozi huyu mwenye UCHUNGU na nchi.

Picha za JUMA Jux Zamtoa Mate Jack Wolper...

$
0
0
Muigiza wa Filamu Bongo, Jackline Wolper amedai anataka kurudi shule mara baada ya kuona picha za Jux alizopiga katika mahafali yake ya kumaliza elimu ya juu nchini China.


Wolper kupitia instagram ameandika, “nimekumbuka mbali kweli nilivyoiona hii picha, nakumbuka siku hizo mwenyewe ndo nakupeleka airport unaenda kuanza kusoma mpaka na mimi nilitamani kuwa mwanafunzi ili twende wote yaani naandika hii caption huku nasmile nikikumbuka hiyo siku ndo unaenda kusoma mwenyewe…am very happy for you mwanafunzi wangu! yani verrrrry happy…!

Ameongeza, “hongera sana siku hizi vijana wanafanya yote na shule ipooo ndo unazidi kuwa mnyamweezi, mimi mwenyewe hapa nataka nirudi shule ya kutafuta hela manake maisha magumu sana… Hongera sana kwa kuhitimu..!!nisaidieni kumtag mwanafunzi wangu,” amemaliza kwa kuandika.

JE Wajua Sababu za Rais Magufuli Kumteua Mama Salma Kikwete Kuwa Mbunge? JPM Afunguka

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameweka wazi sababu sababu ya kumchagua kuwa mbunge kwamba aliona atawawakilisha vizuri watu wa Lindi.


Rais Magufuli ameeleza sababu hizo Alhamisi hii wakati akizungumza wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.

“Nilimchangua mama Salma kikwete kwanza ana sifa nyingi, ya kwanza ni first lady mstaafu lakini pia yeye pia atawawakilisha vizuri watu wa Lindi lakini nilijua kwa upendo mkubwa alionao kwenye moyo wake ambapo alitoka kote Lindi njia zote hakuona mwanaume wakumuoa akaja hapa nikaona ana upendo mkubwa na nikaona nimpe ubunge kwahiyo ndugu zangu nina washukuru sana,”alisema Rais Magufuli.

Mrembo Jokate na Ndoto za Kupata Watoto Mapacha

$
0
0
Mjasiriamali na Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo, ameweka wazi kuwa anatamani kuwa na watoto mapacha katika maisha yake.



Jokate ameliambia Gazeti la Mtanzania kuwa mwanamume atakayekuwa mume wake atamuweka wazi hivi karibuni lakini anapenda wawe na watoto mapacha atakaowalelea kijijini.

“Kuna umri ukifika unajikuta unatamani kupata mtoto, napenda nipate watoto mapacha na wote niwalee maisha ya kijijini na mjini ili wajue maisha ya pande zote. Napenda niwalee watoto hao maisha ya kijijini ili wajifunze kilimo, kula chakula vya asili na wajifunze tabia nzuri na za kupendeza jamii,” alieleza Jokate.

Napata Wasiwasi Sana Na Uelekeo Wa "DiamondPlatnumz"

$
0
0
Naomba nikiri kwamba me ni shabiki namba moja wa Diamond,Lakini dah! kiukweli kwa ule ukimya wa mda mref kutoka kwa diamond nilitegemea akirudi safari hii hatakua level zile tulizomzoea za kufanya kolabo na wasanii wa nigeria, Nilitegemea huu upepo walionao kina Davido ama Wizkid ungemuamsha na kwenda level za mbali zaidi lakini badala yake ameniangusha na amerudi kule kule nigeria, Dah!

Yani ile juzi niliposkia Kua kesho yake diamond ataachia hit nikajua kama sio feature Alicia Keys basi itakua ni French Montana ili kuzima ule upepo wa wakina davido na wizkid maana kusema ukweli kwasasa wanigeria wanazidi kuongeza gape kati yao na sisi tofauti na kipindi cha nyuma kidogo.


anyway,yote kwa yote nimpongeze kwa hit nzuri aliyoiachia japo haijakuna mtima wangu haswa lakini nashkuru kwa Kuliamsha Dude maana na najua wasanii wengine nao watafuata kuachia hit kwakua kaka mkuu kashaliamsha DUDE.

UKWELI Unauma..Hivi Ndio Vitu Kumi Msichana Anavyoangalia Kwa Mvulana Siku ya Kwanza Mnapokutana

$
0
0

Ngoja nikwambie wasichana hukufikiriaje wakikuona siku ya kwanza.

1.Kwanza hutazama tembea yako, kisela au kiheshima ili wajue kama una kazi au la.

2.Kama nguo zako zimefubaa unatembea juani, kama hazijanyooshwa basi hata pasi kwako huna.

3.Kama viatu vina vumbi moja kwa moja gari huna.

4.Kama pesa hutoi kwenye waleti hujazoea kuwa na pesa tena yawezekana hata laki hujawahi kushika.

5.Kama hunukii vizuri basi wanawake huwajui vizuri, na hujui romance, hata hug hujawahi kupewa.

6.Kama hutunzi nywele zako hata zake hutazigharamia.

7.Ukiongea nae muda mrefu na maswali mengi, hata kama hujamtongoza, anajua umempenda.

8. Ukimshika au kumgusa popote kwenye maongezi basi unamtaka kimwili.

9.Kama mkanda wa suruali na viatu havimachi rangi, hujawa na mwanamke kwa muda mrefu.

10. Usipomtazama machoni, yawezekana muongo au hujiamini na unamuogopa.

Mkishindana na Mimi Nitawaacha - Alikiba

$
0
0
Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu anayeshindana naye na kudai ila kama kuna watu wanataka kushindana na yeye basi atawaacha na kuendelea na mambo yake.


Alikiba anasema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa katika njia yake, ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi, kwani anaamini akiwapa nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya hasa zaidi katika muziki wake.

"Unajua kila binadamu ana tabia yake, kuna wengine wanajua kabisa kwamba wanakosea lakini wanafanya hivyo kwa sababu na wapo wengine wanakuwa wanaongea pasipokujua kama wanakosea, hivyo mimi kama msanii sitakiwi kusikiliza hivyo vitu sababu nakuwa na mipango na malengo yangu, hivyo sitaki mtu yoyote aniingilie kwenye mipango yangu  kwa hiyo ukiwafuata unaweza kujiangusha" alisema Alikiba 

Mbali na hilo Alikiba amesema yeye haangalii ushindani na wala hashindani na mtu
"Mimi siangalii ushindani na wala sishindani na mtu ila kama wapo wanashindana na mimi nitawaacha washindane na mimi lakini mimi sishindani ila naangalia malengo yangu na mipango yangu katika muziki" alimalizia Alikiba 

Mbunge Bashe Amkalia Kooni JPM, Ahadi ni Deni

$
0
0

HUSSEIN Bashe, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, mkoani Tabora ameitaka Serikali kutoa kauli juu ya Sh. 200 milioni ambazo Disemba 2016, Rais John Magufuli aliahidi kuzitoa kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya maji katika jimbo hilo,

Bashe ameliambia Bunge kuwa Disemba mwaka jana, Rais Magufuli alitoa ahadi ya Sh. 400 milioni kwa ajili ya kutatua tatizo la maji, Nzega Mjini lakini mpaka sasa ametoa Sh. 200 milioni tu na kumtaka Isack Kamwelwe, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji kueleza ni lini fedha zilizobaki zitatolewa.

“Tulipokea milioni 200 tu, Mhe. Naibu Waziri unawaambia nini Wananchi wa mji wa Nzega juu ya utekelezaji wa fedha iliyobaki ambayo tumekuwa tukisubiri tangu Aprili mwaka huu?” alihoji Bashe.

Ambapo naibu waziri Kamwelwe alijibu akisema, “Ni kweli Rais alitoa ahadi ya kupeleka milioni 400 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Nzega. Milioni 200 tumeshaikabidhi Mamlaka ya Maji ya Tabora na tutapeleka fedha zilizobaki siku za hivi karibuni.

Kamwelwe alisema kupitia mradi mkubwa wa maji wa kutoka Solwa kwenda Nzega na Tabora  uliosainiwa hivi karibuni miundombinu itakarabatiwa.

Kwa upande wake John Mnyika Mbunge wa Kibamba, swali lake liliulizwa na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia ambapo lilihoji;

“Jimbo la Kibamba linapaswa kuhudumiwa kwa sehemu kubwa na maji ya kutoka mtambo wa Ruvu Juu, je ni kwanini miradi ya maji imechelewa kukamilika kinyume na ratiba inayotolewa  na Serikali?” alihoji na kujibiwa;

“Maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu ni pamoja na Mlandizi, Visiga, Picha ya Ndege, Tumbi na Pangani.
“Maeneo haya yataanza kupata maji baada ya kukamilika kwa mradi wa mfumo wa kusambaza maji ambao unaendelea kutekelezwa na kampuni ya Jain Irrigation System Ltd.”

Kauli ya Spika wa Bunge Job Ndugai Yalipasua Mbunge Vipande Viwili

$
0
0

Dodoma. Kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu mgawanyo wa bajeti katika majimbo yanayoongozwa na wapinzani imezidi ‘kulipasua’ Bunge baada ya pande mbili za kisiasa kushambuliana ndani ya chombo hicho jana.

Jumanne wiki hii, muda mfupi kabla ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali, Spika Ndugai alisema kupiga kura ya hapana katika bajeti hiyo ni kukataa fedha za maendeleo.

Wakichangia Muswada wa Sheria ya Fedha ya 2017 jana, pande mbili za wabunge, wa CCM na upinzani waliendelea kulumbana kuhusu suala hilo.

Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul ndiye aliyelianzisha kwa kusema kuwa Bunge linaongozwa na kanuni na kwamba kupiga kura jambo lolote ni hiari.

“Nyie Serikali mnaongoza na sisi ni wapinzani tunaotegemea kuingia madarakani, hatuwezi kuunga mkono bajeti yenu, hili ni wazi. Hata keshokutwa mkawa upinzani mnaweza kuwa na mawazo yenu mbadala na msiunge mkono ya kwetu,” alisema.

“Nilishangaa sana, haijawahi kutokea mwongozo mmoja mtu akiomba wanapewa wengine sita the same (sawa)... ndiyo maana ilitushangaza sana na bahati mbaya mlifanya zile siasa mkiwa mmeachia wazi televisheni.”

Alisema Watanzania waliona kuhusu ubaguzi uliofanywa wa kuwataka wanapopelekewa jambo katika vikao vyao vya chama, kujiongeza.

“Leo nchi nzima miji mikubwa tunaongoza sisi wapinzani mkiamua kwa kauli zenu za ubaguzi ndugu zetu mlioko madarakani na sisi tukaamua kukusanya kodi zetu wenyewe (katika halmashauri zinazoongozwa na upinzani) tutashindwa?”

Alisema wakiamua kukusanya kodi za majengo na mabango ambazo Serikali Kuu imekuwa ikichukua na kutorudisha katika halmashauri, wataweza kugharamia shughuli za maendeleo katika halmashauri wanazoongoza.

“Mnawaambia Watanzania kwamba mtakusanya (kodi) katika miji yetu hamtoturudishia na tukienda kwa Watanzania tukawaambia msilipe kodi je? Mlianza na waliwaona mlipowaambia wasipeleke maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani.”

Alisema kauli hiyo inaleta matatizo katika Taifa na kwamba kwa kauli hiyo, wamejichonganisha na kujichora kwa Watanzania.

“Na hii ni aibu, tunafahamu mlishaanza siku nyingi. Posho ya mfuko wa jimbo huku wapinzani mmeshaanza kutukata mmejiongezea nyinyi. Nilishaliombea mwongozo hapa. Mlishaanza iko wazi,” alisema.

Alisema wapinzani wako tayari kukusanya fedha katika majimbo yanayoongozwa na wapinzani na kutorejeshwa.

“Msifanye siasa za kitoto, Watanzania wanawaona. Mnatia uchungu tatizo hili,” alisema Gekul.

Hata hivyo, akichangia muswada huo, Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia alisema hakuna ubaguzi katika Bunge hilo na kwamba walichouliza na kukisimamia ni suala la kukaa miezi mitatu wanajadili bajeti wakitoa mapendekezo na Serikali kukubali halafu mmoja wa wabunge anasema haungi mkono.

Alisema kulikuwa na njia tatu ikiwa ni pamoja na kusema hapana, ndio na sina uamuzi ambayo inamaanisha yapo mambo mtu anayakubali na mengine hakubaliani nayo.

“Lakini hakuna mtu ambaye alisema hana uamuzi na badala yake wanakataa,” alisema na kukatishwa na mbunge aliyekuwa akiomba taarifa hatua ambayo ilimkera na kusema, “Naomba mtulie, kama sindano imeingia simtulie.” Ghasia aliendelea, “Waswahili wanasema ukilikoroga lazima ulinywe, tumeikataa bajeti kwa hiyo madhara ya kuikataa bajeti lazima yawafikie.

“Nashukuru naona sindano zangu zimeingia vizuri sana na ndiyo maana watu wote wanashindwa, wanagumia kama vile watoto wakichomwa sindano wanalia, poleni sana mwakani mjifunze jinsi ya kuunga mkono bajeti.”

Hata hivyo, kabla ya kuahirisha kikao cha asubuhi, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema kanuni ziko wazi za namna ya uendeshaji wa Bunge. “Ikiwa kiti kimefanya uamuzi, au jambo ambalo huridhiki nalo kanuni ya tano inakupa utaratibu wa kufanya.

“Si jambo zuri kabisa mtu aliyekuwa amekaa kwenye kiti unatoa maelezo kuhusu mtu huyo akiwa si yeye aliyeketi katika kiti wakati kanuni zinaelekeza nini cha kufanya.”

Alifafanua kuwa aliyekalia kiti kwa wakati husika ndiye mwenye mamlaka na kama mbunge hakubaliani na jinsi alivyotumia mamlaka, kanuni ya tano inampa utaratibu wa kufuata.

“Hoja ya kuhusu ubaguzi kama kuna mtu ana hoja hiyo achukue kanuni ya tano aisome afuate utaratibu,” alisema.

“Hatuwezi kuendelea kuijadili hoja hiyo hapa ndani kana kwamba haikuamuliwa. Kwa hiyo tusiilete kwa namna ambayo tunaenda mbele tunarudi nyuma.”

Kuhusu hoja ya kwamba kiti kilitoa nafasi ya mwongozo kurudiwa na zaidi ya mbunge mmoja, Dk Tulia alisema pande zote mbili (CCM na upinzani) walisimama wabunge wengi na kuzungumzia jambo hilohilo moja.

“Si jambo la kulaumu upande mmoja, uzuri nilikuwapo na majina ya wabunge waliozungumza ninao ni mbunge mmoja tu na huyo nitamtaja kwa sababu alifanya jambo jema alisimama na kusema jambo limeshazungumzwa,” alisema.

Kwa mujibu wa kanuni ya tano, kipengele kidogo cha nne, mbunge ambaye hakuridhika na uamuzi wa Spika anaweza kuwasilisha sababu za kutoridhika kwa Katibu wa Bunge ambaye atawasilisha malalamiko yake kwa Spika.

Kipengele kidogo cha tano kinasema Spika atawajibika kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge na kulijulisha Bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa na kamati hiyo.

Lakini kipengele kidogo cha sita kinasema Spika au Naibu Spika hatakuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge inapokaa kujadili uamuzi unaolalamikiwa, bali wajumbe watachagua mwenyekiti wa muda kwa asilimia 50 ya kura za siri.    

Nasubutu Kusema Rais JPM Yupo Sahihi Kabisa Kwa Hili la Mimba Mashuleni....Sababu Hizi Hapa

$
0
0

Rais yupo sahihi katika sense hizi

Ukiruhusu shule watoto wazae utakuwa umeruhusu indirectly
1) ngono iliyokithiri kwa watoto wadogo from primary school...

2) Umeruhusu floodgate ya mimba za utotoni huku serikali inazipinga kila siku kwamba watu hawa wanauliwa ndoto zao kwa sababu wanakuwa na majukum ya kulea hivyo wanashindwa;
i) kuendelea na shule wenyewe hata kabla hawajalazimishwa kuacha shule.
ii) ku-enjoy maisha kama watoto bali wanakuwa wazazi prematurely hivyo stress na lack of esteem and confidence mbele ya wenzao kwa sababu hili swala siyo la kawaida bali linakuja bila kupangwa kupitia ngono ambayo wawili hao ndo lilikuwa kusudi lao, siyo mtoto.
iii) una - vitiate "vita" ya women emancipation

3) Taifa lenye vijana wa kike tegemezi kutokana na kwamba mtoto kama sheria inavyomtambua mwenye umri wa miaka 17 downwards anakuwa na mtoto na hivyo anakuwa na majukumu mazito ya kizazi *(mtoto ana mtoto: can you imagine!!)*

Sheria y a Elimu, the Education Act as amended prohibits marrying a school girl or impregnating her.

So, wakipigwa mimba hawa wanakimbiwa hivyo wanakuwa tegemezi kwa wazazi wao kama wazazi na wao, siyo watoto tena. Mzazi anachokifanya ni kumfukuza nyumbani.

4) Venereal diseases: serikali inapambana na maradhi kila siku halafu mnaruhusu watoto indirectly wafanye ngono. Na kwa hiyo mtakuwa mmeruhusu
i) ngono zembe indirectly(unsafe sex) kwa sababu hana sababu nyingi ikiwemo ya shule zitakazomsukuma kuvaa kinga.

ii) Ukimwi. Hii ni kwa sababu unaruhusu ngonozembe.

Etc.

Kuhusu Ben Pol na Abitoke....Wamefunga Ndoa...Ben Pol Afunguka Kumkubalia

$
0
0

Moja ya story kubwa ambayo ilimake headlines siku kadhaa zilizopita ni kuhusu Mchekeshaji Ebitoke kuweka wazi hisia zake kuwa anampenda staa wa RnB Tanzania Ben Pol akimuomba waonane na ikiwezekana wafunge ndoa akisema anajitunza kwa ajili yake.

Sasa leo June 23, 2017 kupitia Instagram yake Ben Pol ameweka picha akiwa naEbitoke na kuweka maneno ambayo yanaelezea hisia zake pia kwa kilichofanywa na mchekeshaji huyo kwa kuheshimu hisia zake.

“Hakuna kitu kizuri kama kujishusha na kukubali kujifunza pale unapoona kuna jambo zuri la Kujifunza. Ikiwa unampenda mtu Au unatamani nafasi fulani, utajuaje kama unaweza kuipata hiyo nafasi au la Ikiwa haujaiomba kwa Mhusika?

“Naamini watu wengi sana wameoa ama kuolewa na watu wasiowapenda kwa sababu tu walipoteza nafasi za kuwaambia hisia zao wale Wawapendao, Mwishowe walipokuwa tayari kuwaambia, ikawa Too late. Ikumbukwe humu duniani sisi sote TUNAPITA, labda huyo Mtu kesho hatokuwepo.

“Ebitoke umenifundisha jambo KUBWA SANA maishani, najua wengi walikubeza sana , wengine walikuambia hautaweza hata kuonana na Mimi.. lakini huwezi amini Mimi nimefurahi mno!! kukutana na wewe na kuongea, na nimepata jambo kubwa sana. Na Nitayaishi Maneno yako... Nakushukuru sana, Mwenyezi Mungu akuzidishie. You are THE BEST !!@ebitoke #blessed” – Ben Pol.

Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images