Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

VIDEO: Kilichomtoa Machozi Q Chillah Wakati Akiwa Kwenye Interview ya XXL ya Clouds FM (Exclusive)

$
0
0
Kutoka Bongoflevani ukitaja wasanii wakongwe kwenye game sio rahisi kuliacha jina la Shaban Katwila a.k.a Q Chief au Q Chillah kama anavyojiita kwasasa, kupitia XXL ya Clouds FM June 22, 2017 alikuwa On Air kuitambulisha single aliyoshirikishwa na rapa Chid Benz alionekana akiongea kwa hisia kali hadi kutoa machozi.

AyoTV na millardayo.com zimempata Q Chillah Exclusive na ameeleza sababu za yeye kulia wakati akiwa kwenye interview live. Chillah amesema
 “Niliguswa na hali ya Chid Benz, na najua nimepitia hali nyingi sana kwenye maisha ambazo Chid amepita”

“Lakini kikubwa kilichoniliza nimewahi kuwapoteza marafiki wakubwa sana ambao niliwapenda, wasanii wakubwa, majina makubwa Tanzania mtu kama Albert Mangweha “Ngawair” Mwanahiphop ambaye mimi sijawahi kumuona zaidi yake”<<<  – Q Chillah

Kufahamu zaidi alichokingea Chillah bonyeza play kwenye video hapa chini kutazama.

Wanawake ACT Wazalendo wapingana na Rais

$
0
0

Ngome ya Wanawake ya Chama Cha ACT Wazalendo imempinga Rais Magufuli juu ya kauli yake ya dhidi ya watoto wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni kuwa hawapaswi kuendelea na shule, Wanawake wa ACT Wazalendo wanasema kitendo hicho ni kinyume na Katiba

Rais Magufuli wakati akihutubia mkoani Pwani tarehe 22/06/2017 alipiga marufuku wanafunzi wajawazito kuendelea na masomo na kusema kuwa katika serikali yake hawezi kusomesha wazazi hivyo ukijiona umepata mimba ukiwa shule ya msingi au sekondari basi usahau kuendelea na shule.

"Ngome ya Wanawake ya ACT Wazalendo inaiona marufuku hiyo kama hatua kali inayomkandamiza na kumbagua mtoto wa kike kwa kumnyima haki yake ya msingi ya kupata elimu. Marufuku hii ni kinyume cha matakwa ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 11(2) inayosema: "Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake". Alisema Esther Kyamba, Katibu, Ngome ya Wanawake

Wanawake wa ACT Wazalendo wanasema kuwa watoto wengi wa vijijini ndiyo wamekuwa wahanga wakubwa wa matatizo ya kupata ujauzito wakiwa mashuleni kutokana na mazingira na miundombinu mibovu inayokuwa ni chanzo cha watoto hao kupata ujauzito.

"Watoto wengi wa kike hasa waishio maeneo ya vijijini ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa matatizo ya kupata ujauzito wakiwa shuleni kutokana na miundombinu isiyo rafiki ya elimu kama vile ukosefu wa mabweni, kusafiri mwendo mrefu kwenda na kurudi shuleni, kusaidia shughuli za nyumbani na shughuli za kuziingizia kipato familia zao ambapo kote huko hukabiliana na changamoto kadhaa wa kadha zinazoweza kuwasababishia ujauzito. Ngome inaamini ni wajibu wa Serikali iliyopo madarakani kuhakikisha inatengeneza mazingira rafiki na salama kwa mtoto wa kike ili nae aweze kupata haki yake ya msingi ya elimu kama ilivyo kwa watoto wengine na sio kumbagua, kumkandamiza na kumnyima haki yake ya elimu" alisema Esther Kyamba

Mjadala wa wanafunzi kupata mimba wakiwa shule wakolea

$
0
0

Kauli ya Rais John Magufuli kuwa hakuna mwanafunzi atakayeendelea na shule baada ya kujifungua, imepokewa kwa hisia tofauti.

Wanaharakati, wadau wa elimu na wabunge wanaipinga kauli ya Rais huku ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ikitofautiana na msimamo wa kiongozi huyo wa nchi.

Wapo wanaotaka wanaopata mimba shuleni wapewe fursa ya kuendelea na elimu na wengine wamempongeza Rais wakisema kuzuia kuendelea na masomo katika shule za Serikali kutapunguza mimba za utotoni.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizindua Barabara ya Bagamoyo – Msata mkoani Pwani na kusisitiza kwamba katika utawala wake, hakuna mwanafunzi yeyote mwenye mtoto atakayeruhusiwa kurudi shuleni kwa sababu Serikali inatoa elimu bure kwa watoto na si wazazi.

Kutokana na maudhui ya shughuli ya uzinduzi wa barabara, haikutegemewa kama Rais Magufuli angetoa msimamo huo mkali, hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inatafuta mbinu za kusaidia wasichana wanaopata mimba shuleni kutokana na baadhi yao kupata ujauzito kwa kubakwa, mazingira magumu ya shule, hasa vijijini na wengi wao kutokana na umaskini.

Rais alitoa kauli hiyo wakati akizungumzia wafungwa wanaoishi kwa starehe gerezani, akiagiza wafanye kazi ya kulima, kama hao wanaowapa mimba wanafunzi na kutakiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

Hata hivyo, Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, inaitaka Serikali kuweka mazingira ya kuwezesha wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo.

“Wasichana wote wa elimu msingi, wanaoacha shule kwa sababu ya kupata ujauzito, wataendelea na masomo,” inasema ilani hiyo.

Lakini Rais alisema wanaotaka wasichana hao waendelee na masomo waanzishe shule zao za wazazi.

Akizungumzia kauli hiyo, mtaalamu wa saikolojia kutoka Kituo cha Afya ya Akili cha Mehota, Dk Bonaventura Bagile alisema mwanafunzi aliyewahi kubeba mimba anaporudi shule anajenga picha mbaya kwa wanafunzi wenzake.

Alisema wanafunzi wanafundishwa kutofanya mambo fulani wakiwa shuleni, lakini wakiona mwenzao kafanya mambo hayo na bado amerudi shule, hawatakuwa na nidhamu kwa sheria na kanuni zinazowaongoza.

“Mwanafunzi mzazi akiruhusiwa kurudi shule, itajenga image (taswira) mbaya kwa wenzake kwamba you can do something bad and there are no consequences (unaweza kufanya jambo baya na usipate matokeo yoyote),” alisema mtaalamu huyo.

Dk Bagile aliunga mkono kauli ya Rais Magufuli akisema mtu anapofanya jambo baya, lazima ajue kwamba kuna matokeo fulani atakabiliana nayo na mengine yanaweza kumgharimu maisha yake.

Kauli hiyo iliungwa mkono na katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Kigoma, Jackson Gaima ambaye alisema mtoto akipata mimba wakati akiwa shuleni anakuwa amevunja kanuni na maadili ambayo hayaruhusu wanafunzi kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi.

“Kuna kesi za ubakaji kweli, lakini suala hilo lisiwe ndiyo ajenda ya kuhalalisha wanafunzi kubeba mimba na kurudi shule,” alisema Gaima.

“Serikali iweke utaratibu maalumu wa kushughulikia masuala ya ubakaji na kuwaangalia kipekee watoto wanaopata mimba kwa kubakwa.”

Hata hivyo, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya HakiElimu, John Kallaghe alisema wameipokea kauli ya Rais Magufuli na kwamba watatafuta nafasi ya kuzungumza naye ili wamueleze ni kwa nini wanapigania watoto kurudi shule baada ya kujifungua.

Kallaghe alisema ripoti mbalimbali za utafiti zinaonyesha kwamba zaidi ya watoto 70,000 wanashindwa kuendelea na masomo kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo mimba za utotoni, jambo linaloonyesha kwamba kuna tatizo.

“Tunaamini kwamba kupata mimba si mwisho wa mtoto kuendelea na masomo. Leo (jana) wadau wa elimu tutakutana kwa ajili ya kujadili suala hilo. Ninaamini tutatoka na kauli moja,” alisema mkurugenzi huyo wa taasisi ambayo imekuwa ikipigania wanafunzi waliojifungua waruhusiwe kuendelea na masomo.

Wabunge Ukawa waja juu

Mjadala wa msimamo huo wa Rais pia ulitawala kwa wabunge huku wale wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakipinga kwa maelezo kwamba kuruhusu hali hiyo ni kukiuka mikataba ya kimataifa na Katiba.

Waziri Kivuli wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Suzan Lyimo alisema jana kuwa watoto wote wana haki sawa ya kupata elimu kikatiba.

“Mimi kama mzazi nilisikitishwa sana na kauli ile. Muda mrefu sana tumekuwa tukitetea elimu ya watoto wetu. Taasisi mbalimbali zimezungumza kuhusu jambo hili,” alisema.

Alisema pia ipo nyaraka ya Serikali ya jinsi gani watoto wanaopata mimba wanavyoweza kurudi shuleni na kwamba Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya akijibu swali katika vikao vya Bunge vya Februari aliwaambia kuwa mwongozo wa jambo hilo unaandaliwa.

Alisema suala hilo lilirejea katika Bunge la Bajeti wakati Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambayo yeye ni mjumbe, ilipolizungumza katika maoni yake.

Alisema Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kufanya jambo hilo akisema hata Zambia na Kenya zinafanya utaratibu huo.

“Sisi kama nchi tumesaini mikataba mbalimbali ya haki za mtoto, vilevile tuna Sheria ya Mtoto na tumesaini mikataba mbalimbali,” alisema.

Alisema jambo alilolifanya Rais Magufuli linakwenda kinyume na maazimio waliyoyasaini.

Mbunge wa viti maalumu (Chadema), Upendo Peneza alisema mara kadhaa amekuwa akizungumzia umuhimu wa kuwapo kwa elimu ya uzazi shuleni ili kuwezesha watoto wa kike kutambua miili yao na wakati gani kushiriki vitendo vya ngono.

“Watu wengi elimu hii wanaichukulia kuwa inaweza kuwa kichocheo cha kufanya haya mambo, lakini si kweli,” alisema Upendo.

Alisema kuwa Rais alisema kuwa watoto wanaopata mimba waende Veta lakini katika vyuo hivyo vya ufundi hawachukui mtoto ambaye hajamaliza kidato cha nne.

“Kwa lugha nyingine unawaambia wasipate elimu ya shule ya msingi, sekondari wala Veta,” alisema.

Mbunge wa Buyungu (Chadema), Kasuku Bilago alisema hivi sasa hali ni ngumu na inawalazimu watoto kusafiri umbali mrefu kwenda shule na wakiwa njiani wanakumbana na vishawishi.

Alisema waliwahi kwenda Zambia na kujionea jinsi utaratibu wa watoto wanaopata mimba kurejea shuleni unavyotekelezwa.

Alisema utaratibu huo umefanikiwa na umepunguza mimba kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wanaporudi shule kuona aibu na kuwafanya wenzao kujichunga.

Wasemavyo wengine mitandaoni

Baadhi ya wanasiasa na watu maarufu pia wametoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii huku wakionyesha tofauti zao za misimamo kuhusu kauli ya Rais Magufuli ambayo imekuwa gumzo nchini.

Katika akaunti yake ya Twitter, mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe ameandika: “Ni marufuku mtu yeyote au mamlaka yeyote kubagua mtu mwingine chini ya sheria yeyote au katika utendaji wowote wa dola – Katiba JMT 13(4)(5).”

Aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimri), Dk Mwele Malecela ameandika pia ameandika: “Mama Kamm ni mwanamke jasiri aliyetafuta njia za kuhakikisha watoto wa kike wanasoma baada ya kupata ujauzito na Baba wa Taifa alijua hilo.”

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameandika: “Anayeamini kila mtoto aliyepata mimba amefanya uhuni anatakiwa kunyimwa fursa!! Ni janga kubwa sana!”

Mkurugenzi wa taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi ameandika:“Naamini elimu ya afya ya uzazi kwa wasichana ni suluhu ya muda mrefu. Ila wale wanaojikwaa pia ni muhimu tuweke mifumo ya kuwapokea.”

Wakuu wa mikoa 11 watoa tamko hili kwa JPM

$
0
0

Singida. Wakuu wa mikoa 11 wamempongeza Rais John Magufuli kwa kazi kubwa, nzuri na ya kizalendo anayoendelea kuifanya ya kutetea na kulinda rasilimali za nchi kwa masilahi ya Watanzania.

Wakuu hao ni kutoka mikoa ya  Singida, Rukwa, Katavi, Kagera, Tabora,Dodoma, Manyara, Geita, Shinyanga, Mwanza na Kigoma.

Wametoa tamko hilo   jana Ijumaa ( Juni 23) kwenye mkutano wa kawaida wa ujirani mwema katika mikoa hiyo ambao  ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.

Mwenyekiti wa mkutano huo, alikuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry.

“Sisi wasaidizi wake (Rais Magufuli) tutaendelea kutekeleza na kuzingatia maelekezo katika utendaji wetu wa kila siku.

Aidha, wakati wote tutakuwa pamoja na wananchi na kuwatumikia kwa kutimiza wajibu wetu kwa uaminifu, uadilifu na tutahakikisha masilahi ya wananchi na Taifa yanapewa kipaumbele cha kwanza,” limesema tamko hilo.

Pia, wakuu hao wa mikoa wametoa wito kwa wananchi na wawekezaji halali wa ndani na nje ya nchi, wamuunge mkono Rais Magufuli kwa kufanya kazi na wakati wote wazingatie sheria za nchi.

“Tutumie fursa nyingi zinazoendelea kutengenezwa kwa hatua hizo za kizalendo anazochukua mheshimiwa wetu Rais Magufuli.  Kwa mafanikio, maendeleo na tija kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati na uchumi wa viwanda,” limeongeza tamko hilo.

Mkutano huo wa aina yake kufanyika mjini hapa umesisitiza kwamba kuna haja ya kumtia moyo Rais Magufuli ili aendelee na ujasiri wake huo wa kulinda rasilimali za nchi.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa mkutano huo, Mwanry amesema pamoja na mambo mengine wametumia fursa hiyo kubadilishana uzoefu na wamekubaliana kupeana taarifa mbalimbali za kimaendeleo.

 “Tumekutana hapa kwa mapenzi ya nchi yetu na ya Rais wetu Magufuli. Tuliokutana leo hii, changamoto za mikoa yetu zinafanana. Changamoto hizi ni pamoja na uharibifu wa mazingira, uhaba wa mvua, kilimo cha kuhama hama na uhamiaji haramu,” amesema Mwanry na kuongeza;

“Kwa hiyo tukiacha kila mkoa utatue changamoto hizi kivyake, hatutafanikiwa kizitatua.Tumekubaliana kukutana mara kwa mara ili changamoto zinazotukabili sote tuzipatie ufumbuzi wa kudumu kwa pamoja.”

KIMENUKA..Shirika la Wanawake Barani Afrika Limemtaka Rais Magufuli Kuomba Msamaha

$
0
0

Matamshi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo yamezua gumzo kubwa na mijadala mbalimbali ndani na nje ya nchi.


Shirika la wanawake barani Afrika limemtaka Rais Magufuli kuomba msamaha kutokana na matamshi yake aliyoyatoa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Pwani kuwa mwanafunzi atakayepata ujauzito katika utawala wake hataweza kuendelea na masomo.


Hata hivyo, katika sheria iliyopitishwa mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu suala la mtoto wa kike kupata ujauzito akiwa shule inaruhusu kufukuzwa shule na kifungo cha miaka 30 kwa yule aliyesababisha ujauzito huo.

Diamond Platnumz na Penzi la Wema Sepetu...Amuandikia Nyimbo......

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema si kweli wimbo wake mpya ‘I Miss You’ aliuandika maalumu kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu.

Akizungumza na kipindi cha The Playlist cha Times FM, Diamond ameeleza yeye kuandika nyimbo kutokana na hisia alizonazo kwa wakati huo na huangali soko lipo vipi.

“Hapana, sio kweli kwa sababu Wema hana mtoto, hana familia is just to me, unajua Mwenyenzi Mungu amenibariki sana kuandika nyimbo za feeling, unajua tunatafuta market na ili tukue kimuziki ni lazima na muziki mwingine tufanye ili tusi-disappoint wa nyumbani ni lazima uwape chao na kule (kimataifa) ufanye,” amesema Diamond na kuongeza.

“Huwezi kuamini ilikuja tu, nikiandika nyimbo za mahusiano kama hizi sometime chozi linanitoka, nakumbuka mara ya kwanza huu wimbo nimeuandika nipo kwenye ndege sijui nilikuwa naenda wapi, nikawa napata feeling nikiandika topic hii itakuwa vizuri na Mungu kanijalia naweza kubadilika katika muziki wa tofauti tofauti,”

Rayvanny Aibuka Shujaa Kwenye Tuzo za BET...Aweka Rekodi Tanzania

$
0
0
Hatimaye kwa mara ya kwanza Tanzania imefanikiwa kunyakua tuzo ya BET.
 
Tuzo hizo ambazo zimegaiwa usiku huu mjini Los Angeles, katika ukumbi wa Microsoft Theater Centre, Rayvanny ambaye alikuwa akiwania tuzo hizo kupitia kipengele cha Viewer’s Choice Best New International Act amefanikiwa kuibuka kidedea.

Wasanii wengine ambao alikuwa akishindana nao katika kipengele hicho ni Dave (Uingereza), Amanda Black (Afrika Kusini), Changmo (Korea Kusini), Daniel Caesar, Remi na Skip Marley (Jamica).


Baada ya kushinda tuzo hiyo, Ray kupitia mtandao wake wa Instagram ameshukuru kwa kuandika, “God is good all the time.Asante Mungu wangu Ulieniumba,Unaejua mwanzo na mwisho wangu.Uliyaona machozi yangu nilipokua mpweke sina furaha na mwenye majonzi mengi.WEWE NDIYE MUWEZA…”

“Asanteni wadau Wote mlio VOTE kwa Ajili yangu Ushindi umerudi Nyumbani.SITOACHA KUSHUKURU UONGOZI MZIMA #WCB @babutale @sallam_sk @Diamondplatnumz @mkubwafellatmk @kameboy_j @ricardomomo thanks Alot @bet_intl @betawards @bet_africa #WCBFORLIFE MAMA I LOVE YOU,” ameongeza

Hali ya Mwigizaji Wastara ni Tete...Apoteza Fahamu

$
0
0
Hali ya kiafya ya muigiza wa Filamu Bongo, Wastara si nzuri kwa sasa ambapo inaelezwa kuwa jana usiku alipoteza fahamu.



Tatizo hilo limemkumba Wastara akiwa nchimi alipokwenda kufanya kazi zake. Taarifa zilitolewa na uongozi wake kupitia ukurasa wa Instagram anaoumiliki yeye mwenyewe umesema hadi sasa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania kumuombea ili kupona haraka.

Habari za Asubuhi Wapendwa Naomba Tumuweke kwenye Sala Zetu Dada Yetu mpendwa Wastara, kutokana na hali yake Anasumbuliwa na maumivu ya mgongo ambayo yanampelekeaga kupoteza Fahamu, Jana usiku yamemkuta matatizo hayo akiwa nchini Kenya ambako yupo kikazi.Amelazwa huko na hali yake bado siyo nzuri . Tunaomba Dua zenu wapendwa iliarudi kwenye hali yake ya kawaida.
#Imetolewanauongozi

Je Una Tatizo la Nguvu za Kiume, Kukosa Hamu ya Tendo na Maumbele Madogo..Soma Hapa

$
0
0
JE, UNA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO NA MAUMBILE MADOGO? SOMA HAPA 👇👇👇👇

Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, sio Tanzania tu bali duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo sio ugonjwa ila ni dalili ya ugonjwa. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili. UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME HUSABABISHA MAMBO KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa ☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni ☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa. @Markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye kisukari kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @220000@220,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6.5 @130000@130,000/=
3.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @130000@130,000/= KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WA @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr.

Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa no 
(+255)0767447444 na 0714335378 

NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na hazina kemikali wala madhara kwa mtumiaji.

< WELCOME ALL>

MCHEZAJI wa Tottenham Victor Wanyama Akutana na Msanii wa Bongo Fleva Anayemkubali

$
0
0
Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya nchini Uingereza na timu ya Taifa ya Kenya, Victor Wanyama ambaye yupo nchini kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza August 12 ambapo timu yake ya Tottenham ikiwa ugenini kuvaana na Newcastle.

Mara kadhaa katika mahojiano yake na baadhi ya vyombo vya habari nchini, Wanyama amesikika akisema anamkubali mkali wa nyimbo ya O’rugambo ya Saida Kaloli na anapenda sana kufuatilia baadhi ya vibao vya msanii huyo hasa nyimbo hii anayo tamba nayo kwa sasa.

Katika hali isiyo kuwa ya kawaida hatimaye mchezaji huyo kutoka Afrika Mashariki anaecheza ligi kuu nchini Uingereza amekutana na msanii Saida Kaloli na kukabidhiwa CD yenye kibao cha wimbo huo.

Wakati akiwa katika kipini cha Sports Extra kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds FM, Wanyama aliutaja wimbo huo .

“Nafuatilia sana Bongo Flava na wasanii wote wanafanya vizuri kwasasa na nimependa wimbo huu mpya wa ‘O’rugambo’ wa Saida Kaloli.”

KAMANDA Sirro Aibukia Moshi Mauaji ya Kibiti

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema mauaji ya polisi, viongozi na raia katika maeneo ya Kibiti, Rufiji na Ikwiriri ni ya muda na kusisitiza majibu yake yako mbioni kupatikana.

Sirro ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi) katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), wakati wa kufunga mafunzo ya upandishaji vyeo kwa maofisa na askari 222 wa Jeshi la Uhamiaji nchini.

Kauli ya Sirro imekuja huku kukiwa na mfululizo wa mauaji ya polisi na raia katika maeneo hayo ambapo zaidi ya watu 35 wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakiwamo polisi 13.

Hadi sasa, licha ya polisi kufanya operesheni kubwa katika maeneo hayo, bado halijaweza kubaini chanzo cha mauaji hayo na kwa nini wanawalenga polisi na baadhi ya watu na nani wanayatekeleza.

Tukio la hivi karibuni kabisa lililotokea Jumatano iliyopita, ambapo watu wasiojulikana waliwashambulia kwa risasi na kuwaua polisi wawili wa kikosi cha usalama barabarani huko Kibiti.

Akizungumza katika sherehe za kuhitimu mafunzo kwa maofisa na askari hao 222 wa Jeshi la Uhamiaji, Sirro amesema japokuwa nchi ni salama, lakini inakabiliwa na kitisho cha usalama eneo hilo.

“Tuna shida Kibiti Ikwiriri lakini wanasema sisi ni wengi wao ni wachache. Tusikubali hata siku moja makabila yetu, madhehebu yetu, majimbo yetu yatugawanyishe,” amesema Sirro na kuongeza;-.

“Umoja wetu ndio nguvu yetu. Suala la Kibiti ni la muda mfupi. Tunakwenda na tutapata majibu. Hatutakubali kikundi cha watu wachache wafanye Kibiti, Ikwiriri, Rufiji yasikalike,”.

Akizungumzia changamoto zinazolikabili Jeshi la Uhamiaji, Sirro aliyekuwa mgeni rasmi amesema moja ya changamoto kubwa ni uingiaji wa wahamiaji haramu wanaopitia njia zisizo rasmi kuingia nchini.

“Hili litawezekana kwa kuimarisha intelijensia. Mnapopanda vyeo sio mfurahie tu kupanda cheo mjue majukumu yanaongezeka pia. Idadi ya mnaoenda kuwaongoza sasa itaongezeka,”amesema Sirro.

“Kazi yenu Uhamiaji na sisi polisi hazitofautiani sana na mara nyingi tumekuwa tukifanya kazi za operesheni pamoja. Changamoto tunayokutana nayo ni usimamizi wa kazi”alisisitiza na kuongeza;-

“Askari anakosea huchukui hatua. Konstebo anafikia mahali anamtuma Koplo amletee soda na anakimbia anakwenda kumletea soda. Mnaona ni sawa hii?”alihoji na kujibiwa “Hapana”.

“Heshima yetu sisi askari ni kutokuwa waoga na unakuwa sio muoga kwa sababu kazi unaifahamu, unakuwa sio muoga kwa sababu unatii sheria na unasimamia sheria na hubabaiki,”amesema.

“Ninawaelekeza suala la uoga, suala la ulegelege katika awamu hii tusiipe nafasi,”ameongeza kusema na kusisitiza maofisa hao kufanya kazi kwa weledi pasipo kuwasumbua au kuwazungusha wananchi.

Kamishina Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Dk Anna Makakala, amesema mafunzo hayo ni ya kwanza katika historia ya jeshi lake baada ya Jeshi hilo kufanya maboresho ya kimuundo na sheria.

“Jeshi la Uhamiaji limefanya maboresho yakiwamo ya kimuundo na sheria ili kuliingiza Jeshi la Uhamiaji katika tume ya polisi na Magereza. Hatua hii imechangia kuwepo kwa mabadiliko,”amesema.

“Uhamiaji lina askari na watumishi wasiozidi 3,000, hawatoshi kutokana na ongezeko la majukumu ya uhamiaji. Ili kufanya kazi kwa ufanisi linalihitaji kuwa na askari wasiopungua 10,000,”amesisitiza.

Kamishina Jenerali hiyo amesema Taifa kwa sasa linakabiliwa na changamoto ya wahamiaji haramu wanaoingia kupitia njia zisizo rasmi, lakini akasema wanapata ushirikiano mkubwa toka polisi.


USOME Ujumbe Uliotumwa na Wauaji wa KIBITI Wakieleza Sababu za Mauaji

$
0
0
Siku mbili tangu kuuawa kwa polisi wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambao walikuwa kazini katika kijiji cha Bungu B, hali ya wasiwasi imezidi baada ya wauaji hao kusambaza ujumbe unaoeleza kuwa wanaendelea kusaka askari kwa kuwa ni wadhulumaji.

Watu hao wametuma ujumbe mfupi ulioandika kwenye karatasi na kisha kuutuma katika mitandao ya kijamii, ukidai kuwa waliouawa (japo hawajatajwa majina yao) wanadhulumu watu kwa kutumia kazi yao.

“Tunawatangazia wananchi tumewaua hawa kwa sababu wanadhulumu watu kwa kutumia kazi zao na yeyote atakayefanya kazi hapa au nje ya hapa tutamtafuta hadi nyumbani kwake.”

Sisi tumejitolea kufa kuliko kuishi, kwa hiyo dereva au raia popote uwaonapo toa taarifa iwe nyumbani au kazini”, unasema ujumbe huo.

“Hakuna njia ya kumaliza dhuluma isipokuwa chuma tu, hapa chuma tuuu!”

Ujumbe huo ambao umeandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu ya rangi ya bluu unadaiwa kuwa unazungumzia vifo vya askari polisi wawili wa kituo cha polisi Kibiti, Sajent Salum na PC Masola waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa kazini.

Mmoja wa madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Kibiti) jina tunalo) alisema ujumbe huo unawalenga askari wa kawaida na wa kikosi cha usalama barabarani.

Diwani huyo alisema kundi hilo linalofanya mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji bado lina nguvu.

“Linaonyesha bado lina uwezo mkubwa wa kufanya mauaji na kutokomea kusikojulikana”, alisema

Alisema kwa sasa Serikali inapaswa kuongeza nguvu zaidi ya wapelelezi ili kukomesha kikundi hicho ambacho hakijulikani kinafanya hivyo kwa sababu zipi na wala kinakojificha.

Akizungumza ujumbe huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga alisema jeshi la polisi litaendelea kuwasaka.

“Tutapambana nao tu”, alisema Kamanda Lyanga na kukata simu.

Chanzo: Mwananchi

Mwanamke Ni Kiumbe Katili Sana Kuliko Unavyodhani ! Check Out Hapa

$
0
0

Mara nyingi sana watu wamekuwa wakiwasifu wanawake kwamba ni watu wapole lakini ukweli haupo hivyo.

Mwanamke ni mtu wa maamuzi ya haraka na pengine anapotaka kufanya jambo huwa hafikiri madhara yake huwa anakuja kutafakari wakati nambo yamesha haribika.

Mwanamke akiwa na hasira anakutoa roho muda wowote na anabadilika tabia muda wowote. Ukitaka kuamini embu siku moja muulize mkeo kwamba hivi nikizaa nje mtoto upo tayari kuishi naye halafu usikie majibu atakayokupa. Niliwahi kumueleza mke wangu nataka kuoa mke wa pili jibu alilonipa kwamba nisimtafutie mada kesi tafadhari , jibu ambalo mpaka leo huwa najiuliza alikusudia nini.

Mwanamke si mtu wa kumsaidia kwa sababu hawana shukrani na wepesi mno kusahau fadhira walizo tendewa. Unaweza kuwa na mke ukampa kila kitu lakini siku moja akimpata wa nje utapata tabu.

Wanawake ni wepesi sana kudanganyika hata asome vipi ni wachache mno unao weza kuwakuta na misimamo imara.

Au siku moja partner wako akiwa na mimba jaribu kumwambia mimba hii nina mashaka si yangu halafu uone response ya kikatili utakakuta katoto kenyewe kametupwa jalalani huko .

By Stan

JE unakubaliana na Wazo la huyu Mdau?

EAST AFRICA TV & RADIO Walivyotilia Shaka Uwepo wa Rayvanny Tuzo za BET....Aibu Kwao

$
0
0

Hatimaye......Rayvanny Winning BET AWARDS 2017
.
.

Ila tujikumbushe kidogo....mnamo tarehe 9 June👇 .
EAST AFRICA TV & RADIO watilia shaka uwepo wa @Rayvanny kwenye Tuzo za BET .
.

SHAKA LA KWANZA....ni msanii huyo kutowekwa katika website yao ambapo wasanii wote ambao wapo nominated wamewekwa katika website hiyo
.
.

SHAKA LA PILI....ni page ya BET iliyompost Rayvanny kumuombea kura kwamba ina followers wachache na haipo verified.
.
Je kwa hili la Rayvan Je Aibu yao au Aibu ya nani??? .

Kutana na Maalim Fadhil Rashid Kutoka Komoro ni Mtaalam wa Tiba za Asili Anayetibu Magonjwa Yafuatayo

$
0
0
KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM

KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO

DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239

WhatsApp IMO +255785786436

MTOTO Atunukiwa Zawadi ya Kusafiri Kwa Ndege Maisha yake yote

$
0
0
 Shirika la ndege la binafsi nchini India limemtunuku safari za bure mtoto aliyezaliwa ndani ya ndege moja ya shirika hilo iliyokuwa safarini kutoka Saudi Arabia kuelekea India.

Mhudumu mmoja wa ndege, ambaye alikuwa amepata mafunzo ya uuguzi alimsaidia mama kujifungua mtoto wakati ndege hiyo ikiwa umbali wa futi 35,000 angani.

 Kutokana na tukio hilo, shirika hilo lilimpa zawadi ya kudumu maishani, ambayo itakuwa ni kusafiri bure kwa ndege ya shirika hilo katika maisha yake yote.

Mama na mtoto wake walipelekwa hospitalini baada ya ndege hiyo aina ya Boeng 737 kutua katika mji wa magharibi ya Mumbai.

Shirika hilo liliiambia BBC kuwa mama na mtoto wake walikuwa katika afya nzuri.

Kampuni iliwashukuru wahudumu kwa kumsadia mama kujifungua salama.

Shirika hilo lilisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza mtoto kuzaliwa kwenye ndege zake.

Tukio kama hilo lilitokea nchini Uturuki ambapo mtoto wa kike alizaliwa katika ndege ya Shirika la Turkey Airline, Aprili mwaka huu.

DIAMOND Atoa Siri ya Mtoto Wake Aliyoko Mwanza......

$
0
0
Mkali wa muziki wa Bongo fleva nchini, Diamond Platnumz, hatimaye ametoboa siri ya maisha yake baada ya kueleza kwamba ana mtoto wa miaka saba aliyezaa na mwanamke anayeishi jijini Mwanza ambaye alikuwa naye kwa usiku mmoja tu.



Akizungumza na redio moja, Diamond alisema kuwa mtoto huyo alimpata baada ya kwenda mkoani humo kufanya shoo ya muziki.

Alisema kuwa awali alikuwa akiwasiliana na mwanamke huyo, kabla ya kupoteza mawasiliano baada ya kumpata mpenzi mwingine ambaye alimlewesha kimahaba.

“Nina mtoto jijini Mwanza, sijui kama yupo kwani sijamuona tangu azaliwe kutokana na mama yake kushindwa kunitumia picha. Nakumbuka siku moja nilipokwenda huko nilikutana na mama yake, akaniambia kuwa amezaa mtoto lakini kila ninapomwambia anitumie picha hataki,” alisema Diamond.

“Siku moja nilimuuliza kama kajifungua lakini akakataa, baadae nikaja kuambiwa ana mtoto lakini kila nilipomuomba nimuone alikataa.”

Diamond hakuwahi kumtaja mwanadada huyo mwenye mtoto wake.

TID afunguka baada ya Quick Rocka na OMG kutumia Chorus yake bila ruhusa

$
0
0
Leo June 24, 2017 upepo wa Bongofleva huenda ukaenda sivyo kwenye studio za Switch Records ikiwa ni mastaa tu tangu Quick Rocka na kundi la OMG waachie video yao mpya “Watasema” ambayo wametumia melody na maneno ya wimbo wa zamani uliofanywa na TID “Watasema Sana” na inaonekana TID hajashirikishwa na kuamua kudai haki zake.

TID ameandika  “Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema

Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 in Kenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo – TID

HII Hapa Historia Fupi ya Freemasons Itakayokuacha Mdomo Wazi

$
0
0
Ni shirika ambalo mambo yake ni siri kuu. Mimi nilifanya utafiki kwenye mitandao, nikafatilia historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa mara kwenye makala za historia katika televisheni za magharibi pamoja na kuongea na watu waliofuatilia kwa karibu mambo yao.
Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.

Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.
1. Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).

Niliambiwa walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs).

Niliambiwa wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.

2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k

3. Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.

4. Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani. Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki.

Ndio maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama Jesuits.

Jesuit Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye elimu ya juu zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti ndani ya kanisa katoliki.

5. Kuhusu imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini Yesu na Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mabaya. alimfanyia hila Lucifer aonekane mbaya.

6. Kinachoendelea ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna daraja ambazo muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea katika imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya juu kabisa ni nyuzi ya 33 (33rd degree)

7. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi.

Wafuasi wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini manake hata wao hawaambiwi kitu. Kwa wafuasi wa daraja ya chini wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa wasio jua kitu kule kwenye lodge zao ni kama ywca au wmca au club hivi. Kwenye nchi kama marekani watu wasio jua siri wanachukulia kama sehemu za kusocialize tu.

8. Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri, yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya utawala.

VIDEO: Emanuel Okwi alivyopokelewa na Makamu wa Rais wa Simba

$
0
0
Usiku wa June 24 2017 mshambuliaji wa zamani wa Simba Emanuel Okwi aliwasili kimya kimya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage nyerere Dar es Salaam ili kujiunga na wekundu wa Msimbazi Simba, Okwi alipokelewa na makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange Kaburu na kutotaka kuongea chochote na waandishi wa habari.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images