Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104414 articles
Browse latest View live

EMMANUEL Mbasha Amkana ‘Mchumba’ke’

0
0
BAADA ya kudaiwa kumvisha pete ya uchumba mshiriki wa Miss Tanzania 2008, Jacqueline Chuwa ‘Jack’, Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha amemkana akidai hamfahamu mlimbwende huyo.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Mbasha alisema hamfahamu msichana huyo na kwamba hana mchumba wala rafiki wa kike kwa sasa, akisema picha ambayo alipiga akiwa dukani na shela, ilikuwa ni kwa ajili ya kuomba miujiza kutoka kwa Mungu ili apate mke mwema.


“Sina mchumba wala mpenzi na picha niliyoweka kwenye ukurasa wangu wa Instagram niliamua kupiga nikiwa nimeshika tu shela ili Mungu afanye jambo kwangu, nikipata mchumba nitawaambia mashabiki wangu wala wasijali kwa hilo, huyo Jack simfahamu,” alisema Mbasha.

Bifu la Diamond na EATV & Radio..Je Litaweza Kumshusha Diamond Kimuziki?

0
0

Bifu la Diamond na Alikiba naliona linafifia kila siku iitwayo leo, huenda likaisha kimya kimya bila hata wao kuonekana wakiwa pamoja katika picha au kufanya wimbo lakini kwa upande wa Diamond namuona kwenye Bifu zito na Ipp Media Especially EATV & RADIO, Ila bifu la aina hii (Msanii na Media) huwa halizungumziwi sana kwasababu hiyo media yenyewe haitataka msanii huyo asikike kupitia vipindi vyao tofauti na bifu kati ya Msanii na Msanii watawaita kila mmoja kwa wakati wake na kupiga nao story nini chanzo cha bifu lao .
.

Mara nyingi msanii anapokuwa na bifu na Media hasa ile yenye nguvu na ushawishi, msanii hujikuta akishuka kimuziki. Mfano mzuri #Ruby na #Clouds. Lakini hili la EATV na Diamond kiukweli ni ngumu kutabili itakuwaje kwasababu EATV hawapo vizuri kama zamani na kwa upande wa Diamond yupo vizuri kimuziki na mashabiki zake ambao wapo active sana. Hivyo ni ngumu kusema kuwa EATV ndio watayumba kwasababu ile ni taasisi na vile vile ni ngumu Diamond kushuka kimuziki kisa EATV kwasababu yupo pamoja na Media yenye nguvu kwasasa (Clouds) .
.

Sijawahi kuona Msanii aliyeshuka kimuziki kisa alikuwa na Bifu na EATV ila CLOUDS....ishawatoa wengi kwenye ramani na Wasanii hao hao EATV walijaribu kuwashika mkono lakini hawakuwa na nguvu hiyo.


TOA MAONI YAKO HAPA

Breaking News: Jamali Malinzi hatoweza kushiriki uchaguzi TFF

0
0

Rais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais.

Malinzi hataweza kwa kuwa kesi iliyomfikisha mahakamani leo itasikilizwa tena Jumatatu Julai 3 na Malinzi atakaa rumande hadi siku hiyo.

Usaili wa viongozi wanaogombea uongozi TFF unafanyika kuanzia leo hadi keshokutwa wakati huo Malinzi atakuwa mahabusu.

Malinzi amefikishwa leo mahakamani akiwa na katibu wake, Mwesigwa Celestine.

Baadhi ya mashitaka hayo ni kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa imeridhia kubadilishwa kwa Signatories (watu wanaosaini nyaraka za benki kutoa fedha). Shitaka hilo linawahusu Malinzi na Mwesigwa.

Malinzi amedaiwa kugushi risiti za kwamba anaidai TFF na ziko risiti 20 ambazo anatuhumiwa kuzifoji.

Shitaka jingine ni utakatishaji na hii wote watatu, Malinzi, Mwesigwa na Nsian wanatuhumiwa kutakatisha kiasi cha dola 375418.

HAMISA Mobeto Kakosea Sana Kama Kweli ana Mimba ya Diamond Huku Anajua Anafamilia

0
0
MSANII wa sinema Bongo, Faiza Ally amemchokonoa Video Queen, Hamisa Mobeto baada ya kunasa kibendi na kusema kuwa, anamshangaa mwanadada huyo kwa kutochagua mtu stahiki wa kuzaa naye.

Akipiga stori na 3 Tamu, Faiza alisema kuwa, wasanii wengi hawajithamini miili yao na mfano mzuri ni mwanadada huyo ambaye anasikia ana ujauzito unaodaiwa ni wa msanii wa Bongo Fleva ambaye tayari ana familia yake na kuona alichofanya si sahihi.

Unajua wasichana wengi hawajithamini wanafanya vitu bila kufikiria, kama huyo Hamisa nasikia ana ujauzito wa huyo msanii (jina kapuni) na kama ni kweli mimba ni ya huyo mtu, kakosea sana, napenda kuongea kitu kinachonigusa kwenye nafsi yangu akichukia atajijua,” alisema Faiza.

VIDEO: Humphrey Polepole Aliamsha Dude Kwa Lowassa...Adai ni Mchochezi

0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi amesema Humphrey Polepole  kuwa Serikali imchukulie hatua kiongozo aliyesikika hivi Karibuni akifitinisha kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu na Serikali.

Juzi aliyekuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chadema Edward Lowassa alihojiwa na Jeshi la Polisi kwa Kilichodaiwa kuwa ni Maneno ya kichochezi aliyoyatoa kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu kwa Serikali.

Hata hivyo Polepole atoa neno kuhusu tuhuma anatuhumiwa Rais Mwinyi na Wapinzani.

WAZIRI Mkuu Ampongeza RC Anna Mghwira Kwa Kuzuia Malori 100 ya Mahindi

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira kwa kuyazuia malori zaidi ya 100 yaliyokuwa yanasafirisha mahindi nje ya nchi.

Jumatatu hii, Majaliwa alipiga marufuku usafirishaji wa mahindi alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya sherehe za Sikukuu ya Eid el Fitr.

Baada ya agizo hilo, malori hayo yalikamatwa na kuzuiwa. Akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni leo  ( Alhamisi) juu ya zuio hilo, Waziri Mkuu amesema uamuzi huo ni moja ya hatua za kuhakikisha Taifa linajihadhari na ukosefu wa chakula hasa ikizingatiwa kwamba kulikuwa na uhaba wa mvua mwaka jana.

"Nampongeza Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kwa kuyazuia malori hayo," amesema Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  jana Jumatano, Mghwira alisema magari hayo yalikamatiwa eneo la Himo  huku akipiga marufuku usafirishwaji wa nafaka pamoja na sukari kwenda nchi jirani bila ya kuwa na kibali maalumu.

“Baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari na nafaka nyakati za usiku huku wakishirikiana na baadhi ya askari polisi ambao si waaminifu, ni vema askari hao wakaacha mara moja kwani ni kinyume cha maadili ya kazi zao,”alisema mkuu huyo wa mkoa.

Chagua Kufanya Mambo Haya, Ili Yakupe Mafanikio Makubwa

0
0
Siku zote maisha ya binadamu  yanaongozwa na uchaguzi tunaoufanya kila siku. Uchaguzi huo ndio unatufanya tuwe na maisha haya au yale. Kama uchaguzi unaoufanya ni mbovu kila siku, basi ni wazi na maisha yatakuwa mabovu vilevile. Na kama uchaguzi wako ni mzuri, halikadharika na maisha yako yatakuwa mazuri vivyo hivyo.

Kitu cha kuwa makini nacho hapa, angalia uchaguzi unaoufanya kila siku na kila wakati. Uchaguzi huo ndio unaoamua maisha yako ya kesho yaweje. Kama ni hivyo, ni lazima kwetu kufanya uchaguzi utakaotupa maisha bora. Jaribu kujiuliza, ni uchaguzi wa mambo gani unaotakiwa kuufanya ili kukupa mafanikio makubwa?

1. Chagua kutumia fursa vizuri.
Kwa fursa yoyote inayojitokeza mbele yako, jifunze kuitumia vizuri. Kama ni fursa ya kibiashara au elimu itumie vizuri mpaka uone mafanikio yake. Acha kucheza na fursa yoyote ya kimafanikio inayojitokeza mbele yako. Ikiwa utafanya hivyo elewa ni lazima ipo siku utakuja kujuta kwa uamuzi ulioufanya leo.

Kuna watu ambao wameshindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutokuwa makini na fursa zilizojitokeza kwao. Bila shaka umeshawahi kuwaona watu hawa ambao wana majuto na majonzi makubwa kila wakikumbuka ujinga walioufanya. Hili ni tatizo linalosababisha ndoto za wengi kukwama. Ili ufanikiwe, jifunze kutumia kila fursa vizuri.

2. Chagua kuishi na watu chanya.
Siku zote ukiwa mtu wa kuishi na watu hasi basi ni wazi utapata matokeo wanayopata watu hao. Kama ni kulalamika, kulaumu ama kukosa mafanikio, utapata matokeo kama hayohayo. Hakuna kikubwa utakachoweza kukibadilisha. Mara nyingi maisha yetu yanathiriwa sana na wale watu wanaotuzunguka.

Siri kubwa ya mafanikio ipo kwenye watu wanaokuzunguka pia. Sio rahisi kuishi na watu hasi, halafu ukategemea mafanikio, sahau hilo. Ni lazima watakurudisha nyuma. Watu wenye mafanikio makubwa wanalijua hili. Hata wewe ukitaka kufanikiwa chagua kuishi na watu chanya. Utajifunza mengi huko na utafika mbali kimafanikio.

3. Chagua kufanya kazi kwa bidii.
Kitu kitakachokutoa hapo ulipo na kukufanikisha ni kufanya kazi kwa bidii. Kazi yoyote unayoifanya jitoe kuifanya kwa nguvu zote mpaka uifanikishe. Acha kufanya kazi kwa mkono mlegevu utajikwamisha kwenye kwa mambo mengi kuliko unavyofikiri. Ile hali ya uvivu uliyonayo jitahidi uitoe na kisha endelea kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii.

Watu wenye mafnikio makubwa siku zote wanafanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kuona mipango na malengo yao yanatimia. Kumbuka hakuna kitu utakachokipoteza ikiwa utajitoa kwa moyo kufanya kazi zako kwa bidii. Zaidi utajiongezea ujuzi, maarifa na uzoefu mkubwa utakaoutumia leo na kesho kwa maisha yako.

4. Chagua kukabiliana na matatizo na kuyashinda.
Tatizo lolote unalokabiliana nalo unao uwezo wa kulishinda. Hakuna tatizo lilokubwa kwako ambalo linaweza likakushinda. Kwa kulijua hilo chukua jukumu la kuchagua kukabiliana na tatizo lako na acha kuruhusu hata kidogo hilo tatizo likakushinda.

Tumia uwezo wako mkubwa wa akili uliopewa, tafakari kisha tafuta njia sahihi za kuweza kukabilana na tatizo lako. Kwa kufanya hivyo utakuwa mshindi na hakuna ambacho kitashindikana kwao. Wanamafanikio wote siku zote huwa ni watu wakukabiliana na matatizo yao na siyo kuyakimbia.

5. Chagua kujifunza.
Ipo haja ya kutafuta mafanikio huku ukiwa unajifunza. Unapojifunza inakusaidia kujua mambo mengi sana ambayo utayatumia katika safari yako ya mafanikio. Huu ni uchaguzi muhimu sana kuufanya ili kujihakikishia nafasi kubwa ya mafanikio katika maisha yako. Jifunze kupitia vitabu, semina au warsha mbalimbali itakusaidia sana.
Hivi ndivyo ambavyo unaweza ukachagua mambo haya na yakawa nguzo na msaada mkubwa wa mafanikio siku zote.
Nikutakie ushindi katika safari yako ya mafanikio na kumbuka tupo pamoja.

Maneno ya Babu Tale kwa DJ Choka Baada ya Kuweka wazi Kuwa Aliugua TB

0
0
Meneja wa kundi la Tip Top Connection pamoja na mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz, Babu Tale ameizungumzia issue ya DJ Choka kuweka wazi kuwahi kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) mpaka alivyopata matibabu na kupona.

Babu Tale alitumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza DJ Choka kwa kuamua kuweka wazi alichokuwa anaumwa akisema ni mfano wa kuigwa kwani watu wengi wamekuwa wanaficha juu ya magonjwa yanayowakibili.

“Wahenga walisema mficha uchi hazai, wakazidi kusema mficha maradhi kifo humuumbua, kwanza kabisa nimeguswa na kufurahishwa na kitendo cha kijasiri alicho kifanya ndugu yangu @chokadj kwa kuiwekea wazi jamii nini alikwa anaumwa na kwa kudra zake Mungu akapona.

“Imekuwa ni jadi sikuhizi kwa vijana wengi alwatan kuficha maradhi yao huku wakisahau hofu na wasiwasi pia nayo ni ugonjwa, na kadri unavo zidi kuficha ndivyo kadri ugonjwa unazidi kukomaa.

“@chokadj kawa mfano mzuri kwa jamii yetu ya sasa kudhihirisha kuwa kuficha maradhi si suluhisho wa tiba ya ugonjwa wako, ni wangapi jana walikuwa wamejifungia ndani wakiugulia TB huku mioyo yao ikiamini TB haitibiki lakini baada ya @chokadj kujitokeza na kuiambia jamii ameuguwa ugonjwa huo na kupona leo wagonjwa hao hao wapo kwenye foleni hospitalini wakingojea huduma ya matibabu.

Ndugu zangu halimpati mtu jambo isipo kuwa Mungu kutaka kwan kwa hakika ni yeye pekee atupae mitihani na majibu yake akakupatia. Sasa nazidi kuaminu TB ina tibika. #AsanteChoka“ – Babu Tale.

Umeisikia ya Mwanamke wa Mombasa Kumleta Mtoto wa Alikiba? (U-heard)

0
0
Leo June 29, 2017 kwenye XXL ya Clouds FM Soudy Brown ametuletea hii inayomhusu mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba anayedaiwa kufuatwa na mwanamke aliyetoka Mombasa Kenya hadi Tanzania akiwa na mtoto anayedai ni wa AliKiba hivyo anahitaji matunzo ya mtoto.

Inadaiwa mwanamke huyo alikutana na Alikiba alipokuwa kwenye show Mombasa na amekuja Tanzania ili kupata haki yake kwa kuwa tangu ajifungue hakuwa na mawasiliano naye.

Soudy Brown alimtafuta Alikiba ili kujua ukweli na majibu yake yalikuwa:
“Dada gani..? Amlete mtoto sasa. Kama kuna mtu anaongea hivyo vitu si unaenda unamuona na unamsikiliza na kama ana mtoto lazima apime damu (DNA).” – Alikiba. 

KILA Mwanaume Anaye Lala na Mimi Harudii Tena na wala Simu zangu Hapokei

0
0
Mimi  ni  mwanamke.Naomba msaada wa  mawazo  maana  sijui nina nini mimi...
Umri unanitupa mkono maana nakaribia miaka 35 lakini sijampata aliyewahi kunitangazia ndoa.Cha ajabu kila anayelala na mimi siku ya pili harudii tena na hata nikimpigia simu hapokei

Hapo ndo linapoanzia tatizo na  kunifanya nijisikie vibaya...Saivi  hata mtaani nachagua kwa kupita...
Kuna mwanaume mmoja huyo ndo aliwahi kunichana live kuwa nina maji mengi na MAMBO  yangu ni kubwa kiasi kwamba ha piz hadi amfikirie mpenzi wake wa zamani...

Jamani naomba msaada nifanyaje mie. Je kuna dawa ya kupunguza haya maji na kuifanya hii MAMBO  iwe  ndogo?
Hide My Name.

Kutana na Jambazi Aliyeiba Fedha Kwenye Banks 50 Kwa Ustadi wa Hali ya Juu zaidi Duniani

0
0

Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17.

Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'! Muhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber)

Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'!

Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na FBI washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza kumzuia au kumkamata.

Mbinu, weledi na nidhamu aliyokuwa nayo na kutumia kutekeleza matukio yake yalikuwa ni siri na kitendawili mpaka pale alipokamatwa na kuamua kuwasimulia FBI ili kujaribu kuwashawishi kumpunguzia adhabu ya kifungo.. Na hii ni historia yake 'kwa kifupi' tu

ALIWEKA DHAMIRA AWE "MUHALIFU MWELEVU"

Akiwa na miaka 15 Carl alitekeleza tukio lake la kwanza la ujambazi ambapo alijaribu kuiba fedha katika candy store bila mafanikio na alipigwa risasi tumboni na kukamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa katika jela ya watoto ya Camp Hill kwa miezi 18.

Baada ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu mwenye weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio na hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo (majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha, ajue namna ya kujihami (self defense) na namna atakavyo toroka na fedha.

Baada ya kuweka dhamira hiyo Carl akachukua hatua ya kwanza na alichofanya ilikuwa ni kujiunga na Chuo kikuu cha Villanova ambapo alisomea Uhandisi wa umeme. Akiwa chuoni alitumia mwanya huo kujiunga na programu maalum ya jeshi la marekani kwa ajili ya kurecruit vijana walioko chuoni! Baada ya kumaliza Chuo akaenda kutumikia jeshi kwa muda mfupi kituo cha Fort Bragg na akiwa huko akapata mafunzo maalumu ya kijeshi (Special Forces and tactical weapons training)

Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi Carl akarudi Chuo kusoma masters degree ya System Analysis na alipomaliza masters degree akafanya mafunzo ya awali kwa ajili ya shahada ya uzamivu katika Statistics.

Pia mtaani alipokuwa anaishi alijiunga na kituo cha kufundisha mafunzo ya kujihami (karate and judo) ambapo alifanikiwa kupata mkanda mweusi (third degree black belt)

Baada ya kufanikiwa kufanya maandalizi yote hayo na kupata kila aina ya mafunzo na uzoefu aliyohitaji ili kuwa 'muhalifu wa daraja la kwanza' sasa ulikuwa ni wakati kwake kupita kila benki kukomba hela na kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakujapata kuwepo na itachukua miaka mingi kutokea muhalifu professional kama yeye Carl 'the Friday night bank robber'.

MAANDALIZI KABLA YA TUKIO.

Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio! Carl alikuwa anatumia had I miezi kadhaa katika kupanga utekelezaji wa tukio moja tu.

Kwanza kabisa Carl ali scout bank zilizopo katika miji midogo. Baada ya kupata orodha ya benki katika miji kadhaa midogo then Carl aliangalia kati ya bank hizo ni bank gani haziko katikati ya mji (kwa maana kwamba ziko pembezoni/nje ya mji). Kisha Carl aliichagua bank moja wapo kati ya hizo na bank ambayo inakuwa haiko karibu sana na makazi ya watu au iko karibu na msitu basi bank hiyo anaipa kioaumbele katika orodha yake.

Baada ya kuamua ni bank gani atafanya tukio, Carl alianza tafiti juu ya tukio lenyewe atakavyolitekeleza... Kwanza kabisa Carl alianza kwa kusoma mandhari yanayozunguka bank na interest yake kubwa inaelezwa kuwa alitafiti zaidi msitu ambao unakuwa karibia na bank.. Inaelezwa kuwa Carl angeutembelea msitu huo na kuukagua nukta baada ya nukta, haijalishi ni muda gani angetumia mpaka kumaliza kuukagua!

Inaelezwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kujua ni maeneo gani ya msitu ambapo watu huwa wanamazoea ya kupita au kutembelea, ni eneo gani la msitu limejificha zaidi, ni upande gani wa msitu unakuwa rahisi kuifikia barabara, ni eneo gani la msitu lina umajimaji na eneo gani ni kavu na kadhalika na kadhalika.. Inaelezwa kuwa Carl angeutafiti huo msitu na kuufahamu kuliko hata wenyeji wa eneo hilo husika.. Angeufahamu msitu nukta kwa nukta!

Baada ya kuufanyia tafiti msitu, inaelezwa kuwa Carl alikuwa anageukia kuitafiti bank yenyewe na wafanya kazi wake.. Kuhusu bank, angetafiti je hiyo bank inafungwa na kufunguliwa saa ngapi, ni siku zipi huwa wanachelewa kufunga, ni siku gani wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha n.k! Kisha akimaliza hapo anageukia kuwatafiti wafanyakaxi wa bank husika.. Hapa alitafiti kuhusu 'shifti' zao za kazini, nanj ni teller, nani ni manager na pia kitu kingine cha msingi alijitahidi kuwasoma personality zao.

Baada ya kumaliza kufanya 'tafiti' zake Carl alienda hatua ya pili ya maandalizi ambapo ilikuwa ni kuandaa 'makazi na stoo' yake ya muda katika msitu uliopo karibu na bank ambapo alichimba handaki dogo kwa ustadi mkubwa na kulificha kabisa kwa juu mtu asiweze kujua kwa namna yoyote ile.. Moja ya wapelelezi ambao walihusika kufanikisha kumkamata Carl anaeleza Bw. Carr anaeleza kuwa siku ambayo walifanikiwa kugundua na kuliona handani mojawapo ambalo lilichimbbwa na Carl walistaajabu (kumbuka Carl alikuwa na zaidi ya mahandaki 30 sehemu tofauti tofauti za nchi ya marekani)! Inaelezwa kuwa kinachostaajabisha kuhusu mahandaki ya Carl ni jinsi yalivyo chimbwa kiustadi na kujengewa kwa ndani kwa vitofali vidogo vidogo.. Pia handaki lilikuwa linampangilio wa hali ya juu wa kiwango cha kijeshi (military precision). Ndani ya handaki kulikuwa na kila kitu ambacho angekihitaji, silaha, nyaraka za 'research', kifurushi cha kujikimu (survival kit), madawa ya dharura (first aid kit), vinyago vya kuficha sura (masks), fedha taslimu, majarida ya mazoezi ya kawaida na kijeshi na vitu vingine vingi..

Baada ya kumaliza maandalizi haya ya msingi Carl alijichimbia katika maktaba ya umma ya Philadelphia ambapo ndio alipafanya kama ofisi yake kwani inaelezwa kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia muda mwingi hapo akifanya 'tafiti' na angekuwa hapo kwa wiki kadhaa ili ku-fainalize mpango wake na kufanya conclusion ya jinsi atakavyotekeleza tukio lenyewe.

UTEKELEZAJI WA TUKIO.

Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema!

Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la 'The Friday Night bank robber'..

Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza kipindi cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika Masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha kuwa ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.. Lakini pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..

Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka 'harufu' kwenye nyumba zote zilizo karibu na bank ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu kutafuta trail ya alikoelekea!

Siku ambayo Carl alikuwa anafanya tukio alivaa kinyago cha kutisha usoni ambacho kili-fit sawa sawa kabisa ili kuficha ngozi yake na! Pia alivaa manguo mengi ili kuleta muonekano kwamba ni mnene.. Na alikuwa akiingia ndani ya bank alitembea dizaini kama amechuchumaa mfano wa Kaa (crab)! Vitu vyote hivi alivyovifanya watu walihisi labda alikuwa na matatizo ya akili lakini hawakujua kuwa alivifanya kwa kusudi kabisa.. Alivaa kinyago cha kutisha ili kuleta effect ya kuogofya na kuficha tone ya ngozi yake, pia alivaa manguo mengi ili kuficha body size, na alitembea kama kaa akiwa kama amechuchumaa ili kuficha height!! Hii ilimsaidia sana kwani kwa miaka 30 FBI walishindwa kung'amua mtu wanayemtafuta alikuwa wa size gani, height gani au skin color ipi?

KUVAMIA.

Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia..

Akishavamia bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimuangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ma-teller na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimuangalie na kabla hawajang'amua kinachoendelea Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya bank na kutokomea katika msitu ulio karibu..

Inaelezwa kuwa katika matukio yake yote aliyatekeleza ndani ya muda usiozidi dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari amevamia, amekomba hela na ameshatokomea msituni..

Carl anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu alikuwa anakimbia kwa dakika kadhaa kama kumi hivi mpaka mahala ambapo anakuwa ameficha baisikeli kisha anaendesha mpaka ndani ndani kabisa ya msitu kulipo na handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha alizoiba, masks, nguo, gloves etc kisha anavaa nguo nyingine za kawaida anaendesha baisikeli anaondoka! Carl anasema kuwa ataendesha baisikeli kwa muda wa kama dakika ishirini au zaidi mpaka upande wa pili wa msitu ambapo kuna barabara na hapo kunakuwa kuna gari amepaki linamsubiri.. then anawek baisikeli ndani ya gari anaendesha kama raia wa kawaida na kuelekea nyumbani.

Carl anasema alikuwa anacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio la ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua 'hela zake'. Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza 'tafiti' kwa ajili ya tukio linalofuata.

KUKAMATWA NA HUKUMU.

Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno! Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa.. Baada ya kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao wakashauri vipelekwe polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani.. Polisi walipoifuatilia ile ramani ikawqpeleka moja kwa moja kwenye handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana na vitu vilivyokutwa ndani ya handaki hilo polisi wakapata wasiwasi kuwa inawezekana wanadeal na ishu serious kuliko uwezo wao hivyo wakawataarifu FBI! Baada ya FBI kuwasili iliwachukua masaa kadhaa tu kung'amua kuwa vitu hivyo vinahusiana moja kwa moja na Jambazi wanayemtafuta kwa miaka 30, The Friday night bank robber.

FBI walitumia alama za vidole walizozikuta kwenye ile handaki na pia walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo cha mafunzo ya karate kumtrack down Carl mpaka wakampata.
Siku Carl anakamatwa alikutwa "ofisini kwake" Maktaba ya Philadelphia Free Library akiwa anafanya "tafiti"

Baada ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani ilikuwa ni dhahiri kuwa Carl atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo uwezekano wa kupata parole kutokana na mashitaka yanayomkabili lakini mwisho wa siku Carl alikubaliana deal na FBI kuwa awaeleze nukta kwa nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na FBI kutengeneza programu maalum kuwasaidia maafisa wa FBI kutambua namna ya kuwabaini 'serial criminals', na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo perfect.!

Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..

Hivyo basi ikifika 2021 Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa huko gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na ameendeleza desturi yake ya kupenda mazoezi hivyo yuko katika afya njema sana na wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salimini.

Hili lingine la Rayvanny na BASATA Kuhusu Mapokezi na Tuzo ya BET

0
0
Siku moja baada ya mwimbaji Rayvanny kuwasili Bongo na kukutana na mapokezi makubwa Airport DSM akiwa na tuzo yake ya BET akiwa msanii kwanza wa Bongofleva kutwaa tuzo hiyo…story gumzo ni kuhusu kutooneakana mwakilishi wa BASATA Airport.

255 ya XXL ya Clouds FM leo June 29, 2017 imempata Katibu Mkuu wa BASATA, Godfrey Mngereza ambaye ameelezea sababu za kutoonekana mwakilishi wa Baraza hilo akisema kulikuwa na mawasiliano finyu kati ya Rayvanny na BASATA wakati anakwenda na kurudi kuchukua tuzo hiyo.

 “Hakukuwa na mawasiliano mazuri alivyokuwa amekwenda na ujio wake lakini tungekuwa tunaifahamu ratiba yake Baraza kama ilivyo ada huwa hatuna budi ya kwenda kumpokea Airport, kwanza inaleta heshima.


“Kwa hiyo, hakuna sababu ya kusema tusingeenda kumpokea ni kwamba mawasiliano hayakuwepo tangu anaenda na pia ningependa nikumbushe wasanii wanavyokwenda nje ya mipaka ya Tanzania ni vizuri tukaagana ili tukajua ratiba ikoje hata wakirudi tuwapokee.”– Godfrey Mngereza.

Wakati huo huo Rayvanny amefunguka akidai kuwa sasa hivi kila kitu kipo wazi kutokana na mitandao lakini pia BASATA walitakiwa kusoma chochote kipindi tu walipoona amechaguliwa kwa kuwa ndio wazazi wa muziki wa Bongofleva na kama viongozi wao walipaswa kutoa support.

 “Kwa mafano, mimi nilivyochaguliwa kama BASATA walikuwa wameona. Wao ni wazazi walikuwa na chochote cha kusema lakini wakisema kwamba wanasubiri niende mimi mwenyewe au tunasubiri watuambie au hatuwezi kwenda kwa sababu hatujaambiwa. Wale ni wakubwa kwetu ni wazazi wetu tunategemea kwamba wanakuza sanaa yetu na sisi tunawaangalia wao walitakiwa kuwa kipaumbele sisi kutusaidia.”– Rayvanny.

Hatimaye Kijana Aliyedhaniwa Gaidi na Kuuwawa Kwenye ATM Kuzikwa

0
0

HATIMAYE mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Salum Almas (28), unatarajiwa kuzikwa leo ikiwa ni siku takribani ya 50 tangu kuuawa na polisi kwa tuhuma za ujambazi.

Almasi ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo hicho Kituo cha Kompyuta (UCC), akichukua masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT), aliuawa na polisi jirani na mashine ya kutolea fedha ya kielektroniki (ATM) ya benki ya CRDB iliyopo kandoni mwa ofisi za Uhamiaji, Kurasini kwa madai ya kutaka kupora fedha.

Mwili wake ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Mjomba wa marehemu, Tulleyha Abdulrahman, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana kuwa mwili huo ulikuwa ukifanyiwa uchunguzi Muhimbili jana, chini ya mwanasheria wa familia, ndugu, polisi, tume ya haki za binadamu na kiongozi kutoka Serikali ya Mtaa wa Kurasini ambako ndiko marehemu alikuwa akiishi.

Awali, baada ya mauaji ya Salum, ndugu waligoma kuuzika mwili huo wakitaka Jeshi la Polisi limsafishe mtoto wao dhidi ya tuhuma za ujambazi kwa maelezo kuwa kijana huyo hakuwahi kujihusisha na vitendo hivyo katika maisha yake.

Hata hivyo, baada ya kuuawa kwa Almasi, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam, Simon Sirro (sasa ndiye Mkuu wa Jeshi hilo, IGP), aliwataka wale wanaobisha kuwa kijana huyo hakuwa jambazi waende eneo la tukio kuwauliza mashuhuda.

Licha ya kauli hiyo, ndugu wa marehemu waligoma kuuchukua mwili huo na hatimaye walimwandikia barua Rais John Magufuli pamoja na Mkurugenzi wa Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, wakisisitiza kuwa Almasi aliuawa kimakosa kwa sababu hakuwahi kuwa jambazi na hivyo, wakataka Polisi wamsafishe ndipo wamzike.

Wiki mbili zilizopita, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz alithibitisha makao makuu kufanya uchunguzi dhidi ya tukio hilo.

“Ni kweli tunachunguza ili kuthibitisha ukweli ni upi. Ndugu walituandikia barua ya malalamiko ya kuuawa ndugu yao wakati siyo jambazi. Bado uchunguzi unaendelea…haujafikia mwisho, tukimaliza watataarifiwa. Ila kila mara tumekuwa tukiwapa mrejesho,” alisema DCI Boaz.

Mjomba wa marehemu, Abdulrahman, alisema jana kuwa baada ya uchunguzi huo, wanatarajia kumzika mtoto wao Ijumaa (kesho) katika makaburi ya Kisutu.

“Leo (jana) tupo hapa Muhimbili. Mwili wa Salum unafanyiwa uchunguzi kabla ya kuzikwa. Hivyo ndivyo naweza kukueleza kwa sasa… ila tutazika Ijumaa makaburi ya Kisutu,” alisema.

Abdulrahman ambaye ndiye aliyekuwa akiishi na Salum enzi za uhai wake eneo la Kurasini, Shimo la Udongo, wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, alisema baada ya uchunguzi huo watazika wakati wakingojea majibu ya uchunguzi.

Awali, akisimulia kuhusu tukio hilo, Abdulrahman alisema Salum aliuawa muda mfupi baada ya (yeye) kumpigia simu amfuate kituo cha daladala cha JKT kwa ajili ya kuchukua fedha za matumizi za nyumbani.

“Tulionana saa 3:30 asubuhi Jumapili baada ya kumtaka aje kituo cha daladala cha JKT, nilimpatia Sh. 30,000 akaondoka kurudi nyumbani, saa nane baadaye nikapigiwa simu kujulishwa kuhusu kifo chake,” alisema siku hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa siku moja baada ya mauaji hayo ilieleza kuwa kijana huyo aliuawa wakati akijaribu kupora fedha za benki ya CRDB zilizokuwa zinasambazwa na gari la kampuni ya G4S katika mashine zake za kutolea fedha, huku majambazi watatu waliokuwa katika pikipiki mbili wakikimbilia kusikojulikana.

Mwalimu afumwa akifanya mapenzi na mwanafuzi wake darasani

0
0

Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge ameagiza kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Wanike, iliyopo katika wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wake darasani usiku.

Kasinge ametoa agizo hilo baada ya kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea tofauti na tukio.

"Kuanzia wanafunzi walitimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe pia aendelee kushikiliwam huyo ambaye anatuhumiwa aendelee kushiliwa na polisi mpaka tupate majibu, kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira ya kutengeneza mtandao wa kutaka kumsaidia na kupotosha ushaidi" alisema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge

Mbali na hilo shule ya sekondari ya Wanging'ombe pamoja na Wanike zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea wanafunzi wa kidato cha tano, walimu wa shule hizo wameweka wazi kuwa shule hizo zinachangamoto ya walimu wa sayansi ambao ni wachache ukilinganisha na walimu wa masomo ya sanaa.

Miujiza ya Maalim Khatibu Kutoka Kigoma Kusini Sasa Yupo Bagamoyo Mkoa wa Pwani...

0
0

MIUJIZA YA MAALIM KHATIBU KUTOKA KIGOMA KUSINI SASA YUPO BAGAMOYO MKOA WA PWANI.

Wengi wamepata tiba na kutatuliwa MATATIZO yao wewe unasubiri nini?

✨Kwanini umapata pesa haikai? Na haufanyi kitu cha maana?
✨Kwanini mapenzi yakutese?
Kwanini uachwe na Mke! Mme au mpenzi wako?
✨Kwanini hamuelewani katika familia yenu kwaaji ya kugombea mali?

Majibu yote utayapata kwa MAALIM KHATIBU, mwenye kubri kubwa kutoka kwa Allah,✔

MAALIM KHATIBU ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili na nimtambuzi wa nyota za binadamu, pia nimtatuzi wa matatizo yote yanayo watesa binadamu,

MAALIM KHATIBU anatibu kwa kutumia kitabu cha quran dawa za asili dawa za kiarabu, na majini, Anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango kwa kina mama, ngiri maji na n.k, anakuvutia mali zilizo potea au kudhulumiwa, pia anatoa Pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali, Wenye matatizo ya uzazi, jini mahaba, mapepo ya kichawi, vifungo vya kimaisha, ndoto mbaya za usiku, uelewa mdogo wa ufahamu shuleni kwa watoto wote, pia anauwezo mkubwa wa kumaliza kazi zilizoachwa na wataalamu wengine ndani ya masaa 48 tu,Pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo.

WASILIANA NAE KWA SIMU NA WhatsApp
Tigo - No:+255 710 -332103
Voda - No:+255 766-705404,
Insta follow @maalim_khatibu

USHAURI: ni vyema kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate huduma kwa haraka.

Kesi ya Viongozi wa TFF, jopo la Mawakili 5 Wajipanga Kushinda Kesi (Video )

0
0
Mmoja kati ya jopo la mawakili watano wanaosimamia kesi ya viongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania,TFF, Jerome Msemwa amesema watahakikisha wateja wao wanakuwa huru kwa kupatiwa dhamana juu ya mashitaka wanayo yakabili.


Wakili, Jerome Msemwa akizungumza na vyombo vya habari mahakamani Kisutu

“Mahakama itatoa tafsiri ya kisheria je, wakati kesi imeanza kusikilizwa, upande wa upelelezi unaweza ukaomba na ukapewa ruksa ya kupeleleza kesi wakati washitakiwa wapo mahakamani na kwa sheria hipi, ndio mahakama itakuja kulitolea ufafanuzi swala hilo ?, kwa washitakiwa kukamatwa kufikishwa mahakamani na halafu wanaomba tena upelelezi wakesi wakati swala lipo mahakamani.


Rais wa TFF,Jamal malinzi(katikati), makamu wa klabu ya Simba,Geofrey Nyange ‘Kaburu’(kulia) na katibu Mkuu wa TFF,Mwesigwa Celestine (kushoto)


“Na pointi yetu ya pili ni maombi ya dhamana, mahakama hii tumeiomba itoedhamana kwa wateja wetu kwasababu tunaamini kwamba kunasheria ya bunge inayokataza dhamana na kunakatiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoruhusu dhamana kwahiyo vituviwilivitakuja kuamuliwa siku ya Jumatatu ya tarehe tatu mweziwa saba” amesema wakili Jerome Msemwa.

Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva,(kulia) makamu wake,Geofrey Nyange ‘Kaburu’ (wapili kutoka kulia) Katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine (wamwishokushoto) na ,rais TFF, Jamal malinzi (wapili kutoka kushoto) wakiingia mahakamani leo

Naye wakili Msomi Aloyce Komba amesemakuwa hojawalizotoa ni katika kuhakikisha haki inatendeka

“Tumetoa hoja zinazozingatia haki inatendeka na inaonekana kutendeka iliwateja wetu kwa mashitaka waliyoshitakiwa yaanze mara moja na yaishenawao wapate hakizaozigine ikiwemo haki ya dhamana tuliyoiomba. Natumesema mashitaka yotetukiyaangalia ni ya kugushi kugushi ingawa mengine kama matatu wameyabadilisha yakawa ya kutakatisha fedha ilitu wakose dhamana” amesema wakili Msomi Aloyce Komba.


Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Mwesigwa Selestine walitiwa nguvuni siku ya Jumanne mchana na kufikishwa mahaka ya hakimu mkazi Kisutu leo kwa lushitakiwa na makosa 28 yakiwemo ya kugushi na utakatishaji fedha hivyo mahakama imeamuru kupelekwa mahabusu katika Gereza la Segerea hadi Jumatatu ya Julai 3 kesi yake itakaposikilizwa tena.

Jopo la mawakili watano likiongozwa na Jerome Msemwa, wakili Msomi Aloyce Komba, James Bwana, Komba na wakili Mpedule ndio wanaosimamia kesi ya viongozi hao wa ngazi ya juu ndani ya shirikisho kuhakikisha nawakuwa huru kama wenyewe walivyoeleza.

Taifa Stars Yatinga Robofainali COSAFA

0
0

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefuzu hatua ya robo fainali ya mashindano ya michuano ya COSAFA inayo endelea huko nchini Afrika Kusini baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Mauritius.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakiingia uwanjani

Stars ambayo inaongoza kundi A kwa kuwa na jumla ya alama tano sawa na timu ya taifa ya Angola, inatofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa.


Bao pekee la Stars lilifungwa na mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simon Msuva na kuiwezesha Tanzania kutinga hatua ya robo fainali ambapo itakabiliana na mwenyeji wa michuano hiyo timu ya Afrika Kusini.

Gigy Money Atoa Povu Kuhusu Lenzi za Macho..Wema Ahusika

0
0

Baada ya kuambiwa ameiga kuweka lenzi katika macho yake ili avutie, Gigy Money ameamua kutoa povu kwa wale wanaomwambia ameiga kitendo hicho kutoka Wema Sepetu.


Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram mrembo huyo asiyeishiwa na vituko ameporomosha mapovu hayo kwa kuandika.

“Yani kuna watu wengine makubwa jinga etiii kabisaaa kisa lens za macho tena bandia watu wanapaniki mm mtu wa ajabu kwel cos nimeamua kuvaa miwani tu lens vaaeni nyie muwe vibonge kama zinanenepesha #kuwafakehakujawaikumuachamtusalama #bilakisahausiwaogopi 😂😂😂,” ameandika Gigy.

Ameongeza
“Povuuuu linaruhusiwa kwanza mnasemaga hakuna wakunijibu sasa alie nijibu ni wema rapper sijuiii?!!!!😂😂😂😂😂😂 alafu nyie timu yake waswahili sana yani wengi wenu mnatokea magomen keko na mwananyala so hamniboi cos mm mwenyewe mtoto wa kurasin so byeeeeeeeeeeee bythiiiiizzzzss pia anaecoment ananikubal kama hunikubal pita kimyaaaaa😂😂😂.”

Magufuli si Mchezo...Miswada MITATU ya Madini yatua Bungeni

0
0
IKIWA ni siku kadhaa zimepita baada ya Rais John Magufuli kulitaka Bunge lipitie upya sheria na mikataba ya madini, miswada mitatu inayohusu madini tayari imesomwa bungeni kwa mara ya kwanza jana.

Aidha, ili kutoa fursa ya wabunge kujadili miswada hiyo iliyowasilishwa bungeni kwa hati ya dharura, vikao vya Bunge la Bajeti vilivyokuwa vifikie tamati leo, vimesogezwa hadi Julai 5 mwaka huu ili kutoa fursa kwa wabunge kupitia miswada hiyo. Miswada iliyosomwa kwa mara ya kwanza bungeni hapo ni Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017.

Muswada huu unapendekeza kuweka utaratibu ambapo wananchi kupitia chombo chao cha uwakilishi ambacho ni Bunge, kitapitia na kujadili makubaliano na mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi, ambayo imefungamana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujiridhisha na masharti. Muswada mwingine ni Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya nchi Kuhusu Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017.

Muswada huu unakusudia kuweka masharti yatakayohakikisha kwamba hatua yoyote inayochukuliwa kuhusu uwekezaji wa rasilimali za taifa, inatambua na kuzingatia haki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama taifa huru lenye mamlaka ya kusimamia na kutumia rasilimali zake kwa maslahi ya taifa. Muswada mwingine ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2017.

Wakati anapokea ripoti ya pili ya Kamati Maalumu ya Uchumi na Sheria kuhusu Taarifa ya Makinikia, Rais Magufuli aliliomba Bunge kupitia upya sheria na mikataba yote ya madini na gesi ili kuiepusha nchi kuingia katika mikataba mibovu.

“Kamati ya uongozi ilikaa jana (juzi) kubadilisha ratiba ambapo sasa mkutano huo wa Bunge la bajeti utaahirishwa Julai 5 mwaka huu, badala ya Juni 30 kama ilivyokuwa imepangwa awali, miswada mitatu mipya ya sheria iliyosomwa kwa mara ya kwanza, itapelekwa katika kamati za Bunge,” alisema Spika Job Ndugai, ili kutoa nafasi kwa wabunge kujadili miswada hiyo, Bunge limebadili ratiba kwa Bunge kuendelea na shughuli zake hadi Julai 5 mwaka huu, ambapo bunge hilo litaahirishwa.

Alisema Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali wa mwaka 2017 kwa kuangalia upungufu uliojitokeza itafanyiwa kazi na Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria inayoongozwa na Mohammed Mchengerwa.

Ndugai alisema pia Bunge limeunda kamati maalumu itakayoundwa na wajumbe wa kamati nne za Nishati na Madini, Kamati ya Ardhi, Kamati ya sheria Ndogondogo na Kamati ya Katiba na Sheria, itakayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dotto Biseko ambayo itapitia miswada miwili ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka 2017.

Pia kamati hiyo itafanyia kazi Muswada wa Sheria ya Mamalaka ya nchi kuhusu Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017. “Kamati hizo zitafanya kazi kuanzia leo (jana) kwa kukutana na wadau mbalimbali na kisha taarifa itawasilishwa bungeni Jumanne, kabla ya bunge kuahirishwa Jumatano (Julai 5 mwaka huu),” Baada ya kuwasilishwa kwa miswada hiyo, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika aliomba mwongozo wa Spika, ambapo aliliomba bunge kuondoa hati ya dharura ya kujadili miswada hiyo.

“Muda mfupi uliopita tumekabidhiwa ratiba ya bunge, serikali inaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura, mwaka 1997 mikataba ya madini ilipitishwa haraka haraka, mikataba ya ngesi hivyo hivyo, “Kazi ya bunge ni kutunga sheria, sisi ndio wawakilishi wa wananchi, kwa umuhimu wake na maslahi kwa wananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa kukutana na wananchi, hivyo ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza na hati ya dharura ikaondolewa na kuletwa bunge lijalo.

Aliongeza: “Kwa maelezo uliyotoa wadau wataitwa kwa short notice wafike Dodoma kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichambue. Huu ni mtego kwa kutufanya tushindwe kuishauri serikali kwa kazi yetu ya kibunge”. Akitoa majibu ya serikali kuhusu muongozo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulamavu, Jenista Mhagama alisema masharti ya kutunga sheria na masharti ya jumla, yamewekwa katika fasihi ya nane ya Kanuni za Bunge, masharti yameongezwa na kanuni ya 80 na kanuni nyingine.

“ Muswada ambayo imeletwa imekuja kwa hati ya dharura, ili bunge liridhie kama miswada hii inastahili kujadiliwa na bunge ama la, kanuni 80(4) inasema muswada wowote wa dharura hautaingizwa katika shughuli za Bunge bila kuwa na hati iliyowekwa sahihi na rais kuthibitisha kwamba muswada huo ni wa dharura. “Sisi kama serikali tumeshatimiza masharti yote, tumeshakamilisha hatua zote za kufikishwa muswada huo kwa hati ya dharura. Wanaoweza kulishauri Bunge baada ya kuona uzito wa kazi iliyolewa na serikali ni kamati husika itakayopewa kazi ya kujadili miswada hiyo,” alisema.

Alisema sio busara kwa wabunge kabla hawajaona yaliyomo katika miswada husika, kujenga hoja ya kuikataa ndani ya bunge, mana kinachofanyika ni kwa maslahi mapata ya taifa. Akijibu mwongozo huo, Spika Job Ndugai alisema kwa niaba ya wabunge alipokea hati ya dharura huku akiwataka wabunge kulifanyia kazi jambo hilo.

“Tulijadiliana na kamati ya uongozi yenye uwakilishi wa tukakubaliana suala hili lisonge mbele. Wakati Rais (Magufuli) akipokea ripoti ya pili ya mainikia, kwa niaba yenu nilikubali kama kuna mambo yenye maslahi kwa nchi tutayafanyia kazi, mambo yameletwa katika kamati husika, kamati itajadili kama muswada inastahili kuingia bungeni ama la hoja nitatokea huko.

Aliongeza, “kwa muda mrefu tulikuwa tunataka Bunge kuwa na nafasi fulani katika masuala ya yanayohusu maadini na gesi, liwe na nafasi fulani ili kuzuia nchi kuingia katika mikataba mibovu. “Miswada hii kama mtanzania yeyote mwenye kuhitaji ataipaata katika tovuti,”alisema Ndugai.

Nafasi za AJIRA Zilizotangazwa leo Ijumaa

Viewing all 104414 articles
Browse latest View live




Latest Images