Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Mambo Yanayokuzuia Kupata Furaha Ya Kweli Maishani Mwako

$
0
0
Inaweza kuonekana ni kitu cha kawaida lakini kuwa na furaha ya kweli na ya kudumu ni kitu ambacho kinatafutwa sana na watu wengi. Ndio maana ukichunguza, harakati nyingi za kutafuta maisha zinalenga hasa kupata furaha.

Hata hivyo pamoja na watu wengi kuitafuta furaha sana, lakini bado wengi pia wanaendelea kugubikwa na huzuni nikiwa na maana ni watu ambao wanaishi maisha hayana furaha sana kwa sehemu kubwa.

Je, hebu tujiulize ni mambo gani ambayo yanasababisha mtu mmoja akawa na furaha au mwingine akaikosa furaha? Majibu ya maswali haya utayapata kwenye makala haya. Kikubwa fuatana nasi tuweze kujifunza pamoja.

1. Kufanya kazi usiyoipenda.
Ipo asilima kubwa sana ya watu ambao wanafanya kazi ambazo mara nyingi wanakuwa hawazipendi sana. Kwa lugha rahisi wanakuwa ni watu wanafanya kazi ambazo hawazifurahii, kikubwa kwao inakuwa ni kutaka kuingiza kipato tu basi.

Kama unafanya kazi ya namna hii ambayo huifurahii, lakini lengo lako ni kuingiza kipato basi elewa unabeba  moja ya kitu ambacho kinakuzuia kupata furaha katika maisha yako kwa namna moja au nyingine.

Watu wote wenye mafanikio wanafanya vile vitu ambavyo wanavipenda kutoka moyoni mwao. Kama hufanyi kitu unachokipenda, leo hii ukianza kufanya kitu ambacho unakipenda, uwe na uhakika utaanza kujenga furaha yako.

2. Kujilinganisha na wengine.
Ni tabia ya wengi wetu tangu tukiwa watoto wadogo kutaka kujilinganisha na watu wengine. Kwa bahati mbaya tabia hii imekua ikikua hadi kuweza kufikia ukubwani na kwa wengi wetu tena tumekuwa tukiindeleza pasipo hata kujua.

Mara nyingi tumekuwa tukijilinganisha katika vipato vyetu, tumekuwa tukijilinganisha katika mavazi na mambo mengine chungu nzima. Hivyo, kutokana na kujilinganisha huko sana imekuwa ikipelekea sisi kukosa furaha.

Kikawaida huwezi kuwa na furaha kama kila wakati unajilinganisha na wengine. Maisha na furaha yako inabaki kuwa yako kama kweli unaishi wewe kama wewe. Kujilinganisha na wegine ni sawa na kutengeneza mazingira ya kupoteza furaha yako moja kwa moja.

3. Kuogopa mambo mengi.
Ni asili ya binadamu kuwa na hali fulani ya woga. Kuna wakati tunakuwa tunaogopa mambo yanayotudhuru au kuna wakati tunakuwa tunaogopa kujiingiza katika jambo fulani , mathalani hata uthubutu wa kufanya kitu fulani.

Sasa inapotokea unakuwa ni mtu wa kuogopa sana mambo mengi na kila wakati, hiyo inakuwa ni changamoto mojawapo ambayo inakuzuia moja kwa moja wewe kuweza kupata furaha ya kweli.
Furaha ya kweli mara nyingi inapatikana hasa kwa wewe unapokuwa huru na mambo yako.

Unapokuwa huru huna hofu ya mambo mengi na kuishi kwa kujiamini, hapo ndipo unakuwa na furaha ya kweli.

4. Kuishi wakati uliopita.
Kuna watu ambao wengi wetu badala ya kuishi sasa, hujikuta ni watu wa kuishi kwa kukumbuka sana matukio mengi yaliyopita. Kama unaishi hivi kwa kukumbuka mambo mengi yaliyopita na ambayo yalikuumiza kwa namna moja au nyingine uwe na uhakika, furaha yako utaipoteza.

Kujenga furaha ya kweli unatakiwa kuishi sasa na wala si kesho. Fanya mambo yako kwa kuzingatia sana sasa. Watu wngi wenye mafanikio na furaha ya kweli wanaishi sasa na kusahau mambo mengi yaliyopita.

Kumbuka wewe ndiye unayewajibika na kutengeneza furaha ya kweli katika maisha yako. Zingatia mambo hayo yanayokuzuia kupata furaha ya kweli.

Jinsi Ya Kujiweka Wa Thamani Kwa Mpenzi Wako

$
0
0
Marafiki zangu tunaendelea na mada yetu ambayo kwa hakika imekuwa ndefu lakini yenye manufaa makubwa kwenye uhusiano wetu. Nilianza kwa kueleza kwamba yapo mambo mengi sana ambayo husababisha thamani ya mtu kushuka kwa mpenzi wake.

Nilishazungumza mengi katika matoleo yaliyopita lakini leo nitaendelea na kukazia zaidi kwenye athari za kuharakisha faragha. Karibu darasani.

ATHARI ZA KUHARAKISHA FARAGHA
Wiki iliyopita nilifafanua zaidi matatizo ya moja kwa moja ambayo mtu anaweza kuyapata kwa kuharakisha faragha ambapo nilisema kwamba kuna suala la kuchokwa na kuonekana wa kawaida.

Lingine ni kuonekana mwepesi kwenye suala la mapenzi hivyo mwanaume kuwa na mashaka kwamba hata kama akifikia uamuzi wa kukuoa unaweza kuwa mwepesi kutoa penzi kwa wengine kama ulivyofanya kwake. Tuangalie vipengele vinavyofuata.

(i) Hupunguza thamani
Heshima ya penzi ni kwenye ndoa. Kuna uwezekano mkubwa sana wa kushushwa thamani baada ya kutoa penzi. Wanaume wengi huanza kuwa wasumbufu (kama ni kasumba yao) kwa wapenzi wao baada ya kutoka nao kimapenzi.

Pamoja na kwamba ni tendo la furaha lakini kwa mwanamke linampa unyonge na wakati mwingine huwa mwanzo wa utumwa wa mapenzi kwa kuogopwa kuachwa wakati tayari ameshatumika!
Hebu jiulize; utatumia/utatumika kwa wangapi? Ukifikiri kwa makini juu ya jibu la swali hili bila shaka utabadilisha mtazamo wako.

(ii) Hupunguza msisimko
Penzi la kienyeji mara nyingi hata wahusika huwa wanajua kabisa kuwa wanakosea. Makosa haya husababisha kupoteza msisimko wa ndani. Ni jambo la kisaikolojia sana na huenda muathirika asigundue tatizo hili kupitia dalili za kitaalamu atakazozionesha.

Mkishaibana huko nje huwa kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kupoteza msisimko wa kawaida. Mfano mawasiliano hupungua, hamu ya kuonana inapungua sana n.k
Hapa nisipoteze muda sana, wengi mnafahamu inavyokuwa; MWANAUME AKISHATEMBEA NA MWANAMKE, TARATIBU ATAANZA KUJIWEKA PEMBENI. Kama alikuwa anapiga simu mara nne au tano kwa siku, hupunguza idadi na wakati mwingine hupitisha siku nzima kabisa.

Mbaya zaidi, unaweza kumpigia wewe na bado asipokee, ukituma ujumbe mfupi hatajibu au atachelewa. Kesi nyingi sana nilizokutana nazo za wanawake wanaolalamika wapenzi wao kubadilisha utaratibu wa mawasiliano, baada ya kuwahoji walisema jambo hilo limejitokeza baada ya kuwapa penzi.

MUHIMU KWAKO KUJUA
Mwanaume wa aina hii ni yule ambaye hakuwa na mpango wa ndoa baadaye au hakuwa na uhakika na aina ya uhusiano anaotaka kwa mwanamke wake.

Sasa jiulize, ikiwa alikuwa kwenye majaribio, utajaribiwa na wangapi? Tumia hekima rafiki yangu ili kujinasua katika mtego huu.

(iii) Upungufu
Ukishautoa mwili wako kwa mwanaume, kama ni aina ya wale ambao huchunguza sana ni rahisi kukutoa kasoro. Utamsikia akisema, aaah! Huyu mwanamke bwana ana sijui nini...hakuna hoja za maana.

Kikubwa unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba kuutoa mwili wako hovyo kunakupeleka kwenye kujichoresha na pengine kama umekutana na mwanaume kicheche ataishia kukutumia na kukuacha kama alivyokukuta!

(iv) Msimamo
Pamoja na kwamba wanaume wengi ndiyo hasa wanaokuwa wa kwanza kushawishi kupewa mapenzi, ukweli ni kwamba ni wepesi wa kulaumu (vipengele vilivyopita nilikazia zaidi) na kuwaona wenzi wao hawana msimamo na maisha yao.

Kukuweka kwenye kundi hilo kutakukosesha nafasi ya uhakika ya kuingia kwenye ndoa, maana wengi wanapenda kuwa na wenzi wenye msimamo thabiti.

(v) Mimba
Kuna suala la mimba. Nimekutana na kesi nyingi sana za aina hii. Wanaokutana kimwili na wenzi wao bila mpangilio huwa hawazingatii sana suala la mimba lakini inapotokea ndiyo huanza kuhangaika kutafuta ushauri.

(VI) Magonjwa
Kuharakia mapenzi kuna matatizo mengi. Ukiacha kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa pia kuna suala la ujauzito. Mathalan utakuta msichana amepata mimba isiyotarajiwa, anatafuta shotikati na kwenda kuitoa, hapo kuna matatizo mengine mengi anayoweza kuyapata kutokana na kitendo hicho.

Zifahamu Mbinu Mbalimbali za Kumpata Mpenzi Bora Katika Mapenzi

$
0
0
KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana.

Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza.
Ndio ukweli wenyewe

Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea.

Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi.

Maneno ya kusikia kutoka kwa wanawake
Wakati wa kumtongoza mwanamke tarajia maneno kama;

1. Nina mume au mchumba
Inakuwa kuwa ni kweli au njia ya kukataa

2. Niko bize na kazi`
Hii humaanisha kwamba hana muda wa kuzungumza au hata kuonana, ni dalili pia ya kukataa au kuvuta muda ili aendelea kukutafiti

3. Nimeokoka nampenda Mungu
Hii huwa na maana kwamba yeye ni mtu asiyependa uchafu hasa kama unamtongoza kwa lengo la kufanya ngono tu

4.Mimi nasoma, sitaki hayo hadi nimalize
Sitaki! Ni kwamba anaweza kujisemea kwamba hataki uhusiano uwepo. Anaweza kueleza sababu au kutoeleza.

5. Wewe sio mwanaume wa aina yangu;
Hapo huwa mwanamke anamaanisha labda una sifa tofauti na anazotaka, huenda wewe mwanaume ni mfupi, mweusi au tabia zingine zozote ambazo haziendani nae.

Msingi wa kuomba urafiki 
Kwa mwanamume mwenye umakini, huwa hakosi kupata anachotaka. Jiwe lake lazima litapiga anachokitaka, hasa kama atakuwa mwenye kufanya utafiti wa kina kabla ya kuamua kufanya kitu. Msingi sahihi wa kutongoza ni kufanya utafiti na kuongea kwa mitego, kabla ya kumfikia msichana unayemuhitaji.

Kwa mfano badala ya kusema twende tukale chakula cha mchana, sema utakuwa na muda kweli tukale, au uko bize? Maana yake ni kwamba huenda ni kweli akawa bize au la, lakini kama hataki atakwambia niko bize kama ndivyo unaweza kumuuliza nikuletee nini ninapotoka kula. Kwa namna anavyojibu vibaya au vizuri unaweza kupata mwelekeo wa nini unaweza kujibiwa kama unaongea wazi unachokitaka kwake.

Wanawake wanajua fika nini ambacho mwanaume anakitaka anapoanza kuongea hiki na kile, mara nyingi huwa wanafanya kana kwamba hawajui.

Mambo ya kuzingatia katika hatua ya uchumba
Ukweli ni kuwa uchumba ni wakati mzuri sana wa kuangaliana tabia ili hatimaye kuwa na chaguo jema. Hata hivyo ili kuwa na uhusiano mzuri ni lazima kufahamu kuwa wanadamu wanatofautiana, aidha kitabia au kimuonekano. Ni lazima kujifunza namna gani unaweza kuishi na watu wengine wenye hali tofauti.

Unaweza kuona watu wanatofautiana kitabia, huyo ni mzunguzaji sana, mwingine ni mpole, kiasi kwamba hata ukiwa nae ni kama uko peke yako. Kumlazimisha asiye na uwezo wa kuzungumza sana, awe mzungumzaji, sio sahihi sana, wala kumzuia mzungumzaji asifanye hivyo, pia sio sahihi
Wachumba wanaweza kutofautiana kwa kiwango cha elimu, uchumi, ufahamu juu ya mambo mbalimbali, kikabila, umri na hata kwa rangi pia. Kufahamu hili ni suala la msingi sana ili kuhakikisha.

Ingawa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakilazimisha kwamba wawe wanaoana na wale ambao ni wa kutoka kwenye madhehebu yao tu, wachumba wanaweza wakatoka katika madhehebu/makanisa tofauti na hili ni kwa kuzingatia madhehebu/makanisa mengi yaliyopo.

Baada ya siku 45, Hatimaye Aliyeuawa na Polisi kwa ‘Ujambazi’ Azikwa Dar

$
0
0
Mwili wa denti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Salum Almas aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi kwa madai kuwa alikuwa Jambazi, Mei 14, mwaka huu maeneo ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar, ukiwa umebebwa tayari kwa kuzikwa katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar.

HATIMAYE mwili wa denti wa UDSM (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), Marehemu Salum Almas aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi kwa madai kuwa alikua jambazi, Mei 14 mwaka huu, maeneo ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa Julai 30, 2017 umezikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar amba mamia ya watu walijitokeza, ikiwa ni siku 47 tangu auawe kwa tuhuma hizo, ambazo familia ya marehemu imezipinga vikali mahakamani kuwa ndugu yao hakuwa jambazi na kulitaka Jeshi la Polisi kukiri kosa.

Mwili wa Denti huyo wa UDSM uligomewa kuzikwa na ndugu zake kwa madai kuwa aliuawa kimakosa kwa kudhaniwa ni jambazi aliyetaka kupora fedha kwenye ATM iliyopo maeneo ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar. Mwili wa Marehe,mu uliswaliwa katika Msikiti wa Kichangani, Magomeni, Dar mara baada ya swala ya Ijumaa. Hapa chini nimekuwekea picha 12 za msafara kuelekea makaburini.

VIDEO: Familia yasusia maiti jeshi la Polisi Dsm

Kuanzia Leo Mashoga na Wasagaji Ruksa Kuoana Katika Nchi Hii

$
0
0
Wabunge nchini Ujerumani wameidhinishwa, kwa wingi wa kura, sheria ya kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Wamefanya hivyos iku chache baada ya Kansela Angela Merkel kuondoa upinzani wake dhidi ya mpango huo.

Chini ya mabadiliko hayo sasa, wapenzi wanaotaka kuoana ambao awali walikubaliwa tu kuwa na ushirika, hadhi ya ndoa kamili na wana haki ya kuasili watoto.

Wapinzani wa Bi Merkel kisiasa walikuwa wanaunga mkono sana hatua hiyo.

Lakini kansela huyo, ambaye alionekana kuunga mkono kufanyika kwa kura hiyo Jumatatu, alipiga kura ya kupinga.

Mswada huo uliungwa mkono na wabunge 393, 226 wakaupinga na wanne wakasusia.

Sheria nchini Ujerumani sasa itasoma: "Ndoa inafanikishwa na watu wawili wa jinsia tofauti au jinsia moja," shirika la habari la AFP limeripoti.

Baada ya kura hiyo ya Ijumaa, Bi Merkel amesema kwamba kwake ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke.

Lakini amesema anatumai kwamba kupitishwa kwa mswada huo kutafanikisha "utangamano zaidi wa kijamii na amani".

Wakati wa kampeni 2013, Bi Merkel alisema kwamba anapinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja, kwa msingi wa "maslahi ya watoto", alkini akakiri kwamba amekuwa na wakati mgumu kuhusu suala hilo.

Msanii Bobi Wine Ashinda Ubunge Nchini Uganda

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu kama, Bobi Wine ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo nchini humo.

Tokeo la picha la bobi wine
Bobi Wine mwenye suti katikati akikabiliana na Askari Polisi mapema wiki hii

Wine, ambaye aliwania kama mgombea huru, aliwashinda wagombea wenzake wanne katika jimbo la Kyadondo Mashariki mwa Uganda kwa ushindi wa kura 25,659 kati ya kura elfu  33,310 zilizopigwa.

Kwa mujibu wa Gazeti la New Vision la nchini humo limeeleza kuwa baada ya kutangazwa Gazeti hilo linasema baada ya kutangazwa kuwa mshindi, aliahidi kurudisha umoja na mshikamano jimboni humo.

“Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki…Ninataka siasa zitulete pamoja… jinsi muziki ufanyavyo.“amesema Bob Wine.

Mwanamuziki huyo mapema wiki hii alikamatwa na polisi na kuhojiwa kwa muda kabla ya kuachiwa huru.

Kiti hicho cha ubunge kiliachwa wazi baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha FDC Kizza Besigye amempongeza mwanamuziki huyo kwenye kupitia ukurasa wake wa Twitter.


obi Wine alianza muziki mapema miaka ya 2000 kabla ya kujitosa kwenye siasa uchaguzi mkuu mwaka 2016 na ngoma ambayo ilimfanya ajizolee umaarufu nchini humo ni wimbo wake wa Situka.

Kwenye wimbo huo, anatoa wito kwa raia wa Uganda kuchangia katika vita dhidi ya rushwa na ukiukaji wa haki nchini mwao.

Wema Sepetu Aanza Kuimba Bongo Fleva

$
0
0
Imebainika kuwa msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu ameamua kuingia kwenye muzuki wa Bongo Fleva.

Prodyuza kutoka MJ Records, Daxo Chali ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa Wema Sepetu ameshiriksha katika wimbo wa Haitham ambao unatoka kesho, na kubainisha kuwa Wema ni muimbaji mzuri.

Daxo ameeleza kuwa awali alitaka wimbo huo afanye mwenyewe Haitham na ulipokamilika aliona kuna haja ya mtu mwingine kuwepo katika ngoma hiyo ingawa alisita kutokana Haitham wimbo wake wa kwanza alimshirikisha Mwana FA hivyo watu wataona anabebwa lakini alipokaa na kuweza aliona Wema anafaa ndipo wakamtafuta.

“Kuna siku kweli akaja, so tukamuingiza studio tukamuonyesha mashairi aingize wala hakusumbua, kwanza Wema anajua kuimba sema watu wengi hawajui ilo suala ila kitu kilichokuwa kinamsumbua sana ni zile melodi kwa sababu ile ngoma ni ya kiswahili lakini imeimbwa kama kifaransa, so ndio kitu kilichokuwa kinamsumbua sana ni kutamka yale maneno  lakini kwenye kukaa kwenye key yupo vizuri sana,” amesema Daxo.

Inawezekana Kupata Mume au mke Mzuri Kupitia Facebook?

$
0
0
Katika safari ya mapenzi wanandoa huwa wanakutana katika maeneo mbalimbali, wapo wanaokutana vyuoni,shuleni, kwenye nyumba za ibada, sokoni, kwenye daladala, kuunganishwa na mtu mwingine, au baada ya kusikia sauti kwenye simu, redioni, hotelini na sasa wengine kupitia mitandao ya kijamii kama facebook

Ukweli ni kwamba katika mitandao unapoanzisha uhusiano na mtu usiyemfahamu inawezekana ameona picha yako tu nakukuambia kuwa anakupenda na wewe ukiona picha yake ukaridhika naye mkaamua kuanzisha uhusino ni vyema kuonana kabisa ili kuwa na uhakika na uhusiano mnaotaka kuanzisha  kwani unahitaji kumfahamu zaidi  na ndipo utakapoweza kufanya maamuzi ya kukubali au kukataa.

Anaweza kuwa rafiki yako wa kawaida lakini uhusiano ukaja baada ya kuonana mkafahamiana zaidi, kwani ukikurupuka na kutaka kuoana haraka haraka na yule ambaye mna chat tu kwenye mitandao unaweza kujikuta unajuta baadaye kwa maamuzi yako ni vyema kufahamiana zaidi ya kuchat ili kuwa na uhakika na maamuzi yako.

Ndugai Ajibu Hoja ya Bunge Kuitwa "Dhaifu"

$
0
0
Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amefunguka kuwa wabunge wanaodai kuwa bunge ni dhaifu basi ni wazi watakuwa na mambo yanawasumbua ndio maana wanatoa kauli za kudhihaki chombo hicho.

Mhe. Ndugai amesema hayo leo mjini Dodoma baada ya kuwepo kwa baadhi ya wabunge wanaotoa kauli zisizokuwa rasmi katika vikao vya bunge bila kufikiria kwamba wanachokifanya hakina taswira nzuri kwa wapiga kura wao pamoja na kwa serikali kwa ujumla.

"Yupo mwenzetu alisimama hapa na kulalamika kuwa bunge hili ni dhaifu, kwa maoni yangu hizi ni lugha za kuudhi kwa sababu wenzako wengi namna hii waliochaguliwa na watu wakaletwa hapa halafu wewe unawaona kwa wingi wao ni dhaifu haipendezi. Unajua sisi tunaokaa hapa mezani hatuchangii kama nyinyi, kazi yetu ni kuwapa nafasi  mseme, wakati mwingine zinatoka shutuma ambazo hatuna nafasi ya kubishana au kulumbana lakini wakati mwingine ni vizuri kutumia fursa hizi kusafisha baadhi ya mambo. Binadamu ni lazima uwe na staha ile ndogo tu kuwaheshimu binadamu wenzako," alisema Ndungai

Pamoja na hayo, Ndugai ameendelea kwa kusema "Katika bunge letu kinacholeta matatizo humu ndani ni tabia na lugha, tukirekebisha hayo mawili tutaenda vizuri tu lakini najua kundi hili ni kubwa hatuwezi kuwa wote tupo sawa, nitaendelea kulisemea lakini pale kwenye ulazima tutachukua hatua," alisisitiza Ndugai.

Meya wa Ubungo Dsm, Amefanya Uzinduzi Huu Jana

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ya petroli ambayo imeshuka kwa asilimia moja ukilinganisha na bei iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.

Kuanzia kesho, bei hizo zitashuka na kuuzwa kwa Sh37 kwa lita (sawa na asilimia 1.81 wakati dizeli itauzwa kwa Sh 14 kwa lita (0.73 asilimia). Mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 19 kwa lita (sawa na asilimia 1.03)

Ukilinganisha na bei zilizotangazwa mwezi Juni, nishati hizo zitapungua pia katika bei ya jumla.

Kwa bei za jumla, mafuta ya petroli yamepungua na sasa yanauzwa kwa Sh 37.21 kwa lita(sawa na asilimia 1.92)na dizeli itauzwa kwa Sh 13.70 kwa lita(sawa na asilimia 0.77) na mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 18.85 (sawa  asilimia 1.10)

Punguzo hilo la bei linatokana na kushuka kwa bei ya mafuta katka soko la dunia.

Hata hivyo Ewura imetangaza kuwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mkoa wa Tanga itapanda ukilinganisha na ile iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.

Kwa bei ya rejareja, petroli itapanda kwa Sh 43 kwa lita na dizeli itauzwa kwa Sh 4 kwa lita.

Kwa bei ya jumla, petroli mkoani Tanga imeongezeka na sasa itauzwa kwa Sh 43.07 na dizeli itauzwa Sh 3.81 kwa lita.

Ongezeko la bei ya mafuta kwa mkoa wa Tanga linatokana na kuongezeka kwa bei katika soko la dunia kwa shehena iliyoingizwa bandari ya Tanga ukilinganisha na bei ya shehena iliyopokewa Aprili 2017.

Uchapa Kazi wa RC Anna Mghwira Wamgusa Waziri Mkuu

$
0
0
Mrembo aliyewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania mwaka 2014 na kushinda kisha kupokwa taji hilo, Sitti Mtemvu (Sitti), ameibuka na kuweka wazi kwamba alikuwa kimya muda mrefu kwa kuwa alirudi masomoni nchini Marekani kwa ajili ya kusaka cheti.


Sitti alisema wakati Rais Magufuli alivyoagiza wasio na vyeti wachunguzwe, aliamua kurudi chuoni nchini Marekani kwa ajili ya masomo na kupata vyeti kwa ajili ya kumsaidia kuendesha harakati alizokuwa amezianzisha baada ya kupokwa taji la Miss Tanzania kwa madai ya kudanganya umri mwaka 2014.

Sitti, ambaye alifanikiwa kushinda taji hilo kisha ushindi wake kutenguliwa na kupewa aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa, kimya chake cha muda mrefu kitafikia kikomo hivi karibuni, atakapoendeleza harakati zake, ikiwamo uandishi wa kitabu chake cha Chozi la Sitti ni Kampuni yake.

“Kimya changu kwa muda mrefu ni kutokana na kurudi masomoni Marekani kisha kupata vyeti, lakini kwa sasa nimeshamaliza na mambo mbalimbali yataendelea, ikiwamo uzinduzi wa taasisi yangu ya Sitti,” alisema Sitti.

Bei ya Petroli, Dizeli, Mafuta ya Taa zashuka

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji, (EWURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ya petroli ambayo imeshuka kwa asilimia moja ukilinganisha na bei iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.

Kuanzia kesho, bei hizo zitashuka na kuuzwa kwa Sh37 kwa lita (sawa na asilimia 1.81 wakati dizeli itauzwa kwa Sh 14 kwa lita (0.73 asilimia). Mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 19 kwa lita (sawa na asilimia 1.03)

Ukilinganisha na bei zilizotangazwa mwezi Juni, nishati hizo zitapungua pia katika bei ya jumla.

Kwa bei za jumla, mafuta ya petroli yamepungua na sasa yanauzwa kwa Sh 37.21 kwa lita(sawa na asilimia 1.92)na dizeli itauzwa kwa Sh 13.70 kwa lita(sawa na asilimia 0.77) na mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 18.85 (sawa  asilimia 1.10)

Punguzo hilo la bei linatokana na kushuka kwa bei ya mafuta katka soko la dunia.

Hata hivyo Ewura imetangaza kuwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mkoa wa Tanga itapanda ukilinganisha na ile iliyotangazwa Juni 7 mwaka huu.

Kwa bei ya rejareja, petroli itapanda kwa Sh 43 kwa lita na dizeli itauzwa kwa Sh 4 kwa lita.

Kwa bei ya jumla, petroli mkoani Tanga imeongezeka na sasa itauzwa kwa Sh 43.07 na dizeli itauzwa Sh 3.81 kwa lita.

Ongezeko la bei ya mafuta kwa mkoa wa Tanga linatokana na kuongezeka kwa bei katika soko la dunia kwa shehena iliyoingizwa bandari ya Tanga ukilinganisha na bei ya shehena iliyopokewa Aprili 2017.

EXCLUSIVE: Fahamu Mambo 8 kuhusu Train za umeme zinazoletwa Tanzania

$
0
0
Rais JPM April 12, 2017 alizindua ujenzi wa reli ya kisasa ‘standard gauge’ kutoka DSM hadi Mwanza ambayo itakamilika Oct 2019 jambo lililozua gumzo kwa baadhi ya Wananchi wakiwa na wasiwasi kuhusu train hizo kutokana na tatizo la umeme.

Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Mhandisi wa Miundombinu ya Reli ambaye pia ni Mkuu wa Mradi huu Maizo Mgeni kutoka Kampuni inayojihusisha na ujenzi wa reli Tanzania RAHCO na kuelezeea mambo makubwa manane yanayohusiana na Standard Gauge.

Mambo manane hayo ni:

1: Treni itakuwa inasimama kwenye vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo itasimama Pugu, Soga, ruvu, Stesheni ya Ngerengere na mwisho Treni itasimama Morogoro.

2: Kutokana na Treni kutumia umeme Serikali imejipanga kutoa umeme wa uhakika kwa 100% na wananchi wasiwe na shaka yoyote kwani umeme wa Treni hujengewa nyaya zake maalum zinazotofautiana na nyaya za umeme wa kawaida.

3: Treni hii itakuwa na uwezo wa kusafirisha wagonjwa mahututi kwani ni za kisasa na zina mwendo wa haraka ambapo itatumia saa moja na nusu kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam.

4: Umeme utatumia vyanzo vyenye nguvu kutoa umeme wa Treni kama vyanzo vya maji na makaa ya mawe.


5: Kwa tathmini ya sasa nauli ya Treni hizi haitokuwa sawa na Treni za mita kwani ni Treni zinazotumia teknolojia kubwa na za kisasa, hivyo nauli itakuwa juu zaidi ya Treni za kawaida.

6: Treni haitosimama kama umeme kutoka Tanesco ukikatika ghafla.

7: Kiwango cha nauli kwa wanafunzi bado kinafanyiwa kazi.

8: Kwa sasa watu binafsi hawataruhusiwa kuwa na Treni binafsi kwani Shirika la Reli ndilo litakuwa msimamizi mkuu.

Miujiza ya Maalim Khatibu Kutoka Kigoma Kusini Sasa Yupo Bagamoyo Mkoa wa Pwani...

$
0
0
MIUJIZA YA MAALIM KHATIBU KUTOKA KIGOMA KUSINI SASA YUPO BAGAMOYO MKOA WA PWANI.

Wengi wamepata tiba na kutatuliwa MATATIZO yao wewe unasubiri nini?

✨Kwanini umapata pesa haikai? Na haufanyi kitu cha maana?
✨Kwanini mapenzi yakutese?
Kwanini uachwe na Mke! Mme au mpenzi wako?
✨Kwanini hamuelewani katika familia yenu kwaaji ya kugombea mali?

Majibu yote utayapata kwa MAALIM KHATIBU, mwenye kubri kubwa kutoka kwa Allah,✔

MAALIM KHATIBU ni mtaalamu wa tiba mbalimbali za asili na nimtambuzi wa nyota za binadamu, pia nimtatuzi wa matatizo yote yanayo watesa binadamu,

MAALIM KHATIBU anatibu kwa kutumia kitabu cha quran dawa za asili dawa za kiarabu, na majini, Anakuvutia mpenzi alie kuacha au alie mbali, anazo dawa za mapenzi, nguvu za kiume, chango kwa kina mama, ngiri maji na n.k, anakuvutia mali zilizo potea au kudhulumiwa, pia anatoa Pete za bahati zilizoambatanishwa na jini mali, Wenye matatizo ya uzazi, jini mahaba, mapepo ya kichawi, vifungo vya kimaisha, ndoto mbaya za usiku, uelewa mdogo wa ufahamu shuleni kwa watoto wote, pia anauwezo mkubwa wa kumaliza kazi zilizoachwa na wataalamu wengine ndani ya masaa 48 tu,Pia anatibu kwa njia ya simu popote ulipo.

WASILIANA NAE KWA SIMU NA WhatsApp
Tigo - No:+255 710 -332103
Voda - No:+255 766-705404,
Insta follow @maalim_khatibu

USHAURI: ni vyema kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate huduma kwa haraka.

Fahamu Matumizi ya Overdrive (OD) Kwenye Magari ya Automatic

$
0
0
Overdrive (OD) ni gia katika mfumo wa gari ambayo huifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi. OD hukupa mwendo wa kasi, uliotulia lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (revolutions per minute rpm). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Overdrive ni kama gia ya ziada inayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya injini yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo, maana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya injini.

Mfano katika gari ya kawaida yaani 180km/h ili ufikishe spidi 120 basi RPM inaweza ikawa 4000rpm katika barabara ya tambarare. Lakini ukiweka overdrive unaweza kutembea spidi hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara ya tambarare.

Utatambuaje kama Overdreive (OD) ipo on au off?

Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako, inamaanisha kuwa overdrive ipo off na pindi kitaa hicho kisipoonekana basi tambua kuwa overdrive ipo on. Overdrive imewekwa kama chaguo (option) la kutumia wakati ukiwa unatembelea spidi chini ya 60km/h.

Unaweza kutumia ukiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalani kwenye milima ambapo gari yako inakuwa imepunguza nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4) na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukishamaliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la gari lako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa gari pia.

Katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa gari, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea gari kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lililopasuka, nikiwa na maana kwamba hapo gari itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au on na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gia kubwa na mwendokasi chini ya 60km kwahiyo unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa.
-Mwananchi

Nahisi Mke wangu Anawapenda Kimapenzi Wanawake Wenzake

$
0
0
I think my wife likes women
------------------------------------
I would like to know if there are other men out there who think their wives are into women? I think mine is. I went through her Phone the other day and I couldn't believe the Whats app chat I read between her and someone I thought was just her friend. Another married woman for that matter. Their chat was of a sexual nature, something you would expect between a man and a woman. This lady even sent photos of her boobs and private parts to my wife.
I eventually confronted my wife about it and she said they were just joking around. Who jokes around with p**sy photos? What should I do now?

LMAO at who jokes around with vag*na photos. No, nobody does! So what should he do, other than ask for a three.some? Lol. *kidding*

Tazama Diamond alivyo Copy Na Ku-Paste Video ya Jason Darulo

$
0
0
SOKO la nyimbo katika dunia ya sasa linakuzwa na video za muziki, ubora wa video umekuwa ukichangia kuufanya wimbo kuwa mkubwa hata kama ni wa kawaida.

Kuna vitu vingi vinavyochangia video kuwa bora, baadhi ni ubora wa picha, ubora wa mandhari na ubora wa ubunifu wa kile kinachoonekana katika video husika.

Msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz anajulikana kwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye kutengeneza video zenye kiwango cha juu, hilo halina ubishi.

Pamoja na sifa hizo, imekuwa ni kawaida kuona Diamond akiiga matukio kadhaa ya video za wasanii wa Marekani na kuziingiza kwenye video za nyimbo zake.

Mfanano wa video au jambo lolote ni kitu cha kawaida lakini kuna mazingira ambayo yanaweza kumfanya mpaka shabiki au mtazamaji wa video akaelewa kuwa hakuna mfanano wa bahati mbaya bali ni makusudi.

Jinsi Bilionea wa IPTL-Tegeta Escrow Alivyonaswa Airport Akitaka "Kutoroka"

$
0
0
Haikuwa ajali, pesa ya ESCROW kupita katika bank ya kanisa katoliki, mgawo kuwafikia mapadre na maaskofu,mawaziri na vigogo wa kila namna katika nchi hii. Ili siku inapobumburuka, basi msururu wa watu ujumuishwe na kuwe na "aibu" ya kuwakamata wote waliohusika.

Harbinder Singh aliitumia njia hii pia,alijenga vituo vya polisi,alikarabati nyumba za viongozi na kuwajengea "mabangaroo" wale aliohisi watamsaidia kuukwepa mkono wa dola.Alinunua pikipiki za doria za polisi,alichangia vifaa na pesa katika mahitaji ya ziada ya jeshi letu la polisi (ushahidi wa picha upo)

Pale Airport ya Dar es Salaam,kuanzia kaunta za VIP mpaka kwenye mlango wa ndege wakati wa kuondoka,wahudumu wote na wafanyakazi walijua leo Singasinga anarudi au anaondoka.Kila alipofika Singasinga au kuondoka,aliachia "tips" bila hiyana. Kuanzia kwa askari wa uhamiaji,check in counter,polisi wa Airport,mbeba mabegi,dereva wa gari la VIP mpaka mfagizi,aliinusa pesa ya singasinga.

Hii ndio maana, Singasinga kabla ya kukamatwa, alishapenyezewa taarifa kuwa anatafutwa kwa muda mrefu ili aweze kukamatwa sababu faili la ESCROW lipo juu ya meza ya "mkuu" na ameagiza kesi ianze ila tu ni lazima hawa wahusika wawili akiwemo singasinga wakamatwe.

Siku ya Ijumaa tarehe 16/06/2017,Seth alikuwa aondoke na ndege ya shirika la ndege la South Africa,flight number SA187 inayotoka Dsm kuelekea Orival Reginald Tambo International Airport,iliyotarajiwa kuondoka saa 1535(masaa ya Afrika Mashariki).Afrika Kusini ndiyo yalipo makazi ya Seth baada ya kupata mgogoro wa kifisadi na kupata shida ya kuishi Nairobi Kenya,alihamia huko Afrika Kusini.

Siku kadhaa kabla ya safari yake ya "ghafla" ya kwenda South Africa,watu kadhaa wa "mfumo" waliokuwa wanapitiwa na mgawo wa Seth, walimtonya mpango wake wa kukamatwa na kufikishwa mahakamani. Kama kawaida yake, Seth alipitisha mgawo kuhakikisha suala hilo halitokei, kuanzia yule wa chini mpaka wa juu, kila pesa ilipokuwa inamfikia, aliikimbia kwa hoja kuwa "siku hizi sio kama zamani", wote tutakwenda na maji.

Mpaka Ijumaa asubuhi,Harbinder na wapambe wake wakawa wamegonga mwamba katika kila kona walizopita ili kuzuia kupelekwa mahakamani,suluhisho alilopewa na watu wa "mfumo" ambao walikuwa "watii" kwake sababu ya mgawo,ni kuondoka haraka nchini na kukimbilia Afrika Kusini mpaka pale mambo yatakapotulia kama zamani.

Majira ya saa nane mchana,Seth na mwanamke mmoja,walifika eneo la VIP Terminal II tayari kwa safari ya kwenda nje ya nchi ili kukwepa mkono wa mfumo. Eneo la VIP Terminal II hutumiwa na wageni mashuhuri wanaotoka au kuingia ndani ya nchi, Marais, Wabunge,Wawaziri na viongozi wengine wa hadhi ya juu na wafanyabiashara wakubwa hupitia lango hili kwa safari zao.

Seth alikamilisha taratibu zote za safari,kama kawaida yake "tips" za "kimyakimya" zilianzia mlangoni anapoingia na VIP lounge. Kilichomstua kwa haraka ni baadhi ya "tips" zake kukataliwa na baadhi ya wahudumu,alipotoa wengine waliishia kusema tu "Asante".

Taarifa zilishafika mahali husika,kuwa Singasinga yupo Airport tayari kwa safari,akiwa na "boarding pass" mkononi na muda wowote ataingia kwenye ndege tayari kwa safari.

Bila kutarajia,wakati amevuka vihunzi vyote,akiwa anajongea kuingia katika gari la VIP,linalotumika kuwatoa wageni wa VIP eneo la VIP Lounge kuelekea kwenye ndege,ghafla ikatokea gari nyingine,kutoka mahali kusipoeleweka,likiwa limepitia mlango wa dharula na kusimama mkabala na lango la kutokea VIP lounge.

Palepale Harbinder akaamuliwa kuingia kwenye gari hilo lililokuwa na vioo vya giza,na kuachana na benzi la VIP VAN lenye maandishi ya kampuni ya Swissport kwa pembeni,mara moja gari ikageuzwa na kupelekwa kusikojulikana,mpaka mapema Jumatatu,Seth na Rugemalila walipoibukia mahakama ya Kisutu tayari kwa kusomewa mashitaka ya Escrow.

Mchezo wa kumkamata Harbinder hakuwa mdogo,hii ni kwa sababu kwa muda mrefu Harbinder amekuwa anawatumia viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kukwepa mikono ya dola pale anapotakiwa ama kuhojiwa au sakata lake kuibuliwa bungeni.

Safari yake ya kukamatiwa Airport akiwa tayari kuingia kwenye gari kuelekea kwenye ndege,ni matokeo ya kuvujishiwa siri kuwa anatafutwa na anatakiwa kukamatwa,hivyo uwezo wa kuizima kesi haupo zaidi ya yeye kutoroka.

Hii inatupa picha,jinsi ilivyo ngumu kwa kazi hii ya kupambana na "mapapa" aina ya Singh.Inatukumbusha kauli ya Waziri Mkuu Pinda aliposema kuwa,hawa "mafisadi" wana nguvu sana,ukiwakamata nchi lazima itikisike.

Na hakika,kukamatwa kwao,nchi imetikisika,kuanzia Kanisa Kuu la Bukoba alipo Askofu Kilaini mpaka St.Joseph Cathedral Dsm alipo Askofu Nzigilwa.Parokia ya Bikira Maria wa Rozari Makongo Juu anaposali James Rugemalila mpaka makao makuu ya bank ya Mkombozi hali si shwari.

Viunga vya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nako ni tumbo joto,kuanzia kwa mwenyekiti wa Bunge na baadhi ya wabunge hali si shwari,ofisi za RITA na Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali ni matumbo joto.

Isingelikuwa mkwara wa Magufuli,Harbinder Singh angetutoroka mchana kweupe,na watu wangejiuliza,inakuwaje mahakamani tunamuona James Rugemalila peke yake?Kuna mambo JPM yanamshinda,ila kuna mengine anaamua kiasi unasahau hata yale aliyoharibu.Kumkamata Seth haikuwa kazi ndogo,alinyakuliwa wakati abiria wengine wameshaingia ndani ya ndege,akisubiriwa yeye tu wa VIP.

Hili la Escrow tukipita salama na kushinda,tumshukuru Mungu na tumpe pongezi Rais bila itikadi.Anakumbana na nguvu kubwa sana inayomsaliti katikati ya mapambano,kuna wachache wanauza "ramani ya vita" kwa adui.

By Barafu/Jamii Forums

Ndugai: Hamna Cha Kesi, Mimi Ndio Spika Watakaa Benchi Mwaka Mzima

$
0
0
Mahakama zetu zimeendelea kudharaulika baada ya leo bungeni spika ndugai kusema wabunge waliosimamishwa vikao mwaka mzima wanakimbia kimbia tu hakuna cha kesi mimi ndio Spika.
Nimejiuliza,Ndugai anahakika gani kama mahakama itaamua tofauti na maamuzi yake ya kuwasimamisha mwaka?

Je,Ina maana Ndugai anauwezo wa kuingilia maamuzi ya mahakama mpaka kujipiga kifua hamna cha kesi?"Na kejeli"

Kauli kama hizi endapo mahakama itaamua kuendana na majigambo ya Spika ndugai hata kama maamuzi yake yatakuwa ya haki,zinapunguza imani ya wananchi kwa mahakama zao.Lazima mahakama ijipange la sivyo hadhi yake inaweza kuporomoka kabisa.

By Kibo10

Unaambiwa FIFA Bado Hawajaamini Kilichotokea Kwa Rais wa TFF Tanzania, Wameamua Kufanya Jambo Hili

$
0
0
Shirikisho la soka Duniani FIFA litatuma wajumbe wake kwa ajili ya kuja kufanya uchunguzi juu ya kinachoendelea ndani ya TFF, hatua hiyo ya FIFA imefikiwa baada ya viongozi wa juu wa TFF Rais Jamal Malinzi na Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa kupandishwa kizimbani kusomewa mashtaka yanayowakabili ikiwemo utakatishaji fedha.

Makamu wa rais wa TFF Wallace Karia amethibitisha kupokea taarifa ya ujio wa wajumbe wa FIFA nchini kwa ajili ya kufanya kiko cha pamoja.

“Wenzetu wa FIFA wametupigia walihitaji namba zangu kwa hiyo tutaongea nao lakini pia tutafanya kikao cha kamati ya utendaji wakiwemo wajumbe wa FIFA ambao watatumwa ili tuweze kufanya tathmini jinsi hali ilivyo na kutoa maamuzi ili mpira uendelee na maisha yaweze kuendelea.”

“Tumeona tuwashirikishe wenzetu wa FIFA kwa sababu kuna hali ya sintofahamu imeanza kuwepo kwa hiyo ni vizuri kuangalia katiba ya TFF inazungumza nini na ikiwezekana tuende katika utaratibu mzuri kwa hiyo tutafanya kikao cha FIFA na tunategemea tukifanye Jumanne, kama Rais wetu atafanikiwa kupata dhamana tunatarajia awepo kwenye hicho kikao.”

“Baada ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutoa habari kuhusu Rais na Katibu kushikiliwa walipiga simu wakiwa na taarifa kwamba wote tuko ndani, wakamtafuta mtu ambaye katiba inamtaja kwamba atakuwa anaendeleza shughuli za ofisi, kwa hiyo wamepewa namba yangu nasubiri mawasiliano nao na wanataka kuja ili tuwe na kikao cha pamoja.”

“Katiba ya TFF inasema Rais anapokuwa hayupo, makamu wake ndio anaendea kuongoza vikao na kila kitu kama makamu pia hayupo, mjumbe wa kamati ya utendaji ambaye amekaamadarakani  kwa muda mrefu atakuwa kiongozi wa taratibu zote.”

“Kikao chetu cha kesho leo tutaangalia ni jinsi gani tutaweza kumkaimisha ukatibu mmoja wa wafanyakazi wa hapa ili shughuli za taasisi ziweze kuendelea.”

Malinzi na Mwesigwa watapandishwa tena mahakamani Jumatatu Juni 3, 2017 ambapo mahakama itatoa uamuzi kuhusu dhamana ya viongozi hao.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images