Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Serikali yamtuhumu Balozi wa Uingereza

0
0
 Serikali imetangaza rasmi mgogoro wa kidiplomasia kati yake na Balozi wa Uingereza nchini ikimtaka kujieleza kwa madai ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi.

Mgogoro huo ulitangazwa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Maselle aliyemtaka balozi huyo kufika Wizara ya Mambo ya Nje kujibu tuhuma hizo.

Kiini cha Serikali kumtuhumu balozi huyo ni hatua ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) kuihusisha Uingereza na urejeshwaji wa Sh76 bilioni za chenji ya Rada.

“Katika mchango wake (Kafulila), ameongea jambo moja nyeti sana na hili bora niliseme ili liwe fundisho kwa wengine… Hii ni nchi huru baada ya mwaka 1961,” alisema Naibu Waziri.

“Zimekuwapo ripoti kwamba Balozi wa Uingereza amekuwa akijihusisha kuratibu vikao mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam na Dodoma kinyume cha utaratibu na hadhi ya kidiplomasia.”

Huku akionyesha kuwa na hasira, Maselle aliongeza kusema: “Vikao hivyo vina malengo ya kuhujumu mipango na mikakati ya maendeleo, ushahidi huo upo na utakapohitajika utatolewa.”

“Inasikitisha na kuchukiza balozi wa taifa kama Uingereza akifanya vitendo kinyume cha maadili… Anahusishwa kushawishi marafiki wa maendeleo wasitishe misaada ya kibajeti kwa Tanzania,”alisema.

Balozi wa Uingereza

Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Balozi wa Uingereza Dianna Melrose, azungumzie suala hilo, msemaji wake Tamsin Clayton ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Siasa, Miradi na Mahusiano alisema wameshtushwa na taarifa hizo, lakini kwa sasa hawawezi kusema chochote mpaka wafahamu chanzo cha tatizo.

Aidha Naibu waziri Maselle alisema kuwa hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), alikuja Tanzania na kwamba upo ushahidi kuwa Balozi huyo wa Uingereza, alitamka kuwa anafikiria kuishawishi Serikali yake isitoe fedha za Miradi ya Maendeleo ya Millenia (MCC2).

“Ni aibu kwa Serikali ya Waziri Mkuu, David Cameron kwa balozi wake kufanya uwakala wa Benki ya Standard Chartered, kuishawishi Serikali ya Tanzania ikope fedha ili kulipa kampuni binafsi,” alisema Maselle huku akipigiwa makofi na wabunge wengi wa CCM na kuongeza:

“Rais Kikwete amelikataa kwa nguvu zote…, Serikali haiwezi kubeba mzigo wa kampuni binafsi.”

Shaa Naye Atupia Picha Akiwa Kwenye Bikini Kwa Mara ya Kwanza

0
0

Kama unam-follow kwenye instagram @Shaa_tz basi utakuwa umesha like au kuona jinsi comment na like nyingi zinazopata picha hizi.
Sarah Kaisi amepost picha mbili akiwa kwenye boti...
Any Comment?

Venessa Mdee Afunguka Kwanini Aliacha Kufanya Kipindi cha The One Show, Amtaja Marehemu George Tyson

0
0
Venessa Mdee hajawai kusema sababu ya kuacha kufanya The One show ambayo alianza hadi ku-shoot. Hivi sasa amesema sababu hiyo akimhusisha George Tyson kama mtu aliyempa moyo kwenye maamuzi yake
Soma Hapa Chini:

Mboni Afunguka Kuhusu George Tyson 'Yaani Zile Ahadi Zote Ulizonipa Kumbe ni za Uongo'

0
0
Kazi kubwa ya George Tyson ilikuwa ni ku-direct vipindi vya TV vya Mboni Show na Vingine vingi

TID adai kitu ambacho hawezi kukisahau kwenye maisha yake ni kwenda jela

0
0
Mnyama TID amesema kitu ambacho hawezi kukisahau katika maisha yake ni kwenda jela.
“In fact time ambayo nilipata fight nikaenda jela, I was down ,nimeenda jela , so it’s like falling down,” alikiambia kipindi cha XXL.

“Nilivyokuwa nimekaa kula jela and love ambayo nimepata kutoka kwa watu wa mule ndani lakini nimetoka mpaka leo am still shining, lakini ili ilikuwa down fall, Mungu amepanga this guy is an artist, tumembless afanye muziki, inspiration yangu ni kubwa sana, wasanii wengi ambao wamefanya kazi na mimi wamepata hata mafanikio in one way or another kabisa.”

Kwa upande mwingine muimbaji huyo amesema anatarajia kuachia album iitwayo ‘Chumvini’.

“Plan yangu hivi sasa tunatoa album ya Chumvini ,pia tunamaliza kushoot filamu, tumeanza kushoot baadhi ya scene ili tuzipresent kwa sponsor, we have a teaser, lakini tutaendelea kufanya vitu ambavyo tunatakiwa kufanya. Nashukuru ,ungu Jay Mo in the plan , na Jay Mo ni actor mzuri sana he is a comedian.”

Manchester United Yammendea Kiungo wa Real Madrid Kwa Dau La £25m

0
0
Klabu ya Manchester United ipo tayari kutoa kiasi cha £25million kwaajili ya kumsajili Angel Di Maria baada ya winga huyo kukiri anaweza kuiacha Real Madrid.

Kwa mujibu wa mtandao wa Merto Sport, maafisa wa Old Trafford wamemuweka Di Maria kuwa miongoni mwa wachezaji wa juu kwenye orodha ya majina ya wachezaji ambayo wanayafanyia kazi. Pia kwa mujibu wa ripoti za Hispania, United wapo tayari kutoa £25million na zaidi ili Di Maria aweze kutua Old Trafford.

Di Maria, ambaye alifunga mabao 11 na kuisaidia Real Madrid msimu uliopita amesema ana furaha kuendelea kuichezea Real Madri na pia anaweza kuiacha klabu hiyo.

Mhadhiri UDSM Ndio Rais Mpya wa Malawi

0
0
Kwa ushindi wa Profesa Mutharika katika kiti cha urais wa Malawi, anaongeza idadi ya jamii ya wasomi waliopitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ama wakiwa wahadhiri au wanafunzi, kwani alifundisha chuoni hapo mwishoni mwa miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Nje ya kazi za uhadhiri, Profesa Mutharika aliyebobea katika masuala ya sheria ambaye pia ni mwanasiasa mzoefu na mashuhuri, ameshika nyadhifa za uwaziri katika wizara mbalimbali zikiwamo Wizara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, nafasi aliyoishika hadi anaingia katika uchaguzi mkuu hivi karibuni.

Mbali ya Profesa Mutharika, wasomi wengine waliopitia UDSM na kufanikiwa katika ulingo wa kisiasa na hata kuwa marais au viongozi waandamizi katika nchi zao ni Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Rais wa zamani wa Zaire (sasa DRC) Laurent Desire-Kabila.

Aidha, Makamu wa Rais wa zamani wa Uganda, Eriya Kategaya alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kama ilivyo kwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan, John Garang.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye kwa sasa ni Waziri wa Sheria na Katiba, naye alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama ilivyo kwa Mawaziri wakuu watatu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba, Edward Lowassa na Mizengo Pinda.

Getrude Mongella, Rais wa zamani wa Bunge la Afrika ambaye pia alishika wadhifa wa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Wanawake Duniani uliofanyika Beijing, China mwaka 1995.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa sasa wa Tanzania,naye amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Watu wengine mashuhuri waliosoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni pamoja na mwanasheria Mkuu wa Kenya, Dk Willy Mutunga na Donald Kaberuka, Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ambaye ni raia wa Rwanda.

Mastaa Mbali Mbali Walipokuwa Hospitalini Wakisubiri Mwili wa Marehemu Tyson

0
0
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere, akiwasili katika Hospitali ya Kairuki kusubiri mwili wa marehemu. Steve alivalia tisheti yenye ujumbe 'Why always me'

Mke wa marehemu Tyson, Beatrice Shayo akiwa na simanzi wakati akiusubiri mwili wa mumewe.

Wema Sepetu akihojiwa na mwanahabari wakati wa kupokea mwili wa Tyson.

Mwigizaji Aunt Ezekiel naye alikuwepo kupokea mwili wa Tyson.

Msanii wa filamu za Kibongo, Kelvin akihojiwa kuhusu alivyopokea taarifa za kifo cha mwongozaji filamu, George Tyson.
GPL

Movie ya Kibongo Ambayo Nimeangalia Nikatoa Machozi ni Hii Hapa , Wewe Je ?

0
0
Huyu Gabo Muuza Maji kwenye Hii Movie ni Kibako , Nimeipenda sana hii Movie Kuna Sehemu mpaka nimetoa Mchozi...Je wewe ni Movie Gani ya Kibongo Ambayo imewahi kukugusa?

Mtoto wa Miaka Mitatu Amuua Mdogo Wake kwa Risasi

0
0
Payson Ariz, mtoto wa kiume wa miaka mitatu amemuua mdogo wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu kwa kumpiga risasi.

Mtoto huyo alimuua mwenzake baada ya kukuta mfuko wa silaha hiyo katika chumba cha jirani na kwenda nao katika chumba kingine kabla ya kumfyatulia risasi mdogo wake.

Mkuu wa Polisi wa Jimbo la Arizona, Don Engler alisema uchunguzi wa idara yake kuhusu tukio hilo lililotokea Jumanne wiki hii, utachukua wiki moja, huku matokeo yakipelekwa katika ofisi ya mwanasheria iwapo kukiwa na mashtaka yoyote.


“Kitakachoangaliwa zaidi ni kuhusu utunzaji silaha kwa usalama zaidi na namna watoto hao walivyoweza kuibeba silaha hiyo ikilinganishwa na uzito wake, sisi tunaendelea na uchunguzi wetu,” Don aliliambia Shirika la Habari la Associated Press.

Alisema kuwa ni mapema kueleza mapendekezo ya idara yake, lakini anapisha uchunguzi ufanye kazi yake.

Wavulana hao pamoja na mama yao walikuwa wamemtembelea jirani yao mwenye umri wa miaka 78 katika jengo analoishi, kabla ya mlio wa risasi kusikika kwenye chumba cha kulala cha mzee huyo. Mtoto aliyempiga mwenzake risasi alikutwa akiwa ameshikilia bastola hiyo, huku akiendelea kushangaa kilichotokea

Mama Mzazi Wa Zitto Kabwe Amafariki Dunia Baada ya Kuugua kwa Muda Mrefu

0
0
Siku ya Leo Mbunge Zitto Kabwe Amempoteza mtu muhimu sana katika Maisha yake ambaye ni Mama yake Mzazi aliyekuwa Akimuuguza Muda Mrefu sasa, Zitto Ameconfirm kupitia ukurasa wake wa Facebook na Kuandika hivi:

"My mother has just passed away. Inna lillah wainna illaih raajiun"
RIP

Breaking Newzz: Masikini! Yule mtoto aliyefichwa Ndani ya Boksi kwa Miaka 4 Afariki dunia

0
0
MTOTO Nasrah Rashid (4) aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki dunia. Nasrah alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake mzazi kufariki. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Ommy Dimpoz Amefunguka na Kudai Kuwa Mitandao ya Kijamii Imempa Mchumba

0
0
Ommy amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa yeye na msichana huyo waliweza kukaa kwa muda wa mwaka mmoja wakichati bila kuonana.

“Social network zilisaidia kutuunganisha lakini matokeo yake mpaka tukaja kuonana. Mpaka nikaja kwenye tour tukaonana, si unajua kuna zile mzee unashangaa ma Instagram mtoto ka like picha kama tisini hivi, halafu ukichekecha unaona mbona kama umechorwaee ,bahati nzuri ilipoanzishwa instamessage kwahiyo kama unajiiba hivi. Ni Mtanzania, mpaka kuonana ilichukua kama mwaka, tumechat tumechat mpaka ikafikia time, sina haraka kwanini niwe na haraka, kufahamiana kunakuja automatically,” alisema.

“Unajua mambo ya mapenzi Mungu mwenyewe ndio anajua, pengine wengine anaweza wewe ukawa muuza mkaa demu akaja kununua mkaa. Lakini lile kopo unavyolishika kimachejo wakati wa kupima yeye anapenda ule upimaji wako, kwahiyo kuna kitu kama hivyo haijalisha mnakutana wapi, ikiwa tu mmewekea mipaka yenu, masharti hivi na hivi maisha yenu yanaenda.”

RAY C Alitamani Penzi la Babu Kizee…Adai Kuchoshwa na Vijana

0
0
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu, na kama ikitokea basi atamtaka kuwa na miaka kuanzia 60.

Akizungumza katika kipindi cha ‘The Sporah Show’, Ray C alisema anahitaji wanaume wa umri mkubwa, kwa kuwa wanajua wanachokifanya, na kukiri kwamba vijana walichangia katika kurudisha nyuma maisha yake.

Msanii huyo ambaye kwa sasa ameanzisha asasi yake ya kupambana na dawa za kulevya, kutokana na yeye kuwa mmoja wa waathirika wa dawa hizo, alisema katika moja ya mambo anayoyajutia ni kuwa na mahusiano na vijana, jambo ambalo hataki kukumbuka walichomfanyia hadi kudhalilika mbele ya jamii.

Hata hivyo, alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi kutowatenga watoto wao ambao wamejidumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya na badala yake, wawakumbatie na kuwaonyesha njia kama mama yake alivyofanya na kurudia hali yake ya kawaida.
Kuhusu kurudi kwenye muziki, Ray C alisema yupo mbioni na tayari ameshatengeneza nyimbo kadhaa, ambapo hivi sasa atakuwa akiimba miondoko tofauti tofauti, ikiwemo taarabu.
Katika kurudi kwenye muziki, jambo la kwanza alisema anatarajia kupunguza mwili wake kwa kufanya mazoezi, kwani hata daktari wake alishamwambia anatakiwa kupungua kutokana na umri wake kutoendana na kilo alizonazo.
Alipoulizwa mwanamuziki ambaye kwa sasa anamkubali Bongo, Ray C alisema wa kwanza ni AT akifuatiwa na Recho kutoka Jumba la Kukuza Vipaji (THT).

Matokeo ya Tanzania vs Zimbabwe na Wafungaji Magoli – Ingia Hapa

0
0
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kuvuka hatua ya kwanza ya michuano ya kuwania kucheza michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani.
Stars leo ilikuwa inacheza Zimbwabwe kwenye mchezo wa marudiano baada ya kuwafunga Zimbwabwe 1- 0 uwanja wa taifa wiki moja iliyopita, kwenye mchezo huo Stars imefanikiwa kufuzu baada ya kulazimisha sare ya 2-2.
Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 28. 
Muda mchache baadae  Thomas Ulimwengu aliongezea Tanzania bao la pili dakika ya 46, kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe kusawazisha na kufanya matokeo 2-2.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki 2-2, na sasa Tanzania wanaingia hatua ya pili ambapo watacheza na Msumbiji.

Taarifa Rasmi ya Yanga Kuhusu Uenyekiti wa Manji na Kocha Maximo Hii Hapa

0
0
Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga umefanyika na kumalizika salama na furaha kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Yusuf Manji amewaongoza wanachama hai wapatao 1,560 kupitisha kipengele hicho kipya kwa ajili ya maslahi na faida ya Wana Yanga kwani bila kufanya hivyo timu isingeweza kuruhusiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Aidha katika mkutano huo Manji amewatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa usajili unaendelea kufanyika na nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi utakapokamilika basi wataweka wazi kila kitu.
Kuhusu nafasi ya Kocha Mkuu Manji amesema Kamati ya Mashindano imemkabidhi mapendekezo yao na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na Marcio Maximo aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania kuja kukinoa kikosi cha Jangwani.
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mama Fatma Karume aliongoza kikao cha waachama kilichomuomba Bw Manji kuendelea na uongozi ambapo mwenyeikti alitoka nje na kamati yake ya utendaji na pindi waliporejea walikubali ombi hilo na kusema watafuata taratibu za kikatiba.
Mwisho kupitia mkutano mkuu wa leo wa wanachama umeazimia kuwaongezea muda wa mwaka mmoja Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja na Makamu wake Clement Sanga ili waweze kukamilisha masuala ya katiba na kuweza kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya katiba kupitishwa na TFF.

Tabia Kumi Mbaya Ambazo Zinazokufanya Ushindwe Kutunza Hela na Kubaki Kulalamika Maisha Magumu

0
0
1.Unanunua nguo bila mpangilio..
Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na
nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.

2.Unanunua Viatu bila mpango.
Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea
chache zenye ubora ili zidumu.

3.Unatoa ofa bar bila mpango.
Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae
kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale
kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4.Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo
sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya
sh 7000 au 10000 ili uchati na marafiki Fb au
wasaap Huo ni ujinga. Badilika.

5.Unakopa hela banki na kununua vitu kama
simu ya milioni na gari ambazo sio productive.
Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini
kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi
Wa kuzalisha ndio ununue gari?

6.Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako
au hamuendani kivipato hivyo unajikuta
unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili
uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa
sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe
meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye
salary yako?? Zinduka.

7.Huna timetable ya kudumu ya maisha yako,
unajikuta unaburuzwa Tu na marafiki zako kwa
kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.
Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie
kikamilifu, usiburuzwe!

8.Una michepuko inayokutegemea wewe kwa
kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu
huzinduki. Badilika.

9.Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani
kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji
hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu.
Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila
anaekupiga mzinga unapigika.

10.Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au
mshahara wote kwenye wallet au handbag au
nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash
nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia
hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na
hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.
Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi
tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa
kufanya vitu vikubwa endelevu

Yako Namba Ngapi Hapo?

TAIFA STARS kicked out of hotel in Zimbabwe

0
0
Tanzania's national football team, Taifa Stars on Thursday was kicked out of the hotel they were booked in ahead of their crucial return leg against Zimbabwe this Sunday, it has been reported. 

This is because the Zimbabwe Football Authority (ZIFA) hosting the team, failed to pay their accommodation, broadcast journalist Ezra Tshisa Sibanda says.
"This is a disgrace and a total failure by those in charge of the football association. I wouldn't mind the players and technical staff deserting camp and going back to their clubs leaving Cuthbert Dube, CEO Mashingaidze and their board to play against Tanzania," said Sibanda.  (zimeye.org report).

The visitors were caught up in the cold war between ZIFA and Pandhari Hotels in what was a veryembarrassing incident. The Tanzanians, who checked into their hotel on Thursday, returned from their training session yesterday to find their rooms locked as the management wanted ZIFA to make a payment first.

ZIFA is believed to owe the hotel a substantial amount of money after the Warriors used the hotel as their camp in the past, while it has also hosted functions for the association.

The association's spokesman, Xolisani Gwesela, who was out of town sitting for his examinations, said he was not aware of the embarrassing incident and needed time to verify before he could comment.

Sinta Kaa Nimwamini Mganga Yoyote wa Mapenzi Baada ya Hili Kunitokea

0
0
Nakumbuka nilipokuwa darasa la 4 nilitokea kumpenda dada mmoja alikuwa anaitwa Rusi. 
Nilihangaika sana namna ya kumpata lakin nilikuwa naogopa kutongoza kipindi hicho. Ikabidi nimweleze kaka mmoja ambaye ni mkubwa kwangu kumbe naye domo zege akanishauri niende kwa mganga ili anipe dawa ya mapenzi.
Kipindi hicho hata hela sina sikuwa na uwezo wa kupata ikabidi nikaenda kweli kwa mganga. Yule mganga akaniambia dawa ipo lakin nmpe shilingi elfu 2.
Nikaumiza kichwa namna ya kuipata nikaona ngoja nimdanganye baba kuwa nmepoteza kitabu cha mwalim, nilipomweleza baba akanipa hyo hela nikaenda kumpa yule mganga naye akanipa dawa nikarudi nyumban.
Nikaanza kila asubuhi napaka ile dawa nikiwa naenda shule na namsubir huyo Rusi tunaongozana huku nikisubiri yeye ndiyo aanze kuniambia ananipenda kwasababu nilijua ile dawa itamvuta na anipende.
Nikaona wiki inakatika Rusi hana mpango hata wa kunitamkia kuwa ananipenda nikazidi kujisiliba hayo mafuta ya dawa lakin kimya. Nikaona acha nibadili dini nimfuate anakosali yeye huku nikizidi kupaka ile dawa lakin hakuna hata siku moja aliyoweza hata kunichekea. Nikaishiwa nguvu baada ya kuona dawa inaisha bila hata kuona tabasam la Rusi pamoja na jitihada zote. Tangu siku hyo simwamini mganga yoyote nyamaafu

Mwigulu Nchemba: "Nataka Niwe Rais ili Niwafundishe Adabu Watanzania!"

0
0

Leo jioni, mjini Iringa kwenye viwanja vya Mwembetogwa, Mh Mwigulu Nchemba alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, alisema kuwa Watanzania wana uhuru mkubwa sana wa kuongea mpaka wanakosa adabu hata kwa wazee wao "..najua mnaona natumia lugha kali, lakini ndio kawaida yangu kusema ukweli, ...natamani niwe Rais wa nchi hii ili niwafundishe adabu Watanzania, ndio!" Labda inawezekana alimaanisha kuwafundisha adabu Watanzania fulani, lakini kwakuwa alikuwa akiongea kwa jazba aliteleza ulimi, au alimaanisha hivyo. Watu waliohudhuria mkutano huo walipigwa na butwaa, aliliona hilo na kubadilisha mada haraka. Aliwafurahisha watu pale aliposema"..kule kwetu Singida, ng'ombe mpole ndie anaekamuliws sana maziwa, lakini yule mkorofi anaachwa, kadhalika (serikali) inawatoza kodi wajasiriamali wadogo bila msamaha lakini wawekezaji wakubwa wanasamehewa mabilioni ya fedha!) suala hilo ameahidi kupambana nalo.

Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images