Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live

Sakata la Mbasha: Kanisa la Ufufuo na Uzima Latoa Tamko Lake Kuhusu Tukio Hilo

$
0
0
Kwanza tutoe pole Kwa watu wote mliofikwa na maafa mbalimbali pamoja na pole kwa kiongozi na mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe kwa kufiwa na Mama Yake mzazi. 

Ni wiki sasa pamekuwa na gumzo hapa jijini juu ya tuhuma Za Ubakaji zinazomkabili mume wa mwimbaji mashuhuri Flora Mbasha. Na Kwa Makusudi na yamkini kikundi flani cha watu wamehusisha sakata hili na Kanisa letu la Ufufuo na Uzima, tena Kwa maneno makali sana. Bahati mbaya watu hawa wamewakosesha baadhi ya watanzania wasiojua Chochote na kujikuta nao pia wamo kwenye kumbo la kutukana, kumkashifu na wakati mwingine kutukana viongozi wa Dini kitu ambacho ni kibaya kinawaletea laana Binafsi. Kwa mustakabali huo ni Vema Basi waziwazi tukaongea sintofaham hii na kujibu maswali ya kila mwana jamii juu yetu. Siku zote Ufufuo na Uzima tumekuwa mbele kutolea ufafanuzi kila sentensi inayolenga huduma hii na kanisa la Mungu kwa ujumla wake hapa Tanzania.

Ifahamike tu wazi kwamba sakata hili tunalisikia sana mitandaoni. Kanisa kama kanisa hatujui lolote wala Chochote juu ya sakata hili, lilianza wapi linakwenda wapi na litafikia wapi. Ni Kweli Flora Mbasha na Mumewe mara Nyingi hupenda kushiriki nasi Kwenye ibaada zetu. 

Kanisa limejikita zaidi na huduma ya kiroho. Hatumaanishi kwamba washirika wetu hawapati mitatizo ya kiutu au kijamii, tunaamini Msingi Wetu hasa ni Maombi. Na Kama kukiwa Na tatizo la kijamii viko vyombo husika vya serikali yetu ambavyo ni wajibu wao kutekeleza majukumu Yao. 

Kama kuna swali uko huru kuuliza ni vema kupata jibu kwenye Chanzo sahihi.

Naacha Buku 15 Daily Nakuta Ugali na Dagaa

$
0
0
Nimevumilia vya kutosha hii tabia sasa naona itakua imefika kikomo. 

Naishi na mpenzi wangu hatujafunga ndoa tatizo nashindwa kumuelewa kila siku niendapo kazini na kurudi jioni lazima nimuachie elfu kumi na tano 15,000/-kusudi nikirudi jioni nikute mezani kumependeza nadhani mmenielewa cha ajabu jamani nakuta ugali na dagaa akibadili sana tembere kaomba kwa jirani.

Huu ni ungwana jamani? kumuambia nashindwa naona kama takua naingilia mambo ya jikoni ambayo hayanihusu na nisipokula huo ugali ananuna.

Sielewi nifanyeje na Nilikuwa nafikiria Kumuoa

Yay! Chris Brown Has Been Released From Jail

$
0
0
TMZ is reporting that Chris Brown has been released from jail after being locked up for 59 days. He was reportedly released around midnight yesterday. Chris was sentenced to a year in jail on May 9th but got credit for the 116 days he spent in Rehab. He still has his D.C case to answer. 

Je, Tume ya Uchaguzi wa Tanzania Inaweza Kudhubutu Kukaidi Amri ya Serikali au Hata Rais Kama Walivyofanya Malawi

$
0
0
Natafakari mchakato wa uchaguzi wa viongozi Malawi ukihusisa kumchagua Rais wa nchi hiyo jinsi ulivyofika mahali ukaleta sintofahamu hasa pale Rais aliyeondoka madarakani mh. Joyce Banda alipoamuru tume isitishe shughuli za uchaguzi hadi utakaporudiwa upya baada ya siku 90. 

Tume ilionyesha msimamo kinyume na amri haram ya mh. J. Banda na kujitanabaisha kama chombo huru chenye kuendesha shughuli zake kwa kufuata taratibu na mamlaka huru za kisheria na kikatiba pasipo kuingiliwa wala kuamrishwa ni lipi walifanye na lipi wasifanye. Hatimaye kama wengi tujuavyo tayar tume imemtangaza Prof. kuwa mshindi na Rais mpya wa Taifa la Malawi.

Je, tume yetu ya uchaguzi wa Tanzania inaweza kudhubutu kukaidi amri ya serikali au hata Rais na kufafanua kwa nini amri yake haitekelezwi? Tume hii ambayo hata katibu tu mwenezi wa CCM anaipa maagizo na maelekezo nayo inayatekeleza mara moja!! Tume ambayo inasema mikutano isifanywe siku fulan lakini CCM wanaweza kufanya ila kikifanya chama cha upinzani ni haramu yanapigwa mabomu na m/kiti wa tume anasema kilichofanyika ni sawa......!!!!!

Bado naendelea kutafakari................

Sintah Amchana Irene Uwoya Kiana 'If I were You I would Remain Single for A While'

$
0
0
Blogger Sintah Amemchana Irene Uwoya baada ya Picha zake za Mahaba kusambaa Akiwa na Kiserengeti Boy cha THT.
Jisomee Alichosema Sintah
"Katika dawati letu hatusemi mengi zaidi ya kusema Irene, Irene, Irene??? why?

this is what we call jumping from the frying  pan into the fire, if i were you (Irene) would remain single for a while..... 

hivi bila kuonyesha mahaba hadharani ndio hupendwi vile? mmmmh au ndio tujue mwenzetu umezama katika dimbwi la mahaba sasa tukuwacheee....

Je wewe mdau una la kuongeza hapo??" Sintah

Collabo ya Diamond na Msanii Mkubwa wa Marekani Yanukia, ni Trey Songz!?

$
0
0
Diamond Platinumz anazidi kung’aa na kuvuka mipaka ya Tanzania na baada ya kufanya collabo kadhaa na wasanii wakubwa Afrika Magharibi, mkali huyo wa Ngololo amejisogeza kwa wasanii wakubwa wa Marekani.

Diamond ambaye yuko Marekani ameonekana akiwa na Kevin Liles ambaye aliwahi kuwa rais wa Def Jam Record na makamu wa rais wa Def Jam Music Group kuanzia mwaka 1999 hadi 2004.

Hivi sasa Kevin Liles ni meneja wa wasanii wakubwa akiwemo Trey Songz na Big Sean.

Picha ya Diamond akiwa na Kevin Liles imewekwa na mmoja ya watu wa timu yake na kuandika, “Don’t ask Me what’s Next...” huku maandishi mengine yakiwataka mashabiki kumpigia kura Diamond kwenye tuzo za MTV (MAMA 2014) ikiwa ni siku mbili tu zimebaki.

Katika hatua nyingine, Diamond ametisha zaidi leo kwenye ukurasa wa Facebook wa BET baada ya kupata comments nyingi zaidi ya Davido na hivyo kuonekana anaungwa mkono na wafuasi wengi zaidi kwenye Facebook. Diamond na Davido wanawania tuzo za BET mwaka huu katika kipengele kimoja.

All The Best Diamond, nyota kutoka Tandale inayong’aa kama jina lake.

Unyama: Msichana Mwenye Umri wa Miaka 15 Abakwa kwa Zamu na Wanaume zaidi ya 38

$
0
0
Kuna baadhi ya binadamu wana roho mbaya zaidi ya wanyama wakali wa mwituni na ukisimuliwa matukio waliyofanya unaweza kujiuliza kama kweli ni binadamu au ‘mashetani’!

Siku mbili baada ya kuripotiwa habari ya kusikitisha ya wasichana wawili ndugu wa nchini India waliobakwa na baadae kunyongwa, mtandao wa MailOnline umeripoti tukio la ubakaji alilofanyiwa msichana mdogo mwenye umri wa miaka 15 na wanaume zaidi ya 38 nchini Malaysia.

Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo limefanyika Kaskazini mwa Kelantan, Malaysia, May 20 ambapo msichana huyo alienda sehemu fulani kukutana na rafiki yake mwenye umri wa miaka 17 lakini alijikuta akipelekwa kwenye jumba bovu wasiloishi watu.

Akiwa kwenye jumba hilo, msichana huyo alibakwa kwa zamu na wanaume hao ambao miongoni mwao ni kundi la watu wanaojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya.

Msichana wa miaka 17 ambaye ni rafiki ya msichana huyo anasadikika kuwa ndiye aliyemtenezea mazingira ya kuingia mikononi mwa watu hao wanyama japo polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi ili waweze kufahamu kama kweli msichana huyo alihusika kupanga njama ama na yeye alibakwa.

Polisi wa Malaysia wamewakamata watuhumiwa 13 hadi sasa na kwamba kati ya hao yupo baba na watoto wake wawili wa kiume.

Wanajeshi wa Tanzania ( JWTZ ) wazuiwa kupita Rwanda

$
0
0
Serikali  ya  Rwanda  imedaiwa  kuwazuia  kupita  nchini  humo  baadhi  ya  askari  wa  jeshi  la  wananchi  wa  Tanzania  (JWTZ)  waliotoka  kukisambaratisha  kikundi  cha  waasi  wa  M23  kilichokuwa  Jamhuri  ya  Kimokrasia  ya  Kongo  (DRC) .....

Kwa  mujibu  wa  chanzo  chetu  cha  habari  kilichozungumza  jana  na  MTANZANIA  Jumatatu  kimedai  wanajeshi  hao  walitakiwa  kuanza  safari  leo  kuja  nchini  kupitia  Rwanda  lakini  walizuiliwa  bila  sababu  za  msingi.

Chanzo  hicho  kilisema: "Hali  ya  usalama  kati  ya  Tanzania  na  Rwanda  sio  nzuri  hata  kidogo,Wanajeshi  waliomaliza  majukumu  yao  nchini  Kongo  walikuwa  waanze  safari  yao  kurudi  Tanzania  kesho ( leo )  kwa  kupitia  Rwanda, lakini  katika  hali  isiyo  ya  kawaida  Rwanda  wamekataa  kupitisha  askari  hao  nchini  mwao.

"Mungu  jalia  viongozi  wetu  hekima  na  busara  katika  kuamua  suala  hili  zito  kwa  kuwa  kama  tutaingia  katika  vita  wanaoteseka  ni  watoto, wanawake  na  wazee  ambao  hawana  uwezo  wa  kwenda  kuishi  nje  ya  nchi, sala  na  dua  zinahitajika  sana  kwa  kuwa  Mungu  ndo  kila  kitu," mwisho  wa  kunukuu

Akizungumzia  suala  hilo, msemaji  wa  JWTZ,Luteni  Kanali  Erick  Komba  alisema  hafahamu  kama  wanajeshi  hao  walikuwa  wameanza  kurejea  nyumbani, hivyo  apewe  muda  hadi  atakapofika  ofisini  leo  ndipo  atahakiki  taarifa  hizo.....

Mgogoro  wa  Tanzania  na  Rwanda  ulianza  kufukuta  baada  ya  Rais  Kikwete  kumshauri  Rais  Kagame  wa  Rwanda  azungumze  na  waasi  wa  serikali  hiyo  wanaofahamika  kama  FDLR,  ambapo  Kagame  aligoma  na  kuanza  kumtolea  maneno  ya  kashifa  Rais  Kikwete.....

Hata  hivyo, hali  ilizidi  kuwa  mbaya  baada  ya  M23  kusambaratishwa  na  JWTZ walioungana  na  wanajeshi  wengine  wa  vikosi  vya  Umoja  wa  Mataifa (MUNUSCO).

M23  ni  kikundi  kilichodaiwa  kuundwa  na  askari  wa  makabila  ya  Rwanda, jambo  linalopingwa  vikali  na  Rais  Kagame.....

Katika  hatua  nyingine, waziri  wa  mambo  ya  nje  na  ushirikiano  wa  mataifa, Benard Membe  alikiri  kuwapo  kwa  uhusiano  mbaya  kati  ya  Tanzania  na  Rwanda.Kauli  hiyo  aliitoa  bungeni  mjini  Dodoma  hivi  karibuni  alipowasilisha  bajeti  ya  makadirio  ya  mapato  na  matumizi  ya  wizara  yake  kwa  mwaka  wa  fedha  wa  2014/ 2015.

Alisema  uhusiano  kati  ya  nchi  hizo  mbili  umekuwa  mbaya  kwa  sababu  kuu  mbili  kubwa.

"Ni  kweli  tuna  uhusiano  mbaya  na  Rwanda, kwanza  tunaogopana  kwa  kuwa  kila  upande   mmoja  ukiongea  na  hasimu  wa  mwenzake  inaonekana   kama  kuna  hujuma  inataka  kufanywa.

"Pili  kuna  watu  wanapeleka  maneno  ya  chokochoko.Pia  M23  ni  wanamgambo  wa  Rwanda  na  kuna  ushahidi  kwamba  Rwanda  ilipeleka  wanajeshi  kuwasaidia  wakati  wa  mapigano  na  serikali  ya  DRC  yakiendelea, ushahidi  huo  upo," alisema  Membe

Tanzania  ina  historia  iliyotukuka  katika  ukombozi  wa  nchi  za  kusini  mwa  jangwa  la  Sahara  na  ndio  maana  ilichaguliwa  kuongoza  majeshi  ya  kulinda  amani  DRC

Mwaka  2008, makamanda  na  wapiganaji  wa  JWTZ  waliongoza  vikosi  vya  washirika  katika  kazi  ngumu  ya  kumng'oa  kanali  Bacar  wa  Visiwa  vya  Comoro  na  Anjouan.

Uamuzi  wa  AU  kuipa  kazi  hiyo  Tanzania  kuongoza  mapambano  hayo  haukuwa  wa  bahati  mbaya, bali  ulitokana  na  kutambua  kuwa  ni  nchi  iliyoshiriki  na  kufanikiwa  katika  vita  mbalimbali  ya  ukombozi

Mkurugenzi wa Clouds 'Kusaga' Ajitosa Kuwapatanisha Ali Kiba na Diamond

$
0
0
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema atajaribu 
kukaa na wasanii wa muziki Diamond na Ali Kiba na kuangalia tofauti zao ili kuwapatanisha

Akizungumza na The Sporah Show hivi karibuni, Kusaga amedai kuwa alikuwa hatambui kama 

wasanii hao wana matatizo kwenye kazi zao na kuahidi kuwa ataliangalia tatizo lao.

“Kiukweli wote ni watoto wangu, Diamond ananipa heshima sana mimi ,namshukuru, Ali Kiba

is the same, nafanya nao kazi na sijawahi kugombana nao. Lakini sijui kama walikuwa wana

tatizo ndo nasikia sasa, lakini ngoja nijaribu kuwapigia ni find out kwanini? na kuna tatizo

gani between wao, lakini sijawahi kujua wana matatizo hayo.”

Lissu Arusha Kombora Lingine kwa Mawaziri

$
0
0
Dodoma. Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Binilith Mahenge, jana walituhumiwa kutumia vibaya nafasi zao kwa kuweka fedha nyingi za miradi ya maji katika maeneo wanakotoka, huku sehemu zenye matatizo ya huduma hiyo zikitengewa fedha kiduchu.

Ilielezwa bungeni jana kuwa Profesa Maghembe ambaye ni Mbunge wa Mwanga, Kilimanjaro, wizara yake imetenga Sh1.4 bilioni kwa ajili ya miradi ya maji, ambazo ni zaidi ya mara saba ya Sh190 milioni zilizotengwa kwa ajili hiyo katika Wilaya ya Ikungi, Singida.

Akichangia Bajeti ya Wizara ya Maji jana, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alihoji kile alichokiita upendeleo wa wazi katika ugawaji wa fedha za maji, unaoipa kipaumbele baadhi ya mikoa wanakotoka mawaziri.

Pia aliitaja Wilaya ya Makete, Njombe anakotokea Dk Mahenge ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Maji kuwa imetengewa Sh1.9 bilioni na kusema: “Upendeleo wa aina hii haufai kwa sababu utaleta matatizo na siyo haki hata kidogo.”

“Profesa Maghembe atueleze sababu za kutenga bajeti hii kwa upendeleo, huku mikoa isiyokuwa na vyanzo vya maji, mito ya kudumu na mabwawa ya maana imepewa bajeti kidogo ikilinganishwa na ile yenye mifumo mizuri ya maji,” alisema Lissu.

Alisema licha ya Profesa Maghembe katika hotuba yake kutaja mikoa ya Dodoma, Singida, Simiyu na Shinyanga kuwa inakabiliwa na upungufu wa maji, imetengewa kiasi kidogo cha fedha, huku mikoa inayopata mvua za kutosha na vyanzo vya uhakika vya maji ikitengewa mabilioni ya fedha.

“Dodoma imetengewa Sh7.2 bilioni, Singida Sh3.2 bilioni, Shinyanga Sh3.2 bilioni na Simiyu Sh2.8 bilioni, wakati mikoa yenye vyanzo vya maji na mvua za kutosha imetengewa fedha nyingi; mfano ni Tanga Sh10.7 bilioni, Kilimanjaro Sh6.3 bilioni, Mbeya Sh9.2 bilioni na Mtwara Sh7.5 bilioni,” alisema.

Lissu alisema hali hiyo inaweza kutafsiriwa kuwa mawaziri hao wanatumia mamlaka yao kujipendelea na kuhoji kama huo ndiyo utaratibu wa Serikali ya CCM... “Kama utaratibu wa mgawanyo wa fedha ndiyo huu sisi tunaotoka mikoa yenye ukame tutapataje maji?”

Jana Profesa Maghembe aliendelea kuwa katika wakati mgumu, baada ya kuandamwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ambaye alimwita kuwa ni mzigo kutokana na kutokutolewa kwa fedha za miradi ya maji.

Mnyika alionyesha kushangazwa na wabunge wenzake kuunga mkono bajeti ya wizara hiyo, licha ya kuwa ndogo na fedha za miradi zimekuwa hazitolewi kama inavyotakiwa.

“Kwa kufanya hivi sidhani kama tunamsaidia Profesa Maghembe ambaye ni CCM. Fedha zilizotengwa mwaka jana kuisaidia wizara hii hazijatoka na za bajeti hii hazitatoka kwa kiwango cha kuwezesha utekelezaji. Namna bora ya kumsaidia ili viongozi wa CCM wasiendelee kumwita mzigo ni kuikataa bajeti hii ili Serikali irudi mezani na kujiuliza.”

Rais Mpya wa Malawi ana Msimamo Mkali Ziwa Nyasa, Asema Haya

$
0
0

Wingu jeusi limeanza kutanda kuhusu hatima ya mzozo wa Ziwa Nyasa kutokana na msimamo wa hivi karibuni wa kiongozi wa Democratic Progressive Party (DPP), Peter Mutharika ambaye sasa ni Rais mpya wa Malawi.

Hiyo inatokana na msimamo wa Mutharika ambaye ni Profesa wa Sheria wa kupinga kuendelea kujadiliana na Tanzania kuhusu nani mwenye haki ya kumiliki ziwa hilo alioutoa wakati alipowatembelea wananchi wa Chipoko, kando ya ziwa hilo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu ambao ulimwigiza madarakani.

Pamoja na kwamba mazingira ya msimamo huo yanaweza kutofautiana na hali halisi ya sasa, tofauti za kisiasa baina yake na mtangulizi wake, Joyce Banda zinaweza kuongeza msukumo mpya wa kutaka kutoendelea na mazungumzo ya mpaka wa ziwa hilo.

Akizungumza na wananchi hao, Profesa Mutharika aliwatoa wasiwasi na kuwataka kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa maelezo kuwa ziwa hilo lipo kwenye himaya ya Malawi na kwamba kuendelea kujadiliana na Tanzania ni kupoteza muda.

“Hakuna haja ya kuendelea kujadiliana, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi na litaendelea kuwa la Malawi daima,” alisema Mutharika ambaye pia amewahi kufundisha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alimshutumu Banda na kudai alikuwa dhaifu kiasi cha kutoa fursa kwa Tanzania kutumia udhaifu huo kutaka kupora ziwa hilo.

“Ziwa hili letu ila Tanzania inatumia tu udhaifu wa Serikali iliyopo kwani wenyewe wanajua ndani ya mioyo yao kuwa hawana chochote katika ziwa hilo. Tutakaporejea serikalini mwakani haya mambo yote yasiyo na kichwa tutayamaliza. Nataka niwahakikishie kwamba tutapeleka meli zaidi kwenye ziwa hili ili kuinua shughuli zetu za kiuchumi na kutengeneza ajira kwa vijana wetu.”

Hata hivyo, wiki iliyopita Serikali ya Tanzania ilitoa msimamo wake kuhusu mzozo huo wa mpaka na kudaia kuwa itaendelea kujadiliana na Malawi.

Akizungumza bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema Tanzania ilikuwa ikifuatilia kwa karibu uchaguzi wa Malawi na kwamba iko tayari kufanya kazi na serikali yoyote itakayoingia madarakani.

Hii Sasa Kali…Cheki Picha Mpya za Rihanna Zinazoleta Gumzo Kwenye Internet

$
0
0



Rihanna amewahi kuacha gumzo mara nyingi kutokana na picha zake zinazosambaa mtandaoni. Mara nyingine tena picha za Rihanna ndio zinakuwa picha zinazoangaliwa sana hivi sasa kwenye mtandao.
Picha hizi amepiga akiwa kwenye red carpet ya CFDA Fashion Awards huko New York.

Mbasha 'Bora nijiue Sipo Tayari Kupata Aibu. 'Mke Wangu Amekuwa Tatizo Kwenye Ndoa Yetu'

$
0
0
Upande wa pili wa shilingi! Kwa mara ya kwanza tangu ahusishwe na skendo ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17, mume wa mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameibuka na kuzungumza na Uwazi katika mahojiano maalum dhidi ya kashfa yake hiyo huku akitishia kujiua.

Akizungumza kwa njia ya simu kwa zaidi ya saa moja mwishoni mwa wiki iliyopita huku akikanusha kukimbilia mafichoni baada ya kuondoka nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar hivi karibuni, Mbasha ambaye pia ni mwimba Injili kama mkewe, alianika kila kitu akidai cha siri kwamba anajua anachezewa mchezo mchafu baada kuwepo kwa gogoro zito kati yake na mkewe hadi kutishia uhai wa ndoa yao.

ASIMULIA TUHUMA
“Tuhuma zilizoripotiwa na binti aitwaye... (anamtaja jina) ambaye kweli ni ndugu wa mke wangu (Flora) kwenye Kituo cha Polisi Tabata-Shule (Dar) si za kweli.
“Anayefanya mambo hayo yote ni mke wangu, anataka nipotee ili awe huru. Mimi najua hilo.”

KASHFA YA KUTENGENEZA
“Hii kashfa ni ya kutengeneza ili nipotee lakini sipo tayari kupata aibu, bora nijiue.
“Mke wangu amekuwa tatizo kwenye ndoa yetu.
“Kweli ndoa yangu na Flora ina matatizo lakini matatizo yetu ya ndani sana hakuwa na sababu ya ‘kuinjinia’ mpango mchafu wa kunimalizia gerezani mimi ili yeye aponde raha.
“Nyuma ya haya mambo kuna vitu mtu ukivisema ni aibu sana kwa upande wa pili. Lakini navijua.”

MKE ALIONDOKA NYUMBANI
“Mke wangu aliondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini. Hebu fikiria hapo. Mwanzo alianza kwenda ‘gym’ saa 11:00 alfajiri na kurudi saa 4:00 asubuhi. Pia saa 10:00 jioni aliondoka tenda kwenda gym akawa anarudi kati ya saa 3:00 hadi 4:00 usiku.

“Nilipomuuliza alinijibu kuwa ni kwa sababu anatembea umbali mrefu. Hebu ona sababu ilivyo dhaifu jamani! Hata kama ungekuwa wewe mwandishi, unaonaje?”
“Mimi ni mtu maarufu, ningetaka mwanamke ningepata, iweje nibake?

“Jaribu kufikiria, katika tatizo kubwa kama hili ambalo linaweza kunifanya nifungwe, nilitarajia mke wangu awe upande wangu, lakini cha ajabu yeye ndiye amekuwa nyuma ya adui zangu, niamini nini mimi zaidi ya yeye kuhusika na kuniangamiza?”
“Hausigeli wangu ni mzuri, kwa nini nisimbake yeye?”

AFUATILIA
“Nilipofuatilia niligundua tayari kuna tatizo kwenye ndoa yetu. Mdudu alikuwa ameingia ndani ya ndoa kwani hadi sasa mke wangu siishi naye. Anaishi hotelini.
“Anachokifanya mke wangu ni kitu kibaya mno. Alimtengeza yule binti ambaye nilikuwa namsomesha sekondari pale (anataja shule maarufu Dar), akampa semina ya kutosha kwamba aseme nimembaka ili nipate misukosuko na yeye awe huru.

“Kama hiyo haitoshi, akala dili na madaktari,  wakafoji majibu ya vipimo vikionesha kweli yule binti ameingiliwa, sasa sijui kama vipimo vilioneshaje kama ni mimi.
“Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia kuona napandishiwa kizimbani kwa jambo la kutengenezewa.
“Napiga picha nitakapofikishwa mahakamani jinsi ambavyo vyombo vya habari vitakavyoandika na picha zangu kwa kesi ya ubakaji ambayo si ya kweli.

“Dah! Inaniuma sana. Mke wangu nimemfanyia vitu vingi sana. Hakustahili kunitendea ubaya huu. Alikuwa hafahamiani na mtu yeyote mkubwa. Mimi ndiye nimempeleka kwa watu wakubwa wakamsaidia sasa amenigeuka, siamini. Narudia tena, heri kufa kuliko fedheha hii,” alisema Mbasha kwa uchungu.

HAYUKO MAFICHONI
Kuhusu kuwa mafichoni, Mbasha alisema: “Sipo mafichoni, sijaambiwa na mtu yeyote nikatoe maelezo polisi. Nipo nimejaa tele, nikiambiwa nahitajika nitakwenda kutoa maelezo yangu kwani sijawahi kutenda kosa hilo na Mungu awe shahidi yangu.”

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Dar, Marietha Minangi alithibisha kuwepo kwa ishu hiyo na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.
Flora na Mbasha walifunga ndoa Agosti 22, 2002 hivyo mwaka huu wametimiza miaka 12 wakiwa pamoja ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Elizabeth.
Stori: Sifael Paul na MAKONGORO OGING’,GPL

Ukweli Kuhusu Kifo cha Dent wa Chuo Kikuu Aliyekutwa Amekufa Hostel

$
0
0
HATIMAYE familia ya denti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marehemu Sekabenga Pius Mwakimenya (21) kilichotokea hivi karibuni na kugubikwa na utata, imeanika ukweli kuhusiana na tukio hilo.

Akizungumza na Uwazi, mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baba mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Mwigune alisema, taarifa waliyopewa na daktari aliyemfanyia uchunguzi inamaliza utata na minong’ono yote inayoendelea chuoni.

Alisema, kwa mujibu wa ripoti hiyo, kifo cha Sekabenga kimetokana na mzunguko wa damu katika mishipa kutokuwa sawa, jambo lililosababisha ajisikie vibaya na hatimaye kufariki dunia
“Daktari amesema kwamba mishipa ya damu haikuwa ikifanya kazi vizuri hali iliyomsababishia ajisikie kuchoka kwa sababu damu haikuwa ikifika sehemu zote za mwili wa marehemu,” alisema Mwigune.

Uwazi lilifunga safari hadi chuoni na kuzungumza na baadhi ya wanafunzi ambao walionyesha wasiwasi kuwa huenda marehemu aliamua kujiua kwa sumu kwa maelezo kuwa, siku chache kabla ya kifo chake alionekana mwenye mawazo mengi.

“Hakuwa mwenye furaha, ni kama alikuwa na jambo zito linalomsumbua ndiyo maana unasikia wanafunzi wengi hapa chuoni wanahusisha kifo chake na sumu,” alisema denti mmoja kwa sharti la kutotajwa jina lake.

Hata hivyo, taarifa kutoka kwa familia inayonukuu ripoti ya daktari inaziba minong’ono yote kwa kuwa haionyeshi mahali popote kuwa marehemu alijiua kwa sumu.

Marehemu Sekabenga alikuwa mwaka wa pili chuoni hapo  akichukua Shahada ya Kwanza ya Biashara na Uhasibu, mwili wake  umesafirishwa Jumamosi Mei 31, mwaka huu kwenda mkoani Mbeya kwa maziko yaliyotarajiwa kufanyika jana Jumatatu.
Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa


Ulimbukeni wa Pesa Waanza Kumchafua Young Killer..Amwanika Demu wake Kifua Wazi

$
0
0
Picha hizi zimezua story kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii, baada ya Demu wa Rapper anaechipukia kutoka Tz kuonekana akiwa amejimwagia pesa juu ya kifua chake huku sehemu ya chuchu upande mmoja ikiwa wazi.
Pengine ni furaha ya pesa imesababisha mpigaji picha na mpigwaji kutokuona hiyo sehemu, pia imeleta mtazamo tofauti kwa watu kuwa Rapper huyo ameshaanza kuvuta mpunga kwa sasa hivyo kama pesa zinampa mzuka wa kufanya haya, Na hii Picha ni yeye aliyompiga huyu Demu ...Young Killer Bado ni Mdogo Sana kufanya hivi Vitu ...Kama ana Manager Basi Yabidi kumuonya..Justin Bieber Alianza hivi hivi kidogo kidogo


Diamond Azidi Kumgalagaza Davido Kwenye Maoni ya BET Awards, Sasa Amzidi Katika Instagram ya BET

$
0
0
‘Die hard fans’ wanaweza kufanya lolote kuhakikisha wanampa ushindi msanii wao katika shindano lolote linalohiotaji ushiriki wao hasa wa kupiga kura au maoni, kama kinachofanywa hivi sasa na mashabiki wa Diamond Platnumz katika tuzo za BET.

BET wanaendelea kuweka majina ya nominees katika page zao za mitandao ya kijamii ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuwaongezea ushawishi wa kupewa ushindi wasanii wao. Kama ilivyokuwa jana picha ya Diamond imeendelea kupata likes na comments nyingi katika Facebook ya BET, mpaka sasa ina likes 2649 na comments 5471 huku Davido akiwa na likes 1465 na comments 619 tu.

Upande wa Instagram ya BET Awards picha ya Diamond iliyowekwa jana usiku na maelezo haya:
‘Dbl tap this pic if you want #DiamondPlatnumz to win #BestInternationalAct: Africa @ the #BETAwards this yr’,
Hadi sasa ina likes 3275 na comments 4354 huku picha ya Davido katika akaunti hiyo ya IG ya BET iliyowekwa siku mbili zilizopita ina likes 518 na comments241 tu.
Cha kushangaza mashabiki wa Diamond wameamua kutoka nje ya kile kinachotarajiwa baada ya kuamua ku-comment jina la Diamond katika picha hiyo ya Davido.
Bongo5

Good News:Wema Sepetu na Kajala Wamepata na Kushikana Mikono

$
0
0
Unaweza kuona kama bado drama zinaendelea lakin ni kama movie imefika mwisho, kwani wale wakali wawili waliotengeneza headline hapa mjini kwa social media wamepatana, Kajala Masanja na Wema sepetu.  Hii imetokea jana kwenye msiba wa director na aliyekuwa mzazi mwenzie Monalisa.

Juzi kwenye msiba wa Rechal pale makaburini kulikuwa na makundi huku Kajala akiwa na sare tofauti na as well Wema alivaa sare ya peke yake lakini hii inaweza kuwa tofauti katika msiba wa Tyson kwani wawili hao walipatanishwa wakiwa msibani hapo na kuamua kuyamaliza kwani hakuna mfano mzuri katika maisha ya mwanadamu kama kifo, kwani kinamkumbisha kila mmoja wetu kuishi vema na kwamba kesho tutaondoka

Wawili hao walitofautiana kwa sababu wanazojua wao wawili na  Instagram kuchochea ugomvi na kuwasemea vitu ambavyo hata wawili hao hawajaongea mwisho wa siku Wema na Kajala ikawa wanapishana kama train za Umeme au bus ya mwendo kasi but final wamepatana na kupeana mikono .lets hope wamesafisha mioyo yao na waishi kama zamani.

Maskini:Utumbo wa Pacha Aliyekuwa Ameungana na Mwenzake Uko Nje

$
0
0
Mmoja wa watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana na kutenganishwa kwa upasuaji nchini India, hali yake ni mbaya na utumbo wake mkubwa sasa umetoka nje.

Mtoto huyo Eliud Mwakyusa na mwenzake Elikana walizaliwa Februari 20, 2013, Kyela, Mbeya wakiwa wameungana kiunoni na Serikali iliwapeleka India ambako walitenganishwa.

Walirejea Februari, mwaka huu na kusherehekea siku yao ya kuzaliwa wakiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili walikofikia baada ya kutoka India katika hafla iliyoandaliwa na gazeti hili.

Hata hivyo, siku chache baada ya watoto hao kurejea kijijini kwao Kasumulu maarufu kwa jina la Juakali, Kyela, afya ya Eliud ilianza kubadilika baada ya sehemu kubwa ya utumbo wake mpana kuanza kutokeza nje.

Utumbo wa mtoto huyo umetoka nje kupitia tundu lililoachwa na madaktari jirani na kitovu chake kwa ajili ya kutolea haja kubwa.

Wakizungumza na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki nyumbani kwao, wazazi wa watoto hao, Grace Joel na Eric Mwakyusa walisema tatizo la Eliud lilianza mwezi mmoja uliopita.

Grace alisema hali hiyo imesababisha mwanaye aanze kudhoofika naye akiwa hajui cha kufanya kutokana na hospitali iliyowafanyia upasuaji kuwa mbali.

Alisema baada ya kutenganishwa walitengenezewa mirija maalumu ya kutolea haja. “...Waliingiza kwa ndani na kubakiza kidogo nje ya tumbo kwa ajili ya kutolea haja kubwa. Hivyo baada ya kuanza kuugua akawa anatapika na anapotapika utumbo huu ukawa unatoka nje kidogokidogo kama unavyoona,” alisema huku akionyesha utumbo huo.

Alisema kuwa hali hiyo ya utumbo kutoka nje iliwahi kumtokea mtoto huyo hata wakiwa bado hospitalini nchini India, lakini haikuleta madhara yoyote.

Mama huyo alisema afya ya Eliud imekuwa ikidhoofu kila kukicha na sasa imefikia hatua anashindwa kukaa peke yake tofauti na aliporejea kutoka India.

Mwenzake aendelea vizuri

Afya ya pacha mwenzake, Elikana ni nzuri na muda mwingi amekuwa akikaa na bibi yake mzaa baba, Subira Kasekele.

Wanawake CCM Wamfariji Vicky Kamata Baada ya Harusi Yake Kukwama

$
0
0
Wabunge wanawake wenye muda mrefu bungeni pamoja na mke wa waziri mkuu, Mama Tunu Pinda juzi walimuandalia sherehe ya kumfariji mbunge wa viti maalum (CCM), Vicky Kamata baada ya harusi aliyotarajia kufunga wiki iliyopita, kukwama.

Sherehe hiyo ya faraja, ilifanyika Hoteli ya Dodoma kati ya saa 1.00 jioni na saa 6.45 usiku juzi mjini hapa.

“Unajua hata yeye mwenyewe tulim-surprise (tulimshtukiza). Alijua kuwa ni chakula cha jioni, lakini alipofika alikutana na muziki, kwaya na wabunge wengine waliompokea kwa vifijo na nderemo,” alisema mmoja wa wabunge waliohudhuria hafla hiyo. Sherehe hizo zilitumbuizwa na kwaya ya kikiristo ya Mvuke ya kanisa la Anglican mjini Dodoma.

Alisema Vicky alijua kuwa amealikwa na mbunge wa viti maalum (CCM), Magreth Sitta kwa ajili ya chakula cha jioni lakini alipofika aka kutana na sherehe.

“Tuliona ni vyema kumuandalia sherehe kidogo ili kumpa moyo kwamba hayo yametokea kwa sababu Mungu alitaka kumuepushia na mambo makubwa siku za usoni,” alidokeza mmoja wa waliohudhuria sherehe hiyo.

Baadhi ya wabunge waliohudhuria ni wabunge wa viti maalum kutoka CCM ambao ni Magreth Sitta, Anna Abdallah, Felister Bura, Hilda Ngoye, Agness Hokororo na Anastazia Wambura.

Wengine waliohudhuria ni Asumpta Mshama (Nkenge-CCM), Anne Kilango (Same Mashariki-CCM) na Waride Bakari Jadu (Kiembe Samaki-CCM). Chanzo hicho kilisema wabunge Anne Kilango, Magreth Sitta na Anna abdallah, walielezea jinsi baadhi ya wanawake viongozi walivyokumbwa na mikasa kama ya Vicky na wengine hata kuacha wakiwa makanisani.

“Wengine walieleza jinsi walivyoteswa na wenza wao na kwamba amshukuru Mungu pengine amemuepushia mambo makubwa ambayo yangeweza kutokea kama ndoa ingefungwa,”alisema shuhuda huyo.

Alisema sherehe hiyo ilikuwa kama ibada maana muda mwingi ulitumika katika kumuhubiria Vicky na kumsihi asikatishwe tamaa na badala yake asonge mbele.

Alipoulizwa kuhusu sherehe hiyo, Vicky alikiri kufanyika lakini akakataa kuielezea kwa kina.

“Mimi niliitwa kwenye chakula cha jioni lakini nilipofika pale nistaajabu kukutana na sherehe,”alisema Vicky ambaye alikataa kuelezea kwa kina kuhusu sherehe hizo.

Sikiliza Mume Wa Flora Mbasha Akikubali Kubaka Na Kuomba Msamaha Kwa Shemeji Yake. Sikiliza Hapa

$
0
0
Clip hiyo Hapo chini ya Audio Kwa sasa inazunguka Mitandaoni inasemekana ni Mume wa Flora Akiongea na Shemeji yake Ambaye Inadaiwa Kambaka hatuna huhakika nayo ila na wewe sikiliza:

"Tunaomba usikilize hii audio Mume wa Flora Mbasha akiomba msamaha na akifichua mambo magumu mazito yanyoendelea ndani ya famili hiyo ambayo imezua gumzo mtaani kwa kile kinachofikiriwa kua imepoteza uaminifu kutokana na jamii inavyoichukulia ,kua ni familia yenye hofu kubwa ya Mungu,lakini jamii imesahau kua hawa ni binadamu 100% kuna kuanguka Tunaomba maoni yako unasemaje juu ya hili"

Source:Jipange Media
Viewing all 104774 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>