Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Unaambiwa Vigogo wote wa Escrow presha inapanda na kushuka

$
0
0

WAKATI majaji wawili wa Mahakama Kuu waliopata mgawo wa fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow wakijiuzulu nyadhifa zao, hatua hiyo sasa huenda ikawa imehamishia joto kwa wanasiasa, viongozi wa dini na watumishi wa umma ambao nao walinufaika.


Majaji waliojiuzulu ni Profesa John Ruhangisa, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye juzi Ikulu ilitoa taarifa kwa umma ikisema Rais Dk. John Magufuli ameridhia kujiuzulu kwake na Jaji Aloysis Mujulizi pia wa mahakama hiyo, ambaye alijiuzulu Mei 16, mwaka huu.


Baada ya kutajwa kwenye kashfa hiyo, waliokuwa kwenye nyadhifa za kisiasa, wakiwamo mawaziri na wabunge, waliitwa Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma, ambako baadhi walihojiwa, ingawa hatua zilizochukuliwa hazijawekwa wazi.


Kwa viongozi wa umma, baadhi walifikishwa mahakamani, ingawa wengine kesi zilifutwa zikiwa kwenye hatua mbalimbali za usikilizaji.


Homa ya walionufaika na mgawo huo wa fedha za Escrow, ilianza kupanda baada ya Serikali kuamua kufufua sakata hilo, lililodhaniwa kuwa limekwisha kwa kuwafikisha mahakamani hivi karibuni vinara wawili.


Vinara hao ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, aliyekuwa pia mwanahisa wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), iliyoletwa nchini miaka 23 iliyopita, James Rugemalira na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Pan African Power (PAP), Habinder Sethi Sigh, waliofikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 19 na kusomewa mashtaka sita, yakiwamo ya uhujumu uchumi.


Julai 3, vigogo hao walifikishwa tena kwenye mahakama hiyo na kuongezewa mashtaka sita, yakiwamo ya utakatishaji fedha.


Kwa jumla wake mashtaka 12 waliyosomewa Rugemalira na Sethi Julai 3, ni pamoja na kutakatisha fedha na kuisababisha hasara Serikali ya USD 22, 198,544.60 (Sh 309,461,300,158.27).


Kutokana na hali hiyo, na hatua ya majaji wawili kuamua kuachia nyadhifa zao, ni wazi walionufaika na fedha hizo presha zao zitakuwa zinapanda na kushuka, kutokana na kutojua hatima yao ya ama kuunganishwa au kutounganishwa kwenye kesi inayoendelea mahakamani.


Miongoni mwa viongozi wa kisiasa na umma ambao wakati fedha hizo zinatolewa walikuwa madarakani, ama kwa namna moja ama nyingine walihusika kuiingiza IPTL nchini, huenda sasa wakawa kwenye wakati mgumu zaidi.


Hii ni kwa sababu baada ya kutajwa kwenye kashfa hiyo, waliishia kwenye Baraza la Maadili na wengine kesi zao zikifutwa baada ya kufika mahakamani.


Novemba 2014, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwataja vigogo wa Serikali, wanasiasa na viongozi wa dini watatu walionufaika na Akaunti Tegeta Escrow, huku ikishindwa kuweka wazi walionufaika na sehemu ya fedha zilizodaiwa kuchotwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ilipokuwa akaunti hiyo na kupelekwa Benki ya Stanbic.


PAC wakati ikisema Rugemalira aliwagawia baadhi ya watu fedha kupitia akaunti zao walizofungua kwenye Benki ya Mkombozi, ilisema sehemu ya fedha nyingine iliwekwa Stanbic, ambako watu walizichota kwa mifuko ya plastiki, maarufu kama sandarusi.


 WALIONUFAIKA NA MGAWO WA RUGEMALIRA


Akisoma maoni ya PAC, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, ambaye wakati huo alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo, aliwataja waliochukua fedha hizo kutoka kwa Rugemalira, kiwango walichopokea katika mabano kuwa ni Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (Sh bilioni 1.6) na Mbunge wa Muleba ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (Sh bilioni 1.6).


Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (Sh milioni 40.4), aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh milioni 40.4), Mbunge mstaafu wa Sumbawanga, Paul Kimiti (Sh milioni 40.4) na aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk. Enos Bukuku (Sh milioni 161.7).


Kwa upande wa majaji, ni Jaji Profesa Ruhangisa (Sh milioni 404.25) na Jaji Mujulizi (Sh milioni 40.4).


Kwa upande wa watumishi wa umma, Zitto alisema aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko, alipewa Sh milioni 40.4, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Daniel ole Naiko (Sh milioni 40.4) na Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Lucy Appollo (Sh milioni 80.8).


“Kwa upande wa viongozi wa dini ambao waliingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi, ni Askofu Methodius Kilaini (Sh milioni 80.9), Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh milioni 40.4) na Padri Alphonce Twimannye Simon (Sh milioni 40.4),” alisema Zitto.


Alisema Rugemalira alipata mgawo wa Dola za Marekani milioni 75 kutoka katika fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow na kuzigawa kwa watu mbalimbali.


Rugemalira, ambaye alikuwa na hisa 3 kati ya 10 za kampuni ya IPTL, alichukua kiasi hicho cha fedha na kukipeleka katika Benki ya Mkombozi, inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.


 KUHUSU MAJAJI


Mwaka jana katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga, alinukuliwa na gazeti hili akisema dawa ya kumaliza mambo ni kuwa wazi.


“Suala la majaji waliohusishwa katika Escrow limeshaletwa katika tume, lipo na taratibu zinaendelea,” alisema Katanga.


Naye Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Enzeel Mtei, alinukuliwa katika maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria akisema tume hiyo iliundwa na wajumbe sita.


Alisema ilikuwa na jukumu la kumshauri rais juu ya uteuzi wa Jaji Kiongozi au majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Msajili Mkuu, Msajili wa Mahakama ya Rufani na Msajili wa Mahakama Kuu na kutokuwa na uwezo kwa watendaji hao.


Majukumu mengine ni kuchambua malalamiko dhidi ya majaji hao na kuchukua hatua za utawala dhidi ya Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi au Jaji na hatua zilizoainishwa katika Katiba.


Alisema kwa majaji wanaokwenda kinyume na maadili, tume huchunguza madai hayo na kupeleka mapendekezo kwa rais kwa ajili ya uamuzi.


 VIONGOZI WA KISIASA


Machi 2015, Ngeleja alidai mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kwamba msaada aliopewa na Rugemalira hauna tofauti na  mingine aliyowahi kupokea kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa kama vile Reginald Mengi, Said Salim Bakhresa na Yusuf Manji.


“Msaada niliopewa na Rugemalira hauna tofauti na misaada mingine wanayopewa wabunge wenzangu au misaada mingine niliyowahi kupokea kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa kama vile akina Mengi, Bakhresa, Yusuf Manji, mashirika ya hifadhi ya jamii kama vile NSSF, PSPF, NHC, NHIF na benki ya CRDB na NBC,” alisema.


“Sijawahi kuomba wala kupokea fadhila za kiuchumi kutoka kwa Rugemalira, isipokuwa kama Mbunge wa Sengerema kwa nyakati tofauti kama wabunge wengine wanavyofanya, niliomba misaada ya kiuchumi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla,” alisisitiza.


 CHENGE


Kwa upande wake, Chenge, alidai mbele ya baraza hilo kuwa amri ya Mahakama Kuu inazuia mamlaka zozote kujadili au kulifanyia kazi suala lolote linalohusu kashfa ya akaunti hiyo.


Kutokana na hali hiyo, hakuhojiwa na baraza likatenga siku moja kuipitia amri ya zuio hilo la mahakama kabla ya kutoa uamuzi juu ya pingamizi hilo.

Baada ya kuipitia, mwenyekiti wa baraza hilo aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Jaji mstaafu Hamisi Msumi, alisema zuio hilo la mahakama halilihusu wala kulizuia baraza kufanya kazi yake, isipokuwa Bunge, wasaidizi wa sheria au mawakala wanaofanya kazi za kisheria.


Baada ya Jaji Msumi kutoa uamuzi huo, Chenge hakukubaliana nao na kusema anakata rufaa kwenda Mahakama Kuu kuomba mwongozo juu ya kuendelea kujadiliwa suala hilo au la.“Sitaki kubishana na maamuzi yaliyotolewa na baraza, lakini nafikiri wanasheria wa baraza hili wangejaribu kwenda masjala kusoma zaidi, naamini wangeelewa hili ninalozungumza. Ninakubaliana na maamuzi, lakini naomba nikate rufaa, niende Mahakama Kuu kwa ajili ya kupata mwongozo zaidi juu ya suala hili,” alisema Chenge.


 TIBAIJUKA


Kwa upande wake, Profesa Tibaijuka alikiri kuomba fedha hizo, lakini si kwa masilahi yake binafsi, bali ni kwa ajili ya Taasisi ya Barbro Johannson Girls Trust.

Alipoulizwa sababu ya kutoa fedha hizo kwenye akaunti yake katika Benki ya Mkombozi na kuzitumia katika kazi zake binafsi, alisema fedha hizo ziliingizwa tarehe 12 mwaka 2014 na kuanza kufanya miamala binafsi tarehe 14, ambapo Sh milioni mbili alizitumia kununua hisa Makongo Parish.


Profesa Tibaijuka alisema baada ya hapo alitoa Sh 400,000 na kununua hisa Kijiwe Parish na siku hiyohiyo alitoa Sh milioni 10 ambazo hazina maelezo sahihi.

“Sh milioni 10 nilitoa kwa ajili ya kununua mboga kwa sababu fedha hizo ni zangu.


“Nashangaa kuambiwa nimevunja maadili, kwanza fedha hizi ni ndogo japo ni hela, lakini mimi sina shida na fedha hizi.


“Mimi ni mstaafu wa miaka mingi, nina pensheni ya kila mwezi, sina shida na fedha hizo, ndiyo maana hata hizo fedha zilizobaki kwenye akaunti hiyo sijaenda kuziangalia kwa sababu sina shida za hivyo,” alisema.


 VIONGOZI WA DINI


Hadi sasa haijulikani kama kuna hatua zozote zimechukuliwa kwa viongozi wa dini waliotajwa kwenye sakata hilo.


 VIONGOZI WA UMMA


Baadhi ya wafanyakazi wa umma, wakiwamo wa  Mamlaka ya Mapato (TRA), Msajili wa Vizazi na Vifo (Rita), na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kesi zao zinaendelea, huku wengine zikiwa zimefutwa ama kumalizika.

TAHARUKI Baada ya Majambazi Sita Kuuwawa Mwanza...

$
0
0

Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kuwaua watu sita wanaodaiwa kuwa majambazi na wengine wawili kukimbia katika Mtaa wa Fumagila Mashariki Kata ya Igoma wilayani Nyamagana jijini Mwanza, taharuki imeendelea kuwakumba wananchi wa eneo hilo wakihofu kuwa huenda wakarudi.

Akizungumza na gazeti hili leo Jumapili, Julai 9, Mwenyekiti wa mtaa huo, William Ngemela amesema tukio hilo limetoa elimu tosha katika mtaa huo na mitaa jirani huku akidai tangu azaliwe hajawahi kushuhudia tukio kama hilo.

“Hii ni elimu tosha kwasababu haya yote hatukutegemea kama yanaweza kutokea kwenye mtaa kama huu, lakini angalia silaha zote na vitu vilivyokamatwa, kwakweli inatishia amani,” amesema Ngemela.

Katika tukio hilo polisi walikamata silaha ya SMG AK47, magazine mbili kila moja ikiwa na risasi 30, risasi 36 za AK 47ambazo zilikuwa nje ya magazine, risasi moja aina ya rafal, risasi nane za shortgun.

Silaha nyingine ni bastola nne za kienyeji, sare za jeshi za nchi jirani, kofia sita za kuziba uso, kitambaa cha kichwani, nusu kanzu, nguo mbalimbali za kiume, mabegi matatu yaliyokuwa yakihifadhi silaha hizo, baiskeli mbili, pikipiki moja, unga na dagaa.

Mwenyekiti huyo amesema watu hao walikuja mtaani hapo kama waumini wa dini ya kiislamu kumbe walikuwa na mambo yao, lakini hili limekuwa fundisho kwetu ni wajibu wetu wote kushirikiana, mimi ni mwenyekiti mmoja lakini jamii ninayoingoza ni kubwa inapaswa kutoa taarifa.”

Amesema tangu lilipotokea tukio hilo jana, baadhi ya wakazi wa eneo hilo hawakutoka nje ya nyumba zao walijifungia wakiogopa kuwa hao waliokimbia wanaweza kurudi kufanya jambo baya, kwahiyo hali bado haijawa nzuri kwa wakazi wangu.”

Ishmael John, mkazi wa mtaa wa Kanenwa, alisema, “kiukweli hatuwezi kuwa na amani ya kutosha kutokana na jinsi hali ilivyokuwa juzi.”

Mkazi mwingine wa mtaa huo, Robert Musabi amesema itakuwa vigumu kuamini kwamba hali itakuwa salama hususani ukizingatia baada ya wawili kukimbilia kusikojulikana.

Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa wa Kanenwa jirani na mtaa huo, James Buduma amesema serikali za mitaa eneo hilo tayari zimeanza kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella la kusajili kila mtu ambaye anafika akiwa mgeni na ajitambulishe uhalisia wake.

Kamanada wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema zoezi hilo la kuwasaka wahalifu ni endelevu na hakuna atakayesalimika katika operesheni hiyo hivyo kuwataka wanaofanya vitendo hivyo waache mara moja.

Wanawake Walioachika na Ushuhuda wa Uongo Kwa Wadada Ambao Bado Hawajaolewa....

$
0
0

Nimegundua ya kwamba wanawake wengi walio achika katika ndoa zao wana ushuhuda wa uwongo kwa wanawake wasio olewa.


Utamkuta mdada mzima amezalishwa halafu ameachwa kwa makosa yake anawaambia wanawake wasio olewa kwamba kuolewa kitu gani, kwani wewe huwezi kuendesha maisha bila mwanaume, kwani mwanaume nani bwana asikunyanyase , watu tumeona wanaume sembuse magume gume, mwanaume kitu gani bwana, wewe waza maendeleo yako ,usiwaze kuolewa ,kuolewa ni kupoteza muda , kuolewa ni kutiana umaskini tu.


Katika hali isiyo ya kawaida wanawake hao wakipata tena waume wa kuwaoa utaona wanaolewa,halafu cha ajabu hamna shughuri yoyote ya maendeleo wanayofanya zaidi ya kutwa kujadili wanaume za wtu na kuendelea kuzalishwa tu nyumbani.


Waacheni mabinti waolewe na si kuwaharibu kisaikolojia kwamba kuolewa hakuna maana na maana zaidi kuzalia nyumbani kila mtoto na babake. Waacheni kila mtu akaone yeye wenyewe. Kama wewe umeachika wacheni wakajaribu maisha.


Kama una binti yako mzuie kuambatana na akina mama waliotendwa.

Al Shabab Wamekata Vichwa Wakenya 9

$
0
0

Wapiganaji wa Al Shabab wenye asilia ya kisomali wamewachinja wakenya 9 katika kijiji cha Poromoko siku ya Jumamosi.


Kwa mujibu wa habari,polisi wameviambia vyombo vya habari kuwa washambuliaji hao wanahisiwa kuwa wameingia Kenya kupitia mpaka wa Kenya na Somalia.


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa nchi yake imepata majanga mawili kwa wakati mmoja kwani  Kenya bado ilikuwa inaomboleza kifo cha waziri Joseph Nkaissery.


Vilevile rais Kenyatta  amewaahidi wananchi kuwa nchi yake itaongeza mbinu za kulinda usalama wa raia wake.


Hata hivyo polisi wameongezwa kulinda zaidi mahala tokeo hilo lilipotokea.

Zimbabwe yatwaa Kombe la Cosafa

$
0
0

Timu ya Taifa ya Soka ya Zimbabwe imetwaa ubingwa wa mashindano ya COSAFA2017 baada ya kuifunga Zambia mabao 3-1


Magoli ya Zimbabwe yalitiwa wavuni na  22' K. Mutizwa, 57' T. Chawapiwa pamoja na 67' O. Mushure

Huku goli moja la Zambia kifungwa na 39' L. Mundia

Siri 6 Muhimu Zitakazofanya Mahusiano ya Ndoa Kudumu

$
0
0

Zipo changamoto ambazo zinazosababisha ndoa nyingi kufa.  Hata hivyo kufa kwa ndoa hizo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu wengi wamekuwa hawavitilii maanani.  Hata hivyo siku ya leo nimeona ni vyema nikujuze siri ya kudumu katika mahusiano ya ndoa. Je ni vitu gani? Twende sawa:

1 mapenzi ya kweli.
Ili uweze kudumu katika ndoa yako ni lazima uwe na mapenzi ya kweli kwa mwezi wako. Upendo wa kweli mara kadhaa huwa haupimwi kwa maneno tu bali ni kwa vitendo. Hivyo katika kuhakikisha unafurahia maisha ya mahusiano hakikisha unajua ni kipi kitokachomfanya mpenzi wako ajue ya kwamba unampenda. Hilo ni suala la msingi ambalo ni vyema ukalijua.

2. uvumilivu.
Kitu ambacho pia kitakusaidia kuweza kukaa kwa muda katika ndoa yako ni kuhakikisha unalijua lile somo la uvumilivu. Kama ambavyo siku ya ndoa yenu mliampa ya kwamba mtadumu katika ndoa yenu katika shida na laha.  Hivyo ili kuweza kulitimiza hilo ni lazima ukumbuke kiapo chenu.  Hii itawasidia sana kuweza kutengeneza maelewano ndani ya nyumba.

3 hofu ya mungu.
Ndoa yeyote ile ambayo inataka kuwa imara ni lazima iwe na hofu ya Mungu ndani yake.  Kama mliapa ya kwamba mtaishi pamoja mpaka kifo kitakapo watenganisha, hivyo ili yote hayo yawe kweli ni lazima Mungu atawale katika ndoa yenu ili muweze kutimiza lile ambalo mlikuwa mmeliahidi mbele ya Mwenyezi Mungu pamoja na mashaidi wengine.

4 uwezo wa kujishusha.
Hakuna kitu muhimu katika  mahusiano kama hiki. Kuwepo na uwezo wa kujishusha katika mahusiano kunafanya mahusiano hayo kuimarika. kwani ndoa    nyingi hufa kwa sababu ya kutokuwa na mtu mmoja ambaye anajishusha. Hata ugomvi wa wanandoa wengi hutokea kwa sababu ya kutokuwepo kwa kitu hicho.  Hivyo ili uweze kudumu katika ndoa ni kazima uwe na uwezo kujishusha hasa pale unapokosea.  Pia katika suala la kujishusha ni lazima ujue matumizi ya samahani. Neno samahani lina thamani kubwa katika kuongeza upendo kwa mwenzi wako.

5 Matumizi mazuri ya pesa.
Hili ni la muhimu kwa wanandoa. Kwa upande wa wanaume ili uweze kuwa bora, ni lazima uweze kuepuka matumizi mabaya ya fedha ambayo kwa mkeo yatakuwa ni kero.  Na pia kwa mwanamke ili kumfurahisha mwanaume ni lazima awe na nidhamu ya fedha,  hapa nikiwa na maana ya kwamba fedha za matumizi ambazo unaachiwa au kutafuta mwenyewe ni lazima uweze kuzitumia katika mpangilio.

6. Uchaguzi mzuri wa marafiki.
Ukiwa katika ndoa ni lazima uwe na marafiki sahihi ambao mwezi wako watampendeza kitabia, kwani wapo baadhi ya marafiki wao kazi yao ni kuvunja ndoa za watu.  Watu hawa kazi yao ni kichwa maneno kutoka upande A kwenda upande B.

Marafiki wa aina hii hawafai hata chembe. Hivyo ili kudumu katika mahusiano ya ndoa lazima ufanye uchaguzi sahihi wa marafiki.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada tukutane hapa hapa tunazungumzia kuhusu elimu ya mahusiano.

Njia Tatu (3) za Kukuza Biashara ili Kupata Faida Kubwa

$
0
0

Uhali gani mpenzi msomaji wa makala hii ya muungwana blog? Ni matumani yangu u mzima wa afya tele na pia kama haupo vizuri kiafya basi usisajali kwa uweza wa mwenyezi  Mungu utapona na kuendeleza kulisukuma gurudumu hili la mafanikio.Katika somo letu la leo kama linavoeleza hapo juu tutaangalia ni hatua gani ambazo endapo utazifanya zinaweza kukusaidia kukuza biashara yako ambayo unaifanya au una mpango wa kuifanya. Matumaini yetu makubwa katika kufanya biashara ni kuona tunapata faida kubwa.Lakini matumini hayo hugeuka ghafla na kujikuta tunaacha kufanya biashara hii mara na kuanza biashara nyinyine huku tukiamini kufanya hivi ni kuzikwepa changamoto.

Ndugu msomaji  naomba nieleweke vizuri hapa , sina maana ya kwamba kufanya biashara nyingine na kuiacha biashara  ya mwanzo ni kosa la hasha sio kosa  ila tatizo ni kuhama na mtazamo uleule wa biashara ya mwanzo  kuutumia kwenye biashara mpya na kujikuta huupati faida kama ulivyokuwa ukitarajia hapo awali.Kuna biashara hasa hizi ndogondogo huwa tunaziona zipo vilevile siku zote.Huenda ukawa ni wewe muhusika wa biashara hiyo au kuna mtu na jamaa,ndugu au rafiki ambaye huwa unamuona akiwa katika hali hiyo,nitakochokieleza katika makala hii utaweza kumshirikisha pia.

Zifutazo ndizo hatua (3) za kukuza biashara ili kupata faida kubwa;

1. Panga malengo na mipango ya biashara.
Hili ni jambo la msingi kuweza kulizingatia.Kama wewe ni mfanyabiashara au unataka kuwa mfanya biashara unaweza ukapanga malengo na mipango ya kuweza kuiendesha biashara yako ili kuweza kupata faida kubwa zaidi. Malengo na mikakati yako lazima uyaandiike vizuri na uyatekeleze pia. Unaweza ukapanga malengo na mipango ya mauzo katika mwaka kwa mfano  unaweza kupanga kwa mieze mitatu mitatu.

Kwa mfano unafanya biashara Fulani lazima upange labda kila baada ya miezi mitatu uuze million tatu au zaidi na kama juu ya mpango na malengo usipokamilika unaweza ukafanya tathimini ni wapi ulipokesea? ili urekebishe ili miezi ijayo uweze kufikia malengo yako.Pia unaweza ukafanya taathimini  kama utakuwa umewajiri watu katika biashara yako kwa kujiuliza je wana mchango wowote katika kukuza biashara? Au wao ndo sababu ya ewe kushindwa?

Pia katika kupanga malendo na mipango juu ya biashara yako lazima upange juu ya muda wa kufanya biashara.Katika hili lazima ujiulize je biashara yako ni ya msimu? Kwa mfano wewe ni unafanya biashara ya kuuza makoti lazima ujue ni misimu ipi ni ya baridi kwani uhitaji wa wateja juu ya bidhaa hii ndio huwa wengi zaidi. Vilevile lazima upange ni jinsi gani utakavyochangamana na wateja ili kuweka mahusiano ya karibu na wateja wako.

2. Tazama ni wapi unakosea na kufanya marekebisho.
Mara nyingi changamoto katika biashara yeyote ile lazima zijitokeze.Hakuna binadamu ambaye amekamilika kokosea ni shemu ya mafanikio ya kibiashara hivyo usigope pindi changamoto zinapojitokeza,na pindi tunapokosea ndipo tunapojifunza zaidi.Inawezekana biashara yako haileti faida kutoka na wafanyakazi wako na vitu vingine jaribu kufanya uchunguzi wa kina na kuvirekebisha. Ewe mpenzi msomaji wa makala hii ili kukuza biashara ni lazima ufanye tathimini ni mipango ipi inakuletea faida katika biashara? kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuuzingatia. Kwani sio kila mipango unayopanga huleta faida.

3. Tambua namna ya kuongeza wateja.
Hii ni hatua nyingine pia ya kuzingatia.Inawezekana wewe ni mfanyabiashara mdogo au mkubwa au unatamani kuwa miongoni mwa wafanyabiashara tambua ya kwamba kuna baadhi ya biadhaa mteja akizinunua anaweza kukaa muda mrefu bila kununua tena mfano wa biashara hiyo ni magari,samani na vitu vingine. Katika hili jaribu kujenga mahusiona mazuri na wateja pia jaribu kuwa na kumbukumbu nzuri na wateja ili watakapokuja siku nyingine uweze kuwakumbuka.

Unaweza ukawa unawatumia wateja wako juu ya ujio mpya wa bidhaa,mabadiliko ya bei ili wakija kununua bidhaa wasishangae pia unaweza kuwaambia asante kuwa miongoni mwa wateja wako wazuri kwa kufanya hivi ni njia nzuri ya kuongeza wateja. Hivo kama utafanya hivi wateja hao hao ndio watakao kufanya upate wateja wapya kutokana na ukarimu na nidhamu uliyo nayo juu yao.

Pia unaweza kuongeza wateja kwa kutaangaza bidhaa yako kupitia njia mbali kama vile vyombo vya habari na mitandao mingine ya kijamii njia hii pia itafanya uongeze wateja pia. Fahamu ya kwamba kumpata mteja mpya ni kazi katika biashara yako ni ngumu hivo hakikisha mteja/wateja ulionao hauwapotezi.

Roma "Ningesema Walichonifanyia Watekaji WATEKAJI Hakika Hakuna Mtu Angetaka Kuwa Karibu na Mimi"

$
0
0
Mwanamuziki Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki” amesema kuwa tukio lililotokea miezi mitatu iliyopita lilikuwa na sababu nyingine zaidi ya muziki anaoufanya, tofauti na watu wanavyodhani.

Roma amesema katika mahojiano na EATV kwamba alijua kuwa atawakwaza baadhi ya watu kwa kutosema na kuweka wazi mambo kadhaa kuhusu tukio hilo ikiwemo kutekwa, walipopelekwa, kilichowatokea wakiwa huko walikopelekwa n.k lakini aliamua kutumia busara na kutosema kitu ili aweze kulinda sanaa na maisha yake kwa ujumla.

“Mimi najua nini kilipelekea wale jamaa kututeka. Ni zaidi ya muziki, japo chanzo ni muziki ndio maana walikuja kututeka tukiwa studio na si kanisani wala nyumbani. Unajua wananchi tayari walikuwa na video kichwani wakijua Roma anakuja kuongea hiki na kile, tunamaliza pale halafu usiku mwema.”

“Lile tukio lilikuwa linahitaji busara ili maisha yaweze kuendelea. Labda ningesema ukweli pengine ungekuwa ndio mwisho wa Roma kwenye muziki. Mashabiki wangeshangilia lakini kwa wadau mbalimbali mchango ndio ungekuwa umekwisha,” alisema.

Roma alisisitiza kuwa kama angeweka wazi jambo hilo siku ile ambayo alitoka, ingepelekeaa yeye kuacha muziki na kurudi Tanga kufanya mambo mengine, kwani hakuna mtu ambaye angetaka kuwa karibu naye tena.

“Toka nimetoka mpaka sasa sitaki kutazama video mbalimbali ambazo zinaonesha jinsi watu walivyokuwa wakihangaika kututafuta. Sitaki kutazama kwa sababu sitaki kukumbuka kabisa hali ambayo nilikuwa nayo kipindi kile. Pia sipendi kabisa kuona mtu mwingine yeyote anakwenda huko chimbo ambako tulikuwa tumewekwa tukipata mateso,” alisema.

Roma na wenzake walitekwa mwezi wa nne mwaka huu walipokuwa katika studio za kutayarisha muziki za Tongwe Records na kupelekwa kusikojulikana kwa muda wa siku tatu na kuja kuonekana wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini.

Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Ally Hapi Ajivua SAKATA la Kukamatwa Mbunge Halima Mdee

$
0
0
BAADA ya Jeshi la Polisi kumshikilia kwa zaidi ya saa 48 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, ambaye ndiye chanzo cha kukamatwa kwa mwanasiasa huyo, amejivua kwenye sakata hilo.

Jana jeshi hilo lilimuhamisha Mdee kutoka katika mahabusu za Kituo cha Oysterbay alikokaa kwa siku nne na kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi (Central), ambako anaendelea kushikiliwa kwa kosa la uchochezi.

MTANZANIA Jumapili lilipomtafuta Hapi ili kufahamu kama amri ya saa 48 alizozitoa kwa polisi kumshikilia Mdee ina mabadiliko yoyote, alisema kwa sasa suala hilo asiulizwe yeye bali Jeshi la Polisi.

“Muulizeni Kaimu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,” alisema Hapi bila kufafanua.

MTANZANIA Jumapili lilipomtafuta Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya na kumuuliza kuhusu hilo, alijibu kuwa yuko likizo.

“Niko likizo, sijui kama (Mdee) yupo hapo, mtafute Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,” alisema Mkondya.

Alipotafutwa kwa simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, alikiri kuwa ni kweli mbunge huyo alipelekwa hapo kwa mahojiano.

“Aliletwa hapa kwa mahojiano, lakini ni suala la Kanda Maalumu,” alisema Kamanda Hamduni.

Alipoulizwa msingi wa mahojiano hayo, Kamanda Hamduni alisema kuwa hilo ni suala la kipelelezi kupitia Kanda Maalumu.

“Mimi si mpelelezi, anayepeleleza ni Kanda Maalumu,” alisema.

Mdee ambaye alihojiwa kwa saa kadhaa jana mara tu baada ya kuhamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi, hakupatiwa dhamana kwa kile kilichoelezwa askari waliopewa jukumu la kumuhoji hawakuwa na maelekezo mengine.

Awali, MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Wakili wa Mdee, Hekima Mwasipu ambaye alifafanua kuwa mteja wake alihojiwa kwa kosa la uchochezi.

“Ni kweli alihamishiwa Kanda Maalumu leo (jana),” alisema Mwasipu.

MTANZANIA Jumapili lilitaka kufahamu sababu za Mdee kuhamishwa kutoka Kituo cha Oysterbay na kupelekwa Kanda Maalumu ambako ameendelea kushikiliwa licha ya saa 48 kupita, Mwasipu alisema hata yeye alihoji na kujibiwa kuwa ni suala la polisi kanda hiyo.

“Sababu za kumtoa kule na kumleta Kanda Maalumu sielewi ni nini, lakini ninachoweza kusema ni kwamba Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa kushirikiana.

“Ila kwa maelezo yao hata mimi nilipowahoji walijibu kwamba makosa hayo yako chini ya Kanda Maalumu, ni ‘special’ (maalumu), kesi ziko chini ya kanda hiyo,” alisema Mwasipu.

Alipoulizwa kuhusu hali ya mbunge huyo ambaye awali aligoma kula na suala la dhamana, Mwasipu alisema hivi sasa anakula na alihojiwa kwa takribani saa moja, lakini dhamana yake ilishindikana.

“Suala la kufikiswa mahakamani ama kutofikishwa mahakamani hilo ni suala lao polisi, lakini maelezo kaandika na tulifuatilia suala zima la dhamana ikawa ngumu.

“Walisema wao hawana maelekezo yoyote kuhusu dhamana, ni wale ambao walikuwa wanamsimamia Halima kuandika maelezo, hadi jioni hii walinipigia simu, kimsingi leo hatapata dhamana, labda kesho,” alisema Mwasipu.

Awali, waandishi wa MTANZANIA Jumapili walifika kituoni hapo, lakini walizuiwa getini baada ya kujitambulisha kwa madai kuwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalumu hakuwapo ofisini na wala hakukuwa na mtu mwingine aliyekuwapo ili kutoa taarifa kwa waaandishi wa habari na kutakiwa kusubiri nje ya eneo la kituo.

Wakiwa nje ya kituo hicho ambako walikaa kwa saa kadhaa, walishuhudia hali ya utulivu huku ukaguzi ukiendelea, huku baadhi ya watu waliosadikika kuwa wafuasi wa Chadema walizuiwa kuingia na kukaa kando kwa muda kabla ya kuondoka.

Mdee, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), alikamatwa Julai 4, mwaka huu, baada ya Hapi kutoa amri ya kushikiliwa kwa saa 48 kutokana na matamshi aliyodai kuwa ni ya kumkashifu Rais Dk. John Magufuli.

Matamshi hayo anadaiwa kuyatoa katika mkutano aliofanya na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, Dar es Salaam.

Mdee alidaiwa kumkashifu Rais Magufuli kutokana na kuhoji baadhi ya kauli zake zikiwamo zile alizotumia wakati akitangaza kupiga marufuku wanafunzi wa kike wanaopata mimba kurejea shuleni.

Si hilo tu, Mdee pia alihoji kauli nyingine zinazotolewa na Rais Magufuli ambazo alidai kuwa zinakiuka misingi ya sheria.

NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO INGIA WWW.AJIRAYAKO.COM

Kutana na Maalim Fadhil Rashid Kutoka Komoro ni Mtaalam wa Tiba za Asili Anayetibu Magonjwa Yafuatayo

$
0
0
KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM

KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO

DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239

WhatsApp IMO +255785786436

Mchezaji Wayne Rooney Aacha Simanzi Kubwa Man United: Aungana na Everton Tayari Kuja Tanzania

$
0
0
Tayari klabu ya Everton  imethibitisha kumalizana na mshambuliaji wa Man United, Wayne Rooney kwa kumrejesha kwenye klabu hapo kwa mkataba wa miaka miwili.

Kupitia mtandao wa Klabu ya Everton taarifa zimesema wamefikia makubaliano hayo kwa mazungumzo ya muda mrefu na baada ya kutathmini uwezo wake na umri pamoja na uzalendo wake kwa klabu hiyo ambayo ndiyo imemkuza tangia akiwa na mika nane kabla ya kununuliwa na Man united mwaka 2004.

Dili la Manchester United kumchukua mshambuliaji wa Everton, Romelu  Lukaku limehusishwa pia na usajili wa nahodha huyo kipenzi cha mashabiki wa Man united, Wayne Rooney .

Tayari Rooney amekubali kujiunga na Everton kwa kupunguza mshahara wake wa wiki kutoka paundi 250,000 anazolipwa sasa na Manchester United mpaka 180,000 kiasi ambacho Everton wamekiri kukimudu.

Rooney kukubali kujiunga na Everton ni kujipatia tiketi ya kutembelea Tanzania kuja kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia alhamisi ya wiki lijalo (tarehe 13 julai).

Hii itakuwa fursa pekee kwa watanzania kumshuhudia nahodha huyo wa muda mrefu wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United kutua kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Mwishoni mwa mwezi juni afisa utawala na utekelezaji wa kampuni ya SportPesa nchini Abbasi Tarimba alisema kuwa  klabu ya  Everton imethibitisha kuleta timu yake ya kikosi cha kwanza nchini tanzania kitu ambacho kinatupa uhakika kuwa huenda hata Rooney akaja Tanzania wiki ijayo.

Mwanamke Anayefuga Ndevu Kama Mwanaume Avunja Rekodi ya Dunia.........

$
0
0
KATIKA umri wa miaka 25 alionao, mrembo Harnaam Kaur anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa mwanamke mwenye nywele mwilini. Hata hivyo, ameikubali hali hiyo na kuamua kufuga ndevu, jambo linalowashangaza wengi, ikionekana ni jambo geni kwa wanawake.

Amedhihakiwa shuleni, mtaani, kazini kwake na hata katika mitandao ya kijamii, lakini kamwe hakuthubutu kuzinyoa nywele zake, akiamini Mungu alikuwa na sababu za kumfanya awe na mwonekano huo.

Ndiyo maana, leo hii ukikutana naye, ni sura na maumbile yake ya kike ndiyo yatakayokutambulisha kuwa ni mwanamke, ingawa kidevu chake kimechakaa ndevu mithili ya mwanaume, huku mdomo wake ukiwa umezungukwa pia.

Kaur ana tatizo la homoni lifahamikalo kwa Kiingereza kama polycystic ovary syndrome, ambalo humfanya mwanamke kuwa na nywele nyingi zaidi usoni. Anasema awali, wakati anaanza kuota ndevu baada ya kupevuka akiwa na umri wa miaka 11, alipata wakati mgumu shuleni na hata mtaani, akidhihakiwa, jambo lililomkera mno.

Akiwa na umri wa miaka 15, anasema kero dhidi yake zilizidi na hata kufikiria kutaka kujiua, kwani hakuyafurahia tena maisha na hata alilazimika kuwa mtoro shuleni. “Ndiyo, nilitaka kujidhuhuru kwa sababu ya hizi ndevu.

Kuna siku nilinunua vidonge vingi na kutaka kuvimeza ili nife, ulikuwa uamuzi wangu wa mwisho… lakini kama miujiza, sijui kilitokea nini sikuendelea kuwaza kujiua,” anasema Kaur, mkazi wa Slough huko Berkshire, Kusini Mashariki mwa England.

Anasema, awali alijaribu kila njia kuzinyoa nywele zilizokuwa zikiota usoni kwake. Alijaribu pia kubadilisha rangi ya ngozi, kunyoa, kutumia mafuta ya kuondoa nywele mwilini, lakini bila mafanikio. Ikafikia hatua ya kunyoa ndevu kila siku.

Lakini nywele hizo ziliendelea kuwa nyeusi na ndefu zaidi. “Nilikuwa na marafiki waliokuwa karibu nami, walinifariji lakini pia familia ilinisaidia katika wakati mgumu niliokuwa nao,” anasema. Anaongeza kuwa, baadaye alianza kujikubali na kufurahia maisha, licha ya kwamba watu wengi waliendelea kumshangaa.

Wapo pia waliotishia kumuua endapo ataendelea kuziacha ndevu zake. Na katika kuthibitisha kuwa amejikubali, Machi mwaka jana, Kaur alikuwa mwanamke wa kwanza kushiriki maonesho ya Wiki ya Mitindo London akiwa na ndevu zake, Amekuwa akishiriki pia maonesho mengine katika nchi mbalimbali.

Kwake, anasema ni heshima kubwa kwake kutambuliwa na kuwekwa kwenye Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness. Na baada ya kuacha ualimu, amekuwa mwanaharakati akipambana kuelemisha wanawake na wasichana wengine wenye matatizo ya aina yake wajiamini, kwani hawana tofauti na binadamu wengine.

“Kuna niliokosana nao kwa sababu niliamua kuachia ndevu zangu. Lakini nashukuru nimepata nguvu na sasa nataka kuionesha dunia kwamba hili ni tatizo la kawaida, watu hawapaswi kunyanyasika. “Binafsi nimegundua nina nguvu, mimi ni mrembo na mtu asiyeogopa.

Tuzo ya Guinness imenipa nguvu na ujasiri zaidi. Sasa ninajipenda kama mwanamke, ninavutia, nina marafiki na ninapata mikataba ya kazi, kimsingi maisha yanaendelea,” anasisitiza kimwana huyo ambaye amekiri kutokuwa na mahusiano kimapenzi, ingawa anaamini wakati ukifika atampata mwandani wake.

Chanzo:Habarileo

Mwanamke Ukiona Unatongozwa na Kila Mwanaume Ujue wewe ni....

$
0
0
Kuna wanawake kadhaa huwa wanafurahia sana kuwa wao kila wanapopita wanaume wanawatongoza. wanaongea kwa majidai sana na furaha kama vile ni jambo la kujivunia.

Ukweli ni kuwa mwanamke ukiona unatongozwa kila sehemu na kila mwanaume ujue wewe ni kimeo sana. sana yaani kila mtu anaona kuwa ana uwezo wa kukupata. unakuwa kama vile daladala au bodaboda kila mwenye uwezo wa kusimamisha anasimamisha. ni kuwa upo kiwango cha kuwa used anytime na anybody. so epuka hali inayokufanya uonekane cheap.

usifurahie kuwa kila unapopita watu wanapiga miluzi na kukufurahia wakikuita ukaona kuwa una nyota ya kupendwa. ujue una nyota ya mbwa kupigiwa miluzi au nyota ya uchafu kufuatwa na inzi. haiwezekani kila mtu anakusimamisha kukutaka kimapenzi. muuza maji, dereva wa boda boda, dereve wa daladala. dereva taxi, jamaa tu njiani kakuona, mwanasheria,ukienda hosp dokta anakutaka, nurse naye anakutaka, ukienda shule mwalimu naye anakutongoza. ukienda ofis flan hr naye anakutaka, mlinzi naye...

yaan wewe unatakwa na kutongozwa na kila mwanaume hapa duniani kasoro tu wale wenye kujiheshimu sana ingawa nao ukiwa kalia maeneo yao ya siri nao wanakugagadua. halafu unajisifu kwa wenzio kuwa wewe unapendwa sana na wanaume una mvuto.... hata uchafu nao husema una mvuto kwa kuwavutia inzi na wadudu wengine kama funza,kunguru n.k

By Komeo Lachuma

Mtoto wa Jakaya Kikwete Aula Etihad Airways......

$
0
0

Mtoto wa Jakaya Kikwete Aula Etihad Airways......Apata kazi ya Urubani wa Ndege....


SOMA Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo Jumatatu


Breaking News: Waziri wa Kikwete Arudisha Hela za Escrow

$
0
0
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amerejesha Tsh 40.4 milioni alizopewa katika mgao wa fedha zilizochotwa kutoka akaunti ya Tegeta Escrow

Download App ya Bongo Specially Kwenye Simu Yako Kupata Habari za Mastaa na Udaku Bongo

$
0
0
Bonyeza Hapa Kudownload Application ya Bongo Specially

Usipitwe na Mambo Mazuri

Faini za Sh12.8 Bilioni Makosa ya Barabarani zaibua Mjadala

$
0
0
Mwananchi
Dodoma. Kuongezeka kwa makusanyo yatokanayo na faini za makosa ya barabarani na mbinu zinazotumiwa na trafiki, kumeibua mjadala kwa wadau wa usafiri na usafirishaji.

Pamoja na mjadala huo, Kamanda wa Trafiki wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Awadh Haji amesema askari wake wataendelea kuvizia barabarani ili kukamata madereva wanaovunja sheria.

Kamanda Awadh ametoa msimamo huo jana  alipoulizwa kuhusu ongezeko la kiwango kinachokusanywa kwa makosa ya barabarani na sababu za askari wa usalama barabarani kujificha wakiwa na kamera maalumu wakati wakivizia kukamata  madereva wanaoendesha kwa kasi isiyolingana na viwango vilivyopo barabarani.

Mwananchi ilitaka maoni ya wadau mbalimbali wa barabara baada ya Kikosi cha Usalama Barabarani kutangaza ongezeko kubwa la makusanyo ya faini kutoka Sh7.3 bilioni kwa kipindi cha kati ya Januari na Mei mwaka 2016, hadi kufikia Sh12.8 bilioni kwa kipindi kama hicho mwaka huu.

“Kujificha ni mbinu ya medani kufanikisha ukamataji wa madereva wasiotii sheria,” alisema Kamishna Awadh.

“Tutaendelea kufanya hivyo ili kubadilisha tabia zao. Wakiwa na hofu ya kukamatwa, huepuka kufanya makosa.”

Wananchi na wadau wa usafirishaji wamekuwa na maoni tofauti baada ya Kaimu Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya kutoa taarifa ya mapato yaliyokusanywa na trafiki kati ya Januari na Mei mwaka huu kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka jana.

Taarifa hiyo aliyoitoa katikati ya mwezi uliopita ilibainisha kukusanywa kwa Sh12.8 bilioni mwaka huu kutokana na makosa 404,571 zikilinganishwa na Sh7.3 bilioni baada ya makosa 246,695 kukamatwa na askari hao mwaka jana.

Wakati idadi ya makosa ni ongezeko la takriban maradufu, ni ongezeko la theluthi moja tu ya kesi zilizofikishwa mahakamani mwaka huu kulinganisha na mwaka jana.

Mkondya anaamini ufanisi wa kikosi hicho kukabiliana na makosa ya barabarani unaongezeka ikilinganishwa na ongezeko la vyombo vya usafiri vya moto.

Pia, kuwepo kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara dhidi ya makosa yaliyoripotiwa.

“Makosa hayalingani na ongezeko la vyombo vya moto. Kazi kubwa imefanyika,” alisema Mkondya alipozungumza na gazeti hili jana.

Akibainisha ongezeko la changamoto zilizochangia kuongezeka kwa makosa hayo, Awadh alisema licha ya ongezeko la vyombo vya moto barabarani, wakazi wa jiji la Dar pia wameongezeka hivyo kuongeza changamoto za usafiri.

Kutokana na ongezeko la makosa hayo sambamba na faini kubwa zilizotozwa, mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi alisema kikosi hicho na Jeshi la Polisi kwa ujumla kimejisahau hivyo kuanza kutekeleza majukumu ya taasisi nyingine.

Alisema ongezeko la makosa hayo halipaswi kuwa jambo la kujivunia kwa kuwa linathibitisha kushindwa kwa watendaji waliopewa jukumu hilo ambao wanaona ni rahisi kwao kuongeza makusanyo ya faini, kazi ambayo inatakiwa kufanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Kimsingi aliyetangaza suala hilo alipaswa kujiuzulu kwa sababu amethibitisha kushindwa kukabiliana na changamoto zilizopo,” alisema mbunge huyo maarufu kama Sugu.

Ili kupunguza makosa hayo pamoja na madhara yake kwa jamii ikiwamo vifo vitokanavyo na ajali pamoja na ulemavu wa kudumu, Mbilinyi alilitaka jeshi hilo kuongeza juhudi za kuelimisha madereva badala ya kugeuza makosa kuwa chanzo muhimu cha mapato ya Serikali.

Vilevile alidai askari huwekewa malengo ya makusanyo kwa siku, akisema hata askari hulalamikia suala hilo.

“Tunaokutana nao barabarani wanatuambia tuwasemee. Wakati mwingine wanawabambikia makosa madereva ili kufikia malengo waliyowekewa,” alisema.

Kadhalika alipinga namna tochi zinavyotumika vibaya akieleza kwamba kamera hizo hazitakiwi kufichwa badala yake zitumike hadharani kama ilivyo kwenye mataifa mengine yaliyoendelea.

“Dereva akijua tochi ilipo ataenda mwendo mdogo lakini akishaipita basi atakimbia kufidia muda wake. Hilo halifai nchini kwa wakati huu,” alisema.

Kuhusu kubambikiwa makosa, Jonas Mangula, mkazi wa jijini hapa alisema Machi aligundua leseni yake inatakiwa kurudishwa baada ya pointi zake kumalizika kutokana na makosa lukuki aliyoandikiwa.

Alisema mpaka muda huo, alikuwa amekamatwa mara nne kwa kosa la kuendesha kasi, lakini alikuwa bado hajalipa faini zake. “Nilichanganyikiwa. Kurudisha leseni, maisha yangekuwa magumu hapa mjini,” alisema.

Alisema hata alipojaribu kuomba ushauri kutoka kwa trafiki mmoja, naye alikuwa hajui chochote kuhusu kuisha kwa pointi hizo hivyo akalazimika kwenda kulipa kiasi alichokuwa anadaiwa.

“Nilipolipa tu, makosa yote yalifutika na sasa sidaiwi tena,” alisema Mangula.

Kuhusu makosa hayo, alisema alikuwa anakamatwa akiwa na haraka hivyo kuruhusu aandikiwe: “Wakati mwingine unaona spidi haizidi hata 30 lakini ili kuokoa muda, unapunguza maneno.”

Lamishna Awadh pia alizungumzia hoja ya baadhi ya wadau kwamba makosa hayo yanachangiwa na madereva wanaopewa leseni bila ya kupitia mafunzo, akisema kwa taratibu zilizopo za kupata leseni  ni ngumu na yeyote anayebainika hushtakiwa kwa kughushi nyaraka.

“Hatutoi leseni kwa wenye vyeti feki. Shule za udereva huwaleta wahitimu wake wakiwa na magari waliyotumia kuwafunza kwa majaribio. Wanaofuzu pekee ndiyo hupewa leseni. Hata anayekuja mwenyewe, lazima ajaribiwe,” alisema.

Akizungumzia ongezeko la ajali kwa asilimia 60 ndani ya mwaka mmoja, Mratibu wa Shirikisho la Vyama vya Wasafirishaji Afrika Mashariki (Fearta), Emmanuel Kakuyu alisema usimamizi umeongezeka na kuimarishwa tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

“Askari wameongezeka barabarani na madereva wanasimamishwa zaidi,” alisema Kakuyu.

Licha ya kuimarika kwa usimamizi unaohusisha doria kama alivyobainisha Awadh, mchumi na mwanaharakati wa kijamii, Profesa Samwel Wangwe alisema ongezeko la mapato hayo huenda likawa limechangiwa na kubadilishwa kwa mfumo wa malipo unaotumiwa na jeshi hilo.

“Madereva wamelipa zaidi kutokana na makosa yao. Mfumo wa kielektroniki unaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye hili,” alisema Profesa huyo. 

Benjamini Mkapa Kukabidhi Nyumba 10 Hospitali ya Wilaya ya Chato Kwa Magufuli......

$
0
0
RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amewasili wilayani hapa mkoani Geita ambapo leo anatarajiwa kukabidhi nyumba kumi kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato zilizojengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.

Mkapa ambaye alikuwa ameambatana na mkewe, Mama Anna Mkapa walipokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli aliyekuwa sambamba na mkewe, Mama Janeth Magufuli.

Katika msafara huo pia Rais mstaafu Mkapa ameambatana na Balozi wa Japan hapa nchini, Masaharn Yoshida ambaye leo anakabidhi mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti kwa chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato (AMCOSS). Rais mstaafu, Mkapa anatarajiwa pia leo kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na mwenyeji wake Rais Magufuli utakaofanyika katika Uwanja wa Mazaina ulioko mjini

Chanzo: Habarileo

Mtanzania Akimbia Mshahara wa Sh 400 Milioni Marekani...Arudi Tanzania

$
0
0
Kwa uamuzi huu, huwezi kuhoji kiwango cha uzalendo cha Benjamin Fernandes, Mtanzania wa kwanza kuhitimu shahada ya uzamili Chuo Kikuu cha Biashara Stanford nchini Marekani.

Fernandes, ambaye awali alikuwa mtangazaji wa televisheni, ameeleza siri ya kukataa mshahara wa Sh425 milioni kwa mwaka na  badala yake kurudi Tanzania kujenga Taifa.

Baada ya kumaliza masomo yake Marekani, Fernandes alikuwa akifanya kazi katika taasisi ya tajiri namba moja duniani, Bill Gates iitwayo Bill and Melinda Gates Foundation. Sasa ameamua kuacha kazi yenye mshahara mnono na kurejea nchini kusaidia vijana.

Fernandes pia alikuwa akikaa meza moja na mmiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg alipokuwa akifanya kazi katika taasisi hiyo ya familia ya Gates.

Akihojiwa na televisheni ya Millard Ayo, Fernandes alisema kampuni mbalimbali Marekani zinamtafuta kwa ajili ya kwenda kufanya kazi kwa ahadi ya mshahara mnono, lakini amekataa kwa kuwa anataka kuwasaidia Watanzania.

“Watu wengi wananiuliza kwanini nimerudi nyumbani. Ni kweli nilikuwa napewa offer (dau) ya Sh425 milioni kufanya kazi kampuni mbalimbali Marekani, lakini huwa nilikuwa nawaambia nimesharudi nyumbani. Mimi motivation (motisha) yangu si hela ila upendo kwa nchi yangu,” alisema Fernandes.

Alisema alifikia uamuzi huo akijua kuna changamoto atakazokutana nazo.

Alisema ana mpango wa kuwatengenezea njia vijana ili elimu yao iwe msaada kwa jamii.

“Nasikitika watu wananipigia simu wananimbia nina vyeti hivi na hivi, mimi sijali sana elimu yako. Kapige kazi kwa bidii na hiyo kazi itakuheshimu,” alisema Fernandes.

Alieleza asilimia 70 ya watu  ni vijana wenye umri chini ya miaka 25 ambao wanatakiwa kuwa na  mchango katika maendeleo.

Fernandes alisema anataka kuonyesha jinsi teknolojia inavyoweza kuwa msaada kwa kutumia simu za kisasa zinazotumiwa na watu takribani 11.5 milioni nchini.

Aliiomba Serikali kusaidia vijana ili wawe chachu kwa ajili ya mafanikio ya wengine.

“Vijana wanatakiwa watamani kuwa mtu fulani, jambo ambalo linasaidia watoto kukua  na kutimiza ndoto zao,” alisema.

Fernandes alisema endapo atakutana na Rais John Magufuli, atakuwa na mengi ya kumwambia  hasa maendeleo ya Taifa.

“Kwa mfano, nitamshauri Rais kuimarisha mahusiano mazuri na sekta binafsi, biashara na Serikali kuzingatia sheria ili kukuza uchumi na kufanya biashara kuwa nyingi nchini.

Alisema teknolojia bado haijapewa kipaumbele ili kusaidia wanaoishi vijijini na kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu kwa watoto wadogo walio na umri chini ya miaka 10 wanaoweza kuwa chachu ya maendeleo.

“Kitu cha nne ningeshauri Serikali iwasikilize wawekezaji wa nje ili sisi kama nchi tufaidike. Kingine ni nidhamu ambayo Rais Magufuli amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inazingatiwa hivyo ahakikishe vijana wanakuwa na nidhami,” alisema Fernandes.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Hamis Mwinyimvua alisema ni jambo zuri kwa Watanzania wanaosoma nje ya nchi kurudi na kuleta ujuzi wao nchini.

“Kama amejisomesha kwa fedha zake, anaweza kurudi au kuamua kubaki, lakini kikubwa anaweza kufanya kama wafanyavyo diaspora (wazawa wanaoishi nje), fedha wanazopata zinatumwa Tanzania na zinatumika kwa maendeleo,” alisema.

 Mwananchi
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images