Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104663 articles
Browse latest View live

Kocha Pluijm Avunja Ukimya Tetesi za Kurudi Yanga

$
0
0
Kocha mkuu wa timu ya Singida United, Hans Pluijm amesema kubaki kwake ndani ya timu  hiyo kutategemea uamuzi wa mlezi wa timu, Mwigulu Nchemba ambaye alimpeleka kwa lengo la kuifanya timu hiyo kuwa tishio kwenye Ligi Kuu.

Timu hiyo imeondoka mjini Dodoma ilipokuwa imeweka kambi ys muda mfupi ili kuuzoea Uwanja wa Jamhuri.

 Taarifa zinasema timu hiyo ngeni Ligi Kuu itautumia kwenye mechi zake za mwanzo wa ligi pamoja na zile watakazocheza na vigogo Simba na Yanga.

Gazeti hili lilizungumza na kocha huyo kuhusu mipango yake kwenye timu hiyo mpya, ambapo moja ya jambo aliloongelea ni kuhusu tetesi kuwa yupo Singida United kwa muda na kwamba atarajeshwa Yanga iwapo George Lwandamina atatimuliwa, jambo ambalo alilikanusha.

 

Mwimbaji Rose Mhando Awashukia Wanaomsema Vibaya.......

$
0
0
STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha kuwa mwimbaji ambaye nyimbo zake zinawabariki wengi.

Rose aliliambia Wikienda kuwa, watu wamekuwa wakimzushia mambo mengi ya ajabu, lakini hawajui anachokifanya kwa sasa ila siku wakija kugundua wataumbuka ndiyo maana yupo kimya hata kwenye muziki huo hivyo wanaomsema na kumtakia mabaya anawaombea kila kukicha na Mungu atawalipa kila mmoja kwa wakati wake.

“Najua aliyeniita katika huduma ya uimbaji ni Mungu na siyo mwanadamu, hivyo kwa kila jambo namsikiliza yeye siyo mwanadamu mwenzangu, siogopi wanaonisema vibaya maana ninaamini aliyeniita hataniacha,” alisema Rose ambaye mara kwa mara amekuwa akiandikwa kwa stori za utapeli.

Mimba ya Mrembo Hamisa Mobeto Kizungu Mkuti.......

$
0
0

WAKATI yakisemwa mengi juu ya ujauzito alionao ambao kwa sasa hauhitaji miwani ili kuuona, mwanamitindo matata Bongo, Hamisa Mobeto amepasua jipu juu ya mimba hiyo kufuatia kutajwa kwa msanii wa Bongo Fleva.

Kwa siku kadhaa sasa, kumekuwa na habari nyingi juu ya Hamisa kudaiwa kubeba ujauzito wa jamaa huyo ilihali akijua msanii huyo ana mpenzi wake ambaye amekuwa akikwaruzana naye mara kwa mara.

HAMISA AJIFICHA
Ilielezwa kwamba, kufuatia maneno mengi juu ya jambo hilo, Hamisa amekuwa akijifi cha kukwepa vyombo vya habari, lakini Wikienda limefanikiwa kumbana na kufunguka mazito.


KWELI MJAMZITO
Hamisa ambaye wengi wamekuwa hawana uhakika kama kweli ni mjamzito, mbali na kukiri kuwa kweli ni mjamzito wa mtoto wa pili baada ya yule wa awali wa kike aliyezaa na bosi maarufu wa redio jijini Dar, aliliambia Wikienda kuwa, yanasemwa mengi juu ya mimba yake hasa aliyempachika lakini yeye hajali kwani yupo tayari kupokea matusi ya jumla na rejareja.

Wikienda: Je, ni kweli mimba ni ya msanii wa Bongo Fleva kama inavyosemekana?
Hamisa: Siko tayari kusema ujauzito ni wa nani. Watu waelewe hivyohivyo wanavyoelewa.

Wikienda: Lakini kila mtu anajua ni wa msanii huyo, je, ni kweli?
Hamisa: Wanaomtaja baba wa ujauzito wangu hawanisumbui kabisa na wakae wakijua hivyo.

Wikienda: Lakini huoni kwamba ni tatizo kuzaa tena nje ya ndoa baada ya yule wa kwanza uliyezaa na bosi wa redio bila kufunga ndoa?

Hamisa: Hayo ni maisha yangu na kama nilivyosema, maneno ya watu hayanisumbui.
Hata hivyo, mazungumzo kati ya Wikienda na Hamisa yaliishia hapo kwa maelezo kwamba hataki tena kuulizwa jambo hilo kwani kila kitu kinajulikana.

MIMBA YA PILI?
Hii ni mimba ya pili ambayo Hamisa anadaiwa kupachikwa na msanii huyo baada ya ile ya awali aliyopachikwa mwaka jana kuchoropoka na kuwa gumzo kubwa baada ya mpenzi wa mwanaume huyo kuja juu na kuanzisha bifu ambalo halijawahi kuzimwa hadi leo.

STORI: IMELDA MTEMA NA MUSA MATEJA | IJUMAA WIKIENDA, DAR

Siku Tatu za Hatma ya Lowassa Polisi

$
0
0
ZIMEBAKI saa 72 kuanzia leo zenye umuhimu mkubwa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Hali hiyo inatokana na taarifa kuwa kiongozi huyo ataripoti polisi siku ya Alhamisi ambako huko itajulikana kama ataendelea kuhojiwa na jeshi hilo kuhusiana na tuhuma za kutoa kauli ya uchochezi, kuachiwa huru au kufikishwa mahakamani. Siku moja ina saa 24, hivyo jumla ya saa 72 ndizo zinazokadiriwa kubaki kuanzia leo hadi kufikia Alhamisi.

Awali, Lowassa ambaye sasa ni mmoja wa makada muhimu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliripoti polisi Juni 27 mwaka huu kwa amri ya jeshi hilo kutokana na madai ya kutoa kauli ya uchochezi.


Akizungumza na Nipashe jana, Wakili wa Chadema), Peter Kibatala, alisema hatima ya Lowassa ya kuachiwa huru au kufikishwa mahakamani inatarajiwa kujulikana atakaporipoti tena makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam Alhamisi wiki hii.


Hiyo itakuwa ni mara ya tatu kwa mwanasiasa huyo aliyekuwa Waziri Mkuu wakati wa utawala wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete kufika kwenye ofisi za jeshi hilo kuhusiana na madai hayo ya uchochezi.

Awali, Lowassa aliyehama Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa mchakato wa kumsaka mgombea urais wa chama hicho tawala katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015, aliripoti kwa mara ya pili Juni 29, mwaka huu.


Lowassa ambaye alijiunga na Chadema Julai 28, 2015 na kupewa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho kuwania urais katika uchaguzi mkuu uliopita na kuungwa mkono na muungano wa vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF), anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam, Mwita Waitara (Chadema).


Katika hafla hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa kauli ya kumshauri Rais Magufuli kutafakari upya hatima ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu, maarufu Uamsho, wanaoshikiliwa mahabusu kwa zaidi ya miaka minne wakikabiliwa na mashtaka ya tuhuma za ugaidi.


Kwenye hafla hiyo, Lowassa anadaiwa kutamka kuwa ni jambo la fedheha kwa nchi illiyopata uhuru zaidi ya miaka 50 kuwaweka mahabusu viongozi wa dini bila kesi kusikilizwa mahakamani.
Kutokana na kauli hiyo, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI) ilimwandikia barua ya kumhitaji katika ofisi za makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Juni 27, mwaka huu ambako alihojiwa kwa saa nne kisha kuachiwa na kuhitajika kuripoti tena kituoni hapo siku mbili baadaye, lakini siku hiyo alipangiwa tena siku ya kuripoti ambayo ni Alhamisi ya wiki hii kwa madai kuwa upelelezi ulikuwa bado haujakamilika.

Katika mazungumzo yake na Nipashe jana, Wakili Kibatala alisema tarehe ya kuripoti kwa Lowassa kituoni hapo haijabadilika na ataitikia wito huo kama alivyoambiwa awali.
Julai 2, mwaka huu, ikiwa ni siku chache baada ya Lowassa kutoa kauli hiyo, Rais Magufuli alilitaka Jeshi la Polisi kuwaweka mahabusu watu wote wanaowatetea masheikh hao ili wasaidie upelelezi.


Wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam wiki iliyopita, Rais Magufuli aliwaonya wanasiasa wanaowatetea masheikh hao na kuwataka kukaa kimya.


“Wanaoropoka wote wakamateni wawekeni ndani wasaidie polisi, nataka polisi mfanye kazi yenu, wajifunze kufunga mdomo wao, wataumia.

Wengine wanajitokeza hadharani kupinga, nasema wakamateni hata kama wanatembea taratibu,” alisema Rais Magufuli.


Am Very Beautiful but Cant Keep a Man for Long

$
0
0
Hi Guys My Name is Cynthia. Iam a young beautiful woman and alot of men keep chasing me. But i have noticed a very worrying thing, i cant keep a man for more than 4 months. Every man who hooks up with me drops me after some time. Iam financially stable so i cant say iam a burden to them. Whenever i try to ask them what is the problem, none has told me the truth. They simply say, You are a very beautiful and sexy lady but you are not my Type. Iam now losing my self esteem. Is this Beauty of mine a curse?

yours Cynthia

Makosa Makubwa Tunayofanya Wanaume Katika Mapenzi

$
0
0
NAWAPA KISA KIFUPI TUU AMBACHO KINANISIBU KWA SASA,

Mimi ni mwanaume, nimeoa ila kwa sasa mke wangu na mtoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine kikazi.
Familia yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko tayari kukopa mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume). Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially akina mama.

Hivi karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye, naye yuko mbali na mkewe japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi miwili hivi, then hurudi kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa akinisumbua sana mara kwa mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani nilimpa, akanirudishia. Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa ulipofika akaniambia kuwa Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela, hivyo afanye atakaloweza kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba nimkopeshe tena, basi nikawa mpole tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela kubwa (30,000).

Baada ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake anaumwa anatakiwa aende kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr. atatuma hela wiki ijayo. Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake akafariki ikawa ni msiba huku mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole. Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua alipatwa na matatizo, acha iwe msaada.

Baada ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa anamdai laki 4, ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa nimshauri afanyeje maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba alitaka nimsaidie tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo kidogo hivyo hivyo.

Siku moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna kitu anataka kuniambia. Nilipompigia alinishukuru kwa yote niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo baadaye akaniambia njoo tulale, nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji kuwa na mimi. Ameniambia hawezi kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo na liwe lazima awe na mimi anipe tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata simu na tangu hapo nimejikuta kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na hali ya kuchanganyikiwa kimawazo. ananitumia message za mapenzi kibao, japo mimi nimeamua kutokujibu message hizo.

Najua fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu ni kuwa haya yote yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na familia yake. Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na hatumi hela kwa visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau, naombeni comment zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the situation. Sisemi kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna wakati wa kupata na kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe mwanaume fanya juu chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni wako, lakini hawa wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia majaribuni. Mimi sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya mapenzi lakini mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani alaumiwe?

Halima Mdee Afikishwa Kwa Pilato.......

$
0
0
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Kisutu leo asubuhi  akisubiri kesi yake.

Mdee, alikamatwa na Polisi siku sita zilizopita kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi kwa madai ya kumkashifu Rais John Magufuli.

Hapi aliagiza Mdee akamatwe na kuwekwa ndani kwa saa 48 kwa makosa hayo pamoja na ya uchochezi.

JE Una Tatizo la Nguvu za Kiume , kukosa Hamu ya Tendo, Kushindwa Kurudia Tendo au Maumbile Madogo ya Uume?

$
0
0
JE, UNA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME, KUKOSA HAMU YA TENDO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO AU MAUMBILE MADOGO YA UUME? SOMA HAPA 👇👇👇👇
Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, sio Tanzania tu bali duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo sio ugonjwa ila ni dalili ya ugonjwa. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili.

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME HUSABABISHA MAMBO KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
@Markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye kisukari kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @220,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6.5 @130,000/=
3.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @130,000/=
4.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kurudia tendo hata mara 3 bila kuchoka @130,000/=
KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :-
@Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr.

Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa no (+255)
0767447444 na 0714335378

NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na hazina kemikali wala madhara kwa mtumiaji. Zimethibitishwa kiafya.

Mume Wangu Hanitoshelezi Kitandani-Now I’m Sleeping With My ex'' - lady

$
0
0
Hello, please post this as you might just be helping me save my future.

My name is Daisy. I’m 25 and might be getting married in December, if only I will say yes to my man.

He’s 31 by the way, but I told him I was going to think about it. To cut the story short, I’m really scared of getting married to him because I wouldn’t want to cheat on my husband. This guy is not even a one minute man when it comes to scx. He is a 5 seconds person. I’ve complained severally and he has tried to take all kinds of drugs to make him last but they don’t work.

Whenever we are ready to get down and he is inside me, he just thrusts for 5 seconds and that’s it. Then he leaves me wanting and he can’t go a second round because his body can’t do it. There was a time I was so horny, I had to go meet my ex and yes he made me feel like a woman. But with my soon to be hubby I don’t feel that way. He does not smooch me, he just goes straight in and then everything is over in a blink. I’m just frustrated and I need advice because he has tried basically every solution including Viagra, but the after effect was bad.

How can I be a faithful wife after I get married to this guy when he can’t even satisfy my urge? What should I do?

Rais Magufuli Awataja Waliotengeneza Maisha yake ya Kisiasa Hadi Kuwa Kiongozi

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa Marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ndio waliotengeneza maisha yake ya kisiasa hadi kuwa kiongozi.

Rais Magufuli ameyasema hayo Jumatatu hii, wilayani Chato wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation. “Nakumbuka siku hiyo tulikuja hapa Chato na wewe (Mkapa) Msafara ulisimamishwa na ukawaambia wananchi wa Chato nichagulieni huyu, nakumbuka ulikuwa umevaa viatu vyekundu,” amesema na kuongeza: “Kwa bahati nzuri, wananchi wa Chato wakanichagua, baadaye ukanichagua kuwa naibu waziri. Wewe ulinitangaza, sikustahili chochote, maneno yako yalikuwa na nguvu kwa Watanzania.” “Kwangu mimi nyinyi mlitengeneza maisha yangu katika uongozi. Pia nawashukuru sana viongozi wa awamu ya kwanza, Nyerere na Mwinyi ambao walitengeneza mazingira mazuri ndani ya Chama cha Mapinduzi. Mimi sina cha kuwalipa jukumu langu ni kuwatetea na ninawaahidi Watanzania kuwa nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote, namuomba Mungu asinifanye nikawa na kiburi namuomba asinifanye nikasahau nilipotoka.”

TOA MAONI YAKO HAPA

Mbunge Halima Mdee aachiwa kwa Dhamana

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Victoria Nongwa imemuachia Mbunge Halima Mdee kwa Dhamana ya ahadi ya Shilingi 10 pamoja na Wadhamini wake wawili, na atatakiwa  kurudi mahakamani tarehe 7,

Katika kesi namba 218 ya 2017, Kupitia Nasorro katuga Wakili wa Jamhuri, Halima Amesomewa shitaka la kutumia lugha ya matusi Dhidi ya Rais Magufuli "Rais anaongea Hovyo, Afungwe Breki" Hata hivyo alipoulizwa kama nikweli Mdee alikana shitaka hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee alifikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Leo Jijini Dar es salaam majira ya Asubuhi.

 Halima Mdee (Chadema), alikamatwa Julai 4 Jioni, na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi. Kwa kile kilichodaiwa alitoa lugha ya kumtukana Rais Magufuli.

Kisiwa Cha Wanaume Pekee Japan Chatambuliwa na Unesco

$
0
0
Kisiwa cha Okinoshima nchini Japan, ambapo wanawake hawaruhusiwi kufika, kimetambuliwa kama Turathi ya Ulimwengu na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, Unesco.

Kisiwa hicho cha Okinoshima huchukuliwa kuwa kitakatifu kiasi kwamba ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kuzuru, gazeti la Asahi Shimbun linasema.

Na hata wanapofika huko, hawaruhusiwi kuondoka na chochote, hata kipande cha nyasi.
Jopo maalum liliwasilisha pendekezo kwa Unesco watambue rasmi kisiwa hicho kama turathi ya ulimwengu mwezi Mei.

Katika kisiwa hicho, kuna madhabahu ya Munakata Taisha Okitsumiya, ambayo ni ya kumtukuza miungu wa baharini.

Katika kisiwa cha Okinoshima, kuliandaliwa matambiko kwa ajili ya usalama wa meli na pia wakazi wa Japan walitumia kisiwa hicho kuwasiliana na wakazi wa rasi ya Korea na China kati ya karne ya nne na tisa, gazeti la Japan Times linasema.

Bado kuna miiko kuhusu kisiwa hicho, mfano wanawake kupigwa marufuku.
Wageni wa kiume pia hutakiwa kwanza kuvua nguo zao zote na kufanya tambiko la kujitakasa.
Aidha, hawatakiwi kufichua chochote kuhusu waliyoshuhudiwa wakiwa kwenye kiswa hicho.

"Haya ni baadhi ya mambo ambayo itabidi yazingatiwe iwapo kitaorodheshwa kuwa turathi," anasema Asahi Shimbun, na kueleza kuwa huenda kisiwa hicho kikawa maarufu sana kwa utalii.

Zamani, hata kabla ya madhabahu kujengwa, kisiwa cha Okinoshima kilikuwa kikitumika kwa matambiko na mabaharia na pia kilihusika katika mashauriano ya kibiashara kati ya watu wa Korea na watu wa China.

Maelfu ya vitu vya kale, vilivyowekwa katika kisiwa hicho kama zawadi kutoka maeneo ya mbali, vimepatikana katika kisiwa hicho ikiwa ni pamoja na pete za dhahabu kutoka rasmi ya Korea, gazeti la Japan Times linasema.

Kisiwa hicho kwa sasa hupokea wageni siku moja pekee, 27 Mei, na sheria za kale bado hufuatwa.
Idadi ya wageni wanaoruhusiwa kufika kisiwa hicho kwa mwaka ni 200 pekee, Na lazima watimize matambiko yote baharini, na lazima wawe wanaume.

"Msimamo wetu kuhusu jinsia hautabadilika hata kama kitaorodheshwa kuwa Turathi ya Ulimwengu," afisa wa Munakata Taisha aliambia gazeti la Mainichi Daily, awali.

Chadema Wamkalia Kooni Prof Lipumba..Waja na Operation 'Ondoa Msaliti Buguruni (OMB)

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza operesheni maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la kutatua mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).

Operesheni hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi leo Julai 10, ambapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga mkono Katibu wa CUF, Maalim Seif.

Akizungumza leo wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una athari kubwa kwa vyama vya upinzani hivyo  wameamua kuungana pamoja ili kuimarisha vyama vya upinzani chini ya mwavuli wa Ukawa.

Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, ameeleza kuwa baada ya kukaa na viongozi wa CUF ili kujua kiini cha mgogoro huo wamebaini kuwa siyo mgogoro ndani ya chama, bali unachochewa na CCM wanaomtumia Profesa Lipumba ambaye wamemuita kama ni msaliti.

"Sisi kama Chadema tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF kumuondoa msaliti Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi halali wa CUF watarudi Buguruni, "amesema Kubenea.

 Kadhalika amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa mameya wa Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa viongozi wenye ushirikiano na Profesa Lipumba.

CUF Lipumba, CUF Maalimu Seif Wazichapa tena Mahakamani

$
0
0
HALI ya Taharuki Kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeibuka Leo wakati wafuasi wa pande wa Chama cha Wanachi (CUF)  kukutana kwenye kesi zilizfunguliwa na bodi ya wadhamini ikidai ruzuku za chama hicho zilizodaiwa kuzuiliwa na Msajili wa vyama vya siasa Nchini.

Wafuasi hao waligawanyika kundi moja likiwa  upande wa katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Ahmad na wengine kuwa kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Professa Ibrahimu Lipumba walishikana na mashati na kurushina maneno mahakamani hapo.

Watanzania Wamechoka Kuonewa – Rais Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka viongozi wa halmashauri za Wilaya na Mikoa kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu na kutumia vizuri fedha za serikali huku akisema serikali yake itakuwa upande wa wanyonge kwa sababu Watanzania wamechoka kuonewa kila siku.


Rais Magufuli ameyasema hayo Jumatatu hii, wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 za wahudumu wa afya, zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.

Soma taarifa kamili:


Kutana na Maalim Fadhil Rashid Kutoka Komoro ni Mtaalam wa Tiba za Asili......

$
0
0

KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239/

WhatsApp IMO +255785786436/

Rais Magufuli Atoboa Siri "Hata Mtoto wa Mdogo Wangu Alizaa Akiwa Shuleni"

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema anapenda taasisi zinazohimiza maendeleo kama Mkapa Foundation na si zinazohamasisha wanafunzi wazae kisha warudi shule.



Rais Magufuli ameyasema hayo Jumatatu hii, wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 za wahudumu wa afya, zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.

“Nazipenda taasisi zinazohimiza maendeleo kama Mkapa Foundationa na si zinazotaka watu wazae halafu warudi shuleni. Mmekalia kusema kuwa watu wazae halafu warudi shule, sasa si watazaa kila mahali,” alihoji Rais Magufuli.

“Hata kwangu kuna watu wanaozaa na wala hawajabakwa, hata mtoto wa mdogo wangu alizaa bila kubakwa, alipoulizwa imekuwaje akajibu kwa kisukuma alafu akanizalia mtoto akamuita John, akakaa kidogo akazaa tena mtoto mwingine akamwita Samia,” alisema Rais Magufuli huku watu wakicheka.

Na Emmy Mwaipopo

Diamond Platnumz Athibitisha Yeye ni King Of Bongo Flava...Atoa Nyimbp ya Tatu Ndani ya Mwenzi Mmoja..Itazame Hapa

$
0
0
Siku 20 baada ya Diamond Platnumz kuachia video zake mbili mpya ya ‘Fire’ aliyomshirikisha muimbaji wa Nigeria Tiwa Savage na ‘I Miss You’, leo July 10 2017 ameamua kuachia video nyingine mpya ya wimbo wake mpya wa ‘Eneka’ ambao aliuachia kwa kushitukiza.

Unaweza kutazama video mpya ya Diamond Platnumz na kuniachia comment yako, Diamond atapita kuzisoma.

Afya ya Robert Mugabe Utata Mtupu....Adaiwa Kufichwa Hospitalini Nchini Singapore

$
0
0
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, yuko nchini Singapore kwa ajili uchunguzi wa afya yake, huku maofisa wa serikali wakikanusha taarifa za kiongozi huyo kuzidiwa,

Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Sunday Mail Rais Mugabe aliondoka nchini humo Ijumaa wiki iliyopita kuelekea nchini Singapore kwa matibabu na kwamba kiongozi huyo anatarajiwa kurejea katikati ya wiki hii.

Safari za rais Mugabe nchini Singapore zimeongezeka kwenye miaka ya hivi karibuni ambapo mara ya mwisho kuwa nchini humo ilikuwa ni mwezi Mei ambapo pia alisafiri kwa sababu za kimatibabu na mwaka 2011 na 2014 alifanyiwa upasuaji wa jicho.

Afya ya Rais Mugabe imeendelea kuzua mijadala nchini mwake ambapo mwezi Machi mwaka huu mamlaka nchini humo ziliwakamata waandishi wa habari wawili walioandika kuwa afya ya kiongozi huyo imezorota.

Licha ya umri alionao, chama chake cha ZANU-PF mwaka jana kilimteua kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao, huku kukiripotiwa mgawanyiko ndani ya chama hicho.

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Amchambua Live JPM

$
0
0
Mkapa alisema moyo wa kujitoa na kuwatumikia wananchi alionao Rais Magufuli ndiyo chachu iliyomsukuma kumwamini na kumteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi kisha waziri kamili.

Rais wa tatu Mkapa aliyasema hayo jana wakati wa sherehe ya makabidhiano ya nyumba 50 za watumishi wa afya kwa mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

"Mimi ninawashukuru zaidi nyie kwa kutambua nguvu zake, utawala wake, hali yake, upeo wake, moyo wake wa kujitoa na kutumikia, na ndivyo vilivyonivutia kumteua kuwa naibu waziri hadi kumpa uwaziri kamili," alisema Mkapa.

Alisema mafanikio yanayopatikana sasa katika sekta ya afya ni juhudi za Rais Magufuli hivyo anapaswa kupongezwa kwa asilimia mia moja.

"Kafanya kazi nzuri, na ataendelea kufanya kazi nzuri," alisema Mkapa. "Mafanikio haya yote ni katika sekta moja tu ya afya."
"Inatunza uaminifu wake, mnastahili kutoa kiongozi wa nchi nzima, tumshukuru Mungu kwa kutupa kijana huyu."

Miongoni mwa mafanikio ya Rais Magufuli katika sekta ya afya, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema jana, ni ongezeko kubwa la bajeti ya wizara yake kwa miaka miwili iliyopita na upatikanaji wa dawa kutarajiwa kuwa asilimia 90 na 100 kuanzia mwaka huu wa fedha.

Waziri Ummy ambaye Rais Magufuli alimsifu kwa kuwa mchapakazi hodari, alisema hatua hiyo inatokana na MSD kutiii maagizo ya mkuu wa nchi huyo kuitaka serikali iagize dawa kutoka kwa wazalishaji bila kupitia kwa dalali.

KAMPENI 1995
Kwa upande wake, Rais Magufuli alisema anamshukuru Mkapa kwa kumpiga kampeni mwaka 1995 wakati anagombea nafasi ya Ubunge wa Chato.

Alisema wakati anagombea Ubunge, Mkapa wakati huo alikuwa anawania nafasi ya Urais na alimnadi kwa wananchi wa Chato kuwa anafaa na hatimaye alichaguliwa.

"Nakumbuka mwaka 1995 ulipokuja ulikuwa umevaa viatu vyekundu... ulisimama pale (akionesha sehemu ya uwanjani) na ukaniita jukwaani, ukanishika mkono na kuniombea kura kwa wananchi wa Chato... asante sana," alisema Rais Magufuli.

Aidha, Magufuli alisema anamshukuru Rais mstaafu wa nne, Jakaya Kikwete kwa kumwamini na kumteu kuwa Waziri katika wizara mbalimbali.

Rais Magufuli aliishukuru Taasisi ya Mkapa Foundation kwa jitihada zake za kujenga nyumba hizo kwa ajili ya watumishi wa afya, na kwamba taasisi zingine ziige mfano huo.

"Mkapa Foundation wameshatoa ajira zaidi ya 900 kwa madaktari, pia wameshajenga nyumba zaidi ya 400," alisema Rais Magufuli. "Hayo ndiyo maendeleo tunayoyataka, siyo zile taasisi zinaopigia debe wanafunzi kuzaa."

Alisema serikali imeongeza bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka huu kutoka Sh. bilioni 31 hadi Sh. bilioni 200 huku akiwataka wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri kutumia vizuri pesa za kununulia dawa pindi watakapopelekewa.

Kati ya nyumba hizo, 20 zimejengwa katika mikoa ya Geita, nyumba 20 katika mkoa wa Simiyu na nyumba 10 katika mkoa wa Kagera.
Viewing all 104663 articles
Browse latest View live




Latest Images