Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

KIBITI: Taarifa Mpya za Mama Aliyedaiwa Kuuawa kwa Risasi

$
0
0
Mwanamke aliyejeruhiwa kwa risasi usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, Tabia Mbonde anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mchukwi, kinyume na taarifa zilizoenea kwamba amefariki.

Awali iliarifiwa kuwa watu wasiojulikana walimuua kwa kumpiga risasi, mkazi wa Kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, Ramadhani Mzurui, usiku wa kuamkia juzi na kumjeruhi mguuni kwa risasi mke wa marehemu ambaye alikimbizwa hospitali kwa matibabu.

Mtandao huu ulifunga safari mpaka hospitalini hapo na kufanikiwa kumpata majeruhi huyo ambaye alishuhudia mumewe akiuawa kwa risasi na yeye kukimbilia msituni baada ya kupigwa risasi tano mguuni.

Baada ya tukio hilo, mama huyo anadai alianguka msituni ambako alikuja kuchukuliwa na Wasamaria wema na kupelekwa hospitali. Mama huyo amefunguka mengi kuhusu mauaji hayo

Mpenzi Wangu Akitongozwa na Wanaume Ananiambia Hii ni Sawa?

$
0
0
*Wadau wa Udaku , Naomba mnipe mwongozo kwa hili la mpenzi wangu.
 *Kuna mambo mawili yamejitokeza hv karibuni:

 * kwanza, juzi alinipigia simu[hatuko mkoa mmoja, anasoma] na katika maongezi akasema kuwa X-boy wake kampigia simu nanukuu.."eti kanipigia simu, nikamuuliza leo umekumbuka nini?....akaniambia eti anakuja huku[alipo huyu demu] mm nikamwambia nasafiri, sitakuwepo"

  *Pili, jana kaniambia "mpenzi kuna sms zinachekesha...ngoja nikuforwadie...sms 1 ilisomeka "nakuhitaji"....
Sms ya Pili ipo hv.."leo umependezaa, nataka nije kwako"..hz sms anadai katumiwa na mshikaji anayeonyesha kumtaka kimapenzi

    *Hapa najiuliza ana maana gani kwa haya?

    #Naombeni mniambie, na kufafanua haya.

    Asanteni sana

Everton inafungulia Milango Tanzania - Mwakyembe

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema ujio wa timu ya Everton nchini utaweza kufungua fursa nyingi kwa kuwa dunia nzima sasa itaitazama Tanzania kupitia mchezo kirafiki dhidi ya Gor Mahia.


Mwakyembe amebainisha hayo muda mchache alipoupokea ugeni huo huku akizisisitizia timu za Tanzania kutumia viwanja vilivyopo nchini vizuri ili waweze kuinua vipaji kwa hali ya juu.
"Hii ni fursa kubwa kwa watanzania kwanza kuwaona hawa nyota wa Everton ni timu kongwe kutoka Uingereza lakini pili inafungua fursa sana maana inatutangaza watanzania kidunia, wamekuja na watangazaji kutoka nchi mbalimbali. Kwa hiyo inafungua milango kwa timu nyingi zaidi, nasi tuzishawishi zaidi timu zetu zije kutumia viwanja vyetu vya kisasa tulivyo navyo", amesema Mwakyembe.

Pamoja na hayo, Mwakyembe amewatuliza wanahabari pamoja na wapenzi wa soka kuwa na moyo wa uvumilivu kwa kuwa hawataweza kupata nafasi ya kukiona kikosi hicho kikiwa kinafanya mazoezi yake kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kutokana na kuwepo na ulinzi mkali.

"Nafikiri kesho kutakuwa na mchezo mzuri kweli, leo watafanya mazoezi katika uwanja Taifa lakini naona wenzetu hawataki kabisa kuona vyombo vya habari pale, hatuwezi kuwapinga kwa hilo. Kwa hiyo vijana wangu msihangaike hata kwenda pale maana kuna ulinzi mkali lakini kesho nitahakikisha kila mmoja wenu anapata nafasi nzuri kuweza kufuatilia mchezo huo jioni", amesisitiza Mwakyembe.

Everton itashuka dimbani kesho (Alhamis) kuchapana na Gor Mahia mchezo wa kirafiki baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa michuano ya Sportpesa Super Cup 2017.

Duh.. Afande Sele Amuombea Mabaya Aliyekuwa Rais wa TFF...Acha Magufuli Awanyooshe

$
0
0
Msanii mkongwe wa Hip hop nchini Afande Sele amefunguka na kumuombea mabaya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi na kusema ni bora aende kwani katika kipindi chake hakuna jambo lolote la maendeleo amelifanya.

Afande Sele ametumia ukurasa wake wa facebook na kusema yake ya moyoni kwa kulinganisha ofisi na hatua ambazo zimepigwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Sudan na kusema Malinzi anapaswa kuondoka tu kwani ni aibu.

"Ofisi ya chama cha soka cha Sudan na ofisi ya chama cha soka Tanzania..aibu yetu..acha Magufuli atunyooshe tu kwani tulizidisha uwendawazimu. Nenda Malinzi nenda tuuu" alisisitiza Afande Sele

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi ambaye alikuwa ni mmoja kati ya watu ambao walikuwa wanagombea nafasi ya Urais katika shirikisho hilo lakini jina lake lilienguliwa katika mchakato huo baada ya kushindwa kuhudhuria katika usaili wa wagombea uliofanyika siku ambayo yeye yupo rumande kutokana na kesi inayomkabili ya matumizi mabaya ya ofisi.

KIMENUKA...CUF ya Lipumba Yatangaza Vita Kwa Chadema.....

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Bara anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Magdalena Sakaya, amejibu mapigo baada ya mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea kutangaza jana ‘Oparesheni Ondoa Msaliti Buguruni’. Kubenea amedai kuwa oparesheni hiyo inalenga kumuondoa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizoko Buguruni jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Akijibu mpango huo uliotangazwa na Chadema inayomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Sakaya ambaye ni kambi ya Profesa Lipumba alisema kuwa anawasikitikia Chadema kwa kuingilia mgogoro usiowahusu.

Sakaya ameongeza kuwa Mpango huo wa Chadema hautafanikiwa kamwe na kwamba wanachokifanya ni Kuingilia mambo yasiyowahusu.

Katika hatua nyingine, Kubenea alipozungumzia majibu ya Sakaya amedai kuwa CUF ni sehemu ya Ukawa, hivyo inapoonekana inataka kudhoofishwa ina maana kuwa Ukawa itadhoofika pia, hivyo hawako tayari kuliona hilo.

KIMENUKA...Watumiaji waTwitter Wampeleka Trump Mahakamani

$
0
0

Rais wa Marekani, Donald Trump ameshtakiwa  na  watumiaji wa mtandao wa Twitter aliowafungia  wasione anachoandika katika ukurasa wake.

Watu saba wamefungua mashtaka katika mahakama moja jijini New York nchini humo wakimtaka rais huyo awafungulie kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha Katiba.

Wanasema kwa kuwa Rais wao huwa anatumia ukurasa wake @realDonaldTrump kutoa taarifa mbalimbali za Serikali, ni haki yao kuona na kujibu anachoandika.

“Ukurasa wake unawawezesha wananchi kuwasiliana naye moja kwa moja hivyo ni haki ya kila raia kuweza kuuona, kutufungia ni sawa na kutunyima haki yetu ya kikatiba ya kupata taarifa,” inasema sehemu ya mashtaka hayo.

Kabla ya kufungua mashtaka hayo, watu hao waliandika barua kwenda kwa Rais Trump iliyokuwa na orodha ya majina yao wakitaka awafungulie waweze kusoma na kujibu anachoandika, hata hivyo, barua hiyo haikujibiwa.

Usikatishwe Tamaa Kwa Kukataliwa Na Dunia

$
0
0
Kama upo kwenye mbio sahihi za mafanikio, kati ya kitu ambacho unatakiwa kujifunza sana ni kutokukatishwa tamaa na kukataliwa. Upo wakati utakataliwa kwenye biashara yako na kukosa wateja.

Hiyo haitoshi kuna wakati utakataliwa sana kwa kazi unayoomba na pia kuna wakati unaweza kukataliwa na mazingira na kushindwa kuvuna hata kile ulichopanda. Hiyo ni mifano michache kati ya mingi.

Kitu cha kujiuliza kukataliwa kwa namna yoyote kunapotokea kwako, huwa unachukuliaje? Huwa unajiona ni mpumbavu au mjinga au unakuwa unatumia kukataliwa huko kama sababu ya kusonga mbele?

Kwa wengi sina shaka sana kukataliwa kokote kunapotokea, ndani mwao hujisikia vibaya sana kiasi cha kwamba kutokutamani kuendelea tena. Je, hi ndiyo hali ambayo hutokea hata ndani mwako?

Usichokijua wapo watu wengi sana ambao walikataliwa mwanzoni na kazi zao lakini leo ni mabilionea. Sylvester Stalone alimaarufu Rambo alishindwa kupata uzamini wa kutoa filamu yake ya kwanza hadi aliuza mbwa wake.

Naye pia Alexander Graham Bell alipopeleka kwa mara ya kwanza kuiza teknolojia yake ya Simu  kwa Carl Orton ambaye ni mmliki wa Western union aliambiwa kampuni kubwa kama yake haiwezi kununua doli kama hilo.

Hebu jiulize ni kitu gani ambacho alikuwa akiwaza Rambo pale alipoambiwa hawezi kuigiza, au ni kitu gani alichokuwa akifikiri Bell pale alipoambiwa kazi yake ni hovyo na kufananishwa na doli?
Kwa ujasiri na ushujaa, hakuna aliyekata tamaa, waliamua kusonga mbele, leo hii dunia nzima inatumia simu na leo hii wengi wanamfahamu Rambo. Katika mazingira yoyote ulionayo hapo ulipo, usikubali kukatishwa tamaa na kukataliwa, simamia ndoto yako kikamilifu.

Ni kweli kuna wakati utapita katika mazingira magumu na kuonekama kila kitu kimekataa kabisa kwenye maisha, lakini hiyo usichukulie kwamba ndio uhalisia ulivyo. Chukua jukumu la kuendelea kusonga mbele.

Asikuzuie mtu kwa maneno yake, yasikuzuie mazingira yoyote yale, kitu cha msingi usikubali kushindwa kwenye akili yako kwanza, ukishindwa huko na huku nje utakuwa umeshindwa. Kabisa.
Hapo ulipo unajijua vizuri hali uliyonayo, hali hiyo kama huipendi sana amua kuibadili mara moja, kama unaona huoni matokeo ya haraka usikate tamaa, vumulia mambo yatakaa sawa kadri siku zinavyokwenda.

Huu Ndio Utajiri Mkubwa Utakaoupata, Kama Utaamua Kufanya Biashara Hii

$
0
0

MAKALA HII IMEANDIKWA NA MESHACK MAGANGA WA IRINGA TANZANIA.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza ujasiriamali. Ninaandika makala hii kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kuniletea mafanikio makubwa.

Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa kuuza vocha na  kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo yachuo. Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa Iringa mjini, baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya.

Na baadaye nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambaye pia anajishughulisha sana na kilimo cha miti. Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini Kalenga, nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba, leo nina ekari nyingi.

Albert sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu mimi:- “UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSss! UNAWEZA KUFA MASIKINI! Nina rafiki yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, "Sanga nimeamua kuanza kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu ishirini na tano, (25,000?/=).

Nikamwambia "Kupata ekari moja si chini ya laki sita na wewe una tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!", Sikumwelewa! Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo moja linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango. Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua Tsh. 7,000/=.

Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja. Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/= (laki nane). Alipokuja na fedha hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine akairudisha shambani.

Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia” Akaendelea kwa kusema:-

Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa.

Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala. Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama mbao.Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho. Miti ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake.

Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000).

Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni thelathini na mbili (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji (demand) wa mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi  laki moja na 20 elfu (120,000) na laki moja, kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja  na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea na umri wa miti unayotaka.

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne.

Uponunua mashamba haya kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo. Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako.

Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning).

Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima. Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.

Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu.

Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa.  Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya uzalishaji katika ardhi yetu.

Inawezekana! Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie.

Yupo Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira, ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.

Mayweather na McGregor nusura wazichape kavu kavu

$
0
0

Rais wa UFC, Dana White (katikati) akijaribu kuwatenganisha Floyd Mayweather (kushoto) na Conor McGregor wasipigane 'kavu kavu' usiku wa jana ukumbi wa LA's Staples Center mjini Los Angeles, Marekani

MPIGANAJI Conor McGregor ametamba kummaliza katika raundi ya nne bingwa wa dunia wa ngumi za kulipwa ambaye hajawahi kupoteza pambano, Floyd Mayweather katika ufunguzi wa ziara ya promosheni ya pambano lao la Agost 26, mwaka huu mjini Los Angeles, Marekani.

Mbele ya mashabiki 11,000 ukumbi wa LA's Staples Center, Mayweather na McGregor walikutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu kuthibitishwa kwa pambano lao la utajiri mkubwa.

Licha ya kutokea mbele ya umati wa mashabiki wa nyumbani na kuvaa tracksuti yenye rangi za bendera ya Marekani, lakini Mayweather alijikiuta akizomewa huku mpinzani wake kutoka Ireland, McGregor akishangiliwa kila alipotokea kwenye kioo kikubwa chaTelevisheni.

"Atazimika ndani ya raundi nne. Hana uzoefu wa hii. Simuogopi. Huu ni mchezo wenye sheria zinazokubana na kulifanya hili liwe nusu pambano. Kama hili lingekuwa pambano, asingemaliza raundi hata moja,"alisema McGregor akimaanisha wangepigana katika mchezo wake wa UFC wa kuchanganya na mateke angemmaliza mapema zaidi Mayweather.

Lakini 'bishoo' Mayweather naye hakuwa kimya, kwani alijibu tambo za mpiganaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anayejiandaa kwa pambano la kwanza kabisa la ngumi bila mateke kiasi cha wawili hao kukaribia kupigana 'kavu kavu'.

"Ni bwana mdogo, yupo katika miaka ya 20, nipo katika miaka ya 40. Damu yake inacheka, siyo mimi" alisema Mayweather ambaye pia alidai pambano hilo lina mvuto mkubwa wa kishabiki.

"Nimekuwa nikifanya hivi kwa miaka 20. Nimekuwa hapa kabla. Lakini ni mgumu. Ni shujaa. Bora lazima apigane na bora. Mashabiki wamelitaka pambano hili, McGregor amelitaka pambano hili, nimelitaka hili pambano. Agost 26 itakuwa machozi, jasho na damu tangu kengele ya ufunguzi," amesema.

Boko Haram waua 11 nchini Nigeria

$
0
0

Watu 11 wameuawa  kufuatia mashambulio mawili yaliyofanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na vyanzo vya ndani ya nchi zinasema kuwa watu  5 pia walijeruhiwa katika shambulio lililofanyika mjini Maiduguri.

Vikosi vya usalama viliendelea na operesheni ya kudhibiti hali huku majeruhi wakiwahishwa hospitalini.

Kundi la Boko Haram ambalo lilijitokeza nchini Nigeria mwanzoni mwa miaka ya 2000, lilikuja kuwa tishio na kuanzisha mashambulizi mwaka 2009 baada ya kifo cha kiongozi wao mkuu Muhammad Yusuf ambaye aliwekwa kizuizini.

Maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram.

Mwimbaji Diamond Platnumz na Mabomu yake Kama ya Korea Kaskazini...

$
0
0

UNAPOTAKA KUINGIA KWENYE VITA LAZIMA UHAKIKISHE UNA SILAHA ZA KUTOSHA.

Wakati dunia nzima inaangalia mzozo baina ya Korea Kaskazini na Marekani utamu unakuja kwa Rais wa Korea kaskazini ambaye yeye hana maneno sana zaidi ya kuendelea kufanya majaribio ya silaha zake.

Katika muziki Tanzania mfano wa rais wa Korea kaskazini Kim ni @diamondplatnumz .Wakati mashabiki wanalalamika kuwa jamaa anachelewa kutoa ngoma alisema anataka ku push vijana wake kwanza ndio naye aachie sasa nahisi amepania kukata kiu ya mashabiki wake.

@diamondplatnumz ndani ya muda mchache ameachia makombora ya masafa marefu na mafupi yani I MISS YOU,FIRE na ENEKA ila kabla ya mashabiki hawajakaa vizuri wanapata taarifa kutoka kwa @patorankingfire kuwa mwezi ujao wanaachia bomu la masafa marefu majini ndani yake akiwemo tena @diamondplatnumz .

Kitu ambacho kinamfanya @diamondplatnumz kuwa kama Rais wa Korea kaskazini ni kutosikiliza criticism za maadui wake na kuendelea kuachia silaha zake ila watu wasichojua kila silaha ina target zake.
Nilisema ngoma ya FIRE target yake ilikuwa kumuweka @tiwasavage ambaye ndani yake kuna #rocknation chini ya #JAYZ mpaka hapo lazima Fire imepita machoni mwa #Jigga.
Lakini #ENEKA watu wanasema ni sample beat ya #FALL kutoka kwa @davidoofficial lakini ukweli hiyo inaweza kuwa sababu inayofanya ngoma hii ina heat kwa kasi sana maana wanavyozidi kulinganisha ndio wanaipa rotation.

@diamondplatnumz ni mfanya biashara wa muziki kwa mana hiyo akiona mtu anauza matikikiti na anauza sana naye anapeleka matikikiti pale pale ili wagombanie wateja mwisho wa siku wakitoka pale kila mtu kauza.

Leo jiulize #FALL ya @davidoofficial inavyokimbiza halafu ndani yake imeletewa pacha wake #ENEKA unategemea nini hapo lazima zote ziende kwa kasi.

@diamondplatnumz ameonesha nia ya kupambana na @wizkidayo @davidoofficial na kina @teknoofficial na njia nzuri ya kupambana nao ni kupeleka bidhaa kama zao nazo ndio hizo #eneka na #fire.

Music is business and business is all about creativity ndio mana diamond anafanikiwa mana anafanya biashara ya muziki.

RAHA YA VITA UWE NA HAZINA YA SILAHA KWENYE GHALA.
.
By @Abby1_thebest
@abby1_thebest
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Ngeleja Aendelea Kuweweseka...Aelezea Kwanini Alirudisha Hela Serikalini na si Kwa Rugemalila Aliyempa...

$
0
0
Siku chache baada ya kutangaza kuwasilisha shilingi milioni 40 katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amefafanua sababu za kutomrejeshea fedha huyo mfanyabiashara, James Rugemalira ambaye alimpa awali kama msaada.
Fedha hizo ni sehemu ya shilingi bilioni 306 zilizotolewa katika akaunti maalum ya Tegeta Escrow mwaka 2014 iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, fedha zizotolewa kimakosa wakati kesi ya mgogoro wa kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL ikiwa bado haijatolewa maamuzi.
Kwa mujibu wa taratibu, fedha hizo zilipaswa kutolewa baada ya kesi husika kukamilika na pande zote mbili kukaa pamoja kukokotoa kiasi cha fedha ambacho kila upande ungepaswa kupata kwa mujibu wa maamuzi.
“Kwa mazingira halisi yanayomkabili aliyenipa msaada, mahali salama pa kurejesha hizo fedha sasa ni serikalini. Serikali itajua kuwa fedha hizo zinastahili kwenda kwa Rugemalira sasa au wasubiri hatima ya kesi,” Ngeleja anakaririwa na Gazeti la Mwananchi .
“Ningerudisha kwa Rugemarila watu wangeweza kuibua hoja kwamba labda napiga changa la macho tu,” aliongeza.
Mfanyabiashara huyo maarufu ambaye kampuni yake ya VIP Engineering ilikuwa inamiliki asilimia 30 ya IPTL, pamoja na Mwenyekiti wa Pan African Power Solution (PAP), Harbinder Singh Seth wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na bado wako mahabusu.

Mgao wa fedha hizo pia uliwafikia Anna Tibaijuka aliyekuwa waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Andrew Chenge ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Methodiu Kilaini, Jaji John Ruhangisa na wengine.

-Mwananchi

Mwanamuziki Peter Msechu Alia na Clouds FM...Adai Ananenepa Kwa Vile Hapati Show.....

$
0
0
Msanii wa Bongo Flava, Peter Msechu amedai kuwa ananepa kwa sababu hafanyi show.


Muimbaji huyo ambaye ameachia ngoma mpya ‘Yakawa’, ameiambia XXL ya Clouds Fm licha ya kukosa show lakini bado anajitahidi kupunguza unene na kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiomba ushauri kwake kujua namna ya kupungua.

“Nanenepa sometime sio kwamba sifanyi mazoezi, ni kwamba nakosa show, nikija jukwaani nikiruruka napungua,” amesema Msechu.

Pia ameongeza kuwa, “sasa hivi nimepungua kuna jamaa jana wamenicheki kwenye mtandao anaulizia namna ya kupungua. Sasa nina kg kama 120 nilikuwa na kg 160”.

Kisa Kusambaza Picha za Uchi za Mpenzi Wake...Rob Kardashian Kafanya Jambo Hili Kwa Familia yake

$
0
0
Kijana kutoka familia ya Kardashian, aliyekuwa akitoka kimapenzi na mwanamitindo Blac Chyna, Rob Kardashian ameipigia magoti familia yake kwa kuomba radhi kwa kitendo alichokifanya kwa mama mtoto wake.


Rob alifunguliwa mashitaka siku ya Jumatatu na mazazi mwezake  kwa kosa la  kumdhalilisha na kumyanyasa kijinsia kwa kuposti picha zake za utupu.

Chanzo cha karibu na familia kimeeleza kuwa Rob ameongea na dada zake pamoja na mama yake na kuwaomba radhi kwa kuposti picha yenye udhalilishaji katika mitandao ya kijamii. Pia mtu huyo ameeleza kuwa Rob anajutia kuweka hadharani malumbano yake na mwanamke huyo na hato fanya hivyo tena.

Hata hivyo baba  Dream hakuomba radhi kwa madai yaliotolewa ya kuwa alikuwa akimnyanyasa kijinsia Blac, bali alisema anajutia kupuuza ushauri aliopewa na dada zake juu ya kuto kuwa na mahusiano na mwanamke huyo.

Inaelezwa kuwa familia hiyo imemshamsamehe kijana huyo na ndio maana hawakusapoti alichokuwa akikifanya katika mitandao.

Na Laila Sued

Mwimbaji Ray C Adaiwa Kukesha Studio Siku Mbili........

$
0
0
Msanii wa Bongo Flava na hitmaker wa ngoma ‘Unanimaliza’, Ray C inaelezwa kutokana na uwezo wake wa kazi si ajabu yeye kukesha studio siku mbili akifanya kazi.


Mmoja wa mameneja wake, T Fighter ameeleza kwa malezi aliyolelewa Ray C ni tofauti na wasanii wengine kwani amezoea kurekodi albamu na si single.

“Tukienda studio tunakesha hata siku mbili, mimi nishazoea nikienda studio nakaa lisaa limoja naondoka ila yeye akiingia studio anakaa siku mbili anarekodi nyimbo tatu au nne kali,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.

Ameongeza kuwa kutokana na uwezo wake wa kazi wimbo wa Unanimaliza ulirekodiwa ndani ya saa mbili tu.

Tabia sugu zinachangia kwa kiasi kikubwa wanamke kutokuolewa

$
0
0

Kuoa au kuoelwa ni jambo ambalo watu wengi hutamani kwani ni miongoni mwa hatua kubwa katika maisha ya kila mmoja. Ukifanya utafiti kwa watu ambao hawajaoa wengi watakwambia wanatamani siku moja wawe na familia bora na yenye furaha, kwani kila mmoja anaamini hayo ni mafanikio kwenye maisha.

Licha ya kuwa kuolewa au kuoa ni jambo jema, baadhi ya watu huwa hawaoi au hawaolewi. Kutokuoa au kuolewa kunaweza kuelezewa na sababu nyingi sana.

Leo tutazungumzia suala la mwanamke kuolewa, na tutaweka bayana baadhi ya tabia chache ambazo zinaweza (zinachangia kwa kiasi kikubwa) mwanamke kuto kuolewa.

1. Utumiaji mbaya wa mitandao ya kijamii.
Hili najua si kwa wanawake tu, lakini kwa sababu leo wao ni walengwa wa mada, tutazungumzia upande wao tu. Baadhi ya wanawake hutumia vibaya mitandao  ya kijamii ambapo huchati tangu asubuhi hadi jioni, wakiinua macho basi wanaangalia Tv na akimaliza channel hii atahamia nyingine, akimaliza mtandao huu atahamia mwingine.

Kutwa nzima unakuta anafuatilia staa huyu alifanya nini usiku, huyu alipiga picha gani, kikapanda kikashuka.

Mwisho wa siku mwanamke kama huyu atakuwa hana cha maana alichojifunza kwenye mitandao au kutazama Tv zaidi ya kuanza kuiga yale aliyoyaona. Na hakuna mwanaume muoaji anayetaka mwanamke ambaye akili yake imetawaliwa na mitandao ya kijamii hakumbuki hata kufanya usafi ndani.

2. Kutokupenda kufanya kazi za nyumbani.
Wanawake wengi wa ki-Afrika kwa vile wamekwenda shule wakatambua mambo ya haki sawa kwa wote na wengine kuona kwenye filamu wanaume wakifanya kazi ambazo mara nyingi hufanywa na wanawake, basi na wao ndio wameweka nukta kufanya kazi za nyumbani.

Kutokana na hali hii, wanawake wamekua wakujiremba tangu mawio hadi machweo, ukitazama kucha zao zilivyondefu unajiuliza huyu anafua kweli?

Wengine wameamua kuajiri watu wa kuwafulia hadi nguo za ndani. Kwa hali hii usitarajie mwanaume akuoe kwa sababu anajua ni matatizo anapeleka nyumbani.

3. Kujipodoa hadi sura yako ya asili inasahaulika.
Ni kweli wanaume hupenda mwanamke mrembo na mwenye kupendeza. Lakini hii haimaanishi ndio ujipodoe hadi uchukize. Kila kitu kwa kiasi chake kwa sababu kitu chochote kikizidi huwa ni sumu.

Jirembe kwa kiasi, hili litavutia watu walio-serious kutaka kukuoa, lakini ukiwa ni wa kujiremba hadi ukapindukia, hakuna muoaji atakaye kuta. Tena ikumbukwe kuna baadhi ya wanaume wao hupenda mwanamke asiyejiremba (wenyewe huita natural)

Hizi ni baadhi tu, na wewe unaweza kuongezea ili kuwakumbusha wasichana wanaotaka kuolewa.

Kutana na Maalim Fadhil Rashid Kutoka Komoro ni Mtaalam wa Tiba za Asili......

$
0
0
KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239/

WhatsApp IMO +255785786436/

Kimenika Mbaya... Vigogo 12 NSSF Waachishwa Kazi Kwa Tuhuma za Ubadhirifu na Matumizi Mabaya ya ofisi

Mwanamuziki AT Amwangushia Jumba Bovu Mwanamuziki Avril wa Kenya...Amchana na Maneno yake ya Shombo

$
0
0
Msanii wa muziki miondoko ya mduara nchini, AT amedai kuwa katika muziki wake haangalii ukubwa wa msanii kama umeimba hovyo kwenye ngoma yake basi hana budi kuifuta verse yako .

Mkali huyo kutoka zanzibar amesema hayo kupitia cloudsfm huku akimtaja msanii kutoka kenya 'Avril' ambae alishamfuta kwenye wimbo wake baada ya kuimba vibaya

. "Nilishaenda ogopa Dj kufanya wimbo na Avril lakini Avril aliimba utumbo mtupu mimi nilimtoa. Avril sio msanii sio kabisa yani sio msanii ambaye unategemea kumsikia halafu unamkuta kama vile alivyo Linah...no yani she very fake kabisa yani mpaka nimeshangaa nilikuwa najua jina lake ni kubwa anauwezo mkubwa lakini nimeenda kufanya nae wimbo aisee ni shughuli mpaka nimemtoa nimemuweka Alice wa THT na ngoma imekuwa kali lakini sijaitoa" alisema @at_original .

Aidha AT ameongeza na kusema kuwa yeye haangalii ukubwa wa jina la msanii bali anazingatia uwezo wa msanii na siku upepo wa promotion ukikaa sawa ataitoa ngoma hiyo ambayo alimtoa Avril (@theavieway) na kumuweka Alice wa THT.

Shilole Achafukwa na Wezi wa Walioiba INSTAGRAM Yake...Adai Kuwaendea Kwa Mganga wa Kienyeji

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shilole amefunguka na kuwataka vijana wa mjini ambao wanachukua 'Account' za watu mitandaoni waende kuiba kwenye taasisi za fedha na si kwenye mitandao ya jamii kwa kuwa huko hakuna fedha.

Shilole amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kusema licha ya mwizi wake kumuachia account yake ya Instgram lakini anataka mtu huyo apatikane ili ikiwezekana afungwe kabisa kama fundisho kwa vijana wengine wanaofanya michezo hiyo kwani wamekuwa wakiwakwamisha na kuwarudisha nyuma wasanii.

"Mimi account yangu imesharudi saizi nashukuru Mungu ila nasema hao vijana wanaojifanya wao wamesomea IT na kuanza kuiba account za watu za mitandao ya jamii, wakaibe bank huko, kama wao wasomi wakaibe Ikulu, au wakatengeneze ndege huko, siyo mnakuja kuiba account za sisi wasanii sitawasaidia nini? Huko kwenye mitandao hakuna hela kama mnataka pesa nendeni bank huko. Mimi nasema hata kwa mganga wa kienyeji nitakwenda nimjue mtu aliyeiba account yangu ili afungwe tu iwe fundisho kwa vijana wengine" alisema Shilole

Shilole aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha account yake kuwa hacked kwa mwezi mzima imemuingizia hasara kubwa kwani ameshindwa kutoa wimbo wake mpya na ameshindwa kutangaza juu ya biashara yake ya chakula.

"Watu wanaweza kuona kama ni utani lakini mimi nipo serious hawa watu wanatupotezea focus yetu, mimi Instgram inanisaidia kutangaza muziki wangu, inanisaidia kutangaza biashara yangu ya chakula, mambo yangu mengi yamekwama kwa mwezi mzima toka huyo mtu ameiba account hiyo, halafu yeye alikuwa amekaa nayo hakuna anachofanya, nasema hawa watu wanaojifanya wanajua sana IT watumie vyema elimu zao kufanya mambo ya msingi" alisisitiza Shilole
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images