Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

VIDEO:Tazama Jinsi Shabiki Alivyoingia Uwanjani na Kumkumbatia Wayne Rooney Wakati Mpira Unaendelea

$
0
0

VIDEO:Tazama Jinsi Shabiki Alivyoingia Uwanjani na Kumkumbatia Wayne Rooney Wakati Mpira Unaendelea

TUMUOMBEE! Mama Mzazi wa Zarinah Hassan Aendelea Kupumulia Mashine ICU

$
0
0
TUMUOMBEE! Mama mzazi wa Zarinah Hassan ‘Zari Boss Lady’, Halima Hassan anadaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.

Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.
“Tangu Ivan afariki dunia afya ya mama Zari imekuwa ikizorota siku hadi siku kutokana na wawili hao kuwa na maelewano ya karibu na mazuri,” kilisema chanzo na kuongeza;

“Kwa sasa anapumua kwa kutumia mashine ya oksijeni. Wiki iliyopita Zari na dada zake walilazimika kurejea haraka nchini (Uganda) wakitokea Afrika Kusini baada ya kupata taarifa za kuzidiwa kwa mama yao.”

Hata hivyo, Jumatatu ya wiki hii ilitolewa taarifa kuwa Zari na madaktari wanaomuuguza mama yake walikuwa kwenye mazungumzo ya siri kutokana na afya ya mama yake kutoridhisha.

Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, ni Zari na dada yake pekee ndiyo wanaoruhusiwa kumjulia hali mama yao na kama hali yake itakuwa hairidhishi basi watalazimika kumsafirisha.

Mkurugenzi wa Upelelezi Ajitosa Sakata la Mchele wa Plastiki....Atoa ONYO Kwa Aliyesambaza Video

$
0
0
Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Robert Boaz, ametoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao ya jamii kwa lengo la upotoshaji na kuliagiza Jeshi la polisi kuanza mara moja kuwashughuliakia na kuwachukulia hatua za kisheria watu wenye tabia hiyo.

Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi huyo mara baada ya mitandao ya kijamii kusambaza video yenye habari inayonyesha uwepo wa mchele wa plastiki nchini.

Boaz amekanusha uwepo wa mchele huo wa plastiki na kumsaka kwa udi na uvumba mtu aliyerekodi video hiyo ili asaidie kutoa taarifa zaidi.

Na amewaomba wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kujiepusha kusambaza taarifa zisizokuwa na ukweli, kwani ni hatari na husababisha madhara makubwa katika jamii.

”Kabla ya kusambaza taarifa kwanza uwe na uhakika wa vyanzo vyako, wahsuika wanaweza kuingia kwenye matatizo yasiyokuwa ya msingi”. amesema Boaz.

Aidha waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia na wazee na watoto , Ummy Mwalimu ametaarifiwa na  Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), kuwa hakuna mchele wa aina hiyo nchini.

Waziri Ummy amewasisitizia watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, na kuepuka upotoshaji.

Maskini Jack Wolper Hana Bahati..Boyfriend Wake Mpya Katika Skendo ya Ushoga....

$
0
0
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza Boyfriend mpya wa Jack Wolper anayejulikana kwa jina la Brown ameingia katika Skendo ya Ushoga baada ya picha zake akiwa katika mikao ya kimahaba na Mwanaume Mwenzake kuvuja huko Instagram

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Yalaani Matamshi ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

$
0
0
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania imesema imesikitishwa na matamshi ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema imesikitishwa na kauli ya rais wa awamu ya tatu akirudia maneno ya kejeli ya watanzania wenye maoni tofauti.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Mkapa alisema akiwa Chato, Geita kuwa Takwimu zilizotolewa na Waziri wa Afya siku hiyo( Julai 10, 2017)  ya makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na Mkapa Foundaton  Zitawasaida kupunguza Upumbavu Wale aliowaita hivyo Wakati wa Kampeni  2015.

Taarifa hiyo imesema kuwa matamshi ya Mkapa hayapendezi kusikika yakitoka kwa kiongozi wa kitaifa, na ni matamshi yasiyoheshimu maoni tofauti.

Anthony Diallo Atoa Ufafanuzi Baada ya TRA Kuzifunga Akaunti Zake

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imekamata akaunti za Kampuni ya Sahara Media Group kwa kushindwa kulipa deni la Sh4 bilioni kama kodi iliyopaswa kulipwa na kampuni hiyo.

Taarifa zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa akaunti zote za kampuni hiyo zimefungiwa mpaka pale watakapolipa deni hilo, lakini kampuni hiyo imetoa ufafanuzi.

Ujumbe huo uliongeza kuwa kampuni hiyo imefikishwa mahakamani na benki moja hapa nchini kwa madai ya kutaka kulipwa Sh600 milioni, baada ya kuingia makubaliano ya kulipa wafanyakazi wake mishahara pamoja na mikopo lakini mpaka sasa imeshindwa kurejesha fedha hizo.

Hata hivyo, akizungumzia suala hilo mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Sahara, Anthony Diallo alikiri mamlaka hiyo kufungia akaunti ya kampuni yake.

Diallo ambaye ndiye mmiliki wa kampuni hiyo alisema ni akaunti moja tu iliyofungiwa na kwamba anaamini baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mamlaka hiyo watafikia muafaka ili biashara ziendelee kama kawaida.

“Tutalimaliza hakuna kitakachoenda mrama,” alisisitiza Diallo ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii na Naibu Waziri wa Maji, Maendeleo ya Mifugo katika Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Amesema deni la TRA linatokana na kodi iliyopatikana baada ya ukaguzi wa vitabu kwa miaka mitatu.

“Ni ukaguzi wa kawaida hufanyika kama taratibu. Sasa kwa sababu ya kuhamisha matangazo yetu kutoka analojia kwenda digitali ilibidi tukope benki, ujenzi na kumaliza mradi imechukua miaka mitatu. Wakati wote tumekuwa tukilipa riba benki na zinazobaki toka mauzo ya matangazo tunalipa mishahara, umeme na malipo ya kodi za kawaida,”alisema.

“Ni kawaida ila wamefanya hatua za kutuaibisha tu. Kampuni yetu ya ving’amuzi ni ya Kitanzania na mapato yote yanaingia nchini wakati kampuni nyingine kubwa zote ni za kigeni kutoka China, Afrika Kusini, Mauritius na Kenya! Ukweli sisi tunahitaji kusaidia nchi kiuchumi na kutuharibia ni hasara kwa nchi.”

Mwapachu Astaafu Ujumbe wa Bodi ya Acacia

$
0
0

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya uchimbaji ya Acacia, Balozi Juma Mwapachu amestaafu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa vipindi viwili.

Mwapachu amechukua uamuzi huo leo, Julai 13 baada ya muhula wake wa pili wa miaka mitatu mitatu wa ujumbe wa bodi hiyo, kumalizika.

Taarifa iliyotumwa leo na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Acacia imeeleza kuwa inamshukuru Balozi Mwapachu kwa utendaji wake na ushirikiano wake wote  alipokuwa mjumbe.

“Tunamtakia maisha mema,” imesema taarifa hiyo.

Kutokana na mabadiliko hayo, Bodi ya Acacia itabaki na wajumbe saba, wakiwamo wanne wakurugenzi na wasio wakurugenzi.

Everton yaifunga Gor Mahia 2 - 1, Rooney apiga bao

$
0
0
Mpira umekwisha kwa Everton kushinda bao 2-1, magoli yakifungwa na Rooney dakika ya 35 kabla  Tuyisenge wa Gor Mahia kusawazisha dakika mbili baadaye. Goli la ushindi la Everton limepatikana dakika ya 82 kupitia kwa Dowell.

Kanuni 6 Za Mafanikio, Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger

$
0
0
Wengi wetu bila shaka umeshawahi kumuona au kumsikia mcheza sinema maarufu duniani kwa kipindi hicho ambaye kwa sasa ni Gavana wa jimbo la calfornia, Anord Shwarzenegger. Enzi zake alicheza sinema nyingi ambazo zilimpa mafanikio makubwa sana. Leo hii akiwa kama Gavana, Anorld anatushirikisha baadhi ya kanuni za mafanikio alizozitumia hadi kufikia viwango vya juu vya mafanikio.

Zifuatazo Ni Kanuni 6 Mafanikio Za Kutoka Kwa Arnold Shwarzenegger.

1. Jiamini wewe mwenyewe.
Watu wengi mara nyingi hutafuta ushauri wamafanikio kwa watu mbalimbali ili kuwafanikisha. Ni jambo zuri. Lakini kitu cha cha muhimu hapa kwako ni kujiamini wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanikiwa. Tafuta ni kipi unachokipenda, unataka kuwa nani na kisha tekeleza kwa kujiamini kabisa, UTAFANIKIWA.

2. Vunja sheria zinazokuzuia kufanikiwa.
Tunaishi katika ulimwengu ambao unasheria nyingi nyingi za uasili zinazoweza kutuzuia kufanikiwa. Sasa hizi ni sheria ambazo kwa vyovyote vile ni lazima zivunjwe. Sheria hizi zinaweza zikawa ni uvuvi au mazoea fulani mabaya tuliyojijengea. Kwa kung’ang’ania sheria hizi hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana.

3. Acha kuogopa kushindwa.
Siri kubwa ya mafanikio  ni kujifunza kutokuogopa kujaribu. Kama kuna fursa imejitokeza jaribu kufanya kwa ujasiri mkubwa na acha kukaa katika mkao wa kuogopa hiyo haitakusaidia sana. Hautaweza kufanikiwa kwa kukaa tu. Jitoe mhanga na hakikisha mpaka mipango na malengo yako makubwa yatimia.

4. Acha kusikiliza maneno ya wanao kukatisha tamaa.
Yatasemwa mengi kwamba huwezi kufanya hili wala lile. Wasikilize kisha achana nao. Lililo kubwa kwako jiamini mwenyewe kuwa utafika kule unakotaka kufika na kisha endelea mbele. Najua ni mara nyingi umewahi kusikia kauli hizi zikija kwako. Jambo la kufanya zipuuze kauli hizo, halafu fanya kile unachoamini kitakupa mafanikio.

5. Fanya kazi kwa bidii sana.
Hiyo ni nguzo kubwa ya mafanikio yako. Fanya kazi kwa bidii kwa kuamua kujituma na kulipia gharama zote za mafanikio. Hakuna mafanikio ambayo yatakuja kwako bure zaidi ya wewe kuwekeza nguvu na uwezo wako wote mkubwa kwenye kufanya kazi kwa bidii na maarifa makubwa siku zote. Hapa ndipo mafanikio makubwa yanapopatikana.

6. Kumbuka kutoa.
Mafanikio yoyote utakayokuwa umeyapata , hakikisha unatoa kwa jamii yako kiasi fulani  kama sehemu ya shukrani. Hii ni sheria au kanuni ya asili ambayo itakusidia kufikia mafanikio makubwa siku zote.

Hizo ndizo kanuni za mafanikio ambazo unaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa, kama zilivyotolewa na Arnold Shwarzenegger, Gavana wa jimbo la Calfornia marekani.

Mange Kimambi Amshauri Jack Wolper Baada ya Mpenzi Wake Mpya Kuaibika na Skendo Chafu ya Ushoga...

$
0
0
By Mangekimambi_ - Leo ntakushauri humu insta Kama navyomshaurigi mdogo wangu Wema......

Huyo Hamo mmeachana muda mrefu na ulikuwa unajua yuko na Huyo Mzungu na uliweza kumove on na Masha yako bila kujidhalikisha hivi na kiboyfriend ila Mara tu habari ilipowafikia wananchi na imekuwa sio siri tena unataka kushindana na huyo mtoto na Mzungu wake... Unajiabisha bwana..
.
.
Huwezi shindana na mwanaume kwenye hayo mambo mwisho wa siku unajiharibia zaidi. Huna Hana Haja ya kuwaonyesha walimwengu na wewe una kiboyfriend. Wana kusaidia nini zaidi ya kukucheka? Huu ni ushauri kutoka kwa mwanamke aliepitia situation ngumu kushinda yako, Mimi nilikuwa nimeolewa kabisa na watoto juu then Mara mwanaume kalipuka na mapicha ya mapenzi kwenye insta tena anawapa adui zangu warushe. Zile picha zilikuwa kila konaaaaaa insta, nilichekwa, nilibezwa ila sikudhubutu kufanya ujinga ili nishindane na Mzungu. Nilijiheshimu. Yawezekana hata nilikuwa nna stress na labda niligawa K kwa wanaume ambao hawakuni deseve Ila hakuna atakaejua na hakuna wa kuja kumuonyesha picha my hubby to be za Mimi nikiwa nalambana na kiserengeti boy kipindi kile...Yani kama nilifanya ujinga itakuwa siri yangu mimi ntakufa Nayo. .
.
Kwanini uruhusu mwanaume akuharibie future yako ya kupata mwanaume wa maana wa kukuoa? Seriously Wolper ni mwanaume gani mwenye Maisha yake mazuri atataka kukuoa kwa upupu huu? Juzi tu mapicha ya kulambana na Hamo Leo mapicha ya kitandani na hiko ki-useless kingine. Why??hufikiriiii future yako? Hujaolewa huna mtoto why unajiharibia chances zozote za kupata mwanaume wa maana?? Kwani huwezi kutiwa kimya kimya???Hivi ni mpaka Watu wajue na wewe unatiwa ?? Kha!! .

Aliyemvua Mvamia Mchezaji Wayne Rooney Uwanjani Asamehewa Kwa Amri ya Makamu wa Rais Samia Suluhu

$
0
0

MMOJA wa mashabiki wa Tanzania waliofika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaamamejitoa ufahamu na kumvamia mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney kwa nia ya kumkumbatia wakati wa mchezo dhidi ya Gor Mahia ya Kenya ukiendelea uwanjani hapo.

Baada ya kitendo hicho ambacho amekifanya wakati mpira ukiwa umesimama kwa muda kufuatia mmoja wa wachezaji wa Gor Mahiakuumia na kulala chini, polisi walimvaa shabiki huyo na kumwondoa uwanjani humo mpesempese.
Hata hivyo shabiki huyo ameachiliwa huru kwa amri ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo. (Picha na Musa Mateja na Richard Bukos/GPL)

Mwanamke zingatia Haya Wakati wa Kuomba hela Kwa Mwanaume la Sivyo Utaonekana Kicheche

$
0
0

Ukweli ni kwamba raha ya mapenzi ni pamoja na kupunguziana makali ya maisha. Na katika kupunguziana uko makali ya maisha ndio matumizi pesa yanapochomoza.

Kusaidiana ni kwa pande zote iwe kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume au kinyume chake, Ingawa kwa kiasi kikubwa ni wanaume ndio wanawajibika zaidi kutunza wapenzi au wake zao.

Nilichotaka kuwakumbusha wanawake zaidi ni kwamba kweli ni haki yao kutunzwa na waume zao lakini kunavigezo na masharti uzingatie kwa mfano:-

1. Mda gani hasa unapaswa kuomba HELA tangu mahusiano kutokea.
Mapenzi ata wiki bado umeshaomba uchongeshewe kabati LA vyombo.

Haiwezekana kuomba HELA Mara tu mpenzi wako anapokuomba kukutana ata kwa salam tu za kawaida. Mkutano WA kwanza ushaomba HELA ya kusukia mweeh.

2. Usimuombe HELA kwa mume au mpenzi ambayo anatoaga ata bila kuomba, ni uroho.

3. Angalia aina ya kazi anayofanya mpenz au mume na kipato chake ujue aina ya kizinga kinachomfaa, usije kumuova dozi.

4. Weka nafasi ya kutosha kati ya kizinga kimoja na kingine.Isiwe Jana pango ya NYUMBA imeisha, wiki ijayo simu imeingia kwenye ndoo ya maji .

5. Muandalie mazingira mazuri ya furaha kutoka kwako,ikiwezekana baada ya kumpa mavituz yalioenda shule ndio unamkurupusha na kizinga.

6. Kukosa kupo pia sio kila utakapoomba utapata wakati mwingine atakua anasaidia na ndugu pia.
Mume au mpenzi akikuambia cna ujue ana na inatakiwa maisha yaendelelee sio ndio unaanza cm hapokei ppchi hautoi sio poa.

7. Vizingi vikue taratibu usianze tu kuomba laki noo!, anza na kitu cha msimbz then unaangalia upepo ukiona anakuja poa unaendelea usikurupuke tu.

8. Pima aina ya mapenzi unayotoa kwa mtu yana hadhi ya kupewa unachotaka kutokana na ulichotoa. Umenipa mende kafa,laki yangu unaitaka ya nini? Yako wewe ni 5000 kwa services hii.

9. Jitaidi na wewe kumpa chochote ata kama kitatokana na HELA yake nwenyewe poa tu si anajua wewe huna kazi na kipato chako kidogo.

10. Sio lazima kila mkikutana kimwili lazima afungue pochi cku nyingine muagane tu. Kuna watu waajabu mno udhani kila gemu inamtonyo sio ivo.

NB.
Nazungumzia wale wasioelewa ayo apo juu na sijamaanisha wanawake wote.
Ruksaa kuongeza kitu au kupunguza, onesha na namba iliokugusa

Unatamani Kumuacha ila Unashindwa? Ngoja Nikwambie Kitu

$
0
0

Kuna watu wanna Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno ya shombo, wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi tu'', unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana mrija wa Oxygen yangu ya kutumia kesho?? Kama nilizaliwa peke yangu kwanini nisiweze kuishi wewe ukiondoka??

Maneno ya mkosaji haya, usiyasikilize kamwe! Unapoamua kufanya Maamuzi magumu usisikilize kingine chochote, Follow your heart. Wengi wamegeuzwa watumwa kwa kuamini they cant live bila watu fulani, kisa wamezoeana, au wamekaa muda mrefu kwenye mahusiano, unahisi kama hutaweza... Hamna kitu kisichowezekana, Mungu ameumba kusahau, utapona maumivu na utasonga! Hakuna destiny rahisi ya Kimapenzi bila kufanya maamuzi magumu, lasivyo Jiandae kuwa mtumwa wa mtu fulani, binadamu fulani ambaye naye amegundua wewe ni dhaifu na anatumia udhaifu wako kukutesa maisha yote...

Amua leo, Uwe mtumwa wa mtu au utengeneze furaha yako kwa Kumove on kupata Lover of you life

Mapumziko ya Rais Magufuli Chato ni Fundisho

$
0
0
Kwa Mara kadhaa,watanzania tumeshuhudia Mh.RAIS wetu kipenzi cha watanzania akitumia Muda wake mwingi,Nguvu zake na Akili zake zote kuwatumikia watanzania usiku na Mchana.Ameonesha Uzalendo kwa watanzania na Taifa kwa ujumla.

Mh.Rais yupo nyumbani kwake Chato kwa mapumziko mafupi baada ya Ziara na kazi kubwa ya kujenga Taifa.Mapumziko ya Mh.Rais yanatufundisha nini?,Ingalikuwa ni Rais asiye mzalendo wa kweli,Mapumziko haya angeweza kuyafanya nchi za ng'ambo,Marekani,Dubai,Uingereza na Mataifa mengine makibwa yenye Nguvu ya Kiuchumi.

Mh.Rais,kwa kuthamini,Kujali na kutetea maslahi mapana ya kodi za Watanzania,Mh.Rais Yupo Chato kijijini kwake,Amekomaa na Tanzania yake.Najua Jamaa zetu wanatamani sana Mh.Rais asafiri nje ya nchi hata kwa siku moja tu.Lakini Mjomba ni Boda tu Boda.(Home movement).Serikali ya JPM INA sikio la usikivu sana,Kwanini imesikia ?

Vyama vya siasa vilijipatia umaarufu sana kumseama sana Mh.Kikwete na viongozi waliopita kuwa safari zao za nje ya nchi ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Chai Ikulu ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Semina na walsha ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania,Posho za vikao ni Matumizi mabaya ya kodi za watanzania nk,nk.

JPM,kwa hekima ,unyenyekevu na kwa Sauti ya upole akasema "NIMESIKIA KILIO CHENU" sasa everything STOP.Hakuna safari Nje ya nchi,hakuna posho,hakuna chai ya Ghalama nk,Wakaanza ooooh,Ooooh mbona Rais hasafiri nje jamani!!!!! Oooooh mbona posho hazitoki jamani!!!!!!!,Ooooh Safari za nje wabunge vipi jamani!!!!!!! nk,nk.

"Nimesikia kilio chenu,Sasa ni kila MTU awajibike sawa sawa na Maombi yake" Huyu ndiye Rais anayeendelea kugonga vichwa vya HABARI Duniani nzima kwa utendaji wake,kwa misimamo yake,kwa uzalendo wake,na kwa Uadilifu wake wa hali ya Juu.Lazima tuige mfano wa Kiongozi wetu Mkuu.

Tuendelee kumuombea matashi mema MH.Rais na serikali yake,Tuendelee kuwaombea Viongozi wetu wa chama cha mapinduzi ,Lakini tuendelee kuwaombea pia wale wa upande wa Pili ili waendelee kubatizwa kwa moto.Watanyooka tu.

Mungu Ibariki Tanzania

Serikali Yatangaza Ajira Mpya 10, 184 Kuziba Mapengo ya Waliogushi Vyeti

$
0
0
Ofisi  ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetangaza kutoa vibali vya ajira 10,184 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, imefahamika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais, Utumishi, Florence Temba, ilieleza kuwa agizo hilo linazihusu Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala wa Serikali, pamoja na Taasisi na Mashirika ya Umma.

Ilimnukuu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akitoa agizo hilo wakati akizungumza katika kikao kazi na watumishi wa Umma wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam jana.

“Mgawanyo wa vibali vya ajira umezingatia upungufu uliojitokeza baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki, vipaumbele vya Taifa kwa sasa na upatikanaji wa watumishi kutoka katika soko la ajira,” alisema Kairuki.

Kairuki aliongeza kuwa taratibu za kukamilisha mgawo wa nafasi za ajira 4,816 zilizosalia unaendelea ili kuwezesha wizara na taasisi nyingine zilizokamilisha uhakiki wa watumishi wa umma hivi karibuni kuajiri watumishi wapya kuziba nafasi wazi zilizojitokeza.

Alieleza kuwa serikali imetoa kibali kuajiri watumishi wapya 15,000 ili kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti baada ya zoezi la uhakiki.

“Watumishi wa umma watakaoajiriwa kuziba nafasi hizo wanatarajiwa kuripoti kazini kuanzia mwezi Agosti, 2017,” alieleza Waziri Kairuki, na kuongeza kuwa utaratibu wa ajira mpya za serikali upo palepale na amewataka wananchi kutokuwa na wasiwasi wowote wa ajira hizo.

“Napenda kusisitiza kuwa vibali tulivyovitoa leo ni vile vilivyoziba pengo la walioghushi vyeti, naomba wananchi watambue kuwa suala la ajira mpya bado liko pale pale kama serikali ilivyojipanga,” alisema Kairuki.

Aprili mwaka huu, Rais John Magufuli alipokea ripoti yenye orodha ya watumishi wa umma ambao kati yao wanadaiwa kuwa na vyeti pungufu, vyenye utata na vya kughushi kutokea kwa Waziri Kairuki.

Waliokuwa na vyeti vya kughushi walikuwa 9,932, na Rais aliapa kwamba hawatarudi kazini. Rais Magufuli aliagiza kufutwa kazi kwa wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo na kuzuia mishahara yao ya mwezi huo, lakini hata hivyo bado mlango uliwekwa wazi kwa wenye pingamizi na wapo waliokataa rufaa huku wengine wakienda kwenye mamlaka husika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

Wiki iliyopita akiwa Dodoma, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alitangaza kuwa wiki hii serikali itatoa vibali 3,000 vya ajira katika sekta ya afya vikiwemo vya madaktari na wauguzi pamoja na maofisa hesabu 535 kwa ajili ya vituo vya afya vya kata ili washug

Mbunge wa Chadema Ataka Viongozi wa Kisiasa Waombewe

$
0
0
MBUNGE viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza amewaomba wananchi waliombee Taifa liendelee kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa wawe na uvumilivu ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.

Aliyasema hayo jana (Jumatano, Julai 12, 2017), katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Likangara wilayani Ruangwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo Peneza, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

“Wananchi wa Ruangwa nawatakia maisha mema ili mzidi kusonga mbele, tuombee amani ya nchi yetu na mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa.”

Mbali na Mheshimiwa Upendo, pia mkutano huo uliudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Mheshimiwa Hassan Masala (Nachingwea), Mheshimiwa Zubery Kuchauka (Liwale), Mheshimiwa Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na Mheshimiwa Hamida Abdalaah (Viti Maalumu).

Kwa pamoja wabunge hao walisema lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi aliwataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kudumisha na kuilinda amani iliyoko kwa sababu ndiyo inayowawezesha kufanya shughuli zao za kimaendeleo.

Alisema licha ya kuwepo kwa matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza katika baadhi ya maeneo vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na mikoa jirani limejizatiti kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote kwa mtu mmoja mmoja au vikundi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, JULAI 13, 2017

Rama Dee (Kinega) Aomba Poo....Amaliza Beef na Ruge na Clouds FM

$
0
0
Baada ya beef na mvutano wa muda mrefu baina ya Ruge (clouds media) na msanii Rama dee sasa wameamua kuzika tofauti zao

Itakumbukwa Rama dee ni miomgoni mwa wasanii waliokuwa wanaendesha kampeni ya ant virus kuidiss clouds na kujiita vinega yaani wanaharakati, lakini mpaka sasa
yamekwisha, wamesahau yote na muda huu kinega yupo live XXL na b12, mchomvu na wengineo wanareview mziki wa album wake na story zote zilizowahi tokea kipindi iko


Hongera Ruge kwa kukubali kusamehe na kuendelea kusonga mbele licha ya matusi na mabango mengi waliyokumwagia vinega!

Hongera pia kwako Rama dee, umethubutu.


Hii itakua somo kwa wasanii kama akina Ruby, muziki si bifu!

By Mr swax

Kutana na Maalim Fadhil Rashid Kutoka Komoro ni Mtaalam wa Tiba za Asili......

$
0
0
KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239/

WhatsApp IMO +255785786436/

Upinzani Katika Tanuru la Moto.....Magazeti ya Leo Tarehe 14 Jul 2017

$
0
0

Upinzani Katika Tanuru la Moto.....Magazeti ya Leo Tarehe 14 Jul 2017

Kimenuka..Ofisi ya CCM Yachomwa Moto Pwani

$
0
0
Watu wasiojulikana wameichoma moto ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Mshonzini iliyopo Wilayani Mafia Mkoani Pwani na kuteketeza mali mbalimbali za chama hicho.

Katibu wa CCM Wilayani Mafia, Mohammed Dhikiri, amethibitisha kutokea kwa tukio na kusema ofisi hiyo imechomwa moto usiku wa kuamkia leo na kuongeza kuwa moto huo umeteketeza kabisa ofisi hiyo na samani za ndani.

Bw. Mohammed amesema bado haijajulikana sababu za ofisi hiyo kuchomwa moto kwa kuwa wakati tukio linatokea hakukuwepo na viashiria vyovyote vya vurugu miongoni mwa wanachama wa chama hicho.

Naye Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dan, amesema, vipo viashiria vinavyoonesha kuwa alifika mtu asiyejulikana karibu na ofisi hiyo kisha kuwasha na kurusha kijinga cha moto kwenye paa la makuti la ofisi hiyo na kwamba, mtu huyo baada kutekeleza kitendo hicho aliondoka kuelekea kichakanani kama ambavyo alama za nyayo za miguu yake zinavyoonesha.
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live


Latest Images