Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Usibadilike Temporarily Kwa Sababu Unataka Uonekane Wife/Husband Material ili Umu Impress Mtu

$
0
0
Usibadilike TEMPORARILY kwa sababu unataka uonekane Wife/Husband Material ili umu-impress mtu halafu mkifika ndani unarudia rangi-rangi zako zilezile ambazo ndio NATURAL YOU
Muache akupende kwa Ulevi wako,Kwa Umbea wako,Kwa Kutoa kwako udenda ukilala,Kwa kuwa mchafu na kutofua Boxer,Kwa kunuka kikwapa cha njano,Kwa Umaharage ya Mbeya wako,Kwa sababu kama akikupenda KAMA ULIVYO LEO hata mkiingia ndani ATAKUPENDA TU kwa sababu alijua aina ya mtu anayeingia naye ndoani na ameshajipanga kisaikolojia kuvumilia harufu ha Boxer zako...Ukimuimpress kwamba hunywi kwa miezi mi3 akakuoa halafu HAMAD anakuta chupa za Ndovu stoo PATACHIMBIKA
Zimwi likujualo halikuli likakwisha,Muonyeshe rangi zako halisi akupende kwa Uhalisi wako lasivyo utaolewa leo SAWA na bajeti ya milioni 96 lakini Jiandae kuwa mjane baada ya Miezi 6 kwa karatasi ya Talaka ya Sh 50 Steshenari.
BE YOURSELF.
By Seth

Ujumbe Mzito wa Mchungaji Msigwa Kwa Mwigulu Nchemba

$
0
0
Huyu bwana mkubwa jimboni kwake kuna wananchi hawajawahi kuona mabomba ya maji, wanatafuta na kubeba maji kwa Mnyama Punda, YAANI HAKUNA MAJI, HAKUNA UMEME , HAKUNA BARABARA ,WANAPITA KWENYE BARABARA ZILIZOTENGENEZWA NA NG'OMBE.

HAKUNA VYUO , BARABARA YA LAMI NI ILE IENDAYO MWANZA ETI LEO AJE AKOSOE JIMBO LA IRINGA MJINI.

WANACHI WA IRAMABA MAGHARIBI WAKIJA IRINGA MJINI WATADHANI WAKO MBINGUNI, WANAIRINGA HAWANA LA KUJIFUNZA KUTOKA IRAMABA MAGHARIBI, ....WANAIRINGA KITU gani cha kujifunza kwa mtu huyu mwongo,anayewatumia tu WATU maskini wa IRAMABA

Mh.Zitto: Ukawa Rudini Bunge la Katiba Kumuenzi Marehemu Mama Yangu

$
0
0
Zitto Jana katika maziko ya Shida, ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wa kuteuliwa na Rais, Zitto aliwataka wajumbe wenzake kumuenzi mama yake kupitia viongozi wao, Mwenyekiti wa Kamati namba nane, Job Ndugai na Mwakilishi wa Ukawa, Profesa Ibrahimu Lipumba.

Alitoa ujumbe huo nyumbani kwa marehemu mama yake, mtaa wa Kisangani Mwanga, muda mfupi kabla ya kwenda makaburi ya Rubengela mjini Kigoma ambako mwili wa Shida Salum ulizikwa. Zitto alisema kama kweli viongozi hao wanataka kumuenzi mama yake, wamalize tofauti zao na kulifanya Bunge Maalumu la Katiba, kuendelea na shughuli yake ya kuwaletea Watanzania Katiba itakayowafaa kwa muda mrefu.

Alisema kuwa mama yake alikuwa mjumbe wa Bunge hilo baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, nafasi ambayo ingempa fursa ya kuandika historia ya kuwa mmoja wa wajumbe wa Bunge hilo, katika kuandika Katiba mpya ya Tanzania.

Hata hivyo, alisema kwa kuwa mama yake aliugua na Mwenyezi Mungu kwa kudra zake akamuondoa katika nafasi ya kuandika historia hiyo, kilichobaki ni viongozi na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kufikia maridhiano na kuandika Katiba hiyo.

Zitto alisema amejitahidi kwa kadri ya uwezo wake kumsaidia mama yake kupata matibabu ambayo yangerudisha afya yake, na kumpa fursa ya kushiriki katika shughuli zake za kawaida, lakini Mungu alipitisha uamuzi wake ambao hakuna wa kumpinga.

Naye Ndugai, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeongoza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye maziko hayo, alisema Shida alikuwa mtetezi wa Watanzania wa hali ya chini.

Alisema yaliyotokea ni mapenzi ya Mungu na kuitaka familia wasihuzunike kiasi cha kupitiliza, badala yake wakae pamoja na kuweka familia pamoja na kusonga mbele katika utekelezaji wa majukumu yao ya Taifa.

Naye Profesa Lipumba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, alisema kuwa Shida alisimama kuwapigania watu wenye ulemavu mchango ambao alikusudia kuutoa kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

Hata hivyo Lipumba alionya kuwa kama kweli watu wana nia ya kumuenzi Shida, hawana budi kusikiliza maoni ya wananchi walio wengi katika kuipata Katiba mpya, badala ya watu wachache kutaka kuichakachua.

Kilichomuua ‘Mtoto wa Boksi’ Chabainika; Wahusika Kunyongwa!

$
0
0
Kufuatia kifo cha mtoto Nasra, almaarufu kama ‘mtoto wa boksi’, kuna kila dalili kwamba kifo chake kimetokana na maradhi aliyoyapata wakati akiwa anaishi kwenye boksi. Kwa kuwa imethibitika kwamba mtoto alifariki kutokana na ugonjwa wa pumu—kufuatia kufungiwa kwenye mazingira machafu, kutoogeshwa na kupigwa na baridi masaa 24, na kwa kuwa wahusika waliokuwa wakimfanyia ukatili huo tayari walishakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kula njama za kumtesa mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia na asiyeweza kujitetea, mawakili wanaosimamia kesi hii watabadilisha masitaka ya kesi na kuwa KESI YA MAUAJI YA KUKUSUDIA.

Adhabu kwa mtu anayeua kwa kukusudia ni KUNYONGWA MPAKA KUFA. Kwa hiyo, wahusika wanasubiri kunyongwa hadi kufa pindi hukumu ya kesi hii itakapotoka. Na kwa kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani hawa wanadamu wasokuwa na haya, wajiandae kupokea kitanzi ili liwe fundisho kwa washenzy wengine wenye tabia za kinyama kawa hawa wendawazimu.

NIONAVYO:
Natoa wito kwa watanzania wenzangu kutoa taarifa polisi haraka pindi waonapo ukatili wowote dhidi ya wanyonge, hasa watoto wadogo, ili sheria ichukue mkondo wake. Tatizo la watanzania walio wengi ni kwamba hatujaliani. Unaweza ukamuona mzazi/mlezi akimtesa mtoto lakini ukakaa kimya. Kufanya hivyo ni kutomtendea haki yule kiumbe anayeonewa au kunyanayaswa. Tuweni na huruma kwa viumbe hawa wa mwenyezi Mungu wanaoonewa bila sababu za msingi huku wakiwa hawawezi kujitetea kwa namna yoyote ile. Tukio la mtoto Nasra, ambaye Mungu amemuita kwake, liwe fundisho kwa watu wengine wanaofumbia macho ukatili kwa watoto na wanyonge.

Nawasilisha.

Maskini Hapiness Magese Hata Weza Kupata Mtoto Maisha Yake Yote

$
0
0
Februari  ya  kila  mwaka  huenda  ikawa  ni  kumbukumbu  mbaya  kwa  mwanamitindo  na  Miss Tanzania  2001, Hapiness Millen  Magese  ambaye  mwezi  huo  ndipo  alipogundulika  kuwa  hataweza  kupata  mtoto  katika  maisha  yake  yote.....
Hali  hiyo  ndio  imemlazimu  mwanamitindo  huyo  kuanzisha  taasisi  ya  kuwasaidia  wanawake  wengine  hapa  nchini  ili  waepuke kile  ambacho  kimemkuta  yeye  baada  ya  kuondolewa  uzazi  kwa  ugonjwa  ambao  hapendi  kusikia  unamtokea  mwanamke  mwingine.....

"Nikiwa  sekondari  nilikuwa  napatwa  na  ugonjwa  ambao  kwa  wakati  huo  niliona  ni  wa  kawaida.Nilikuwa  napata  maumivu  makali  wakati  wa  hedhi  yaliyonisababishia  kutapika  na  wakati  mwingine  kupoteza  fahamu," anasema.

"Kila  nilipoingia  kwenye  hedhi  nililazimika  kulazwa  kwa  siku  sita  hadi  kumi  hospitalini,kutokana  na  maumivu  hayo  kuna  wakati  wanafunzi  wenzangu  waliwahi  kunihoji  ni  kwa  nini  mimi  kila  mwezi  lazima  niugue," anasimulia

Anasema  ilifika  wakati  wakawa  wanamhesabia  tarehe  kutoka  siku  anayotoka  hospitali  hadi  mwezi  mwingine  atakapolazwa  tena

"Niliteseka  sana, nakumbuka  kuna  siku  nilizidiwa  wakati  mama  yangu  hayupo.Baba  akachukua  jukumu  la  kunibeba  na  kunipeleka  hospitali," anasema.

"Nilipokuwa  kwenye  maumivu  makali  aliniambia  nijikaze  kama  mwanamke,  hivyo  nikawa  namficha  baba  maradhi  yangu, ingawa  ilikuwa  kila  mwezi  kama  siyo  kunipeleka  hospitali  yeye  basi  lazima aje  kunitazama  hospitali."

Anasema  hata  baada  ya  kujiingiza  kwenye  masuala  ya  urembo, bado  hali  ya  maumivu  wakati  wa  hedhi  iliendelea  na  siku  alipoamua  kujiingiza  kwenye  uanamitindo  kuna  watu  walimuuliza  atamudu  kweli  kufanya  mitindo  na  hali  aliyonayo?

"Nikiwa  hapa  nyumbani  sikujua  nasumbuliwa  na  nini. Siku  moja  nikaamua  kwenda  kupima  wakati  huo  nikiwa  Afrika  Kusini, nikagundulika  kuwa  na  ugonjwa  wa  Endometriosis   na  tiba  pekee  ikawa  kufanyiwa  upasuaji," anasema  Magese.

Anasema  alifanyiwa  upasuaji  mara  ya  kwanza  na  kuonyesha  yai  lake  moja  ni  bovu  hivyo  kutakiwa  litolewe  ingawa  alikuwa  na  uwezo  wa  kubeba  mimba.

"Nilifanyiwa  upasuaji  mara  ya  pili,kila  siku  nikalazimika  kuwa  nafanyiwa  uchunguzi  ili  kubaini  maendeleo  ya  hali  yangu, lakini  cha  kushangaza  hali  ilizidi  kuwa  mbaya.Kuna  wakati  nilijiuliza  kwa  nini  mimi?" anasema  Magese.

Anasema  katika  kipindi  hicho  alikuwa  anachoma  sindano  kila  asubuhi  kwa  siku  63  ili  kunusuru  kizazi  chake  bila  mafanikio, aliendelea  kufanyiwa  upasuaji  mara  12  zaidi.

Endometriosis  ni  nini?  Dalili  zake  ni  zipi?
Daktari  bingwa  wa  magonjwa  ya  akina mama  na  uzazi  wa  Hospitali  ya  Taifa  Muhimbili, Dr. Fadhlun  Almy  anasema  bado  hajapata  jina  la  Kiswahili  la  ugonjwa  wa  Endometriosis, lakini  unasababishwa  na  seli  za  tumbo  la  uzazi  kuwa  nje   ya  kizazi.


"Dalili  za  ugonjwa  huu  ni  maumivu  makali  wakati  wa  hedhi  na  maumivu  hayo  yanasababisha  makovu  ndani  ya  ukuta  wa  tumbo.Makovu  hayo  yakizidi  yanasababisha  mirija  ya  uzazi  kuungana  na  Ovari," anasema

Mawaziri Saba ‘Mahututi’

$
0
0
Msuguano mkali umekuwa wakati Bunge linapokaa kama kamati kupitia vifungu vya bajeti za wizara husika. Hata hivyo, bajeti hizo zimepitishwa baada ya maelezo marefu na wakati mwingine msaada wa kiti cha Spika au pale Waziri Mkuu au Kaimu wake ndani ya Bunge anaposimama ‘kuokoa jahazi’.

Mawaziri ambao hadi sasa wameingia katika orodha ya bajeti zao kupita kwa mbinde na wizara zao kwenye mabano ni Profesa Jumanne Maghembe (Maji), Profesa Anna Tibaijuka (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini), Dk John Magufuli (Ujenzi), Dk Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), Sophia Simba (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) na Dk Seif Rashid

(Afya na Ustawi wa Jamii).

Sababu za kasheshe

Kwa sehemu kubwa, bajeti nyingi zilipata upinzani kutokana na Hazina kutoa fedha kidogo za maendeleo kati ya asilimia 19 na 30 tu, wakati wizara nyingine zilitikiswa na tuhuma za ufisadi wa watendaji wake.

Sophia Simba

Miongoni mwa mivutano ni ule uliohusu taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama) ambayo Mwenyekiti wake ni mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma, hoja iliyoibuka wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Mbunge wa Ole (CUF), Rajab Mbarouk Mohamed alitaka taasisi hiyo ifutwe, kwa maelezo kwamba inajihusisha na masuala ya kisiasa na kwamba mwaka 2010, Mama Salma aliitumia kumfanyia kampeni mumewe.

Katika hoja hiyo alisema mmoja wa wajumbe wa bodi ya taasisi hiyo ni Waziri wa wizara hiyo, Sophia Simba kinyume na sheria na taratibu.

Waziri Simba akajibu: “Nipo Wama lakini kazi ninayoifanya pale ni ya kujitolea na silipwi kitu. Kanuni na sheria zinakataza mtu kujihusisha na taasisi nyingine kama tu anakuwa analipwa mshahara”.

Profesa Maghembe

Juzi, Profesa Maghembe alipata wakati mgumu baada ya hoja iliyoshika mshahara wake iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika kujadiliwa kwa dakika 31, hadi Kaimu Waziri Mkuu, Profesa Mark Mwandosya alipoingilia kati.

Wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao, waliungana kutetea hoja ya kutaka suala la upatikanaji wa maji liwe ajenda ya kwanza ya Serikali. mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Pauline Gekul alitaka bajeti hiyo ifumuliwe ili kuondoa posho za vikao na safari.

Mbunge wa Lushoto (CCM), Henry Shekifu alisema tatizo la maji ni zito na akapendekeza kuanzishwa kwa mfuko wa maji.

Profesa Mwandosya alisimama na kutoa uthibitisho kwa niaba ya Serikali kwamba muswada huo wa fedha utapelekwa bungeni kabla ya kuvunjwa kwa Bunge 2015 na alikubaliana na wabunge kwamba suala la maji litakuwa ni nambari moja katika vipaumbele vya Serikali.

Dk Magufuli

Kauli ya Waziri wa Ujenzi, Dk Magufuli kwamba ujenzi wa barabara si sawa na chapati, ilisababisha baadhi ya wabunge kumjia juu wakati wa kupitisha vifungu vya bajeti ya wizara yake.

Baadhi ya wabunge wa mikoa ya kusini mwa nchi, walichachamaa kutokana kile walichodai kuwa ni kutotengwa kwa fedha za ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.

Suala jingine lililotawala mjadala huo ni sakata la malori kuruhusiwa kuzidisha uzito barabarani, hoja ambayo iliibuliwa na Machali ambaye alimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwaomba radhi Watanzania kutokana na hatua yake ya kuyaruhusu kubeba mizigo mizito na kusababisha barabara zinazojengwa kwa mamilioni ya fedha za kodi za wananchi kuharibika. Pinda alitoa ufafanuzi mzuri.

Dk Mwakyembe

Wabunge walitaka maelezo ya kina juu ya uendeleshaji Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), Shirika la Ndege (ATCL), ukarabati wa meli ya MV Victoria na upanuzi uwanja wa ndege Mwanza.

Wabunge waliokuwa vinara wa kupinga bajeti hiyo wakitaka mambo hayo manne kupatiwa ufumbuzi ni wabunge wa CCM, Dk Hamisi Kigwangalla (Nzega), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi), Charles Mwijage (Muleba Kaskazini), Richard Ndassa(Sumve) na mbunge wa Ilemela (Chadema), Ezekiah Wenje.

Profesa Muhongo

Ni kati ya bajeti ambazo zilipita kwa mbinde huku wabunge wakiibua hoja na ufisadi mbalimbali uliofanywa ndani ya wizara hiyo.

Sakata la IPTL ni moja kati ya mambo yaliyotikisa mjadala wa bajeti hiyo huku Mnyika na mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka wakiwasilisha ushahidi kuhusu tuhuma kadhaa za wizara hiyo.

Mashambulizi hayo yaliibua tuhuma mpya dhidi ya wabunge, Profesa Muhongo alipodai kwamba baadhi ya wabunge wakiwamo wa upinzani wamehongwa na IPTL.

Katika maelezo yake, Profesa Muhongo alisema ana ushahidi wa kamera za CCTV zinazowaonyesha vigogo hao wa upinzani wakisaini nyaraka na kuchukua fedha hizo.

Sakata jingine lililoibuka ni kukosekana kwa umeme katika maeneo ya vijijini na kulazimika Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa ufafanuzi akisema kuwa fedha zitakazotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Nishati Vijijini (Rea) hazitaguswa.

Profesa Tibaijuka

Waziri Tibaijuka alijikuta katika wakati mgumu baada ya wabunge, wengi wa Dar es Salaam kumbana kuhusu ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni.

Suala hilo lililohusishwa na ufisadi lilionekana kumchanganya waziri huyo na wakati mwingine alishindwa kujibu maswali na badala yake kuwashambulia wabunge wa upinzani hasa Halima Mdee wa Chadema.

Alisema wapo wabunge ambao walikuwa na hoja na wengine walikuwa wakipiga kelele, akitoa mfano tuhuma dhidi yake kuwa anamiliki kiwanja katika Mji wa Kigamboni kwamba hazina ukweli wowote.

Dk Seif Rashid

Nayo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilikumbwa na dhoruba jana kabla ya kuokolewa na Profesa Mwandosya baada ya wabunge wengi hususan wanawake, kutaka kuikwamisha.

Imeandikwa na Daniel Mjema, Fidelis Butahe na Habel Chidawali

Utafiti Wabaini Milima ya Samunge Kwa Babu wa Loliondo Imejaa Dhahabu

$
0
0
Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, Kanda ya Kaskazini wamethibitisha uwepo wa hazina ya madini ya dhahabu katika Mlima Rankiroga na Mto Karabaline katika Kijiji cha Mgongo, Kata ya Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane alisema jana kuwa Ofisi yake imefanya utafiti wa awali katika Kijiji cha Mgongo na kubaini uwepo wa dhahabu hiyo.

Wamiminika

Gazeti hili lilikuwa la kwanza kuripoti uwepo wa dhahabu hiyo baada ya maelfu ya watu kumiminika tena katika eneo la Samunge, lililokuwa maarufu baada ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile kutangaza kuwa na dawa inayonywewa kwa kikombe kutibu maradhi sugu.

Habari kutoka Samunge zinasema wachimbaji wanazidi kumiminika kusaka madini hayo yaliyogundulika kuwapo kwenye mashamba ya watu na maeneo ya kingo za mto huko Mgongo, kijiji kilichopo jirani na kwa Mchungaji Mwasapile, maarufu kama Babu wa Loliondo.

Diwani wa Samunge, Jackson Sandea alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika kijiji hicho... “Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000 na bado wanaongezeka. Hii inaweza kuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu. Dhahabu hii inapatikana mtoni tu. Watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye anachimba.”

Alisema tofauti na maeneo mengine, dhahabu ya Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi. “Kuna wengine wanapata (dhahabu), hata mashambani lakini mtoni ndipo inapatikana kwa wingi zaidi.”

Matokeo ya utafiti

“Ni kweli kuna dhahabu katika eneo la Mto Karabaline na kiasi kikubwa kipo katika eneo la Mlima Rankiroga,” alisema Magayane. Mlima huo upo jirani na Mto Karabaline ambako dhahabu ilianza kugundulika. Wachimbaji wamekuwa wakiomba idhini ya Serikali kuchimba dhahabu katika mlima huo.

Magayane aliwataja wataalamu waliofanya utafiti huo kuwa ni Mtaalamu wa Miamba, Fatuma Kijanda; Fundi Sanifu Mkuu, Zephelin Kalunde na Fundi Sanifu Mwandamizi, Aloyce Mlaga.

Alisema uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua ujazo wa dhahabu katika eneo hilo na muda ambao uchimbaji unaweza kuchukua... “Tumepeleka baadhi ya miamba katika ofisi za uchunguzi Dodoma na tunatarajia kupata taarifa karibuni.”

Hata hivyo, alisema dhahabu inayopatikana kwenye Mto Karabaline inaweza kumalizika ndani ya miaka miwili tofauti na ile ya mlimani ambayo alidokeza kuwa itachukua muda kuisha.

Jamaa Aliyeigiza Kama Idi Amini Amefariki Dunia.

$
0
0
Wakati Tanzania tukiendelea kuwa na majozi ya vifo 3 mfululizo kutoka kwenye tasnia ya filamu Tanzania,wenzetu nao  wamempoteza jamaa aliyeigiza kama Idi Amini.
Kupitia filamu ya  The Rise and Fall of Idi Amin jamaa alicheza kama Idi Amini  na filamu hii ilikua ikielezea matukio yote aliyowahi kuyafanya Idi Amini enzi za uhai wake.
Joseph Olita ambaye ndiye aliyecheza kama Idi Amini amefariki jumapili ya June 01 akiwa na umri wa miaka 70 kusini mashariki mwa Alego huko kogelo Nchini Kenya na ilikua baada ya kumaliza mazishi ya mama yake mzazi.

Mmoja wa ndugu wa Joseph,Bi.Risper Odero amesema kifo cha Joseph Olita kimetokana na shinikizo la damu iliyosababishwa na shughuli nyingi na majonzi wakati wa kumuaga marehemu mama yake mzazi.
Bi Odero amesema kifo cha Olita ni pigo kwa familia hiyo hasa baada ya kumuaga mama yao mzazi masaa kadha kabla ya kifo cha olita,Olita alikua anafanana sana na aliyekua kiongozi wa kiimla Uganda bwana Idi Amin Dada.
Miongoni mwa vitu walivyokuwa wanafanana ni pamoja urefu wa futi sita nchi 5.5 na uzito wa kilogramu 150 na ndiyo maumbile pekee yaliyo wafanya wengi kudhani kuwa olita alikua ndiye Idi Amin.
Mbali na filamu ya The Rise and Fall of Idi Amin ya miaka ya 80 iliyobeba maisha ya Idi Amin kama kiongozi wa kimila aliyeingia madarakani mwaka wa 1971 na kutolewa mwaka 1979 pia ameigiza kwenye filamu ya Mississippi Masala mwaka 1991 na amewahi kuigiza kama polisi kwenye filamu ya Sheena ya mwaka 1984.

Maximo Awapa Jeuri Tegete, Cannavaro

$
0
0
Na Wilbert Molandi 
WACHEZAJI mahiri wa Yanga, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na straika Jerry Tegete, wamefurahishwa na ujio wa Kocha Mbrazili, Marcio Maximo katika kikosi cha Yanga na wakatamba kuwa timu yao itakuwa tishio msimu ujao.

Maximo ambaye yupo katika mazungumzo ya mwisho kabla ya kusaini mkataba Yanga, ndiye aliyemuibua Tegete akimtoa kwenye kikosi cha Shule ya Sekondari Makongo jijini Dar, kuja kuichezea Stars na Cannavaro ndiye aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho enzi za Mbrazili huyo.

“Hakuna asiyejua uwezo wa kufundisha wa Maximo, kila mtu anaujua, anaweza kuhamasisha wachezaji ndani na nje ya uwanja, hivyo mashabiki watarajie mengi mazuri.
“Maximo anajua kumtengeneza mchezaji na akawa bora, ninaamini ujio wake Yanga utakuza na kuwaendeleza wachezaji ili wawe na viwango vikubwa, ninajua uwezo wake, aliwahi kunifundisha,” alisema Tegete.

Kwa upande wa Cannavaro, alisema: “Wapinzani wenzetu wajiandae msimu ujao wa ligi, ninaamini timu yetu itakuwa bora zaidi, kama wachezaji tukimpa ushirikiano Maximo, atafanya vizuri.
“Alishawahi kunifundisha nikiwa ninacheza katikati na (Kelvin) Yondani kwenye kikosi cha Stars, hivyo ninafurahia ujio wake.”

Asha Baraka: Sitamsamehe Ally Choki na Wala Hatujapatanishwa na Mtu Yoyote

$
0
0


MKURUGENZI wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka, amesema kamwe hawezi kumsamehe mwanamuziki Ally Choki ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, ambaye ana bifu naye la muda mrefu.

Hivi karibuni habari zilienea kuwa wawili hao wameshapatana baada ya kukutanishwa na chombo kimoja cha habari nchini, jambo ambalo Asha amelikanusha.

“Siwezi kupatana na Choki kwa sababu sioni haja ya kufanya hivyo. Nimesikia kwenye mitandao kuwa eti tumepatanishwa... watu bwana! Labda waliopatana ni wao siyo mimi. Nasisitiza habari hizo ni za uongo na ninaomba Choki akae mbali na mimi,” alisema Asha.

Kwa upande wa Choki, alipoelezwa kuhusiana na majibu ya Asha, alicheka kisha akasema: “Kama yeye amesema hivyo, acha iwe hivyohivyo. Kwanza hayo mapatano yenyewe sijafanya kwa ajili yake maana hakuna kitu ninachotaka kwake. Nina mambo mengi ya kufanya.”
GPL

Big up Rais Wetu Kwa Kumtafutia Fursa Diamond

$
0
0
Big up Rais wetu kwa kumtafutia fursa Diamond
Rais wetu ni mtu wa kujituma sana yaani usiku na mchana, USA hadi Oman kwa ajili ya kuwatafutia maisha bora watanzania kwa ujumla, kama hapa anavyoonekana akiwa busy kumtafutia Diamond wasanii wa kupiga naye kolabo. Hapo yuko busy akichart na 50cent kama ataweza kumpa tafu kijana wetu mkali cause no matter what Diamond is more important than staying back in the country to deal with some minor issues like ESCROW account or wasting his energy and time to address the issue of our new constitution or even wasting his valuable time thinking about the measures of tackling unemployment and corruption in our country cause at the end of the day his workaholics ministers like Wasira, Lukuvi, Juma Nkamia, Sophia simba under the supervision of the commander himself Mizengo Pinda can fix all the minor problems in fixing the country while our dear President deal with more urgent and important issue of promoting diamond 

Nani Mkali Kati ya Hawa..Kushoto ama Kulia

$
0
0

Wadada fulani kwenye harusi ya rafiki yao , waliamua kuingia kati na kuonyesha uwezo wao wakucheza mziki kwa shangwe na mitindo mbali mbali...Unavyoona hapo Nani mkali zaidi kwa Kucheza?

Picha Hizi Zimenipa Jibu Kwanini Anamjali Shoga Yake Zaidi Kuliko Mimi Mpenzi Wake

$
0
0
Machale yalianza kunicheza pale nilipokuta picha za ajabu kwenye simu ya mpenzi wangu akiwa na rafiki yake wa kike chumbani wakifanya mambo yanayo husiana na usagaji, Picha hizo zilinitisha ikabidi nimuulize hakuonyesha kujali nakuona nikama kitu cha kawaida, baadhi ya picha walionekana wakikiss, na nyingine kukumbatiana, ila mpaka leo anabisha anasema walikuwa wancheza tu ...ila nimepata jibu kwanini muda mwingi anaspend na huyo rafiki yake zaidi yangu sometimes hatuonane weekend nzima nikumuuliza anasema yupo kwa shoga yake
Ushauri wadau nimpige chini au Kuna Jinsi ya Kumrekebisha?

Nchi iko Kwenye Auto Pilot.....Imesetiwa Inajiendea tu Rubani Kalala Hana Habari

$
0
0
Marry Nagu ametoa taarifa bungeni kuwa kauli ya Steven Masele ni yake na si ya serikali,ila ile ya ikulu ndio ya serikali.
Maneno ya Kakobe sasa yanatimia. Watavurugana kama Babeli. Ikulu yakana Masele, Nape atampinga Mwigulu, Nagu atasema Masele kakosea, Kinana atawakana mawaziri na kuwaita mizigo hivyo ni indirect attack kwa Rais aliyewateua, Muhongo atasema Ole sendeka ni mnafiki na hana elimu alifeli shule, Mwigulu atachahamaa eti viongozi wanatoa sana misamaha ya kodi ndio maana nchi ina matatizo, Kesho lukuvi atamkana nagu. Alhamisi waziri mkuu atasema taarifa ya ikulu sio ya serikali,ni ya sefue. Yani mchezo bado unaendelea.
Orodha ni ndefu ila wanapingana kwa maneno sasa na waishia kuzipiga ngumi Siku moja.

Nape Amfyatua Mwigulu kuhusu Bunge la Katiba

$
0
0
SIKU moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba kunukuliwa na gazeti la serikali la Habari Leo akitamba kupinga nyongeza ya siku 60 za Bunge la Katiba, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, amempinga akisema hawezi.

Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alitoa tambo hizo juzi mjini Iringa wakati akihutubia mkutano wa hadhara, akisema kuwa atapinga kwa nguvu zake zote Bunge hilo kukutana kwa siku nyingine 60.

Hata hivyo, msimamo wake unakinzana na chama chake ambacho kimeapa kwamba hata kama wajumbe wenzao wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wasiporudi bungeni, wao wataendelea na Bunge hadi katiba mpya ipatikane.

Katika kikao chake cha Kamati Kuu cha hivi karibuni, CCM iliazimia kupambana na UKAWA popote, nje na ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, huku ikisisitiza kwamba haiwezi kuwabembeleza warudi bungeni kwa sababu chama hicho kinao wajumbe wa kutosha kutimiza theluthi mbili ya kura zinazotakiwa kikanuni.

Kufuatia mkorogano huo, Tanzania Daima Jumatano lilimtafuta Nape jana kwa simu akiwa ziarani mkoani Manyara ili kupata msimamo wa chama kuhusu katiba mpya.

Katika majibu yake kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu, Nape alisema: “Gazeti la Habari Leo limemnukuu vibaya Mwigulu. Hawezi kupinga jambo ambalo rais amelipitisha.

“Chama kupitia vikao halali kimeishatoa tamko na msimamo unajulikana. Vinginevyo ili ampinge rais, yeye kama naibu waziri alipaswa ajiuzulu kwanza. Hata hivyo, naibu waziri haruhusiwi kuwasilisha hoja binafsi.”

Kwa mkanganyiko huo, ni dhahiri CCM wanakinzana katika suala zima la upatikanaji wa katiba mpya inayotokana na matakwa ya wananchi.

Itakumbukwa kuwa katika siku za hivi karibuni kwenye mikutano yao ya hadhara iliyofanyika visiwani Zanzibar na mkoani Tabora, CCM kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana na Nape walisema kuwa hawahitaji katiba mpya kwa sababu sio muarobaini wa matatizo waliyonayo wananchi.

Viongozi hao walisisitiza kuwa hata katiba mpya ikipatikana itawekwa kabatini, huku Nape akizidi kuwashambulia wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, akisema wamekengeuka kwa mapendekezo yao ya muundo wa serikali tatu.

Licha ya rasimu ya katiba kupendekeza muundo wa serikali tatu, CCM imekuwa ikiendesha harakati za kuipindua, ikitetea muundo wa sasa wa serikali mbili uendelee, jambo linalopingwa na UKAWA hadi kufikia hatua ya kutoka nje ya Bunge hilo.

Katika mkutano wake wa mjini Iringa, Mwigulu alipinga Bunge hilo lisiongezewe muda kwa madai kwamba likiendelea kwa mtindo kama wa awamu ya kwanza, itakuwa sawa na kutumia vibaya fedha ya walipa kodi.

Aliahidi kumshauri Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta, amuandikie barua Rais Jakaya Kikwete, ili avunje Bunge hilo endapo wajumbe wake watashindwa kutumia wiki mbili za mwanzo kujadili mambo ya msingi katika rasimu hiyo.

Source: Tanzania Daima

Ofisi ya Kanumba Imeishia Wapi? Movies Zenyewe Hatuzioni

$
0
0
Hivi najiuliza sana ile ofisi ya Kanumba mdogo wake Seth alidai anaiendeleza na wakaja watoto wengine wa yule baba yao wakajidai wamejipanga kuendeleza mtanange,
HIvi imeishia wapi mana hata muvi zenyewe hatuoni...HAIJAFUNGWA KWELI na vifaa kuuzwa?
Kuna kitu Kinaendelea ? Mwenye habari Atujuze

Johari Amtupia Vijembe Chuchu Hans Msibani

$
0
0

Staa wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kumtupia vijembe kiaina msanii mwenzake , Chuchu Hans ambaye ‘anabanjuka kimalovee ’ na mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya RJ, Vincent Kigosi ‘ Ray TheGreatest’.

Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye msiba wa mwigizaji Sheila Haule ‘ Recho ’ Sinza -Palestina , Dar , hivi karibuni ambapo vijembe viliibuka baada Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘ Nyerere ’ kumuuliza kwa lugha ya utani Chuchu kuwa RJ itachangia nini msibani hapo.

Johari akadakia: “Kampuni yangu si ya uchochoroni au ya chumbani , ninaTIN namba kabisa siyo kama hiyo nyingine ,iweje umuulize asiyehusika.” Baada ya Johari kutamka maneno hayo ,waombolezaji waliokuwepo msibani hapowalipigwa na butwaa na kuhoji kulikoni? 

Johariamekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano na Ray kipindi cha nyuma huku kukiwa na taarifa kuwa Chuchu ana kampuni iitwayo Chura ikimaanish aChuchu na Ray hivyo ilitafsiriwa kuwa alikuwa akiipiga kijembe kwamadai kuwa haiwezi kufikia levo za RJ.

Alipofuatwa na mwanahabari wetu ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo , Johari hakuwatayari kwani alisema ana majonzi yakuondokewa na kipenzi chake Recho hivyo hakutaka malumbano na watu katika kipindi hiki kigumu .

Samweli Eto’o Aendelea Kumchimba Mourinho

$
0
0
SAMUEL Eto’o aliwaduwaza Ujerumani kwa bao lake juzi Jumapili wakati Cameroon ilipotoka sare ya 2-2 na Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia.

Eto’o alimzidi ujanja beki, Mats Hummels, kisha akamchambua kipa Roman Weidenfeller, lakini kubwa lililovutia kwenye mchezo huo ni ushangiliaji wake baada ya kufunga bao hilo.

Eto’o aliendeleza vita yake na kocha Jose Mourinho, aliyehoji kuhusu umri wake kwa kudai kwamba straika huyo amezeeka na hivyo staa huyo kumjibu baada kukimbia hadi kwenye kibendera za kona na kisha kushika mti wa kibendera hicho na kuigiza mzee anayetembea na mkongojo. Eto’o aliwahi kushangilia kwa staili hiyo pia kwenye mchezo wa Chelsea.

Mabao mengine katika mchezo huo yalifungwa na Thomas na Andre Schurrle kwa upande wa Ujerumani na Eric Choupo-Moting kwa upande wa Cameroon.

Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Shilole na Ney wa mitego walipotajwa bungeni.

$
0
0
Kutoka Dodoma 104.4 kabla ya kujadiliwa kwa bajeti ya wizara ya afya na ustawi wa jamii ilianza sehemu ya maswali na majibu kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa nne.
Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Juma Nkamia ndio alijibu swali la Catherine Magige kuhusiana na udhalilishaji wa Wanawake unaofanywa kwenye kumbi mbalimbali za starehe Tanzania.

Waziri Nkamia alisema ‘nakubalia kabisa kwamba kumbi za starehe zimekua zikitoa burudani na ajira kwa vijana hapa nchini lakini ndani ya kumbi hizo kumekua na vitendo vinavyofanyika kinyume na maadili ikiwemo udhalilishaji wa Wanawake’
‘Katika kukomesha hali hiyo serikali kupitia baraza la sanaa BASATA wamefanya vikao kadhaa na wamiliki wa bendi, maafisa utamaduni, wakuu wa polisi, wamiliki wa kumbi na wanaojihusisha na uchezeshaji wa mtindo wa kanga moja ili kujadili ukiukwaji wa maadili kwenye sanaa’

Kwenye sentensi ya tatu Waziri anasema ‘Pia serikali imeacha kutoa usajili kwa vikundi kama cha kanga moko kwa kuwa uchezaji wake unakwenda kinyume na maadili ya Tanzania na kutoa onyo kwa wamiliki wa kumbi, Wasanii na hata asasi zinazojihusisha na sanaa ambazo hazifati maadili’
Anasema ‘Wasanii waliopewa Onyo ni Ney wa Mitego, Shilole, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na kwa upande wa kumbi ni Mama’s and Papa’s lakini pia maonyesho ya urembo ya Miss Utalii yalifungiwa ambapo pia Serikali imeunda kamati ya kitaifa ya kuzuia ukatili na unyanyasaji dhidi ya Wanawake/Wasichana watoto’

Mtoto Mchanga Auwawa Kwa Kufungwa Plasta Mdomoni na Puani Kisha Kutupwa

$
0
0
Mtoto mchanga, amekutwa ametupwa pembezoni mwa barabara ya Kawe-Beach, huku puani na mdomoni akiwa amefungwa plasta, iliyosababisha kukosa pumzi na kufariki.

Katika hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja ambaye hakujulikana jina lake wala kujua anapoishi, anasadikika kutenda ukatili na unyama wa hali juu kwa kumuua huyo mwanaye na kisha kumtupa pembezoni mwa barabara hiyo.

Wavuvi wa eneo hilo waliona mfuko pembezoni ukiwa na damu hali ambayo iliwashtua na kuamua kusogea karibu, ndipo walipomkuta mtoto huyo mwenye jinsi ya kike, akiwa amefariki huku akiwa amefungwa plasta mdomoni na puani.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images