Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104745 articles
Browse latest View live

ZITTO Kabwe Awaamshia DUDE Chadema.......

$
0
0
KIONGOZI Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, katika kile kilichoonekana kuwapa kijembe Chadema, akisema kutaka nchi kunyimwa misaada ni uhayawani, kwani vita dhidi ya kuminywa kwa demokrasia inapaswa kupiganwa ndani.

Zitto alitoa kauli hiyo kupitia akaunti yake katika Mtandao wa Kijamii wa Twitter, ikiwa ni siku moja tu baada ya Chadema kupitia kwa mwanasheria wake, Tundu Lissu kuitaka Jumuia ya Kimataifa kuinyima Tanzania misaada kufuatia kitendo cha kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa viongozi wa upinzani, hasa kutoka chama chao.

“Huu ni uhayawani, hii ni nchi huru, kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa, tupambane ndani kuleta demokrasia,” aliandika Zitto.

Hata hivyo, kufuatia kauli hiyo baadhi ya watumiaji wa mtandao huo walianza kumuuliza maswali kadha Zitto ambaye aliwajibu na kuufanya mjadala huo kuwa mrefu, baadhi wakimuunga mkono na wengine wakipingana naye.

BABY Madaha Akimbilia Mwanza Kufanya Zindiko........

$
0
0
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha Joseph, amekiri kuwa kila mwaka hurudi kwao Mwanza kwa ajili ya kuonana na wazee wake ‘kutambika’ ambao humsaidia kufanya mambo yake yaende vizuri mjini, kitu alichosema ni muhimu sana katika wakati huu ambao maisha ni magumu.
Akizungumza na Za Motomoto News, Baby Madaha alisema huwa anakwenda kwao kila mwaka na hivi sasa yupo huko kwa ajili ya kuwaona wazee wa kimila kwani huwa wanamsaidia, hasa pale mambo yanapokuwa magumu.

“Bila wazee mambo hayaendi kabisa, niko kwetu Mwanza kwa ajili ya kufanya mambo ya kimila ili walau mambo yaende vizuri mjini maana hali imekuwa mbaya sana, nimekuwa nikifanya hivyo kila mwaka na nimeona huwa inasaidia sana,” alisema.

ZARI Hassan Anaweza Kuwa Anajuta Kujiingiza Kwa Watanzania Ambao Muda Mwingi ni Kufuatilia ya Watu

$
0
0

KAMA KUNA KITU ZARI HASSAN ANAWEZA KUWA ANAJUTA NIKUJIINGIZA KWA WA TANZANIA AMBAO WANA MUDA MWINGI WA KUFATILIA MAISHA YA WATU KULIKO YA KWAO.

NADHANI HAWA NDIO WANAJUANA NA WANAJUA SIRI ZA FAMILIA YAO KATIKA KIPINDI HIKI SIDHANI KAMA WA TANZANIA TUNAWEZA KUMPA NAFASI SHETANI YA KUANZA KUJADILI FAMILIA ZA WATU KWA MABAYA TENA FAMILIA AMBAZO ZIKO KWENYE MAJONZI.

TUSIJISAHAU KUWA HII MITANDAO YA KIJAMII HAINA THAMANI KULIKO UTU WAKO.

USIJISAHAU NA KUANZA KUPOST UJINGA KISA TU ETI NI FAKE ACCOUNT USISAHAU MUNGU HAFICHWI NA NDIO MAANA KUNA WALIKUWA NA FAKE ACCOUNT ILA WAKAPATA MATATIZO KILA MTU AKAWAJUA.

ANYWAY ZARI MUNGU AKUPE UJASIRI KATIKA KIPINDI HIKI AMBACHO UNAPITIA KATIKA MAUMIVU HUKU UKIWA UNAKUTANA NA CHANGAMOTO ZA WATU WALIOKOSA KAZI ZAIDI YA KUFATILIA NA KUJADILI SYSTEM YA MAISHA YA WATU.

SEMA KAMA SWALA LA KABURI LA IVAN KUFUKULIWA NA KUAMBIWA HAJAFA LIMEPITA NAAMINI NA HILI LITAPITA.

ILA TUSINYOOSHEE WATU VIDOLE WAKATI WENYEWE HATUIJUI KESHO YETU.

UNAWEZA FANYA KITU UKIAMINI HAKUNA ANAYEKUJUA ILA USISAHAU SEKUNDE MOJA INATOSHA MUNGU KUKUONESHA UBAYA WAKO KWA WATU.

TUSIMRUHUSU SHETANI KUTUTOA UFAHAMU KIASI HIKI CHA KUSHINDWA KUHESHIMU HATA MISIBA YA WATU.


BY ABBY

Wanaotapeli Watalii, Ujumbe huu uwafikie

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema atapambana na matapeli wote ambao wamekuwa wakiuza safari za watalii kwa njia ya mtandao.


Amesema kumekuwepo na malalamiko yanatolewa na baadhi ya watalii kuwa wanalipia huduma zote, lakini wanapofika nchini kwa ajili ya utalii hawakutani na waliowalipa fedha hizo.


Ameyasema hayo leo Alhamisi, Julai 20, wakati akizungumza katika ufunguzi wa jengo jipya la Lake  Nyasa lililopo chini ya ukumbi wa mikutano wa AICC  mjini hapa.


Amesema atahakikisha anawashughulikia wale wote wanaofanya utapeli huo kwenye mitandao kwani wamekuwa wakiitia aibu nchi.


"Kwa kweli hii ni aibu kubwa na utapeli huu umeshamiri kwa kiasi kikubwa na mwisho wa siku watasababisha tukose watalii, tunaomba sana hata wananchi watoe ushirikiano kuwafichua maana wengine nyie mnawajua pia, " amesema Maghembe.


Pia, Maghembe ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wote wanaoingiza mifugo hifadhini kuacha mara moja kwani wanasababisha usumbufu mkubwa kwa watalii pindi mifugo hiyo inapokatiza maeneo ya hifadhi.


Naye, Mwenyekiti wa bodi ya AICC, Ladislaus Komba alisema kuwa kuwepo kwa ukumbi huo kutasaidia kuongeza kasi ya maendeleo kwa Jiji la Arusha na hata wajasiriamali kutokana na kuwa na eneo maalumu la kuonyesha bidhaa zao.


Komba amesema kuwa taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha inaleta maendeleo kwa wakazi wa Arusha ambapo ina mpango wa kujenga kitega uchumi kingine cha ukumbi wa mikutano wa maonyesho jijini Arusha cha Mount Kilimanjaro.


Kwa upande wa Mkurugenzi wa AICC, Elishilia Kaaya amesema kuwa jengo hilo limegharimu kiasi cha Sh3.2 bilioni na kwamba uwepo wake utasaidia kuondoa changamoto mbalimbali za ukosefu wa eneo la kufanyia maonyesho.

Kilichojiri baada ya Lowassa kufika kuhojiwa na DCI

$
0
0

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Edward Lowassa leo July 20, 2017 ameripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kuhojiwa ‘DCI’ kuhojiwa kwa mara ya nne.


Lowassa ametakiwa kurudi tena kwa DCI baada ya wiki tatu kutokana na kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Lowassa ameambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.

Hii ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa  Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani  akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru.

Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.

WARUNDI Mrudi Nchini Kwenu Hapa sio Kwenu- Rais Magufuli

$
0
0
Rais John Magufuli amewataka wanachi wenye asili ya urundi waliopo nchini Tanzania wafanye wawezavyo kwa hiari yao warudi kwao wakaijenge nchi wasisingizie kuna vita kwa kuwa Rais wao Pierre Nkurunziza ameshawahakikishia kuwa kuna amani ya kutosha.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika viwanja vya Posta baada ya kupokea ugeni kutoka nchini Burundi wa rais huyo pamoja na baraza lake la mawaziri mchana wa leo uliyokuja kwa mazungumzo ya kiuchumi.
"Ndugu zangu warundi mmesikia taarifa iliyotolewa na Rais Nkurunziza anawaomba mrudi kwenye nchi yenu, mkajenge nchi yenu, mkajitafutie maisha. Ni kama wanaotoka Afrika kwenda Itali lakini kuna wakimbizi wamezoea kukimbia tu, sasa kwa sababu Rais ameshawaambia murudi nyumbani sasa mchukue hatua za kurudi nyumbani kwa hiyari wala sisi hatuwafukuzi. Ninafahamu wapo baadhi ya watu ambao hufanya biashara na wakimbizi kwa sababu ndipo wanaotoa vyakula, wanaomba misaada kule nje ya kusema kuna wakimbizi sana na saa zingine wanaelezea hali ambayo haipo", amesema Rais Magufuli. 
Pamoja na hayo Rais Magufuli ameendelea kwa kusema "nimesikia wakimbizi wengine wameahidiwa kwamba mtakuwa mnapewa  elfu kumi kumi wabaki sasa nasema wakawapeni hizo hela mkiwa Burundi, nataka tuelezane ukweli kwasababu tunawajibu wa kulinda amani katika nchi zetu na Mhe. Rais ameshazungumza hapa lakini nchini Tanzania tumekuwa na uzalendo mzuri kwamba wakimbizi wanapokuja muda mwingine tunawapa uraia. Sasa kama wapo watu wanakimbia kule kwa sababu waje tuwape uraia waziri wa mambo ya ndani simamisha zoezi la kuwapa uraia wanaokuja huko".

Rais Magufuli akiwa na wageni wake kwenye uwanja wa Posta.
Aidha, Rais Magufuli ameunga mkono ombi la Rais wa Burundi aliyowataka wananchi wake warundi kwao wakaijege kwa pamoja nchi hiyo kwa kuwa hakuna shida ya aina yoyote katika kipindi hiki.
"Na mimi niwaombe nitoe wito kwa ndugu zangu wa Burundi kwa hiyari yao mimi siwafukuzi ila kwa hiari yao warudi nyumbani na niwapongeze wale laki moja na hamsini elfu waliorudi kwa hiari yao pia niyaombe Mashirika yanayoshughulikia wakimbizi waache kuwahubiri wakimbizi kwamba Burundi kuna matatizo, waanze kuhubiri amani ya kweli kwamba wanao uwezo hawa wakimbizi kwenda Burundi", amesisitiza Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amemthibitishia Rais Nkurunziza kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa majirani zake wote waliopo ndani ya Afrika Mashariki ndani ya SADC pamoja na nchi ya Burundi.

SHETTA "Sijawahi kuathirika"

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva, Shetta amefunguka kwamba kuachia nyimbo nyingi katika kipindi kimoja siyo ishara au njia ya kumfanya mtu aweze kufanya vizuri katika soko la muziki.

Msanii Shetta.
Shetta ameeleza hayo kwenye 'story' tatu za kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio baada ya kuwepo tabia ya wasanii kufululiza kutoa kazi zao kwa wakati mmoja jambo ambalo watu wengi wanadhani msanii huyo hajiamini katika kile anachokifanya huku wengine wakifikili ndiyo njia nzuri ya wao kupata kile wanachokitaka ili waweze kuburudika zaidi.
"Mimi siamini sana kwenye hilo ndiyo kutasababisha ku-trend au kufanya vizuri, kwa upande wangu nafikiri kujipanga kwangu ndiyo kuna ni sababisha nifanye vizuri huwenda labda naweza kujipanga 'faster faster", amesema Shetta.
Pamoja na hayo, Shetta amesema hajawahi kuathirika na kukaa kimya kwake.

MAN Fongo Ampigia Magoti Meneja.....

$
0
0
Mkali wa muziki wa singeli Bongo, Man Fongo amekubali yaishe baada ya kumaliza tofauti zilizokuwepo kati yake na meneja wake wa zamani, kutoka 'Makers Entertainment' G Maker kwa kurudi na kuomba radhi.

Msanii huyo aliyetamba na ngoma ya ‘Hainaga ushemeji’ mwaka 2015 akiwa chini ya usimamizi wa G Maker, aliingia katika ‘bifu’ kali na meneja wake huyo katikati ya mwaka 2016- 2017 huku chanzo kikitajwa kuwa ni kutofautiana katika suala la pesa.
Baada ya kutengana kwa takriban mwaka mmoja, Man Fongo ambaye ametambulisha rasmi ngoma yake mpya jana aliyoipa jina  ‘popcorn’, amesema aligundua kosa lake na kuamua kurudi kwa G Maker, kwa kuwa aliona hawezi kuwa mbali naye kikazi kutokana na uhusiano wao kama ndugu.
“G Maker mimi ni kama kaka yangu….. Mimi ndio nilimfuata, nilikwenda kwake na kuomba tuyamalize yale matatizo hivyo saizi nimerudi kwenye uongozi wangu wa zamani,” Man Fongo amefunguka kwenye East Africa radio.
Ngoma ya Man Fongo aliyoiachia jana ipo chini ya uongozi wa G Maker na huku mpikaji wa ngoma  akiwa ni Mensen Selekta ambaye kwa pamoja hiyo ndiyo timu iliyotengeza 'hit' ya 'Hainaga Ushemeji'.
Msanii huyo amesema video ya ngoma hiyo ipo katika hatua za mwisho, na wakati wowote itakuwa hewani.

KIMENUKA...Mbunge Saed Kubenea Aitwa Polisi.......

$
0
0
Mbunge wa jimbo Ubungo,(CHADEMA) Saed Kubenea ameitwa polisi na kutakiwa kuripoti leo tarehe 20/7/ 2017 kutoa maelezo kituo cha polisi kufuatia malalamiko aliyotoa Profesa Lipumba Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Mbunge wa Ubungo Mh Saed Kubenea wiki iliyopita alifanya mkutano na vyombo vya habari kama Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa CUF iliyochini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif na kutangaza oparesheni ya kumuondoa Profesa Lipumba katika ofisi za chama cha CUF Buguruni.
Baada ya Kubenea kutangaza oparesheni hiyo siku mbili mbele aliibuka Profesa Lipumba na kwenda kituo cha polisi kutoa malalamiko juu ya kile alichokisikia kutoka kwa kiongozi huyo na oparesheni hiyo aliyotangaza.

"Ni kweli Kubenea ameitwa na kuitwa kwake kumekuja baada ya wiki iliyopita kufanya mkutano na waandishi wa habari kama Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani akiwa pamoja na viongozi wa CUF inayoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, Julius Mtatiro na Katibu Mkuu Maalim Seif na kutangaza operesheni inayoitwa 'Operesheni Ondoa Msaliti Buguruni (OMB). Operesheni hiyo itaendeshwa kwa ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA" ilisema taarifa ya CHADEMA 
Profesa Lipumba na baadhi ya viongozi wa CUF wapo katika mgogoro kutokana na kiongozi huyo kipindi cha uchaguzi mwaka 2015 kuandika barua ya kujiuzulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa CUF taifa na kubaki mwanachama wa kawaida, lakini baada ya uchaguzi kupita kiongozi huyo akataka kubatilisha maamuzi yake ya kujiuzulu jambo ambalo viongozi wa CUF na baadhi ya wanachama wamekuwa wakilipinga na kukataa, japo  Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi yeye bado anamtambua Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF taifa.

JINSI ya Kupunguza Uzito Wako (Diet plan)

$
0
0
Kuna njia nyingi sana ambazo hujaribiwa na watu ili kupunguza mwili na tumbo lakini zinakuwa ngumu sana au zinakuwa haziendani na mazingira wanayoishi hivyo kupelekea kushindwa njiani. Zipo njia za kutumia madawa kama kahawa na vinginevyo ambazo huwa si za kudumu. Kwa kuwa kahawa huwezi kutumia zaidi ya round 3 kwa maana hiyo ukinenepa tena inabidi utafute njia nyingine.

Lakini njia hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako ya kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyo hivyo bila kuongezeka mwili. Mara nyingi vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokunywa npyo vinatuponza.

Tutakuwa tunakuletea ratiba ya kupunguza uzito wako kwa muda wa mwezi mzima.
Vidokezo muhimu Kupungua uzito kunategemea na kiwango cha mafuta cha mtu mwilini (body fat), uzito wa mtu, calories anazohitaji kwa siku, BMI yake pamoja na lengo la mtu la kupungua uzito. Je vyakula ninavyokula hunipa nguvu (calories) na uwezo wa kumudu majukumu yangu ya kila siku? Nahitaji kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kwa kiasi gani? Kwa wengine wanahitaji kupunguza asilimia 10, 20 au 25 ya kiwango cha mafuta mwilini.

Kwa maana hiyo, si kila diet plan humfaa kila mtu, inaweza ikakufaa wewe lakini isimfae mtu mwingine.

Cha kuzingatia ili kupungua uzito ni kufuata ushauri wa wataalamu wa lishe (nutritionists), daktari, wataalamu wa mazoezi na nk. Kama utafuatilia diet plan hii, utaona kila siku unahitaji kunywa kikombe kimoja cha kahawa, ni vizuri kubadilisha unywaji wa kahawa kwa chai, yaani kama leo utakunywa kahawa kesho kunywa chai na  kadhalika. Kwa wale wenye ugonjwa wa shinikizo la damu (hypertension), anxiety disorders na nk, wanashauriwa kuepuka kahawa kabisa na hivyo wanywe chai. Wagonjwa wa kisukari wanaweza kunywa chai au kahawa kwa kukamulia ndimu au limao ndani yake na hivyo kuongeza ladha.

Siku ya Kwanza (Day 1)

Tembea kwa muda wa dakika 30 asubuhi au jioni kabla ya kula chakula chochote. Kwa wale wenye mashine ya tredmill basi pia tembea kwa muda wa dakika 30 kwa kuanza na spidi ndogo (kama namba 5 na kuongeza hadi spidi namba 8). Unaweza pia kukimbia kwa muda wa nusu saa au kukimbia kwenye mashine ya tredmill kwa muda wa nusu saa. Anza kukimbia kwa spidi ndogo (kwenye tredmill) halafu ongeza spidi yako, au unaweza kukimbia kwa spidi ya juu kama spidi 8 kwa muda wa dakika 5 na kisha kupunguza hadi spidi 5, hii inaitwa interval training, lengo ni kukupa uwezo wa kufikisha dakika 30, kuchoma mafuta mwilini, kupunguza mapigo ya moyo yarudi kwenye kiwango cha kawaida kwani wakati unafanya mazoezi mapigo ya moyo huongezeka sana, kuupa uwezo moyo wako wa kufanya kazi vizuri.

Wale wenye matatizo ya kiafya ya mapigo ya moyo au wale ambao walishawahi kuugua hapo awali matatizo haya kama atrial fibrillation, ventricular tarchycardia na nk, wagonjwa wa pumu, ni vizuri kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa wataalamu wa mazoezi (sports therapist) pamoja na kushauriana na daktari.

Fanya mazoezi ya tumbo (sit-ups) kati ya 15-20. Ukiona ni ngumu sana unaweza kuanza hata na sit-ups 10 na utakuwa unaongeza kadri siku zinavyoenda na kadri utavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu na tumbo.

Unaweza kutumia bench au kulala sakafuni. Ukimaliza kutembea na kufanya sit-ups kunywa maji ya uvuguvugu glass 4. Siyo lazima unywe yote kwa wakati mmoja. Unaweza kuwa unakunywa huku unaendelea na mambo mengine mpaka glasi 4 ziishe. Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo ya uvuguvugu. Limao na ndimu siyo tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza mafuta mwilini.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kunywa kikombe kimoja cha kahawa au chai kwa kuweka kijiko kimoja kidogo cha sukari (2.5ml spoon). Yai moja la kuchemsha. Slice moja ya mkate wa brown bread (mikate inayotengenezwa kwa ngano nzima nzima). Usithubutu kuweka siagi wala vinavyofanana  na hivyo.Kula matunda kadri uwezavyo lakini epuka ndizi tamu.

Chakula cha mchana (Lunch): ¼  Kuku wa kuchoma au wa kuchemsha na si vinginevyo. Salad au kachumbari ya mboga mboga tofauti lakini isiwe na mayonnaise. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 tena. Jitahidi kuepuka snacks kama ice cream, chocolate, biskuti nk. Jizoeshe kula matunda kwa wingi kila unapohisi njaa.

Jioni: Tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa (dakika 30) pamoja na kufanya sit-ups wakati unasubiri chakula cha usiku.

Chakula cha usiku (Dinner): Supu ya samaki yoyote yule bakuli kubwa la kutosha. Unaweza kutumia karoti, nyanya au tungule, broccoli, cauliflower, pilipili boga na za kuwasha, ndimu au limao, kitunguu maji na thomu na nk, epuka viazi vyovyote vile kwenye supu.

Siku ya pili (Day 2)
Tembea kwa nusu saa asubuhi (dakika 30) na fanya sit-ups 15-30. Baada ya mazoezi kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa kuweka kijiko kimoja cha sukari kidogo kama nilivyoeleza hapo awali. Sausage moja ya kuchemsha ya kuku au ya nyama ya ngombe. Slice moja ya brown bread pamoja na matunda mengi.

Chakula cha  mchana (Lunch): Ndizi moja ya kuchoma pamoja na kachumbari au salad ya mboga mboga aina yoyote lakini isiwe na mayonnaise. Mishikaki 2-3 ya nyama ya ngombe (isiwe ya nundu au nyama ya mafuta), kuku, samaki.

Jioni: Tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa (dakika 30) na baada ya hapo fanya sit-ups 15-20 kisha kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. Epuka juisi aina yoyote ile iwe fresh au za kwenye boksi kwani mara nyingi watu wanahadaiwa na juisi za kwenye boksi zinazosema ni fresh na hazina kemikali yoyote, ukweli ni kwamba kampuni zinazotengeneza juisi hizi huwapa tenda kampuni za kutengeneza manukato ambazo ndizo hutengeneza maboksi haya na kuweka syrup na harufu kulingana na harufu ya tunda linalohitajika, mfano kama kampuni ya kutengeneza juisi inahitaji boksi la harufu ya embe basi watawatengenezea boksi hilo kwa kutumia syrup ya embe na harufu ya embe.
Pia juisi za kwenye boksi, wakati wa kutengenezwa huhifadhiwa kwa muda mrefu na kupitia mlolongo mrefu wa utengenezaji hivyo kuondoa virutubisho asilia muhimu pamoja na fibre ambazo ni muhimu sana kiafya.

Chakula cha usiku (Dinner): Supu ya mboga mboga (vegetable soup) pamoja na matunda. Epuka ndizi mbivu. Epuka vilevi vya aina yoyote vile km pombe, wine, sigara, tumbaku, khuberi na nk.

Siku ya Tatu (Day 3)
Mazoezi kama kawaida. Kimbia au tembea kwa dakika 30, kisha fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa kikiwa na kijiko kimoja cha sukari.

Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla au baada ya kula. Ndizi 2 za kuchemsha Bukoba siyo ndizi tamu (sweet banana). Bakuli la kutosha la supu ya mboga mboga (vegetable soup) ukishushia kwa matunda kwa wingi. Epuka ndizi mbivu. Hakikisha wakati wa kupika supu yako huweki mafuta ya kupikia au siagi n.k.

Jioni: Tembea au kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 baada ya kufanya mazoezi. Unaweza kula matunda wakati unasubiria chakula cha usiku.
Chakula cha Usiku (Dinner): BBQ sausage 3 pamoja na salad au kachumbari.

Siku ya nne (Day 4)
Tembea au kimbia kwa muda wa nusu saa, kisha fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha kahawa au chai, weka kijiko kimoja cha sukari. Sindikiza kwa matunda ya aina yoyote. Epuka ndizi mbivu.

Chakula cha mchana (Lunch): Kiazi kimoja cha kuchemsha pamoja na mboga mboga za majani kama njegere, karoti, pilipili boga, broccoli, cauliflower, na nk. Sukumizia na supu ya uyoga (mushroom soup). Jitahidi supu zako usiweke mafuta wakati unapika. Glasi moja ya maziwa fresh (250ml-300ml).

Jioni: Mazoezi kama kawaida.
Chakula cha Usiku (Dinner): Vegetable platter, mboga za aina zozote unazopenda bila kuweka mafuta hata tone ikishindikana weka kijiko kimoja cha olive oil au mafuta ya alizeti. Samaki wa kuchoma au kuchemsha, kula mzima lakini asizidi robo kilo. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Siku ya Tano (Day 5)
Kimbia kwa dakika 30, kama utatembea, tembea kwa dakika 45. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu galsi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha kahawa au chai chenye sukari kijiko kimoja. Slice 1 ya mkate mweupe uliyopakwa siagi kidogo sana pamoja na mayai mawili ya kukaanga (Spanish omelet). Malizia kwa matunda.

Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla ya kula chakula cha mchana. Supu ya kuku bakuli moja tu. Hakikisha kuku wako umemtoa ngozi ya juu kabla ya kumpika. Unaweza kuweka tambi (spaghetti) kidogo kwenye bakuli la supu lakini siyo lazima. Tambi zisipikwe kwa mafuta bali zichemshwe tu.

Jioni: Kimbia kwa dakika 30 au tembea kwa dakika 45. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Chakula cha usiku (Dinner): Kula mboga mboga aina yoyote ile pamoja na matunda kwa wingi.

Siku ya Sita (Day 6) 
Tembea kwa dakika 45 au kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Cornflakes na maziwa ambayo ni skimmed milk ama low fat (yenye mafuta kidogo). Kula matunda yoyote unayopenda.

Chakula cha Mchana (Lunch): Kula beefcubes zilizochemshwa kiwango kidogo kama robo kilo. Unaweza kupendezesha kwa karoti, cauliflower, broccoli, pilipili hoho au njegere nk, weka kijiko kimoja cha mafuta ya alizeti au olive oil.

Jioni: Mazoezi kama kawaida. 
Chakula cha usiku (Dinner): Kula tambi (noodles au spaghetti) zilizochemshwa na sauce yoyote utakayopenda ila isiwe na mafuta zaidi ya kijiko kimoja. Usisahau matunda kwa wingi.

Siku ya Saba (Day 7) 
Tembea kwa dakika 30-45, kama unakimbia basi kimbia kwa muda wa nusu saa. Fanya sit-ups 20-30 kisha kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4.

Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kikombe kimoja cha chai au kahawa, yai moja la kuchemsha pamoja na maziwa fresh glasi moja.

Chakula cha mchana (Lunch): Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 kabla ya kula. Supu ya mboga mboga bakuli moja la kutosha, ndizi ya kuchemsha moja (ndizi bukoba), malizia kwa matunda mengi, leo unaruhusiwa hata kula ndizi  mbivu au ndizi tunda.

Jioni: Mazoezi kama kawaida 
Chakula cha usiku (Dinner): Nusu kuku au beef sausage, pamoja na wali maharage na salad au kachumbari ya aina yoyote ile ya kutosha lakini isiwe na mayonnaise, cheese au butter.

Unaruhusiwa kunywa glasi 2 za white wine baada au wakati unakula kama ni kuku. Au glasi 2 za red wine baada au wakati unakula kama ni beef sausage. Ila kama ni kuku iwe kuku, kama ni beef sausage iwe hiyo na siyo vyote viwili.

HAYA Ndio Madhara 6 Ya Kutoa Mimba

$
0
0
Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote.

Breaking News: Tundu Lissu Akamatwa Uwanja wa Ndege wa Dar

$
0
0

Moja ya Habari zilizotufikia kutoka Dar es Salaam ni kuhusu Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika ‘TLS’ ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu kukamatwa na Polisi akiwa Airport Dar es Salaam akielekea Kigali, Rwanda  kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza kesho.

Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martn Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi.

Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema,  John Mrema amesema kwamba mwanasheria huyo amekamatwa  jioni hii.

Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kwamba ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Asilimia Kubwa ya Wanaume Hawana Nguvu za Kiume

$
0
0

Utafiti wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) umebaini kuwa asilimia 33 ya wanaume 672 mkoani Dar  es salaam wamebainika kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.

Hayo yamezungumzwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Dk. Pedro Pallangyo ambaye ameeleza kuwa idadi kubwa ya wagonjwa hao wanasumbuliwa na tatizo kubwa la shinikizo la damu  na kisukari.

Utafiti huo uliofanywa na JKCI, umebainsisha kuwa  katika wanaume watatu mmoja aligundulika kukosa nguvu za kiume.

”Hali hii inaashiria kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara jambo ambalo linasababisha athari ya nguvu za kiume kuwa kubwa ,” amesema Dk. Pallnagyo.

Aidha amesema changamoto hiyo inaweza kutatuliwa iwapo jamii itakuwa na utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema na kupata matibabu.

Pia alichukua nafasi kutoa ushauri kwa wanaume kupunguza sana matumizi ya chumvi nyingi mwilini na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi kwani hivyo hucgangia kwa kiasi kikuibwa sana magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari na kupelekea nguvu za kiume kushindwa kufany akazi ay ake kama mabavyo inatakiwa.

HIZI Ndio sehemu 10 zenye Msisimko Mkali zaidi Kwenye Mwili wa Mwanamke

$
0
0
Kila mwanaume anapenda kua fundi wa tendo la ndoa akiwa faragha na mke au mchumba wake lakini bahati mbaya sana hakuna kanuni maalumu ya kumsisimua mwanamke kwani kila mwanamke ana eneo lake ambalo likiguswa anakua taabani hivyo ni wajibu wa mwanaume kulitafuta na kuligundua eneo hilo.

Mazoea ya kufanya mambo yaleyale kila siku kwa muda mrefu hufanya tendo hilo la ndoa lianze kua baya na huenda ikawa chanzo  cha mtu kuchepuka kutafuta ladha zingine.

Kitaalamu katika sayansi ya binadamu kuna maeneo kadhaa ambayo wanawake wote wakiguswa hupata msisimko mkali lakini msisimko hutafautiana kutokana na mwanamke husika kama ifuatavyo.

1. Kichwani; juu ya kichwa cha binadamu kuna mishipa mingi ya damu na ile ya fahamu hivyo maeneo haya yakishikwa homoni kama oxytocin na serotoinin huachiwa mwilini na kuleta msisimko mkubwa.


Jinsi ya kufanya; mshike kwanzia nyuma ya sikio kisha ingiza vidole katikati ya nywele kama unamkuna kichwa bila kutumia nguvu.


2. Sikio; sikio ni sehemu yenye mishipa ya fahamu inayoenda kwenye ubongo, mara nyingi sikio watu hua wanalipuuza sana na kuzani halihusiki lakini naomba nikwambie ni moja ya sehemu inayoweza kumfanya mtu achanganyikiwe.


Jinsi ya kufanya; anza kwa kumnong'oneza kwa sauti nzito, kisha libusu sikio lake baada ya hapo unaweza kulamba sehemu ya sikio la nje na baadae kuingiza ulimi ndani ya sikio kabisa. hapa msisimko ni mkali sana na anaweza kukukwepa na kutoa sauti kali ya kimahaba.


3. Ulimi ; ulimi ni sehemu ya mwili ambayo ina mishipa mingi mara mia moja zaidi kuliko ile mishipa ya fahamu ya viganja vyetu. msisimko wa ulimi unasababishwa kumwagika kwa homoni ambazo zinatuletea furaha ya mioyo yetu.


Jinsi ya kufanya; busu tu  inatosha kusisimua ulimi wa mtu wako, bahati mbaya kuna watu hawajui kubusu. ukiwa unabusu mtu usipanue mdomo mzima kama samaki mfu... fungua mdomo wako kidogo kisha nyonya lips za juu wakati mtu wako ananyonya za chini na hii ndio busu linavotakiwa kua.


4. Shingo; hii ni sehemu ya mwili yenye ngozi laini sana ambayo inasisimka hata kwa kuipumulia tu na pua. ni moja ya sehemu nzuri sana kunyonya, kulamba na kubusu.


Jinsi ya kufanya; ukiwa umemkumbatia mtu wako basi busu upande wa kulia au wa kushoto wa shingo huku ukinyonya ngozi la eneo hilo.


5. Chuchu; wanaume wengi wanatumia sehemu hii kama sehemu kuu kumsisimua mwanamke, ni kweli kabisa tafiti zinaonyesha kwamba sehemu ya ubongo ambayo husisimuka chuchu za mwanamke zikiguswa ni sehemu hiyohiyo ambayo inasisimka kinembe na uke vikiguswa. kwa hiyo ni moja ya sehemu muhimu sana.


Jinsi ya kufanya; tomasa matiti yote ya mwanamke kwa kutumia mikono yako miwili kisha nyonya chuchu yake taratibu huku kama unaing'ata na kuiachia. badilisaha kwa kuchocha chuchu ya kulia na kushoto.


6. Kiuno au mgongo wa chini; kama umechunguza ni kwamba wanawake wengi husisimka sana wakiguswa viuno vyao ghafla hata wakati wa kukumbatiwa tu. hii ni sababu ya mishipa ya fahamu inayoenda hadi kwenye sehemu zake nyeti hupita huko.


Jinsi ya kufanya; tomasa kama unafanya masaji sehemu ya chini kabisa ya kiuno kabla makalio hayajaanza. hii itamfanya arelax sana lakini pia kuongeza damu kwenda sehemu zake nyeti tayari kwa tendo la ndoa.


7. Tumbo; tumbo ni sehemu ambayo watu wengi hawaitilii manani sana lakini misuli ya tumbo imeungana na uke moja kwa moja ndio maana baadhi ya wanawake hufika kileleni kwa kufanya mazoezi ya tumbo kitaalamu kama core exercises..


Jinsi ya kufanya; tomasa tumbo lake kwanzia juu kabisa ya tumbo na kwenda tumbo la chini na kisha busu taratibu maeneo mbalimbali ya sehemu ya tumbo na unaweza kumalizia kwa kunyonya kitovu.


8. Katikati ya mapaja; hii ni sehemu yenye msisimuko mkubwa kwenye mwili wa mwanamke, watu wanaondesha magari wanajua siri hii kwani wakimpakia mwanamke wanatumia njia hii kumsisimua kwa kuweka mkono mmoja kwenye mapaja yake.


Jinsi ya kufanya; shikashika sehemu za katikati ya mapaja kwanzia magotini kwenda mpaka karibu na uke.unaweza fanya hivyo wakati ukiwa unambusu.


9. Nyayo za miguu; nyayo za miguu zikiguswa hata kwa mtu ambaye sio wa kike zina msisimko sana kama wa kutekenywa hivi na sina msisimko mkubwa kuliko sehemu nyingi nilizotaja.


Jinsi ya kufanya; shika nyayo moja ya mguu kisha kwa kutumia viganja viwili tomasa katikati ya mguu kwanzia kwenye kisigino mpaka kwenye vidole.usitumie nguvu nyingi...


10. Kinembe [critoris]; hii ni sehemu ya mwanamke ambayo kazi yake ni kuleta msisimko tu na raha kwa mwanamke..eneo hili linazaidi ya mishipa ya fahamu 8000, ni eneo dogo sana lakini shughuli yake sio ndogo. naweza kusema ndio eneo lenye msisimko mkali kuliko yote niliyotaja hapo juu na likiguswa tu mwanamke analoana kabisa.


Jinsi ya kufanya; kidole chako kikubwa cha kinganyani bonyeza na kuachia sehemu hiyo kama mtu anayekagua parachichi pia sugua kwenda chini, juu na pembeni kuangalia muhusika anapenda wapi zaidi pia kama una uhakika na usafi au afya ya muhusika unaweza lamba lwa kuzungusha ulimi sehemu hiyo.


Mwisho; sehemu zote nilizotaja hapo juu ni muhimu sana kwa ajili ya kumuandaa mwanamke japokua kila mwanamke anapata msisimko zaidi kutokana na yeye mwenyewe alivyo yaani mwingine shingo linaweza kua na msisimko wa kawaida likiguswa lakini mwingine ikawa  msisimo mkali zaidi.

MREMBO Sanchoka Kugeukia Kilimo cha Nafaka....

$
0
0

VIDEO queen mwenye umbo matata Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ ameweka wazi dhamira yake ya kujitosa kwenye biashara ya kilimo cha nafaka mbalimbali.
Sanchi aliiambia 3-Tamu kuwa, hivi karibuni anafikiria kujiingiza kwenye kilimo am­bacho anaamini kina mafanikio makubwa ingawa wengi wa­naona ni kazi ya kishamba. “Urembo nauweka kando kwa muda kwanza ili ni­jikite zaidi kweye kilimo, nimeo­na kuna fursa kubwa ukizingatia warembo wengi wanachukulia kilimo kama biashara ya wa­shamba,” alisema Sanchi.

JE ATAWEZA KILIMO AU ANAZINGUA?

BIDHAA za Tanzania zafutiwa Kodi China

$
0
0

Kiwango cha biashara kati ya Tanzania na China kimefikia Dola bilioni 4.7 katika kipindi cha mwaka 2015 na kwamba kiwango hicho kinatarajiwa kuongezeka zaidi.

Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Masuala ya Uchumi na Biashara, katika Ubalozi wa China hapa nchini, Bw. Lin Zhiyong, amesema hayo Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya forodha kuhusu maboresho na Vihatarishi vya kiforodha, yanayotolewa kwa maafisa wa forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wataalamu kutoka Chuo cha Forodha cha Shanghai-China.

Bw. Lin Zhiyong amesema hivi sasa nchi yake ni kama imeondoa kabisa kodi kwa bidhaa za Tanzania zinazosafirishwa kwenda China hadi kufikia 97% na kwamba anatarajia kuona wafanyabishara wa Tanzania wakichangamkia fursa hiyo na kuongeza kiwango cha bidhaa za Tanzania zenye ubora zinazosafirishwa kwenda nchini China.

Mbali na hilo Zhiyong amedai hivi karibuni China iliipatia Tanzania seti 3 za makontena ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam, vyenye uwezo mkubwa wa kugundua pembe za ndovu, dawa za kulevya na silaha zinazosafirishwa kimagendo kutoka ndani na nje ya nchi.

Pata Dawa ya Kuongeza Hips, Makalio, Kuwa Mweupe na Kuongeza Maumbile ya Mwanaume....

$
0
0

PENDEZA NA MARKSON BEAUTY. ONGEZA HIPS NA MAKALIO, KUWA MWEUPE NA SOFTI, ONGEZA MAUMBILE YA KIUME, NGUVU NA HAMU YA TENDO N.K
@markson_beauty_pr Tunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa kiafya.
NB. Matokeo ni uhakika na garantii.
🍉🌿🍅🍍🍒🍉🍓🍅🍒
BIDHAA ZETU:-

1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @130,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200,000/=
(b)Vidonge @180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @150,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:-
(1)Mafuta @120,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka @130,000/=
(b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu hata kwa wenye kisukari @130,000/=
(C)Handsome up original @220,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @130,000/=
7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula @130,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @130,000/=
(b)Mkanda wa kawaida @100,000/=
(c)Micro-computer belt wa umeme @200,000/=
9.Kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @130,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @130,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120,000/=
12.Kurudisha usichana (bikra) @120,000/=

Wasiliana nasi :- (+255)
0767447444 au.
0714335378


TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.
👉Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu. ...............
Follow us on instagram @Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

DAKTARI Aeleza Chanzo Cha Wanaume wa DAR Kuwa na Upungufu wa Nguvu za Kiume...

$
0
0
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) amesema kuwa, asilimia 33 ya wanaume 672 wakazi wa Dar es Salaam wamebainika kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.

Daktari Pedro Pallangyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema utafiti huo umefanyika JKCI ambapo kati ya wanaume watatu, mmoja aligundulika kukosa nguvu za kiume.

Pallangyo alieleza kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wamebainika kuwa na shinikizo la damu na kisukari.

Utafiti huo ni miongoni mwa tafiti 16 zilizompa ushindi  wa tuzo ya Watafiti Vijana wa Afrika mwaka 2016/17 (Young Africa Research Awards 2017) zilizotolewa nchini Misri.

“Hali hii inaashiria kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara jambo ambalo linasababisha athari ya nguvu za kiume kuwa kubwa.”

Aidha, akielezea ufumbuzi wa tatizo, Pallangyo alisema, “Changamoto hivyo inaweza kutatuliwa iwapo jamii itakuwa na utaratibu ya kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema na kupata matibabu.”

Dk Pallangyo alisema kuwa, kati ya Machi mwaka jana hadi Machi mwaka huu alifanya tafiti hiyo katika ripoti ya muda mfupi na muda mrefu.

Dk. Pallangyo ambaye ni Mtanzania wa kwanza kupata tuzo hiyo anatarajia kukabidhiwa na Rais wa Misri, Abdi El-Fatah Al Sis mwezi  Agosti mwaka huu.

-MTANZANIA

KIMENUKA....Majambazi Wawili Wameuawa na Polisi Kibiti…Risasi zarindima

$
0
0
Kupitia Taarifa ya Habari kwenye Televisheni za Tanzania leo July 20, 2017 zipo taarifa nyingi zimeripotiwa na moja kubwa ni kuhusu mapambano ya Polisi dhidi ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika operesheni maalum Kibiti, Pwani.

Taarifa hiyo ambayo imerushwa na Kituo cha Channel 10 ambapo wakati wa zoezi la kuwasaka wahalifu likiendelea Kibiti leo imeripotiwa kuwa Jeshi la Polisi limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu hao.

Mkuu wa Operation hiyo Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabaas amesema tukio hilo limetokea katika eneo la Utende lililopo Kata ya Ukwiriri Wilayani Rufiji baada ya Polisi kuwatilia shaka watu watano na walipowafuatilia walikimbia na kuwashabulia Askari kwa risasi na katika majibizano Askari walifanikiwa kuwajeruhi wawili ambao walifariki njiani wakati wanapelekwa Hospital ya Taifa Muhimbili.
 ”Baada ya kuwasimamisha watu wale hawakusimama walikimbia na kisha kufyatua risasi hewani kuelekea walipokuwa Askari. Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi watuhumiwa wawili kati ya wale watano na wakati wanapelekwa Hospitali walipoteza maisha.” – Liberatus Sabaas.

VIDEO: “Wampeleke Mahakamani, Tutakutana Huko Huko” – Kibatala Baada ya Lissu Kukamatwa

$
0
0
Jana July 20 Mwanasheria, Mbunge wa CHADEMA na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika TLS, Tundu Lissu amekamatwa akiwa Airport Dar es Salaam akielekea Rwanda kwenye mkutano wa Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki.

Ayo TV na millardayo.com zimempata Wakili wake Peter Kibatala na amezungumzia tukio hilo
”Mimi sijaongea naye moja kwa moja kwa sababu simu zake ni ama zimezimika au zimezimwa lakini taarifa nilizopata kutoka kwa watu wake wakiwemo ambao wamemuacha Airport muda si mrefu na wengine ninaowaamini ni yes amekamatwa na anapelekwa Central Police Station.

“Kuna Wakili mwenzangu anaelekea huko kwenda kushughulikia Haki zake za kisheria na pengine kusisitiza kwamba apelekwe Mahakamani na sisi kama ni kweli amekamatwa rai yetu ni hiyo kama wamemkamata na waliomkamata wanaamini kwamba wana tuhuma dhidi yake wakamilishe taratibu zao mapema kama inavyowezekana wampeleke Mahakamani tukakutane naye huko.” – Peter Kibatala.
VIDEO:
Viewing all 104745 articles
Browse latest View live




Latest Images