Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Gari Inauzwa Kwa Bei Nafuu Piga Simu Kujua Bei na Kwa Maelewano

0
0

CAR TYPE: Daihatsu Atrai 7 AGE: SINCE AUGUST 2002, PLATE NO. T 793 BYK ENGINE CAPACITY: 1298CC WEIGHT: 2 TONES CAR STATE: VERY GOOD DOCUMENTATION: VERY VERY UP TO DATE MILEAGE: 175,000 FUEL CONSUMPTION: VERY GOOD STATE SEAT CAPACITY: 8 WHERE FOUND: KINONDONI DSM PRICE: 5.5 MILLION TSH PRICE DISCUSSION: YES CONTACT: 0719159214, 0716417688, 0784305199








Ndoa ya Flora Mbasha Chali..Flora Ahamia kwa Gwajima, Prado Ladaiwa Kuwa ni Chanzo

0
0
BAADA ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena inawezekana lakini ni kazi kubwa, Amani limefukunyua mazito

Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi.

Imeelezwa Flora na mumewe ambao walifunga ndoa Agosti 22, 2002 wamepita katika migogoro mizito lakini wawili hao walikuwa wakiyamaliza kifamilia hadi kufikia hili la hivi karibuni ndilo lililoziba mataumaini ya wawili hao kuishi kama mume na mke.

Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili hao kugombana ulichochewa na mwanamke mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa akikinzana na ushauri wa Mbasha mara kwa mara.
“Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili  na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana,” kilisema chanzo.

TUJIUNGE NA MBASHA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Emmanuel alizungumza na mwandishi wetu ambapo alikiri ndoa yake haina uhai tena na si rahisi kurejea katika hali ya kawaida licha ya kudai kuwa bado anampenda mkewe.
“Tulikuwa tunagombana sana na Flora lakini tulikuwa tukipatana ila mama… (anamtaja jina) alichangia ugomvi,

Flora naye alikuwa na nyendo zake mbaya, kuna wakati alikuwa anatoka kwenda gym (sehemu ya mazoezi) anachelewa kurudi ikafika wakati na nguvu ya ndugu wa mke ikawa kubwa kiasi cha kunizidi mimi na hapo ndipo mambo yalipofikia pabaya kabisa.”

FLORA ATIMKA NYUMBANI
Mbasha anaendelea: “Ugomvi ulizidi, ilifika wakati tulipishana kiasi cha yeye kuondoka nyumbani na kwenda kuishi katika nyumba ya wageni kwa miezi kadhaa wakati huo.

“Ndani ya ugomvi huo nilisikia mengi, baadhi ya watu wananiambia mke wangu anaonekana na Prado na mwanaume mwingine mwenye pesa, iliniuma sana ingawa sijawahi kumuona moja kwa moja,” alisema Emmanuel.

Kuhusu ugomvi huo, hivi karibuni Flora alikaririwa katika vyombo vya habari akisema hana tatizo na mumewe na ameshasamehe na kusahau yote yaliyopita hivyo ajitokeze tu ili akajibu mashitaka ya kudaiwa kubaka binti wa miaka 17 yaliyofunguliwa.

“Mimi sina tatizo kabisa na mume wangu, nimeshasamehe yote yaliyopita, kuhusu mashitaka ningeweza kuyafuta kama ningekuwa mimi ndiye niliyemshitaki,” alisema Flora.

FLORA ADAIWA KUHAMIA KWA GWAJIMA
Wakati gazeti hili likiendelea kusaka undani juu ya sakata hili, kuna chanzo kingine kilipenyeza data kuwa baada ya ugomvi kuwa mzito, Flora alihamia kwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar, Josephat Gwajima ambako ndiko alikuwa akisali kila Jumapili.

“Kwani nyinyi Global hamna habari? Flora amehamia kwa Gwajima Jumapili iliyopita, kwanza alihudhuria ibada jioni akaenda kuishi maana Gwajima ni mchungaji wake kwa sasa,” kilisema chanzo.

GWAJIMA ACHOMOA
Ili kupata mizani ya madai hayo, juzi Amani lilimpigia simu Mchungaji Gwajima na kumuuliza kama kweli Flora amehamia kwake kufuatia ugomvi kati yake na mumewe ambapo alikataa katakata.
“Flora hayupo hapa…mnataka niwaambiwe yuko hapa  halafu vyombo vya habari muanze kuandika vibaya? Hakuna kitu kama hicho,” alisema Gwajima.

KWA NINI CHALI?
Ndoa kuwa chali ni ile ambayo imeanguka lakini inaweza kusimama tena tofauti na ndoa kuvunjika. Global iliwahi kuandika NDOA YA THEA CHALI baadaye ikasimama tena. Thea ni msanii wa filamu alifunga ndoa na Michael Sangu ‘Mike’ ambaye pia ni mwigizaji.

Wakati Emmanuel akizungumza na mwandishi wetu, alikiri kuwa Flora ameshamgeuka na nguvu kubwa imemuingia ndani ya moyo wake hivyo kuna ugumu sana wa kurudiana.

“Flora ambaye nilitegemea awe msaada katika hili lakini amefikia steji ya kuacha kunisikiliza, anasema haniamini, kwamba ninaweza kumfanyia lolote, sasa si bora kama anataka tuachane kwa heri kuliko kuniundia zengwe ambalo linataka kunipeleka mimi jela?” alihoji Mbasha.

Kutokana na mvutano huo pamoja na kesi hiyo ya kudaiwa kubaka inayomwandana Mbasha ni dhahiri kwamba kila mmoja hana imani na mwenzake tena hivyo suala la wawili hao kuishi kama zamani linakuwa gumu kuliko ngamia kupenya kwenye  tundu la sindano.

Emmanuel Mbasha alishitakiwa katika Kituo cha Polisi cha Tabata Shule, Mei 30, mwaka huu kwa madai ya kumbaka shemejie.Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea hadi sasa shitaka ambalo mwenyewe amelikanusha.
GPL

Aunt Lulu Alia Kukosa Bwana wa Kizungu kutoka Thailand

0
0
Na Hamida Hassan

MKALI wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa anasikitika kukosa bwana aliyeahidiwa na marehemu Amina Ngaluma.

Akizungumza na paparazi wetu, Aunt Lulu alisema kabla marehemu Amina hajapatwa na mauti nchini Thailand, alimuahidi kumtafutia bwana nchini humo lakini mauti yalimkuta kabla hajamtimizia ahadi hiyo.

“We acha tu, aliniahidi kunitafutia mume baada ya kugundua nasumbuliwa na wanaume kila wakati lakini ndiyo hivyo tena Mungu akamchukua kabla hajanitimizia ahadi,” alisema Aunt Lulu.
Amina alifariki mwezi uliopita nchini humo ambapo chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa ni uvimbe kwenye kichwa.

Chaz Baba:Simwelewi Sajent Amegoma Kunipa Mwanangu Niliye zaa Naye

0
0
Na Musa Mateja
PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ amefunguka kuwa anatamani kuishi na mwanaye aliyezaa na mwigizaji Husna Idd ‘Sajent’ lakini mzazi mwenziye huyo amekuwa akimgomea.

Akizungumza na paparazi wetu, Chaz Baba alisema kabla hajaoa alikuwa akimg’ang’ania akae naye lakini alipooa, amegeuka na kukataa katakata.

“Kiukweli simuelewi kabisa Sajent maana katika hali na akili ya kawaida tu, sijaona mantiki ya kumkatalia mtoto wangu labda angeniambia kama mwanangu amekataa mwenyewe hapo kidogo nisingekuwa na swali,” alisema Chaz Baba.
Chaz Baba ambaye alikuwa akibanjuka na Sajent miaka ya nyuma, kwa sasa ni mume halali wa ndoa na bi dada anayefahamika kwa jina la Rehema.
GPL

Hii Kali:Kila Mtanzania Sasa Anadaiwa Sh 600,000

0
0
Wakati Serikali ikibanwa na wabunge kwa kushindwa kutekeleza Bajeti ya mwaka 2013/14 kutokana na kutegemea fedha za wahisani, Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara imesema deni la taifa limeongezeka kwa Sh8.2 trilioni kwa kipindi cha miezi saba tu.

Ilisema jana kuwa hadi Juni, mwaka jana deni hilo lilikuwa Sh21.2 trilioni lakini hadi Januari mwaka huu, deni hilo lilipaa hadi Sh29.4 trilioni na fedha hizo zimekopwa kwa ajili ya kuendeshea warsha, semina, safari, mafunzo na matengenezo ya magari.

Akiwasilisha taarifa ya kambi ya Upinzani, Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia alisema ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi atakuwa anadaiwa Sh600,000.

Kati ya Sh5.8trilioni za bajeti ya Wizara ya Fedha mwaka 2014/15, Sh4.3trilioni zimetengwa kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa

Akiwasilisha taarifa ya Kamati, Mwenyekiti wake, Luhaga Mpina alisema Sh24.18trilioni ni deni la Serikali, Sh3.75trilioni ni deni la sekta binafsi na Sh1.15trilioni ni deni la Benki Kuu Tanzania (BoT).

“Ongezeko hili la deni haliendi sambamba na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ujenzi wa miundombinu ya uchumi. Hali hii inajenga hofu kuwa huenda deni hili limekuwa ni uchochoro wa ubadhilifu wa fedha za umma,” alisema Mpina.

Alisema licha ya Serikali mara kadhaa kueleza kuwa deni hilo ni himilivu, kuna viashiria vinavyoonyesha kuelemewa kwa taifa na mzigo mkubwa wa madeni.

“Mfano ni mapato ya ndani yamezidiwa na matumizi ya kawaida hivyo kuifanya Serikali kukopa hata kwa ajili ya warsha, semina, safari, mafunzo na matengenezo ya magari,” alisema Mpina.

“Deni la Taifa sasa limefikia asilimia 47 ya Pato la Taifa na kwa kipimo cha bei ya sasa deni la taifa limefikia asilimia 24, huku deni la nje pekee likiwa ni asilimia 19” alisema Mpina na kuongeza:

“Licha ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kuahidi kwa muda mrefu kufanya ukaguzi maalumu wa deni la taifa, hadi sasa taarifa yake haijawasilishwa. Ni lini taarifa hiyo itawasilishwa bungeni ili kuwawezesha wananchi kufahamu undani wa jambo hili?” alihoji.

Kamati hiyo pia iliilipua Serikali kwa kuuza mashine za elekroniki (EFD), kati ya Sh600,000 hadi 700,000 kwa maelezo kuwa kiwango hicho ni kikubwa kwa mzunguko wa biashara ya mtaji wa Sh14 milioni kwa sababu mtaji wake hauzidi Sh5milioni.

Mpina alisema mashine hizo zinatakiwa kugawiwa bure kwa wafanyabiashara wenye kipato chini ya Sh40milioni na kufafanua kuwa chombo hicho chenye taarifa muhimu za mapato ya Serikali hakitakiwi kuuzwa na kufanyiwa matengenezo na mtu binafsi.

Kiwango cha Ujinga wa Watanzania Kitaliangamiza Taifa

0
0
Mwaka 1961-1964 tangu taifa la Tanganyika litoke kupata uhuru lilikuwa na watu milioni 10+, na 88% walikuwa ni wajinga sana, 10% walikuwa ni wajinga wastani wakati 1% walikuwa ni werevu, na 1% walikuwa ni werevu sana!

Kutoka 1965-1985 sasa tukiitwa Tanzania, taifa lilikuwa linakadiriwa kuwa na watu milioni 30+, na watu 78% walikuwa ni wajinga sana, 12% walikuwa ni wajinga wastani, wakati 7% walikuwa ni werevu, na 3% walikuwa ni werevu sana!

Mwaka 1985-2000 taifa likikadiriwa kuwa na watu milioni 40+, watu 68% walikuwa ni wajinga sana, 22% walikuwa ni wajinga wastani, wakati 8% walikuwa ni werevu, na 2% walikuwa ni werevu sana!

Mwaka 2000-2013 taifa likikadiriwa kuwa na watu milioni 44+ watu 76% walikuwa ni wajinga sana, 30% walikuwa ni wajinga wastani, wakati 5% walikuwa ni werevu, na 1% walikuwa ni werevu sana!

Sababu za kushuka kwa ongezeko la werevu na kupanda kwa ongezeko la wajinga miaka ya hivi karibuni kunatajwa kuwa kumechochewa na mfumo mbovu wa elimu nchini.

Sasa kwa wafanya siasa hii ni rahisi sana kwao kwakuwa haiwalazimu kutumia sheria ya MIMMK ambazo humuongoza mwanasiasa kuendesha siasa zake!

Taifa la wajinga hushangilia uovu na kuuchukia ukweli!
Yericko Nyerere Via JF

Hongera Mheshimiwa James Mbatia kwa kuwafundisha CHADEMA jinsi ya Kuandika Maoni ya Upinzani

0
0

Wadau, 

Natumai kuwa wengi wetu tumemsikiliza Mheshimiwa James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI na Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha wakati akitoa maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2014/2015. 

Kwa wale waliosikiliza, kusoma au kuona maoni hayo ya Upinzani, watakubaliana nami kuwa yapo tofauti kabisa na maoni tuliyokuwa tumezoea kuyasikia kutoka Kambi ya Upinzani wakati huo ikiwa na wabunge wa CHADEMA pekee.

Hakika Mbatia amejitahidi kujenga hoja na kutoa ushauri stahiki kwa mustakabali mwema wa nchi hii.

Wengi walitegemea kuwa Mbatia atajikita kueleza au kulalamika juu ya masuala mbalimbali kama vile ESCROW Acount au hili sakata la UDA. Mbatia hakugusia kabisa masuala hayo kwa vile hayana tija katika ukuaji uchumi wa nchi yetu.

Pia Mbatia anajua kuwa kama kulikuwa na udhaifu wowote kwa siku za nyuma, hawezi kuwabebesha mzigo huo hawa vijana wachapakazi waliochaguliwa kuongoza wizara hiyo. 

Alichokifanya Mbatia ni kuwaonesha njia na si kuwakatisha tamaa kama walivyozoea kufanya CHADEMA.

Hebu tujiulize, hivi ile taarifa ya John Mnyika kwenye Wizara ya Nishati na madini ina tija gani kwa taifa?

Katumia dakika 25 kusoma introduction tu wakati James Mbatia katumia chini ya dakika 30 kuwasilisha maoni yake. 

Hakika Mbatia kawaonesha njia CHADEMA na hii inadhihirisha kuwa uwepo wake kwenye kambi ya upinzani utasaidia kuokoa Jahazi la CHADEMA lisizame japo uwezo huo najua hana. 

Atakachokifanya Mbatia ni kuokoa jahazi lake tu. kwani mpaka sasa Watanzania wenye akili timamu wanajua kuwa ndani ya CHADEMA hakuna upinzani wa dhati bali wamejaa walalamikaji na wanung'unikaji.

CHADEMA, alichokifanya Mbatia leo iwe fundisho kwenu katika kujitathmini upya juu ya mustakabali wenu kisiasa.

Mawaziri vivuli karibu wote ambao si wabunge wa CHADEMA wameandaa taarifa nzuri sana na zenye tija kwa taifa hii tofauti na za wabunge wa CHADEMA.

Huwezi kulinganisha taarifa za Sugu, Lema, Wenje, Msigwa na Mnyika na zile zilizoandaliwa na akina Mkosamali, Kafulila, Mbatia na Machali. 

Hakika kuna utofauti mkubwa na Watanzania wenye akili zao hawahitaji mikutano ya hadhara kupima juu ya jambo hilo. 

Nawashauri CHADEMA. Kujifunza si ujinga. Japo mmekaa miaka 3 kama kambi rasmi ya upinzani, mjifunze hiki kipindi cha miezi miwili mlichofanya kazi pamoja na akina Mbatia. Mnapojifunza hakika mnaangamia.

Najua kuna mizengwe inasukwa na baadhi yenu kwa kutaka kuwaandalia kashfa nzito akina Mbatia ili hatimaye kambi yenu ivunjike. Huo si ushindani wa kisiasa. Anayejua anajua tu. cha kufanya ni wewe kujifunza kutoka kwake

Nawasilisha.

Huyu ndiye binti anayedai kubakwa na mume wa Flora Mbasha

0
0
Huyu Ndio Msichana Ambaye Anahusika na Sakata linaloongelewa sana la Mume wa Flora Mbasha Kumbaka Shemeji yake...Basi huyu Ndio Shemeji Mwenyewe Wajameni
Angalia muonekano wake utapata maswali mengi.
Any Comment?

Fashion Police:Maimatha wa Jesse Punguza Kidogo Kope Hizo Too Much Artificial

0
0
Jamani kwenye Urembo Sikatai Kuna Kuweka Kope Bandia ili uzidi kuonekana mrembo zaidi , na Kuna Wataalamu wakikuwekea Kope Unapendeza na Wala mtu wa Kawaida Hawezi Jua kuwa Umeongezea Kope ...Kamera Ilimnasa Mwanadada huyo Hapo Juu kope Zimesimama Dede yaani hapo Hata mtoto Mdogo Anajua kuna kamchezo kamefanyika Kwenye Kope...Punguza Kidogo Bibie

Huu Ndio Mshahara Ambao Maximo Anataka Ili Kuja Kuifundisha Yanga

0
0
YANGA chini ya Mwenyekiti wake, Yusuf Manji inataka kuonyesha kwamba ina nguvu na jeuri ya kufanya chochote kile inachotaka kwa vitendo ndani na nje ya ardhi ya Tanzania.

Mbrazil Marcio Maximo, amewaambia kwamba wakimpa mkataba watafurahia wenyewe lakini akawapa na masharti matatu ambayo yanahitaji kuvunja benki ila wametikisa kichwa wakamwambia haina noma.

Manji amewaambia Yanga kwamba wako kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na bosi huyo wa zamani wa Stars na atatua nchini kwavile ana hadhi ya Yanga.

Ujio wa kocha huyo unaonekana kuwashtua mastaa kadhaa wa Yanga hususani wazalendo kwani kocha huyo huwa hapendi masihara na ni mwepesi kufanya uamuzi mgumu kama kumsweka mtu benchi msimu mzima.

Habari za ndani ya Yanga zinasema kwamba kwanza, kocha huyo amewaambia viongozi anataka kuja na msaidizi wake ambaye ni mtaalam wa viungo lakini mabosi wa timu hiyo hajakubaliana na hilo wakitaka afanye kazi na mzalendo Boniface Mkwasa.

Kocha huyo aliwahi kufanya hivyo wakati akitua nchini miaka kadhaa iliyopita wakati aloipokabidhiwa Taifa Stars. Alikuja nchini na Itamar Amorim ambaye alikuwa mtalaam wa viungo kwa kikosi hicho.

Taarifa kutoka ndani ya kamati ambayo ipo chini ya Manji ikishugulikia ujio wa kocha huyo zinasema kwamba Maximo pia amependekeza msaidizi wake huyo alipwe mshahara wa Dola 4,000 ( Sh6.4milioni) kwa mwezi jambo ambalo viongozi hao wanadai utakuwa mzigo mkubwa Yanga.

Sharti jingine la kocha huyo ni kutaka alipwe mshahara wa dola 15000 (Sh24milioni) ambalo bado Yanga wanalifanyia kazi na unaeza kupungua kidogo. Lakini pia anataka apewe nyumba ya gharama kama ambayo alikuwa akilipiwa na serikali wakati akiifundisha Stars ambapo kidogo hapo Yanga wameona wanaweza kutafuta kutokana kuwa na chaguo la nyumba nyingi nzuri.

Lakini Maximo pia ametaka apewe gari nzuri ya kisasa atakayoitumia katika kazi zake ambapo tayari Yanga wamemwambia watampa Prado la kisasa.

“Msaidizi wake atakuwa na kazi ya kushughulikia mazoezi ya viungo ni jambo zuri lakini ni gharama sana ukijumlisha na gharama zake ambazo tutampa kocha mkuu, tunataka kumwambia amuache kwanza aje afanye kazi na Mkwasa,”alisema bosi huyo..

Kila Anayenitongoza Namwona Hafai

0
0
Naamini wote mu wazima wa afya.
kama kichwa kinavojieleza hapo juu naombeni ushauri wenu nifanye nini coz kila anayenitongoza namuona hafai hata kama ni mtu mwenye hela zake.

Mimi huwa nina tabia ya kuangalia sana tabia ya mtu sasa kila anayenifuata naona hana vigezo na wengi nawaona wananitamani tu.

Hii hali inanitesa sana kwamaana najikuta wanaonifuata ni wengi lakini bado upweke unanitesa.

Mawazo yako yatakayojenga please.

Namsubiri Kwa Hamu Maximo Yanga Afufue Vipaji Vilivyopotea

0
0
Na Baraka Mbolembole
MARCIO MAXIMO alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa muda wa miaka minne. Kuanzia, juni, 2006 hadi juni, 2010 kocha huyo raia wa Brazil alifanikiwa kusaidia, Stars kufuzu kwa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN 2009. Zaidi ya hapo alijitahidi kila awezalo kuisaidia, Stars kupiga hatua lakini mwishowe akaondoka baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
Japokuwa alionesha dalili ya kutaka kuendelea na kazi hiyo nchini, mashabiki, wadau na baadae, TFF, walihitaji kuona mabadiliko yakifanyika kwa kuamini kuwa hakuwa na kipya na uwezo wake wa kuisogeza mbele kisoka, Tanzania ulifikia mwisho baada ya kushindwa kuisaidia, Stars kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika na michuano ya kombe la dunia, mwaka 2010..
Miaka miwili iliyopita, Mwalimu huyo alihusishwa na kujiunga na Yanga kama mbadala wa kocha, Kostadin Papic lakini nafasi hiyo ikaangukia kwa Mbelgiji, Tom Saintfiet ambaye alikuja kutimuliwa ndani ya miezi miwili kufuatia kujibizana maneno na mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji. Yanga ilimchukua kocha raia wa Uholanzi, Ernie Brandts ambaye alitimuliwa disemba mwaka jana baada ya Yanga kuchapwa magoli 3-1 na mahasimu wao Simba katika mchezo wa hisani.
Brandts aliondolewa siku chache baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili baada ya kuingoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2012/13. Yanga walimchukua, Hans Van der Pluijm na kumpatia mkataba wa muda mfupi wa miezi sita na kocha, Muholanzi tayari ameingia mkataba klabu ya Al Shoalah ya Saudi Arabia hivyo timu hiyo ipo katika mazungumzo na kocha, Maximo kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kilichopoteza ubingwa wa ligi kuu msimu uliomalizika kwa Azam FC kutwaa taji lao la kwanza.
JE, MAXIMO ATAITULIZA YANGA NA TIMUATIMU YA MAKOCHA…
Katika nchi ambayo mashabiki wa soka si wavumilivu hata pale timu inapopoteza mchezo mmoja kwa mwaka, anaweza kupata wakati mgumu. Kama mashabiki wa Yanga walikuwa sehemu ya mashabiki wa soka nchini waliotaka kuona, Mbrazil huyo akiondoshwa, Stars miaka minne iliyopita, Maximo atapambana nao klabuni. Wakati akiwa kocha wa Stars iliwahi kusema kuwa ana mapenzi na Yanga kwa kuwa huvaa jezi zenye rangi wanayoitumia timu yao ya Taifa.
Ukitoa yote hayo, kufanya kazi na viongozi, wachezaji, na mashabiki wanaotaka matokeo wakati wote wa klabu ya Yanga ni kazi nyingine inayohitaji moyo wa uvumilivu, busara na kuwa tayari kupambana na vyombo vya habari ambavyo havitaacha kuandika kuhusu mambo ya ndani ya klabu. Brandts aliondolewa japo alipoteza mchezo mmoja tu wa kimashindano. Kuifunga mara kwa mara, Simba ni kigezo ambacho kitawekwa mstali wa mbele kupima kama anaweza kufuta ‘ timua timua’ ya makocha ndani ya timu ya Yanga. Kigezo hicho kinaweza kisiwe tatizokama atakuwa ngangari na katika kuelezea sababu za kimpira  zaidi mara baada ya matokeo mabaya uwanjani
. Kama mashabiki huwa wanasema kuwa wachezaji baadhi huuza mechi wakati wa mipambano ya watani wa jadi katika soka la Tanzania, basi, makocha wa timu za Yanga na Simba wasingekuwa wanatimuliwa. Hivyo, pamoja na ubora wake wote unatajwa kuwa utaipaisha Yanga endapo akipewa kazi ya ukocha kama inavyotarajiwa, Maximo anatakiwa kujipanga kuwashinda mahasimu wao kila wanapokutana.
Wachezaji hutolewa ‘ kafara’ tu pale mambo yanapokwenda mrama kwa kuwa hakuna mchezaji yoyote aliyetiwa hatiani kwa tuhuma hizo za uuzwaji wa michezo ya Simba na Yanga. Anaweza kutumia uzoefu wake wa kuifundisha, Stars kwa miaka minne na kuisaidia, Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho barani baadae mwaka ujao. Atakumbana na wachezaji ambao aliwatuhumu ni watovu wa nidhamu wakati akitanga kikosi cha Stars. Juma Kaseja, Athumani Idd, Kelvin Yondan ila anaweza kumaliza tofauti na nyota hao na kutengeneza timu kabambe ambayo ina wachapa kazi na wachezaji wenye vipaji vya haliya juu.
Ni mtaalamu wa kutengeneza timu katika kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza, mbinu hizo zilimfanya kuwa tishio kwa timu nyingi kubwa za Afrika  wakati zikija nchini kucheza na Stars wakati akiwa kocha mkuu wa kikosi hicho. Endapo atatua klabuni hapo itakuwa faraja kwa mshambuliaji Jerry Tegete ambaye pamoja na makali yake ya ufungaji mchezaji huyo amepoteza kujiamini na kufanya vibaya uwanjani, Maximo ndiye muibua Tegete wakati akiwa sekondari ya Makongo kwa kumuita katika kikosi cha Stars akiwa hana timu ya ligi kuu.
Atakutana na vipaji vya ufungaji kama Hamis Kizza,  Said Bahanunzi, Hussein Javu ambao wanaweza kumaliza tatizo lililomuondoa Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa kocha wa Stars. Maximo alishuhudia Stars ikiosa magoli ya wazi  katika mechi muhimu hivyo inawezekana   kufanya kwake kazi katika klabu Brazil kwa miaka mine kunaweza kuwa kumempatia tiba ya tatizo hilo. Kama akifanikiwa kuifanya Yanga ifunge magoli bila shaka timua timua  ya makocha itapungua, ila akishindwa hakutakuwa na kitu kigeni akioneshwa mlango wa kutokea. Namsuribi kwa hamu, Marcio Maximo afufue kipaji cha Tegete na vipaji vingene vilivyosahulika ndani ya Yanga.
0714 08 43 08

Maskini Penny Yupo Hoi Kitandani Apumulia Mashine

0
0
Ni siku ya tatu sasa yule mtangazaji wa Radio mpya ya EFM na ex-girfiend wa Diamond Platnumz , DJ Penny akisumbuliwa na ugonjwa wa Asthma  na hali yake kwasasa bado haijawa nzuri.

Kwasasa penny anasaidiwa kupumua kwa mashine kutokana na Asthma hiyo kufika pabaya.

Mungu amsaidie DJ Penny aweze kupona mapema na arudi akiwa mwenye  afya njema
CREDIT : VIBE

BET Watajuta Kumtaja Diamond Kwenye Tuzo..Wabongo Wazishambulia Kurasa zao za Facebook na Instagram kwa Comments za Kiswahili

0
0
Hii sasa ni shida!!! Huenda wafanyakazi wa kituo cha BET, kama hawatakuwa wanajichekea tu kwa jinsi wabongo walivyo na fujo kwenye ukurasa wao wa Facebook na Instagram, basi watakuwa wanajuta kumtaja kwenye tuzo hizo.Katika utaratibu wake wa kuweka picha za nominees mbalimbali wa tuzo hizo kupitia mitandao ya Instagram na Facebook, BET wamejikuta wakishangaa na namna ambavyo jina la Diamond limekuwa likitajwa katika asilimia kubwa ya comments hata kwenye picha zisizomhusu staa huyo wa Tanzania.

Hiyo ni kutokana na kampeni iliyoanzishwa na mashabiki wa muimbaji huyo wanaoitaka BET ifahamu nguvu yake. Kwa wengine comments hizo zimeanza kuwa kero kwenye ukurasa huo japo BET wanaweza kufurahia jambo moja kubwa – wamepata followers wengi kutoka Tanzania.

Pamoja na kwamba comments hizo zinaweza zisiwe na mchango wowote wa kumfanya ashinde, kituo hicho cha BET kinapata ujumbe muhimu kuhusiana na kukubalika kwake Afrika Mashariki. Ujumbe huo unaweza kuwa mwanzo mwingine wa Diamond kupata airtime kwenye kituo hicho kwa video zake zinazokuja hasa ya wimbo aliomshirikisha Iyanya ambayo video yake ilifanyika nchini Uingereza mwezi uliopita.

Ujumbe mwingine jumuiya ya muziki wa kimataifa inaoupata kupitia mashambulizi hayo ya mashabiki wa Diamond, ni ukubwa na ushawishi alionao hitmaker huyo wa My Number 1.

Haya ni baadhi ya maoni ya wabongo kwenye picha za Instagram za mastaa wengine yanayomhusu Diamond.

jandareal
Yupo kwenye best actor pia? Bet watakuwa wanajichekea tu

twissyben
Wabongo nomaaa kila sehemu ni sisi,,,wataisoma D’s tym iwe movie ,music ni #diamondplatnumz

nico_agust
@twissyben shida tupu!! hapa lazma watuone kuwa tuna uelewa mdogo wa mambo haya!!

jusseee
Hahhah siwanesema akuna kura bat mtu akiongelewa Sana ila sisi noma ata kwa washereheshaji atujali no daimondplatnomz tu ata kwenye movie ivyo ivyo kweli watatupa tu tuzo na kutujua atujielewi. Unazani uwongo kweli wataangalia kahistoria ketu watatupa tu tuzo ole wao wachakachue tunamtuma kikwete nikuandamana mwanza mwisho kwa hali hii kila kit BMT ni diamond tu watunyime tuzo sasa waone

salmaasaidy
Hahahahahahaha nyamani mi nacheka sana kila post @diamondplatnumz .nimecheka kweli @jusseee

janeelingerie
Hahahaaaaaa uuuuwiii nacheka balaa daaahh kweli watu hawaelewi daaahh ila @diamondplatnumz uko juu hata hawa jamaa wataashangaa @wemasepetu

berthamagodi
Kashapata umaarufu jamaa mana kila mtu atataka amjue mana kachafua mbaya wabongo tumetisha aiseee

jandareal
Dah lkn licha ya kupata umaarufu pia itaonyesha ni kiasi gan wabongo tunaakili nzito. Aliyetoa instruction kufanya haya alikosea sana, sema bado tunahitaji elimu juu ya hili,jishtukien had movie mnacoment diamondplatnumz @diamondplatnumz tolea ufafanuzi wa hili

berthamagodi
Shida tunakurupuka hao wahusika walito bio tuingie kupiga kura kumbe kituo cha redio pia kule diom kashine mbaya sasa uku ndo kafunga kaz marekan nzima watakua wanashangaaa. Bongo noma sana

rehemaessy
Wapenzi wa dai kuweni waelewa jazeni ktk picha ya dai sio kila picha mnatuzalilisha wabongo inaonekana hatujui kusoma @desmondmshana @thatgud_girl_g @mnayanda waelewesheni na wenzenu

telhom
Guys nendeni kwa picha ya Diamond ndo mukaandike jina lake la hasha mkiandika hapa nikujisumbua hii si picha yake so hawatoihesabu please go back to @betawards then chagua jina la @diamondplatnumz ndo uandike jina lake mbona mko wagumu kuelewa jamani

nakupendapia
Tanzanians I love the way you guys got @diamondplatnumz back. But na hope mnavote kwenye bet website coz the kelele here doesn’t really count.

magazinequeendrika
Y’all. There is nothing you can say to convince BET to get this man to perform. They made this decision months ago, so stop trying!!!!!

Katika hatua nyingine, kituo cha redio cha Kenya cha Home Boyz Radio jana kilitaka kujua muziki wa nani kati ya Diamond na Davido unaopendwa zaidi na Wakenya. Tweets hizi zinaongea zenyewe.
Bongo5

Mwanzilishi wa Instagram Ngangari, Awashushia Rungu Wanaoweka Picha za Utupu

0
0
Mtandao wa kijamii wa Instagram umezidi kuwa maarufu kutokana na jinsi ambavyo unampa nafasi mtumiaji kuionesha dunia taswira yake binafsi au hata kuhusu hisia zake.

Hata hivyo watu mbalimbali wamekuwa wakipost picha tata za nusu utupu na nyingine zikipitiliza kitu ambacho mwanzilishi wa Instagram, Kevin Systrom hakiafiki kabisa na amekivalia njuga kukikomesha.

Akiongea na mtandao wa BBC Newbeat, Kevin amesema kampuni yake imepiga marufuku na haitaruhusu picha za aina hiyo kwa kuwa wanahitaji mtandao huo kuwa salama na rafiki kwa watu wa lika zote (wakubwa na watoto).

Kevin amefanya mahojiano na mtandao huo baada ya Scout Wills,  mtoto wa kike wa mcheza filamu maarufu, Bruce Wills kupinga hatua ya Instagram kuondoa picha yake aliyo aliyoweka huku matiti yakiwa wazi.

Rihanna ambaye aliwahi kupewa onyo na Instagram kwa picha alizokuwa anaweka, alimsapoti Scout kabla hajaamua kujitoa siku iliyofuata.

Mchumba wa Kwanza wa Flora Mbasha Afunguka, Kumbe Nae Alibambikiziwa Skendo

0
0
Flora Mbasha alikuwa na mchumba anaitwa Imma Lushanga Ambae Baba yake ni Mmiliki wa Mabasi ya Lushanga huko Mwanza kabla hajaja Dar akiwa amechumbiwa tayari Wiki mbili kabla ya kufunga ndoa Flora akapata safari ya kwenda UK ambako wenyeji wake walimshauri kwamba kwa uzuri wake atapata Mume mzungu mwenye pesa kuliko Imma yule wa Mwanza. Ili kumkimbia Imma Flora na familia yake wakamtengenezea ishu Imma mchumba wake kwamba ana Ukimwi kwa hiyo Flora hawezi kuolewa naye, Hii Nakumbuka ilikuwa Stori kubwa Sana Mwanza Kipindi Hicho zaidi ya Miaka kama Kumi na nne iliyopita mpaka leo Imma hajawahi kuoa tena na wala hana hamu 

Huta Msikia Tena Dinna Marios wa Clouds FM Kwenye Kipindi cha Leo Tena, Awaaga Mashabiki Wake

0
0
Wapenzi wangu najua kila kitu kilianzia kwenye leo tena hadi wewe kuamua kufatilia kazi zangu na kila kitu ninachofanya.Ila wanasema safari moja huanzisha nyingine ndivyo ilivyo kwangu.
Baada ya muda wa miaka nane kuongoza leo tena na mie kuilea kwa kila hali kuhakikisha inakuwepo.Leo tena ilikuwa maisha yangu nikilala,nikiamka,nikiwa barabarani ili mradi niwe na jambo kwa msikilizaji wangu kila siku.Iwe ni segment mpya,topic,wimbo,jingle,yaani chochote ambacho naona kitanogesha kipindi.
Nilichukua likizo ya martenity na niliporejea nikaambiwa dada tunakuhamishia sehemu nyingine,TV.Daah haikuwa kazi rahisi kukubali na kuipokea niliona daah itakuwaje jamani mbona leo tena ndio kila kitu kwangu.
Nikaelezwa vile ofisi ina malengo makubwa na kipindi kipya nitakachoanzisha ambayo siwezi kuyaanika hapa lol basi kidogo kidogo nikaanza kuelewa somo na sasa nipo tayari.Kuna wale ambao bado mnaendelea kuulizia kwa nini hamnisikii ukweli ndio huo kwa sasa sipo tena kwenye leo tena najiandaa na kipindi changu kipya cha tv kitakachoruka clouds tv hapo baadae.
Japo nina changamoto ya mwili mmenenepa mie ila kila kitu kitajiset mbele ya safati.Nikiwa najiandaa na kipindi kipya pia najiaandaa na ule utaratibu wangu wa kusaidia watoto yatima kupitia dada dina cares ambayo itakuwa ni mwezi ujao.
Najua tayari nina mawazo yangu ya nini nitafanya kwenye hicho kipindi lakini pia naomba nikuulize.Ungependa kuona nini kwenye kipindi changu cha tv?

PICHA za Capt. Komba zenye Utata Zasambazwa Kwenye Mitandao ya Kijamii!

0
0

Picha zinazomwonyesha mh. Captain John Komba zenye mapozi tofauti na mabinti tofauti zimeanza kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania. 

Kuna picha nyingine nyingi lakini kutokana na maadili hatuwezi kuziweka hadharani; hizi ni baadhi tu

UTETEZI WA KOMBA:
Kuhusiana na hizi picha 2 zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuznia asubuhi ya leo, zikimuonyesha Mheshimiwa Mbunge huyo wa CCM Kapteni John Komba akiwa kwenye mahaba na Mwanadada mmoja anayeishi Kinondoni. 

Mbunge huyo amesema kwamba picha hizi zimetengenezwa na maadui wake wa kisiasa na kwamba yeye sio Kiongozi wa hovyo hovyo namna hiyo. 

Kapteni Komba amesema kwamba anawakaribisha wataalamu wa Picha na Mitandao kutihibitisha ukweli wa picha hizo zinazoonyesha Mwana-Dada akiwa na kipande cha khanga tu huku Mbunge huyo akiwa pembeni yake akionyesha kutokuwepo kabisa kwenye Mahaba yanayotakiwa kuwa yanaendelea baina yao. 

Mbunge huyo ameuliza zaidi iweje awe kwenye mapenzi kama picha zinavyo onyesha halafu awe na nguo zake zote huku msichana akiwa na khanga tu? 

Kapteni Komba amesema kwamba kama kweli Taifa hili limefikia hapa pa kuchafuana namna hii kisa mitizamo tofauti ya kisiasa ya namna ya kuongoza Taifa letu basi kama Taifa tumefikia pabaya sana. 

Mbunge huyo amemalizia kwa kusema kwamba wale wote wanaomuamini kama Kiongozi shupavu wa Taifa, wasikatishwe tamaa na wajinga wachache wenye mawazo ya kitumwa ambao wanadhani wanaweza kummaliza kisiasa kwa kumtengenezea picha chafu kama hizi picha 2 za leo!
Source:JF

Sura Mpya ya Sakata la Uda, Kuna Mchezo Mchafu Kila Kona

0
0
Sakata la nani mmiliki halali wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), limeendelea kuchukua sura mpya. Wakati Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu akitoa tuhuma kwamba limeuzwa kinyemela, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Simon Group, Robert Kisena ameibuka na kudai kuwa halikuwahi kuuzwa.

Juzi, akichangia mjadala wa Bajeti wa Wizara ya Fedha, Mtemvu alisema kulifanyika ujanjaujanja kati ya Simon Group na Meya wa Jiji, Didas Masaburi kukopa benki na taasisi nyingine kwa ajili ya kununua kampuni hiyo.

Mtemvu alisema baada ya Simon Group kuuziwa Uda kwa bei poa, wahusika walishindwa kulipa fedha hizo ndipo (wadai) walipokwenda mahakamani na kutaka walipwe chao.

Alisema baada ya kampuni na benki walizokopa kushinda kesi mahakamani, kampuni moja ya udalali ilipewa kazi ya kuipiga mnada depo ya Uda na Februari 23, ilinunuliwa na Jazeera kwa Sh12bilioni.

Jana, Mtemvu alisema: “Tunaambiwa kulikuwa na zuio, hapa tunataka kujua, kwanza huyu aliyeweka hati za Uda kwa zuio isipigwe mnada... utaratibu uliotumika kuiuza Uda, hapa kuna mchezo mchafu umefanyika, iweje mambo yafanyike bila wadau, wahusika wa mkoa kushirikishwa?”

Alisema Uda haiwezi kuuzwa kwa bei chee ya Sh280 milioni... “Ina viwanja Stesheni, ina nyumba Msasani, Chang’ombe, Ilala Sharif Shamba, Kijitonyama, Upanga hivi vyote ni zaidi ya Sh280 milioni.”

Katika maelezo yake bungeni juzi, Mtemvu alisema wabunge wa Dar es Salaam hawakatai kubinafsishwa kwa Uda ila wanataka uhalali na haki katika ubinafsishaji huo.

Kisena

Akizungumza jana, Kisena alisema Uda haijauzwa na hawana mpango wa kuiuza na akahusisha tuhuma hizo na mkakati mbaya unaofanywa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya shirika hilo.

“Mimi ndiyo kwanza nasikia habari hizo eti Uda imeuzwa kwa Kampuni ya Jazeera… sijui kwa nani… huo ni uzushi.

Nenda kwa Mtemvu akupe document (nyaraka) za uuzwaji wa Uda… akwambie iliuzwa lini na kwa sababu zipi na kama iliuzwa kwa madeni ni benki gani inadai ili uweze kufuatilia na kuuambia umma ukweli.”

“Watu wote watambue kuwa Uda inamilikiwa na watu wawili: Simon Group na Serikali kupitia Msajili wa Hazina na hakuna mmiliki mwingine na halijauzwa. Hii kampuni ni kubwa sana hivi iuzwe bila waandishi wa habari na umma kujua na mnada hutangazwa siku 14 kabla… yaani siku zote zipite watu wasijue?” alihoji Kisena.

Brela

wakati mvutano huo ukiendelea, Wakala wa Usajili na Utoaji wa Leseni za Biashara (Brela), umesema hauna taarifa zozote za kampuni hiyo kuuzwa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyus alisema jana kuwa ofisi yake haina nyaraka zozote zilikuwa zikionyesha Uda kuwa iliuzwa kwa Kampuni ya Jazeera.

“Tulisikia taarifa hizo lakini hatukupata document (nyaraka) zozote zinazothibitisha jambo hilo. Nimewaomba maofisa wangu waendelee kufutilia suala hilo na kama kuna chochote tutawajulisha,” alisema Kanyus.

Sakata la Uda liliibuka tena juzi kwa Mtemvu na Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Kapuya kuchafua hali ya hewa bungeni kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa anahongwa kutetea ufisadi katika shirika hilo.

Mvutano huo umeibuka wakati Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge ikiwa tayari imemhoji, Kisena baada ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika kusema aliingilia uhuru wa Bunge kuhusu mgogoro wa uwekezaji katika shirika hilo.

Juzi bungeni

Juzi bungeni, Mtemvu alisema: “Kwanza niseme kitu kimoja kibaya sana, humu ndani kuna mjumbe wa Bodi ya Uda (Profesa Kapuya), alikuwa akizunguka sana humu ndani (ndani ya Bunge) huku akiwaona wa wabunge kitendo hicho si kizuri.”

Alisema kuwa mwekezaji huyo wa Uda ameliuza shirika hilo kwa Sh280 milioni na kuhoji kama kiasi hicho cha fedha ni hadhi ya Uda na kuwa mwekezaji huyo hakukabidhiwa shirika hilo na vikao halali vya jiji la Dar es Salaam, bali na Meya wa Jiji.

“Tunapoongea tusiangalie sambusa za Dodoma Hotel, tuangalie uasilia wa jambo, hivi tunauza mali ya Serikali bila Baraza la Mawaziri kujua?” alihoji.

Mtemvu alikatishwa na taarifa kutoka kwa Profesa Kapuya ambaye alisema si haramu kwa mbunge kuwa mwekezaji.

“Sera inaruhusu kwa mbunge kuwa mfanyabiashara. Afadhali mimi nimezunguka kuona watu kuliko anayezunguka kwa madhumuni ya kurudisha imprest (masurufu),” alisema Profesa Kapuya.
“Na aliyezungumza ni mmojawapo (Mtemvu)… hakuna mali ya Serikali iliyouzwa bila idhini ya Baraza la Mawaziri, zilizouzwa ni hisa za jiji ambazo yeye alikuwemo katika kikao (Mtemvu)”alisema.

Imeandikwa na Fidelis Butahe, Sharon Sauwa, Habel Chidawali (Dodoma) na Nuzulack 

Daktari wa Watoto Pacha kwenda Mbeya Baada ya Utumbo wa Mmoja Kutoka Nje

0
0
Daktari aliyewapokea watoto pacha waliokuwa wameungana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwapeleka India kufanyiwa upasuaji, Zaituni Bokhary anatarajia kuwasili nchini leo akitokea masomoni Misri na kwenda Mbeya kuwajulia hali watoto hao.

Pacha hao, Elikana na Eliud walizaliwa Februari 20 mwaka jana katika Hospitali ya Wilaya ya Uyole kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na baadaye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuzaliwa wakiwa wameungana kiunoni.

Akizungumza kwa uchungu baada ya kusikia taarifa ya kuzorota kwa afya ya mtoto Eliud, daktari Bokhary ambaye yupo masomoni nchini Misri alisema: “Usinilize jamani naona uchungu, naomba tushauriane nini cha kufanya...yaani hadi tumbo linaniuma.

“Roho inaniuma sana kusikia utumbo wa Eliud uko nje, ingekuwa siyo shule ningekaa nao hadi wapone kabisa,” alisema Bokhary, ambaye alisisitiza kwenda Mbeya kuwaona watoto hao.

Afya ya Eliud yazorota

Hali ya mtoto Eliud inazidi kuwa mbaya kutokana na sehemu kubwa ya utumbo wake mpana unaotumika kutolea haja kubwa kutoka nje hali inayomfanya kudhoofu kiafya.

Baba mzazi wa watoto hao, mkazi wa Kasumulu Kyela, Eric Mwakyusa alisema jana kuwa hali ya mtoto wake inazidi kumchanganya kutokana na kuzidi kubadilika kila wakati.

Hivi karibuni alisema baada ya hali ya mtoto huyo kubadilika alimpeleka Hospitali ya Wilaya ya Kyela ambako daktari aliyemwona alishauri mtoto huyo asubiri hadi atakapokwenda India, Agosti mwaka huu. Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Festo Dugange aliliambia gazeti hili kuwa hajawahi kusikia wala kumwona mtoto aliyetoka utumbo hospitalini hapo.

Wakati huohuo, baba wa watoto hao, Mwakyusa amepewa msaada wa pikipiki na msamaria mwema ili kukidhi maisha yake.

Mwakyusa amewashukuru wasamaria mbalimbali wanaomsaidia kwa njia tofauti ikiwemo wasamaria waliompatia pikipiki ili afanye kazi ya kubeba abiria na mapato yake yatumike kuboresha maisha ya familia yake.

‘’Nawashukuru waandishi wa Mwananchi kwa kuandika hali halisi ya watoto wangu, kwani jana nimepewa pikipiki na msamaria mwema wa jijini Dar es Salaam ambaye alipata taarifa za watoto wangu kupitia magazeti yenu’’, alisema.

Alisema kwa kipindi kirefu alikuwa akiendesha pikipiki ya mtu ambaye alikuwa akipewa Sh8,000 kila siku na yeye kubaki na kati ya Sh1,000 au 2,000 kwa siku ambazo ndizo zilikuwa zikitumika kuwahudumia watoto na familia nzima.
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images