Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

VIDEO Jinsi Zitto Kabwe Alivyokutana Live Bila Chenga na Rais Magufuli na Alichoongea

0
0
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia chama cha ACT Wazalendo alipata nafasi ya kuongea mbele ya Rais Magufuli aliyekua kwenye mkoa wa Kigoma kwa ziara.

Zitto Kabwe mbele ya Rais Magufuli alisema “Mh. Rais mwenyewe ulishuhudia watu walivyokua barabarani kuanzia njia panda ya Mwandiga mpaka unaingia IKULU ndogo, watu wa Kigoma wanataka maendeleo na wewe unatuletea maendeleo ndio maana wanakupenda”

“Mh. Rais jambo moja tu kwamba mradi huu ni kweli umechelewa lakini toka umeingia madarakani, wizara yako, wizara ya maji, Waziri na Watendaji wa wizara wamefanya kazi kubwa sana kuhakikisha kwamba tunauokoa huu mradi”
VIDEO:

Povu Zito Kutoka Kwa Mama Ashura wa Timamu Comedy Akidai Kuwa KIBA Anasafiria Nyota ya Diamond

0
0
Kwa upande wangu napinga kabisa kwa sababu kiba kawepo kitambo kwenye game kipindi iko domo anaonsha vyombo kwa kina Bob junior. Sasa uyu anapodai kuwa kiba anamtegemea mond ili avume nashindwa kumwelewa kabisa, nahisi ni mtafuta kiki tu au we Mdau Unaonaje?


TAZAMA VIDEO:

Ben Saanane Amezimika Kama Moto wa Kibatari, Nobody Cares. Binadamu Wanasahau Haraka Sana

0
0
Nilikuwa mara nyingi sana najaribu kufuatilia maandishi ya mmoja ya waandishi waliopata kutokea kusimamia walichoamini haijalishi kina athari au ukweli kiasi gani. Ben Saanane alikuwa na kitu ana kiamini. Alisimamia hicho. Dunia ya leo ni ngumu sana kupata watu wenye kitu wanachoamini zaidi ya vyeo,madaraka na pesa ni ngumu sana.

Ben Saanane sikuwa nakubaliana na kila alichoandika. kuna mengine nlikuwa napingana naye. lakini nliendelea kumheshimu kuwa alikuwa au ni kijana anayejua kutafuta support na kile anachoamini ili watu wengine pia wapate kukifahamu.

Naamini alikuwa Mwaminifu kwa mtu au watu fulan. Ben Saanane aliishi maisha yake akiamua kuwa mwanasiasa wa Aina yake ambaye hakuwa na jukwaa ambalo angesimama na kuongea kwa kutumia kipaza sauti.

Yeye alitumia kalamu.Iinawezekana kuna infos alikuwa anapewa au ni juhudi yake mwenyewe kuzitafuta. Lakini kinachonifanya leo hii niukumbushe umma habari hizi ni yu wapi Ben Saanane? Jitihada za kumtafuta zimeishia wapi? Je, watu wamekubali kuwa hayupo, amejificha au amepotea?

Tulimtia nguvu, tulimsifu kwa ujasili wake , leo haonekani mbona hatusaidii kumtafuta? hatukumbushi kumtafuta? Je ni kweli kuwa tumeshamwacha apotee?

Kwa namna hii ya usahaulifu, mnadhani tunaweza kuwa na mashujaa siku zijazo? ni nani anajua alipo ben saanane?

By Chizi Maarifa/Jamii Forums

JPM Amgeukua Sakaya wa CUF Adai Ana Damu ya CCM.....

0
0
Rais John Magufuli amemmwagia sifa mbunge wa jimbo la Kaliua - Tabora (CUF) Magdalena Sakaya kwa kupigania maendeleo ya wananchi na kusema kuwa, mwili na tabia yake ni za CUF lakini roho na damu yake ni ya CCM.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Julai 23 wakati wa ziara yake mkoani Tabora na kuwataka wabunge wa CCM kumpa ushirikiano anapofanya shughuli za maendeleo.
“Nimpongeze mbunge wa jimbo hili. Ingawa mwili na maneno na tabia zake ni CUF, lakini roho yake na damu ni CCM. Inawezakana hata siku zijazo akahamia CCM. Anajitahidi kuleta maendeleo ingawa hayachagui chama  ” amesema.

Aidha Dkt. Magufuli ameongeza kuwa "Ni mara 10 uwe na CUF, Chadema au NCCR anayefanya mambo ya CCM kuliko uwe na CCM anayefanya mambo ya vyama vingine. Hasara yake ni kubwa mno, mnafikiri ni mwenzenu wakati siyo mwenzenu, nani hayajui haya hata wakati wa kampeni yalitokea unafikiri siyajui,” amesema.

Pamoja na hayo amewataka wabunge wa CCM kumpatia ushirikiano mbunge huyo na kuwataka wasimbague kama yeye jinsi asivyowabagua.

Mwanasheria Tundu Lissu Amefikishwa Mahakama ya Kisutu.......

0
0
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu anapelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu muda huu....Taarifa Kamili tutawaletea Baadae

JE Dada Unahitaji Kuwa Mrembo na Mkaka Kuwa Mtanashati na Rijali.....Waona Hawa Black Beauty

0
0
BLACK BEAUTY COMPANY
je Dada unahitaji kuwa Mrembo na ule muonekano bomba wa kisuperstar👌🔥,kaka unahitaji kuwa mtanashati na mvuto zaidi wa KIUME?fika black beauty company utatimiza ndoto zako,hawakosei hata siku moja kwa products original na zenye matokeo yaharaka sana,bila madhara,ni kampuni yenye uzoefu wa hali ya juu sana🔥
1)kuongeza hips,makalio,mapaja@150000
(b)kuongeza hips,makalio,mapaja na miguu@200000/=
2)kuongeza miguu ,kuondoa vigimbi@120000/=
3)kuwa mweupe mwili mzima (Rangi moja)@150000/=
4)Kupungua mwili mzima@150000/=
5)kupunguza tumbo@100000/=
6)kupunguza au kuongeza matiti@100000/=
7)kukuza nywele@100000/=
8)kuondoa michirizi @100000
9)kuondoa madoa,mabaka na chunusi sugu@100000/=
10)kuongeza uume na nguvu za kiume@150000/=
Dawa zetu niuhakika sana100%na utaletewa popote ulipo,mikoani tunatuma,nje ya nchi tunatuma DHL,ofic zetu zipo kariakoo msimbazi police,🔥

karibuni kwa mawasiliano zaidi WhatsApp+255657778924, au call 0743534406

au unaweza kutufollow
👇👇👇👇👇👇
@black_beauty_company
@black_beauty_company
@black_beauty_company

Nedy Music na ishu ya Kutafutiwa Menejimenti Mpya na Ommy Dimpoz – Bongo5.com

0
0
Mkali wa wimbo ‘Dozee’ Nedy Music kutoka label ya PKP ya Ommy Dimpoz amefunguka kuwaweka sawa baadhi ya mashabiki wake ambao amedai hawajaelewa kauli aliyoitoa Ommy Dimpoz kuwa anatafutiwa management nyingine ya kusimamia kazi zake za kimuziki.




Dedy amedai kwa sasa bado yeye ni msanii wa PKP na muziki na ishu ya yeye kutafutiwa menejimenti mashabiki wameielewa vibaya.

“Watu walishindwa labda kujua nini alichokiongea nikiwa na maana kujua tafsiri ya neno lake kwasababu mswahili unaweza ukamuelekeza kitu yeye akatafsiri kivyake lakini yupo ambaye utamuelekeza kitu akajua maana yake maana yake ni kwamba kama itatokea Records Label kubwa kama aliyokuwepo yeye kwamba ikataka kufanya kazi kwasababu si tunafanya kazi na biashara kwahiyo kama kutakuwa na makubaliano ya kufanya kazi ya na biashara basi kutakuwa na utayari wa hivyo lakini si kwamba eti sasa hivi Nedy hayupo kwenye uongozi kwamba yupo ‘Yatima’ sio kweli,”

Jumatano iliyopita kupitia Clouds fm Boss wa PKP Ommy Dimpoz alisema “Ni vitu muhimu sana msanii kuwa na menejimenti, hata Nedy nimemtengenezea timu ambayo itakuwa inamsimamia mambo yake, kwa hiyo mimi sina he deck hivyo tunasimamia biashara yetu ya PKP kwa sababu tumewekeza pale, hakuna kilichoharibika, Kanye West alikuwa chini ya Jay Z lakini ana Good Music,”

Rapa Kutoka Marekani, Future Adata na Hip Hop ya Afrika...Afunguka Haya

0
0
Rapa kutoka Marekani, Future amesema Hip Hop inayofanywa na Wasanii wa Afrika ni nzuri kwani inawavutia wasanii wengi wakubwa wa Marekani kuisikiliza.

Future amesema Hip Hop ya Afrika inaelezea uhalisia wa Mazingira ina’sound nzuri pia hata midundo yake inavutia kuisikiliza.

“Hip Hop ya Afrika inasound vizuri sana inavutia kuisikiliza kwani imejaa ubunifu na huwa naingia studio kusikiliza midundo yake kuona kama ninaweza kufanya kitu“,amesema Future.

Hata hivyo, Rapa Future baada ya kunogewa na midundo ya kiafrika amethibitisha kuwa tayari amefanya kolabo na WizKid kutoka Nigeria .

Kisa cha Simba Kumtoa kwa Mkopo Manyika

0
0
RASMI, Simba SC imesema itamtoa kwa mkopo kipa wake, Peter Manyika kwenda timu ambayo atapata nafasi ya kucheza kama chaguo la kwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema leo kwamba, Manyika bado ana miaka miwili ya kuendelea kuwa mchezaji wa klabu hiyo kulingana na mkataba wake, lakini msimu ujao atacheza timu nyingine.

Lengo la Simba ni kuokoa kipaji cha kipa huyo, mtoto kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Manyika Peter aliyewika Yanga SC. Hata hivyo, Hans Poppe hajasema Manyika anakwenda timu gani

Pamoja na Manyika, Simba imeachana na kipa wake mwingine mdogo, Dennis Richard iliyempandisha kutoka timu B.

Na Simba inaachana na makipa wake hao, baada ya kuwasajili kwa mpigo makipa namba moja na namba mbili wa timu ya taifa, Taifa Stars, Aishi Manula kutoka Azam FC na Said Mohammed kutoka Simba SC.

Manyika aliyesajiliwa Simba SC Julai mwaka 2014, amedaka jumla ya mechi 51 za mashindano tofauti, nyingi za kirafiki akifanikiwa kusimama langoni mara 30 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa huku akiwa amefungwa jumla ya mabao 34.

Madhara Yatokanayo na Kuvaa Sidiria Ndogo 'Kubusti' ili Kunyanyua Maziwa

0
0
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na tabia ya wanawake kunyanyua maziwa yao, ambapo watu wengi hufahamu kama ‘kubusti’, bila ya wao kujua kuwa jambo hilo lina madhara katika afya yao.

Ili kuweza kubusti, wanawake hulazimika kuvaa sidiria ambazo ni ndogo kuliko ukubwa wa maziwa yao na hivyo kuyabana. Baadhi ya wanawake hununua sidiria hizi bila kujua ukubwa halisi wa maziwa yao na hivyo kujikuta wakibusti bila kupenda wakati wengine hudhamiria kabisa kununua sidiria hizo.

Kufuatia utafiti uliofanywa na timu ya wataalamu Lingerie Curvy Kate kutoka nchini Uingereza ulionyesha kuwa wanawake asilimia 95 huvaa sidiria zisizo na ukubwa sawa na matiti yao jambo linaloweza kusababisha uharibifu wa tishu mihimu katika matiti (kifua).

Timu hiyo ilitumia aina mbili za sidiria. Ya kwanza ni ile iliyokuwa ndogo kuliko matiti na nyingine ilikuwa sawa na matiti na kumvalisha mwanamke na kisha kumtaka atembee ili kuweza kugundua tofauti iliyopo.

Kupitia utafiti huo waliweza kugundua kuwa , madhara ya kiafya yanaweza kumpata mwanamke ambaye anavaa sidiria isiyoendana na ukubwa wa maziwa yake.

Mtaalamu mwingine, Chantelle Crabb alisema, uvaaji wa sidiria ambayo haiendani na ukubwa wa maziwa ya mwanamke kunaweza kusababisha maumivu ya matiti, aibu na uharibifu wa matiti. Lakini alifafanua zaidi kwamba, uvaaji vibaya wa sidiria unaweza kupelekea matiti ya mwanamke kulegea/kulala.

Mbali na hayo, madhara mengine ni pamoja na maumivu ya mgogo kwani mwenye maziwa makuba akivaa sidiria ndogo hulazimika kuinama anapopita katika eneo lenye mwinuko.

Maumivu ya bega ni madhara mengine yatokanayo na uvaaji wa sidiria ndogo kutokana na kamba za sidiria kuyabana mabega yako kwa nguvu.

Kuhusu kupata saratani ya matiti/titi, Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Cyrill Massawe alisema kuwa,  wanawake wanapaswa kuvaa sidiria zinazoendana nao ili wawe huru, huku akisema hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kuvaa sidiria ndogo na saratani ya matiti.

Chanzo: Mwananchi

Maisha Yalivyombadilikia Hawa wa Diamond na Kuanza Kunywa Gongo

0
0
Hawa wa Diamond anaumwa, amekongoroka na anatia huruma. Mwenyewe hajui anaumwa nini, hajui nini kinachomtafuna lakini mama anajua siri hiyo. Analia usiku na mchana akimuomba Mungu amuokoe mwanaye. Lakini mwenyewe anahisi kuwa huenda ni unywaji wa kupindukia ndiyo adui wa maisha ya mtoto wake.

Hapa inaonesha kuwa kuwa kudhoofu kwa mwili wake kiasi cha wakati mwingine kuvimba miguu kama mama yake anavyosema, kunatokana moja kwa moja na unywaji wa pombe haramu aina ya gongo.

Hawa ni msanii aliyeibuliwa na msanii wa Bongofleva, Nassib Abdul (Diamond Platnumz) kwenye moja ya singo zake za mwanzo kabisa ‘Nitarejea’ iliyotoka mwaka 2014. Ikumbukwe kwamba licha ya Diamond kumshirikisha katika wimbo huo, walikuwa wapenzi kiasi ambacho Diamond alikuwa hatoki nyumbani kwa hawa.

Ukiangalia video ya wimbo huo na ukamuangalia vizuri, basi ujue si hawa huyu wa sasa kwa sababu unaweza kutokwa machozi. Achilia mbali kukanda, lakini urembo aliokuwa nao umekwisha kiasi hata mama yake mzazi anaonekana kijana kuliko yeye.

Hawa na mama yake kwenye kipindi kimoja cha televisheni nchini walikuwa wakielekea ni nini kilichomsababishia kuwa hivyo na ni vipi ataondokana na hali hiyo ili kuendeleza kipaji chake alichopewa na Mwenyezi Mungu, cha kuimba.

“Ni makundi tu ndiyo yaliyoniponza. Nilikuwa nakunywa pombe ya aina yoyote ile, hata gongo, ilimradi tu nilewe, nibembee,” amesema Hawa. Baada ya wimbo huo alioshirikishwa na Diamond, alitoa ngoma yake mwaka 2015 aliyoiita ‘Mawazo’ amabapo amesema kuwa kitu kingine kilichomfanya kuingia kwenye kadhia ya unywaji ni mawazo kama jina la wimbo wake baada ya mzazi mwenzake kumtelekeza na mtoto, lakini pia mzazi mwenzake huyo ndiyo chanzo cha yeye kunywa pombe, kwani alimfundisha kwa kumnunulia bia.

“Aliponiacha nilikuwa nimeshazoea kunywa. Mawazo ya kutelekezwa yalinifanya nitake kuendelea na unywaji zaidi, lakini uwezo sina, kwahiyo nikajikuta nakunywa kila aina ya pombe ya kienyeji ya bei nafuu inayopatikana,” alibainisha.

Mama mzazi wa msanii huyo mara kwa mara mazungumzo yake yalikuwa yakikatishwa na kilio, kilio cha uchungu kama mzazi. Kwanza alikiri kuwa binti yake ni mnywaji zaidi wa pombe ya kienyeji aina ya gongo. Pia alisema kuwa hata mtoto anayedai Hawa kuachiwa na mzazi mwenzake ni yeye ndiyo anayemtunza na kumsomesha.

“Mimi ndiyo namtunza huyu mjukuu, mama yake anazurura huko. Mimi natafuta pesa ya ada ndiyo asome, kwa sasa nadaiwa ada,” amesema mama Hawa na kuongeza kuwa miaka mitatu iliyopita binti yake hakuwa hivyo.

“Njiani tukiongozana, yeye ndio anapata ‘shikamoo’ na mimi naonekana kijana,” ameongeza.

Hawa amesema kuwa anataka kubadilika na kwa kuanza ameamua kuacha pombe za aina zote. Pia amewaomba wasanii Diamond Platnumz, Barnaba na Nay wa Mitego wamsaidie ili aweze kushaini tena.

PENDEZA na Kessy Products, Kutoa Mvi, Kurefusha Nywele, Tengeneza Shepu na Mengine

0
0

PENDEZA NA KESSY PTODUCT:-MSIMU MPYA WA 2017_ BIDHA AINA ZOTE KWA UBORA MZURI%
PATA DAWA ZA ASILI ZISIZO NA MAD, HARA NA MATOKEO NI KWAHARAKA BAADA YA WEEK (2-/-4) 🍎🍌🍉☘
1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _80,000/
2) KUREFUSH NYWELE KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA _80,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO FIGA UMBO (8) NA KUJAZA HIPC NA KALIO @ KUPAK _80,000/
@ KUNYWA AU VIDONGE _130,000/ 4) KUPUNGUZA NYAMA ZA MIKONO TUMBONI ZILIZOTEPWETA _80,000/
5) PUNGUZA KITAMBI KWA HARAKA KWA DAW HIZI ZA KUNYWA
@) KUNYWAA _100,000/
@) VIDONGE _100,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KGM 150 ADI 80 KIASI UNACHOTAK WEWE KWA DAW HIZI
@) DAW YAKUNYWA YA _100,000/
@) VIDONGE VYA HARAKA _100,000/
7) PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KWA MUDA WA WEEK MOJA _70,000/
8) ONGEZA MAZIWA NA SAIZ UNAYOTAKA WEWE _70,000/
9) ONGEZA MWILI MZIMA NA KUKUPA HAMU YAKULA KWA RIKA LOLOYE _80,000/
10) TOA MICHIRIZI SUGU PIA NA ILE YAKUJIFUNGUA MWILI MZIMA _70,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KATIKATI YA MAPAJA _70,000/
13) KUWA MWEUP NA SOFTI MWILI MZIMA NA KUTOA WEUS MACHON NA VIMISHIPA VIDOGO VIDOGO @ MAFUTA YA KUPAKA _80,000/(@) VIDONGE (WHITE SOLUTION) _120,000/
14) ONDOA NDEVU NA VINYWELEO MWILINI _80,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME NA KUIMARISHA MISHIPA ILIYO LEGEA KWA DAW HIZ
@) JEL KUPAKA (MEN GEL) _70,000/
@) VIDONGE (MAXMAN) _80,000/
16) ONGEZA MAUMBIL YA KIUME SAIZI UNAYOITAKA WEWE KWA:
@) (HANDSOME UP) MASHINE _170,000/
@) JELI YAKUPAKA INABORESHA ANZIA NCHI (4 ADI 6 )_100,000/ PIA NA VIDNGE VYAKE VIPO
17) RUDISHA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WALIOPOTEZA KUTOKANA NA NGIRI, KISUKARI NA MAGONJWA MENGINE KWA _80,000/
18) RUDISHA USICHAN(BIKRA)Na KUTO UCHAFU SEHEMU ZA SIRI _80,000/
19) FANYA USO WAKO KUWA MKAVU NAKUTOA VIJIPELE ILIYOSABABISHWA NA MAFUTS MAKALI _80,000/
20) ONDOA MAKUNYANZI USONI _70,000 (21) ENGEZA MGUU WAKO _70,000/ TUNAPATIKAN K/ KOO NA SINZ
MAPAMBAN, KWA MIKOAN DUNIAN KOTE UTAPATA
🍎🍏🍐🍊🍌🍉🍇🍀 (+255) 0719955528
0756259180
0785371237
@dr_kessy_product
Delivery POPOTE ULIPO,

Diamond Platnumz Afunguka Kuhusu Mziki wa Tanzania Kukua

0
0
Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka wazi mawazo yake kuwa muziki wa Bongo Fleva na kiwanda kizima cha burudani nchini Tanzania kwa sasa kimekua ndiyo maana makampuni makubwa kutoka nje yanakuja kuwekeza .
 

Diamond amesema kwasasa muziki wetu umefikia sehemu nzuri ambapo wadau na Wasanii wananufaika kukua kwake na ndiyo maana Makampuni ya kigeni yanakuja kuwekeza nchini.

“Muziki wetu unazidi kukua kwa kwa sababu mpaka Watu wa nje wanakuja kufanya kitu nyumbani lazima tasnia yetu iwe imekua, kwa hiyo tasnia yetu imekua sio tu kwa Wasanii hata Industry nzima Vyombo vya Habari, Wadau kila mtu anayehusika na burudani, tumepiga hatua“,amesema Diamond Platnumz .

2020:Jee Tundu Lissu Ndiye Asimame na Magufuli?...Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli

0
0
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali tuu, Ili uchaguzi wa 2020 usiwe ni igizo tuu la uchaguzi, Jee Tundu Lissu ndiye asimamishwe na upinzani kumkabili Magufuli?, sababu mpaka sasa, ndie mwanasiasa wa upinzani ambaye so far, ameonyesha ana uwezo wa kumkabili Magufuli kwa vile uwezo wake ni zaidi ya Magufuli!.

Kama kawaida yangu, kwenye kila mijadala yenye kuhusisha maoni ya kisiasa, mimi hupenda kuanza kwa declaration kuwa sina chama, sina kambi na sina upande, kwangu ni maslahi ya taifa mbele.

Baada ya rais Magufuli kuingia madarakani na kuanza na zile tumbua tumbua, nikauliza humu kama kweli Tanzania tunataka maendeleo ya kweli, jee tuna haja ya kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?,
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020 ...

hivyo nikashauri Magufuli aachwe tuu hadi 2025 na ikibidi tubadili katiba aendelee ttuu kama Mkuruzinza, Kagame na Museveni hadi awe kama Mugabe.

Pia kufuatia trend ya chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, Chadema kutoonyesha seriousness yoyote kuelekea 2020,
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
nikaconclude kuwa Uchaguzi wa 2020 kwa upande wa urais, litakuwa ni igizo tuu la uchaguzi kwa ushindi wa walkover kwa CCM.
In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa ...

Lakini kwa mwenendo na matamshi ya Tundu Lissu ya hivi karibuni kumhusu Magufuli, kwa maoni yangu, kwa hapa tulipo, ukimuondoa Zitto ambaye he looks compromised, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani aliyeonyesha uwezo wa kumkabili John Pombe Magufuli kwenye Uchaguzi wa 2020 na Magufuli akapata joto la Uchaguzi.

Kwa jinsi nilivyomsikia Tundu Lissu na namna anavyoongea, then huyu Tundu Lissu ni typical Magufuli type tena yeye ni zaidi ya Magufuli.

Hivyo kwa vile Watanzania huwa hawachagui sera wala hawachagui vyama bali huchagua watu, kama, Magufuli huyu huyu jinsi hii hii alivyo ameweza kuchaguliwa kihalali na kumshinda Edward Lowassa, then you cannot tell about Watanzania huwa wanachagua nini, hivyo Tundu Lissu ambaye ni zaidi ya Magufuli, akisimama na Magufuli, you can never tell what will happen!, Magufuli naweza akaachwa mbali sana! , ila litabaki swali moja tuu ndogo, with reference ya kilichotokea Zanzibar, hata huku bara, jee akishinda atapewa?.

NB. Sijasema Lissu ni zaidi ya Magufuli kwenye nini, na nawaomba sana msiniulize!.

Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali/JF

Mrembo Anaswa Airport na iPhone 102 Kiunoni Akiziingiza China (+Picha)

0
0
Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika mpaka sasa amekamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Shenzhen nchini akitokea Hong Kong na simu aina ya iPhone 102 akiwa amezifunga kiunoni tayari kwa kuziingiza nchini humo kiholela.



Mwanamke huyo aliyejifunga simu hizo kiunoni kwa kutumia tepu huku akiwa amevalia nguo nzito nzito alishitukiwa na wahudumu wa uwanja huo wa ndege baada ya kubaini muonekano wake kutokuendana na viungo vingine kama mikono na miguu.

“Tulimuona akiwa na wasiwasi na aliyevaa nguo nzito nzito ilehali kwa sasa ni kipindi cha joto ndipo tukapatwa na mashaka nae tukaanza kumkagua zaidi”,amesema mmoja wa Wahudumu wa Uwanja wa ndege wa Shenzhen nchini China kwenye mahojiano yake na mtandao wa News in China.

Wakaguzi hao wamesema walimkuta na simu na saa za mikononi ambapo kwa ujumla vilikuwa na uzito wa Kilogramu 19 .


Mharifu akiwa amebeba mzigo wake wa iPhone

Hata hivyo tukio hilo sio la kwanza kutokea nchini China kwani mwaka 2015 mwanamme mmoja walikamatwa na simu aina ya iPhone 146 uwanjani hapo wakijaribu kuingiza simu hizo kiholela nchini China.

Watu wengi wanafanya biashara hiyo kutokana na bei ya simu aina ya iPhone kuuzwa bei kubwa ukilinganisha na bei inayouzwa simu hizo, Hong Kong.

Serikali ya China ilitangaza kuongeza ushuru kwa bidhaa zote za Kampuni ya Apple INC ili kuchochea mauzo ya bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.

Diva Kufanya Kama Kim Kardashian.........

0
0
Mtangazaji wa kituo cha radio cha Clouds Fm, Diva The Bawse ameamua kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kufanya biashara kistaa zaidi.

Akiongea na Bongo5 hivi karibuni mrembo huyo ambaye amekuwa akipendwa na watu kutokana na uzuri wa sauti yake, amesema ameamua kuingia katika biashara kwani alikuwa na ndoto ya kufanya hivyo kwa muda mrefu.

“Nimeamua kufanya biashara ya vipodozi kwa njia ya mtandao, hii ni ndoto yangu ya muda mrefu sana nimevutiwa zaidi ufanya biashara hiyo kistaa zaidi kama wanavyofanya mastaa kutoka nje, unajua ukifanya biashra kwa njia hiyo unaingiza hela zaidi,” amesema Diva.

ADC Wajitosa kwa Rais Magufuli, Waomba Abadili Msimamo wake

0
0
Chama cha ADC  kimemwomba Rais Magufuli katika miaka hii mitatu iliyobaki kubadilisha msimamo wa kuzuia kufanywa kwa   mikutano ya hadhara inayotakiwa kufanywa na vyama vya upinzani.

Akizungumza katika kuelekea maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa  chama hicho  Katibu mkuu wa chama cha ADC , Doyo Hassan Doyo amesema wao wanania nzuri ya kufanya siasa nakusema Rais  asione kwamba vyama vyote vinakauli mbovu katika kufikisha  ujumbe kwa jamii.

Doyo amesema suala la Magufuli kuzuia mikutano ya kisiasa  vyama vingine vya Demokrasia na kusema wao hawana mbunge wala diwani hivyo wana ufinyu mkubwa wa kufanya siasa, na kusema kuwa  wao wanapaswa kufanya siasa kwa nguvu zote ili kuongeza wananchama na hatimae kujipatia viti vingi vya uongozi.

"leo umezuiwa kusema inamaana hutoweza kupata sapoti ya watu  na watu hawatoweza kufahamu sera za chama chako kutokana kutoweza kufanya mikutano ya kisiasa" Alisema Doyo.

Aidha Chama hicho kinafanya maadhimisho hayo kwa njia ya ziara ambapo watatembelea baadhi ya taasisi za kidini,magereza ,hospitali,pamoja na vyombo vya habari.

Ziara ya chama hicho imeanza leo katika katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Dar es salaam lakini hawakupata fursa ya kukutana na mkuu mkoa huyo Paul Makonda  kutokana na kuwa nje ya ofisi.

Hata hivyo chama hicho kimefanya jitihada ya kuwasiliana na mkuu huyo na kuwaahidi katika ratiba zao zinazoendelea waweze kuwasiliana nae ili waweze kuzungumza kama ilivyo kusudiwa.

Ukweli Mchungu: Siku Hizi Wazee Wako Shapu Kuliko Vijana, Rais Magufuli Afunguka

0
0
Rais Magufuli amesema siku hizi siyo vijana peke yao wanao haribu wanafunzi, na kwamba wapo wazee walioko shapu na hawapitwi kuwapa mimba wanafunzi, na kuwataka wenye tabia hiyo waache kwa sababu watafungwa kwa miaka 30.

Rais John Magufuli amesema wanaowapa mimba wanafunzi hawana budi kufungwa miaka 30 ili kukomesha suala hilo na kuwapa fursa watoto wasome kwani hao ndiyo viongozi wa kesho.

Rais amezungumza hayo jana  wakati wa uzinduzi wa barabara Kaliua, mjini Tabora, ambapo aliweka wazi kwamba wanaowapa mimba watoto wa shule siyo  vijana pekee bali wapo wazee nao wameingia kwenye mkumbo huo hali ambayo inawafanya mabinti washindwe klumaliza elimu ya sekondari.

“Wazee siku hizi wapo shapu kuliko vijana, wanawapa mimba wanafunzi, muwaache wasome, ukimpa mimba mwanafunzi unafungwa miaka 30 nguvu zako zikaishie gerezani,” amesema na kuwataka wanafunzi kusoma ili watimize ndoto zao.

".....Soma kwanza, usipate mimba ukiwa shule, subiri umalize sekondari ndipo upate mimba,” amesema.

Pamoja na hayo Mhe. Magufuli amesema kuwa serikali yake imedhamiria kuwapatia wanafunzi wa kitanzania elimu.

"Tumeamua kutoa elimu ndiyo maana tumetenga bilioni 18.777 tunataka watoto wasome na wasipate mimba, naomba wajiepushe na mimba mpaka watakapotimiza malengo yao," aliongeza.

Ebitoke: Ben Pol si Chochote Mpaka Leo Bado Hajaweza Kunitoa Bikira

0
0
Msanii wa vichekesho Ebitoke amefunguka na kusema Ben Pol mpaka dakika hii bado hajafanikiwa kufungua mlango wa binti huyo hivyo anadai mpaka sasa bado hajawahi kulala na mwanaume yoyote yule katika maisha yake.

Ebitoke amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV na kudai Ben Pol bado hajafanikiwa kumuondoa bikra.

Ben Pol na Ebitoke wanadaiwa kuwa ni wapenzi wenye malengo ya mbali ikiwa ni pamoja na kupeana support katika kazi zao za sanaa, ingawa wapo baadhi ya watu ambao wanaona kama watu hao wanafanya maigizo na mapenzi yao kuonekana kama njia ya kujitangaza na kuzidi kupata kiki katika kazi zao, ingawa kwa Ben Pol siku ya Jumamosi alikiri kuwa kwa mara ya kwanza kukutana na Ebitoke walikutana Bahari beach na kuzungumza mambo mengi zaidi ya mapenzi yao.

Flora Mbasha na Mumewe wa Zamani Waliamsha Dude la Bifu Upyaaaaa........Kisa Kizima Hichi Hapa

0
0
Waimba Injili Bongo ambao walikuwa wanandoa kabla ya kutalikiana mahakamani, Flora Daud Kusekwa ‘Madam Flora’, zamani alikuwa akitambulika kama Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha wameonekana kuliamsha dude la bifu lao upyaa, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda kamili.

Kikizungumza na Ijumaa Wikienda kwa sharti la kutotajwa gazetini, chanzo makini cha sakata hilo kilielezwa kuwa, wawili hao kwa sasa wameingia kwenye bifu upya baada ya hivi karibuni Flora kudaiwa kumtolea maneno (hayaandikiki gazetini wala mitandaoni) aliyekuwa mumewe, Mbasha ambayo yalisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuzua gumzo.

“Yaani mambo siyo mambo kwani Flora na Mbasha kwa sasa bifu limeanza upya kama zamani wakati wanaachana baada ya mwanamama huyo kudaiwa kutoa maneno mabaya ambayo yalimuudhi Mbasha naye kuamua kufunguka kwenye vyombo vya habari.



“Kwenye habari hiyo mitandaoni ilionesha Flora alizungumza maneno hayo yanayosemekana yamo kwenye kitabu chake ambacho kimeshatoka kinachoitwa Siri za Flora Mbasha, maneno ambayo alisema ndiyo chanzo cha ndoa yake kuvunjika.

“Inasemekana aliwaita watu kupata ufafanuzi zaidi kwenye kitabu chake licha ya kwamba Flora baada ya habari kusambaa mitandaoni alikanusha kuwa hakuwahi kusema maneno yale,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata habari hiyo kutoka kwa chanzo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Mbasha ambaye alionekana kuwa mwenye hasira kali akisema:

“Sipendi ujinga kwani watu hawawezi kuuza hicho kidaftari chao mpaka watafute kiki kwangu? Mbona wengine wanauza vyao kwa utaratibu mzuri?

“Mimi ninaingiaje kwenye ishu za huyo Flora? Zaidi ya miaka mitatu sipo naye na ni mke wa mtu, ninamuomba atulie na akome kunitajataja.”

Kwa upande wa Flora alipotafutwa ili kujibu hayo aliendelea kusisitiza kuwa habari hizo za mtandaoni hazikuwa za kweli isipokuwa ni kweli kitabu chake hicho kimeshatoka na kinaelezea kiundani mambo aliyoyapitia kwenye ndoa yake na Mbasha kabla ya kuolewa na David Kusekwa
GPL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images