Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Shaffih Dauda Afunguka Kuhusu Kukamatwa na TAKUKURU

$
0
0
Jumatano ya July 26 2017 zilienea taarifa za kukamatwa na TAKUKURU kwa mwenyekiti wa chama cha mpira Dar es Salaam DRFA Almas Kasongo, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es Salaam na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda pamoja na wanafamilia wengine wa mpira Mwanza.

Taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kukamatwa kwa watu hao zinadai ni viashiria vya rushwa na kuhusishwa na kampeni za chini kwa chini za uchaguzi Mkuu wa TFF, hivyo TAKUKURU ikawakamata kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa kadhaa kabala ya kuwaachia kwa dhamana.

Baada ya kurejea Dar es Salaam akitokea Mwanza Shaffih Dauda alipokuwa amekwenda na viongozi wa DRFA kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup kupitia Clouds FM ameeleza tukio la kukamatwa kwao lilivyokuwa ambalo linadaiwa kulenga kuwachafua katika uchaguzi Mkuu wa TFF.

“Nimehojiwa na TAKUKURU nikiwa Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup ambayo inaweza kuanza Mwezi wa 9, nilichogundua ni siasa za uchaguzi wa TFF, nilikutana na viongozi wa mpira Mwanza kwa ajili ya mipango ya Ndondo Cup Nilikua na viongozi wa DRFA tulioanzisha nao Ndondo Dar”: Shaffih Dauda

“Viongozi wa DRFA walikuwepo Mwanza kuwaeleza uzoefu viongozi Mwanza kabla hawajafanya na wao mwaka huu, baadhi ya watu na mawazo yao walitoa taarifa za uongo na kufanya mipango ya hovyo wakijua nafanya mipango ya uchaguzi, sigombei TFF kutaka cheo, nagombea kuleta mabadiliko kwenye soka, ndio maana napambana kupeleka Ndondo Cup kila sehemu” >>> Shaffih Dauda MSIKILIZE HAPA:

UTAFITI: Madhara ya Kuendesha Gari Kwa Muda Mrefu Usiyoyafahamu

$
0
0
Utafiti mpya uliofanywa umeonesha kuwa kuendesha gari kwa umbali urefu kunaweza kuleta athari kubwa kwenye ubongo na kuathiri kiwango cha IQ, wanaonya Wanasayansi.

Kwa mujibu wa Watafiti hao ni kwamba matokeo ya utafiti huo yanaweza kuelezewa kwa hoja kwamba ubongo hufanya kazi chini ya kiwango wakati wa safari ndefu.

Project hiyo ilishuhudia zaidi ya nusu milioni ya wakazi wa Briton wenye umri wa kati ya miaka 37 na 73 kufanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka mitano huku watu 93,000 kati yao wakikiri kuendesha gari kwa zaidi ya saa mbili kwa siku ambapo Watafiti wamebaini sio tu kuwa husababisha kudhoofisha nguvu za ubongo lakini pia kiwango cha IQ hupungua haraka ukilinganisha na ambao hawatumii muda mrefu wakati wakiendesha.

Dr. Kishan Bakrania, kutoka University of Leicester, aliiambia The Sunday Times:
”Tunajua kwamba kuendesha gari kwa zaidi ya saa mbili au tatu kwa siku ni mbaya kwa moyo wako. Utafiti huu unaeleza ni hatari kwa ubongo wako pia, huenda kwa sababu hufanya kazi chini ya kiwango katika saa hizo.”

WANAWAKE Waliotekwa na Kuolewa na BOKO HARAM Wataka Kurudi Kwa Wapiganaji Hao.....

$
0
0

Habari zilipoenea kuhusu baadhi ya wasichana wa shule ya Chibok waliotekwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram mwaka 2014 kukataa kurejea nyumbani na wenzao walioachiwa kwenye kundi la 82 lililoachwa huru mwezi Mei, dunia nzima haikuamini kwamba jambo hilo lingeweza kutokea.
Video iliyotolewa na wapiganaji wa Boko Haram ikiwaonesha wanawake na wasichana walioshika bunduki wakisema kuwa wanafurahia maisha yao mapya haikutosha kuwaaminisha watu. “Itakuwa wamelazimishwa tu,” baadhi ya watu walikuwa wakisema. Nini zaidi ya hicho kitamfanya msichana au mwanamke yeyote kuamua kubaki na wanaume wa aina hiyo? Ndio swali kubwa lililowasumbua wengi.

Hata hivyo, baadhi ya wanawake waliookolewa na majeshi ya Serikali ya Naijeria wamekuwa tayari kurudi kwa wapiganaji wa Boko Haram waliopo kwenye msitu wa Sambisa kwa hiyari yao wenyewe.
Mwezi Januari, muandishi wa BBC alikutana na kuzungumza na Aisha Yerima (25) ambaye alitekwa na wapiganaji hao zaidi ya miaka minne iliyopita. Alipokuwa huko, aliolewa na kamanda mmoja wapo ambaye alikuwa akimpenda sana na kumpatia zawadi za gharama na kumuimbia nyimbo za mapenzi za Kiarabu.

Amesema kwamba maisha haya mazuri aliyokuwa akiishi msituni yalikatishwa kwa kutokea kwa majeshi ya Naijeria mwanzoni mwa mwaka 2016 wakati mumewe alikuwa amekwenda kwenye mapigano akiwa na makamanda wenzake.

Mwandishi alipofanya mahojiano na Aisha kwa mara ya kwanza ilikuwa mwanamke huyo alipokuwa polisi kwa zaidi ya saa nane, na kumaliza programu ya kumfanya asiwe na msimamo mkali aliotoka nao porini aliyokuwa akifanyiwa na mwanasaikolojia Fatima Akilu, muanzilishi wa programu hii.
“Kwa sasa naona kabisa kwamba vitu vyote ambavyo tuliambiwa na Boko Haram ilikuwa ni uongo. Sasa hivi nikiwa nawasikia redioni najikuta nacheka,” alisema Aisha.
Wanavutiwa na madaraka waliyokuwa nayo?

Lakini ilipofikia mwezi Mei ikiwa ni chini ya miezi mitano toka awe huru na kuanza kuishi na wazazi wake jijini Maiduguri, Aisha alitoroka na kukimbilia msituni yalipo maficho ya Boko Haram.
Kwa miaka mitano iliyopita, Dkt. Akilu amekuwa akifanya kazi na waliokuwa wafuasi wa kundi la Boko Haram – wakiwamo baadhi wa makamanda, wake na watoto za – na mamia ya wanawake waliookolewa kutoka kwenye himaya yao.

“Ni jinsi gani wanawake walivyokuwa wanafanyiwa walipokuwa mikononi mwa Boko Haram inategemea walikuwa wameshikiliwa kwenye kambi ipi. Inategemea kamanda gani alikuwa anaongoza kambi hiyo,” alisema.

“Kwa wale waliokuwa wakiishi vizuri ndio waliridhia kuolewa na viongozi na wafuasi wa Boko Haram au wale waliojiunga na wapiganaji hao kwa kujitolea, ambao ndio wengi sana. Wanawake wengi hawakuwa wakipata matunzo sawa.”

Aisha alijisifu kwa mwandishi kuwa alikuwa na idadi kubwa ya watumwa alipokuwa kwenye msitu wa Sambisa, heshima kubwa aliyokuwa akiipata kutoka kwa makamanda wengine wa Boko Haram na nguvu kubwa ya ushawishi aliyokuwa nayo juu ya mumewe. Na alijisifu kuwa mara moja alimsindikiza na kwenda naye mpaka kwenye uwanja wa mapambano.

“Hawa ni wanawake ambao kwa muda mwingi hawajawahi kufanya kazi, hawakuwa na mamlaka yoyote, hawakuwa na sauti kwenye jamii, na mara inatokea wanakuwa na madaraka ya kuongoza wanawake kati ya 30 na 100 ambao sasa wanakuwa moja kwa moja watumwa wao wakitumwa na kufanya lolote watakaloambiwa,” aliongeza Dkt. Akilu.

“Ni ngumu sana kujua ubadilishe vipi hali hiyo ukisharudi kwenye jamii kutoka ulipokuwa mateka kwa sababu wengi wa wanawake hao wanarudi kwenye jamii ambapo hawataweza tena kuwa na mamlaka waliyokuwa nayo kabla ya kuokolewa.”
Bado mshangao ni mkubwa

Mbali na kutokuwa na mamlaka tena, sababu nyingine ambayo Dkt. Akilu anaamini inaweza kufanya wanawake hao kuwa tayari kurudi kwa Boko Haram ni pamoja na kutengwa na jamii inayowaona kama ni miongoni mwa wapiganaji hao tu kwakuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na hali ngumu ya kiuchumi wanayoipata wakiwa kwenye jamii ambayo hawawezi kuipata wakiwa na Boko Haram.

“Kuwaondoa misimamo mikali waliyojengewa ni jambo moja. Kuwafanya waweze kuishi kwenye jamii ni jambo la pili kwenye programu hii. Baadhi yao hawana watu wa kuwafanya wajisikie salama kuishi nao. Mara nyingi wanafanikiwa kuondoa misimamo yao mikali lakini wanapata tabu kuishi kwenye jamii na ni tabu inayowapelekea mara nyingi kujikuta wanarudi,” amesema Dkt. Akilu.
Mama wa Aisha amesema kuwa anakumbuka wanawake angalau saba ambao waliolewa na Boko Haram ambao wote walikuwa ni marafiki wa mwanaye walisharudi kwenye msitu wa Sambisa muda mrefu kabla ya Aisha.

“Kila mara mmoja wao alipotoweka, familia yake walikuwa wanakuja kwetu na kumuuliza kama Aisha kama wamewasiliana na mtoto wao,” alisema. “Na hivyo ndio tulikuwa tunajua.”
Baadhi ya wanawake hao walikuwa wanawasiliana na Aisha baada ya kurudi kwa wapiganaji wa Boko Haram. Mdogo wake, Bintu, alisikia mazungumzo ya simu ya dada yake angalau mara mbili.
“Walikuwa wanamwambia arudi na aungane nao lakini alikuwa anakataa,” alisema Bintu. “Alikuwa anawaambia kwamba hataki tena kurudi.”

Tofauti na baadhi ya waliowahi kuwa “wake” wa Boko Haram niliowahi kukutana nao ambao labda wanaishi maisha magumu au wanakumbana na unyanyapaa, kwahiyo maisha ya Aisha yalikuwa ni kama yanajulikana yatakavyokuwa.

Alikuwa anapata pesa kutokana na biashara ya nguo, alikuwa akihudhuria matukio mbalimbali ya kijamii na mara nyingine huweka picha zake kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wenzake.

“Nadhani wamaume kama watano hivi walitaka kumuona,” alisema mama Aisha, akimaanisha kwamba jamii ilishakubali kuishi vizuri na mwanaye, na kusema kuwa hii inaashiria kuwa mwanaye hakukumbwa kabisa na unyanyapaa kabisa kutoka kwenye jamii.

“Mmoja wa wanaume waliokuwa wanamtaka anaishi jijini Lagos. Aisha alikuwa anafikiria kuolewa kabisa,” alisema.

Lakini kila kitu kilibadilika alipopigiwa simu na rafiki zake waliorudi porini wakimwambia kwamba mumewe wa Boko Haram alikuwa na mwanamke mwingine ambaye alikuwa mpinzani wa Aisha alipokuwa porini.

Tangu siku hiyo, Aisha tuliyemzoea anayependa kukaa na watu hakuwa yeye tena. “Aliacha kutoka, kuongea na watu au kula,” alisema Bintu. “Alikuwa na hasira muda wote.”

Wiki mbili baadaye aliondoka nyumbani na hakurudi tena. Baadhi ya nguo zake hazipo. Simu zake hazipatikani. Aliondoka na mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka miwili aliyopata na kamanda wa Boko Haram kwenye msitu wa Sambisa, lakini amemuacha mkubwa kwa aliyekuwa mumewe ambaye waliachana kabla hajatekwa.

WAZIRI Mkuu Avishukia Vyuo Vinavyolalamika Kwa Kufungiwa na TCU.......

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuhakikisha kwamba programu zote zinazotolewa na taasisi za elimu ya juu zinawawezesha wahitimu kujiajiri na kuwa na sifa za ushindani katika soko la ajira kimataifa.

Amesema wakati umefika sasa kwa wasomi katika vyuo vyetu vikuu tujiridhisha kuwa mitaala inayotolewa kama inawaandaa wahitimu kupata taaluma na stadi za kuweza kujiajiri na kupambana na changamoto za kimaisha.

Amesema taasisi za elimu ya juu nchini ziangalie mitaala yake na kuimarisha mfumo wa ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ili kwenda sambamba na dunia ya kazi inayoendana na agenda ya maendeleo ya Taifa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Julai 26, 2017) wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 12 ya Elimu ya Juu, jijini Dar es Salaam ambapo amevutaka vyuo hivyo badala ya kuendelea kulumbana kwenye makongamano na vyombo vya habari, vifanye maboresho yanayotakiwa ili viweze kuendelea na ufundishaji. Aidha amesema kuwa, lengo la serikali ni kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa bora na kwamba maboresho yanayotakiwa kufanyika yanawezekana.

Waziri Mkuu amesema maonesho hayo ni jukwaa la kipekee ambalo litaibua mjadala sahihi kuhusu uhalali wa kozi zinazotolewa na vyuo husika vya elimu ya juu. “Hivyo mnayo nafasi ya kuonesha kwa vitendo uwezo wenu katika utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia zinazotumika katika maendeleo ya viwanda.”

Amesema ni vema mfumo wa ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ukaimarishwa ili kuhakikisha asilimia 60 ya wanafunzi wanahitimu shahada kwenye sekta ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi.

Amesema taasisi za elimu ya juu ziweke mikakati ya kuinua na kuboresha taaluma wanayoitoa ili ilete tija kwa maendeleo ya Taifa na Dunia. Pia kuanzisha program za mafunzo zenye kukidhi mahitaji na kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuzingatia mahitaji ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amezitaka taasisi hizo kuendelea kuimarisha mfumo wa udahili na kujipanga kutumia fursa za elimu na mafunzo ndani na nje ya nchi kwa makundi yote ya jamii kwa usawa katika ngazi zote hususan ufundi, hisabati, sayansi na teknolojia.

Pia Waziri Mkuu amesema ni wakati muafaka kwa taasisi za elimu ya juu nchini kuandaa mikakati ya kuongeza udahili kwa kuzingatia mahitaji ya rasilimali watu na ujuzi unaohitajika katika sketa zinazokua haraka mfano mafuta, gesi na madini.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, JULAI 26, 2017

TAFITI: Wanaosoma Habari Mitandaoni Hupoteza Kumbukumbu Haraka Kuliko Magazetini....

$
0
0
Kama wewe ni mfuatiliaji na msomaji wa habari mitandaoni basi bila shaka huenda ulishawahi kukumbana na hali ya kusoma habari ambayo baada ya kumaliza ukaanza kukumbuka kama ulishawahi kusoma habari hiyo sehemu fulani lakini umesahau, basi utakuwa upo sahihi kabisa.



Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na muandishi wa habari mkongwe wa Gazeti la Financial Times,  Michael Skapinker amebaini kuwa wasomaji wa habari mitandaoni wengi wao hupoteza kumbukumbu ya kuhifadhi habari walizosoma kwa muda mfupi sana ukilinganisha na wale wanaosoma habari kupitia Magazeti.

Mwandishi huyo amesema asilimia kubwa ya wasomaji wa habari mitandaoni hufikiria zaidi kutoa maoni na kushare habari walizozipenda na sio kutilia maanani kwenye usomaji wa habari.

Utafiti huo uliofanyika kwenye nchi 60 tu umeonesha kuwa wasomaji wengi wa habari mitandaoni wanasoma habari nyingi kwa muda mfupi huku wakifanya shughuli nyingine kitu ambacho kinawafanya wakose umakini wa kuzingatia kile wanachokisoma tofauti kabisa na wale wanaosoma habari kwenye magazeti ambao hupaswa kupumzika kabisa ili kuweza kusoma gazeti.

Kwenye nchi 60 alizofanya utafiti huo, Michael Skapinker amesema kuwa asilimia 85 ya vijana chini ya miaka 40 ndiyo wanaopendelea zaidi kusoma habari za mitandaoni huku 15% wakisoma habari kupitia Majarida na Magazeti.

Hata hivyo utafiti huo umeonesha ingawaje vijana wengi wanasoma habari mitandaoni ila ni wepesi sana kusahau habari walizoma yaani kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi ukilinganisha na wale wanaosoma habari kwenye Magazeti.

Utafiti huo pia umeonesha kuwa ingawaje kuna ongezeko kubwa la wasomaji wengi wa habari mitandaoni lakini bado kuna kundi la wasomaji hawaamini habari hizo mpaka wazikute kwenye magazeti.

Bwana Skapinker amesema ingawaje wasomaji wa mtandaoni hupoteza kumbukumbu haraka lakini bado watu wengi huvutiwa na habari za mitandaoni kutokana na uharaka wa kuzipata, kuokoa muda, kupunguza gharama na urahisi wa kutoa maoni ya walichokisoma.

SHAMSA Ford Awachana Wanaume Wanaopenda Kulelewa

$
0
0
Msanii wa Filamu nchini, Shamsa Ford amewatolea uvivu wanaume wanaopenda kulelewa na wanawake.

Kupitia mtandao wa Instagram muigizaji huyo ameonyeshwa kukerwa na tabia hiyo ambayo inapekea wawe tegemezi kwa wapenzi hao kutokana na kuchagua kazi.

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,” ameandika mrembo huyo.

Akaongeza “Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah.”

SHAFFI Dauda Akiri Kufanyiwa Mchezo Mchafu

$
0
0
Siku ya Jumatano ya July 26 2017 zilienea taarifa za kukamatwa na TAKUKURU baadhi ya wadau wa soka wakiwemo wagombea wa uchaguzi katika nafasi mbalimbali za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).



Miongoni mwa hao ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Dar es Salaam (DRFA) Almas Kasongo, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es Salaam na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda pamoja na wanafamilia wengine wa mpira Mwanza.

Mara baada ya tukio hilo kupita, Shaffi Dauda akiri kuhojiwa na TAKUKURU Mwanza, asema alikuwa katika vikao vya maandalizi ya Ndondo Cup na si vikao vya uchaguzi.

Kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra kinachorushwa na radio Clouds Fm Dauda amesema.
“Kwenda jioni na Mkazuzu kwenda kuangalia “logistics” za Vila Park, Press tufanyie sehemu gani kesho. Tunafika pale tumeyamaliza tunamtafuta Rama hata Rama sijaonana nae maskini” amesema Dauda.

Shaffi Dauda ameongeza kwa kusema kuwa “Tumekaa tunakula chakula mara wazee hao wamevamia dakika tano hazikufika kulikoni ?, eeh mnafanya nini ?, difenda na takukuru. Kumbe siasa za mpira zimeanza mambo ya uchaguzi”.

“Kumbe sisi tunakuja huku Mwanjala anaambiwa usiende huko Mwanza kunawatu walikuwa washapanga mipango yao huku ambao wao wanafikiri kuongoza mpira wanchi hii ndiyo wenye haki miaka yote wameshakuwa viongozi lakini sasa hawapo kwenye mfumo wanalazimisha kuwemo”. Na sisi kwa sababu zimeshakuja mamlaka unakuwa mpole tumewasilikiza tukaenda tukaojiwa maelezo tukawapa mpaka saa tisa baada ya hapo tukaruhusiwa tumetoka kwa dhamana lakini ni siasa za uchaguzi”.

“Kumbe tumekaa pale kunamtu anamtumia mtu meseji ebwana toka hapo sasa hivi kunakuja TAKUKURU maskini simu ilikuwa Silence watu hawajui lakini nashukuru Serikali imefanya kazi yake”.

Kontena 10 Dawa Kulevya zakamatwa

$
0
0
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini imekamata makontena 10 yaliyokuwa na kemikali aina ya ethanol yenye ujazo wa lita 200000 (Laki mbili) kupitia bandari ya Dar es salaam kutokea nchini Swaziland.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa kupambana na dawa za kulevya nchini Rogers Sianga inasema kuwa kemikali ziliingizwa nchini na kampuni ya 'Hamid Ibrahim Saambaya' na kusema kwamba makontena hayo yamekamatwa kutokana na kampuni hiyo kutofuata miongozo na ya sheria zilizopo kutoka katika mamlaka husika za kujihusisha na kemikali bashirifu.

Taarifa ya Sianga imedai kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiingiza kemikali hizo nchini tangu mwaka 2016 na kufikia jumla ya ujazo wa lita milioni moja na nusu na kwamba kampuni hiyo haijawahi kusajiliwa wala kuweka kumbukumbu wapi kemikali hizo zinakopelekwa.

"Pamoja na kwamba kemikali hizo zinatumika kwa matumizi mengine viwandani kama kutengeneza pombe na vinginevyo pia kwa kutumia kemikali hizi zikichepushwa zinaweza kutengeneza dawa za kulevya" Taarifa iliyotolewa na Kamishna Sianga ilieleza.

Hata hivyo mamlaka kwa kushirikiana na mamlaka nyingine zinaendelea na uchunguzi juu ya uhalali wa biashara za kampuni hiyo na kufahamu mahali sahihi kemikali hizo zinapopelekwa na baada ya hapo hatua za kisheria zitachukuliwa.

ZITTO Kabwe Awajibu Chadema

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewajibu baadhi ya watu wanaomkosoa na kumuita msaliti kutokana na kitendo cha kumsifia Rais John Magufuli alipokuwa ziarani jimboni humo.

Zitto alijibu mapigo hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kigoma Mjini, ambapo alisema asingeweza kumkosoa Rais Magufuli wakati ule kwa kuwa alikuwa mgeni jimboni kwake, pia alikuwa anafanya shughuli za maendeleo ya wananchi wa jimboni kwake.

“Rais alikuja hapa akafungua mradi wa maji tukaenda ziwa Tanganyika, kuna watu walikasirika sababu Rais alinisifia sana, hawezi akaja Kigoma mtu akanisema mimi vibaya msingekubali, na mgeni akija siwezi nikaanza kumsema vibaya, mgeni akija unamkaribisha anafanya kazi yake anaondoka, kwani rais akienda kwenye majimbo yao wanamsema, rais alikwenda Bukoba Mjini wakati wa tetemeko, mbunge wa jimbo hilo alimsema ? alikwenda Arumeru kwa mdogo wangu Joshua Nasari, alimsema rais kwa nini akija kigoma mimi ndio nimseme,” alihoji Zitto.

Aliongeza kuwa “Mimi hamkunifundisha kuwa mazwazwa wazee mlinifundisha adabu na kuhakikisha maendeleo yanapatikana lakini sio kwamba rais akikosea hatutamsema tutamsema, na tumeshamsema sana, sisi ndio chama cha mwisho kufanya mkutano wa ziara, tukaja operesheni ya linda demokrasia tumemaliza mikutano ikapigwa marufuku.”

“Lakini toka serikali ya awamu ya tano iingie madarakani uhuru umeanza kuminywa sasa ni lazima, hatuwezi kukaa kimya haki ya watu kuwa na mawazo tofauti hatuwezi kuikalia kimya hata kidogo, lakini wakati huo huo hatuwezi tukasimamisha kila kitu kusubiri haki ya kuwa na mawazo huru, lazima haki ya mawazo huru ipiganiwe wakati tunapigania maendeleo,” amesema

PETER Msechu Aponzwa na Kauli ‘Nafumaniwa Kila Siku Mtaani Kwetu’

$
0
0
Muimbaji Peter Msechu alijikuta matatizoni wiki iliyopita baada ya kutoa kauli ya mzaha kwamba yeye ni mtu anayefumaniwa kila siku mtaani kwake.

Msechu amedai muda mchache baada ya kauli hiyo kusambaa mke wake alianza kupigiwa simu na watu mbalimbali kitu ambacho kilimfanya achanganyikiwe.

Kauli hiyo aliitoa Msechu baada ya kuulizwa swali na kituo kimoja cha redio kwamba wasichana wengi hawapendi kutoka kimapenzi na wanaume wenye vitambi ndipo muimbaji huyo akajibu mbona yeye mtaani kwake wasichana wengi wanamgombania huku akidhihaki tena ameshikwa ugoni mara kadhaa.

Akiongea Jumatano hii katika kipindi cha Yaliyomoyamo cha Redio One Stereo, Msechu amedai kauli hiyo aliitoa kwa mzaha na baadhi ya watu walishindwa kuielewa.

“Yaani baada ya ile kauli kusambaa hawakunitafuta mimi wala media, wakatafuta mzazi wangu, nilikwambia mwanao mwambie aache muziki sasa angalia anafumaniwa kila siku. Mke wangu akajazwa maneno ametoka ofisini amedata,” alisema Msechu.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Yakawa’ amedai muziki kwa sasa unawafanya wasanii kubadilisha aina ya muziki waliokuwa wanafanya awali na kuingia kwenye muziki wa kutegemea kiki.

Usiogope Kukopa...Hizi Hapa Faida za Kukopa Katika Afya Zetu.....

$
0
0

Faida Za Madeni Mwilini..


1 .Kuchangamka Kwa Ubongo,Yaani Akija Anayekudai Unakuwa Umeshaandaa Majibu Mazuri Ya Kumpa Na Anaondoka Akitabasamu Bila hela

2. Kuwa Na Akili Nyingi, Maana Madeni Humfanya Mtu Aishi Kwa Wasiwasi Na Kama Mnavyojua Wasi Wasi Ndo Akili

3. Mazoezi Ya Viungo, Anayekudai Atajifanya Akulie Timing Saa Kumi Na Moja Alfajiri Kumbe Wewe Ushaaplan Utoke Saa Kumi Kumkimbia,


4. Madeni Huzuia Sound Pollution Yaani Hata Kama Umelewa Na Ulikuwa Ukiimba Nyimbo Njia Nzima Ukipita Mtaa Anaoishi Anayekudai Tu Unanyamaza Automatic Na Hata Ukifika nyumbani Pia Majirani Zako Wanapumua Maana Huwashi Kile Ki , Sabuufa Chako Pasua kichwa..


5. Kupungua Ama Kuzorota Ķwa Kitambi, Anayekudai Akikusakama Sana Nayo Sometimes Inapelekea Kuyeyuka Kwa Mafuta Yazungukayo Tumbo Hivyo Kiafya Unatengemaa.. Tukope jamani kudumisha afya zetu

Acacia Yalipa Ushuru Milioni 460

$
0
0

Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu (BGML) uliopo katika Halmashauri ya Msalala, mkoa wa Shinyanga jana Jumatano Julai 26,2017 umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi 460,732,841.08/= kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew alisema kiasi hicho ni asilimia 67 ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka huu ambacho ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma wa mgodi huo katika kipindi hicho.

 “Jumla ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni shilingi za Kitanzania 687,660,956.84/=,ambapo malipo hayo yamegawanywa katika halmashauri mbili ambazo ni Msalala inayopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopo mkoani Geita inapata asilimia 33”,alifafanua Crew.

Alisema kutokana na mgawanyo huo,halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 460 (460,732,841.08/= ) na Nyang’wale shilingi Milioni 226 (226,928,115.76/=.

“Ushuru umepungua kwa kuwa mgodi haujafanya mauzo ya makinikia ambayo yamezuiwa tangu mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu, hivyo tunafahamu kuwa tutalipa zaidi tutakapouza makinikia ambayo yapo yanaendelea kukusanywa mgodini”,aliongeza Crew.

Katika hatua nyingine Crew alisema tangu mwaka 2000 mpaka sasa mgodi huo umelipa zaidi ya shilingi 10,247,742,957/= za kodi ya ushuru wa huduma na kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika mwaka 2014.

 “Mgodi wetu unaendelea kuwa na matarajio ya kuchangia kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji madini katika halmashauri ya Msalala huku tukiendelea kutekeleza mkakati wa Jamii Endelevu wa Acacia ulioanzishwa mwaka 2016 kwa kushauriana na wadau lengo likiwa ni kuchangia maendeleo ya Jamii Endelevu inayonufaika na kukua kwa uchumi ndani ya jamii ili kujenga mahusiano ya kuaminika”,alisema Crew.

Akipokea hundi hiyo kisha kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliushukuru mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa huduma kwa jami.

“Hiki kiwango cha shilingi milioni 460 tulichopokea ni kiwango kizuri ingawa kimepungua ulikinganisha na kipindi cha miezi sita cha Mwezi Juni hadi Desemba 2016,furaha inatujaza kwamba ile shilingi milioni 300 na zaidi ipo ndani ya Makinikia, yatakapouzwa tutaipata na tutaendelea kuboresha huduma za kijamii”,alieleza Nkurlu.

Nkurulu alimuomba mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha zilizotolewa na mgodi huo zitumike kwa huduma za kijamii kama zilivyokusudiwa ikiwemo kuboresha huduma za afya na miundombinu.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege alisema mapato waliyopokea kutoka mgodi huo yako chini kwa shilingi milioni 300 ukilinganisha na kipindi kilichopita cha kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2016 ambapo mgodi huo ulipokea shilingi milioni 760.

“Sisi tumepokea mapato haya kama tunavyopkea mapato mengine tunayopata katika halmashauri zetu,mapato haya ni yako chini ukilinganisha na kipindi kilichopita,tunaambiwa mapato yamepungua kutokana na Makinikia ambapo sasa yamesimama,hii inaleta changamoto katika ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yetu, tunaamini mazungumzo baina Acacia na serikali yakiisha halmashauri yetu itapata mapato mengi Zaidi,” aliongeza Berege

VIDEO: Lipumba atolea tamko zito kikao cha kina Maalim Seif

$
0
0
Leo Julai 27, Mwenyekiti  wa chama cha wananchi taifa (CUF) Prof Lipumba amewafahamisha waandishi wa Habari kuwa amepata taarifa kuhusu upande wa Katibu wa mkuu wa chama hicho Maalim Seif wamepanga kuafanya kikao visiwani Zanzibar, jambo ambalo amesema kikao hicho ni batili kwakuwa hakina baraka zake na kwamba vyombo vya dola viwashughulikie Kwa kile alichodai kuwa watakuwa wamekiuka sheria namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imewateua 8 kuwa Wabunge wa Viti Maalum CUF

$
0
0
Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 86(8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 27 Julai 2017imewateua wafuatao kuwa Wabunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF).

1- Ndugu Rukia Ahmed Kassim;
2- Ndugu Shamsia Aziz Mtamba;
3- Ndugu Kiza Hussein Mayeye;
4- Ndugu Zainab Mndolwa Amir;
5- Ndugu Hindu Hamis Mwenda;
6- Ndugu Sonia Juma Magogo;
7- Ndugu Alfredina Apolinary Kahigi; na
8- Ndugu Nuru Awadh Bafadhili,

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo kwa nafasi waza nane (8) za Wabunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi CUF.

Jamii Forums

IJUE SHERIA: Namna ya kumsaidia ndugu yako kupata dhamana Polisi

$
0
0
DHAMANA NI NINI? 

Dhamana ni hatua ambayo mtuhumiwa wa kosa fulani huachiwa huru kwa muda, ili kusubiri hatua za kufikishwa mahakamani, au kama tayari amefikishwa mahakamani husubiri kuendelea na kesi kwa siku zijazo.

Kwa hiyo, ili lije suala la dhamana ni lazima uwe umetuhumiwa polisi au tayari umefikishwa mahakamani. Ieleweke kuwa kuna aina kuu mbili za dhamana. Kwanza dhamana ya polisi na pili dhamana ya mahakamani. Hapa tunazungumzia dhamana ya polisi.

UKIOMBWA FEDHA KWA AJILI YA DHAMANA KATAA

Dhamana hutolewa bure. Ieleweke wazi kuwa hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa ili mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana. Mchezo huu wa kuomba fedha ili mtu apate dhamana umetamalaki zaidi vituo vya polisi.

Wewe kama raia, unalotakiwa kujua ni moja tu kuwa hakuna sheria inayomtaka raia kutoa fedha ili apate dhamana. Serikalini hakuna risiti ya malipo ya dhamana. Kama wewe utaamua kutoa fedha hiyo ujue umetoa kwa sababu zako lakini sheria iko hivyo. Ifikie hatua raia wajisimamie kwa kukataa kutoa fedha kununua dhamana.

Hakuna kitu ambacho askari anaweza kukufanya ikiwa utakataa kutoa fedha kwa ajili ya dhamana. Hakipo kabisa kinachohitajika ni ujasiri wako tu kwa kumwambia askari kwamba ‘sikupi fedha kwa kuwa dhamana hainunuliwi.

Usikubali kutoa fedha kwa ajili ya dhamana, ni kosa na fedha hizo ni rushwa. Na hiyo ni kwa dhamana zote — ya polisi pia ya mahakamani. Katika taratibu za kupata dhamana hamna kulipa fedha.

POLISI WANALAZIMIKA KUKUPA DHAMANA

Hapo juu nimesema kuwa ili upate dhamana hutakiwi kutoa chochote kitu isipokuwa kuna mambo yanazingatiwa ili upate dhamana.

Baadhi ya mambo hayo ni haya;

(a) Kisheria ikiwa makazi yako au anuani yako ya makazi inajulikana vyema au haijulikani, lakini umewafanya polisi kuijua na wakajiridhisha kwamba kweli fulani haya ndiyo makazi yake, basi ni sababu ya kupatiwa dhamana. Hii ni kwa sababu lengo kuu la dhamana ni ili utakapohitajika upatikane kwa urahisi.

(b) Ikiwa kosa alilotenda mtu ni la kudhaminika, hakuna haja ya kuendelea kumshikilia. Sheria imeshaweka wazi makosa yapi dhamana ya mtu itolewe na makosa yapi isitolewe. Baadhi ya makosa ambayo mtu hatakiwi kupata dhamana ni kama kuua kwa kukusudia (murder), uhaini (treason), wizi wa kutumia silaha na kadhalika.

Ajabu ni kuwa kwenye vituo vyetu vya polisi unakuta hata mwenye kosa la kutukana naye ananyimwa dhamana. Hii ni kinyume cha sheria na muda umefika wa raia wenyewe kuyakataa haya.

(c) Pia kama mtuhumiwa hana kumbukumbu (criminal records) zozote za uhalifu, nayo ni sababu au kigezo cha kumfanya apewe dhamana haraka. Hakuna sababu ya kuendelea kumshikilia mtu ambaye kwa kumbukumbu hakuwahi kutenda kosa lolote la jinai hapo kabla. Kisheria kutokuwa na kumbukumbu za uhalifu hapo awali ni dalili za uaminifu na ukweli. Hii nayo ni sababu ya kisheria na yafaa izingatiwe sana huko vituo vya polisi.

(d) Pia ikiwa polisi itajiridhisha kwamba mtuhumiwa atatimiza masharti ya dhamana atakayopewa kama kufika siku na saa atakayoamriwa, basi hakuna haja ya kumng’ang’ania. Hii nayo ni kati ya sababu za kisheria ambazo huwa hazipewi nafasi kwenye vituo vya polisi na hivyo kuendelea kulifanya suala la dhamana kuwa gumu.

NAMNA YA KUJIANDAA NA DHAMANA

Ni vema sana unapopata taarifa za ndugu yako kushikiliwa kituo cha polisi kujiandaa na dhamana. Usitoke nyumbani kwenda kituoni bila kujiandaa na dhamana. Na hii ni iwe una uhakika amefanya kosa fulani au huna uhakika. Zaidi kama unajua kosa lake ni la kudhaminika basi umuhimu wa kujiandaa na dhamana huongezeka.

La kuzingatia sana; hakikisha unapotoka nyumbani una barua inayokutambulisha kwa suala la dhamana kutoka Serikali za Mitaa. Ukienda Serikali za Mitaa wanazijua hizi barua. Pia kama ni mwajiriwa usisahau kwenda na kitambulisho chako cha kazi.

Hii husaidia kutopoteza muda kwa kurudishwarudishwa huku ndugu yako akiendelea kusota polisi. Kwa kujiandaa utamwokoa ndugu yako na zahma ya kulala au kukaa selo. Usiende polisi ukiwa hujajiandaa kwa kuwa kufanya hivyo ni kupoteza muda tu.

OMBA KUJIDHAMINI MWENYEWE, INARUHUSIWA

Kuna watu wamekuwa wakikosa dhamana kwa kukosa wadhamini. Lakini polisi wamekuwa hawawaelezi watu hawa haki hii ya kujidhamini wenyewe. Mtu akikosa mdhamini na polisi nao wanakaa kimya mtu anaendelea kusota. Hili si sawa kwa kuwa moja ya majukumu waliyonayo polisi ni kuwaelimisha watuhumiwa haki zao za msingi.

Aidha, kama ulikuwa hujui ndiyo ujue kuanzia leo kuwa inaruhusiwa kujidhamini mwenyewe na ukaondoka kituo cha polisi bila kuhitaji ndugu yeyote kukudhamini.

Unachotakiwa kufanya kama uko mikononi mwa polisi ni kusema tu kwamba ‘nahitaji kujidhamini’ ili upewe fomu maalum uijaze na uondoke. Usisahau kuliomba hili ni haki yako.

By Allan Harold/JF

VIDEO: Lissu Achiwa Kwa Dhamana Asimulia Alivyoombwa Kupimwa Mkojo

$
0
0
Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imempa dhamana Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu Lissu .

Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo leo baada ya  Kusikiliza hoja za pande zote mbili.

Hata Hivyo Lissu ameesimulia alivyakataa kupimwa mkojo wake na Mkema Mkuu wa Serikali

Pata Matibabu ya Asili Kutoka Kwa ALLAH shalifu musa...Anatibu Kwa Nyota na Dua Matatizo Mbali Mbali

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shalifu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na ALLAH shalifu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
ALLAH shalifu musa Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali1 kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

Piga Simu +255 629793352 au 0679119679


NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Umesikia Habari ya Simba Kuchapwa Bao 7 Mechi ya Kirafiki?

$
0
0

Uongozi wa Klabu ya Simba wenye makao makuu yake Msimbazi Jijini Dar es Salaam umekanusha vikali taarifa iliyotembea katika mitandao ya kijamii inayodai timu hiyo imechapwa bao 7-0 katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Royal Eagles ya nchini Afrika Kusini walipoweka kambi yao.

Hayo yameweka bayana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa timu hiyo Haji Manara na kusema kama kweli wamechezea kichapo hicho kutoka kwa timu ya daraja la kwanza hakuna mtanzania asingeweza kuona matokeo hayo katika vyombo vya habari kutokana na sasa utandawazi umetawala.

"Kiukweli Simba haina rekodi za hovyo kama hizo kokote inapocheza duniani na haijawahi kufungwa na klabu yoyote idadi ya magoli kama hayo, kama zilivyo timu nyingine nchini hususan Klabu ambayo mashabiki wake ndiyo wanaozusha upuuzi huo", amesema Manara.

Kwa upande mwingine, Manara amewataka watanzania na mashabiki wa wekundu wa msimbazi watambue kuwa siku zote walizokuwa huko nchini Afrika Kusini, benchi lake la ufundi limejikita katika kutengeneza miili ya wachezaji kistamina ili iweze kufanya vizuri katika michezo yake ambayo ipo usoni kuanza.

Baraka The Prince Aendelea Kuiponda Lebo ya Ali Kiba RockStar4000...Afunguka Haya Mengine

$
0
0

Msanii Baraka The Prince amefunguka kwa kudai sababu kubwa zilizomfanya yeye kujiengua katika usimamizi wa kampuni ya RockStar4000 ni kutokuwa makini na ukweli katika kazi wanazozifanya dhidi yake.

Baraka amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuona takwimu zake zimezidi kushuka katika kazi zake alizokuwa anasimamiwa na uongozi huu pamoja na kutolewa nyimbo moja kwa mwaka tofauti na yeye alivyokuwa anategemea atafanya.

"Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu hii ndiyo kazi yangu na mwisho wa siku hii mimi ndiyo kila kitu na sina kazi nyingine, kwa hiyo nikiona kuna vitu havipo 'serious' na havipo 'sure' kwa upande wa watu ninaofanya nao kazi sina budi kujiengua na kufanya mwenyewe. Nipo sawa na hakuna mtu ambaye anaweza kuniingilia juu ya hilo mwisho wa siku mimi ndiyo ninajua kazi ninayofanya na ugumu wake katika kujenga 'brand' yangu, najua ugumu wa kila kitu 'so' haya ni maamuzi yangu", amesema Baraka.

Pamoja na hayo, Baraka ameendelea kwa kusema "mimi ndiyo mwenye kauli ya mwisho. Sitaki kuongelea masuala ya mikataba kwa sababu kipindi nina saini tokea awali sikuweza izungumzia wakati naingia kwa hiyo sitasema lolote juu ya hilo kwa sasa",amesisitiza Baraka.

Kwa upande mwingine, Baraka amesema yeye hafanyi muziki kwa ajili ya menejementi bali anafanya muziki kwa mashabiki wanamuwezesha kumlipa katika nyimbo zake wanazozipakua katika mitandao.

Waziri Mhagama Awachimba Mkwala Waajiri...Awapa Siku 30

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, ametoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao hawajasajili, kujisajili katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) na kutoa michango kwa wakati.

Mh. Mhagama ametoa agizo hilo leo jijini Mbeya wakati wa ukaguzi wa kushtukiza jijini humo na kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeleza Sheria ya fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 Marejeo ya Mwaka 2015 kifungu cha 5, ambayo inawataka waajiri wote kutoka sekta ya Umma na binafsi Tanzania Bara kujisajili kwenye mfuko huo.

Mhagama amefafanua kwamba, mwajiri ambaye hajajisajili kwenye mfuko, anaweza kufikishwa mahakamani na adhabu ni pamoja na kutozwa faini ya kiasi cha fedha kisichozidi shilingi milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka 5 jela au vyote kwa pamoja,
Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa kushtukiza Mh. Mhagama alifuatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi, Dk. Abdulsalaam Omar, na aliikagua hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati na Shule ya Sekondari ya Saint Aggrey iliyoko Uyole na kubaini kuwa taasisi hizo hazijajisajili katika mfuko.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images