Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live

TAKUKURU Yasababisha Shaffi Dauda Ajiengue Uchaguzi TFF

0
0
Mgombea wa nafasi ya ujumbe katika uchaguzi wa TFF na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania, Shaffih Dauda amejiondoa katika kinyang’anyiro hicho, siku 3 baada ya kuhojiwa TAKUKURU.

 
“Nimejitoa kwenye uchaguzi wa TFF, nitaendelea na harakati zangu za kuendeleza soka”

“Nimetumia muda mrefu kujenga brand yangu hakuna haja kuendelea kung’ang’ania. Suala la Rushwa ni kunichafua na mimi sitaki”. Amesema

Dauda ambaye alichukua fomu ya kugombea nafasi ya ujumbe katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Juni 17 mwaka huu, zilienea taarifa za kukamtwa kwake na TAKUKURU akiwa na baadhi ya wadau wa soka hapa nchini wakiwemo wagombea wa uchaguzi katika nafasi mbalimbali siku ya Jumatano ya July 26 2017.

KIMENUKA..Baraka The Prince aanika kile alichokiona ndani ya RockStar4000

0
0
Msanii Baraka The Prince amedai moja ya sababu ya yeye kuachana na label yake ya zamani ya RockStar4000 ni usimamizi mbovu juu yake.


Muimbaji huyo amedai takwimu zake zimezidi kushuka katika kazi zake alizokuwa anasimamiwa na uongozi huu pamoja na kutolewa nyimbo moja kwa mwaka tofauti na yeye alivyokuwa anategemea atafanya.

“Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu hii ndiyo kazi yangu na mwisho wa siku hii mimi ndiyo kila kitu na sina kazi nyingine, kwa hiyo nikiona kuna vitu havipo ‘serious’ na havipo ‘sure’ kwa upande wa watu ninaofanya nao kazi sina budi kujiengua na kufanya mwenyewe. Nipo sawa na hakuna mtu ambaye anaweza kuniingilia juu ya hilo mwisho wa siku mimi ndiyo ninajua kazi ninayofanya na ugumu wake katika kujenga ‘brand’ yangu, najua ugumu wa kila kitu ‘so’ haya ni maamuzi yangu”, Baraka aliiambia Enewz ya EATV.

Pamoja na hayo, Baraka ameendelea kwa kusema “mimi ndiyo mwenye kauli ya mwisho. Sitaki kuongelea masuala ya mikataba kwa sababu kipindi nina saini tokea awali sikuweza izungumzia wakati naingia kwa hiyo sitasema lolote juu ya hilo kwa sasa”,amesisitiza Baraka.

Kwa upande mwingine, Baraka amesema yeye hafanyi muziki kwa ajili ya menejementi bali anafanya muziki kwa mashabiki wanamuwezesha kumlipa katika nyimbo zake wanazozipakua katika mitandao.

MAALIM Seif Amvaa Job Ndugai Baada ya kuwafuta wabunge 8 wa CUF

0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi, CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kwamba hatua ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwavua Ubunge, Udiwani na kuteua wengine wapya inalenga kudhoofisha kambi ya Wabunge wa CUF na Muungano wa Ukawa.


Maalim Seif amesema, Watanzania wanapaswa wajikumbushe kwamba hata kama hicho kinachoitwa ‘kuwafukuza uanachama’ Wabunge halali wa CUF kingekuwa kiko sawa, hatua kama hiyo hufuata taratibu zote za kisheria na kikanuni za Bunge kujiridhisha kwanza.

Amesema Spika amejiridhisha vipi ikiwa hata hakuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama ambaye kwa mujibu wa Katiba ya CUF ndiye Mtendaji Mkuu wa shughuli za chama na pia kwa nafasi hiyo ndiye Katibu wa vikao vya Mkutano Mkuu wa Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama

Amesema yeye kama Katibu, alimuandikia Spika Ndugai barua, Jumanne, Julai 25 akimueleza kwamba hilo lililoitwa Baraza Kuu la Uongozi la CUF halikuundwa na wajumbe halali wa Baraza Kuu.

Ameongeza kwamba, Mh Ndugai ameyapuuza yote hayo kwa sababu ni kinyume na mkakati wa Dola wa kuihujumu CUF na kuua demokrasia Tanzania.

JUKWAA la Wahariri(TEF) Laikemea CHADEMA kwa Kuwafukuza Waandishi wa TBC ktk Mkutano wa Tundu Lissu

0
0
Jukwaa la wahariri limepokea kwa masikitiko taarifa za kufukuzwa kwa waandishi wa habari wa kituo cha runinga cha TBC wakati wakitekeleza majukumu yao.

Wamesema kwamba vitendo vya kuwabugudhi waandishi wa habari haviwezi kupewa nafasi katika jamii na Uongozi wa CHADEMA uchukue hatua stahiki kuhusu suala hili.

MUME Wangu Hanitoshelezi, Kimwili na Kimahitaji........!!

0
0
Mume wangu ana tatizo la kuwahi kumwaga. Yaani dakika 2 tu ameshamaliza na kuniacha nikiwa nateseka huku nikiwa nina hamu. Tatizo hili limekuwa linanisababishia maumivu ya tumbo na kiukweli nikiwa naye sikuwahi kufika kileleni na kwa kuwa alinioa nikiwa bikira sikuweza kugundua mapema tatizo ni la nani.

Muda mwingi nilikuwa najichukia na kuwaza huenda mimi ndio nina tatizo na yeye mwenyewe wakati nikilalamika alikuwa ananiambia kuwa mimi ndio nina tatizo kwanini kila siku sifiki kileleni; mara nilikuwa siko tayari basi tu ilimradi nionekane tatizo liko kwangu.

Basi siku moja niliamua kujaribu nje, lol sitasahau ilikuwa ndio siku yangu ya kwanza kujua raha ya mapenzi. Sasa toka wakati huo nimekuwa simpendi kabisa mume wangu na nina mpango niachane naye kwani mbali na kutokuwa mzuri kitandani pia hatoi huduma kwa familia, kiufupi ni mvivu kila idara.

Naombeni ushauri wenu nifanyeje ili niweze kuachana naye coz siwezi kuishi na mume ambaye anamaliza haja zake tu (mbinafsi).

ALICHOSEMA John Mnyika Baada ya Spika Kubariki Kufutwa Uanachama Wabunge 8 wa CUF

0
0
Mbunge wa Kibamba John Mnyika leo July 28, 2017 ameielezea hatua ya Spika Ndugai kubariki kufutiwa uanachama Wabunge wa Viti Maalumu wa CUF akisema ni makosa kwa kuwa kuna kesi Mahakamani kuhusu utata wa uongozi wa Chama hicho.

Aidha, Mnyika amemuomba Spika kutangaza wateule ambao wametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi July 27, 2017 kuwa hawataapishwa mpaka mashauri yao yaliyopo Mahakamani yamalizike.

Hatua ya John Mnyika imekuja siku chache baada ya Spika kuridhia kufutiwa uanachama Wabunge wanane wa CUF baada ya kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wake Prof. Lipumba kisha kutangaza nafasi zao kuwa wazi na kumuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya taratibu zilizostahili ambapo alitangaza majina ya Wabunge wengine wanane kuziba nafasi zao.

MWANAMKE Usiringie Shep, Mwanaume Usiringie Hela, Bahati tu ndo ya Kuringia.....

0
0
Unaweza ukawa na shep kama umeshushwa vile, yaani hujazaliwa, lakini kama huna bahati ni kazi bure. Utakuwa na furaha kipindi ambacho umevaa nguo tu unatembea huku wanaume wakikuangalia kwa macho ya tamaa na kukusifia.

Jiheshimu, mheshimu ulokuwa nae, kisa una shep, unaamini hata ukiachwa Leo utapata mwingine. Utamaliza waganga ukitafuta mume. Wenzako na shep zao za mstatili wanaolewa tu, shauri yako .



Mwanaume pesa zisikupe kiburi, utaishia kupendwa na wanawake wanaokuja kwa ajili ya hela zako tu, kisa umepata hela unamdharau mloanza nae maisha , kuanzia ukiwa kapuku mpa unaitwa boss,unamwambia sio hadhi yako, utakuwa unamkosea sana.

Usidharau ulichokuwa nacho. Kikitoweka utakikumbuka
Laana sio lazima uipate kwa mzazi alokuzaa tu.
Ujana haubagui.

WEMA Afunguka Mazito Baada ya Ndugu yake Kupigwa na Polisi Mahakamani

0
0
Moja ya story ambayo inatrend kwa sasa kwenye mitandao mbalimbali ni pamoja na issue aliyoiandika Mwigizaji staa wa Bongomovie na Miss Tanzania 2006 Wema sepetu katika ukurasa wake wa Twitter akizungumzia hali ya mtu aliyedai ni ndugu yake.

Wema ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter leo July 28, 2017 akisema:
”Ninachojua mimi ni kwamba Binadamu ana haki ya kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya ndugu yake… Imeniuma sana kilichomtokea kaka angu jana. Only now nakuja kujua kwamba alichukuliwa na mapolice wakaenda kumpiga mpaka sasa yupo hospital amelazwa.




KABLA Ya Kufanyia Kazi Ushauri Wa Kibiashara Unaopewa, Zingatia Haya

0
0
Kama kuna kitu ambacho kila mtu anaweza kushauri kadiri ya utashi wake, basi ni ushauri wa kibiashara. Watu wengi wamekuwa wakipokea ushauri wa biashara unaotolewa na kila mtu, tena kwa bure, lakini wanapoufanyia kazi ndipo wanagundua haukuwa ushauri mzuri.

Kila kipindi kuna aina za biashara ambazo huwa zinashabikiwa na watu wengi, biashara ambazo kila mtu anaongelea na wale wanaozifanya kuonekana waipata faida. Hapa ndipo unakuta kila mtu anashauriwa kuingia kwenye biashara hiyo, kwa sababu ndiyo ‘habari ya mjini’ kwa wakati huo na hivyo wengi wanakimbilia kuchukua hatua kabla fursa haijawapita.

Changamoto nyingine kubwa inayowafanya watu kupewa ushauri ambao siyo makini kwenye biashara ni kutokuwa tayari kulipa gharama za ushauri. Wengi wamekuwa wakichukulia ushauri kama kitu kidogo ambacho hakipaswi kulipiwa. Hivyo wanachukua ushauri wa bure ambao unawaumiza sana.

Leo tutakwenda kujifunza mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kufanyia kazi ushauri wowote unaopewa kibiashara. Kwa kuzingatia mambo haya utaepuka kufanya maamuzi ya msukumo ambayo yatakuingiza kwenye hasara.

Jambo la kwanza; fanya utafiti wako mwenyewe.
Usipokee maneno ya watu na kuyaamini kwa asilimia mia moja. Fanya utafiti wako kujua kama kweli biashara unayoambiwa inalipa kama ni kweli. Angalia ukubwa wa soko la biashara hiyo, ona ni kwa kiasi gani bado wateja hawajafikiwa. Pia angalia uwezekano wa kukua zaidi kwenye biashara hiyo. Fanya utafiti wako mdogo kulijua soko na hata kuwajua wale waliopo kwenye biashara hiyo kwa sasa.

Jambo la pili; ongea na wale wanaofanya.
Kwa kuwa umesikia biashara inalipa, usifikiri kwamba haina changamoto zake. Na ili kujua changamoto za biashara yoyote, angalia wale ambao wanafanya biashara hiyo. Ongea nao au wafuatilie ili kuona changamoto yao hasa ni nini. Ni vyema ukazijua changamoto za biashara yako mapema kabla hata hujaingia ili uweze kupambana nazo.

Wengi wa wanaoshindwa kwenye biashara mpya ni kutokana na kukutana na changamoto ambazo hawakuzitegemea hapo awali.

Jambo la tatu; mwangalie yule anayekupa ushauri wa biashara.
Watu wengi wamekuwa wakitaka kusikia tu ushauri mzuri wa biashara, hivyo wakiusikia hawajali anayewaambia ni nani. Hivyo unakuta mtu kasikia wengine wanasema biashara fulani inalipa, na yeye anatoka na taarifa hizo kuja kukupa wewe. Hajafanya utafiti wowote na wala hana utaalamu wa biashara, ila amesikia inalipa na anakuambia na wewe ukafanye kwa sababu inalipa.

Hakikisha mtu unayechukua ushauri wa biashara kwake ana utaalamu wa biashara au anafanya biashara hiyo anayokushauri ufanye. Kama na yeye amesikia inalipa ila hajui kwa kina kuhusu biashara hiyo, ni vyema ukaokoa muda wako au kufanya utafiti zaidi kabla hujaingia kwenye biashara hiyo.

Ni rahisi kushauri kuliko kufanya, hivyo mara zote unapopokea ushauri chunguza kwa makini kabla hujachukua hatua. Usiharakishe kufanyia kazi ushauri unaopewa kwa sababu tu unaonekana ni biashara itakayokulipa. Fanyia kazi ushauri unaopewa na utoke na mpango ambao unaweza kuupigania mpaka kufanikiwa kwenye biashara yako.

RAIS Magufuli Amtumbua 'Kigogo' Uhamiaji

0
0
Rais John Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa naibu kamishna wa uhamiaji kwa tuhuma za kuingiza nchini humo raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi.

Kupitia waziri mkuu Kassim Majaliwa kiongozi huyo ametaka kusimamishwa kazi mara moja kwa bi Grace Hokororo na kuundwa kwa tume itakayochunguza utoaji wa vibali vya uraia nchini humo.


Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji kilichofanyika katika makao makuu ya uhamiaji jijini Dar es salaam.

Tayari Majaliwa amemuagiza waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kubuni tume hiyo ya uchunguzi.

Amesema kuwa haiwezekani raia wa kigeni kuingizwa nchini humo na baadaye kupewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.

"Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu."

Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini ni kitu gani kilichomsukuma kuwapatia vibali Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini.

''Wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi kuivumilia."

Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu.

"Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ili kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."

Pia majaliwa ameiagiza idara ya Uhamiaji kudhibiti kitengo cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda kutopewa tena.

" Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya."
Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi iwapo wanakidhi matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.

PAUL Makonda Atoa Siku 10 mji wa Dar Kufungwa CCTV.

0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amefanya mkutano leo na wadau mbalimbali jijini Dar kwa ajili ya ufungaji wa mfumo wa ufuatialiji wa makosa mbalimbali yanayotokea hapa Dar ikiwemo ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani zinazofanywa na baadhi ya madereva wa magari.

Ametoa siku kumi kwa tume atakayoiunda ije na majibu ya suluhisho la namna mfumo huo utakavyoweza kufanya kazi,ameeza kwamba, "wako wataam walishakwenda mpaka China na serikali kugharimia safari na mafunzo tangu serikali ya awamu ya nne na akaagiza CAMERA zifungwe lakini mpaka leo hakuna lolote"

Alisema,"Sasa mimi siendi nchi yoyote nipo hapahapa Dar es Salaam na nitahakikisha CAMERA zitafungwa".

Mfumo huo ni Tanzania Tracking Technology of Security Monitoring System. Mfumo huu waweza kusaidia kutambua aina ya gari,jina la driver na hata kuweza kuzima/switch off gari iliyoibiwa.

HOMA ya Ini Hatari zaidi ya UKIMWI

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa homa ya Ini umetajwa kuwa ugonjwa hatari zaidi na wenye kuuwa watu wengi polepole, huku takwimu zikiwa zinaonyesha una maambukizo makubwa mara 10 kuliko

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
ya UKIMWI.

Mhe. Ummy amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari katika kilele cha maadhimisho ya siku ya homa ya Ini duniani yaliyofanyika leo.

"Nikiwa Waziri mwenye dhamana ninachotaka kuwaeleza Watanzania kwamba ugonjwa wa homa ya Ini umetajwa kuwa ugonjwa wa hatari na unaouwa watu wengi polepole. Kati ya watu 100, wanane wanaweza kuwa na maambukizi sugu ya ugonjwa huo na mbaya zaidi wanaweza wasiweze kuonyesha dalili za ugonjwa", amesema Ummy.

Pamoja na hayo, Waziri Ummy ameendelea kwa kusema "kwa mara ya kwanza ugonjwa huu unapewa kipaumbele unaostahili na kupitishwa na Shirika la Afya duniani katika mpango mkakati wa kwanza wa homa ya ini na kuanza kufanya kazi kuanzia mwaka 2016 mpaka 2021. Sisi serikali ya Tanzania tumekubali mkakati huu wa kwanza kwa maana tunataka kutokomeza kabisa ugonjwa huu", amesema Ummy.

Kwa upande mwingine, Ummy amesema kati ya watu laki mbili mwaka jana (2016) waliochangia damu, asilimia sita wamekutwa na maambukizi ya virusi vinavyosababisha homa ya Ini.

Utajiri wa Dangote wapungua

0
0
Bilionea raia wa Nigeria Aliko Dangote ameshuka katika nafasi ya watu matajiri duniani hadi 105 kutoka nafasi ya 51.

Jarida la Forbes limeripoti kwamba mali za Dangote zimepungua kutoka dola bilioni 15.4 mwaka 2016 hadi dola bilioni 12.2 mwaka huu kutokana na kushushwa thamani kwa sarafu ya Nigeria.
 Dangote alijipatia utajiri wake kupitia uzalishaji wa saruji, sukari, na unga wa ngano. Aligonga vichwa vya habari 2016 wakati aliposema kuwa alitaka kuinunua klabu ya soka ya Arsenal katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Hapo jana Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos alimpiku Bill Gates kwa muda mfupi kama mtu tajiri duniani kabla ya kushuka hadi nafasi ya pili.

USHAURI Mchumba Wangu Anatembea na Lecturer wake

0
0
Mimi ni kijana wa kitanzania, najitokeza hapa mbele yenu kuomba ushauri kwa haya makubwa yaliyonikuta.

Nilianza chuo miaka mitatu iliyopita, nikimaanisha kwa sasa nipo mwaka wangu wa mwisho katika hii kozi ninayoichukua. Nilianza chuo bila kuwa na uhusiano wowote ule wa kimapenzi na msichana hapa chuoni kwa mwaka wote ule wa kwanza.

Hali hiyo ilibadilika baada ya kuingia mwaka wa pili, kwani kipindi hicho kukawa na mwaka wa kwanza wanaingia na bahati nzuri nikatokea kumpenda msichana mmoja mrembo wastani sema ni mstaarabu haswaa. Nilijaribu bahati yangu na mungu si athumani huyu msichana akanikubalia na tukaanza mahusiano yeye akiwa mwaka wa kwanza,mimi wa pili. Tuliishi kwa amani na  furaha kwa kipindi chote kile(nikimaanisha semester zote mbili za mwaka wangu wa pili).

Kinachonifanya kuandika hapa ni hiki sasa, mwanzoni mwa semester iliyopita nilianza kusikia tetesi kutoka kwa marafiki zangu ya kuwa huyu msichana niliye naye anatoka na mmoja wa ma-lecturer wanaomfundisha. Sikuliamini hilo, nikaamua kumuliza mwenzangu kwamba nimesikia hili na hili, je kuna ukweli wowote? Alikataa kata kata na kusema huo sio ukweli na nisiamini kila ninalolisikia, kwa kuwa ni mstaarabu sana na kwa jinsi alivyokuwa akiongea basi nikamuelewa kwa muda ule.

Ila sikuishia hapo nikaendelea na uchunguzi wa chini chini bahati mbaya sikuambulia lolote kuhusu uhusiano wake na  huyo lecturer zaidi ya yeye kuwa na ratiba ya  kwenda kwao kila baada ya wiki mbili kuanzia ijumaa jioni mpaka jumapili ambao ni utaratibu wake toka anaanza chuo. Na hiyo ijumaa mpaka jumapili akiwa nyumbani mawasiliano yalikuwa yakipungua sana kwa sababu alikuwa akisema anakuwa busy sana na shughuli za nyumbani kwao na hata usiku ukimpigia simu alikuwa hapokei kwa madai analala na ndugu yake na kwahiyo atakuwa anampigia kelele.

Leo mchana sasa, nilimpigia simu twende tukapate chakula cha mchana lakini alikataa na kuniambia kuna kazi anaifanya kwanza mpaka aimalize ndio ataenda kula, mimi nikatangulia kwenda kula ila wakati narudi nikakutana na rafiki yangu, akaniuliza mbona nimekutana na bibie(mchumba wangu) anakula na Mr. X (huyo lecturer niliyeambiwa anatembea naye ) sehemu flani(ma-lecturer wengi ndio wanapokula hapo na kama utakuta wanafunzi basi ni mmoja mmoja ambao wako vizuri sana kifedha)… sikuamini, nikaenda kuhakikisha… Nilichokiona aisee sikuamini macho yangu, wote wawili walikuwa wamekaa wakipata lunch tena wakionekana wenye furaha.

Nilimpigia simu lakini hakupokea, aliishia kuiangalia tu simu yake na kuirudisha kwenye meza… Nikamtumia meseji ya kwamba nimemuona na nimezima simu yangu mpaka sasa, hapa natafakari nimfanyaje huyu msichana kwa hili alilonifanyia??? It hurts kwa kweli ikizingatiwa huyu lecturer ana mke kabisa so what if ndio tabia yake hiyo kutemebea na wanafunzi? Si  ndio kuambukizana magonjwa huku??

Naombeni ushauri wenu , nimfanyeje huyu kiumbe??

MWANAMKE Msagaji Ameniomba Nimpe Ujauzito ili Azae Mtoto

0
0
Kuna dada mmoja nje ya nchi ambaye anataka kuja hadi hapa Sikonge ili nimtungishe Mimba na hatimaye azae mtoto. Huyu mdada ni mtu ambaye ninafahamiana naye kwa miaka mingi kidogo tangu nikiishi nje ya nchi ambapo siku hizo, hakuwa au nilikuwa sijajua kama ni SHOGA.

Anasema yupo tayari kuwekeana kabisa mkataba na mie kwamba gharama zote za mimba na kulea mtoto hatanidai na mtoto ataandikishwa kwa jina lolote nitakalokubali mie na hata akitaka atanilipa. Sijui kaona kitu gani cha ajabu kwa Mnyamwezi mie ingawa kiukweli hadi leo hii sijawahi hata kumbusu, acha kutembea naye.
Kuhusu Mimba anasema inaweza kuwa kwa njia ya kawaida kwa kufanya mapenzi au kwenda hospital na huko wakafanya kupandikiza kama wanavyofanya kwa wale wanaotoa mbegu za Kiume na kuwapa akina mama ambao hata hawawajui.

Shida kubwa iliyopo ni kuona kuwa Mtoto wangu anaweza kukulia kwenye familia au nyumba ambayo Mama anaishi na GIRLFRIEND wake na kwa maana nyingine ni kwamba, hawa ni Wasagaji. Mbaya zaidi kakiwa ka kike, si ndiyo itakuwa shida kwa mtoto huyo? Itabidi ajifunze kuwa Mliberali mapema sana au aungane nao.

Hebu nyie wakali na wazoefu wa haya mambo mniambie, kwa hili NIKUBALI au NIKATAE?

ANGALIZO: Hii ni habari ya kweli, utani pembeni Bandugu.

Pata Tiba za Asili Toka Kwa Chief Sultan Makata...Anayetibu Kwa Kutumia Nyota na Dua ....

0
0

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika
Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote


..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Chief Sultan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14.

Na Mengi zaidiWhatsapp/Calls +255 710 279 458 
+255 710 279 458 

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

SPIKA Job Ndugai Ageuziwa Kiba, Magufuli Kikwete Wazidiana Kete....Magazeti ya leo Jumamosi....!!

0
0


SPIKA Job Ndugai Ageuziwa Kiba, Magufuli Kikwete Wazidiana Kete....Magazeti ya leo Jumamosi....!!

TUNDU Lissu Kiboko yao...Afunguka Makubwa 'Nitanyamaza Nikifa tu Lasivyo'

0
0
Mwanasheria  Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusema kuwa atanyamaza tu baada ya kufariki dunia.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alipata dhamana jana baada ya mahakama hiyo kubaini hoja za Serikali za kumnyima haki hiyo hazina mashiko.

Baada ya kutoka mahakamani, alikwenda katika ofisi za Chadema zilizopo Kinondoni, ambako pamoja na mambo mengine, alisema ataendelea kuikosoa Serikali hadi pale atakapokufa.

“Hakuna gereza litakalotunyamazisha, watu wakipelekwa mahabusu watazungumza wakiwa mahabusu, wakifungwa watazungumza wakiwa kifungoni, hivyo ili wanyamaze itabidi kwanza wafe… tutanyamaza tukiwa wafu kwa sababu wafu hawasemi,” alisema.

Lissu alisema kuna haki ya kuwasema na kuwakosoa wale waliopewa madaraka na wananchi.

Alisema katika sheria ya uchochezi ya mwaka 1953, kutoa kauli yoyote yenye lengo la kukosoa matendo ya Serikali, sera si kosa na wala kumkosoa rais na Serikali yake si kosa.

“Sasa ukisema wanakukamata, wanakushtaki kwa uchochezi, wanakupiga, wanakupeleka central (kituo kikuu cha polisi) au Oysterbay wakikupeleka sio kosa, bali unatumia akili zako kuikosoa Serikali,” alisema Lissu.

Akizungumzia kuhusu kupimwa mkojo, Lissu alisema alipelekwa na askari kwenye nyumba iliyo karibu na Ocean Road, lakini alikataa kutekeleza hilo.

“Niliwaambia nyie maaskari mimi nimeshtakiwa kwa uchochezi, unathibitishaje uchochezi kwa kupima mkojo?” alisema Lissu.

Alisema askari hao walimjibu kuwa kuna vitu wanavitaka, akawaeleza: “Nendeni mkanishtaki, hamjapata oda ya hakimu, hamtaona mkojo wangu.”

Baada ya kauli hiyo, alisema askari hao walimwambia kuwa wao wana mamlaka.

“Nikawaambia mimi ni Rais wa Mawakili (TLS). Siku ukikamatwa, ukaambiwa kupimwa damu, mkojo waambie hutaki hata kama wamekushtaki.

“Ukitoa mkojo na usiposaini hakuna dili, walichokuwa wanatafuta wapate dili ya kutengeneza ‘headline’ (kichwa cha habari), ‘huyu anasema hivi kwa kuwa anatumia dawa’, nani asiyejua polisi wanabambika? Nikakataa, nikawaambia mnataka twende kunisachi twendeni.”

Lissu alisema akiwa Segerea alikutana na wafanyabiashara James Rugemalira na Harbinder Singh Sethi wanaokabiliwa na kesi ya uhuhumu uchumi na utakatishaji fedha.

“Mwaka jana nilisema hawa lile dili (kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow) watu lazima wawajibike, waliowapa hela, waliosaini BoT (Benki Kuu ya Tanzania), walioruhusu hizo fedha kwa kusema James Rugemalira na Harbinder Singh wapewe wako wapi?” alihoji.

Lissu alihoji wapi walipo waliopewa mgawo wa fedha za Escrow.

Kabla ya kutoa uamuzi wa dhamana jana, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri, alipitia hoja za pande mbili zilizokuwa zinapingana, zilizowasilishwa mahakamani hapo mwanzoni mwa wiki.

“Hii kesi ina dhamana, hoja kwamba anakabiliwa na kesi nyingi zenye viashiria va uchochezi haina mashiko kwa sababu hakuna taarifa kuwa aliwahi kuruka dhamana.

“Kwangu mimi hiyo haitoshi kumuweka mahabusu, hoja ya kwamba aendelee kuwepo rumande kwa usalama wake, hakuna taarifa kwamba akipewa dhamana maisha yake yatakuwa hatarini.

“Mshtakiwa anawakilishwa na mawakili 18 wanaomuombea dhamana, wanafanya hivyo kwa upendo walionao dhidi ya mshtakwa, hivyo haiwezekani akipewa dhamana atadhurika.

“Mahakama inakubali maombi ya dhamana, mshtakiwa atadhaminiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili, watasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10 kila mmoja na mshtakiwa hatakiwi kusafiri bila kibali cha mahakama,” alisema.

Baada ya kutoa masharti ya dhamana, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi kwa nusu saa ili watafutwe wadhamini hao ambao walipatikana kwa juhudi za Wakili Peter Kibatala aliyetoka nje ya mahakama kuwatafuta.

Awali wadhamini hao walishindwa kuingia eneo la mahakama kutokana na kuimarishwa kwa ulinzi kulikotokana na kuwapo kwa kesi za ugaidi mahakamani hapo.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali Mkuu, Simon Wankyo, alidai mahakamani kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 24, mwaka huu kwa kuanza usikilizwaji wa awali.

Lissu alidhaminiwa na wadhamini wawili walioweka dhamana ya maandishi ya Sh milioni 10 kila mmoja.

MBOWE Amvaa Humphrey Polepole...Adai Ndio Kwanza Anajifunza Siasa

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amejibu kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole aliyesema kuna mtu mzito wa Chadema atakayehamia chama tawala hivi karibuni.

Mbowe amesema kuwa Chadema haiwezi kutetereka kwa kuondoka kiongozi yeyote kwani imejengwa katika misingi imara kama taasisi isiyotegemea mtu.

“Kwanza kabisa sitaki kuzungumzia propaganda za Polepole ambaye najua anajifunza siasa. Wapo wazito zaidi waliohama au kufukuzwa. Lakini niseme tu chama hiki kina misingi yake, mtu awe mdogo au mkubwa ni tafsiri tu, ingawa wapo wenye mchango mkubwa,” Mbowe anakaririwa na Mtanzania.

“Mtu yoyote anaweza kuondoka lakini Chadema kama taasisi itabaki imara. Mimi kama Mwenyekiti ninajua tumejenga taasisi imara ambayo haiwezi kutetereka kwa wanachama au kiongozi wa ngazi yeyote kuondoka,” aliongeza.

Kauli hiyo ya Mbowe imekuja wakati ambapo kumekuwa na matukio ya madiwani wa Chadema kuhamia CCM katika mikoa ambayo inasadikika kuwa ni ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani kama Arusha na Kilimanjaro.

Mwenyekiti huyo wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai amesema kuwa walifahamu hatua za madiwani hao zaidi ya 10 kufanya kile alichokiita usaliti hata kabla hawajatangaza kuhama.

NIONYESHE Demokrasia Ndani ya CHADEMA, Nami Nitakuonyesha Udikteta Ndani ya UKAWA

0
0
Na Fred Mpendazoe

Wakati Zitto Kabwe anafukuzwa ndani ya, Freeman Mbowe aliwaaminisha watanzania kuwa Zitto ni Msaliti na kwamba hastahili kushirikiana kwa lolote na msaliti. Freeman Mbowe akaendambali kwa kusema kuwa Zitto anashirikiana na
Serikali na CCM kuihujumu CHADEMA wakitoa
mfano wa Waraka wa Siri wa Zitto Kabwe.

Taarifa zipo zikionyesha kwamba Mwaka 2004, Freeman Mbowe alifanyamarekebisho ya Katiba ya CHADEMA kinyemelakwa kuondoa ukomo wa uongozi ili awe
Mwenyekiti wa kudumu, sifa mojawapo ya
kiongozi dikteta. Hadi Leo hii kila kiongozi anayetaka
kugombea uenyekiti wa CHADEMA anafukuzwa uanachama kamailivyotokea kwa ZITTO
KABWE. Yaliwakuta pia akina Kitila Mkumbo na
Samson Mwigamba. Je Mh Tundu Lissu hiyo ni demokrasia pana ?

Mchakato wa kumpata mgombea wa UKAWA hakika umeacha maswali mengi na wengiwamekuwa na majeraha yasiyopona. Ni sababuya Dr Slaa kuachia nafasi ya Katibu Mkuu CHADEMA na Prof Lipumba kuachia nafasi ya Mwenyekiti wa CUF. Hakukuwa na ushindani
wowote ndani ya CHAMA wala ndani ya UKAWA. Ni udikteta wa viongozi ndani ya Ukawa ndio uliofanya
CHADEMA kumteua Lowasa kuwa mgombea Urais tena akiwa mwanachama wa chama hicho kwa siku zisizozidi 10 tu.

Mwaka 1967 Mwl Nyerere alisema, "udikteta ni Serikali ya mtu mmoja au kukundi cha watu wachache na wao ndiyo huwa sheria. Anayepinga watakayo, basi huonyeshwa cha mtema kuni. "

Udikteta haufanywi na kiongozi wa Serikali tu. Udikteta unaweza kufanywa na mtu au kikundi cha watu nje ya Serikali.

Kuna kikundi au mtu mmoja ndani ya Chadema ambaye huamua anayotaka na akitokea mtu mwenye maoni tofauti hutwa msaliti kama ilivyotokea wakati wa kumwonyesha cha mtema kuni Mh Zitto, Mh Kitila Mkumbo, Mh Kafulila na kumpokea Mh Lowassa. Lakini hayo yote hayamkasirishiMh Lissu na haoni sababu ya kuyapigania. Ni unafiki.

Kwa nini Mh Lissu hatoi taarifa Polisi ya kufanya maandamano ya kupinga uonevu na kudai haki na demokrasia ndani ya Chadema ? Kwa nini Mh Lissu haondi boliti hiyo kwenye Ukawa na ndipo atuonyeshe fulana yake iliyoandikwa ukuta ?. Upuuzi.

Demokrasia ipi anayoidai Mh Lissu wakati demokrasia ndani ya Chadema imewashinda?

Nionyeshe demokrasia ndani ya Chadema , nami nitakuonyesha Udikteta ndani ya Ukawa.
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live




Latest Images