Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Unampenda au unajilazimisha? Jipime kwa maswali haya

$
0
0

Watu wengi wako kwenye uhusiano wa kimapenzi bila kujua kama kweli wanapenda kwa dhati au wanajilazisha? Ili kutambua upendo wako jipime kwa maswali yafuatayo:

1 - Unapoamka asubuhi wazo la kwanza kukujia linamhusu mpenzi wako au unafikiria zaidi kazi na mambo mengine? Una msukumo wa kutaka kumsalimia na pengine kumuuliza anapenda afungue kinywa kwa chakula gani?

2 - Je umekuwa mwepesi na mwenye furaha kubwa kuwaambia rafiki zako wa karibu juu ya hisia zako kwa mpenzi wako? Unajisikiaje wanapokushawishi vibaya kuhusu yeye?

3 - Je, anapokwambia anakuja kukutembelea huwa unajisikia hamasa moyoni kiasi cha mwili kusisimka?

4 - Unapokuwa peke yako mawazo yako yanatawaliwa na yeye au unafikiria kucheza gemu kwenye simu yako na kujifariji kwa vitu vingine?

5 - Unapompima kwa kumlinganisha na wengine anachukua nafasi ya kwanza au anazidiwa?

6 - Je, unapomfikiria na kupata kivutio fulani ndani ya moyo wako kuhusu ucheshi na utani wake huwa unatabasamu hata ukiwa peke yako?

7- Unajisikiaje wazo la kusalitiwa linapokujia, unaona ni sawa au unahuzunika kiasi cha kupoteza furaha na kutamani uambatane naye kila aendako ili usiibiwe?

8 - Hebu jiulize ni mara ngapi umekuwa ukishawishika kumnunulia mpenzi wako nguo, mapambo au vitu kwa lengo la kumfanya avutie au ndiyo umemtelekeza na kumwacha aonekane mchafu na asiyevutia mbele za watu?

9 - Je, umekuwa mtu wa kujijali mwenyewe kwa mavazi na mwonekano wako kwa lengo la kumfanya mwenza wako afurahie kuwa na wewe au ndiyo unajiweka katika mazingira ya ovyo yanayomtia aibu kwenye jamii?

10 - Unapoota ndoto za kimapenzi usiku, amekuwa akikutokea yeye au kuna wanaume/wanawake wa pembeni ndiyo wanajitokeza katika kuota kwako?

11- Unaposikiliza nyimbo za kimapenzi huwa unahisi ujumbe huo ni kwa huyo umpendaye au unauelekeza kwa mtu mwingine?

12 - Je, marafiki wa karibu wa mpenzi wako wamekuwa wakikupa kipaumbele au wanakudharau na kutopenda kukutana na wewe?

13 - Unajisikia furaha kuwa naye au huwa unapenda ubaki mwenyewe nyumbani ili ufanye mambo yako unayodhani uwepo wa mpenzi wako ni kikwazo?
14 - Je, umekuwa ukitafuta kwa nguvu nafasi za kukutana na mwezako au ndiyo kila siku uko bize na kazi?’

15 - Unapomtathmini mpenzi wako unajiona umepata au umejishikiza wakati ukitafuta mwingine?

16 - Umekuwa mwepesi kiasi gani kukumbuka ahadi zako kwake au kila unachopanga kumfanyia unasahau? Kumbuka kuhusu kumpigia simu, umekuwa ukijikuta ukisahau mara kwa mara?

17 - Vipi mpenzi wako anapopata nafasi ya kukushika sehemu yoyote mwilini wako, huwa unahisi msisimko mkali au mpaka ulazimishe hisia?

18 - Je, uko tayari kumwamini kiasi cha kumwekea dhamana?

19 - Kama utasikia mpenzi wako anakusifia kwa wenzake au kukuthamini kwa lolote utajiona mwenye bahati duniani?

20 - Unapofikiri hadhi yako unaona inalingana na mwenzako au unahisi umemzidi na kwamba mapenzi yako ni kama umemsaidia kumweka juu?

21 - Unapopata siku ya kupumzika, mtu wa kwanza kumpa kipaumbele cha kujumuika naye ni huyo mpenzi wako au unapenda kufanya mambo mengine?

22 - Je, umekuwa ukitamani kumpigia simu kwa lengo la kusikia tu hata sauti yake na ukahisi furaha?
Mpenzi msomaji wangu, haya ni baadhi ya maswali ya msingi ambayo majibu yake yanaweza kukusaidia kujua kama unampenda au unaulazimisha moyo wako. Naomba ukae peke yako na ujibu maswali haya ambayo mengi yako kwenye msingi wa jibu la ndiyo au hapana.

TANZIA...Mmiliki wa Impala Afariki Dunia

$
0
0

Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Mwananchi ndugu wa marehemu,Vincent Laswai alithibitisha msiba huo akiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha.

Akihojiwa na gazeti hili Laswai amesema kwamba alipokea taarifa za kifo cha marehemu jana saa 12 jioni na uongozi wa familia utatoa taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo leo.

Laswai, amesema kwamba ni mapema kuzungumzia chanzo cha kifo kwa sababu bado hawajapata taarifa kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini humo.

Hivi karibuni marehemu Mrema alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ambapo Juni mwaka huu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.


MAJI Kukatwa Dar, Pwani........

$
0
0
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini hapa (Dawasco) limesema kesho kutakuwa na katizo la maji kwa saa nane kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni kwa maeneo ya mkoa wa Pwani na Dar.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo leo, imeelezwa kuwa sababu ya kukata maji ni kuzima mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu ili kukamilisha mfumo wa umeme kwa mtambo mpya.

Dawasco imesema mtambo huo wa Ruvu Juu upo Mlandizi, Pwani na kuwataka wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi hicho.

Taarifa hiyo iliyataja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu na Picha ya Ndege.

Mengine ni Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba njia panda shule ya Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Kimara, Ubungo na baadhi ya maeneo ya Tabata.


UCHIMBAJI Kokoto Wapigwa Marufuku Kunduchi

$
0
0

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imependekeza eneo la Kunduchi Machimbo lirasimishwe kuwa eneo la makazi.

Taarifa ambayo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Mipangomiji Manispaa ya Kinondoni, Maduhu Ilanga, inasema kwamba eneo hilo lilimilikishwa kwa wachimbaji mbalimbali ambao walimilikishwa kwa kupatiwa leseni za uchimbaji wa kokoto na mawe.

"Eneo hilo lilikuwa na leseni za uchimbaji na leseni zake ziliisha Machi 30, 2010,'' inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema kwamba Machi, 2006,Serikali iliamua kupiga marufuku shughuli za uchimbaji wa kokoto na mawe katika eneo la machimbo la Kunduchi, uamuzi huu wa Serikali ulifikiwa baada ya kudhihirika kuwa kulikuwa na uchimbaji usiozingatia sheria ukiendelea na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwemo Barabara Kuu iendayo Bagamoyo.

MZEE Mkapa Yuko Sahihi,Tanzania Kuna Wajinga na Wapumbavu....

$
0
0
Ulishaona nchi wageni wanawafanyia wazawa mambo ya ajabu halafu baadhi ya wanainchi wanashangilia!

Rais anasafishasafisha uchafu Serikalini baadhi ya wanainchi hawataki.!!

Viongozi wanaiba rasilimali za nchi na Rais anahakikisha viongozi wote wa hivyo wanatimuliwa na kushtakiwa baadhi yetu wahataki

Sasa tuwaitaje watu kama hao ambao kila Kitu wao hawataki.

By tramadol

RC Geita Amzuia Waziri Kuzindua Filamu Yenye Utata ya Magwangala......

$
0
0
Uzinduzi wa Filamu ya Magwangala  ambayo imechezwa na wasanii wa Mkoani  Geita pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Mji   ulikuwa ufanyike siku jana (Julai 27) umekwama kutokana na kuwepo kwa madai ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kulalamika kuwa filamu hiyo inaonekana kuwa na mahudhui ya  uchochezi baina ya wananchi na mgodi Mkoani humo.

Uzinduzi  huo ulitarajia kufanywa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika ukumbi wa Desire Park .

Akizungumza  juu ya hatua ya kukwama  kwa uzinduzi huo Naibu Waziri  Wambura, amesema kuwa kilichotokea alipatiwa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kwamba kuna picha ambayo sio nzuri na kwamba wao kama mgodi walilalamika juu ya picha hiyo na kwamba wameangalia na kuona kuwa kuna maeneo ambayo yamerekodiwa sio mazuri na tatizo ni mawasiliano baina ya Afisa utamaduni na Mkoa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wasanii  Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya wachezaji wa Filamu Hiyo  Bi, Rosemery Michael, amesema kuwa wao hawakuona mapungufu yoyote kwa maigizo ambayo wameigiza kwenye filamu hiyo ni uhalisia wa maisha ambayo yapo ndani ya Mkoa husika.

Baadhi ya wasanii na wananchi ambao wameudhuria siku ya jana kwenye uzinduzi wa Filamu Hiyo, Sagari Mganga na Neema Philipo wamesema kuwa hata wao wameshindwa kujua ni maswahibu gani ambayo yamejitokeza ambayo yamesababishwa filamu hiyo kutokuzinduliwa.

Manase Ndoroma ni meneja mwandamizi wa mgodi  ambaye anashughulika na maswala ya jamii, ndani ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita  (GGM)  amefafanua kuwa wao  hawana ugomvi na sanaa wala na wasanii ila kumetokea shida ambayo wametoa kwa jamii kwa makusudi na kwamba mgodi huo una athari kwa jamii ambayo inauzunguka.

CHADEMA Kumshughulikia Aliyemfukuza Mwandishi wa TBC Kwenye Mkutano wa Tundu Lissu

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa, kimepokea kupitia vyombo vya habari taarifa za tukio la mwandishi wa habari wa TBC kushindwa kutimiza wajibu wake katika ofisi za Makao Makuu yake zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

CHADEMA imesemema, tukio hilo halikufanywa kwa maelekezo ya kiongozi yeyote na kama chama, hawajawahi na hawana sera wala msimamo wa kubagua chombo chochote cha habari.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema wamesema kwamba, katika hatua za awali wanafanyia uchunguzi tukio hilo ili kuweza kubainisha nini hasa kilitokea katika siku hiyo na wanategemea kupata ushirikiano kutoka kwa mwandishi husika katika uchunguzi wao.

Aidha, taarifa hiyo kutoka CHADEMA aliwahakikishia waandishi wote wa habari kuwa wataendelea kuwa salama katika matukio yote ambayo yatakuwa yakifanywa na chama hicho na watapata ushirikiano unaostahili.

“Baada ya uchunguzi wetu kukamilika tutatoa taarifa kamili juu ya tutakachokuwa tumebaini na hatua tutakazochukua. Sisi tunaamini katika uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa waandishi wa habari na haki ya kupata na kutoa habari/taarifa kuwa ni nguzo kuu katika kujenga taifa la kidemokrasia na hatimaye kufikia maendeleo ya kweli.”

Katika kudhihirisha kwa vitendo kuwa wanathamini uhuru wa habari na uwajibikaji, Mrema alisema, CHADEMA ni taasisi ya kwanza ya kisiasa iliyotia saini na kukubaliana na Azimio la Dar es Salaam Juu ya Uhuru wa Uhariri na Uwajibikaji, na kwamba hawana uhakika kama kuna taasisi nyingine ya kisiasa iliyofanya hivyo.

“Tunapenda kutumia fursa hii kuwahakikishia wadau wote wa habari, wakiwemo waandishi, wahariri na wananchi, kuwa tutaendelea kuionesha imani hiyo kwa vitendo katika shughuli zetu zote za kisiasa,” alisema Mrema.

KUTANA na Mtaalam wa Tiba za Asili Toka Komoro Maalim Fadhili..Anatibu Magonjwa Mbali Mbali na Kusafisha Nyota

$
0
0

KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239/

WhatsApp IMO +255785786436/

VYAKULA Vinavyoongeza HAMU ya Kufanya Tendo la Ndoa

$
0
0
Historia inaonesha kuwa kwa kipindi kirefu, wanawake na wanaume wamekuwa wakitumia chakula kumvutia mpenzi. Mara nyingine chakula hicho kinakuwa kinaongeza hamu ya kujamiiana na kuna wakati ni harufu au ladha ya chakula hicho ndiyo inayokufanya kupata hisia hizo. muonekano wake, ladha yake unapokila, uhaba wake.

Asali

Pamoja na utamu wake, asali ina nafasi kubwa ya kuongeza hamu ya kujamiiana kwakuwa ina aina zote za madini ya Vitamin B, ambayo ndio yanasaidia sana kuupa mwili nguvu.

Unaweza kula vijiko kadhaa kila siku, wengine huichanganya wakiwa wanaotengeneza keki, kuipaka kwenye mkate au chakula chochote.

Shayiri

Maji ya shayiri asubuhi au jioni yanasaidia kuongeza hamu ya kujamiiana. Shayiri madini ya L-arginine yanayoongeza homoni za testosterone, pia ina wingi wa kundi la Vitamin B. Shayiri huuzwa bei nafuu na ni njia rahisi sana ya kuongeza msukumo wa damu, jambo ambalo hutokea unapofanya mapenzi. Shayiri inapotumiwa kwa muda mrefu inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya kusimama kwa uume.

Parachichi

Wataalamu wa masuala ya mapenzi wanasema kuwa parachichi linaingia kwenye kundi hili kwakuwa umbo lake linafananishwa na maumbile ya mwanaume au mikunjo katika mwili wa mwanamke na kwamba ulaini wake na jinsi linavyotoa majimaji huongeza hisia za mapenzi. Yanaweza kuliwa yenyewe au kwa kuchanganywa kwenye vyakula vingine.

Yana kiwango kikubwa cha mafuta na vitamin E vyenye kazi ya kuongeza msukumo wa damu, hivyo kuongeza kiwango cha utengenezwaji wa testosterone. Kama hutaki kutumia parachichi kwa kazi hii, basi litakusaidia kwa kung’arisha ngozi kutokana na madini ya vitamin E.

Mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina wingi wa madini ya tyrosine (aina mojawapo ya asidi aina ya amino inayosaidia kuchangamsha mwili). Mbegu hizi pia zina virutubisho vingi vinavyosaidia kuongezeka kwa msukumo wa damu mwenye viungo vya uzazi.

Unaweza kuzioka kwenye oveni, kuzisaga au kula kwa kuzichanganya na vyakula vingine, ikiwamo asali pia – ili kuongeza faida zaidi.

Tikiti

Wataalamu wanasema kuwa watu wengi hawajui jambo moja kuhusu tiketi: kwamba kama ambavyo tiketi linaweza kukata kiu yako kwa wingi wa maji yaliyomo, ndio hivyo hivyo inavyoweza kukusaidia kwenye maswala ya kujamiiana. Utafiti umeonesha kuwa tunda hilo lina kiwango kikubwa cha viambata aina ya citrulline, ambayo ina kazi sawa na dawa aina ya Viagra kwa mwanaume.

Tangawizi
Tangawizi inafanya damu iende kwa kasi jambo linaloweza kusababisha mwili uweze kupata msisimko wa kimapenzi kirahisi sana. Pia inasaidia kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula, jambo linalosaidia sana kukufanya ubaki kuwa na hamu ya kufanya mapenzi kama umekula chakula kingi.

Chokleti

Wataalamu wanasema kuwa dawa pekee ya ukweli kwenye maswala ya mapenzi ni cocoa. Cocoa inachochea uzalishaji wa homoni zinazofanya ujisikie vizuri aina ya serotonin na dopamine, na ina kemikali aina ya phenylethylamine, inayotengenezwa kwa wingi kwenye ubongo unapoingia mapenzini. Cocoa inafanya kazi hii hasa inapochanganywa na chokoleti kwakuwa inayeyuka kirahisi na kuleta hamasa ya kimapenzi mdomoni. Kwakuwa chokleti ni nzuri unapoila—na inafanya tujisikie vizuri baada ya kuila—zawadi inayomfanya mtu apate hisisa nzuri siku zote lazima itapendwa.

KIBITI Mambo Shwari: Gesti na Viwanja Vyapanda Bei

$
0
0
Maisha ya Kibiti sasa ni shwari hamna shari na tayari bei za vitu kama viwanja na huduma kama za nyumba za kulala wageni (gesti) zimeanza kupanda bei upya kama ilivyokuwa awali.


Taarifa hiyo yenye kuashiria dalili njema za kurejea kwa amani na utulivu kwa wakazi wa wilaya hiyo iliyopo mkoani Pwani, ilithibitishwa na jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake, Barnabas Mwakalukwa.

Hivi karibuni, wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani, zilielekea kuwa tishio jipya la ulinzi na usalama nchini baada ya kuwapo kwa taarifa za mauaji ya kila mara ya watu wasio na hatia, wakiwamo viongozi wa vijiji, vitongoji, polisi na hata raia wa kawaida. Jumla ya watu zaidi ya 30 waliripotiwa kuuawa katika matukio tofauti ya kipindi cha takribani mwaka mmoja tu uliopita.

Tishio hilo la usalama Kibiti lilisababisha baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo kukimbia na kwenda kuishi maeneo mengine nchini na pia, taarifa zilisambaa hata kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na athari za kiuchumi zilizosababisha bei za viwanja, mashamba, nyumba na hata huduma kama za gesti kushuka kwa kiasi kikubwa.

Mwakalukwa amesema hali ya Kibiti sasa ingali ikitengemaa kila uchao kutokana na jitihada kubwa zilizofanyika katika kudhibiti uhalifu na kwamba sasa, hakuna tena tishio na hata bidhaa zimeanza kupanda tena bei kuashiria kurejea kwa hali ya amani na utulivu.

Hata hivyo, Mwakalukwa amesema kuwa kuwepo kwa ushirikiano kati ya Wananchi na Jeshi la polisi na kuanzishwa kwa kanda maalumu inayohusisha wilaya hizo tatu na Mafia kumeimarisha doria kwa kiasi kikubwa na matunda yake ni kurejea kwa hali ya usalama.

“Kwa mfano, sasa Kibiti iliyokuwa na sifa mbaya inaondoka. Eneo lolote ambalo lilikuwa na uhalifu na serikali ikaimarisha usalama, mfano Tarime, ikiwa na kanda maalumu, hali huimarika. Sasa kumetulia, si huko tu, hata Amboni mkoani Tanga kwenye mapango, Arusha…kote tumeimarisha ulinzi baada ya kujua chanzo cha uhalifu huo ni nini”, amesema Mwakalukwa kwenye mahojiano yake na Gazeti la Nipashe.

Imeelezwa kuwa katika baadhi ya maeneo ambako bei ya nyumba za kulala Wageni (Gesti) ilishuka kwa kukosa wateja wa uhakika, kwa sasa iko katika kiwango cha kuanzia Sh. 15,000 hadi 40,000 kulingana na eneo na ubora wa gesti husika.

VIDEO: Diamond Akichezewa na Mpenziwe Zari The Boss Lady Sehemu za ikulu

$
0
0
Sikutegemea kukutana na video ya aina hii inayomuhusu platnum, sijuwi ni umaarufu au ndio katika harakati za kupambana na hali zao ndio wakaamua kujirekodi wakifanya hayo mambo.

Diamond anatakiwa awaige wasanii wenzie wakubwa katika inshu za ku expose faragha zao. Diamondi naweza kusema ndio msanii anayeongoza kwa ku expose faragha zake akiwa na mpenzi wake.

Nadhani video hii haiwezi kukuacha salama:

MSAGA Sumu: Mwanaume Mashine imeniletea Mgogoro Mkubwa Kwenye Ndoa yangu....

$
0
0
Mwanamuziki ambaye pia ni hit maker wa ngoma inayosumbua kwa sasa ijulikanayo kama "Mwanaume Mashine" Msaga Sumu amedai kuwa ngoma hiyo licha ya kumletea mafanikio ya muda mfupi kulinganisha na ngoma zote zilizopita lakini ngoma hiyo imeleta mtafaruku mkubwa katika ndoa yake kwa madai kuwa amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa madada wengi hapa mjini wengi wamekuwa wakimtaka kimapenzi mara baada ya kugundulika kuwa ana muhogo wa jang'ombe .


'Wanawake wengi wamekuwa wakiahidi mambo kedekede ili mradi tu niwatimizie haja yao ya kimapenzi' alisikika akisema hivyo msaga sumu ambaye pia aliwahi kutamba na ngoma ya UNANITEGA SHEMEJI.

Huu ndio Ukweli Kuhusu Uteuzi wa Wabunge Viti Maalum

$
0
0
Huu ndio ukweli kuhusu uteuzi wa Wabunge Viti Maalum

Ugonjwa wasababisha Gwajima kutokufika mahakamani

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 30, 2017 itatoa hukumu katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha na risasi inayomkabili Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu.

Hukumu hiyo ilipaswa kutolewa leo Jumatatu, Julai 31 kwa Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha lakini ilishindikana kwa sababu hakimu huyo alikuwa na udhuru.

Hata hivyo, Wakili Peter Kibatala amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati kesi ilipoitwa mbele yake kuwa Askofu Gwajima ni mgonjwa na mahakamani hapo amewakilishwa na mdhamini wake.

Hayo yametokea baada wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuiambia mahakama kuwa washtakiwa George Mzava, Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Milulu wapo mahakamani lakini Askofu Gwajima hayupo.

Pia, amedai kesi ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa hukumu lakini wamepata taarifa Hakimu Mfawidhi, Mkeha anayeisikiliza kesi hiyo anaudhuru.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo kesi imeahirishwa hadi Agosti 30, 2017 ambapo watasomewa hukumu.

Mzava, Bihagaze na Milulu wao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki bastola aina ya berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa siku hiyo na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha mara baada ya mashahidi wa upande wa mashtaka na utetezi kutoa ushahidi wao na kuufunga.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali, Shedrack Kimaro na Joseph Maugo.

Huku upande wa utetezi uliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala ambapo washtakiwa walijitetea pamoja na mashahidi wao wawili akiwamo Nesi wa hospitali ya TMJ, Devotha Bayona na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima George Kiwia.

Katika ushahidi wa upande wa utetezi wa shahidi, Devotha alidai kuwa yeye ni afisa muugizi daraja la pili katika Hospitali ya TMJ na yupo kitengo cha ICU.

Machi 29, 2015 aliingia zamu usiku akipokea zamu toka kwa Nesi Rebecca ambaye aliacha kazi 2016 wakati huo Askofu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo kwa siku ya tatu.

Anakumbuka siku hiyo walikwenda askari wawili na mtu mwingine Bihagaze wakagonga mlango wa ICU wakahitaji begi la mgonjwa, walivyojitambulisha alitaka kuhakikisha ni kweli akamfuata Gwajima na kumuuliza. Alieleza ushahidi.

Amedai Gwajima alimueleza ni kweli Bihagaze ni msaidiziwake na kwamba Bihagaze alimwambia yupo pamoja na askari hao wanataka begi la mgonjwa.

Muuguzi huyo amesema Gwajima alisema hawezi kutoa begi hadi wapewe maelezo maalumu na kwamba begi hilo lilikuwepo pembeni ya kitanda cha Gwajima.

Baada ya kupewa majibu hayo na Gwajima, aliwaambia polisi amesema hawezi kulitoa hadi polisi waandike maelezo, wakamueleza wanachohitaji ni begi na maelezo wataandika kesho.

Wakati wanajibizana Gwajima alisikia na akamwambia nesi atawapa hilo begi kwa sababu ndani Lina silaha yake.

“Polisi walitaka kuingia kinguvu nikawaambia hapa ni ICU hamuwezi kuingia kinguvu, " alieleza nesi huyo na kwamba Gwajima alimwambia kama wanalihitaji kinguvu chukua begi mpe Bihagaze awape polisi.

Amedai kabla hajampatia begi hilo Bihagaze polisi walimpokonya, akafunga mlango akaendelea na mgonjwa wake lakini alimuona mgonjwa anamawazo.

Washtakiwa wengine mbali na Gwajima wao wanadaiwa kuwa Machi 29, 2015 katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A walikutwa wakimiliki Bastola aina ya Berretta yenye namba ya siri CAT 5802 bila ya kuwa na kibali toka kwa mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.

Imeendelea kudaiwa kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 32 (1) na cha 34 (1) (2) na(3) cha sheria ya Silaha na Milipuko sura ya 223 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Pia, wanadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio washtakiwa hao pia walikutwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya Shotgun.

Washtakiwa hao wapo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti waliyopewa ya kuwa kila mshtakiwa awe na mdhamini mmoja anayeaminika ambaye alisaini hati ya maneno ya dhamana yenye thamani ya Sh1 milioni.

VIDEO: Mbowe aliamsha 'Dude' la Makenikia

$
0
0
"Rais Magufuli aliunda kamati mbili..., ni jambo jambo jema kulinda rasimali za nchi, hata hivyo ulindaji huo hauhitaji kuwa na pupa na hasa baada ya TRA kuiandikia ACACIA mdai ya kodi yanayofikia kiwango cha shilingi Trilioni 425, Taarifa hizi zimesambazwa katika vyombo mbalimbali vya kimataifa, kutangazwa huku ni kwa misingi ya kejeli zaidi, ikihoji kuna uwezekano gani wa kampuni kudaiwa kodi ambayo ni zaidi ya mara 10 ya bajeti ya Taifa husika?" Hayo ni sehemu ya manneo ya Mweneyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 31, 2017 Jijini Dar es salaam.

 TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI

DIVA Achafukwa Awatolea Mapovu Timu Kiba....Awakana Mchana Kweupee...!!!

$
0
0

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Diva amewacharukia vikali wale wanaodai yeye ni Team Kiba baada ya kufanya interview ya mchekeshaji Mama Ashura ambaye alitumia muda mwingi kuukosoa mwenendo wa Alikiba katika muziki kwa sasa.

Diva amesema yeye hana team na anaheshimu kazi yake na watu wanapaswa kuelewa kuwa kwa sasa yupo buys sana hawezi kushughulika na mambo kama hayo. “Nimepata malalamiko baadhi ya watu Oh kwanini umemualika Mama Ashura, wewe si team Kiba Oh Diva this and that. Naomba ni make it very clear mimi sina U team, mambo ya Uteam yanagawa mashabiki wangu, sitaki kwanza hata kusikia mambo hayo tena, Im over that Path. Mungu mwenyewe anajua nilivyo busy saa hii building my life and my future jaman , have alot in my plate sahan yangu imejaa sana. “Huo muda tena sina tena and love everybody yes napenda kila mtu ata haters sababu wananifanya niwe famous, yes ila sichagui sibagui ataenizika simjui wanasema waswahili, Mi nahudumia watu wote sihudumii pande moja tu, Sitaki Gawa shabiki zangu sababu ya vitu ambavyo havinipi faida maishani, tuendeleen kuwa marafiki tuheshimiane,” ameandika Diva Instagram na kuongeza. “Hivyo basi namualika yeyote kwenye show yangu nikijisikia na watu wakimuhitaji, sina pande yoyote ile niko busy nafanya kazi yangu na naiheshimu sana kama ninavyoiheshimu serikali, nawapenda sana ila being professional kumenipenda zaidi, I choose to be happy and means i’ll support good music regardless, na ukinikosea I m free shot you with Nothing but the truth, I m free soul, peace out!!,” amesisitiza.
.
.
JE NI KWELI DIVA HANA UPENDELEO KWA WASANII?? .
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

HATIMAYE Barrick Wajisalimisha na Kuanza Mazungumzo Kuhusu Uchimbaji wa Madini Nchini...!

$
0
0
Kamati Maalum iliyoundwa na Rais Dkt. John Magufuli imekutana na Wawakilishi  kutoka Barrick Gold Corporation leo kuanza mazungumzo kuhusu uchimbaji wa madini hapa nchini.



Soma taarifa kamili.

UCHAGUZI Kenya Wakumbwa na Doa Kubwa.....Mkuu wa TUME ya Uchaguzi Nchini Kenya Akutwa Amefariki

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha TEHAMA wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amepatikana akiwa amefariki.


Polisi wamesema kuwa mwili wa afisa huyo aliyetambulika kwa jina la Chris Musando  pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la kikuyu lililo vitongoji vya jiji la Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

♦Uchaguzi Kenya: Mkuu wa kitengo cha TEHAMA wa tume ya uchaguzi atoweka

Bwana Musando alikuwa akihusika na usambazaji wa vifaa vyaa eletroniki ambavyo vingetumiwa kutambua wapiga kura na kwa upeperushaji wa matokeo wakati wa uchaguzi mkuu wiki ijayo.

NAJ Atoboa Siri "Baraka The Prince Ashauriki"

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva na mpenzi wa Baraka the Price, Naj Dattani amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hakumshauri mmewe kuachana na lebo ya RockStar4000 bali yalikuwa ni maamuzi yake.


Naji amesema Baraka sio mtu wa kushaurika kirahisi kwa mambo anayoyaamini yeye kuwa yanafaida kwake hivyo hata suala la kutemana na RockStar 4000 yeye hakumshauri chochote.

“Sio kweli mimi Baraka sijawahi kumuingilia kwenye maamuzi yake na hata watu wanaomjua Baraka sio mtu wa kushauriwa sijui vitu vitu yaani anakuwaga na maamuzi yake, Sometimes hata kuna vitu vingine mimi mwenyewe huwa ninampinga lakini yeye akiamua kitu, ameamua”,amesema Naj huku akisisitiza kuwa amemsapoti yeye kujitoa RockStar 4000.

“Mimi ofcourse ninamsupport na namuamini anajua anachokifanya na asingetoka kama angeona kuna faida kwake, na yeye ni mtu ambaye yupo serious na kazi zake na anaamini kwenye kipaji chake so hataki kutegemea kitu ambacho hakimuingizii faida kwake, so nikamuelewa na ninam’support na maamuzi yake”,amesema Naj kwenye mahojiano yake na TBC International.

Hata hivyo Naj amewathibitishia mashabiki wa Baraka The Prince kuwa kuna ngoma nyingi kali zinakuja hivyo wakae mkao wa kula.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>