Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Dr.Kigwangalla Apasua Jipu..Adai Mkojo Una Uhusiano na Vitendo vya Uchochezi...

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Hamisi Kigwangalla amesema mkojo waweza kuwa na uhusiano na vitendo vya uchochezi.

Akifafanua suala hilo baada ya mdau kuuliza kwa njia ya mtandao. Je kipimo cha mkojo kinaweza kugundua vimelea vya uchochezi?

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dr. Kigwangalla alijibu kuwa 

"Huwezi kujua, pengine mtu akiwa kwenye 'influence' ya dawa ndiyo anakuwa na propensity ya 'uchochezi' ikigundulika ndivyo anaweza kusaidiwa.

"Ukiwa hujui sayansi unaweza kudhani mkojo hauna uhusiano na vitendo vya uchochezi! Raia mwema huwezi kukataa kipimo chochote, labda mharifu",

Uchochezi waweza kuwa na uhusiano na matumizi ya kemikali zenye kuvuruga akili, hili liko wazi labda uwe mbumbumbu wa sayansi au nyumbu!

aliandika Dr. Kigwangalla.

Rais Magufuli Kafanikiwa Kudhibiti Maandamano na Migomo iliyokuwa Fasheni ya Huko Tulikotoka

$
0
0
Wakati Rais Magufuli anatoa kauli hii, wapo waliobeza wakidhani kuwa haitekelezeki. Hata hivyo, hadi sasa ukweli ni kwamba Rais Magufuli kafanikiwa kudhibiti maandamano na migomo nchi nzima. Ukiona maandamano basi ujue ni ya kuunga mkono juhudi zake anazofanya kuwaletea maendeleo wananchi. Hakuna mtutu wa bunduki wala virungu vilivyotumika kuzima migomo na maandamano. Ni mikwara yake tu pamoja na kushungulikia chanzo cha migomo na maandamano hayo.

Hongera Rais Magufuli. Kwa hili umeinyoosha nchi.

Download App ya Ajira Yako Kwenye Simu Yako Kusoma Kirahis Nafasi za Kazi Zinazotangazwa Kila Siku

$
0
0
JE una Tafuta Ajira au Unataka Badilisha Ajira uliyonayo?

Fanya Kuinstall App ya Ajira Yako Kwenye Simu ili kusoma na Kuapply Nafasi za kazi zinazotangazwa kila siku katika magazeti....


Bonyeza HAPA Kuinstall Bure

Hali ya Msanii Jini Kabula Yamtoa Jack Wolper Machozi....Afunguka Kumsaidia

$
0
0

BY@wolperstylish - Kabula wangu💔💔💔Natamani niongee mambo mengi sana juu yako lakini natamani ata kukusaidia urudishe akili yako swali ni kwamba nimechelewa??
Nakama nimewahi je nitafanikiwa kweli ?

Sasa tuzungumze jambo jamani maana siju hizi tarfa tunazipata insta naona nalangu niliongelee insta wanatasnia wenzangu tunamsaidiaje mwenzetu nini kimekuta kipi je nayoyasikia ndio hayo????nakama ndio mbona kuna wataalam wakusena nae naakakaaa sawa
Basi watanzania wenzangu naombeni tuchangie maoni yenu hapa nakama nim2 uwezi toa ushauri hapa basi tuma msg kwakupitia cm hii 0765776776 basi tuweze kumrudisha kabula jamani .

Naandika msg hii huku nalia namoyo mdogo sana usiweza kuvumilia naumivu nakumbuka nimishawahi kumwambia kabula we nimwanamke mzuri sana bongo movie lkn natamani kujua tatizo nini kacheka tuu akachukua nguo akaondoka sikupata muda wakuzungunza nae ....sasa npo safarini hope kesho au kesho kutwa nikijaliwa tukutane kwaoamoja .. Bongo movie tumfwate alipo jamani tujue tunamsaidiaje nimeona vdio anaongea sjui niamechanganyikiwa masikn me ata nashindwa kuandika jamani ....

Breaking News: Waziri Lukuvi Awarudishia Watu 180 Viwanja Walivyozulumiwa

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amefuta hati za viwanja 180 na kuvirejesha viwanja hivyo kwa wamiliki wake halali, waliokuwa wamedhulumiwa haki zao na viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini, kwa kushirikiana na watu wenye fedha.

Waziri Lukuvi ameyazungumza hayo, leo, Agosti 2, ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea matokeo ya oparesheni maalum za kushughulikia matatizo ya adrhi kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Waziri Lukuvi amesema katika awamu ya kwanza, waliwasikiliza watu 200 wenye matatizo ya kudhulumiwa ardhi kwenye maeneo ya Kinondoni, Kibaha, Mkuranga na Bagamoyo, awamu ya pili ikahusisha wakazi 100 wa Temeke na Kigamboni huku awamu ya mwisho, ikiwahusisha watu 100 kutoka wilaya ya Ilala.

Waziri Lukuvi amesema katika kuwasikiliza watu hao, wamebaini kwamba kwa kipindi kirefu kulikuwa na mchezo wa wamiliki halali wa ardhi kutapeliwa viwanja vyao na viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini, kwa kushirikiana na watu wenye fedha.

Kabla ya Mr Nice, Nilitaka Kumuweka Bwana wa Jack Wolper Kwenye Video yangu ya Sina - Harmonize

$
0
0
Kabla ya Mr Nice, Nilitaka Kumuweka Bwana wa Jack Wolper Kwenye Video yangu ya Sina - Harmonize
Harmonize amesema kuwa Kabla ya Mr Nice, nilitaka kumuweka Bwana wa zamani wa Wolper (Dallas) kwenye Video yake ya Sina. Unaweza bonyeza play kumsikilize akifunguka mengi hapo chini.

VIDEO:

Hivi kuna Ukweli Kwamba Wanawake Walioajiriwa Hujitongozesha kwa Mabosi?

$
0
0
Kuna dhana kwamba wanawake walioajiriwa wanakabiliwa na mazingira ambayo yanawalazimisha kuingia kwenye vitendo vya kutoka nje ya ndoa zao, ukilinganisha na wanawake ambao hawajaajiriwa hususani mama wa nyumbani jambo ambalo katika maisha ya kawaida bila utafiti linaonekana kama vile ni kinyume yaani akina mama walio majumbani ndio ambao hutoka nje zaidi.

Niliwahi kuwahoji wanawake kadhaa jijini Dar, mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Nilifanya mahojiano hayo ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.

Lakini bila shaka suala la mapenzi kwa wanawake walioajiriwa lina nguvu na kwa hiyo limekuwa likifanyiwa tafiti katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya kumi walioajiriwa huwa anaonyesha tabia za kimapenzi au kujitongozesha kwa bosi wake.

Tafiti hizi zinaonyesha kuwa yule mmoja kati ya kumi ambaye hujitongozesha kwa bosi huishia kutembea naye au hata kuolewa naye kama hana mume na pengine kuvunja ndoa yake. Inaelezwa pia kuwa mmoja kati ya wanawake kumi wanaojitongozesha kwa mabosi huwa anapandishwa cheo. Hii ina maana kwamba wanawake wanaopandishwa vyeo kwenye maeneo ya kazi huenda mmoja kati ya kila kumi hupandishwa kwa sababu za kimapenzi hata hivyo siyo lazima iwe hivyo.

Katika mahojiano na jarida moja nchini Marekani mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Jarida hilo halikufanya mahojiani ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.

Wanawake wenye watoto ambao walihojiwa kwenye tafiti hizo walisema kwamba ajira zinawasumbua na wamefikiria kuwa ni ngumu kujigawa kazini na nyumbani kishughuli.

Tafiti hizo hata hivyo hazikulenga katika kuonyesha kwamba wanawake ni dhaifu bali huenda zimelenga katika kuonyesha kwamba idadi ya wanawake wanaojitongozesha kwa mabosi ni ndogo kuliko inavyotazamwa au kuaminika na pia kuonyesha kwamba bado wanawake walioajiriwa wako kwenye nafasi kubwa zaidi kushiriki mapenzi kuliko wale walioko majumbani. Ni juu ya wanawake ambao wanadhani ni halali kuuza thamani zao kwa ajili ya kazi kubadili mwenendo huo..

Ndoa ya Nuh Mziwanda Chali....Aliyekuwa Mkewe Aolewa na Mwanaume Mwingine

$
0
0
Ndoa ya Nuh Mziwanda na mkewe Nawal ilioyofungwa Novemba imeingiwa na kidudu mtu kilichopelekea ndoa hiyo kuvunjika licha ya kuwa imeweza kuleta tunda la Anyagile (Anya).

Akiongea katika U-Heard ya Clouds FM Jumatano hii, Nawal amethibitisha yeye na msanii huyo wa ‘Jike Shupa’ wameachana na kila mtu anaishi maisha yake kwa sasa na tayari yeye ameshafunga ndoa nyingine.

“Sina mume mimi, Nuh wakati anaamua kurudi kwenye dini yake (Ukristo) hakunishirikisha na mimi sasa hivi nipo kwa bibi yangu Msasani, pia nimesha olewa na mtu mwingine,” amesema mrembo huyo.

Pia Nawal amedai kuwa ni kweli ameondoka kwake kutokana na Nuh kuwa mkosaji na mpaka sasa hamjali mtoto wao kwa chochote ila kama aliweza kumzaa basi anauwezo wa kumlea mtoto huyo.

Video: Diva Anunua Ugomvi wa Vanessa Mdee na Baby Madaha

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds FM, Diva The Bawse ameamua kuununua kwa bei rahisi ugomvi wa Vanessa Mdee na Baby Madaha.

Mara kadhaa Baby Madahga amekuwa akisikika kwa kusema Vanessa ni msanii ambaye anabebwa ndio maana kila tuzo anazoshiriki za nje anakuwa haibuki mshindi – Kauli hiyo imeonekana kumgusa Diva na kuamua kumpa makavu msanii huyo.

Akiongea na Bongo5, mtangazaji huyo amesema, “ Sasa Baby Madaha kweli wakujifananisha na Vanessa kweli? Namfahamu lakini Yule siyo wakujifananisha na Vanessa, atafute level yake ya kujifananisha nao. No disrespect, am not try disrespect her lakini yule asijifananishe kabisa na Vanessa, Vanessa ni hard working you can see, ana focus yeye yule ana focus nini?”



“Yaani anamzungumzia hivyo Vanessa yeye katoa nyimbo gani ambayo atleast watu wanaijua au kafanya video au kafanya kolabo na huyu. Mimi nahisi Baby Madaha sawa sawa na wale wa page hizo za udaku, you can’t compare Baby Madaha na Vanessa, Shout out to Vee Money,” ameongeza.

Mwezi uliuopita Baby Madaha alipokuwa akiongea katika kipindi cha 180 Power cha Sibuka FM, alisema, “Tunapeleka watu kuwania tuzo wengine hawana vigezo vya hizo tuzo, especially nazungumzia kwa madada kuna dada mmoja yaani kila tuzo anaendaga lakini ashindi kutokana na nini hana qualification za hizo tuzo.”

Ulimbukeni wa Wanaume Linapokuja Swala la Mapenzi na Uzuri wa Mwanamke

$
0
0

Leo inabidi tuambiane ukweli, kuna baadhi ya wanaume ambao sijui ndo tuite "nzi kufia kwenye kidonda" yani utakuta mwanaume anamfukuzia mwanamke kwa miaka 3, kisa ni nini? eti oh yule demu ni mzuri, oh i have a crush on her, ooh nimemzimia..utakuta huyo mwanamke anaefukuziwa wala hamuwazi huyo mwanaume tena usiku analala usingizi mnono na vijambo juu.

Mtu anakaa kwenye relationship isiomfaidisha wala kumpa furaha eti kisa demu ni mzuri, aise i advise ni bora kuwa single tu kuliko kupitia haya mateso ya kujitakia, sisemi mtu usiwe na crush kwa demu, ila wanaume (including me) tuwe tunajaribu kusoma upepo, mpende demu ukiona haeleweki na hakutilii maanani.. sepa fasta it will be good for ur emotional health, naamini ukitubu dhambi kiukweli na ukimuomba Mungu atakupa mke mwema.

Some of my friends wanaapa kutumia hela nyingi sana kwa demu wanaemuona kuwa ni mzuri, they're like yule demu bwana ni high status ngoja ntamchukua na prado, kumbe huyo demu anapigwa mate na muuza duka..just imagine mtu mwaka wa 4 bado anatajataja jina la demu ambae ana crush nae mm huwa mpaka nakereka, nawakataza wasitaje ovyo majina ya madem ambao hawana time nao..

Bora hata wanawake, akiona mwanaume hueleweki na hupendeki ..anafunga virago (labda cjui awe kwenye ndoa)

Nimemaliza.

Jinsi Ya Kupunguza Uzito Kwa Kutumia Saladi

$
0
0

Ulaji saladi ya spinachi, matunda ya apple na parachichi unaweza kumsaidia mtu kuwa na uzito unaotakiwa kiafya.

Kabla mtu hajaanza kula mlo wake wa asubuhi, mchana au usiku anashauriwa aanze na mboga za majani za spinachi au aina nyingine.  Ulaji wa aina hii unamwezesha mtu kula kidogo vyakula vyenye wanga, sukari au mafuta ambavyo vinasababisha kuongezeka uzito na unene.

Saladi ya mboga za majani hujaza tumbo na kumfanya mtu ajihisi ameshiba na hivyo kuzuia tabia ya kutamani kula hasa vyakula vya wanga au sukari.  Mboga za majani za spinachi pia, zina kirutubisho kinachoitwa thylakoids, ambacho kinachochea mwili kuzalisha homoni inayopunguza hamu ya mtu kutaka kula hasa vyakula vyenye sukari.

Kuhusu matunda ya apple, kwa siku mtu akila tunda moja ni jambo zuri.  Matunda ya apple yana maji na nyuzi lishe ambazo zinalifanya tumbo kujisikia limeshiba.  Matunda ya epo pia yana kirutubisho cha pectin, ambacho kinakifanya chakula kilichomo tumboni kusagwa kwa muda mrefu na kumfanya mtu kujisikia ameshiba.

Mtu akila tunda zima la epo (siyo juisi), kabla ya mlo atajisikia hali ya kushiba na hivyo atakula kidogo chakula cha wanga au sukari.
Kwa upande wa matunda ya parachichi, kula nusu ya tunda hilo kwa siku kunaupa mwili mafuta bora kiafya na nyuzi lishe ambazo zinamfanya mtu ajisikie ameshiba muda mwingi na kutokutamani chakula mara kwa mara.

Anachopaswa kufahamu mtu ni kwamba kula vyakula vya wanga, sukari au mafuta kwa wingi ndipo mwili unaongezeka uzito na unene kupita kiasi. 

Sababu ya Tatizo la Kuharibika Mimba kwa Wanawake Wengi Hizi Hapa

$
0
0
Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu waawake wengi wamekuwa wakaiharibikiwa na mimba bila kujua sababu.

Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba.

1.Mama anapokuwa na matatizo  uvimbe (fibroid),  huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara.

2. Uzito mkubwa (unene)
Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda.

3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara
Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika.

4. Utoaji mimba
Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi tisa, hivyo epuka kutoa mimba.

5. Matumizi ya Pombe,Sigara
Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya k?kumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo.

6. Magonjwa sugu
Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia.

Kutana na Maalim Fadhal Rashid Kutoka Komoro ni Mtaalam wa Tiba za Asili

$
0
0

KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239/

WhatsApp IMO +255785786436/

RAIS Magufuli Ahani Msiba wa Mwalimu Wake wa CHUO Kikuu....

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Agosti, 2017 amewapa mkono wa pole familia ya Dkt. Steven Juma Mdachi aliyefariki dunia jana tarehe 01 Agosti, 2017 katika Hospitali ya Tumaini Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dkt. Steven Juma Mdachi alikuwa Mhadhari wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Uhandisi, Idara ya Kemia.

Akiwa nyumbani kwa Marehemu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Rais Magufuli ametia saini kitabu cha maombolezo na kuwapa mkono wa faraja Mjane wa Marehemu Mama Mary Mdachi, watoto wa Marehemu, wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na ndugu jamaa na marafiki.

MAKOSA Makubwa Aliyofanya Maalim Seif na Mtatiro na Kusababisha Kushindwa KUMFUKUZA Lipumba CUF,,,,,

$
0
0

Wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilipokuwa kwenye misukosuko baada ya kupokea barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba, dhamana ya uimara na amani ya chama hicho ilikuwa chini ya Mwenyekiti wa muda wa chama hicho Julius Mtatiro ambaye aliteuliwa na Baraza la Uongozi la chama hicho ambapo alikuwa na dhamana ya kuhakikisha kuwa chama kinaendeshwa kwa mafanikio. Yeye ndiye alipaswa kutoa dira ya chama kielekee wapi.

Kwa bahati mbaya sana, chama kilipopigwa na mawimbi, Mtatiro (bila shaka baada ya kushauriana na Katibu Mkuu, Maalim Seif Shariff akatoa muongozo ambao kwa kiasi kikubwa umewapotosha wana-CUF nchi nzima kiasi kuwa leo hii wanajikuta katika sintofahamu kubwa ambayo inatishia muelekeo wa chama hicho.

Wakati Profesa Lipumba alipotangaza kufuta barua yake ya kujiuzulu na kuamua kurejea katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Mtatiro alikuwa mmoja wa viongozi wa awali kabisa wa CUF kuonesha dharau kwa Profesa Lipumba. Mbaya zaidi hakuonesha dharau yeye binafsi tu, kauli zake ziliwaelekeza wanachama wengine wa CUF wampuuze Profesa Lipumba na kundi lake. Hili lilikuwa kosa kubwa sana ambalo Mtatiro anapaswa kulijutia.

Kama kiongozi ambaye anapaswa kutoa dira ya uongozi wa chama, Mtatiro, pamoja na mambo mengine, alipaswa kufahamu kuwa ni nani adui wa chama na ana nguvu kiasi gani. Wakati ule Mtatiro alimhesabu Profesa Lipumba kama mmoja wa maadui wa chama hicho lakini akafanya kosa kubwa sana la kumdharau adui huyo.

Kauli alizokuwa anazitoa wakati huo zilionesha kana kwamba Profesa Lipumba na kundi lake wasingeweza kufanya chochote cha kukiathiri chama hicho, lakini leo tunashuhudia mambo yanayofanywa na Profesa Lipumba ambayo yameiweka CUF katika nafasi ngumu sana.

Lipumba ambaye Mtatiro aliwataka wanachama wa CUF wampuuze, kwanza alifanikiwa kusimamisha akaunti ya chama na kufungua akaunti mpya ambayo inatumika kupitisha ruzuku ya chama hicho(swala hili bila shaka lilifanya uongozi wote uliokuwepo bila yeye – kuanzia kwa Makamu Mwenyekiti kushuka chini kupata ukata wa hali ya juu hivyo kukosa kabisa nguvu ya kupambana naye), Pili akafanikiwa kukamata ofisi za Makao Makuu ya chama yaliyopo Buguruni, jijini Dar es salaam na tatu akafanikiwa kufuta bodi ya wadhamini ya CUF na kupitisha bodi mpya.

Kama hilo halitoshi, Profesa Lipumba ambaye Mtatiro alitaka apuuzwe, ndiye anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kama kiongozi mkuu wa CUF.

Juzijuzi hapa, Lipumba alifanikiwa kuwafukuza wanachama nane wa chama hicho ambao pia walikuwa ni wabunge wa viti maalum na kwa kufukuzwa huku, wamepoteza nafasi yao ya ubunge na amefanikiwa kuteua watu ambao wanaonesha kumuunga mkono kujaza nafasi hizo bungeni.

Pamoja na hayo, ni Lipumba huyu huyu aliyeamua kumuweka kando kwa muda Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad na nafasi yake kushikwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena Sakaya – jambo ambalo linaweza kudhihirika wazi kuwa ni mahesabu mazito ya kudhoofisha kambi ya Maalim Seif na Mtatiro kwakuwa ndiyo iliyojiunga kumpiga vita Lipumba kwa muda wote huu.

Kwa hakika, kabla Mtatiro hajawaambia wanachama wampuuze Lipumba, alipaswa kufahamu nguvu aliyonayo au iliyopo nyuma ya Profesa Lipumba. Ufahamu huo ungemuwezesha Mtatiro kama kiongozi mkubwa kwenye chama kufahamu anapambana na nani.

Lakini inavyoelekea Mtatiro hakuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu nguvu ambayo Profesa Lipumba alikuwa nayo. Inaonekana yeye akatimiza kwa vitendo kile ambacho aliwataka wanachama wengine wa CUF wakifanye – kumpuuza Profesa Lipumba. Matokeo yake, yule aliyeamua kumpuuza leo hii amekuwa tishio kubwa kwa uhai wa chama hicho.

Kama Mtatiro angekuwa makini tangu mwanzo, kamwe hakupaswa kumpuuza Profesa Lipumba. Alitakiwa kuwa na mikakati ya kuhakikisha kuwa Profesa Lipumba na kundi lake hawaleti madhara katika chama. Lakini kwa bahati mbaya sana inaonekana Mtatiro hajalifahamu kosa lake kwa sababu mpaka leo bado anaendelea na kauli yake hii ya kuwataka wana CUF wampuuze Profesa Lipumba.

Kwa bahati mbaya sana Mtatiro na wenzake wamechelewa sana kurekebisha kosa lao. Hivi sasa Profesa Lipumba na kundi lake tayari wameshaanza kuweka mizizi na ni kazi kubwa sana kuwaondoa bila kukiharibu chama hicho.

Awali ilionekana kuwa Profesa Lipumba na wenzake ndio walikuwa wakipigania uhai wao, lakini sasa hali imegeuka na ni Mtatiro na wenzake ndio wanaonekana wanapigania uhai wao ndani ya CUF. Kama Profesa Lipumba asingepuuzwa, haya yasingetokea.

HT @ MTANZANIA

KIMENUKA..Mbunge Mwingine wa CHADEMA Akamatwa na Polisi

$
0
0
Muendelezo wa wabunge wa upinzani kutiwa nguvuni kwa tuhuma mbalimbali umezidi kushika kasi baada ya leo Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe, Pascal Haonga, kukamatwa na Polisi leo mchana akiwa katika mji mdogo wa Mlowo-Mbozi.

Mbunge huyo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatuhumiwa kwa makosa ya uchochezi na kufanya mkusanyiko usio halali.

Licha ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange, kuthibitisha kumshikilia Haonga lakini hakutaka kueleza suala hilo kwa kina kwa madai kuwa hayupo ofisini.

Meshack Mgaya ambaye ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Songwe amesema kuwa chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu kukamatwa kwa kada huyo na kwamba baada ya kujiridhisha watato tamko.

KUNANI...Unaambiwa Msajili wa Vyama vya Siasa AIGOMEA Barua ya Maalim Seif ya Kuwavua Uanachama Wabunge wa CUF.....

$
0
0

Mgogogoro ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) bado unaendelea kufukuta baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kuwasilisha barua kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jon Ndugai akimtaarifu kuwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limewasimamisha uanachama wanachama wawili wa chama hicho ambao ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya (Mbunge wa Kaliua) na Maftaha Nachuma (Mbunge wa Mtwara Mjini) uamuzi uliofikiwa kutokana na wajumbe wa mkutano huo kupiga kura za siri na kuamua kuwavua uanachama, hivyo kumuomba Spika Ndugai afanye utaratibu wa kuwavua ubunge wao kwa kuwa si wanachama halali wa chama hicho.

Baada ya barua hiyo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amejibu barua ya Maalim Seif kwa kuwa kueleza kutomtambua yeye kama Katibu Mkuu wa CUF kwakuwa barua kutoka chama hicho ilisema kuwa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama inakaimiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haijapokea barua nyingine kutoka chama hicho ikionesha kumrejeshea Maalim Seif mamlaka yake.

Pia Jaji Mutungi amekataa matokeo ya kikao hicho kilichoitishwa na Maalim Seif kwakuwa kikao hicho kilitakiwa kiwe chini ya mtu mwenye dhamana ya Katibu Mkuu wa chama (Magdalena Sakaya) au Mwenyekiti wa CUF (ambaye ni Profesa Ibrahim Lipumba) na Jaji Mutungi akamkumbusha Maalim Seif arejee Katiba ya CUF ibara ya 91(c) inayotaka vikao vyote vya Baraza Kuu la chama hicho viongozwe na Mwenyekiti wa chama.

NAFASI za Kazi Zilizotangazwa Leo Serikalini na Kampuni Binafsi

$
0
0

GEITA: CHADEMA Wavuna Wanachama 60 Wa CCM, Wengi Wajihusisha na Tundu Lissu

$
0
0
Leo katika sherehe ya vikundi Katika Tawi la Nyantorontoro B jimbo la Geita mjini tumepokea wanachama Wa ccm 60 na kuwakabidhi za Chadema.

Wamesema wameamua kuungana na wana mabadiliko hasa Tundu Lisu kupigania Demokrasia na wao hawapendi udikteta.

Wamesema serikali ya ccm imekuwa inawaonea sana wapinzani wamekuwa wanawatisha sana wapinzani wameamua kuungana na upinzani ili wawatoe ccm.

Maana wameona wapinzani hawana matatizo kwani wameongozwa na Mwenyekiti serikali ya mtaa tangu 2014 wa Chadema hawabagui ila ccm wanawabagua wapinzani .

Wamesema walidanganywa na ccm wataletewa kila kijiji 50 lakini kumbe ulikuwa ni uongo tu hali ya maisha imekuwa ngumu sana.

Kadi hizo wamekabidhiwa na Mwenyekiti Wa Wilaya Ndg Amos Nyanda akishuhudiwa na Mwenyekiti Wa Bavicha Wilaya ya Geita Kamanda Mhere Mwita.

Katika sherehe hiyo vikundi vya Ujasiriamali ambayo vina wanachama wapatao 100 Chadema tumeweza kuwapatia Fedha pamoja na Sehemu ya kufugia kuku wa mayai kama sehemu ya Mradi.

Vile vile Uongozi wa chadema Wilaya ya Geita uliwakabidhi wakina mama wajiriamali vyeti vya kutambua Mchango wao katika kuleta maendeleo katika mataa vilivyotengenezwa na Chadema jimbo la Geita mjini.

Imetolewa na:~
Mimi Mhere Mwita
M/Kiti Bavicha (W) Geita
02/08/2017

MAREKANI na Urusi Hapatoshi....Watangaziana Vita...

$
0
0
Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amesema kuwa vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.

Amesema kuwa mikakati iliotiwa saini na rais Trump inaonyesha udhaifu wa rais huyo wa Marekani ambaye alisema ameaibishwa na bunge la Congress.

Sheria hiyo inalenga kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016 pamoja na vitendo vyake dhidi ya Ukraine.

Katika kutia saini makubaliano hayo dhidi ya adui wa Marekani kupitia sheria ya vikwazo siku ya Jumatano, aliweka taarifa akisema kuwa mkakati huo sio wa sawa.

Sheria hiyo pia inaiwekea vikwazo Iran na Korea Kaskazini, Iran imesema kuwa vikwazo hivyo vipya vinakiuka makubaliano ya mpango wa nyuklia na kwamba itajibu kwa njia ilio ''sahihi na sawia'' kulingana na chombo cha habari cha Isna.

Korea Kaskazini kwa upande wake haijatoa matamshi yoyote kuhusiana na hatua hiyo ya Marekani.
Bwana Medvedev pia alionya kwamba hatua mpya zinazolenga kumuondoa rais Trump madarakani zitachukuliwa kwa kuwa sio mtu aliye na utaratibu.

Moscow ambayo imekana kuingilia uchaguzi wa Marekani tayari imelipiza kisasi wiki iliopita wakati bunge la Congress lilipopitisha muswada uliowatimua maafisa 755 kutoka katika ubalozi wa Marekani nchini Urusi mbali na kuzuiwa kutumia jengo moja la Marekani pamopja na ghala moja nchini Moscow.

Mataifa kadhaa ya Ulaya ikiwemo Ujerumani yanahofia vikwazo hivyo vipya na rais wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker ameonya kwamba athari yake itaathiri maslahi ya kawi ya Ulaya.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images