Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Sakata la House Girl Aliyefungiwa Ndani na Bosi Wake Jijini Dar kwa Miaka Mitatu na Kupewa Mateso Makali

$
0
0
Mfanyakazi wa ndani, Yusta Lucas (20) amekumbana na masahibu yanayofanana na yale ya mtoto Nasra Mvungi (4) aliyekuwa amefungiwa kwenye boksi kwa miaka karibu minne huko Morogoro. Huyu amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam akiuguza majeraha yanayotokana na kuteswa na kufungiwa ndani kwa miaka mitatu.
Binti huyo, mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, katika Kijiji cha Kampala amedai kuwa amekuwa akiteswa na kufungiwa ndani ya nyumba na tajiri yake, Amina Maige wa Mwananyamala, Kwa Manjunju katika kipindi chote hicho.
Amina anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba OB/RB/9967/2014.

Akisimulia masahibu yaliyompata akiwa katika Wodi Namba Tatu ya hospitali hiyo, Yusta alisema: “Nililetwa Dar es Salaam mwaka 2010 kufanya kazi za nyumbani baada ya bosi wangu (Amina) ambaye ni binamu yangu kuzungumza na mama yangu na kuniomba nije kumsaidia kazi ndogondogo.

Alisema aliishi vizuri na mwajiri wake huyo, lakini mwaka 2012 ndipo mambo yalipoanza kubadilika akidai kuwa Amina alianza kumwadhibu kwa kumng’ata na kumchoma kwa pasi kila alipomtuhumu kutokufanya kazi zake vizuri.
“Alikuwa akinichapa na kuning’ata sehemu mbalimbali wakati mwingine usoni, pia kunichoma kwa pasi yenye moto kila aliponituhumu kutokufagia au kupiga deki vizuri.”
Hakuwahi kupelekwa hospitali
Alisema licha ya kupata vidonda kutokana na adhabu hizo, mwajiri wake huyo hakuwahi kumpeleka hospitali na pale alipoona hali ni mbaya alimnunulia dawa… “Tunaishi wawili tu baada ya kuondoka mumewe na mtoto wake kumpeleka shule ya bweni… niliugulia hadi nikapona bila mtu mwingine kufahamu.”
“Akienda kazini anafunga geti na kunikataza kufungua hata kama mtu atagonga… sokoni nilikuwa naenda siku ambazo yeye yupo tu na huwa akiniamrisha niende haraka na kurudi pasipo kuzungumza na mtu yeyote.”
Alisema mwajiri wake huyo alikuwa akituma pesa za mshahara wake kwa mama yake akisema ndiye anayepaswa kulipwa, jambo ambalo anadhani limemfanya mama yake kuhisi mwanaye yuko katika mikono salama… “Kila alipotuma alipiga simu na kunipa niongee na mama kuhakikisha kama zimefika huku akinisimamia na baada ya hapo anachukua simu.”
Ataka kurudi kwao
Binti huyo ambaye sehemu kubwa ya mwili wake ina alama za kung’atwa meno na majeraha ya kuchomwa na pasi, alisema: “Ninaomba mtu yeyote mwenye hela, nataka nikitoka hapa hospitali nirudi Tabora kwa mama. Nina shaka na maisha yangu hapa kwa huyu mama… sitaki tena kubaki Dar es Salaam kutokana na mateso ninayoyapata.”
Polisi wasema
Mkaguzi Msaidizi wa Dawati la Jinsia Polisi Mkoa wa Kinondoni, Prisca Komba alisema taarifa za binti huyo ziliwafikia baada ya majirani kupeleka taarifa hizo katika Kikundi cha Kipange kilichopo Kwa Manjunju ambacho nacho kilitoa taarifa polisi na ndipo mtego wa kumnasa mwanamke huyo ukawekwa.
Majirani walichukua hatua hiyo kutokana na kusikia kelele za kilio mara kwa mara zikitokea ndani ya nyumba ya mtuhumiwa. “Tumekagua makovu na majeraha mbalimbali yaliyo katika mwili wake na kupata jumla kuwa yako 91,” alisema Komba na kuongeza:
“Toka jana amekuwa akinitaka nisiondoke mbali naye amekuwa na hofu, lakini sasa afadhali kidogo baada ya kumpatia ushauri na kumhakikishia kwamba hapa yuko salama.”
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Thobias Edoyeka alisema suala hilo linashughulikiwa na polisi pamoja na ustawi wa jamii, kauli iliyoungwa mkono na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mwananyamala, Rose Temu ambaye alisema wanafuatilia kwa karibu matibabu yake pamoja na usalama wake. “Hali yake ikishaimarika na kujiridhisha kuwa anaendelea vizuri, tutakuwa na jukumu la kumuunganisha na familia yake,” alisema.
Ofisa Muuguzi Msaidizi Wodi Namba Tatu ambayo ni ya kinamama, Rose Mussa alisema Yusta anaendelea vizuri.
“Anaendelea vizuri kwa kweli, jana (juzi) hakuwa hivi alikuwa mwoga hawezi kujieleza tofauti na leo (jana)… bado anaendelea na vipimo, tutakapoona anafaa kuruhusiwa tutafanya hivyo na kumkabidhi kwa ustawi wa jamii.”
Credit: Mwananchi

Makahaba wa Kinyarwanda Wanaswa Dodoma Wakinyemelea Wabunge

$
0
0
Wanawake wanne raia wa Rwanda wametiwa mbaroni mjini Dodoma kutokana na kuingia nchini kinyemela na kujihusisha na biashara ya ukahaba.
Watuhumiwa  watatu kati ya hao, Saidat  Umotoni (28), Asha Abimana (25) na Asia Umotoni  Wase (30), hii ni mara yao ya pili kukamatwa mjini hapa wakidaiwa kujihusisha na biashara hiyo.
Mara ya kwanza ilikuwa Novemba mwaka jana ambapo wote  ( Asia, Asha na Saidat) baada ya kukamatwa, walirudishwa kwao baada ya kulipa faini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma,  Proches Kuoko, alimtaja mwingine aliyekamatwa ni Chalote Uwase (28) ambaye ameshahukumiwa kifungo cha miaka miwili anachotumikia katika Gereza la Isanga, mjini hapa.
Alisema wahamiaji hao wote kwa pamoja walikamatwa na maofisa wa kikosi cha Uhamiaji, baada ya kupata taarifa kwa kuwepo raia hao katika eneo la barabara ya Bahi ndani ya Manispaa ya Dodoma.

Alisema wanawake hao walikamatwa  usiku kwenye mitaa hiyo huku wakiwa kwenye harakati za kutafuta  wateja na walipohojiwa wote kwa pamoja hawakuwa na hati ya kusafiria na kuishi hapa nchini na walizokuwanazo zilikuwa zimeisha muda wake wa matumizi.
“Hata  walipopekuliwa,  walikutwa wakiwa na hati ya kusafiria iliyokuwa imeisha muda wake wa kuwawezesha kuishi hapa nchini na walipohojiwa zaidi walisema wao kazi yao ni uchangudoa,”alisema Kuoko.

BRAZIL 2014: Messi amfunika Ronaldo vibaya

$
0
0
Lionel Messi ni mchezaji mwenye thamani kubwa duniani kutokana na kulipwa karibu mara mbili zaidi ya Cristiano Ronaldo anayemfuatia.

Hiyo ni kwa sababu umri wa Messi ni miaka 26 wakati Ronaldo ana miaka 29.

Pia Raheem Sterling ni mchezaji mdogo (19) na mkubwa ni Andres Iniesta (30) walioingia katika orodha hiyo ya wachezaji 25 wanaolipwa zaidi kwenye fainali za Kombe la Dunia.

Utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Uswisi kiitwacho Neuchatel kwa kushirikiana na OptaPro, uliangalia thamani za wachezaji wa ligi tano kubwa za Ulaya kwa kutazama mishahara yao na gharama za uhamisho.

Messi kwa sasa ana thamani ya Pauni 175.6 milioni za Kiingereza akifuatiwa na Cristiano Ronaldo mwenye thamani ya Pauni 92.7 milioni za Kiingereza huku Eden Hazard akishika nafasi ya tatu kwa thamani ya Pauni 66.7 milioni,

Wachezaji 23 kati ya 25 walioshika nafasi za juu kwenye tafiti hiyo ni washambuliaji. Walobaki ni viungo wakabaji ambao ni Sergio Busquets na Paul Pogba.

Katika kundi hilo la wanasoka 25, 11 wanatoka Ligi Kuu ya Uingereza, nane wanacheza Hispania huku Ufaransa, Ujerumani na Italia zikitoa wachezaji wawili kila mmoja.

Katika soko la juu la nyota hao 11, Ronaldo na Gareth Bale (Pauni 51.2m) wamenunuliwa kwa gharama kubwa zaidi kwani Messi hajahama Barcelona toka ajiunge nao.

Kyle Walker na Luke Shaw pia wameingia katika kikosi cha wachezaji 11 wenye thamani zaidi duniani, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na CIES Football Observatory.

Umbea Wa Insta..!! Unaambiwa Huyu Ndiye Msanii Mdogo Wa Bongo Movies Ambaye Anamahusiano Na Mheshimiwa Komba.

$
0
0


Mie nawasilisha tu kwa Umbea Mwingi zaidi Ingia Instagram Mwenyewe ujioneee umbea wa mjini

Kenya locks out TZ tour operators, cars

$
0
0
Dar es Salaam. Kenya’s Tourism Regulatory Authority (TRA) has banned Tanzania’s tour operators and vehicles from taking visitors to Kenya’s game reserves and parks.

According to the Kenya News agency, the move by TRA is in response to a similar action by Tanzanian tourism authorities, whom it accused of deliberately locking out Kenyan tour operators from key reserves and parks.

However, Tanzania National Parks Authority (Tanapa) told The Citizen on Saturday, that the move was in compliance with Tanzania’s regulations providing that such services be conducted within each country’s boundaries.

Speaking at a recent tourism stakeholders meeting in Kisumu, TRA acting director-general Korir Lagat said, such cases have now become common-place and Kenya is not going to take it lying down. “Through a letter to Kenya Wildlife Services (KWS), all vehicles bearing Tanzanian number plates will be denied entry into our parks,” said Lagat. He said, TRA has also informed by letter all county governments that have tourist attractions of major significance not to allow Tanzanian registered vehicles into their parks.

Tanapa’s Public Relations manager Paschal Shelutete said, it is not true that all vehicles bearing Kenyan numbers were being troubled or denied access to national parks.

“Kenyan families in their private cars are welcomed at any moment they wish to tour our parks.”

He said, the ban “is on tour operators and tour operations registered vehicles,” and that was agreed by the two countries way back in 1985.

He said, according to the agreement, tour operators from the two countries were allowed to swap tourists along border towns, and not to enter with them in the parks since they didn’t have the respective countries’ operating licences.

“That is the agreement that we follow and Kenyan authorities too are supposed to respect it, if they are not adhering to it, it’s not upon us to comment,” said the Tanapa PR manager.

He explained that the agreement was set to ensure there’s sanity in the industry and each country gains from the same market.

“Remember, this is one market that we are all competing for, there should be a level-playing field. There are major Kenyan companies that have opened sister companies here, they pay required taxes and are allowed to operate in our parks since they are licensed to do so,” he said.

According to Shelutete, other claims and demands against the spirit of the agreement between Kenya an Tanzania “are politically motivated and are of no value to Tanzania.” He stressed that the 1985 agreement did set up the required operating standards between the two countries.

Single Mothers Tunashida Sana Katika Mahusiano

$
0
0
Watu wengi wanachukulia single momz kama hawana umuhimu tena na hawafai katika mahusiano. Siku hizi wanaume wengi ambao hawajakuwa na watoto utasikia wakisema "Mimi mwanamke wenye mtoto simtaki amechoka na amekongoroka kabisa huyo" 

Kumbuka hapa kuna wanawake wengine hata ukikutana nae na asipokuambia ana mtoto huwezi jua, anajipenda na ni mrembo wa kuvutia na mwenye maendeleo.

Wanaume wengi sana wanaona hana thamani, na wengine kusema ni wameshindikana walikotoka yaani na jaamaa aliyezaa nae.Tukumbuke NOT EVERYMAN MEANT TO BE A DADY, kuna wengine ni waharibifu tu, pengine pia tofauti za maisha zinazotokea zinapelekea yote hayo kutokea, Watu hawaelewi...

Single moms haimaanishi hawatakiwi kuwa na mahusano mengine mapya labda na mwanaume ambaye hana mtoto, wengi hudhani ukijitumbukiza hapo basi utalea mtoto. 

Jamani kuna watu wanauwezo wa kutake care ya watoto wao bila msaada, jiulize kabla yako nani alikuwa anamsaidia kama sie mwenyewe. Ni faraja na upendo tu anahitaji kutoka sehemu nyingne.

Hawa watu haimaanishi waolewe au wawe na mahusiano na wanaume ambao nao wanawatoto...eti sababu wasaidane kulea... Tena na zile familia zikisikia kijana anasema "nina mwanamke ila ana mtoto" moto unawaka, jamani jamani? Huu si ubaguzi lakini?

Mwenye mawazo hayo wewe ni katili na mbinafsi kabisa. Na ndo maana inafikia hatua wanaume mnafichwa mnakuja kutambua kwamba ana mtoto imepita hata miaka 10, halafu unalaumu oooh hakuniambia. Hakukuambia kwasababu anajua mtazamo wenu kwao...

Mimi naomba tu niwaambie ndugu Kaka zangu, wadogo zangu, Mwanamke aliyezaa ni sawa na wengine tu, tena bora yeye kazaaa anajua ana kizazi, kuliko hao wasiozaa na wanaokesha kila siku kutafuta watoto kwa waganga..

Mimi mwenyewe ni mfano mzuri, nimepata unyanyasaji sana na wanaume, pale nilipokuwa nawaambia nina mtoto, wengine walishia kimya kimya, wakidai eti tuna kawaida ya kupasha kiporo na mzazi mwenza HIYO NI UONGO NA FIKRA MBOVU ZA WATU
Na kamwe sikuweza kuficha kama sina mtoto kwasababu najua nini maana ya mtoto. Mtoto ni zaidi ya thamani ya vitu ulivyonavyo ndani...
Tena wanawake ambao mmekutana na haya wala msifiche ukweli, Mwanaume akikimbia ujue mungu kakuepushia jambo.

WANAUME HEBU TOENI NA MBADILIKE NA HIZO IMANI AMBAZO SIO...

Swali lolote linakaribishwa... Asanteni

Mbunge Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari amefunga ndoa

$
0
0
Mbunge Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari amefunga ndoa na Anande Nko kwenye Kanisa la Pentekoste lililopo Kilinga, Arumeru ikifuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hoteli ya Ngurdoto.
Sherehe hiyo ilianza mishale ya saa 7:00 mchana ambapo watu wote walialikwa wakiwemo ndugu, marafiki, jamaa na wananchi wote wa Arumeru Mashariki ambao wamepiga ‘mpunga’ wa kutosha na vinywaji hadi kila mtu akaondoka akisema ‘Nassari ameacha historia’.

Mambo 6 kutoka hapa Durban South Africa kuhusu Diamond Platnumz na tuzo za MTV

$
0
0
Wote mpaka sasa tunafahamu toka siku nyingi kwamba Diamond Platnumz ni mwimbaji pekee kutoka Tanzania aliechaguliwa kuwania tuzo kwenye tuzo za MTV BASE ambazo zinatolewa leo June 7 2014 hapa Durban South Africa ila kuna mengine mapya yamejitokeza hatukuwa tunayafahamu.
1.Diamond alipokelewa kistaa na kama mastaa wengine wote walivyopokelewa ambapo meneja wake Bab Tale anasema ‘imefika sehemu unaona kabisa jamaa wanatukubali sasa hivi, Airport tumepokelewa na magari matatu… mi sijawahi kupokelewa na kuendeshwa na Mwanamke mzungu yani ila kiukweli Diamond amepokelewa kifahari kama wengine’
2.Babtale amethibitisha kwamba Diamond ndio atakua msanii wa kwanza kufungua show leo kweye utolewaji wa tuzo hizi ‘kitendo cha msanii kupewa nafasi ya kufungua, kwa sababu MTV ni kubwa…. kitendo hicho ni kikubwa kwa msanii pia‘
‘Wakati wa mazoezi tulikutana na  Mafikizolo wasanii kutoka Afrika Kusini ambao wamekuja wenyewe kuomba kolabo na Diamond, wao wenyewe wanasema bwana tunaomba kolabo na wewe…….. sisi tulitakiwa kurudi bongo Jumapili lakini wao ndio wamesema watalipia gharama za sisi kuendelea kukaa hapa na mabadiliko ya ticket yetu ili turudi Tanzania Jumanne’ – Bab Tale

‘Hatukua tunajua kwamba Diamond ndio atafungua show kwenye utolewaji wa tuzo hizi za MTV, jana wakati tukiwa kwenye mazoezi ndio tukaambiwa’
‘Muziki unahitaji elimu na kujitambua, hata Mafikizolo walivyokuja kwetu wanasema kabisa wanahitaji umoja wa Afrika wakati nyumbani bongo tu yenyewe kwa wenyewe hawazimiani, Mafikizolo walivyofanya mkutano na waandishi wa habari yani kwa jinsi walivyoelezea kuwa na ndoto ya kufanya kolabo na Diamond….. imeonyesha ni jinsi gani Diamond ana nguvu’ – Bab Tale
Msimamizi mwingine wa Diamond ni meneja Mkubwa Fela ambae amethibitisha kwamba kwenye safari yake ya kuja South Africa ameambatana na Watanzania wengine saba ila kilichomfurahisha zaidi ni kwamba amekuja kukuta washkaji zake zaidi ya 20 wanaoishi Durban wameshanunua ticket tayari kwa ajili ya kumshangilia Diamond’
Wakati wa chakula cha jioni, Ommy Dimpoz ambae nae yuko hapa Durban alitania baada ya kuisikia hiyo habari kwenye AMPLIFAYA na kusema ‘yani sipati picha Diamond akishinda ile tuzo, shangwe zitakazotoka kwa hawa wabongo ni kama goli la Taifa stars’
Watanzania waliofunga safari kutoka Tanzania mpaka Durban ni pamoja na Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Bab Tale, Salam ambae pia ni meneja wa Diamond, Mkubwa Fela, Watangazaji Sam Misago, B12, Adam Mchomvu, Millard Ayo, Shadee lakini pia Nancy Sumari na mpenzi wake Lucas, Ommy Dimpoz, Shetta na mpiga picha Michael Carter Mlingwa.

Diamond Akosa Tuzo ya MTV Award, Mwenzake Davido Aibuka na Tuzo

$
0
0
Jana Usiku Ndio ilikuwa Mwisho wa Kinyanganyiro cha Tuzo za MTV Awards Ambapo wasanii Mbali Mbali waliochaguliwa kushindania tuzo hizo walijumuika South Africa akiwemo Diamond aliyekuwa anagombani Tuzo ya The Male na Best Collaboration

Diamond hakufanikiwa kupata tuzo Ambapo tuzo ya The Best Male ilichukuliwa na Davido na Ile ya The Best Collaboration ilichukuliwa na Wengine...Anyway Hongera Diamond kwa Kufika Hatua hiyo Kazi Booti sasa Mwakani Uchaguliwe Tena.....Hongera Davido

Hii Hapa List ya Wasanii Walio Shinda Tuzo za MTV Base, Sad Own Diamond Name is Not There!

$
0
0
THE WINNERS OF THE 2014 MTV AFRICA MUSIC AWARDS
Best Male: Davido (Nigeria)
Best Female: Tiwa Savage (Nigeria)
Best Group: Mafikizolo (South Africa)
Best New Act: Stanley Enow (Cameroon)
Best Live Act: Flavour (Nigeria)
Best Collaboration: “Y-tjukutja” – Uhuru Ft. Oskido, DJ Bucks, Professor and Yuri Da Cunha (South Africa/Angola)
Best Hip Hop: Sarkodie (Ghana)
Best Alternative: Gangs of Ballet (South Africa)
Best Francophone: Toofan (Togo)
Best Lusophone: Anselmo Ralph (Angola)
Artist of the Year: Davido (Nigeria)
Song of the Year: “Khona” – Mafikizolo ft Uhuru (South Africa)
Best Video: Clarence Peters (Nigeria)
Best Pop: Goldfish (South Africa)
Best International: Pharrell
Personality of the Year: Lupita Nyong’o (Kenya)
MTV Base Leadership Award: Ashish J. Thakkar (Tanzania)
Transform Today Award by Absolut: Clarence Peters (Nigeria

Ki Ukweli Davido Alistahili Kupata ile Tuzo na Kumbwaga Diamond

$
0
0

Kwa Mahesabu ya Haraka haraka Ukiangalia nani alistahili kushinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume lazima ungempa Davido badala ya Diamond no matter What ....
Kwa haya Mawili tu utakubali kuwa ni Msanii Bora kumzidi Diamond :

1.Nyimbo zake Mbili Skelewu na Aye Zimetamba sana Africa nzima na nje ya Nchi na Kwenye TV nyingi zimeshika chat ya Juu sana, Diamond nyimbo iliyofanikiwa kushika chat ya Juu nchi zingine ni hiyo moja ya Remix ya Number One ambayo nayo alisaidiwa na uwepo wa Davido.

2. Katika Ufanyaji wa Show Davido Amfanya Show Nyingi zaidi nchi Mbali Mbali Ikiwemo Hapa Tanzania kuliko Diamond Alizofanya sana nje ya nchi  hasa Africa, Kenya Ndio huwa nasikia anafanya Show na huko UK na USA.

So huu Davido Hongera Sana, Diamond Huo ni Mwanzo Mzuri Usikate Tamaa Kazi Mgongo Mwana

Baada ya Kukosa Tuzo ya MTV Music, Diamond Afunguka na Kusema Haya

$
0
0
"Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV...Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo... pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema....

Shukrani zangu nyingi ziende kwa ashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine...Next stop #BET!!!... Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii"

Bibi Harusi Mtarajiwa Afumwa Geto Kwa Njemba Akiliwa Uroda

$
0
0
Dada huyu ameharibu ndoa yake mwenyewe na kujikuta anajuta, zikiwa zimebakia wiki mbili tu kufanya kufanya harusi  mpango ulivurugika baada 
ya picha za uchi ya huyu dada kunaswa akiwa getoni kwa jamaa akiwa amejiachia uchi wa mnyama akicheki TV. Tunaposisitiza kuwa michepuko haifai watu wanatuchukulia kama wajinga, wewe unajua kabisa ulikuwa na mwanaume fulani  na sasa umepata mchumba kwanini usiende ukampigia magoti na kumweleza ukweli akutunzie siri kwa kuwa tayari umepata mchumba? Haya ona sasa maji yashamwagika.

Ray C Ashawishiwa Kugombea Ubunge 2015 ili Kupigana na Vigogo Wanaoingiza Madawa Nchini

$
0
0

Makundi  mengi  ya  vijana  ndani  ya  mtandao  wa  facebook  yamekuwa  na  imani  kuwa  msanii  Rehema  Chamila  anaweza  kuwa  mtetezi  wao  mkubwa  endapo  ataamua  kuingia  kwenye  siasa...
Vijana  hao  wanaamini  kuwa  Ray C kwa  sasa  amepitia  changamoto  nyingi   hivyo  wanaamini  kama  akipewa  nafasi  ya  kuingia  bungeni  inaweza  kuwa  chachu  ya yeye  kupigana  na  watu  wanaoingiza  madawa  ya  kulevya  nchini  na  kuwaokoa  vijana  wengi  wanaopotea  kutokana  na  matumizi  ya  dawa  hizo


"Ray C kwa  nini  asiingie  tu  kwenye  siasa  na  akatutetea  kwenye  mambo  ambayo  hata  yeye  alikutana  nayo  hadi  yakataka  kumtoa  roho, tunaamini  anaweza  endapo  ataamua  kufanya  hivyo" alidai  kijana  mmoja  ndani  ya  mtandao  wa  facebook

Majanga Mengine Bongo Movies-Mzee Small Afariki Dunia

$
0
0
Muigizaji mkongwe nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku huu akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa Muhimbili. Mtoto wa marehemu aitwaye, Muhidin amethibitisha kifo cha Mzee Small. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

JOHARI: Baada ya Vifo Mfululizo Wasanii Tumenyooka

$
0
0
MKONGWE kwenye sanaa za Kibongo, Blandina Chegula ‘Johari’ amesema kufuatia vifo vya mfululizo vya wasanii, kwa kiasi kikubwa wasanii wamebadilika kitabia

Akipiga stori na paparazi wetu alisema, wasanii hao wamejitambua kuwa duniani watu wanapita, jambo ambalo kwa muda mrefu walikuwa wamelisahau na kuponda raha mfululizo.

“Tangu wenzetu wafariki mfululizo, wasanii wengi tumepata mshtuko na kujitambua, naona wengi wamebadilika, wamenyooka na kuanza kumrudia Mungu,” alisema Johari.
Vifo vya wasanii vilivyotokea hivi karibuni ni pamoja na cha Adam Kuambina, Sheila Haule ‘Recho’ na George Tyson.

Mbowe na Viongozi CHADEMA Wahudhuria Warusi ya Nassari, Wakwepa Msiba wa Mama Zitto

$
0
0
Kweli Dunia ina mambo. Hivi karibuni kulitokea msiba wa Mama yake Zitto Kabwe huko Kigoma lakini jambo la kushangaza viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe hawakuweza kuhudhuria lakini la kushangaza leo ameweza kuhudhuria harusi ya Joshua Nassari huko Arusha.
Kutokana na hili unapata picha gani juu ya Chadema na viongozi wake?

Diamond Kukosa Tuzo MTV, Je Kwa Maoni Yako Ameonewa?

$
0
0
Wakuu, nimekuta taarifa za kusikitisha kwa Watanzania wengi na mashabiki wengine wa msanii nguli wa mziki wa kizazi kipya Diamond. Je kukosa kwake tuzo hizi ni kutotendewa haki kwa msanii huyu? Je Msanii kama Davido aliyechukua tuzo hizi kweli alimzidi vigezo msanii diamond? Je suala la lugha (communication barrier) huenda ndio limemuadhibu Diamond na kufanya majaji 'wasimkubali'? Je Pesa ya Msanii kama Davido huenda imekuwa na influence kama vile tunavyosikia ya Qatar kuhusu kombe la dunia?

Nategemea mchango wenu!

Shamsa Ford Aongelea Picha Fake Zinazosambaa Mtandaoni Akiwa Kitandani na Mbunge

$
0
0
Picha chafu zinazodaiwa kuwa za star wa filamu nchini Shamsa Ford na mbunge wa Chadema, Salvatory Machemli zimeanza kusambaa kwa kasi mitandaoni tangu jana,. Picha hizo zinawaonyesha wawili hao wakiwa kitandani kwenye mahaba mazito. Hata hivyo picha hizo zinatia shaka kuwa sio halisi ni za kutengenezwa ingawa hatuna uhakika kwa asilimia zote kwasababu msichana anayedaiwa kuwa Shamsa Ford ana umbo tofauti na la star huyo, Shamsa ana umbo la kawaida ki-shape lakini msichana huyo anaonekana kuwa na umbo namba nane. 
Jana baada ya kuona picha hizo ambazo zimeenezwa hasa kwenye pages za kisiasa kwenye mitandao ya kijamii zikimuandama mbunge huyo wa ChademaSwahiliworldplanet ilimtafuta Shamsa na kumueleza kila kitu na kwa kujiamini Shamsa alisema sio zake hizo picha zimetengenezwa na pia msichana anayeonekana kiumbo wako tofauti na hata sura na akasema anajiheshimu sana na ana familia yake asingeweza kufanya jambo kama hilo, alipoulizwa je anafahamiana na Mh. Salvatory Machemli pia alikana kujuana nae achilia mbali kuwahi kukutana nae "zimedaiwa kuwa ni mimi but sio mimi, naomba uangalie hizo picha vizuri au kama upo WhatsApp nikutumie halafu uone je ni mimi? kabla sijakujibu" Shamsa alifunguka 
Star huyo anayefanya vizuri na filamu kibao aliendelea kwa kusema "si umbo hata sura ni tofauti, sijawahi hata kumuona huyo mheshimiwa, nahisi ni watu ambao wananichukia wanataka kunichafua, kiukweli nawaomba mashabiki wangu kabla ya kuanza kunihukumu waziangalie kwanza hizo pictures vizuri, mimi nina familia na najiheshimu"

Kwa upande mwingine baadhi ya wachangiaji mitandaoni wamedai kuwa picture hizo ni za kutengenezwa kwasababu Mh.Machemli ana kitambi lakini katika picha hizo hazimuonyeshi akiwa na kitambi, wengine wamesema kuwa picha hizo zimechukuliwa katika mtandao mmoja wa ngono na kufanyiwa photoshop lengo lake likiwa ni la kumchafua kisiasa mbunge huyo ambaye anadaiwa kukumba na misukosuko ya mara kwa mara. Hata hivyo ukweli wanaujua wenyewe.

NB. Tumeshindwa kuziweka picha hizo zikiwaonyesha mwili mzima kutokana na sababu za kimaadili.


PICHA: Msanii Nazizi Aki KISS na Mpenzi Wake Mpya!!!

$
0
0
The First lady of rap Nazizi kutoka Kenya ametupeleka kwenye maisha yake ya Mahusiano..Baada ya kuachana na  mume wake toka hapa 255.. kwa sasa yupo kwenye mahusiano ya KIMAPENZI na jamaa mwingine......Hivi karibuni ameshare nasi PICHA


Tazama picha za ndege hawa wawili katika mapenzi;
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images