Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Kimenuka...Magari Yenye Tinted Yapigwa Marufuku Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Kaimu Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dsm amepiga marufuku uwepo wa magari yenye vioo vya tinted ktk jiji la Dar.

Amesema imebaidinika magari hayo hutumika kwa mambo ya ujambazi na uvunjifu mwingine wa maadili ikiwemo ngono, hivyo kuanzia Jumatatu itafanyika operesheni maalumu ya kukamata magari hayo.

Utafiti; Mwanaume Akiwa na Mwanamke Mrembo, Anakuwa na Mvuto Kwa Wanawake Wengine.

$
0
0
Heshima kwenu wakuu.

Utafiti umedhihirisha kwamba mwanaume akiwa na mpenzi mrembo, basi wanawake wengine humwona kuwa mzuri au ana mvuto zaidi. Utafiti ulifanyika katika awamu tatu;

Kwanza, Wanawake 148 walionyeshwa picha ya mwanaume wakaambiwa waeleze kama (a)Hana mvuto/sio mzuri kabisa (b)ana mvuto/mzuri wa wastan na (c)ana mvuto sana/mzuri sana. Katika kundi hili wanawake wote walisema huyo mwanaume ana mvuto wa wastan au ni mzuri kiasi.

Kundi lingine la wanawake 97 walionyeshwa picha ya huyo mwanaume, lakini pembeni yake akiwa na mwanamke mrembo. Wakaambiwa kuwa huyo ni Dada au Shangazi yake. Sasa wakaambiwa waelezee mvuto/uzuri wa huyo njemba. Kundi hili pia walisema kuwa jamaa ana mvuto wa kawaida tu.

Kundi la mwisho lilihusisha wanawake 127. Walionyeshwa ile ile picha ya mwanaume akiwa na mwanamke mrembo. Lakini safari hii waliambiwa huyo mrembo ni MPENZI wake. Waliambiwa waelezee jamaa ana mvuto/mzuri kiasi gani. HAWA WANAWAKE WOTE WALISEMA HUYO MWANAUME ANA MVUTO SANA/MZURI SANA.

Sababu walizotoa ni kuwa huyo mwanaume atakuwa na akili sana, mwaminifu, mcheshi, tajiri na msikivu.

Watafiti walihitimisha kuwa, wanawake wanaamini kwamba mpaka kufikia mwanaume ammiliki mwanamke mrembo, ni lazima atakuwa "Smart"

So, - Men look better when they're a proven commodity.

By chifu77

Rais Magufuli Anatukonga Nyoyo zetu Watanzania

$
0
0
Utendaji wake makini. Hacheki cheki ovyo, hafanyi mchezo na mafisadi, anamaanisha anachokiongea/anaenenda katika maneno yake. Ni rais ambaye Tanzania ilipaswa kumpata miaka kadhaa iliyopita na haipaswi kumpoteza kizembe. Shikamoo Magufuli. Shikamooni watanzania mliomchagua Magufuli. Wafinye wezi wote wafinye mafisadi. Wafinye wahujumu uchumi

By utaifakwanza/JF

Video: Tundu Lissu Afunguka Mkojo wa Wema Sepetu Kupokelewa Mahakamani

$
0
0
Wakili wa malkia wa filamu nchini Wema Sepetu, Tundu Lisu ameongea na waandishi wa habari Ijumaa hii mahakamani Kisutu baada ya Hakimu Thomas Simba kuupokea na kuukubali ushahidi wa mkojo wa muigizaji huyo ambao ulipimwa na Mkemia Mkuu wa serikali na kukutwa na chembe chembe za dawa za kulevya aina ya Bangi.

 VIDEO:

Breaking News: Rais Kagame Ashinda Uchaguzi Kwa Kura Nyingi Rwanda

$
0
0
Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.

Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba.

Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa, Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana.

Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbart ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.

Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa ndiyo imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura.


Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Siku ya Leo Ingia >>www.ajirayako.co.tz

Wasanii Mbalimbali Wapata Shavu Kumsupport Magufuli Akizindua Mradi wa Bomba la Mafuta Tanga...Kukiwasha Leo Tanga

$
0
0
Wasanii mbali mbali wakiwa njiani kuelekea Tanga kumsupport Rais Magufuli atakapoweka jiwe la msingi katika mradi wa Bomba la Mafuta Tanga Kesho, Kwenye Video Hapa Chini Namuona Stamina,@shilolekiuno_badgirlshishi na huyo anaongea ni @rosa_ree from the Industry

VIDEO:

Imebainika....Ofisa wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya Aliteswa na Kunyongwa Mpaka Kufa....

$
0
0
Uchunguzi uliofanywa kwenye mwili wa aliyekuwa mkuu wa idara ya Tehama ya tume ya uchaguzi ya Kenya Bw Chris Msando, umeonyesha kuwa aliteswa na kuuawa.

Kwa mujibu wa mwanapatholojia mkuu wa serikali Dk Johansen Oduor na daktari wa familia Dk Bessie Byakika, mwili wa Bw Msando umeonesha kuwa wauaji walitumia mikono kumnyonga na pia walimpiga na kitu chenye ncha kali na kumsababishia jeraha.

Matokeo ya uchunguzi wa kipatholojia umekuwa ni msingi wa uchunguzi kufuatia kifo chake, na tayari watu watatu wametiwa mbaroni kuhusiana na kifo cha Bw Msando, lakini bado haijulikani walihusika vipi na kifo chake.

Mwili wa Bw Msando pamoja na wa msichana mwanafunzi mwenye umri wa miaka 21 uliokotwa jumamosi kwenye msitu wa viunga vya Nairobi.

Wakwe Wavunja Ndoa ya Mziwanda...Wamuozesha Nawal Kwa Mwanaume Mwingine Mwenye Pesa Bila Nuh Kutoa Talaka

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nuh Mziwanda ambaye hivi karibuni kumeibuka minong'ono kuwa ndoa yake imesambaratika, amefunguka kuhusu hilo na kukiri kuwa kweli ndoa hiyo imekufa bila talaka, huku mke wake akiwa mbioni kuolewa na mtu mwingine.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Nuh Mziwanda amesema mke wake huyo hajampa talaka lakini ameolewa na mtu mwengine, huku vuguvugu kubwa lilianza kwa wakwe zake (wazazi wa mke wake)

Mimi na Nawal tulitengana tu, lakini baada ya hapo kumbe mwenzangu ameshaandaliwa mume wa kumuoa, mimi baada ya kugundua hilo nikaona bora nirudi kwenye dini yangu, kwa hiyo wazazi wa mke wangu walikuwa wanajua kuwa mtoto wao ananisaliti", alisema Nuh Mziwanda.

Nuh Mziwanda alipoulizwa kama alitoa talaka kwa mke wake huyo kama sheria ya ndoa inavyotaka watu wanapoachana, Nuh alisema hajatoa talaka na hawezi kutoa kwani tayari Nawal mke wa mtu.

"Mimi sijatoa talaka, na kufuatilia suala la talaka itakuwa kama najichoresha kwani wao wazazi wanajua kabisa kama ni mke wangu lakini wao wakaamua kumuozesha kwa mtu mwingine, kwa hiyo mimi naacha tu, mimi nitaangalia utaratibu wa kumlea mwanangu kwani bado mdogo hivyo bado yuko na mama yake", alisema Nuh Mziwanda.


Mume wa Zamani wa Irene Uwoya Akerwa na Irene Uwoya Kutembea na Viben Ten....Amfungukia na Kumpa Makavu live....

$
0
0
Mume wa Zamani wa Irene Uwoya Akerwa na Irene Uwoya Kutembea na Viben Ten....Amfungukia na Kumpa Makavu live....

Ameandika Haya Kwa Uchungu:

Dogo Janja Apasua Jibu: Irene Uwoya ana Mvuto wa Kimapenzi, Anafaa Kuwa Mpenzi Wangu

$
0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Janja kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu mahusiano yake, na kutoa sintofahamu kuhusu kutoka kimapenzi na muigizaji wa filamu za kibongo Irene Uwoya.

Akizungumza na East Africa Television, Dogo Janja ambaye mara nyingi hapendi kuzungumzia maisha yake binafsi, ameamua kusema kuwa msanii huyo anafaa.

"Irene ni mwanamke mzuri, anavutia, kila mwanaume anayejua mwanamke mzuri anafaa kuwa naye, ila kwa upande wangu mimi namkubali sana Irene Uwoya, kwani anaigiza vizuri, hivyo namkubali kwa kazi zake pia", alisema Dogo Janja.

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za Irene Uwoya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Dogo Janja, ambapo watu wengi wamekuwa na mtazamo tofauti wakisema si sahihi kwani Irene Uwoya ni mkubwa sana kwa Dogo Janja. Jambo ambalo Dogo Janja anaonekana kutoliafiki.

Jack Wolper Achukizwa na Aliyekuwa Mume wa Irene Uwoya Mchezaji Ndikumana...Amtolea Mapovu Haya.....

$
0
0
Jack Wolper si wa nchi hii Achukizwa na Aliyekuwa Mume wa Irene Uwoya Mchezaji Ndikumana...Amtolea Mapovu Haya.....

Hizi Hapa Faida 6 za Kuoa Mwanamke Kama Zari Hassan wa Diamond Platnumz

$
0
0
Mwanadada maarufu nchini Uganda, Zari Hassan, ambaye pia ni mfanyabiashara mkubwa na mzazi mwenza wa mwanamuziki Diamond Platnumz amekuwa akitajwa sana kwenye vyombo vya habari kuliko wanawake wengi, na mara nyingi kati ya hizo amekuwa akitajwa kwa ubaya.

Mwanadada huyu mwenye taswira ya utata amekuwa akitajwa kwenye vyombo vya habari vya nchini Uganda vikimuelezea kwa taswira kadhaa kama mrembo wa Uganda mwenye watoto watano, mtalaka wa milionea – Ivan Don Ssemwanga na sasa mzazi mwenza wa mmoja wa wanamuziki wanaolipwa pesa nyingi zaidi hapa Tanzania, Diamond Platnumz.

Shutuma nyingi anazopewa kwenye vyombo vya habari zimesababisha achukiwe na baadhi ya mashabiki zake na wakati huohuo kumuongezea mashabiki wapya wengi zaidi ya wanaomchukia. Japokuwa wengi, hasa mahasimu wake hawatakubali, Zari ni mwanamke ambaye kila mwanaume angependa kuwa naye.

Zifuatazo ni sababu 6 za kumfanya mwanaume atake kumuoa Zari wakati wowote:

1. Anajua kupika

Tunaanza na hili kwakuwa tofauti na wengi ambao wanaotengeneza kucha na kuosha mikono kwa bei ghali kama yeye wasingekubali kuingia jikoni kupika na badala yake wangetumua wafanyakazi wa ndani kwa ajili ya kazi hiyo. Mara mbili ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa jikoni akipika na hilo huwezi kuliona kwenye akaunti nyingi za ‘wanawake wa mjini.’

2. Ana uhusiano mzuri sana na wanae

Ingawa inaonekana anapitia mengi akiwa na mzazi mwenzie (Diamond), Zari amekuwa na uhusiano mzuri sana kati yake na watoto wake. Muda mwingi anakuwa nao na moja kati ya nyakati zilizodhihirisha hili ni katika mazishi ya mtalaka wake, Ivan. Hata wakati ambao Diamond alikuwa hajafika, alibaki kuwa imara kwa ajili ya wanae wakubwa.

3. Tukiongelea uimara alionao, tazama jinsi anavyokabiliana na maneno mengi yanayosemwa na mahasimu wa mapenzi kati yake na Diamond Platnumz

Hakumshambulia wala kumkosoa mpenzi wake huyo Diamond aliposema kwamba huwa anamtafuta akiwa na hamu ya kufanya mapenzi kwakuwa Zari si muaminifu. Pamoja na utoto huu aliofanya Diamond, ambao bila shaka Zari haupendi, bado ameweza kumsamehe na kuendelea maisha yao ya pamoja.
Kwa wengi, hili halikuchukuliwa kama ni uamuzi wa busara uliofanywa na mwanamke huyo, bali lilitafsiriwa kama anang’ang’ania mapenzi na Diamond, hata kama ananyanyaswa. Mbali na tafsiri zote zitazotolewa na mashabiki, uwezo wa mwanamke kusamehe jambo kama hilo kutoka kwa baba wa wanae linaonesha ungangari wa hali ya juu kabisa, hasa ukizingatia kwamba mambo mengi maishani mwake yalikuwa yanamuendea kombo, ikiwemo kifo cha mtalaka wake mwezi Mei.

4. Anajiweka kwenye mvuto wa hali ya juu siku zote, muda wote

Akiwa na umri wa miaka 35 na watoto watano, Zari bado ana muonekano wa kuvutia sana kana kwamba ni binti wa miaka ishirini. Amekuwa akiwatoa udenda wanaume wengi akiposti picha akiwa amevaa kivazi cha kuogelea kinachoweka wazi maumbile yake akiwa mapumzikoni, ikiwemo ya hivi karibuni alipokuwa mapumzikoni jijini Mombasa na mpenzi wake Diamond. Anafanya mazoezi, anakula vyakula sahihi na pia anawaambia mashabiki zake wa Instagram siri za urembo wake. Tuweke kando nguo za bei ghali anazovaa.

5. Kuhusu watoto, hajali kuhusu kujiwekea idadi wala uzazi wa mpango

Ukiacha watu maarufu nchini Kenya kama Julie Gichuru mwenye watoto wanne na Akothee mwenye watoto watano, Zari ni mtu pekee maarufu anayejulikana kwa kuzaa watoto wengi kwa urahisi. Kwa kuangalia picha zake tu, mtu yeyote anaweza kukubali kwamba Zari anapenda kuwa mama na jambo hilo ni nadra sana kulipata kwa wanawake kwenye tasnia ya sanaa na burudani.


6. Anaweza kusimamia vizuri biashara na miradi ya familia

Zari hapati tabu kabisa kubadili muonekano wake wa mvuto wa kimapenzi na kuvaa suti kuwa tayari kibiashara. Mtalaka wake Ivan Don alipofariki, Zari amepewa mamlaka yote kuhusu usimamizi wa mali za watoto wake na ameachiwa kuendesha biashara nyingi ambazo walikuwa wakizifanya kwa ubia. Kwa upande mwingine, Zari ameshaanza kuwekeza kwa ajili ya watoto wake wadogo kwani mpaka sasa mtoto wa mwisho ni balozi wa kampuni ya nguo za watoto. the difference:  Zari is one of the few who chose not to let them define her.

Hali ya Yusuf Manji Yahuzunisha Wengi Mitandaoni... Kulia Ndio Muonekano Wake wa Sasa

$
0
0
August 4 2017 Upande wa serikali umewasilisha pingamizi la awali Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga maombi ya dhamana ya mfanyabiashara Yusuf Manji. Pingamizi hilo limewasilishwa leo na wakili wa serikali, Paul Kadushi mbele ya Naibu Msajili, Sian Mustafa kutokana na Jaji Isaya Arufan anayesikiliza maombi hayo kutokuwepo.

Katika pingamizi hilo, wakili Kadushi amedai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana ya Manji. Pia kiapo kilichowasilisha cha kuhusu dhamana kinadosari kisheria, pamoja na kuwepo kwa vifungu visivyo sahihi. Baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Msajili Mustafa ameahirisha kesi hiyo hadi August 7/2017 kwa ajili ya kusikilizwa.

Mambo ni Moto, Ndikumana Mume wa Irene Uwoya..Amtusi Jack Wolper Kwa Kuingilia Yasio Muhusu....

$
0
0
Mambo ni Moto, Ndikumana Mume wa Irene Uwoya..Amtusi Jack Wolper Kwa Kuingilia Yasio Muhusu, Baada ya Wolper kuandika waraka kupitia ukurasa wake wa instagram akimshutumu Ndikumana......

Haya Hapa Ndio Mambo aliyoandika Jack Wolper kufanya ndiku Amjibu:



Toa Maoni Yako Hapo Chini:


Nafasi za Kazi Zilizotangazwa leo ingia www.ajirayako.co.tz

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo


Baada ya Kutangaza Kununua Ndege, Sasa Askofu Gwajima Kuleta Umeme Megawati 250

$
0
0
Baaada ya kimya cha muda mrefu Askofu Mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima, Mchungaji Josephat Gwajima ameibuka na kutangaza kuleta ndege aina ya 'Jet' Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wake.

Mchungaji Gwajima ambaye hivi sasa yupo mjini Birmingham, Alabama nchini Marekani kwa shughuli zake za injili na mikutano mbalimbali ameahidi ataleta ndege aina ya 'Jet'

"Muda si mrefu nitaleta Tanzania ndege hii 'Jet' kwa lengo la kukuza falme ya Mungu" alisema Gwajima

Mbali na hilo Mchungaji Gwajima akiwa katika ziara zake hizo za kiroho alidai kuwa amepata umeme megawati 250 kutoka nchini Ujerumani ambazo anaamini zitasaidia taifa letu la Tanzania katika kukuza sekta ya viwanda.

"Nimepata Umeme Megawati 250 kutoka Ujerumani kwa ajili ya Taifa letu katika juhudi za kuunga mkono Tanzania ya Viwanda. Nilimtuma Engineer Mkuu wa Ufufuo na Uzima Duniani Eng.Yeconia Bihagaze huko Ujerumani kufanya ufuatiliaji, Umeme huu ni kwa ajili ya Watanzania wote na ujenzi wa uchumi imara wa Tanzania ya Viwanda" alisema Mchungaji Gwajima

Hata hivyo mchungaji Gwajima aliwahi kuahidi pia ataleta treni la kisasa linalotumia Umeme Tanzania.

Mwanamuziki Ben Pol Ajibu Tuhuma za Kwanini Mziki Tanzania Havuki Mipaka zilizoletwa na Pana Music....

$
0
0
Msanii Ben Pol amejibu tuhuma zilizotolewa na kampuni ya kimataifa ambayo ilimsajili kusimamia kazi zake ya Pana Music, kwamba wasanii wengi wa Tanzania wanafeli kwenda kimataifa kwa sababu muziki wao unalenga soko la ndani pekee.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television Ben Pol amesema msanii yoyote hapa nyumbani soko la ndani ndio muhimu, kwani kipato kikubwa kinatokana na dili za hapa hapa ndani, tofauti na zile za nje.

"Tukubali tukatae, mpaka sasa hivi tunavyozungumza 'potential market' ya muziki wetu ni Tanzania, vipato vya wasanii na maproducer asilimia zaidi ya 85 vinatokea nyumbani, kwa hiyo hapa tukiongelea mifano ya wasanii wenzetu ambao wana kasi zaidi ya kimataifa, tukiangalia soko lao, source za vipato vyao kwa asilimia kubwa wanavipata kwa Watanzania wenzao na kwa makampuni ya Tanzania, hii inamaanisha kwamba soko la nje kasi yake ni ndogo kidogo", alisema Ben Pol.

Pia Ben Pol amesema kitendo cha mtu kukwambia uache soko la muziki la ndani na kufikiria la nje sio kitu kizuri, kwani soko la nje kwa wasanii wa Tanzania bado halijafanikiwa kwa asilimia kubwa.

"Hatutakiwi kukata tamaa, hatutakiwi kuishia njiani, mtu akikwambia uachane na soko la ndani huyo ni adui yako, lazima ulinde soko lako la ndani alafu hayo mengine ndiyo yanaongeza soko la nje", alisema Ben Pol.

Taarifa ya Polisi Kuhusu Watu Wanaojifanya Kuwa Maafisa wa Polisi....

$
0
0
Katika siku za hivi karibuni kumejitokeza kikundi cha watu wanaotumia vibaya jina la Jeshi la Polisi kwa kujifanya ni Maafisa wa Jeshi la Polisi na kuwatapeli watu kwa kigezo cha kuwapatia ajira.

Watu hao wamesambaza taarifa kupitia mitandao ya kijamii inayosomeka ‘Vigezo sifa za kujiunga na Jeshi la Polisi’, huku ndani yake ikitaja sifa ambazo kwa mujibu wa kikundi hicho ndizo anazopaswa kuwa nazo mtu anayeomba nafasi ya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Jeshi la polisi linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa taarifa hizo ni za uongo na zenye lengo la kupotosha Umma kwa madhumuni wanayoyajua wao wenyewe. Pia zipo taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa wapo watu wanaoombwa kutoa fedha na matapeli hao ili waweze kuwapatia nafasi ya ajira hizo.

Wananchi watambue kuwa Jeshi la Polisi lina utaratibu wake mzuri na wa wazi wa kuajiri. Pale Serikali itakapotoa idhini ya kuajiri watumishi wapya  utaratibu huo utatangazwa kwa  wananchi ili waweze kuufuata kuomba nafasi hizo.

Jeshi la Polisi linawataka wananchi kutoa taarifa juu ya kikundi hicho kupitia kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nawe au ofisi za Serikali ili watu hao waweze kukamatwa na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Wananchi mnashauriwa kupata taarifa sahihi za Jeshi la Polisi kupitia website yake ambayo ni www.policeforce.go.tz au akaunti ya twitter www.twitter.com/tanpol pamoja na Facebook www.facebook.com/tanpol

Imetolewa na:

Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
Dar es Salaam

Hausigeli Amchoma Moto Mtoto wa Bosi

$
0
0
Inasikitisha! Hausigeli aliyetajwa kwa jina moja la Maua anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Mbezi kwa Yusufu kwa kudaiwa kumchoma moto mdomoni, mkononi na kumpiga kwa mwiko kwenye uti wa mgongo, mtoto wa miaka miwili aitwaye Nasra.

NI KIMARA DAR

Tukio hilo la kusikitisha, limetokea hivi karibuni maeneo ya Kimara- Bonyokwa jijini Dar, nyumbani kwa bosi wa hausigeli huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Karan.

SIMULIZI YA UCHUNGU

Akisimulia kwa uchungu, mama wa mtoto huyo, mama Karan, alianza kwa kuelezea jinsi alivyompata hausigeli huyo na kusema kwamba amesikitishwa na kitendo cha kinyama alichokifanya binti huyo.

MSIKIE MAMA KARAN

“Msichana huyu nililetewa na rafiki yangu kutoka Morogoro, alikuwa hajamaliza hata mwezi mmoja tangu afike. “Alipofika kwa mara ya kwanza alionesha kuwapenda sana watoto mpaka nikamuamini na kuondoa wasiwasi, nikawa naenda kazini na kuwaacha watoto nikirudi nawakuta salama na kila kitu kipo sawa.

UPEPO WAGEUKA…

“Baada ya kupita kama wiki hivi, watoto wangu walianza kunililia, wa kiume mwenye miaka 5 na wa kike mdogo mwenye miaka 2. “Mkubwa ndiyo akawa analia sana na kuniambia mama usiende kazini nikamuita dada mbele yao na kumuuliza kwani dada unawapiga watoto? Mbona wananililia? Nikamuuliza na mtoto mkubwa akawa haongei, anamuangalia dada muda mwingi,” alisema mama Karan.

Akizidi kuzungumzia tukio hilo huku mara kadhaa akitokwa na machozi, mama Karan alisema baada ya kuona kitendo hicho, alipata shaka. “Nilihisi kuna tatizo, nikawaita majirani zangu mbele yake na kuwaambia watoto wanavyonililia na jinsi nilivyohisi kuna jambo limetokea. “Wakaniahidi kuwaangalia watoto kama kuna jambo baya wangenifahamisha.

Niliendelea na kazi bila wasiwasi kwani nilijua kama kuna kitu kinachoendelea nitafahamishwa,” alisema mama huyo.

HAUSIGELI AIFUNGA SIMU YA BOSI

Mama Karan alisema, siku chache baadaye, baada ya kuona majirani watakuwa wakimtonya matukio yake kwa simu, aliomba simu ya bosi wake kijanja na ‘kuibloku’. “Baada ya siku chache nimerudi nyumbani dada akaniomba simu yangu ya mkononi na kuniambia kuwa simu yake haina vocha anaomba aongee na dada yake, nilimpa sasa sijui aliifanya nini maana baada ya hapo sikupata tena simu yoyote. Aliiblok kila sehemu nilipomuuliza akaniambia kuwa yeye hajui kuitumia inawezekana amegusa sehemu ambayo siyo. “Sikujali nilikwenda kazini lakini pia nilimwambia mume wangu ili aje aitengeneze lakini kabla haijatengenezwa ndiyo tatizo likatokea,” alisema.

SIKU YA TUKIO

Mzazi huyo alizidi kuelezea tukio hilo kwamba siku binti huyo alipofanya unyama huo, alichelewa kupata taarifa kwani simu yake ilikuwa haipo hewani. “Siku ya tukio nilikuwa kazini kumbe nyumbani watoto wanapigwa sana na dada yao majirani walikuwa wakinitafuta lakini hawakunipata.

“Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumamosi (iliyopita) nilipotoa tu mguu kwa maelezo ya majirani aliyeanza kupigwa alikuwa ni mtoto wangu mkubwa akaomba msamaha akahamia kwa mdogo akampiga sana, kaka yake akaanza kumuomba amsamehe lakini akachukua rungu na kumpiga kisha akamwambia anyamaze.

KIPIGO KIKAENDELEA

“Kipigo kwa mtoto mdogo kiliendelea wakawa wanalia kwa sauti huku mkubwa akimuombea msamaha mdogo wake kwani alikuwa akimpiga na mwiko mpaka akauvunja.

AWANYAMAZISHA KWA KUWATISHIA MOTO

“Wakati wakiendelea kulia msichana huyo aliwaambia atawachoma moto wakiendelea kupaza sauti.

MAJIRANI WAINGILIA KATI

“Majirani waliposikia kelele walikwenda kumuita msichana huyo wakimsihi kufungua mlango kwani alikuwa amewafungia kwa ndani ili mtu asifungue lakini aliwaambia hayawahusu. “Huwezi amini, jirani mmoja alifika akagonga mlango kwa nguvu ndiyo sauti ya mtoto ikasikika ikilia mama ananichoma moto na mkubwa akaendelea kusema mama dada anamchoma moto mtoto,” alisema.

MAJIRANI WAKIMBILIA KWA MJUMBE

Mama huyo alisema, baada ya kumkosa kwa njia ya simu majirani walikimbilia kwa mjumbe ambapo hawakumkuta wakaamua kurejea pale nyumbani.

BOSI AFIKA

Bi mkubwa huyo aliweka bayana kuwa wakati majirani wanarejea pale nyumbani, bahati nzuri na yeye akawa amefika. “Nilipofika nikiwa sina hili wala lile lililotokea nyumbani muda wa saa kumi na moja hivi nikagonga mlango ukawa haufunguliwi nilipoita Maua akaitika na kusema mama umerudi akafungua mlango.

“Nikawauliuzia watoto kwani sikuwaona akaniambia mmoja amelala na mwingine alikuwa amekwenda tuisheni kwani kulikuwa kumepoa lakini akajistukia na kuniambia huyu mtoto mdogo anaumwa hawezi hata kutembea alianguka alipokwenda kwa jirani. “Kiukweli nilichanganyikiwa nikamchukua na kumvua nguo kumuangalia amepatwa na nini kwani nilishakuwa na mawazo mengine. “Nilikuta mtoto ana majeraha ameumia hawezi hata kutembea.

Nilimbana dada wa kazi ili aseme ukweli lakini alikataa katakata na kusema kuwa hajamfanya lolote, wakati namuuliza majirani wakaja wakanikuta na kuanza kumpiga Maua tukambemba mpaka kwa ili aseme kilichomkuta mtoto.

ASEMA UKWELI

“Alipofika kwa mtendaji msichana huyo alikataa katakata lakini alipobanwa na walinzi shirikishi alikubali na kusema amempiga na mwiko na huwa anawapiga kila siku na kuwazuia wasiseme kila wanapokataa kula chakula.

MTOTO MKUBWA ATOA USHUHUDA

“Mtoto mkubwa alipotakiwa kutoa ushuhuda wa kilichotokea akasema dada amekuwa akiwapiga kila siku na kusimulia mkasa mzima wa siku hiyo ambapo dada aliwapiga na kumchoma moto mtoto mdomoni pamoja na mkononi lakini mwisho pia alimpiga mtoto na mwiko wa kupikia kwenye mashughuli (mwiko mkubwa anaoutumia mama yao) na mwiko huo umevunjika,” alisema.

Baada ya ushuhuda wa mtoto na dada wa kazi kukiri kisha kuomba msamaha, mama Karan na majirani walimpeleka Maua Kituo cha polisi Mbezi kwa Yusufu ambapo alifunguliwa kesi kwa namba ya faili iliyosomeka RB: KMR/RB/10570/2017 KUJERUHI ili sheria ichukue mkondo wake.

MTOTO APELEKWA HOSPITALI

Kutokana na majeraha mbalimbali aliyoyapata mwilini mtoto huyo, mama yake alilazimika kuchukua kibali cha polisi na kumkimbiza Hospitali ya Palestina kwa ajili ya matibabu. Alipotafutwa Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, ACP Murilo Jumanne ili kuzungumzia tukio hilo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa ila tunaamini Jeshi la Polisi lililo chini ya IGP Simon Sirro litatenda haki ili kama binti huyo amefanya ukatili huo, sheria stahili zichukuliwe ili iwe fundisho kwa wengine.

NENO LA MHARIRI

Kutokana na matukio ya aina hii kuanza kushamiri, ni vyema wazazi wakawa makini na wasichana wa kazi wanaowaajiri kwa kufuatilia mienendo ya watoto wao na mabinti hao kudhibiti matukio haya.

Source: Global Publisher

Mbwana Samatta Alimwa Kadi ya Njano na Kufungwa 2-1

$
0
0
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Champion Boy’ usiku wa Ijumaa alionyeshwa kadi ya njano timu yake, KRC Genk ikifungwa mabao 2-1 na wenyeji, Standard Liege katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege.

Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo katika mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu ya Ubelgiji, Genk ikicheza bila kushinda baada ya Jumamosi iliyopita kulazimishwa sare ya 3-3 na Waasland-Beveren Uwanja wa nyumbani, Luminus Arena.

Samatta jana alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 41 ikiwa ya tano tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kisemokrasia ya Kongo (DRC) na bahati nzuri kwake hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu.

Mbwana Samatta jana ameonyeshwa kadi ya njano timu yake, KRC Genk ikifungwa mabao 2-1 na Standard Liege

Katika mchezo huo, Genk walitangulia kupata bao, lililofungwa na mshambuliaji kinda wa miaka 21, Siebe Schrijvers dakika ya 36, kabla ya kiungo Mbrazil Edmilson Junior kuwasawazishia wenyeji dakika ya 48 na mshambuliaji Mkongo, Paul-Jose M'Poku Ebunge kufunga la ushindi dakika ya 63.

Huo unakuwa mchezo wa 57 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, kati ya hiyo mechi 34 alianza na mechi 21 alitokea benchi.

Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar e Salaam, amefunga jumla ya mabao 19.

Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Vukovic, Maehle, Brabec, Colley, Khammas/Nastic dk55, Berge, Heynen/Ingvartsen dk69, Writers, Buffalo/Malinovskyi dk80, Trossard na Samatta.

Standard Liege Setup: Ochoa, Agbo/Marin dk45, Dossevi, Scholz, Pocognoli, Bope, Fai, Edmilson, Laifis, Mpoku/Kosanovic dk83 na Sa.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images