Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Masogange na Nywele za Rihana.....Jionee ...Nishidaah

$
0
0
Kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM mwanadada Agnes Gerald aka Masogange, Bila kuandika chochote ameweka picha kuonyesha mtindo wa nywele za mwanadada RIHANA na kisha kuweka mtindo wa nywle aliouweka, ambao unafanana na ule wa RIHANA....pendeza sana mama.....we unaonaje?

Wabunge Waumbuana Kupokea Rushwa Bungeni

$
0
0
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga (Chadema), amewaumbua wabunge wenzake kuwa wanapeana na kuchukua rushwa ndani ya Bunge.

Suzan aliyasema hayo juzi jioni wakati akichangia katika mkutano wa Chama cha Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Rushwa (APNAC). Suzan alisema vitendo hivyo vya rushwa vilionekana wakati wabunge hao walipokuwa wakiwachagua wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

“Rushwa ilikuwa ni wazi wazi ukienda chooni unapewa laki mbili (Sh200,000) unaondoka,”alisema Suzan.

Alisema wao kama viongozi ambao wanatunga sheria na wanatakiwa kuisimamia serikali wanapaswa kuwa waadilifu. Hata hivyo, Mbunge wa Njombe Kaskazini, Deo Sanga (CCM), alisema hakuna ukweli kuhusu jambo hilo la baadhi ya wabunge kuchukua rushwa hadi chooni.

Hata hivyo, Mbunge wa Tunduru, Mtutura Mtutura (CCM), alimuunga mkono Suzan na kusema suala hilo ni la kweli na kwamba kama Sanga hakuliona walikuwa wanamkimbia.

“Alichokizungumza Suzan ni cha kweli. Kaka yangu (Sanga) walikuwa wanakukimbia. Ni kweli hilo lilifanyika,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu wa APNAC, Vita Kawawa, alisema si vyema wabunge wenye taarifa kuhusiana na masuala ya rushwa wakatoa taarifa katika ofisi za Spika na kamati ya maadili ili liweze kufanyiwa kazi mara moja.

“Ni vyema mkatupa taarifa kitu ambacho kinaashiria rushwa sisi tupo, ofisi ya spika ipo na kamati yetu ya maadili,”alisema.

Alisema rushwa ni mdudu ambao unatakiwa kukataliwa na kila mtu. Alisema rushwa imesababisha maisha ya wananchi kutobadilika ingawa uchumi wa nchi unakuwa.

Mvutano Mkali Bunge, Mahakama

$
0
0
Kitendo cha Mahakama kufungua milango kwa mawaziri na wabunge kufunguliwa mashtaka kutokana na kauli watakazozitoa bungeni ambazo ni kinyume cha Katiba na Sheria, kimeonekana kuwachanganya viongozi hao ambao wamesema kuwa wanalindwa na sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.

Wamesema licha ya kuwa kazi ya Mahakama ni kutafsiri sheria, Bunge kutunga na Serikali kusimamia sheria, nchi nyingi duniani wabunge wake wana kinga na hawashtakiwi kwa kauli watakazozitoa bungeni.

Kauli za wabunge hao zimekuja ikiwa imepita siku moja tangu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kutoa msimamo huo wakati ikitoa uamuzi wa pingamizi la awali katika kesi ya kikatiba iliyokuwa ikimkabili Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililowasilishwa na Jopo la Mawakili wa Serikali wakiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG, George Masaju.

Kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013 ilifunguliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), dhidi ya Pinda na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), aliyeunganishwa kama mlalamikiwa wa pili.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake juzi ilikubaliana na baadhi ya hoja za mawakili wa utetezi (Serikali) na kuitupilia mbali kesi hiyo, lakini ikatamka kuwa wabunge na mawaziri wanaweza kushtakiwa kwa kauli au jambo walilolitamka bungeni, linalokiuka sheria na haki za binadamu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, Naibu Spika Job Ndugai alisema, “Mahakama ikisema, imesema licha ya kuwa Katiba inaeleza wazi kuwa Bunge lipo huru.”

Alisema kuwa suala hilo linaweza kuwekwa sawa katika Katiba Mpya ambayo mjadala wake utaendelea Agosti mwaka huu.

“Nchi nyingi duniani wabunge wana kinga kwa kauli zao watakazozitoa bungeni. Kama hapa kwetu tumeamua hivyo ni sawa tu, ila mashtaka yatakuwa mengi kwelikweli,” alisema Ndugai.

Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla (CCM) alisema, “Sidhani kama tafsiri hii ni sahihi sana kwa sababu wabunge wanalindwa na Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.”

Kigwangalla alisema sheria hiyo ipo wazi kwamba mbunge akizungumza lugha isiyofaa mtu ambaye anataka kuchukulia hatua anatakiwa kuiandika barua Ofisi ya Bunge.

“Barua hiyo itakwenda kwa Spika wa Bunge na kama akiridhika atalipeleka suala hilo katika Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge ambayo inaweza kumwita mlalamikaji ili kumsikiliza,” alisema Kigwangalla.

Alifafanua kuwa sheria hiyo haijawahi kufanyiwa marekebisho na kama mahakama imetoa tafsiri hiyo maana yake ni kwamba kesi za wabunge zitarundikana mahakamani.

Jay Z Amemtimua Bodyguard aliyedaiwa Kuchepuka na Beyonce!

$
0
0
Tuhuma za Beyonce kumsaliti Jay Z na kutoka na mlinzi wake aitwae Julius De Boer zilisambaa mwezi uliopita huku likiwaacha mashabiki wao midomo wazi.

Katika hali inayoonekana kuwa Jay Z amezifanyia kazi kwa msisitizo zaidi, Beyonce ameonekana mitaani akiwa mlinzi mwingine ambaye hakufahamika huku wengi wakiuliza nini kimemkuta Julius? Au ndio katimuliwa kabisa?

Taarifa za awali zilidai kuwa Julius alikuwa karibu sana na Beyonce huku ikielezwa kuwa mara nyingi waliposafiri pamoja kwenda ziarani, walikaa hotel moja na mlinzi huyo  huku akiingia mpaka chumbani kwake.

Inadaiwa kuwa Jay Z aliamua kumfukuza kazi Julius lakini Beyonce aliweka ngumu.

Rihanna Awajibu TLC Waliomponda Kuwa Anauza Ngono kwa Kuvaa Nusu Mtupu

$
0
0
Vazi la Rihanna katika tuzo za mitindo za CFDA mwaka huu limeendelea kuwa gumzo na wengi wamemshambulia kwa madai ya kutojali maadili.

Member wa kundi la TLC, Chilli na T-Boz nao hawakusita kumpa makavu live wakati wanafanya mahojiano na kipindi cha SunRise cha televisheni ya Australia. Walisema kuhusu mavazi hayo na kueleza kuwa Rihanna anauza ng9no.

“Ni vigumu kwetu kusema kitu kwa sababu wakati wowote tukifanya hivyo, ‘oh, lazima TLC wanaona wivu’, lakini hivyo ndivyo ilivyo. Naliita koleo..koleo.

“Sisi tuliuza na kuwa kundi kubwa la wasichana la muda wote lililouza zaidi, tukiwa tumevaa nguo zetu. Ni rahisi kuuza ng9no.” Amesema T-Boz.

Ujumbe umemfikia Rihanna nae hakulaza damu akajibu mashambulizi. Kwanza alibadili picha yake ya Twitter (Twitter header) na kuweka picha ya wasichana hao wa TLC, Chilli na T-Boz wakiwa vifua wazi. Katika picha hiyo wasichana hao wawili wanaonekana wakiwa wamefunika vifua vyao na mikono.

Baadae alibadili na kuweka picha yake akiwafanya mzaha na kutoa ulimi nje, halafu akaiandika,  “When there’s no changing the fact that I’m me, and they’re well…they’re them.”

Ray C Anakuja na Taarab, Asema Khadija Kopa Ajiandae

$
0
0
Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kudai kuwa ujio wake mpya kwenye muziki atakuja pia na nyimbo za taarab, huku akimtaka Khadija Kopa ajiandae.

Akizungumza na Sporah Show hivi karibuni, Ray C amesema kwenye albam yake ambayo inakuja hivi karibuni kunamchanyiko wa nyimbo mbalimbali zikiwemo taarab na zakihindi.

“Nimefanya taarab kama mbili na zook, yani nimebadilishika kabisa, kuna kwaito , kuna bongoflave ,uwindi hindi kidogo, taarab nimeimba pia ,kwaiyo Khadija Kopa ajiandae”Alisema Ray C.

Pia Ray amedai kuwa aina ya muziki anaokujanao kwa sasa hivi ni ule wa kuonyesha kipaji chake zaidi cha kuimba na siyo kucheza.

Lulu Michael na Nando wa Big Brother Mambo Hadharani si Siri Tena

$
0
0
Stori: Musa Mateja na Mayasa Mariwata

Mambo hadharani! Uhusiano wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013, Amir Nando umewekwa kweupe.

Kabla ya wawili hao kufunguka, kulikuwa na madai mazito kuwa Lulu na Nando ‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando kutolewa BBA kwa ukosefu wa nidhamu.

Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Nando ambaye mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu ni mwanamke anayefaa kuolewa (wife material) lakini alipoulizwa kwa msisitizo, alikana kuwa na uhusiano na mrembo huyo.

“Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake,” alisema Nando.
Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa.

Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema.”

CCM na Chadema Ngoma Droo Picha Fake za Wabunge Wakila Uroda

$
0
0
VITA ni vita! Siku mbili zimekatika tangu sakata la picha ya pozi inayodaiwa kuwa ni ya mheshimiwa Komba na msichana aliyetajwa kwa jina moja la Angel kutoka kwenye baadhi ya vyombo vya habari Bongo, lingine limeibuka!

Hili la safari hii ni zito pia. Lenyewe linamhusu mheshimiwa mmoja ambaye anadaiwa ni mbunge wa Chadema. Na yeye anasemekana kwamba alipiga picha katika pozi tata na ‘totoz’ ambaye jina lake halikupatikana.

Baadhi ya watazamaji wa picha hizo ambazo zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, walisema kwa vile mheshimiwa Komba ni wa CCM na mwenzake ni wa Chadema ni kama ngoma droo!

KWA NINI NGOMA DROO?
Maoni ya watu yanasomeka kwamba, vyama hivyo viwili ndivyo vyenye ushindani mkubwa katika jamii hivyo viongozi wao kuning’inizwa kwenye mitandao kwa madai hayo hakuna atakayesema mwenzake anahusika na hujuma hiyo huku wale wa Cuf, NCCR-Mageuzi na vyama vikingine vikionekana kuachwa nyuma kwenye ‘fasheni’ hiyo mpya.

“Ingekuwa mwingine ni wa CCM pia, si ajabu CCM wangesema Chadema wanahusika, sasa ni CCM kwa Chadema. Hapo mnasemaje? Hamuoni kwamba ngoma droo?” Alihoji mmoja wa wachangiaji hao kwenye mjadala huo wa wanasiasa kuzidi kuchafuana kwa kasi.

MITANDAO YA KUCHAFUA
Habari zilizochimbwa na Ijumaa Wikienda zilidai kuwa, katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 kumeibuka kundi linalojiita Umoja wa Kambi Huru ‘Ukahu’ ambao kazi yao kubwa ni kuwachafua wanasiasa kwa habari za kweli au za kuwatungia.

“Kuna watu wanasema kuna Ukahu, yaani Umoja wa Kambi Huru wakiwa na maana hawapo CCM wala Chadema. Wao kazi yao ni kuwachafua wanasiasa tu kwa ajili ya kuelekea uchaguzi mkuu mwakani,” kilisema chanzo.

Kikaendelea: “Lakini nasikia hawa watu wanatumiwa na viongozi wa wapinzani wa wanasiasa. Mfano, Komba kama ana mwanasiasa anataka ang’oke kwenye jimbo lake mwakani, basi anawindwa kuanzia sasa ili achafuke na watu wasimame wakisema yeye si msafi.

“Unaambiwa hao jamaa wa Ukahu, hata kama ulifanya madudu mwaka 2005, wao wanayapata tu, kama huna wanakutengenezea madudu ya kufanana na wewe.”
WABUNGE WAJIPANGE, PICHA ZAIDI ZIPO
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa bado kundi hilo lina picha ambazo baadhi ya wabunge walipiga au walitengenezewa wakiwa na vimwana ambazo zimepangwa kutolewa moja baada ya nyingine kadiri siku zinavyokwenda kuelekea uchaguzi mkuu.

WABUNGE WENGI KUANGUKA
Taarifa zanasema kundi hilo limejipanga kuhakikisha kwamba kwenye mizengwe hiyo, katika kila wabunge 10, 4 hawatarudi kwenye majimbo yao mwakani bila kujali vyama.

WABUNGE VIJANA WAKAE CHONJO
Ikazidi kudaiwa kuwa wabunge vijana, hasa wenye umri wa kuanzia miaka 25 hadi 50 ndiyo wapo kwenye tageti hiyo. Mheshimiwa Komba ana miaka 60, mwenzake 44.

KISA NINI HASA?
Ijumaa Wikienda liliendelea kuchunguza zaidi na kubaini kwamba, kisa cha mambo yote hayo ni kukomoana hasa kwa wale wanasiasa ambao wanatamani kuwa wabunge kwenye majimbo ambayo wanaamini kuwatoa wahusika waliopo sasa madarakani si rahisi.

“Mimi jamani najua siasa, wapo wanasiasa wanatamani sana majimbo ya wenzao, sasa kwa vile wanajua kuwatoa si rahisi, wanapendwa sana ndiyo maana wanatumia njia ya kuwachafua ili wapiga kura wasiwapende na wao washike nafasi,” alisema mbunge kutoka jimbo moja la Mkoa wa Dar.

Akaendelea: “Siamini kama wabunge wetu wako hovyo kiasi hicho, kwamba wanaweza kuwa wapo ndani ya vyumba vya gesti na wanawake halafu wakaamua kupiga picha chafu, wana akili zao.”
GPL


Htaimaye Flora Mbasha Ajitokeza Baada Ya Sakata La Mdogo Wake Kubakwa na Mumewe, Na Hiki Ndicho Alichokipost

$
0
0
Baada ya kutokea sakata la mdogo wa Flora Mbasha Kubakwa na mume wa Flora, hatimaye Flora ajitokeza katika akaunt yake ya facebook. atupia picha hiyo hapo juu lakini bila caption yeyote ile ikiwa na Maana Maisha yanaendelea Kama Kawa

Picha za Harusi ya Mbunge wa Chadema Joshua Nassari ilivyofana Jijini Arusha

$
0
0



Hatimae mbunge wa Arumeru mashariki mh. Joshua Nassari na Bi. Anande Nnko wafunga pingu za maisha na kuwa mwili mmoja katika kanisa la Kilinga na baada ya hapo kuelekea katika viwanja vya Usa- River Academy ambako ndiko sherehe ilipofanyika.
Siku ya Jumamosi tarehe 7 Juni 2014 itakumbukwa na wawili hawa kama siku yao ya kumbu kumbu ya ndoa yao, pamoja na wageni wengi waliojitokeza, viongozi wa kiserikali pamoja na wale wa kisiasa, taasisi na dini walikuwepo kwa wingi. Tunawatakia ndoa njema na Mungu awalinde.

Kizazi cha Wanaume Wahongaji Chapotea Taratibu, Kizazi cha Wanaume Bahili Chashika Chati kwa Kasi!

$
0
0
Mwenzangu IS IT JUST ME AU NDO GAME LIMECHANGE SIKU HIZI? Au ndo nimeshakuwa mbuzi mzee bila taarifa? Naaaaaaah! Wanaume mnakoelekea siko. SIKO SIKO KABISAAAAA! Whats up with the NEO COLONIALISM? Msisahau nyie ni Waafrica, mambo ya kuiga iga uzungu unaweza jikuta unaunga mkono harakati za Cameroon bila kujijua.

Tukiangalia history kidogo ya uhongaji na ulaji bata TZ na Africa kwa ujumla utagundua vijana wa zamani au wazee wa leo wlikuwa in their 20's - 40's miaka ya 70 ndo walikula bata batani. Wanawake walifaidi vibaya mnoo. Hata mipedeshee inayohonga sana mjini hapa ni ya vijana wa early 70's manake uchumi ndo ulikuwa umekolea mahala pake, mambo ya ndustrial substitution program, mikazi ya kumwagaaaaaaaa! Kwenda nje kama kwenda chooni tu, ukimaliza kozi hii unaenda hi. Kanisa nalo ndo llimwaga mischolarship, transition ile raisi mwenyewe janki tu. Vijana walikula bata batani. Starehe ilikuwa enzi hizo, saivi kuosha macho tu, Marijaniiii alihamia mtaa wa 7 Baraka mwishee na marashi ya pemba, Jojinaa oooh jojinaaaaaaa! Acheni kabisaaa.

Late 70's ikapita vita vya kagera hapo, mambo yakawa si mambo, devaluation of currency ikafuatia, na Economic depression ya 1980's bata kidogo lilisitishwa na nchi ikaingia crash program. Maisha yalivaa bukta kidogo. endi zikafa zikafa, ndo maisha yakawa ki communist. Bata lilianza kusahaulika, vijana wakakimbilia kuiona bahari,wengine ndo wakazamia us uk, dubai n.k.

Alhamdullilah miaka ya 1990's bata lilirudi kwa kasiiii! Mashallah na mie nilikua dogo tu primary ila bata nililifaudu kidogo. Maisha yakawa si haba. Vijana 1990's pia bata waliligegedua. Na vijana sio haba wanawake walifaidi sio masikhara. Wengi walikuja mjini na mbio za mwenge na malori kuolewa 1990's. Na ugolkipa enzi hizo 1990's haikuwa big issue kabisaa.

2000 mpaka leo hali inazidi kuwa BORA YA JANA NA JUZI! Kizazi cha wanaume BAHILI kinasambaa kwa kasi mnooo. Mnoo mnooo! kHAAA! Tena hawa wadogo ndo balaaaaaaa! Sijui binti zetu wataishije. Looooooooh! Ndo maana watu wanajiweka kwa vizee, vijana wa 1970's na 1990's

Nimeuwa alarmed sabab juzi ki cousin changu 21, kimenialika na Bf wake out, sipendi kuwadoea watoto lakini a sster needs to be Polite, basi BF anamwambia live ALIPE? Na chenyewe kinalipa!? Kidogo nimnas mambao! Eti kaniambia IM OLD SCHOOL, siku hzi ukiwa tegemezi hupati BF wa ukweli!!!!!!!!! WTF? Damnnnnnnn! Nikasema YOUNG LOVE! She will GROW OUT OF IT IN NO TIME! Chezea jiji hili.

Next shosti wangu ananikopa like 3m, na sio kawaida yake manake ni BAHILI hatari. Nikawa curious tu nikamuuliza za nini kam ni emergency nikukopee kwa loan sharks. Akaniambia Baba D (Mume wa mtu ila wamezaa na huyu shosti wangu) ndo anamuomba ampige tafu! I was like IM REALLY GETTING OLD SCHOOL! Say whaaaaaaat? Nikamwambia maybe its about time you REPENT AND RETURN TO CHURCH! Haya mambo ya mume wa mtu, you have waited for so long, the kid ana 4yrs hajamuacha mkewe, hatoaa amuache, you shuld come to terms na hilo uanze kudate, u aint too old, God is mercyfull anaweza kukupa mumeo. (Not that i care she repents or not ila kuzaa na mume wa mtu na wewe kumuhudumia huyo mwanaume IT IS INSANITY! of the highest order too.)

Siku hizi hata waume za watu sio SAFE ZONE tenaa! Nako kuna KUSAIDIANA. Mmmh! KALI A MWAKA! Shosti yangu kaja kuniomba ushauri, ana BF (A very good man, will make best husband ever) wana date 5 YRS, Sasa ndo kaja kumwmbia anataka amuoe ila HELA YA HARUSI HANA/ MSICHANA NDO AFINANCE MCHONGO MZIMAA! Wooo! Woo! Woo! Yaani mwanaume anataka na ana nia ya dhati ya kumuoa ila bank hana hata mia!! Loh! So bibie ndo asimamie SHOW YOTE! Hela ikitakiwa kuanzia mahari, utambulisho, harusi, gauni lake ETC. Hata ya mwaname kwenda nayo kuanzisha kamati. Na kitachopelea kwenye kamati ajipange mdada! Mm!!! Msichana akamwambia NITAFIKIRA! (Uwezo wa kufanya hivo anao ILA IS IT RIGHT JAMANI? IS IT FAIR? Ujigharamie mpaka pete yako ya harusi.? Ndo idea yenu ya mgawanyo wa majukumu??) Mama mkwe akampigia anampa budget a utambulisho huko kijijini Mil 2? Yaaani msichana awatumie ili wajiandae akatambulishwe!!! LIKE SERIOUSLY! Mimi nibakia tu SPEECHLESS! Manake nikita neno wakaoana wasije ninyima chansi la kusimamia bureee!

KIZAZI HIKI CHA WANAUME CHANITISHA NA KUNIOGOFYAAAAAAAAA!

Hali ni Mbaya Brazili Wafanyakazi wa Usafiri Waendeleza Mgomo..Kombe la Dunia Wahaha

$
0
0
Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa muda usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama ya nchini Brazil, kuamuru wafanyikazi hao kurudi kazini mara moja.

Amri ya mahakama ya kazi nchini Brazil imewataka wakuu wa vyama vya wafanyikazi wa usafiri wa mjini Metro, kufuata taratibu za kudai haki zao nasi kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuanzisha mgomo ambao umedumu tangu juma lililopita.

Wakiandamana katika mitaa mbali mbali ya mjini Sao Paulo wafanyakazi wa idara ya usafiri walibeba mabango yaliyoonyesha malalamiko yao, kwa kudai nyongeza ya mishahara, huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa na msongamano wa magari umezidi kuongezeka mjini humo.

Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.  

Hali ya sintofahamu imeendelea kutanda miongoni mwa viongozi wa serikali ya nchini Brazil pamoja na wajumbe wa kamati ya maandali ya fainali za kombe la dunia, kwa kuhofia huenda hali ikawa mbaya zaidi juma hili ambapo siku ya Al-khamis mji huo utakuwa mwenyeji wa shamra shamra za ufunguzi wa fainali za kombe la dunia.

Robin Van Parsie: Nilicheza soka kwa uchungu kwa kipindi cha miaka sita

$
0
0
Mshambuliaji wa klabu ya Man utd pamoja na timu ya taifa ya Uholanzi Robin Van Parsie amesema yupo fit kwa ajili ya kulitetea taifa lake kwenye fainali za kombe la dunia ambazo zitaanza kuunguruma siku tatu zijazo huko nchini Brazil.

Robin Van Parsie ametangaza kuwa tayari kwa ajili ya fainali hizo, akiwa mbele ya waandishi wa habari nchini Brazil ambao walitaka kufahamu maendeleo ya afya yake ambayo kila mara imekua ikikumbwa na mushkel.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema hakuwahi kuwa fit kama ilivyo sasa, hasa ikizingatiwa alikuwa akitumikia mchezo wa soka kwa kipindi cha miaka sita iliyopita kwa uchungu kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimkabili.

Amesema baada ya kutaabika kwa muda mrefu hana budi kulishukuru jopo la madaktari lililomtibu na kufikia alipo sasa na pia anaamini jopo la madaktari wa timu ya taifa ya Uholanzi wanajua namna ya kukabiliana na hali yake pale itakapokwenda tofauti.

Baada ya Diamond Kukosa Tuzo Instagram Pamechafuka, Diva Ajitoa Team Wema

$
0
0
Daah hii ni NOUMA sana...Kama mnavyojua, Msanii wetu hapa 255,  Diamond hakufanikiwa kupata TUZO  za MTVmamaAWARD hapo jana  huko South Africa. (Sio mbaya sana kushiriki tu kwangu Diamond ni ushindi)

Na kama unavyojua tena huko kwenye mtandao wa  INSTAGRAM kuna AKAUNTI  mbalimbali ambazo zina  WSAPOTI Diamond na Wema na zingine hazi WASAPOTI... Kwa kifupi wapo walio ponda na wengine kumpongeza kwa hatua aliyofikia...ISHU YENYEWE NI HIVI!!

Diva wa Clouds FM kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM na alijitokeza na kumpongeza DAVIDO kwa kuchukua TUZO kuwa ndio alikuwa ana DEZEVU (Best Male: Davido (Nigeria) ambayo pia Diamond alikuwa anashindania)....hapa ndio MOTO ukawaka...wale wote (wengi wao) wanaojiita TEAM WEMA walimuibukia na kumponda sana DIVA ambae hivi karibuni sema hadharani kuwa yeye ni TEAM WEMA [SOMA HAPA]

Kufuatia KOMENT  nyingi kutoka kwa watu wa TEAM WEMA kumtukana na ku DIS na Kususia kwenda kwenye SHOW  yake ambayo itafanyika leo BILLS

Diva amewaponda Team  Wena na kujitoa Rasmi :

Vibamia Jitahidini Basi Mnatutesa Wanawake

$
0
0
Ni kitu kisichopingika, wanaume wengi wazurii chini hawana kitu kabisaa,samahani kama nitakuwa nimewatukana ila ni ukweli mtupu,
Pia licha ya maHB kuna wengine hawana UHB ila nao vibamia..Hapo kuna mgawanyiko wa wanaume sasa,

Kuna wale ambao,kwenye mambo yote are zero,yaani kwenye kukushika anashika kama anabofya keypad au anatomasa embe,denda ndo kabisa hajui kitu,akija kwenye kumalizia yaan daah,ni shida na kibamia chake.

Kuna wale ambao wako so romantic yaani,wanahendo safi kabisa yaani unaona pepo hii, akija kutoa mamaaaa kibamiaa, yaani mtu hata akivesha ndom inakuwa kama soksi ya mkubwa kavaa mtoto kha!!!! 
Na wengi hata kwenye kuvua utaona anajishaua,ukimuwahi utaona anajizugisha kumbe anajua utaona mapema

SWALA NI KWAMBA:Tunajua kwamba Mungu kawapa maumbile hayo,hauwezi ukabadilisha hata iweje,basi jitahidini hata kuchagua styles ambazo zitasaidia mwenzio kujisikia kidogo raha,Maana vinginevyo unamuacha mwenzio na magenye ya ajabu,unadhani ataenda kumalizia wapi imagen wewe ndo babysweet wake au wewe ndo mume?si ndo mwanzo wa usaliti huu?

Wanawake tulio wengi hatupendi vibamia,ila ikatokea kibamia akawa mtaalamu wa kujihami unaweza ukadumu na kushinda game,otherwise hapo tegemea kudharauliwa haijalishi we ni HB wala nini UHB ni kwenye yaliyomo kwenye suruali bana..
Wewe kibamia ukiona umedumu na mwanamke,jua huyo dada ni mgeni na akijanjaruka tu utamsahau hata jina lake..
Mimi mwenyewe sifeel kibamia kabisa,na ikatokea nimekutana nacho nasepa kimya kimya.mambo gani ya kuchomeka mtu akikohoa knatoka,tena vingine bila hata kukohoa...

Natanguliza samahani kwa #Teamkibamia lakini nimekuja tu kuwaelezea ni jinsi gani mnavyotuachia maumivu..

Huyu Irene Uwoya ni Mzuri Wema Sepetu Hapa Anasubiri Miaka Mia

$
0
0
Mtoto Mlaini Mayai Hajui Mkorogo ni nini na hana majigambo ya ovyo kikubwa nachokipendea kwa Irene Hana Magroup na Ushoga wa Kijinga hapa mjini wala hapendi umbea, akiongea kama hataki , ana mtoto mmoja lakini bado yupo Fit ....

Kifo cha Recho Chamfanya Wolper Afute Mipango ya Kuzaa kwa Kuogopa Kifo

$
0
0
Mwana Bongo Movies amejitokeza na kufunguka kuhusu yeye kushika mimba na kuzaa Jisomee hapa chini alichosema:
"Najua ni Wajibu Wetu kuzaa ila nimekuwa muoga sana wa kushika mimba kwa sababu naogopa kuzaa na nikikumbuka kifo cha Recho ndio Kabisa Hofu Inazidi 

Naitaji Mtoto ila si leo wala kesho nahitaji kujenga ujasiri upya , ila kama ikitokea nitajitahidi kuvumilia"

Mrembo Vera Sadika Awaacha Mashabiki Huo, Wabaki Midomo Wazi

$
0
0


Mrembo Maarufu Kenya Vera Sadika Akifanya Yake Jukwaani Huku watazamaji wakimuangalia wakiwa hawaamini anachofanya ......

Nando Afunguka Kuhusu Stori zilizo Sambaa Kuwa Ana Mahusiano ya Kimapenzi na Lulu Michael

$
0
0
Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa (the chase) 2013, Amir Nando ameweka wazi kuwa hajawai kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanadada wa filamu, Elizabeth Micheal aka Lulu, lakini anakubali sana.

Akizungumza na Global Tv ,Nando amezungumzia pia mipango yake ya kufanya filamu na mwanadada huyo wa filamu.

“Lulu nishaonana nae, mara mbili mara tatu lakini sina uhusiano nae na sijawai kuwa na uhusiano nae, ila namkubali sana, mwanamke unajua mzuri, shepu, mwonekano wake, michezo yake, tunaonana tu ile oya niaje mara mbili mara tatu. Na proposal mimi, akitaka tukae chini tutengeneze movie, hicho ndicho nachotaka nifanye, akikubali tutafanya, lakini Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake” Alisema Nando

Bajeti yampeleka Kikwete Dodoma, Ataraji Kukutana Kwanza na Wawakilishi

$
0
0

Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili Dodoma keshokutwa, ikiwa ni siku moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/15.

Habari zilizopatikana jana zinasema Rais ataongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachopewa muhtasari kuhusu Bajeti ya Serikali ya mwaka ujao wa fedha na baadaye atafuatilia uwasilishaji wa bajeti hiyo bungeni akiwa Dodoma.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yuko likizo lakini akaweka bayana kwamba kwa kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa bungeni, lazima Baraza la Mawaziri lipewe muhtasari wa bajeti husika.

“Ni kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa, Rais huongoza kikao cha Baraza la Mawaziri yaani pre budget cabinet meeting ambako Waziri wa Fedha hutoa briefing (muhtasari) kuhusu maeneo muhimu ya bajeti, kwa hiyo siyo jambo jipya ni suala la kawaida,” alisema Rweyemamu.

Itakumbukwa kuwa mwaka jana kabla ya kusomwa kwa bajeti ya 2013/14, Rais Kikwete alikuwa Dodoma ambako pamoja na kukutana na mawaziri, pia alifanya kikao na Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Hata hivyo, uwepo wake mjini Dodoma safari hii umekuja wakati kukiwa na dalili za mvutano mkubwa kati ya Bunge na Serikali kutokana na kutotolewa kwa fedha za kutosha za maendeleo kwa mwaka wa fedha unaoisha Juni 30 mwaka huu.

Taarifa zinasema bajeti inayomalizika mwishoni mwa mwaka huu, inapungukiwa kiasi cha Sh1.8 trilioni, huku Serikali ikilaumiwa na wabunge kwa kutoa misamaha ya kodi inayofikia Sh1.52 trilioni, ambayo ingepunguza nakisi iliyopo kwenye bajeti kwa asilimia 84.4.

Wakati wa mjadala wa bajeti za wizara tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Mei 6 mwaka huu, wabunge wamesikika mara kadhaa wakilalamika kwamba fedha za maendeleo zilizotolewa kwa wizara katika bajeti ya 2013/14 ni kati ya asilimia 25 na 30, jambo ambalo limesababisha kukwama kwa miradi mingi.

Keshokutwa itakuwa siku ya mwisho ya mashauriano baina ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Bunge kupitia Kamati yake ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.

Mazungumzo hayo yaliyoanza Juni 5 mwaka huu, yalilenga kuangalia uwezekano wa kutafuta vyanzo vipya vya mapato ili kuwezesha kuzingatiwa kwa ushauri wa wabunge, pamoja na kusaka fedha kuziba pengo la Sh1.8 trilioni katika bajeti ya 2013/14.

Alipoulizwa jana, Chenge hakuwa tayari kuzungumzia hatua iliyofikiwa katika mashauriano hayo na badala yake alisema kwa ufupi: “Ndugu yangu mambo ya Bunge, tutakutana kwenye taarifa yetu ya kamati tutakayoiwasilisha bungeni.”
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images