Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104764 articles
Browse latest View live

Mahakama Kuu Imepiga Chini Pingamizi la Maalim Seif

$
0
0
August 11, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali maombi ya Bodi ya CUF inayomuunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif ya kutaka Msajili wa Vyama vya Siasa asitoe ruzuku kwa CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba.

Maombi hayo namba 21 ya mwaka 2017 yametupiliwa mbali na Jaji Wilfred Dyansobera, baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata anayemuwakilisha mdaiwa wa pili Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kusema kesi imeitishwa kwa ajili ya uamuzi.

Katika uamuzi maombi hayo ambayo mdaiwa wa kwanza ni Prof. Lipumba, Jaji Dyansobera amesema anakubaliana na moja kati ya pingamizi la AG kwamba vifungu vya sheria vilivyotumika kufungua shauri hilo sio sahihi.

Hata hivyo, amesema anakubaliana na hoja za Bodi hiyo iliyo upande wa Maalim Seif kwamba suala la Bodi hiyo kutokuwa na uhalali linahitaji ushahidi wa kina.

Aidha, kuhusu suala la Maalim Seif kusaini hati mbalimbali za shauri hilo bila kupewa mamlaka, amesema hilo sio pingamizi kwani Mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa kuangalia kiapo tu.

”Hivyo mahakama imetupilia mbali maombi hayo, kwa sababu sheria iliyotumiwa kufungua maombi hayo sio sahihi, lakini waombaji wanaweza kukata rufaa ama kufungua kesi nyingine.”

Baada ya kuelezwa hayo, upande wa Maalim wamesema watafungua upya kesi hiyo


Historia Fupi ya Mlinzi wa Mbunge Aliyeshinda Ubunge Kenya

$
0
0

Historia Fupi ya Mlinzi wa Mbunge Aliyeshinda Ubunge Kenya
Aliyekuwa Afisa wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, Nimrod Mbithuka alipofika katika Bunge Kenya mwaka 1998 alipewa jukumu la kumlinda Waziri Francis Nyenze.

Nyenze alikuwa ameibuka mshindi katika kiti cha ubunge katika jimbo la Kitui Magharibi na ndipo aliteuliwa kuwa waziri na hivyo kupewa mlinzi atakayehakikisha usalama wake.

Siyo yeye tu aliyekuwa amepewa jukumu hilo la ulinzi, bali pia polisi wengine walipewa wabunge wakuwalinda ambapo kazi yake kila siku ilikuwa kuhakikisha usalama wa Waziri Nyenze alipokuwa akitoka nyumbani kwenda bungeni au kwenye shughuli nyingine.



Mbai alikuwa mlinzi wa mbunge huyo kwa miaka minne (1998-2002). Baada ya Waziri Nyenze kushindwa kutetea kiti chake mwaka 2002, Mbai aliteuliwa kuwa mlinzi wa Dr Alfred Mutua aliyekuwa ameteuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali.

Aliifanya kazi hiyo kwa miaka 10 kabla ya kungatuka na kwenda kugombea nafasi ya Ugavana katika Kaunti ya Machakos kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Mwaka 2013, Mbai alijiuzulu kutoka katika utumishi wa jeshi la polisi, na hivyo kuteuliwa na Dr Mutua katika nafasi ya ngazi ya juu kwenye uongozi wa Kaunti.

Katika uchaguzi wa ubunge uliofanyika Agosti 8 mwaka huu, Mbai aliibuka na ushindi katika eneo hilo lililotawaliwa na Chama cha Narc akimshinda mbunge wa sasa wa eneo hilo, Meja Mstaafu Marcus Mutua Muluvi.

Katika uchaguzi huo, Mbai ambaye ni Mbunge Mteule wa Kitui Mashariki alijizolea kura 14,256 akimuacha mbali mpinzani wake Militonic Kitute aliyepata kura 10,899 akiwa ni mgombea wa Chama cha Narc huku Meja Muluvi wa Chama cha Wiper akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 5,436.



Wakati akifanya shughuli za kiutendaji katika ofisi ya Gavana Mutua ndipo alianza msingi wa kujikita zaidi katika siasa. Kabla ya hapo amewahi kufanya kazi kama afisa anayehusika na masuala ya ugatuzi, kilimo, mifugo na maendeleo ya uvuvi.

Wakati akisoma katika Shule ya Sekondari ya Wavulana iliyopo Kitui Kusini, walimu wengi walikuwa wakimsifia kwamba anaweza kuwa kiongozi kutokana na tabia walizoziona ndani yake.

Awali alikuwa mlinzi wa mtu, lakini kuanzia atakapoapishwa kuwa mbunge, mtu mwingine ataajiriwa kupepeleka kazini, kufungulia mlango wa gari kama sheria inavyoagiza na pia kama alivyofanya yeye kwa Waziri Nyenza na Msemaji wa Serikali, Dr Mutua.

Madaraka na upendeleo wanaopataiwa viongozi mbalimbali huenda vikawa ni sababu za kijana huyo aliyekua akichunga mbuzi katika eneo la Zombe, Kaunti ya Kitui enzi za utoto wake kujiunga katika siasa za ushindani.

KENYA: Tume ya Uchaguzi (IEBC) Imemtangaza Uhuru Kenyatta Kuwa Mshindi wa Urais

$
0
0
KENYA: Tume ya Uchaguzi (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kupata kura asilimia 54.2%.

Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Wanaume Wenye Michepuko

$
0
0

Wanawake wengi walio kwenye ndoa wanahangaika na waume zao kwakuwa na uhusiano wa kimapenzi na michepuko. Yafuatayo ni mambo kumi ambayo yawezekana ulikuwa huyajui kuhusu wanaume wenye michepuko:

1: Wanaume wengi wanakuwa bado wanawapenda sana wake zao wakati huo wakiwa wanachepuka. Wengi huwa wanafanya hivi ili kuona mwanamke mwengine anaweza kumridhisha kwa kiasi gani, au wanaamua kuchepuka kutokana na migogoro iliyopo ndani ya uhusiano au ndoa yao.

2: Mara nyingi, wanaume wanachepuka na wanawake wanaojuana nao. Ni rahisi sana kwa mwanaume kuchepuka na mwanamke anayejuana naye kwakuwa kwa yule asiyejuana naye vizuri, inamaanisha mchakato wa kutongoza inabidi uchukue nafasi yake, wakati mwanaume anahitaji kumaliza shida zake za kufanya mapenzi kwa muda huo. Kuanza kuzungushana na mwanamke mpya ni sawa na kuishi matatizo ya uhusiano wake kwa mara nyingine zaidi, lakini kwa mwanamke anayejuana naye, hasa anayejua mgogoro wao wa uhusiano, ni rahisi kutimiza haja za mwanaume huyu kwa kumfariji.

3: Wanaume huchepuka kuokoa ndoa zao. Wanaume wanawapenda wake zao lakini wengi hawajui jinsi ya kutatua matatizo ya ndoa yao, kwahiyo wanajikuta wakienda nje ya ndoa kuziba mapengo yaliyomo kwenye ndoa yao. Wanaume wanataka kupata kila kitu na wengi wana mawazo kwamba mchepuko utamfanya asahau matatizo kwenye ndoa yake. Baada ya hapo wanaume wanarudi kwa wake zao na kuishi maisha ya furaha—wao na wake zao—bila kutafuta suluhu ya matatizo ya ndoa yao.

4: Wanaume huwa wanajilaumu baada ya kuchepuka. Wanaume wengi wakipata matatizo kwenye ndoa zao hukimbilia kwa michepuko kujaribu kupoza machungu yoyote waliyoyapata na mara baada ya kumaliza starehe alizofata hujikuta akijilaumu kwa kumsaliti mkewe na kutofanya jitihada ya kutafuta suluhu ya matatizo ya ndoa yao.

5: Wanaume wengi wenye michepuko hujificha wanapoanzisha uhusiano wa nje. Kujificha huku kunatokana na wao kujua wazi kwamba wanachokifanya si sahihi hivyo hawataki kuwasababishia machungu wake zao wakiwa na ufahamu kwamba matatizo yaliyopo kwenye ndoa yao hayana haja ya kuchochewa zaidi kwa kufanya uhusiano na mchepuko kuwa wazi kwa watu wengi, jambo litakalomuumiza zaidi mkewe.

6: Wanawake nao wanachepuka kwa spidi ileile ya wanaume na uhusiano huu ambapo mwanamke huwa anachepuka huwa ni hatari zaidi ya yale ambayo mwanaume ndiye anayechepuka. Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Indiana nchini Marekani unaonesha kuwa wanaume na wanawake wanachepuka kwa uwiano sawa, lakini sababu zao za kuchepuka ni tofauti. Wameeleza kwamba wanawake wanapochepuka huwa ni kutokana na sababu za kujiridhisha kihisia. “Kuchepuka kwa mtandao—bila uhusiano wa kimwili—ni uchepukaji wenye madhara makubwa zaidi,” utafiti huo umebaini. Kutengeneza uhusiano wa kihisia (kinachofanywa na wanawake) na mtu mwingine inamaanisha umekubali kuachana na ndoa yako. Lakini kama ni muingiliano wa kimwili tu (unaofanywa na wanaume) huwa na hauumizi sana kwakuwa huchukuliwa ni kitendo kinachomuumiza mwenzio tu, na si kwamba amemponda mtu kihisia.

7: Mara nyingi mke huwa anajua kwamba mumewe ana mchepuko. Ingawa mwanaume huwa anadhani anajificha au anaficha uhusiano wake na mchepuko ili kuepuka kumuumiza mkewe, imebainika kuwa mara nyingi sana mke huwa anajua kuhusu mchepuko huo ila anabaki kuangalia nyendo za mumewe kuona kama zitasaidia kupoza mtafaruku uliopo kwenye ndoa yao.

8: Wanandoa hawawezi kutatua mgogoro wowote uliopo kati yao endapo mwanaume atakuwa na mchepuko. Hii ni kwa sababu mke anakuwa na kinyongo kwakuwa mumewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, na mwanaume anakuwa na wasiwasi wa kuongea na mkewe kwa sababu ya kuhofia kuwa mazungumzo hayo yanaweza kuibua uhusiano wake na mchepuko. Hivyo, matatizo kwenye ndoa yanabaki kutotatuliwa kwakuwa wanandoa wenyewe hawapati muda wa kuyazungumza na kutafuta suluhu.

9: Mara nyingine kuwa na mchepuko husaidia kutatua matatizo ya ndoa. Je, michepuko ndio chanzo cha kuvunjika kwa ndoa? Si mara zote. Kwakuwa uhusiano mpya unakuwa na hamasa kubwa, mchepuko unaweza kusaidia kuamsha hisisa za mapenzi yenu. Mwanaume hujua nani anayemtaka maishani mwake na kwamba uhusiano alioanzisha na mchepuko hauna utulivu kama alivyotarajia. Kama ilikuwa ni kujisahau kwa mara moja tu basi ni rahisi kwa mwanaume huyu kurudi kwa mkewe.

10: Mke si wa kulaumiwa kwa mumewe kuwa na mchepuko. Zingatia mfano ufuatao: kama mumeo ana mchepuko, hili si kosa lako, haijalishi watu watakwambia nini. Mwanaume anapochepuka ujue ameamua mwenyewe kufanya hivyo. Mawazo kwamba ameshawishika au ameteleza na kujikuta amefanya mapenzi na mchepuko si kweli kabisa. Mwanaume hachepuki kwa sababu ya vitu atakavyovipata kwa mwanamke mwingine, anachepuka kwa kufikiria vitu anavyovikosa kwa mwanamke wake. Lawama zinaibuka kwa sababu ya wawili hao kudharau matatizo waliyonayo na kutoyatafutia suluhu.

Kutana na Mtabibu wa Asili Allan Shariffu Musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH shariffu musa Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na shariffu musa Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi

+255 629793352 au watsap
+255 679119679

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Hali ya Kenya Baada ya Kutangazwa Kenyata Mshindi

$
0
0
Hali ya Kenya Baada ya Kutangazwa Kenyata Mshindi
Hali ya kawaida imeanza kurejea mjini Garissa siku moja baada ya matokeo ya uchaguzi wa urais kutangazwa.



Rais Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais Ijumaa usiku baada ya kupata kura 8, 203, 290 sawa na asilimia 54.2 zilizopigwa.

Mgombea wa upinzani Raila Odinga alipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.7

Baada ya matangazo, visa vya maandamano viliripotiwa katika baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani, mfano Kisumu, Homa Bay na Migori magharibi mwa nchi hiyo.

Sehemu ya soko kuu mjini humo iliteketezwa Jumatano wakati wa ghasia kati ya wafuasi wa wagombea wawili wa ugavana. Lakini jana na leo hali imekuwa tulivu.

Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay, amepiga picha hizi za wananchi wakiendelea na shughuli zao za kawaida leo asubuhi.

 

Mke wa Roma Ataja Mstari Unaomnyima Usingizi Katika Wimbo wa 'Zimbabwe’

$
0
0
Mke wa Roma Ataja Mstari Unaomnyima Usingizi Katika Wimbo wa 'Zimbabwe’
Mke wa R.O.M.A ,Nancy au Mama Ivan  amefunguka mengi kuhusu masahiri yaliyomo kwenye  ngoma  mpya ya mume wake iliyotambulishwa hivi karibuni katika vyombo mbalimbali vya habari aliyoipa jina la ‘Zimbabwe’ 



Akifanya mahojiano maalum kupitia kipindi cha Exclusive Interview cha Global TV, mama Ivan ameutaja msitari unaomuumiza na kumnyima usingizi ni kuhusu mmoja wa wabunge aliyetamka hadharani bungeni kuwa msanii huyo amemtukana Mkuu.

Msitari wenyewe;

..Na kuna mbunge alisema eti nimemtukana Mkuu, atahukumiwa na mkono wa Mungu,…. kwanza lini na kwa nini? Mimi nimtukane Mjomba? Umepewa gari la wagonjwa mimi Tanga ananijengea bomba…!

“Huo ndiyo msitari ambao unaniumiza, nikikumbuka yule mbunge aliyesema muacheni atekwe, anamtukana Rais? Kiukweli R.O.M.A hajawahi kumtukana Rais, ameimba kitu kilichomtokea, kilichomgusa na kipo moyoni. Sisi tumemwachia Mungu, tunasali sana na Mungu ndiye atahukumu mwisho wa siku,” alisema Mama Ivan.

Mama Ivan ameshukuru namna wimbo huo ulivyopokelewa na mashabiki wa R.O.M.A ambayo yamewashangaza wengi na kuvunja rekodi kwa muda mfupi ikiwa ni pamoja na kuwashukuru watanzania wote walioungana naye na kumfariji wakati wa matatizo.

Dodoma Pamenoga Leo Uchaguzi Mkuu TFF

$
0
0

Dodoma Pamenoga Leo Uchaguzi Mkuu TFF
Shughuli ya Uchaguzi Mkuu wa TFF imeanza mkoani Dodoma ambapo wajumbe kutoka mikoa tofauti hapa nchini wameanza kujitambulisha.


Tangu jana mjini hapa kumekuwa na heka heka kwa wajumbe na wagombea kuhakikisha kambi zao zinapata kura nyingi kuelekea katika uchaguzi huo.

Wagombea wengi mpaka kufiki jana walikuwa wako bize kuomba kura kwa wajumbe ikiwa jana ilikuwa siku ya mwisho wa kampeni.

Hata hivyo, hadi kufikia jana hakuna mgombea ambaye alikuwa na uhakika wa nani anachakua nafasi ya Jamal Malinzi katika nafasi hii ya urais.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu jana, ulionyesha Wallace Karia na Ally Mayayi walikuwa wakipewa nafasi kubwa katika nafasi ya urais.

Mmoja wagombea wa nafasi ya Urais, Fredrick Mwakalebela, aliliambia Nipashe kuwa kwa sasa jukumu limebaki kwa wajumbe huku akijipigia upatu kuwa yeye ndiye mtu sahihi wa kuiongoza TFF.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Revaocatus Kuuli, aliliambia Nipashe kuwa mpaka kufikia leo mchana majibu ya nani amekuwa kiongozi wa TFF yatakuwa yamepatikana.

“Uchaguzi utakuwa wa haki na halali kwa kila mgombea, tutampata mtu ambaye atakuwa amechaguliwa na wajumbe,” alisema Kuuli.

Alisema Kamati yake inasimama kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki na kwa yeyote atakayekiuka kanuni ya uchaguzi chombo husika, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), itafanya kazi yake.


Baba Achapwa Viboko na DC Baada Watoto wake Kuvunja Kioo cha Gari

$
0
0


 Baba Achapwa Viboko na DC Baada Watoto wake Kuvunja Kioo cha Gari


MKUU wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amemcharaza viboko mzazi wa mmoja wa watoto walioshambulia gari lake kwa mawe na kuvunja kioo cha nyuma jana.

Gari hilo lenye namba za usajili STL 669, lilishambuliwa na watoto watatu katika barabara kuu ya Kondoa-Dodoma, kwenye kijiji cha Paranga wilayani Chemba.

Kufuatia kupasuliwa kwa kioo hicho, DC alisimamisha gari hilo na kuwakimbiza watoto waliolipiga mawe, hali iliyozua purupushani kwa muda.

DC huyo aliwakimbiza watoto hao kwa lengo la kuwakamata na kuwaadhibu lakini hakuweza kuwakamata baada ya kumzidi mbio.
Hata hivyo, wananchi walioshuhudia tukio hilo walimtajia DC majina na sehemu wanakoishi watoto hao ili awafuate majumbani kwao.

Ndipo mmoja wa wazazi wa watoto waliohusika na shambulio hilo alikutwa nyumbani akiendelea na shughuli zake na alipohojiwa na DC kuhusu malezi ya mtoto wake, aliingia katika majibizano yaliyomkera DC Odunga.

"Malezi? Malezi gani unataka kwangu? Mtoto ametoka shule, mimi nitajuaje anayoyafanya mtaani?" Aliuliza mzazi huyo wa kiume na kufafanua kuwa "mimi najua (mtoto) yuko shule, sijui kama amevunja kioo chako."

Ndipo DC alipoonekana kukerwa na majibu hayo hivyo kuchukua fimbo na kuanza kumcharaza mzazi huyo huku akimshutumu kwa malezi mabaya.

DC alimcharaza viboko mzazi huyo wa kiume kabla ya kumuingiza kwenye gari la polisi akiwa amefungwa pingu, kwa madai ya kuendelea kujibu kwa jeuri wakati akiulizwa maswali kuhusu malezi ya mtoto wake.

Mzazi huyo aliendelea kujibu kuwa hastahili kupigwa kwa kuwa kosa si lake na kusema kuwa apelekwe popote pale, lakini haki yake itajulikana kwa sababu wakati watoto hao wanapiga mawe kioo cha gari yeye hakuwepo.

Watoto watatu hao waliofanya tukio hilo wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka saba hadi 10.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia Odunga na mzazi huyo wakivutana huku mzazi akisikika akisema "aliyevunja kioo ni mtoto... chukueni tu hatua vyovyote haki yangu nitaipata".

Mwenyekiti wa kitongoji anakoishi mzazi huyo aliingilia kati na kudai kuwa matukio hayo ya kurushia mawe magari katika eneo hilo yapo na walishayakemea katika mkutano wa kitongoji yakapungua.

Alisema wahusika huwa ni watoto na vijana wa eneo hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Odunga alisema kijiji hicho kimekuwa na tabia ya kuweka mawe barabarani pamoja na kupiga magari mawe jambo ambalo siyo sahihi.

Alisema wanajipanga kwa ajili ya kuanza operesheni ya kuhakikisha tabia hiyo inakomeshwa kabisa "kwa sababu ni hatari kwa wasafiri na jamii kwa ujumla".

Alisema wataendelea na msako wa polisi ili kubaini familia ambazo zina vijana wenye tabia hiyo kupitia jamii inayowazunguka.
Kufuatia purukushani hiyo gari la polisi wilaya lilitinga katika eneo hilo na kuwachukua watu sita wakiwahusisha na upigaji mawe magari, akiwemo mtoto mmoja aliyetajwa kuhusika jana.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema ameagiza watu hao waliokamatwa watolewe rumande.

Alisema Jeshi la Polisi litaendelea na upelelezi kwa ajili ya kukusanya ushahidi wa tukio hilo na baadaye hatua zaidi zitachukuliwa kwa wahusika.

Kamanda Mambosasa alisema amechukizwa na kitendo cha Mkuu huyo wa Wilaya kujichukulia sheria mkononi na kumjeruhi mzazi huyo.

"Amemjeruhi maeneo ya kichwani kwa rungu na mkono wake umevimba kutokana na kipigo alichokipata." alisema Kamanda Mambosasa. "Hii si haki kiongozi kujichukulia sheria mkononi."

Aidha, Mambosasa alisema mtoto aliyevunja kioo ni wa miaka tisa hivyo kisheria hawezi kushtakiwa popote kwa kuwa analindwa na sheria.

Wapiga Debe Wapigwa Marufuku na Jeshi la Polisi

$
0
0
Wapiga Debe Wapigwa Marufuku na Jeshi la Polisi

Kutokana na kuwepo kwa vitendo vya wizi na uporaji wa mali za abiria katika vituo vya daladala vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojulikana kwa jina la wapiga debe ,Jeshi la Polisi kanda Dar es salaam limepiga marufuku shughuli za upiga debe


Jeshi la Polisi limeahidi kuwachukulia hatua baadhi ya madereva na makondakta watakao ruhusu magari yao kupigiwa debe na vijana hao


Kaimu kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lucas Mkonya amesema wananchi wengi wamekua wakipeleka malalamiko juu ya wizi huo unaotokea kwenye vituo vya daladala unaofanywa na baadhi ya wapiga debe kwenye vituo hivyo ambapo amesema jeshi hilo litaendesha oparesheni maalum katika vituo vyote vya daladala siku ya Jumatatu kwaajili ya kuwaondosha wapiga debe.


Suala la uwepo wa matukio ya uporaji wa mikoba pamoja na mabegi ya wakina mama na baadhi ya wageni kutoka mataifa mengine katika maeneo ya mijini ikiwemo Posta, Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewakamata watu ishirini na tatu wakiwemo vinara wanne wa matukio hayo ya uporaji kwa kutumia boda boda.


Aidha Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam katika oparesheni zake limefanikiwa kuwakamata zaidi ya watu 270 wanaotuhumiwa kujihusisha na makosa mbalimbali ya hihalifu ikiwemo unyang'anyi kwa kutumia nguvu na silaha na kukutwa na dawa za kulevya.

Niyozima Awapa Shule Yanga

$
0
0
Niyozima Awapa Shule Yanga



KIUNGO mpya wa kimataifa wa Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amewafichulia wapinzani wao wote wa Ligi Kuu Bara mambo ya ndani kuhusu kiwango chao akiwataka kujipanga vilivyo kuelekea ligi hiyo hapo Agosti 26, mwaka huu.


Akizungumza na gazeti hili jana, Niyonzima alisema kiwango walichoonyesha katika mechi dhidi ya Rayon ni sehemu ndogo ya "ufundi" walionao wachezaji wa timu hiyo ambao msimu ujao wamejipanga kuipa klabu yao mataji.


Kiungo huyo aliyetua Simba hivi karibuni kwa kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, alisema kila mchezaji aliyesajiliwa Simba anafahamu kiu ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambao wamekosa ubingwa kwa miaka minne.


Niyonzima alisema kuwa kwa sasa wanaendelea kujifua na kabla ligi haijaanza, watakuwa wameimarika zaidi kwa sababu wachezaji wote wamekamilika na wanafanya mazoezi ya pamoja.


"Tutakuwa wazuri zaidi ligi itakapoanza, tulionyesha kiasi kidogo tu cha uwezo wetu, naamini mashabiki wetu watafurahi zaidi," alisema kiungo huyo wa zamani wa APR.


Naye kipa Aishi Manula alisema kuwa kikosi chao kinaimarika zaidi kila siku zinavyoongezeka huku ushindani wa namba ukiongezeka.


"Kambi ilianza kwa makundi, baadhi tulikuwa katika timu ya Taifa (Taifa Stars) na wengine mchakato wa usajili ulikuwa haujakamilika, sasa tuko pamoja na tunaahidi kuendelea kujituma," alisema kipa huyo aliyetua Msimbazi akitokea Azam FC.


Wakati huo huo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara, alisema kuwa wako katika mazungumzo ya mwisho ya kupata mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo inatarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


Soma Nafasi 10 za Kazi Zilizotangazwa Siku ya Leo

$
0
0

Kutana Mtaalam wa Tiba Asili Mwenye Uwezo Mkubwa wa Kutatua Matatizo Kwa Nyota na Dua

$
0
0
KUTANA NA TABIBU MWENYE KUBRI KUTOKA KWA ALAH MAALIM ISSA NAJIMU. NI SHARIFU
MWENYE UWEZO WA KUBAINI TATIZO LAKO PUNDE TU UNAPO MFANYIA MAWASILIANO KUPITIA
WASAA NA SIKU KWA MAWASILIANO:-
MAALIM ISSA NAJIMU KUTOKA MKOA WA TANGA MWAMBONI MAGOFU KATA YA NGUVU MALI
NCHINI TANZANIA, NI TABIBU MWENYE KUBRI TOKA KWA ALAH ANATIBU KWA NJIA YA VITABU VYA
QUR-AN, DAWA ZA ASILI PAMOJA NA DAWA ZA KIARABU.
ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE / MKOA WOWOTE KWA MATATIZO YAFUATAYO:-

 ULIJALI (NGUVU ZA KIUME)
 MIGUU KUWAKA MOTO
 KUTAFSIRI NDOTO
 MFARAKANO WA WANANDOA
 MFARAKANO KAZINI
 KUPANDSHWA CHEO
 KUTOA PETE YA BAHATI
 ANAO UWEZO WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUBASHIRI
 KUFUNGUA UZAZI KWA WALIYO FUNGWA KWA NJIA YA USHIRIKINA
 KUTOA VIFUNGO VYOTE VILIVYO FUNGWA IKIWA NI KWENYE MWILI WA BINADAMU /MAJUMBANI NA KWENYE BIASHARA.
 ANA UWEZO MKUBWA WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUMPATA YEYOTE UMPENDAYE KWA
KUMUOA AU KUWA NAYE.
 ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIYE MBALI PIA ALIYE CHUKULIWA KWA NJIA YA MSUKULE
 ANAO UWEZO WA KUUAq KESI SUGU NA PYA NDANI SIKU 7 TU.

 MENGINEYO MENGI ZAIDI YALIYO KUWA SUGU PIGA-

 Mobile; 0717 70 32 41.
 WhatsApp 06226 535419.

Mgogoro wa Prof Lipumba na Maalim Seif hautaiacha CHADEMA salama

$
0
0
Lipumba ameshinda kesi ya akina Maalm kibatara na Lissu..

Kwa maneno halisi AMEUBWAGA UKAWA...

Nachekaaaa....hata kama Kipumba wanamwita manina yootee....mimi nilishaa sema toka mda ule kua UKAWA hawana uwezo wa kushinda kesi hii...Na sasa Lipumba anatoka na nguvu mpyaa. Anaanzakuchukua Ruzuku iliyofungiwa na MAALM na wenzake....kifo hiki ni matanga yanayo anuliwa leo tokea KIFO CHA UKAWA miaka miwili iliyo pita!

Kwa Bahati mbaya wengi hawajui...CDM hawapiganii UKAWA ila wanampigania MAALIM hii nikete ya CDM ili iweze kuingia VISIWANI... sio mda mrefu. Kwa taarifa nilizo nazo mkononi....MAALM anajiunga CHADEMA na anapewa UONGOZI mkubwa tuu ili iwe Daraja la kukubalika kwa Cdm...na maalm atagombea ZANZIBAR ....

wanachama wa CUF hawaja jua hadi leo...ugomvi huu ni wa CDM NA CCM...Uwanja wa VITA umechaguliwa uwe CUF... Hapa kinacho gombaniwa ni VISIWA VYA ZANZIBAR...
wana CUF wanaweza kuamua kusimama wenyewe. Bila ccm wala cdm wakaweka mikakati yao wakafunga milango ya kuingia CCM NA CDM hakika wange jinusuru na chama chao.....leo sio mda wanachama wata gawanyika makundi haya...Baada ya Maalm kujiunga na CHADEMA wanachama wengine watamfuata Maalim Cdm na wengine wata Bakia CUF. Nawengine waenda Act wazalendo na wengine wataenda CCM wapo pia watakao amua kuacha SIASA hawa wa kuamua kuacha siasa wata kua wachache wataamua mwa mda kwa ajili ya Hasira lakini kabla ya uchaguzi wa 2020 watarudi kwenye vyama...

Huu mgogoro pia hauta iacha salama CHADEMA...baada tuu ya Maalmu sef kujiunga Cdm na kupewa Uongoz mda mfupi ...ndipo wanachama wenye mapenzi na CUF watapata akili na kujua nani amekua mchichezi wa mgogoro huu...na wanao Zuia Maalm aspatane na IBRAHIM LIPUMBA ni Cdm. Kwa kua Cdm wanaamini Lipumba msimamo wake hataki kuamini juu UKAWA NA LOWASSA...lipumba alikataa mapema na alitoka CUF juu ya ujio wa Lowassa...Cdm Aliye kua mgombea U Rais mwaka 2010 na KATIBU MKUU Dr Slaa alimua kuachana na cdm na kuacha Siasa hii yote ni kwa Ajili ya ujio wa Mzee Lowassa aliye aminishwa na chadema kua Lowassa alikua Fisadi wa nchi namba 9 Cdm walitumia garama kubwa sanaa kutangaza mafisadi akiwemo mzee Lowassa...

Ngoja tuone nini kitaendelea kuelekea 2020.....

Tujadili pamoja

By Francis Jackson/JF

Rais John Magufuli Ampongeza Rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta...Soma Hapa Alichoandika

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter, amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kuchaguliwa kuiongoza Jamhuri ya Kenya kwa muhula mwingine wa miaka 5. Amemtakia mafanikio mema.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (IEBC), Ndugu Wafula Chebukati usiku wa kuamkia leo alimtangaza Uhuru Kenyatta kuwa Mshindi wa kiti cha Urais baada ya kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27 ya kura zote huku mpinzani wake aliyegombea kupitia Muungano wa Upinzani wa NASA Ndugu, Raila Odinga akipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.74 ya kura zote.


Wafanyabiashara Wanaotoa huduma Uwanja wa Ndege (JNIA) Wapewa Mwezi Mmoja Kulipa Kodi na Prof. Mbalawa

$
0
0



Wafanyabiashara Wanaotoa huduma Uwanja wa Ndege (JNIA) Wapewa Mwezi Mmoja Kulipa Kodi na Prof. Mbalawa
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa Mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) kulipa kodi ya Majengo kama mikataba yao inavyolekeza.

Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo leo wakati alipokutana na wafanyabiashara hao ili kujadili changamoto mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzitatua ili kuendelea kutoa huduma bora katika uwanja huo.

“Kulipa kodi za majengo hapa ni suala la lazima, hivyo ifikapo Septemba mwishoni nataka kuona wafanyabiaashara wote mmeshalipa kodi ya pango, makusanyo haya ni muhimu kwetu ili tuendelee na hatua nyingine za uboreshaji wa viwanja vya ndege na huduma nyinginezo,” alisisitiza Profesa Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameutaka uongozi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA), Kuhakikisha mikataba yote ya upangishaji wa majengo inapitiwa upya na kufanyiwa marekebisho ili thamani ya fedha iendane na wakati huu.

Profesa Mbarawa amewahimiza wafanyabiashara hao kubadilika na kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ili kuweza akuendana na ushindani wa kibiashara uliopo ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri kwa wafanyabiashara nchini ili waweze kufanya biashara zao ili kujiingizia kipato  binafsi na kukuza pato la Taifa.

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amekagua sehemu ya kuingilia abiria katika uwanja huo ambapo amesema Serikali itaweka mpango maalum wa muda mfupi kwa wasafiri wanaoenda nje kutotumia muda mrefu katika ujazaji wa fomu wakiwa uwanjani hapo.

“Kwa kushirikiana na taasisi zote zinazotoa huduma katika uwanja huu tutaweka  mpango maalum utakaowezesha wasafiri kuhudumiwa kwa haraka na kwa muda mfupi, Msafiri yoyote anataka huduma za haraka ili waweze kuwahi na sisi tutahakikisho tunakidhi mahitaji ya wateja,” alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi amesema Mamlaka imeshapitia mikataba yote ya wafanyabiashara kiwanjani hapo na hatua inayofata ni kufatilia madeni yote ili kuboresha huduma katika kiwanja hicho.

Bwa. Msangi ameongeza kuwa kwa yale madeni ambayo hayataweza kulipwa kwa wakati taratibu za kisheria zitafuatwa.

Niko Njia Panda..Mchumba Wangu Ana Uume Mkubwa sana....

$
0
0
Nimepata Mchumba japo simpendi sana anataka kunioa.tatizo lake ana uume mkubwa kila tukifanya tendo naumia sana.

Nimejaribu kwa jamaa mwingine naona siumii naenjoy sana. Huyu anaenifurahisha kitandani sijui kama ni muoaji au ananichezea tu ila huyu mwenye uume mkubwa hata nyumbani ameshaenda na wanampenda sana wazazi.

Nimechanganyikiwa sijui nifanyeje japo ana hela na maisha mazuri ila tatizo tu ni maumivu nayopata Naombeni ushauri maana kuolewa nataka ila maumivu sitaki

By Joyce

Rais Magufuli Atuma Salamu za Pongezi Kwa Kenyatta

$
0
0
Rais Magufuli Atuma Salamu za Pongezi Kwa Kenyatta



 Rais John Magufuli amemtumia salamu za pongezi Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa mhula wa pili.

Rais Magufuli ametuma pongezi hizo leo Jumamosi kupitia ukurasa wake wa twitter ‘Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema’ ameandika Rais Magufuli

Matokeo ya urais yalitangazwa jana saa nne usiku ambapo Rais Kenyatta alipata kura 8, 203,290 sawa na asilimia  54.27 huku Raila Odinga aliyegombea kwa mwamvuli wa muungano wa Nasa akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 6, 762,224 sawa na asilimia 44.74.

Hata hivyo, marais wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) walituma salamu zao za pongezi muda mfupi baada ya matokeo hayo kutangazwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati.

Wakauu hao wa EAC waliotuma salamu zao za pongezi kupitia kurasa zao za twitter ni pamoja na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye amechaguliwa hivi karibuni kuongoza nchi hiyo kwa mhula wa tatu.


Ofisi ya Waziri Mkuu Yaanzisha Programu Maalum kwa Vijana ili Kukuza Ujuzi Wao

$
0
0
Ofisi ya Waziri Mkuu Yaanzisha Programu Maalum kwa Vijana ili Kukuza Ujuzi Wao
Ofisi ya Waziri Mkuu imeanza programu maalum ya kukuza ujuzi kwa vijana katika kukabiliana na tatizo la ajira nchini.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ys Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi Vijana na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema mara baada ya kupokea maandamano ya vijana kutoka mikoa mbalimbali  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya vijana duniani.

Amesema vijana watakaohusika katika programu hiyo ni pamoja na wale wako katika maeneo ya kazi na wale waliomaliza elimu ya vyuo vikuu na kwamba vijana 13,400 walioko katika maeneo ya kazi watanufaika .

Amesema mafunzo hayo yatafanyika katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, kilimo, mifugo na viwanda vidogo vidogo nchini.

Kwa mujibu wa Jenista sensa ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi ni milioni 25 kati ya milioni 44 na kwamba asilimia 56 wana umri kati ya 15 na 35 lakini asilimia 11.7 wameathirika na ukosefu wa ajira.

Maadhimisho hayo yanazishirikisha taasisi mbalimbali za umoja wa mataifa.




Kenyatta Ahutubia na Kuwashukuru wa Kenya Kwa kuwa na Imani Naye

$
0
0
Kenyatta Ahutubia na Kuwashukuru wa Kenya Kwa kuwa na Imani Naye
Rais Uhuru Kenyatta, akihutubia baada ya kutangazwa mshindi wa urais  wa Kenya, amewashukuru wananchi kwa kuwa na imani naye na serikali yake.


“Nawaahidi tutaendelea na kazi tuliyoianza. Nawashukuru sana Wakenya. Kadhalika, naishukuru tume ya uchaguzi kwa kazi nzuri waliyoifanya,” amesema.

“Nawapongeza wote walioshinda, na kwa walioshindwa pia tutaishi kupambana siku nyingine.”
Kwa upinzani amesema: “Sisi si maadui, ni raia wa nchi moja. Kila shindano, kutakuwa na washindi na wanaoshindwa, lakini tutasalia kuwa Wakenya. Nawapa moyo wa ushirikiano, twafaa kuungana pamoja. Wakenya wanataka sisi tufaulu.

“Sana kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote waliochaguliwa kupitia upinzani, tutafanya kazi pamoja, tutashirikiana, tutakua pamoja na kuendeleza nchi pamoja.

“Kwa Wakenya wenzangu, uchaguzi huja na kuondoka lakini Kenya itaendelea kuwepo, tukumbuke daima kwamba sisi ni ndugu na dada. Jirani yako bado ni jirani yako. Tuendelee kudumisha amani. Hakuna haja ya fujo, sisi wanasiasa pia huja na kuondoka. Lakini jirani yako atabaki.”


Viewing all 104764 articles
Browse latest View live




Latest Images