Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104657 articles
Browse latest View live

Ally Mayay Afunguka Haya Baada ya Kushindwa Urais wa TFF

$
0
0
     nnnnBaada ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa shirikisho la soka Tanzania TFF Revocatus Kuuli kutangaza matokeo na wengi kusikika wakipongeza kutokana na kuamini mchakato huo uliendeshwa kwa uhuru na haki.

 Ally Mayay Tembele ambaye alikuwa ni miongoni mwa wagombea sita wa nafasi za Urais, vipi kwa upande wake ameridhishwa na matokeo.

“Uchaguzi nimeridhishwa na matokeo kwa sababu katika demokrasia ni kitu ambacho kinatokea hamuwezi kufanana mitazamo, wewe unaweza ukaona hivi mwingine akaona vile sasa unapokuja kugombea ni lazima uwe umejiandaa kupokea chochote” Ally Mayay
VIDEO:

Hivi ndivyo Mwanamke Anatakiwa Kufanya kwa Mume ili Asitoke Nje Ya Ndoa

$
0
0

Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati.

Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.

Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani.

Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee kwake.

Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.

Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.

Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.

Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji.

Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.

Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.

Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?

Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.

Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia waume zao.

Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazooonekana kuwashika waume za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.

Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye kama yale wanayofanya nyumba ndogo? Kuna dada mmoja nilizungumza naye hivi karibuni akaniambia eti amenuniana na mumewe huu ni mwezi wa pili baada ya mwanaume wake huyo kutaka afanyiwe mambo ambayo yeye aliona kinyaa kuyafanya.

Kabla ya kumjibu kwanza niliguna, sababu ya kuguna ni kwamba niliyagundua hayo mambo ambayo aliona kinyaa kumfanyia mumewe. Niseme tu kwamba, mapenzi wakati mwingine ni uchafu, wanaojua mapenzi wanajua kwa nini nasema hivyo.

Nilichomjibu mwanamke huyo ni kwamba, kama mwanaume huyo anampenda amfanyie kila atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi  kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa, mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo wengine wamekuwa wakiyafanya na wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.

Naomba niseme tu kwamba, huenda unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.

Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatilizia.

JE Kunyonyana Ulimi au Kula Denda Kunaweza Kunasababisha Kuambukiza Ukimwi?

$
0
0
Swali:
Je kunyonyana ulimi au kula mate kunaweza kuambukiza VVU?

Jibu:
Njia ya mdomo inaweza kuchangia mtu kupata VVU kama mtu atakutana na mtu mwenye VVU mwenye vidonda au michubuko mdomoni nawe pia ukawa una michubuko au vidondamdomoni, ni jambo gumu kidogo lakini kuwa makini.....

Una App ya Udaku Special Kwenye Simu yako? Kama Huna Bonyeza Hapa Kuinstall Fasta na Bure

$
0
0
Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Kutana Mtaalam wa Tiba Asili Mwenye Uwezo Mkubwa wa Kutatua Matatizo Kwa Nyota na Dua

$
0
0
KUTANA NA TABIBU MWENYE KUBRI KUTOKA KWA ALAH MAALIM ISSA NAJIMU. NI SHARIFU
MWENYE UWEZO WA KUBAINI TATIZO LAKO PUNDE TU UNAPO MFANYIA MAWASILIANO KUPITIA
WASAA NA SIKU KWA MAWASILIANO:-
MAALIM ISSA NAJIMU KUTOKA MKOA WA TANGA MWAMBONI MAGOFU KATA YA NGUVU MALI
NCHINI TANZANIA, NI TABIBU MWENYE KUBRI TOKA KWA ALAH ANATIBU KWA NJIA YA VITABU VYA
QUR-AN, DAWA ZA ASILI PAMOJA NA DAWA ZA KIARABU.
ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE / MKOA WOWOTE KWA MATATIZO YAFUATAYO:-

 ULIJALI (NGUVU ZA KIUME)
 MIGUU KUWAKA MOTO
 KUTAFSIRI NDOTO
 MFARAKANO WA WANANDOA
 MFARAKANO KAZINI
 KUPANDSHWA CHEO
 KUTOA PETE YA BAHATI
 ANAO UWEZO WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUBASHIRI
 KUFUNGUA UZAZI KWA WALIYO FUNGWA KWA NJIA YA USHIRIKINA
 KUTOA VIFUNGO VYOTE VILIVYO FUNGWA IKIWA NI KWENYE MWILI WA BINADAMU /MAJUMBANI NA KWENYE BIASHARA.
 ANA UWEZO MKUBWA WA KUPANDIKIZA NYOTA YA KUMPATA YEYOTE UMPENDAYE KWA
KUMUOA AU KUWA NAYE.
 ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIYE MBALI PIA ALIYE CHUKULIWA KWA NJIA YA MSUKULE
 ANAO UWEZO WA KUUAq KESI SUGU NA PYA NDANI SIKU 7 TU.

 MENGINEYO MENGI ZAIDI YALIYO KUWA SUGU PIGA-

 Mobile; 0717 70 32 41.
 WhatsApp 06226 535419.

VIDEO:Shuhudia Jinsi RC Paul Makonda Alivyokosa Penati.....

$
0
0
IKIWA ni sehemu ya shamlashamla za Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika hapa katika Uwanja wa Taifa wa Uhuru Dar kumekuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii pamoja mchezo wa mpira wa miguu ambapo wamechuana mabalozi wa usalama barabarani na wabunge.


 Katika mchezo huo uliomalizika dakika 90 bila kufungana hivyo refa kaliamua kuepeleka mpira kwenye matuta ili apatikane mshindi.

Katika mikwaju hiyo ya penati ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda aliyeyekuwa akichezea timu ya Wabunge, alikosa penati ya kwanza.

 VIDEO:

Maajabu....Ng’ombe wa Rangi ya Blue Aliyeonekana Mto Ruvu.....

$
0
0
Dunia ina maajabu mengi ambayo hayaishi ambapo kama hujayaona basi utasimuliwa lakini katika maajabu ambayo nisingependa yakupite ni pamoja na haya yaliyotokea Mto Ruvu ambako alionekana Ng’ombe wa rangi ya blue akinywa maji.

Mtazame kwenye hii video:

Fedha za Ushahidi wa Kesi ya Takururu Zaibiwa Zikiwa Mahakamani

$
0
0

Fedha taslimu Sh200,000 zilizokuwa kielelezo katika kesi ya kuomba na kupokea rushwa inayomkabili ofisa wa polisi wa mkoani Njombe, zimeibwa wakati kesi ikiendelea.

Mbali na fedha hizo, pia hati ya utaifishaji mali (seizure note), ambayo hujazwa wakati wa ukamataji na kusainiwa na mshtakiwa na mashahidi ambayo ni kielelezo, nayo imetoweka.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa vielelezo hivyo muhimu vya upande wa mashtaka ambao ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), vilitoweka Jumatano iliyopita.

Tayari mshtakiwa katika kesi hiyo pamoja na karani mmoja wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi wamehojiwa na polisi mkoani Kilimanjaro, kutokana na kuibwa kwa vielelezo hivyo muhimu.

Imeelezwa kuwa siku hiyo baada ya shahidi wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wake mahakamani, aliomba kupatiwa kielelezo hicho ili akitumie kumuuliza maswali shahidi wa TAKUKURU.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa baada ya kumaliza kukitumia kielelezo hicho, hakukirudisha kwa karani na siku iliyofuata wakati kesi ikiendelea na kielelezo kutakiwa tena, ndipo ilipobainika hakipo.

“Karani alipoulizwa kielelezo akasema hakurudishiwa ile jana yake na ndipo kukawa na kutupiana mpira kati ya karani, mwendesha mashtaka na mshtakiwa,” alidokeza mmoja wa watoa habari wetu.

Chanzo hicho kilidai kuwa, kwa kawaida kielelezo kikishakabidhiwa na kupokewa mahakamani, kinakuwa ni mali ya Mahakama na kinapotumika kwenye ushahidi hurudishwa kwa karani.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, wakati vielelezo hivyo vinatoweka, mashahidi wengine muhimu ambao walishiriki katika ukamataji na wanaotakiwa kuvitumia katika kesi hiyo, walikuwa hawajatoa ushahidi.

Naibu Msajili ya Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Bernard Mpepo alipoulizwa juzi jioni baada ya taarifa hizo kusambaa, alisema hajui lolote kuhusu suala hilo kwa kuwa alikuwa kwenye kikao cha Mahakama ya Rufani jijini Arusha.

Lakini jana, Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutoweka kwa vielelezo hivyo na kusema tayari Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi juu wa tukio hilo lisilo la kawaida.

“Inavyoonekana kulifanyika kosa pale mahakamani siku ya kesi. Mshtakiwa aliondoka na vielelezo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ndiyo maana tulimhoji,” alisema.

Polisi huyo alikamatwa Mei mwaka huu na TAKUKURU akidaiwa kupokea 200,000 kutoka kwa mfanyabiashara mmoja aliyekuwa akituhumiwa kukamatwa akiwa na lori linalodaiwa kutumika kusafirisha mahindi ya wizi.

Hata hivyo, alipofika mkoani Kilimanjaro na kumkamata mmiliki wa lori hilo, ilibainika kuwa gari hilo halikuwa la kubeba mizigo, bali la mafuta na halijawahi kutembea tangu linunuliwe.

Pamoja na kubaini tofauti hizo, bado inadaiwa polisi huyo alimweka mahabusu huku akindelea kumtuhumu mmiliki kuhusika na kosa hilo la jinai akisisitiza lazima asafirishwe kwenda Njombe.

Ni katika mazingira hayo, ofisa huyo anadaiwa kuomba kiasi hicho cha fedha ili suala hilo limalizike pasipo mfanyabiashara huyo kuchukuliwa hatua, na ndipo taarifa zilipotolewa TAKUKURU.

Chanzo: Mwananchi

Aliyekuwa Mke wa Barnaba Afunguka nini Alikuwa Anakosa Kwa Barnaba Mpaka Kukimbia Ndoa.....

$
0
0
Aliyekuwa mke na mama mtoto wa mwanamuziki Barnaba Elias, Zuu Namela, ametoa kile kinachoitwa la moyoni, na huenda ndio sababu iliyomtoa kwa mzazi mwenzake na kuanzisha mahusiano mapya.
 
Kwenye ukurasa wake wa instagram Zuu Namela ameandika ujumbe kuwa kwa miaka mitano (ambayo ilikuwa ndani ya mahusiano na Barnaba) alikuwa anakosa furaha ya kweli na amani ya moyo, lakini sasa ameipata furaha hiyo baada ya kuachana.

"Ni watu wachache sana wanaojua nikitu gani nilikua nakosa katika maisha yangu! Unaweza ukapata kila kitu kwenye maisha ila ukakosa furaha,amani,heshima......kwa zaidi ya miaka mitano ichi ndo nilicho kuwa nakitafuta #AMANIyaMOYO " aliandika Zuu Namela.

Hivi karibuni Zuu Namela ameonekana akimpost mwanaume mwengine kwenye ukurasa wake, huku akiandika jumbe mbali mbali za mapenzi, na kuacha mashabiki wake kuwa ndiye mbadala wa Barnaba ambaye ni baba mtoto wake.

Haji Manara Afunguka.."Enzi za Kubebana zimeisha TFF,na Simba Hatutaki Mbeleko Tunataka Haki"

$
0
0
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amempongeza Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia huku akipiga dongo kwa kudai enzi za kubebana zimeisha na sasa ni wakati wa kupeleka soka mbele.


Manara amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Istragram masaa machache kupita tokea Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi mkuu wa (TFF), Revocatus Kuuli kumtangaza Wallace Karia kushinda nafasi hiyo kwa kura 95 kati ya 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo, ambapo ataongoza kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa Katiba ya shirikisho hilo.

"Enzi za kubebana zimeisha TFF,na Simba hatutaki mbeleko tunataka haki, narudia haki. Hongera Wallace karia na Michael Wambura pelekeni soka mbele", ameandika Manara.

Shamba Lingine la Sumaye Lafutwa na Rais Magufuli

$
0
0

Shamba Lingine la Sumaye Lafutwa na Rais Magufuli
Waziri Mkuu wa mstaafu, Frederick Sumaye ameingia matatani tena baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kumpokonya shamba lake lenye ukubwa wa ekari 326 kwa madai ya kutoendelezwa huku ikisema Rais John Magufuli ameridhia hatua hiyo.

Hili ni shamba la pili Sumaye kunyang’anywa baada ya ekari 33 zilizopo eneo la Mabwepande kuchukuliwa Novemba mwaka jana huku Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akisema Serikali ilifikia uamuzi huo baada ya kiongozi huyo mstaafu kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90 ilivyoeleza.

“Oktoba 28, mwaka huu, Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba namba 3,074 lililopo Mabwepande. Shamba hilo lilikuwa na hati namba 53086. Jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye,” alisema Hapi.

Jana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero, Frolent Kyombo alisema Rais Magufuli amekubali kufutwa kwa umiliki wa shamba hilo kupitia ilani ya ubatilisho ya Mei mwaka huu.

Kabla ya kupokonywa shamba hilo, Kyombo alisema Sumaye alipewa notisi ya siku 30 iliyomtaka kueleza sababu za kutoendeleza matumizi ya shamba hilo kwa shughuli za kilimo kama lilivyosajiliwa lakini hakutoa sababu zilizoweza kushawishi kutofanyika kwa mabadiliko hayo.

“Hatua ya pili, tukatoa ilani ya ubatilisho wa shamba hilo, kuna maelezo alitoa lakini tuliona hayakuwa na uzito, tukayatupilia mbali, shamba hilo alikuwa anaendesha shughuli za kilimo pamoja na ufugaji. Alikuwa anatumia asilimia 15 hadi 20 tu ya shamba lote,” alisema Kyombo.

Alisema mbali na kutumia sehemu ndogo huku nyingine ikiwa haitumiki, Mwenyekiti huyo wa Chadema Kanda ya Pwani alikuwa amekiuka Sheria ya Mipango Miji, namba 8 ya mwaka 2007 pamoja na Sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999.

“(Sumaye) alitakiwa kutumia shamba hilo kwa ajili ya kilimo tu na siyo kwa shughuli nyingine za ufugaji, hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria hizo. Kwa hiyo mchakato umeashaanza wa kuligawa shamba hilo kwa wananchi na tunategemea miezi minne ijayo tutakuwa tumemaliza taratibu zote,” alisema.

Desemba 15, 2015, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alitangaza kiama kwa watu wanaomiliki mashamba bila kuyaendeleza huku wakiyatumia kama dhamana ya kukopea fedha benki.

Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli, alisema kuna watu wamehodhi mashamba makubwa lakini hawayaendelezi, hawayalipii kodi na mbaya zaidi, wanayatumia kukopa fedha benki.

Kabla ya DED huyo kulithibitishia Mwananchi habari hizo, mapema asubuhi ya jana, taarifa iliyoelezwa kuwa imeandikwa na Sumaye, ilisambaa kwenye mitandao ya jamii ikieleza hatua kwamba Rais Magufuli amechukua shamba jingine la kiongozi huyo.

“Mtakumbuka baada tu ya kuingia Serikali hiyo madarakani, ilitishia muda mrefu kuchukua mashamba yangu bila sababu za msingi, hata wakati wa kampeni baadhi ya viongozi wa CCM walitamka hadharani kuwa huyu dawa yake ni kumnyang’anya mashamba yake,” taarifa hiyo inamnukuu Sumaye.

Hata hivyo, akizungumza hatua za upokonyaji wa mashamba yasiyoendelezwa katika Halmashauri ya Mvomero, Kyombo alisema katika awamu ya kwanza mwaka 2014, iliorodhesha mashamba makubwa 63 na saba kati ya hayo, Rais Magufuli aliyafuta.

“Awamu ya pili nikiwa tayari DED wa Mvomero, tuliwasilisha mapendekezo ya ubatilisho kwa mashamba matatu na yote Rais Magufuli aliyafuta, yalikuwa na ukubwa tofauti. Kwa sasa tumepeleka mapendekezo ya ubatilisho wa mashamba mengine manne kwa Rais, lakini bado hayajajibiwa,” alisema Kyombo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendelezo ya Makazi, utaratibu wa ilani ya ubatilishaji umeanza kufanyika baada ya Serikali kuagiza halmashauri zote nchini kukagua mashamba na kuwasilisha taarifa zake wizarani kwa hatua stahiki ili kama kutakuwa na ambayo hayajaendelezwa, wakurugenzi husika watume ilani hizo kwa wamiliki.

Baada ya siku 90 kumalizika, halmashauri hizo zitatakiwa kuwasilisha mapendekezo ya ubatilisho wizarani.

Akizungumzia ubatilishwaji huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Jonas Zeeland alisema walipewa taarifa hiyo katika baraza la madiwani lililokutana Ijumaa Agosti 11.

“Ni kweli umiliki wa shamba hili umebatilishwa kutoka kwa Sumaye na taarifa tulipewa jana (juzi) kwenye kikao cha baraza,” alisema Zeeland.

Mwenyekiti huyo alimpongeza Rais kwa kuridhia kubatilisha umiliki wa shamba hilo akisema kwa muda mrefu walikuwa wakiomba warejeshewe.

Alisema bado kuna mashamba mengi katika halmashauri hiyo ambayo hayajaendelezwa hivyo amemuaomba Rais kuharakisha ubatilishaji wake ili waweze kuyapangia matumizi mengine.

Hata hivyo, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Mashariki, Juliana Pilla alisema mashamba waliyoombea kubatilishwa ni zaidi ya ekari 30,000.

“Kuna wamiliki wamesharejea na kuanza kuendeleza mashamba yao baada ya kutoa notisi, kama Mvomero waliombea mashamba 26 lakini hadi sasa wamiliki 17 wamesharudi na wanaendeleza mashamba yao,” alisema kamishna huyo.

Alisema ameziagiza Halmashauri zote kufanya uhakiki kwa mara ya mwisho ili mashamba hayo yabatilishwe huku akizitaja wilaya za Mvomero, Morogoro na Kilosa kuwa ndizo zenye mashamba mengi yasiyoendelezwa.

Alipotafutwa jana kuzungumzia suala hilo, Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 mfululizo kuanzia Novemba 27, 1995 mpaka Desemba 28, 2005, alisema hawezi kuzungumza suala hilo mpaka atakapowasiliana na mawakili wake.

       

Viroba vya Muhibua Dudu Baya Afunguka Anavyoumia Baada ya Serikali Kupiga Marufuku Matumizi Ya Viroba

$
0
0


Viroba vya Muhibua Dudu Baya Afunguka Anavyoumia Baada ya Serikali Kupiga Marufuku Matumizi Ya Viroba
Msanii Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya, amesema kitendo cha serikali kufungia pombe aina ya viroba kumemuathiri kwa kiasi kikubwa, kwani na yeye alikuwa mtumiaji wa kilevi hiko.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dudu Baya amesema alikuwa anakunywa viroba kama pombe ya kawaida kwani ina ubora ule ule na ya kwenye chupa.

"Unajua mi sivuti sigara, situmii unga, kilevi ninachotumia ni bapa, hata nikiwa na mke wangu nampa hela akanunue bia mi nanunua bapa yangu napiga, lakini mara nyingi nikiwa mtaani naagiza viroba vyangu nakunywa, unajua hii ni sehemu na ile ambayo ipo kwenye chupa, haina tofauti, kwa nini nione kinyaa kutumia viroba, mi sina ubishoo, kwa hiyo kidogo kufungiwa kwa viroba kumenimuiza", alisema Dudu Baya.

Mnamo mwezi Februari mwaka huu serikali ilipiga marufuku uzalishaji na utumiaji wa pombe aina za viroba, ambayo inaelezwa kuathiri vijana wengi na kuzorotesha uzalishaji mali kwa uchumi.

Rama Dee Awapa Makavu Wasanii

$
0
0

Rama Dee Awapa Makavu Wasanii
Mkali wa R&B nchini Tanzania, Rama Dee amewataka wasanii kuacha tabia ya kujikweza na kuishi maisha ambayo siyo ya kwao kwa kuwa kufanya hivyo ipo siku itawagharimu katika utendaji kazi wao.


Rama Dee amebainisha hayo  baada ya kuwepo desturi ya baadhi ya watu wakiingia katika 'industry' ya muziki kukana maisha yake amabyo anayoishi kila siku na kujifanya yupo vizuri kila leo.

"Siyo lazima kujikweza maana ukijikweza ina kugharimu kwa sababu unaishi sehemu ambayo huwezi kukanyaga chini yani kwa hiyo ishi vile unavyoweza kuishi hata kama una chumba kimoja. Watu wanapaswa wawe wazi, usiogope shabiki yako kukuona wewe upo katika hali gani", alisema Rama Dee.

Kwa upande mwingine, Rama Dee amesema anajisikia furaha kwa sasa kuona watu wanajua kutofautisha muziki mzuri pamoja kiki.



Waziri Nchemba Ashangazwa na Hali ya Kituo cha Polisi cha Mkalama mkoani singida

$
0
0

Waziri Nchemba Ashangazwa na Hali ya Kituo cha Polisi cha Mkalama mkoani singida
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ametembelea kituo cha polisi cha wilaya ya mkalama mkoani singida kuangalia hali ya kituo na utendaji kazi wa askari polisi na mazingira wanayofanyia kazi askari hao.

Waziri Mwigulu amejionea hali ambayo si nzuri ya kituo cha polisi cha wilaya ya mkalama ambayo ni wilaya mpya iliyomegwa kutoka wilaya ya Iramba.

Waziri huyo alisema kwamba kituo hiki cha wilaya ya mkalama hali si nzuri kwani ni chakavu sana na kidogo ambacho kina mahabusu moja ya wanaume tu huku wanawake wakiwekwa mapokezi.

Waziri Mwigulu amesema atakaa na wenzake wa wizarani akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro kupanga utaratibu wa kumalizia ujenzi wa vituo vyote polisi ambavyo ujenzi wake umekwama hasa wa hizi wilaya ya mpya ambazo zimemegwa katika wilaya mama.

 Amewahidi kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya mkalama kuwa ujenzi wa kituo hicho utaisha na anakwenda kuonana na IGP kupanga kumalizia ujenzi wa vituo hivyo mapema.

Naye Kamanda wa Polisi wilaya ya Mkalama (OCD) John Ntilima amesema kwasasa wanatumia kituo kidogo cha polisi Nduguti kama kituo cha polisi cha wilaya ambacho ni kidogo sana hakitoshelezi kwa ufanyaji kazi wake kwani wanatumia ofisi tatu ambazo ni mbovu na chakavu  hivyo wana ujenzi wa kituo kikubwa cha kisasa lakini wamekwama kumalizia na kumuomba waziri awasaidia katika kukamilisha hilo.



Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo Jumapili


BREAKING NEWS:Mzee Kilomoni Asimamishwa Uanachama Simba

$
0
0



BREAKING NEWS:Mzee Kilomoni Asimamishwa Uanachama Simba
Klabu ya Simba imetangaza kumtoa mzee Hamisi Kilomani kwenye Baraza la Wadhamini kwa kosa la kuvunja katiba ya klabu hiyo.

Pia, wanatarajia kumpekelea barua ya kumfuta uanachama na ikiwa hatafuta kesi na kushindwa kujitetea watamfukuza uanachama moja kwa moja.

Aidha, profesa Juma Kapuya ameteuliwa kuziba pengo la Ally Sykes ambaye kwa sasa ni marehemu katika baraza hilo, nafasi ya mzee Kilomoni imejazwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Alhaj Adam Mgoyi.

Kofi Annan Amshauri Odinga Kufuata Njia Sahihi za Kisheria

$
0
0

Kofi Annan Amshauri Odinga Kufuata Njia Sahihi za Kisheria
Kofi Annan alikuwa mpatanishi mkuu mzozo wa baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka kumi iliyopita, ametoa wito kwa walioshindwa kutumia mifumo ya kisheria kutafuta haki.

Bw Annan alikuwa mpatanishi mkuu baada ya ghasia kuzuka baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 uliokumbwa na utata.

Bw Mwai Kibaki alitangazwa mshindi wakati huo lakini Bw Raila Odinga na chama chake cha ODM wakapinga matokeo hayo.
Katibu mkuu huyo wa zama ni wa UN amempongeza Bw Kenyatta kwa ushindi wake na pia akamsifu Bw Odinga kwa kuendesha kampeni yake kwa njia ya amani.

"Namshukuru kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kampeni ya uchaguzi ya amani aliyoiendesha. Amekuwa mtetezi jasiri wa demokrasia," amesema Dkt Annan kupitia taarifa.
"Kwa hivyo, namhimiza sasa afuatilie malalamiko yake kupitia mifumo ya kisheria iliyowekwa na aweke maslahi ya taifa mbele, kama alivyofanya kwa uzalendo mara nyingi awali."
Upinzani umekuwa ukidai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na matokeo kuchakachuliwa kumfaa Rais Kenyatta.

Bw Annan pia ametoa wito kwa Rais Kenyatta, ambaye alitangazwa mshindi wa urais Ijumaa afanye juhudi kuunganisha tena taifa.

Alhamisi, muungano wa upinzani National Super Alliance (NASA) ulidai Bw Odinga ndiye aliyeshinda uchaguzi huo na kuitaka tume hiyo kumtangaza kuwa mshindi.
Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290 ambayo ni asilimia 54.27 naye mpinzani wake mkuu, mgombea wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga akapata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.74.

Maajenti wakuu wa NASA waliondoka ghafla kikao cha tume hiyo cha kuafikiana kuhusu matokeo hayo kabla ya kutangazwa kwa Bw Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi huo Ijumaa usiku.

Naibu ajenti mkuu wa muungano huo James Orengo, amesema muungano huo hautaenda kortini. Amesema hawana imani na idara ya mahakama kwamba itashughulikia malalamiko yao kwa njia ya haki bila mapendeleo.


Kiongozi huyo amesikitishwa na mauaji ambayo yametokea kwenye makabiliano kati ya waandamanaji waliokuwa wanapinga matokeo na polisi.

"Amani, uthabiti na ustawi vinategemea viongozi wa kisiasa Kenya. Wanafaa kuwa makini sana katika mambo wanayosema na vitendo vyao katika hali hii ya sasa. Nawaomba wawajibike."
Naibu rais na mwakilishi mkuu wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini pia ameutaka upinzani kutumia njia za kisheria kufuatilia malalamiko yao kuhusu uchaguzi.

"Sawa na ulivyofanya Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya unatarajia upinzani uheshimu matokeo na ktuumia njia za kisheria zilizopo kukata rufaa na kuwasilisha malalamiko," amesema kupitia taarifa.
Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani katika mitaa ya Mathare na Kibera jijini Nairobi, katika katika maeneo ya Homa Bay, Migori na Kisumu ambayo ni ngome ya Bw Odinga magharibi mwa Kenya.

Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Apata mkataba mpya wa Miaka Mitatu Katika Timu Hiyo

$
0
0

Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Apata mkataba mpya wa Miaka Mitatu Katika Timu Hiyo
Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ameafikiana na mabingwa hao wa Ulaya na Uhispania kuhusu mkataba mpya wa miaka mitatu.

Kiungo huyo wa kati wa zamani wa Real, katika katika miezi 18 ambayo amekuwa kwenye usukani, ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili na taji la La Liga mara mbili.

Akiongea mkesha wa mechi ya kwanza ya mkondo wa kwanza ya Super Cup ya Uhispania itakayochezewa Barcelona, alisema: "Hadithi yangu na Real Madrid ni zaidi ya mikataba na saini.
"Nina furaha kubwa kuhusishwa na klabu hii. Lakini mkatana hauna maana yoyote."

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye miaka 45 alikuwa mkufunzi wa Timu B ya Real kabla ya kuchukua nafasi ya Rafael Benitez Januari 2016.

Aliongeza: "Unaweza kutia saini mkataba wa miaka 10, 20. Najua niko wapi na nataka kufanya nini.
"Katika mwaka mmoja, pengine sitakuwa hapa. Mimi na Real Madrid hatutajibizana, daima.."

Real watacheza dhidi ya Barca Jumapili mechi itakayoanza saa 21:00 BST (saa tano usiku Afrika Mashariki). Mechi ya marudiano itachezewa Bernabeu Jumatano saa 22:00 BST (Saa sita Afrika Mashariki).

Maskini Barnaba Kayaandika Haya Hapa Baada ya Aliyekuwa Mke wake Kumtoa Kasoro zilizofanya Amkimbie .

$
0
0
Maskini Barnaba Kayaandika Haya Hapa Baada ya Aliyekuwa Mke wake Kumtoa Kasoro zilizofanya amkimbie

By Barnaba
"Mama aliniambia Ukimtukana mwanamke Basi umenitukana na Mimi |- siku zote. nawaona kama mama zangu Hongera wanawake Wote duniani Salamu zangu Juu Yenu jumapili Ya Leo nawapenda Sana Na wale mliopoteza mama zenu Fanyeni Ibada Juu Yao waweze Punguziwa Adhabu Ya Kifo au kufutiwa kabisa Bwana Yesu Asifie Sana Jumapili Ya mungu Tumpe mungu Wacristo Wenzangu"

Mpe neno lolote Barnaba kumtia moyo

Q chief Awachana Wasanii Wanaotoa Ngoma Nyingi kwa Wakati Mmoja

$
0
0




Q chief Awachana Wasanii Wanaotoa Ngoma Nyingi kwa Wakati Mmoja
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Q chief amewatolea uvivu wasanii wanaotoa nyimbo nyingi kwa muda mfupi kwa kusema hawajiamini ndio maana wanaachia nyimbo nyingi kwa muda mfupi.



Q Chief amesema kama msanii anafanya muziki unaodumu kama yeye haina haja ya kutoa nyimbo nyingi mfululizo kwa muda mfupi huku akidai wasanii wanaofanya muziki wa Big G au ‘Bubble Gum’ ndio wanaohangaika kutoa nyimbo kila siku.

“Naamini kabisa mimi ni mgodi unaotembea, naogopa ninapoona ngoma inaHit siku mbili na kupotea, nia yangu ni kufanya muziki ambao utaishi hata nikiondoka… mimi nadhani wanaotoa ngoma nyingi kwa muda mfupi bila mpangilio ni waoga, hawajiamini ndiyo maana wanahangaika na ngoma kila kukicha kama unafanya muziki unaodumu haina haja”,amesema QChief kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha EFM.

Hata hivyo Q Chief amesema muziki wetu unapoteza ladha yake asili kila kukicha kutokana na wasanii kujikita kuiga aina nyingine ya miziki kutoka nje.

“Nafurahi kuona wadogo zangu wanapeleka Bongo fleva Mbele lakini nikiingalia Bongo Fleva naona kabisa tunahama kwenye misingi yetu na hii inatokana na baadhi yao wanaopata nafasi ya kwenda mbele sio wasanii ndio maana wanapokutana na wasanii wenye uwezo wanaruhusu Identity ya Bongo Fleva ipotee na kuanza kuwaiga”,amesema Q Chief
Viewing all 104657 articles
Browse latest View live




Latest Images