Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Lulu Diva: Vanessa Mdee, Nandy na Maua Sama Wanafanya Vizuri Lakini Siwahofii

$
0
0






Lulu Diva: Vanessa Mdee, Nandy na Maua Sama Wanafanya Vizuri Lakini Siwahofii
Baada ya kufanya TOUR ya kimuziki katika miji ya Mombasa na Nairobi, Kenya Mwimbaji staa Lulu Diva kutoka Bongoflevani amelezea mapokezi makubwa ambayo hakuyategemea.

Mbali na kuelezea tour yake hiyo Lulu Diva amezungumzia pia uwezo wa baadhi ya waimbaji wa kike wa Bongofleva akiwataja Vanessa Mdee, Nandy na Maua Sama akisema wanafanya vizuri na wana uwezo lakini hawahofii.

”Kati ya Nandy na Vanessa hakuna ninayemuhofia kukaa nafasi yangu. Sijui Watanzania wenyewe ndio wanaofahamu ukweli kabisa. Nandy anafanya vizuri kwa nafasi yake na Vanessa anafanya vizuri kwa nafasi yake, hata Lulu Diva anafanya vizuri kwa nafasi yake. Maua atabaki kuwa Maua hata kama atajitokeza mtu na kujifanya kama Maua Sama.” – Lulu Diva.



Kidoa Ashindwa Kuyamudu Mambo ya Kindoa...Mambo Yake ya Chumbani Yaanikwa

$
0
0


Kidoa Ashindwa Kuyamudu Mambo ya Kindoa...Mambo Yake ya Chumbani Yaanikwa
Msanii wa filamu ambaye ndiye The Ijumaa Sexiest Girl 2015, Asha Salum ‘Kidoa’ amegandwa na madai ya kuwa bonge nyanya tofauti na alivyokuwa huko nyuma kiasi cha kuathiri uwezo wake awapo faragha.

 Mmoja wa mashosti wa staa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, mara kwa mara Kidoa amekuwa akijilaumu kwa kushindwa kuukontroo mwili wake huku akihofia kuachwa na ‘baby’ wake.

“Unajua sasa hivi Kidoa amekuwa bonge sana na anahisi hata mpenzi wake atamuacha maana yale mambo ya chumbani atakuwa hayamudu,” alimwaga siri za chumbani za kidoa  sosi huyo. Katika kujua ukweli wa ishu hiyo, paparazi wetu alimtafuta Kidoa na alipobanwa juu ya madai hayo alifunguka:

“Mh! Aliyewaambia hayo ni mmbeya sana, hata niwe bonge vipi bado siwezi kushindwa kujimudu faragha. Mimi ni msichana niliyefundwa, ni mtundu na mbunifu, hata mpenzi wangu anajua hilo. Kuhusu ubonge, nafanya jitihada za kurudisha ule mwili wangu na umbo namba nane,” alisema Kidoa.

R.O.M.A Arejea Kutoka Zimbabwe Aahidi Kufunguka Kuhusu Wimbo Wake

$
0
0




R.O.M.A  Arejea Kutoka Zimbabwe Aahidi Kufunguka Kuhusu Wimbo Wake
Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Roma Mkatoliki amewasili jana usiku akitokea nchini Zimbabwe alikoenda kikazi.



Roma Mkatoliki ambaye ameachia wimbo wake mpya wa Zimbabwe wiki iliyopita amejikuta akisakwa na vyombo vya habari kuzungumzia wimbo huo wenye mashairi yenye mafumbo lakini hakuwepo nchini na kumuachia jukumu hilo la kutambulisha wimbo huo kwenye Media, mke wake.

“Kiukweli nimechoka wanangu what i need ni kuona familia yangu, mke wangu na mtoto na ndugu, jamaa na marafiki”,amesema Roma Mkatoliki jana usiku alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. JK Nyerere, jijini Dar es salaam.

Alipoulizwa ni kwanini alimtuma mke wake aachie wimbo huo ile hali alikuwa nje ya nchi Roma Mkatoliki amesema alifanya hivyo kwa sababu muda ulifika wa kutoa ngoma hiyo na tayari alifanya booking na Media, lakini alikataa kuzungumzia wimbo huo wala kueleza alichoenda kufanya Zimbabwe huku akiahidi mashabiki wake kuwa kuanzia leo ataanza Media Tour kuuzungumzia wimbo huo wenye mashairi yenye mafumbo .

Wakazi, Stamina, Ndugu jamaa na Marafiki zake wa karibu wa Roma walikuwepo kwenye mapokezi hayo ambayo yalikuwa kimya kimya.


Mashabiki Wamshambulia Mobetto Baada ya Kuweka Picha ya Tumbo lake

$
0
0




Mashabiki Wamshambulia Mobetto Baada ya Kuweka Picha ya Tumbo lake
Hamisa Mobetto anaendelea kupost picha zinazoonyesha tumbo lake la ujauzito lilivyokuwa kabla hajajifungua wiki iliyopita.



Mlimbwende huyo wa Tanzania, amepost picha mbili katika mtandao wa Instagram akiwa amevaa “kufuli” huku tumbo lake akiwa ameliacha wazi kitendo ambacho baadhi ya mashabiki wameonekana kutokifurahia.



Missing my baby bump 😰🤰🏽.. By the way Happy one week my handsome 👑 @tanzanian_baby . @buoart shot it 🔥,” ameandika kwenye picha hiyo hapo juu ambayo ameiweka katika mtandao huo.

Hizi ni baadhi ya comment za mashabiki katika picha hizo.

am_ommy: Ni kujizalilishaa hukoo nyie wasichana

kushokahassan: Yaani mi naona ni ujinga tu sa si bora ungekaa uchi kabisa tukaona na iyo ….

sashamchomvu96: ovyoo kweli sielewi wanawake wanaofanya upuux uo

kidafu: Ovyooooo mwanamke huna Ata aibu mimba TUNU? Kujitia mikosi buree
richardisgodbles😍😍

ibrahtib: dah! picha zingine aibu tupu


Madee Afunguka Diamondi Alivyosaidia Kolabo Yake na Tekno

$
0
0

Madee Afunguka Diamondi Alivyosaidia Kolabo Yake na Tekno
Msanii Madee amebainisha kuwa Diamond Platnumz anahusika kufanikisha kolabo yake na Tekno.



Madee amesema haikuwa ngumu sana kumpata muibaji huyo kutoka Nigeria na pia si yeye aliyeangaikia kolabo hiyo na hata pale Tekno alipoangalia kazi zake hakuwa na pingamiza kuhusu kufanya hiyo ngoma.

“Nilimuelezea tu Babu Tale pamoja na Diamond, bwana naweza kufanya kazi na Tekno?, wakasema inawezekana ngoja tumuambie nakumbuka alikuwa hapa hapa Dar es Salaam, wakamwambia akasema nipeni kama lisaa limoja ili nimuangalie huyu Madee,” ameiambia Bongo5 na kuongeza.

“Nadhani katika hilo lisaa limoja ndio akawa anamuangalia Madee ni nani, amefanya nini na ana impact gani baada hapo akawajibu its ok tunaweza kufanya lakini production nafanya mimi kwa sababu yeye ana studio,” amesema.

Ameongeza kuwa, “kwa hiyo akapiga ile biti akafanya vocal akaja tena Dar es Salaam kwenye mishe zake akatupatia ile biti pamoja na vocal nikaweka vocal zangu akapewa tena alipoona ipo ok,  ndio ikanyika mixing WCB,” amesema

Kiongozi Mkuu wa Upinzani Nchini Zambia, Hakainde Hichilema Atoka Jera

$
0
0
.
Kiongozi Mkuu wa Upinzani Nchini Zambia, Hakainde Hichilema Atoka Jera
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema aliyekuwa amewekwa mahabusu akikabiliwa na shtaka la uhaini ameachiliwa huru asubuhi hii.

Hichilema ameachiwa huru baada ya Mwendesha Mashtaka kumfutia mashtaka kiongozi huyo aliyekuwa mahabusu tangu Aprili mwaka huu.

"Mwendesha Mashtaka Mkuu ameamua kusitisha mchakato wa kesi kwa mamlaka ya kikatiba aliyonayo. Kwa hiyo, anaachiwa huru kuanzia sasa,” amesema Jaji wa Mahakama Kuu, Charles Chanda.

Hichilema na wenzake walikamatwa kwa madai ya kutaka kuhatarisha maisha ya Rais Edgar Lungu baada ya kiongozi huyo na wafuasi wake kukataa kupisha msafara wa rais huyo.

Habari za kuachiwa huru zilivuja tangu mwishoni mwa wiki, ikielezwa kwamba ni kutokana na juhudi zilizofanywa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland ambaye alifanya ziara nchini Zambia kuangalia hali ya siasa. Katibu huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Lungu na pia alimtembelea Hichilema katika gereza la Mukobeko.








Umoja wa Mataifa Umekataa Ombi la Odinga Kukagua Matokeo ya Uchaguzi Kenya

$
0
0
Umoja wa Mataifa Umekataa Ombi la Odinga Kukagua Matokeo ya Uchaguzi Kenya
Umoja wa Mataifa umekataa ombi la kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kukagua matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti.
Msemaji wa umoja huo alikataa ombi hilo akisisitiza taarifa ya katibu mkuu wa Umoja huo Antonio Gutierrez ambapo amewataka viongozi wa Kenya kusuluhisho mgogoro wowote wa uchaguzi huo katika taasisi zinazofaa kikatiba.

Umoja huo umesema kuwa utatazama mpango mpya wa Raila Odinga ambao anapanga kutangaza siku ya Jumatano.
Wiki iliopita kiongozi huyo wa Nasa alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kukagua matokeo hayo ya uchaguzi uliokamilika.

Akizungumza na gazeti la Financial Times bwana Odinga alisema kuwa ana ushahidi wa kuthibitisha kwamba uchaguzi huo wa urais ulifanyiwa udanganyifu.
''Tutaonyesha ulimwengo ule mchezo uliochezwa, Kile tunachotaka ni Umoja wa Mataifa kubuni jopo la wataalam ambalo litatusaidia kutathmini matokeo hayo''.
Kiongozi huyo wa upinzani alisema kuwa tume ya uchaguzi nchini IEBC ilikuwa chini ya shinikizo kali kutoka kwa maafisa wa serikali inayoongozwa na rais Kenyatta.

''Kufuatia mauji ya mtaalam wa maswala ya kiteknolojia katika tume hiyo Chris Msando, wafanyikazi wengine waliogopa''.
''Kile kilichotokea kimeshinikizwa na serikali. Sio kuhusu mimi, Sio Kuhusu Raila Odinga sitokuwa mgombea tena. Tunataka Wakenya kujua kilichofanyika, kile ambacho dunia nzima haielewi kinafanyika''.
''Hakuna haja ya watu kwenda kupanga milolongo mirefu ya kupiga kura kwa saa kadhaa ama kufanya kampeni na huku kompyuta moja katika tume ya IEBC inatumiwa kuchakachua matokeo hayo''.

Zijue Dalili, Athari na Tiba ya Upungufu wa Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo na Kuongeza Uume...

$
0
0
ZIJUE DALILI, ATHARI NA TIBA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO NA KUONGEZA UUME. Tatizo la kukosa au upungufu wa nguvu za kiume limekuwa kubwa sana duniani kote. Kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume husababishwa na mambo mengi kama KISUKARI, UNENE ULIOPITILIZA, KUJICHUA (MASTER BLASHION), UNYWAJI WA POMBE, HOMONI kushindwa kufanya kazi ipasavyo n.k. Upungufu wa nguvu husababisha tendo la ndoa kutokufanyika kwa kujiamini na kwa usahihi na hivyo kusababisha ndoa na mahusiano kuvunjika.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa ☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni ☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo. Kwa kutumia mimea na matunda @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 6.5 hadi 7 @150,000/=
3.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari na kuweza kurudia tendo @150,000/=
4.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni @130,000/= BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA NA ZIMETHIBITISHWA KIAFYA. KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE KAMA
>Kupunguza unene na manyama uzembe @150,000/=
>Kuondoa mvi milele zisiludi @150,000/=
>Kutengeneza shepu (hips, makalio na mapaja) 200,000/=
>Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni @130,000/=

Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa (+255) 0767447444 na 0714335378

NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

Roma Mkatoliki: Nimechoka Kukaa Zimbabwe Nimeridu Sasa......

$
0
0
Rapa Roma Mkatoliki ambaye alikuwa amepiga kambi kwa Robert Mugabe nchini Zimbabwe amerejea nchini tayari na kusema amechoka kukaa huko alikokuwa hivyo ameamua kurejea nchini Tanzania kwa Rais Magufuli ili awe karibu na familia yake.

Roma anasema alimtuma mkewe aweze kumuwakilisha katika kuachia kazi yake mpya Zimbabwe anadai sasa amerudi hivyo sasa kazi yake ni kupita kila Radio na Television ili aweze kuongea na watu wake na kuwaeleza maana halisi ya Zimbabwe.

Mtazame hapa Roma akifunguka zaidi

Bodaboda Wapigwa Marufuku Kubeba Wanafunzi na Watoto Chini ya Miaka 10

$
0
0
Jeshi la Polisi  August 15, 2017 limetoa tamko la kupiga marufuku Waendesha Bodaboda kubeba watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 na kwamba atakayekiuka agizo hilo pamoja na mzazi aliyeruhusu mwanawe kubebwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na faini, kifungo au vyote viwili.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Theopista Malya, amesema kuwa watoto wamekuwa kwenye hatari kubwa wakipandishwa kwenye Bodaboda na wakati mwingine waendesha bodaboda hubeba watoto zaidi ya mmoja jambo ambalo ni lazima likemewe.

Aidha, alisema kuwa Jeshi hilo limeandaa kipindi maalumu cha Radio kitakachorushwa na Clouds FM kila siku ya Jumatano saa 2:00 Usiku kikiwa na lengo la kuongeza elimu kwa waendesha Bodaboda katika kuzingatia Usalama Barabarani pindi wanapofanya shughuli zao.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama barabarani (TSA), John Seka alisema kipindi hicho kitalenga kuwapa elimu waendeshaji wa bodaboda.

Pia, alitumia nafasi hiyo kuwataka wafuate sheria zilizowekwa na Sumatra ili waepukane na mkono wa sheria.

Paulina Shayo ambaye ni mwakilishi kutoka WAT Saccos alisema kuwa wanatoa mikopo kwa bodaboda na kwamba mikopo hiyo itawasaidia kuwa wamiliki halali wa vyombo hivyo.

Niki Awatolea Uvivu Wasanii

$
0
0


Niki Awatolea  Uvivu Wasanii
Msanii kutoka kampuni ya Weusi Nikki wa Pili amefunguka na kuwachana wasanii wenzake ambao wanapuuzia vikao vinavyoitishwa na kudai endapo hawatobadilika na tabia hiyo basi watambue haki zao zitachelewa kuwafikia.

Nikki amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya yeye kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wasanii wa kusimamia mfuko wa wasanii wa bongo fleva ambao utawasaidia wasanii watakao kuwa wanahitaji fedha kutoka katika mfuko huo.

"Wasanii ambao wanapuuzia kuja katika vikao nawaambia haki zao zitachelewa kuja, mpaka pale mtakapoamua kukaa mstari wa mbele haki ndipo zitakuja lakini mkiendelea kukaa hivyo mtatoa nafasi kwa watu wengine kutengeneza sheria ambazo zitakuja kuwaathiri", alisema Nikki wa Pili.

Kimenuka Mgodi wa Acacia Wananchi Waandamana Kushinikiza Malipo Yao.

$
0
0

Kimenuka Mgodi wa Acacia Wananchi Waandamana  Kushinikiza Malipo Yao.
Wananchi wanaoudai mgodi wa Acacia North Mara fidia ya maeneo yao kwa kukaa muda mrefu bila kuwalipa, wameandamana kwenda mgodini kushinikiza malipo yao.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe amesema maandamano hayo yanafanyika mara kwa mara kutokana na baadhi ya  majina kuondolewa kwenye orodha ya waliohakikiwa.

Kamanda Mwaibambe amesema kuwa majina ya watu hao yaliondolewa kwenye orodha hiyo na mgodi huo baada ya kukutwa yameongezeka wakati wa kuwasilishwa mgodi hapo kwa malipo yaliyotakiwa kutolewa na kufanya shughuli ya ufidiaji kukwama.

Hata hivyo, kundi hilo la wananchi limetawanywa na polisi waliokuwa na gari la maji ya kuwasha ambalo limesimama kwenye lango mkuu la kuingia mgodi .

"Nina taarifa ya kuwepo kwa maandamano hayo siku za nyuma, lakini kwa siku ya Leo sina hiyo taarifa labda nifuatilie utanicheki baadaye," amesema Kamanda Mwaibambe.

Ameongeza kuwa baada ya mgodi huo kubaina kuwepo kwa ongezeko la idadi ya wanaodai wafidiwe maeneo yao, waliandika barua kwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga ili kulishughukikia.

"Mkuu wa wilaya ndiye anayeweza kulisemea hilo vizuri maana nijuaavyo mimi alikabidhiwa orodha hiyo kwa ajili ya kuishughulikia," amesema.

Hata hivyo, simu ya mkononi ya Mkuu wa Wilaya, Luoga ilipopigwa kujua hatua iliyofikiwa kwa wananchi hao kupata haki yao, haikuwa hewani.

Hivi karibuni kundi la wananchi lilivamia kwa siku mbili mfululizo mgodi huo likitaka kuokota mawe ya dhahabu ambapo watu zaidi ya 60 walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uvamizi na hadi sasa wapo rumande.

Shirika la Kutetea Haki Lavamiwa na Maafisa wa Serikali Kenya

$
0
0
Shirika la Kutetea Haki Lavamiwa na Maafisa wa Serikali Kenya
Polisi na maafisa wa mamlaka ya mapato nchini Kenya (KRA) leo walifanya jaribio la kuvamia afisi za shirika moja la kutetea haki ambalo lilikuwa limefutiwa usajili Jumanne.
Maafisa hao waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia walifika katika afisi za shirika la Africa Centre for Open Governance (AfriCOG) katika mtaa wa Lavington, Nairobi mapema asubuhi.

Walikuwa kwenye magari wawili wakiwa na agizo walilosema lilitoka kwa mahakama kuwapa idhini ya kufanya uchunguzi katika afizi hizo, wakisema lengo lao lilikuwa kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za ukwepaji kodi.
Maafisa hao hata hivyo walizuiwa kuingia na viongozi wa mashirika ya kutetea haki za kibinadamu.
Wakili Haron Ndubi amesema walitilia shaka uhalali wa agizo la mahakama ambalo maafisa hao walikuwa nalo.

odi ya kusimamia mashirika yasiyo ya kiserikali ilikuwa imetoa agizo la kutaka shirika hilo lifunge ikisema limekuwa likiendesha shughuli zake kinyume cha sheria.
Mkuu wa bodi ya kusimamia mashirika yasiyo ya kiserikali Fazul Mohammed, pamoja na kufutia usajili shirika hilo, alikuwa amependekeza wakurugenzi wake wakamatwe.

Shirika la AfriCOG liligonga vichwa vya habari mwaka 2013 baada ya kuwasilisha kesi ya kupinga kuchaguliwa kwa Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi uliokuwa umefanyika mwezi Machi.
Taarifa kwenye vyombo vya habari zimekuwa zikidokeza kwamba huenda shirika hilo linapanga kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ambayo yalitangazwa Ijumaa ambapo Bw Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi.


Hatua ya kufunga shirika hilo ilitangazwa Jumanne siku moja baada ya serikali kufutia usajili shirika jingine la haki za binadamu, Tume ya Haki za Kibinadamu Kenya (KHRC).
Umoja wa Mataifa na shirika la Amnesty International wameshutumu hatua ya kuyafunga mashirika hayo mawili na kuitaka serikali kuruhusu mashirika ya kutetea haki pamoja na wanahabari kuruhusiwa kufanya kazi bila kuhangaishwa.

Mkurugenzi wa Amnesty International katika kanda ya Afrika mashariki Muthoni Wanyeki amesema njia iliyotumiwa na maafisa hao kuvamia afisi za AfriCOG ni kinyume cha sheria.
Amesema ana wasiwasi sana kwamba serikali ya Bw Kenyatta imeanza kuandama mashirika ya kutetea haki za kibinadamu.

Povu Hili la Bella Alijamuacha Wolper na Wenzake Salama

$
0
0

Povu Hili la Bella Alijamuacha  Wolper na Wenzake Salama
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Issabela Mpanda au Bella Fasta amewatolea povu wasanii wenzake wa kike wenye tabia ya kupenda kuwa kwenye mahusiano na wanaume wanaowazidi umri, na kuwaambia kuwa hawajielewi


Akizungumza na mwandishi wetu, Bella Fasta amesema wasanii hao wanapenda ku 'fake' maisha, na ndipo wanapoangukia kwenye mambo ya kutia aibu, licha ya matukio mbalimbali  waliyoipitia kwenye mahusiano yao siku za nyuma.

Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Kenya Azuiwa Uwanja wa ndege

$
0
0

Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Kenya Azuiwa Uwanja wa ndege
Roselyn Akombe alikuwa akielekea nchini Marekani kwa ziara rasmi ya kikazi wakati maafisa wa uwanja wa ndege wa JKIA walipomkamata kwa kukosa kibali cha kumruhusu kutoka nchini kutoka kwa mkuu wa maafisa wa umma.

Alizuiwa katika kituo cha polisi cha uwanja wa ndege kabla ya ubalozi wa Marekani kuingilia kati na kulazimu apalekwe katika anga ya serikali katika uwanja huo.
IEBC ilithibitisha kisa hicho ikisema kuwa Akombe alikuwa akielekea Marekani kwa ziara rasmi na alitarajiwa kurudi siku ya Jumapili Agosti 20.

Baadaye aliruhusiwa kuondoka baada ya mkuu wa maafisa wa umma Joseph Kinyua kuingilia kati.
Aliondoka nchini Kenya alfajiri ya siku ya Jumatano tarehe 16.
Akombe ni mmoja wa makamishna waliosimamia uchaguzi mkuu nchini Kenya ambapo rais Uhuru Kenyatta aliihifadhi kiti chake.

Upinzani nchini humo Nasa umepinga matokeo hayo na unatarajiwa kutoa mwelekeo kwa wafuasi wake siku ya Jumatano, Agosti 16.
Baadhi ya wafuasi wa muungano huo wamekabiliana na maafisa wa polisi wakipinga matokeo hayo.
Hatua hiyo imesababisha mauaji ya raia huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Kutana na Muuza Maji ya Madumu Anayetengeneza Pesa Nyingi Kwa Mwezi zaidi ya mtu Mwenye Degree.

$
0
0
Salaam wakuu,
Siku chache tu zilizopita, nilihamisha makazi yangu kutoka Sinza na kuhamia magomeni makanya.

Hapa pana shida ya maji sana. Sasa kuna kijana mmoja wa kisukuma almaharufu kwa jina la Ngosha, anauza maji ya madumu kwa ajili ya matumizi. Dumu moja anauza Shilingi 500.

Ana jumla ya madumu 50. Huamka asubuhi na mapema sana majira ya saa kumi. Huyafuata maji na mkokoteni wake hadi majira ya saa moja, anakua amejaza madumu yote 50 na kuyaleta makanya kuyauza.

Ikifika mida ya saa nane mchana, hua anakua ameuza madumu karibu 40, hivyo anafuata madumu mengine kama 20 hivi kwa ajili ya kuuza jioni. Anauza maji hadi saa tano usiku. Kuna wakati ikifika mida ya saa tatu usiku, anakuwa amemaliza maji na anakwenda kupumzika.

Nilimuuliza siku biashara ikiwa mbaya, anakuwa ameuza madumu mangapi, akaniambia 50. Sasa tuchukue hii minimum tuifanye ndo kwa kila siku, kwa mwezi inakuwa ni pesa nyingi zaidi ya hata mtu anayelipwa mshahara wa degree.

Chukua 50x500= 25,000. Alafu chukua 25000x30=750,000.
Kwahiyo huyo kijana anapata shilingi laki saba na nusu kwa mwezi ambayo hata hatozwi kodi.. Hiyo ni take home.

Huyu kijana maisha yake ni mazuri, ana mke na watoto wawili. Amekodi vyumba vitatu kwa ajili ya kuishi yeye na familia yake. Mtoto wake wa kwanza yupo darasa la kwanza.

Asubuhi anapata breakfast nzito ambayo ni chapati mbili, maharage bakuli moja, supu ya utumbo bakuli moja, soda moja ya pepsi na maji ya masafi lita moja. Hiyo ni asubuhi tu. Jioni lazima apate bia mbili pia.

Kwa sasa amenunua kiwanja huko mbezi na anajenga nyumba yenye Rumu nne.
Huyu kijana hata mimi mshahara wangu ni mdogo zaid ya anachoingiza.
Kweli kusoma siyo kupata pesa mingi na kufanikiwa.

Wakati huo huo mimi ninawaza hapa napata wapi hela ya kodi mwezi ujao landlord ameanza kukumbusha...
Ngoja nipate chai ya Tangawizi +asali +mdalasini.. Then narudi.

Imeandikwa na Mjina Mrefu

Idadi ya Waliofariki Kwenye Mafuriko Siera Leone yafikia 300

$
0
0




Idadi ya Waliofariki Kwenye Mafuriko Siera Leone yafikia 300
Sierra Leone imeingia kwenye headlines mbalimbali duniani baada ya kuingia kwenye maombolezo makubwa kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku tatu katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Freetown.

Inaelezwa kuwa zaidi ya watu 300 wamefariki huku wasiwasi ukiongezeka kuwa zaidi ya watu 600 hawajulikani walipo.

Dayna Nyange Aamua Kumjibu Shilole

$
0
0

 Dayna Nyange Aamua Kumjibu Shilole
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amesema hakuna msanii ambaye anaweza kufanya kitu na kuweza kuwapoteza wasanii wengine.



Kauli hiyo ni jibu kwa Shilole ambaye wakati anakaribia kutoa wimbo ‘Kigori’ alidai amewapa nafasi wasanii wa kike lakini wameshindwa kufanya vizuri hivyo anakuja kulichukua game

“Mimi nafikiri yeye ndio anaweza kuwa majibu yote kwamba kwa nini amekuja kuchukua game yake, labda alikuwa kimya kwa muda mrefu akawa anaona bado nafasi yake ipo. Unajua kila mmoja ana riziki yake kwenye hizi kazi usitengemee kwamba Dayna atakuja kufanya kitu fulani nimpoteze mtu fulani, hapana kila mta na riziki yake na kila mja na wakati wake,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“I think ni wakati wake kama alifanya kitu fulani akaona mafanikio yake lakini akaona huku bado kulikuwa na mafanikio yake au anahitaji zaidi, so ana haki ya kufanya, kusema anachuku game ni misamiti tu ya lugha zetu za kisanii,” amesema Dayna.

Kuhusu lini atatoa ngoma mpya amesema, “watu wameona kimya baada ya kuachia Komela, lakini niseme always sipendi kukurupuka napenda nifanye kila kitu kwa wakati kiwe kizuri zaidi ya Komela, so very soon Mungu akijalia kazi yangu mpya itakuja,” amesema Dayna.

Ratiba ya Mapokezi ya Majeruhi wa Lucky Vicent Hii Hapa

$
0
0




Ratiba ya Mapokezi ya Majeruhi wa Lucky Vicent Hii Hapa
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ametoa ratiba ya majeruhi wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha ambao walikuwa nchini Marekani kimatibabu kufuatia ajali walioipata.



Mhe. Nyarandu kupitioa ukurasa wake wa instagram ameweka ratiba hiyo kuwa watapitia katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) ambapo mgeni rasmi atawasili saa mbili asubuhi.

RATIBA ya MAPOKEZI KIA: Familia na Wananchi wanatarajiwa KUWASILI KIA saa 3 asubuhi, Mgeni Rasmi atawasili saa 2 asubuhi, na Ndege aina ya DC-8 inayowaleta WATOTO itakua saa 3 asubuhi. Hafla itafanyika KIA, upande wa Magharibi mwa UWANJA kupitia VIP. Wote mnakaribishwa! Kesho nitatoa RATIBA ya vile HAFLA ya uwanjani itakavyofanyika. (Mapema leo nilitembelea KIA kushiriki kupanga ITIFAKI na MPANGILIO wa HAFLA utakavyokuwa, na tayari nimempokea Daktari Bingwa Steve Meyer (akiwa n.a. mke wake Dana Meyer) aliyeongoza matibabu ya WATOTO, sote tukiwa tayari kwa mapokezi.KARIBUNI sana!

Watoto hao Doreen Wilson na Sadia wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa hii Augost 18, 2017 ambapo watapokelewa katika uwanja huo.


Mercy Masika na Angel Bernard kuwapokea majeruhi Lucky Vincent

$
0
0




Mercy Masika na Angel Bernard kuwapokea majeruhi Lucky Vincent
Msanii wa muziki wa injii kutoka nchini Kenya, Mercy Masika pamoja na Angel Bernard wanatarajiwa kuudhuria hafla ya kuwapokea watoto walioenda kutibia nchini Marekani ambao walinusurika katika ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ya Arusha.



Watoto hao Doreen Wilson na Sadia wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa hii Augost 18, 2017 ambapo watapokelewa katika uwanja wa ndege wa KIA, kilimanjaro.

“Shukrani wanamuziki wa injili Mercy Masika kutoka Nairobi (ikiwa ni mara yako ya kwanza kukanyaga ardhi ya Arusha) na Angel Bernard wa Arusha kwa kujitolea kwenu kushiriki baraka hizi za kuwapokea watoto wetu,” ujumbe huo ameuandika Mbunge wa Singida Kasikazini, Lazaro Nyalando na kuongeza

“Nimefurahia utayari I wenu, na shauku mliyonayo kuhusu hafla hii. Naamini wana familia, ndugu, jamaa na marafiki, ikiwa ni pamoja na viongozi wetu wote watafurahia sana vipawa vyenu katika kumtukuza Mungu. Watoto Doreen, Wilson na Sadia wataikumbuka siku kuu ya ujio wao kwenye nchi yao pendwa Tanzania wakiwa wameuona mkono wa Mkombozi katika maisha yao,”. ameandika katika Instagram.


Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images