Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Mzungu Akosa Dhamana Aendelea Kusota Rumande

$
0
0
Mzungu Akosa Dhamana Aendelea Kusota Rumande
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, le0 Agosti 18, 2017 imemnyima dhamana raia wa Afrika Kusini ambaye ni mhandisi, Menelaos Tsampos, anayetuhumiwa kwa kosa la kumtishia mtu kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa kompyuta.

Upande wa utetezi unaoongozwa na wakili Deus Singa ulikuwa ukiiomba mahakama hiyo kumpa dhamana Menelaos wakati kesi yake ikiendelea, huku upande wa mashitaka ukipinga kupewa dhamana kwa kile walichokieleza kuwa akiachiwa huru anaweza kumdhuru aliyemtishia maisha.
Kutokana na hoja hizo, hakimu aliiahirisha kesi hiyo hadi kesho Agosti 18, 2017 ambapo itaelezwa iwapo atapewa dhamana. Mshitakiwa wamerudishwa rumande.

Menelaos anadaiwa mahakamani hapo kuwa Juni 22, mwaka huu maeneo ya jijini Dar es Salaam, kupitia mfumo wa kompyuta alituma ujumbe wa baruapepe (E-mail) uliokuwa na maneno ya vitisho kwa mtu anayeitwa Costa Gianna, ikiwa ni kinyume na sheria ya mtandao kifungu cha 23(1) na (2) namba 14 ya mwaka 2015.

Mzungu huyo amekua gumzo mahakamani hapo alipoanzisha timbwili kortini hapo juzi baada ya kuwachimba mkwara mzito waandishi wa habari waliokuwa wakimpiga picha siku ya kwanza alipofikishwa mahakamani0.

Wanaume Watakiwa Kupima Tezi Dume

$
0
0




Wanaume Watakiwa Kupima Tezi Dume
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee ma Watoto, Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wanaume kupima saratani ya tezi dume huku akiwatoa hofu kuwa kipimo cha kupima saratani ya Tezi dume unapima kwa kutoa damu na sio kipimo kinachotembea mitandaoni.



Waziri Ummy ametoa wito huo mkoani Katavi Manispaa ya Mpanda pamoja na wananchi waliotoka wilaya ya Mlele na Tanganyika mara baada ya kuzindua zoezi la upimaji magonjwa ya sio ya kuambukizwa.

“Lakini inaweza kuwa wanaume mnaogopa kupima saratani ya tezi dume na mimi nitoe wito kwa wanaume mpime kwasababu pia sio kile kipimo kinachotembea mitandaoni kipo kipimo cha kupima saratani ya Tezi dume ambapo unapima kwa kutoa damu na sio vile mnavyofikiria kile kipimo ambacho watu wanakiogopa hicho sicho kipo kipimo rafiki,” aliongeza Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy alisema kuwa serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watumishi wa afya wasiotoa huduma za kuridhisha na wenye kashfa ya kutokuwa na maadili ya kazi.

“Pale ambapo muuguzi amekujibi vibaya, daktari amekujibu vibaya na mkunga hajakufanyia vizuri, wauguzi wa hospitali ya Mpanda wengi ni wazuri tutajie jina na sisi tutamchukulia hatua na tutamwambia atupishe wapo watu wengi sana wanaotaka kufanya kazi katika hospitali za serikali,” alisema Ummy.


Nchemba Ataka Uchunguzi Ufanyike Kuungua Soko la Sido

$
0
0




Nchemba Ataka Uchunguzi Ufanyike Kuungua Soko la Sido
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameagiza jeshi la zimamoto na Uokoaji na kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mbeya kuchunguza wa kina juu ya chanzo cha kuungua soko la Sido lililopo mkoani humo.



Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ambapo alitoa rai kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanashirikiana na jeshi la Zimamoto wakati wa ujenzi ili kuweka miundombinu itakayoweka shughuli za uokoaji.

“Uchunguzi ufanyike kuhusu ni vyanzo vya matukio ya moto ambavyo vimeanza kujitokeza na naelekeza maeneo mengine yote kuchukua tahadhari kufuatana na mazingira yao kuhusu masuala haya ya moto yanayoweza kujitokeza yanatupozea mali za watu lakini pia ni matukio ya hata yanayoweza kutugharimu zaidi hata ya hizo mali zitakazo weza kujitokeza,” alisema Nchemba.

“Zaidi nitoe lai kwa halamashauri ambapo taratibu za ujenzi zinafanyika, mar azote wanapofanya shughuli za ujenzi wahakikishe wanashirikiana na mamlaka ya zima moto ili kuweka kwenye mpangilio matarajio ya namna vifaa vya uokoaji vinavyoweza kupita punde yanapotokea matukio kama haya,”Waziri Nchemba


Odinga Akimbilia Mahakamani Kupinga Matokeo ya Urais

$
0
0




Odinga Akimbilia Mahakamani Kupinga Matokeo ya Urais
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kwamba muungano wake wa National Super Alliance (NASA) utawasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya ushindi wa Rais mteule Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne ya tarehe 8 Agosti 2017 wiki iliyopita.





Bw. Odinga amesema ingawa muungano huo ulikuwa umeapa kutowasilisha kesi kortini wakati huu, wameona ni heri kufanya hivyo ili kufichua uovu uliotokea wakati wa uchaguzi mkuu.

“Tumeamua kwenda kortini kufichua jinsi uongozi wa kompyuta ulivyofanikisha kuiba kura zetu, “,amesema Bw Odinga akiwahutubia wanahabari jijini, Nairobi.

Kiongozi huyo wa upinzani ameendelea kusisitiza msimamo wa NASA kwamba uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki huku akidai mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) ilidukuliwa na matokeo kuvurugwa na kumfanya Bw Kenyatta ashinde.

“Mtindo huu ulitokea pia katika maeneo mengi uchaguzi wa ugavana, Jambo kama hili halijawahi kutokea katika uchaguzi wa kidemokrasia pahala pengine popote duniani lakini ilitokea hapa“,amesema Odinga.

Bw Odinga amesema udukuzi huo una uhusiano na kuuawa kwa meneja wa teknolojia katika tume hiyo Chris Msando ambaye aliuawa wiki moja kabla ya uchaguzi.

Kwa upande mwingine NASA wameishutumu tume ya uchaguzi kwa kusema ilikuwa ikitangaza matokeo ya uchaguzi bila kutoa Fomu 34A za kuonesha matokeo yalivyokuwa katika vituo vya kupigia kura.

NASA wamebaini udanganyifu mwingi uliotokea na kuwashutumu waangalizi wa uchaguzi ambao walisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.



Jamii ya kimataifa ilikuwa imehimiza upinzani, pamoja na wagombea wengine ambao hawakuwa wameridhishwa na uchaguzi, kutumia mifumo iliyowekwa kikatiba kutafuta haki.

Kwa mujibu wa matokeo ya IEBC, Rais Kenyatta alipata kura 8,203,290 huku mgombea mwenza Raila Odinga akipata kura 6,762,224.


Maneno ya Manara kwa Yanga Baada ya Taarifa ya Jengo lao Kupigwa Mnada

$
0
0


Maneno ya Manara kwa Yanga Baada ya Taarifa ya Jengo lao Kupigwa Mnada
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kuwapa pole watani wake wa jadi klabu ya Yanga kufuatia taarifa iliyotoka katika moja ya gazeti kuonyesha jengo lao litapigwa mnada Jumamosi ya wiki hii.


Haji Manara ametoa pole hiyo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kuwaombea watani wao wajadi kwa kusema hivi sasa hali yao si nzuri hivyo kama jengo hilo kitauzwa watakwenda kukaa wapi.
"Mungu wangu,Jumosi hii jengo la Yanga linapigwa mnada, Wizara ya Ardhi waoneeni huruma kidogo wenzetu wana Swaumu kali, Daah!!sasa watahamia wapi? Shubamit" alimalizia Haji Manara

Jengo la klabu ya Yanga jijini Dar es Salaam linatarajiwa kupigwa mnada Agosti 19 kwa amri ya Mahakama baada ya kudaiwa kodi ya ardhi zaidi ya milioni 300.
Mbali na hilo klabu ya Simba na Yanga zote zipo visiwani Zanzibar zikijipanga kwa ajili ya mchezo wa ngao ya jamii unaowakutanisha watani hao katika uwanja wa Taifa siku ya Jumatano ya tarehe 23 Agosti 2017.



Nay wa Mitego Akumbwa na Kashfa ya Kufumaniwa

$
0
0
Nay wa Mitego Akumbwa na Kashfa ya Kufumaniwa
Msnii‘Nay wa Mitego’ amedaiwa kukwaa skendo ya kufumaniwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Tina.
Tukio lililokusanya ‘nzi’ wa kutosha, linadaiwa kutokea hivi karibuni nyumbani kwa msanii huyo, Kimara- Mwisho jijini Dar mida ya saa moja usiku ambapo Nay anadaiwa kuwa, aliingia mchana na gari yake akiwa na mrembo mwingine kabla Tina hajafika ‘kuliamsha dude.’

Chanzo makini kilichoshuhudia mtiti huo mwanzo mwisho, kimesema

“Yaani nilishuhudia mwanzo mwisho kwa sababu mimi naishi maeneo haya na Nay ni jirani yetu. Awali nilimuona Nay akiingia ndani na mrembo mmoja simjui jina lake. Wakaingia ndani. Baada kama ya saa tatu, alikuja mrembo mwingine na Bajaj.

“Sasa huyu aliyekuja na Bajaj alipofika getini, akagonga ndipo akatoka yule mrembo aliyekuja na Nay, ghafla nashangaa wanaanza kurushiana maneno. Yule aliyekuja na Bajaj akawa anamzodoa yule aliyemkuta ndani na kumuambia amefuata nini kwa bwana’ke,” kilieleza chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga ubuyu zaidi, chanzo hicho kilisema mara baada ya kurushiana maneno Nay alitoka na kuwaamulia huku akimuingiza ndani yule binti aliyekuwa naye na kumsihi yule dada aliyekuja kufumania aondoke kabla hajamuitia polisi.
“Nay alikuwa mkali kweli akamuambia yule binti aondoke haraka sana kwani hana mpango naye asije akamuitia polisi, yule dada akawa mpole akaondoka zake,” kilisema chanzo hicho.

  Kwa upande wake Nay Alisema
“Hii ishu si kwamba ni fumanizi, huyo Tina aliwahi tu kuwa mpenzi wangu zamani sana, sasa nikashangaa amekuja kufanya fujo home na ndio maana umeona amekuwa mpole baada ya mimi kutokea. Sina mpango naye, ana maisha yake na mimi nina maisha yangu.
“Kwanza hata huyu binti wa watu aliyemletea fujo si mpenzi wangu. Ni msanii ambaye tunafanya naye kazi, bado hajatoka kivile.”

Ndalichako Ashiriki Zoezi la Ufuatiliaji wa Miradi ya Elimu Mkoani Kigoma .. Atoa Neno

$
0
0

Ndalichako  Ashiriki Zoezi la Ufuatiliaji wa Miradi ya Elimu Mkoani Kigoma .. Atoa Neno
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo ameshiriki zoezi la ufuatiliaji wa miradi ya elimu Wilayani Kibondo, mkoani Kigoma inayotekelezwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara yake.

Akizungumza katika mkutano na baadhi ya watendaji wa serikali na washirika wa maendeleo, Waziri  Ndalichako amesisitiza kuwa dhamira ya  serikali ya awamu ya tano ni kuahakikisha elimu bora inatolewa ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya shule.

Ndalichako amesema serikali inafarijika sana kuona wananchi wanajitolea katika kuboresha miundombinu hivyo ameahidi kuchangia mabati 100 ambayo yatasaidi kuboresha ujenzi wa shule shikizi ya Nyamilembi ambayo inajengwa kwa nguvu za  Wananchi.

"Sisi serikali tunawapongeza sana kwa kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha  watoto wote wanapata elimu, na tunapenda sana watoto wote wasome bila kujali maumbile yao, sasa kwa kuwa mmeonyesha dhamira ya dhati ya kujenga shule shikizi na mimi nitawaunga mkono na ninawaahidi kuwaletea mabati 100", alisema Ndalichako.

Waziri Ndalichako amesema Ziara hiyo pia inalenga kubaini changamoto mbalimbali zinazozikabili shule ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kibondo Louis Bura amesema kuwa shule shikizi ya Nyamilembi inajengwa na Wananchi kwa kuona na kutambua umuhimu wa Elimu kwa watoto wao.
Shule nyingine ambazo ujumbe huo umezitembelea ni pamoja na Shule ya msingi jumuishi  Nengo pamoja na shule ya Sekondari  wasichana Kibondo

Viongozi wengine walioshiriki ziara hiyo ni pamoja na Mkuu wa  Wilaya ya Kibond Louis Bura, baadhi ya watendaji kutoka Tamisemi, Wizara ya Elimu, wadau wa Elimu, na washirika wa Maendeleo wakiwemo SIDA na DFID.

Ofisi ya Mkemia mkuu Yaelemewa na Kemikali

$
0
0

       



 Ofisi ya Mkemia mkuu Yaelemewa na Kemikali
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema imelemewa na kiwango kikubwa cha kemikali za matumizi ya nyumbani na viwandani zinazoingizwa nchini kwa siku.

Akizungumza leo Alhamisi, Agosti 17 jijini Dar es Salaam, Mkemia Mkuu wa Serikali, Samwel Manyele amesema ongezeko hilo linatokana na waagizaji wengi kuagiza mzigo wa kemikali bila kufuata sheria.

Amesema kabla ya mwaka 2013 walikuwa wakitoa vibali vitano hadi saba kwa siku, lakini kuanzia mwaka huo wamekua wanatoa vibali 100 hadi 150 kwa siku huku wakilazimika kufanya kazi saa 24.

"Sheria inamtaka muagizaji wa kemikali kuomba kibali, kusajiliwa kabla ya kuagiza mzigo, lakini walio wengi wanakiuka sheria kwa kuagiza mzigo ukiwa bandarini ndiyo wanaanza kuomba nyaraka hizo muhimu," amesema Profesa Manyele.

Profesa Manyele amesema mrundikano wa mizigo unakuwa mkubwa kutokana na kuwa na wafanyakazi wasiofika 100 nchi nzima.

"Kuna vituo vingi vya kupokelea kemikali, ndani ya bandari vipo sita na nje vipo 17.

" Kutokana na wingi huo wakaguzi wanalazimika kutumia muda mwingi kutembea kufuata mizigo ilipo,"amesema Profesa Manyele.

       

Makao Makuu ya Jengo la Yanga Kupigwa Mnada na Mahakama

$
0
0

Makao Makuu ya Jengo la Yanga Kupigwa Mnada na Mahakama
Mahakama imetoa amri ya Jengo la Klabu ya Yanga lililopo mitaa ya Jangwani kunadiwa.
Hii inatokana na deni la kodi ya Majengo la Sh milioni 360 ambazo klabu hiyo inadaiwa na Serikali.

Siku ya mnada imepangwa kuwa Agosti 19 yaani keshokutwa kuanzia saa 4 asubuhi na Msolopa Investment ndiyo itakayohusika na mnada huo.
Hali hiyo inaonekana kuwashitua mashabiki wengi wa Yanga.
Mtandao huu ulifanya juhudi za kumtafuta msemaji wa Yanga Dismas Ten, simu yake iliita bila kupokelewa ndipo alipotafutwa msaidizi wake, Godlisten Anderson Chicharito na kusema yeye hafahamu chochote na atafutwe katibu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa ndio mwenye majibu ya madai hayo.

Hata hivyo, baadaye Kampuni ya Msolopa kupitia kwa mkurugenzi wake, Ibrahim Msolopa, ilitangaza kuahirisha kwa mnada huo kutokana na makosa yaliyofanyika kabla ya kutoka kwa tangazo hilo kwani walipanga mnada huo ufanyike leo na sio Jumamosi kama ambavyo tangazo linavyosomeka magazetini.

Mobetto Amaliza Utata Athibitisha Kuzaa na Diamondi

$
0
0




Mobetto Amaliza Utata Athibitisha Kuzaa na Diamondi
Mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobetto Jumatatu hii ametimiza siku saba toka azaliwe Agosti 8 mwaka huu ambapo amepewa jina la Abdul Naseeb. Jina ambalo limeanza kumaliza maswali mengi ya mashabiki ambao walitaka kumjua baba wa mtoto huyo.


Awali mrembo huyo alifungua akaunti ya Instagram kwa jina ‘Tanzania Baby’ lakini Jumanne hii alibadilisha jina na kuandika ‘Abdul Naseeb’ ambapo kwa sasa akaunti hiyo tayari ina wafuasi zaidi 50,000.

Mobetto kupitia Instagram alipost picha yake ya wakati ni ujauzito huku akii-tag akaunti ya mtoto wake huyo na kuandika “Goodnight 😘 .Thank U for this outfit love @fifi_sugardesign . Love U baby dee @abdulnaseeb_tz,”


Wiki iliyopita kupitia kipindi cha Shalawadu cha Clouds TV, mama Diamond pamoja na dada yake Diamond, Esma walionekana katika nyakati tofauti wakiwa katika hospitali moja ambayo alijifungilia mrembo huyo.

Diamond ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul, hajatoa kauli yoyote juu ya mtoto huyo licha tetesi hizo kuonyesha zinaukweli ndani yake.

Kwa sasa muimbaji huyo ambaye ni rais wa WCB, ni baba wa watoto wawili aliozaa na Zari The Bosslady.


Alikiba Atangaza Ujio Wake Mpya

$
0
0




Alikiba Atangaza  Ujio Wake  Mpya
Hit maker huyo wa ‘Aje’ amekuwa na utaratibu wa kutoa ngoma chache kwa mwaka hali ambayo inawafanya mashabiki wake kuwa na shauku kubwa ya kusikia kazi zake mpya.

Wiki hii muimbaji huyo ameanza kuibua matumani mpya kwa mashabiki wake baada ya kuanza kutoa dondoo kuhusu ujio wake mpya ambapo alipost picha katika mtandao wake wa Instagram na kuandika wananiita ‘Kipusa’.


Katika picha nyingine muimbaji huyo amepost picha na kuandika “they call me a heartbreaker?#kingkiba” kauli ambayo imewafanya mashabiki wengi wa muimbaji huyo kuwa na shauku kubwa na kazi mpya ya muimbaji huyo baada ya Diamond anayedaiwa kuwa mpinzani wake kuachia nyimbo nyingi mfululizo.

Mpaka sasa Diamond tayari ameachia wimbo, Eneka, I Miss You, Fire akiwa akiwa amemshirikisha Tiwa Savage pamoja na Marry You aliyomshirikisha muimbaji wa R&B kutoka Marekani, Ne-Yo.

Mpaka sasa Alikiba bado hajaweka wazi ni lini ataachia kazi yake hiyo mpya inayosubiriwa kwa hamu.

Madee Asifia Umbile la Katuni Iliyotumika Katika Nyimbo Yake

$
0
0





Madee Asifia Umbile la Katuni Iliyotumika Katika Nyimbo Yake
Msanii Madee amesema ameridhika jinsi umbile la Jacqueline Wolper lilivyoweka kwa mfumo wa katuni katika video yake mpya ‘Sikila’ aliyomshirikisha Tekno kutoka Nigeria.



“Yeah, kwa sababu ni katuni ni kama comedy tu, inachekesha kwani hata mimi kile ni kichwa changu wewe umeridhika nacho?,  ndiyo tunasea hiyo ni comedy hakuna ukweli wowote ni kujaribu kufanya kitu kingine ambacho hakijawahi kufanyika, then maisha yaendelee,” Madee ameiambia Bongo5.

Katika hatua nyingine Madee amefafanua cover photo ya ngoma hiyo ambapo anaonekana yeye akiwa amesema na Wolper lakini msichana aliyesimama na Tekno hajaweza kujulikana.

“Huyo alikuwa anatakiwa awe Lulu, sasa huyo hajapatiwa kakosewa ndio maana yeye (mchoraji) akasema tuachane naye na tusijaribu kumtaja kwa sababu hajampatia. Tekno ni rafiki yake sana na Lulu kwa hiyo alikuwa anajaribu kutengeneza hicho kitu,” amesema Madee

TMA Yawatoa Hofu Wakazi wa Dar Kuhusu Mvua zinazonyesha

$
0
0


TMA Yawatoa Hofu Wakazi wa Dar Kuhusu Mvua zinazonyesha
Kufuatia kuendelea kwa mvua za hapa na pale jijini Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesema mvua hizo haziwezi kusababisha madhara kwani zinatokana na mabadiliko tu ya muda mfupi.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi, Agosti 17, Meneja kituo kikuu cha utabiri, Samwel Mbuya amesema  manyunyu na mvua zinazoonekana zimesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa hali ya hewa kama ambavyo taarifa ya hali ya hewa ya mamlaka hiyo ya Juni ilieleza.

Amesema  Mamlaka ya Hali ya Hewa itaendelea kutoa taarifa za hali na mwenendo wa mvua hizo ili kusaidia jamii kupata taarifa muhimu kuhusiana na maendeleo ya hali ya hewa.

 Ameongeza kuwa sambamba taarifa hizo  mamlaka itatoa taarifa ya utabiri wa mvua za vuli 2017 mwishoni mwa Agosti 2017.



Machinjio ya Nyama Yafungwa na TFDA

$
0
0


 Machinjio ya Nyama Yafungwa na TFDA
Baada ya mamlaka ya chakula na dawa kanda ya kati kufunga machinjio ya manispaa ya Singida, wakazi wa manispaa ya Singida wapo hatarini kupatwa na magonjwa yatokananyo na kula nyama kufuatia baadhi ya wauza nyama kuchinja Ng'ombe bila kupimwa.

Akiteketeza kwa moto kilo themanini na nne (84) za nyama ya Ng'ombe ambazo zilikutwa zikiuzwa katika mazingira machafu huku zikiwa zimehifadhiwa chini, Mkaguzi wa chakula kutoka TFDA kanda ya kati Bwana Aberl Deule, amesema wamefikia uamuzi wa kuteketeza nyama hiyo kwa sababu licha ya machinjio kufungwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakichinja ng'ombe vichochoroni na kuhatarisha maisha ya walaji.

Pamoja na madai hayo, wachinjaji wanyama wa manispaa ya Singida wametupia lawama kwa mkurugenzi wa manispaa ya Singida kuacha kufanyia matengenezo na usababisha machinjio kufungwa mara kwa mara, huku wao wakiwa wamekopa fedha katika sekta za benki.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida Bwana Deusi Luziga amekiri kuwa machinjio hayapo katika hali nzuri, ila manispaa imeanza kufanya ukarabati wa machinjio hayo na wameshatenga eneo la kujenga chinjio jingine jipya kulingana na kuongezeka kwa watu.

Watoto Lucy Vincent Waondoka Marekani Kupokelewa Kesho Uwanja wa KIA

$
0
0



Watoto Lucy Vincent Waondoka Marekani Kupokelewa Kesho Uwanja wa KIA
WATOTO watatu wa Shule ya Msingi Lucky Vincent waliokuwa majeruhi wa ajali iliyotokea Karatu na kwenda kutibiwa nchini Marekani, watawasili kesho asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mjini Arusha.
Watoto hao ambao ni Doreen, Sadia na Wilson waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani tayari wameshapanda ndege kutoka nchini humo kurejea Tanzania baada ya kupata nafuu.


Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.
Shukrani kwa madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea na kuchangia chochote kusaidia matibabu ya watoto hao.

Mkwasa Atoa Neno Kuhusu Kupigwa Mnada Jengo la Yanga

$
0
0


Mkwasa Atoa Neno Kuhusu Kupigwa Mnada Jengo la Yanga
Katibu Mkuu wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Charles Boniface Mkwasa amekiri kuwa klabu yao inadaiwa kodi na serikali huku akiwataka mashabiki na wanachama wa jangwani kuwa watulivu katika kipindi hiki.

Mkwasa amebainisha hayo leo baada ya taarifa kuwepo taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu jengo lao kupigwa mnada siku ya Jumamosi
“Ni kweli tuna deni kubwa tunadaiwa na ardhi lakini tayari tulifanya nao mazungumzo na kukubaliana namna ya kulilipa kupitia mapato yetu ya milangoni. Tatizo ni kwamba hapa katikati ligi ilisimama, lakini hivi karibuni inaanza na tutaendelea kulipa, Tutatoa taarifa rasmi baadaye”, alisema Mkwasa.

Mkwasa amesema kiasi wanachodaiwa ni kikubwa lakini hakizidi shilingi milioni 500, huku akiweka wazi kuwa pesa wanayotakiwa kulipa kwa mwaka ni shilingi milioni 59.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia kwa kampuni ya udalali ya Msolopa Investmenst Limited leo imetangaza kulipiga mnada jengo hilo endapo Yanga hawatalipa kabla ya Agosti 19, mwaka huu.

Nape Aguswa Zanzibar Kuvuliwa Uanachama CAF

$
0
0
Nape Aguswa  Zanzibar Kuvuliwa Uanachama CAF
Shirikisho la soka barani Afrika CAF lilitangaza kuivua Zanzibar uanachama wa CAF ikiwa ni miezi minne imepita toka shirikisho hilo liitangaze Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa CAF.

CAF waliivua uanachama Zanzibar katika utawala wa Rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad, baada ya utawala wa Rais  Issa Hayatoue kuondolewa katika nafasi hiyo na kurithiwa na Ahmad, moja kati ya sababu za Zanzibar kuvuliwa uanachama CAF wanadai hawaoni ulazima wa kuwa na wanachama wawili ndani ya taifa moja.

Waziri wa zamani wa habari, utamaduni, sanaa na michezo ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama kwa sasa Nape Nnauye ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika mtazamo wake kuhusiana na kuvuliwa uanachama wa CAF na inavyomsikitisha.



“Jambo la Zanzibar kuonyang’anywa uanachama Wa CAF, nimejaribu kulielewa nimeshindwa! Jambo hili nililisimamia mpaka likawa baada ya kushindikana kwa miaka!kukubali kuondolewa kirahisi tu SI SAWA! Tena kwa fitina ya nchi moja! SI SAWA! Nashauri TUSIKUBALI KIRAHISI HIVI!”


Kibabu Chaguswa na Ukimya wa Ali Kiba Aamua Kumfungia Safari

$
0
0

Kibabu Chaguswa na Ukimya wa Ali Kiba Aamua Kumfungia Safari

Mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Msaka amefunga safari kutoka Wazo Hill anakoishi mpaka studio za East Africa Radio kuja kuonana na Big Chawa, kumletea malalamiko yake kuhusu Alikiba.

Mzee huyo amesema anamtaka Alikiba aachie ngoma kali ambazo zitafunika kwa mwaka huu wote, kwani ukimya wake umemchosha.
Mashabiki wa Alikiba wamekuwa wakilalamikia kwa muda mrefu kitendo cha msanii huyo kukaa kimya muda mrefu bila kutoa kazi yoyote, wakati wasanii wenzke wakiachia ngoma kila siku.
Mtazame hapa chini alivyokuwa akimlilia Alikiba


Mtatiro Yamemfika Hapa...Adai ni Bora Kufanya Kazi na CCM Kuliko Lipumba

$
0
0
Mtatiro Yamemfika Hapa...Adai ni Bora Kufanya Kazi na CCM Kuliko Lipumba
Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amefunguka na kujibu hoja za baadhi ya watu ambao wanataka CUF kukubaliana na Professa Lipumba kwa kuwa Mwenyekiti huyo ameshika makali kutokana na vyombo mbalimbali vya serikali kumtambua.

Julius Mtatiro ambaye sasa yupo nchini Marekani alipokwenda kimasomo amesema hilo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema ni jambo ambalo halitawezekana wao kukubali yaishe na Profesa Lipumba na kusema wataendelea na harakati zao kuhakikisha haki yao inapatikana.

"Nasoma maoni ya baadhi ya watanzania kuja kwetu, kwamba kwa sababu serikali, dola, CCM, polisi, bunge, NEC, RITA, na Msajili wa Vyama vya Siasa wameshikamana kumuunga mkono Lipumba, na kwa hiyo ati Lipumba ameshikilia mpini na chama kimeshikilia makali kwa nini tusikubali yaishe? Lipumba apewe kila kitu...hadi roho zetu, lakini misingi yetu, misimamo yetu, umoja wetu na mshikamano wetu, hawezi kupewa. Hizi ndizo silaha zetu na niwaambie kuwa zina faida ya muda mrefu kuliko zile anazozitizama msaliti" alisema Mtatiro
Aidha Mtatiro anasema kuwa ni rahisi sana wao kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Profesa Lipumba

"Ni mara kumi kumsamehe jirani yako aliyembaka mwanao, kuliko kumsamehe baba yako mzazi aliyembaka mwanao. Adui wa ndani, ni hatari zaidi kuliko adui wa nje. CCM ni adui bora kuliko Lipumba na kwa hiyo ni rahisi sana kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Lipumba" alisisitiza Mtatiro

Paul Makonda Aanza Tena Kuwachokonoa Wauza Madawa ya Kulevya...Aomba Boti Kuwafuata Huku Huku Baharini

$
0
0
Paul Makonda Aanza Tena Kuwachokonoa Wauza Madawa ya Kulevya...Aomba Boti Kuwafuata Huku Huku Baharini
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meshimiwa Paul Makonda leo amepokea ugeni wa Wanajeshi wa Jeshi la Maji kutoka Nchini China waliokuja Nchini kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kijeshi ambapo amesema atandeleea na mikakati ya kudhibiti uingizwaji wa Dawa za kulevya zinazoingizwa Nchini kwa kutumia Bahari ya Hindi.

Katika mazungumzo kati Mkuu wa Mkoa na kikosi cha Jeshi hilo  amewasilisha ombi la kupatiwa Boti za kisasa zitakazotumiwa  Jeshi la polisi katika kuimarisha Doria kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi ili kukomesha Biashara za magendo ikiwemo ya Dawa za kulevya na Bandari bubu.

Ombi hilo la Boti limepokelewa kwa mikono miwili na Jeshi hilo ambalo pia limeonyesha kufurahishwa na namna Mheshimiwa Makonda anakali wananchi wake kwa kuhakikisha wako salama katika kazi zao za kila siku.

Aidha Jeshi hilo limemualika Mkuu wa Mkoa kwenda kutembelea Meli kubwa na ya kisasa ya Jeshi hilo ambayo tayari ipo nchini kwaajili ya kuona namna inavyofanya kazi.


Lengo la ujio wa Jeshi hilo Nchini kuimarisha mahusiano ya kijeshi baina ya Tanzania na China ili kwa pamoja waweze kupambana na uhalifu.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Majini la China Real Admiral Shen Hao amesema kuwa ombi la Mkuu wa Mkoa la kupatiwa Bodi za kisasa watalitimiza na kueleza kuwa wataendelea kuimarisha mahusiano ya kijeshi baina ya Tanzania na China.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images