Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mwanafunzi Afungwa Jela Miaka 20, Akutwa Akiwaonesha Wanafunzi Picha za Ngono Kupitia Simu yake ya Mkononi

$
0
0
Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) Tawi la Tabora Marick Mbega amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya kuwadhalilisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Isike mkoani hapa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, Emmanuel Ngigwana alitoa adhabu hiyo juzi baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka wakiwamo wanafunzi waliodhalilishwa.

Kabla ya kutolewa adhabu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Upendo Malulu uliieleza Mahakama kuwa Mbega alitenda makosa hayo Aprili 4 mwaka huu, kinyume na kifungu namba 138 A cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya 2002.

Wakili Malulu alidai siku hiyo katika eneo la Shule ya Msingi Isike katika Manispaa ya Tabora, mshtakiwa alikutwa akiwaonesha wanafunzi picha za ngono kupitia simu yake ya mkononi.

Alisema mbali na Mbega kuwashawishi wanafunzi hao wamshike sehemu za siri, pia alikuwa akiwachezea.

Wakili Malulu alisema baada ya kufanya upekuzi katika simu ya mshtakiwa, ilikutwa ikiwa na picha 197 za ngono na video 40 zikiwamo za watoto, watu wazima na wanyama.

Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Hakimu Ngigwana alisema mtu anayeonyesha sehemu zake za siri, kuchezea za watoto, kuonyesha picha za ngono au filamu za ngono anafanya udhalilishaji na ni kinyume cha sheria.

Alisema mtoto hana uamuzi kisheria, hivyo hawezi kuchukuliwa kwamba alikubali matendo hayo.

Hakimu Ngigwana alisema Mahakama imeona mashtaka ni mtu mzima tena Mwanafunzi wa Chuo cha Umma aliyedhaniwa kuwa na maadili kwa jamii, mstaarabu, mwenye kujali, kulinda na kutetea maslahi ya watoto, lakini alitenda kosa hilo, hivyo anastahili adhabu.

Pia, alisema mshtakiwa alipaswa kuhakikisha mtoto anakuwa vizuri kiakili, kimwili, kiroho na kisaikolojia badala yake amekwenda kinyume.

Alisema ili iwe fundisho kwake na onya kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo, atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka kumi jela kwa kila kosa.

Chanzo: Mwananchi

Lwandamina: Tupo Safi Tunawasubiri Simba

$
0
0




Lwandamina: Tupo Safi Simba Tunawasubiri
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba kutokana na mazoezi anayoendelea kuwapa vijana wake katika kambi yao iliyopo Pemba.

Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, timu hizo zitapambana katika mchezo huo kuashiria kufunguliwa kwa msimu mpya ambapo Yanga ikiwa imepiga kambi Pemba, wap­inzani wao Simba wame­jichimbia Unguja.

Lwandamina amesema wapo tayari kwa mchezo huo kwani anaona kila siku kikosi chake kinaendelea kuima­rika kutokana na wachezaji wake kufuata kile ambacho amekuwa akiwafundisha.

“Huku sisi tupo vizuri tu­naendelea na mazoezi kama kawaida, kikubwa ambacho naweza kusema ni kwamba vijana wangu kila siku wa­nazidi kuwa imara na ku­nipa matumaini ya kufanya vizuri dhidi ya Simba.

“Kwa namna siku zina­vyozidi kwenda, naona tupo tayari kwa mchezo huo, wapinzani wetu waje tu tupambane,” alisema Lwandamina.


Install App ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu Yako Kupata Habari zetu Kwa Urahisi..Bonyeza Hapa

$
0
0


Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Download App ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu Yako Kupata Habari zetu Kwa Urahisi..Bonyeza Hapa

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 


Au Kama Unayotayari Bonyeza HAPA Ku Update Uweze Kupata Ikiwa na Muonekano Mpya

Mtatiro Yamemfika Hapa...Adai ni Bora Kufanya Kazi na CCM Kuliko Lipumba

$
0
0
Mtatiro Yamemfika Hapa...Adai ni Bora Kufanya Kazi na CCM Kuliko Lipumba
Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amefunguka na kujibu hoja za baadhi ya watu ambao wanataka CUF kukubaliana na Professa Lipumba kwa kuwa Mwenyekiti huyo ameshika makali kutokana na vyombo mbalimbali vya serikali kumtambua.

Julius Mtatiro ambaye sasa yupo nchini Marekani alipokwenda kimasomo amesema hilo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema ni jambo ambalo halitawezekana wao kukubali yaishe na Profesa Lipumba na kusema wataendelea na harakati zao kuhakikisha haki yao inapatikana.

"Nasoma maoni ya baadhi ya watanzania kuja kwetu, kwamba kwa sababu serikali, dola, CCM, polisi, bunge, NEC, RITA, na Msajili wa Vyama vya Siasa wameshikamana kumuunga mkono Lipumba, na kwa hiyo ati Lipumba ameshikilia mpini na chama kimeshikilia makali kwa nini tusikubali yaishe? Lipumba apewe kila kitu...hadi roho zetu, lakini misingi yetu, misimamo yetu, umoja wetu na mshikamano wetu, hawezi kupewa. Hizi ndizo silaha zetu na niwaambie kuwa zina faida ya muda mrefu kuliko zile anazozitizama msaliti" alisema Mtatiro
Aidha Mtatiro anasema kuwa ni rahisi sana wao kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Profesa Lipumba

"Ni mara kumi kumsamehe jirani yako aliyembaka mwanao, kuliko kumsamehe baba yako mzazi aliyembaka mwanao. Adui wa ndani, ni hatari zaidi kuliko adui wa nje. CCM ni adui bora kuliko Lipumba na kwa hiyo ni rahisi sana kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Lipumba" alisisitiza Mtatiro

Manji Ashindwa Kufika Mahakamani Katika Kesi Yake ya Uhujumu Uchumi

$
0
0
Manji Ashindwa Kufika Mahakamani  Katika Kesi Yake ya Uhujumu Uchumi
Mfanyabiashara Yusuf Manji leo ameshindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya uhujumu uchumi kwa sababu za kiafya.

Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati shauri lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo alidai kuwa amepata taarifa kutoka kwa Askari Magereza kwamba Manji anaumwa na amepewa (AD) ya siku mbili.

Licha ya Yusuf Manji kutofika Mahakamani kwa sababu za kiafya, washtakiwa wenzake Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere walifika ambapo baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi August 25, 2017

Kutana Na Mnajimu wa Nyota na Mtaalam wa Tiba Asili Africa na Dunia kwa Ujumla Kutoka ANJUAN COMORO AL_WATWAN MAFUSHO sasa yupo Tanzania

$
0
0
Kutana Na Mnajimu wa Nyota na Mtaalam wa Tiba Asili Africa na Dunia kwa Ujumla Kutoka ANJUAN COMORO AL_WATWAN MAFUSHO sasa yupo East Africa (Atakuwa Nairobi,Mombasa,Uganda,Burundi,Rwanda na Sehemu Yoyote Atakayo hitajika.. Tanzania Atazunguka Mikoa Yote..)

AL_WATWAN MAFUSHO Ni Mtafiti wa Dawa za Mitishamba na ana uzoefu wa zaidi ya Miaka 18 katika kutoa Huduma zake.. Amesha toa Huduma zaidi ya Nchi 23 Duniani..
AL_WATWAN MAFUSHO Bado anaendelea Kupokea Salam na Shukrani nyingi kwa wale wote waliofanikiwa baada ya kupata HUDUMA na wale wanao Endelea Na TIBA MBALIMBALI..
      Anatibu kwa Kutumia Dawa za Asili ya Africa, Dawa za Kiarabu, Majini na QUR-AN Ukiwa Nchi yoyote...

Kwa Matatizo ya Fuatayo..
•Love spell
•Money spell casting
•Traditional Healer
•Protection Rituals
•Marriage Spells(to heal marriage problems and restore Affection
•Traditional bad luck Removal
•To Prevent divorce and bind lovers together

 MAGONJWA kama > Miguu kuwaka Moto na kufa Ganzi,Kuvimba tumbo,Kisukari, Ngiri ya ndani na Ngiri ya Nje(Busha) Chango kwa Kina Mama,Kifungua Kizazi kwa waliofungwa kishirikina)..Ulijari(Nguvu za kiume?
MAPENZI.Kumrudisha Mpenzi ndani ya Saa  12 tu.. Kumtuliza(Limbwata) Akusikilize na Akupatie chochote unacho hitaji kwa Wakati. Hutuliza wana Ndoa na na Kuzuia Talaka.. Kama Mpenzi wako Anaishi na Mtu mwingine Anao Uweza wa Kusambalatisha mahusiano yao ndani ya Nusu saa tuu(Mfarakano)...

MAFANIKIO.. Mali Bila Masharti, Bahati kwa Wachimba madini.. MAGIC WALLET, PETE ya Bahati, KUSHINDA BAHATI NASIBU na Kusafisha NYOTA(Nuksi Mikosi).. Umaarufu, Heshima mahala pa Kazi,Cheo kazini. Mafuta maalum Yenye Nguvu ya Ziada..
(Amesaidia Watu maarufu, Wachungaji na Wafanya Biashara wengi Duniani)
KINGA..Huzuia Kabisa Chuma Ulete na Kukupa Kinga ya Mwili na Biashara na Kujilinda na mali zako.Humaliza kabisa Kesi ndani ya siku 12 tu(Zindiko) nk..
PIA HUMALIZA KAZI ZILIZOACHWA AU KUSHINDIKANA....
Acha Kuhangaika Njoo Umaliziwe Tiba yako

AL_WATWAN MAFUSHO

Piga Simu +255 759 084 996

Lulu Diva Amesema Anaishi Maisha Yake Aigizi Atoa kichambo Kwa Watu Wanaomuongelea Vibaya

$
0
0

Lulu Diva Amesema Anaishi Maisha Yake Aigizi Atoa kichambo Kwa Watu Wanaomuongelea Vibaya
Msanii wa bongo fleva  Lulu Diva ameibuka na kuwachamba watu wanaomuongelea vibaya  juu ya vitu vya gharama na magari anayotumia kuwa ni ya kuazima kwa kusema kwamba wengi wanaomzungumzia wana maisha duni .

 Lulu amesema  yeye ni mtafutaji hivyo siku zote anafanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba anaishi maisha anayohitaji na siyo kuigiza maisha kama jinsi watu wanavyomfikiria.
'Niseme tu ukweli Lulu anaishi maisha  yake halisi na kila kitu ambacho unakiona kwa Lulu Diva ni mali yangu sina tabia za kuazima vitu, mimi ni mtafutaji na natumia mda wangu mwingi kuhangaika kutafuta vya kwangu sipendi kuigiza maisha"aliongea Lulu

Hata hivyo Lulu aliendelea kusema kuwa kwa upande wa magari kuna wakati natumia magari ya menejiment yangu ambayo ni kama magari ya office ninayofanyia kazi na sioni tatizo na hilo kwa kuwa mimi nafanya kazi na pia ni mmiliki wa baadhi ya magari ninayotumia.
Pia Lulu aliendelea kusema kuwa hajali maneno ya watu wanayoyaongeaa juu yake kwani anachikifanya ni kuhakikisha anawaziba midomo wote wanaomsema vibaya kuwa anaanzima vya watu na waamini kile anachokifanya maishani mwake.
Mtazame hapa chini Lulu akifunguka zaidi

Maskini Watoto Watatu wa Lucky Vicent Waliowasili Leo Wawaliza Watanzania Walioenda Kuwapokea Uwanja wa Ndege wa (KIA)

$
0
0

Maskini Watoto Watatu  wa Lucky Vicent Waliowasili Leo Wawaliza Watanzania Walioenda Kuwapokea Uwanja wa Ndege wa (KIA)
Wazazi, watoto na watu mbali mbali wameshindwa kujizuia na kumwaga chozi walipokuwa wakiwapokea watoto Sadia Ismail, Doreen Eribariki na Wilson Tarimo, ambao wamerejea rasmi nchini wakitokea nchini Marekani walikokuwa wakipatiwa matibabu.


Watoto hao ambao ni manusura wa ajali iliyoua takriban wanafunzi 32 wa shule ya msingi Lucky Vicent, wamepokelewa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Anna Mghwira, Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, wazazi na wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent, waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Watu mbali mbali walihudhuria uwanjani hapo wakiwa na mashada ya maua kuwalaki huku kukiwa na burudani mbali mbali kutoka kwa sanii Mercy Masika wa Kenya, Angel Bernad wa Tanzania na Kwaya ya Shangwe kutoka jijini Arusha.

Shirika la Samaritan Purse la Marekani lilijitolea kusaidia watoto hao kuanzia usafiri na gharama za matibabu kwa muda wote ambao walikuwa nchini humo wakitibiwa, katika Hospitali ya Sioux City tangu mwezi Mei 15, kufuatia majeraha makubwa kwenye ajali kubwa waliyoipata tarehe 6 Mei 2017, wakitokea hospitali ya Mt. Meru Arusha.

Kimenuka Tayari Dimond Atupa Dongo kwa Mobetto Basi Hali si Hali

$
0
0




Kimenuka Tayari Dimond Atupa Dongo kwa Mobetto Basi Hali si Hali
Rais wa WCB, Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz ametema cheche za mwaka mtandaoni huku moja kwa moja wadau wa mambo wakilihusisha tukio hilo na kitendo cha mwanamitindo, Hamisa Mobetto ambaye amejifungua mtoto wa kiume Agusti 8 mwaka huu na kumpachika jina la Naseeb Abdul.

Diamond alimtumia Mobetto katika video ya wimbo wake, Salome uliotoka mwezi Disemba mwaka huu.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Eneka, ameonyesha kuchukizwa na baadhi ya mambo yanayoendelea.

“BITCH IS DYING FOR FAME,” alitweet Diamond.

Wadau wa mambo wanadai kauli hiyo imekuja baada ya Mobetto kumpatia mtoto wake jina Naseeb Abdul hali ambayo imewafanya watu wengi watambue kwamba mtoto huyo aliyejifungua hivi karibuni ni wa Diamond ambaye kwa sasa ni baba wa watoto wawili aliyozaa na Zari The Bosslady.


Diamond hajawahi kutoa kauli yoyote kuhusiana na tukio hilo licha ya mama yake pamoja na dada yake Asma kuonekana mara kadhaa katika hospitali aliyojifungua mwanamitindo huyo.

Mashabiki katika mitandao ya kijamii wamekuwa na maoni tofauti juu ya Diamond Platnumz huku wengi wakimshauri muimbaji huyo kumkubali mtoto kwa madai Mobetto ni mtu mzima na anatambua kile anachokifanya.

Kwa upande wa Mobetto huyo ni mtoto wake wa pili ambapo wa kwanza alizaa na Mkurugenzi wa EFM, Majay.


Mambo Yazidi Kuwa Magumu kwa Manji Kampuni Yake Kufutiwa Leseni na TCRA

$
0
0

Mambo Yazidi Kuwa Magumu kwa Manji Kampuni Yake Kufutiwa Leseni na TCRA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Mycell inayomilikiwa na Quality Group Limited (QGL) ambayo imekuwa ikiongozwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Yussuf Manji.


Kwa mujibu wa sheria, TCRA iliyoanzishwa mwaka 2003 ina jukumu la kusimamia, kutoa na kufuta leseni za mawasiliano kwa kampuni yoyote ambayo imeshindwa kutekeleza majukumu iliyoyabainisha.

“Kampuni ya Mycell imeshindwa kurekebisha ukiukwaji wa masharti ya leseni,” inasomeka taarifa iliyotolewa na kuwekwa kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.

Kutokana na upungufu huo, “TCRA inauarifu umma kuhusu kusudio la kufuta leseni za Mycell za kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao na kutumia masafa ya mawasiliano.”

Kuonyesha juhudi ilizochukua kabla ya uamuzi huo, TCRA imesema Januari 27, 2016 ilitoa amri ya utekelezaji kwa kampuni hiyo kwa kukiuka masharti ya leseni walizopewa na kushindwa kutoa huduma kinyume cha Kifungu 21 (a) na (b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoca) ya mwaka 2010.

Hata hivyo, Mycell haimo kwenye orodha ya kampuni zilizopewa leseni na TCRA ambazo zimo kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.

Mamlaka hiyo imeeleza kwenye taarifa yake ya kusudio la kuifuta Mycell kuwa iliipa kampuni hiyo leseni nne tofauti Novemba 21, 2008.

Inafafanua kuwa leseni hizo ni ya kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao wa mawasiliano na kutumia masafa ya mawasiliano.

Kwenye ujumbe wake alioutoa Oktoba, 2011 wakati Quality Group ikitimiza miaka 35 tangu ianzishwe nchini, mwenyekiti wake wakati huo, Yusuf Manji alitabainisha vipaumbele vya utekelezaji walivyonavyo.

“Mycell inatekeleza mpango biashara unaoiruhusu kukodisha masafa iliyopewa na TCRA kwa kampuni ya nje yenye uwezo na uzoefu mkubwa. Inatarajia kujenga miundombinu imara itakayofanikisha miradi mbalimbali,” alisema Manji.

Alisema mpango huo unatokana na fursa kemkem zilizopo kwenye sekta ya mawasiliano nchini hasa kwa kuzingatia njia za kawaida za kufikishiana ujumbe ambazo zimekuwa hazikidhi mahitaji yaliyopo kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia hasa ya habari na mawasiliano (Tehama).

“Sekta hii ina fursa nyingi kwa kampuni zenye teknolojia ya kisasa kuwekeza na kukua. QGL inaona kwamba kuna haja ya kuwekeza kwenye miundombinu na kuziruhusu kampuni za mawasiliano kuongeza ufanisi. Gharama za kupiga simu na data zipo juu nchini ikilinganishwa na ilivyo kwa nchi za Asia zinazonufaika na Tehama kwa kiasi kikubwa,” alisema Manji kwenye ujumbe wake wa mwaka 2011.

Mwaka 1997, Manji alianza kuiongoza QGL akihudumu kama ofisa mtendaji mkuu kabla ya baadaye kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kundi hilo, nafasi aliyojiuzulu lakini baadaye akarejea tena na kuendelea kuiongoza

Msichana Aliyepigwa na Mke wa Mugabe Aobwa Kuyamaliza nje ya Mahakama

$
0
0
Msichana Aliyepigwa na Mke wa  Mugabe Aobwa Kuyamaliza nje ya Mahakama
Familia ya mwanamke aliyedaiwa kushambuliwa na bi Grace Mugabe imedaiwa kufuatwa na kuombwa na mtu asiyejulkani kukubali fedha kama fidia ya kutupilia mbali kesi hiyo , wakili wake amesema.

Familia haitaki kufanya hivyo, Gerrie Nel alisema.Walisema tuzungumze na tuwache kesi hii, lakini hakuna kiwango cha fedha kilichotajwa ,aliongezea.
Bwana Nel anajulikana kwa jina la utani kama ''the Pitbull''. Alifanikiwa kumshtaki mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius kwa mauaji.

Wakati huohuo katika mahojiano marefu ya simu na bi Gabriella Engels ambaye amemtuhumu bi Grace Mugabe kwa kumpiga, Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani alitulia na kuonekana kuwa mtu aliyekuwa na wasiwasi mwingi mara kwa mara.

Akielezea tukio hilo bi Engels mwenye umri wa miaka 20 alisema kuwa yeye na watu wengine wanne, wawili wakiwa wana wa kiume wa rais Mugabe na bi Grace Mugabe walikuwa wakinywa vinywaji siku ya Jumapili usiku katika chumba kimoja cha hoteli mjini Sandton, makaazi ya kifahari yaliopo Johannesburg.

Baadaye alienda katika chumba chengine na bi Mugabe akamfuata akiwatafuta wanawe.
Bi Mugabe alikuwa ameshikilia waya wa umeme mkononi mwake....alinizuia na kuanza kunipiga .
Nilijiangusha chini na kuanza kubingirika ili kukwepa kichapo hicho, na ni hapo aliponipiga na waya hiyo. Na nakumbuka nikiwa katika sakafu huku nikiwa nimejaa damu usoni na shingoni, bi Engels alidai.

Nilikuwa nikifikiria nitoke katika chumba hicho kabla ya mwanamke huyu kuniuwa.
Watu waliokuwa katika chumba hicho ni walinzi wake na walikuwa wamesimama nyuma yake huku akitupiga.
Tulimsihi kuwacha kufanya hivyo ,lakini hakutaka kusikia aliendelea kutupiga...alitupiga akiwa na chuki nyingi .

Hadi leo marafiki zangu sielewi kwa nini mwanamke huyu alitushambulia vile bila ya sababu yoyote, Engels aliongezea.
kabla nitambue alikuwa bi Mugabe, nilijua nilifaa kumshtaki kwa kunishambulia kwa kuwa nilijeruhiwa vibaya
Sikujua yeye ni nani. na nilipojua yeye ni nani, sikutaka kumshtaki .. lakini mamangu akanisukuma kuwasilisha mashtaka hayo mahakamani, kwa sababu aliniambia: Kile mwanamke huyu alichotenda sio sawa.

Hatuwezi kuruhusu kukwepa kitendo alichofanya, alisema bi Engels.
Mwanamke huyo wa miaka 20 alisema: Ningefurahia sana iwapo angepelekwa jela.. hilo ndio lengo langu kwa sasa.
Bi Mugabe hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

Mkapa Kushuhudia Kuapishwa Kwa Kenyatta

$
0
0

Mkapa Kushuhudia Kuapishwa Kwa Kenyatta
Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wa Afrika wanaohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame aliyeshinda katika uchaguzi uliofanyika Agosti 4.

Mkapa ambaye ujumbe wake uko nchini Burundi kwa ajili ya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo katika jitihada za kusuluhisha mzozo wa kisiasa aliwasili jana mjini Kigali akiwa miongoni mwa viongozi zaidi 20 ambao wanahudhuria sherehe hizo.

Sherehe hizo ambazo zinatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali zinafanyika katika Uwanja wa Taifa wa Amahoro. Rais Kagame atakuwa anaanza muhula wa kwanza wa miaka saba tangu taifa hilo lilipofanyia marekebisho katiba yake.

Miongoni mwa viongozi wa Afrika wanaohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera ambaye alikuwa wa kwanza kuwasili nchini humo.

Wengine ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenya,  Rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh, Rais wa  Niger, Mahamadou Issoufou, Rais wa Senegal, Macky Sally, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Rais wa Congo Brazaville,  Sassou Nguesso

       

Mr. Nice Akili Kukubarika Kenya na si Tanzania

$
0
0
.

Mr. Nice Akili Kukubarika Kenya na si Tanzania
MWANAMUZIKI wa miondoko maarufu kwa jina la Tanzania, Kenya na Uganda (Takeu), ambaye alijizolea umaarufu miaka ya 2000 na baadaye kupotea kidogo kutokana na sababu za hapa na pale, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ amesema kuwa anaamini kuna baadhi ya Watanzania wenzake hawampendi.

Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa amerejea upya katika gemu, amefunguka mambo mengi katika makala haya:

Showbiz: Mashabiki Bongo walikumisi kwa muda mrefu wangependa kujua ulikuwa wapi na unafanya nini kwa sasa?

Mr Nice: Maisha yangu kwa sasa yapo Kenya, huko nina zaidi ya miaka mitatu nikifanya muziki wangu, nimeamua kuhamishia makazi huko kwa sababu kule wenzetu mambo ya burudani wako mbali sana hivyo kazi zinapatikana kwa wingi tofauti na Bongo.

Showbiz: Vipi kuhusu mazingira ya huko hayakukupa shida? Mr Nice: Hapana halafu unajua maisha yangu ya muziki yamekuwa ya kwenda hapa na pale nchi mbalimbali hivyo hiyo haikunisumbua.

Showbiz: Unazungumziaje habari zilizokuwa zikizagaa kuhusu kifo chako?

Mr Nice: Ni chuki tu za baadhi ya Watanzania wenzangu na ninashindwa kuelewa kwa nini wananichukia kiasi hiki wakati nchi nyingine wananiona lulu? Kwa nini wananifanyia hivyo wakati Kenya naishi kama mfalme maana hata nikiambiwa nije kufanya shoo Tanzania, najifikiria mara mbili mbili kwa sababu naona watu wangu wamenitenga.

Showbiz: Kuna siku ulikuwa ukiimba wimbo wako wa Mama huku ukibubujikwa na machozi na kusema unaumia watu wanasema una ugonjwa wa Ukimwi, unazungumziaje hilo?

Mr Nice: Ni kweli watu walinipakazia hivyo na wimbo ule wa Mama unaniliza kwa sababu najua mama yangu angekuwepo angewakemea waache kuzungumza maneno hayo maana mastaa wenye mama zao wakisakamwa tu, mama zao wanaibuka kukanusha.

Showbiz: Kwa nini unasema baadhi ya Watanzania wanakuchukia? Mr Nice: Kwa sababu wamekuwa ni watu wa kunidharau, kunidhihaki kwa sababu heshima ambayo ningeipata hapa nyumbani naenda kuipata nchi nyingine.

Showbiz: Mashabiki wako wangependa kufahamu huko Kenya upo na familia yako?

Mr Nice: Kenya, nafanya kazi tu, familia yangu yote ipo Tanzania, lakini sijaoa na wala sitegemei kufanya hivyo kwa sababu tayari nina watoto wawili ambao nataka kuwalea bila karaha ya mama wa kambo.

Showbiz: Najua muigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ huko nyuma alikuwa ni mpenzi wako vipi unazungumziaje kuhusu matatizo yaliompata?

Mr Nice: Namuombea ila kwa upande wa Watanzania, waache kushabikia mtu anapopatwa na janga na kuanguka. Wamuombee na waache manenomaneno.

Showbiz: Ni faida gani umeipata mpaka sasa kutokana na muziki?

Mr Nice: Nyingi sana, kwanza nina mijengo ya maana minne, nina usafiri wangu na nina mashamba kutokana na muziki huohuo na miradi yangu mingine mingi.

Nawal Aamua Kufuta Tattoo ya Nuh Mziwanda

$
0
0


Nawal  Aamua Kufuta Tattoo ya Nuh Mziwanda
Baada ya Jini Mkatakamba kuipitia ndoa ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda, aliyekuwa mkewe Nawal amefunguka kuwa yupo katika harakati za kuifuta tattoo ya Nuh aliyoichora mkononi mwake.

Nawal ambaye baada ya kuachana na mzazi mwenziye Nuh Mziwanda, ameolewa tena na mwanaume anayefahamika kwa jina la Masoud, amefunguka Kwa kusema; “Nitaifuta tattoo ya Nuh Mziwanda, mume wangu ana fedha, atanipa ili niende kuifuta.”


Baada ya kutemana na Shilole, Nuh Mziwanda aliingia katika uhusiano wa kimapenzi na Nawal  ambapo Novemba, 2016,  walifanikiwa kufunga ndoa na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Anyaghire.

Hivi karibuni ndoa yao ilivunjika baada ya kupitiwa na jini mkatakamba, kwa kile kinachodaiwa kuwa Nuh amerudi katika dini yake ya Kikristo na kwa kufanya hivyo ni kama amemkana mkewe aliyemuoa kwa dini ya Kiislamu, ambapo baada ya kutengana kwao, Nawal akaolewa tena na mwanaume anayefahamika kwa jina moja la Masoud.


Rais Magufuli Afanya Uteuzi Mpya wa Viongozi Watatu

$
0
0

Rais Magufuli  Afanya Uteuzi Mpya wa Viongozi Watatu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi.


Taarifa rasmi iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es salaam inasema Rais Magufuli amemteua Prof. Evaristo Liwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, kuchukua nafasi ya Prof. Idrissa B. Mshoro ambaye amestaafu.

Wakati huo huo Rais Magufuli amewateua Prof. Abdulkarim Khamis Mruma kuwa Mwenyekiti wa kampuni ya kuhifadhi mafuta (TIPER), ambaye kabla alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Jiologia Tanzania, na Prof. Joseph Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania LTD.
Prof. Buchweshaija alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).

Ali Kiba Kuja na Ngoma Tatu Baada ya Kuwapoza Mashabiki Zake

$
0
0

Ali Kiba Kuja na Ngoma Tatu Baada ya Kuwapoza Mashabiki Zake
Msanii Alikiba ambaye yupo kimya kwa muda mrefu ameamua kukata kiu ya mashabiki wake na kumaliza hasira zao kwa kushusha ngoma tatu mfululizo pindi atakaporejea Tanzania kutokea nchini Marekani alipokwenda kwa ajili ya kufanya show.


Siku mbili zilizopita Alikiba kupitia mitandao yake ya kijamii alianza kuweka post ambayo ilionyesha ni ishara ya ujio wake mpya baada ya kuweka 'post' iliyokuwa na jina la 'Kipusa' na kuaindikia maneno kuwa "Wananiita Kipusa' baada ya siku moja aliweka nyingine iliyokuwa inasema 'they call me a heartbreaker" hali ambayo ilianza kuwachanganya mashabiki wake wengine wakidhani kuwa ni mistari kutoka kwenye wimbo huo.
Lakini siku moja mbele aliweka post nyingine inayosema 'Pasua Kichwa' hali ambayo ilizidi kuongeza maswali mengi kwa mashabiki wake, lakini mdogo wake na Alikiba anayefahamika kwa jina la Zabibu ameweka wazi kaka yake Alikiba ataachia kazi tatu kwa mpigo na kuwataka mashabiki wakae mkao wa kula pindi atakaporudi kutoka nchini Marekani ataachia kazi hizo.

Alikiba siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Agosti atakuwa akikiwasha nchini Marekani katika mji wa New York ambapo atakuwa na wasanii wengine kibao kutoka Afrika wakiwepo P Square, 2 Baba, Tiwa Savage pamoja na  Cassper Nyovest

Zaidi ya Marais 20 Kutoka Mataifa ya Afrika Kushuhudia Kuapishwa kwa Kagame Leo

$
0
0
Zaidi ya Marais 20 Kutoka Mataifa ya Afrika Kushuhudia Kuapishwa kwa Kagame Leo
Rais wa Rwanda Paul Kagame anaapishwa leo kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu wa miaka 7
Hii ni baada ya kushinda uchaguzi wiki mbili zilizopita kwa kupata asilimia 98 ya kura.
Sherehe za kula kiapo zinafanyika kwenye uwanja wa taifa Amahoro mjini Kigali.
zaidi ya marais 20 kutoka mataifa ya Afrika wanahudhuria sherehe hizo.
Miongoni mwao ni rais wa Sudan Omar Al Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.

Rwanda siyo mwanachama wa mahakama hiyo.
Katika uchaguzi wagombeaji wengine 2 Philippe Mpayimana na Frank Habineza wa chama cha Green waliambulia asilimia 1 jumla ya kura zao.

Uchaguzi huo ulikosolewa na baadhi ya mataifa kama Marekani ambayo ilisema hali ya siasa nchini Rwanda inatoa fursa tu kwa mtu mmoja pekee kwendelea kuiongoza nchi hiyo.

Lissu Amkumbusha IGP Simon Sirro Kuwapa Polisi Uweledi Mzuri

$
0
0

Lissu Amkumbusha IGP Simon Sirro Kuwapa Polisi Uweledi Mzuri
Rais wa chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amefunguka kwa kuwataka wakuu wa vyombo vya usalama nchini wawaelekeze watumishi wao kazi za kufanya na siyo kupoteza muda na rasilimali za nchi.

Lissu amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliyoitishwa na CHADEMA wenye lengo la kuzungumzia namna nchi inavyoenda kufilisika na ndipo alipomtaka Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Kamanda Modestus Francis Kipilimba na Mkuu wa Majeshi Tanzania, IGP Simon Sirro kuwapa uweledi mzuri wa kufanya kazi vijana wao.
"Wale vijana wenu ambao mmekuwa mkiwatuma wanifuate kila nilipo kwa kipindi cha wiki tatu sasa, jana nimefanikiwa kuwakaba kanisani St. Peters. Hivyo wakubwa hawa wa vyombo vya usalama wawaelekeze watumishi wao namna ya kutumia muda na rasimali ya nchi hii", alisema Lissu.
Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "Wafanye kazi ya kupambana na wahalifu na siyo kupoteza muda wao na pesa za walipa kodi kuhangaika na raia ambao wanatimiza uhuru wao wa kuiwajibisha serikali iliyoko madarakani".
Kwa upande mwingine, Lissu amemtaka Kamanda Sirro pamoja na Kamanda Kipilimba kupamba na wahalifu na wamuachie yeye kazi ya kuwajibisha waliyoko madarakani kwa mujibu wa sheria za nchi.

Lipumba Akwaa Kisiki Mahakamani Jaji Akataa Maombi Yake

$
0
0

Lipumba Akwaa Kisiki Mahakamani Jaji Akataa Maombi Yake
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake wamekwama mahakamani leo baada ya Jaji Ndyansobera kukataa maombi ya Profesa Lipumba na kundi lake.

Jaji Ndyansobera amekataa kufuta kesi Namba 28/2017 kama ilivyoombwa na Lipumba ili wapate Ruzuku ya Chama  Cha Wananchi wa CUF inayofikia shilingi billion moja na million mia nne toka Julai mwaka jana.

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Mbarala Maharagande amefunguka na kusema kufuatia maamuzi haya ya mahakama hivyo hakuna pesa ambayo Profesa Lipumba anaweza kuchukua hata shilingi moja.

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images