Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live

TID: Sijarudia Madawa Kwanini Watu Wanizushie Huo ni Uchochezi

0
0


TID: Sijarudia Madawa Kwanini Watu Wanizushie Huo ni Uchochezi
MKONGWE kunako Muziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ amewajia juu wanaoendelea kumhusisha kurudia matumizi ya madawa ya kulevya kwa kusema kuwa hakuna kitu kama hicho na wanaoeneza taarifa hizo wana lengo la kumchafua tu.

TID ambaye kipindi kifupi cha nyuma aliwahi kukiri kutumia madawa alisema, alishatangaza ameacha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda hivyo hawezi kurudi nyuma akatumia tena hivyo vitu.

“Sijarudia jamani, hayo mambo ni ya uchochezi hakuna la zaidi, nimeshaacha hayo mambo kwa nini watu wanizushie, sijarudia madawa,  cha muhimu ni kujua mikakati ya kazi zangu kimuziki ndio ninachowaza si hayo mambo. “Sina cha kuwashauri wasanii wanaoendelea kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, sababu nilishaongea mengi tangu awali nilipotangaza nimeacha,” aliongeza TID.



Amba Lulu Atoa Sababu Inayompelekea Kujiacha Mitandaoni

0
0




Amba Lulu Atoa Sababu Inayompelekea Kujiacha Mitandaoni
Msanii wa muziki na video vixen Bongo, Amber Lulu amedai kuwa familia yake haifuatilii mitandao hivyo yupo free kujiachia kwa kuweka picha anazotaka.



Video Vixen huyo ambaye ameingia kwenye muziki wa Bongo Flava na kutoa ngoma ‘Watokoma’ ambayo alimshirikisha Country Boy, ameiambia Leo Tena ya Clouds Fm kuwa hata familia ikiona picha zake hamna tatizo.

“Familia yangu hawafatilii mitandao ya kijamii na hata wakiona picha zangu kwa sasa wanaelewa nini nafanya. Siyo kila kitu tunachoposti kwenye mitandao ya kijamii ndivyo maisha yetu tunayoishi” amesema Amber Lulu.

Kabla ya kuingia katika muziki na kutangaza kuachana na u-video vixen, Amber Lulu alishatokea kwenye video kama Inde ya Harmonize na Dully Sykes, Usimsahau Mchizi ya Roma na Moni n.k.


Matokeo Simba vs Yanga Kujulikana Kibarua cha Omog

0
0




Matokeo Simba  vs Yanga Kujulikana Kibarua cha Omog
Kufuatia matokeo mabaya waliyopata mabingwa wa kombe la FA Simba SC dhidi ya Mlandege ya visiwani Zanzibar mchezo wa kirafiki uliyopigwa usiku wa jana, mashabiki wa klabu hiyo wamemtaka kocha mkuu mcameroon, Joseph Omog atimuliwe mapema.



Simba ambayo imeweka kambi viziwani Zanzibar kwaajili ya kujiwinda na mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya hasimu wake Yanga SC mchezo unaotarajiwa kupigwa Agosti 23 mwaka huu ilikubali kutoka sare tasa ya bila kufungana na Mlandege  jambo ambalo halikutarajiwa na wengi kutokana na usajili waliyoufanya msimu huu hivyo kupelekea wapenzi watimu hiyo kumtolea uvivu kocha huyo.



Mashabiki wa timu hiyo wamesikika akisema “Kocha hatumtaki tena hatufai aende zake kwanza hata alivyokuwa Azam yeye ushindi wake ulikuwa mwembamba sare ndiyo nyingi hajui kupanga kikosi, asepe mapema ila ngoja mechi ya Yanga iishe tukitoa sare out, tukifungwa out, tukishinda moja out, hatufai aje Ndailagije muone moto wake,”.






Uamuzi Pingamizi Kesi ya Wema Kutolewa Agosti 31

0
0

         
Uamuzi Pingamizi Kesi ya Wema Kutolewa Agosti 31
Uamuzi wa kupokea au kutopokea   kielelezo cha ushahidi cha msokoto mmoja wa bangi na vipisi viwili vya bangi katika kesi inayomkabili mlimbwende wa Tanzania 2006, Wema Sepetu utatolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwisho wa mwezi huu.

Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amesema uamuzi huo ulipaswa autoe leo, lakini bado kuna tafiti anazifanya, hajakamilisha hivyo aliuahirisha hadi Agosti 31,2017.

Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa uamuzi huo shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka ataendelea kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Septemba 12 na 13, 2017.

Uamuzi huo umefuatia baada ya shahidi huyo ambaye ni mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima ambaye alipima msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi, kuomba kuvitoa mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.

 Mulima kupitia wakili wa Serikali, Costantine Kakula aliomba kuitoa bahasha iliyofungwa juu yenye muhuri, saini ya shahidi huyo na namba ya maabara 291 ya 2017  ambayo ndani yake kulikuwa na msokoto na vipisi viwili vya bangi mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.

Hata hivyo wakili wa Wema, Tundu Lissu alipinga kisipokewe kama kielelezo cha ushahidi kwa sababu ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.

Kutokana na hoja hizo, Hakimu Simba alisema Agosti 18, 2017 atatoa uamuzi juu ya hoja hizo na kesi hiyo pia inaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.


Dogo Janja Afunguka Namna Anavyomzimikia Irene Uwoya

0
0






Dogo Janja Afunguka Namna Anavyomzimikia Irene Uwoya
 Mwimbaji staa wa Bongofleva Dogo Janja ambaye amefunguka kuhusu maisha yake, muziki wake na namna walivyotofautiana na Producer P Funk Majani mpaka akaacha viatu studio za Bongo Records.

Mbali na hayo Dogo Janja kazungumzia pia kuhusu kudaiwa kuwa mapenzini na mwigizaji Irene Uwoya.

”Mtu kama Irene Uwoya ni namu-admire, nampenda lakini sipo naye kama vile watu wanavyofikiria. Love yangu kwa Irene Uwoya haifichiki ila suala la kuwa kwenye mahusiano naye mimi sina. Nimeshawahi kuwa na mtu aliyenizidi umri na nachezaga na wa mwaka 1987 au kuivuta 89.

“Anakuwa amenizidi miaka kama sita au mitano na nakuwa sawa kabisa japo huwezi nikuta nikitembea na mwanamke siwezi kabisa.” – Dogo Janja








Mbaroni kwa Kumpa Mtoto Kinyesi cha Mbuzi

0
0
Mbaroni kwa Kumpa Mtoto Kinyesi cha Mbuzi

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza, linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Chakechake, Sospeter Rajabu (42), kwa kosa la kumpaka kinyesi  cha mbuzi kwenye majeraha yaliyotokana kuungua   moto  mtoto wake, Neema Sospeter (10) mwanafunzi wa darasa la  kwanza na kusababisha hali yake kuwa mbaya.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi jana, ilisema mtuhumiwa  alikamatwa juzi  saa 10:30 jioni  Mtaa wa Chakechake  wilayani  Nyamagana.

Alisema Sospeter anatuhumiwa  kumpaka mavi ya mbuzi  mtoto wake kwenye majeraha ya moto aliyoungua maeneo ya mapaja ya miguu yote miwili kwa muda wa wiki mbili na kusababisha  majeruhi kuwa na hali mbaya kiafya ambapo  wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo, askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi maeneo hayo na kufanikiwa kumkuta mtoto akiwa kwenye hali mbaya na  kushirikiana na wananchi kumkimbiza hospitali na  kumkamata baba wa mtoto.

“Huyu mtoto aliungua moto Agosti 4, mwaka huu saa 1:45 usiku  Mtaa wa Kitangiri wilayani Iilemela ambapo alikuwa akiishi na mama yake kwani wazazi wake walitengana kwa muda mrefu, inadaiwa alimwagikiwa na mafuta ya taa alipokuwa akiweka kwenye  kibatari na kuwasha  na njiti ya kibiriti na  moto kulilipuka kisha  kumuunguza.

“Baada ya mama yake  kukosa fedha za matibabu, aliamua kumpeleka  kwa baba yake Mtaa wa Chakechake alipokua akiishi na mke mwingine ili amsaidie mtoto apate matibabu, lakini baada ya mtoto kufikishwa kwa baba yake hakupelekwa hospitali na  badala yake alikuwa akipakwa mavi ya mbuzi na kusababisha  hali yake kuzidi kuwa mbaya,” alisema Kamanda Msangi.

Alisema polisi wapo kwenye upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa dhidi ya ukatili aliyokuwa akimtendea mwanae pindi uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani, majeruhi amelazwa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza  Sekou Toure akiendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Waziri Nchemba Atembelea Shule Mbalimbali na Kukuta Ubovu wa Miundombinu

0
0

Waziri Nchemba Atembelea Shule Mbalimbali na Kukuta Ubovu wa Miundombinu
Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba ameendelea na ziara yake kutembela kila Kijiji katika kila Kata zilizopo Jimboni mwake kuzungumza na wapiga kura na kukagua shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Leo ametembela Kijiji cha Ujungu katika Kata ya Mekente na kukuta ubovu wa miundombinu katika Shule ya Msingi Ujungu katika kijiji hicho huku Walimu wakiishi katika mazingira magumu ambapo aliamua kulibeba jukumu la kuboresha miundombinu akiahidi kulishughulikia mapema iwezekanavyo.

Waziri Nchemba amesema “Kwa kazi nzuri mnayoifanya naahidi leoleo kwa kushirikiana na marafiki zangu tutatengeneza mkaakti wa kushughulikia ukarabati wa madarasa pamoja na nyumba za walimu, walimu tisa kukaa kwenye nyumba tatu hesabu hii haina uwiano kabisa”

“Hii ni hatua moja kubwa sana na baada ya miaka 15,20 utaona Mbunge anatoka huku, kwasababu hata kijijini nilipotoka walikuwa wanapaita kijijini hivihivi kwa hiyo nitakarabati darasa kama njia ya kuweka mfano bora” –Waziri Nchemba


Mwanamke Aliyejeruhiwa na Mke wa Rais Mugabe Apigiwa Magoti

0
0

Familia ya mwanamke aliyedaiwa kushambuliwa na Bi Grace Mugabe imedaiwa kufuatwa na kuombwa na mtu asiyejulikana kukubali fedha kama fidia ya kutupilia mbali kesi hiyo, wakili wake amesema.

Familia haitaki kufanya hivyo, Gerrie Nel alisema.”Walisema tuzungumze na tuwache kesi hii, lakini hakuna kiwango cha fedha kilichotajwa,” aliongezea.

Wakati huohuo katika mahojiano marefu ya simu na bi Gabriella Engels ambaye amemtuhumu bi Grace Mugabe kwa kumpiga, Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani alitulia na kuonekana kuwa mtu aliyekuwa na wasiwasi mwingi mara kwa mara.

Akielezea tukio hilo bi Engels mwenye umri wa miaka 20 alisema kuwa yeye na watu wengine wanne, wawili wakiwa wana wa kiume wa rais Mugabe na bi Grace Mugabe walikuwa wakinywa vinywaji siku ya Jumapili usiku katika chumba kimoja cha hoteli mjini Sandton, makaazi ya kifahari yaliopo Johannesburg.

Baadaye alienda katika chumba chengine na bi Mugabe akamfuata akiwatafuta wanawe.
Bi Mugabe alikuwa ameshikilia waya wa umeme mkononi mwake….alinizuia na kuanza kunipiga .
Nilijiangusha chini na kuanza kubingirika ili kukwepa kichapo hicho, na ni hapo aliponipiga na waya hiyo. Na nakumbuka nikiwa katika sakafu huku nikiwa nimejaa damu usoni na shingoni, bi Engels alidai.

Nilikuwa nikifikiria nitoke katika chumba hicho kabla ya mwanamke huyu kuniuwa.
Watu waliokuwa katika chumba hicho ni walinzi wake na walikuwa wamesimama nyuma yake huku akitupiga.

ulimsihi kuwacha kufanya hivyo ,lakini hakutaka kusikia aliendelea kutupiga…alitupiga akiwa na chuki nyingi .

Hadi leo marafiki zangu sielewi kwa nini mwanamke huyu alitushambulia vile bila ya sababu yoyote, Engels aliongezea.

kabla nitambue alikuwa bi Mugabe, nilijua nilifaa kumshtaki kwa kunishambulia kwa kuwa nilijeruhiwa vibaya
Sikujua yeye ni nani. na nilipojua yeye ni nani, sikutaka kumshtaki .. lakini mamangu akanisukuma kuwasilisha mashtaka hayo mahakamani, kwa sababu aliniambia: Kile mwanamke huyu alichotenda sio sawa.

Hatuwezi kuruhusu kukwepa kitendo alichofanya, alisema bi Engels.
Mwanamke huyo wa miaka 20 alisema: Ningefurahia sana iwapo angepelekwa jela.. hilo ndio lengo langu kwa sasa.

Bi Mugabe hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

VIDEO...Tundu Lissu Awalipua Siro na Kapilima..Adai Kuna Vijana Wametumwa Kumfatilia Maisha yake

0
0
Leo Tundu Lissu ametoa ya Moyoni kwamba anawindwa na kufuatiliwa na vyombo vya Usalama. Amewasihi Vyombo vya Usalama vipambane na Wahalifu sio Wanaoikosoa Serikali

"Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro, wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV, jana niliwakaba Kanisani St. Peter's.

Wakubwa hawa wa Vyombo vyetu vya Usalama wawaelekeze watumishi wao watumie muda na rasilimali za nchi hii wafanye kazi ya kupambana na Waharifu sio kupoteza muda wao na pesa zetu kuhangaika na raia ambao wanatimiza wajibu wao wa kuiwajibisha Serikali iliyoko Madarakani.

Kwahiyo Afande Sirro na Afande Kipilimba, fanyeni kazi ya kupambana na Wahalifu na tuachieni kazi ya kuwaajibisha walioko Madarakani kwa mjibu wa Sheria za Tanzania". VIDEO:

Video:Kwa Hili la Msanii ROMA na Wasanii Wengine wa HIP HOP Mjitafakari Upya

0
0
Kama umepata bahati ya kuusikiliza wimbo mpya wa ROMA na STAMIN unaoitwa HIVI AMA VILE ambao ndio huo hapo juu basi unaweza kunielewa haya machache ninayo taka kuwaambia wana HIP HOP

Kwanza wanatakiwa kutambua kuo mziku huo ni harakati ambao unalenga hasa kuelimisha jamii na kuonyesha uhalisia wa maisha na katika utendaji wa viongozi wetu

Bahati mbaya wasanii wetu ambao wanajaribu kuimba nyimbo za harakati wameanza kwenda kinyume na malengo hayo kwa kuanza kuelezea hisia zao za makundi

Katika huo wimbo wa juu wasanii hao wawili wamejisifia zaidi ktk kuwakubali baadhi ya watu wakasahau kuwa wao kama wanaharakati sio watu wa kusifia au kuwa upande fulani...wao wanatakiwa wawe kwa wale watu ambao wanaenda sawa ndio wanaweza kuwasifia lkn sio kuwa kubali

Mwanaharakati unatakiwa usifie lakini sio kuwa kubali watu maana kumkubali mtu yaani ww hata akikosea ni sawa tu


Lakini pia wao wanatakiwa kujua wana carrier kubwa sana katika industry na zaidi mashabiki zao wamegawanyika

Hivyo basi nawashauri wanaharakati wa mziki wasiweke wazi msimamo wao kwamba wana mkubali mtu fulani bali ikiwezekana wamsifie tu inatosha kuepuka kuleta mgawanyiko ambao unaweza kuleta chuki


Kwa wasanii kama hao kuimba nyimbo zenye kuleta matabaka ni uchochezi wa wazi...maana wanajaribu kuleta chuki baana ya pande mbili


Napenda kuwasihi sana wasanii wetu wawe waangarifu sana huku wakizingatia maslahi ya taifa kama watu wamoja

TID Afungukia Kurudia Madawa ya Kulevya

0
0
MKONGWE kunako Muziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ amewajia juu wanaoendelea kumhusisha kurudia matumizi ya madawa ya kulevya kwa kusema kuwa hakuna kitu kama hicho na wanaoeneza taarifa hizo wana lengo la kumchafua tu.

Akipiga stori na Ijumaa, TID ambaye kipindi kifupi cha nyuma aliwahi kukiri kutumia madawa alisema, alishatangaza ameacha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda hivyo hawezi kurudi nyuma akatumia tena hivyo vitu.

“Sijarudia jamani, hayo mambo ni ya uchochezi hakuna la zaidi, nimeshaacha hayo mambo kwa nini watu wanizushie, sijarudia madawa,  cha muhimu ni kujua mikakati ya kazi zangu kimuziki ndio ninachowaza si hayo mambo. “Sina cha kuwashauri wasanii wanaoendelea kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, sababu nilishaongea mengi tangu awali nilipotangaza nimeacha,” aliongeza TID.

Madee Awapigia Magoti Jack Wolper na Lulu Michael Kwa Kuwatengeneza Katuni Bila Ruhusa yao...

0
0
Msanii wa muziki Madee amemuomba radhi Jacqueline Wolper baada ya kumhusisha kwenye video yake ya wimbo ‘Sikila’ bila makubaliano. Pia rais huyo wa Manzese amedai yule anayeonekana akicheza na Tekno ni Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anadaiwa kuwa karibu na muimbaji huyo mahiri kutoka Nigeria.

VIDEO:

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo Magazetini na Mitandaoni

0
0

TID Ampachika Mimba Mwanamuziki Recho...Mwenyewe Aruka Viunzi.....

0
0
Msanii Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID, ameruka viunzi na kukana tetesi za kumpachika ujauzito msanii mwenzake Rachel.

Akizungumza kwenye kipindi che eNewz kinachorushwa na East Africa Television, T. I. D amesema kwa sasa hatarajii mtoto yeyote na mwanamke yeyote, na kwamba habari hizo hazina ukweli.

“Hapana, sitarajii mtoto yeyote na Rachel, sina mimba ya Rachel, siyo kweli bwana, hamna mtu mwenye mimba wala nini, kila mtu anataka kuwa na mimba ya Mnyama, sasa wanawake wangapi wanataka kuwa na ujauzito wa mtoto wangu?”, alisikika T. I. D

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa wasanii hao wana mahusiano ya kimapenzi, zilizoibua habari kuwa Rachel ana ujauzito wake.

Ummy Mwalimu Atoboa Siri "Tezi Dume Inapimwa Kwenye Damu 'Sio Kile Kipimo Kinachotembea Mitandaoni'

0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee ma Watoto, Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wanaume kupima saratani ya tezi dume huku akiwatoa hofu kuwa kipimo cha kupima saratani ya Tezi dume unapima kwa kutoa damu na sio kipimo kinachotembea mitandaoni.

Waziri Ummy ametoa wito huo mkoani Katavi Manispaa ya Mpanda pamoja na wananchi waliotoka wilaya ya Mlele na Tanganyika mara baada ya kuzindua zoezi la upimaji magonjwa ya sio ya kuambukizwa.

“Lakini inaweza kuwa wanaume mnaogopa kupima saratani ya tezi dume na mimi nitoe wito kwa wanaume mpime kwasababu pia sio kile kipimo kinachotembea mitandaoni kipo kipimo cha kupima saratani ya Tezi dume ambapo unapima kwa kutoa damu na sio vile mnavyofikiria kile kipimo ambacho watu wanakiogopa hicho sicho kipo kipimo rafiki,” aliongeza Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy alisema kuwa serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watumishi wa afya wasiotoa huduma za kuridhisha na wenye kashfa ya kutokuwa na maadili ya kazi.

“Pale ambapo muuguzi amekujibi vibaya, daktari amekujibu vibaya na mkunga hajakufanyia vizuri, wauguzi wa hospitali ya Mpanda wengi ni wazuri tutajie jina na sisi tutamchukulia hatua na tutamwambia atupishe wapo watu wengi sana wanaotaka kufanya kazi katika hospitali za serikali,” alisema Ummy.

Kibano Kingine...Manispaa ya Ilala yapiga Marufuku Kuosha Magari Pembeni ya Barabara

0
0
Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam imesema kila kijana atakayekutwa anaosha magari pembezoni mwa barabara za manispaa hiyo atapigwa faini ya shilingi laki mbili papo hapo huku mmiliki wa gari husika nae akitozwa faini kama hiyo.

Aidha Mkurugenzi wa mazingira amesema licha ya kupigwa faini kwa watu hao lakini bado watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Mkuruegenzi wa mazingira na udhibiti wa taka katika manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda amesema kumezuka tabia kwa baadhi ya vijana kugeuza maeneo mbali mbali ya manispaa hiyo kuwa maeneo ya kuosha magari huku maji wanayotumia yakitiririka barabarani na kusababisha kutuama jambo ambalo ni uchafuzi wa mazingira.

Amesema tangu kuanza kwa zoezi hilo mwezi Juni mwaka huu wameshafanikiwa kukamata vijana hao pamoja na wamiliki wa magari wasiopungua 50 na kuwapiga faini pamoja na kuwafikisha mahakamani.

Wanafunzi Wawili wa Shule ya Msingi Wafariki Wakichimba Mchanga wa Kujengea Darasa

0
0
Wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Chikomo Tarafa ya Nalasi, Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma wamefariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga wa kujengea darasa walipokuwa kwenye mafunzo ya vitendo.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa ukurasa huu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa mkoani Rukwa SACP Gemini Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba  wanafunzi waliofariki ni Selina Selemani Kazembe (12) wa darasa la tatu pamoja na Sofia Sillo (9) darasa la tatu kwa kusema kuwa watoto hao waliangukiwa kwa kufunikwa na ukuta wa shimo la mchanga ambao ulikuwa ukitumika kujengea darasa.

Kamanda Mushi amefafanua kwamba "Kwa mujibu wa taarifa tulizopewa na uongozi wa shule hiyo wanafunzi hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo yajulikanayo kama elimu ya Kujitegemea (EK).

Pamoja na hayo Kamanda huyo amesema jitihada zilizofanyika ni kuwakimbiza watoto hao katika hospitali ya Mbesa lakini kwa bahatI mbaya wakati watoto hao wanafikishwa hospitali walikuwa wameshakata roho.

Kwa mujibu wa Kamanda Mushi amesema jukumu la mazishi familia hizo zimeachiwa.

Refa Huyu Mwenye Miaka 28 tuu Ndio Atachezesha Mechi ya Simba na Yanga

0
0
Mwamuzi bora wa msimu uliopita, Elly Sassi mwenye umri wa miaka 28 ndiye atakayecheza mechi ya watani Yanga na Simba.

Simba na Yanga zinakutana Jumatano ijayo katika mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Sassi ambaye ndiye mwamuzi bora Ligi Kuu msimu ulioisha 2016/2017.

Mwamuzi huyu kijana, amekuwa akitabiriwa kufika mbali kutokana na ubora wa kazi yake.

IGP Simon Sirro Atoa Agizo Kwa Makamishna Wastaafu Wanapokuwa Huko Mtaani...

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Makamishna wastaafu wa Polisi kuendeleza elimu ya Polisi Jamii pamoja na kutoa msaada katika jeshi la Polisi pindi wanapokuwa katika maisha ya uraia ili kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi.

IGP Sirro ameeleza hayo wakati wa sherehe zilizoambatana na Gwaride maalumu la kuwaaga Makamishna wastaafu wa Polisi Paul Chagonja, Hamdan Omar Makame na Kenneth Kaseke lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi jijini Dar es Salaam ambapo wastaafu hao walisukumwa kwenye gari maalumu na Makamishna Wasaidizi Waandamizi sita ikiwa ni utaratibu wa Jeshi hilo katika kuwaaga maofisa wakuu.

“Upolisi ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine hivyo utaalamu hauzeeki na kwetu sisi tunaondelea kubaki Jeshini tutaendelea kufuata yale yote mazuri mliyofanya na nyie mnapokuwa nje ya utumishi endeleeni kutusaidia kwa mawazo na milango yetu ipo wazi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama” Alisema IGP Sirro.

Katika hatua nyingine, Kamishna Paul Chagonja akizungumza baada ya kuagwa rasmi ambaye alikuwa Kamishna wa Oparesheni na mafunzo kwa muda mrefu amewaasa Maofisa na askari kuendeleza tamaduni na maadili ya Polisi pamoja na kufanya kazi kwa weledi pamoja na nidhamu kwa kuwa ndiyo msingi wa askari Polisi popote pale wafanyapo kazi zao hivyo amewaomba kuendelea kusimamia sheria bila ya kumuonea mhalifu yeyote.

Mrembo Sanchoka Aelezea Siri ya Umbo Lake Kumfunika Wema Sepetu.....

0
0
Mrembo Sanchoka Aelezea Siri ya Umbo Lake Kumfunika Wema Sepetu.....
WIKI iliyopita ilikuwa ya kihistoria katika Shindano la Figa Bomba 2017 linaloendeshwa na gazeti hili baada ya kufika kilele na modo, Sanchoka ‘Sanchi’ kuibuka kidedea kwa kuwafunika wenzake wawili, Sasha pamoja na Wema Sepetu walioingia tatu bora.

Katika shindano hilo lililodumu takribani miezi miwili likijumuisha mastaa mbalimbali wenye figa matata Bongo zaidi ya 22, Sanchi aliweza kudhihirisha kuwa ni namba moja baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki.

Leo katika kona hii, Sanchi anafunguka siri ya ushindi na jinsi alivyoweza kumfunika Wema kwa kalio.



Ijumaa: Unajisikiaje kuwa mshindi wa Ijumaa Figa Bomba 2017?
Sanchi: Najisikia vizuri nimeweza kuudhihirisha uzuri wangu kwa washiriki wote nilioshindana nao.
Ijumaa: Unajisikiaje kuwa mmoja wa wasichana warembo Bongo? Sanchi: Najisikia vizuri sana na uzuri umenifanya kujiamini popote ninapoenda. Ijumaa: Kutokana na umbo lako ni usumbufu gani unapata?
Sanchi: Unajua kuna kipindi mtu unatamani kukaa hata ndani siku nzima tu hata siku tatu kwa ajili ya kukwepa usumbufu.

Ijumaa: Picha zako mara nyingi zinaachaga viungo vyako wazi ni kwa nini?
Sanchi: Ni hobi yangu tu na najisikia furaha kufanya hivyo kwa sababu niko huru na kazi zangu.
Ijumaa: Kuna tetesi kuwa maisha yanaenda kutokana na umbo lako ni kweli?

Sanchi: Hakuna maisha yanayoenda ukiwa na umbo kwani watu wasiokuwa na maumbo maisha yao yanaendaje?
Ijumaa: Vipi una mpango wa kuzaa hivi karibuni?

Sanchi: Huo mpango upo mwakani nalifanyia kazi hilo suala.
Ijumaa: Unaweza kutuambia siri ya kumfunika Wema kwenye shindano la Figa Bomba?

Sanchi: Kikubwa ni kujiamini na kura za mashabiki kwenye shindano. Sijisifii sana lakini mashabiki ndiyo walioamua baada ya kuona umbo langu kuwa naweza kuwafunika hao watu.

STORI: IMELDA MTEMA
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live




Latest Images